• Anza
  • Iliyopita
  • 6 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 16212 / Pakua: 2084
Kiwango Kiwango Kiwango
UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

Mwandishi:
Swahili

2

UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

WATUMWA KATIKA HISTORIA YA UISILAMU

Kutoa mfano kuonyesha namna gani Uislamu umenyanyua hali na hadhi ya watumwa na kuwatendea wema kama binadamu badala ya kuwafanya mzigo wa mhayawani (ambavyo ndivyo walivyo fanyiwa kabla ya Uisilamu), hadithi ifuatayo ni yenye mvuto maalum. Siku moja Mtume aliketi mahali akiwa na Salman, Bilal, Ammar, Shuhayb, Khabbab (wote walikuwa watumwa kabla ya hapo) na kundi la Waisilamu fukara, ambapo watu fulani wasio Waisilamu walipita karibu na hapo. Walipowaona hawa watu "duni" wapo pamoja na Mtume, walisema, "Umewachagua watu hawa kutoka miongoni mwa watu wako? Unataka si si tuwafuate wao? Je, Mwenyezi Mungu amewaneemesha wao, hivyo kwamba wao wameamini na sio sisi? 34. Cherfils, Banaparte, et l'Islam (Paris, 1914). Ni vizuri zaidi utokane nao na usishirikiane nao; ukifanya hivyo, basi labda tunaweza kukufuata wewe." Mtume hakukubaliana na matakwa yao, na Mwenyezi Mungu akateremsha aya ifuatayo kuhusu suala hili: "Wala usiwafukuze wanaomwabudu Mola wao Mlezi asubuhi na jioni kwa kutaka radhi yake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, (hata uwafukuze). Ukiwafukuza utakuwa mion-goni mwa wenye kudhulumu. Na hivi ndivyo tunavyo wajaribu wao kwa wao, ili waseme: Je, hao ndio Mwenyezi Mungu amewafadhilisha miongoni mwetu? Je, Mwenyezi Mungu hawajui wanao mshukuru? Na wanapokujia wanaoziamini ishara zetu waambie: "Asalamu alaikum! Amani iwe juu yenu! Mola wenu Mlezi amejilazimisha rehema..." (6:52 -54) Salman, Bilal, Ammar na masahaba wao wanasema: "Wakati Mwenyezi Mungu alipo teremsha aya hizi, Mtume alituelekea sisi, akatuita twende karibu zaidi naye, na akase-ma; 'Mola wenu amejiamrishia rehema juu Yake.' Halafu tulikuwa na kawaida ya kukaa pamoja naye, na alipotaka kusimama (na kuondoka hapo) alifanya hivyo. Halafu Mwenyezi Mungu akateremsha aya: "Na isubirishe nafsi yako pamoja na wanao muomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni hali ya kuwa wanataka radhi Yake. Wala macho yako yasiwaruke..." (18:28)

"Ulipoteremshwa ufunuo kama huu, Mtume alikuwa na mazoea ya kututaka tuketi karibu naye sana hivyo kwamba mapaja yetu yalikaribia sana kuguuza mapaja yake; na hakusimama kabla yetu. Tulipo hisi muda wake wa kusimama umefika, tulimuomba ruhusa yake kuondoka; na halafu alisimama baada ya sisi kwisha kuondoka. Na alikuwa na desturi ya kutuambia; Nina mshukuru Mungu ambaye haku-niondoa hapa duniani mpaka Aliponiamuru kuwa na subira na kikundi cha ummah wangu. Nitakuwa na nyinyi katika maisha yangu, na, baada ya kufariki, nitaendelea kuwa na nyinyi."35. Ninaorodhesha kwa ufupi majina ya baadhi ya watumwa JJ- al-Majalisi, M.B., Hayatul Qulub, j. 11 (Tehran: Kitabfurushi-e-Islamia, 1371 A.H.), uk. 562-3; Abu Na'im Ahmad al-Isfahani, Hilyatul Awliya, j. 1 (Beirut, 1967), uk. 146-7.

ambao daraja lao la kiroho limenyanyuliwa juu sana katika Uisilamu na katika jamii ya Kiisilamu, tangu hapo Uisilamu ulipoanza kuwepo: Salman, Muajemi: Wa kwanza na wa mbele kabisa ni Salman al Farsi (Muajemi). Alikuwa mtoto wa mchungaji wa dini ya Zoroasta katika jimbo la Fars. Tokea mwanzo kabisa, alikuwa na shauku ya kuwa mfuasi wa dini isiyokuwa na nyongeza au pungufu zilizofanywa na binadamu. Hali hii alikuwa nayo siku nyingi hata kabla ya ujio wa Uislamu.

Akabadili dini ya uzoroasta akaingia kwenye Ukristo, na akawa mtumishi wa mchungaji maarufu mmoja baada ya mwingine akiwa katika harakati ya uchunguzi wa elimu ya kidini. Baada ya kupata matatizo na shida kwa muda mrefu alijihusisha na mtawa mmoja huko Antiokia, ambaye wakati wa kufa kwake, alimpa ushauri kwamba muda muafaka ulikwisha fika wa kuja kwa Mtume wa mwisho hapa duni-ani. Akamwambia afanye safari ya kwenda Hijaz, jimbo la Arabuni ambalo ndani yake mna miji ya Makka na Madina. Alipokuwa njiani anaelekea huko, alikamatwa na kuwa mateka na kikundi cha wapiganaji, na akauzwa kutoka bwana mmoja hadi mwingine, hadi akafikisha wamiliki kumi. Hatimaye, alinunuliwa na mwanamke wa Kiyahudi huko Madina. Si rahisi kutoa maelezo ya kina kuhusu mate-so aliyofanyiwa wakati akiwa mateka kwa kipindi kirefu. Hata hivyo ilionyesha kwamba hatima yake hiyo ilikuwa inamsogeza karibu na lengo lake, kwa sababu ilikuwa katika mji wa Madina alikutana na Mtukufu Mtume wa Uisilamu. Baada ya majaribu magumu Salman alidhihiriki-wa ndani ya nafsi yake na "Mtume" yule ambaye alikuwa anangojewa kwa muda mrefu kama ilivyotabiriwa katika Agano Jipya, (Yohana 1: 19-25) akakubali kuwa Mwisilamu.36. Mtukufu Mtume wa Uisilamu akamnunua kutoka kwa bimkubwa wake wa Kiyahudi na akamwacha huru. Ilikuwa ni baada ya vita ya Badr, vita ya kwanza ya Uisilamu, na kabla ya vita ya Uhud.37. Imani, ujuzi na uchaji Mungu wa Salman na mafanikio yake yasiyo na mfano wa kulinganisha, ilimuweka juu ya masa-haba wengine wote wa Mtukufu Mtume. Yeye ni mmo-jawapo wa nguzo nne za Waisilamu wa kweli katika dini (pamoja na Abu Dharr al-Ghifari, Miqdad na Ammar.) Salman anayo sifa pekee ya kujumuishwa kwenye Ahlul Bayt (Nyumba ya Mtume) kwa sababu ya imani na uchaji Mungu wake. Hadithi zinazoonyesha ubora na uadilifu na wema wake haziwezi kuorodheshwa kwenye kitabu hiki kidogo. Hata hivyo, ninazinukuu baadhi ya hadithi hizo ili msomaji apate picha ya haraka ya hadhi yake mbele ya Mtume na warithi wake.

