HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 20%

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2 Mwandishi:
Kundi: VITABU VYA HADITHI

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

Mwandishi: AMIRALY M.H.DATOO
Kundi:

Matembeleo: 19990
Pakua: 3232

Maelezo zaidi:

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 11 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 19990 / Pakua: 3232
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

Mwandishi:
Swahili

HADITH ZA MTUME (s.a.w.w) NA MA-IMAMU(a.s)

SEHEMU YA PILII

ZIMEKUSANYWA NA KUTARJUMIWA NA AMIRALY M.H.DATOO

700. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) , ameripoti riwaya kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . kuwa amesema: "Enyi wenye shida na masikini! Tunzeni heshima zenu na mpeni Allah swt furaha ya mioyo zenu ili kwamba Allah swt awalipe mema kwa ufukara na shida zinazo wakabili na kama nyie hamtafanya (isije mkakufuru na kuvuka mipaka kwa sababu ya kukosa subira na hikima) hivyo basi mtambue kuwa mtapata adhabu na gadhabu za Allah swt ."

701. Imenakiliwa riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Itakapo tokea miongoni mwenu mtu akazingirwa kabisa kwa hali mbaya, basi inambidi awajulishe jamaa na ndugu zake na asiiweke nafsi yake katika shida ."

702. Al Imam 'Ali bin Abi Talib(a.s) . amesema katika Nahaj -ul - Balagha kuwa: "Mtu yeyote atakayemwambia mahitaji yake dharura zake kwa muumin basi ajue kuwa ameweka habari zake hizo kwa Allah swt, na yeyote yule atakayeleta dharura na mahitajio yake kwa kafiri basi ajue kuwa amekwenda kinyume na maamrisho ya Allah swt ."

703. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Katika hali tatu tu ndipo kunapo ruhusiwa kuomba ama sivyo hairuhusiwi ."Kwanza katika kujinusuru mtu mwenyewe,kujinusuru na hasara kubwa kabisa ya mali na tatu iwapo kwa kutokuomba kutakuja kumpatia udhalilisho wa hali ya juu sana. Yaani mtu katika vitu hivyo vitatu kujiokoa na hali hizo tatu mtu anaweza kuomba msaada kwa wengine ."

704. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema kuwa: "Mtu mmoja alimwijia Al Imam Hassan ibn 'Ali bin Abi Talib(a.s) . na kuomba chochote: Kwa hayo Imam(a.s) . akamwambia haistahiki kuomba isipokuwepo hizo sura tatu. "Kwanza ama kuzuia umwagikaji wa damu,ama mtu akiwa na shida ya hali ya juu kabisa au kujizuia kuja kudhalilika vibaya sana.

Sasa hebu wewe niambie wewe upo katika sura ipi kati ya hizi tatu? Yeye akasema 'Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) .! Katika sura tatu ulizozitaja ipo mojawapo. Basi bila kusita kwa haraka sana Al Imam Hassan ibn 'Ali bin Abi Talib(a.s) . akamtolea dinar elfu hamsini na kumpa, na Al Imam Hussein ibn 'Ali bin Abi Talib(a.s) . akampa dinar elfu arobaini na tisa na 'Abdulah bin Ja'afar akampa dinar elfu arobaini na nane."

705. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Heshima ya muumin ni kule kuamka kwa ajili ya sala za usiku, na vile vile heshima yake ni kule kutokuwa mwombaji wa watu ."

706. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili riwaya kutoka kwa Al Imam 'Ali bin Abi Talib(a.s) . kuwa amesema: "Wewe lazima uwe na moyo wa kuishi vyema na watu na kuwaheshimu na kutosheka nao. Na kuishi nao vyema ni kule kuongea nao kwa upole na utamu na uwe na uso wenye tabasamu na uishi nao vile kwamba kila wakuonapo uwe ukionyesha furaha usoni mwako na hivyo utakuwa umejiwekea heshima katika jamii ."

706. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema: "Iwapo kutatokezea miongoni mwenu anayemtegemea Allah swt azikubalie kila dua zake anazoziomba basi awe akiishi na watu wote kwa wema na kamwe asimtegemee mtu yeyote isipokuwa Allah swt peke yake na atakapo jiona kuwa yeye kwa hakika anao moyo kama huo basi atambue wazi kuwa chochote kile atakachomwomba Allah swt atampatia na kumjaalia ."

707. Al Imam Zaynul 'Abediin bin Hussein bin 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . anasema kuwa: "Iwapo mtu atataka wema wote kwa ajili yake ni kwamba yeye ajiepushe mbali na tamaa za kila aina ya kutamani yale waliyonayo watu, na kama yeye ana matamanio yoyote au maombi yoyote basi asiwategemee hawa watu bali zote azielekeze kwa moyo mkunjufu na halisi kwa Allah swt na lazima Allah swt atazikubalia dua na maombi yake na atamtimizia ."

708. Abul A'ala bin A'ayan anasema kuwa mimi nimemusikia Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akisema: "Enyi watu nyie mtajidhuru pale mtakapo peleka maombi yenu na mahitaji yenu kwa watu, na kwa hakika inafukuzia mbali heshima na adabu. Mkae na watu katika hali ya kuridhika na kuwa na uhusiano nao mzuri na kwa hakika hiyo ndiyo kwa ajili ya usalama. Kwa hakika tamaa yenu ndiyo dalili ya ufakiri wenu ."

709. Ahmad bin Muhammad bin Abi Nassr anasema kuwa yeye siku moja alimwambia Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) : "Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w).! Ninaomba uniandikie barua moja kwa Ismail bin Daud, ili kwamba niweze kupata chochote kutoka kwake. Kwa hayo Al Imam 'Ali ar-Ridha (a.s). akamwambia iwapo mimi kitu unachokitaka au cha kukutosheleza wewe ningekuwa nimekukataa, ndipo ningekuandikia, ama sivyo uchukue kile nilicho nacho mimi kwangu na ukitegemee hicho ."

710. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . amesema: "Kwa hakika yale waliyonayo watu katika uwezo wao na kuridhika nayo ndimo humo kuna heshima ya muumin ya imani yake, je nyie hamjaisikia kauli ya Hatim? Hatim alisema kuwa pale mtakapoona nafsi zenu zimevutiwa kwa mali za watu wengine basi muelewe kuwa shida na taabu ziko zinawakaribia, na kwa hakika tamaa ni ufakiri ulio dhahiri ."

711. Abdullah Bin Sinan anasema kuwa yeye amemsikia Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akisema: "Kwa ajili ya muumin mapendezi ya dunia na akhera yako katika mambo matatu. Kwanza ni sala katika sehemu ya mwisho wa usiku, kutokuvutiwa na kutokuwa na husuda na mali na miliki wanayomiliki watu wengine na kuwa mwaminifu na mtiifu kwa ukamilifu wa Ahlul Bayt (a.s). na mapenzi yao ."

712. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Alikuwapo mtu mmoja mbele ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w). na akamwuliza, 'Ewe Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w).! naomba unionyeshe unieleze jambo moja nilifanye jambo ambalo Allah swt atakuwa radhi pamoja nami. Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w). alimujibu: Udumishe amani na upendo katika utamaduni wa dunia, jambo ambalo kimatokeo utapata mapenzi ya Allah swt na usiwe na kijicho na wivu wala tamaa kwa mali na miliki za watu jambo ambalo litahifadhi heshima yako machoni na mioyoni mwao ."

713. Ja'bir bin Yazid ananakili riwaya kutoka kwa Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . kuwa amesema: "Usiwe na wivu choyo wala tamaa kwa mali za watu kwa hakika ni jambo jema kabisa kwa kuitakasisha nafsi yako kuliko hata kutoa mhanga wa mali. Vile vile wakati wa shida na dhiki fanya subira. Kuhifadhi heshima yako na utakatifu wako, mambo haya ni afadhali hata kuliko kugawa mali kwa watu. Kwa hakika kuwa na imani kamili juu ya Allah swt na kutotaka kutovutiwa kutokuwa na wivu au kijicho au tamaa kwa mali waliyonayo watu wengine ndio hayo mambo yaliyo bora kabisa katika maisha ya mwanadamu ."

714. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alikuwa akisema: "Allah swt amechukia hafurahishwi na sifa sita na vile vile mimi sizifurahii hizo sifa sita na ndio nimefanya usia kwa mawasii na waumini wote kuwa vitu hivyo sita wajiepushe navyo na mojawapo ni kule baada ya kutoa sadaka mtu akaanza kumsema na kuvisema ."

715. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Baada ya kutenda mema mtu atakapovizungumzia hayo basi atayateketeza mema yake yote ."

716. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili riwaya kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . kuwa: "Allah swt hakupendezewa na mambo sita na mimi vile vile katika kizazi changu Maimam wote sikupenda kutokezee sifa hizo, na vile vile Maimam pia nimewahusia kuwa wasizipende sifa hizo ziwepo katika muumin. Hivyo kila muumin anabidi ajiepushe na sifa hizo. Katika sifa hizo sita mojawapo ni ile baada ya kumfanyia mtu wema mtu anaanza kuyazungumzia huku na pale ."

717. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . anasema kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Allah swt hapendi sifa sita na hizo sifa sita mimi sikupendezewa kwa ajili ya mawasii watakao nifuata na waumini wote watakaonifuatia. Kwanza kusali isivyo kwa makini, pili katika hali ya saumu kujamiiana na mwanamke, tatu baada ya kutoa sadaka kutangaza na kuonyesha. Nne kuingia msikitini katika hali ya Janaba, kuwa na shauku ya kutaka kujua mambo ya watu majumbani mwao kunatendeka na kunaendelea nini, na sita kucheka makaburini mtu anapokuwa baina ya makaburi mawili ."

718. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kwa mamlaka yake amenakili riwaya kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . kuwa: "Mtu yeyote atakaye msaidia muumin ndugu yake na baadaye akaja akamwambia kuhusu wema huo akausema basi Allah swt hulirudisha tendo hilo halikubalii. Basi mtoaji atabakia na uzito juu yake na kwa lile jema alilolitenda hana malipo yoyote kutoka kwa Allah swt ."

Imam(a.s) . akaendelea kusema: "Kwa sababu Allah swt anasema kuwa yeye ameiharamisha Jannat kwa ajili ya yule anayesema baada ya kutenda tendo jema na bahili na mchonganishi. Muelewa wazi kuwa yule mtoa sadaka, hata anayetoa kiasi cha Dirham moja, basi Allah swt humlipa zaidi ya ukubwa wa mlima wa Uhud kwa neema za Jannat na yeyote yule atakaye saidia kufikisha hiyo sadaka kwa yule ambaye anahitaji basi Allah swt atamlipa mema hayo hayo, na kamwe hakutakuwa na punguzo lolote katika neema za Allah swt kwa ajili ya wote hao ."

719. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . katika hotuba yake alisema: "Yeyote yule atakaye tenda wema na kuwawia wema ndugu wenzake, na akaanza kutanganza mema aliyoyafanya basi matendo ya watu kama hawa yatatupiliwa mbali na hayatakuwa na maana yeyote .

Allah swt amewaharamishia Pepot watu wafuatao:

"Kwanza ni wale wanao tangaza mema waliyowafanyia watu wenzao, na wale wanaowapotosha watu wengine, wafitini,wanywaji wa pombe,wale wanao tafuta makosa ya watu na aibu za watu,wale wenye tabia mbaya,wale walio makatili kwa wenzao na vile vile,wale watu wanao watuhumu watu wengine kwa tuhuma za kuwazushia maovu ."

720. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili riwaya kutoka kwa mababu zake kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Allah swt amewazuieni nyinyi kwa matendo maovu takriban ishirini na manne na mojawapo ni jambo lile ambalo baada ya kutoa sadaka mtoaji anamwambia maneno aliyempatia ."

721. Bwana Abu Zahar Al Ghafar amenakili riwaya kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . kuwa: "Kuna aina tatu ya watu ambao Allah swt kamwe hatazungumza nao siku ya Qiyama. Kwanza ni yule mtu ambaye hatoi kitu chochote bila ya kumsema au kumwambia yule anayempa, na pili ni yule ambaye hachukui jukumu wala haoni umuhimu wa kuficha zehemu zake za siri na wa tatu ni yule ambaye anauza mali yake na kutaka faida kupindukia kiasi ."

722. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Mtu yeyote baada ya kumsaidia muumin atamuudhi kwa kumwambia au kwa kumsengenya kiasi kwamba roho yake ikaumia basi Allah swt huibatilisha sadaka na wema kama huo ."

723. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Aina tatu ya watu kamwe hawataingia Jannat. Moja ni yule ambaye wazazi wake wamemfanya Aak, wa pili mnywaji wa pombe (daima anakunywa pombe) na tatu ni yule baada ya kufanya mema huanza kusema na kutangaza ."

724. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: Al Imam 'Ali bin Abi Talib(a.s) . siku moja alimtumia mifuko mitano za Tende za Baqi' (Jannatul Baqi', ipo Madina ). Mtu huyo alikuwa muhtaji mwenye shida na daima alikuwa akitegemea msaada kutoka kwa Al Imam 'Ali bin Abi Talib(a.s) ., na kamwe alikuwa harefushi mikono yake kwa wengine kwa ajili ya kuomba kwa watu wengineo. Mtu mmoja alipo yaona hayo basi alimwambia Al Imam 'Ali bin Abi Talib(a.s) : "Kwa kiapo cha Allah swt, huyu mtu hajakuomba chochote wewe kwa hivyo badala ya kumpa mifuko mitano mfuko mmoja tu ulikuwa ukitosha, na kwa hayo Al Imam 'Ali bin Abi Talib (a.s). akamwambia: "Allah swt asiongezee idadi ya muumin kama wewe humu duniani! Wewe mtu wa ajabu sana, mimi ndiye ninayempa lakini ubahili unaufanya wewe! Kumbuka kuwa mtu mwenye shida na anaye kutegemea wewe hakuombi, Je ni haki kuwa mwenye shida asipoomba basi asisaidiwe mpaka lazima aombe? Basi hapa inaonyesha heshima yake. Uso ule ambao unawekwa juu ya udongo kwa ajili ya ibada ya Allah swt katika hali ya sujuda itakuwa basi mimi nimeubadilisha ule sura badala ya kumwangukia Allah swt utakuwa umeniangukia mimi ! Na jambo ambalo silitaki mimi na wala silifanyi hivyo ."

725. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Kwa hakika uwema ni ule ambao mtu anamsaidia mtu kabla hajaombwa, na kumpa baada ya kujua hali yake inamaanisha umempa baada ya kujua hivyo. Inawezekana maskini huyo mtu usiku kucha akawa anatapatapa iwapo atafanikiwa au hatafanikiwa, huku akiwa amejawa mawazo niende kwa nani nisiende kwa nani, na hatimaye moyo ukiwa unadunda mwili ukiwa unatetemeka na akiwa amejawa na aibu kubwa anatokezea mbele yako ."

726. Yas'ab bin Hamza anasema kuwa: "Mimi siku moja nilikuwa pamoja na Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) ., watu walikuwa wamekaa huku wamemzunguka, yaani watu wengi walikuwapo. Watu walikuwa wakiulizia masuala ya halali na haramu, na mara tukaona akaingia mtu mmoja mrefu na akaanza kusema, "Iwe salamu juu yako ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . ! Mimi ni mpenzi na mfuasi wako wewe na baba na mababu zako, na hivi nimerudi kutoka Hijja Tukufu. Mimi nimeibiwa mali yangu yote na hivyo sitaweza kufika nchini kwangu (yaani nyumbani). Mimi naomba nisaidiwe sadaka kiasi kwamba niweze kufika nyumbani kwangu, na mimi nitakapo rudi katika mji wangu kiasi hicho cha fedha nitakitoa nigawe katika kuwasaidia wengine kama sadaka. Imam(a.s) . akamwambia: "Naomba ukae kidogo upumzike, Allah swt akurehemu. Na Imam(a.s) . aliendelea na mazungumzo yake pamoja na umati uliokuwa pale katika kuulizana na kueleweshana kuhusu maswala mbalimbali. Hatimaye mimi Khaysama na Suleiman Al-Ja'afari ndio tuliokuwa tumebakia na hapo Imam(a.s) . kwa kuniangalia mimi akasema: "Je unaniruhusu mimi niende chumbani kwangu?" Suleiman akasema "Allah swt aiendeleze amri yako".

