HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 218%

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2 Mwandishi:
Kundi: VITABU VYA HADITHI

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2
  • Anza
  • Iliyopita
  • 11 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 22250 / Pakua: 4849
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

Mwandishi:
Swahili

11

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KWANZA

AL - BAQARAH (NG’OMBE)

﴿ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴾

47.Enyi wana wa Israil, ikumbukeni neema Yangu niliyowaneemesha, na nikawatukuza kuliko viumbe wengine.

﴿ وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا شَفَاعَةٌ وَلَا يُؤْخَذُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ﴾

48.Na iogopeni siku ambayo nafsi haitafaa nafsi kwa lolote.Wala hayatakubaliwa kwake maombezi (shufaa), wala hakitapokelewa kikomboleo; wala hawatanusuriwa.

WANAWA ISRAIL TENA!

Aya 47 - 48

MAELEZO

Enyi wana wa Israil ikumbukeni neema Yangu.

Aya hii inatilia mkazo Aya iliyotangulia, na ni maandalizi kwa yatakayokuja baada yake. Tutaonyesha katika sehemu itakayofuatia hekima ya kukaririka. Makusudio ya kukumbuka hapa ni kushukuru; yaani zishukuruni neema zangu kwa usikizi na twaa. Na nikawatukuza kuliko viumbe wengine.

Mwenyezi Mungu aliwafadhilisha kuliko mataifa mengine ya wakati huo. Herufi lam katika neno Alamin ni ya kuenea kwa kawaida, sio kuenea kwa kiuhakika. Inatosha kuwa ubora ni katika upande mmoja na sio pande zote. Upande ambao Waisrail wamepambanuka na watu wengine ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwapelekea idadi ya Mitume; kwa mfano Musa, Harun, Yoshua, Zakaria na Yahya na wengineo. Wote hao ni Waisrail. Vyovyote ilivyo, kuwa bora kwao kwa watu wa zama zao kwa upande fulani, hakufahamishi kuwa bora katika kila upande kwa watu wa wakati huo; wala sio kwamba mtu wao ni bora kuliko mtu mwingine. Bali kule kuwa Mitume wengi wamekuja kutokana na kabila lao ni hoja juu yao na wala sio hoja yao, kwa sababu hilo linafahamisha kwamba wao walikuwa katika upotevu sana, ikawa kuna haja sana wapate waonyaji na wahadharishaji. Na ogopeni siku mbayo nafsi haitaifaa nafsi nyingine kwa lolote. Yaani kila mtu na lake hakuna dhahiri wala batini, hakuna kusaidiana wala kuoneana huruma.

﴿ يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ ﴾

Siku ambayo mtu atamkimbia ndugu yake. (80:34).

Wala hayatakubaliwa kwake (hiyo nafsi) maombezi (shufaa), wala hakitapokelewa kikomboleo; wala hawatanusuriwa. Yaani Kiyama ni sawa na mauti, haufai usaidizi wowote, haitafaa fidiya yoyote, hata ikiwa ghali, wala haitazuia nguvu yoyote hata iwe kubwa kiasi gani. Hakuna chochote isipokuwa Rehema ya Mwenyezi Mungu:

﴿ لَئِن لَّمْ يَرْحَمْنَا رَبُّنَا وَيَغْفِرْ لَنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴾

Kama hataturehemu Mola wetu na kutusamehe, bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliopata hasara. (7:149)

KUKARIRIKA KATIKA QURAN

Mara ya pili Mwenyezi Mungu anawaku-mbusha wana Israil neema Zake na amerudia baada ya Aya tano. Hiyo siyo Aya peke yake iliyorudiwa katika Quran, zimeka-ririka Aya nyingi hasa zile zinazofungamana na wana wa Israil pamoja na Musa(a.s.) . Wengi hujiuliza sababu ya kukaririka Aya.Wameafikiana wafasiri kwamba hekima ya kukaririka ni kutilia mkazo. Baada ya kupita siku, wakuu wa vyama, wanasiasa, wafanyibiashara na wenye mashirika wamegundua kwamba, kukar-irika jambo ndio njia nzuri ya kulipendekeza, kulikinaisha na kulifanyia propaganda. Kwa ajili hiyo ndio wakaweka mitindo mbali mbali ya matangazo, kukawa na watu maalum wa kuhusika nayo na yakawa ghali sana.

Gustave Lebon anasema katika kitabu chake kiitwacho The man and his work: Mwenye kulikariri tamko mara kwa mara hulibadilisha kuwa itikadi. Dr Gibson katika kitabu kilichotarjumiwa kwa kiarabu kayfa tufakkir (Vipi utafikiri) anasema Ibara zina sumaku zinapokaririka mara kwa mara mbele ya macho yetu na masikio yetu, zinapumbaza akili zetu kabisa. Kwa hivyo basi Quran inakariri kwa mfumo mwingine pamoja na kuzidisha makemeo na mengineyo kwa kiasi cha hekima inavyotaka.

SHUFAA (UOMBEZI)

Hapana budi shufaa iwe na pande tatu: Mwenye kuombwa, mwenye kuombewa na muombezi ambaye anakuwa kati ya hao wawili, anaomba kwa yule wa kwanza ili amsaidie wa pili ni sawa apate idhini ya yule mwenye kuombwa au la. Hiyo ndiyo Shufaa kwa viumbe. Ama shufaa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) maana yake ni msamaha na maghufira kwa mwenye dhambi; haitakuwa shufaa mbele ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa idhini yake.

Amesema mwenye Majmaul-Bayan Shufaa kwetu ni yenye kuhusika na kuondoa madhara na kuondoa mateso kwa mumin mwenye dhambi. Muutazila na Khawarij wamekanusha Shufaa ya Muhammad(s.a.w.w) kwa wenye madhambi makubwa katika umati wake, kwa maana hii tuliyoinakili kutoka kwa mwenye Majmaul-Bayan, lakini Imamiya na Ashaira wameithibitisha kwamba iko.Akili haihukumu kutokea Shufaa au kutotokea, lakini haioni pingamizi yoyote ya kupatikana. Kwa hiyo, kusihi kwake na kuthibiti kwake kutategemea kunakili kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Ambaye kumemthibitikia kunakili huko, basi ni wajibu kwake kuamini Shufaa, na kama hakuthibitikiwa basi atasamehewa. Kwa hali hiyo inatubainika kuwa shufaa si msingi wa dini na kwamba mwenye kuikanusha na huku anamwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi huyo ni Mwislamu bila shaka.

Tukirudi kwenye Aya za Quran tunakuta nyingine zinakanusha; kama ile inayosema:

﴿ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خُلَّةٌ وَلَا شَفَاعَةٌ ﴾

...Siku ambayo hapatakuwa na bishara wala urafiki wala Shufaa (uombezi).... (2:254)

Hapo inaonyesha kukanusha Shufaa kabisa.Na Aya nyingine zinathibitisha kwa sharti; kama ile inayosema:

﴿لَا تُغْنِي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا إِلَّا مِن بَعْدِ أَن يَأْذَنَ اللَّـهُ لِمَن يَشَاءُ وَيَرْضَىٰ ﴾

....Hautafaa chochote uombezi (shufaa) wao isipokuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia. (53:26)

Tukiziunganisha Aya mbili hizi na tukazikusanya pamoja, natija itakuwa, Mwenyezi Mungu atakubali Shufaa kutoka kwa mwombezi baada ya kumpa idhini. Sio lazima kupatikana idhini ya Mwenyezi Mungu kwa jina la mmoja mmoja, bali inatosha tu kwa Mtume kujua kwamba Shufaa ni halali ikiwa yule mwenye kuombewa si katika wenye kuwakandamiza watu na kunyanganya riziki zao; bali ni katika watu wa kawaida tu, ambao wanafanya madhambi ya kawaida.

Kwa maneno mengine ni kwamba makusudio ya idhini ya Mwenyezi Mungu kwa Shufaa ni kumpa wahyi Mtume wake kwamba Mimi nimekuruhusu kuwaombea uwatakao katika Umma wako ambao wamefanya mad- hambi maalum. Hapo basi mambo ya hao wenye madhambi yatakuwa mikononi mwa Mtume(s.a.w.w) ; naye atamwombea yule mwenye kustahiki kuombewa. Imethibiti kwamba yeye amesema: Nimeuweka akiba uombezi wangu kuwaombea wenye madhambi makubwa katika Umma wangu.

Sisi tuna yakini kuthibiti Shufaa katika Uislamu.Lakini hatujui kwa ufafanuzi; wakati huo huo tunaamini kwa imani ya mkato, kwamba mwombezi bora wa mtu ni matendo yake, na kwamba kitakachowaombea wenye dhambi ni toba. Hakika Mwenyezi Mungu haweki kizuizi kwa mwenye kutaka kuokoka akiwa na ikhlasi na akakimbilia kwenye ukarimu wa Mwenyezi Mungu hali ya kunyenyekea.