Ingawaje alikwisha ukubali Uislam, Salman hakushiriki kwenye vita ya Badr kwa sababu wakati huo alikuwa bado mateka. Baada ya Badr, alishirki kikamilifu kwenye vita vya kutetea Uisilamu na Waisilamu. Wakati Quraysh wa Makka na makabila mengine mengi 36. Ibn Sa'd, op. cit., j. 4:1, uk. 58. 37. al-Majilisi, Bihar al-Anwar, j. 22 (Tehren, n.d.), uk. 355; Abu Na'im, op. cit., j. 1, uk. 193-5; Ibn Hajar al-Asqalani, al-Isabah fi Tamyiz's-Sahabah, j. 3 (Calcutta: Asiatic Society of Bengal, 1853-88), uk. 224. pamoja na Wayahudi wa Madina, walipozingira Madina, Salman ndiye aliye mshauri Mtume kuchimba handaki kuzunguuka mji wa Madina ili liwe kizuizi kwa adui asi-weze kushambulia sehemu dhaifu za jiji. Na ikawa ni kwa sababu hii vita hiyo ikapewa jina la "Vita vya Handaki."38. Ilikuwa ni kwenye vita hivi ambapo mahojiano ya kirafiki yalipoanza baina ya Muhajirina wa Makka na Ansari wa Madina. Mada ilikuwa: Je, Salman alikuwa Muhajirina au Ansari? Ansari walidai kwamba kwa kuwa Salman alik-wenda kwa Mtume huko Madina, alikuwa kwenye kundi la Ansari; Muhajirina wakadia kwamba kwa sababu Salman aliacha maskani na familia yake; alikuwa Muhajirina.

Ubishi huu wa kirafiki pia unaonyesha jinsi gani daraja la Salman lilikuwa kubwa katika kipindi kifupi cha miaka mitatu ambapo kila kundi lilikuwa linadai kuwa ni mtu wa kundi lao. Vyovyote vile, mgongano huo ulifikishwa kwenye mamlaka ya juu - kwa Mtume, ambaye aliamua kwamba Salman kamwe hakutokana na makundi hayo maw-ili Muhajirina au Ansari, akasema: "Salman anatoka kwetu (Nyumba ya Mtume)."39. Ilikuwa heshima kubwa ya aina hiyo ambayo imeendelea kutajwa kwenye hadithi na mashairi. Mshairi anasema: Moyo wa ibada na utii wa Salman ilikuwa ni jadi yake, ambapo hapakuwepo na uhusiano baina ya Nuhu na mtoto wake. Mtukufu Mtume pia alisema, "Salman ni bahari isiyokauka 38. Ibn Sa'id, op. cit., j. 11:1, uk. 47.

39. al-Majilisi, Bihar, j. 20, uk. 189, 198; Ibn Sa'id, op. cit., j. 4:1, j. 7:2, uk. 65.

na hazina isiyo kwisha. Salman anatoka kwetu, familia (Nyumba ya Mtume), amepewa hekima, na amejaaliwa akili."40. Imam Ali anasema; "Salman alikuwa kama Luqman, Mtu mwenye Hekima."41. Wasomi wengi wa Kiisilamu wanafikiri Luqman alikuwa Nabii. Imamu Jafar as-Sadiq alisema Salman ni bora zaidi kuliko Luqman.42 Imamu Muhammad al-Baqir alisema kwamba Salman alito-ka kwa watu (Mutawassiman) watu wanaotambua tabia za ndani za watu.)43. Hadithi nyingi zinasema kwamba Salman alikuwa anajua al-Ismul a'dham (jina kuu kabisa la Mwenyezi Mungu);44. na kwamba alitoka kwa Muhaddathin (wale watu ambao malaika huwasemesha.)

Kuonyesha ukuu wa Salman, inatosha kwamba Mtume alisema: "Imani ina madaraja kumi, na Salman yupo kwenye daraja la kumi (yaani daraja la juu zaidi), Abu Dharr yupo kwenye daraja la tisa, na Miqdad yupo kwenye daraja la nane." Wakati wowote malaika Jibril alipomtokea Mtume, alikuwa na kawaida ya kumwomba afikishe salamu za Mwenyezi Mungu kwa Salman na amfundishe elimu ya mambo yajayo.46. Kwa mujibu wa hali hiyo, Salman alikuwa na desturi ya 40. al-Majilisi, Bihar; j. 22, uk. 348.

41. al-Majilisi, op. cit., j. 22,uk. 330, 391; Ibn Sa'id, op. cit., 4:1, uk. 61; Abu Na'im, op. cit., j. 1, uk. 187.

42. al-Majilisi, op. cit., j. 22 uk. 331.

43. Ibid, uk. 349.

44. Ibid, uk. 346.

45. Ibid, uk. 327, 349.

46. Ibid, uk. 347.

kumtembelea Mtume wakati wa usiku, ambapo Mtume na Amiri wa Waumini Ali walimfundisha elimu ya siri kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambayo kamwe hakufundishwa mtu mwingine kwa sababu hakuna mtu ambaye angeihimili. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba Imamu Ali alisema, "Salman alipata ujuzi wa watu wa kwanza na ujuzi wa watu wa mwisho, yeye ni bahari isiyokauka kamwe na anatoka kwetu Nyumba ya Mtume."47.

Allama Majlisi anaandika kwenye kitabu kiitwacho Aynul l-Hayat kwamba inaeleweka kutoka kwenye hadithi za Shia na Sunni kwamba baada ya masumin hakuna mtu aliye kuwa sawa na Salman, Abu Dharr na Miqdad, miongoni mwa masahaba wa Mtume. Imamu Musa al-Kazim alisema, siku ya ufufuo kuna mtu ataita kwa niaba ya Mwenyezi Mungu kwamba wako wapi hawariyyin na waumini wa Muhammad bin Abdullah, ambao walidumu bila kutetereka kwenye njia waliyoonyeshwa naye na kamwe hawakuvunja mila yake?' Halafu watafufuka Salman, Miqdad na Abu Dharr. 48 Mtukufu Mtume alisema, "Mwenyezi Mungu ameniamuru kuwapenda masahaba wanne miongoni mwa masahaba wangu." Watu wakauliza ni nani hao masahaba wanne. Mtukufu Mtume akasema, Ali bin Abi Talib, Salman, Miqdad na Abu Dharr."49. Kwa mujibu wa hadithi, Mwenyezi Mungu alimpelekea 47. Ibid, uk. 319; Ibn Sa'id, op. cit., j. 4:1, uk. 61; Abu Naim, op. cit., j. 1, uk.187. 48. al-Majilisi, op. cit., j. 22, uk. 342. 49. Ibid, Uk. 321.

