HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 227%

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2 Mwandishi:
Kundi: VITABU VYA HADITHI

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2
  • Anza
  • Iliyopita
  • 11 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 22244 / Pakua: 4849
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

4

3

HADITH ZA MTUME (s.a.w.w) NA MA-IMAMU(a.s)

SEHEMU YA PILI

ULAWITI

896. Amesema al-Imam as- Sadique(a.s) . katika Al-Kafi: "Kuingiza (uume) mwanzoni mwa nafasi ya haja kubwa ni dhambi kubwa kabisa hata kuliko kuingizia katika sehemu ya mbele ya siri ya mwanamke. Kwa hakika Allah swt ameangamiza ummah mzima wa Mtume Lut(a.s) . kwa sababu wao walijiingiza katika laana ya ulawiti. Allah swt kamwe hakumteketeza hata mtu mmoja kwa dhambi za zinaa."

897. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) . ,Wasa'il al-Shiah: "Mtu yeyote anayetenda ulawiti pamoja na kijana wa kiume atapatwa na janabah (uchafu) ambao hautaweza kutakasishwa hata kwa maji ya dunia nzima. Allah swt atamghadhabikia na kumlaani vikali. (Yaani Allah swt atazichukua rehema na baraka kutoka kwake na kumlipa Motoni i.e. Jahannam). Kwa hakika ni mahala pabaya kabisa! Pepo (Jannah) zitakuwa zimemkasirikia mno. Na mtu ambaye anakubali kulawitiwa kwa nyuma, basi Allah swt humweka ukingoni mwa Jahannam (motoni penye moto mkali kabisa) na atamweka huko hadi hapo atakapo maliza kuwahoji watu wote. Hapo ndipo atakapo mwamrisha kuwekwa Motoni. Atapitia adhabu moja baada ya pili hadi kuzimaliza adhabu zote za Jahannam na hadi atakapofikia daraja la chini kabisa. Na kamwe hataweza kutoka hapo."

898. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema katika Al-Kafi "Ulawiti ni moja ya Madhambi Makuu na inaadhibu pale mtu mmoja anapompanda mtu bila ya kumwingilia. Na iwapo atamwingilia kwa nyuma basi hiyo itakuwa ni kufr (ukafiri)."

899. Hudhaifa ibn Mansur anasema: "Mimi nilimwuliza al-Imam as- Sadique(a.s) . kuhusu Dhambi Kuu.

900. Amesema al-Imam as- Sadique(a.s) . katika Wasa'il al-Shiah: "Kubana kwa sehemu za kiume baina ya mapaja mawili kwa njia isiyoruhusiwa ."

901. Nikamwuliza tena, "Je ni mtu gani anayetenda dhambi la ulawiti ?"

902. Al-Imam as- Sadique(a.s) . alinijibu: "Yule ambaye amekufuru kwa Allah swt kwa yale aliyoteremshiwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) . (Qur'an tukufu)."

903. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kwa kumjibu Abu Basir kuhusu Qur'an Tukufu, Surah Hud, 11, Ayah 82, isemayo : 'Basi ilipofika amri yetu, Sisi tuliibinua (mji) juu chinii, na kuwateremshia mvua ya mawe magumu ya udongo uliopikwa, tabaka juu ya tabaka.'

904. Al-Imam as- Sadique(a.s) . alimjibu: "Yupo mtu ambaye anaiaga hii dunia huku akisadiki kuwa ulawiti ni halali, lakini Allah swt anampiga kwa jiwe moja ambalo liliwadondokea watu wa Mtume Lut(a.s) . Walivyoadhibiwa Umma wa Mtume Lut(a.s) .

905. Qur'an tukufu imeelezea aina tatu za adhabu zilizoteremshiwa umma wa Mtume Lut(a.s) . " Sauti kubwa ya kutisha na mayowe ya kusikitisha na makubwa mno Kupigwa kwa kutupiwa mawe juu yao Kupindua ardhi juu chini.

906. Baada ya kutaja adhabu hiyo ya tatu, imeelezwa katika Sura Hud, 11 : 83 '(Mawe hayo ya udongo uliopikwa) yalikuwa yametiwa alama (za adhabu) za Mola wako; Na wala haipo (maangamizo ya miji) mbali kutoka wadhalimu (wengine kama hawa watu wa umma huu wanaofanya machafu haya)'

907. Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . amesema: katika Fiqh-i-Ridha "Jiepusheni na ulawiti na zinaa, na huu ulawiti ni chafu na mbaya kabisa kuliko zinaa. Madhambi haya mawili ndiyo vyanzo vya mabaya sabini na mbili ya humu duniani na Aakhera."

908. Qur'an tukufu imetumia neno 'utovu wa adabu, uchafu' kwa ajili ya zinaa kwa njia ambayo imetumika vile vile kwa ajili ya ulawiti. Twaambiwa katika Surah A'araf, 7: Ayah 80 - 81 'Na (Sisi tulimpeleka) Lut, wakati alipowaambia watu wake:"Je! Mwatenda jambo chafu ambalo halikutendwa na yeyote kabla yenu katika ulimwengu.' "Nyinyi mnawaendea wanaume kwa hamu (ya kufanyiana uchimvi) badala ya wanawake; Ama nyinyi ni watu wafujaji.'

909. Kumtazama kijana mdogo wa kiume kwa macho ya ashiki au uzinifu ni Haraam kabisa, hususan kijana ambaye bado hajaota nywele za usoni mwake. Madhara na adhabu za mtazamo wa ashiki au uzinifu vinazungumziwa kwa mapana na marefu katika maudhui yanayozungumzia zanaa. Vile vile Mtume Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) . katika Wasa'il al-Shiah "Jiepusheni na kuwatazama kwa macho ya ashiki au uzinifu vijana wa matajiri na watumwa, hususan wale ambao hawajaota hata ndevu. Kwa sababu uchokozi unaofanywa kwa mitazamo ya aina hiyo ni mbaya kabisa kuliko uchokozi wa kuwatazama hivyo wasichana wadogo walio katika hijabu."

910. Ni haraam kumbusu kijana wa kiume kwa kuashiki. Amesema al-Imam as- Sadique(a.s) . katika Al-Kafi kwa kumnakili Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Iwapo mtu atambusu kijana wa kiume kwa kuwa ashiki, basi Siku ya Hukumu (Siku ya Qiyama) , Allah swt atamfunga mdomoni mwa mtu huyo hatamu ya moto."

911. Al-Imam ar-Ridha(a.s) . amesema katika Fiqh-i-Ridha : "Wakati mtu anapombusu kijana wa kiume kwa kuwa ashiki (mapenzi au nyege) basi Malaika wa mbinguni na Malaika ardhini , Malaika wa Rehema na Malaika wa adhabu wote kwa pamoja humlaani huyo mtu. Na allah swt humtolea hukumu yake kwenda Motoni (Jahannam). Loh ! mahala pakutisha mno."

912. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) . katika Mustadrakul Wasail: "Allah swt atamwadhibu Motoni (Jahannam) kwa maelfu ya miaka mtu ambaye anambusu kijana wa kiume kwa ashiki au matamanio ya mapenzi."

913. Wanazuoni wanasema kuwa wanaume wawili kulala pamoja chini ya blanketi au shuka moja bila mavazi kunawapa adhabu kwa mujibu wa Sharia za Kiislamu, navyo pia ni miongoni mwa madhambi makuu.

914. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) . ,Wasa'il al-Shiah : "Tengenezeni vitanda vya kulalia tofauti kwa ajili ya watoto wenu wanaozidi umri wa miaka kumi. Ndugu wawili wa kiume au ndugu wawili wasichana au ndugu na dada yake wasilazwe pamoja katika kitanda kimoja."

915. Kwa mujibu wa Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ., "Mtu aliyetenda dhambi kama hili, mwili wake uchomwe moto hata baada ya kuuawa kwa njia nyingine. Yaani akishauawa kwa adhabu atakayoiamua Qadhi, basi baada ya kuuawa mwili wake uchomwe moto.

916. Tunakuleteeni hadith ya Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . aliyoisema: "Mtu yeyote anayestahili kuuawa mara mbili kwa kupigwa mawe basi huyo ni mlawiti ."

917. Ni lazima ujilikane wazi wazi kuwa mwanamme yeyote anayemlawiti kijana wa kiume (anamwingilia sehemu za haja kubwa), basi wafuatao watakuwa wame haramishwa kwake: " mama wa kijana huyo,dada na binti yake huyo kijana kwa maisha yake yote. Yaani, mtu huyu (mlawiti) kamwe hataweza kumwoa mama yake, au dada au binti ya huyo kijana.

918. Imam Jaafer Sadiq (a.s). amesema: "Allah swt ameweka adhabu sita kwa wale watendao zinaa ambapo adhabu za aina tatu wanazipata humu humu duniani na zinazobakia hizo tatu wanazipata huko Akhera. Adhabu hizo zilizowekewa humu duniani ni: " Wanapoteza nuru, Wanakuwa maskini

Maisha yao yanakuwa mafupi. Adhabu tatu zilizowekewa Akhera ni:- " Allah swt atakuwa amewakasirikia mno, Watahesabiwa siku ya Qiyama kwa Sharia kali, Wataishi milele Jahannam.

