HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.27%

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s. Mwandishi:
Kundi: VITABU VYA HADITHI

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.
  • Anza
  • Iliyopita
  • 13 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 30836 / Pakua: 10404
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

4

5

7

HADITH ZA MTUME (s.a.w.w)NA MA-IMAMU (a.s)

JAHANNAM

211. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kuhusu adhabu katika daraja la tatu la Jahannam (iitwayo Saqar) ni kama ifuatavyo: "Humo yako Mateso makali mno, inapopumua wakazi wake huungua kuwa majivu kwa kutokana na joto lake, lakini hawatakufa. Nyama yao itaunganikana tena Humo pia kuna kisima kiitwacho Saqar ambayo ni kwa ajili ya wale wajivunao, wakandamizaji na wadhalimu, na walioasi na ambapo mateso yatakuwa makubwa zaidi. Iwapo hii ndiyo itakuwa hali ya daraja la nne la Jahannam sasa hebu fikiria hali itakayokuwa katika daraja la tano, sita na saba. Tumwombe Allah swt atuepushe na Jahannam! Amin .

212. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . amesema: "Muelewe waziwazi kuwa hakuna atakayeishi katika Jahannam kwa milele isipokuwa kafiri, Munafiki na watendao madhambi na uasi. Ama kwa watu wataomaliza kutimiza kipindi cha adhabu zao, watatolewa huru kutoka Jahannam ."

213. Qur'an Tukufu Surah ya Al-Balad, 90, Ayah ya 19-20 zisemazo:Lakini waliokanusha Aya Zetu, hao ndio watu wa upande wa shari. Moto uliofungiwa (kila upande) utakuwa juu yao .

214. Qur'ani Tukufu Surah al-Humazah, 104, Ayah 5 - 9:Hasha! Bila shaka atavurumizwa katika (Moto unaoitwa) Hutama. Na ni jambo gani litakalokujulisha (hata ukajua) ni nini ( Huo Moto unaoitwa ) Hutama? Ni Moto wa Allah swt uliowashwa (kwa ukali barabara). Ambao unapanda nyoyoni. Hakika huo (Moto) watafungiwa (wewemo ndani yake ). Kwa magogo marefu marefu.

215. Qur'ani Tukufu Surah al-Mursalat, 77: Ayah ya 32: "Hakika (Moto huo) hutoa macheche yaliyo kama majumba ."

MILANGO YA JAHANNAM

216. Mlango wa kwanza "Yeyote yule atakayekuwa na matumaini katika Allah swt basi daima atakuwa mtu mwenye furaha na mafanikio; "Yeyote anayekuwa na khofu ya Allah swt basi anajaaliwa usalama; " mtu mwovu na aliyepotoka na mstahiki wa adhabu za Allah swt ni yule ambaye hana matumaini yoyote kwa Allah swt na wala hana khofu ya aina yoyote ile ya Allah swt.

217. Mlango wa pili "Yeyote yule asiyetaka kufanywa uchi Siku ya Qiyama, basi awavalishe nguo wale walio uchi humu duniani, " Yeyote yule asiyetaka kupatwa na kiu Siku ya Qiyamah, basi awanywishe wale wenye kiu humu duniani, "Yeyote yule asiyetaka kupatwa na njaa Siku ya Qiyamah, basi awalishe wale wenye njaa humu duniani .

218. Mlango wa tatu "Allah swt huwalaani wale wasemao uongo" Allah swt huwalaani wale walio mabakhili, "Allah swt huwalaani wale wanaowanyanyasa na kuwakandamiza wanyonge.

219. Mlango wa nne " Allah swt humdhalilisha yule ambaye anaidharau Dini ya Islam, " Allah swt humdhalilisha yule anayewakashifu Ahl ul-Bayt(a.s) . ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) "Allah swt humdhalilisha yule ambaye anawasaidia wadhalimu katika kuwadhulumu watu.

220. Mlango wa tano "Msiendekeze matamanio yenu, kwani matamanio yanapingana na tendo la kusadikisha; "Musiyaongelee zaidi yale yasiyowahusu kwani mtaondoka katika Baraka za Allah swt; "Na kamwe msiwe wasaidizi wa madhalimu.

221. Mlango wa sita " Mimi nimeharamishiwa kukubalia Mujtahid (hawa ni wale ambao wamefikia upeo wa Ijtihad, uwezo wa kutoa fatwa. Rejea vitabu vya Fiqh ndipo utakapoweza kupata ilimu zaidi katika somo hili). " Mimi nimeharamishiwa kukubalia wale wanaofunga saumu.

222. Mlango wa saba "Ujihisabie mwenyewe matendo yako kabla hujafanyiwa hisabu ya matendo yako; "Uikaripie nafsi yako kabla wewe hujakaripiwa; "Na mwabudu, Allah swt aliye Mkuu na aliyetukuka, kabla ya wewe hujafika mbele yake na ambapo hautaweza tena kumwabudu na kumtukuza.

223. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amenakiliwa katika uk.145, J.1 ya al-Zamakhshari's Rabee' al-Abrar akiwa amemwuliza Malaika Jibrail(a.s) ., "Je ni kwa nini mimi kamwe sijamwona Malaika Mikaili(a.s) . akicheka au kutabasamu?" Malaika Jibraili(a.s) . alimjibu: "Mikaili kamwe hakucheka wala kutabasamu kuanzia pale Jahannam ilipoumbwa."

224. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema: "Katika safari yangu ya usiku wa ('Israa), mimi nilisikia sauti kubwa mno, hivyo nilimwuliza Malaika Jibrail(a.s) ., 'Je sauti hii kubwa ni ya nini, Ewe Jibraili ?' Naye alinijibu, 'Ni jiwe lililotupwa kutokea juu kuangukia ndani mwa Jahannam , na imekuwa ikianguka kwa muda wa vipindi sabini vya baridi, na sasa ndipo ilipofika chini."

225. Abu 'Asim 'Ubayd ibn 'Umayr ibn Qatadah al-Laythi, Hakimu wa Makkah (aliyeariki 68 A.H.), amesema, "Jahannam hupumua mara moja kwa sababu yake Malaika na Mitume(a.s) . yote hutetemeka, kiasi kwamba hata Mtume Ibrahim(a.s) . hupiga magoti na kusema, "Ewe Mola wangu! Nakuomba uniokoe! "

226. Abu Sa'eed al-Khudri amenakiliwa akisema, "Iwapo milima itapigwa kwa rungu mara moja inayotumiwa na Malaika wa Jahannam , basi itavunjika vipande vipande na kuwa vumbi ."

227. Tawoos ibn Keesan al-Khawlani amenakiliwa akisema, "Wakati Jahannam ilipoumbwa, Malaika walishtushwa mno, na wakati nyie wanaadamu mulipoumbwa, basi walitulia ."

228. Al-Hasan ibn Yasar al-Basir amesema, "Kwa kiapo cha Allah swt! Hakuna hata mja mmoja wa Allah swt anayeweza kustahimili joto la Jahannam! Tumeambiwa iwapo mtu atasimama Mashariki na Jahannam ikawa upande wa magharibi na ikafunuliwa kidogo tu, basi bongo ya mtu huyo aliye Mashariki itachemka. Iwapo kama kiasi cha ndoo moja ya usaha wa Jahannam ukimwagwa juu ya ardhi hii ya dunia, basi hakuna hata kiumbe kimoja kingalibakia hai."

229. Abu Zar al-Ghaffari, Allah swt amwie radhi, alikuwa akisema, "Waambieni wale ambao hupenda kulimbikiza utajiri wao kuwa watachomwa nayo juu ya paji la uso wao, pembeni mwao, na migongoni mwao hadi watakapokuwa wamejaa kwa mioto ."

230. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema, kama vile tuambiwavyo, "Hakuna Mja wa Allah swt mwenye utajiri au mali na hataki kulipa Zaka isipokuwa kwamba atachomwa kwa vipande hivyo vya mapesa vitakavyokuwa vimepashwa moto katika moto wa Jahannam na kwamba watatumbukizwa katika adhabu hizo kuanzia juu ya vipaji vyao vya nyuso zao na migongo yao hadi pale Allah swt atakapokuwa amemaliza kupokea mahisabu na adhabu za waja wake Siku ya Qiyamah, muda ambao ni wa maelfu ya miaka kwa mujibu wa mahisabu yetu. Hapo ndipo watakapotumwa ama kuingia Jannat au Jahannam ." [150]

231. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema : "Italetwa mbele yake, naye atachukizwa nayo; na itakapoletwa karibu yake, itauchoma uso wake na kifuvu kitadondoka. Iwapo ataweza kunywa hata kidogo kutokamo, basi matumbo yake yatakatika vipandevipande na kutokezea sehemu za nyuma ya kutokezea haja kubwa."

271. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ameripotiwa akisema, "Sala za mtu anayekunywa pombe hazikubaliwi kwa siku arobaini; na iwapo atakufa huku pombe ikiwamo tumboni mwake, basi Allah swt atamlazimisha anywe sadiid, maji yatokayo kwenye sehemu za uchi wa malaya ambayo yatakusanywa katika birika huko Jahannam na kupewa watu hawa, na kwayo matumbo na ngozi zao zitachomwa ."

232. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . anavyotupatia picha ya Jahannam, tumwombe Allah swt asitutumbukize humo:'Janga kubwa kwa mtu ni kule kutumbukia katika Jahannam; yeye atajihisi kuwa anachemshwa mzimamzima, na ataona mateso yake yasiyona mwisho, na kiumbe fulani kinakoroma na kupumua, viumbe vyote vilivyo humo hukosa raha na kamwe hawapati fursa ya kupumzika, na kamwe hawatapata kupumzika kutokana na adhabu zake au mauti ya uhakika. Yeye hasinzii hata kidogo wala hakutakuwa na mapumziko katiko mateso yake: Kutakuwa na maumivu yakudumu kiasi ambacho tunamwomba Allah swt atunusuru na kutusaidia .' (Hotuba 83).