﴿وَإِذْ نَجَّيْنَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ ﴾

49.Na tulipowaokoa kwa watu wa Firaun waliowapa adhabu mbaya; wakiwachinja watoto wenu wakiume na kuwaacha hai wakike; na katika hayo ulipatikana mtihani mkubwa uliotoka kwa Mola wenu.

﴿وَإِذْ فَرَقْنَا بِكُمُ الْبَحْرَ فَأَنجَيْنَاكُمْ وَأَغْرَقْنَا آلَ فِرْعَوْنَ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ﴾

50.Na tulipoitenga bahari kwa ajili yenu na tukawaokoa, na tukawazamisha watu wa Firaun na hali mwatizama.

NA TULIPOWAOKOA

Aya 49 - 50

LUGHA

Neno: Aal, lina maana ya kurudi; kwa hiyo kila mwenye kurudiwa kwa nasaba, rai au itikadi basi yeye ni Aal wa wale wanaomrudia, kisha likawa linatumiwa zaidi kwa maana ya watu wa nyumba ya huyo mtu atakayetajwa, lakini hawezi kuitwa mtu Al mpaka awe na utukufu fulani. Makusudio ya Al-Firaun hapa ni wafuasi wake ambao walikuwa wakiwatesa wana wa Israil kwa amri yake. Abu-Hayan Al-Andalusi (Mhispania) amesema: Katika tafsir yake kubwa Al-Bahrul Muhit; Firaun ni lakabu (msimbo) ya wafalme wa Misri wakati huo; kama vile Kisra wa Fursi, Kaizari wa Roma, Najashi wa Uhabeshi, Tubba wa Yemen na Khaqani wa Uturuki.

Lakini alhamdulillah misimbo hii yote imebakia kuwa ni vigano tu!

MAELEZO

Baada ya Mwenyezi Mungu kuwakumbusha neema zake kwao kwa ujumla, sasa anawakumbusha kwa ufafanuzi. Bora zaidi ya neema aliyoidokeza ni kuwaokoa na Firaun na wafuasi wake ambao waliwapa Mayahudi adhabu kali. Mwenyezi Mungu ameifasiri adhabu hiyo kwa kusema: wakiwachinja watoto wenu wakiume na kuwaacha hai wakike. Yaani wanawaua watoto wanaume na kuwaacha wanawake waje kuwafanya watumishi.

* 18 Mwenye Majmaul Bayan anasema: Firaun aliota mambo yaliyomtisha. Wakamfasiria makuhani kuwa atazaliwa kijana wa kiume kutoka kwa wana wa Israil ambaye atakuja muua, ndipo Firaun akawafanyia hivyo wana wa Israil. Zaidi ya hayo Wamisri walikuwa wakiwadhalilisha Wayahudi kwa kuwatuma kazi za kuvunja mawe, kuchimba mifereji na kazi nyinginezo za sulubu. Msemo umewaelekea Mayahudi waliokuwepo zama za Mtume Muhammad(s.a.w.w) , kwa sababu wao walikuwa kwenye dini ya mababu zao na waliridhia amali zao. Na,mwenye kupenda amali ya watu wengine anakuwa ameshirikiana nao.

Na katika hayo ulipatikana mtihani mkubwa uliotoka kwa Mola wenu: Yaani, Enyi wana wa Israil, Mwenyezi Mungu amewatahini katika shida na raha, ili ijulikane kuwa je mtapigana jihadi na kuwa wavumilivi katika shida? Na je,mtashukuru raha? Au mtasalimu amri katika shida na mkufuru katika neema? Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamtahini mtu ili ajue, la! Yeye anajua lenye kuwa kabla ya kuwa; isipokuwa yeye anamtahini mtu kwa ajili ya kusimamisha hoja juu yake. Kwani hakuna madai kwa asiyekuwa na hoja, hata kama yenye kudaiwa yanathibiti katika elimu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Mwenyezi Mungu amewaonyesha Waisrail neema ya pili aliposema: Na tulipoitenga bahari kwa ajili yenu na tukawaokoa, na tukawazamisha watu wa Firaun

Yaani tulitenga bahari na tukafanya njia kumi na mbili kwa hisabu ya wajukuu. Wajukuu katika wana wa Israil ni koo katika kizazi cha Yaqub(a.s) Kwa ufupi Wayahudi walikuwa katika unyonge na udhalili wa hali ya juu; na adui yao alikuwa na nguvu za hali ya juu. Lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akabadilisha hali hiyo kupitia mikononi mwa Mtume wake Musa(a.s) , wao wakawa ndio wenye nguvu; na adui yao akawa dhalili, hilo wakaliona kwa macho yao; kama inavyosema Aya: Na hali nyinyi mnaangalia. Mwenyezi Mungu alimdhalilishia yule aliyewadhalilisha na akamwangamiza yule aliyetaka kuwaangamiza. Kwa hivyo basi wamelazimiana na hoja na imewalazimu kuwaidhika na kuzingatia, wala wasiwafanyie wengine yale waliyofanyiwa na wengine.

Lakini hivi leo mfano ule ule waliokuwa wakifanyiwa na Firaun ndio wanawafanyia Wapelestina. Na waendelee hivyo, lakini wajue hali itakuja wabadilikia tu, na yatawafika yale yaliyompata Firaun. Na waangalie ilivyokuwa kwa Nebukadnezzar na Warumi; na kwamba shujaa huvuma kisha akaisha. Jambo la kustaajabisha sana kwa mtu ni kwamba anapokuwa kwenye shida, kisha akaokolewa na Mwenyezi Mungu, basi hupetuka mipaka akafanya uovu na kusahau kila kitu. Wafasiri wengi wamesema, kwamba bahari iliyotajwa ni Bahari nyekundu (Red Sea).

﴿وَإِذْ وَاعَدْنَا مُوسَىٰ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِن بَعْدِهِ وَأَنتُمْ ظَالِمُونَ﴾

51. Na tulipomwahidi Musa masiku arobaini mkafanya ndama (kuwa Mungu) badala ya Mwenyezi Mungu mkawa madhalimu (wa nafsi zenu).

﴿ثُمَّ عَفَوْنَا عَنكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴾

52.Kisha tukawasamehe baada ya hayo ili mpate kushukuru.

﴿وَإِذْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَالْفُرْقَانَ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ﴾

53.Na tulipompa Musa kitabu na upambanuzi ili mpate kuongoka.

NA TULIPOMWAHIDI

Aya 51 - 53

LUGHA

Neno: Musa kwa lugha ya Kiarabu lina maana ya: kifaa cha kunyolea nywele kilichotengezwa kutokana na chuma; lakini maana yanayokusuduwa kwa Musa bin Imran siyo ya Kiarabu, bali ni ya Kikibti ambayo ni matamko mawili: Mu lenye maana ya maji na Sa lenye maana ya mti. Kwa hiyo maana ya Musa ni maji ya mti, Ama maana ya kuitwa Maji ya mti, kama ilivyoelezwa katika Majmaul-Bayan, ni kwamba wajakazi wa Asiya(mke wa Firaun), walitoka kwenda kuoga wakakuta sanduku lililokuwa na Musa ndani yake baina ya maji na mti; wakawa naye.

MAELEZO

Baada ya Firaun kuangamizwa na Mwenyezi Mungu na waliokuwa pamoja naye, Waisrail Walipumua, wakarudi Misri wakiwa salama; kama livyoelezwa katika Majmau.Wakati huo, Tawrat ilikuwa bado haijateremshwa, wakamtaka Musa awaletee kitabu kutoka kwa mola wao. Basi Mwenyezi Mungu akamwahidi kumteremshia Tawrat na akamwekea wakati. Musa akawaambia: Hakika Mola wangu ameniahidi kitabu ambacho ndani yake mna ubainifu wa ambayo ni wajibu kwenu kuyafanya na kuyaacha. Akawambia wakati wake ambao ni masiku arobaini, na masiku hayo - kama ilivyosemwa - ni mwezi wa Dhul-Qaada, na siku kumi za mwezi wa Dhul- Hijja.

Musa akenda kwa Mola wake ili awachukulie watu wake kitabu; ndugu yake Harun akawa naibu wake. Kabla ya kwisha muda wa kuja Musa, walianza kuabudu ndama badala ya Mwenyezi Mungu, wakajidhulimu wao wenyewe.

Hiyo ndiyo maana ya dhahiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

Na tulipomwahidi Musa masiku arobaini mkafanya ndama (kuwa Mungu) badala ya Mwenyezi Mungu mkawa madhalimu ( wa nafsi zenu).