Hapo Imam(a.s) . aliinuka na kuelekea katika chumba chake a baada ya muda si muda akatoka nje akafunga mlango na mwenyewe akasimama nyuma ya mlango na akatoa mkono tu nje huku akisema, je huyo msafiri kutoka Khurasan yuko wapi?" Hapo mimi nikamjibu: "Ya Imam(a.s) .! Mimi niko hapa." Na kwa hayo Imam(a.s) . akamwambia" "Nimekupa hizi Dinar mia mbili ambazo zitakusaidia wewe katika gharama na matumizi ya safari yako na vile vile napenda nikujulishe kuwa hakuna haja tena ya hizi pesa kuzitolea sadaka ufikapo nyumbani kwako, asante na unaweza kuendelea na safari yako na itakuwa vyema tusitazamane nyuso. Msafiri huyo akachukua hizo pesa na kuondoka zake." Seleiman Al-Ja'afar akauliza: "Niwe fidia juu yako ewe Mwana wa Mtume(s.a.w.w) .! Kwa hakika wewe umefanya wema na ihsani mkubwa sana wenye huruma, lakini pamoja na hayo kwa nini umejificha?" Kwa hayo Imam(a.s) . akamjibu "Hakuna sababu nyingine ila sikutaka kuona uso wa mwombaji ukiwa umeingiwa na aibu na unyonge sababu ya kuomba. Je wewe hujaisikia hadith ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . ambamo amesema, kwa yeyote yule anayeficha wema hulipwa thawabu za Hijja sabini na yeyote yule baada ya kutenda maasi na madhambi anatangaza basi daima hubakia dhalili. Na yeyote yule anayeficha madhambi na maovu basi Allah swt humsamehe."

727. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Kwa hakika uwema ni ule ambao mtu anamsaidia mtu kabla hajaombwa, na kumpa baada ya kujua hali yake inamaanisha umempa baada ya kujua hivyo. Inawezekana maskini huyo mtu usiku kucha akawa anatapatapa iwapo atafanikiwa au hatafanikiwa, huku akiwa amejawa mawazo niende kwa nani nisiende kwa nani, na hatimaye moyo ukiwa unadunda mwili ukiwa unatetemeka na akiwa amejawa na aibu kubwa anatokezea mbele yako ."

728. Yas'ab bin Hamza anasema kuwa: "Mimi siku moja nilikuwa pamoja na Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) ., watu walikuwa wamekaa huku wamemzunguka, yaani watu wengi walikuwapo. Watu walikuwa wakiulizia masuala ya halali na haramu, na mara tukaona akaingia mtu mmoja mrefu na akaanza kusema, "Iwe salamu juu yako ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . ! Mimi ni mpenzi na mfuasi wako wewe na baba na mababu zako, na hivi nimerudi kutoka Hijja Tukufu. Mimi nimeibiwa mali yangu yote na hivyo sitaweza kufika nchini kwangu (yaani nyumbani). Mimi naomba nisaidiwe sadaka kiasi kwamba niweze kufika nyumbani kwangu, na mimi nitakapo rudi katika mji wangu kiasi hicho cha fedha nitakitoa nigawe katika kuwasaidia wengine kama sadaka. Imam(a.s) . akamwambia: "Naomba ukae kidogo upumzike, Allah swt akurehemu. Na Imam(a.s) . aliendelea na mazungumzo yake pamoja na umati uliokuwa pale katika kuulizana na kueleweshana kuhusu maswala mbalimbali. Hatimaye mimi Khaysama na Suleiman Al-Ja'afari ndio tuliokuwa tumebakia na hapo Imam(a.s) . kwa kuniangalia mimi akasema: "Je unaniruhusu mimi niende chumbani kwangu?" Suleiman akasema "Allah swt aiendeleze amri yako". Hapo Imam(a.s) . aliinuka na kuelekea katika chumba chake a baada ya muda si muda akatoka nje akafunga mlango na mwenyewe akasimama nyuma ya mlango na akatoa mkono tu nje huku akisema, je huyo msafiri kutoka Khurasan yuko wapi?"

Hapo mimi nikamjibu: "Ya Imam(a.s) .! Mimi niko hapa." Na kwa hayo Imam(a.s) . akamwambia" "Nimekupa hizi Dinar mia mbili ambazo zitakusaidia wewe katika gharama na matumizi ya safari yako na vile vile napenda nikujulishe kuwa hakuna haja tena ya hizi pesa kuzitolea sadaka ufikapo nyumbani kwako, asante na unaweza kuendelea na safari yako na itakuwa vyema tusitazamane nyuso. Msafiri huyo akachukua hizo pesa na kuondoka zake." Seleiman Al-Ja'afar akauliza: "Niwe fidia juu yako ewe Mwana wa Mtume(s.a.w.w) .! Kwa hakika wewe umefanya wema na ihsani mkubwa sana wenye huruma, lakini pamoja na hayo kwa nini umejificha?" Kwa hayo Imam(a.s) . akamjibu "Hakuna sababu nyingine ila sikutaka kuona uso wa mwombaji ukiwa umeingiwa na aibu na unyonge sababu ya kuomba. Je wewe hujaisikia hadith ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . ambamo amesema, kwa yeyote yule anayeficha wema hulipwa thawabu za Hijja sabini na yeyote yule baada ya kutenda maasi na madhambi anatangaza basi daima hubakia dhalili. Na yeyote yule anayeficha madhambi na maovu basi Allah swt humsamehe."

729. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Jambo jema kabisa linalonisaidia mimi katika kufanya wema katika kuwasaidia ni mkono ambao unawafikishia na mkono mwingine unashirikiana naye. Na kwa hakika hao wanaokuja kuomba wanakuja na maombi yao ndipo wanapokuwa karibu nami zaidi. Kwa hakika nimeona kuwa wale wanao sahau waliyoyatenda mema kabla na baada ya kuurudisha mkono wao nyuma huonekana kuwa wao wanaanza kuyasahau mema yote. Kwa hakika moyo wangu kamwe haukuniruhusu kuwafukuza na kuwakatalia waombaji. Na baada ya hapo Imam(a.s) . alisoma mashairi ifuatayo: Wakati unapokuijia mtihani kwako kwa heshima zako pia inabidi uombe, Basi uende kwa mtu mmoja aliye mkuu na aliye Sharifu kwa ajili ya kuomba kwake. Kwa hakika, huyo mtu Sharifu na mkuu atakapokusaidia basi humo ndani hakutakuwa na maonyesho wala masengenyo, na badala yake ndani kutakuwa na unyenyekevu na kuhuzunika pamoja nawe. Kumbuka wakati utakapotaka kupima katika mzani uombaji na utoaji sadaka na mema basi utaona sahani ya mzani ya uombaji utakuwa daima ni mzito kuliko nyingine yote."

730. Warram bin Abi Faras ameandika riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kuwa: "Wenye imani dalili zao ni nne, kwanza nyuso zao huwa zina bashasha, ndimi zao zinakuwa zenye ukarimu na mapenzi, nyoyo zao zinakuwa zimejaa huruma, na wanakuwa na mkono wenye kutoa mkono unaopendelea kutoa sadaka na misaada nk ."

731. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alikuwa akisema: "Kila kila aina ya wema na huruma ni sadaka ."

732. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akizungumzia neno Ma'arufu katika Qur'an Tukufu, Surah Nisaai, 4, Ayah 114: Hakuna kheri katika mengi ya wanayo shauriana kwa siri, isipo kuwa kwa yule anaye amrisha kutoa Sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhai ya Mwenyezi Mungu, basi tutakuja mpa ujira mkubwa.

733. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Kwa ma'arufu kuna maanisha kule mtu kutimiza wajibu wake aliofaradhishiwa ."