233. 'Kwa hakika ni mahala pabaya kabisa kuliko sehemu yoyote ile, mahala ambapo mikono ya wakazi wake yanakuwa yamefungwa shingoni mwao, na vichwa vyao vimefungwa na miguu yao kwa minyororo na mavazi yao yametengenezwa kwa lami. Mashati yao yametengenezwa kwa moto wakati ambapo adhabu zao za moto usiozimika kamwe hazitakwisha kamwe mahala ambapo mlango wake utakuwa umejazwa watu, katika moto mkali kabisa kiasi kwamba sauti zao zinasikitisha na kutisha, na miale ya moto ikipaa na kufikia kila sehemu na wala hakuna kujitoa kutoka humo na wala hakuna muda utakaokwisha,na wala haina mwisho wake kwa wale wanaoteketezwa na kuchomwa humo.' ( Hotuba 109 ).

234. 'Joto lake ni kali mno, kufikia chini kwake ni mbali mno, sakafu yake ni chuma, vinywaji vyake ni usaha.' (Hotuba 120 ).

235. 'Siku ya Qiyamah, madhalimu wote wataletwa bila ya kuwapo na mtu yoyote wa kuwasaidia au kuwatetea, na hivyo watatumbukizwa katika moto wa Jahannam na humo atasagwasagwa kama vile machine za kusaga zifanyavyo, hadi hapo atakapojigonga kichwa katika sakafu ya chini kabisa.' ( Hotuba 164 )

236. 'Iwapo Malik (msimamizi wa Jahannam) atakuwa mkali, husababisha sehemu yake moja kuminyana na sehemu zingine, anapogombeza, milango yake huruka juu na chini (hutema kama volkeno). (Hotuba 183 )

237. Ayah 23 ya Surah al-Fajr, 89 na katika Ayah zinginezo pia:Basi Siku hiyo italetwa Jahannam. Siku hiyo mwanadamu atakumbuka, lakini kukumbuka huko kutamfaa nini ?

238. Qur'ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4, Ayah 140: Naye amekwisha kuteremshieni katika Kitabu hiki ya kwamba mnaposikia Aya za Allah swt zinakanushwa na zinafanyiwa kejeli, basi msikae pamoja nao, mpaka waingie katika mazungumzo mengine. Hivyo mtakuwa nanyi mfano wao hao. Hakika Allah swt atawakusanya wanafiki na makafiri wote pamoja katika Jahannam.

239. Vile vile Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Surah al-Nisaa,4, Ayah 145:Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka ya chini kabisa Jahannam, wala hutompata yeyote wa kuwanusuru .

240. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu, Sura al-Nisaa, 4, Ayah 55 : Basi wapo miongoni mwao walioamini, na wapo walioyakataa. Na Jahannam yatosha kuwa ni moto wa kuwateketeza.

241. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al-Jinn, 72, Ayah 23:Na wenye kumuasi Allah swt na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannam wadumu humo milele .

242. Allah swt antuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4 , Ayah 115 : Na anayempinga Mtume baada ya kudhihirikia uwongofu, na akafuata njia isiyokuwa ya Waumini, tutamuelekeza aliko elekea, na tutamwingiza katika Jahannam. Na hayo ni marejeo maovu.

243. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al-Kahaf, 18, Ayah 106: Hiyo Jahannam ni malipo yao kwa walivyokufuru na wakafanyia kejeli Ishara zangu na Mitume wangu.

244. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu,Sura al-'A'raf, 7, Ayah 179: Na tumeiumbia Jahannam majini wengi na watu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni nyama howa, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walio ghafilika.

245. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al-'A'raf, 7, Ayah 18: Akasema : Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote.

246. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura az-Zumar, 39, Ayah 32:Basi ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule aliyemsingizia uwongo Allah swt na kuikanusha kweli imfikiapo? Je! Siyo katika Jahannam makazi ya hao makafiri?

247. Na vile vile Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al-A'raf,7, Ayah 36:Na wale watakaokanusha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi, hao ni watu wa Motoni; humo watadumu.

248. Allah swt anatuambia katika:

وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ ﴿١١٣﴾

Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Allah swt, wala tena hamtasaidiwa. (Qur'ani, 11: 113).

249. Allah swt anatuambia:Na saidianeni katika wema na ucha Mungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui . (Qur'ani,5: 2).

250. Allah swt anatuambia: Na walisema:

وَقَالُوا مَا هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا يُهْلِكُنَا إِلَّا الدَّهْرُ وَمَا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ عِلْمٍ إِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ ﴿٢٤﴾

Hapana ila huu uhai wetu a duniani - twafa na twaishi, na hapana kinacho tuhiliki isipokuwa dahar. Laini wao hawana ilimu ya hayo, ila wao wanadhani tu. (Qur'ani, 45:24)

251. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . anasema:Safari ndefu lakini matayarisho ya safari ni madogo. Tukiwa watumwa wa dunia basi tutatumbukia Jahannam .

252. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema katika Mizanul Hikmah kuwa: "Mapenzi ya dunia ndiyo chanzo chote cha kila aina ya madhambi ."

253. Allah swt anatuambia:

مَّن كَانَ يُرِيدُ الْعَاجِلَةَ عَجَّلْنَا لَهُ فِيهَا مَا نَشَاءُ لِمَن نُّرِيدُ ثُمَّ جَعَلْنَا لَهُ جَهَنَّمَ يَصْلَاهَا مَذْمُومًا مَّدْحُورًا ﴿١٨﴾

Anayetaka yapitayo upesiupesi, tutafanya haraka kumletea hapa hapa tunayoyataka kwa tumtakaye. Kisha tumemwekea Jahannam; ataingia humo hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa na kufurushwa. (Qur'ani, 17:18).

254. Allah swt anatuambia katika:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ كَثِيرًا مِّنَ الْأَحْبَارِ وَالرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٣٤﴾ يَوْمَ يُحْمَىٰ عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنُوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ هَـٰذَا مَا كَنَزْتُمْ لِأَنفُسِكُمْ فَذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَكْنِزُونَ ﴿٣٥﴾

Enyi mlioamini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa batili na wanazuilia Njia za Allah swt. Na wanaokusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Allah swt. Wabashirie khabari ya adhabu iliyochungu. Siku (mali yao) yatakapotiwa moto katika moto wa Jahannam , na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, "Haya ndiyo (yale mali) mliojilimbikia nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya ) yale mliyokuwa mkikusanya." (Qur'ani, 9: 34 – 35).

(Imeelezwa katika riwaya kuwa neno lililotumika katika Ayah hii kanz inamaanisha mali yoyote ile ambamo zaka haijatolewa).

255. Allah swt anatuambia:Enyi Mlioamini! Mkikutana na waliokufuru vitani msiwageuzie mgongo. Na atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo - isipokuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi - basi atakuwa amestahiki ghadhabu ya Allah swt Na pahala pake ni Jahannam, na huo ni mwisho muovu . (Qur'ani, 8: 15 – 16)

256. Allah swt anatuambia:Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika wakiwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi . (Qur'ani, 5: 32).

257. Allah swt anatuambia:Na mwenye kumuuwa Mumiin kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannam humo atadumu, na Allah swt amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa . (Qur'ani,4:93).

258. Qur'ani Tukufu, Sura al-Ali Imran, 3, Ayah 21 : Hakika wanaozikataa Ishara za Allah swt , na wakawauwa Manabii pasipo haki, na wakawauwa watu waamrishao Haki wabashirie adhabu kali.

259. Watu wa Jannat watawauliza watu wa Jahannam kile kilichowaingiza Jahannam. Nao watawajibu kuwa wao hawakuwa miongoni mwa waliokuwa wakisali. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu, Sura al-Muddathir,

إِلَّا أَصْحَابَ الْيَمِينِ ﴿٣٩﴾ فِي جَنَّاتٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٤٠﴾ عَنِ الْمُجْرِمِينَ ﴿٤١﴾ مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ ﴿٤٢﴾ قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ ﴿٤٣﴾ وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ ﴿٤٤﴾ وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِينَ ﴿٤٥﴾ وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ ﴿٤٦﴾

Isipokuwa watu wa kuliani. Hao watakuwa katika mabustani, wawe wanaulizana Khabari za wakosefu: Ni nini kilichokupelekeni Motoni (Saqar)? Waseme: Hatukuwa miongoni waliokuwa wakisali. Wala hatukuwa tukiwalisha masikini. Na tulikuwa tukizama pamoja na waliozama katika maovu. Na tulikuwa tukiikanusha Siku ya malipo. (Qur'ani: 74: 39 – 46).

260. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu,Surah al-Fussilat,41, Ayah 7:Ambao hawatoi Zaka na wanaikataa akhera .

301. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu:

إِنَّ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَالَ الْيَتَامَىٰ ظُلْمًا إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ نَارًا وَسَيَصْلَوْنَ سَعِيرًا ﴿١٠﴾

Hakika wanaokula mali ya mayatima kwa dhuluma, hapana shaka yoyote wanakula matumoni mwao moto, na watingia Motoni. (Qur'ani, 4: 10).

302. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu:

الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا وَأَحَلَّ اللَّـهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا فَمَن جَاءَهُ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَانتَهَىٰ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللَّـهِ وَمَنْ عَادَ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٧٥﴾

Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu. (Qur'ani, 2:275).

Allah swt huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka.

303. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ بَدَّلُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ كُفْرًا وَأَحَلُّوا قَوْمَهُمْ دَارَ الْبَوَارِ ﴿٢٨﴾ جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا وَبِئْسَ الْقَرَارُ ﴿٢٩﴾

Hebu hukuwaona wale walio badilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru, na wakawafikisha watu wao kwenye nyumba ya maangamizo?!. (Qur'ani, 14: 28-29).

304. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Surah al-Mutaffifiin,:

وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ ﴿١﴾ الَّذِينَ إِذَا اكْتَالُوا عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ ﴿٢﴾ وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ ﴿٣﴾ أَلَا يَظُنُّ أُولَـٰئِكَ أَنَّهُم مَّبْعُوثُونَ ﴿٤﴾ لِيَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٥﴾ يَوْمَ يَقُومُ النَّاسُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦﴾ كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٍ ﴿٧﴾ وَمَا أَدْرَاكَ مَا سِجِّينٌ ﴿٨﴾ كِتَابٌ مَّرْقُومٌ ﴿٩﴾ وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿١٠﴾

Ole wao hao wapunjao! Ambao wanapojipimia kwa watu hudai watimiziwe. Na wao wanapowapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza. Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa Katika Siku iliyo kuu, Siku watapomsimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote? Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin. Unajua nini Sijjin? Kitabu kilichoandikwa. Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha! (Qur'ani, 83: 1 – 10).

305. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu:

وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ ﴿١﴾ الَّذِي جَمَعَ مَالًا وَعَدَّدَهُ ﴿٢﴾ يَحْسَبُ أَنَّ مَالَهُ أَخْلَدَهُ ﴿٣﴾ كَلَّا لَيُنبَذَنَّ فِي الْحُطَمَةِ ﴿٤﴾ وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْحُطَمَةُ ﴿٥﴾

Ole wake kila safihi, msengenyaji! Aliyekusanya mali na kuyahisabu. Anadhanim kuwa mali yake yatambakisha milele! Hasha! Atavurumishwa katika Hutama Na nani atakujuvya ni nini Hutama? Moto wa Allah swt uliowashwa. Ambao unapanda nyoyoni. Hakika huo utafungiwa nao Kwenye nguzo zilionyooshwa. (Qur'ani, 104: 1 – 5).

306. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu, Surah al-Mumin, 23, Ayah 43:Hapana umma uwezao kutanguliza ajali yake wala kuikawiza .

307. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu:

إِنَّ الْمُبَذِّرِينَ كَانُوا إِخْوَانَ الشَّيَاطِينِ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِرَبِّهِ كَفُورًا ﴿٢٧﴾

Kwa hakika wabadhirifu ni ndugu wa Masheitani. Na Shaitani ni mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi. (Qur'ani, 17: 27).

308. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu:

إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي عَذَابِ جَهَنَّمَ خَالِدُونَ ﴿٧٤﴾ لَا يُفَتَّرُ عَنْهُمْ وَهُمْ فِيهِ مُبْلِسُونَ ﴿٧٥﴾

Kwa hakika wakosefu watakaa katika adhabu ya Jahannam Hawatapumzishwa nayo na humo watakata tamaa. (Qur'ani, 43: 74 – 75).

309. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu:

وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُ يُدْخِلْهُ نَارًا خَالِدًا فِيهَا وَلَهُ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿١٤﴾

Na anayemuasi Allah swt na Mtume wake, na akaipindukia mipaka yake, (Allah swt) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha. (Qur'ani, 4: 14).

310. Allah swt amewaamrisha Malaika kuwa: Mtu anaponuia kutenda jambo jema wamwamdikie thawabu. Na anapoanza kutembea katika kulifanya tendo jema basi hapo pia anaongezewa thawabu nyingi na pale anapolianza kutenda tendo jema basi huongezewa zaidi ya hayo na anapomaliza kulitenda tendo jema basi hapo analipwa thawabu nyingi mno zisizo na hisabu. Lakini mtu anaponuia kutenda dhambi basi hapo haandikiwi adhabu, na anajitoa kwenda kutenda dhambi napo pia haandikiwi kwa sababu inawezekana akarudia njiani na anapolianza tendo ovu pia kuna uwezekano wa kutolikamilisha na kwa masikitiko makubwa, anapolikamilisha basi kwa huruma zake Allah swt, huandikiwa dhambi moja tu.

TAWBA

311. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) katika, Al-Mahajjat-ul-Baydha: "Majonzi makubwa ya watu wa Jahannam ni kuahirisha kwao Tawba "

312. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) : "Yeyote yule anayefanya Tawba ni sawa na yule mtu ambaye hana mzigo wowote wa madhambi ya aina yoyote ile ."[151]

313. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) Amesema: "Wapo waahirishaji ambao huahirisha kufanya Tawba hadi hapo mauti inapowafikia ."[152]

314. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwambia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Ewe 'Ali! Amebarikiwa yule ambaye anatazwa na Allah swt wakati pale anapolia kwa ajili ya kutaka msamaha wa madhambi ambayo hakuna mwingine ajuaye illa Allah swt tu ."[153] .

(Baadhi ya Ahadith zinasisitiza kuwa haimpasi mtu kuwaambia watu wengine juu ya madhambi yake mwenyewe. Hivyo inambidi aungame madhambi yake kwa Allah swt tu na wala si kwa mtu mwingine.)

315. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Katika kila sehemu ya tatu ya usiku na usiku wa kuamkia Ijumaa kuanzia usiku uingiapo( hadi alfajiri) Allah swt huwauma Malaika mbinguni ili kuita: 'Je yupo mwenye kuomba ili nimtimizie ombi lake?' Je yupo yeyote mwenye kufanya tawba ili nimrejee? Je yupo aombaye msamaha ili nimsamehe ?" [154] .

Tanbihi : Katika utamaduni wa Kiislamu, tunafundishwa kuwa kulala katika usiku wa kuamkia Ijumaa kunaitwa usingizi wa masikitiko; kwa sababu Siku ya Qiyama watu watakuwa wakisikitika mno kwa kulala usiku hizo.

316. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Fungeni milango ya madhambi kwa kumwomba Allah swt, na mufungue milango ya utiifuu kwa kusema: Bismillah Rahmaan Rahiim ."[155]

KULINDA HESHIMA YA WAUMINI

317. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) : "Ni faradhi kwa kila Mwislamu kusitiri na kuzificha aibu sabini (70) za Mwislamu mwenzake (ili kulinda heshima yake) ."[156]

(Makosa na kasoro zake zote zishughulikiwe kibinafsi na wala zisienezwe na kutangazwa kwa watu wengine).

318. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) Amesema: "Kubali msamaha akuombao Nduguyo Mwislamu na kama hakufanya hivyo, jaribu kumvumbulia hivyo ."[157]

319. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) Amesema: "Hali mbaya kabisa ya uhaini ni kutoboa habari zilizo siri ."[158] .

320. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) Amesema: "Kumuonya kwako aliyetenda makosa miongoni mwa au mbele ya watu ni kumdhalilisha ." (Inakubidi uongee naye katika faragha)."[159]

321. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Katika matendo yote aypendayo Allah swt, ni kule kumletea furaha Mwislamu kwa mfano: kumshibisha, kumwondolea majonzi yake, au kumlipia madeni yake ."[160]

MATENDO MEMA

322. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Kwa kufanya usuluhisho na amani miongoni mwa watu wawili (kwa kulinganisha) ni borai kuliko ibada za sala na saumu zake mwenyewe ." [161]

323. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) Amesema: "Iwapo mtu atakufikia wewe kwa mema, basi inakubidi uhakikishe kuwa fikira zake zinabakia kweli ."[162] .

324. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Yeyote yule awaongozaye watu kwa taqwa (atalipwa) sawa na yale ayatendayo (aliyeongozwa) hayo matendo mema. ." [163]

325. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Yapo matendo sita ambayo Mwislamu Momiin anaweza kufaidika nayo hata baada ya kufariki kwake: " Kumwacha nyuma mtoto atakaye mwombea maghfira, " Kuacha Mus.-hafu sharifu ambao watu watakuwa wakisoma, " Kuchimba kisima cha maji kitakachokuwa kikiwafaidisha watu, "Mti alioupanda yeye, "Sadaka aliiyoitoa katika kusababisha maji yakatirika vyema, "Ahadith na Sunnah nzuri atakazokuwa ameacha nyuma yake na zikifuatwa na watu.[164]

326. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Iwapo isingalikuwa vigumu kwa Ummah wangu basi ningalikuwa nimewaamrisha kupiga miswaki kwa kila Sala ." [165]

DHULUMA NA UONEVU

327. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Siku ya Qiyama, mwitaji ataita:' Je wako wapi wadhalimu na wasaidizi wao na wale wote waliowatengenezea wino au waliowatengenezea na kuwakazia mifuko yao au waliowapatia wino kwa ajili ya kalamu zao? Kwa hivyo, wakusanye watu wote hawa pamoja nao! " [166] .

328. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) Amesema: "Kwa kiapo cha Allah swt, Iwapo nitapewa umiliki wa nchi sana pamoja na yale yote yaliyomo chini ya mbingu zilizo waz ili nimuasi Allah swt kwa kiasi cha mimi kunyofoa punje moja ya shairi kutoka kwa sisimizi, basi mimi kamwe sitafanya hivyo ."[167]

329. Amesema Al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) : "Zipo aina tatu za dhuluma: moja, ni ile ambayo Allah swt anasamehe, pili, ile ambayo Allah swt haisamehe, na tatu ni ile ambayo Allah swt haipuuzii. Hivyo, dhuluma ambayo Allah swt haisamehe ni ukafiri dhidi ya Allah swt. Na dhambi ambalo Allah swt anaisamehe ni kile mtu anachojifanyia dhidi yake mwenyewe na Allah swt. Lakini dhambi ambalo Allah swt haipuuzii ni ile ambayo inavunja haki za watu ."[168]

Ufafanuzi : Aina ya tatu ya dhuluma ni ile ambayo mtu hukiuka na kuvunja haki za watu. Njia saheli ya kutaka kusamehewa ni kwanza kumridhisha yule ambaye haki zake zimekiukwa na kuvunjwa. Iwapo mtu huyo atamsamehe yule aliyemvunjia haki zake, basi hapo dhuluma hiyo itageuka kuwa dhuluma dhidi yake binafsi. Na hapo ndipo ataweza kuwa mstahiki wa kuomba msamaha wa Allah swt.

330. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Amesema: "Dhuluma husababisha miguu kupotoka, inaondoa baraka na kuangamiza umma au taifa ."[169]

331. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Amesema: "Hakuna kitu kinachovutia na kuharakisha kuondolewa kwa neema za Allah swt spokuwa kuendekea kwa dhuluma, kwa sababu Allah swt anazisikiliza dua za madhulumu na huwa yuko tahadhari pamoja na madhalimu."[170]

HAKI ZA WAISLAMU WENZAKO

332. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Yeyote yule anayemhuzunisha Mwislamu mwenzake basi kamwe hawezi kumfidia hata kama atamlipa dunia nzima kwani haitatosha (ispokuwa iwapo atatubu na kumfurahisha Mwislamu huyo) ." [171]

333. Al-Imam Musa al-Kadhim(a.s) . Amesema: "Moja ya faradhi miongoni mwenu kuelekea Mwislamu mwenzenu ni kutokumficha kitu chochote ambacho kinaweza kumfaidisha humu duniani au Aakhera ."[172]

334. Al-Imam Al-Hassan Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Amesema: "Watendee watu vile utakavyopenda wewe kutendewa ."

335. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) .Amesema: "Alla swt humrehemu mtu ambaye anahuisha yaliyo haki na kuangamiza na kuteketeza yale yaliyo batili, au hukanusha dhuluma na kuimarisha uadilifu ."[173]

336. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Tabia hizi nne ni kutokea tabia za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w): haki, ukarimu, subira na kuvumilia katika shida, na kusimamia haki ya Mumiin ."[174] .

337. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) Amesema: "Kwa hakika ni watu wa kawaida ndio walio nguzo za Din, nguvu ya Waislamu na hifadhi dhidi ya maadui. Hivyo mwelekeo wako daima uwe kuelekea wao na uwanynyekee ."[175] .

338. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Allah swt haabudiwi zaidi ya thamani kuliko kutimiza haki ya Mumiin ."[176]

339. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Yeyote yule anayemuudhi Mumiin, basi ameniudhi mimi ." [177]

340. Amesema Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) katika,: "Yeyote yule atakayemdhulumu Muumin mali yak pasi na hakie, basi Allah swt ataendelea kumghadhibikia na wala hatazikubalia matendo yake mema atakayokuwa akiyatenda; na hakuna hata mema moja itakayoandikwa katika hisabu zake nzuri hadi hapo yeye atakapofanya tawba na kuirudisha hiyo mali kwa mwenyewe ."[178]

SALAAM -- KUSALIMIANA

341. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Pale munapokutana miongoni mwenu basi muwe wa kwanza kwa kutoa salaam na kukumbatiana; na munapoachana, muagane kwa kuombeana maghfirah ." [179]

342. Al-Imam Hussein ibn Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Amesema: "Thawabu sabini (70) ni kwa ajili ya yule ambaye anaanza kutoa salaam na thawabu moja ni kwa ajili ya yule anayeijibu hiyo salaam ."[180]

(Wakati watu wawili wanapoonana, mtanguliaji katika kutoa salaam hupata thawabu zaidi).

343. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema: "Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) aliwakusanya watoto wa 'Abdul Muttalib na kuwaambia: Enyi watoto wa Abdul Muttalib! muwe waanzilishi wa salaamu, mujali Jama'a zenu, musali sala za usiku wakati watu wengine wanapokuwa wamelala, walisheni vyakula watu, na muongee maneno mazuri na hayo kwa hakika mutaingia Peponi kwa amani ."[181]

344. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema: "Yeyote yule anayekuwa ni muanzilishi wa kutoa salaamu basi atakuwa ni mpenzi sana wa Allah swt pamoja na Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w)" .[182]

KUTENDA MEMA NA KUKATAZA MABAYA

345. Allah swt anatuambia katika Qur'an:

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٠٤﴾

Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.(Qur’an, 3:104).

346. Amesema Mtume Mtukufu(s.a.w.w) . "Itakapofika wakati katika umma wangu ambapo Waislam watakuwa wakitekenya wengine wafuate mema na wajizuie na mabaya, basi kwa hakika watakuwa wametangaza vita dhidi ya Allah swt ." [183]

347. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Yeyote yule anayeacha kukataza wengine wasifanye maovu kwa maneno na kwa matendo (ni tofauti na kuona maovu yakitendeka) basi huyo ni maiti inayotembea miongoni mwa walio hai ."[184]

348. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Kumzuia Muislam asitende matendo maovu ni sawa na Allah swt kumlipa thawabu za Hija 70 zilizokubaliwa "[185]

349. Alisema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Ambizeni miongoni mwenu kutenda mamea; basi mtakuwa miongoni mwa watendao mame. Muwazuie wengine wasitende maovu kwa maneno yenu, na mujiepushe, na uwezo wenu wote, na yeyote yule anayetenda hivyo. Mumtumikie Allah swt kama ni wajibu wenu; na angalieni kusiwepo na mulaumiaji au lawama yoyote itakayoweza kuwazuia nyie katika kutekeleza maswala ya Allah swt. Jitupeni jitumbukizeni katika hatari kwa ajili ya kunusuru ukweli popote pale itakapo hitajika ."[186] .

350. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . Amesema: "Kwa hakika kuwaambia watu yaliyoyakweli na kuwazuia kwa yale yaliyo potofu ndiyo sirah ya Mitume (a.s). na waja wema. Kwa hakika ni jambo moja kubwa (wajib) kutokana na hiyo mambo mengine mengi yaliyo faradhishwa yanaweza kubakia, Ummah zingigine zinawea kunusurika, maelewano ni halali, dhuluma imekatazwa, na hakikaamani itajaa juu ya ardhi hii "[187]

351. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Uimara wa dini ni kule kuamrisha yaliyo mema na kukatza yale yaliyo maovu, na kubakia katika mipaka ya Allah swt ."[188]

352. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) "Yeyote anayeona maovu au mabaya yanatendeka basi ayazuie kwa matendo yake, kama ana uwezo huo, bila shaka; kama hawezi kufanya hivyo, basi azuie kwa ulimi wake, na kama hawezi kufanya hivyo pia basi anaweza kulaani kimomoyo ." [189] .

353. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Yeyote yule katika 'Umma wangu anayechukua jukumu nakumamrisha mema na kukataza maovu na anaye jihusisha katika ucha-Allah swt,wataishi kwa raha na mustarehe na watakapo acha kufanya hivyo, basi baraka na neema za Allah swt zitaondolewa kwao ." [190]

354. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Akiwambia Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib (a.s). na Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib (a.s). wakati Ibn Muljam (Laana za Allah swt zile juu yake) alipompiga dharuba kali katika Masjid Kufa"Muogopeni Allah swt (Na akasema tena)Muogopeni Allah swt katika mambo ya Jihad, (Jitihada za vita vitakatifu), kwa misaada ya mali, maisha na mazungumzo yenu katika njia ya Allah swt "[191] .

Msiache kuamrisha mema na kukataza maovu isije hawa waovuwakachukua nafasi juu yenu, na baadaye(Katika hali hiyo)mtakapo Sali basi salah zenu hazita kubaliwa

355. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Kuamrisha mambo memani jambo mmoja jema kabisamiongoni mwa watu ."[192]

356. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Matendo mema yote kwa ujumla, ikiwemu Jitihada za vita vitakatifu vya Jihad katika njia ya Allah swt, kwa kulinganisha na kuamrisha mema na kukataza maubaya, ni sawa na kyasi kidogo cha mate ya kilinganishwa na bahari yenye kina kirefu ."[193]

357. Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) : "Allah swt alimteremshia Wahyi Mtume Shua'ib(a.s) "Mimi nitawaadhibu watu wako kiasi cha laki moja na kati yao arobaini elfu ni waovu na elfu sitini ni katika watendao wema." Mtume Shua'ib(a.s) aliulizia hawa waovu wanastahili adhaabu lakini hawa watendao wema je akasema kwa hayo Allah swt alimterenshia wahi tena" Wao (walio wema)wamehusiana na watendao dhambi na hawa kuwa wakali hawa kughadhabishwa kwasabasbuadhabu na khofu zangu.[194]

358. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Wambieni wenzenu wa tende wemana wajizui na ubaya kwani hamutambui kuwa kwakuamrisha mema kamwe haikaribishi mauti wala kukatisha riziki .

359. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Ole wale watu ambao hawaisaidi Dini ya Allah swt kwa kuamrisha mema na kwa kutaza maovu .[195]

2

MUANDAMO WA MWEZI

SURA YA PILI

JAWABU KWA WANAFUNZI WA BACHOO JAWABU YA UTANGULIZI

Wahusika ndugu zetu wa Masjid Al-Sunna Zanzibar, wameanza kitabu chao hicho kwa utangulizi wenye kumshukuru na kumuhimidi Allah na kumtakia rehema na amani Bwana wetu Muhammad (s.a.w.) kama zilivyo khutuba na vitabu vya kiislamu. Na hayo yote yamefanyika chini ya utangulizi wenye anwani:

UKWELI JUU YA KUANDAMA KWA MWEZI

Na hii ndio sehemu ya kwanza ya kitabu chao. Wakasema katika utangulizi huo: Msisitizo wetu mkubwa katika kitabu hiki ni ile nukta muhimu ya kwamba suala la kufunga na kufungua kwa muandamo mmoja kwa dunia nzima si jambo jipya kama wanavyodhani baadhi ya watu, ni jambo la kale mno ambalo linaweza kutekelezeka na kwamba huo ndio uliokuwa msimamo wa 'Jamhur' ya wanavyuoni.