Baada ya Musa kurejea kwa watu wake, walitubia na wakarudi kwa Mola wao; Mwenyezi Mungu akawakubali toba yao, na hii ni neema ya tatu ambayo imeelezewa katika Aya:Kisha tukawasamehe baada ya hayo .

Ama neema ya nne ni; kitabu cha Mwenyezi Mungu:Na tulipompa Musa kitabu na upambanuzi ili mpate kuongoka. Kitabu chenyewe ni Tawrat; yenye kukusanya kila kitu kwa ajili ya kubainisha haki na batili, na halali na haramu.

Kunganisha kati ya neno, kitabu na kupambanua, ni kuunganisha sifa kwenye kile kinashosifiwa. Kwa muhtasari ni kwamba: Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewakumbusha Waisrail katika Aya zilizotangulia, neema nne, Kuwaokoa kuchinjiwa watoto wao wa kiume na kuachwa wa kike wawe watumwa, kuangamia kwa Firaun, kusamehewa na kuletewa Tawrat.

Maelezo mazuri zaidi niliyoyasoma kuhusu maudhui haya, ni kauli ya Abu Hayan Al-Andulusi katika Tafsir Al -Bahrul Muhit; namnukuu: Tazama uzuri wa safu hizi ambazo zimepangika kwa mpango wa mtungo wa lulu na wa sayari katika falaki zake, kila safu katika hizo, yaani neema, imeishia kwa mnasaba wake na ikafikia daraja ya juu ya ufasaha ukitoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia mdomoni mwa Muhammad mwaminifu wake, bila ya kusoma kitabu chochote kabla yake, wala kuandika kwa mkono wake.

Abu Hayan anaonyesha kuwa mpangilio huo wenye kupangika vizuri ni katika miujiza ya Muhammad; kwamba yeye anauelezea bila ya kujifundisha. Mwenyezi Mungu awarehemu wahenga, awasamehe na awape neema nyingi. Kwani hakika wao hawakuona chochote chenye harufu ya kuitilia mkazo dini hii na Mtume wake mtukufu isipokuwa walikinyooshea shingo kwa pupa na shauku; wakafanya haraka kukisherehesha, kukifafanua na kukitolea dalili. Lakini tuko wapi sisi wanavyuoni wa sasa ambao twapupia zaidi dunia; hatuoni umuhimu wowote isipokuwa umuhimu wetu tu; wala matatizo isipokuwa matatizo ya watoto wetu tu! Tuko wapi sisi na hao watukufu waliojitolea kila kitu kwa ajili ya kuutukuza Uislamu na Mtume wa Uislamu? Mwenyezi Mungu awasamehe na awainue, na kila mwenye kuitumikia dini, kwenye daraja ya juu.

﴿وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِنَّكُمْ ظَلَمْتُمْ أَنفُسَكُم بِاتِّخَاذِكُمُ الْعِجْلَ فَتُوبُوا إِلَىٰ بَارِئِكُمْ فَاقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ عِندَ بَارِئِكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴾

54.Na Musa alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmejidhulumu kwa kufanya kwenu ndama (kuwa ni Mungu). Basi tubuni kwa Muumba wenu na jiueni; hilo ni bora kwenu mbele ya Muumba wenu.Basi akapokea toba yenu.Hakika Yeye ndiye apokeaye toba Mwenye kurehemu.

﴿وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ نَرَى اللَّـهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْكُمُ الصَّاعِقَةُ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴾

55.Na mliposema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpaka tumwone Mungu waziwazi.Ukawanyakua ukelele na hali mwatizama.

﴿ثُمَّ بَعَثْنَاكُم مِّن بَعْدِ مَوْتِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴾

56.Kisha tukawafufua baada ya kufa kwenu ili mpate kushukuru.

﴿وَظَلَّلْنَا عَلَيْكُمُ الْغَمَامَ وَأَنزَلْنَا عَلَيْكُمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴾

57.Tukawatilia kivuli kwa mawingu na tukawateremshia Manna na Salwa: Kuleni katika vitu vizuri tulivyowaruzuku.Na hatukuwadhulumu, lakini wamejidhulumu wenyewe.

MUSA ALIPOWAAMBIAWATU WAKE

Aya 54 - 57

LUGHA

Manna ni kitu fulani kinachonata mithili ya asali, na Salwa ni tombo (aina ya ndege wa jamii ya kware, kama kuku).

MAELEZO

Na Musa alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mumejidhulumu kwa kumfanya kwenu Ndama (kuwa ni Mungu). Basi tubuni kwa Muumba wenu. Maana yoyote inayofahamika kwa kusikia tu haihitaji tafsiri, bali kuifasiri na kuisherehesha ni ufedhuli tu! Na Aya hii iko katika hali hiyo.

Na jiueni Makusudio ya kujiua yako wazi, ni kujitoa roho: wala hapana haja ya kufasiri vingine, kwa maana ya kuhalifu mapenzi na kuidhalilisha nafsi kwa kukiri dhambi na makosa au kumwabudu sana Mwenyezi Mungu; kama ilivyosemwa. Makusudio ya kujiua hapa, ni baadhi wawaue wengine. Kwa hivyo yule ambaye hakurtadi dini yake kwa kuabudu ndama ndio atamuua yule aliyertadi dini yake. Sawa na kusema kwake Mwenyezi Mungu:

﴿فَإِذَا دَخَلْتُم بُيُوتًا فَسَلِّمُوا عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ ﴾

...Mnapoingia katika majumba jitoleeni salamu.... (24:61).

Na vile vile kusema kwake

﴿وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ ﴾

...Wala msijikejeli: yaani msikejeliane (49:11)

Amesema Tabrasi katika Majmaul-Bayan kwa upande wa Shia, na Razi katika Tafsir Al-Kabir, kwa upande wa Sunni, kuwa Mwenyezi Mungu aliijaalia toba yao ni huko kujiua, sio kwamba wajiue baada ya kutubia. Hukumu hii ina mfano wake katika sharia ya Kiislamu, pale ulipozingatia kuua kuwa ni hadi na adhabu ya kosa la kurtadi.Hilo tutalieleza katika kifungu cha kurtadi kinachofuatia. Zinaendelea Aya kueleza maovu ya Waisrail: Na mliposema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpake tumwone Mungu waziwazi Wakati Musa alipowaendea na Tawrat, baadhi yao walisema: Hatuamini kuwa kitabu hiki kinatoka kwa Mungu mpaka tumwone kwa macho; bila ya kizuwizi chochote kati yetu sisi na Yeye; na atueleze ana kwa ana kuwa Yeye amekutuma na kitabu hiki.

Sijui kama wale wanaokanusha kuwepo Mwenyezi Mungu wakati huu, kwa kuwa tu hawajamuona kwa wazi, wanategemea Waisrail na inadi yao? Au vipi? Mayahudi walimwambia Musa: Hatutakuamini mpaka tumwone Mungu. Hawa wa sasa nao wanasema: Hakuna chochote chenye kupatiana isipokuwa kile tunachoweza kukiona kwa jicho, kukigusa kwa mkono, kukinusa kwa pua au kukionja kwa mdomo. Hivyo ndivyo inavyokaririka historia ya picha ya upinzani wa haki katika kila kizazi.

Yakawanyakua mauti ya ghafla na hali mwalizania Yaani adhabu kutoka mbinguni iliwapata wale waliomwambia Musa hatukuamini mpaka tumwone Mungu wazi wazi, wakaangamizwa mbele ya macho ya wale wasiopinga. Kisha tukawafufua baada ya kufa kwenu ili mpate kushukuru. Baadhi ya wafasiri kama vile Muhamad Abduh, katika tafsiri Al-Manar, amesema: Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakuwarudishia uhai mara ya pili baada ya kuchukuliwa na ukelele; na kwamba makusudio ya kufufuliwa kwao ni kizazi chao kuwa kingi. Wengine wakasema kuwa sio hivyo, hayo hayafahamiki kutokana na dhahiri yake ilivyo, na kwamba waliorudishwa ni wale wale waliouliwa na ukelele.Na hii ndiyo sawa, kwani hapana sababu inayolazimisha taawil, madamu kurudishwa kuwa hai kunawezekana kiakili. Na hilo lilimtokea Uzair, kama inavyofahamisha Aya:

﴿قَالَ أَنَّىٰ يُحْيِي هَـٰذِهِ اللَّـهُ بَعْدَ مَوْتِهَا فَأَمَاتَهُ اللَّـهُ مِائَةَ عَامٍ ثُمَّ بَعَثَهُ﴾

Akasema: Mwenyezi Mungu atauhuisha vipi (mji) huu baada ya kufa kwake? Mwenyezi Mungu Akamfisha kwa miaka mia, kisha akamfufua.... (2:259)

Kimsingi,lililotokea haliwezi kuwa muhali. Kwa hakika inaonyesha kwamba makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu: Yakawanyakua mauti ya ghafla, na kauli yake tukawafufua ni wale waliokuwa wakati wa Musa waliosema: Mpaka tumwone Mungu waziwazi Kwa hiyo, kauli haiwahusu Mayahudi waliokuwa na mtume, msemo umeele-kezwa kwao kwa kuangalia kuwa wanatokana na kizazi kilichosema hivyo.

