HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 227%

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2 Mwandishi:
Kundi: VITABU VYA HADITHI

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2
  • Anza
  • Iliyopita
  • 11 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 22247 / Pakua: 4849
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

4

5

6

7

8

7

HADITH ZA MTUME (s.a.w.w).NA MA-IMAMU(a.s)

SEHEMU YA PILI

MAADILI YA ISLAM

Nafs aina na sifa zake Masomo ya akhlaq- maadili katika Islam ni mojawapo ya bora ya sayansi na inamwelekeza asomaye hadi katika elimu ya kujielewa nafsi yake mwenyewe ambayo Islam inaamini kuwa ni faradhi. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Yeyote yule aliyeitambua nafsi yake (mwenyewe) basi kwa hakika ametambua Allah ."

Hivyo hivyo kuna mapokezi mengi ya habari kuhusu umuhimu wa somo hili hata Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amebainisha kuwa: "Mimi nimetumwa kuja kukamilisha maadili. Tuanze kuzichambua aina za nafsi alizonazo mwanadamu vile alivyo: Hapana shaka kuwa mwanadamu hana nafs zaidi ya moja, lakini hii nafsi au inayo masharti fulani fulani. Kwa hiyo, hali ya kuonyesha kama 'nafsi ya kujilaumu' 'au nafsi ya kuamrisha' 'nafsi inayotosheka' (kama vile vielezwavyo katika Qu'rani), na hivyo haidhihirishi idadi ya nafsi. Upande mwingine, yote haya ni miongoni mwa ngazi za sifa ambazo zinaleta kwa ukamilifu na ustawi wa hali ya nafsi, pamoja na yale yanayoozesha nafsi na kuleta maovu.

NAFSI SAFI AU THABITI

1494. (Thabit.) Katika Qur'an Tukufu, Surah Ash Shua'raa, 26, Ayah 89, aina mbili hizo za masharti za nafsi zinaelezwa:- "Isipokuwa mwenye kuja kwa Allah swt na moyo safi" Uhalisi huu ni aina ya moyo, na moyo halisi (safi) ni ule ambao haufungamani na upande wa kuhangaika wala upande ule wa wapotofu. Imenakiliwa kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kuwa: "Moyo ulio msafi- halisi ni ule ambamo hakuna chochote kile isipokuwa Allah swt tu" Katika hali hii, Nafsi imetunukiwa hatua mojawapo ya umuhimu kuwa kamilifu. Hivyo inamaanisha kuwa hakutakuwa na mapenzi mbali na ile ya Allah swt tu.

Kuna habari nyigine iliyonakiliwa kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . ambamo twaambiwa: "Imani ya mtu haitokamilika hadi hapo mimi niwe mpenzi wake kuliko hata baba, mama, watoto wake, mali yake na hata kuliko maisha yake." Ndivyo hivyo, nafsi safi ni nafsi ambamo hakuna mapendo mengine yoyote yale isipokuwa Allah swt na wale wapendwao kwa ajili ya Allah swt (Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . na Ahali yake (a.s) .

NAFSI YENYE KUTUBU (AL-NAFS AL- MUNIIB)

1495. Sharti lingine la moyo au Nafsi ni kutubu na hivyo huitwa moyo wenye kutubu au nafsi yenye kutubu. Hivyo huwa daima inarudi kwa Allah swt, Qur'an Tukufu, Surah Qaaf, 50, Ayah 33:

"Anayemuogopa ( Allah swt Mwingi wa kurehemu), na hali ya kuwa humuoni na akaja kwa moyo ulioelekea ( kwa Allah swt) ."

Kuwa na khofu ya Allah swt pale mtu awapo peke yake ni mojawapo ya masharti bora ya nafsi, na hii ina maanisha kuwa nafsi imemtambua Allah swt kiasi kile kuwa hakutakuwa na tofauti yoyote itakapokuwa pekee yake au katika kundi la watu. Hata kama hakutakuwa na mtu yeyote karibu nayo, basi ile khofu ya Allah swt imo ndani yake thabiti. Hii haipo katika kundi la zile nafsi zilizo ghafilika katika maasi na matendo maovu wakiwa katika kundi la watu au wakati wengine watakapokuja julishwa, na hawatajizuia nayo na hata kama iwapo watakapopewa habari zilizo bainika. Hii ni ile aina ya nafsi ambayo haielewi kuwa Allah swt yupo anaangalia yote na Aliye dhahiri popote pale na kwa hakika aina hii ya nafsi haipo pamoja na Allah swt na wala haitorudi kamwe kwa Allah swt.

NAFSI ONGOFU (AL- NAFS AL- MUHTADI)

1496. Sharti lingine la nafsi ni ile iongozwayo. Qur'an Tukufu, Surah Attaghaabun, 64, Ayah 11, inatuambia:

"Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Allah swt. Na anayemuamini Allah swt huuongoza moyo wake. Na Allah swt ni Mjuzi wa kila kitu ."

Mtu ambaye moyo wake ukiwa umeongozwa na kujitosa katika habari ya imani na sheria Tukufu za Allah swt, yeye anaielewa njia yake vyema kabisa. Zile imani atakazokubalia na matendo yake yampasa kuyatenda huwa ni dhahiri kwake kuelewa vyote hivyo kwa uadilifu.

NAFSI ILIYO RIDHIKA (AL-NAFS AL- MUTMAI'NA)

1497. Sharti lingine lijulikanalo vyema la moyo au nafsi ni kuridhika. Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Ar-Raa'd, 13, Ayah 28 " Sikiliza: Kwa kumkumbuka Allah swt nyoyo hutulia." Na vile vile mwishoni mwa Qur'an Tukufu, Surah al-Fajr, 89, Ayah 28, twaambiwa: "Ewe nafsi yenye kutua"! "Rudi kwa Mola wako, hali ya utaridhika na umemridhisha." Nafsi iliyo ridhika ni ile iliyokwisha ridhika, ina maanisha kuwa mtu yupo anapigana vita vikali na matakwa yake na kwa kuyatimiza yale yaliyo fardhi kwake katika dini na kujiepusha na yale yaliyoharamishwa, na anajipa umuhimu kwa kuelimisha na kuikamilisha nafsi yake hadi hapo yeye hapindukii kutii chochote kile isipokuwa Allah swt tu. Ni marufuku kwake kuelekea pale penye madhambi na huwa ni mwenye kupenda amani na utulivu na huwa ni mwenye kujiridhikia mwenyewe hadi hapo yeye huwa thabiti kama jabali madhubuti. Hakuna madhambi, matakwa ya ubinafsi, tamaa, mvutano wa dunia, mapenzi ya mali au cheo yatakayoweza kuja kumpotosha yeye na kumwelekeze pengine na vile vile hakuna sheitani atakayeweza kumghalibu na kumpotosha yeye. Hali ya juu kabisa ya sharti hili kama ilivyokuwa katika Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . na ma - Imamu(a.s) . waliokuwa halisi kuwa hata mawazo ya kutaka kutenda madhambi hayakutokea kamwe.

NAFSI YA TAHADHARI YA UADILIFU (AL-NAFS AL MUTTAQI)

1498. Sifa nyigine ya nafsi inajulikana kama uangalifu wa uadilifu wa nafsi, nafsi ambayo imejaa kwa khofu na tahadhari. Hali hiyo inatokana na nyakati fulani kwa kupotoshwa na (kwa akili na ) huzungukwa na uchafu na ubovu ili nafsi iingie sharti sawa sawa na itahadharishwe na madhambi. Nafsi ikiwa katika hali hiyo huitwa nafsi ya tahadhari ya uadilifu. Qur'an Tukufu, Surah Al Hajj, 22, Ayah 32:

"Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Allah swt, anayezihishimu alama za (dini ya ) Allah swt, basi hili ni jambo la katika utawala wa nyoyo ."

Kwa mtu yule ambaye imani yake inafikia kiwango hiki cha Taqwa kiwango cha tahadhari ya uadilifu, huheshimu na kumthamini Allah swt na yale yote yaliyotolewa ishara nae kama Dini, Msikiti, shariah, waumini wake, Makkah, Al-Ka'abah Tukufu n.k. Kwa ufupi chochote kile kinachohusika na Allah swt huwa kina kuwa na umuhimu na ta'adhima kubwa kwa mtu kama huyu wa namna hii. Na hii ndiyo kwa hakika matokeo ya taqwa

NAFSI NYENYEKEVU (AL- NAFS AL- MUKHBIT)

1499. Hali nyingineyo ya Nafsi ni unyenyekevu na uvumilivu, yaani humaanisha kuwa mtu mwenye nafsi hali hii huwa mnyenyekevu mbele ya maamrisho ya Allah swt Kwa mara nyingine tena twaambiwa katika Qur'an Tukufu, Surah al Hajj, 22, Ayah 54:

"Na ili walio pewa ilimu wajue kuwa hayo ni Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi na waamini, na zipate kutua nyoyo zao. Na hakika Allah swt anaye waongoa wenye kuamini kwenye Njia iliyo nyooka ."

Kwa sababu nyoyo hizi hujiinamisha chini mbele ya Allah swt na maamrisho yake, na wale wenye kuwa na nyoyo hizo hujiwakilisha kwa Allah swt nao kamwe hawavunji maamrisho ya Allah swt na wala hawazisaliti au kuzipinga.

NAFSI HALISI (AL-NAFS AL-ZAKIYYAH)

1500. Aina nyigine ya nafsi ni ile nafsi au iliyo mtakatifu. Katika Qur'an Tukufu, Surah Ash-Shams, 91, Ayah 9-10, Allah swt anakula kiapo cha jua, mwezi mbingu, ardhi na vitu vingine na baadaye akiisemea nafsi, anatuambia: "Bila shaka amefaulu aliyeyeitakasa (nafsi yake) na bila shaka amejihasiri aliyeiviza (nafsi yake)" Ni dhahiri kuwa inambidi mtu afanye jitihada ili kufikia hatua hii. Kabla ya yote yale mengineyo, nafsi lazima iwe huru kutoka sifa zote zile zilizo ovu na hapo ndipo uwanja utakuwa tayari kwa kuzitambulisha sifa zilizo nzuri na bora kabisa na kwa uanzishaji na uendelezaji. Mtu ambaye nafsi yake itatakasika, basi amehakikishiwa msamaha (ukovu) na kufikia kipeo cha furaha ya milele.

NAFSI YA KUKARIPIA - LAUMU (AL-NAFS AL- LAWWAMA)

1501. Inawezekana wakati mwingine kuwa hivyo kwa vyovyote vile na kiasi chochote kile cha madhambi ayafanyayo, mtu hajisikii chochote cha kutenda kosa, wala hasikitiki, wala hajilaumu mwenyewe. Nafsi kama hiyo ni ile iliyoshindikana. Hata hivyo, ile nafsi baada ya kuanguka na kutenda madhambi na itajikaripia yenyewe na kujishutumu yenyewe, kabla ya yeyote yule kufanya hivyo, basi imeingia katika sharti tukufu mojawapo la nafsi itakiwavyo kuwa. Qur'an Tukufu, Surah Al Qiyamah, 75, Ayah 1-2, inatuelezea:

"Naapa kwa siku ya Qiyamah. Tena naapa kwa nafsi inayojilaumu; (kuwa mtafufuliwa na mtalipwa )".

Ni dhahiri kuwa iwapo Allah swt akiapia kwa vitu, basi kuna utukufu wake humo. Nayo pia ni wazi kuwa yeyote yule aifunzae nafsi yake vyema hadi ule wakati wa kutenda madhambi, yenyewe (nafsi) hujaa masikitiko na kujilaumu, basi imefikia mojawapo ya vina vya utakatifu.