734. Siku moja Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . aliwasaidia waombaji watatu na wa nne alipokuja hakumpa chochote. Na hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akasema: "Iwapo mtu atakuwa na Dirham elfu thelathini au arobaini na zote akazigawa kwa kusaidia au sadaka bila ya kubakiza chochote kwa ajili ya wana nyumba wake basi huyo mtu atakuwa mmoja miongoni mwa watu watatu ambao dua zao hazikubaliwi na Allah swt. Na katika watu hawa watatu: mmoja ni yule ambaye bila kutimiza wajibu wake anagawa mali yote kama sadaka au kusaidia, na baada ya hapo anakaa akiomba dua: "Ewe Allah swt naomba unipe riziki." Basi hapo atajibiwa, "Je mimi nilikuwa sikukufanyia njia ya kujipatia riziki ?"

735. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Bora ya sadaka zote ni ile kufanya wakati mtu anapofanya katika hali unapokuwa sawa ."

736. Hisham bin Al Muthanna anasema: "Kuna mtu mmoja alimwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kuhusu tafsiri ya ayah Surah An A'Am, 6, Ayah 141: Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisio tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana na isiyo fanana. Kuleni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala mstumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo.

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alimjibu, "Katika Ansaar alikuwako mtu mmoja (aliwapa jina lao) ambaye alikuwa ana shamba. Pale mazao yake yalipokuwa yakiwa tayari yeye alikuwa akigawa yote katika sadaka, na alikuwa hawapi chochote watoto na wana nyumba yake; na kwa tendo lake hili Allah swt alikuwa akimhesabia yeye kama ni mfujaji na mbadhirifu ."

737. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Baada ya mtu kujitolea kile kiasi alicho na dharura nacho kwa mujibu wa mahitaji yake na baadaye katika kiasi kinachobaki akitoa sadaka basi hiyo sadaka ni bora kabisa ."

738. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema: "Mojawapo katika Nasiha na Mawaidha ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . ilikuwa ni kila aina ya wema ni sadaka mojawapo, na sadaka iliyo bora kabisa ni pale kutoa wakati mtu ameshajitimizia wajibu wake na ametosheka, na mkumbuke kuwa muwape wale ambao kwao nyie mnawajibika kuwatimizia mahitaji yao. Mkono wa mtoaji ni afadhali kuliko mkono wa mpokeaji. Kwa hakika mtu ambaye anachuma kwa uwezo wake na kutumia kwa ajili yake na kuwatimiza mahitaji yao basi Allah swt kamwe hatamlaumu."

739. Mtu mmoja alimwijia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . na kumlalamikia kuhusu njaa: "Basi Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alimtuma mmoja wa wake zake naye alipowaendea wakamwambia kuwa wao walikuwahawana chochote isipokuwa maji ya kunywa tu, na kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . akamwambia, je kuna yeyote yule atakaye mchukua mtu huyu kuwa mgeni wake kwa usiku huo?" Na kwa hayo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) . akasema, "Ewe Mtume wa Allah swt ! Mimi nakubali kumchukua huyu kama mgeni wangu kwa usiku wa leo." Na walipofika nyumbani kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , Imam(a.s) . alimwuliza Bi Fatimah az-Zahra(a.s) . "Je nyumbani kuna chakula chochote?" Kwa kusikia hayo Bi. Fatimah az-Zahra(a.s) . akasema, tuna chakula kiasi cha kuwalisha watoto wetu tu lakini na mgeni pia ana haki yake." Na hapo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . akasema "Wewe walaze watoto, na uizime taa." Asubuhi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . alipokuja mbele ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . akamwelezea kisa kilivyotokea na wakati bado akiwa anaelezea kisa hicho ayah ifuatayo iliteremshwa Surah Al Hashri, 59, ayah ya 9: Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.

740. Muhammad bin Yaqub Kuleiyni amenakili riwaya kutoka Abu Nasar kuwa yeye amesoma barua ambayo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . alimwandikia Abu Ja'afar (Mutawakili, mtawala wa Ki Abbasi). Humo kulikuwa kumeandikwa: "Ewe Abu Ja'afar! nimepata habari kuwa wewe unapotoka nje wakati umekaa juu ya usafiri wako basi wafanyakazi wako wanakutoa nje kwa kupitia mlango mdogo, ili kwamba yule ambaye ana shida na mwenye kuuhitaji msaada wako asiweze kufaidika hivyo. Mimi kwa kiapo cha haki yangu ninakusihi kuwa kutoka kwako na kuingia kwako uwe kupitia mlango mkubwa na uwe na wingi wa dhahabu, fedha na mali ili atakapo tokezea mbele yako mwombaji mwenye shida uweze kumsaidia. Wajomba zako wanapokuomba uwape Dinar hamsini na wake zao wanapokuomba uwape Dinar ishirini na tano na usiwape chini ya hapo kama utawapa zaidi basi hilo ni shauri lako. Na hii nakuambia kwa sababu iwapo wewe utafuata hivyo basi Allah swt atakuwia wema, hivyo utumie na usiwe na shaka katika ahadi na neema za Allah swt mmiliki wa malimwengu yote ."

741. Safwan anasema kuwa siku moja Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . alimwuliza mmoja wa wahudumu wake: "Je leo mmetoa chochote katika njia ya Allah swt ?" Naye alijibu hapana, leo sijatoa chochote bado." Kwa hayo Imam(a.s) . alisema "Sasa usipotoa hivyo unategemea Allah swt atupe baraka kwa misingi gani? Lazima utoe kwa njia ya Allah swt hata kama itakuwa ni Dirham moja ."

742. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa Ayah ya Qur'an Surah Al-Hajj, 22, Ayah ya 28: Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya nyama hoa alio waruzuku. Basi kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri. "Allah swt katika ayah hii anamaanisha kuwalisha wale walio na shida na kuwasaidia, ambapo wao kwa heshima zao wenyewe hawajitokezi nje mbele ya watu kuomba ."

743. Isack bin Ammar amenakili riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kuwa: "Utafika wakati mmoja ambapo waombaji wanaorefusha mikono yao kwa watu watakuwa wakiishi kwa starehe na wale watakao kaa kimya kwa kutunza heshima zao watakuwa wakifa kwa shida zitakazo kuwa zikiwakabili. Kwa hayo mimi nikamwuliza Imam(a.s) ., "Ewe Maula ! Je yakitokea hayo katika zama za uhai wangu mimi nifanyeje?" Kwa hayo Imam (a.s) akamjibu, "Kwa hakika kile ulichonacho wewe uwasaidie hao watu kwa hali na mali na kwa hata cheo chako ulicho nacho na kwa wadhifa wako ulio nao uwasaidie ipasavyo ."

744. Abu Basir anasema kuwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . aliitolea maelezo Ayah ya Qur'an Tukufu Surah Al Baqara, 2, ayah ya 267 isemayo: Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa. amesema Kuwa: "Zama kabla ya Islam watu walikuwa wamejilimbikizia mali iliyopatikana kwa njia zisizo halali (kwa njia zilizo haramu) na baada ya wao kusilimu, walikuwa wakidhani kuwa kwa kutoa mali iliyo patikana kwa njia haramu, watakuwa wametakasisha mali yao iliyo halali, kwa hivyo Allah swt alitoa amri kuwa sadaka itolewe kutoka mali iliyo halali tu."

745. Kwa kuzungumzia ayah hiyo ya juu Shahab amenakili riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kuwa: "Ambamo amesema kulikuwa na kaumu moja ambayo walikuwa na mali nyingi iliyo chafu (iliyopatikana kwa njia za haramu ). Wakati wao walipoukubalia Islam walianza kuchukizwa na malimbikizo yao hayo machafu na wakataka kutoa kwa njia za sadaka. Allah swt aliwaonya kwa kuwaambia kuwa sadaka hutolewa kutokea mali iliyo halali tu ."

746. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Iwapo watu watachuma au watajipatia mali kwa mujibu wa hukumu za Allah swt na wakaitumia kinyume na hukumu za Allah swt au iwapo watachuma kwa njia zilizo kinyume na hukumu za Allah swt na wakazitumia kwa mujibu wa hukumu za Allah swt; katika hali zote mbili Allah swt hazikubalii. Katika kutaka kukubaliwa sharti ni kwamba mapato hayo yawe yamepatikana kwa njia zilizo halali na zitumiwe katika njia zilizo halali vile vile ."

