HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 20%

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2 Mwandishi:
Kundi: VITABU VYA HADITHI

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

Mwandishi: AMIRALY M.H.DATOO
Kundi:

Matembeleo: 19983
Pakua: 3231

Maelezo zaidi:

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 11 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 19983 / Pakua: 3231
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

Mwandishi:
Swahili

4

HADITH ZA MTUME (s.a.w.w) NA MA-IMAMU(a.s)

SEHEMU YA PILI

UMMA WA WAISLAM KATIKA ZAMA ZA MWISHO

992. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Kutakuja zama kutakuja wakati katika zama miongoni mwa watu kuwa: Wao hawatawaheshimu Wanazuoni wao (yaani Maulamaa) ila kwa mavazi yao mazuri; wao hawatasikiliza Qur'an Tukufu ila kwa sauti ya kuvutia; Na wao hawatamwabudu Allah swt isipokuwa katika mwezi wa Ramadhani tu; wanawake wao hawatakuwa na aibu, maskini miongoni mwao hawatakuwa na subira, na matajiri wao hawatakuwa wakarimu, kwani wao hawataridhirika kwa kidogo na wala hawatakinai kwa wingi. Wao hawatashiba kwa kingi, wao watafanya kila jitihada kwa ajili ya matumbo yao; dini yao itakuwa ni mapesa (mali na utajiri); na wake zao ndio watakuwa Qiblah zao (tunapoelekea kusali huko Al-Ka'abah tukufu); na majumba yao ndio itakuwa Misikiti yao; wao watakimbia kutoka Maulamaa wao kama vile kondoo anavyo kimbia kutoka kwa mbwa mwitu. Hapo watapokuwa kama hivyo (basi Allah swt atawatumbukiza katika mambo matatu). Atawaondolea baraka katika mali zao. Watatawaliwa na mtawala dhalimu. Watakufa (kutoka humu duniani) wakiwa hawana imani iliyo halisi."[175]

993. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Utafika wakati katika umma wangu kwamba: watawala wao watakuwa wakatili na wadhalimu, Maulamaa na Wanazuoni wao watakuwa waroho wa mali na utajiri na watakuwa na imani kidogo, waumini wao watakuwa ni wanafiki, wafanya biashara wao watakuwa wakijishughulisha kwa kutoa na kupokea riba na kuficha maovu na kasoro ya vitu wanavyonunua na kuuza na wanawake wao watakuwa wamejihusisha mno na mambo ya kujirembesha ya dunia .Hivyo, wakati huo, mwovu kuliko wote miongoni mwao ndio watakaokuwa wakiwaongoza wao, na wema miongoni mwao watakuwa wakiwaita watu lakini hakuna mtu atakaye wajibu ." [176]

994. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Utafika wakati katika Umma wangu ambapo wao watakuwa wakipenda vitu vitano na kuvisahau vitu vitano: Wao watakuwa wakiipenda dunia na kuipuuzia Akhera. Wao watapenda mali na kusahau hesabu ya siku ya Qiyamah Waume zao watawapenda wanawake waovu na kuwasahau Hur al-'Ayn Wao watapenda majumba na watayasahau makaburi yao. Wao watajipenda wenyewe kupita kiasi na kumsahau muumba wao. Kwa hakika watu kama hawa hawanipendi mimi na mimi pia siwapendi wao ." [177]

UMRI WETU TUUTUMIE VYEMA.

995. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alimwambia Abu Dhar: "Ewe Aba Dhar! Faidi vitu vitano kabla ya vitu vitano: Ujana kabla ya uzee, Siha yako kabla ya magonjwa, Utajiri wako kabla ya umaskini, Ufaragha wako kabla hujawa mashughuli, na maisha yako kabla ya kifo chako ." [178]

996. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , amesema: "Itakapofika siku ya Qiyamah, kikundi cha watu kitasimama na kuja kubisha hodi katika mlango wa Jannat. Nao wataulizwa ni nani wao, nao watajibu: Sisi ni watu wa subira na kwa hayo wataulizwa ni kitu gani walichokifanyia subira, nao watajibu sisi tumefanya subira kwa ajili ya Allah swt dhidi ya kumwasi Allah swt. Kwa hivyo Allah swt atasema kuwa hao ni wasema ukweli na atawaruhusu waingie Jannat. Kwani Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu: Sura Az-Zumar, 39, Ayah 10: 'Sema: Enyi waja wangu mlio amini ! Mcheni Mola wenu Mlezi. Wale wafanyao wema katika dunia hii watapata wema. Na ardhi ya Allah swt ni kunjufu. Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu."[179]

997. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , amesema: "Aliye na furaha ni yule ambaye hana matamanio na matarajio makubwa katika maisha yake na anafaidi kila fursa anayoipata ."[180]

DINI NA KUSOMEA MAMBO YAKE

998. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Ole wake yule Mwislam ambaye habakizi siku moja katika juma zima kwa ajili ya kujifunza masuala ya dini yake na wala kujaribu kufanya uchunguzi na utafiti wa dini yake ." [181]

999. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Yeyote yule anayesomea dini ya Allah swt, basi kwa hakika ana uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo yake na kumpatia yeye riziki kutokea mahala ambapo yeye alikuwa hata hajaweza kuwazia ." [182]