NAFSI ILIYOFUNGULIWA HERI (AL-NAFS AL-MULHAM)

1502. Sharti lingine la nafsi ni kuongozwa na Allah swt. Twaambiwa katika Qur'an Tukufu, Surah Ash-Shams, 91, Ayah 8 " Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake" Maongozi haya ni kutia moyo kwa nafsi wakati itapokuwa katika hali ya kutakasika- Nafsi halisi si ambayo tumeishaizumgumzia. Ni lazima iwapo nafsi itaelekezwa kwa mujibu wa madhambi basi muongozo na kufunguliwa kwa heri kutoka kwa Allah swt yatafikia kikomo chake. Kwa kupingana na sifa na masharti ya nafsi ambazo ni sababu ya furaha ya milele na utakatifu, baadhi ambazo zimekwisha tajwa hapo awali, pia hapo hapo kuna sifa na masharti yanayosababisha maovu ya nafsi, sasa tuziangalie.

NAFSI YENYE MADHAMBI (AL-NAFS AL-AATHIMA)

1503. Iwapo nafsi ya mtu ikiwa na tabia ya kutenda madhambi, basi huitwa yeye madhambi. Qur'an Tukufu, Surah Al Baqara, 2, Ayah 283 inazungumzia kulipa kwa amana:

"Na mkiwa safarini na hamkupata mwandishi, yatosha kukabidhiwa rahani. Na mmoja wenu akimwekea amana mwenziwe basi aliye aminiwa airudishe amana ya mwenzake, na amche Allah swt, Mola wake Mlezi. Wala msifiche ushahidi. Na atakaye ficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Allah swt ni Mjuzi wa mnayo yatenda ."

Hii inathibitisha kuwa nafsi ya yeyote yule ambaye ameshajizoelesha madhambi ni nzito na ni wazi na tayari kwa kutenda madhambi wakati wowote ule.

NAFSI ILIYO SINZIA (AL-NAFSAL-GHAFIL)

1504. Sababu mojawapo ya kushidwa na kufifia kwa nafsi ni kulegea au kusinzia au kuwa zembe. Kwa kutenda mambo maovu na kwa kuendelea kutenda madhambi ndiko kunakosababisha nafsi kuelekea palipo paovu na kutomsikia Allah swt. Anaelezea Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Al Kahf, 18, Ayah 28:

"Na isubirishe nafsi yako pamoja na wanao muomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka radhi yake. Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka pambo la maisha ya dunia. Wala usiwatii wale ambao tumezighafilisha nyoyo zao wakafuata matamanio yao yakawa yamepita mpaka "

NAFSI ZILIZOTIWA MUHURI (AL-NAFS AL- MATBU')

1505. Hapa inamaanisha kufungwa muhuri juu yake na hivyo ndivyo hatua ya mwisho,Amesema Allah swt katika Quran:

"Na watakaokuwa na uzani khafifu, basi hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao kwa sababu ya kuzifanyia ujeuri Aya zet u."

Popote pale mtu anapokuwa fidhuli au juvi kuelekea Allah swt hadi kudharau na kutokubali ujumbe Wake na maamrisho ya Allah swt ambayo amemwekea mbele yake, au , iwapo yeye atazikubalia, anazipa umuhimu kidogo na kuwa na kosa la upinzani basi hapo nafsi yake inaingia katika hatua ile ambayo ni sawa na kama tahadhari, maamrisho matukufu na yale yaliyo haramishwa hayatakuwa na athari yoyote ile kwake yeye. Na hii ni hatua mojawapo ya kudidimia kwa nafsi na kushindwa kwake.

NAFSI ILIYO POFUKA ( AL-NAFS AL- AMYA)

1506. Hali nyingine ya Nafsi ni kupofuka. Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Al Hajj, 22, Ayah 46:

"Je! Hawatembei katika ardhi ili wapate kuwa na nyoyo zao za kuzingatia, au masikio ya kusikia? Kwa hakika macho hayapofuki, lakini nyonyo ambazo zimo vifuani ndizo zinapofuka ."

Nyoyo hizi zinaona vingine mbali na Allah swt na hazimwoni Allah swt. Nyoyo za aina hizi huona yale tu yatakayo yenyewe bila ya kuyazingatia yale maamrisho ya Allah swt na kwa hakika ndizo zilivyo kama vile vimepofuka tu.

NAFSI YENYE MARADHI (AL-NAFS AL-MARIDHA)

1507. Qur'an Tukufu, Surah Al Baqara, 2, Ayah 10:

"Nyoyoni mwao mna maradhi, na Allah swt amewazidishia maradhi. basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uongo ."

Ugonjwa wa aina hii inawezekana kuonekana mioyoni mwetu kwa sababu ya yale madhambi tuyafanyayo sisi siku hadi siku. Kama vile mtu mgojwa huwa hana hamu ya vyakula wala madawa ambavyo ni vyenye manufaa kwake na vile vile vyakula vizuri havitakuwa na ladha yoyote kwake, ndivyo vivyo hivyo kuhusu NAFSI iliyougua, kwani inapatikana kuonywa (na Allah swt) na kukaribia kwa upole kwa mapendo na matakwa yake ya humu ulimwenguni na Aakhera kuwa yenye adhabu kali sana na yenye kutisha mno. Kilicho zaidi ni kwamba mtu aliyeugua hivyo ni yule mwenye, kuipendelea kwa ajili ya nafsi yake yale yote yaliyo mabaya na maovu, kwani huwa anavutiwa navyo kama kwamba ndivyo vyenye kumfaa yeye. Kwa hakika hii ndiyo ile nafsi iliyokwisha ugua; kama vile ilivyo kifo kwa mtu hatakayetibiwa magonjwa yake na hivyo ndivyo vinaweza kutokea kwa ajili ya aina hii ya nafsi iwapo haitoweza kutibiwa kabla ya ugonjwa kuenea pote na hatimaye mtu aweza kuangamia. Popote pale mtu aonapo kuwa yeye hatamani chochote kile atakiwacho kukifanya yaani kumkumbuka Allah swt katika sala na kutii Sharia Tukufu za Dini ambazo hazimfai na ambazo ni chungu kwake, kwa hivyo ni wazi kabisa kuwa atambua kuwa hiyo nafsi wake imeshaanza kuugua maradhi, na bila ya kusita inambidi afanye kila hila awezayo ili ajielekeze kwa mujibu wa aya za Qur'an Tukufu, kwa watawa na walio waumini halisi na wale walio hodari katika elimu na ujuzi huu: waganga wa moyo, wanavyuoni waelewao na wafuatao mienendo ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ., ili waweze kuitibu nafsi ya aina hiyo iliyopatwa na maradhi.

NAFSI INAYOKWENDA UPANDE (AL-NAFS AL-ZA'IGHA)

1508. Moyo au Nafsi pia inaweza kusemwa kuwa inakwenda upande au inapotoka. Aina hii ya Nafsi ni ile ichaguayo upotofu wakati ipatiwapo chaguo katika hali mbili ya wema na uovu. Kama mategemeo yote ya maisha, katika sehemu zote za Imani, maadili na matendo, mambo yake yote yaliyo dhahiri na yale yote yaliyo batili mwake, mwanadamu daima anakumbwa na mgawanyiko wa njia mbili mbele yake , mtu ambaye amefaulu na kufurahika ni yule ambaye daima anachagua njia ile aitakayo Allah swt. i.e njia iliyonyooka (Sirat al-Mustaqeem) ya dini katika kila hali. Hata hivyo, mtu ambaye moyo wake unampotosha, huwa daima ndiye achanguaye njia ya upotofu Katika Qur'an Tukufu, kuzungumzia mifano na mafumbo ya aya na kwa kuelezea wazi wazi, Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Surah Al I'mran, 3, Ayah 7:

"Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazobabaisha kwa kutaka kuwaharibu watu kutaka na kujua hakika yake vipi. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. lakini hawakumbuki hayo isipokuwa wenye akili ."

Hivi kwa kuchagua mfano (mutashabih) wa aya za Qur'an Tukufu ili kuitumia Qur'an Tukufu kwa kuhakikisha matakwa ya mtu binafsi ni sampuli ya ile nafsi iliyopotoka.

NAFSI YA MOYO MGUMU (AL-NAFS AL-QASIYA)

1509. Sharti lingine la nafsi kuwa hivyo ni kutokana na moyo mgumu na katili. Katika Qur'an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 13:

"Basi kwa sababu ya kuvunja agano lao tuliwalaani, na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanayabadilisha maneno kutoka pahala pake, na wamesahau sehemu ya yale waliyo kumbushwa. Na huachi kuvumbua khiana kutokana nao, isipo kuwa wachache miongoni mwao. Basi wasamehe na waache. Hakika Allah swt huwapenda wafanyao wema ."

Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu Surah Al H'adiid, 57, Ayah 16:

"Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Allah swt na haki iliyo teremka? Wala wasiwe kama walio pewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, Kwa hivi nyoyo zao zikiwa ngumu na wengine wao wakawa wapotovu ."

Hali kama hii inaelezewa katika aya zinginezo pia. Nyoyo kama hizi zina sifa kama zile za jiwe na chuma, kuwa hakuna chochote kile kiwezacho kuathiri au kuacha alama yoyote juu yake ila kwa mshindo mkali tu moto. Hadi kufikia hali ya moyo kuwa mgumu kiasi hiki ni dhahiri ikionekana vile maovu yalivyo mteka huyo mtu hadi akawa mtumwa wa matakwa na maovu yake. Kwa hakika imepotoka!

NAFSI WASIWASI (AL-NAFS AL-MURTABA)

Nafsi ya aina hii imo katika hali hii ya wasiwasi kuhusu vile vitu ipasavyo kuvijua na kuviamini. Shaka kuhusu mizizi ya Dini ya Islam kama vile kushuku kuwapo kwa Allah swt, Aakhera, Utume wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . na vile vile Uimamu (wa ma-Imamu(a.s) , na kushuku matawi ya Dini kama vile sala, saumu na mema na mengineyo mengi. Katika Qur'an Tukufu, Surah Tawba, 9, Ayah 45:

"Wasio muamini Allah swt na Siku ya Mwisho na nyoyo zao zina shaka, hao tu ndio wanao kutaka ruhusa. Basi hao wanataradadi katika shaka zao ."

Hii ni mojawapo ya sababu ya upotofu wa Nafsi na ni fardhi kwa watu wale walio katika hali kama hii kujielekeza katika Ayah za Qur'an Tukufu na Ahadith Tufuku za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . na Ma-Imamu(a.s) . na kwa wanavyuoni wa dini ili kuweza kutokomeza hali hii kabla ya kutanda juu ya Nafsi nzima undani mwake. Ama sivyo, iwapo hali kama hii haitashughulikiwa na badala yake ikapuuzwa na kubakia Nafsini, basi itamwelekeza mtu katika hali ya kukatiza na kukataliwa (kupuuzwa na kudhoofika).