919. Mtume Mtukufu(s.a.w.w) . amesema: "Manukato ya Jannat yataweza kusikika hadi umbali wa miaka. Hata hivyo yule mtoto ambaye amekanushwa na wazazi yaani wazazi wamesema sio mtoto wao tena, na mtu yule ambaye haonyeshi huruma kwa jamaa zake na yule mtu mzee anafanya zinaa, hao ndio watu hawataweza kusikia manukato ya Jannat."

(2413) Iwapo mwanamme aliyebaleghe atafanya Ulawiti na kijana wa kiume, basi mama, dada na binti wa mtoto huyo atakuwa haramu kwa ajili yake. Na Sharia kama hii itatumika wakati ambapo mtu ambaye amelawitiwa ni mwanamme mtu mzima, au wakati mtu anayelawiti ni kijana ambaye hajabaleghe. Lakini iwapo mtu atakuwa na shaka iwapo kikofia cha uume wa mwanamme umeingia katika sehemu za haja kubwa au haikuingia, basi katika sura hiyo mwanamke katika kikundi cha hapo juu hawatakuwa haramu kwa ajili yake.

(2414) Iwapo mwanamme atamuoa mama au dada wa kijana mvulana, na akamlawiti huyo mvulana baada ya ndoa kwa misingi ya tahadhari hao watakuwa ni haramu kwa ajili yake.

USAFI KATIKA ISLAM

920. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Kuna mema matatu ambayo Allah swt huyapenda katika watu: Ufupi katika uzungumzaji, usingizi mfupi, na ulaji mdogo; Na mambo matatu ambayo hayamfurahishi Allah swt: Kuzungumza kupita kiasi Kulala kupita kiasi, na Kula kupita kiasi ." [110]

921. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Jaribuni kuwa wasafi kila muwezavyo. Kwa hakika Allah swt ameweka misingi ya Islam juu ya usafi; hivyo kamwe mtu mchafu hawezi kuingia Jannat mpaka awe msafi ." [111]

922. Al Imam Amiril Muuminin 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , Amesema: "Kula kupita kiasi kunasababisha wingi wa magonjwa ."[112]

923. Amesema Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) : "Zipo Sunnah tano kuhusu kichwa na tano zingine kuhusu mwili. Sunnah tano zinazohusiana na kichwa ni: Kuosha mdomo, kunyoa mashurubu, kuchana nywele, kupitisha maji kupita mdomo na pua .[113]

Sunnah tano zinazohusiana na mwili ni: Kukaa jando, kunyoa nywele za sehemu za siri, kunyoa nywele kwenye mabega, kupunguza na kukata makucha, na kusafisha na kuosha sehemu za siri (kwa maji au kwa karatasi, kwa kitambaa, au chochote kile kinachoweza kukufaa n.k.)"

924. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . alimwambia Al Imam Hasan ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Je nikufundishe mema manne ambayo hautahitaji dawa ya matibabu ya aina yoyote? "Naam" alijibu Al Imam Hasan ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Kwa hayo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . alimjibu: Usikae kula chakula hadi uwe una njaa; Na usiondoke juu ya meza ya chakula bila ya kubakiza njaa kidogo; Tafuna chakula chako vyema mdomoni mwako; Na unapotaka kwenda kulala, uende ukajisaidie haja. Iwapo utatekeleza haya basi kamwe hautahitaji matibabu ya aina yoyote."[114]

BIASHARA NA UHUSIANO WA KIJAMII

925. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ., Amesema: "Iwapo mtu atanunua mali ambayo katika vyakula ambacho ni muhimu katika jamii na akakificha kwa siku arobaini kwa matumaini kuwa bei yake itapanda miongoni mwa Waislam, na kama atafanikiwa kukiuza kwa bei ya juu hicho chakula basi kama fedha zote atazigawa katika sadaka kwa na wenye kuhitaji misaada maskini, basi hiyo haitapunguza adhabu yoyote mbele ya Allah swt kwa kile alicho kitenda (kuhujumu uchumi) ." [115]

926. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ., amesema: "Yeyote yule anayefanya biashara bila ya kuzingatia sheria na kanuni za Islam, basi kwa hakika ataingia katika riba, (bila ya yeyemwenyewe kujijua) ."[116]

927. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . ananakili kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . kuwa Amesema: "Yeyote yule aliye katika biashara na anayenunua na kuuza vitu lazima ajiepushe mambo matano, ama sivyo asinunue wala asiuze kitu chochote: Riba, Kula kiapo, Kuficha ubaya na kasoro za mali, Kusifu kitu kama hakistahili hivyo wakati wa kuuza; na kutafuta kasoro au ubaya wakati wa kununua . " [117]

928. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . Amesema: "Yeyote yule anayetafuta riziki humu duniani ili aondokane na shida za kutegemea watu katika mahitaji yake, na ili kuwalisha na kuwasaidia wananyumba wake, na kueneza mapenzi yake kwa majirani zake basi atakutana na Allah swt siku ya Qiyamah huku uso wake ukiwa uking'ara kama mwezi ."[118]

KUGHUSHI KATIKA BIASHARA

929. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Yeyote yule anaye lala huku akiwa amepanga njama dhidi ya Muislam mwenzake moyoni mwake, basi amelala katika adhabu za Allah swt, na atabakia katika hali hiyo hadi pale afanye Tawba ." [119]

930. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Na yeyote yule anayemlaghai ndugu yake Mwislam, basi Allah swt humwondoshea riziki kwa wingi na huharibu maisha yake na kumwachia katika hali yake mwenyewe . [120]

931. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w). ameharamisha kuchanganywa kwa maji katika maziwa wakati wa kuuza ."[121]

932. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema, "Yeyote yule anayewaghushi Waislam kwa ujumla basi huyo hayupo nas i."

933. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Mtu yeyote anaye walaghai Waislam wenzake katika kununua au kuuza kitu chochote, hayupo miongoni mwetu, na siku ya Qiyamah atainuliwa akiwa miongoni mwa Wayahudi, kwa sababu wao wamekuwa daima wakiwadanganya na kuwaghushia Waislam ." [122]

MATAMANIO NA TAMAA ZISIZO HALALI

934. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Baada yangu mimi, ninawahofia umma wangu katika vitu vitatu: Upotofu baada ya kuelimika, matamanio yanayo potosha na Tamaa ya tumbo na sehemu za siri ." [123]

935. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) ., amesema: "Hakuna 'ibada ya Allah swt iliyo na thamani zaidi kuliko usafi, uhalisi wa tumbo la mtu na sehemu zake za siri kutokana na matamanio au tamaa ."[124]

936. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Kwa mtu ambaye anakuwa na matamanio na maovu yanapokuwa daima yako tayari na yeye anayaepukana nayo kwa sababu ya hofu ya Allah swt, basi Allah swt atamharamishia moto wa Jahannam na atamhakikishia kuwa hatakuwa na tishio kubwa ."[125]

937. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Yeyote yule anayejinusuru na maovu ya tumbo, ulimi, na sehemu zake za siri basi kwa hakika amejinusuru kutoka madhambi ." Al-Muhajjat-ul-Baidha.

938. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ., amesema: "Kumbuka (wakati wa kutenda dhambi), kuwa raha zinapotea wakati matokeo (yatakayotokea) yake yanabakia. "[126]

939. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Yeyote yule anayembusu kijana wa kiume kwa matamanio ya kitamaa, basi Allah swt atamadhidhibisha na kumchapa kwa miale ya moto ." [127]

940. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . amesema: "Je kuna jitihada gani iliyo afadhali kuliko usahihi wa tumbo na wa sehemu za siri ."[128]

MALI YA DUNIA NA ULIMBIKIZAJI KWA UROHO

941. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Kwa yeyote yule ambaye siku zake mbili za maisha yakawa sawa (hakuna maendeleo ya kiroho) kwa hakika yupo katika hasara ." [129]

942. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . amesema: "Mfano wa dunia hii ni sawa na maji ya bahari. Kiasi chochote yule anywacho mwenye kiu kutoka bahari, kiu chake kitaendelea kuongezeka hadi kinawez kumuua ."[130]

943. Al Imam Muhammad at-Taqi(a.s) . amesema: "Watu wanaheshimiwa humu duniani kwa kuwa na mali na Akhera watu wataheshimiwa kwa kuwa na matendo mema ."[131]

944. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema, Makusanyo ya Waram: "Maangamizo ya wanawake wangu yako katika mambo mawili: Dhahabu na mavazi yasiyo ya heshima; Na maangamizo ya wanaume wafuasi wangu yapo katika kuiacha elimu na kukusanya na kulimbikiza mali ."