Jawabu Nakubali kuwa hili ni jambo la zamani, lakini kudai kuwa hii ni kauli ya Jumhuri ni madai hewa: hayana ushahidi. Leo hii duniani hakuna madhehebu yoyote ambayo inaitendea kazi kauli hio kama ni madhehebu nzima, bali kuna baadhi ya watu tu katika kila madhehebu ambao wanafata kauli hio. Hata zile madhehebu ziliotajwa kuwa ni zenye kufata kauli hio kama vile Malik, Hanbal na Hanafi, basi hawaitendei kazi kauli hio ila baadhi yao tu. Libya, Algeria na nchi nyengine za Afrika Kaskazini na Magharibi - kwa mfano - ni nchi za wafuasi wa madhehebu ya Malik, nao wanafata miandamo yao wenyewe. Kwa hivyo, dai kuwa hii ni kauli ya Jumhur ya wanavyuoni, si dai sahihi.

SEHEMU YA PILI

Katika sehemu ya pili, ndugu waandishi wanasema:

2. Si Fikra Za Shaykh Naaswir Bachuu "Ndugu yetu Juma Muhammad Rashid Al-Mazrui amejitahidi kuandika kitabu alichokiita: "Ushahidi Uliowekwa Wazi Katika Suala La Miandamo Ya Mwezi. Makusudio yake yalikuwa ni kutaka kukijibu kitabu kilichoandikwa na Shaykh Naaswir Abdullah Bachuu kinachojulikana kwa jina la "Ufafanuzi Wa Mgogoro Wa Kuandama Kwa Mwezi."

Jawabu Kidogo na mimi naomba niweke wazi kwamba kitabu changu hakikuwa kabisa na lengo la kujibu kitabu cha Sheikh Nassor Bachoo. Hili la kunukuu maneno yake na kuyajadili lilikuwa ni jambo la kutokea tu baada ya mtu Fulani kuniletea kitabu chake. Kwa havyo, kama mulivyosema nyinyi katika kitabu chenu kwamba: Kitabu hiki ni kama nasaha kwa Waislamu wote ili kuweza kudumisha umoja wetu hususan pale ambapo pamejitokeza misimamo tofauti katika mambo ya ibada. Wala lengo la kitabu hiki sio kuendeleza malumbano baina ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe hata kwa wale wenye misimamo tofauti. Kutajwa ndugu yetu Juma Muhammad Rashid lilikuwa ni jambo lisilobudi wala hapakuwa na lengo la kumkashifu au kumuumbua bali ni kutokana na kuwa hapakuweza kupatikana njia mbadala kwa vile ameshaandika kitabu ambacho ameshakichapisha chapa ya kwanza na ya pili.

Basi na mimi nakuombeni munielewe hivyo hivyo, kwamba wakati mimi naikubali fikra Fulani na kuikataa fikra Fulani, hakuna budi ninukuu fikra pinzani na kuonesha kwanini siikubali; na kwa upande wa pili ni lazima nioneshe kwanini naikubali fikra ninayoikubali. Na nitaposema kuwa kuna watu wana fikra hii, basi nadhani haitokuwa jambo la busara kama watu hao sikuwataja na nikiwataja ni lazima nitaje marejeo. Kwa sababu hii ndio maana nimekuwa nikinukuu maelezo ya Sheikh wetu Nassor Bachoo na kumjadili mule nisimokubaliana naye. Naomba musihuzunike kwani kujibizana katika kutafuta ukweli ni suala mashuhuri katika uwanja wa elimu. Wanavyuoni wakubwa wa kale na wa sasa wamekuwa wakijibizana ili kutafuta ukweli na hatimae huwabainikia woa pamoja na wasomaji. Kwa hivyo, hamukuwa na haja ya kutumia lugha: "Wala hapakuwa na lengo la kumkashifu": hii si kashfa hata kidogo: hii ni elimu.

Lakini, hakuna haja ya kufichana; kitabu chenu mumeandika kwa kujibu kitabu changu. Hamuna haja ya kusema: "Wala lengo la kitabu hiki sio kuendeleza malumbano baina ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe hata kwa wale wenye misimamo tofauti. Kutajwa ndugu yetu Juma Muhammad Rashid lilikuwa ni jambo lisilobudi wala hapakuwa na lengo la kumkashifu au kumuumbua bali ni kutokana na kuwa hapakuweza kupatikana njia mbadala kwa vile ameshaandika kitabu ambacho ameshakichapisha chapa ya kwanza na ya pili", kwani kitabuchenu kimeanza kwa kunitaja mimi mwanzo hadi mwisho na kuniaga kwa kunipa nasaha mimi. Ama mimi naandika jawabu hii kukujibuni nyinyi: sikufichini wala sisemi uwongo.

Munasema Kutokana na jambo hilo , sisi kwa upande mmoja tunashukuru kwa juhudi yake hiyo na kwa upande wa pili tunatuma masikitiko yetu kwake kwa kutokuwa makini na muadilifu katika kulifafanua jambo hilo muhimu. Kwani kitabu chake hicho kimeandikwa katika mfumo wa chuki, kibri, kejeli na malumbano huku akisisitiza kwa mara nyingi kauli chafu ambazo muandishi hapaswi kuzitumia katika kitabu au katika mijadala ya Dini. Jawabu Hizi chuki, kibri na kejeli, mimi nimezisoma kwenu, kwa hivyo na iwe kama msemo wa Waswahili: "Papa akipea mafuta huwapa wanawe". Je nyinyi munayakumbuka haya:

1) Munaukumbuka muhadhara wa Sheikh Bachoo ambao alisema kuwa wasionyanyua mikono katika sala wanasali kama mipopoo? Jamani! Hii si kejeli? Je katika nyinyi yuko aliyetoa muhadhara au kuandika kitabu ili kumjibu Sheikh wetu. Sasa uadilifu uko wapi?

2) Je munaukumbuka muhadhara wa Sheikh Bachoo aliozungumzia mas-ala ya udhu kasha akasema: "Wengine wakitia udhu kiungo hiki huomba dua hii na kiungo hiki huoma dua hii; upumbavu mtupu". Je haya si matusi? Je hii si kejeli?

3) Siku moja palikuwa na maziko. Maiti alisaliwa msikiti wa wajiitao "Watu wa Sunna". Kijana mmoja akasimama akasema: "Leo tunataka kukuonesheni vipi Mtume (s.a.w.) kamsalia maiti: si kama wanavyofanya Ibadhi na Shia.

4) La nne ni kuwa ikiwa nyinyi mumethubutu kunita mjeuri, mwenye kibri na kejeli; maneno ambayo mimi sikukwambieni wala kumwambia Sheikh Nassor; mimi nimemtoa makosa tu Sheikh wetu: na hii ni kawaida katika uwanja wa elimu; sasa je na nyinyi pia ni majeuri, wenye kibri na kejeli? Katika uwandishi wenu, pia mumesema: "Hatujui dhana hii potofu ameitoa wapi." Mwenye dhana potufu naye ni mpotufu, kwa hivyo na nyinyi hamukutoa nasaha bali mumetukana. Nakupeni mifano hii mitatu ya Sheikh wetu na mmoja wenu nyinyi wenyewe enyi wenye kuandika Radan mardudan na mifano iko mingi. Inatosha kuwaita kwenu watu wengine kuwa ni watu wa bidaa na nyinyi ndio watu wa Sunna. Kwa hivyo, hii hali mumeiuda nyinyi wenyewe: Zanzibar bali Afrika Mashariki na Dunia kwa ujumla haikuwa hivi. Chuki mumeziunda nyinyi; mukijirekebisha kwa kutumia lugha nzuri nadhani hakuna atayekwambieni jambo kwa lugha nzito.

Mnasema Mfano wa kauli zake mbaya ni kama zifuatazo:

(vuta-nikuvute) [uk. 6]

(hii ni ajabu katika ajabu za dunia!) [uk. 124]

(Kwa hivyo, uwezekano huo alioutoa Sheikh hauwashi wala hauzimi [uk. 124]

(Ninasema: Enyi walimwengu wenzangu tazameni hoja za kielimu hizo!!!!!!! Kwani nyinyi Wazanzibari kabla ya kuja fikra hio ya Sheikh Nassor Bachoo ya kufunga kwa muandamo mmoja,)

(Utaona kwamba masuala yote haya si yenye kima katika soko la elimu, bali ni masuala ya kuwababaisha watu wasiojua nini cha kujadiliwa katika mas-ala haya ya funga) [uk. 167]

(Hoja nyengine - nayo pia ni hoja ya mitaani - ni kuwa watu wengi wa kawaida wanapouona mwezi mkubwa husema: "E basi ule ndio mwezi wa leo ule?!!!")

(Jawabu hii ya mwisho, inaufanya upinzani mzima wa Sheikh Bachoo kuwa hauna maana yoyote.) [uk. 132]

(Kwa ufupi ni kuwa hicho walichokidai watetezi wa rai pinzan) [uk. 32]

(utaona jinsi gani mwanamume alivyokuwa bingwa wa kubadilika! Na hili si jengine bali ni lile Waswahili wanalolisema: "Mfa maji hukamata maji.") [uk. 128]

(Hakuna hapa kinachoonesha mas-ala ya kufunga kwa muandamo mmoja wala kumi na moja.)) [uk. 125] (haina maana kwamba usiku ukiingia sehemu moja ndio umeingia dunia nzima. Kwa ufupi ni kuwa hii ni hoja ambayo haina faida yoyote ya kielimu, lakini tunaijadili kwa ajili ya watu wa mitaani tu.)