1000. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "(Vijana wa Kish'ia lazima wawe na program au utaratibu wa kujifunza masuala ya dini). Mimi ninapomwona kijana wa Kishi'a ambaye hana program au utaratibu kama huu basi mimi nitamfundisha somo ."[183]

1001. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) , amesema: "Wajulishe wafuasi wetu kuwa kwa hakika bila shaka wao watakuwa miongoni mwa wale watakao okoka siku ya Qiyamah kwa masharti iwapo wao watakuwa watimizaji wa yale wanayo amrishwa."[184]

1002. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Yeyote yule kutokea Ummah wangu atakaye hifdhi ( kariri ) hadithi arobaini ambazo zinahitajiwa na watu katika maisha yao ya kidini (kwa ajili ya Tabligh na muongozo), basi Allah swt atamwinua akiwa hakimu kutoka waliokufa Siku ya Qiyamah ." [185]

UPOLE NA MATOKEO YAKE MAZURI

1003. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Kwa hakika mja anaweza kujipatia daraja la yule anayefunga saumu katika nyakati za mchana na anayesali usiku kucha, kwa tabia zake nzuri za upole ." [186]

1004. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . alimwambia mtoto wake Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Ewe Mwanangu! Hakuna utajiri uliona thamani kuliko akili na hakuna umasikini uliosawa na ujahili; hakuna ugaidi ulio mbaya kabisa kama kiburi,na hakuna maisha yenye raha kuliko kuwa mpole ."[187]

1005. Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Kwa hakika, bora ya bora zote ni tabia njema ."[188]

1006. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Tabia njema ipo katika njia tatu: Kujiepusha na vitu vilivyo haramishwa, kutafuta yale yaliyo halalishwa, na kutendea haki wana nyumba wake ."[189]

1007. Al Imam Zaynul 'Abediin(a.s) , amesema: "Kauli njema huongezea mali, utajiri, na riziki, na huahirisha ajali, na hutengeneza mapenzi miongoni mwa wenye nyumba, na humfanya mtu akaingia Jannat ."[190]

1008. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Yapo mambo matatu ambayo yeyote yule atakayezifikisha kwa Allah swt, basi Allah swt atamfaradhishia Jannat kwa ajili yake: Kutoa mchango katika umaskini, desturi nzuri pamoja na watu wote, na kujitendea haki nafsi yake."[191]

1009. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Kwa mambo ambayo umma wangu utajipatia Jannat ni hasa kwa mema yote, na desturi nzuri ." [192]

ATHARI MBAYA ZA HASIRA NA TABIA MBAYA

1010. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Hasira inaiharibu imani kama vile siki(huwa chachu) inavyoharibu asali ." [193]

1011. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Ghadhabu ni ufunguo wa kila aina ya shari ."[194]

1012. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . amenakili kutoka kwa mzazi wake(a.s) . ambaye amenakili kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . ambaye Amesema kuwa: "Mtu mmoja alimwijia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . ili afundishwe tendo ambalo litaondoa kizuizi baina yake na Jannat. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alimwambia: Usiwe mkali; usiwaombe watu vitu, watakie watu kile ujitakiacho wewe mwenyewe." [195]

1013. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Yeyote yule anayezuia ghadhabu zake, basi Allah swt atazificha siri zake ."[196]

1014. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Ghadhabu ni kitu kinacho teketeza moyo wa hakimu; kwani yeyote yule asiyeweza kudhibiti vyema ghadhabu yake basi kamwe hawezi kuitumia busara yake ."[197]

KUOMBA TAWBA YA ALLAH SWT

1015. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , amesema: "Mjipake manukato ya Istighfar ili hata tone na mabaki ya madhambi yenu yasiwadhalilishe nyie ."[198]

1016. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . alimfundisha mtu mmoja kwa kumwomba Allah swt dua kwa kumwambia: "Sifa zote ni za Allah swt kwa kila neema; na mimi ninamwomba kila la kheri na kila la wema; na naomba Allah swt aniepushe na kila aina ya shari; na ninamwomba Allah swt msamaha kwa madhambi yote ."

1017. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . amesema kuwa: "Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w). aliulizwa kuwa bora wa waja ni nani, naye alijibu: Wao ni: "Wanapofanya mema wanafurahia hayo; wanapofanya mabaya basi wanaomba Tawba na Istighfar; wanapojaaliwa chochote wanashukuru; wanapokuwa katika hali ngumu, wanaonyesha subira; wao wanapo mghadhabikia mtu, humsamehe ."[199]

1018. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) , amesema: "Anapozidisha muumin Mwislam kwa kuomba Istighfar ya Allah swt, basi rikodi ya matendo yake mema yataongezeka na yatakuwa yaking'ara ."[200]

SALAA YA JAMA'A

1019. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Allah swt huheshimu sana yule mja anayesali sala kwa Jama'a na baada yake anapoomba kitu chochote basi Allah swt lazima humtimizia ." [201]

1020. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) , amesema: "Fadhila za sala ya Jama'a kwa sala ya mtu anayesali peke yake ni kila raka'a moja katika Jama'a ni bora kuliko raka'a elfu moja (1000) zinazosaliwa na mtu peke yake ."[202]

1021. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Sala moja ya mtu katika Jama'a ni bora kuliko sala za miaka arobaini anazosali akiwa nyumbani kwake (peke yake) ." [203]