747. Halabi anasema kuwa mtu mmoja alimwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kuhusiana na ayah hii katika Qur'an Tukufu Surah Al Baqarah, 2, ayah ya 267: Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa. Na hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akasema: "Wapo baadhi ya watu ambao baada ya kuingia katika Uislam bado wameendelea kubakia na mali iliyopatikana kwa njia zisizo halali. Na humo kulikuwa na mmoja ambaye kwa makusudi alianza kutoa sadaka kutoa mali hiyo isiyo halali. Na Allah swt alimzuia kufanya hivyo yaani sadaka haiwezi kutolewa isipokuwa kutokea mali iliyotokana kwa njia halali ."

748. Katika Ma'anil Akhbar Al Imam Hassan al-'Askari(a.s) . kwa kupitia sanad amenakili riwaya moja kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kuwa amesema: "Wale ambao wanajiona utukufu na wakubwa na ambao wanatenda matendo kwa mujibu wa nafsi zao, mfano wake ni wa yule mtu ambaye mimi nilisikia watu wakimsifu sana na kumheshimu sana, na hivyo mimi nikawa na shauku ya kutaka kuonana na mtu huyo lakini katika hali ambayo yeye hataweza kunitambua. Siku moja mimi nilimwona alikuwa amezingirwa na watu. Baada ya muda mchache kupita mimi nikamwona yeye ametoka humo na akawa anaondoka, basi mimi nilimfuata nyuma yake. Tulipita katika duka la muuza mikate, huyo mtu kwa kuficha macho yake na kificho ficho akaiba mikate miwili. Kwa hakika mimi nilistaajabishwa mno, na nikadhani kuwa labda wao wana maelewano fulani kabla ya tukio hilo. Tukaendelea mbele yeye akamghafilisha mfanya biashara huyo na akaiba makomamanga mawili humo. Na hapa pia nikafikiria kwa labda wao watakuwa na maelewano kama hayo kabla ya kutokea tukio hili, nikiwa hapo nikaingiwa na wazo kuwa je iwapo watakuwa na maelewano kama hayo basi kwa nini achomoe vitu kimafichoficho?

Basi mimi niliendelea kumfuata nyuma yake, tukafika njiani akamwona mtu mmoja mgonjwa basi huyo akasimama kwa mgonjwa huyo na akatoa ile mikate miwili na hayo makomamanga mawili, akampa huyo mgonjwa. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akamwuliza huyo mtu kulikuwa na dharura gani kwa kufanya hivyo. Mtu huyo kwa kuniona mimi akasema je wewe ni Ja'afar bin Muhammad? Nami nikamjibu naam, basi yeye hapo akaanza kusema nasikitika sana kwa kutokujitambulisha kwako hapo kuja kukufikishia faida (kwa sababu Imam(a.s) . alikuwa hakujionyesha kuwa yeye ni Imam bali alikuwa amejiweka kama yeye ni mtu wa kawaida) Imam(a.s) . akamwambia kwa hakika matendo yako hayo yana aibisha. Basi yeye akasema kuwa Allah swt anasema katika Qur'an Tukufu Surah An A'Am, 6, Ayah 160: Afanyae wema atalipwa mfano wake mara kumi. Na afanyae ubaya hatalipwa ila sawa nao tu. Na wao hawatadhulumiwa. Ama kwa mujibu wa ayah ya Qur'an Tukufu mimi nimeiba mikate miwili hivyo nimetenda madhambi mawili na nimeiba makomamanga mawili hivyo nimetenda madhambi wawili na kwa ujumla nimetenda madhambi manne. Na pale mimi nilipompa mgonjwa sadaka mimi kwa kila wema nimepata malipo kumi ya thawabu hivyo jumla nimepata malipo ya thawabu arobaini. Na kutoka arobaini ukitoa nne ninayo mema thelathini na sita bado." Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akamjibu: "Mama yako akae kwenye kilio chako! Wewe kwa hakika umeitoa maana isivyo ya Ayah za Qur'an Tukufu. Je wewe huelewi ayah ya Qur'an Tukufu isemayo Surah Al Ma'ida, 5, Ayah ya 30:

Basi nafsi yake ikampelekea kumuuwa nduguye, akamuuwa na akawa miongoni mwa wenye kukhasirika. Kwa mujibu wa ayah hiyo wewe umeiba mikate miwili umetenda madhambi mawili na kwa kuiba makomamanga mawili umetenda madhambi mawili mengine na hivyo jumla umetenda madhambi manne, na pale ulipotoa hiyo mali yaani mikate na makomamanga, kama sadaka bila idhini ya mwenye mali basi umetenda madhambi mengine manne. Kwa hivyo umetenda madhambi nane kwa pamoja. Sasa wewe unafikiria mema hayo arobaini yametoka wapi?" Kwa hakika mtu huyo aliduwaa, akimwangalia Imam(a.s) . na akajiondokea zake. Baada ya hapo Imam(a.s) . akasema kwa kujitolea maana potofu ya ayah za Qur'an Tukufu vile isivyo sahihi ndio matokeo yake haya na vile vile kuwapotosha watu wengine pia."

749. Katika tafsiri Ayyashi Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . amenakiliwa akitoa tafsiri ya ayah Surah Al Baqara, 2, ayah ya 267: Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa. Imam(a.s) . akaelezea: "Miongoni mwa watu kulikuwa kumelimbikwa mali iliyopatikana kwa riba na njia zingine zisizo za halali, basi wao walinuia kutoa sadaka humo, na ndipo Allah swt alipowakataza kufanya hivyo (kutoa sadaka kutoka mali iliyopatikana kwa njia za haramu hairuhusiwa)."

1

HADITH ZA MTUME (s.a.w.w) NA MA-IMAMU(a.s)

SEHEMU YA PILI

750. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . ameripoti riwaya kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kuwa amesema: "Katika vitu vya kuleta uokovu mojawapo ni kuwalisha chakula wale wenye kuwa na shida na dhiki, na pili mtu awe ni mwanzilishi awe ni mwanzo wa kutoa salamu na vile vile wakati watu wamelala usingizi mtu anaamka kwa ajili ya kusali na kufanya 'ibada ."

751. Muhammad Yakub amenakili kutoka 'Ali bin Ibrahim ambaye naye amenakili kutoka Muhammad bin 'Isa bin 'Ubaid ambaye naye amenakili kutoka Ahmad bin Muhammad naye amenakili kutoka ibn Fazzal Ma'aruf naye kutokea Tha'alaba bin Maymun ambaye naye pia amenakili riwaya hiyo kutoka kwa Zararah, kuwa

752. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . amesema kuwa: "Allah swt hupendezewa mno kulishwa chakula wale wenye dhiki na shida na njaa, na vile vile hupendezewa kutolewa kwa dhabihu (qurbani) ."

753. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . amesema: "Yeyote yule ambaye hakubahatika kutufanyia sisi wema basi ni wajibu wake kuwafanyia mema na kuwatimizia mahitaji ya marafiki zetu. Na yeyote yule ambaye hakubahatika kudhuru makaburi yetu basi adhuru makaburi ya wafuasi na marafiki zetu ."

754. Muhammad bin Ali bin Hussein Jamil amenakili riwaya moja kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kuwa: "Miongoni mwenu mtu aliye bora kabisa ni yule mwenye moyo mkarimu yaani mwenye moyo wa kutoa na mtu mwovu kabisa ni yule ambaye ni bahili. Na usafi wa imani dalili yake ni kwamba huwawia kwa wema muumin wenzake na kuwatimizia dharura na mahitajio yao. Bila shaka yeyote yule anayewafanyia hisani ndugu zake katika imani basi ndiye mpenzi wa Allah swt kwa sababu katika kufanya wema huko kuna mambo mengi yanayomzuia mtu asiingie katika mitego ya Sheitani na vile vile asiingie Jahannam, na kwa matokeo yake ndiye mtu anayeingia Jannat." Baada ya hapo Imam(a.s) . alimwambia Jamil, "Ewe Jamil! Habari hizi uwafikishie wenzako. Kwa hayo mimi nikasema, "Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . ! Niwe fidia juu yako. Je ni watu gani hao?" Imam(a.s) . akasema: "Hao ni wale ambao wanawafanyia wema ndugu zao katika imani wakati wa shida huwa pamoja nao na vile vile wakati wa furaha pia huwa nao. "

755. Sheikh Sadduq(a.s) . amenakili riwaya kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . ambaye amesema kuwa: "Yeyote yule ambaye hakupata fursa kufanya wema nasi, basi awafanyie wema wapenzi na wafuasi wetu basi atapata thawabu za kutufanyia wema sisi. Na vile vile ambaye hakubahatika kutuzuru sisi katika uhai wetu na uhai wake basi awazuru wapenzi na wafuasi wetu, basi atapata thawabu kama za kutuzuru sisi ."