Tukawatilia kivuli cha mawingu na tukawateremshia Manna na Salwa. Hayo yaliyotokea wakati Waisrail walipotoka Misri wakahangaika katika jangwa la Sinai, kusikokuwa na majengo; wakamlalamikia Musa kwa joto la jua; Mwenyezi Mungu akawaneemesha kwa wingu lililowafunika na kuwakinga na joto la jua kali. Vile vile Mwenyezi Mungu akawaneemesha kwa Manna na Salwa ili wale. Yatakuja maelezo katika tafsiri ya Aya ya 60 kuwa maji yaliwabubujikia kutoka katika jiwe alilolipiga Musa kwa fimbo yake. Inashangaza kuona baadhi ya wafasiri, wakifasiri yale aliyoyanyamazia Mwenyezi Mungu kuyabainisha; kama vile idadi ya waliojiua kwa toba ya kuabudu ndama, kuwa ni watu elfu moja; vile vile walionyakuliwa kuwa ni watu sabini. Ama kuhusu Manna, wanadai kila mtu alikuwa akipata pishi moja na kwamba Salwa ilikuwa ikishuka kutoka mbinguni ikiwa moto moto huku ikifuka moshi, na mengineyo ambayo hayana kauli yoyote iliyopokewa au kudhaniwa.

Imethibiti Hadith kutoka kwa Mtume mtukufu(s.a.w.w) :Hakika Mwenyezi Mungu amenyamazia mambo si kwa kusahau, ni kwa kuwaonea huruma, kwa hiyo msijikalifishe nayo.

Katika Nahjul-Balagha amesema Imam Ali(a.s) :Hakika Mwenyezi Mungu amewafaradhisha faradhi msizipoteze, na amewawekea mipaka msipetuke; na ameyakataza mambo basi msifanye; na ameyanyamazia mambo si kwa kusahau, basi msijikalifishe (nayo).

Na hawakutudhulumu sisi, lakini wamejidhulumu wenyewe .Kukanusha dhulma kwa Mwenyezi Mungu ni sawa na kukanusha kuwa na watoto na mshirika; yaani kumwepusha kabisa na hilo; sawa na kumwambia mseja kuwa hana mtoto. Ama kujidhulumu kwa Mayahudi ni kwa sababu ya usafihi wao na kuzikanusha neema za Mwenyezi Mungu ambaye hanufaiki na twaa ya mwenye kumtii wala hayamdhuru maasi ya mwenye kuasi na madhara ya uasi yanamrudia mwasi. Anasema Ali bin Abu Twalib (a.s.):Ewe mwanadamu ukiona Mola wako anaendelea kukuneemesha nawe unamwasi, basi mhadhari.

Kwa ufupi Aya hizi zinaonyesha ibada ya Waisrail kwa ndama, kutubia kwao kwa kujiua na kutaka kwao kumwona Mwenyezi Mungu. Vile vile kuangamia kwao na kufufuliwa kwao, kufunikwa na kiwingu na kulishwa Manna na Salwa.. Tutaelezea kisa cha Nabii Musa na Waisrail katika surah ya Maida (5) Inshallah. Waliposema kumwambia Musa:

﴿فَاذْهَبْ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَاتِلَا إِنَّا هَاهُنَا قَاعِدُونَ﴾

...Basi nenda wewe na Mola wako mkapigane sisi tutakaa hapa (5:24).

Hilo ni tamko linaloonyesha ukhabithi na uduni wa Mayahudi. Wa kwanza waliogundua uhabithi na uduni wao ni watu wa Firaun ambao waliwachinja watoto wao wa kiume na kuwaacha wa kike. Kumwona Mungu Kutokana na Aya tukufu:Mpaka tumwone Mungu waziwazi.

Tutaonyesha mzozo uliopo katika madhehebu ya Kiislamu na tofauti zao kuwa akili inajuzisha kuonekana Mwenyezi Mungu kwa macho au la?!

Wamesema Ashari (Sunni): Hakika kuonekana Mungu kwa macho kunawezekana kiakili, kwa sababu Yeye yupo na kila kilichopo kinawezekana kuonekana.

Imamiya na Mu’utazila wamesema; Haijuzu kuonekana Mwenyezi Mungu kwa macho katika hali yoyote ile, si duniani wala akhera, kwa sababu Yeye si umbo hata akaonekana, wala haingii katika umbo wala upande fulani.

Baada ya akili kuthibitisha kutoonekana, wamechukulia kwamba ataonekana kiakili sio kwa macho na kwa hakika ya imani sio ya viungo vya mwili, kwa mujibu wa alivyosema mwanafalsafa mkubwa na mashuhuri, Muhammad bin Ibrahim Shirazi, maarufu kwa jina la Mulla Sadra. Katika aliyoyatolea dalili Mulla Sadra kuhusu kutoonekana, ni kauli yake: Kuhisi kitu ni hali inayozuka kwa kile kinachohisi kikikutanishwa na kinachohisiwa kilichozuka. Hivyo basi, kulazimisha kitu ambacho hakikuzuka kuwa kinahisiwa ni kama kulazimisha kitu kisicho na upande kuwa kina upande.

Kauli yake hii - kama ninavyoona - ni kwamba jicho haliwezi kuona kitu isipokuwa kwa sharti mbili:

Liwe linaweza kuona na kiwe kile kinachoangaliwa kinaweza kuonekana kwa jicho. Hilo ni jambo la msingi; likikosa jicho uwezo wa kuona, au kikiwa kitu hakina uwezo wa kuonekana; itakuwa kuona hakuko. Jicho ni dogo na duni zaidi kuweza kuona dhati tukufu; kama vile ambavyo, Mwenyezi Mungu ni mkubwa wa kuonekana na jicho. Nilipokuwa nasoma ibara hii, tukufu akili yangu ilienda kwa mwanafalsafa wa Kiingereza John Luk, anayesema kuwa: kitu kina sifa yake ya kwanza yenye kukithibitikia, ambayo haipambanuki nayo, ni sawa mtu aitambue au asiitambue; kama vile vitu vinavyosimamisha kitu hicho.

Vile vile kuna sifa ya pili ambayo haiwezi kuepukana na kuhisiwa au kujulikana; kama rangi, sauti na ladha. Rangi siyo sifa ya kitu, kama inavyoonekana, isipokuwa ni mawimbi ya kimwangaza yanayohusika kati ya kitu na jicho; kama wasemavyo wataalamu. Vile vile sauti ni mawimbi ya kihewa; na ladha isingekuweko kama si mdomo. Kwa hiyo ladha inahitilafiana kwa uzima wa mdomo na ugonjwa.Kwa ufupi anataka kueleza kuwa hakuna rangi bila ya jicho; wala sauti bila ya sikio; au ladha bila ya mdomo. Hakuna mwenye kutia shaka kwamba nuru ya Mwenyezi Mungu imezidi mawimbi ya kimwanga na mengineyo.Kwa hivyo yakikosekana mawimbi haya, ndio kumekosekana kuona.


2

3

4

5

6

7

8

9

10

9

HADITH ZA MTUME (s.a.w.w) NA MA-IMAMU(a.s)

SEHEMU YA PILI

UBASHIRI WA IMAM JAAFER AS-SADIQ(a.s)

1684. Mazungumzo yafuatayo yamefanywa na Imam Jaafer as-Sadiq(a.s) . ambamo ameripoti ubashiri wa siku za mwisho wa dunia hii. Yametolewa kutoka Darul Islam,Bihar-ul-Anwar na Raudhat-ul-Kafi. Wanaoripoti habari hizo ni Allamah Naraqi na Sheikh Kulaini r.a. kutokea kwa Himran. Imam(a.s) . alisema:

1. "Haki itakuwa imetokomezwa na watu walio katika haki hawatapatikana.

4. Dhulma na uonevu utaenea katika miji yote.

5. Kufuata Qur'an kimatendo itajulikana kama tabia ya kizamani.

6. Zitatolewa maana ya Aya za Qur'an kwa mujibu wa matakwa ya watu,hivyo mafhum ya Qur'an itakuwa imebadilishwa na kupotoshwa.

