HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.0%

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s. Mwandishi:
Kundi: VITABU VYA HADITHI

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

Mwandishi: AMIRALY M.H.DATOO
Kundi:

Matembeleo: 27402
Pakua: 7867

Maelezo zaidi:

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 13 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 27402 / Pakua: 7867
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

Mwandishi:
Swahili

9

HADITH ZA MTUME (s.a.w.w) NA MA-IMAMU (a.s)

KUSEMA UONGO

498. Anas Ibn Maliki Khisal-i-Sadduq, Uk. 321: Anaelezea kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema: "Chukueni mambo sita kutoka kwangu, na mimi nakubalia, na kutoa dhamana (Ya wewe kuingizwa Jannat)

1. Usiseme uongo

2.Unapo toa ahadi, usivunje

3. Unapo pewa amana na wengine, basi uwemuaminifu

4. Tazama chini ( usitende dhambi ).

5. Chunga heshima yako

6. Idhibiti mikono yako na ulimi wako.

499. Amesema Imam Al Hassan al-'Askari(a.s) : "Iwapo maovu yote yatawekwa katika nyunba moja, basi ufunguo ( wa milango yake ) itakuwa ni uongo ."[213] .

500. Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin(a.s) : "Jiepusheni na kusema uongo hata kama ni uongo mgogo au mkubwa, kama kwa wadilifu au unasema kwa kdhihaki, kwasababu mtu anapo sema uongo mdogo basi anaweza kudiriki kusema uongo mkubwa pia.[214] .

501. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : Wakati mmoja Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . aliulizwa kuhusu umbali baina ya ukweli na uongo naye akiwa akionyesha umbali huo baina ya macho yake na maskio yake kwa vidole vinne katika kutoa jibu hilo, "Kile majo yako yanayooonani ukweli na mengi na yale yanayo sikilizwa na maskio yako ni sehemu kubwa ni uongo."[215] .

502. Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) : "Kwa hakika Allah swt ameyawekea maufuli maovu fulani, na ufunguo wake Allah swt ameweka katika pombe, lakinimaovu yatokanayo na kusema uongo ni zaidi hata kuliko pombe yenyewe ."[216]

503. Amesema Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) : "Muwe wasema ukweli na mujiepushe na usemaji uongo ."[217]

504. Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) : "Kwa hakika Allah swt ameya wekea maufuli maovu fulani, na ufunguo wake Allah swt ameweka katika pombe, lakinimaovu yatokanayo na kusema uongo ni zaidi hata kuliko pombe yenyewe ."[218] .

505. Amesema Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) : "Muwe wa sema ukweli na mujiepushe na usemaji uongo ."[219] .

MARAFIKI NA URAFIKI

506. Mtume Muhammad(s.a.w.w) Amesema: "Mtu anaathirika kwa imani ya marafiki zake. Kwa hivyo, muwe waangalifu kabisa katika urafiki wenu pamoja nao . " [220]

507. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) , Amesema: "Uwe rafiki wa yule ambaye atakuwa ndio heshima yako, si wewe uwe heshima yake. (Ufanye urafiki na wale walio juu yako ili wewe uweze kupata maendeleo kutokana na urafiki huo).[221] .

508. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema: "Ndugu yangu mpenzi ni yule (anayenitambulisha) makosa na kasoro zangu.[222]

509. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Amesema: "Kwa hakika kuna marafiki wa aina tatu kwa ajili ya Muislam:

1. Rafiki anayesema mimi niko pamoja nawe iwapo upo hai au umekufa: Na hili ndio matendo yake.

2. Rafiki anayesema mimi nipo rafiki wako hadi ukingoni mwa kaburi na nitakuacha:hawa ni watoto wake.

3. Rafiki anayesema mimi nitakuwa nawe hadi pale utakapo kufa:hii ni mali ambayo ataiacha humu duniani kwa warithi wake baada ya kifo chake.[223]

Tanbih Kutokana na riwaya hii, na kama hizi sisi tunaelewa kuwa kitu ambacho kitakuwa pamoja na huyo mtu aliye kufa na kuaga dunia hii katika siku ya Qiyamah imani na matendo yake mema. Na suala hili limezungumziwa katika ahadithi nyingi sana za Kiislam na vile vile katika ayah za Qur'an tukufu, kwa mfano:

510. Allah swt anatuambia: Wale walio amini na wakatenda mema watakuwa na raha na marejeo mazuri. (Qur'an, 13:29).

511. Allah swt anatuambia: Hakika wale walio amini na wakatenda mema - hakika Sisi hatupotezi ujira wa anaye tenda mema. (Qur'an,18: 30).

512. Allah swt anatuambi: Hakika wale walio amini na wakatenda mema mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi. (Qur'an, 18: 107).

513. Allah swt anatuambia:" Hakika walio amini na wakatenda mema Arrahmani Mwingi wa Rehema atawajaalia mapenzi. (Qur'an,19: 96).

514. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Muwe waangalifu katika kutafuta marafiki wa kweli na mujaribu kuwafanyia majaribio, kwa sababu wao watakuwa ndio msaada wenu pale mnapokuwa katika hali nzuri na watetezi wenu pale mtapokuwa katika shida na matatizo."[224]

515. Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin(a.s) : "Kukutana pamoja na wacha Mungut kunawaleteeni mema ."[225]

516. Al Imam Zaynul 'Abediin(a.s) . Amesema: "Jitahadharisheni na urafiki wa watendao madhambi, na kuwasaidia madhalimu ."[226]

MARAFIKI WASIO WEMA

517. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Anayetafuta uhusiano na marafiki wa wale wanao wadhalilisha wapenzi wa Allah swt basi watambue kuwa wao wamemuasi Allah swt ."[227]

518. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema: "Mnapojulishwa kuhusu marafiki zenu wanapotenda maovu, nendeni mumwambie: Ewe fulani bin fulani ! Ama acha kutenda madhambi au ukae mbali nasi: Na hapo utengane naye hadi atakapo acha kutenda maovu.[228]

519. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili kutoka baba yake Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . ambaye Amesema kuwa baba yake Al Imam Hussein ibn Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Amesema: "Ewe mwanangu! Jichunge na makundi matano na kamwe usifanye urafiki nao, wala usiongee nao na wala usifanye urafiki pamoja nao. Kwa hayo Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . alimuuliza baba yake Je ni makundi gani hayo matano. Imam(a.s) . alimujibu: Jitahadharishe na wala usifanye urafiki pamoja na yule msema uongo kwa sababu yeye ni kama mazua mazua anaye kufanyia vitu vya mbali vikawa karibu, na anakifanya kiwe mbali kile ambacho kiko karibu nawe.[229]

Jihadhari na usifanye uhusiano pamoja na mtu ambaye hana tabia njema, kwa sababu atakuuza kwa thamani kwa tonge moja au hata chini ya hiyo. Jihadhari na wala usifanye uhusiano na bahili kwa sababu yeye atakunyima kutoka mali yake pale wewe utakapo hitaji hasa. Jihadhari na usifanye urafiki pamoja na mpumbavu, kwa sababu yeye atataka kukufaidisha wewe lakini kwa uhakika anakudhuru zaidi. Jihadhari na usifanye uhusiano pamoja na yule ambaye hawajali ndugu na maJama'a zake, kwa sababu mimi nimemona mtu kama huyo akilaaniwa katika kitabu cha Allah swt (yaani Qur'an Tukufu) katika sehemu tatu.

Nayo ni: Sura Al Baqarah, 2, Ayah ya 27; Wanao vunja ahadi ya Allah swt baada ya kwisha ifunga, na wakayakata aliyo amrisha Allah swt kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye Khasara. Sura Al-Raa'd, 13, ayah ya 25 Na wale wano vunja ahadi ya Allah swt baada ya kuzifunga, na wanakata aliy amrisha Allah swt yaungwe, na wanafanya fisadi katika nchi: Hao ndio watakao pata laana, na watapata Nyumba mbaya. Sura Muh'ammad, 47, ayah 22 Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe Jama'a zenu ?

520. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Ewe Kumail ! sema kile kilichopo katika hali yoyote ile. Uwe marafiki pamoja na wacha Allah swt na jiepushe na watendao maovu, jiweke mbali na wanafiki na usiwe pamoja na wadanganyifu na wahalifu na wahaini ."[230]

KUWAHUDUMIA WATU

521. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Yeyote yule atakaye mpuuzia ndugu yake Muislam mwenzake matatizo na shida za dunia hizi, basi Allah swt atampunguzia shida na matatizo yake huko Akhera ." [231]

522. Amesema Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Kwa hakika, maombi ya shida za watu zinazokuijia wewe ni miongoni mwa neema na baraka za Allah swt juu yako. Hivyo usisikitike kwa sababu ya neema na baraka hizi ."[232]

523. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Popote pale utakapoona ndugu yako Muislam ana shida, jaribu kuangalia kama utaweza kumusaidia. (Usimpuuze mpaka akutamkie shida zake.) "[233]

524. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kuwa amenakili kutoka mababu zake(a.s) . ambao wamemnakili Mtume Muhammad(s.a.w.w) akisema: "Yeyote yule anayemlisha muumin aliye na njaa akashiba basi Allah swt atamlisha mpaka ashibe kutoka matunda ya Jannah; Na yeyote yule atakaye mvisha nguo yule aliye na shida za nguo, Allah swt atamvisha nguo zilizofumwa na za hariri, na yeyote yule atakaye mumalizia kiu muumin basi Allah swt atamjaalia kinywaji kilichopigwa lakiri; Na yeyote atakaye msaidia muumin kupunguza shida yake, basi Allah swt atamweka chini ya Arshi yake siku ya Qiyama siku ambayo hakutakuwa na kivuli chochote isipokuwa kivuli cha Arshi yake."[234]

525. Mtume Muhammad(s.a.w.w) Amesema: "Watu wanamtegemea Allah swt kwa ajili ya riziki, kwa hiyo mpenzi miongoni mwa watu kwake Allah swt ni yule ambaye anawasaidia wale watu wanaomtegemea Allah swt na kuwafanya watu wa familia ya nyumbani wakawa na furaha."[235] .

526. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Yeyote yule atakaye wasaidia Waislam ndugu zake wakati wa shida, Allah swt atamwondolea shida na matatizo sabini na tatu, moja ambayo ni ambayo iko humu duniani na sabini na mbili zingine zitakazo kuwa wakati wa shida kubwa, ambapo watu watakuwa mashughuli katika mambo yao ya binafsi (katika Akhera) ." [236]

KUTOA MIKOPO

527. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Yeyote yule anayeijiwa na ndugu yake Muislam kwa ajili ya kukopa na kama yeye hampi mkopo, basi Allah swt atamharamishia kuingia Jannat siku ambayo waja mema watakuwa wakilipwa na kufidiwa ." [237]

528. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Yeyote yule anayetakiwa na ndugu yake Muislam kwa kukopeshwa na kama yeye hamkopeshi mkopo, Allah swt atamzuia kuingia Jannat siku ambayo waja wema watakuwa wakilipwa mema yao ." [238]

KUWASAIDIA WENYE SHIDA

529. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Waulizeni maswali walio elimika, muongee pamoja na wale wenye hekima, na mujihusishe pamoja na masikini."[239]

530. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Sababu mojawapo ya kuteketea na kupotea kwa mali na utajiri wa mtu ni kule kutowajali na kutowasaidia wale wenye shida."[240]

531. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Mtume Muhammad (s.a.w.w) amemnakili Allah swt kwa kuameambiwa usiku wa Mi'raj: Ewe Ahamad! Mapenzi yangu ni kule kuwapenda masikini. Wafanye masikini wawe karibu nawe na uwaweke karibu nawe ili mimi niweze kukufikia wewe .."[241]

532. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Yeyote yule anayemmalizia muumin njaa yake kiasi kwamba akaridhika kikamilifu, basi hakuna binadamu yeyote miongoni mwetu au miongoni mwa Malaika wanaojua kiasi cha thawabu yake siku ya Qiyamah isipokuwa Allah swt mmiliki wa Malimwengu yote. Na aliongezea: Kumlisha Muislam aliye na njaa ni njia moja kubwa sana ya kuomba Tawba( usamehevu)."[242]

Baada ya hapo alisoma ayah ya Qur'an Tukufu Sura Al-Balad, 90, ayah 14 - 16. Au kumlisha siku ya njaa Yatima aliye Jama'a, Au masikini aliye vumbini.

ZAWADI NA KUWAFURAHISHA MUUMIN

533. Mtume Muhammad(s.a.w.w) Amesema: "Wakati sadaka inapotolewa na mtu kutoka mikononi mwake, basi hiyo sadaka inasema: Mimi nilikuwa kitu cha kwisha, lakini wewe umenipa maisha; Mimi nilikuwa sina thamani sasa wewe umenifanya niwe na thamani kubwa; mimi nilikuwa ni adui nawe umenifanya mie kuwa rafiki; Wewe ulikuwa daima ukinilinda na kunihifadhi lakini sasa mimi nitakulinda na kukuhifadhi hadi siku ya Qiyamah ." [243]

534. Amesema Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) : "Yeyote yule atakaye mfurahisha Muumin, basi kwa hakika kwanza kabisa amemfurahisha Allah swt, na pili amemfurahisha Mtume Muhammad (s.a.w.w) na tatu ametufurahisha sisi Ahlul Bayt (a.s) "[244]

535. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Allah swt ameweka mahitaji ya wale wasio na uwezo katika mali ya matajiri. Kwa hivyo atakapokuwa mtu asiye na uwezo akabakia katika hali ya njaa basi ni kwa sababu matajiri wamemnyima haki yake ."[245] .

536. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema: "Kwa kiapo cha Allah swt! Yeyote yule anayeizuia mali yake isiwasaidie Mumin wenye shida basi siku ya Qiyamah kamwe hawataonja chakula cha Jannat wala Kinywaji kilichopigwa Lakiri."[246]

SADAKA NA MISAADA

537. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Sadaka inalipia madeni na inaongezea katika barakah ."

538. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili riwayah kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa: "Sadaka inamwepusha mtu na ajali mbaya ."

539. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema kuwa: "Mtu yeyote yule aliye mja wa Allah swt akiwa Mumin akatoa Sadaka, basi Allah swt baada ya kifo chake huyo mtu huwaweka vyema na kuwasaidia wananyumba yake katika hali njema." Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akaendelea kusema: "Faida ya kutoa Sadaka ni kwamba inamsaidia kulipia madeni na viile vile kuongezea katika barak a."

540. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Kusaidia na kutoa sadaka vyote hivyo vinaondoa umasikini na hurefusha umri wa mtu. Na yule anayetoa huweza kuepukana na aina sabini za ajali mbaya .

541. Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) . katika kuelezea tafsiri ya aya, ya Qur'an Tukufu, Sura Al-Layl, 92, Ayah ya 5 na 6: Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali Ama mwenye kutoa na akamcha Mungu. Ndipo amesema kuwa; Allah swt ndivyo anavyo walipa wale watendao mema, kwa mema yao mara kumi, au hata mara laki moja na hata zaidi ya hapo. Na vile vile amesema kuwa: anayetoa katika njia ya Allah swt basi Allah swt humjaalia kila aina ya tawfiqi katika kazi hiyo ya khairi."

542. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amemnakili Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa "Mtu yeyote yule ambaye anamwamimi Allah swt kuwa atamlipa na atamwongezea zaidi ya kile anacho kitoa basi huyo mtu kwa moyo mkunjufu na bila aina ya ubakhili wowote atatoa sadaka na misaada kwa wingi kabisa."

543. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amemnakili Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa: "Siku ya Qiyama ardhi itakuwa imepata moto kupita kiasi na mumin watakuwa katika kivuli na kivuli hicho itakuwa ni kile alicho kuwa akitoa Sadaka ."

544. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili riwayah moja kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akisema kuwa: "Enyi watu! Toeni sadaka bila shaka sadaka inaongezea katika mali yenu, na hivyo mtoe sadaka na Allah swt atawarehemu ."

545. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . amesema kuwa: "Toeni sadaka mjipatie riziki ."

546. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Toeni sadaka mjiongezee riziki yenu. Bila shaka anayeamini kuwa Allah swt hulipa mambo yote. Basi yeye huwapa sadaka masikini kwa kupita kiasi. Allah swt humjaalia riziki kwa njia mbalimbali kwa kile huyu mtu akitoacho katika mali yake ."

547. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . amenakili riwayah kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akisema kuwa: "Kuwa na akida ya Tawhid ni nusu ya sehemu ya dini, enyi watu! Toeni Sadaka ili mpate riziki zaidi ".

548. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . ametoa riwayah kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa: "Kuwa mali halisi ya mtu ni ile ambayo yeye ametolea sadaka ."

549. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema kuwa: "Toeni Sadaka asubuhi na mapema ili balaa zisiwafikieni katika siku nzima ."

550. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili riwayah kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . kuwa: "Sadaka ni kinga dhidi ya moto wa Jahannam ."

551. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alikuwa akisema: "Enyi watu muwatibu wagonjwa wenu kwa kutoa Sadaka ."

552. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . katika Nahjul Balagha amesema kuwa: "Mnapoona riziki yenu inapungua na kuwa finyo basi muwe mkitoa sadaka ndivyo mtakuwa mkifanya biashara na Allah swt ."

553. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Imani ya muumini inakuwa na sifa nne za lazima, "Awe na tabia njema, "Awe mkarimu na mwepesi wa kutoa "Asizungumze zaidi ya yale yanayo takikana (hazungumzi mambo ovyo ovyo) " Hutumia kile kiasi kinacho takiwa ,siyo mfujaji (anaotoa katika njia ya Allah swt ).

554. Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) . amesema kuwa: "Iwapo mimi nitakwenda Hijja moja basi afadhali niwafanye huru watumwa kumi, lakini iwapo mimi nitajichukulia jukumu la kuwalisha familia ya Waislamu ambao wanashida ya chakula na ambao wanaishi kwa njaa nikawamalizia shida zao, nikawavalisha nguo wale ambao hawana nguo, na nikawarudishia heshima yao miongoni mwa watu, basi mimi ninaona jambo hili ni afadhali na bora zaidi kuliko hata kwenda kuhiji Hijja sabini. "

555. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . aliijiwa na mtu mmoja na aliyeuliza, "Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w)! Mimi ninazo pesa na utajiri je ni jambo gani afadhali nitoe sadaka au nimnunue mtumwa na kumfanya huru ?"

556. Kwa hayo Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . alimjibu kuwa: "Kuwa mimi ninaonelea kuwa kutoa Sadaka ni afadhali zaidi."

557. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Siku moja Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwuliza Maimuna binti Harun, Je Kijakazi wako amekuwaje? Akasema Maimuna kwa hayo alimjibu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , 'Ewe Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ! Mimi nimemfanya huru.' Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwambia "Iwapo kama wewe ungelichukua jukumu la kumlisha, kumtunza, kumsaidia na kumwonea huruma basi ingekuwa afadhali zaidi."

558. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Muwatibu wagonjwa wenu kwa Sadaka, na muzuie maafa kwa kuomba dua na kutoa sadaka muongezee riziki zenu zipanuke, na kwamba Sadaka inawaepusheni na mitego ya mashetani sabini ."

559. Siku moja walikuja wagonjwa wakilalamikia magonjwa yao mbele ya Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) ., naye akawaambia; "Nendeni mtoe Sadaka kwa ajili ya magonjwa yenu na mtapona, iwapo mtu atatoa Sadaka kwa kile akitumiacho kwa siku dharura wake, basi Allah swt huahirisha hata kifo chake na vile vile humwepusha na ajali mbaya ."

560. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . aliulizwa na Sahaba mmoja: "Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ! Mimi watoto wangu wawili wamefariki na amebakia mtoto wangu mdogo." Kwa hayo Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . kamwambia: "Basi toa Sadaka kwa niaba ya mtoto wako huyo." Na siku moja Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . alipomtembelea huyo mtu akamwambia, "Mwambie mtoto wako huyo atoe Sadaka kwa mkono wake walau kiasi kidogo chochote kile au hata kama kitakuwa ni kipande kidogo tu. Utambue wazi kuwa kiasi chochote kile hata kikiwa kiasi gani kama kitatolewa kwa roho safi basi mbele ya Allah huwa ni kipenzi, kwani Allah swt ameelezea kuwa: Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! Na anaye tenda chembe ya uovu atauona! (Qur'an,99: 7 – 8).

561. Vile viel Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . alimwelezea kuwa: "Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu, Surah Al-Balad,90, Ayah11 - 16 Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? Kumkomboa mtumwa; Au kumlisha siku ya njaa Yatima aliye jamaa, Au masikini aliye vumbini

"Hivyo ewe Sahabi uelewe kuwa Allah swt anaelewa wazi wazi kuwa si watu wote wenye uwezo wa kuwanunua na wenye kufanya huru watumwa hivyo yeye ameweka thawabu hizo hizo kwa wale watakao toa Sadaka au watakao walisha yatima na masikini."

562. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . alijiwa mtu mmoja mbele yake na kuelezea habari za mtoto wake, na kwa hayo Al Imam akamjibu: "Toa Sadaka kwa niaba yake." Na mtu huyo akajibu kuwa "Sasa mtoto wake amekuwa na umri yaani amekuwa kijana." Basi Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . alimwambia kuwa "Mtoto wako atoe Sadaka kwa mkono wake, hata kama itakuwa ni kipande cha mkate, na hapo ndipo Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . alisema riwayah ya Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) . kuwa: "Katika Israil alikuwa mtu mmoja aliyekuwa akimpenda mno mtoto wake, na akaona katika ndoto yake anaanmbiwa kuwa, mtoto wako huyo umpendaye mno atakufa usiku wa ndoa yake. Kulipowadia usiku wa arusi baba mzazi wa mtoto huyo, usiku kucha akawa katika wasiwasi na hakupata usingizi na kamwe hakupata raha usiku huo. Na kulipo pambazuka asubuhi na mtoto alipotoka chumbani mwake akiwa hai basi baba yeke alimwuliza 'Ewe mwanangu! Je katika usiku huu wako wa kuamukia leo umefanya mema yoyote?' Kwa hayo mtoto akajibu "Ewe baba yangu! hakuna jambo la maana sana lililotendeka, bali alitokezea masikini mmoja akaja mlangoni kuomba chakula, alikuwa na njaa na kile chakula walichokuwa wameniwekea, mimi nikampa chakula chote huyo mtu aliyekuja kuomba.' Kwa hayo baba yake akasema "Kwa sababu hii tu ndiyo Allah swt amekuondoshea balaa kubwa iliyokuwa ikupate wewe usiku huo."

563. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema kuwa: "Kwa kutoa Sadaka kwa mkono wako mwenyewe basi unajiepusha na ajali mbaya, unajiepusha na balaa na maafa sabini na mitego ya mashetani sabini na ambamo kila shetani yuko anakwambia 'ewe fulani! Usitoe Sadaka kamwe."

564. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Mgonjwa atoe Sadaka kwa mkono wake mwenyewe na anayempa amwambie amwombee dua ".

565. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) katika hadith zake amesema kuwa: "Mkono uliye juu yaani mtoaji ni afahali kuliko mkono ule ulio chini yake, yaani mpokeaji ."

566. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema kuwa: "Kuna aina tatu ya mikono wa " kwanza ni mkono ule wa Allah swt ambao uko juu kabisa na kwa hakika neema zote ni za Allah swt, " mkono wa pili ni ule mkono wa yule mtu anaye toa, ambaye anatoa katika njia ya Allah swt na " mkono wa tatu ni wa yule anaye pokea ambao mkono uliochini wa yule anayetoa. Kwa hivyo enyi watu chochote kile kinachobakia miongoni mwenu mtoe katika njia ya Allah swt na musikalifishe nafisi zenu".

567. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alikuwa amemfanyia usia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ; Ewe Ali! Ninakufanyia usia wa mambo mema machache na uyakumbuke vyema.

Ewe Allah swt umsaidie Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Baada ya hapo wakati akifanya usia, Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alisema: Ama kuhusiana na sadaka tafadhali usiwe na mnunguniko wowote. Utoe kiasi kwamba mpaka uhisi kwamba wewe umefuja mali yako, lakini utambue wazi kuwa hiyo sio ufujaji bali hiyo umetoa katika njia ya Allah swt."

568. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema kuwa kuna riwayah kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa "Toeni Sadaka, angalau hata kwa sa' ya tende, na kama sa' moja hiyo hamnayo basi mtoe tende kwa kiganja kimoja na hata kama hivyo haitawezekana basi mtoe tende kiasi chochote kile na kama hivyo haitawezekana basi mtoe angalau kokwa moja ya tende, na kama hivyo pia haitawezekana basi yule masikini aliyekuja kuwaomba mumwambie maneno mazuri na matamu na maneno matakatifu katika kumwelezea kuwa hakuna chochote, na hayo pia ni sadaka. Kwa sababu isitokee Siku ya Qiyama kwamba Allah swt atakapo kuuliza hesabu ya neema alizokujaalia akakuambia 'Ewe mja! Mimi nilikupa mambo chungu nzima, sasa hebu angalia nafsini mwako je kwa kutumia neema hizo wewe umejiandalia nini?' Na hapo wewe utaangalia sehemu zote nne za dunia na utajawa na masikitiko, na utakuta hakuna jambo lolote lile litakalo kuokoa dhidi ya adhabu za Allah swt."

569. Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) . amesema kuwa: "Mtoe tende kiasi fulani kwani itawaokoa na moto wa Jahannam , mpanue riziki zenu na mteremshiwe riziki nyingi kwa kutoa Sadaka na kupitia dua mziondoe balaa na shida zenu." Mkumbuke kuwa kwa kutoa Sadaka hamtapungukiwa katika mali yenu. Na miongoni mwa jamaa zenu wanapokuwa na shida muwasaidiapo hiyo siyo Sadaka bali hiyo ni wajibu wenu."

570. Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) . amesema kuwa: "Kulikuwa na mja mmoja aliyekuwa akifanya ibada ya Allah swt kwa umri wake wa miaka themanini. Siku moja alimwona mwanamuke mmoja mzuri aliyekuwa akipendeza naye akawa ameingia katika mtego wake. Yeye alitimiza matamanio yake visivyo halali na mara akatokezea Malakul mauti (malaika anayetoa roho). Ulimi wake ulifunga kuongea na jasho lilianza kumtoka na kutokwa kwa roho na mara hapo alipita masikini akiomba. Basi mtu huyu ambaye alikuwa katika hali ya kukata roho alimwambia yule masikini kwa ishara kuwa mahala fulani kuna mkate hivyo auchukue hivyo aweze kula huyo masikini, na masikini huyo alivyoelekezwa akauchukua mkate akaondoka zake. Kwa hiyo ikatokea kwamba Allah swt aliibatilisha ibada zake za miaka themanini kwa sababu ya kuzini na ikatokea kwamba Allah swt akamsamehe madhambi yake yote kwa sababu ya kutoa Sadaka kwa moyo mkunjufu."

571. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . amesema kuwa; " Katika zama za Bani Israil kuliwahi kutokea baa la njaa ambao uliendelea kwa muda wa miaka mingi. Katika wakati huo ikatokezea kwamba bibi kizee mmoja akiwa amekabwa na njaa hali ya juu alikuwa ameketi akiwa na kipande kidogo cha mkate huku akitaka kukila kipande hicho, mara akasikia mlangoni sauti ikisema ya masikini aliyekuwa amekuja kuomba: 'Ewe mja wa Allah swt! Mimi nakufa kwa njaa naomba unisaidie, bibi kizee huyo akajiambia kwa hakika Sadaka ndiyo wakati huu muafaka wa kutoa, na kile alichokuwa akila akakitoa haraka akampa huyo aliyekuwa akiomba.

Bibi kizee huyo alikuwa na mtoto mmoja aliyekuwa amekwenda porini na ghafla kule alishambuliwa na mnyama. Kwa kusikia sauti ya mtoto wake huyo bibi kizee ikimwita, alikimbia kumfukuza mnyama huyo na kwa muujiza wa Allah swt ni kwamba, Allah swt alimtuma Malaika Jibrail(a.s) kwenda kumwokoa mtoto huyo katika mdomo na mabano ya mnyama wa huyo muuwaji, na Malaika Jibraili(a.s) . akamwambia 'Ewe bibi kizee! Je umefurahi sasa? Kwa kile ulichokitoa sadaka basi Allah swt naye amekulipa mema yake."

572. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema kuwa: " Mfanye mema katika hali ya shida na ufakiri, na wema huo ni Sadaka. Toeni Sadaka kama itakuwa ni kiasi gani kwa udogo wake. Mnaweza kutoa kiasi cha tende mkajiokoa na Jahannam. Kwa hakika udogo huo siyo hoja na Allah swt ataulea udogo huo kama kwamba nyie mnavyo walea watoto wadogo wanaonyonya maziwa, na siku ya Qiyama wakati mema yenu hayo (mliyokuwa mkisema ni madogo) yatakapoletwa mbele yenu mtaona kuwa ni sawasawa na ukubwa wa milima mikubwa sana."

573. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . ameseama kuwa Allah swt anasema kuwa : "Hakuna kitu kingine mbali na Sadaka ambacho mtu anaweza kumpatia mtu mwingine kidhahiri, na kwa hakika mimi ndiye wakili wake musitahiki, na mimi ninayepokea kwa mikono Sadaka hiyo halafu hata ikiwa kama ni tende kidogo haidhuru mimi ndiye ninaitunza, kama vile mwanadamu anavyowatunza watoto wake.

Siku ya Qiyama huyo mtoa Sadaka atastaajabishwa mno kwa Sadaka zake ndogo alizokuwa akitoa zimekuwa kubwa kama milima ya Uhud, milima mikubwa sana."

574. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili riwayah kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa: "Toeni Sadaka asubuhi na mapema kwa sababu kunaondoa balaa kwa siku nzima ."

575. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Kwa kutoa Sadaka asubuhi na mapema basi mtoa Sadaka huepukana na kila aina ya matatizo na mabaya yote kwa siku nzima ."

576. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Toeni Sadaka asubuhi, na kwa mapenzi kabisa, mwenyewe kutoa Sadaka amebahatika. Basi humwomba Allah swt amani kutokana na balaa zote zilizoko ardhini na mbinguni, na kwa hakika Allah swt humjaalia hivyo kwa sababu ya kutoa Sadaka ."

577. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anaelezea kuwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) alimwusia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . kuwa: "Ewe Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s).! Sadaka huondoa balaa ambazo lazima zitatokezea, na kwa kutenda mema pamoja na ndugu na majamaa kunarefusha umri .

Ya Ali! Iwapo jamaa na ndugu ni watu wenye shida, basi kuwapa Sadaka hao haitakuwa ni Sadaka. Ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) .!Kusema maneno bila vitendo ni ya bure hayana maana, na Sadaka bila kuwa na nia nayo haiwi Sadaka ."

578. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema kuwa: Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwuliza mtu mmoja "Je leo umefunga Saumu?" Mtu huyo alijibu "La hapana! Ewe Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) " Tena Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwuliza: "Je leo umeshawahi kumtembelea aliye mgonjwa?" Naye akajibu: "Hapana! Ewe Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) " Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliendelea kumwuliza naye aliendelea kumjibu hapana hakufanya hivyo.

579. Mwishoni Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliendelea kumwuliza: "Je umemlisha masikini yeyote?" Naye akajibu: "Hapana Ewe Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) !" Na hapo ndipo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alipomwambia huyo mtu: "Nenda kwa wananyumba wako, nenda ukawatendee na uwe nao kwa mema na uwawie wema, basi hayo ndiyo yatakuwa Sadaka yako kwao."

580. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . ameripoti riwayah kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ambaye ameseama: "kwa baraka za Sadaka Allah swt humwondolea mwenye kutoa Sadaka balaa sabini, ambamo kuna magonjwa, madhara yatokanayo na moto, kuzama maji, kufunikwa na majumba mpaka kufa na atamwepusha ili asiwehuke au asiwe mwehu."

581. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . ameripoti riwayah kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . kuwa: "Ili kutaka kuepukana na shari za madhalimu basi toeni Sadaka ."

582. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anaelezea kuwa: Siku moja Myaudi mmoja likuwa akienda kukata miti porini na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwangalia na kuwaambia Ma-Sahaba wake : "Myahudi huyu leo ataumwa na nyoka na kifo chake kitasababishwa na sumu ya nyoka. Myahudi huyo kama kawaida yake alikata kuni na alijitwisha kichwani mwake na akarud akiwa salama. Na tena Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alipomwona Myahudi huyo akamwambia ateremshe mzigo wa kuni huo na auweke chini. Na Myahudi akafanya hivyo alivyoambiwa, na katika mzigo huo wa kuni wakaona kuna nyoka mweusi mwenye sumu kali sana huku akiuma kuni. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwuliza Myahudi yule,'Je wewe leo umefanya jambo gani?' Myaudi huyo akasema: Mimi nimekata kuni na kuzifunga tu, lakini wakati nilivyokuwa nikirudi nilibakiwa na vipande viwili vya mkate na kipande kimoja mimi nikala na kipande kimoja nikampa masikini Sadaka. Hapo ndipo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akasema kwa kiapo cha Allah swt ni kwa sababu ya Sadaka ndiko balaa hii imekuondokea, kwa hakika Sadaka humwepusha mtu na ajali mbaya."

583. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . siku moja alikuwa pamoja na Ma-sahaba wake katika Masjid Nabawi, na upande mmoja wa ukuta ukaanguka chini. Kulikuwa na mtu mmoja hapo ambaye aliponea chupu chupu tu, kulianguka kizingiti kizito karibu na muguu wake. Lakini yeye bahati nzuri hakupata udhuru wowote. Hapo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . aliwaambia Ma-sahaba wake, hebu mwulizeni huyu mtu leo amefanya matendo gani? Na wakati alipoulizwa huyo mtu akasema: "Mimi nilipotoka nyumbani mwangu leo nilikuwa na kokwa chache za tende. Na kukatokezea na masikini mmoja akaniomba basi mimi nikampa kama Sadaka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . akajibu "Basi kwa sababu hiyo tu leo, Allah swt amekuepusha na balaa hii ambayo ingekumaliza."

584. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . siku mmoja alimwambia Sahabi wake Mayassari kuwa: "Ewe Mayassari je wajua kuwa wewe umeisha fikiwa na mauti mara nyingi, lakini Allah swt amekuongezea umri wako zaidi kwa sababu ya wewe kuwa mkarimu na kuwajali jamaa na ndugu zako umewawia wema ndio maanake umri wako umezidi."

585. Al Imam Hasan al-'Askary(a.s) . anasema kuwa: " Wakati mmoja Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akiwa pamoja na wenzake walikuwa safari na wenzake hao walikuwa na mali nyingi sana. Na njiani wakapata habari kuwa wako majambazi wanaowapora matajiri mali zao. Kwa kusikia hayo hao matajiri walianza kutetemeka na wakaingiwa na hofu na wakaanza kumwuuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . je tufanyeje sasa? Na kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akawajibu: 'Mkabidhini mali yenu yule ambaye ataweza kuifadhi mali yenu, na kwa kweli ataitunza sana na baada la kupungua hata itazidi pia, sio hayo tu na pale mutakapokuingiwa na shida ya mali yenu basi yeye kila siku atawarudishia pamoja na nyongeza yake. ' Kwa kusikia hayo hao wenzake aliokuwa nao katika safari wakamwuliza : "Je ni nani huyo?" Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akawajibu: "Yeye ni miliki wa malimwengu zote Allah swt." Basi hao wenzake wakamwuliza je tunaweza kumkabidhi vipi mali zetu hizi? Hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akawaambia: Toeni Sadaka muwape wale wanaostahiki. Kwa kusikia hayo wakauliza ewe mjukuu wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ! Hapa tulipo tutawatoa wapi hawa masikini na mafakiri tutawatafuta wapi? Basi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . aliwajibu: munuie kuwa sehemu moja ya mali yenu mtatoa Sadaka basi na msiwe na wasiwasi Allah swt atailinda mali yenu yote.

"Wale waliokuwa naye pamoja safarini walinuia hivyo kama vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alivyowaambi,a na Imam(a.s) . akawaambia sasa nyie mko katika amani ya Allah swt, na wakiwa wanaendelea na safari majambazi hao walikumbana nao na kwa kudura za Allah swt wao wakawapita salama usalimini bila ya kudhurika na kusumbuliwa, hadi wakafika mwisho wa safari yao. Waliopofika tu mwisho wa safari yao wao wakatoa sehemu moja walizokuwa wamenuia kama Sadaka na sehemu iliyo bakia walifanyia biashara yao, na Allah swt akawajaalia baraka kiasi kwamba wakapata faida hata zaidi ya mara kumi."

586. Siku moja Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alikuwa Mina pamoja na Ma-sahaba wake wakila zabibu. Mara akatokezea mtu mmoja na akaomba. Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kwa mkono wake akachukua fungu moja la zabibu akampa basi huyo akakataa kupokea, akisema "mimi sitaki zabibu hizi bali ninataka pesa tasilimu kama zipo ndio nichukue". Basi kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akamwambia "Allah swt atakuzidishia" na Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . hakumpa chochote, baada ya muda si muda huyo mwombaji tena akarudi kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . na akamwambia Imam(a.s) . "Nipe zile zabibu ulizokuwa ukitaka kunipa." Na Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akamwambia Allah swt atakutafutia njia yake, pamoja na hayo Imam(a.s) . hakumpa chochote.

Wakati bado wakiwa wamekaa akatokezea mtu mwingine kuja kuomba, na Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alitoa mbegu tatu tu za zabibu akampa huyo mwombaji. Mwombaji huyo alianza kumshukuru Allah swt kwa kumjaalia riziki hiyo na akaonyesha shukurani kwa ujumla. Kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alichota mikono ya zabibu miwili akampa na hapo tena huyo mwombaji akaendelea kumshukuru Allah swt zaidi na zaidi. Kwa kusikia hayo tena Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akamwambia mtumwa wake kama tuna pesa zozote zile tulizo nazo kwetu mpe huyo. Na huyo mfanyakazi wa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kwa amri yake alimpa Dirham Ishirini alizokuwa nazo. Mwombaji akiwa anachukua Dirham akasema: 'Ewe Allah swt! Nakushukuru mno sana na hakuna mwingine wa kushirkishwa nawe. Kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . nguo aliyokuwa amejifunika akampa huyo mwombaji na huyo mwombaji baada ya kuivaa na kujifunika na hiyo nguo akamshukuru Allah swt ambaye amemjaalia nguo ya kujifunika. 'Ewe Aba 'Abdillah! Allah swt akulipe kila la heri. Na baada ya kusema hayo akaondoka zake. Kwa kuona haya Ma-sahaba wakamwambia Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kuwa kila alivyoendelea yeye kumsifu Allah swt ndivyo wewe ulivyoendelea kumpa na kama asinge omba kwa kutaja jina la Al Imam(a.s) . lazima angeendelea kumpa chochote zaidi ya hayo."