Jawabu Sikubaliani na nyinyi kwamba humu muna maneno mabaya. Lakini hata nikikubali basi nasema kwamba lugha ya namna hii sababu ni nyinyi, na kwa hivyo, utaona kwamba ninapojadiliana na watu wengine basi lugha yangu hubadilika. Kwa hivyo, tujirekebisheni sote na tujadili tafauti zetu kwa lugha ya kiungwana. Ama ukinita mpopoo, basi usinilaumu na wewe nikikwita mnazi: unanilaumu nini na wewe unakifanya kile kile nikifanyacho?! Bali hata katika kitabu hiki munachonijibu, basi nanyi mumetumia lugha hizo hizo. Katika baadhi ya sehemu umesema: "Kwa hakika katika kitabu chake hicho kwenye uk 6, anajionyesha alivyo na kauli mbili tofauti..". Na mwishoni mwa kitabu mumesema: "Dhana ya pili ya ndugu Juma imejengeka katika msingi dhaifu wala haina nafasi katika uwanja wa fani (kitaalamu) nao ni kule kusukuma kwake juu ya elimu ya Jiografia". Na yamo mengi katika kitabu chenu. Sasa nyinyi mwasema nini na mwatenda nini?

Munasema "Kwa hakika katika kitabu chake hicho kwenye uk 6, anajionyesha alivyo na kauli mbili tofauti: Kwanza anakubali kwamba suala la muandamo wa mwezi lina ikhtilafu katika kufunga kwa kumuelezea Shaykh Naaswir Bachuu kwamba: (Tunampongeza kwa juhudi) Kisha pale pale anageuka kwa kusema: (madamu hili ni suala la khilafu - basi i likuwa ni kutolizungumza kabisa,) Sasa hebu tumuulize ndio anapongeza nini? Na ni nani aliyemwambia kwamba jambo lenye khitilafu halizungumzwi? Yeye angezungumza nini katika kitabu chake kama si masuala ya ikhtilafu? Pia anatwambia haya ni katika mambo ya furui (matawi) za Kidini, kwa hivyo zisizungumzwe. Kwani ni nani aliyemwambia kuwa furui za Kidini hazizungumzwi?"

Jawabu Ikiwa lugha hii ndogo hamukuweza kuifahamu, vipi mutaweza kufahamu kitu chenye kuhitaji fani za lugha na usuli na mengineo. Ikiwa mimi niliingia msikitini kwenu Raha Leo nikakuta juu ya ubao wenu munawasomesha vijana na katika darsa hio Mubtadaa mumemwita Fa'il (vipi mutaweza kujadili masuala haya?!!! Mimi nimempongeza Sheikh Bachoo kwa juhudi au moyo wake; na sikumpong eza kwa kulikuza suala ambalo:

1) Ni la furuu'i

2) Lina khilafu. Na hii haina maana kuwa Furu'i zisizungumzwe; suala la Furu'i huwa halishadidiwi; bali unawaacha watu kama walivyo tu. Lakini yeye anapenda kushadidia katika mas-ala kama haya; ndio maana akashadidi hata katika suala la kufunga mikono hata kuwaita watu mipopoo bali na kuwambia kuwa hawana Sala. Kwa hivyo, nieleweni kwamba ninachokipinga ni kushadidia au kuwakoroga watu katika kitu ambacho ni furu'i za dini ilhali yeye kawakuta na msimamo tafauti tangu zamani. Katika mas-ala ya furu'i, wanavyuoni huwa hawashadidi juu ya Mas-ala kama haya. Mimi leo nikisimama nikaanza kufanya kampeni kwamba watu wasiitikie amina wa kisali, nalo ni jambo la furu'i, si nitakuwa natia fitna tu? Jambo kama hili huwachwa wasomi wakalitafiti kaiha kila mmoja akafanya vile ilivyombainikia. Lakini kufanya kampeni maalumu na da'awa kana kwamba waliotangulia wote ni wapotovu, hili ndilo jambo la kulaumiwa.

Ama kauli yenu: "Kwanza anakubali kwamba suala la muandamo wa mwezi lina ikhtilafu katika kufunga kwa kumuelezea Shaykh Naaswir Bachuu kwamba: (Tunampongeza kwa juhudi) Kisha pale pale anageuka kwa kusema: (madamu hili ni suala la khilafu - basi ilikuwa ni kutolizungumza kabisa,) Sasa hebu tumuulize ndio anapongeza nini?" Mwisho wa kunukuu. Na mimi nikuulizeni nyinyi mumenishukuru kwa juhudi yangu kisha mwisho wa kitabu mukaniambia: "Mwisho tunachukua fursa hii kumuonya ndugu Juma kuwa amuogope Mwenyezi Mungu hususan katika mas-ala ya kielimu. Akumbuke kuwa Mwenyezi Mungu Ameonya juu ya mtu kusema jambo au kufanya asilolijua. Aelewe kwamba ataulizwa juu ya hilo. Lingekuwa jambo la busara kama ndugu Juma angalikubali kuuliza na kufanya utafiti zaidi juu ya mas-ala haya kama agizo la Mwenyezi Mungu linavyotutaka". Sasa na nyinyi munanishukuru nini?

Munasema "Sisi tunapenda kumfahamisha kuwa suala hili la kwamba mwezi ukiandama sehemu moja unatosheleza kufuatwa kwa kufunga au kufungua ulimwengu mzima, si suala jipya bali ni jambo la kale. Tunasikitika kwamba hakuangalia vizuri maoni ya Wanavyuoni wakubwa walivyoelezea msimamo huo. Angalia katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu uk 51-58. Hapa tunanukuu baadhi ya kauli hizo:

Imamun-Nawawy aliyekisherehesha Kitabu cha Sahihi Muslim anasema:

"Na jambo lililo sahihi kwa wenzetu (Mashaffi) ni kuwa muandamo mmoja hauwahusu watu wote bali unawahusu wale walio karibu kwa kiasi ambacho hawaruhusiki kupunguza Sala (Sala ya safari). Pia imesemwa kuwa iwapo matlai ni mamoja watalazimika (watu) kufunga pamoja. Pia imesemwa kuwa ikiwa (wanaishi) katika eneo la Iklimu moja (maili 72 au km 89) (watalazimika kufunga pamoja) vyenginevyo kila mmoja atafunga kwa muandamo wake. Na wakasema wenzetu wengine (Mashaffi) kuwa muandamo katika sehemu moja utawahusu wote wa dunia nzima".

Shaykh Jaadul Haq wa chuo kikuu cha Al-Azhar katika kitabu chake "Bayaanullinnas" J. 2 uk 203 - 204 ameandika yafuatayo juu ya kauli hiyo ya Imamun-Nawawy:

"Hapa Imamu An-Nawawy ametaja kwa mukhtasari kauli zilizomo katika madhehebu ya Kishaffi (juu ya kuandama kwa mwezi) na ambazo pia zimo katika madhehebu mengine ya Kiislamu. Kauli hizo tunaweza kuzigawa katika maf ungu matatu makuu: "...Hapo Imamu An-Nawawy ametaja kwa mukhtasar kauli zilizomo katika madhehebu ya Shaffi (juu ya kuandama kwa mwezi) na ambazo pia zimo katika madhehebu nyengine za Kiislam. Kauli hizo tunaweza kuzigawa katika mafungu matatu makuu: Kauli ya kwanza: "Kila nchi iwe na matlai yake, wala muandamo wa nchi moja hautalazimu nchi nyengine ya mbali wala karibu". Kauli ya pili: "Muandamo wa nchi moja unalazimu nchi zote za dunia hata kama ziko mbali".

Kauli ya tatu: "Muandamo wa nchi moja unalazimu nchi iliyo karibu nayo au inayowafikiana kimatlai". Kisha, Shaykh Jaadul-Haq akaendelea kusema kwamba:

"Na (kauli) zote hizo ni maoni yatokanayo na Ijtihaadi ambazo hazikusimama juu ya hoja kat-ii, si sanad wala matni. Kwa hivyo ingefaa ichaguliwe kauli ambayo inakubaliana na maslahi ya (Waislam wote wa) dunia nzima kwa jumla"."

Jawabu Sikubaliani na mtazamo wa Sheikh Shaykh Jaadul Haq wa chuo kikuu cha Al-Azhar, kwamba zote hizi ni rai na itihad kwani kanuni ni kuwa "Hakuna ijtihadi mbele ya andiko" Ijtihad mwahala mwake ni musimo andiko. Wakatika katika suala hili, utaona kwamba asemaye kuwa tufunge kwa muandamo mmoja, hoja yake ni Hadithi "Fungeni kwa kuuona"; na anayesema kuwa kila mahala na muandamo wake, anatoa ushahidi wake ni Hadithi ya Ibn Abbaas na Kuraib. Kwa hivyo, ijtihad ni katika kuyafahamu maandiko: si ijtihad kwa maana ya rai tupu pasi na andiko kama alivyosema Sheikh. Kilichobaki ni kuzijadili riwaya mbili hizi zina maana gani?