7. Wadhalimu watakuwa wakiwa kandamiza wale walio katika haki.

8. Uchokozi na uchochezi utatokea kutoka kila pande na pembe.

9. Matendo maovu na kukosa aibu vitaenea na kuzagaa kila mahala.

10. Ulawiti utakuwa ni jambo la kawaida.

11. Muumin atakuwa akionekana kama mtu dhalili ilhali waovu watakuwa wakiheshimiwa

12. Vijana hawatakuwa wakiwaheshimu wakubwa wao.

13. Huruma itakuwa imepotea kabisa.

14. Waovu watakuwa wakitukuzwa kwa udhalimu wao na hakutakuwapo na mtu yeyote wa kuwapinga.

15. Wanaume watafurahishwa mno kwa kuingiliana na wanaume wenzao.

16. Wanawake watawaoa wanawake wenzao.

17. Mapesa yatatumika kwa ajili ya matumizi yale yaliyo haramishwa na Allah swt.

18. Starehe, anasa na zinaa zitashamiri.

19. Zinaa itajulikana kama maadili yaliyopitwa na muda.

20. Muumin atatengwa kwa sababu ya kufanya ibada za Allah swt.

21. Jirani mmoja atafurahi mno kwa kumuudhi na kumbughudhi jirani mwenzake.

22. Wazushi (kama Salman Rushdie wa Uingereza) watatukuzwa na kusifiwa katika kueneza fitina na yale wanayozusha.

23. Ushauri mzuri utakanwa.

24. Milango ya wema yatafungwa wakati milango ya maovu yatafunguliwa.

25. Al-Kaaba haitatumika au haitafikika kwa sababu ya vikwazo na ugumu utakaowekewa mahujaji.

26. Watu watalazimishwa kuacha kwenda Makkah kuhiji.

27. Watu hawatakuwa wakitimiza ahadi zao watakazokuwa wakizitoa.

28. Wanaume watakuwa wakitumia dawa za kuamsha tamaa za kiume kwa ajili kulawiti na wanawake watakuwa wakitumia vyakula vya mafuta ili kujitayarisha kwayo.

29. Baadhi ya wanaume watakuwa wakiishi kwa kujipatia mapesa kwa kuuza mikundu yao.

30. Na wanawake watakuwa wakijipatia mapesa kwa kufanyisha biashara kuma zao.

31. Wanawake wataunda vilabu vyao,mashirika na umoja wao.

32. Wanaume atajigeuza kama wanawake na watavutia na wanawake.

33. Wanaume watajirembesha kama wanawake.

34. Ulawiti utachukuliwa kama ndiyo ustaarabu na starehe ya kweli.

Na Banu Abbas watalipia ulawiti.

35. Wanawake wataona fakhari kwa kuwa na waume nje ya mume mmoja wa ndoa na vivyo hivyo wanaume watakuwa hivyo hivyo.

36. Heshima itakuwa ikitolewa kwa utajiri wa mtu na wala si ucha Mungu.

37. Riba ndiyo itakayokuwa biashara ya kila siku.

38. Ushahidi wa uongo utakuwa ukIssadikiwa mno.

39. Kile alichokiharamisha Allah swt kitachukuliwa ni halali na chochote kile alichokihalalisha Allah swt kitachukuliwa ni haramu.

40. Maamrisho ya Dini yatageuzwa kwa mujibu wa matakwa yao.

41. Wachokozi na waovu watatenda maovu kwa udhahiri bila ya khofu yoyote ile na Muumin hawataweza kuwazuia vyovyote vile.

42. Watawala watawapenda mno Makafiri kuliko Muumiin.

43. Rushwa ndiyo itakuwa njia ya kujitimizia kazi kutoka maofIssa wanaohusika.

44. Wanaume wata walawiti wake zao.

45. Watu watakuwa wakiuawa kwa visingizio vidogo vidogo na magomvi madogo madogo.

46. Wanawake watawafanyia wanaume dhihaka, nao watashawishiwa kufanya uhusiano na wanawake.

47. Wanaume wataishi kwa mapato ya wake zao zitakazopatikana kwa zinaa.

48. Wanawake watakuwa wakiendesha hukumu majumbani huku wanaume wakiwatii wake zao kwa sababu wanawake hao ndio watakuwa wenye mapato.

49. Wanawake watatumiwa katika kupatikana huduma mbalimbali.

50. Kula kiapo kwa jina la Allah swt litakuwa ni jambo lililowekwa ulimini.

51. Pombe na kamari vitapatikana kila mahala na vitakuwa vimezagaa.

52. Wanawake wa Kiislamu wataingiliana na Makafiri,ambapo Waislamu hawataweza kuwazuia na wala hawatakuwa na uwezo kama huo.

53. Maadui wetu watasaidiwa na watawala na marafiki zetu watadhalilishwa kiasi kwamba hata kiapo chao hakitakubaliwa.

54. Udanganyifu na hila ndizo zitakuwa desturi miongoni mwa watu.

55. Usomaji na usikilizaji wa Qur'an utakuwa ni bughudha kwa watu.

56. Kusikiliza mambo fidhuli ndiyo itakuwa ikipendelewa na watu.

57. Jirani hatamstahi jirani mwenzake illa kwa khofu ya ulimi mkali na mchafu.

58. Sheria na kanuni za Allah swt hazitatambuliwa na waovu hawataadhibiwa kwa maamrisho hayo.

59. Ghiba na kulaghaiana ndivyo vitakuwa vitu vya kawaida.

60. Madhumuni ya Hajj na Jihad yatakuwa mbali na yale ya Kiislamu.

61. Misikiti itarembeshwa kwa dhahabu.

62. Watawala watawataka ushauri kwa nia ya Makafiri.

63. Litakuwa ni jambo la kawaida kuibia katika uzani na vipimo vya biashara.

64. Kumwaga damu ya watu wegine litakuwa ni jambo la kawaida.

65. Watu watajigamba kwa ndimi zao chafu zenye matusi mabaya ili kuwatishia watu wengine.

Imam(a.s) . aliendelea kusema:

66. "Watu watakuwa wakipuuzia sala na kutojali.

67. Watu hawatakuwa wakilipa zaka ingawaje watakuwa na utajiri mkubwa.

68. Sanda za maiti zitakuwa zikiibiwa na kuuzwa tena.

69. Mauaji yatakithiri mno kiasi kwamba hata wanyama pia wataanza kuuana wenyewe kwa wenyewe.

70. Watu watakuwa wakIssali katika mavazi ya kiajabu.

71. Macho na mioyo itapoteza nuru zao za heshima na huruma.

72. Watu watakuwa wamejishughulisha na maswala ya kutafuta mali na mapesa tu.

73. Watu watasali kwa kuonyesha tu.

74. Watu watatafuta ilimu ya Dini kwa ajili ya kujipatia mali ya dunia.

75. Ushirika katika makundi yatakuwa ndiyo mambo ya maisha.

76. Wale watakaojipatia riziki kwa njia ya halali,watasifiwa kwa midomo tu.

77. Matendo maovu na machafu yataenea hata Makkah na Madina.

78. Watu waliokufa watafanyiwa mizaha na vichekesho.

79. Mwaka hadi mwaka hali itakuwa ikiendelea kuharibika kuwa mbaya zaidi.

80. Matajiri wataigwa.

81. Masikini, mafukara watafanyiwa dhihaka na kufedheheshwa.

82. Matukio ya kudura kama yale ya mitetemeko,maporomoko n.k. yatakuwapo lakini watu watakuwa hawaviogopi.

83. Matendo maovu yatakuwa yakitendwa kiwaziwazi.

84. Wazazi watatupa watoto wao na watoto watawatusi wazazi wao na daima watakuwa wakitaka mali na utajiri wa wazazi wao.

85. Wanawake hawatawatii na kuwafuata waume wao.

86. Siku itakayopita bila ya mtu kutenda madhambi,basi itachukuliwa ni siku yenye nuksi.

87. Watu wenye uwezo wataficha mali muhimu na kuviuza kwa bei ya ulanguzi.

88. Waombaji na walaghai watajumuika katika kucheza kamari na kulewa.

89. Pombe itatumika kama ni kitu chenye kuponya i.e.dawa.

90. Makafiri watatukuzwa juu ya watu wengine na Muumin watadhalilishwa na kupuuzwa.

91. Kutafanywa malipo kwa ajili ya kutoa Adhan na sala.

92. Misikiti itajaa kwa watu wasiokuwa na khofu ya Allah swt.

93. Watu wenye fahamu na akili kasoro ndio watakaokuwa wakiongoza sala za jamaa' na watu kama hao kamwe hawatashutumiwa au kusutwa na badili yake wataheshimiwa."