DUNIA INAYO HADAA, MAVUTIO NA SUMU YAKE

945. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Wakati Jeneza maiti ya mtu inapoinuliwa na kuchukuliwa kwenda kuzikwa, basi Ruh yake inaifuata maiti na katika hali ya masikitiko makubwa inasema: 'Enyi watoto na Jama'a zangu! Jitahadharisheni sana kuwa ulimwengu huu hauwahadai nyie kama mulivyonifanyia mimi. Mimi nimekusanya mali yote hii bila ya kujali uhalali au uharamu wake na nimeiacha nyuma huku kwa ajili ya wengine. Sasa mimi nimeondoka na mzigo juu yangu (kwa sababu ya kutenda kila aina ya madhambi ya uhalali na uharamu) wakati matunda yake wanafaidi watu wangineo; kwa hivyo, mujiepushe na hayo ambayo sawa na yaliyo nifika mimi."[132]

946. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ., amesema: "Iwapo huyu mtu angeweza kuiona mauti yake na kasi yake inavyo mwelekea yeye basi kwa hakika angechukia na kuiacha dunia na matumaini yake yote ."[133]

947. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) , amesema: "Mfano wa dunia ni kama nyoka ambaye ngozi yake ya nje ni laini na nyororo kwa kugusa wakati kuna sumu kali mno inayoua ndani mwake. Aliye na hekima wanajaribu kujiepusha nayo (lakini watoto wasio na fahamu kamili) wanapendezewa na kuvutiwa nayo na wanatamani kugusa na kucheza kwa mikono yao . "[134]

948. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Mapenzi ya dunia hii itakayo angamia ndiyo chanzo cha maovu yote ."[135]

WATUMWA WAPUUZAJI WA DUNIA HII INAYO HADAA

949. Amesema Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Kwa hakika, watu ni watumwa wa dunia na imani yao haina misingi yoyote, ipo katika ndimi zao tu. Wao wanaitilia maanani ili mradi wanapata mahitaji yao wanayoyahitaji, lakini pale wanapojaribiwa, basi idadi ya waumini halisi inakwenda ikipungua ."[136]

950. Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Mimi nastaajabishwa kuhusu yule mtu ambaye yuko mashughuli kwa ajili ya kula tu lakini hafikirii kwa ajili ya chakula cha akili yake. Hivyo yeye anajiepusha na kile kinachomdhuru tumboni mwake na papo hapo anaiachia akili yake ijae kwa yale yanayoangamiza ."[137]

ULAFI NA MATUMAINI YA KIPUUZI

951. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , amesema Nahjul: "Ingawaje uchoyo, uoga na uroho ni vitu vyenye sifa tofauti, lakini vyote viko sawa katika mambo ya kufikiria kwao kuhusu Allah swt ."[138]

952. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Iwapo mwanaadamu atakuwa na mabonde mawili ambamo kumejazwa dhahabu na fedha, basi yeye hatatosheka nayo bali atakwenda kuitafuta ya tatu ."[139]

953. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) , amesema: "Yeyote yule anaye uendekeza moyo wake kwa dunia hii basi atapatwa na hali tatu: Mateso yasiyoisha, kiu ya matamanio isiyoisha na matumaini yasiyo timika ."[140]

954. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , amesema: "Wako kiasi gani cha watu ambao ni waovu na siku zao ziko zinahesabika lakini bado wanaendelea kwa juhudi zao zote za kuitafuta hii dunia ."[141]

MAJIVUNO NA KIBURI

955. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Msiwe wakaidi (na msing'ang'anie kufuata vile mfikiriavyo nyie wenyewe), kwa sababu watu kama hawa hukumbana na maangamizo ."[142]

956. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ., amesema: "Yeyote yule ajionaye kuwa yeye ndiye mkubwa kabisa (hana mfano mwingine) basi si kitu chochote kile mbele ya Allah swt ."[143]

957. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Mambo mawili yanasababisha watu kuangamia (na kutumbukizwa katika Jahannam): Kuogopa umaskini, na Kutaka ukubwa kwa kupitia majivuno ."[144]

958. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Mjiepushe na kujifakharisha wenyewe, kwa kutegemea yale muyaonayo mazuri ndani mwenu na kwa kupenda kuzidishiwa sifa kwa sababu hayo ndiyo majukumu makubwa yakutegemewa na Shaytani ."[145]

959. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) ., amesema: "Yeyote yule aliye na kiburi hata kidogo moyoni mwake basi hataruhusiwa kuingia Jannat ."[146]

KUBANA MATUMIZI

960. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) , amesema: "Yeyote yule anaye panga matumizi yake basi kamwa hatakuwa fakiri ."[147]

961. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , amesema: "Sera bora kabisa ni katika kutekeleza ukarimu ."[148]

962. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , amesema: "Matumizi ya kupita kiasi cha kile kinachohitajika, ni ufujaji ."[149]

963. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) , amesema: "Lau watu wangekuwa na tabia ya kula kwa kiasi, basi miili yao ingekuwa na nguvu ."[150]

964. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Hakuna mtu anayepita makaburini isipokuwa waliokufa wanamwambia: 'Ewe uliye ghafilika! Je unaelewa yale tulivyoeleweshwa sisi, itakufanya wewe damu yako ipoozwe ." Irshadul- Qulub.

USHAURIANO

965. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Hakuna mtu anayepita makaburini isipokuwa waliokufa wanamwambia: 'Ewe uliye ghafilika! Je unaelewa yale tulivyoeleweshwa sisi, itakufanya wewe damu yako ipoozwe." Irshad-ul- Qulub.

966. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Iwapo watawala wenu ni watenda wema, na matajiri ni wale wenye kukushukuruni, na mambo yenu yanakwenda kwa ushauriano miongoni mwenu, basi kwenu nyinyi kuishi duniani ni vyema kuliko chini yake. Lakini iwapo watawala wenu ni waovu kwenu nyie, na matajiri ni mabakhili miongoni mwenu, na mambo yenu yanakwenda bila kushauriana, kwa hivyo kwenu nyie kutakuwa afadhali kuwa ndani ya ardhi kuliko kuishi juu yake ." [151]

967. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Yeyote yule anayeshauriana pamoja na wenye busara na akili, kwa ajili ya kupata mwangaza ili aweze kupata mwanga katika masuala yake (na ataweza kuona sahihi kile kilicho sawa kutoka na kile kilicho potofu) ."[152]

968. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , amesema: "Yeyote yule anayeshauriana pamoja na watu wa maelewano, basi huonyesha maendeleo yake ."[153]

969. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Hakuna muumin atakaye kuwa mwovu kwa ushauriano, na wala hakuna atakayefaidika kwa ukaidi wake ." [154]

KUFANYA KAZI NA KUKAA BURE

970. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Ibada imegawanyika katika matawi sabini, na bora ni kule mtu kujitafutia riziki halali ." [155]

971. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , amesema: "Kamwe, Kamwe hakutapatikana raha na starehe za maisha kwa kubakia bila kazi au kuwa mvivu ."[156]

972. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) , amesema: "Jiepusheni uvivu na kutokuridhika. Na haya mawili ndio ufunguo wa kila aina ya maovu ."[157]

973. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . aliambiwa na Sa'ad Ansari kuwa mikono yake imekufa ganzi au imekuwa ngozi ngumu ni kwa sababu ya kufanya kazi kwa kutumia kamba na koleo kwa ajili ya kupata pesa kwa ajili ya kutumia yeye, mke na watoto wake. Kwa kusikia hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . aliibusu mikono yake (akionyesha heshima) na akasema: "Kwa hakika huu ndio mkono ambao moto wa Jahannam kamwe hautaugusa ." [158] .

SHAHIDI NA SHAHADA

974. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ., amesema: "Kuna jema kwa kila jema hadi wakati mtu anapouawa katika njia ya Allah swt na zaidi ya hapo hakuna tena jema lingine juu yake. (Kupigana dhidi ya maadui Waislam ambao wanawaua Waislam) "

975. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Yeyote yule anayeuawa katika njia ya Allah swt kama shahidi, basi yeye kamwe hataulizwa chochote kuhusu madhambi yake. (Madhambi yake yote yatakuwa yamesamehewa kwa ujumla) ."[159]

976. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "kwa kiapo cha yule ambaye maisha na roho yangu iko mikononi mwake, iwapo viumbe vyote vya duniani na angani vikijumuika pamoja kumuua muumin ambaye hana kosa hata moja au watakapo shawishiwa kufanya hivyo, basi Allah swt atawatia wote kwa pamoja katika moto wa Jahannam ." [160]

977. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Hakuna tone ambalo linalopendwa na Allah swt kuliko tone la damu ya yule, linalomwagika akiwa anakuwa shahidi katika njia ya Allah swt ." [161]

MTARAJIWA AL-MAHDII(A.S) NA UTAWALA WAKE WA HAKI

978. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Al Mahdi anatokana na kizazi changu kutokea kwa wana wa Fatma Bi Zahra (a.s) . "[162]

979. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema kuwa: "Mwenye furaha ni yule ambaye ataweza kumfikia Al-Qaim(a.s) . wa Ahlul Bayt(a.s) . na kumfuata kabla ya kudhihiri kwake. Mtu huyu atawapenda wapenzi wa Imam Al Mahdi(a.s) . na atawachukia maadui wake, na atakubalia uongozi wa Maimam(a.s) . kabla ya kudhihiri kwake. Na hawa ndio marafiki zangu, na kwa hakika hawa ni watu halisi katika umma wangu ambao mimi ninawatukuza sana."[163]

980. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Allah swt atamwinua mtu mmoja kutokana na kizazi changu, kutokea Ahlul Bayt (a.s). yangu, kwa kuja kwake ardhi hii itajazwa kwa uadilifu kama vile ilivyojaa sasa hivi kwa dhuluma na kukosekana kwa hak i." [164]

981. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Mtu yeyote atakayekufa bila kumjua Imam wa Zama zake (Imam wa zama zetu hizi ni Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan (a.s).) Basi atakuwa amekufa kama vile walivyo kuwa wakifa katika zama za Ujahiliyyah ." [165]

982. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema kuwa: "Atakapo dhihiri Al Qaim (a.s) , basi mbingu itanyesha mvua, ardhi itaotesha miti yake, uadui utakwisha kutoka mioyo ya waja (ili kwamba wote waweze kuishi kwa amani na mapenzi ya kindugu), na wawindaji na wanyama wataendelea kuishi kwa amani kwa pamoja "[166] .