Munasema Tungependa kumueleza ndugu yetu kwamba hata hapa Afrika ya Mashariki jambo hili hakulianzisha Shaykh Naaswir Bachuu kama alivyodai mwenyewe (Nd. Juma) kwamba: (Muafrika wa Mashariki wa kawaida kusikia sauti ya mgogoro)) Inasikitisha hakuweza kuangalia katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu uk 161-163 wametajwa walioonyesha kwa vizuri kabisa misimamo hiyo tofauti. Mashaykh wenyewe ni hawa wafuatao: Al-marhuum Shaykh Juma Abdul Waduud (wa Zanzibar), Shaykh Abdillahi Naaswir ( Nairobi Kenya ), na Shaykh Naaswir Khamis Abdul Rahman ( Mombasa Kenya ).

Jawabu Kwani wapi katika kitabu changu nilisema kuwa Sheikh Nassor Bchoo ndiye aliyeanzisha fikra hii hapo Afrika ya Mashariki hata mukaleta dai hili? Mimi nimeeleza kuwa zamani Afrika Mashariki watu wote wakifata muandamo mmoja. Nilisema: Karne zimepita bila ya sikio la Muafrika wa Mashariki wa kawaida kusikia sauti ya mgogoro juu ya suala la muandamo wa mwezi. Harakati za elimu zilipobadilika na kuelekea zaidi - kwa kujua au bila kujua - katika mrengu wa Kihanbali na Kiwahabi, pakajitokeza mapinduzi ya ghafla ya fikra na matendo. Dr. Ramadhan Al-butti - miongoni mwa wanavyuoni wakubwa wa ulimwengu wa sasa - anaona kwamba harakati hizi hazisifiki kama ni madhehebu: bali ni hatua (phase) katika mapito ya Historia.

Na katika uk. 97, nimesema:

Kwa kwetu - Afrika Mashariki - kusema kwamba mwezi muandamo wa nchi moja ni muandamo kwa nchi nyengine zote za dunia ni kitu kipya. Kwa hivyo, ni wazi kwamba mimi nazungumzia Afrika Mashariki. Na mfano wa hilo pia kalisema Sheikh Nassor Bachoo, lakini yeye hamukumjibu. Anasema: "Pamoja na kuwa mgogoro wa kuandama kwa mwezi umeanza kuonekana hadharani katika jamii za Waislam wa hapa Afrika ya Mashariki katika miaka ya hivi karibuni". Inasikitisha kwamba hata maneno yangu mumeyakata na kuchukua yale ambayo hayakamilishi maana nilioilenga. Maneno "Karne zimepita" hamukuyataka kwani hayakufikisheni kule mutakako!

Pili narejea tena kusema kwamba hao wanavyuoni aliowataja Sheikh Nassor, hawajathibitisha habari za kuwa watu wafunge au wakifunga kwa muandamo mmoja Africa Masharik, ukimtoa Sheikh Nassir Khamis wa Mombasa ambaye naye pia ni mtu wa sasa. Ama sheikh Juma Abdu-Wadood yeye, kwa mujibu wa nakala hio ya Sheikh Nassor Bachoo, kasema hivi: Kuona huku kwa mwezi kumekusudiwa kuonekana na Waislam, na kuonekana na Waislamu huko, sio lazima kuonekana na Waislamu wote. Bali inatosha shahada ya mtu mmoja muadilifu".

Pia inampasa mtu mmoja pekee kama ameuona mwezi yeye afunge na kila aliyemuamini; hata akiwa haijakubaliwa shahada yake. Haya ndio maneno ya Sheikh Juma Abdu-Wadood kwa mujibu wa alivyomnukuu Sheikh Bachoo. Sasa ikiwa ndugu zetu mumeshindwa kuyafahamu maneno haya ya Sheikh Juma Abdu-Wadood, bado mutaendelea kupoteza watu bila ya elimu?! Sheikh Juma Abdul-Wadood hapa anazungumzia mas-ala ya ushahidi kwamba si lazima - katika suala la kuonekana kwa mwezi - kwamba kila mmoja auone: bali akiona mtu mmoja basi inatosha kwa wengine kufunga. Hii ndio kauli ya Sheikh Juma Abdul-Wadood na hili nimelieleza kwa urefu katika kitabu changu.

Kisha Sheikh Juma Abdul-Wadood akazungumzia suala la kufunga kwa muandamo mmoja akasema: "Rai za Maimamu wengine wameifasiri hadithi isemayo: (Fungeni kwa kuuona Mwezi) kwamba ukionekana popote mashariki au magharibi (watu) wafunge; hapana kutazama masafa fulani au nini. Hii ni rai nayo na wengi wamesema (hivyo) kama Imamu Malik , Ahmad na kundi kubwa la Hanafi. Inakurubia kuwa n dio rai ya Jamhuri - kufata rai hii ni kuhakikisha umoja wa dunia nzima. Wala hatuwezi kusema kwamba rai ya Shaffiy ndio ya Jamhur". Hapa Sheikh Juma anasimulia rai za Maimamu wengine: si rai za Maulamaa wa Afrika Mashariki. Mimi dai langu nililodai ni kuwa jambo hili la kufunga kwa muandamo mmoja, napenda munifahamu: ni jipya kwa Africa Mashariki. Mimi sikusudii jambo la wanazuoni kuzungumzia rai mbali mbali: bali nazungumzia jambo la watu kufata muandamo mmoja kwamba karne zimepita ya sikio la Muafrika Mashariki wa Kawaida halijiapata kusikia. Na nimetumia maneno "Muafrika wa Mashariki wa kawaida" ili kuwatoa wanavyuoni wao hata kama walikuwa hawafati kauli hio, lakini wanaijua. Kwa hali yoyote ile:

1) Sheikh Juma Abdul-Wadoo hajazungumzia kwamba Afrika Mashariki watu walikuwa wakifunga au wafunge kwa muandamo mmoja, bali kazungumzia rai za wanavyuoni wasio wa Afrika Mashariki - Al-Imamu Shafi, Hanbal n.k. Na mimi sijakanusha tafauti hizi.

2) Kauli yake ilikuwa ni kuhusu suala la mashahidi.

Ama Sheikh Abdillahi Nassir, yeye ni mwanachuoni wa sasa. Na mimi sijasema kuwa sasa hakuna rai hizo. Pili ni kuwa nakala alizotupa Sheikh Bachoo za kitabu cha Sheikh Abdillahi utaona kwamba Sheikh Abdillahi hazungumzii kuwa kauli ya kufatwa ni ile ya muandamo mmoja; bali yeye kasema kuwa hili ni suala la khilafu kwa hivyo tusigombane kila mtu afate rai anayoiona kuwa ni sawa. Sheikh Abdillah kayasema haya baada ya kutokea mizozo hii ya sasa. Kwa hivyo tunarudi pale pale kwamba "Karne zimepita bila ya sikio la Muafrika wa Mashariki wa kawaida kusikia sauti ya mgogoro juu ya suala la muandamo wa mwezi. Harakati za elimu zilipobadilika na kuelekea zaidi - kwa kujua au bila kujua - katika mrengu wa Kihanbali na Kiwahabi, pakajitokeza mapinduzi ya ghafla ya fikra na matendo". Kwa hivyo, nukta hii hamukuuijibu: na wala sioni kuwa kuna haja ya kuijibu kwani haina umuhimu katika maudhui yetu. Bali kitabu chenu chote, munachagua mambo yasio na umuhimu "Juma kantutukana; Juma kanfanya hivi" nyinyi ndio munajibu baada ya kuzungumzia dalili za kielimu.

Ama Sheikh Nassor: yeye pia ni mtu wa sasa na ni mfuasi wa skuli hio hio munayoifuata nyinyi, kwa hivyo kusema kwake alivyosema hakujapindua nilioyasema kuwa - kimatendo - hili ni suala jipya kwa kwetu Afrika ya Mashariki. Wala mimi sikusema kuwa Sheikh Nassor Bachoo ndiye muasisi wa fikra hio huko kwetu. Naomba munifahamu ninachokisema kwanza kisha ndio munijibu. Na sijui munapinga nini kitu ambacho watu wote wanakijua. Bila ya kusahau kwamba mimi sikusudii kusema kuwa kitu sahihi ni kilichofanywa zamani au kilichofanywa leo: laa! Bali kitu sahihi ni chenye ushahidi sahihi uliojengeka juu ya misingi sahihi ya kielimu. Na kielimu, suala la kuzingatia muandamo mmoja - hamutoweza kulithibitisha.

MNASEMA

Pia Shaykh Ahmad Al Khalil, Mufti wa Omani amethibitisha kwamba Ikhtilaf hii ya muandamo wa mwezi katika hukmu ya kufunga au kufungua ipo na kwamba ni jambo la kale. Kama alivyosema maneno yake yaliyotafsiriwa na Shaykh Muniir Sulayman 'Aziz kwamba: "Hakuna madhehebu iliyokuwa imesalimika na kuwa na Khitilafu baina ya Wanavyuoni wake juu ya suala la kutafautiana miandamo ya mwezi." Jee ndugu Juma anataka kusema kwamba Shaykh Naaswir Bachuu ndiye mwalimu aliyeanzisha madhehebu zote? Au ndiye aliyeanzisha mtafaruku huu kama alivyouita mwenyewe ndugu Juma?

JAWABU

Suala hilo jiulizeni wenyewe; mujijibu wenyewe; kwani nyinyi ndio mulioliunda: mimi sikusema hivyo kamwe bali nilichokisema ni hiki: "Kwa kwetu - Afrika Mashariki - kusema kwamba mwezi muandamo wa nchi moja ni muandamo kwa nchi nyengine zote za dunia ni kitu kipya". Nami sikusudii kusema kwamba upya huo ni katika kuzungunzwa au kusomwa suala hilo katika vitabu; nakusudia kimatendo sula hili lilikuwa halipo Afrika Mashariki. Sasa ili muwe mumenijibu, twambieni nani alikuwa akifata muandamo mmoja hapa Afrika Mashariki. Jamani! Tafuteni hoja mujadili: musijadili kitu kisichokuwa na umuhimu. Kama hamuna hoja nyamzeni musijitie aibu!