1022. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Safu ya mistari katika sala ya Jama'a inayosaliwa juu ya ardhi ni sawa na safu za Malaika huko mbinguni; na Raka'a moja inayosaliwa katika Jama'a ni sawa na Raka'a ishirini na nne na kila raka'a moja inayosaliwa na wapenzi wa Allah swt kuliko sala za miaka arobaini. Hivyo, siku ya Qiyamah ambayo ni siku ya uadilifu wakati Allah swt atakapo wakutanisha wanaadamu wote kuanzia mwanzoni hadi mwisho, basi hakutabakia na muumin yeyote ambaye amesali sala ya Jama'a, kwamba Allah swt atampunguzia shida zake za siku ya Qiyamah na ataambiwa aingie Jannat."[204]

1023. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . siku moja aliijiwa na Kipofu mmoja ambaye alisema: "Kulikuwa hakuna mtu yeyote wa kumchukua Msikitini ili aweze kushiriki katika sala ya Jama'a pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . pale aliposikia Adhana ikitolewa. Hapo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alimwambia: "Funga kamba kutoka nyumbani kwako hadi Msikitini na ushiriki katika sala ya Jama'a ." [205]

1024. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . amesema: "Mtu yeyote ambaye anaiacha sala ya Jama'a bila ya kuwa na Udhuri inayokubalika bali bila sababu yoyote, kwa misingi ya kutotaka kushiriki katika mkusanyiko wa Waislam, basi atakuwa hana Sala yoyote ."[206]

1025. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) , amesema: "Kwa hakika sala ya Jama'a imefaradhishwa ili kuwepo imani halisi katika umoja, katika Islam, na katika kumwabudu Allah swt kiwazi wazina ambayo imedhihirishwa kuwa bayana, kwa sababu, ili iweze kuwadhihirikia watu wa mashariki na wa magharibi (wa dunia hii). Hivyo ukweli na asili wa Uislam utadhihirika na kujulikana na makafiri na mapagani kabla ya Uislam utakuwa ni kama kiza mbele ya nuru, kiza ambacho hatimaye kinapotea. Vile vile sala ya Jama'a husababisha watu kutambuana na kuelewana na inawezekana wengine wakawa mashahidi kuhusu wengineo kuhusu Uislam wao, ambamo kuna uwezekano na vile vile kushirikiana katika mambo mema na ya kumfurahisha Allah swt mambo ambayo yanawazuia wasimuasi Allah swt kupita kiasi ."[207]

NEEMA NNE ZA ALLAH SWT

1026. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema kuwa kila asubuhi, kila Mwislamu anatakiwa azikumbuke neema nne za Allah swt. Hofu yangu ni kwamba asipozikumbuka, kuna hatari ya kuzipoteza neema hizo: "Namshukuru Allah swt ambaye amenisaidia kumtambua Yeye na hakuuacha moyo wangu gizani. Namshukuru Allah swt ambaye ameniweka pamoja na wafuasi wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Namshukuru Allah swt ambaye ameiweka riziki yangu kwake Yeye na si mikononi mwa watu. Namshukuru Allah swt ambaye amezifunika dhambi zangu na aibu zangu na hakunidhalilisha mbele ya watu.

1027. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , Nur al-Absaar Shablanji. "Mwovu wa watu ni yule anayewawekea pingamizi na anakuwa mkali kwa watu wake wa nyumbani ."

1028. Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu: "Enyi mlioamini! Ingieni katika hukumu za Uislamu zote, wala msifuate vyayo za Shaytani; kwa hakika yeye kwenu ni adui dhahiri ."

SIFA ZA KUPENDEZA ZA MWANAMKE

1029. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Malipo ya mwanamke mcha Allah swt kwa kumpa mume wake bilauri moja ya maji ni zaidi ya kufanya ibada mwaka mzima ambamo mchana anafunga saumu na usiku zake anakesha katika kufanya ibada ." [208]

1030. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Ni kwa mwanamke kujiweka msafi kabisa kwa kujipaka manukato bora kabisa na kuvaa mapambo ambayo yatamfanya yeye amvutie bwana wake na ajiweke tayari kwa ajili ya bwana wake usiku na mchana ." [209]

1031. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , amesema: "Jihadi ya mwanamke (vita katika njia ya Allah swt ) ni kuwa na uhusiano mwema na kuwa mshiriki wa bwana wake ."[210]

1032. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ., amesema: "Iwapo ningetaka kukusanya mema yote ya dunia hii na Aakhera kwa ajili ya Mumin basi mimi ningeziweka kwa ajili ya moyo mnyenyekevu, ulimi wenye shukurani na isemayo mema, mwili ufanyao subira wakati wa shida na dhiki. (Kwa ajili ya mwanamme Mimi ningempa) Mke mcha-Allah swt ili anapouona uso wake anajawa na furaha na yeye (mwanamke) anaihifadhi na kulinda mali yake, pale bwana wake anapokuwa hayupo."[211]

1033. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) , amesema: "Amelaaniwa! Amelaaniwa kabisa mwanamke yule ambaye anautonesha moyo wa mume wake na kumfanya akasirike. Lakini amebahatika kabisa mwanamke yule ambaye anamheshimu bwana wake wala hamghadhabishi na huwa mtiifu kwa bwana wake ."[212]