NAFSI ILIYOPATA KUTU (AL-NAFS-AL-RA'INA)

1511. Kutu ni shida nyingineyo ambayo nafsi inaweza kupatwa kwani ni sawa na ule mfano wa kioo cha kujitazamia, iwapo ile poda itabanduka basi hutaweza kujitamazama kiooni. Basi kioo cha nafsi ambavyo ni sehemu umuhimu kwa ajili ya Allah swt utukufu wa ukamilifu wake, fadhila zake zitamorudishwa kwake, hazitoweza kurudishwa iwapo itashika kutu, na hatimaye itaweza kupoteza ile nguvu ya kupeleka ujumbe wako kwa Allah swt. Ingawaje mwanadamu hawezi kumtazama Allah swt kwa macho yake, lakini anao uwezo wa kumwona Allah swt, Utukufu wake na Ukuu wake kwa kupitia NURU iliyomo katika Nafsi yake. Nafsi ile ambayo imeshakwisha shikwa na kutu ambamo sasa hakuna uwezo wa kurudishia kutokana kwa Allah swt, basi bila shaka itatapatapa huko na huko ikimtafuta sheitani na hasa kwa mujibu wa maana yake. Qur'an Tukufu, Surah Al Mut'affifiin, 83, Ayah 14, ikiwa inatukumbusha kuwa:

"Sivyo hivyo! Bali yametia juu ya nyoyo zao (maovu) waliokuwa wakiyachuma." Katika aya hii twaelezewa vyema kabisa kuwa chanzo cha kupatwa kwa kutu kwa Nafsi ni kule kutenda madhambi. Kwa hivyo kila dhambi itatupia uzito (itatanda kiza juu ya moyo; na ifikiapo hali kama hii, inambidi mtu afanye Tawba (Kipo kitabu nilichokitarjumu katika lugha ya kiswahili kinachozungumzia swala hili kwa marefu na mapana ) mara moja kwa ajili ya kuyasafisha hayo matendo maovu na atende matendo mema ili kuzuia kupotea kwa nuru iliyotunukiwa Nafsi yake. Vile vile, twaambiwa katika hadith Tukufu kuwa: "Mtu mwenye furaha kuu katika siku ya Qiyama ni yule atakaye yaona maneno aliyokuwa akiyatamka 'naomba msamaha wa Allah swt' chini ya kila dhambi alilolitenda. Kwa hivyo inambidi kila Mwislam miongoni wetu apige msasa kila ovu alilolitenda ama sivyo, Allah swt azitowazo onyo zake za upole zitabadilika na kuwa ghadhabu kubwa sana.

NAFSI AMURU (al-Nafs al- 'Ammara):

1512. Nafsi isiyofunzwa hasa wakati wa ujana wa mtu, huamuru kutendwa kwa matendo ya madhambi bila kiasi. Katika Qur'an Tukufu, Surah Yusuf, 12, Ayah 53 , kuhusu kisa cha Mtume Yussuf (a.s), inazungumziwa Nafsi:

"Nami sijitoi Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu isipokuwa ile ambayo Mola wangu Mlezi aliyo irehemu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu na Mwenye kurehemu ."

Sentensi hiyo inaonyesha kuwa ilitamkwa na Zuleikha aliyekuwa amependa Mtume Yussuf(a.s) . Pale alipotoa ushahidi, alithibitisha kuwa ndiye chanzo cha uovu huo. Kwani Mtume Yussuf(a.s) . alikuwa hayupo wakati huo wa ushahid, lakini kwa kuwa Zuleikha alikuwa hana hila yoyote ile dhidi ya Mtume Yussuf(a.s) . Pia kuna uwezekano kuwa hayo yametamkwa na Mtume Yussuf(a.s) . au ni wote vyovyote vile, Qur'an Tukufu, Surah Yusuf, 12, Ayah 53, inatuambia kuwa:

"Nami sijitoi Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu isipokuwa ile ambayo Mola wangu Mlezi aliyo irehemu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu na Mwenye kurehemu ."

Nafsi yoyote ile isiyokuwa imeongozwa kwa mujibu wa mfano ya Islam, huwa daima inavutwa popote pale penye madhambi na ma'asiyah kwani yote hayo yako yamedhalilishwa kabisa. Mfano wa Nafsi hii ni sawa na mtoto mchanga atakaye kila kitu kuchezea bila kutazama ubora wake, faida au hasara zake, ilimradi yeye apate kuchezea tu, Nafsi ya yule aliye na utamaduni mzuri, aliyekomaa na kubaleghe inavutika pale penye mema na hujiepusha na maana yake; na ile nafsi iliyo ilimishwa na inavutika pale penye maovu ya kila aina na kwa hivyo lazima ifunzwe vyema, itasaidia kutakasisha hiyo Nafsi.

HATIMAYE

Kile kilichoelezwa hapo kinasema kuwa Nafsi inaweza kuwa bora kabisa ama mbovu kabisa au vinazidiana katika vina na ngazi. Kuna nafsi zifikiapo kuitwa Nafsi halisi na Nafsi ridhika n.k. na vile vile kuna zinapofifia hadi kufikia hali mbaya kabisa na matokeo yake ni majanga, majonzi na maovu na kufikia ile sifa ya kupigwa mihuri au zilizopofuka na zenye maradhi zikiwa ni kama mifano. Hali hii inadhihirisha kuwa Nafsi zinapangwa na kila mtu na kila mtu anayo Nafsi moja tu.

1513. Qur'an inatuambia katika, Sura Ya-Sin, 36; Ayah 79: Sema:

"Ataihuisha yule aliyeiumba mara ya kwanza, naye ni Mjuzi wa kila (namna ya ) kuumba "

1514. Amesema al-Imam Ja'afar as- Sadique(a.s) . katika Al-Kafi : "Kuwazulia uwongo Allah swt na Mtume Muhammad (s.a.w.w). ni Dambi Kuu (dhamb kabirah) ."

FADHAIL ZA IMAM ALI(a.s)

1515. Kutokea 'Ala, amesema yeye: "Mimi nilimwuliza 'Aysha kuhusu 'Ali ibn Abi Talib. Mimi nilimwuliza Mtume (s.a.w.w). kuhusu yeye. 'Ayesha alijibu, naye akasema kuwa 'Ali ni mtu bora kabisa katika Wanadamu, na hakuna mwenye shaka yoyote ile isipokuwa ni mpagani tu ."

1516. Na kutoka 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , kasema: "Aliniambia Mtume Muhammad (s.a.w.w). 'Wewe ni bora wa viumbe vya Allah swt, na hakuna mwenye shaka yoyote ile isipokuwa atakuwa ni kafiri "

1517. Na kutoka kwa Hudhaifa: "Alisema Mtume Muhammad(s.a.w.w) . kuwa 'Ali ni bora wa Wanaadamu. Yeyote yule anayekataa haya kwa hakika ni kafiri."

1518. Kutokea kwa Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . alisema: "Alisema Mtume Muhammad (s.a.w.w). , 'uadui, chuki na bughudha dhidi ya 'Ali ibn Abi Talib ni ukafiri na uadui dhidi ya Bani Hashim ni unafiki .'"

1519. Na kutokea kwake, kutokea Mtume Muhammad(s.a.w.w) . akasema: "Hakuna ampendaye 'Ali ibn Abi Talib (a.s). isipokuwa ni mumiin halisi, na hakuna amchukiaye 'Ali isipokuwa ni kafiri ."

1520. Na kutokea Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . , alisema: "Amesema Mtume Muhammad (s.a.w.w). kuwa yeyote yule atakaye msema vibaya 'Ali ibn Abi Talib, basi ajue kuwa amenisema mimi vibaya hivyo, na yeyote yule anisemaye mimi vibaya, basi amemsema hivyo Allah swt (na hilo ni dhambi kuu) ."

1521. Amesema Al-Imam Ali ibn Abi Talib(a.s) . kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) . amesema: "Kwa hakika Allah swt alitazama kuelekea dunia hii na akanichagua mimi kutoka watu wa dunia; na kwa mara nyingine tena aliangalia duniani na kukuchagua wewe kutoka watu wa dunia; na kwa mara ya tatu alipoangalia akawachagua Maimamu(a.s) . kutokea vizazi vyako miongoni mwa watu wote wa dunia hii; na kwa mara ya nne alipoangalia akamchagua binti yangu Fatimah kutokea wanawake wote wa dunia hii."

1522. Kutokea Ja'abir, anasema kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) . amesema: "Ali ibn Abi Talib (a.s) . ni bora miongoni mwa watu wa dunia. Yeyote yule aliye na shaka, basi ni kafiri ."

1523. Amesema Ibn 'Abbas kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) . amesema: "Ali ibn Abi Talib (a.s) . ni mlango wa Hitta Yeyote yule atakayeingia ndani mwake basi kwa hakika ndiye mumiin wa kweli, na yeyote atakayetoka kutoka humo ni kafiri ."

1524. Al-Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . kutokea baba yake amesema kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) . aliulizwa kuhusu hali ya watu, naye akajibu "Bora kabisa na Mcha Mungu halisi na ambaye aliye karibu kabisa nao ambay yuko karibu nami ni Ali ibn Abi Talib (a.s) . , na hakuna Mcha-Mungu halisi miongoni mwenu, na ambaye yupo karibu nami kuliko Ali ibn Abi Talib (a.s) ."

1525. Jami' bin 'Omair, alisema kuwa yeye alimwuliza 'Ayesha kuhusu daraja la 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . mbele ya Mtume Muhammad(s.a.w.w) ? Yeye alijibu: "Kwa hakika ni mtu mwenye kuheshimiwa mno mbele ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ."

Yeye alimwuliza tena kuhusu nafasi ya Ali ibn Abi Talib(a.s) . katika macho ya Mtume Muhammad(s.a.w.w) . Alijibiwa kuwa: "Ni mtu mwenye kuheshimiwa mno mbele ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ."

1526. Na kutokea Ibn 'Umar amesema kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) . amesema: "Bora wa mtu miongoni mwenu ni 'Ali ibn Abi Talib (a.s). na bora wa vijana wenu ni Al - Hassan na Al -Husayn "

1527. 'Urwah anaripoti kutoka 'Ayesha kuwa: Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) . "Kwa hakika nimeahidiwa na Allah swt kuwa yeyote yule atakayeinuka dhidi ya 'Ali ibn Abi Talib (a.s) . basi kwa hakika ni kafiri na kwa hakika ataingia Jahannam aunguzwe na moto. 'Aisha akasema kuwa "Mimi niliisahau hadith hii siku ya (vita vya) Jamal, hadi hapo nilipoikumbuka au nilipokumbushwa tukiwa Basra (Iraq), nami namwomba Allah swt anisamehe, na sitegemei kuwa miongoni mwao ."

1528. Abu Salim bin Abu al-Jaada amesema kuwa yeye alimwomba Ja'abir azungumze chochote kuhusu 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Ja'abir akasema: "'Ali ibn Abi Talib(a.s) . alikuwa bora miongoni mwa wanadamu." Mimi nilimwuliza tena "Je unasemaje kuhusu mtu atakayemchukia 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ."Yeye alinijibu: "Hakuna atakayemchukia 'Ali ibn Abi Talib (a.s) . isipokuwa kafiri ."

1529. Hashim bin Barid alisema kuwa'Abdullah ibn Mas'ud alisema: "Mimi nilijifunza Sura 70 za Qur'an Tukufu kutokea kinywani mwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) . na Surah za Qur'an zilizobakia nilijifunza kutokea mbora wa Ummah wetu yaani Ali ibn Abi Talib(a.s) ."