Salman makarama na zawadi kutoka Peponi; na Pepo ilim-ngojea kufika kwake kwa shauku kubwa.50. Wakati mmoja Mansur bin Buzurq, yeye mwenyewe akiwa Muajemi alimuuliza Imamu Jafar al-Sadiq kwa nini alikuwa anamkumbuka sana Salman al-Farsi. Imamu akasema: "Usiseme Salman al-Farsi (Muajemi). Sema, Salman wa Muhammad. Sharti ujue kwamba sababu ya mimi kumkum-buka sana mtu huyu ni kutokana na tabia zake jema kuu tatu: Kwanza, aliacha matamanio yake binafsi kwanza, na kuzin-gatia yale ya Amiri wa Waumini, Ali. Pili, aliwapenda fukara na aliwapendelea wao kuliko matajiri. Tatu, alipen-da ujuzi na aliwapenda watu wenye elimu. Hakika Salman alikuwa mtumishi mzuri wa Mungu, Mwisilamu safi na hakutokana miongoni mwa washirikina."51 Wakati fulani masahaba wa Mtume walikuwa wanasimulia juu ya wahenga wao, wakionyesha fahari kwa nasaba za familia zao. Salman alikuwa miongoni mwao. Umar, ambaye baadaye alikuwa Khalifa wa pili, alimgeukia na kumuuliza aeleze kuhusu jadi yake na nasaba yake. Salman akasema: "Mimi ni Salman, mtoto wa mtumishi wa Mwenyezi Mungu, nilikuwa fukara na Mwenyezi Mungu akanipa utajiri kupitia kwa Muhammad (s.a.w.), nilikuwa mtumwa, na Mwenyezi Mungu akanipa uhuru kupitia kwa Muhammad (s.a.w.). Hii ndio jadi yangu na daraja langu, Ewe Umar!"52. Kama ambavyo imekwishaelezwa huko nyuma kwamba Abu Dharr mwenyewe alikuwa mmoja wapo wa nguzo kuu 50. Ibid, uk. 325; Abu Na'im, op. cit., j. 1, uk. 190. 51. al-Majilisi, op. cit., j. 22, uk. 327. 52. Ibid, uk. 381 nne za dini (imani) na alikuwa kwenye daraja la tisa la imani. Lakini hata Abu Dharr hakuweza kumwelewa Salman sawasawa. Wakati fulani Abu Dharr alikwenda nyumbani kwa Salman. Salman aliweka chungu cha kupikia chenye maji katika moto. Wakaendelea na mazungumzo lakini kufumba na kufumbua chungu kilianguka chini na kujifunika.

Lakini ajabu ya majabu, hakuna hata tone moja la maji lililodondoka kutoka kwenye chungu, na Salman akakireje-sha chungu kile motoni tena. Baada ya muda tukio hilo lika-jirudia tena. Hakuna tone la maji lililodondoka, na Salman akakirejesha chungu kwenye moto bila papara. Abu Dharr akaduwaa. Kwa haraka akatoka nje na akaku-tana na Imamu Ali njiani. Alimsimulia yale aliyoyaona. Ali akasema" "Ewe Abu Dharr, kama Salman atakujulisha mambo yote anayo yajua, utashangaa. Ewe Abu Dharr, Salman ni lango la kuingia kuelekea kwa Mwenyezi Mungu hapa duniani. Yeyote anaye mkubali Salman ni muumini, yeyote anaye mkataa ni kafiri. Salman anatoka kwetu -Nyumba ya Mtume."53 Nadhani hadithi hizi chache na za kuaminika zinatosha kuonyesha daraja la juu sana la Salman mbele ya Mwenyezi Mungu, mbele ya Mtume, Imamu Ali na warithi wake.

Salman akateuliwa kuwa gavana wa Iran, alikwenda Madain, makao makuu ya serikali ya wakati huo. Watu wa 53. Ibid,uk.374. Madain, kwa kipindi kirefu walizoea kuona fahari na utuku-fu wa baraza la wafalme wa Iran, walikuwa wanangojea msafara wa kifahari. Lakini hakuna msafara uliotokea. Badala yake, mzee mmoja, alikuwa amebeba vitu begani anatembea kwa mguu anawaelekea wao. Wakamuuliza huyo mgeni kama aliuona msafara wa gavana. Mgeni huyo akasema: "Mimi ndiyo gavana wenu." Na huyo gavana mwenye moyo mkunjufu wa Madain alitawala kwa aina yake ya ujuzi, huruma, haki na umadhubuti hivyo kwamba mnamo kipindi kifupi, Madain yote ilikuwa chini ya mam-laka yake. Ushindi huo haukufanywa na polisi au jeshi la wapiganaji, bali kwa uwezo wa ukamilifu wake wa kiroho, uchaji Mungu na ustahamilivu. Salman alifariki dunia mnamo mwaka wa 36 A.H. huko Madain (Madyan). Imamu Ali alisafiri kutoka Madina kwenda Madain (Madyan) kwa muda wa nusu siku kimiu-jiza ili aweze kutekeleza ibada ya mazishi ya sahaba na ndugu yake wa kuaminika.54 Hii ilikuwa heshima ya pekee ya Salman. Kaburi la Salman huko Madain (Madyan- Iraq) hutembelewa na mamia ya mahujaji kila siku. Hija (ziyara) iliyowekwa inaonyesha ukuu wake kwa Mwenyezi Mungu. 2. Zayd bin Harithah Zayd bin Harithah bin Sharahil al-Kalbi, mvulana wa Kiarabu, alitekwa nyara wakati wa utoto wake na akauzwa kama mtumwa. Jambo hili lililotokea kabla ya kuja kwa Uisilamu. Hakim bin Hizam bin Khuwaylid ndiye aliye mnunua kwenye soko 54. Ibid, uk. 372,380.

la Ukaz, na akampeleka kwa shangazi yake, Khadijah binti Khuwaylid, ambaye naye alimpa Mtukufu Mtume. 55. Baba yake Zayd alikuwa anamtafuta mwanae. Baada ya muda mrefu akagundua kwamba Zayd alikuwa Makka. Alikwenda Makka na akaamua kutoa fidia kwa ajili ya kumkomboa mwanae Zayd. Mtume alisema kwamba kama Zayd anataka kuungana na familia yake, hakuna haja ya kulipa fidia yoyote. Alikuwa huru kuondoka. Lakini Zayd hakutaka kwenda na baba yake na akapendelea kubaki na Muhammad. Harithah, baba yake Zayd, alisikitika sana na akasema; "Ewe mwanangu, wewe unapenda kuendelea kumwacha baba yako na mama yako kwa ajili ya Muhammad?" Zayd akasema: "Yale ambayo nimeyaona katika maisha ya Muhammad ndio yanayo nilazimisha kwamba nisimwache kwa ajili ya mtu mwingine yeyote." Msimamo wa aina hiyo wa mapenzi kwa Mtukufu Mtume uligusa nyoyo za wote wale waliomjua baadaye. Na ilikuwa tabia hii ya pekee ya kutenda wema ambayo ilifanya takrib-an bara Arabu yote kuukubali Uisilamu katika kipindi kifupi cha miaka ishirini na tatu. Vyovyote vile, Harithah alishangazwa na akatangaza kwenye Kaabah kwamba tangu hapo na kuendelea wala yeye hakuwa baba yake Zayd ama Zayd kuwa mwanae.