1034. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Bora ya mwanamke ni yule anayezaa, mvutiaji kimapenzi, mtunza siri zenu, na mcha-Allah swt. Na humtii bwana wake na hupendwa na Jama'a na ndugu zake. Pale anapokuwa pamoja na bwana wake, anamwonyesha urembo na mavazi yake ambayo kwa hakika huyaficha kwa ajili ya wanaume wengine isipokuwa mume wake tu. Kwa hakika huwa msikivu na mnyenyekevu kwa mazungumzo yake na huzitii amri zake. Pale anapokuwa faragha anavaa vizuri kabisa na kutimiza mahitaji ya bwana wake kutoka kwake. Daima huwa anakuwa amevaa vizuri na kujirembesha kwa ajili ya bwana wake tu na kamwe huwa si mtu aliyejisahau kwa ajili ya bwana wake (hujiweka tayari kwa ajili ya bwana wake.)."[213]

1035. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Kutokea kwa furaha ya mwanamme Mwislamu ni kwamba ana mke mcha-Allah swt na nyumba kubwa ya kukidhi wananyumba, usafiri mzuri na watoto wema ." [214]

1036. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Vita vya Jihad kwa ajili ya mwanamke ni kuwa na uhusiano na kuwa mwema kwa mume wake na haki za mwanamme kwa mke wake ni zaidi ya haki za wote juu yake ."

1037. Allah swt amesema:

وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ سَرِّحُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَلَا تُمْسِكُوهُنَّ ضِرَارًا لِّتَعْتَدُوا وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ وَلَا تَتَّخِذُوا آيَاتِ اللَّـهِ هُزُوًا وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَمَا أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّنَ الْكِتَابِ وَالْحِكْمَةِ يَعِظُكُم بِهِ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٣١﴾

Na mtakapo wapa wanawake talaka, nao wakafikia kumaliza eda yao, basi warejeeni kwa wema au waachilieni kwa wema. Wala msiwarejee kwa kuwadhuru mkafanya uadui. Na atakayefanya hivyo, amejidhulumu nafsi yake. Wala msizichukulie Aya za Allah swt kwa maskhara. Na kumbukeni neema ya Allah swt juu yenu, na aliyo kuteremshieni katika Kitabu na hikima anachokuonyeni kwacho. Na mcheni Allah swt , na jueni kwamba hakika Allah swt ni Mjuzi wa kila kitu. (Qur'an, 2: 231).

1038. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , amesema: "Muoe na wala msitoe talaqa kwa sababu 'Arshi Ilahi hutetemeka kwa talaka ." [215]

1039. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) , amesema: "Allah swt hufurahishwa mno kwa nyumba ile ambamo harusi huwapo na hughadhabishwa kwa nyumba ile ambamo huwa na talaka. Na hakuna kinachomkerehesha Allah swt kama talaka ."[216]

SEMI ZA IMAM ALI IBN ABI TALIB (a.s)

UADILIFU

1040. Taji la mfalme ni uadilifu wake mwenyewe.

1041. Utatawala iwapo nawe utakuwa mwadilifu.

1042. Uadilifu huangamiza ulafi , uroho na tamaa.

1043. Ngome ya Utukufu (ya Allah swt) huikinga nchi yenye mtawala mwadilifu.

SHURUTISHO NA SHARI

1044. Kulazimisha/Kushurutisha kunaifanya akili iwe kipofu.

1045. Shari kunamfanya mtu awe mwoga wa uadilifu (ataiongopea)

1046. Uchokozi ni hatua ya kukaribia maangamizi.

1047. Kinachodhulumu haki ni kule kusaidia vilivyo batilifu.

1048. Udhalimu kwa mwenye dhiki ni dhuluma kubwa kuliko zote zile.

1049. Allah swt huharakisha kuanguka kwa wachokozi.

1050. Ushidi wa mshari ni kushindwa kwa nafsi yake.

1051. Kustarehe humu duniani kwa fidia ya akhera ni kujidhulumu nafsi yako.

1052. Kuwakandamiza yatima na wajane kunaleta magonjwa na kupotea kwa ne'ema.

ULIMI NA USEMI

1053. Mtu amehifadhika chini ya ulimi wake.

1054. Ulimi mtamu/mzuri hupata marafiki wengi.

1055. Ulimi wako utasema kile kilichozoeshwa. (Kwa hivyo jihadhari kabla ya kusema).

1056. Akili ni busara. Akili ya mpumbavu ipo chini ya ulimi wake(anasema kabla ya kufikiri).

1057. Ulimi ni mkalimani wa akili.

1058. Ulimi wa mtu ni uzani wake mwenyewe.

1059. Ulimi unaathari za kuchoma zaidi ya mkuki.

1060. Usemi wa kweli ni ulimi mtukufu.

1061. Jihadhari na ulimi, kwani ni sawa na mshale unaoweza kufyatuka kutoka upinde.

1062. Mtu bila kusema (ulimi useme mema na kukataza mabaya) ni ama sanamu au mnyama.

1063. Ulimi wa mwenye busara ipo akilini mwake (huongea na akili yake na hufikiria zaidi na kusema kwa uchache kwani ni yenye manufaa).