VIFO VYEUPE NA VYEKUNDU

1685. Kuhusu kifo cheupe na chekundu, Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . alisema: "Kabla ya kudhihiri kwa al-Qaim (a.s). kutatokezea kwa aina mbili za vifo - nyekundu na nyeupe. Kwa nyekundu kunamaanisha damu yaani kumwagika kwa damu nyingi mno kwa sababu za vita na mauaji ya aina mbalimbali. Na kifo cheupe kinamaanisha kuzuka kwa maafa ya magonjwa ambayo yatakuwa daima yakienea na kuzuka kila mahala ."

Tanbihi : Kwa vifo vyekundu hapo juu tunaelewa kuwa kutakuwapo na vita vya kutisha mno ambapo damu itakuwa ikimwagika kutoka kila pembe ya dunia.Tunasikia kila siku katika maredio na televisheni vile dunia yetu hii ilivyokumbwa na mauaji kila pande. Na ama kuhusiana na kifo cheupe, tunasikia vile magonjwa mbalimbali ya saratani, ukimwi n.k. yanavyoua watu kwa mamilioni.

UBASHIRI WA IMAM 'ALI

1686. Imam Ali ibn Abi Talib(a.s) . alianza kuelezea: "Kumbukeni kuwa kabla ya kuja kwake,

1. Watu watakuwa wakiiona Sala kama jambo hafifu kabisa.

2. Amana zitakuwa zikichukuliwa kiwizi.

3. Kusema uongo ndio itakuwa ikichukuliwa kuwa sahihi.

4. Waislamu wataanza kuchukua riba.

5. Rushwa itakuwa ni jambo la kawaida.

6. Majumba makubwa makubwa na ya fakhari yatakuwa yakijengwa.

7. Dini itauzwa kwa matakwa ya dunia.

8. Watu watawafanya waovu na hakiri kuwa watawala au viongozi wao.

9. Wanaume watawataka wanawake ushauri na uongozi.

10. Hakutapatikana huruma kokote pale,dunia itakuwa imejaa kwa udhalimu.

11. Utumwa utakuwa ni jambo la kawaida.

12. Mauaji na umwagaji wa damu utachukuliwa kama jambo la kawaida na ubabe.

13. Watu wenye ilimu watakuwa wadhaifu na wadhalimu watakuwa wenye nguvu.

14. Watawala watakuwa watu waovu na Mawaziri wao watakuwa wadhalimu.

15. Wasufi na wasomaji wa Qur'an watakuwa wapumbavu.

16. Kutakuwa kukitolewa ushahidi wa kughushiwa.

17. Qur'an Tukufu itakuwa ikirembeshwa kwa nyuzi za dhahabu.

18. Misikiti itakuwa ikijengewa minara mirefu.

19. Watu waovu watakuwa wakiheshimwa.

20. Idadi ya watu itaongezeka lakini wakiikhtilafiana baina yao.

21. Ahadi na mikataba itakuwa ikivunjwa kila hapa na pale.

22. Wanawake watakuwa wakishirikiana pamoja na wanaume wao kwa uroho wa mali.

23. Sauti za Wakomunisti na wapingamizi wa Dini zitakuwa zina nguvu sana.

24. Nao watakuwa wakisikilizwa na kila mtu

25. Viongozi wa Jumuiya watakuwa ndio watu waovu kabisa.

26. Watu waendeshao biashara za Mabenki watakuwa wabadhirifu na wadhulumaji.

27. Ala za muziki zitakuwa zikipatikana kila mahala na kupindukia idadi.

28. Wanawake watakuwa wakipanda mafarasi na wakiendesha magari.

29. Kuiga, hali ya mtu mwingine itaonekana ni kama desturi ya kawaida yaani mwanamme atapenda awe kama mwanamke (ajifanye mwanamke) na mwanamke atapenda ajifanye kama mwanamme

30. Utatolewa ushahidi katika mambo ya mahakama ingawaje mtoa ushahidi mwenyewe atakuwa haelewi kitu chochote kuhusu kesi inayoendelea lakini atatoa ushahidi wa kiuongo katika kesi yoyote ile itakayokuwa ikiendelea.

31. Mbwamwitu watakuwa wengi ,katika makundi ya kondoo.

32. Unafiki utakuwa ndio mambo ya kujivunia

33. Nyoyo za watu zitakuwa zikinuka kuliko hata maiti na mbaya kabisa kuliko kitu chochote kile.

34. Na mahali pa kuishi pema kabisa wakati huo itakuwa ni Jerusalem.Utafika wakati huo mtu atatamani laiti angelikuwa mkazi wa Jerusalem.

Asbagh ibn Nabata alisimama na kusema

"Ewe Bwana, naomba utwambie Dajjal atakuwa ni mtu wa aina gani?"

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . alimjibu "Yeye atakuwa ni Sayyed .Laana iwe kwa mtu atakaye mkubalia Dajjal na atakuwa mtu mwenye bahati yule ambaye atakuwa amemkana Dajjal .

35. Yeye atatokea karibu na Kijiji kinachojulikana kama Isbahan kutokea eneo la Judea, kutakuwa na toto la jicho katika jicho la kulia .Jicho lake la kushoto litakuwa juu ya paji lake la uso na litakuwa liking'ara kama nyota ya alfajiri, na hapo kutakuwa kipande cha nyama kilichojaa kwa damu. Baina ya macho yake mawili kutakuwa na herufi zilizoandikwa katika Kiarabu Kafir yeye atapita katika mabahari makubwa makubwa.

36. Jua litakuwa pamoja naye.

37. Wingu la moshi litakuwa mbele yake na mlima mweupe utakuwa nyuma yake.

38. Watu waliofikwa na majanga ya njaa watafikiria hiyo milima kama ni chakula,

39. Na punda wake mwekundu atakuwa akitembea mamaili na miguu yake itakuwa ikirefuka na kuwa mifupi kufuatana na ardhi ilivyotambaa.

40. Maji yoyote atakayokuwa akiyapitia yeye Dajjal yatakauka hadi siku ya Qiyama,

41. Baadaye atapiga sauti kwa nguvu kwamba kila kiumbe kitamsikia, atasema"Enyi marafiki! Mimi ndiye yule mliyekuwa mkinisubiri,mimi ndiye niliyewaumba,na niliyewafanya nyie mkawa wazuri.Na mimi ndiye mpaji wenu mkubwa sana. "

42. Huyu mwehu wa jicho moja atakuwa mwongo mkubwa sana.

43. Ole wenu, wafuasi wake wengi watakuwa ni wanaharamu na wale waliozaliwa kwa zinaa,

44. Wao watakuwa wakijivika vitambaa vya silki,

45. Huyo Dajjal atauawa mahala panapoitwa Aqba huko Syria, atauawa siku ya Ijumaa mchana,

46. Mtume Issa(a.s) . atasali nyuma ya Imam Mahdi(a.s) .

47. Na baadaye jambo la ajabu kabisa litatokezea.

UDONDOZI WA UBASHIRI

1687. Kutoka dalili na mabashiri ya kudhihiri kwa Imam Mahdi(a.s) . hapa kuna madondoo machache ambayo yamechambuliwa:

1. Uasi wa Sufiani,

2. kuuawa kwa Hasan,

3. Ikhitilafu baina ya Bani Abbas kwa matakwa ya dunia.

4. Kupatwa kwa jua katika mwezi wa Ramadhani, ikifuatiwa na kupatwa kwa mwezi mwishoni mwa mwezi huo wa Ramadhani.

5. Beda (mahala baina ya Makkah na Madina) itadidimia ardhini,

6. Ardhi katika upande wa Mashariki na upande wa Magharibi zitadidimia,

7. Jua wakati wa asubuhi litaonekana liko papo hapo bila kutembea hadi wakati wa mchana na baadaye litachomoza kutoka Magharibi.

8. Mcha Mungu atauawa nyuma ya msikiti wa Kufa pamoja na watu sabini wengine.

9. Mtu mwema kutoka ukoo wa Bani Hashim atachinjwa baina ya Rukn na Makam huko Makkah.

10. Kuta za Msikiti wa Kufa zitaporomoka.

11. Bendera nyeusi zitatokezea huko Khorasan.

12. Mtu kutoka Yemen ataongoza uasi.

13. Mtu atakayetokea nchi za Maghreb ataonekana huko Misri na ambapo atapata mamlaka makubwa.

14. Warusi watafika Bara la Arabia,

15. Wazungu watafika Palestina.

16. Upande wa Mashariki kutaonekana kwa nyota yenye mkia. Mwanga wake utaonekana kama ule wa mwezi na ncha zake zote zitakuwa moja (zitaungana).