Ni hapo ambapo Mtume Muhammad akatangaza kwenye hijr Ismail (pembeni mwa Kaabah) kwamba: "Ninatangaza kwamba tangu sasa na kuendelea Zayd ni mwanangu." Harithah, aliposikia taarifa hii, akarudi nyumbani kwake bila huzuni. 56. 55. Ibn Hajar, op. cit., j. 2, uk. 45. Zayd bin Harithah sasa aliitwa Zayd bin Muhammad. Ubini huu uliendelea hadi mwaka 5 A.H. ambapo aya ifuatayo iliteremshwa: "Mwenyezi Mungu hakumwekea mwanadamu nyoyo mbili kifuani mwake. Wala hakuwafanya wake zenu ambao mnawalinganisha migongo yao na migongo ya mama zenu kuwa ni mama zenu. Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa. Hayo ni maneno ya vinywa vyenu tu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayesema kweli, naye ndiye anaye ongoza njia. Waiteni kwa (ubini wa) baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu..." (Qur'ani 33:4-5) Halafu Zayd kwa mara nyingine akaitwa Zayd bin 56 al-Majilisi, op. cit., j. 22, uk. 314, 318; Ibn Sa'd, op. cit., j.3: 1, uk. 28; Ibn Hajar, op. cit., j.2, uk. 45-6. Harithah57. Mtume alikwisha muoza Zayd kwa binamu yake Zainab binti Jahash, ambaye alikuwa bint wa shangazi yake Umaymah.58. Wana ndoa hawa wawili walianza kugombana, na Zayd akamtaliki Zainab, kwa amri ya Mwenyezi Mungu, Mtume akamuoa Zainab yeye mwenyewe. (Wakati huo Zainab alikuwa na umri wa zaidi ya miaka hamsini.59. Ukweli huu peke yake unatosha kusafisha utando mnene wa hadithi zenye nia mbaya ambazo maadui wa Mtume wamesingizia kuhusu ndoa hii takatifu.)

Mwenyezi Mungu anasema kwenye Qur'an: "...Basi Zayd alipokwisha haja naye alikuoza wewe, ili isiwe taabu kwa Waumini kuwaoa wake wa watoto wao wa kupanga watakapokuwa wamekwisha timiza nao shuruti za talaka. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa. " (33:37)

Kwa hizi ndoa mbili za Zainab bin Jahash, kanuni mbili za kipagani ziliondolewa: 57. al-Majilisi, op. cit., j. 3 uk. 29; Ibn Hajar, op. cit., j. 7, uk. 600. 58. Ibn Sa'd, op. cit., 8, uk. 31; Ibn Hajar, op. cit., j. 2, uk. 46, j. 7, uk. 600. 59. al-Tabataba'i, al-Mizan, toleo la tatu, j. 4 (Beirut: 1974), uk. 195. Kwa ndoa ya kwanza, fikira ya imani ya kuwa taifa fulani ni bora kuliko nyingine au imani kwamba kuwa mtumwa au mtumwa aliyeachiwa huru ilikuwa fedheha kuhusu hadhi ya watu, ilifutwa.60.

Na kuhusu ndoa ya pili, imani ya kwamba mtoto wa kiume wa kupanga alikuwa mtoto halisi, ilisitishwa. Mtume mwenyewe alimuoa mwanamke aliyetalikiwa na mwanae wa kiume wa kupanga, sasa ni vipi liwepo dai la kusema kwamba mtoto wa kupanga alikuwa mtoto halisi wa kuzaa? Kwa hiyo, desturi ya Kiarabu ambayo ilimtambua mtoto wa kupanga kama mtoto halisi iliondolewa kabisa.61. Zayd ni mtu mmoja tu miongoni mwa masahaba wa Mtume ambaye ametajwa kwa jina ndani ya Qur'ani. Alikuwa mtu wa tatu kuingia katika Uisilamu baada ya Khadija binti Khuwaylid na Ali bin Abi Talib. Zayd alikuwa kamanda wa jeshi la Kiisilamu lililopelekwa kupigana na majeshi ya Kikristo huko Muta. Baada ya kifo cha kishahidi cha Zayd, Jafar, binamu yake Mtume, akashika nafasi ya kamanda badala ya Zayd, naye pia alikutana na kifo cha aina hiyo hiyo. 62 Zayd alikuwa na mtoto, Usamah, aliyemzaa na mke wake wa kwanza, Umm Ayman. Usamah alikuwa na umri wa miaka 19 alipoteuliwa kuwa kamanda wa jeshi ambalo lili-jumuisha masahaba wote mashuhuri wa Mtume, pamoja na Abu Bakr, Umari na Uthman. 60. al-Amili, op. cit., j. 14, uk. 43; Ibn Sa'd, op. cit., j. 8:1, uk. 71

61. al-Majilisi, op. cit., j. 22, uk. 187; Ibn Hajar, op. cit., j. 7, uk.600

62. Ibn Sa'd, op. cit., j. 3:1, uk. 32; Ibn Hajar, op. cit., j. 2, uk. 47.

Masahaba wengine walipodharau uteuzi wake, Mtume ali-wakaripia kwa kusema: "Zayd alikuwa mbora zaidi yenu, na mwanae Usamah pia ni mbora zaidi kuliko nyinyi wote." Usamah aliamuriwa na Mtume kwenda na jeshi kulipa kisasi cha kifo cha baba yake huko Muta. 63 3. Ammar bin Yasir: Alikuwa mmoja wapo wa masahaba walio heshimiwa mno wa Mtume na mfuasi mwaminifu wa Imam Ali. Ammar alikuwa miongoni mwa wale walio teswa kikatili kwa ajili ya Uisilamu. Alihama kwenda Ethiopia64. mara mbili na Madina, alisali kuelekea qibla mbili yaani Baytul Maqdis na Ka'ba. Alishiriki kwenye vita zote za Kiisilamu tangu mwanzo,65. na aliuawa kishahidi kwenye vita ya Siffin mnamo tarehe 9. Safar, mwaka wa 3 A.H. Ammar na wazazi wake walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuwa Waisilamu. Baba yake, Yasir alikuwa mtu wa kabila la Qahtan kutoka Yemen. Yeye pamoja na kaka zake wawili, walikwenda Makka kwa madhumuni ya kumtafuta kaka yao aliyepotea. Kaka zake walirudi kwao Yemen lakini Yasir akakaa Makka ambapo alifanya mkataba na Abu Hudhayfah (wa kabila la Bani Makhzum), na akamuoa mtumwa wake msichana, Sumayyah binti Khayyat. Yasir na Sumayyah walizaa watoto wawili, Abdulah na Ammar, ambao kwa mujibu wa mila za Kiarabu waliwekwa katika daraja la watumwa wa Abu Hudhayfah. 66. 63. Ibn Sa'd, op. cit., j. 2:2, uk. 41-2; j. 4:1, uk. 46-7. 64. Ibn Sa'd, op. cit. j.3:1, uk. 179; Ibn Athir, Usdlu'l-Ghabah fi Ma'rifat's-Sahabah, j. 4 (Egypt, n.d.). 65. Ibid. 66. Ibid, j. 3:1, uk. 176.