1064. Kuujaribu (kucheki) ulimi ni afadhali kuliko kulitazama tumbo.

1065. Yeyote yule asiye uhifadhi ulimi wake basi ataujutia mbeleni.

UKIMYA NA KUSEMA

1066. Kila vile busara ya mtu iongezekavyo ndivyo vivyo hivyo maneno yake hupunguavyo.

1067. Ukimya ni majibu ya maswali mengi sana.

1068. Ukimya ni jibu bora kabisa kwa mpumbavu.

1069. Mazungumzo bora ni yale yaliyo mafupi na yenye manufaa.

1070. Bora ya misemo ni ile iliyochujwa na kuhakikishwa.

1071. Ukae kimya ili ukae salama.

1072. Kusema kupita kiasi kunamdharaulisha mtu.

1073. Urefu wa mazungumzo huidhoofisha hotuba.

1074. Hotuba ni kama dawa; kiasi kidogo kinaponya na kwa kuzidi kiasi kunaweza kumwua mgonjwa.

1075. Usimpuuzie yule asemaye bali wewe uyatilie maanani yale ayasemayo.

1076. Kusema kidogo ndivyo kukosolwa kidogo.

KIFO (MAUTI)

1077. Watu wako wamelala hali wako hai na huwa macho baada tu ya kufa.

1078. kujielekeza kwa mabaki ya matamanio ya mtu ndiko kujiuwa haraka.

1079. Ufe kabla ya kifo kukuijia.

1080. Mauti inaidhihaki tamaa.

1081. Mauti ni kutenganisha toka kitakachoisha na kuelekea kule pasipokwisha.

1082. Kuikumbuka mauti kila mara kutampunguzia mtu tamaa za duniani.

1083. Wale watembeao juu ya ardhi siku moja watazikwamo.

1084. Tamaa hukuongoza katika njia ya upotofu.

1085. Wakati hatuna matumaini huwa hatuhuzuniki.

1086. Kufadhaika huwa pamoja na tamaa.

1087. Kinachoipatia madhara na hasara dini ni tamaa.

1088. Waroho ni watumwa wa matilaba yao.

1089. Kutokuwa na mategemeo kunaituliza na kuipumzisha roho.

1090. Uroho huuangamiza uadilifu

1091. Ubinadamu ni wa aina mbili; wale wenye matamanio matupu na wale watakao kuja kuwa wasioridhika.

1092. Tamaa huingamiza hadhi ya mtu bila ya kuongezeka kwa bahati yake.

1093. Hata kama wakiwa uchi na wenye njaa, hao walioridhika huwa ni wenye furaha.

1094. Kuridhika ni hazina isiyo na kifani.

1095. Kuridhika ni hadhi na heshima isiyodidimia milele.

1096. Mwenye kuridhika tu ndiye aishiee kwa amani na usalama.

USTAHIMILIVU, UVUMILIVU NA UTULIVU

1097. Kutokuwa na saburi ya akili ni yenye madhara kuliko ustahimilivu.

1098. Chifu ya sababu ya Islam ni utulivu kwa Allah swt

1099. Ustahimilivu ni matunda ya Imani.

1100. Ujue kuwa utulivu ni hatua ya awali katika dini halisi na uaminifu ni mwili

1101. Kwa ustahimilivu, bahati mbaya huwa sivyo tena bahati mbaya.

1102. Ule uwezo wa uvumilivu wa ghadhabu (hasira) ni bora kuliko kuchukua kisasi.

MALI (UTAJIRI)

1103. Mapenzi ya mali inachochea tamaa na kuharibu wema.

1104. Usia unawafariji warithi

1105. Mali ni chanzo cha hamaki.

1106. Bora ya akiba ni pale ambapo kazi zinatawanywa vyema.

1107. Fedha haimnufaishi mwenye kuwa nayo hadi hapo anapotengana nayo.

AKILI NA UPUMBAVU

1108. Uadui ni kazi ya wapumbavu.

1109. Dhana ya mwenye akili ni mafumbo.

1110. Kwa kumtii Allah swt ni sawa kwa hisa ya akili na hekima ya mtu.

1111. Kupigana vita dhidi ya matakwa yake mtu ni jihad kubwa kabisa.

1112. Sababu ya busara na akili ni kukubalia ujinga wake mwenyewe.

1113. Mwerevu hulenga pale na thabiti.

1114. Mpumbavu hulenga pale penye mali.

1115. Dhana ya mtu inategemea akili yake ilivyo.

1116. Dhana ya mwenye busara na hekima ni sahihi kabisa kuliko kithibitisho cha mpumbavu.

1117. Kwa kujitenganisha na vitu vya muda na kujiweka tayari kwa maisha ya kudumu ndiko kunako busara na hekima hisa kubwa.