17. Kutaonekana uwekundu mkubwa sana mbinguni.

18. Kutazuka moto mkubwa sana katika Mashariki ya kati ambayo itadumu kwa muda wa siku tatu hadi saba.

19. Wale wasio Waarabu watawafukuza Waarabu kutoka ardhi zao.

20. Utawala wa kifalme utakwisha nchini Iran.

21. Wamisri watamuua kiongozi wao.

22. Bendera tatu zitakusanyika Syria.

23. Kutazuka mizozo mikubwa na Syria itateketezwa.

24. Bendera za Waarabu na Bani Qais zitatoka Misri.

25. Bendera ya Banu Kinda itapepea Khorasan.

26. Jeshi kubwa sana litapita Hira.

27. Mabango meusi yatafika kutokezea Mashariki.

28. Maji ya mito ya Furat yatafurika katika mitaa ya Kufa.

29. Kutatokezea watu sitini watakaodai kuwa wao ni Mitume.

30. Sayyid kumi na wawili watadai kuwa wao ni Imamu Mahdi

31. Mtu mwenye heshima kubwa kutoka Bani Abbas atachomwa moto hai karibu na Khankin.

32. Kutajengwa na daraja katika Baghdad katika sehemu za Kharah.

33. Kutakuwa na tufani ya upepo mkali katika Baghdad wakati wa asubuhi na kutafuatiwa na kupasuka kwa ardhi ambamo baadhi ya sehemu itadidimia ardhini.

34. Mauti,vifo na maangamizo yatakithiri huko Iraq kiasi kwamba watu watakuwa kama wamewehuka.

35. Vikundi vitapigana mno huko Iran.

36. Sura za jumuia zitachafuliwa.

37. Watumwa wataanza kutawala nchi za Mabwana wao.

38. Sura kama ya binadamu itaonekana karibu na jua.

39. Makaburi yatafumuliwa na

40. Waliokufa watapewa uhai.

41. Kutakuwa na mvua itakayonyesha kwa mfululizo wa siku ishirini na nne ambayo itahuisha ardhi iliyokuwa imekufa. Kwa hakika wakati huo ndio utakuwa wakati wa kudhihiri kwa Imam Mahdi Sahib az-Zamaan (a.s).

MUKHTASARI WA DALILI

1688.1. Baghdad itateketezwa kabisa.

2. Basra itazama.

3. Waarabu watatawaliwa na mfalme wa ukoo mmoja tu kwa nguvu.

4. Msikiti wa Borasa (baina ya Baghdad na Kazmain) utadhoofika.

5. Kutakuwa na nchi nyingi za Kiislamu na kutakuwa na soko la kawaida

6. Qum itakuwa ni kitovu cha mafunzo ya Kiislamu, kitakuwa ni kituo kipya kuliko kile cha Najaf (Iraq). Na hapo ndipo kutakuwa kukitolewa ahkamu za dini.

7. Kutakuwapo na reli kupitia katika nchi za Kiislamu.

8. Azarbaijan itakumbwa na vita.

9. Wanawake watakosa heshima kabisa.

10. Duniani kote kutaenea sheria za kidemokrasia.

11. Kutakithiri kizazi cha wanaharamu.

12. Kutakithiri riba na rushwa.

13. Kuzaliwa kwa wanawake waovu katika familia nzuri.

14. Watu wenye hali ya chini wataweza kujenga majumba makubwa.

15. Watu wema na waaminifu watakuwa wakiomba mauti ili waepukane na maudhi wanayoyapata.

16. Watoto na majahili watapanda juu ya Mimbar, na watajulikana kama khatib.

17. Wanazuoni watajiingiza katika mambo ya dunia.

18. Madhumuni ya kutafuta Elimu itakuwa ni kutaka kutafuta pesa.

19. Badala ya kusalimiana matusi ndiyo yatakayo kuwa yakitumika watu watakapokuwa wakikutana.

20. Watu watatoka katika dini zao kwa sababu ya ulafi wa vitu.

21. Dini ya Kiislamu itakuwa dhaifu.

22. Mambo ya kuingiliana yatakuwa yakifanyika kidhahiri kama vile wafanyavyo wanyama.

23. Wanawake watasuka nywele zao kama nundu za ngamia.

24. Kupatwa kwa mwezi na jua na mitetemeko vitatokea Mashariki na Magharibi na baadaye katika Bara la Arabia.

25. Kutakuwa na ongezeko katika kuzaliwa watoto wa kike.

26. Ulawiti na pombe vitakuwa ni vitu vya kawaida.

27. Mitetemeko ya kila mara itaongezeka.

28. Wanawake watakuwa na taasisi zao.

29. Wanawake watafanya kazi pamoja na wanaumme katika kutafuta maisha yao.

30. Usafiri utakuwa wa haraka sana.

31. Kutakuwa na muongezeko wa ajali za njiani.

32. Mavazi yatakuwa mafupi.

33. Mwanamme na Mwanamke watajaribu kuonana sawa kijinsia

34. Kutakuwa na ndoa za kuoa jinsia yake yaani mwanamme atamuoa mwanamme mwenzake na mwanamke atamuoa mwanamke mwenzake (na mambo haya hasa yanatokea katika nchi za Ulaya).

35. Wakazi wa Kufa na Najaf watakuwa wamekaribiana sana.

36. Wakazi wa Makkah na Madina wataongezeka.

37. Hijab itakuwa imepotea (hijab, bubui).

38. Maji yataanza kujaa katika ziwa Sawa.

39. Kutakuwapo na nyota yenye mkia karibu na Capricorn.

40. Watu wengi sana watakufa kwa sababu ya kuenea kwa vita

41. Misikiti na Qur'an itarembeshwa kwa dhahabu.

42. Kutatokea na moto mkubwa sana katika mashariki na utaendelea kuwaka kwa siku saba.Na moto huo utatia khofu kubwa sana kwa mioyo ya watu.

43. Kutakusanyika bendera tofauti tofauti huko Kufa na kusababisha mifarakano mikubwa.

44. Utawala wa Kifalme utakwisha huko Iran.

45. Kutatokea na mivurugo katika nchi za Kiaarabu. Kila nyumba ya mwarabu na nchi zote za Kiislamu zitahusishwa humo.

46. Kukosa Imani kutaenea kote.

47. Waislamu wataiga tamaduni na mila za maadui zao.

48. Vifo vya ajali vitaongezeka.

49. Ala za muziki zitaenea kiasi kwamba hakutakuwa na mtu hata mmoja atakayesalimika kwa sauti zao.

50. Watu wataanza kukataa kuwapo kwa Imam Mahdi(a.s) .

51. Kutaonekana sura katika jua, na sauti zao zitasikika duniani kote.

52. Mwanadamu atafika mwezini.

53. Sufiani atatokezea na kueneza utawala wake wa vitisho.

54. Sayyed Hassan atatokezea huko Iran.Na yeye atafika Multan kwa kupitia Kirman huku akiteka sehemu zote. Yeye atamfikia Imam(a.s) . Yeye atamfikia Imam Mahdi(a.s) . na kujIssalimisha mbele yake.

55. Kutatokezea wazushi wa mtume sitini.

56. Mtume Issa(a.s) .atateremka kutoka mbinguni.

57. Maafa, magonjwa ya kuambukiza na ukame utaenea kote.

58. Nafsi ibn Zakia atauawa katika al- Khaaba (mtu mcha Mungu atauawa katika al-Kaaba).

59. Jua litachomoza kutoka Magharibi kwa siku moja.

60. Warusi wataingia Bara la Arabia na watu weupe wataingia Bara la Parestina.Nao baadaye watapambana.

61. Wachina wataingia Bara la Arabia na kusababisha maangamio na maafa ambayo yatakuwa ni mambo ya kawaida.

62. Baadhi ya miji itateketezwa kwa sababu ya maafa na misukosuko.

63. Sauti ya kutisha itasikika kutoka mbinguni.

64. Kutokezea kwa Dajjal.

65. Moto na moshi itakuwa kawaida duniani.

66. Mvua zitatokezea pasipo na misimu yake.

67. Kuongezeka kwa joto katika anga za juu.

68. Kulipuka kwa moto mkubwa katika Aden.

69. Baadhi ya makundi ya wanaume yatakuwa yamegeuka maumbo.

70. Kutatokea na mabadiliko ya ajabu katika sayari ya Capricorn

71. Mkuu wa Dola ya Misri atauawa.

72. Kutakuwapo na mvua ya mfululizo kwa muda wa siku ishirini na nne(24).Dunia nzima itakuwa imejaa michafuko, maafa na maangamizo n.k.

1689. Hadith hii ifuatayo inatuonyesha dhahiri kuwa kuna haja ya kuwapo kwa Imam wa zama na kumtii yeye ni faradhi kwetu sisi,kama vile wanavyoinakili Maimamu wa Kishiah na vile vile Wanazuoni wa Ahli Sunna pia wananakili vivyo hivyo katika vitabu vyao. Hadithi mashuhuri ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . inayopokelewa na madhehbu yote ni kama ifuatavyo: "yeyote yule atakayekufa bila ya kumtambua na kumjua Imam wa zama zake basi mtu huyo atakufa mauti ya ujahili (yaani atakufa kifo cha ukafiri)."