1530. Muhammad bin Salim al-Bazzar anasema kuwa yeye alikuwa pamoja na Said bin al-Musayyib katika Masjidi-Nabi, siku ya Ijumaa, ndipo alipotokezea mhubiri kutoka kabila la Banu Omayyah (laana za Allah swt ziwafikie juu yao ) na akapanda juu ya mimbar na akaanza kumtusi Ali ibn Abi Talib(a.s) . kwa kusema: "Kwa hakika, Allah swt hakumtukuza Ali ibn Abi Talib (a.s). kwa mapenzi yake ba dala yake amefanya hivyo kwa kuhofu uchochezi wake ." Kwa hayo Said bin Al-Musayyib alimlaani na kumwambia: "Kwa hakika wewe unasema uongo mtupu" Na hapo alimtupia nguo aliyokuwa akijifunika juu ya mdomo wa mhubiri huyo. Hapo watu walipomwambia kuwa itakuwaje iwapo Abu Muhammad wakati Imam huyo anatokana na Banu Omayyah ? Hapo Said alijibu: "Kwa kiapo cha Allah swt! Mimi sijui nilichokisema, lakini mimi nilimsikia Mtume Muhammad(s.a.w.w) . akisema haya kutokea makbara haya nami ndipo nilipoyarudia kuyasema."

1531. Ummi Hani binti Abu Talib(a.s) . kasema kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) . kasema kuwa: "Bora wa viumbe vya Allah swt katika mtazamo wake Allah swt, ni yule anayelala kaburini mwake na kamwe hakumshuku 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . na kizazi chake ni bora wa vizazi katika viumbe vyote."

1532. Ja'abir anasema kuwa "Hakuna anayeshuku fadhail za 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . isipokuwa ni kafiri na kasema kuwa "Kwa kiapo cha Allah swt sisi kamwe tulikuwa hatuwajui wanafiki, katika zama za Mtume Muhammad (s.a.w.w). isipokuwa kwa yule mwenye chuki dhidi ya 'Ali ibn Abi Talib (a.s) ."

1533. Said bin Ja'abir alise kuwa yeye alikuwa akimwongoza Ibn 'Abbas baada ya yeye kupoteza nuru ya macho yake, kutokea Msikitini, na aliwapita kundi la watu waliokuwa wakimtukana 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . na aliniambia kuwa nimchukue hapo. Hivyo mimi nilimfikisha kwao. Kufika hapo alisema "Ni nani miongoni mwenu anayemkashifu Allah swt ?! Kwa hakika yeyote yule anayemkashifu Allah swt amekuwa kafiri. Na ni yupi yule anayemkashifu 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ? Na kwa hakika hili limetokea" akasema. Ndipo alipoendelea kusema: "Nashuhudia Allah swt, kwa kiapo cha Allah swt, mimi nilimsikia Mtume Muhammad(s.a.w.w) . akisema 'Yeyote yule anayemkashifu 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . basi amenikashifu mimi na kwa hakika anayenikashifu mimi basi ajue kuwa amemkashifu Allah swt na yule anayemkashifu Allah swt, Mtume wake basi watatakiwa kutoa maelezo yake." Na hapo ndipo Ibn 'Abbas aligeuka.

1534. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Muzirembeshe vikao vyenu kwa mazungumzo na makumbusho ya 'Ali ibn Abi Talib (a.s). kwani dhikr zake ni dhikr zangu na dhikr zangu ndizo dhikr za Allah swt na dhikr za Allah swt ni 'ibadah. Na mwenye kufanya 'ibadah huingia Peponi ."

1535. Amesema: "Siri ya ufanisi ni hii, kwamba uhusiano wetu na wengine uwe wa mapenzi badala ya uhasama. Ikiwa mtu hawezi kufanya urafiki na watu wenye tabia nzuri, basi hataweza kabisa kuishi bila kuwa na fazaa! "

1536. Mwanachuoni mmoja amesema: "Maisha yetu ni kama eneo la milima ambapo ikiwa patapigwa ukelele mmoja, mtu atasikia mwangwi wake ukirudi kwake; hivyo, wale waliojawa na mapenzi ya wengine katika nyoyo zao, wataona hali kama hiyo kutoka kwao. Ni kweli kwamba maisha yetu ya kidunia yamesimama juu ya mabadilishano na malipano. Hatutaki kusema kwamba maisha yetu ya kiroho pia yamesimama juu ya msingi huohuo, lakini vipi inayumkinika kutaraji kuona uaminifu kutoka kwa wengine bila ya wewe mwenyewe kuwa mwaminifu kwao? Na vipi mtu atake apendwe na wengine bila yeye mwenyewe kwanza kuwapenda wao.?"

1537. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . aliwakunjulia watu wote moyo wa mapenzi. Upendo wake mkubwa juu ya watu, upole na mvutio wake ulikuwa ukidhihirika kwenye uso wake wa kimalaika. Alikuwa akiwatendea vizuri na kuwakirimu Waislam wote sawasawa. "Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w). alikuwa akiwashughulikia na akigawa wakati wake kati ya masahaba zake sawasawa ." [234]

1538. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alikuwa akikataza tabia mbovu, na alikuwa akisema: "Tabia mbaya ni kisirani, na mtu mwovu kabisa kati yenu ni yule mwenye tabia mbovu ." [235]

1539. Mahali pengine amesema: "Enyi wana wa Abdul Muttalib! Ninyi hamtaweza kamwe kuwaridhisha watu kwa mali zenu, hivyo kutaneni nao kwa uso mchangamfu na mwendo mzuri ."[236]

1540. Aliyekuwa mtumishi wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , Anas bin Malik, alikuwa daima akikumbuka hulka nzuri ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , na alikuwa akiwaambia watu kwamba katika kipindi cha miaka kumi aliyomtumikia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , hakuwahi kabisa kumwona ameukunja uso wake unaonawiri, wala hakuwahi hata mara moja kumwona amepandisha nyusi zake au ameonyesha uso wa hasira kwa sababu ya kufanya jambo lisilopendeza.

1541. Tabia njema na uchangamfu ni katika sababu zinazozidisha umri wa mtu. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Wema na tabia nzuri hustawisha ardhi na huzidisha umri ."[237]

1542. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Tabia njema ni miongoni mwa ufanisi wa mtu ."[238]

1543. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Tabia nzuri hupanua riziki na huvuta (nyoyo za) urafiki ."[239]

1544. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Watu wenye akili kamilifu kabisa ni wale wenye tabia nzuri kabisa ."

1545. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Vitakavyowaingiza kwa wingi umma wangu katika Jannat ni ucha-Mungu na tabia njema ." [240]

1546. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Chukulia jambo la ndugu yako (wa imani) kwa maana nzuri kabisa mpaka ulione kinyume chake wala usilidhanie vibaya neno analolitoa ndugu yako wakati kuna uwezekano wa kuwa sahihi na kheri ."[241]

1547. Matunda mojawapo ya dhana nzuri ni kupatikana urafiki wa watu wa kuwepo mapenzi na usafi wa moyo. Amirul Muuminin Ali(a.s) . ametaja matokeo na matunda ya dhana nzuri katika maneno yake mbalimbali, amesema: "Mwenye kuwadhania vizuri watu hujifaidia mapenzi yao ."[242]

1548. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Dhana nzuri humwokoa mwenye kufuata madhambi ."[243]

1549. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Dhana nzuri ni raha ya moyo na usalama wa dini ."[244]

1550. Dhana nzuri humpunguzia mtu taabu na matukio mabaya. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Dhana nzuri hupunguza majonzi ."[245]

1551. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Mwenye kuwa na matumaini juu yako huwa amekuamini na kukudhania vizuri, hivyo usiharibu dhana yake (ukamvunja moyo) ."[246]

1552. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Dhana ya mtu ni mizani ya akili yake, na kitendo chake ni ushahidi wa kweli kabisa wa dhati yake ."[247]

1553. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Mwenye kutojali dhana mbaya juu ya ndugu yake, huwa ana akili timamu na moyo mtulivu ."[248]

1554. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Miongoni mwa haki za muumin kwa muumin mwenzake ni kutomkadhibisha (kumsadiki) ."[249]

1555. Qur'an Tukufu, Surah Al Hujaraat, 49, Ayah 12. inasema waziwazi kwamba dhana mbaya ni dhambi, na inawatahadharisha Waislamu wajiepushe na kudhaniana dhana mbaya:Enyi mlioamini! Jiepusheni sana na kuwadhania watu dhana mbaya, kwani kuwadhani watu dhana mbaya ni dhambi .

1556. Mtume Muhammad(s.a.w.w) . amesema: "Allah swt amewaharamishia Waislamu vitu vitatu: damu zao, mali zao, na kudhaniana vibaya ."

1557. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Si uadilifu kutoa hukumu kwa kutegemea dhana ."[250]

1558. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Jihadhari na kudhania vibaya, kwani dhana mbaya huharibu ibada na huifanya dhambi kubwa zaidi ."[251]

1559. Vile vile amesema kwamba kuwadhania vibaya watu wanyoofu ni aina moja ya udhalimu: "Kumshuku mtu mwema ni dhambi mbaya kabisa na ni udhalimu unaochukiza sana."[252]

3

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TISA

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُهُمْ وَلَا يَضُرُّهُمْ وَكَانَ الْكَافِرُ عَلَىٰ رَبِّهِ ظَهِيرًا ﴿٥٥﴾

55. Na wanaabudu wasiowadhuru wala kuwanufaisha badala ya Mwenyezi Mungu. Na kafiri daima ni msaidizi wa mpinzani wa Mola wake.

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا مُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿٥٦﴾

56. Na hatukukutuma ila uwe mbashiri na muonyaji.

قُلْ مَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِلَّا مَن شَاءَ أَن يَتَّخِذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا ﴿٥٧﴾

57. Sema: Siwaombi ujira juu yake, isipokuwa mwenye kutaka ashike njia iendayo kwa Mola wake.

وَتَوَكَّلْ عَلَى الْحَيِّ الَّذِي لَا يَمُوتُ وَسَبِّحْ بِحَمْدِهِ وَكَفَىٰ بِهِ بِذُنُوبِ عِبَادِهِ خَبِيرًا ﴿٥٨﴾

58. Na mtegemee aliye hai ambaye hafi na umtukuze kwa sifa zake. Na yatosha kuwa yeye ni mwenye habari za dhambi za waja wake.

الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ الرَّحْمَـٰنُ فَاسْأَلْ بِهِ خَبِيرًا ﴿٥٩﴾

59. Ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha akastawi juu ya Arshi. Mwingi wa rehema! Uliza habari zake kwa ajuaye.

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اسْجُدُوا لِلرَّحْمَـٰنِ قَالُوا وَمَا الرَّحْمَـٰنُ أَنَسْجُدُ لِمَا تَأْمُرُنَا وَزَادَهُمْ نُفُورًا ﴿٦٠﴾

60. Na wanapoambiwa msujudieni Mwingi wa rehema, wanasema: Ni nani huyo mwingi wa rehema? Je, tumsujudie unayetuamrisha wewe? Na huwazidishia chuki.

تَبَارَكَ الَّذِي جَعَلَ فِي السَّمَاءِ بُرُوجًا وَجَعَلَ فِيهَا سِرَاجًا وَقَمَرًا مُّنِيرًا ﴿٦١﴾

61. Amekuwa na baraka yule aliyejaalia katika mbingu buruji na akajaalia humo taa na mwezi wenye nuru.

وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ خِلْفَةً لِّمَنْ أَرَادَ أَن يَذَّكَّرَ أَوْ أَرَادَ شُكُورًا ﴿٦٢﴾

62. Naye ndiye ambaye ameujaalia usiku na mchana kufuatana, kwa yule anayetaka kukumbuka au anayetaka kushukuru.

KAFIRI NI MSADIZI WA MPINZANI WA MOLA WAKE

Aya 55 – 62

MAANA

Na wanaabudu wasiowadhuru wala kuwanufaisha badala ya Mwenyezi Mungu.

Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 11 (10 18).

Na kafiri daima ni msaidizi wa mpinzani wa Mola wake.

Yaani anawasaidia watu wa batili dhidi ya haki. Kila mwenye kusaidia batili atakuwa amesaidia dhidi ya Mwenyezi Mungu na kuwa adui yake; hata kama atamsabihi na kumtukuza kwa ulimi wake. Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :“Mwenye kumsaidia dhalimu na huku anajua kuwa ni dhalimu basi amejitenga na Uislamu.”

Kadiri nitakavyotia shaka, lakini siwezi kutia shaka kuwa mwenye kumtegemea dhalimu ni kafiri; bali kafiri aliye mwadilifu ni bora kuliko yeye. Aya za Qur’an kuhusu hilo ni nyingi na ziko wazi. Ama Hadith za Mtume zimepituka kiwango cha mutawatir.

Ndio! Ni wajibu wetu kuamiliana naye muamala wa kiislamu kwa vile tu ametamka: Lailaha illallah Muhammadurrasulullah (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.)

Na hatukukutuma ila uwe mbashiri na muonyaji.

Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 15 (17:105).

Sema: Siwaombi ujira juu yake, isipokuwa mwenye kutaka ashike njia iendayo kwa Mola wake.

Mimi sina tamaa ya mali yenu wala siwauzii pepo. Ninalotaka ni kutengeneza tu. Anayetaka kufanya njia ya kumwendea Mola miongoni mwenu, basi malipo yake yako kwa Mungu. Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:90) na Juz.12 (11:88).

Na mtegemee aliye hai ambaye hafi na umtukuze kwa sifa zake. Na yatosha kuwa yeye ni mwenye habari za dhambi za waja wake.

Ewe Muhammad! Toa bishara na onyo ukimtegemea Mwenyezi Mungu kwa kuwa na ikhlasi naye katika kauli yako na vitendo vyako na ujitakashe na kumfanyia mfano na kila lile ambalo halifanani na utukufu na ukuu wake. Yeye anamjua zaidi aliyepotea njia, na atamhisabu na kumlipa.

Ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha akastawi juu ya Arshi.

Makusudio ya kustawi ni kutawala. Lililo na nguvu ni kuwa makusudio ya siku ni mikupuo, kwa sababu hakuna siku kabla ya kupatikana ulimwengu na jua. Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:54), Juz. 11 (103), na Juz. 12 (11:7).

Mwingi wa rehema! Uliza habari zake kwa ajuaye.

Habari yake, ni habari ya huko kuumbwa mbingu na ardhi, ambako kunafahamika kutokana na mfumo wa Aya. Hapa kuna maneno yaliyotan- gulizwa na ya kukadiriwa. Maana ni: Yeye ni Mwingi wa rehema, ulizia habari za kuumbwa mbingu na ardhi kwa yule ajuaye ambaye ni Mwenyezi Mungu.

Na wanapoambiwa msujudieni Mwingi wa rehema, wanasema: ‘Ni nani huyo mwingi wa rehema? Je, tumsujudie unayetuamrisha wewe?’ Na huwazidishia chuki.

Nabii(s.a.w.w) akiwaambia washirikina: ‘Mwabuduni Mwingi wa rehema, wala msiabudu masanamu,’ wao husema kwa kujitia hamnazo, kwa madharau, ni nani huyo unayetuambia tumwabudu unayemuita Mwingi wa rehema? Unataka tukutii wewe na tuwaasi baba zetu katika yale waliyokuwa wakiyaabudu?’

Ujinga na upumbavu huu unatukumbusha ujinga wa vijana wetu wanapoambiwa swalini na mfunge, husema: “Bado kuna Swala katika karne hii ya ishirini? Jambo la kushangaza ni kuwa vijana hawa wanaimba uhuru wa bianadamu; kama kwamba uhuru ni uzandiki na utu ni kujitoa kwenye misimamo.

Hawajui kuwa aliye huru ni yule anayemwabudu Mwenyezi Mungu wala hamnyenyekei asiyekuwa yeye na kwamba utu ni dini ya Mwenyezi Mungu ambayo inakataza maovu na munkar.

Amekuwa na baraka yule aliyejaalia katika mbingu buruji na akajaalia humo taa na mwezi wenye nuru.

Makusudio ya buruji ni mashukio ya jua na mwezi. Tazama Juz.14 (15: 16). Makusudio ya taa hapa ni jua, kutokana na kuunganisha na mwezi. Mahali pengine Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

هُوَ الَّذِي جَعَلَ الشَّمْسَ ضِيَاءً وَالْقَمَرَ نُورًا ﴿٥﴾

“Yeye ndiye aliyefanya jua kuwa mwanga na mwezi kuwa nuru.” Juz.11 (10:5).

Wengine wametofautisha baina ya nuru na mwanga. Kwamba mwanga unategemea sayari moja kwa moja; kama vile mwanga wa jua, unatoka kwenye jua moja kwa moja.

Nuru inategemea sayari kupitia sayari nyingine; kama vile nuru ya mwezi inavyotegmea jua. Wametoa dalili wanaotofautisha, kwa Aya hiyo ya Juz. 11 (10:5) tuliyoitaja punde.

Naye ndiye ambaye ameujaalia usiku na mchana kufuatana, kwa yule anayetaka kukumbuka au anayetaka kushukuru.

Usiku unaondoka kisha unakuja mchana, nao unaondoka kisha unarudi usiku na kuendelea; wala hakuna unaobakia muda mrefu kuzidi kiasi cha haja ya viumbe.

Kufuatana kwa namna hii kunafahamisha kuweko mpangiliaji mwenye hekima. Kufuatana huku kunategemea harakati za ardhi, nazo zinategemea msababishaji wake wa kwanza.

Ama hekima ya mfuatano huu, ni kwamba lau lingelibakia giza tu, au mwangaza tu, maisha yangelikuwa magumu hapa ardhini.

Kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t) ‘Kwa anayetaka kukumbuka,’ maana yake ni kuwa mwenye kutaka dalili ya kuweko Mwenyezi Mungu ataipata katika vitu vyote, vikiwemo kufuatana usiku na mchana.

Na kauli yake ‘Au anayetaka kushukuru,’ ni kuwa anayetaka kumshukuru Mweneyzi Mungu kwa neema yake naashukuru vile vile kwa kufuatana usiku na mchana, kwa sababu hilo ni katika neema kubwa.

وَعِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا ﴿٦٣﴾

63. Na waja wa Mwingi wa rehema ni wale wanaotembea ardhini kwa unyenyekevu. Na wajinga wakiwasemesha, husema: ‘Salama.’

وَالَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا ﴿٦٤﴾

64. Na wale wanaokesha kwa ajili ya Mola wao kusujudu na kusimama.

وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا ﴿٦٥﴾

65. Na wale wanaosema: ‘Mola wetu! Tuondolee adhabu ya Jahannam,’ hakika adhabu yake ni yenye kuendelea.

إِنَّهَا سَاءَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا ﴿٦٦﴾

66. Hakika hiyo ni mbaya kuwa kituo na mahali pa kukaa.

وَالَّذِينَ إِذَا أَنفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَٰلِكَ قَوَامًا ﴿٦٧﴾

67. Na wale ambao wanapotumia hawafanyi israfu wala hawafanyi uchoyo wanakuwa katikati baina ya hayo.

وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا ﴿٦٨﴾

68. Na wale ambao hawamwombi mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaiui nafsi aliyoiharamisha ila kwa haki, wala hawazini. Na mwenye kuyafanya hayo atapata madhambi.

يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا ﴿٦٩﴾

69. Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama na atadumu humo kwa kufedheheka.

إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٠﴾

70. Isipokuwa atakayetubia na akatenda matendo mema, basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللَّـهِ مَتَابًا ﴿٧١﴾

71. Na aliyetubu na akafanya mema, basi hakika huyo ametubu kwa Mwenyezi Mungu toba ya kweli.

وَالَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ الزُّورَ وَإِذَا مَرُّوا بِاللَّغْوِ مَرُّوا كِرَامًا ﴿٧٢﴾

72. Na wale ambao hawawi kwenye uzushi, na wanapopita kwenye upuzi hupita kwa heshima zao.

وَالَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ لَمْ يَخِرُّوا عَلَيْهَا صُمًّا وَعُمْيَانًا ﴿٧٣﴾

73. Na wale ambao wanapokumbushwa ishara za Mola wao hawajifanyi ni viziwi nazo na vipofu.

وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا ﴿٧٤﴾

74. Na wale ambao wanasema: Mola wetu! Tupe katika wake zetu na wanetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wenye takua.

أُولَـٰئِكَ يُجْزَوْنَ الْغُرْفَةَ بِمَا صَبَرُوا وَيُلَقَّوْنَ فِيهَا تَحِيَّةً وَسَلَامًا ﴿٧٥﴾

75. Hao ndio watakolipwa ghorofa kwa walivyosubiri na watakuta humo maamkuzi na salaam.

خَالِدِينَ فِيهَا حَسُنَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا ﴿٧٦﴾

76. Watadumu humo kituo na makao mazuri.

قُلْ مَا يَعْبَأُ بِكُمْ رَبِّي لَوْلَا دُعَاؤُكُمْ فَقَدْ كَذَّبْتُمْ فَسَوْفَ يَكُونُ لِزَامًا ﴿٧٧﴾

77. Sema, Mola wangu asingewajali lau si kupewa kwenu mwito, lakini nyinyi mmewakadhibisha, basi (adhabu) ni lazima.

WAJA WA MWINGI WA REHEMA

Aya 63 – 77

MAANA

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutaja sifa za makafiri na kiaga chao, kama kawaida yake, anataja sifa za waumini na malipo aliyowaandalia. Zifuatazo ndizo sifa zao:

1.Na waja wa Mwingi wa rehema ni wale wanaotembea ardhini kwa unyenyekevu.

Imam Jafar Sadiq(a.s) anasema katika tafsiri ya hilo:“Ni yule mtu anayetembea kwenye asili yake aliyoumbiwa, hajikalifishi wala hajifanyi.” Ndio, anayetembea kwenye umbile lake aliloumbiwa, tena akiwa peke yake bila ya kuwa na wapambe na wafuasi wanaomfuta nyuma na wengine mbele wakiwa wamepanda farasi au pikipiki na kupiga ving’ora vinavyohanikiza watu kwa sauti zake vikitangaza kuja kwake ili aachiwe njia, kwa ajili ya kumheshimu na kumtukuza.

2.Na wajinga wakiwasemesha, husema: ‘Salama.’

Makusudio ya kusemeshwa na wajinga ni kama vile kejeli zao, shutuma zao au mijadala ya hawa na masilahi. Amani ni kinaya cha kuachana nao, kwa kuwadharau na kuchunga mtu heshima yake. Maana ni kuwa, muumini akisikia neno ovu, aachane nalo; kama kwamba hakulisikia au kama anayekusudiwa ni mwingine sio yeye. Huu ndio mwepuko mwema aliousema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَاهْجُرْهُمْ هَجْرًا جَمِيلًا ﴿١٠﴾

“Na uwaepuke mwepuko mwema.” (73:10).

Hakuna mwenye shaka kwamba kuachana na jambo ni pale ikiwa hakuna uwezo au nguvu za kulikabili. Vinginevyo itakuwa ni wajibu kulikabili. Hapana budi kuihusisha Aya na hilo.