Baada ya kuingia kwenye Uisilamu, Abu Jahl, akisaidiwa na wapagani wengine, akaanza kuitesa familia yote kikatili. Misumari ya chuma iliwekwa kwenye miili yao na wakalaz-imishwa kulala chini kwenye mchanga wa jangawani wenye joto kali. Joto la jua na mchanga wa jangwa lilisababisha misumari ya chuma kuwa na joto kama moto; ngozi zao zil-iungua. Mateso haya kwa kawaida yaliendelezwa hadi wahusika kupoteza fahamu. Halafu misumari ya chuma iliondolewa na wakamwagiwa maji.67. Mtume alisikitishwa sana na mateso ya familia hiyo; lakini alikuwa hana uwezo wa kuwasaidia. Hata hivyo alikuwa na desturi ya kwenda karibu nao na kuwapa moyo wa kusta-hamili uonevu wa watesaji wao. Aliwapa salamu nzuri sana za Peponi na kusema: "Kuwemi wavumilivu, Enyi familia ya Yasir, kwa sababu mnayo nafasi nzuri iliyotayarishwa kwa ajili yenu Peponi.68. Yasir na Sumayyah waliuawa kikatili na wapagani wa kabi-la la Quraysh, waliongozwa na Abu Jahl. Hii ni sifa kubwa ya familia hii ya kuheshimiwa kwa ajili ya Uisilamu. Sumayyah alikuwa mchamungu sana na mwanamke aliye muogopa Mungu; alikuwa mwanamke wa kwanza kufa kishahidi kwa ajili ya Uisilamu. Wazazi wa Ammar, walipouawa, Ammar alijifanya kukana Uisilamu, na kitendo hicho kilimwokoa. Halafu akaenda kwa Mtume huku analia kwa uchungu kwamba alilazimika kutamka maneno ya kufuru ili aweze kutoroka kutoka mikononi mwa makafiri. 67. Ibid, j. 3:1, uk.177; Abu Na'imi, op. cit., j. 140. 68. Ibn Sa'd, op. cit., j. 3:1, uk. 178; Abu Naimi, op. cit., j. 1 uk. 140; Ibn Hajar, op. cit., j. 3, uk.1219.

Mtume alimwambia asiwe na wasiwasi, kwani hakusema maneno hayo kwa dhati ya moyoni mwake. Kwa mujibu wa tukio hili aya ifuatayo iliteremka: "Anaye mkataa Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake - isipokuwa aliye lazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya imani, lakini aliye kifungulia kifua chake kukataa - basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao watapata adhabu kubwa." (Qur'an 16:106) "o Ammar aliposimulia maovu aliyofanyiwa Sumayyah aliye rehemewa, Mtume akasema, uvumilivu, "Ewe Abu Yaqzan; Ee Mwenyezi Mungu, usimghadhibikie na kumwadhibu kwa moto wa jahanamu yeyote kutoka katika familia ya Yasir." (Mtume alipokwenda Madina, na msikiti wake (Mtume) ulikuwa unajengwa, Ammar alikuwa anabeba mizigo ya mawe mara mbili zaidi ya kawaida kwa shauku kubwa. Wakati huo huo alikuwa anakariri beti fulani za mashairi, ujumbe uliomo kwenye beti hizo ulimfikia Uthman (ambaye baadaye aliteuliwa kuwa khalifa wa tatu) ambaye alidhani kwamba Ammar alikuwa ana mdhihaki. Uthman alipozidiwa na kutokuelewa kwake, alimpiga Ammar usoni hadi damu ikatoka kwa kasi na akakinga ili 69. Ibn Sa'd, op. cit., j.3:1, uk. 178; Ibn Hajar, op. cit., j. 3, uk. 1220. damu isitoke kwa wingi. Ammar akalalamika kwa Mtume, ambaye mwenyewe alilisafisha na kulifunga jeraha na akasema: "Ammar ni ngozi baina ya macho yangu na pua yangu." Halafu akasema: "Sawa, Ewe Ammar, utauawa na kundi la waasi, wewe utakuwa unawaita watu hao waje Peponi na wao watakuwa wanakuita uende Jahanamu." 70. Umashuhuri na heshima ya Ammar inaweza pia kufuatiliwa kutoka kwenye matamko yafuatayo ya Mtume: "Ammar yuko pamoja na ukweli, na ukweli upo pamoja na Ammar popote pale atakapokuwa.

Ammar ni ngozi baina ya macho yangu na pua yangu; na atauawa na kundi la waasi."71. Pia Mtume alisema; "Ammar amejaa imani kutoka utosini hadi unyayoni (miguuni)."72. Zipo hadithi nyingine nyingi za Mtume na Maimamu kuhusu Ammar. Ammar alikuwa mmojawapo wa masahaba wenye imani ambaye siku zote alimfuata Imamu Ali. Mnamo mwaka wa 70. Ibn S a'd , op. cit., j. 3:1, uk. 177, 180; Ibn Hajar, op. cit., j. 3, uk. 1220; al-Bukhari, al-Sahih, j. 8. (Chapa ya Misr) uk. 185-186; al-Trimidhi, al-Jami' al- Sahih, j. 5 (Chapa ya Misir) uk.669; Ahmad bin Hanbal, al-Musnad, j.2 Chapa ya Misir) uk. 161, 164, 206, j. 3, uk. 5, 22, 28, 91, j. 4, uk. 197, 199, j. 5, uk. 215, 301, 307, j. 6, uk. 289, 300, 311, 315; Ibn 'Abdi'l-Barr, al-Isti'ab fi Ma'rifat'l-Ashab, j. 3, uk. 1140. 71. Ibn Sa'd op. cit.,j. 3:1, uk. 187; Hakim, al-Mustadrak'ala's-Sahihayn, j. 3, (chapa ya Hyderabad) uk. 392; Ibn Hisham, al-Sirahj. 2, (chapa ya Misir Toleo jipya) uk. 143; Ibn Kathir, al-Tarikh, j. 7. uk. 268, 270. 72. Abu Na'im, op. cit., j. 1, uk. 139; Ibn Hajar, op. cit., j. 3, uk. 1219; Ibn Majah, al-Sunan, j. 1 (chapa ya Misir toleo jipya) uk. 65; al-Haythami, Majma'al-Zawa'id,j. 9 (chapa ya Misir toleo jipya) uk. 295; Ibn 'Abdu'l-Barr, op. cit., j. 3, uk. 1137. 35 A.H. wakati Ammar na wengine wengi, walipinga sera ya Uthman bin Affan (Khalifa wa tatu) kuhusu mgawo wa haz-ina ya taifa, Khalifa Uthman aliagiza apigwe, akapigwa sana bila huruma hivyo kwamba mishipa ya tumbo lake ilipa-sukana ikasabaisha ugonjwa wa chango la ngiri (henia).73. Kama alivyo kuwa baba yake, Yasir alikuwa mshiriki wa Banu Makhzum, kwa hiyo wakamchukua Ammar nyum-bani kwao (akiwa bado hana fahamu) na wakasema kwamba kama Ammar akifa wangelipa kisasi chake kwa Uthman.