MNASEMA

Katika kudhihirisha udhaifu wake wa kumuandama mtu fulani; Ndugu Juma anasema: (Kama tunavyojua kwamba Sheikh Nassor Bachoo, ni mmoja wa wenye kusisitiza ulazima wa kuwa na muandamo mmoja.) Sisi kwa upande wetu tunasema: Katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu hakuna pahala alipolazimisha watu wafuate huo aliouita ndugu Juma (msimamo wa Shaykh Naaswir). Bali yeye ameonesha mitizamo ya Wanavyuoni kwa kutumia Aya za Qur-aan, Hadiythi na vitabu vinavyokubalika. Lugha aliyotumia Shaykh Naaswir katika huo unaonekana ni msimamo wake ni maneno yaliyozimuliwa kilugha (polite language) kama vile: (inawezekana) ((inaonyesha) .

JAWABU

Na mimi hapa sijasema kuwa Sheikh Nassir Bachoo kalazimisha watu wafunge kwa muandamo mmoja. Nimesema "Anasisitiza ulazima" yaani yeye analingania msimamo huo kwani kwake ndio msimamo sahihi na ndio wajibu kuufata. Naomba tena tuelewane musiseme kitu kinyume na nilivyosema. Wala musitafute kitu kisicho na maana mukajadili eti ndio jawabu! Pili maneno yenu: "Katika kudhihirisha udhaifu wake wa kumuandama mtu fulani". Sasa je na nyinyi pia munaonesha udhaifu huo huo kwa kumuandama mtu fulani katika kitabu chenu?

MNASEMA

Aliyelazimisha rai ni ndugu Juma mwenyewe kama anavyosema: (Lakini kilicho lazima na ambacho tunatakiwa tukubaliane ni kuwa muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali) [uk. 112]

JAWABU

Bali hata Sheikh Bachoo pia kalazimisha kwani ukidai kuwa huu ndio msimamo wa haki au ndio msimamo sahihi au ndio wajibu kufatwa, bila kusema kuwa rai zote zinafaa basi na wewe huwa umelazimisha rai yako. Sasa je Sheikh Bachoo anakubali hivyo kuwa rai zote ni sawa? Mimi kweli sisemi kuwa rai zote ni sawa: nasema kuwa nyinyi mumekosea na sahihi ni kinyume na munavyofanya, na kwa hivyo bado nipo katika msimamo wangu huo huo kwamba: "Kilicho lazima na ambacho tunatakiwa tukubaliane ni kuwa muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali".

MUNASEMA

"Kisha katika uk 85 ndugu Juma anataja kwamba msimamo huu wa muandamo mmoja kwa dunia nzima ni ((kitu kipya)) na kwamba jambo hilo halitekelezeki na ni kauli iliyobaki vitabuni tu baada ya kutaja baadhi ya nchi zinazofuata miandamo yao - yaani kila nchi na muandamo wake kama Al-yaman , Oman , Misri na Saudia. Kisha hapo hapo akataja: ((isipokuwa Imarati katika miaka ya mwisho wamekuwa wakifata Saudia.)) Inafaa ndugu Juma aulizwe masuala yafuatayo:

i) Kama ni jambo lisilotekelezeka vipi tena Imarat wanalitekeleza?

ii) Je hawa wa Imarat nao ni wanafunzi wa Shaykh Naaswir Bachuu?

iii) Kwani hiyo sio kauli ya Jamhuur ambayo ndio msimamo wa maimamu wakubwa wakiwemo Ahmad bin Hanbal, Malik na Abu Hanifa? (Angalia pia sehemu ya 11 na 13 za kitabu hiki)

JAWABU

Kwanza mumemefanya ghushi: maneno yangu hamukuyanukuu yote. Mimi nimesema: "Kwa kwetu - Afrika Mashariki - kusema kwamba mwezi muandamo wa nchi moja ni muandamo kwa nchi nyengine zote za dunia ni kitu kipya". Nyinyi maneno "Kwa kwetu Afrika Mashariki" mumeyatoa ili ionekane kuwa mimi nasema kuwa hili ni suala jipya kila pahala. Watu kama nyinyi vipi tutakuamini katika dini yenu na uadilifu wenu, ikiwa munaghushi maandiko hivi? Hii ndio kamati ya Msikiti Sunna na hii ndio suna yenyewe?! Halafu mukaendelea na tadlis (ghushi) yenu mukasema: "Na kwamba jambo hilo halitekelezeki na ni kauli iliyobaki vitabuni tu". Mimi sikusema hapa kuwa "Halitekelezeki", bali nimesema:

Lakini ukweli ni kuwa hata katika nchi nyengine zote za dunia taqriban kauli kwamba tufunge kwa muandamo mmoja, ni kauli ilioishia katika vitabu tu, kimatendo (practically) kauli hio haitumiwi isipokuwa na mtu mmoja mmoja. Hadi leo hii: watu Al-yaman wanafata muandamo wao, Oman wanafata muandamo wao, Saudia wanafata muandamo wao, Misr wanafata muandamo wao na nchi zote taqriban ni hivyo, isipokuwa Imarati katika miaka ya mwisho wamekuwa wakifata Saudia.

Haya nionesheni hapa maneno "Halitekelezeki". Mimi nimesema kuwa kimatendo kauli hii, hadi leo haitendewi kazi isipokuwa na baadhi ya watu. Nyinyi mumebadilisha na kuweka ghushi yenu mukasema nimesema halitekelezeki. Kwa hivyo, hilo Sula (a na b) jibuni wenyewe kwani mumesema kinyume na nilivyosema. Suala (d), najibu kuwa sio: hio si kauli ya jumhur bali jumhur kauli yao ni kinyume na hivyo na hili nimelithibitisha katika uk. 189-193 wa chapa ya pili ya kitabu changu au uk. 171 wa kitabu hicho chapa ya kwanza. Na Al-Imamu Malik riwaya zake zimegongana na riwaya kwamba kila watu na muandamo wao ndio ilio bora kwani ni riwaya ya Madina aliko kuweko Al-Imamu Malik, wakati riwaya nyengine ni ya watu wa Irak kulikokuwa na viwanda vya kutunga riwaya!

MNASEMA

Na sisi tunamuongezea habari moja ambayo ni vyema kuielewa, kwamba nchi ya Uganda iliyo katika Afrika ya Mashariki pia inafuata rasmi muandamo mmoja wa duniani. Pia aelewe kwamba huo msimamo wa kila nchi na mwezi wake huku Afrika ya Mashariki haukuwepo tokea zamani. Mashaykh wote wa huku wanakubaliana mwezi ukionekana popote katika nchi hizi tatu ( Kenya , Uganda na Tanzania ) wanafunga pamoja. Yeye anaendelea kushika msimamo wake: (Al-yaman wanafata muandamo wao, Oman wanafata muandamo wao, Saudia wanafata muandamo wao). Lile analoliona yeye halitekelezeki, basi ndio linatekelezeka.

JAWABU

1) Kitu rasmi Uganda hakizingatiwi kwani Uganda kimsingi sin chi ya Kiislamu wala ya Waislamu: Waislamu ni wachache ukilinganisha na Wasio Waislamu. Kwa hivyo, hakuna kitu rasmi. Na jambo hilo ni jambo la sasa. Na mimi sijapinga kwamba sasa fikra hio ipo Afrika Mashariki.

2) Ama kauli yenu: "Mashaykh wote wa huku wanakubaliana mwezi ukionekana popote katika nchi hizi tatu ( Kenya , Uganda na Tanzania ) wanafunga pamoja". Ndio maana nikatumia lafdhi "Kwa kwetu Afrika Mashariki" nikijua kuwa wanavyuoni wote wa kwetu Afrika Mashariki wana msimamo huo. Ama kauli yenu: "Yeye anaendelea kushika msimamo wake: ((Al-yaman wanafata muandamo wao, Oman wanafata muandamo wao, Saudia wanafata muandamo wao,)). Lile analoliona yeye halitekelezeki, basi ndio linatekelezeka". Mwisho wa kunukuu. Inaonesha kuwa kitabu changu mumekijibu bila ya kukifahamu. Nilichosema ni kuwa, ijtihadi ifanywe katika kubainisha wapi hadi wapi watu wafunge pamoja. Kwa vile, hakuna andiko lililobainisha hivyo. Ama muandamo mmoja kwa dunia nzima hili ni kinyume na andiko. Kwa hivyo, wakiwa wanavyuoni wa zamani wamefanya ijtihad hio, sisi tunafata ijtihad yao kwa vile hapa ni mahala pa ijtihad na haikugongana na andiko. Ama madai yenu nyinyi ni kinyume na andiko lilivyoonesha.

MNASEMA

"Kuna suala moja la nyongeza tunapenda tumuulize ndugu yetu Juma: Hata kama hizo nchi alizozitaja ( Al-Yaman , Oman , Misri na Saudia) hazijakubaliana kufuata muandamo mmoja, je hakuna uwezekano (japo wa sadfa) unaoweza kutokea kufunga siku moja ijapokuwa kila mmoja ameona mwezi katika nchi yake? Sasa tuseme kila nchi katika hizo imeona mwezi usiku wa Alkhamisi kuamkia Ijumaa - Wote si watafunga siku moja ya Ijumaa? Basi huo ndio utekelezaji aliosema hautekelezeki. Ni wazi kuwa unatekelezeka.

JAWABU

Munaendelea kuuliza masula haya kwa sababu masuala yenu mumeyajenga katika kitu nisichokisema kamwe. Wapi nimesema kuwa "Hilo halitekezeki" hata mukauliza masuala haya?

9

10

11