3.Na wale wanaokesha kwa ajili ya Mola wao kusujudu na kusimama.

Waumini wanasimama usiku kwenye giza wakifanya ibada ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu hilo liko mbali na ria, wala hawaupitishi usiku mikahawani na kwenye mambo ya mchezo mchezo tu, huku wakifuja mali na kupanga njama dhidi ya waumini na wenye ikhlasi. Mfano wa Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:

كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ ﴿١٧﴾

“Walikuwa wakilala kidogo usiku.” (51:17).

4.Na wale wanaosema: ‘Mola wetu! Tuondolee adhabu ya Jahannam, hakika adhabu yake ni yenye kuendelea. haikwepeki na ni yakudumu. Hakika hiyo ni mbaya kuwa kituo na mahali pa kukaa,

Waliamini Pepo na Moto, kutokana na waliyoyashuhudia na kuyaona; ndio wakauhofia moto wakaitumai pepo. Imam Ali(a.s ) anasema: “Wao na Pepo ni kama walioiona wakiwa ndani yake wananeemeshwa. Na wao na moto ni kama waliouona wakiwa ndani yake wanaadhibiwa.”

5.Na wale ambao wanapotumia hawafanyi israfu wala hawafanyi uchoyo wanakuwa katikati baina ya hayo, hakuna kupitisha kiasi, Si ubakhili wala ubadhirifu.

Huu ndio mwenendo wa Uislamu, wastani katika kila kitu; hakuna ulahidi wala waungu wengi, udikteta wala ukiritimba na hakuna kutaifisha mali ya mtu wala ubepari. Tazama Juz. 15 (17:29) kifungu cha ‘Uislamu na nadharia ya maadili.’

6.Na wale ambao hawamwombi mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu.

Mwenye kufanya riya au akamtii kiumbe katika kumuasi Muumba, basi huyo ni kama aliyemwomba mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu.

Wala hawaiui nafsi aliyoiharamisha ila kwa haki.

Nafsi inayouliwa kwa haki na kwa uadilifu ni ile iliyoua nafsi nyingine bila ya haki, aliyezini akiwa kwenye ndoa, kurtadi dini au kuleta ufisadi katika ardhi.

Ufafanuzi wa hayo uko katika vitabu vya Fiqh.

Wala hawazini

Kwa sababu zinaa ni katika madhambi makubwa. Ndio maana Mwenyezi Mungu (s.w.t). Akaiweka sawa na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kuua nafsi na akajaalia hukumu ya haya matatu ni kuuliwa kwa masharti yaliyotajwa kwenye vitabu vya fiqh.

Na mwenye kuyafanya hayo atapata madhambi.

Hayo ni hayo ya shirk, kuua na kuzini. Na madhambi ni adhabu.

Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama na atadumu humo kwa kufedheheka.

Kuna adhabu gani kubwa na kufedheheka zaidi kuliko adhabu ya Jahannam? Si kwambii tena ikiwa itazidishwa pamoja na kudumu kusiko na mwisho.

Isipokuwa atakayetubia na akatenda matendo mema, basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mwenye kurehemu.

Mwenye kutubia dhambi ni kama asiyekuwa na dhambi, zaidi ya hayo, Mwenyezi Mungu atampa thawabu kwa kule kutubia kwake na atampa mema kulingana na maovu ya dhambi zake; kiasi ambacho toba itafuta maovu ya dhambi.

إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ﴿١١٤﴾

“Hakika mema huondoa maovu.” Juz. 12 (11:114).

Haya ndiyo maana ya ‘Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema’ kwa sababu uovu, kwa ulivyo, haustahiki kuwa wema, wala wema, kwa ulivyo, haustahiki kuwa uovu’

Na aliyetubu na akafanya mema, basi hakika huyo ametubu kwa Mwenyezi Mungu toba ya kweli.

Baada ya kubainisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika Aya iliyotangulia kwamba mwenye kutubia atampa thawabu za mwenye kufanya mema, hapa anamsifu kuwa amerejea kwa Muumba wake kurejea kuzuri.

7.Na wale ambao hawawi kwenye uzushi, na wanapopita kwenye upuzi hupita kwa heshima zao.

Neno ‘hawawi’ limefasiriwa kutokana na neno la kiarabu ‘laa yash-hadu- una’ kama ilivyotumika tafsiri hiyo katika Juz. 2 (2:185). Makusudio ya uzushi ni mambo ya batili na upuzi ni kila lisilo na kheri. Maana ni kuwa waumini hawahudhurii vikao vya ubatilifu wala hawavisaidii, sikwambii kuvifanya. Pia hawashiriki mazungumzo yasiyokuwa na kheri na wanapoyapitia hayo masiko yao huyaepuka; kama wanavyoziepusha ndimi zao kuayatamka; sawa na nyuki anavyopita haraka kwenye mzoga na harufu mbaya.

8.Na wale ambao wanapokumbushwa ishara za Mola wao hawaji- fanyi ni viziwi nazo na vipofu.

Mshairi huwa anasikiliza mashairi kwa umakini kabisa. Vile vile kila mwenye kuhusika na jambo akizungumziwa huwa anakuwa makini nalo sana anapolisikilza. Mtu unapomzungumzia jambo lililo mbali naye atakuepuka na hayo mazungumzo yako, hata kama ni ya uongofu na mwangaza.

Hapa ndipo inabainika siri ya muumini kuikubali Qur’an, na kafiri kuachana nayo. Mumin anakikubali Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa vile anakiamini na kutambua maana yake na makusudio yake. Anakikuta kwenye nafsi yake, itikadi yake, matendo yake mema na malipo aliyomuandalia Mola wake.

Kafiri anakipa mgongo Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa sababu anakipinga na hajui malengo yake na siri yake; wala hapati humo isipokuwa kushutumiwa na kukosolewa itikadi yake na sifa zake na pia makaripio ya ukafiri wake.

9.Na wale ambao wanasema: Mola wetu! Tupe katika wake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wenye takua.

Muovu huwa anatamaani watu wamfuate katika uovu wake, sio kwa kuwa amekinai kuwa yuko kwenye uongofu kutoka kwa Mola wake, hapana! Isipokuwa anataka kupunguza lawama na shutuma na kufunika kosa lake kwa kuwa wengi wakosefu. Lakini hataki mkewe na watoto wake wawe hivyo; kama vile mgonjwa asivyopenda watu wake wapatwe na ugonjwa alio nao.

Ama yule aliye mwema na mwenye takua ana yakini na dini yake na ana busara katika mambo yake. Kwa hivyo huwa anatamaani kwa dhati ya moyo kimsingi na kiitikadi kuwa watu wote wafuate njia yake na kwamba watoto wake wakimuiga yeye huwa anafurahi.

Kwa hiyo wenye ikhlasi humuomba Muumba wao wapate wa kuwaiga, sio kwa kuziba vitendo vyao kwa watu wala kutaka jaha duniani na kuchukua mali kwa kutumia haki za Mwenyezi Mungu; bali ni kwa kujipendekeza mbele ya Mwenyezi Mungu aliye peke yake.

Hao ndio watakaolipwa ghorofa kwa walivyosubiri na watakuta humo maamkuzi na salaam. Watadumu humo kituo na makao mazuri.

Ghorofa ni kinaya cha makao ya juu. Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kubainisha wasifu wa wenye takua na watiifu, sasa anataja malipo yao watakayoyapata kwake, ambayo ni kudumu katika raha, amani na neema pamoja na heshima.

Mwenyezi Mungu amehusisha kutaja subira hapa kuashiria kuwa kila mwenye haki hana budi kupata taabu na udhia kutoka kwa wasio na haki na kwamba thawabu za Mwenyezi Mungu hatazipata ispokuwa mwenye kuwa na uvumilivu na subira na akaendelea kuwa na msimamo kadiri hali itakavyokuwa ngumu.

Sema, Mola wangu asingewajali lau si kupewa kwenu mwito, lakini nyinyi mmewakadhibisha, basi (adhabu) ni lazima.

Makusudio ya neno ‘duakum’ hapa ni kupewa mwito kutokana na maneno yanayovutia, lakini mlikadhibisha. Ni mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu:

فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا لَهُمْ ﴿٥٢﴾

“Basi watawaita nao hawatawaitikia.” Juz. 15 (18:52)

Kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwapa mwito kwenye imani na utiifu kupitia kwa Mtume wake.

Maana ni kuwa nyinyi washirikina hamstahiki hata kutajwa pia lau si kuwa mliitwa kwenye imani na utiifu, ili kuweko na hoja siku ya hisabu na malipo, ikiwa hamtasikia na kuitikia mwito. Nanyi mmeupinga mwito na mkadhibishaji aliyetoa mwito huo, basi adhabu inawastahiki na ni lazima.

Sura Ya Ishirini Na Sita: Surat Shua’rau.

Twabrasiy amesema imeshuka Makka isipokuwa Aya 224 hadi mwisho, zimeshuka Madina. Ina Aya 227

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu.

طسم ﴿١﴾

1. Twaa Siin Miim.

تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿٢﴾

2. Hizo ni Aya za Kitabu kinachobainisha.

لَعَلَّكَ بَاخِعٌ نَّفْسَكَ أَلَّا يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ ﴿٣﴾

3. Huenda ukaiangamiza nafsi yako kwa kuwa hawawi waumini.

إِن نَّشَأْ نُنَزِّلْ عَلَيْهِم مِّنَ السَّمَاءِ آيَةً فَظَلَّتْ أَعْنَاقُهُمْ لَهَا خَاضِعِينَ ﴿٤﴾

4. Tungelipenda tungeliwateremshia kutoka mbinguni ishara zikainyenyekea shingo zao.

وَمَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ مُحْدَثٍ إِلَّا كَانُوا عَنْهُ مُعْرِضِينَ ﴿٥﴾

5. Na hauwajii ukumbusho mpya kutoka kwa Mwingi wa rehema ila hujitenga nao.

فَقَدْ كَذَّبُوا فَسَيَأْتِيهِمْ أَنبَاءُ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٦﴾

6. Kwa hakika wamekadhibisha, kwa hivyo zitakujawafikia habari za yale waliyokuwa wakiyafanyia stihizai.

أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَى الْأَرْضِ كَمْ أَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ ﴿٧﴾

7. Je hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri.

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٨﴾

8. Hakika katika hayo kuna ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٩﴾

9. Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.

HUENDA UKAANGAMIZA NAFSI YAKO

Aya 1-9

MAANA

Twaa Siin Miim.

Umetangulia mfano wake mwanzo wa Sura Baqara, Juz. 1

Hizo ni Aya za Kitabu kinachobainisha.

Hizo ni ishara ya Aya za Sura hii, kitabu ni Qur’an na chenye kubainisha ni kubainisha haki na kudhihirisha.

Huenda ukaiangamiza nafsi yako kwa kuwa hawawi waumini.

Maneno yanaelekezwa kwa Muhammad(s.a.w.w) kwamba asiikere na kuiumiza nafsi yake kwa sababu ya watu wake kuukataa uongofu na haki. Umetangulia mfano wake katika Juz.7 (6:35) na Juz. 15 (18:6).

Tungelipenda tungeliwateremshia kutoka mbinguni ishara zikainyenyekea shingo zao.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamwambia Mtume wake mtukufu: Poa moyo wako! Lau tungelitaka waamini kwa nguvu tungeliteremsha adhabu kutoka mbinguni waione kwa macho na kuwaambia chagueni imani au adhabu; bila shaka wao wangelisalimu amri kwa unyenyekevu.