Kama ambavyo imekwishaelezwa hapo juu, Mtume alik-wisha sema kwamba Ammar angeuawa na kundi lililoasi; na ndivyo ilivyotokea. Ammar aliuawa mnamo 37 A.H. na jeshi la Muawiyah bin Abu Sufyan. Wakati huo alikuwa na umri wa miaka 90 au 91. Siku hiyo alipouawa kifo cha kishahidi, alikuwa anapi-gana kijasiri kabisa dhidi ya jeshi la Muawiyah, wakati mtu mmoja kutoka Syria, Abu Ghandiyah al-Muzani, alimjeruhi vibaya kiunoni; marafiki zake wakambeba na kumpeleka mahali pa salama. Akaomba maji; mtu mmoja akampa kikombe cha maziwa. Ammar akasema: "Usemi wa Mtume ulikuwa wa kweli." Watu wakamwomba awaeleze. Akajibu, "Mtume aliniaarifu kwamba riziki yangu ya mwisho hapa duniani ni maziwa." Basi akanywa maziwa na baadaye akafa.74. Amiri wa Waumini Ali alipata taarifa hiyo kuhusu msiba huo. Alitoka nje haraka na akakiegemeza kichwa cha 73. al-Baladhuri, Ansabu'l-Ashraf, j. 5, uk. 48, 54,88; Ibn Abi'l-Hadid, Sharh Nahj'al-Balagha, j. 3, uk. 47; Ibn Qutaybah, al-Imamah wa 's-Siyasah, j. 1, uk. 35-6; Ibn 'Abd Rabbih, al-Iqdu 'l-Farid, j. 4 (chapa ya Misir) uk. 307; Ibn Sa'd, op. cit., j. 3:1, uk. 185; al-Diyarbakri; Tarikhu'l-Khmis, j. 2, uk. 271. 74. Ibn Sa'd, op. cit., j. 3:1, uk. 184-5; Abu Na'im, op. cit., j. 1 uk. 141. Ammar kwenye mapaja yake. na akakariri wasifu ufuatao kwa ajili ya sahaba wake mwaminifu: Ee kifo, ambacho kinakuja kwangu kwa vyovyote; Afadhali unipumzishe haraka; Kwa sababu umewamaliza marafiki zangu wote; Ninaona kwamba wewe unawatambua marafiki zangu wapendwa wote, Kama vile mtu anakuongoza kwao kwa lengo maalum."

Kisha baada ya kukariri: "Hakika sisi tumetoka kwa Mungu na tutarudi kwa Mungu," akasema: "Mtu yeyote ambaye hakuhuzunishwa sana kutokana na kifo cha Ammar hana fungu katika Uisilamu. Mungu na amrehemu Ammar." Amiri wa Waumini aliisalia maiti yake na akamzika kwa mikono yake. 75. Kifo cha kishahidi cha Ammar, kilimsababishia matatizo Muawiyah kwa sababu watu wengi katika jeshi lake walikumbuka usemi wa Mtume, na wakatambua kwamba kifo cha Ammar, kilionyesha kwamba Muawiyah na jeshi lake walikuwa waasi na hawakuwa katika njia iliyo sahihi. Akiwa katika jitihada za kutuliza jeshi lake, Muawiyah akasema kwamba Ali ndiye aliye sababisha kifo cha Ammar kwa sababu yeye ndiye aliyempeleka kwenye uwanja wa vita. Amiri wa Waumini aliposikia taarifa hii ya ujanja wa Muawiyah, akasema: "Basi, ni Mtume mwenyewe ndiye aliye muua Hamzah kwa kumpeleka kwenye uwanja wa vita wa Uhud!" 76. 75. Qummi, Abbas, Muntaha'l-Amal, j. 1 (Tehran: 1381 AH) uk.92. 76. al-Tabari, al-Ta'rikh, j. 1, uk 3316,-3322; j. 3, uk. 2314-2319; Ibn Athir, al-Kamil, j. 3, uk. 308-312; IObn Kathir, al-Ta'rikh, j. 7, uk. 267- 272.

4. Miytham al-Tammar: Miytham al-Tammar (muuza tende), mtoto wa kiume wa Yahya, alikuwa mtumwa aliyenunuliwa na Imamu Ali. Lakini watu wachache sana walijua kwamba alikuwa mtumwa kwa sababu Ali alimpa uhuru na akawa rafiki mkubwa na wa karibu sana wa bwana wake wa zamani. Miytham alijumuishwa kwenye kundi la hawariyyun. Maana yake "Mwanafunzi" kama ilivyokuwa kwa wanafun-zi kumi na mbili wa Isa. Imamu Ali alimfundisha Miytham elimu ya siri ya Allah, na akampa utambuzi wa mambo yajayo. Miytham akajua undani wa kifo, mateso ya wakati ujao, ambayo nyakati nyingine alikuwa anawaelezea watu na watu walimcheka, lakini matukio yaliyotokea baadaye yalithibitisha kuwa alikuwa sahihi. Ali alipomnunua. Miytham, alikuwa anaitwa Salim. Ali akamwambia kwamba alisikia kutoka kwa Mtume kwamba "baba yako alikwita Miytham huko Ajemi (Iran)." Miytham alishangaa kwa sababu hakuna mtu aliyejua jina hilo hapo Arabuni. Halafu Ali akamwambia aendelee kutumia jina lake la mwanzo; hivyo akaanza kuitwa Miytham tena, na akampanga mtu aitwaye Abu Salim77. Miytham alikuwa mchamungu sana. Imeandikwa kwamba; "...yeye (Miytham) Mweneyzi Mungu na amwie radhi, alikuwa miongoni mwa watu wachajimungu sana na ngozi yake ilikaukia mwilini mwake (kwa sababu ya kufunga saumu na sala za mfululizo.)" 77. al-Mufid, Kitab al-Irshad, Tarjuma ya I.K.A. Howard (London:Muhammad Trust) uk. 243-244; na Rijal ya al-Kashshi kama ilivyonukuliwa na Qummi, op. cit., j. 1, uk. 157. Abu Khalid al-Tammar anasema kwamba siku moja ya Ijumaa walikuwa wanasafiri kwa mashua katika mto wa Frati (Euphrates), ambao dharuba ilizidi kuwa kubwa, Miytham alitazama juu na akawaambia wateremshe nanga na kuisalimisha mashua kwa sababu dalili zilionyesha kwamba dharuba ingekuwa na nguvu sana. Halafu akasema kwamba takriban katika muda huo huo Muawiyah alifariki dunia. Watu waliandika tarehe hiyo, ambayo baadaye ilithibitika kuwa sahihi.78

Shaykh Kashshi anasimulia kwamba siku moja Miytham al-Tamar alikuwa anapita karibu na kundi la watu wa kabila la Asad, wakati Habib bin Muzahir alifika hapo. Wakasimama na kuanza kuzungumza. Habib akasema: "Imekuwa kama vile ninamtazama mzee (ambaye anakipara na ambaye ana tumbo kubwa, na anauza tende na matikiti maji) kwamba amekamatwa, na maadui zake wamemsulubu kwa sababu ya kuipenda familia ya Mtume halafu wameto-boa tumbo lake.' Sifa zote hizo zilikuwa zalengwa kwa Miytham, ni sifa zake." Miytham akajibu: "Mimi pia ninamtazama mtu (ambaye uso wake ni mwekundu) ambaye atakuja kumsaidia mtoto wa Mtume na atauawa kishahidi na kichwa chake kitapelek-wa Kufah." Alimaanisha Habib bin Muzahir. Halafu kila mmoja wao alielekea njia yake. Watu waliosikia mazungumzo haya wakasema kwamba walikuwa hawajapa-ta kuona mtu yeyote muongo zaidi kama hao wawili (Miytham na Habib.) 78. Qummi, op. cit., j.1, uk. 157 Wakati huo huo Rushayd al-Hujri (ambaye pia alikuwa miongoni mwa marafiki wa karibu sana wa Imamu Ali na alipewa ujuzi wa mambo yajayo) alifika hapo na akauliza kama walimuona Habib kwa dhihaka. Rushayd akasema "Mwenyezi Mungu na amwie radhi Miytham! Alisahau kusema kwamba mtu ambaye angekipata kichwa cha huyo mtu mwenye uso mwekundu angepata dinari mia moja zaidi ya wengine kama zawadi." Rushayd alipoondoka watu wakasema kwamba yeye alikuwa muongo zaidi ya wale wawili.79. Baada ya muda mfupi utabiri wote ulitimia kikamilifu: Miytham alisulubishwa, Habib aliuawa kishahi-di huko Karbala, na mtu aliyepeleka kichwa cha Habib, Kufah alizawadiwa dinari mia moja zaidi. Amiri wa Waumini Ali alikwisha mwambia Miytham: "Baada yangu, utakamatwa na watakusulubu na wataku-choma kwa mkuki siku ya tatu damu itatokea puani na mdomoni na ndevu zako zitakuwa nyekundu kwa sababu ya kudondokewa na damu yako. Sharti ungoje rangi hiyo ya nywele. Watakusulubu mlango-ni kwa Amr bin Hurayth na wenzako tisa; na msalaba wako utakuwa mfupi kuliko mingine lakini hadhi yako kwa Mwenyezi Mungu itakuwa ya juu zaidi. Njoo; nikuonyeshe mti ambao utatumika kukusulubu wewe." Halafu akam-wonyesha Miytham mti huo.80. 79. Kashshi, Rijal kama ilivyonukuliwa na Qummi, op. cit., j. 1, uk.143-4. 80. Qummi, op. cit., j. uk. 157; al-Mufid, op. cit., uk. 244.

Hadithi nyingine inasema kwamba Ali bin Abi Talib alimuuliza Miytham; "Utakuwa na msimamo gani hapo wakati mwanaharamu katili wa Bani Umayyah (yaani Ubaydullah bin Ziyad) atakulazimisha kunilaani na kuni-tukana mimi?" Miytham akasema, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, kamwe sitafanya hivyo." Ali akasema: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu usipokubali kufanya hivyo watakuua na kukusulubu." Miytham akasema kwamba angevumilia maovu yote hayo, na kwamba mateso ya aina hiyo hayawi chochote katika njia ya Mwenyezi Mungu. Halafu Ali akam-pa biashara zenye kheri: "Ewe Miytham, utakuwa pamoja nami kwenye daraja langu huko peponi."81. Baada ya Ali kuuawa kishahidi, Miytham alifanya tabia ya kwenda karibu na mti huo na kusali hapo. Alikuwa akisema, "Mwenyezi Mungu na akuneemeshe wewe, Ewe mti; nimeumbwa kwa ajili yako, na wewe unakua kwa ajili yangu." Kila alipokutana na Amr bin Hurayth, alimwambia: "Ninapotembelea jirani na kwako, lazima ukumbuke haki yangu kwamba mimi ni jirani yako." 82. Mnamo mwaka wa 60 A.H. Miytham alikwenda Umrah (hija ndogo). Kule Madina alitembelea nyumba ya Umm Salamah, mke wa Mtume. Alipojitambulisha, Umm Salamah akasema, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mara nyingi nilimsikia Mtume anakupendekeza wewe kwa Ali bin Abi Talib usiku wa manane." 81. Ibid 82. Ibid Miytham alikuwa na haraka hivyo alimwambia Umm Salamah afikishe salamu zake kwa Imamu Husein na amwambie kwamba baada ya muda mfupi "tutakutana kwa Mwenyezi Mungu."

Umm Salamah akamwambia mfanyakazi wake kupaka mafuta uzuri kwenye ndevu za Miytham. Kupaka mafuta uzuri kwenye ndevu ilikuwa alama ya kuonyesha heshima ya juu kwa mhusika katika mila za Kiarabu. Baada ya hapo Miytham akasema: "Ewe Mama wa Waaminio, umepaka mafuta uzuri kwenye ndevu zangu; lakini muda mfupi ujao zitapakwa rangi ya damu yangu kwa ajili ya kuwapenda nyinyi, Ahlul Bayt." Umm Salamah akasema kwamba Imamu Husein alikuwa anamkubuka yeye sana. Miytham akasema: "Mimi pia nina mkumbuka kila mara; lakini sasa hivi nina haraka,a na kuna hatima inayotungojea mimi na yeye, na wote tutafika hapo." Alipotoka nje, Miytham akakutana na Abdullah bin Abbas na akamwambia amuulize chochote kila alichotaka kujua kutoka kwenye tafsiri ya Qur'ani, kwani "Nimesoma Qur'an kutoka kwa Amiri wa Waaminio na ninajua sehemu mbili kuteremka kwake (tanzil) na tafsiri (tawil)." Bin Abbas akaomba karatasi na wino na akaanza kuandika imla ya Miytham. Kwamba mtu wa daraj a la Abdullah bin Abbas hakudharau kuandika imla ya Miytham inaonyesha heshima kubwa aliyopewa katika kundi la wenye elimu ndani ya jamii ya Kiisilamu83. 83. Ibid