983. Abil Jarudi amesema: "Mimi nilimwuliza Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . iwapo yeye alikuwa akijua kuhusu mapenzi yangu na utiifu wangu kwake, naye alinijibu kuwa alikuwa akijua. Nami nikamwambia kuwa nilikuwa na swala nililokuwa nikitaka kumwuliza ili aweze kunijibu, kwa sababu mimi nilikuwa kipofu na nilikua nikitembea kwa uchache sana, na hivyo nilikuwa siwezi kumtembelea kila mara. Naye alinitaka mimi nimwulize swala nililokuwa nikitaka kumwuliza. Hivyo mimi nilimwomba anijulishe dini au madhehebu yeye na Ahlul Bayt(a.s) . wanayoifuata na ambayo inapendwa na Allah swt, ili nami niweze kufanya 'ibada ya Allah swt kwa mujibu wa madhehebu hayo." Kwa hayo Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . alinijibu: "Kwa hakika wewe umeniuliza swala kubwa sana, ingawaje umeniuliza kwa kifupi sana. Kwa kiapo cha Allah swt mimi ninakujibu kuhusu dini yangu na dini ya mababu zangu kupitia huyo tunavyomwabudu Allah swt. Nayo ni: 'Kwa kukiri imani yetu kuwa hakuna Allah swt mwingine isipokuwa ni Allah swt, na kwamba Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . ni Mtume wa Allah swt, na kusadiki kuwa chochote kile kilichomteremkia yeye (Qur'an Tukufu) ni kutoka kwa Allah swt, na kuwa na mapenzi (yetu) ya wapenzi wetu na watiifu kwetu (Ahlul Bayt(a.s) . na kuwachukia maadui wetu, kujisalimisha kwa njia yetu, na kumsuburi Al Qaim(a.s) . (Imam wa kumi na mbili ambaye atadhihiri pale itakapotokea amri ya Allah swt), na kutaka (kudumisha yale yaliyofaradhishwa na mambo yaliyo halalishwa) na kwa kuwa mcha Allah swt halisi (kwa kujiepusha na yale yote ambayo ni haramu).[167]

984. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . amesema: "Atakapo dhihiri Al Qaim(a.s) , basi mikono yake itakuwa juu ya vichwa vya waumini, naye atawapa maendeleo ya kiakili na kukamilisha subira yao na kile wanacho kiangalia mbele. Baada ya hapo Allah swt ataongezea nuru yao macho na uwezo mkubwa wa kusikiliza ili kwamba kamwe kusitokezee vizuizi baina yao na Al Qaim(a.s) . pale atakapo amua kuongea nao, na watakapomsikiliza, wataweza kumwona ilhali atakuwa mahala pake."[168]

985. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) , amesema: "Wakati wa Al Qaim(a.s) . muumin atakaye kuwa mashariki ataweza kumwona muumin mwenzake aliye magharibi, na vivyo hivyo muumin aliye magharibi ataweza kumwona muumini aliye mashariki.[169]

Tanbih : Ndugu msomaji! Kwa hakika sasa hivi tunayo ala za mawasiliano mbalimbali kama vile Satellite, Television yafuatayo ambayo yanaweza kuwa yenye manufaa makubwa kwetu ili kuwaza kuangalia vyema na kuelewa hiyo riwaya vitu ambavyo havikuwapo wakati maneno matukufu ya riwaya hiyo yalipokuwa yakisemwa.

986. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) , amesema: "Huyu Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan(a.s) . atakuwapo mahala ambapo ni karibu na Al Ka'aba Tukufu baina ya nguzo na nafasi ya kusimamia ya Mtume Ibahim(a.s) . na atatoa mwito, atakapo kuwa akisema: 'Enyi watu wangu hasa ambao Allah swt amewawekeni kwa kuwatayarisha nyinyi kwa ya furaha ya kudhihiri kwangu juu ya ardhi hii! Njooni kwangu kwa utiifu. Na kwa hakika kauli hii itawafikia wale wote watakapokuwa nafasi wanaposalia na hata kama watakuwa vitandani wakiwa mashariki ya ardhi au magharibi yake. Na watamsikiliza kwa mwito wake huo mmoja tu ambayo yatafikia kila sikio la kila mtu, nao watajitayarisha kwa ajili ya kuja kwake. Kwa hakika haitawachukua muda wowote isipokuwa pumzi tu kiasi kidogo kukusanyika hapo baina ya mlingoti na nafasi ya kusimama ya Mtume Mtume Ibahim(a.s) , wakimwitikia Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan(a.s) ."[170]

987. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alimwambia mfuasi wake aliyekuwa halisi, Mufadhdhal, mambo fulani kutokea kisa cha Al Imam Muhammad al-Mahdi Sahibuz-Zamaan(a.s) . na kudhihiri kwake, "Ewe Mufadhdhal! Waambie wafuasi wetu habari za Al-Mahdi ili wasiwe na shaka katika Dini yao ."[171]

988. Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan(a.s) , amesema: "Mimi ni Al Mahdi na mimi ni yule ambaye bado nipo hai na ambaye nitaijaza ulimwengu kwa haki na uadilifu kama vile ilivyojazwa kwa maovu na dhuluma. Kwa hakika ardhi haitabakia bila ya kuwa na mbashiri, na watu kamwe hawataisha bila ya kuwa na kiongozi. Na hii ni amana na hivyo msiwaambie wote wale Waislam wenzenu isipokuwa wawe ni watu wa Allah swt (wawe katika haki) ."[172]

989. Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan(a.s) . amesema: "Kwa mambo yanayotokea kwa Waislam, murejee katika riwaya zetu, ( yaani Wanazuoni au Ma'ulamaa), kwa sababu wao ndio wawakilishi wangu kwenu na mimi ni Hujjatullah juu yao ."[173]

990. Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan(a.s) . alimwandikia barua Sheikh Al Mufid: "Sisi tunaelewa hali yako na mazingara yako na hakuna jambo lolote lako lililojificha kwetu sisi ."[174]

991. Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan(a.s) . alimwandikia barua Sheikh Al Mufid: "Si kwamba sisi hatukujali wewe au tumekusahau, kwa sababu kama ingekuwa hivyo, matatizo na balaa zingekuwa zimekuondokea wewe na maadui wako wangekuwa wameisha kumaliza. Hivyo, muogope Allah swt na uwe mtiifu kwake, asifiwe Allah Jalli Jalalahu."

Dua : Tunamwomba Allah swt aharakishe kudhihiri kwa Imam wetu wa kumi na mbili Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan(a.s) . ili aweze kudumisha usawa, ukweli, na haki katika ulimwengu mzima. Amina.

2

MUANDAMO WA MWEZI

SURA YA PILI

JAWABU KWA WANAFUNZI WA BACHOO JAWABU YA UTANGULIZI

Wahusika ndugu zetu wa Masjid Al-Sunna Zanzibar, wameanza kitabu chao hicho kwa utangulizi wenye kumshukuru na kumuhimidi Allah na kumtakia rehema na amani Bwana wetu Muhammad (s.a.w.) kama zilivyo khutuba na vitabu vya kiislamu. Na hayo yote yamefanyika chini ya utangulizi wenye anwani:

UKWELI JUU YA KUANDAMA KWA MWEZI

Na hii ndio sehemu ya kwanza ya kitabu chao. Wakasema katika utangulizi huo: Msisitizo wetu mkubwa katika kitabu hiki ni ile nukta muhimu ya kwamba suala la kufunga na kufungua kwa muandamo mmoja kwa dunia nzima si jambo jipya kama wanavyodhani baadhi ya watu, ni jambo la kale mno ambalo linaweza kutekelezeka na kwamba huo ndio uliokuwa msimamo wa 'Jamhur' ya wanavyuoni.

Jawabu Nakubali kuwa hili ni jambo la zamani, lakini kudai kuwa hii ni kauli ya Jumhuri ni madai hewa: hayana ushahidi. Leo hii duniani hakuna madhehebu yoyote ambayo inaitendea kazi kauli hio kama ni madhehebu nzima, bali kuna baadhi ya watu tu katika kila madhehebu ambao wanafata kauli hio. Hata zile madhehebu ziliotajwa kuwa ni zenye kufata kauli hio kama vile Malik, Hanbal na Hanafi, basi hawaitendei kazi kauli hio ila baadhi yao tu. Libya, Algeria na nchi nyengine za Afrika Kaskazini na Magharibi - kwa mfano - ni nchi za wafuasi wa madhehebu ya Malik, nao wanafata miandamo yao wenyewe. Kwa hivyo, dai kuwa hii ni kauli ya Jumhur ya wanavyuoni, si dai sahihi.