Lakini je, hii itahisabiwa kuwa ni imani? Hapana! Imani ya kweli inakuwa kwa utashi na hiyari, sio kwa kulazimishwa kwa nguvu. Ndio maana tukawakadiria kheri na shari, tukawaamrisha hili na kuwakataza lile; kisha tukawaachia hiyari, waweze kustahiki thawabu kwa utiifu na adhabu kwa uasi.

Unaweza kuuliza : Mwenyezi Mungu (s.w.t) alifanya hivyo katika zama za Musa(a.s) kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na tulipoinua mlima juu yao kama kwamba ni kiwingu kilichowafunika na wakadhani kuwa utawaangukia. Tukawaambia: shikeni kwa nguvu tuliyowapa.” Juz. 9 (7: 171).

Jibu : kwa hakika Qur’an Tukufu inafahamisha waziwazi kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ana muamala maalum na Mayahudi usiofanana na waja wengine. Kwa sababu wao wana tabia za pekee zisizokuwa na mfano. Tumelizungumzia hilo kwa ufafanuzi zaidi kwa anuani ya ‘Mayahudi hawana mfano’ katika Juz. 1: (2:63-66).

Na hauwajii ukumbusho mpya kutoka kwa Mwingi wa rehema ila hujitenga nao. Kwa hakika wamekadhibisha, kwa hivyo zitakujawafikia habari za yale waliyokuwa wakiyafanyia stihizai.

Tumewaongoza washirikina, kupitia kwako ewe Muhammad, kwenye yale yaliyo na kheri yao na masilahi yao, wakaachana nayo, wakayadharau na kuyafanyia masikhara. Basi nawe achana nao na watakumbana na adhabu waliyoahidiwa tu. Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:68).

Je hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri. Hakika katika hayo kuna ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.

Alikufuru Mungu aliyekufuru huku akiona dalili na ubainifu wa kupatikana kwake na ukuu wake. Miongoni mwa dalili hizi ni kutoa mimea ya aina na rangi mbali mbali. Kwa maelezo zaidi angalia Juz.7 (6:99) na Juz. 13 (13:3).

Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.

Kwa nguvu zake anawashinda mataghuti na rehema zake anawapa muda bila ya kuwaharakishia adhabu mpaka awajie mbashiri na muonyaji na kuwapa fursa ya kufikiria vizuri na kutubia.

Imam Ali(a.s) anasema:“Hasira zake hazimfanyi kuacha huruma yake, wala huruma haimfanyi kupuuza adhabu yake.”

وَإِذْ نَادَىٰ رَبُّكَ مُوسَىٰ أَنِ ائْتِ الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠﴾

10. Na Mola wako alipomwita Musa kwamba nenda kwa watu madhalimu.

قَوْمَ فِرْعَوْنَ أَلَا يَتَّقُونَ ﴿١١﴾

11. Watu wa Firauni. Hawaogopi?

قَالَ رَبِّ إِنِّي أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ ﴿١٢﴾

12. Akasema: Mola wangu! Hakika mimi naogopa watanikadhibisha.

وَيَضِيقُ صَدْرِي وَلَا يَنطَلِقُ لِسَانِي فَأَرْسِلْ إِلَىٰ هَارُونَ ﴿١٣﴾

13. Na kifua changu kinadhikika, na ulimi wangu haukunjuki vyema, basi mtumie ujumbe Harun.

وَلَهُمْ عَلَيَّ ذَنبٌ فَأَخَافُ أَن يَقْتُلُونِ ﴿١٤﴾

14. Nao wanalo kosa juu yangu basi naogopa wasije wakaniua.

قَالَ كَلَّا فَاذْهَبَا بِآيَاتِنَا إِنَّا مَعَكُم مُّسْتَمِعُونَ ﴿١٥﴾

15. Akasema, sivyo kabisa! Nendeni na ishara yetu. Hakika sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza.

فَأْتِيَا فِرْعَوْنَ فَقُولَا إِنَّا رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦﴾

16. Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni wajumbe wa Mola wa walimwengu wote.

أَنْ أَرْسِلْ مَعَنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿١٧﴾

17. Ya kwamba uwaachilie wana wa Israil waende nasi.

قَالَ أَلَمْ نُرَبِّكَ فِينَا وَلِيدًا وَلَبِثْتَ فِينَا مِنْ عُمُرِكَ سِنِينَ ﴿١٨﴾

18. Akasema: Je, hatukukulea utotoni, na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi?

وَفَعَلْتَ فَعْلَتَكَ الَّتِي فَعَلْتَ وَأَنتَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿١٩﴾

19. Na ukatenda kitendo chako ulichokitenda, nawe ukawa miongoni mwa wasio na shukrani?

قَالَ فَعَلْتُهَا إِذًا وَأَنَا مِنَ الضَّالِّينَ ﴿٢٠﴾

20. Akasema: Nililifanya hilo nikiwa miongoni mwa wasioelewa.

فَفَرَرْتُ مِنكُمْ لَمَّا خِفْتُكُمْ فَوَهَبَ لِي رَبِّي حُكْمًا وَجَعَلَنِي مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٢١﴾

21. Basi niliwakimbia nilipowahofia. Na Mola wangu akanitunukia hukumu na akanijaalia niwe miongoni mwa mitume.

وَتِلْكَ نِعْمَةٌ تَمُنُّهَا عَلَيَّ أَنْ عَبَّدتَّ بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿٢٢﴾

22. Na hiyo ndiyo neema ya kunisimbulia na wewe umewatia utumwani wana wa Israil?

MUSA

Aya 10 – 22

MAANA

Aya hizi hadi kufikia Aya ya 28 ni za kisa cha Musa ambacho kimetangulia mara kadhaa. Katika Juz. 16 (20: 9) tumeleza sababu za kukaririka kisa hicho.

Na Mola wako alipomwita, Musa kwamba nenda kwa watu madhal- imu watu wa Firauni.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (20:24).

Hawaogopi?

Hii ni jumla nyingine, maana yake ni kuwa, umefika wakati sasa Firauni na watu wake waogope mwisho wa uovu na utaghuti.

Akasema: Mola wangu! Hakika mimi naogopa watanikadhibisha.

Katika Juz. 16 (20 45) ni: “Ewe Mola wetu! Hakika sisi tunaogopa asije akapindukia mipaka juu yetu au kufanya jeuri.”

Yaani asije akatuwahi kutuadhibu kabla kufikishia ujumbe.

Na kifua changu kinadhikika, na ulimi wangu haukunjuki vyema, basi mtumie ujumbe Harun.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimtuma Musa kupeleka ujumbe wake kwa Firauni. Na hili, kwa upande mmoja, ni jambo zito na lenye mashaka sana, kutokana na utaghuti wa Firauni na nguvu za utawala wake. Na kwa upande mwingine, ujumbe wenyewe ni mzito.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimwambia Mtume wake Muhammad(s.a.w.w) :

إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا ﴿٥﴾

“Hakika sisi tutakuteremshia kauli nzito.” (73:5).

Musa alikuwa ni mwepesi wa kughadhibika kwa ajili ya haki, na ulimi wake ulikuwa na kigugumizi kinachomzuia kutamka. Kwa hiyo akahofia kutotekeleza vizuri ujumbe mkuu. Hakuna yeyote anayehofia kutekeleza haki ya Mwenyezi Mungu kuliko mitume; hasa wale Ulul-a’zm. Hii inatokana na isma. Ndipo Musa akamtaka Mwenyezi Mungu kumtuma Jibril kwa nduguye, Harun, ili awe msaidizi wake katika jambo hili muhimu.

Nao wanalo kosa juu yangu basi naogopa wasije wakaniua.

Anaishiria lile tukio la kumuua mtu wa upande wa Firauni pale alipom- saidia mtu wa upande wake; kama ilivyoelezwa katika Aya hii:

فَوَجَدَ فِيهَا رَجُلَيْنِ يَقْتَتِلَانِ هَـٰذَا مِن شِيعَتِهِ وَهَـٰذَا مِنْ عَدُوِّهِ فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ فَوَكَزَهُ مُوسَىٰ فَقَضَىٰ عَلَيْهِ ﴿١٥﴾

“Na akakuta humo watu wawili wanapigana – mmoja ni katika wenzake na mwingine ni katika maadui zake. Yule aliye katika wenzake akamtaka msaada juu ya adui yake. Musa akampiga ngumi akammaliza.” (28:15).

Musa alihofia kuchukua risala ya Mwenyezi Mungu kwa Firauni asije akamuua kabla kukamilisha lengo, lakini akiwa na nduguye na ikatokewa kuuawa, basi atachukua nafasi yake kuendeleza malengo.

Akasema – Mwenyezi Mungu –sivyo kabisa! Nendeni na ishara yetu, Hakika sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza. Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni wajumbe wa Mola wa walimwengu wote. Ya kwamba uwaachilie wana wa Israil waende nasi.

Musa alihofia dhiki ya kifua, kufungika ulimi na kuuliwa, lakini Mwenyezi Mungu akamhakikishia usalama na akamwambia kuwa hakuna kitu kitaka- chokuwa katika hayo, kwa sababu mimi nitawasaidia na kuwanusuru. Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (20: 46 – 47).

Akasema: Je, hatukukulea utotoni, na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi? Na ukatenda kitendo chako ulichokitenda, nawe ukawa miongoni mwa wasio na shukrani?

Musa na Harun walielekea kwa Firauni, wakaingia kwake wakiwa wamevaa deraya ya sufu, mikononi mwao wakiwa na fimbo. Wakampa mwito wa kumwamini Mungu na kumpa sharti la kusilimu na kutii ili utawala wake ubakie na kudumu enzi yake.

Firauni aliwabeza wawili hawa, waliompa masharti ya kudumu utawala na enzi yake, wakiwa hawana cheo chochote wala mali. Hakutaka kuwaua kwa kuhofia asiambiwe kuwa ameshindwa na hoja akakimbilia upanga.

Lakini Firauni anaweza kuwa na hoja gani? Ni kwa mantiki gani atakayoweza kujadili? Hana kitu isipokuwa kuvungavunga na kumtajia Musa yaliyopita.

Je, hatukukulea na ukakaa nyumbani kwetu miaka, kisha ukatuulia mtu wetu na ukakimbia? Hii ndio shukrani yako? Zaidi ya hayo unadai kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwetu? Unataka tukusikize na kukutii na sisi ndio mabwana zako na wafadhili wa neema zako?

Kisha Firauni akawegeukia watu wa baraza lake na akasema: “Basi mbona hakuvikwa vikukuku vya dhahabu?” (43:53). Kwenye dhahabu tu ndio kuna kuwa na siri ya mantiki ya mataghuti. Hakuna utume wala ubwana au ubora isipokuwa kwa ajili ya dhahabu na dhahabu yenyewe.

Musa (a.s) akamjibu kuhusu kuua akasema: “Nililifanya hilo nikiwa miongoni mwa wasioelewa.”

Yaani sikuelewa kuwa ngumi yangu itamuua. Nami nilikusudia kukinga na kutia adabu, nikakosea makusudio. Basi mimi nina dhambi gani katika hilo? Kukusudia ni nguzo ya msingi ya kosa la jinai kwa watu wa sharia.

Basi niliwakimbia nilipowahofia.

Sikukimbia hukumu ya uadilifu, bali nilikimbia dhulma kwa kuhofia kunichukulia kuwa ni muuaji wa makusudi. Kuna mmoja alimwambia Musa:

إِنَّ الْمَلَأَ يَأْتَمِرُونَ بِكَ لِيَقْتُلُوكَ فَاخْرُجْ إِنِّي لَكَ مِنَ النَّاصِحِينَ ﴿٢٠﴾

“Hakika wakubwa wanashauriana kukuua. Basi toka! Hakika mimi ni katika wanaokupa nasaha.” (28:20).

Na Mola wangu akanitunukia hukumu na akanijaalia niwe miongoni mwa mitume.

Firauni alimtajia Musa ufukara na utoro; Musa naye akamwambia kuwa utukufu haupimwi kwa mali wala kwa ufalme; isipokuwa uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu, humpatia amtakaye katika waja wake. Na mimi Mwenyezi Mungu amenitunukia elimu ya dini yake na sharia yake kwa njia ya kheri na usawa na akanitukuza kwa kunituma kwako na kwa watu wako.

Musa aliendelea kumjibu Firauni, kuhusu malezi na akasema:

Na hiyo ndiyo neema ya kunisimbulia na wewe umewatia utumwani wana wa Israil?

Yaani unanisimbulia kwa malezi yako kwangu na unajitia kutojua kuwa sababu ni uadui wako wa kuwachinja watoto wa kiume wa watu wangu na kuwatia utumwani watoto wao wa kike? Mama yangu alipohofia wewe kunichinja akanitupa baharini na matokeo yake yakawa ni kuishi mimi mbali ugenini bila ya huruma ya mama na mapenzi ya baba? Hii ndiyo fadhila yako kwangu? Firauni alizibwa mdomo, akaanza kuwatafuta wabatilifu wake; kama utakavyoona katika kifungu kifuatacho.

قَالَ فِرْعَوْنُ وَمَا رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٢٣﴾

23. Akasema Firauni: Na ni nani huyo Mola wa walimwengu wote?

قَالَ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ ﴿٢٤﴾

24. Akasema: Ni Mola wa mbingu na ardhi ikiwa nyinyi mna yakini.

قَالَ لِمَنْ حَوْلَهُ أَلَا تَسْتَمِعُونَ ﴿٢٥﴾

25. Akawaambia waliomzunguuka: Je, hamsikii?

قَالَ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ ﴿٢٦﴾

26. Akasema: Ni Mola wenu na Mola wa baba zenu wa kwanza.

قَالَ إِنَّ رَسُولَكُمُ الَّذِي أُرْسِلَ إِلَيْكُمْ لَمَجْنُونٌ ﴿٢٧﴾

27. Akasema: Hakika mtume wenu mliyetumiwa ni mwenda wazimu.

قَالَ رَبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَمَا بَيْنَهُمَا إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٢٨﴾

28. Akasema: Ni Mola wa mashariki na magharibi na viliomo baina yake, ikiwa nyinyi mna akili.

قَالَ لَئِنِ اتَّخَذْتَ إِلَـٰهًا غَيْرِي لَأَجْعَلَنَّكَ مِنَ الْمَسْجُونِينَ ﴿٢٩﴾

29. Akasema: Kama ukimfanya mungu mwingine asiyekuwa mimi basi bila shaka nitakufanya miongoni mwa wafungwa.

قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكَ بِشَيْءٍ مُّبِينٍ ﴿٣٠﴾

30. Akasema: Ijapokuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi?

قَالَ فَأْتِ بِهِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٣١﴾

31. Akasema: Kilete basi kama wewe ni katika wakweli.

فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ ﴿٣٢﴾

32. Akaitupa fimbo, mara ikawa nyoka dhahiri.

وَنَزَعَ يَدَهُ فَإِذَا هِيَ بَيْضَاءُ لِلنَّاظِرِينَ ﴿٣٣﴾

33. Na akautoa mkono wake. Mara ukawa mweupe kwa watazamao.

قَالَ لِلْمَلَإِ حَوْلَهُ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ عَلِيمٌ ﴿٣٤﴾

34. Akasema kuwaambia wakuu waliomzunguka: Hakika huyu ni mchawi, mjuzi.

يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُم بِسِحْرِهِ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ ﴿٣٥﴾

35. Anataka kuwatoa katika ardhi yenu. Basi mnatoa shauri gani?

قَالُوا أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَابْعَثْ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ ﴿٣٦﴾

35. Wakasema: Mwache kidogo yeye na ndugu yake, na uwatume wakusanyao watu mijini.

يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَحَّارٍ عَلِيمٍ ﴿٣٧﴾

37. Wakuletee kila mchawi mkubwa, mjuzi.

MAJIBIZANO BAINA YA MUSA NA FIRAUNI

Aya 23 – 37

MAANA

Akasema Firauni: Na ninani huyo Mola wa walimwengu wote?

Ewe Musa! Wewe unadai kuwa ni Mtume wa Mola wa walimwengu wote; hebu tubainishie jinsi yake na hakika yake huyo Mola?

Akasema: “Ni Mola wa mbingu na ardhi ikiwa nyinyi mna yakini.”

Musa alisema: Mwenyezi Mungu hajulikani isipokuwa kwa sifa zake na athari zake; zikiwa ni pamoja na huku kuumbwa ulimwengu huu wa ajabu katika mpangilio wake na nidhamu yake. Basi fikirini na mzingatie ikiwa mna akili zinazoweza kutambua kuwa nidhamu hii haiwezekani ila kwa uweza wa ujuzi na hekima.

Firauniakawaambia waliomzunguuka: Je, hamsikii?

Yaani mnasikia maajabu hayo. Hatujawahi kusikia haya kwa mababa zetu wa kwanza.

Akasema: Ni Mola wenu na Mola wa baba zenu wa kwanza.

Musa alisema kwa kusisitiza kwamba Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa ulimwengu, muumba wenu na muumba wa baba zenu wa mwanzo na pia ndiye muumba wa huyu Firauni mnayemfanya mungu na kumwabudu.

Akasema: Hakika mtume wenu huyu mliyetumiwa ni mwenda wazimu.

Musa ni mwendawazimu katika mantiki ya Firauni, kwa nini? Kwa sababu amesema Firauni si mungu bali ni kiumbe. Mantiki haya ya kifirauni anayo kila anayedai asichokuwa nacho. Yeyote anayedai kuwa na elimu naye ni mjinga, ikhlasi naye ni mhaini au ukweli naye ni mrongo, basi yeye yuko katika mila ya Firauni na desturi yake. Lau atapata wanaomwamini atasema: Mimi ndiye mola wenu au simjui mungu mwingine kwenu zaidi ya mimi; kama alivyosema Firauni.

Akasema: Ni Mola wa mashariki na magharibi na viliomo baina yake, ikiwa nyinyi mna akili.

Musa aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa kila kitu. Akaashiria kuchomoza jua na kuchwa kwake, ambapo Firauni hawezi kujasiri kusema kuwa yeye ndiye anayelichomoza jua mashariki na kulipeleka magharibi.

Kwa hiyo alipigwa na butwaa aliposikia maneno haya kutoka kwa Musa; sawa na alivyopigwa na butwaa Namrud kabla yake, pale Ibrahim(a.s) alipomnyamazisha kwa kusema:

فَإِنَّ اللَّـهَ يَأْتِي بِالشَّمْسِ مِنَ الْمَشْرِقِ فَأْتِ بِهَا مِنَ الْمَغْرِبِ ﴿٢٥٨﴾

“Hakika Mwenyezi Mungu hulichomoza jua mashariki, basi wewe lichomoze magharibi.”

Juz. 3 (2:258).

Firauni alipoishiwa, alikereka, akawa anatoa vitisho naakasema: Kama ukimfanya mungu mwingine asiyekuwa mimi basi bila shaka nitakufanya miongoni mwa wafungwa.

Jela na kutesa ndio silaha pekee ya utawala muovu wa mabavu dhidi ya haki uadilifu na uhuru, tangu zamani. Lakini jihadi ya wakombozi na ukakamavu wao, unaifanya silaha ya mataghuti ishindwe kwenye shingo zao na vifua vyao; kama ilivyoshindwa silaha ya Firauni.

Walisema wa kale: Mwenye kuchomoa upanga wa dhulma atauliwa nao.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

فَكُلًّا أَخَذْنَا بِذَنبِهِ فَمِنْهُم مَّنْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِ حَاصِبًا وَمِنْهُم مَّنْ أَخَذَتْهُ الصَّيْحَةُ وَمِنْهُم مَّنْ خَسَفْنَا بِهِ الْأَرْضَ ﴿٤٠﴾

“Kila mmoja tulimtesa kwa makosa yake. Kati yao wapo tuliowapelekea kimbunga cha changarawe, na kati yao wapo walionyakuliwa na ukelele na kati yao wapo ambao tuliwadidimiza katika ardhi.” (29:40).

Akasema: Ijapokuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi?” Akasema: Kilete basi kama wewe ni katika wakweli.

Musa hakuogopa vitisho vya Firauni na akamwambia kwa kujiamini kuwa utanifanya mfungwa hata kama ni mwenye haki, kwa kukuletea dalili isiyo na shaka kwako na kwa mwingine?

Atajibu nini Firauni? Je, amwambie ndio nitakufunga hata kama ni mwenye haki? Hawezi kumwambia hivi, kwa sababu itakuwa ni kukubali ukweli kuwa Musa ni Mtume wa Mola wa viumbe wote na kwamba yeye ni mzushi katika madai yake ya uungu. Kwa hiyo ndio akalazimika kusema lete hiyo dalili kama wewe ni mkweli.

Akaitupa fimbo mara ikawa nyoka dhahiri. Na akautoa mkono wake. Mara ukawa mweupe kwa watazamao. Akasema kuwaambia wakuu waliomzunguka: Hakika huyu ni mchawi mjuzi. Anataka kuwatoa katika ardhi yenu. Basi mnatoa shauri gani? Wakasema: Mwache kidogo yeye na ndugu yake, na uwatume wakusanyao watu mijini. Wakuletee kila mchawi mkubwa, mjuzi.

Aya hizi sita zimetangulia katika Juz. 9 (7:107 - 112) zikifanana kiutaratibu, kimpangilio na hata herufi; isipokuwa katika mambo mawili:

Hapa imesemwa: ‘mchawi mkubwa’ na kule ikasemwa ‘mchawi’ hakuna tofauti katika maneno haya isipokuwa kutilia mkazo.

Hapa imesemwa: ‘Akasema kuwaambia wakuu waliomzunguka: Hakika huyu ni mchawi mjuzi,’ na kule imesemwa: ‘Wakasema wakuu wa watu wa Firauni: Hakika huyu ni mchawi mjuzi.’ Tofauti hapa ni kubwa kama inavyojionyesha.

Kwa sababu hapa aliyesema ni Firauni kuwaambia wakuu na kule wakuu ndio waliosema kumwambia Firauni. Sasa je, kuna wajihi gani wa kuunganisha baina ya Aya mbili hizi?

Jibu : Sikupata ishara yoyote ya hilo katika tafsiri nilizonazo, wala sijui sababu yake. Kwa vyovyote iwavyo, jibu ninaloliona ni kuwa Firauni ndiye aliyeanza kuwaambia jamaa zake kuwa huyu ni mchawi; kisha jamaa zake nao wakaanza kuambiana kuwa ni kweli Musa ni mchawi; kama ilivyo kwa wanaoongozwa, wanaigiza kiongozi wao na kutolea ushahidi kauli zake.

Hapo basi hakuna kupingana baina ya Aya mbili. Firauni aliwaambia jamaa zake nao wakamwambia yeye kwa kumwigiza.