756. Safwan Al-Jammal anasema kuwa siku moja Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alimwambia Mu'alla bin Hunais: "Ewe Mu'alla! Uwe wa Allah swt, ili Allah swt aweze kukutunza na kukuhifadhi .

Kwa hayo Mu'alla alianza kusema: "Je hivyo inawezekanaje?" Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akamjibu, uwe na hofu ya Allah swt, uwe daima ukimwona yeye katika mawazo yako, kwa hiyo yeye atakifanaya kila kitu kiwe kikikuogopa wewe, na vile vile kitakuwa kikikuwazia wewe na kukujali wewe. Ewe Mu'alla ili kujipatia mapenzi ya Allah swt lazima uwatendee watu matendo mema, na utambue wazi wazi kuwa Allah swt anapendezewa sana na moyo wa ukarimu na huchukizwa sana na ubahili na huwa na uadui nao. Angalia! Wewe kama utaniomba chochote na mwisho wake wewe ukaaza kufanya mapenzi nami, na badala yake mimi nitafurahishwa sana iwapo wewe hautaniomba chochote na hautapata chochote kutoka kwangu na baada ya hayo wewe bado ukawa na mapenzi nami. Na kwa hakika ukiniuliza mema yote naweza kuyafanya kwa ajili yako basi ukweli ni kwamba sifa zote ni za Allah swt kwa sababu yeye amekupitishia neema yake kwa mikono yangu mimi nimekuwa ni kipitishio tu kwa ajili yako kwa hiyo yeye ndiye anayestahiki sifa zote." "Kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alimwambia, "Nyamaza!" Wale mafukara ambao wanawajali ndugu na jamaa zao na kuwawia wema wenzao, Allah swt huwapa ujira mzuri sana, kwa sababu Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu: Surah Sabaa, 34, ayah 37: Na si mali yenu wala watoto wenu watakao kukaribisheni kwetu muwe karibu, isipo kuwa aliye amini na akatenda mema. Hao basi watapata malipo maradufu kwa walio yafanya. Nao watakuwa salama katika maghorofa.

757. Sheikh Quleyni amenakili riwaya kutoka kwa Ahmad bin 'Isa kuwa Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55: Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea

758. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa kwa neno 'Innama' inamaanisha kuwa katika kazi zenu au shughuli zenu zote, mwenye kuwa na haki zaidi kuliko yeyote juu ya nafsi zenu na mali zenu ni Allah swt, baada yake ni Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . na baada yake ni, Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . na hadi kufikia Qiyama Maimamu(a.s) . kutokea kizazi chake.Vile vile Allah swt ameelezea fadhila zao kwa kusema:

نَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ ﴿٥٥﴾

Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea. (Qur'an, 5: 55).

Kisa : katika ayah hii ni kwamba Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . alikuwa akisali sala ya Dhuhuri, alipomalizia raka'a ya pili tu akatokezea mwombaji. Siku hiyo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . alikuwa amevaa Khullah yenye thamani ya Dirham elfu moja ambayo alikuwa amepewa zawadi na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Na Imam(a.s) . alipokuwa katika hali ya Ruku'u, kulitokezea maskini mmoja ambaye akasema, "Ewe Walii wa Allah swt na muumin halisi, iwe salamu juu yako, naomba unipe mimi maskini sadaka yoyote. Kwa hayo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . aliinamisha chini Hulla na kwa ishara akamwambia huyo maskini aichukue." Kwa tukio hili ndipo Allah swt alipoteremsha ayah hii kwa ajili yake na kwa ajili ya kizazi chake na kuonyesha fadhila na kufuzu kwao. Fadhila zao kuwa wanagawa sadaka hata kama watakuwa katika hali ya Rukuu. Kwa hakika imekuja kujulikana kuwa yule maskini aliyekuja kuomba alikuwa si mtu bali alikuwa ni Malaika ambaye alikuja kuomba, na vile vile katika kizazi kizima cha Maimam(a.s) . pia tumeona mara nyingi sana Malaika huwa wanakuja kuomba katika sura ya maskini.

759. Katika kitabu kiitwacho Ihtijaj humo Tabarasi amenakili riwaya kutoka Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . ameelezea kuhusu ayah hiyo kuwa: "Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) . katika hali ya sala akiwa katika Ruku'u alitimiza wajibu wake na akatoa Zaka na Allah swt ndipo alipoiteremsha hiyo ayah na makusudio yake yalikuwa ni kupata ridhaa ya Allah swt ."

760. Ali bin Ibrahim katika kitabu chake Tafsir ananakili riwaya kutoka kwa baba yake Ma'arifat Safwan kuwa Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . amesema: "Siku moja Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alipokuwa amekaa pamoja na 'Abdullah bin Salam kulikuwa na kikundi cha Mayahudi pia. Na wakati huo ikateremshwa ayah ya Qur'an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55: Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea Baada ya hapo mara Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . akatoka nje haraka na akaelekea msikitini na huko njiani alikutana na mwombaji mmoja na hivyo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alimwuliza: "Je kuna mtu aliyeweza kukusaidia?" Basi huyo mwombaji akasema, "Naam, kuna mtu anayesali msikitini humo ndiye aliyenisaidia." Na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alivyoukaribia msikiti akamwona huyo mtu si mwingine bali ni Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) . Na riwaya hii vile vile imenakiliwa na Abu Hamza ambaye ameandika katika Tafsir Ayyashi.

761. Muhammad bin Ali bin Hussein katika kitabu cha Amali amenakili riwaya kutoka Abul Ja'rud Ma'rifat kuwa Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . amenakiliwa riwaya kuwa amezungumzia kuhusu ayah Qur'an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55: Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea

kama ifuatavyo: "Katika Mayahudi ambaye mnafiki mmoja alipoukubalia Uislam akaanza kuiga: "Ewe Mtume wa Allah swt! Je ni nani Wasii na Khalifa wako? Na nani huyo atakaye kuwa Walii baada yako?" Ndipo hapo ayah hiyo ilipoteremshwa na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . akawaambia inukeni, basi hao wote wakainuka na wakaanza kuelekea msikitini. Walipofika msikitini wakakutana na maskini mmoja akitoka nje na hivyo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . akamwuuliza, "Je kuna mtu yeyote aliyekupa chochote ?" Huyo akasema "Kwa nini isiwe hivyo pete hii je niliyoipata?" Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . akasema,"Je ni nani aliyekupa?" Huyo mwombaji akasema "Huyo mtu ambaye bado anasali." Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . akasema "Je alipokupa hiyo pete alikuwa katika hali gani?" Huyo mwombaji akasema alikuwa katika hali ya Ruku'u. Na hapo ndipo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alipopaaza sauti ya Takbira yaani Allahu Akbar na wale wote waliokuwepo pamoja naye nao pia walitoa Takbira kwa nguvu na sauti na hapo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . ndipo alipowaambia wote: "Mtambue wazi kuwa baada yangu Walii ni huyu Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) . na wa si mwingine" Karta anasema kuwa "Kwa mujibu wa riwaya zilizopatikana kuwa katika sala moja aliitoa Hullah, na katika sala ya pili alitoa pete basi inadhihirika kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . anatoa sadaka katika hali ya sala zaidi ya mara moja ndivyo inavyothibitika kwa mujibu wa riwaya zinazopatikana."