SEHEMU YA PILI

Katika sehemu ya pili, ndugu waandishi wanasema:

2. Si Fikra Za Shaykh Naaswir Bachuu "Ndugu yetu Juma Muhammad Rashid Al-Mazrui amejitahidi kuandika kitabu alichokiita: "Ushahidi Uliowekwa Wazi Katika Suala La Miandamo Ya Mwezi. Makusudio yake yalikuwa ni kutaka kukijibu kitabu kilichoandikwa na Shaykh Naaswir Abdullah Bachuu kinachojulikana kwa jina la "Ufafanuzi Wa Mgogoro Wa Kuandama Kwa Mwezi."

Jawabu Kidogo na mimi naomba niweke wazi kwamba kitabu changu hakikuwa kabisa na lengo la kujibu kitabu cha Sheikh Nassor Bachoo. Hili la kunukuu maneno yake na kuyajadili lilikuwa ni jambo la kutokea tu baada ya mtu Fulani kuniletea kitabu chake. Kwa havyo, kama mulivyosema nyinyi katika kitabu chenu kwamba: Kitabu hiki ni kama nasaha kwa Waislamu wote ili kuweza kudumisha umoja wetu hususan pale ambapo pamejitokeza misimamo tofauti katika mambo ya ibada. Wala lengo la kitabu hiki sio kuendeleza malumbano baina ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe hata kwa wale wenye misimamo tofauti. Kutajwa ndugu yetu Juma Muhammad Rashid lilikuwa ni jambo lisilobudi wala hapakuwa na lengo la kumkashifu au kumuumbua bali ni kutokana na kuwa hapakuweza kupatikana njia mbadala kwa vile ameshaandika kitabu ambacho ameshakichapisha chapa ya kwanza na ya pili.

Basi na mimi nakuombeni munielewe hivyo hivyo, kwamba wakati mimi naikubali fikra Fulani na kuikataa fikra Fulani, hakuna budi ninukuu fikra pinzani na kuonesha kwanini siikubali; na kwa upande wa pili ni lazima nioneshe kwanini naikubali fikra ninayoikubali. Na nitaposema kuwa kuna watu wana fikra hii, basi nadhani haitokuwa jambo la busara kama watu hao sikuwataja na nikiwataja ni lazima nitaje marejeo. Kwa sababu hii ndio maana nimekuwa nikinukuu maelezo ya Sheikh wetu Nassor Bachoo na kumjadili mule nisimokubaliana naye. Naomba musihuzunike kwani kujibizana katika kutafuta ukweli ni suala mashuhuri katika uwanja wa elimu. Wanavyuoni wakubwa wa kale na wa sasa wamekuwa wakijibizana ili kutafuta ukweli na hatimae huwabainikia woa pamoja na wasomaji. Kwa hivyo, hamukuwa na haja ya kutumia lugha: "Wala hapakuwa na lengo la kumkashifu": hii si kashfa hata kidogo: hii ni elimu.

Lakini, hakuna haja ya kufichana; kitabu chenu mumeandika kwa kujibu kitabu changu. Hamuna haja ya kusema: "Wala lengo la kitabu hiki sio kuendeleza malumbano baina ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe hata kwa wale wenye misimamo tofauti. Kutajwa ndugu yetu Juma Muhammad Rashid lilikuwa ni jambo lisilobudi wala hapakuwa na lengo la kumkashifu au kumuumbua bali ni kutokana na kuwa hapakuweza kupatikana njia mbadala kwa vile ameshaandika kitabu ambacho ameshakichapisha chapa ya kwanza na ya pili", kwani kitabuchenu kimeanza kwa kunitaja mimi mwanzo hadi mwisho na kuniaga kwa kunipa nasaha mimi. Ama mimi naandika jawabu hii kukujibuni nyinyi: sikufichini wala sisemi uwongo.

Munasema Kutokana na jambo hilo , sisi kwa upande mmoja tunashukuru kwa juhudi yake hiyo na kwa upande wa pili tunatuma masikitiko yetu kwake kwa kutokuwa makini na muadilifu katika kulifafanua jambo hilo muhimu. Kwani kitabu chake hicho kimeandikwa katika mfumo wa chuki, kibri, kejeli na malumbano huku akisisitiza kwa mara nyingi kauli chafu ambazo muandishi hapaswi kuzitumia katika kitabu au katika mijadala ya Dini. Jawabu Hizi chuki, kibri na kejeli, mimi nimezisoma kwenu, kwa hivyo na iwe kama msemo wa Waswahili: "Papa akipea mafuta huwapa wanawe". Je nyinyi munayakumbuka haya:

1) Munaukumbuka muhadhara wa Sheikh Bachoo ambao alisema kuwa wasionyanyua mikono katika sala wanasali kama mipopoo? Jamani! Hii si kejeli? Je katika nyinyi yuko aliyetoa muhadhara au kuandika kitabu ili kumjibu Sheikh wetu. Sasa uadilifu uko wapi?

2) Je munaukumbuka muhadhara wa Sheikh Bachoo aliozungumzia mas-ala ya udhu kasha akasema: "Wengine wakitia udhu kiungo hiki huomba dua hii na kiungo hiki huoma dua hii; upumbavu mtupu". Je haya si matusi? Je hii si kejeli?

3) Siku moja palikuwa na maziko. Maiti alisaliwa msikiti wa wajiitao "Watu wa Sunna". Kijana mmoja akasimama akasema: "Leo tunataka kukuonesheni vipi Mtume (s.a.w.) kamsalia maiti: si kama wanavyofanya Ibadhi na Shia.

4) La nne ni kuwa ikiwa nyinyi mumethubutu kunita mjeuri, mwenye kibri na kejeli; maneno ambayo mimi sikukwambieni wala kumwambia Sheikh Nassor; mimi nimemtoa makosa tu Sheikh wetu: na hii ni kawaida katika uwanja wa elimu; sasa je na nyinyi pia ni majeuri, wenye kibri na kejeli? Katika uwandishi wenu, pia mumesema: "Hatujui dhana hii potofu ameitoa wapi." Mwenye dhana potufu naye ni mpotufu, kwa hivyo na nyinyi hamukutoa nasaha bali mumetukana. Nakupeni mifano hii mitatu ya Sheikh wetu na mmoja wenu nyinyi wenyewe enyi wenye kuandika Radan mardudan na mifano iko mingi. Inatosha kuwaita kwenu watu wengine kuwa ni watu wa bidaa na nyinyi ndio watu wa Sunna. Kwa hivyo, hii hali mumeiuda nyinyi wenyewe: Zanzibar bali Afrika Mashariki na Dunia kwa ujumla haikuwa hivi. Chuki mumeziunda nyinyi; mukijirekebisha kwa kutumia lugha nzuri nadhani hakuna atayekwambieni jambo kwa lugha nzito.

Mnasema Mfano wa kauli zake mbaya ni kama zifuatazo:

(vuta-nikuvute) [uk. 6]

(hii ni ajabu katika ajabu za dunia!) [uk. 124]

(Kwa hivyo, uwezekano huo alioutoa Sheikh hauwashi wala hauzimi [uk. 124]

(Ninasema: Enyi walimwengu wenzangu tazameni hoja za kielimu hizo!!!!!!! Kwani nyinyi Wazanzibari kabla ya kuja fikra hio ya Sheikh Nassor Bachoo ya kufunga kwa muandamo mmoja,)

(Utaona kwamba masuala yote haya si yenye kima katika soko la elimu, bali ni masuala ya kuwababaisha watu wasiojua nini cha kujadiliwa katika mas-ala haya ya funga) [uk. 167]

(Hoja nyengine - nayo pia ni hoja ya mitaani - ni kuwa watu wengi wa kawaida wanapouona mwezi mkubwa husema: "E basi ule ndio mwezi wa leo ule?!!!")

(Jawabu hii ya mwisho, inaufanya upinzani mzima wa Sheikh Bachoo kuwa hauna maana yoyote.) [uk. 132]

(Kwa ufupi ni kuwa hicho walichokidai watetezi wa rai pinzan) [uk. 32]

(utaona jinsi gani mwanamume alivyokuwa bingwa wa kubadilika! Na hili si jengine bali ni lile Waswahili wanalolisema: "Mfa maji hukamata maji.") [uk. 128]

(Hakuna hapa kinachoonesha mas-ala ya kufunga kwa muandamo mmoja wala kumi na moja.)) [uk. 125] (haina maana kwamba usiku ukiingia sehemu moja ndio umeingia dunia nzima. Kwa ufupi ni kuwa hii ni hoja ambayo haina faida yoyote ya kielimu, lakini tunaijadili kwa ajili ya watu wa mitaani tu.)

Jawabu Sikubaliani na nyinyi kwamba humu muna maneno mabaya. Lakini hata nikikubali basi nasema kwamba lugha ya namna hii sababu ni nyinyi, na kwa hivyo, utaona kwamba ninapojadiliana na watu wengine basi lugha yangu hubadilika. Kwa hivyo, tujirekebisheni sote na tujadili tafauti zetu kwa lugha ya kiungwana. Ama ukinita mpopoo, basi usinilaumu na wewe nikikwita mnazi: unanilaumu nini na wewe unakifanya kile kile nikifanyacho?! Bali hata katika kitabu hiki munachonijibu, basi nanyi mumetumia lugha hizo hizo. Katika baadhi ya sehemu umesema: "Kwa hakika katika kitabu chake hicho kwenye uk 6, anajionyesha alivyo na kauli mbili tofauti..". Na mwishoni mwa kitabu mumesema: "Dhana ya pili ya ndugu Juma imejengeka katika msingi dhaifu wala haina nafasi katika uwanja wa fani (kitaalamu) nao ni kule kusukuma kwake juu ya elimu ya Jiografia". Na yamo mengi katika kitabu chenu. Sasa nyinyi mwasema nini na mwatenda nini?