1118. Mtu huyo ni mwenye busara ambaye matendo yake yanathibitisha yaliyoyasema.

1119. Mtu mwenye busara hasemi ila pale penye dharura au penye sababu.

1120. Kila mtu aliye mwenye busara na hekima huwa yuko masikitikoni.

1121. Mwenye busara ni mwenye faida hata kama akiwa katika hali gani ile.

1122. Kujihusisha na wapumbavu ni kuitesa Roho.

1123. Mpumbavu yupo peke yake hata kama akiwa katika jamii.

1124. Kutoka kupata hekima (matakwa yake) hayawezi kufidiwa na fedha.

1125. Hakuna ugojwa ulio mbaya kabisa kuliko kutokwa kwa hekima.

UWEMA NA MATENDO MEMA

1126. Kwa uwema mtu anaweza kumteka mtu aliye huru.

1127. Wema haufi kamwe.

1128. Kazi iliyo bora zote ni kujijumuisha pamoja na walio wema.

1129. Kuwa mwema kwa mema ni uwema na hii ndiyo fahamu ya mtu ya hali ya juu.

1130. Thamani ya mtu inategemea uzani wa uadilifu wake.

1131. Angukia ndani kwa wema na uangukie nje kwa matakwa.

TAMAA

1132. Mapenzi ya mali (utajiri) yanachochea tamaa na kuupoteza uwema.

1133. Tamaa haielewi mipaka yake.

1134. Kuwa na imani ya Allah swt ni jitihada iliyo bora kabisa.

1135. Tamaa iliyo kuuu kabisa ya wanyama ni kule kushibisha tumbo lao wenyewe.

1136. Tamaa iliyo kuu ya wanyama porini kule kuwanyanyasa wengineo.

1137. Tamaa kuu ya mwanamke ni kuivutia dunia kwake na kuchochea fujo humo.

1138. Jitihada kuu kabisa ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s).humu duniani ni kuiongoza dunia.

1139. Tamaa yako iwe ni ile kwa ajili ya akhera na hapo utajirekebisha.

1140. Thamani ya mtu inategemea utukufu wa jitihada zake.

1141. Ukuu na ufahari wa mtu unategemea utukufu wa jitihada zake na wala sio pale penye kuozapo mifupa ya mababu zetu.

REHEHMA NA MSAMAHA

1142. Kusamehe ni taji la ukubwa na fahari.

1143. Rehema inaitukuza nguvu.

1144. Itakuwa ni vyema iwapo rehema itashirikishwa pamoja na ukubwa.

1145. Itakuwa ni adhabu kubwa itakayotolewa mbali na kuombwa msamaha.

1146. Unyenyekevu inatangaza ukubwa.

1147. Unyenyekevu ni matunda ya elimu na hekima.

1148. Unyenyekevu bila ya kutazama panapostahili ni sawa na huna uwezo.

1149. Majivuno huangamiza na kumharibia sifa mtu.

1150. Kwa kuwa na majivuno au kiburi ni sawa na kuipa akili sumu.

1151. Kiburi hukandamiza mwenendo wa maendeleo.

1152. Majivuno huua na kuudhalilisha ukubwa.

1153. Unyenyekevu ni sawa na wavu uliotandwa kwa ukubwa.

1154. Kujivuna na kule kujideka ni matokeo ya wale wenye akili kasoro.

ULIMWENGU

1155. Ulimwengu huu ni sawa na daraja ituvushayo kwenda akhera.

1156. Dunia hii ni sawa na duka la maovu.

1157. Mapenzi ya dunia ni chanzo (mizizi) cha matatizo na maovu yote.

1158. Ufahari wa wapumbavu na walio wajinga ni mapenzi ya dunia.

1159. Dunia ni chungu mno zaidi kuliko ule utamu wake ulio nao.

1160. Kuipatia dunia hii talaka ni sawa na kupanga harusi na Akhera.

1161. Dunia hii ni sumu na wale wailao sumu ni majahili.

1162. Uishi kwa kiwiliwili chako humu duniani na uifanyishe kazi nafsi(imani) yako kwa ajili ya akhera.

WATU

1163. Watu ni zaidi ya vile walivyokuwa awali na huishi zaidi ya walivyokuwa wakiishi mababu zao.

1164. Mtu aliye jasiri kuliko wengine ,atulizaye matamanio yake (subira).

1165. Itakuwa ni jambo la upuuzi iwapo nafsi itakuwa imedhoofika hali mwili wa mtu bado ana siha nzuri na iliyo njema.

1166. Yule aijuaye na kuelewa ubinadamu huchagua upweke.