762. Ayyashi katika Tafsir yake ananakili riwaya moja kutokea kwa mwana wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . kwa Ammar Yasir amesema: "Siku moja Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . alipokuwa akisali sala ya Sunnah aliahirisha tendo moja kiasi kwamba mpaka akavua pete yake kwa ajili ya kumpa aliyekuja kuomba. Na pale Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alipokuja basi alimwelezea hivyo. Na wakati huwo iliteremshwaayah yake hadi kufikia: Qur'an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55: Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea Basi Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alitusomea ayah hiyo na akasema, "Yeyote yule ambaye mimi ni Mawla wake basi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) . ni Mawla wake. Ewe Allah swt! Uwe na mapenzi na yule ambaye anawapenda wao, na uwe na uadui na yule ambaye anafanya uadui pamoja nao."

763. Halabi anasema kuwa yeye alipomwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . basi Imam(a.s) . akamjibu: "Naam kabisa! Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . aligawa nusu ya mali yake katika njia ya Allah swt - hadi kwamba nguo kwa nguo, Dinar kwa Dinar, alivigawa vyote katika njia ya Allah swt, na alikwenda Hija ishirini kwa kutembea na miguu."

764. Mtume Muhammad(s.a.w.w) . Amesema: "Umma wangu utaendelea kuishi kwa heri pale watapokuwa waaminifu miongoni mwao, watakapokuwa wakirejesha amana watakazokuwa wakiachiana, na watakapokuwa wakitoa sadaka kutoka mali zao; Lakini, Iwapo wao hawatatimiza wajibu hizo, basi watakumbwa na ukame na baa la njaa ." [1]

765. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Enyi wana wa Adam! Muwe wawakilishi wenu wenyewe katika mali yenu na mfanye kile chochote kile mnachotaka kufanyiwa nyie baada ya kifo chenu."[2]

Tanbih : Iwapo mtu atataka baada ya kifo chake sehemu fulani ya mali utajir wake utumike katika kutoa sadaka au misaada, basi asisubiri mpaka afe bali aitumie popote pale atakapo katika uhai wake kwa sababu inawezekana kuwa baada ya kifo chake warithi wake wasiweze kutekeleza kwa mujibu wa vile alivyotaka au usia wake na labda inawezekana asipate wakati wa kuandika usia hivyo akakosa fursa hiyo."

766. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Toeni sadaka na muwatibu wagonjwa wenu kwa hayo, kwa sababu sadaka kwa hakika inatoa balaa na magonjwa; na inaongezea umri wenu ukawa mrefu na kuongezeka kwa thawabu zenu ." [3]

767. Imenakiliwa kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . akisema: "Nilipokuwa nimekwenda mbinguni, mimi niliona mistari mitatu imeandikwa juu ya mlango wa Jannat: Mstari wa kwanza ulikuwa umeandikwa Bismillah Rahman Rahim; Mimi ni Allah swt na hakuna Allah swt mwingine isipokuwa mimi na Rehema zangu zinazidi adhabu zangu. Mstari wa pili ulikuwa umeandikwa Bismillah Rahman Rahim; Sadaka inalipwa kwa mara kumi (10) na mkopo unalipwa mara kumi na nane (18), na kuwajali maJama'a na ndugu kunalipwa mara thelathini (30). Mstari wa tatu ulisomwa yeyote yule anayeelewa wadhifa Wangu na Ukuu wangu basi kamwe asinishutumu mimi katika maswala ya maisha ." [4]

768. Taus-ibn-il-Yamani anasema kuwa yeye alimsikia Al Imam Zaynul 'Abediin(a.s) . akisema sifa za muumin ni tano na pale alipoombwa kuzitaja alijibu: "Ucha Allah swt katika hali ya upweke, kutoa sadaka wakati unaohitajika, Subira anapopatwa na matatizo au anapokuwa na shida, uvumilivu wakati wa ghadhabu, ukweli ponapokuwa na hofu ."[5]

KUTOA SADAKA NA UBAKHILI

769. Mali ya mchoyo huliwa na warithi wake au hupeperuka bila

kujulikana.

770. Hakuna mtu mwenye upweke vile alivyo bahili.

771. Mchoyo ni mweka/mtunzi hazina wa warithi wake.

772. Ubahili na uchoyo huangamiza upendo wa urafiki wa kweli.

773. Ubahilifu ni kujipatia ubadhirifu.

774. Kuwa mchoyo kwa kile ulichonacho ni kutomwamini Allah swt.

775. Sifa ya upole na wema huangamizwa kwa ubahili.

776. Fedha haimnufaishi mwenye kuwa nayo hadi hapo atenganapo nayo.

777. Maovu hufichwa kwa ukarimu.

778. Bora wa watu ni yule afaaye watu

779. Hakutakuwa kuwafadhili watu kwa mifuko mitupu.

780. Fadhila huuliwa kwa matumizi fidhuli.

781. Uachie ngome ya Sadaqa iilinde ufanisi wako.

782. Kutoa baada ya kughairi ni bora zaidi kuliko kughairi baada ya kutoa.

783. Uso ulio mcheshi ni mojawapo ya ne'ema mbili.

784. Usimuudhi mtu yeyote yule pale akutakiapo kila la kheri.

785. Fadhila na ukarimu hupatiwa sifa.

786. Fadhila ya kweli (kwa moyo safi) huondoa dhiki zote

787. Makosa ya mwenye kutoa fadhila ni afadhali kuliko dharau ya mchoyo.

788. Fadhila isiongozwe kwa uoga wala kuwa na matumainio ya kupata chochote (tamaa).

KUWAJALI NDUGU NA MAJAMA'A

789. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Yeyote yule anayetaka kuongezewa riziki na baraka na siku yake ya mauti icheleweshwa, basi inambidi awajali ndugu na maJama'a zake ." [6]

790. Amesema Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) : "Mali haiwezi kulimbikana kupita kiasi isipokuwa kwa njia tano: Ubahili kupita kiasi, matarajio makubwa sana, uroho kupita kiasi, kuvunja uhusiano pamoja na ndugu na maJama'a za mtu mwenyewe, na kuijali na kuipenda dunia hii kuliko Akhera."[7]

791. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . Amesema: "Kuwajali Jama'a na ndugu kunaleta faida tano: Kutakasika na kukubalika kwa matendo ya mtu Kuongezeka katika utajiri na mali Kuondoa balaa na shida mbalimbali Kurahisisha maswala yake katika Akhera Umri kuwa mrefu."[8]

792. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Kuna makundi matatu ya watu ambao hawataruhusiwa kuingia Jannat: Wanywaji wa pombe, Wachawi , na wale wanaokana Jama'a na ndugu zao.[9]

KUWAHURUMIA WAZAZI

793. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Furaha ya Allah swt ipo katika furaha ya wazazi wa mtu (kama ndio hivyo ni kweli, basi adhabu na ghadhabu zake pia zipo katika ghadhabu za wazazi wa mtu) ." [10]

794. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Bora ya matendo ni: Kusali kwa wakati wake, kuwa mwema na mwenye huruma na mwenye mapenzi kwa wazazi wake, na kuchangia katika vita vitakatifu vya Jihad (dhidi ya Mapagani) katika njia ya Allah swt."[11]

795. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Iwapo mtu anataka Allah swt ampunguzie makali ya mauti, basi lazima awajali Jama'a na ndugu zake, na awawie wema wazazi wake. Na pale mtu anapofanya hivyo, basi Allah swt atampunguzia makali ya mauti na kamwe hatapata umaskini katika maisha yake."[12]

796. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Yeyote yule anayewatazama wazazi wake kwa macho ya ghadhabu, hata kama wao hawakuwa waadilifu kwake, basi Allah swt hatazikubalia ibada za mtu huyo (hadi hapo atakapofanya Tawba)."[13]

797. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Watendee wazazi wako kwa huruma ili na watoto wako waje wakutendee vivyo hivyo; na uwe mcha Allah swt kwa wake wa watu wengine ili wake zako wabakie wacha Allah sw t."[14]

798. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Safari moja mtu alimwijia Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w). na kumwuliza namna ya kuwashughulikia wazazi. Hapo Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w). alimjibu uwe mwenye huruma kwa mama yako: uwe mwenye huruma kwa mama yako na uwe mwenye huruma kwa mama yako; Uwe mwenye huruma kwa baba yako uwe mwenye huruma kwa baba yako; na uwe mwenye huruma kwa baba yako lakini huruma hiyo uianzie kwa mama yako kabla ya baba yako ."[15]

HAKI ZA WATOTO

799. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alimwambia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Ewe Ali! Allah swt huwalaani wazazi wale wanao wafanya watoto wao wasiwe watiifu kwao kwa sababu ya kuwalaani kwao ."[16]

800. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . alimwambia mmoja ya wafuasi wake: "Usiupitishe wakati wakati wako mwingi pamoja na mke wako na watoto wako waliokuwa wakubwa, kwa sababu kama mke wako na watoto wako ni wampendao Allah swt, basi Allah swt hatawaacha wapenzi wake bila ya kuwajali, iwapo watakuwa ni maadui wa Allah swt, basi kwa nini wewe uwe na wasiwasi na ujiweke mashughuli kwa ajili ya maadui wa Allah swt. Na mambo mawili yanayoweza kuchukuliwa katika wanaume katika kuhusiana na kuwapatiapo familia zao. Moja ni kutokutimiza wajibu wake kwao, na pili kinachotajwa hapa ni kulimbikiza kupita kiasi kwa mali kwa ajili yao."[17]

801. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Chukueni hatua za kuwafundisha watoto wenu riwaya na ahadith za Ahlul Bayt (a.s). kabla watoto wenu hawajaharibika na hawajachafuliwa akili zao ."[18]

802. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Heri ya mtu kwa mtoto wake ni kule kwa mtoto wake kuwa heri kwa wazazi wake ."[19]

803. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Haki ya mtoto kwa wazazi wake ni kwamba apewe jina zuri kabisa, afundishwe adabu njema na afundishwe Qur'an kwa kanuni zake ."[20]

804. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Wafundisheni watoto wenu kuogelea na kulenga shabaha ." [21]

805. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Watoto wenu wanapokua kufikia umri wa miaka saba, wafundisheni sala, wanapokuwa na umri wa miaka kumi, muwalazimishe kusimamisha sala; na mutenganishe vitanda vyao vya kulalia ." [22]

806. Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin(a.s) : "Haki ya mtoto wako ni kwamba wewe utambue wazi kuwa yeye amekuja humu duniani kwa kukupitia wewe, kwa hiyo yaliyo sahihi na yaliyo mabaya yanatokana na wewe. Wewe unawajibika kumpa mafunzo na elimu bora, kumwelekeza kwa Allah swt, na kumsaidia katika kumtii Allah swt. Kwa hivyo iwapo utamsaidia utamfanyia hisani mtoto wako, basi utaweza kufikia malengo hayo; na kama wewe utamwia kiovu, basi hayo yatakurejea wewe mwenyewe."[23]

807. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Muwaheshimu watoto wenu na muwafundishe kuwa wema, mtasamehewa na Allah swt ." [24]

KUNYOYESHA MAZIWA

808. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Naam malipo ya mwanamke wakati wa mimba yake hadi kuzaa mtoto, na wakati pale anapolea mtoto ni sawa na kuwekwa askari katika kituo cha kulinda mipaka ya Waislam dhidi ya hujuma za makafiri, kwa ajli ya Allah swt. Kwa hivyo iwapo atakufa katika kipindi hiki, basi mwanamke huyo atakuwa katika daraja la mashahidi ." [25] .

809. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Hakuna maziwa yenye faida zaidi kwa mtoto isipokuwa maziwa anayonyonya kutoka kwa mama yake ."[26]

810. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Wakati mwanamke anaposhika mimba basi atakuwa ni kama mpiganaji ambaye anafunga saumu wakati wa mchana na anakesha usiku kucha katika 'ibada, na amejitolea mhanga maisha yake na mali yake katika njia ya Allah swt. Hivyo anapozaa anapata malipo makubwa sana ambayo hakuna mtu anayeelewa isipokuwa Allah swt mwenyewe. Na pale anaponyonyesha mtoto maziwa basi atapata thawabu za kumfanya mtoto mmoja kuwa huru kutoka katika kizazi cha Mtume Ismail(a.s) . kwa kila mara atakapo nyonyesha. Na wakati ufikapo kipindi cha kumuachisha mtoto kunyonya, basi malaika aliyekaribu naye humwambia kuanza matendo kwa mara nyingine tena kwani kwa hakika yeye sasa hivi alipo ni katika hali ya kusamehewa kikamilifu (yaani ashike mimba na kuzaa na kunyonyesha tena kwa mara nyingine)."[27] .

811. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Hakuna maziwa yaliyo bora kabisa kwa mtoto isipokuwa maziwa ya mama yake ." [28]

NDOA 'IBADA KUU

812. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Raka'a mbili za sala zinazosaliwa na mtu aliyeoa ni nzito kuliko yule asiyeoa ambaye anakesha usiku kucha katika ibada na kufunga saumu nyakati za mchana ." [29]

813. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Usingizi wa mtu aliyeoa ni afadhali mbele ya Allah swt kuliko ibada afanyazo mtu asiyeoa usiku kucha na anayefunga saumu nyakati za mchana ." [30]

814. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Wengi wa watendao wema katika 'ummah wangu ni wale waliooa na kuolewa wakati watendao maovu wengi wao ni wale wasio oa au kuolewa ." [31]

815. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema: "Siku moja mtu mmoja alimwijia baba yangu naye(a.s) . alimwuliza iwapo alikuwa ana mke naye akajibu alikuwa hana. Hapo baba yangu(a.s) . alimjibu kuwa yeye hawezi kulala usiku mmoja bila ya mwanamke hata kama atapewa badala yake dunia nzima na yale yote yaliyomo ndani yake. Na hapo Imam(a.s) . alimwambia kuwa Raka'a mbili anazosali mtu aliyeoa ni bora kuliko ibada ya yule asiyeoa kwa kukesha usiku kucha na kufunga saumu katika nyakati za mchana. Na baadaye Imam(a.s) . alimpa Dinar za dhahabu saba na akamwambia akaolee kwa hayo."[32]

KUWAPA HIMA KWA AJILI YA KUOA

816. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Mtu anayeoa hujipatia nusu ya imani yake, na nusu ya imani inayobakia lazima awe na Taqwa ." [33]

817. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Wengi wa watu wa Jahannam watakuwa wale wasioolewa (bila kujali mwanamme au mwanamke) ." [34]

818. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Wengi wa wapotofu na walio haribika katika wale walio kufa miongoni mwenu ni wale wasioolewa na wasiooa ." [35] .

819. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Yeyote yule anayetaka awe msafi na aliye takasika wakati atakapo onana na Allah swt, basi aoe na awe na mke ." [36]

820. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Oeni, ama sivyo mtahesabiwa miongoni mwa Rahbani au ndugu wa maShaytani ." [37]

NDOA NI UFUNGUO WA REHEMA ZA ALLAH SWT NA BASHARA NJEMA

821. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ): "Milango ya pepo kwa rehema itafunguliwa katika nyakati nne: Pale inaponyesha mvua, wakati mtoto anapoangalia kwa huruma nyuso za wazazi wake, pale wakati mlango wa Al Ka'aba tukufu inapofunguliwa, na pale ndoa inapofungwa ." [38]

822. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Waunganisheni watoto wenu wavulana kwa wasichana kwa ndoa kwa sababu, humo Allah swt huwajaalia tabia njema, na huwazidishia katika riziki na heshima zao ." [39]

823. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Muolewe na muwaoze mabinti zenu, kwa sababu ni bahati nzuri kwa Mwislamu mwanamme kumtoa au kuwapa mtoto wake aliyekua au dada yake kwa ajili ya ndoa ."[40]

824. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Hakuna kilicho kipenzi mbele ya Allah swt kuliko ile nyumba ambayo kuna maamrisho ya Islam yanatekelezwa kwa ndoa; na hakuna kitu chochote kinacho mghadhabisha Allah swt kuliko nyumba ile ambamo kunatokea talaka na ufarakano na utengano kati ya bibi na bwana ." [41]