Munasema "Kwa hakika katika kitabu chake hicho kwenye uk 6, anajionyesha alivyo na kauli mbili tofauti: Kwanza anakubali kwamba suala la muandamo wa mwezi lina ikhtilafu katika kufunga kwa kumuelezea Shaykh Naaswir Bachuu kwamba: (Tunampongeza kwa juhudi) Kisha pale pale anageuka kwa kusema: (madamu hili ni suala la khilafu - basi i likuwa ni kutolizungumza kabisa,) Sasa hebu tumuulize ndio anapongeza nini? Na ni nani aliyemwambia kwamba jambo lenye khitilafu halizungumzwi? Yeye angezungumza nini katika kitabu chake kama si masuala ya ikhtilafu? Pia anatwambia haya ni katika mambo ya furui (matawi) za Kidini, kwa hivyo zisizungumzwe. Kwani ni nani aliyemwambia kuwa furui za Kidini hazizungumzwi?"

Jawabu Ikiwa lugha hii ndogo hamukuweza kuifahamu, vipi mutaweza kufahamu kitu chenye kuhitaji fani za lugha na usuli na mengineo. Ikiwa mimi niliingia msikitini kwenu Raha Leo nikakuta juu ya ubao wenu munawasomesha vijana na katika darsa hio Mubtadaa mumemwita Fa'il (vipi mutaweza kujadili masuala haya?!!! Mimi nimempongeza Sheikh Bachoo kwa juhudi au moyo wake; na sikumpong eza kwa kulikuza suala ambalo:

1) Ni la furuu'i

2) Lina khilafu. Na hii haina maana kuwa Furu'i zisizungumzwe; suala la Furu'i huwa halishadidiwi; bali unawaacha watu kama walivyo tu. Lakini yeye anapenda kushadidia katika mas-ala kama haya; ndio maana akashadidi hata katika suala la kufunga mikono hata kuwaita watu mipopoo bali na kuwambia kuwa hawana Sala. Kwa hivyo, nieleweni kwamba ninachokipinga ni kushadidia au kuwakoroga watu katika kitu ambacho ni furu'i za dini ilhali yeye kawakuta na msimamo tafauti tangu zamani. Katika mas-ala ya furu'i, wanavyuoni huwa hawashadidi juu ya Mas-ala kama haya. Mimi leo nikisimama nikaanza kufanya kampeni kwamba watu wasiitikie amina wa kisali, nalo ni jambo la furu'i, si nitakuwa natia fitna tu? Jambo kama hili huwachwa wasomi wakalitafiti kaiha kila mmoja akafanya vile ilivyombainikia. Lakini kufanya kampeni maalumu na da'awa kana kwamba waliotangulia wote ni wapotovu, hili ndilo jambo la kulaumiwa.

Ama kauli yenu: "Kwanza anakubali kwamba suala la muandamo wa mwezi lina ikhtilafu katika kufunga kwa kumuelezea Shaykh Naaswir Bachuu kwamba: (Tunampongeza kwa juhudi) Kisha pale pale anageuka kwa kusema: (madamu hili ni suala la khilafu - basi ilikuwa ni kutolizungumza kabisa,) Sasa hebu tumuulize ndio anapongeza nini?" Mwisho wa kunukuu. Na mimi nikuulizeni nyinyi mumenishukuru kwa juhudi yangu kisha mwisho wa kitabu mukaniambia: "Mwisho tunachukua fursa hii kumuonya ndugu Juma kuwa amuogope Mwenyezi Mungu hususan katika mas-ala ya kielimu. Akumbuke kuwa Mwenyezi Mungu Ameonya juu ya mtu kusema jambo au kufanya asilolijua. Aelewe kwamba ataulizwa juu ya hilo. Lingekuwa jambo la busara kama ndugu Juma angalikubali kuuliza na kufanya utafiti zaidi juu ya mas-ala haya kama agizo la Mwenyezi Mungu linavyotutaka". Sasa na nyinyi munanishukuru nini?

Munasema "Sisi tunapenda kumfahamisha kuwa suala hili la kwamba mwezi ukiandama sehemu moja unatosheleza kufuatwa kwa kufunga au kufungua ulimwengu mzima, si suala jipya bali ni jambo la kale. Tunasikitika kwamba hakuangalia vizuri maoni ya Wanavyuoni wakubwa walivyoelezea msimamo huo. Angalia katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu uk 51-58. Hapa tunanukuu baadhi ya kauli hizo:

Imamun-Nawawy aliyekisherehesha Kitabu cha Sahihi Muslim anasema:

"Na jambo lililo sahihi kwa wenzetu (Mashaffi) ni kuwa muandamo mmoja hauwahusu watu wote bali unawahusu wale walio karibu kwa kiasi ambacho hawaruhusiki kupunguza Sala (Sala ya safari). Pia imesemwa kuwa iwapo matlai ni mamoja watalazimika (watu) kufunga pamoja. Pia imesemwa kuwa ikiwa (wanaishi) katika eneo la Iklimu moja (maili 72 au km 89) (watalazimika kufunga pamoja) vyenginevyo kila mmoja atafunga kwa muandamo wake. Na wakasema wenzetu wengine (Mashaffi) kuwa muandamo katika sehemu moja utawahusu wote wa dunia nzima".

Shaykh Jaadul Haq wa chuo kikuu cha Al-Azhar katika kitabu chake "Bayaanullinnas" J. 2 uk 203 - 204 ameandika yafuatayo juu ya kauli hiyo ya Imamun-Nawawy:

"Hapa Imamu An-Nawawy ametaja kwa mukhtasari kauli zilizomo katika madhehebu ya Kishaffi (juu ya kuandama kwa mwezi) na ambazo pia zimo katika madhehebu mengine ya Kiislamu. Kauli hizo tunaweza kuzigawa katika maf ungu matatu makuu: "...Hapo Imamu An-Nawawy ametaja kwa mukhtasar kauli zilizomo katika madhehebu ya Shaffi (juu ya kuandama kwa mwezi) na ambazo pia zimo katika madhehebu nyengine za Kiislam. Kauli hizo tunaweza kuzigawa katika mafungu matatu makuu: Kauli ya kwanza: "Kila nchi iwe na matlai yake, wala muandamo wa nchi moja hautalazimu nchi nyengine ya mbali wala karibu". Kauli ya pili: "Muandamo wa nchi moja unalazimu nchi zote za dunia hata kama ziko mbali".

Kauli ya tatu: "Muandamo wa nchi moja unalazimu nchi iliyo karibu nayo au inayowafikiana kimatlai". Kisha, Shaykh Jaadul-Haq akaendelea kusema kwamba:

"Na (kauli) zote hizo ni maoni yatokanayo na Ijtihaadi ambazo hazikusimama juu ya hoja kat-ii, si sanad wala matni. Kwa hivyo ingefaa ichaguliwe kauli ambayo inakubaliana na maslahi ya (Waislam wote wa) dunia nzima kwa jumla"."

Jawabu Sikubaliani na mtazamo wa Sheikh Shaykh Jaadul Haq wa chuo kikuu cha Al-Azhar, kwamba zote hizi ni rai na itihad kwani kanuni ni kuwa "Hakuna ijtihadi mbele ya andiko" Ijtihad mwahala mwake ni musimo andiko. Wakatika katika suala hili, utaona kwamba asemaye kuwa tufunge kwa muandamo mmoja, hoja yake ni Hadithi "Fungeni kwa kuuona"; na anayesema kuwa kila mahala na muandamo wake, anatoa ushahidi wake ni Hadithi ya Ibn Abbaas na Kuraib. Kwa hivyo, ijtihad ni katika kuyafahamu maandiko: si ijtihad kwa maana ya rai tupu pasi na andiko kama alivyosema Sheikh. Kilichobaki ni kuzijadili riwaya mbili hizi zina maana gani?

Munasema Tungependa kumueleza ndugu yetu kwamba hata hapa Afrika ya Mashariki jambo hili hakulianzisha Shaykh Naaswir Bachuu kama alivyodai mwenyewe (Nd. Juma) kwamba: (Muafrika wa Mashariki wa kawaida kusikia sauti ya mgogoro)) Inasikitisha hakuweza kuangalia katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu uk 161-163 wametajwa walioonyesha kwa vizuri kabisa misimamo hiyo tofauti. Mashaykh wenyewe ni hawa wafuatao: Al-marhuum Shaykh Juma Abdul Waduud (wa Zanzibar), Shaykh Abdillahi Naaswir ( Nairobi Kenya ), na Shaykh Naaswir Khamis Abdul Rahman ( Mombasa Kenya ).