1167. Yule ampandae Allah swt hupigana na aibu za watu.

1168. Yeyote yule asiyejifikiria na kujithamini mwenyewe basi amepotoka.

MATAKWA YA SUBIRA

1169. Hekima iliyo kuu kabisa ni kule kupingana na matakwa na matamanio ya mtu.

1170. Atakuwa ni mtu mwenye furaha kuu iwapo ataishinda nafsi yake mwenyewe.

1171. Adui wa kupindukia wa mtu ni yale matakwa yake.

1172. Vita vilivyo bora kuliko vyote ni vile vita dhidi ya nafsi ya mtu.

1173. Ulafi wa sehemu zetu za siri ndizo nyavu zilizo tegwa na Shaytani.

MADHAMBI

1174. Kuishi kwako hapa (mbali na utukufu) na dhambi lisiloweza kusamehewa.

1175. Usiogopeshwe na chochote kile isipokuwa madhambi yako mwenyewe.

1176. Madhambi yanaharibu ibada ya Allah swt.

1177. Uharibifu ni matunda ya madhambi.

1178. Madhambi yanampotezea mtu utukufu wake.

1179. Kujiepusha na madhambi ni afadhali kuliko kutenda mema

1180. Kutenda madhambi ni ugonjwa na dawa yake ni kujiepusha nayo na kufanya tawaba

MAFUNZO YA TAHADHARI

1181. Kila mtazamo wako wa fahamu ni fundisho kwako

1182. Walio kufa wamewachia mafunzo kwa ajili ya walio hai.

1183. Nijia walizozipitia wale waliokufa na waliotutangulia ni zenye kutufunza na kututahadharisha sisi tuzifuatazo.

1184. Uhakika wa mambo ni mkufunzi wa kutosha kabisa.

1185. Umri mkubwa ni mkufunzi aliye bora kabisa

SHAURI

1186. Kutoa onyo la upole katika umati wa watu ni jambo lililo bure.

1187. Mtoa mashauri asiye na uwema ni sawa na vile upinde unavyokuwa bila uzi.

1188. Mshauri aliye bora kuliko wengine ni yule akuelezeaye makosa na dosari zako.

UAMINIFU,UADILIFU

1189. Ulimi mtukufu ni ule ulio adilifu.

1190. Kwa kutimiza ahadi ni mfano ulio bora kabisa wa uaminifu na uadilfu.

1191. Ukweli ina maana ya kwamba ulinganifu wa matamko kwa mujibu ya maamrisho ya Allah swt atakavyo.

UDANGANYIFU NA KHIANA

1192. Urafiki haupo kamwe katika uongo.

1193. Kwa kubadilisha maana halisi ya jambo kuna haribu asili yake.

1194. Kusema uongo kunaharibu habari.

1195. Kusema uongo panapostahili,kutamlindia heshima za mtu.

1196. Kusema uongo na unafiki kunadhalilisha nidhamu na heshima ya mtu.

UKIASI NA UFUJAJI

1197. Aliyebarikiwa ni yule ambaye anaelewaye vyema thamani yake na asiyevuka mipaka.

1198. Kwa kupima kiasi ni nusu ya hifadhi.

1199. Ufujaji unapotea kabla ya njaa.

1200. Ufujaji unapoteza uwema na sadaka.

1201. Tamaa ya mali kunaharibu ukiasi alionao mtu.

1202. Kiasi kwa uangalifu kinabakia zaidi ya kile kilicho fujwa.

1203. Hakuna ufahari katika ufujaji.

1204. Kupima kiasi ni njia ya usalama na ya amani.

UWEMA (HISANI)

1205. Heshima na ukukuzi hauwezi kamwe kulinganiswa na ubaya,sio yenye wema.

1206. Mwenendo wa mtu ni diraja ya akili yake.

1207. Urithi ulio bora kabisa ni uungwana wa mtu.

1208. Hakuna chochote kile chenye thamani dhidi ya uungwana.

KUWAHESHIMU WAZAZI

1209. Kuwatazama wazazi ni fardhi iliyo kuu kabisa.

1210. Kuwatunza na kuwastahi wazazi wako (kuwalea) na malezi ya watoto wako, ndiyo yatakayo kulea wewe na kukustahi.

PUPA

1211. Hakuna ushindi uliopo katika pupa.

1212. Lawama huwa ni daima kwa yeyote aendeleae kwa pupa

HUSUDA 1213. Husuda humwibia mtu raha zake.

1214. Silaha ya husuda ni malalamiko na mapingamizi.

1215. Husuda huitafuna uwema kama vile moto iharibuavyo mbao.

KAZI 1216. Matendo ndiyo matokeo ya nia.