HADITH YA PILI

1690. Madhehebu yote ya Islam kwa pamoja yanaelezea Hadith ifuatayo na ambayo ni uthibitisho wa ukweli wa Kiislamu na vile vile Sahih Bukhari na vitabu vingine vyote vya Hadith pia vinaelezea kuwa Mtume Mtukufu(s.a.w.w) . alisema: "Baada yangu watakuwapo Maimamu kumi na wawili ambao watatokana na Maqureish. "

HADITH YA TATU

1691. 'Allamah Syed Jamal ud-Din Muhaddath ambaye ni mwachuoni mkubwa wa Ahli Sunna,anaandika katika kitabu chake Rawdhat ul-Ahbaab kwa kumnakili Sahaba Ja'abir ibn 'Abdullahi Ansari wakati Allah swt alimfunulia Aya hii Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) :

"Enyi mlioleta Imani! Mtiini Allah swt na Mtume wake na vile vile mumtiini 'ulil Amr'." "Basi mimi (anaendelea Bwana Ja'abir) niliuliza "Ewe Mtume wa Allah swt! Sisi tunaelewa Allah swt pamoja na Mtume wake.Lakini jee ni wakina nani hao ambao wanajulikana kama 'ulil Amr" ambao utiifu wao umefaradhishwa kwetu sisi?" Hapo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alitoa majibu haya yafuatayo: "Wao watakuwa Makhalifa baada yangu na wa kwanza miongoni mwao ni Ali ibn Abi Talib na amfuataye atakuwa ni mwanae Hasan na atamfuatia Hussein na baadaye atafuatia Ali ibn al-Hussein na baadaye Mohammad ibn Ali na anatambulika katika Tawrati kwa umashuhuri wa jina la Baqir na ewe Jaabir! Karibu utafikia zama zake na hapo tafadhali naomba unifikishie salamu zangu. Baada yake atakuja Ja'afer as-Sadiq bin Mohammad na baadaye Musa ibn Ja'afer na baadaye Ali ibn Musa na baadaye Muhammad ibn Ali na baadaye Ali ibn Mohammad na baadaye Hasan ibn Ali na baadaye Muhammad ibn al-Hasan ambaye atakuwa juu ya ardhi hii kama hujjatillah na bakiyallah katika wamchao Allah swt. Huyo ndiye atakayepata ushindi wa mashariki hadi wa magharibi wa dunia hii. Na yeye mwenyewe ambaye atakuwa hayupo mbele ya wafuasi (Mashiah) wake na wale wampendaye hadi kwamba hao hawatabakia katika itikadi ya Uimamu illa wale tu ambao Allah swt ameshawachukulia mitihani ya nyoyo zao." Ja'abir r.a. anaelezea kuwa: Mimi sikusita kumwuliza Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . "Ewe Mtume wa Allah swt! Je katika zama za Ghaibat, wafuasi (Mashiah) wake wataweza kufaidika naye?" Hapo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alijibu: "Naam! Kwa kiapo cha Allah swt ambaye amenituma nikiwa Mtume wake,kuwa katika zama zake za Ghaibat ,Mashiah wake watang'arika kwa nuru yake na kufaidika kwa Ukhalifa wake kama vile watu wanavyofaidika na jua hata kama litakuwa limejificha katika mawingu."

HADITH YA NNE

1692. Imam bu Dawud ameandika katika kitabu chake Sunan na Imam Tirmidhi anaandika katika Sahih Tirmidhi kwa kumnakili Abu Said Khudhri,kuwa: "Mtume Mtukufu(s.a.w.w) . amesema: "Mahdi anatokana nami na mwenye uso unaong'aa na pua yake iliyo ndefu ataijaza ardhi kwa uadilifu na haki kama vile itakavyokuwa imeshajaa kwa dhuluma na ufIssadi, na atatawala kwa kipindi cha miaka saba. "

HADITH YA TANO

1693. Imam Abu Dawuud katika Sunan amendika kwa kumnakili Sayyidina Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Mtume Mtukufu(s.a.w.w) . amesema kuwa iwapo kwisha kwa dunia hata kama ni siku moja itakayobakia,hivyo pia Allah swt atamtuma mtu mmoja kutokana na Ahlul Bayt yangu (kizazi changu) humu duniani ambaye ataijaza dunia kwa uadilifu na haki kama vile itakavyokuwa imejaa kwa dhuluma na ufIssadi."

HADITH YA SITA

1694. Imam Abu Dawud amemnakili Ummul Moominiina kufuatilia mfululizo huo wake kuwa: Mtume Mtukufu(s.a.w.w) amesema kuwa 'Mahdi atatokana na Itrati (kizazi) yangu,yaani atatokana na kizazi cha Fatimah az-Zahra(a.s) ."

HADITH YA SABA

1695.Imam Bukhari katika Sahih Bukhari , Imam Muslim katika Sahih Muslim na Kadhi ibn Mas'ud Baghawi katika Tasnif Sharh al-Sunnah. Wote wanamnakili Abu Hurayrah akisema: "Amesema Mtume Mtukufu(s.a.w.w) . 'Je hali yenu itkuwaje wakati Mtume Issa(a.s) .atakapoteremka kwenu na Imam wenu atakuwapo ametokea miongoni mwenu? "

HADITH YA NANE

1696. Imam Tirmidhi katika Sahih Tirmidhi na Imam Abu Dawud katika Sunan Abu Dawud wanamnakili Abdullah Ibn Mas'ud akinakili riwaya: Amesema Mtume Mtukufu(s.a.w.w) . "Kuwa dunia haitakwisha hadi hapo mfalme wa Kiarabu hatatokea kutokana na kizazi changu,na ambaye jila lake litakuwa kama jina langu. "

HADITH YA TISA

1697. Imenakiliwa na Maimamu wa Ahli Sunna katika Sahih zao,riwaya ifuatayo: Amesema Mtume Mtukufu(s.a.w.w) . "Atatokezea mtu mmoja katika Ahlul Bayt yangu,atakayetawala na jina lake litakuwa kama jina langu. "

HADITH YA KUMI

1698. Imam Abu Is-haq Tha'alabi katika tafsir yake anamnakili Anas bin Malik kuwa:Mtume Mtukufu(s.a.w.w) . amesema kuwa "Sisi wana wa Abdul Muttalib ni viongozi wa watu wa Jannah,yaani mimi , Hamza, Ja'afer na Ali na Hasan , Hussein na Mahdi. "

1699. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Hakuna watu wanaopoteza utajiri wao isipokuwa kwa kutokana na madhambi yao, kwani Allah swt kamwe hawadhulumu viumbe vyake ."

1700. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Wale wote wanaotukuzwa na kuheshimiwa kwa woga wa maovu yao, kwa hakika wao watakuwa miongoni mwa watu waovu kabisa siku ya Qiyama. "

1701. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Hamaki huziba (nuru ya) moyo wa mwenye hekima. Asiyeweza kudhibiti hamaki yake hawezi kuitawala akili yake. "

1702. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Mwenye kuiacha hamaki yake ipande, huharakisha mauti yake ."

1703. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Jihadhari na hamaki, kwani mwanzo wake ni wendawazimu na mwisho wake ni majuto ."

1704. Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Hamaki ni moto uliokokwa, mwenye kuipoza hamaki huuzima (moto wake); na mwenye kuiachilia huwa ni wa kwanza kuungua humo ."

1705. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Jilindeni kutokana na ukali wa hamaki na jiandaeni kupambana nao kwa kuvunja hamaki na kwa kuvumilia. "

1706. Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Kujidhibiti wakati wa kushikwa na hasira humsalimisha mtu wakati wa maangamizo ."

1707. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . amesema: "Kitu gani kilicho kiovu zaidi kuliko hamaki wakati mtu aliyepandwa na hamaki hutoa roho iliyoharamishwa na Allah swt ."

1708. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Ikiwa mmoja wenu atapandwa na hamaki, kama amesimama akae chini, na kama amekaa alale. Na kama hamaki haikupoa baada ya kufanya hivyo, basi atawadhe kwa maji baridi au aoge kwani moto hauzimiki ila kwa maji."

1709. Mtu mmoja alimwambia Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . na kusema: "Mimi mpaka hivi punde tu nilikuwa nikiamini kwamba wewe na baba yako ni watu wabaya kabisa, lakini sasa ninahisi kwamba huo moyo wangu uliokuwa umejaa chuki na uadui dhidi yenu, sasa umejaa mapenzi na ikhlasi. Hakika hakuna mwingine anayestahiki cheo hiki kitukufu isipokuwa wewe tu.

1710. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Jiepusheni na ghadhabu, kwani huleta mashaka. "

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU