• Anza
  • Iliyopita
  • 6 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 16333 / Pakua: 2219
Kiwango Kiwango Kiwango
UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

Mwandishi:
Swahili

UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

KIMEANDIKWA NA: ALLAMAH SAYYID SA'EED AKHTAR RIZVI

KIMETARJUMIWA NA: AL-AKHY SALMAN SHOU

NENO LA MCHAPISHAJI WA KWANZA

TOLEO LA KIINGEREZA

Kitabu hiki kimerudiwa kimechapishwa tena kwa ruhusa ya waandishi, ili kuafikiana na Kongamano la Kilimwengu la Umoja wa Mataifa dhidi ya Ubagazi wa Rangi, (United Nations World Conference against Racism) ambalo lilitege-mewa kufanyika katika jiji la Durban, Afrika ya Kusini, mwezi Augosti, 2001. Mada mbili zilizo pendekezwa kuwepo kwenye agenda zilisababisha migongano ya kimataifa. Agenda hizi zilikuwa: Malipo ya fidia kwa utumwa na biashara yake ambayo ilifanywa na mataifa ya Ulaya na Marekani (U.S.A) hapa Afrika na nyingine ilikuwa kulin-ganisha Uzayuni (Zionism) na ubaguzi wa rangi. Suala la malipo ya fidia kwa Afrika kutoka kwa mataifa yaliyojihu-sisha na utumwa limeachwa kushugulikiwa kwa muda kwa makubaliano baina ya mataifa yanayodaiwa na Afrika, kuweka nguvu na msukumo mkubwa katika kuisaidia Afrika kuendeleza mpango wake wa kurejesha hali nzuri ya uchu-mi. Mpango mmoja wapo unaojulikana sana ni ule wa: Millenium Africa Recovery Plan, ambao unasimamiwa na Rais Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini. Msaada unaozungumziwa hapa bila shaka unaeleweka kwamba ni aina ya ukandamizaji wa kiuchumi kwa kuendeleza utumwa wa kiuchumi hapa Afrika daima milele. Wayahudi wapatao milioni tatu (3) waliuawa wakati wa vita kuu ya Pili ya Dunia - ambapo zaidi ya Waafrika milioni kumi (10) walichukuliwa kuwa watumwa. Malipo ya fidia kwa ajili ya mauaji ya Halaiki ya Wayahudi yanaendelea hadi leo. Msaada wa ruzuku kwa serikali ya Uyahudi (Israeli) kutoka Marekani ambao ulianza kutolewa tangu 1948 sasa umefika kiwango cha dola za Kimarekani billion 18. Utafutaji wa watu watuhumiwa wa "makosa ya kivita" ambao yasemekana ndio walio husika kuwaua Wayahudi tangu 1939 hadi 1943 unaendelea hadi leo. Kwa mara ya kwanza Wayahudi walidai fidia mnamo mwaka wa 1951 kiasi cha dola za Kimarekani bilioni (1.5) moja na nusu. Madai haya yalifanyika miaka sita baada ya kukoma Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Ni takribani miaka 140 tangu kupig-wa marufuku utumwa katika nchi za Magharibi. Makubaliano yalisainiwa na Chansela akiwakilisha Ujerumani mnamo tarehe 10 Septemba, 1952. Je uhai wa Mwafrika hauna thamani ya kutosha ili ulipiwe fidia? Majumba ya makumbusho na makaburi makubwa yanajeng-wa kwa madhumuni ya kuhuisha kumbukumbu ya wale wanaodaiwa "kuuawa kikatili na Manazi wa Kijerumani." Dunia inalazimishwa kutubu dhambi zake dhidi ya Wayahudi, na pamoja na kisingizio hiki bandia, hakuna uha-lali wa hata kidogo unoifanya Israeli kulundika silaha nyin-gi kiasi hicho kisicho linganishwa. Yeshayahou Lebowtz (Israel and Judaism, Jerusalem, 1987) ameandika kwa ufupi: "Israeli si dola yenye kumiliki jeshi, bali ni jeshi lenye kumiliki dola."

UTUMWA MAMBO LEO

Uendelezaji wa wazi wa aina za utumwa unaweza kufaniki-wa kwa njia ya kusaidia Mipango kama vile "Millenium African Recovery Plan." Utandawazi kupitia umiliki wa nguvu za uzalishaji unaofanywa na"Muungano wa Kimataifa wa Wakiritimba" (Multi Ntional Cartels) tayari upo. Mfumo huu hupenya kwenye kila tabaka la uchumi wa dunia, iwe ni bidhaa zinazo zalishwa, kama sukari, silaha za kivita, madawa ya tiba au biashara ya dhahabu na madini ya platinamu. Utumwa wa kiuchumi kupitia udhibiti mkali wa mtiririko wa mitaji ulimwenguni uko imara mikononi mwa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Uharibifu kwa Afrika ulitokea kwa njia ya utawala wa mabavu wa kikoloni wa moja kwa moja, uliofanywa na Uingereza, Udachi, Ufaransa, Ureno na Ubeligiji. Hii ilifu-atiwa na udhibiti wa nje ya Afrika, kwa kuanzisha serikali kidhalimu ili kuendelea kudhibiti kwa njia za hila zaidi. Kwa kufichuliwa vibaraka hawa kwa ajili ya ulimwengu kuwaona, ikawa vigumu zaidi kuendelea kwa uwazi kusaidia vitendo vyao viovu dhidi ya jamaa zao. Vurugu zilidhibitiwa ili kuhakikisha kuendelea uingiaji kwenye hak-iba kubwa za madini. Njia changamano ilikuwepo kazini kwa zaidi ya miaka 30, ambayo ni kulitumbukiza bara hili (la Afrika) kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe visivyo na maana yoyote. Ahadi za "kusamehe madeni" zinatolewa kwa lengo la kuendeleza utumwa kwa Waafrika. Huu "Utumwa Mpya" unaweza kuonekana tofauti kwa nje na ule wa "West African Slave Trade " (Biashara ya utumwa ya Afrika ya Magharibi), lakini misingi yake inafanana. Kwa kuanzishwa kwa mfumo wa makao makuu ya fedha (Benki ya Dunia na shirika la Fedha la Kimaraifa), Polisi wa Dunia (North Atlantic Treaty Organization), imewarahisishia wakoloni kazi ya kuwa na mamlaka ya kuitawala Afrika. Mfano wa wazi unaoonyeshwa na nguvu hizi za wakoloni na washirika wake, ni kuunda taifa la Israeli katikati ya Rasi ya Arabia. Kwa hiyo ni muhimu sisi kuchambua na kuonye-sha ulinganifu huu baina ya Uzayuni (Zionism) na washirika wake na ukubwa na vipimo vya utumwa unaoendelezwa na nguvu za wanyonyaji.

Kwa hiyo, tumeona ni muhimu kukichapisha kitabu hiki, kiitwacho: "Utumwa, kwa Mtazamo wa Kiislamu na Usio wa Kiisilamu", kilichoandikwa na Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (ambacho kilichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1972). Kwa madhumuni ya: Kuwataarifu kwa mara nyingine washiriki kwenye Kongamano hili kuujua uovu halisi wa utumwa ambao umekuwa unaendelea kwa karne tano zilizopita. Kupanua akili za wasomaji na hivyo kutambua jinsi utumwa ulivyogeuzwa na kuwa kama ulivyo sasa katika hali yake ya udanganyifu zaidi, na njama za nchi ya Israeli na Marekani zenye sera za kuuendeleza ili ziweze kutimiza malengo yao ya siri. "Ahlul Bait(a.s) Foundation of South Africa" inaona fahari kuitambulisha kazi hii rasmi yenye thamani na wanayo matumaini kwamba usiri unaogubika akili zetu utaondolewa na kuamsha akili za watu wote wenye msimamo unaostahili. Kwa kweli sisi ni wadeni kwa Muadhama Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (Dar es salaam, Tanzania) na kwa unyenyekevu tunashukuru juhudi zake za miongo michache katika kueneza mafundisho ya Uislamu hapa Afrika. Tabia yake ya kisomi imeonekana kwenye mfululizo wa mada nyingi zilizo chapishwa zikijumuisha maelekezo ya jumla kama vile "Haja ya Dini", hadi kufikia kazi za kisomi kama hii. Bilal Muslim Mission of Tanzania, imefanya kazi kubwa ya kueneza kazi hii na zingine nyingi za maandishi na akawatia moyo Waislamu na wasio Waislamu duniani kote pamoja na Afrika ya Kusini katika kipindi cha zaidi ya miaka 50 iliyopita.

Mwenyezi Mungu amzidishie neema hapa duniani na akhera, na tunamwomba Muweza wa yote amjaalie nafasi kubwa zaidi ya kutunufaisha kwa kutumia kalamu yake, Insha- Allah.

Syed Aftab Haider

Ahlul Bait Foundation of South Africa

August 2001.

NENO LA MCHAPISHAJI TOLEO LA KISWAHILI

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la "Slavery - Islamic & Western Perspectives kilichoandikwa na Mwanachuoni mkubwa Mar hum Allamah Sayyid Sa'eed Akhtar Rizvi. Kitabu hiki kwa ufupi kinaelezea juu ya biashara ya utumwa ilivyokuwa ikiendeshwa na wazungu hapa Afrika, waki-saidiwa na Kanisa Katoloki na Makinisa mengine yaliyofu-atia. Mwandishi kwa kutumia elimu, akili, mantiki na utafi-ti wa kina, amefichua ukweli wote uliokuwa umejificha nyuma ya biashara hii ya udhalilishaji wa binadamu. Hapa Afrika na duniani kote, watu wangali wanaamini kwamba biashara ya utumwa hapa Afrika (hususan Afrika ya Mashariki) ilianzishwa na kuendeshwa na Waraabu waki-ungwa mkono na Uislamu. Kwa hiyo mbele za watu Uislamu ulionekana kama dini isiyojali ubinadamu, iliy-owaswaga mababu zetu kama wanyama na kuwafanya watumwa kwenye nchi zao. Mwandishi anayakanusha yote haya, na kuonyesha jinsi gani Uislamu ulivyokuwa dhidi ya biashara hii ya tumwa, na ulivyofanya ili kukomesha biashara hii. Na kuonyesha jinsi gani Wazungu walivy-oing'ang'ania biashara hii, na jinsi Mapadre na Maaskofu walivyozibariki meli zilizokuwa zimebeba watumwa. Tumeona tukitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ili kizidishe mwanga wa elimu kwa Waislamu (na wasio kuwa Waislamu) wazungumzaji wa Kiswahili, na hili likiwa ndilo lengo kubwa la Taasisi yetu ya 'AFItrah Foundation' kati-ka kuwahudumia Waislamu hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru Ndugu yetu al-Akh Salman Shou kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu, na kuondokana na dhana hii potofu juu ya biashara ya utumwa. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 1017 Dar-es-Salaam Tanzania.

NENO LA MCHAPISHAJI TOLEO LA KISWAHILI

Utumwa ni moja wapo ya maovu ambayo yamekuwepo katika jamii tangu kuwepo kwa mwanadamu hapa duniani na jitihada za wanamageuzi kujaribu kuuzuia zimeshindwa kwa karne nyingi sana. Ustaarabu wa kale haukuweza kuondoa utumwa, kwa hiyo jamii za wakati huo ziliafiki kuwa nao. Baadhi ya jamii hizo za kistaarabu ziliulea utumwa. Makanisa ya Kikristo yalishiriki katika biashara ya utumwa. Mapadri wao walizibariki meli zilizokuwa zin-abeba shehena za binadamu na waliwaonya watumwa kuwa watiifu, lakini hawakuwasihi mabwana wenye kumiliki watumwa kuwa wapole kwa shehena hizo za watu. Hivi karibuni mnamo mwaka 1970 Kanisa Katoliki lilinunua wasichana 1500 kutoka India, eti kwa sababu wasichana wa kizungu huko Ulaya hawakutaka kuishi maisha ya kitawa (usista). Miongoni mwa dini zote ni Uislamu tu ndio ulio-haribu misingi yote ya uovu huu. Lakini, ni kejeli ya histo-ria kwamba watu walio rutubisha utumwa wakasaidia uen-deleaji wake na walifaidika nao, baadaye ndio wakawa mabingwa wa kuukomesha. Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Mhubiri Mkuu wa Bilal Muslim Missioni of Tanzania, amekiandika kitabu hiki kwa uwezo mkubwa na jitihada. Kama ilivyo kwa msomi mtafi-ti kama yeye, ameshuhgulikia mada ya kitabu hiki bila upen-deleo, Ameupanga ukweli baada ya ukweli kutoka kwenye historia; amenukuu kutoka kwenye Qur'ani, hadithi na waandishi wa zama za leo kuhusu somo hili, na ameonyesha sheria za Kiislamu na zile zilizotumika kabla ya Uislamu. Ameonyesha waziwazi kwamba ustaarabu wa Kimagharibi sio bingwa mkubwa kiasi hicho wa kuwaokoa watumwa kama unavyojionyesha. Kwa kweli kitabu hiki kitathibitisha kuwa kifungua macho kwa wale ambao hukubali bila kuchunguza kuhusu propaganda ya ubinadamu wa Kimagharibi. Peermahomed Ebrahim Trust kwa fahari kubwa wanakileta kitabu hiki kwa wasomaji na wana matumaini kitakubaliwa na jamii. Wadhamini, Peermahomed Ebrahim Trust Karachi, Pakistan 15 Jamadi, 1392 27 June, 1972.

UTANGULIZI WA MWANDISHI KWA TOLEO LA PILI

Kitabu hiki kiliandikwa kwa ombi la marehemu Haji Hasanali P. Ebrahim, ambaye ndiye aliye kichapisha kutoka kwa Peermahomed Ebrahim Trust, Karachi, mnamo mwaka 1972. Mara baada ya kuchapishwa, nakala zote zilinunuli-wa, lakini mahitaji yakawa bado yanaendelea. Kwa kukid-hi mahitaji hayo, mwanangu, Hujjatul Islam Sayyid Muhammad Rizvi sasa ametayarisha toleo la pili. Baadhi ya mabadiliko madogo madogo yamefanywa katika mpangilio wa Sura; ibara zimeongezwa hapa na pale; na mwanangu ametayarisha maelezo ya ufafanuzi chini ya kurasa, ambayo yameongeza ubora wa kitaaluma wa kitabu hiki. Mwenyezi Mungu na amrefushie maisha na amwongeze nguvu za kuendelea kuutumikia Uislamu wa kweli kwa uaminifu. Pia ninawashukuru marafiki ambao wamenisaidia kwa namna yoyote ile katika kufanikisha kuchapishwa toleo hili: S.S. A. Rizvi Gopalpur (India) 28 Novemba 1987.

UTUMWA KATIKA ZAMA ZA KALE

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿١٣﴾

"Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na wana-mume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari." (Qur'an 49:13).

Utumwa sio taasisi iliyoanzishwa na Ukristo au Uislamu. Ni Utumwa ulikuwepo kwa muda mrefu hata kabla ya kuanzishwa hizi dini mbili. Kwa mtazamo wa haraka kuhusu utumwa wa kale, ninamnukuu Jaji Ameer Ali: "Shughuli ya Utumwa ina rika moja sawa na kuwepo kwa binadamu. Kihistoria dalili zake zinaonekana katika kila zama na kila taifa... Wayahudi, Wayunani, Warumi na Wajerumani wa kale, watu ambao taasisi zao za kisheria na za kijamii zilizoathiriwa mno na tabia na desturi za kisasa, walizitambua na kuzifanya aina zote za utumwa, utumwa wa kazi za kiuchumi na wa kazi za nyumbani. Baada ya kuanzishwa kwa makundi ya washenzi wa Magharibi na Kaskazini katika mabaki ya dola ya Warumi, zaidi ya utumwa wa mtu binafsi, utumwa wa taifa moja kulifanya taifa lingine kuwa mtumwa, ambao haukujulikana sana kwa Warumi, ukashamiri kwenye nchi zote mpya zilizo kaliwa... kanuni za kishenzi, kama zile za Warumi, ziliona utumwa kama hali ya kawaida ya binadamu; na kama mtumwa alipewa ulinzi, ilikuwa kwa sababu mtumwa alikuwa mali inayo milikiwa na bwana wake, ambaye ni yeye peke yake baada ya nchi, alikuwa na mamlaka juu ya uhai na kifo kwa mtumwa.1 Katika nchi ya Uajemi (Persia) ikulu ya Mfalme ilikuwa na watumwa wanawake elfu kumi na mbili. Wakati Mfalme wa Byzantine anaketi kwenye kiti chake cha enzi, maelfu ya watumwa walikuwa tayari kutoa huduma kamili na mamia ya watumwa waliinama kuonyesha heshima wakati mfalme anainama kuvaa viatu. Huko Ugiriki au Uyunani, idadi ya watumwa ilikuwa kubwa zaidi ya watu walio kuwa huru, licha ya kwamba Ugiriki ilitoa watetezi wakubwa wa ubi-nadamu na haki. Kila jeshi la Kiyunani ambalo lilirudi nyumbani na salamu za ushindi, lilifuatwa na kuindi la watumwa. Aristotle, mwanasalsafa maarufu wa zamani, alipokuwa anazungumzia suala la iwapo kila mtu alikusudi-wa na maumbile kuwa mtumwa au la, anasema: "Hakuna ugumu katika kujibu swali hili, katika misingi yote miwili, ya akili na kweli.

Ya kwamba watu baadhi fulani watawale na wengine watawaliwe si tu kwamba ni jambo muhimu bali ni kitu chenye manufaa kuanzia saa ya kuzaliwa kwao, watu wengine wameumbwa ili wawe watumwa, wako kwa ajili ya kutii tu, na wengine wameumbwa kwa ajili ya kutawala." Halafu anahitimisha; "... watu wengine kwa asili wako huru, na wengine ni watumwa, na kwa utumwa huu (uliotajwa) wa mwisho, wote ni wenye manufaa na haki."2 Katika utawala wa Rumi, utumwa wa kale ulifika kilele chake, lakini Dola ya Kirumi ilipoanza kuanguka, watumwa wengi wakaanza kuwa na hali nzuri kwa kiwango kidogo.

1 Ameer Ali, Spirit of Islam (London: University paper back, 1965), PP. 259-261; pia angalia Will Duratnt, The Story ofa Civilisation, juzuu ya III (New York, 1944), P.397. Aristotle, Politics, Book one, Sura ya 5 (New York: Modern Library, 1943), uk. 58-60.

Lakini uovu wa utumwa ulionekana wazi kabisa. Uovu huu ulishinda ujuzi wa uhalali wa Kiyunani kama ambavyo imeshinda falasfa stadi ya Kigriki. Kuonyesha mapenzi kwa watumwa lilionekana si tendo la hisia za kawaida lakini ilikuwa tabia pekee ya mtu mwenyewe binafsi. Mtumwa hakuonekana kama binadamu, hakuwa na haki, hakuwa na roho.3 Wakati huo wa ujio wa Uislamu (mnamo karne ya 7 CE) utumwa ulikwisha enea kote kote huko India, Ajemi, Rumi, Rasi ya Arabia, Romania na Ugiriki. Watu waliokuwa na hali nzuri na nafasi nzuri na wasomi wa nchi hizi hawakuwatilia maanani watumwa kustahiki kupatiwa hata angalao pia haki za msin-gi za kibinadamu. Mtumwa alikuwa anaonekana kama bid-haa isiyo na thamani zaidi kuliko hata ya ng'ombe.4 Mara nyingi mtumwa aliuzwa kwa bei rahisi kuliko kondoo na mbuzi. Kwenye hafla maalum za kijamii wageni waheshimiwa wa nchi walikuwa na tabia ya kukusanyika pamoja na Kiongozi wa Nchi kutazama michezo ya kupi-gana watu na katika michezo hii watumwa walifanywa wapigane kwa kutumia mapanga na mikuki kama vile maonyesho ya mapigano ya jongoo wawili na kware katika kipindi cha zamani cha jamii ya kikabaila. Watu walis-hangilia kwa kupiga makofi hadi mtu mmoja miongoni mwa wapiganaji aliuawa. Watazamaji walimshangilia sana mshindi.5 Kwa upande mwingine, Rasi ya Arabia ilizunguukwa na nchi ambazo bado zilikuwa na dalili za ufahari wa ustaaraabu wa Kirumi na Kiyunani uliokuwa unaporomoka, 3 Durant, W., op.cit., Juzuu ya III uk. 397, Juzuu IV (New York), uk. 29). 4 Ibid 5 ibid. na kwa upande mwingine, ilizunguukwa na nchi zilizogu-bikwa na imani za dini za "Zoroastria" na "Uhindi." Kama ilivyo tajwa hapo juu, kwenye nchi zote hizi utumwa ni taasisi iliyo tambuliwa. Vibao kumi na mbili vya maandiko (ya sheria zao) vilitoa mhuri wake rasmi kuithibitisha taasisi hii. Ukali usiopungu-ka wa matatizo na ukatili ambao watumwa walifanyiwa, haukupungua, lakini, kwa namna yoyote ile, watumwa sasa walikubaliwa kama wanyama (hayawani) ambao hatima yao ilikuwa ni kufanya kazi na kufa tu kwa manufaa ya hao walio wamiliki. Sina nia ya kukifanya kitabu hiki kuwa his-toria ya unyama waliofanyiwa watumwa lakini itoshe tu kusema kwamba mtu lazima siku zote abebe hatia katika dhamira yake kwamba wakati fulani alijiingiza kwenye uovu wa utumwa.

UKRISTO NA UTUMWA

Ingawaje utumwa ulikuwa taasisi ya kale ambayo ilianza kabla ya historia ya binadamu haijaanza kuandikwa, ni sala-ma kusema kwamba ukubwa wa biashara hii ulifika kilele chake kwa kuendelezwa na mataifa ya Kikristo ya Ulaya na Amerika ambao kama ilivyo kawaida yao, waliigeuza kuwa biashara yenye utaratibu uliopangwa kwa uangalifu sana na wakaanza kuwakamata watumwa kwa maelfu. Kabla hatu-jaanza kutoa maelezo ya biashara hii mbaya sana ya utumwa ambayo ilianzishwa na Wareno, Wahispania na mamlaka zingine za kiubaharia za Kikristo kutoka Magharibi kwa ajili ya makoloni yao mapya, hebu tuangalie kwanza tuone kama Ukristo, kama mfumo na imani, ulifanya lolote wakati wa siku za mwanzo sana kupunguza ukali wa mateso kwa wengi wa watumwa. Jaji Ameer Ali anaandika kuhusu Ukristo: Ukristo uliona utumwa kuwa ni taasisi iliyo tambuliwa na himaya (dola); na wenyewe ukakubali mfumo huu bila ya hata kujaribu kupunguza uovu wake, au kuahidi kukomesha polepole, au kuboresha hadhi ya watumwa. Chini ya sheria ya nchi, watumwa walikuwa kama mali inayo hamishika. Waliendelea kuwa hivyo chini ya utawala wa Kikristo. Utumwa ulishamiri miongoni mwa Warumi tangu zama za kale. Watumwa hao ama wamezaliwa wazalendo au wamezaliwa kutoka nje, ama walipatikana kutokana na ushindi wa vita au kununuliwa, walijulikana kama mali tu ya kuhamishika. Mabwana zao walikuwa na mamlaka na uwezo wa kuamua juu ya uhai au kifo kwao. Ukristo ulishindwa kabisa kukomesha utumwa au kupunguza uovu wake.6 Will Durant anatoa maelezo kuhusu nafasi ya Kanisa kama ifuatavyo. Kanisa halikulaani utumwa. Kanisa la Orthodox na waasi, Kanisa la Rumi na washenzi wote walidhani taasisi hii ilikuwa ya kawaida na haingeharibiwa. Sheria za kipagani zilimwingiza utumwani mwanamke yeyote aliye huru ambaye aliolewa na mtumwa; sheria za Mfalme Constantine (Mfalme Mkristo) ziliamuru mwanamke wa aina hiyo kuuawa kwa kukatwa kichwa, na mtumwa mwanamume kuchomwa moto akiwa bado yu hai. Mfalme Gratian alitoa amri kwamba mtumwa yeyote aliye mshitaki bwana wake kuhusu kosa lolote isipokuwa uhaini dhidi ya serikali, lazima achomwe moto akiwa bado yu hai 6 ameer Ali, op. cit., uk. 260-261 mara moja bila hata kufanya uchunguzi ili kupata uhalali wa shitaka.7

Rekebisho moja tu lililoagizwa na Ukristo linaonekana kati-ka barua ya Mtakatifu Paulo kwa mtu fulani aitwaye Filemoni alipomrudisha mtumwa wake, aliyeitwa Onesimo, na kupendekeza amfanyie wema. Hakuna zaidi ya hapo. Inavutia kuona kwamba neno "slave " ("mtumwa") la asili ya lugha ya Kiebrania limebadilishwa na kuwa "mtumishi wa nyumbani" kwenye toleo la Biblia liitwalo "Authorised Version of the Bible," na likabadilishwa kuwa "mtumwa mtumishi" katika toleo liitwalo "Revised Standard Version," kwa sababu, katika maneno ya "The Concise Bible Commentary," neno hili (yaani mtumwa) limeachwa kutumiwa kwa sababu ya maana yake.8 Mtu hushanga iwapo mtarjumi anayo haki ya kubadilisha asili ya neno kwa sababu tu ya maana zake au ukumbusho wake?" Itavutia kuona hapa kwamba neno "slave" ("mtumwa") ni la asili ya Wazungu. Lilianza kuwapo na kutumika wakati Wajerumani (Franks) walipokuwa wanajishughulisha na kulipatia "Washenzi" soko la watumwa la Wahispania, na mateka hao walio wengi walikuwa Waturuki kutoka jimbo la Slovakia (sasa ni sehemu ya Czecoslovakia). Watu hawa huitwa "Slav" na kwa hiyo mateka wote wakaitwa "slaves." Nukuu ifuatayo inaonyesha dhahiri mtazamo wa Uislamu na Ukristo kuhusu suala la utumwa na rangi ya ngozi: 7.leeky, W.E. History of European Morals, Juzuu ya II ( New Yolk, 1926), kama ilivyonukuliwa na Will Durant, op. cit., juzuu ya IV, uik. 77. 8. Clarke, Rev. W. K. L, The Concise Commentary (London: S.P.C.K, 1952) uk. 976.

"Mwondoshe mtu mweusi! Siwezi kuzungumza naye," alisema Archbishop Mkristo aliyeitwa Cyrus wakati Waarabu walioshinda walipowatuma wawakilishi wao wenye uwezo mkubwa ili wazungumze kuhusu makubaliano ya kusalimu amri mji mkuu wa Misri, ujumbe huu wa wawakilishi hawa uliongozwa na mtu mweusi aliyeitwa Ubaydah kama mtu mwenye uwezo mkubwa sana kuliko wote. Archbishop, alishangaa alipoambiwa kwamba mtu huyo mweusi alipewa ukubwa na maelekezo na Generali Amr, na kwamba Waislamu huwapa watu weusi na weupe heshima na daraja sawa na huwahukumia watu kwa tabia na si kwa rangi.9 Tukio hili linakupa tu maelezo kwa ufupi kile ninachotaka kueleza kwa urefu zaidi katika kitabu hiki.

1

UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

5. Bilal al-Habashi: Bilal al-Habashi (mtu wa Ethiopia) alikuwa muadhini wa kwanza wa Mtume. Baba yake alikuwa Riyah, na mama yake Jumanah, na lakabu yake ni Abu Abdillah na Abu Umar. Alikuwa mmojawapo wa kundi la watu waliosilimu mwanzoni kabisa. Alishiriki katika vita ya Badr, Uhud, Khandaq na zingine.86. 86. Ibn Sa'd, op. cit., j.3:1, uk. 170; Ibn Hajar, op. cit., j. 1, uk. 336.

Bilal alikuwa mtumwa wa kwanza wa Safwan bin Umayyah. Wakati wa utumwa wake, aliteswa kinyama kwa sababu ya imani yake. Aliamuriwa kulala chini kwenye mchanga wa jangwa la Arabia unaounguza akiwa uchi, jiwe zito liliwekwa juu ya kifua chake na kumfanya asipumue kwa urahisi. Na kama vile hiyo haikutosha, watu wane sana walitumia kuruka juu ya jiwe hilo, katika jaribio la kutaka kumuua kwa njia hiyo. Hata hivyo, sauti moja tu ilisikika kutoka kwa Bilal nayo ni (Mungu Mmoja! Mungu Mmoja!) Ahad! Ahad! 87. Mtume alipoona ukatili aliokuwa anafanyiwa Bilal, alisiki-tika sana. Abu Bakr akamnunua na kumwachia huru Bilal. Mnamo mwaka wa 2 A.H. wakati adhana (wito wa kwenda kusali) ilipoamriwa, Bilal alipewa heshima ya kuadhini.88. Baadaye, watu fulani walishauri kwamba heshima hii angepewa mtu mwingine, kwa sababu Bilal hakuweza kutamka herufi ya Kiarabu "shin" kwa lafudhi ya Kiarabu. Mtume akasema; "Hii 'sin' ya Bilal ni 'shin' inayosikika kwa Mungu." Mwenyezi Mungu hatazami umbile lilivyo, Yeye hupendezwa na utakatifu wa moyo. Wakati mmoja Bilal alikwenda kwa Mtukufu Mtume na akakariri beti ya shairi kwa lugha yake akimsifu Mtume. Mtume akamtaka Hassan bin Thabit al-Ansari kutafsiri katika lugha ya Kiarabu. Hassan akasema: "Tabia bora zinapoelezwa nchini kwetu, Wewe unaonekana kuwa kigezo chetu." 87. Ibn Sa'd, op. cit., j. 166; Abu Na'im, op. cit., j. 1, uk. 336. 88. Ibid, uk. 167.

Ni ukweli unaojulikana sana kwamba Mtume alikuwa na tabia ya ucheshi inayopendeza licha ya kwamba hata kwenye misemo ya uchekeshaji alikuwa mkweli. Siku moja bimkubwa mmoja hapo Madina alimwomba amwombee kwa Mwenyezi Mungu ampatie sehemu ya makazi huko Peponi. Mtume akasema; "Wanawake wazee (vikongwe) hawataingia Peponi." Bi kizee huyo aliondoka akiwa ana-lia. Bilal akamwona na akamuuliza kwa nini alikuwa ana-lia. Bimkubwa huyo akasimulia mkasa wote. Bilal akaenda naye kwa Mtume, na akasema: "Mwanamke huyu ames-imulia hivi na hivi kutoka kwako?" Mtume akasema: "Hata watu weusi hawataingia Peponi." Sasa hata Bilal akaanza kulia. Halafu Abbas, mjomba wake Mtume akafika hapo na alipoelewa kuhusu mkasa huo, akajaribu kuingilia kati kwa kuzungumza na Mtume, ambaye alimwambia kwamba hata mzee mwanamume hataingia peponi. Abbas naye alipoju-muika katika kundi la wenye kulia, Mtume akawaambia wawe na furaha kwa sababu Mwenyezi Mungu atawaumba kuwa vijana tena na wenye nyuso zinazo ng'ara na halafu wataingia peponi. 89. Bilal alikuwa mpenzi wa Ahlul Bayt. Imamu Jafar al-Sadiq amenukuliwa kusema: "Mungu na amneemeshe Bilal! Alitupenda sisi, watu wa Nyumba ya Mtume, na alikuwa mchaji Mungu bora sana miongoni mwa waja wake Mwenyezi Mungu." Imeandikwa katika Kamil Bahai kwamba Bilal hakuadhini au kukimu sala wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr,90. na haku-toa kiapo cha utii kwa Abu Bakr kama Khalifa. Shaykh Abu 89. al-Majilisi, Hayatu'l-Qulub, uk. 129-130; Biihar, j. 16, uk. 295. 90. Shustari, Nurullah, Majalisu'l-Mu'minin (Tehran, 1268 AH.) uk. 54; na vile vile angalia Ibn Sa'd, op. cit., j. 3:1, uk. 169

Jafar al-Tusi amesimulia kwenye Ikhtiyar al-Rijal taarifa isemayo kwamba Bilal alikataa kutoa kiapo cha utii kwa Abu Bakr; na Umari alikamata vazi lake lililotengenezwa kwa ngozi na akasema: "Hii ni zawadi ya Abu Bakr; alikuachia huru na sasa unakataa kutoa kiapo cha utii kwake?" Bilal akasema: "Kama Abu Bakr alinikomboa kwenye utumwa kwa ajili ya radhi ya Mwenyezi Mungu, basi na aniachie niendelee na kumcha Mwenyezi Mungu; na kama aliniachia huru kwa sababu ya kumtumikia yeye, basi nipo tayari kumpatia huduma zihitajikazo. Lakini sitatoa kiapo cha utii kwa mtu ambaye Mjumbe wa Mungu hakum-teua kuwa Khalifa wake." Umari akamkaripia sana akasema: "Hutakiwi kuwa na sisi hapa." Hii ndio sababu baada ya kutawafu Mtume, Bilal akahamia Syria. Baadhi ya mashairi yake kuhusu mada hii ni kama ifu- atavyo: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu! Sikumgeukia Abu Bakr, Kama Mwenyezi Mungu hangenilinda, fisi wangesimama miguuni mwangu.

Mwenyezi Mungu amenipa wema na Ameniheshimu, Hakika kuna wema mwingi sana kwa Mwenyezi Mungu. Hutaniona nina mfuata mtu wa bidaa, Kwa sababu mimi siendekezi bidaa kama wao." Mwandishi wa Istiab anaandika, "Alipo tawafu Mtume, Bilal alitaka kwenda Syria. Abu Bakr akamwambia abaki Madina ili amtumikie yeye (binafsi). Bilal akasema: "Kama umenipa uhuru kwa ajili ya kukutumikia wewe, basi nikamate niwe mateka tena; lakini kama uliniondoa kwenye utumwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi niache niende katika njia ya Mwenyezi Mungu." Abu Bakr akamwacha aendelee na mipango yake."

91. Bilal alifariki dunia huko Dameski kwa ugonjwa wa tauni mnamo mwaka wa 18 A.H. au 20 A.H. na akazikwa huko Bab Saghir.92. Kaburi lake huko Dameski hutembelewa na maelfu ya Waisilamu waaminifu kila mwaka.

6. FIZZAH

Fizzah al-Nubiyyah (kutoka Nuba, sasa iko ndani ya nchi ya Sudan) pia amepata sifa njema ya milele kwa ajili ya kuji-tolea kwake katika Uislamu na kuwapenda Ahlul Bayt. Mwanzoni, alimtumikia Fatimah, binti yake Mtume. Ilipangwa na Mtume kwamba siku moja Fatimah angefanya kazi za ndani wakati Fizzah angepumzika, na siku iliyofua-ta Fizzah afanye kazi ambapo Fatima naye anapumzika. Baada ya kifo cha Fatimah, Ali akamuoza Fizzah kwa Abu Thalabah al-Habashi. Akazaa naye mtoto wa kiume, na halafu Abu Thalabah akafariki dunia. Baadaye Fizzah akaolewa na Malik al-Ghatathan. Siku moja Malik akalalamika kwa Umari kuhusu Fizzah. Umari akasema; "Unywele ambao chimbuko lake ni familia ya Abu Talib unayo elimu zaidi kuliko Adi."93. (Adi lilikuwa kabila la Umari) 91.Shushtari, op. cit., j. 1, uk. 150. 92. Shushtari, op. cit., uk. 54; vile vile tazama Ibn Sa'd, 0p. cit., j.3:1, uk. 170; Ibn Hajar, op. cit., j. 1, uk. 336-337. 93. Shubar, S. 'Abdullah, Masabihul Anwar, j. 2 (Najaf: Matba'ah al-'Ilmiyyah, 1952/1371) uk. 425-6 akinukuu Manaqib ya Ibn Shahr Ashub.

Fizzah alikuza familia yake mwenyewe; lakini aliendelea kuwapenda Ahlul Bayt. Yeye, kwa hiyari yake mwenyewe, alikwenda na Husein hadi Karbala naye akapata masum-buko makali na mateso yaliyo wapata familia ya Imamu Husein. Elimu yake ya Kitabu Kitukufu, cha Qur'an, anasifiwa kati-ka dunia ya Kiisilamu. Imetaarifiwa kwamba angalau kwa miaka yake ishirini ya mwisho wa uhai wake, hakutamka neno lingine lolote isipokuwa Qur'an; na kila mara alizungumza kwa kukariri aya za Qur'an. Kipande kimoja cha kuvutia cha mazungumzo kinanukuliwa hapa kwa lengo la kuonyesha ujuzi wake wa pekee. Abul Qasim al-Qushayri anamnukuu mtu wa kuaminika kwamba wakati mmoja aliachwa nyuma na msafara wake na akawa anasafiri peke yake. Katika jangwa, alimwona mwanamke na akamuuliza yeye alikuwa nani. Mwanamke akakariri aya ya Qur'an:

"Basi wasamehe na uwaambie (maneno ya) Amani: Hivi karibuni watajua ." (43:89)

Akagundua kosa lake, na halafu akauliza: Unafanya nini hapa?" Mwanamke:

"Na wale ambao Mungu huwaongoza hakuna atakaye wapotosha ." (39:37)

Mwanamume: "Wewe ni jini au mwanadamu?" Mwanamke:

يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ ﴿٣١﴾

"Enyi wana wa Adamu! Vaeni mavazi yenu mazuri kila wakati wa sala na mahali pa sala." (7: 31)

Mwanamume: "Unatoka wapi?" Mwanamke: "Hao wanaitwa na hali ya kuwa wako mbali kabisa " (41:44)

Mwanamume: "Unakwenda wapi?" Mwanamke:

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ﴿٩٧﴾

"Na Mwenyezi Mungu, amewajibishia watu wafanye Hija katika Nyumba hiyo, kwa wale wenye uwezo wa kugharamia safari." (3:97)

Mwanamume:

وَلَقَدْ خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ﴿٣٨﴾

"Siku ngapi zimepita tangu uachwe na msa-fara?" Mwanamke: "Na kwa hakika tuliumba mbingu na dunia na vyote viliv yomo ndani humo kwa muda wa siku sita." (50:38)

Mwanamume: "Unataka chakula?" Mwanamke: "Wala hakuwapa wao miili ambayo haikuhitaji chakula ." (21:8)

Hivyo mwanamume akampa mwanamke huyo chakula. Baada ya hapo mwanamume akamwambia mwanamke akimbie haraka. Mwanamke akasema: "Mungu haibebeshi nafsi yoyote mzigo isiyoweza kuubeba ." (2:286)

Hivyo mwanamume akamwambia mwanamke aketi kwenye ngamia nyuma yake. Lilikuwa jibu lililotoka kwa mwanamke huyo:

لَوْ كَانَ فِيهِمَا آلِهَةٌ إِلَّا اللَّـهُ لَفَسَدَتَا ﴿٢٢﴾

"Lau wangeli kuwamo humo miungu wengine isipo kuwa Mwenyezi Mungu basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingeli fisidika. (21:22).

Aliposikia hivi alishuka chini kutoka kwenye ngamia na akamwomba mwanamke apande juu ya ngamia, na amwen-deshe yeye. Alipoketi juu ya ngamia, mwanamke huyo akakariri aya hii:

سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَـٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ ﴿١٣﴾

"Utukufu uwe kwake Yeye ambaye amemtiisha kiumbe huyu ili tumtumie, kwani hatungeweza kusafiri mwendo mrefu sisi wenyewe." (43:13)

Baada ya muda si mrefu, wakaungana na msafara. Mwanamume akamuuliza mwanamke kama alikuwa na ndugu miongoni mwa wasafiri kwenye msafara huo. Mwanamke akasema: "Ewe Dawud! Hakika tumekufanya wewe uwe khalifa hapa duniani; Muhammad ni Mtume tu; Ewe Yahya kishike kitabu kwa nguvu zote; Ewe Musa, Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi!" (38:26, 3:144, 19:21, 20:11-12.) Mwanamke akaita majina haya, na akawaona vijana wanne wanakimbia kuelekea kwake. Hapo hapo akamuuliza mwanamke huyo uhusiano wake na vijana hao.

Mwanamke huyo alisoma ay a hii: "Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia hii ." (18:46)

Wakati huo watoto hao wakafika hapo; mama akawaambia watoto wake: "Ewe baba yangu! Muajiri huyu. Hakika mbora wa kumua-jiri ni mwenye nguvu na mwaminifu ." (28:26).

Watoto wa mama huyo wakampa mwanamume aliyekuja hapo na mama yao ujira kwa ajili ya usumbufu na huduma. Lakini mama wa watoto hao akaona ujira huo ulikuwa mdogo, kwa hiyo akasema:

"Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye ." (2:261).

Kwa hiyo, wanawe wakaongeza ujira wa mwanamume. (Upo uwezekano mkubwa sana kwamba watoto hawa wa kiume baba yao ni mume wa pili wa Fizzah, Malik al- Ghatathani.) Mwanamume huyo akawauliza watoto hao wa kiume mama huyo alikuwa nani. Wakamwambia kwamba alikuwa Fizah, mtumishi wa Fatimah, binti yake Mtume na kwamba tangu miaka ishirini iliyopita alikuwa hajasema neno lolo isipokuwa Qur'an 94. 7. Qambar: Mara nyingi jina la Qambar limetajwa kwenye hadithi. Na amepewa sifa za daima na beti za shairi lifuatalo la Imamu Ali: "Nilipoona jambo ambalo ni kinyume cha sheria, Niliwasha moto na kumwita Qambar.

Mtu mmoja alimuuliza Qambar bwana wake alikuwa nani. Qambar alielezea sifa za Imamu Ali bin Abi Talib kwa namna ya dhahiri na ya kupendeza hivyo kwamba lime-nakiliwa na muhadithin bila kubadili hata kidogo.95. Kwa sababu haki haiwezi kutendeka kwayo katika kulitafsiri, ninaiacha hotuba hiyo. Nimekwisha sema jinsi Qambar alivyokuwa anatendewa wema kwa mapenzi na Imamu Ali. Baada ya kifo cha Imamu, Qambar alikuwa na desturi ya kusimulia kwamba alikuwa ana mtumikia bwana wake mara chache sana kwa sababu Imamu Ali alikuwa akifanya kazi zake yeye mwenyewe; alikuwa anachota maji kwa ajili ya matumizi ya kila siku, alikuwa anafua nguo zake mwenyewe, alikuwa hata anashona nguo zake mwenyewe wakati ihitajikapo; alikuwa anachota maji kisimani yeye 94. Majilisi, Bihar,)A3 (Beirut, 1983/1403) uk. 86-7; Ibn Shahr Ashub, Manaqib Aal Abi Talib, j. 4 (Bombay, 1313 AH.) uk. 15 95.Kashshi, Rijal kama ilvyonukuliwa na Qummi, op. cit., j. 1, uk. 153 mwenyewe kwa matumizi yake ya kila siku; alikuwa anawalisha chakula kizuri na nguo nzuri lakini yeye mwenyewe alikuwa anavaa na kula kama mtu fukara. Mara nyingi alitumia usemi wa: "jihisi upo nyumbani mtoto." Qambar alikuwa na desturi ya kusema: "Ni katika siku moja tu alinikasirikia. Ilikuwa wakati nilipomwonyesha fedha nilizoziweka kama akiba yangu ya matumizi ya baadaye. Fedha hiyo ilikuwa mafungu ya kipato nilichopewa na watu wengine na zawadi nilizopewa na watu wa familia yake. Nilikuwa nimekusanya dinari mia moja. Nilipo mwonyesha kiasi hicho cha fedha, alionekana kukasirika, na kilicho niu-miza mimi zaidi, Ali alionekana na huzuni." Qambar aka-muuliza kwa nini alikuwa na huzuni hivyo. Ali akajibu, 'Qambar, kama ulikuwa huna utumizi na fedha, je, hakuna watu jirani yako ambao wana hitaji fedha? Baadhi yao pengine wanakufa njaa, wengine pengine ni wagonjwa na walio dhaifu. Je, usingeweza kuwasaidia (kwa fedha hiyo?). Sikufikiria kama ungekuwa huna huruma kiasi hicho na unapenda utajiri kwa ajili ya kuwa tajiri. Qambar nina hofu hufanyi jitihada ya kujaribu kupata faida kutoka kwenye Uislamu; jaribu sana kwa dhamira hasa na kwa moyo safi. Ziondoe sarafu hizo nyumbani mwangu." Qambar akagawa fedha hizo kwa masikini haraka sana na kwa wahitaji, Qambar alikwisha achwa huru na Imamu Ali, lakini aliamua kuendelea kubaki naye.

Hajjaj bin Yusuf al-Thaqafi, gavana aliyeteuliwa na Abdul Malik bin Marwan kutawala Iraq, alikuwa katili aliyekuwa na tabia ya kujivuna kwamba, "Kitu kitamu kuliko vyote hapa duniani ninacho kitamani ni kuua." Jina lake limekuwa methali kwenye uovu. Aliua watu 120,000 ambao kosa lao lilikuwa kumpenda Ali bin Abi Talib na Ahlu Bayt. Idadi hii haijumuishi wale watu walio uawa na yeye kwenye vita. Alijaribu sana kuwamaliza Shia wa Ali kutoka Iraq. Said bin Jubayr na Kumayl bin Ziyad ni waathirika wake wawili. Wakati fulani Hajjaj aliuliza, "Yupo aliye bakia miongoni mwa wafuasi wa Abu Turab (yaani Ali) ili niweze kumrid-hisha Mwenyezi Mungu kwa kumuua?" Akajibiwa kwa kuambiwa kwamba alikuwepo Qambar, mtumwa wake. Hivyo Qambar, aliye mtu mzee sana, alikamatwa na akafik- ishwa kwake. Halafu mazungumzo yalikuwa kama ifu- atavyo baina ya Hajjaj na Qambar: Hajja: "Wewe ni mtumwa wa Ali?" Qambar: "Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi na Ali ni mfadhili wangu." Hajjaj: "Kazi yako ilikuwa nini ulipokuwa unamtumikia Ali." Qambar: "Kazi yangu ilikuwa kumpa maji ya kutawadha ili apate udhu." Hajjaj: "Ali alikuwa akikariri nini baada ya kutawadha?" Qambar: "Ali alikuwa na tabia ya kukariri aya hii: "Basi walipo sahau walio kumbushwa, tuliwafungulia milango ya kila kitu. Mpaka walipo furahia yale waliyo pewa tuli- washika kwa ghafla, na mara wakawa wenye kukata tamaa." (6:44) Hajjaj: "Nadhani ni sisi alio maanisha kujumuishwa kwenye aya hii?" Qambar: "Ndio."

Hajjaj: "Ni vema uache dini ya Ali." Qambar: "Kabla sijaacha dini hii, niambieni dini gani ni nzuri zaidi kuliko yake." Hajjaj: "Utafanya nini kama nikikukata kichwa chako?" Qambar: "Basi itakuwa ni bahati njema kwangu na bahati mbaya kwako." Kwenye hadithi nyingine swali hili la mwisho na jibu lake limenukuliwa tofatui. Hajjaj: "Hakika nina taka kukuua. Ni vema uchague namna yako mwenyewe ya kufa." Qambar: "Ni juu yako. Niue kwa namna yoyote unayota-ka, kwa sababu nitakuua kwa njia hiyo hiyo Siku ya Hukumu. Na, ni jambo la ukweli kwamba bwana wangu alikwisha niambia kwamba ungeniua kwa kunikata kichwa." Hajjaj akaamuru akatwe kichwa Qambar aliuawa kifo cha kishahidi kwa ajili ya imani yake. Leo hii kaburi lake huko Baghdad ni mahali panapotembelewa na maelfu ya mahuja-96. 8. Said: Said, mtumwa mwingine wa Ali bin Abi Talib, anasema kwamba ilikuwa siku moja ya joto kali, Ali alikuwa na shughuli ya kuandika barua. Akataka kumtuma Said aende kuwaita baadhi ya maofisa wake. Akamwita mara ya kwan-za, pili, tatu, na kila mara alipoitwa Said alinyamaza kimya kwa kukusudia. 96. Abu Na'im, op. cit., j. 1, uk. 153; Ibn Hajar, op. cit., j. 3, uk. 514. Imamu alisimama mwenyewe na akamuona Said amekaa mahali ambapo si mbali na alipokaa. Akamuuliza kwa nini haitiki wito wake. Saidi akajibu, "Bwana, nilitaka kujua ni mahali gani, wakati gani na kwa jinsi gani ungeweza kukasirika." Ali akatabasamu na akamwambia Said kwamba hangeweza kuamsha hisia za kukasirisha na hivyo kumkasirisha kwa kutumia hila hizo za kitoto. Imamu Ali akamwachia huru, lakini akaendelea kumsaidia hadi kifo chake. 9. Watumwa: Wasaidizi wa Imani. Kama ambavyo Mtume wa Uislamu alileta ujumbe wa undugu ulimwengu mzima, ilikuwa ni dhahiri kwamba ujumbe huu wa kuikomboa roho ya mwanadamu unge-wavutia na kuwapendezesha watu wa mataifa yote na imani; lakini hususan yale makundi yenye kuonewa na kudhulumi-wa. Ilikuwa kawaida kwamba sehemu kubwa zaidi ya wafuasi wake wa mwanzo ilikuwa ya watumwa. Wapinzani walihofu; katika hali ya kukata tamaa, wakaanza kuwatesa watu walioingia kwenye Uislamu mwanzoni. Zaidi ya hayo majina ambayo maelezo yake yamekwisha tolewa hapo juu, yafuatayo ni majina yanayohitaji kuangali-wa kwa makini. Suhayb bin Sinan wa Roma alikuwa mtumwa aliyesilimu na kuwa Mwisilamu wakati wa siku za mwanzo wa Uislamu. Mtu huyu alikuwa mfua chuma stadi, akiten-geneza deraya na panga. Kwa hiyo, alikusanya akiba kubwa ya fedha. Baada ya kuwa Mwisilamu, pia alikutana na mateso ya kikatili aliyofanyiwa na makafiri.97. 97.Ibn Hajar, op. cit., j. 3, uk. 514 Alipotaka kuhamia Madina, makafiri wakamkamata na wakamnyang'anya fedha yake yote. Kwa hiyo, alifika Madina akiwa fukara. Umari, Khalifa wa pili, alimpa dhamana ya kuongoza sala ya jamaa, baada ya kifo chake hadi hapo Khalifa mwingine atakapochaguliwa. - Khabbab bin al-Arrat - alikuwa sahaba maarufu wa Mtume. Alikuwa mtu wa sita k ukubali Uislamu. Alitoka bara la Afrika; na akateswa kwa sababu ya ukweli. 9

Alikuwa miongoni mwa wale walioitwa "Shia (wafuasi wenye ari) wa Ali." Mtoto wake wa kiume, Abdullah pamo-ja na watu wote wa familia yake, waliuawa kishahidi na Makhariji mwaka wa 40 A.H. 100 Kujitolea mhanga kukubwa kabisa kw ajili ya Uislamu kuli-fanyika huko Karbala mnamo mwaka wa 61 A.H. kuliko-fanywa na Imamu Husein na masahaba wake. Kundi la roho 120-lilikabiliana na jeshi la Yazid bin Muawiyah (wapi-ganaji wasiopungua 30,000.) Ni jambo la kuzingatia kwam-ba kwenye kundi hilo la waumini 120, takriban watu 16 walikuwa watumwa au watumwa walioachiwa huru. Walikuwa kama ifuatavyo: Shawadhab - Mwafrika aliyekufa kishahidi, alikuwa mmoja wapo wa wasomi walio heshimiwa sana wa sheria za Kiisilamu na hadithi. Watu walikuwa na kawaida ya kusafiri kutoka mbali kumsikiliza yeye. 1 98. Ibn Sa'd, op. cit., j. 3:1, uk.161-4; Ibn Hajar, op. cit., j. 3, uk. 516. 99. Ibn Sa'd, op. cit., j. 3:1, uk. 116-7; Abu Na'im, op. cit., j. 1, uk. 144. 100. Ibn Sa'd, op. cit., j. 3:1, uk. 21; Ibn Hajar, op. cit., j. 4, uk. 739. 101. Qummi, op. cit., j. I, uk. 266. Aliposikia taabu ya Husein, Shawadhab na bwana wake wa zamani (na sasa ni sabaha) Abis Shakiri waliungana pamoja na wakaingia kwenye uwanja wa vita wa Karbala na wakafia humo. Jonh (Yahya) bin Huwai, - Wa kutoka Ethiopia, inawezekana alisilimu kutoka dini ya Kikristo kama jina lake linavyoonyesha. Alikuwa mtumwa wa Abu Dharr al-Ghifari, sahaba maarufu wa Mtume. Baada ya kifo cha Abu Dharr, aliambatana na Ahlul Bayt ambao walikuwa wanamwangalia. Akafuatana na Imamu Husein huko Karbala, na mbali ya kwamba kwa wakati huo alikuwa mtu mzee, alijaribu kwenda kuingia kwenye uwanja wa vita kupigana. Imam Hussein kwanza alikata; lakini John aling'ang'ania na mwishowe Imam alimruhusu kwenda kwenye uwanja wa mapambano. Alipoanguka Imamu Husein alikwenda kwenye maiti yake, akaweka paji la uso wake kwenye mapaja yake, na akamwomba Mungu ang'ar-ishe uso wa John. Watu wa kabila la Asad walipofika hapo baada ya siku tatu kuwazika mashahidi, walishangaa kuona maiti iliyokuwa inang'aa kwa nuru ya peponi na kufunikwa na mafuta mazuri ya peponi. Hii ilikuwa maiti ya John.

Salim, Zahir bin Amr, Qarib bin Abdullah Du Ali, Mumjih bin Sahm, Sa'd bin Harth, Nasr bin Abi Naizar, Aslam bin Amr na Sulayman walikuwa miongoni mwa waathirika wa "shambulio la kwanza" jaribio lililofanywa na kikosi cha Yazid kukimaliza kikundi kidogo cha Imamu Husein kwa kuwazidi nguvu kwa uwingi, uwezo, uwepesi na masham-bulizi ya kushtua. Jeshi la Yazid lilishindwa katika jaribio lake la kwanza kwa sababu ya ubora wa mbinu za kundi la Husein na utii kamili kwake. Kikosi cha Yazid kilirudi nyuma, na kuacha nyuma, wapiganaji wengi waliouawa. Lakini ushindi huu wa wafuasi wa Imamu Husein uli-patikana kwa gharama kubwa. Masahaba wa Imam Hussein walikuwa wamelala katika uwanja wa mapambano, mion-goni mwao wakiwemo mashahidi sita waliotajwa hapo juu ambao walikuwa watumwa. Pia palikuwepo na watumwa wengine sita waliokufa kishahidi hapo Karbala. Majina yao ni: Harith bin Nabhan, Said, Nafi, Salim, Shabib na Wadih. Maelezo pia yanapatikana kwenye historia za mtumwa wa Kituruki wa Imamu Zaynul Abidin ambaye alipigana na jeshi la Yazid na akajitoa mhanga kwa ajili ya Uislamu. 102.

Aqabah bin Saman, - pia ni mtumwa, alikuwa miongoni mwa masahaba walioaminiwa sana wa Imamu Husein. Imamu alimwachia sahaba huyu nyaraka zake muhimu zote azitunze yeye. Kwa istilahi ya kisasa, tunaweza kusema kwamba alikuwa katibu wa Imamu Husein. Sahaba huyu alijeruhiwa kwenye uwanja wa vita wa Karbala na akatekwa na kuwa mfungwa wa kivita pamoja na familia ya Imamu Husein. Akiwa mmoja wapo wa mashahidi walioona kwa macho wenyewe mauaji ya halaiki ya watu huko Karbala, maandiko ya Aqabah bin Samem ni chanzo muhimu sana cha historia. Bin Jarir al-Tabari, mwanahistoria maarufu Mwisilamu, ameandika maelezo ya Aqabah kwenye kitabu chake kiitwacho Tarikh al-umam wa al-muluk. Orodha hiyo ya matukio ilitenganishwa kutoka kwenye orodha ya matukio ya al-Tabari na kuchapishwa huko India pamoja na maelezo kutoka kwa marhum Mujtaba Husein Kamunpuri wa Aligarh Muslim University. 102. Kwa maelezo zaidi juu ya Imamu Husein na Karbala, tazama Rizvi, S.M., Imam Husayn, the Saviour of Islam, (Vancouver: 1984). Waisilamu wakati wote wamekuwa na fahari kwa mihanga ilyotolewa na mashahidi wa Karbala kwa ajili ya Uislamu. Dhuria wa Imamu Husein wakati wote wamekuwa wana wapa salaam mashahidi hao, wakati mwingine wanawataja mmoja baada ya mwingine, wakati mwingine wanawataja kwa pamoja. Shia Ithna Asharia, wakiongozwa na Maimamu wao, kila mara huwapa salaamu mashahidi hawa kwa tamko lifuatalo, Karibuni siku zote:- Salaamu kwenu, Enyi watakatifu wa Allah na mlio wapendwa wake; Salaamu kwenu, Enyi wateule wa Allah na wapenzi wake;

Salaamu kwenu, Enyi wasaidizi wa Dini (imani) Wazazi wangu nawafidie maisha kwa ajili yenu, Mlio tohara na safi, na imekuwa tohara na safi ardhi mliyozikiwa; kwa hakika mumepata mafanikio (ushindi) makubwa kabisa; Ningependa kwa Mwenyezi Mungu kwamba ningekuwa pamoja nanyi katika kushiriki mafanikio hayo. 103. 10. Watoto wa watumwa: Maimamu na Makhalifa Tangu ujilio wake hadi kipindi cha ukoo wa Umayya, Uislamu uli-pata ushindi wa kiwango cha mafanikio katika vita yake ya wema dhidi ya utumwa. Watumwa hawakuwa tena binadamu wa daraja la kudharauliwa kama wanyama, bali walikuwa watu wanaume na wanawake wenye hadhi na hes-hima. Watumwa wengi walioachiwa na kuwa huru, wali-weza kupata kazi za juu na kupata vyeo vikubwa. Dhuria wa Mtume na wafuasi wao waliendeleza msimamo wa Kiisilamu kwa utumwa. Maimamu kadhaa walioa wanawake watumwa ambao baadaye wakawa mama wa Maimamu. 103. Qummi, Mafatihu'l-Jinan ( Tehran, n.d.) uk. 427. Madhehebu ya Kaysaniyyah yaliamini Muhammad al-Hanafiyyah (mtoto wa Imamu Ali) kuwa ndivyo Imamu baada ya Imamu Husein. Mama yake Muhammad al-Hanafiyyah, Khawla bint Jafar bin Qays alikuwa mateka ambaye Ali alimuoa. Lakini hapana mtu alitoa ushauri kwamba kuzaliwa na mama aliyekuwa mateka, ilikua dosari katika imani ya madhehebu ya Kaysaniyyah. Vivyo hivyo, Madhehebu ya Zaydiyyah wana amini kwamba Imamu, baada ya Imamu Zaynul Abidin, alikuwa ni mwanae Zayd ambaye alizaliwa na mama msichana mtumwa kutoka Sindhi, jina lake Huriya.

Hata Shahr Banu, binti yake Yazd Jurd (mfalme wa mwisho wa Iran) ambaye aliolewa na Imamu Husein na akamzaa Imamu Zaynul Abidin, alifika Arabuni akiwa mateka. Hata hivyo sifa zake binafsi zilimpa fursa ya kupewa cheo cha "Mkuu wa wanawake." Hamidah Khatun, mama yake Imamu Musa al-Kazim alikuwa msichana mtumwa kutoka Berber. Anasifiwa kwa elimu yake na uchamungu wake. Akawa anaitwa Hamidah mtakatifu. Imamu Jafar al-Sadiq alikuwa na desturi ya kuwapeleka wanawake kujifunza kanuni za dini kutoka kwa Hamidah na alikuwa na tabia ya kusema kwamba, "Hamidah ni mtakatifu kutokana na uchafu wote kama kipande cha dhabahu." Mama yake Imamu Ali al-Riza pia alikuwa msichana mtumwa kutoka Afrika Magharibi Kaskazini. Jina lake Taktum (au Najma) na alijulikana kama Tahirah, aliye takaswa. Alijulikana kwa elimu yake na uchamungu wake. Imamu Muhammad al-Taqi alikuwa mtoto wa Sabikah, aliyejulikana zaidi kama Khayzurah, mtumwa msichana kutoka Nuba. Imamu Musa al-Kazim alimwambia Yazid bin Sabt kupeleka salam zake kwa Sabikah. Kwenye hadithi anaitwa Tayyibah. Mama yake Imamu Ali al-Naqi, Sammanah, wa Maghrib, alikuwa mtumwa, lakini alikuwa anaitwa Sayyidah (mkuu wa wanawake) hakuwa na mtu wa kulingana naye kwa uchaji Mungu, mapenzi na kumuogopa Mwenyezi Mungu. Alikuwa akifunga saumu karibu mwaka wote. Imamu Ali al-Naqi alimwambia kwamba alikuwa analindwa na Mwenyezi Mungu na alikuwa wa kwanza miongoni mwa wakweli na waadilifu. Imamu Hasan al-Askari pia alizaliwa na mama ambaye alikuwa mtumwa msichana, Hudayth (au Salil.) Katika kumwonyesha hadhi yake ya juu miongoni mwa Shia, inatosha kusema kwamba baada ya kifo cha Imamu Hasan al-Akari yeye alikuwa mtu wa katikati kabisa ndani ya Ushia na jamii yote ilikusanyika kumzunguuka yeye na ali-waongoza katika njia iliyo bora kabisa. Shia walikuwa wakimwita "Jaddah," bimkubwa. Narjis Khatun, mama yake Imamu wetu wa 12 ambaye yupo hai mpaka sasa, alikuwa mtoto wa mfalme wa himaya ya Byzantine. Lakini pia alifika kwa Imamu Hasan al-Askari kama mtumwa.

Kiasi hiki kitatosha kwa upande wa kiroho. Tukiangalia upande wa siasa, tunaona watumwa wasio hesabika waliofi-ka katika kazi za vyeo vya juu sana vya uwajibikaji, uki-jumlisha na makamanda wa majeshi, kufanya kazi ya uga-vana, na uhakimu. Si tu kwenye utawala, pia tunawaona wataalam wa theolojia (elimu ya dini), wafasiri wa Qur'an, muhadithi, wana sheria na waandishi, ambao ama walikuwa watumwa au watoto wa watumwa, au watumwa walio achwa huru. Ukiwaondoa khalifa wa kwanza, tatu, nne na tano, makhalifa wote wa ukoo Abbas walizaliwa na wanawake watumwa. al-Mansur (khalifa wa pili wa ukoo wa Abbas) maarufu, alikuwa ndiye khalifa wa kwanza kuza-liwa na mama aliyekuwa mtumwa, Salamah, aliyetoka Berber. Kuanzia kwa Mamun al-Rashid (khalifa wa sita wa Banu Abbas) hadi wa mwisho wote walikuwa watoto wa wasichana watumwa. Yafuatayo ni majina ya makhalifa na mama zao watumwa: Mamun al-Rashid: Murajil, mtumwa msichana mweusi Mutasim Billah: Mtumwa msichana kutoka Kufah, jina lake aliitwa Maridah Wathiq Billah: Mrumi, jina lake ni Qaratis Mutawakkil Allallah: Mtoto wa Shuja Muntasir Billah: Mrumi, jina lake ni Habashiyyah Mustin Billah: Mukhariq Mutazz Billah: Mrumi, jina lake ni Qabihah Muhtadi Billah; Wards au Qurb. Mutamid Allallah: Mrumi, jina lake ni Fityan. Mutazid Billah: Sawab (au Hirz au Dhirar) Muktafi Billah: Mturuki mtumwa msichana, jina lake ni Jyaq au Khudi. Muqtadir Billah: Mrumi au Mturuki, mtumwa msichana, Gharib au Shaghab Qahir Billah: Fitnah Radhi Billah: Mrumi, jina lake ni Zalum. Muttaqi Lillah: Khalub au Zuhra Mustakfi Billah: Awjahun Naa au Ghusm. Muti Lillah: Mashalah Attai Lillah: Hazar au Atab. Qadir Billah: Dumanah au Tamami Qaim Billah: Kutoka Armenia, jina lake ni, Badrudduja au Qatrunnada Muqtadi Bi Amrillah: Arjwan Mustazhir Billah: Mtumwa (jina halikuandikwa) Mustarshid Billah: Mtumwa (jina halikuandikwa) Rashid Billah: Mtumwa (jina halikuandikwa Muqtafi Li Amrillah: Kutoka Ethiopia, mtumwa msichana Mustanjid Billah: Kutoka Karjiyya, mtumwa, jina lake ni Taus Mustadi Bi Amrillah: Kutoka Armenia, jina lake ni Dhaddha Nasir Li Dinillah: Mturuki, mtumwa, jina lake ni, Zamurrad Zahir Bi Amrillah: Jina halikuandikwa. Munstansir Billah: Mturuki mtumwa (jina halikuandikwa) Mustasim Billah: Hajir104.

Hata wakati wa karibu sana wa falme ya Ottoman ya Uturuki, familia ya Kifalme inaweza kujumuishwa katika familia ya kitumwa kwa sababu mama wa watoto wa hao masultani walikuwa watumwa. Muda mrefu kabisa kabla ya utawala wa Sulayman, Sultani ama alikwisha acha kuchukua mke kutoka kwenye familia za Kisultani au alimpa daraj a la mke kwa mama wa watoto wao. Mfumo wa utawala wa Ottoman kwa makusudi ulichukua watumwa na kuwafanya mawaziri wa nchi. Ufalme huo ulichukua watoto wa kiume kutoka kwenye zizi la kondoo shambani na kuwafanya washauri wa Sultani na kuwaoza mabinti wa kifalme, waliwachukua wanaume vijana wa nhi ambayo wahenga wao walikuwa na majina ya Kikristo kwa karne nyingi, na kuwafanya watumwa wa nchi kubwa kabisa za Kiislam. 104. Tizama sura zinazohusika za kitabu Rawdatu 's-Safa cha Muhammad Khawind Shah ; vile vile Ibn Rabbih al-Undulusi, al-Iqdu'l-Farid, j. 5 (Beirut: 1983) uk. 113-131.