Jawabu Kwani wapi katika kitabu changu nilisema kuwa Sheikh Nassor Bchoo ndiye aliyeanzisha fikra hii hapo Afrika ya Mashariki hata mukaleta dai hili? Mimi nimeeleza kuwa zamani Afrika Mashariki watu wote wakifata muandamo mmoja. Nilisema: Karne zimepita bila ya sikio la Muafrika wa Mashariki wa kawaida kusikia sauti ya mgogoro juu ya suala la muandamo wa mwezi. Harakati za elimu zilipobadilika na kuelekea zaidi - kwa kujua au bila kujua - katika mrengu wa Kihanbali na Kiwahabi, pakajitokeza mapinduzi ya ghafla ya fikra na matendo. Dr. Ramadhan Al-butti - miongoni mwa wanavyuoni wakubwa wa ulimwengu wa sasa - anaona kwamba harakati hizi hazisifiki kama ni madhehebu: bali ni hatua (phase) katika mapito ya Historia.

Na katika uk. 97, nimesema:

Kwa kwetu - Afrika Mashariki - kusema kwamba mwezi muandamo wa nchi moja ni muandamo kwa nchi nyengine zote za dunia ni kitu kipya. Kwa hivyo, ni wazi kwamba mimi nazungumzia Afrika Mashariki. Na mfano wa hilo pia kalisema Sheikh Nassor Bachoo, lakini yeye hamukumjibu. Anasema: "Pamoja na kuwa mgogoro wa kuandama kwa mwezi umeanza kuonekana hadharani katika jamii za Waislam wa hapa Afrika ya Mashariki katika miaka ya hivi karibuni". Inasikitisha kwamba hata maneno yangu mumeyakata na kuchukua yale ambayo hayakamilishi maana nilioilenga. Maneno "Karne zimepita" hamukuyataka kwani hayakufikisheni kule mutakako!

Pili narejea tena kusema kwamba hao wanavyuoni aliowataja Sheikh Nassor, hawajathibitisha habari za kuwa watu wafunge au wakifunga kwa muandamo mmoja Africa Masharik, ukimtoa Sheikh Nassir Khamis wa Mombasa ambaye naye pia ni mtu wa sasa. Ama sheikh Juma Abdu-Wadood yeye, kwa mujibu wa nakala hio ya Sheikh Nassor Bachoo, kasema hivi: Kuona huku kwa mwezi kumekusudiwa kuonekana na Waislam, na kuonekana na Waislamu huko, sio lazima kuonekana na Waislamu wote. Bali inatosha shahada ya mtu mmoja muadilifu".

Pia inampasa mtu mmoja pekee kama ameuona mwezi yeye afunge na kila aliyemuamini; hata akiwa haijakubaliwa shahada yake. Haya ndio maneno ya Sheikh Juma Abdu-Wadood kwa mujibu wa alivyomnukuu Sheikh Bachoo. Sasa ikiwa ndugu zetu mumeshindwa kuyafahamu maneno haya ya Sheikh Juma Abdu-Wadood, bado mutaendelea kupoteza watu bila ya elimu?! Sheikh Juma Abdul-Wadood hapa anazungumzia mas-ala ya ushahidi kwamba si lazima - katika suala la kuonekana kwa mwezi - kwamba kila mmoja auone: bali akiona mtu mmoja basi inatosha kwa wengine kufunga. Hii ndio kauli ya Sheikh Juma Abdul-Wadood na hili nimelieleza kwa urefu katika kitabu changu.

Kisha Sheikh Juma Abdul-Wadood akazungumzia suala la kufunga kwa muandamo mmoja akasema: "Rai za Maimamu wengine wameifasiri hadithi isemayo: (Fungeni kwa kuuona Mwezi) kwamba ukionekana popote mashariki au magharibi (watu) wafunge; hapana kutazama masafa fulani au nini. Hii ni rai nayo na wengi wamesema (hivyo) kama Imamu Malik , Ahmad na kundi kubwa la Hanafi. Inakurubia kuwa n dio rai ya Jamhuri - kufata rai hii ni kuhakikisha umoja wa dunia nzima. Wala hatuwezi kusema kwamba rai ya Shaffiy ndio ya Jamhur". Hapa Sheikh Juma anasimulia rai za Maimamu wengine: si rai za Maulamaa wa Afrika Mashariki. Mimi dai langu nililodai ni kuwa jambo hili la kufunga kwa muandamo mmoja, napenda munifahamu: ni jipya kwa Africa Mashariki. Mimi sikusudii jambo la wanazuoni kuzungumzia rai mbali mbali: bali nazungumzia jambo la watu kufata muandamo mmoja kwamba karne zimepita ya sikio la Muafrika Mashariki wa Kawaida halijiapata kusikia. Na nimetumia maneno "Muafrika wa Mashariki wa kawaida" ili kuwatoa wanavyuoni wao hata kama walikuwa hawafati kauli hio, lakini wanaijua. Kwa hali yoyote ile:

1) Sheikh Juma Abdul-Wadoo hajazungumzia kwamba Afrika Mashariki watu walikuwa wakifunga au wafunge kwa muandamo mmoja, bali kazungumzia rai za wanavyuoni wasio wa Afrika Mashariki - Al-Imamu Shafi, Hanbal n.k. Na mimi sijakanusha tafauti hizi.

2) Kauli yake ilikuwa ni kuhusu suala la mashahidi.

Ama Sheikh Abdillahi Nassir, yeye ni mwanachuoni wa sasa. Na mimi sijasema kuwa sasa hakuna rai hizo. Pili ni kuwa nakala alizotupa Sheikh Bachoo za kitabu cha Sheikh Abdillahi utaona kwamba Sheikh Abdillahi hazungumzii kuwa kauli ya kufatwa ni ile ya muandamo mmoja; bali yeye kasema kuwa hili ni suala la khilafu kwa hivyo tusigombane kila mtu afate rai anayoiona kuwa ni sawa. Sheikh Abdillah kayasema haya baada ya kutokea mizozo hii ya sasa. Kwa hivyo tunarudi pale pale kwamba "Karne zimepita bila ya sikio la Muafrika wa Mashariki wa kawaida kusikia sauti ya mgogoro juu ya suala la muandamo wa mwezi. Harakati za elimu zilipobadilika na kuelekea zaidi - kwa kujua au bila kujua - katika mrengu wa Kihanbali na Kiwahabi, pakajitokeza mapinduzi ya ghafla ya fikra na matendo". Kwa hivyo, nukta hii hamukuuijibu: na wala sioni kuwa kuna haja ya kuijibu kwani haina umuhimu katika maudhui yetu. Bali kitabu chenu chote, munachagua mambo yasio na umuhimu "Juma kantutukana; Juma kanfanya hivi" nyinyi ndio munajibu baada ya kuzungumzia dalili za kielimu.

Ama Sheikh Nassor: yeye pia ni mtu wa sasa na ni mfuasi wa skuli hio hio munayoifuata nyinyi, kwa hivyo kusema kwake alivyosema hakujapindua nilioyasema kuwa - kimatendo - hili ni suala jipya kwa kwetu Afrika ya Mashariki. Wala mimi sikusema kuwa Sheikh Nassor Bachoo ndiye muasisi wa fikra hio huko kwetu. Naomba munifahamu ninachokisema kwanza kisha ndio munijibu. Na sijui munapinga nini kitu ambacho watu wote wanakijua. Bila ya kusahau kwamba mimi sikusudii kusema kuwa kitu sahihi ni kilichofanywa zamani au kilichofanywa leo: laa! Bali kitu sahihi ni chenye ushahidi sahihi uliojengeka juu ya misingi sahihi ya kielimu. Na kielimu, suala la kuzingatia muandamo mmoja - hamutoweza kulithibitisha.

MNASEMA

Pia Shaykh Ahmad Al Khalil, Mufti wa Omani amethibitisha kwamba Ikhtilaf hii ya muandamo wa mwezi katika hukmu ya kufunga au kufungua ipo na kwamba ni jambo la kale. Kama alivyosema maneno yake yaliyotafsiriwa na Shaykh Muniir Sulayman 'Aziz kwamba: "Hakuna madhehebu iliyokuwa imesalimika na kuwa na Khitilafu baina ya Wanavyuoni wake juu ya suala la kutafautiana miandamo ya mwezi." Jee ndugu Juma anataka kusema kwamba Shaykh Naaswir Bachuu ndiye mwalimu aliyeanzisha madhehebu zote? Au ndiye aliyeanzisha mtafaruku huu kama alivyouita mwenyewe ndugu Juma?

JAWABU

Suala hilo jiulizeni wenyewe; mujijibu wenyewe; kwani nyinyi ndio mulioliunda: mimi sikusema hivyo kamwe bali nilichokisema ni hiki: "Kwa kwetu - Afrika Mashariki - kusema kwamba mwezi muandamo wa nchi moja ni muandamo kwa nchi nyengine zote za dunia ni kitu kipya". Nami sikusudii kusema kwamba upya huo ni katika kuzungunzwa au kusomwa suala hilo katika vitabu; nakusudia kimatendo sula hili lilikuwa halipo Afrika Mashariki. Sasa ili muwe mumenijibu, twambieni nani alikuwa akifata muandamo mmoja hapa Afrika Mashariki. Jamani! Tafuteni hoja mujadili: musijadili kitu kisichokuwa na umuhimu. Kama hamuna hoja nyamzeni musijitie aibu!