1217. Uwemwaminifu katika kazi zako, kwami majaribio ya Allah swt yako macho sana juu yako.

1218. Siku ya mwisho ni siku ya Qiyamah na wala si siku ya kufanya kazi.

1219. Shauku ya uaminifu ni uharibifu mambo mema.

1220. Upande ulio mgumu wa tendo, ni kuhifadhi utukufu wa jambo.

1221. Bila ya uaminifu , kazi zote hazitakuwa na thamani yeyote ile.

1222. Itakuwa ni wema iwapo mambo mema yawe rafiki yako na matilaba, adui yako.

1223. Elimu kiasi kidogo huharibu mienendo na tabia.

1224. Kazi nyingi zenye tamaa, zitaharibu zingine zote.

1225. Hakuna aheshimiwaye zaidi kuliko wengine ila ni yule mwenye kufanya ibada.

1226. Hakuna usalama ulio bora kuliko ibada

1227. Kumtii Allah swt ni sehemu ya busara ya mtu.

1228. Ibadi ni pahala palipobora pa kujihifadhia.

1229. Ibada ni mahala palipo bora pa kujihifadia.

1230. Kujionesha au kujidai kunaharibu na pia kuighasi ibada.

KUFANYA GHIBA

1231. Hakuna uwema au uamnifu katika kufanya ghiba.

1232. Yeyote yule asikilizaye ghiba basi ndiye mfanya ghiba mwenyewe.

1233. Yeyote yule awasemae wengineo kwako, ndivyo vivyo hivyo ujue wazi wazi kuwa ndivyo akusemaye wewe kwa wengineo.

KUCHEKA

1234. Kucheka kwa wastani (bila kutoa sauti) ni mcheko ulio bora kuliko vyote.

1235. Kucheka kwa kupita kiasi kutamharibia mtu heshima yake.

1236. Kucheka kwa kupita kiasi kunaiuwa bongo.

SIFA

1237. Majivuno yanadhihaki sifa na pia kuiharibu.

1238. Uwema na ukarimu kunavuna sifa njema.

1239. Yeyote yule akusifuaye ndiye akuuae.

MISEMO

1240. Utakatifu huambatana na busara.

1241. Kutoridhika kwa mtu kutamfutia utulivu.

1242. Saumu ya akili ni kuiepusha kutoka matamanio yote yaliyo maovu.

1243. Uoga ni kutokana na moyo uliodhoofika na usio na uimara.

1244. Vitu vinavyotuharibu sisi ni karibu tu tutakavyo ungana navyo.

1245. Kufuatilia mateso na matatizo yamkabiliayo mtu, yanadhihirisha ukubwa wake na ustahimilivu na uwema wake.

1246. Yeyote asemaye maneno na misemo ya wale wenye busara, basi ndivyo anavyojivisha utukufu wao.

1247. Maisha marefu hukutana na matatizo mengi.

1248. Ardhi ni msafishaji bora.

1249. Makabiliano ndiyo yanayomsaidia sana mtu.

1250. Ukweli na mabishano ndiyo yaliyo bora kabisa.

1251. Mtu ajigambaye basi ndiye ajidhalilishaye yeye nafsi yake.

1252. Mtu mwenye mafanikio bora kabisa.

1253. Yeyote yule mwenye kuhofu ndiye abakiaye salama.

1254. Tajiri hasemwi kwa kuongezeka kwa uwema na kuiendeleza subira.

1255. Uso wenye mcheko (mcheshi) huuepusha kutoka moto wa uadui.

1256. Kwa kukatalia zawadi ndiko kunamaanisha kutokuwa na shukrani.

1257. Hakuna chochote mbali na kule kufanya Tawbah ila ni kujipunguzia ule mwenendo unaofutilia.

1258. Usiligeuze tumbo lako likawa ni kaburi la wanyama.

1259. Ugonjwa ni moja wapo ya aina mbili za kifungo.

1260. Kuzuzuliwa kwa ghadhabu ni dhambi pia.

1261. Ndugu huongezea na kufurahikia furaha zetu na hutuondolea na kutuponya yale maumivu tuliyonayo.

1262. Ubongo (akili) huwa ni mfano wa ghala (stoo) ambayo ilifungwa kabisa na maswali tu ndio zifunguazo kutoka humo.

1263. Hata kama pazia itaondolewa mbele yangu ,basi hakuna chochote kile kitachoongezeka katika imani yangu.

1264. Pale Allah swt ampendeleapo Mja wake yeyote,Yeye humshugulisha katika mapenzi yake.

1265. Nywele za kijivu huelezea kuwa ni hatua ya kuikaribia mauti

BAADHI YA DUA' ZA IMAM ALI(A.S)

1265. Ewe Allah swt,mbariki yule ambaye hazina yake kuu ni imani na silaha zake ni machozi.

1266. Ewe Allah swt, wewe ni mkuu kabisa kwa kumwangamiza yule ambaye umeshakwisha kumtukuza hapo awali.

1267. Sala ni silaha ya mumini.

1268. Je kuna yeyote yule ambaye anaelewa vyema uwezo wa Allah swt na tena asimwogope Allah swt?

1269. Je kuna yeyote akuelewaye vile wewe ulivyo na tena asiwe na khofu yako?

1270. Ewe Allah swt, ngozi hii yangu hafifu, haitaweza kustahimili moto mkali wa Jahannam.

1271. Mishale yote hailengi penye kuheshimiwa na kwa kupatwa na shida na majaribio.

1272. Ewe muumba ,wewe upo pekee mwenye kuheshimiwa na mwenye kudumu daima milele na umelazimishia viumbe vyako kwa kifo na kwa kupatwa na shida na majaribio.

1273. Ewe muumba, nisamehee madhambi yangu pasipo mimi kujua kwangu

1274. Ewe mola , unisamehe madhambi yangu yale ambayo yanayoweza kuniteremshia juu yangu laana na adhabu na ghadhabu zako.

1275. Ewe mola wangu, nisamehee madhambi yangu yale yanayoweza kuwa sababu ya kuharibu na kuzighasi zile baraka zako zilizo juu yangu.

1276. Ewe mola, nisamehe madhambi yangu ambayo ndiyo yanayozuia na kuzipoteza ibada zangu kabla ya kukufikia wewe.

1277. Ewe mola wangu, nisamehee madhambi yangu yale ambayo inanikatiza mimi katika imani yangu.

1278. Ewe mola, mimi nakukaribia wewe kupitia kwa kukukumbuka wewe

1279. Ewe mola, mimi nakuomba wewe uniweke furaha na niwe nimeridhika na yale wewe uliyonijaalia maishani mwangu na katika bahati yangu (kwa ajili yangu).

1280. Ewe mola wewe ni mwepesi sana wa kubariki na kurehemu, msamehe yule ambaye hana chochote ila ni ibada na sala zako tu.

1281. Ewe Allah swt!, Je wewe utauachilia Moto uzikumbe nyuso ambazo ziko zimeangukia mbele yako kwa unyenyekevu?

1282. Ewe Allah swt, zipatie nguvu mikono na miguu katika kutekeleza wajibu na huduma katika kazi zako.

1283. Na uzipatie nguvu mbavu zangu ili nipate hali ya kukufikia wewe.

DUA

1284. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) : "Ewe Mola wetu sisi kwa hamu kubwa utujaalie haki, Serikali ya Kiislam, (ambayo kwa hakika ipo uadilifu serikali ya Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan(a.s) , tunamwomba Allah swt atuharakishie kudhihiri kwake). Kwa kupitia hii serikali takatifu, uihamasishe na kuipenda Islam na wafuasi wake ambao na papo hapo kuwadhalilisha unafiki na wanafiki. Na, katika kipindi hicho utuweke sisi miongoni mwa wale watu wanaowaita wengine katika utiifu wako na kuwaongoza katika njia yako utukufu; na, utujaalie heshima na ukuu katika dunia hii na Akhera.[217]

DUA. Aamin Ya Rabbal 'Alamiin.