MNASEMA

Katika kudhihirisha udhaifu wake wa kumuandama mtu fulani; Ndugu Juma anasema: (Kama tunavyojua kwamba Sheikh Nassor Bachoo, ni mmoja wa wenye kusisitiza ulazima wa kuwa na muandamo mmoja.) Sisi kwa upande wetu tunasema: Katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu hakuna pahala alipolazimisha watu wafuate huo aliouita ndugu Juma (msimamo wa Shaykh Naaswir). Bali yeye ameonesha mitizamo ya Wanavyuoni kwa kutumia Aya za Qur-aan, Hadiythi na vitabu vinavyokubalika. Lugha aliyotumia Shaykh Naaswir katika huo unaonekana ni msimamo wake ni maneno yaliyozimuliwa kilugha (polite language) kama vile: (inawezekana) ((inaonyesha) .

JAWABU

Na mimi hapa sijasema kuwa Sheikh Nassir Bachoo kalazimisha watu wafunge kwa muandamo mmoja. Nimesema "Anasisitiza ulazima" yaani yeye analingania msimamo huo kwani kwake ndio msimamo sahihi na ndio wajibu kuufata. Naomba tena tuelewane musiseme kitu kinyume na nilivyosema. Wala musitafute kitu kisicho na maana mukajadili eti ndio jawabu! Pili maneno yenu: "Katika kudhihirisha udhaifu wake wa kumuandama mtu fulani". Sasa je na nyinyi pia munaonesha udhaifu huo huo kwa kumuandama mtu fulani katika kitabu chenu?

MNASEMA

Aliyelazimisha rai ni ndugu Juma mwenyewe kama anavyosema: (Lakini kilicho lazima na ambacho tunatakiwa tukubaliane ni kuwa muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali) [uk. 112]

JAWABU

Bali hata Sheikh Bachoo pia kalazimisha kwani ukidai kuwa huu ndio msimamo wa haki au ndio msimamo sahihi au ndio wajibu kufatwa, bila kusema kuwa rai zote zinafaa basi na wewe huwa umelazimisha rai yako. Sasa je Sheikh Bachoo anakubali hivyo kuwa rai zote ni sawa? Mimi kweli sisemi kuwa rai zote ni sawa: nasema kuwa nyinyi mumekosea na sahihi ni kinyume na munavyofanya, na kwa hivyo bado nipo katika msimamo wangu huo huo kwamba: "Kilicho lazima na ambacho tunatakiwa tukubaliane ni kuwa muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali".

MUNASEMA

"Kisha katika uk 85 ndugu Juma anataja kwamba msimamo huu wa muandamo mmoja kwa dunia nzima ni ((kitu kipya)) na kwamba jambo hilo halitekelezeki na ni kauli iliyobaki vitabuni tu baada ya kutaja baadhi ya nchi zinazofuata miandamo yao - yaani kila nchi na muandamo wake kama Al-yaman , Oman , Misri na Saudia. Kisha hapo hapo akataja: ((isipokuwa Imarati katika miaka ya mwisho wamekuwa wakifata Saudia.)) Inafaa ndugu Juma aulizwe masuala yafuatayo:

i) Kama ni jambo lisilotekelezeka vipi tena Imarat wanalitekeleza?

ii) Je hawa wa Imarat nao ni wanafunzi wa Shaykh Naaswir Bachuu?

iii) Kwani hiyo sio kauli ya Jamhuur ambayo ndio msimamo wa maimamu wakubwa wakiwemo Ahmad bin Hanbal, Malik na Abu Hanifa? (Angalia pia sehemu ya 11 na 13 za kitabu hiki)

JAWABU

Kwanza mumemefanya ghushi: maneno yangu hamukuyanukuu yote. Mimi nimesema: "Kwa kwetu - Afrika Mashariki - kusema kwamba mwezi muandamo wa nchi moja ni muandamo kwa nchi nyengine zote za dunia ni kitu kipya". Nyinyi maneno "Kwa kwetu Afrika Mashariki" mumeyatoa ili ionekane kuwa mimi nasema kuwa hili ni suala jipya kila pahala. Watu kama nyinyi vipi tutakuamini katika dini yenu na uadilifu wenu, ikiwa munaghushi maandiko hivi? Hii ndio kamati ya Msikiti Sunna na hii ndio suna yenyewe?! Halafu mukaendelea na tadlis (ghushi) yenu mukasema: "Na kwamba jambo hilo halitekelezeki na ni kauli iliyobaki vitabuni tu". Mimi sikusema hapa kuwa "Halitekelezeki", bali nimesema:

Lakini ukweli ni kuwa hata katika nchi nyengine zote za dunia taqriban kauli kwamba tufunge kwa muandamo mmoja, ni kauli ilioishia katika vitabu tu, kimatendo (practically) kauli hio haitumiwi isipokuwa na mtu mmoja mmoja. Hadi leo hii: watu Al-yaman wanafata muandamo wao, Oman wanafata muandamo wao, Saudia wanafata muandamo wao, Misr wanafata muandamo wao na nchi zote taqriban ni hivyo, isipokuwa Imarati katika miaka ya mwisho wamekuwa wakifata Saudia.

Haya nionesheni hapa maneno "Halitekelezeki". Mimi nimesema kuwa kimatendo kauli hii, hadi leo haitendewi kazi isipokuwa na baadhi ya watu. Nyinyi mumebadilisha na kuweka ghushi yenu mukasema nimesema halitekelezeki. Kwa hivyo, hilo Sula (a na b) jibuni wenyewe kwani mumesema kinyume na nilivyosema. Suala (d), najibu kuwa sio: hio si kauli ya jumhur bali jumhur kauli yao ni kinyume na hivyo na hili nimelithibitisha katika uk. 189-193 wa chapa ya pili ya kitabu changu au uk. 171 wa kitabu hicho chapa ya kwanza. Na Al-Imamu Malik riwaya zake zimegongana na riwaya kwamba kila watu na muandamo wao ndio ilio bora kwani ni riwaya ya Madina aliko kuweko Al-Imamu Malik, wakati riwaya nyengine ni ya watu wa Irak kulikokuwa na viwanda vya kutunga riwaya!

MNASEMA

Na sisi tunamuongezea habari moja ambayo ni vyema kuielewa, kwamba nchi ya Uganda iliyo katika Afrika ya Mashariki pia inafuata rasmi muandamo mmoja wa duniani. Pia aelewe kwamba huo msimamo wa kila nchi na mwezi wake huku Afrika ya Mashariki haukuwepo tokea zamani. Mashaykh wote wa huku wanakubaliana mwezi ukionekana popote katika nchi hizi tatu ( Kenya , Uganda na Tanzania ) wanafunga pamoja. Yeye anaendelea kushika msimamo wake: (Al-yaman wanafata muandamo wao, Oman wanafata muandamo wao, Saudia wanafata muandamo wao). Lile analoliona yeye halitekelezeki, basi ndio linatekelezeka.

JAWABU

1) Kitu rasmi Uganda hakizingatiwi kwani Uganda kimsingi sin chi ya Kiislamu wala ya Waislamu: Waislamu ni wachache ukilinganisha na Wasio Waislamu. Kwa hivyo, hakuna kitu rasmi. Na jambo hilo ni jambo la sasa. Na mimi sijapinga kwamba sasa fikra hio ipo Afrika Mashariki.

2) Ama kauli yenu: "Mashaykh wote wa huku wanakubaliana mwezi ukionekana popote katika nchi hizi tatu ( Kenya , Uganda na Tanzania ) wanafunga pamoja". Ndio maana nikatumia lafdhi "Kwa kwetu Afrika Mashariki" nikijua kuwa wanavyuoni wote wa kwetu Afrika Mashariki wana msimamo huo. Ama kauli yenu: "Yeye anaendelea kushika msimamo wake: ((Al-yaman wanafata muandamo wao, Oman wanafata muandamo wao, Saudia wanafata muandamo wao,)). Lile analoliona yeye halitekelezeki, basi ndio linatekelezeka". Mwisho wa kunukuu. Inaonesha kuwa kitabu changu mumekijibu bila ya kukifahamu. Nilichosema ni kuwa, ijtihadi ifanywe katika kubainisha wapi hadi wapi watu wafunge pamoja. Kwa vile, hakuna andiko lililobainisha hivyo. Ama muandamo mmoja kwa dunia nzima hili ni kinyume na andiko. Kwa hivyo, wakiwa wanavyuoni wa zamani wamefanya ijtihad hio, sisi tunafata ijtihad yao kwa vile hapa ni mahala pa ijtihad na haikugongana na andiko. Ama madai yenu nyinyi ni kinyume na andiko lilivyoonesha.

MNASEMA

"Kuna suala moja la nyongeza tunapenda tumuulize ndugu yetu Juma: Hata kama hizo nchi alizozitaja ( Al-Yaman , Oman , Misri na Saudia) hazijakubaliana kufuata muandamo mmoja, je hakuna uwezekano (japo wa sadfa) unaoweza kutokea kufunga siku moja ijapokuwa kila mmoja ameona mwezi katika nchi yake? Sasa tuseme kila nchi katika hizo imeona mwezi usiku wa Alkhamisi kuamkia Ijumaa - Wote si watafunga siku moja ya Ijumaa? Basi huo ndio utekelezaji aliosema hautekelezeki. Ni wazi kuwa unatekelezeka.

JAWABU

Munaendelea kuuliza masula haya kwa sababu masuala yenu mumeyajenga katika kitu nisichokisema kamwe. Wapi nimesema kuwa "Hilo halitekezeki" hata mukauliza masuala haya?

8

9

10

11