Halafu Miytham akasema: "Hisia zako zitakuwaje, Ewe Bin Abbas, utakaponiona mimi ninauawa kishahidi na wenzan-gu tisa?" Bin Abbas aliposikia taarifa hii, akaanza kuchana karatasi, huku akisema kwamba Miytham amekuwa mchawi. Miytham akasema, Usipasue karatasi hiyo. Endapo utona kwamba yale niliyokwambia hayajatokea, basi utakuwa na muda mwingi sana wa kupasua karatasi hiyo84. Baada ya umrah, Miytham akarudi Kufah. Wakati alipokuwa safarini, Ubaydullah bin Ziyad aliteuliwa kuwa gavana wa Kufah. Siku moja Ubaydullah akamuuliza mpasha habari wa kitongoji jijini Kufah kuhusu Miytham. Alipoambiwa kwamba Miytham alikwenda umrah, akamwambia mpasha habari huyo kwamba kama angeshindwa kumleta (kumtoa) Miytham, angeuawa yeye badala yake. kwa hiyo, mpasha habari alikwenda Qadisiyyah kumngoja Miytham. Alipofika Qadisiyyah, Miytham akakamatwa na kufikishwa kwa Bin Ziyad. Watu wakamwambia Bin Ziyad kwamba Miytham alikuwa karibu sana na Ali bin Abi Talib kuliko wote. Bin Ziyad akashangaa: "Hivi Ali alikuwa anamwamini huyu Mwajemi (asiye Mwarabu) sana?" Halafu mazungumzo yaliendelea ifuatavyo: Bin Ziyad: "Yu wapi mlinzi wako?" Miytham: "Anawangojea waovu, na wewe ni mmoja wao." Bin Ziyad: "Unadiriki kusema hivyo mbele yangu? Sasa unayo njia moja tu ya kuokoa maisha yako: lazi- ma umlaani Abu Turab." Miytham: "Simjui Abu Turab ni nani." 84. Ibid Bin Ziyad: "Mtukane na umlaani Ali bin Abi Talib." Miytham: "Utafanya nini nikikataa?" Bin Ziyad: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu nitakuua." Miytham: "Bwana wangu (yaani Ali) aliwahi kunitaarifu kwamba wewe ungeniua na kunifanya mimi na wengine tisa kuwa mashahidi, pale kwenye mlango wa nyumba ya Amr bin Hurayth."

Bin Ziyad: "Sitafanya hivyo kuthibitisha kwamba bwana wako ni muongo." Miytham: "Bwana wangu hakusema uongo wowote. Chochote kile alichosema, alisikia kutoka kwa Mtukufu Mtume, ambaye naye alisikia kutoka kwa malaika Jibril, ambaye naye alisikia kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Jinsi gani wewe utathibitisha uongo wao? Si hivi tu , hata nina-jua jinsi utakavyoniua na mahali utakapo nifanya mimi shahidi. Na ninajua kwamba nitakuwa mtu wa kwanza kati-ka Uislamu ambaye atafungwa hatamu mdomoni ili nisiongee na mtu wa kwanza ambaye ulimi wake utakatwa." Bin Ziyad akamfunga jela Miytham na Mukhtar bin Abu Ubaydah al-Thaqafi. Miytham akamtaarifu Mukhtar kwamba yeye angeachiwa huru na kwamba angelipa kisasi cha damu ya Imamu Husein na angemuua mtu huyu (yaani Bin Ziyad.) Na ilitokea kwamba Mukhtar alipochukuliwa kwenda kuuawa, mjumbe alifika hapo kutoka kwa Yazid akiwa na amri ya kumwachia huru Mukhtar. Halafu Miytham akatolewa nje na akasulubiwa kwenye mti uliokuwa mlangoni kwa Amr bin Hurayth. Sasa ndipo Amr akaelewa nini ilikuwa maana ya ombi lakeMiytham, na kwa hiyo, alimuamuru mtumishi wake kuchoma ubani kwenye msalaba wake na kufagia ardhi chini yake. Miytham akaugeuza msalaba kuwa mimbari. Akaanza kusimulia hadithi za Mtukufu Mtume akizikweza sifa na ubora wa Ahlul Bait, na pia hadithi kuhusu uovu wa Banu Umayyah na kulaaniwa kwao katika Qur'an na hadithi, na jinsi watakavyo angamizwa. Bin Ziyad aliarifiwa kuhusu ujasiri huu usio wa kawaida na moyo wa kujitolea wa Miytham. Alihofu isije mihadhara ya Miytham ikawafanya umma kuwapinga Banu Umayya na kuwafedhehesha mbele ya watu. Kwa hiyo aliamuru kwamba mdomo wa Miytham ufungwe hatamu ili asiongee. Baada ya muda, ulimi wake ulikatwa. Siku ya tatu, mtu mmoja akamjeruhi Miytham kwa mkuki akisema: "Ninakujeruhi licha ya kwamba ninatambua kwamba kila mara ulifunga saumu wakati wa mchana na unasimama usiku kucha ukisali."

Jioni ya siku hiyo damu ilitokea puani na mdomoni, ikafanya uso na kifua chake kuwa na rangi nyekundu, na akafariki dunia. Miytham aliuawa kishahidi kwa ajili ya Uislamu, siku kumi kabla ya Imamu Husein hajafika Karbala. Maana yake ni kwamba Miytham alikufa tarehe 21 au 22 Dhul hijjah, 60 A.H. Wakati wa usiku wauza tende saba waliuchukua mwili wake kwa siri na kumzika kwenye ukingo wa mfereji na kufuta alama za kaburi. 85. Baadaye wakati hapakuwepo na hatari, kaburi lilidhihirish-wa kwa watu. Leo hii imekuwa ni sehemu ya heshima kubwa ambapo wafuasi wa dini huenda kuhiji. 85. Ibid. uk. 158-9. Neema mojawapo ya Mwenyezi Mungu aliyopewa Miytham ilikuwa kwamba elimu na uchajimungu ilibakia kwa dhuria wake, kizazi hata kizazi. Watoto wake, wajukuu zake na vitukuu vyake walikuwa miongoni mwa masahaba wa kuheshimiwa na Maimamu wa Kishia. Miytham alikuwa na watoto sita: Muhammad, Shuayb, Salih, Ali, Imran na Hamzah. Wote walikuwa miongoni mwa masahaba wa Imamu wa nne, tano na sita. Miongoni mwa wajukuu zake, Ismail, Yaqub na Ibrahim (wote watoto wa Shuayb) walikuwa masahaba wa Imamu wa tano, sita na saba. Ali bin Ismail bin Shuayb bin Miytham anahesabiwa miongoni mwa wana theolojia mashuhuri wa madhehebu ya Shia. Mazungumzo yake na maadui zake yanaonyesha ujuzi, akili yake na uimara wa akili yake. Zaidi ya hayo tunaona majina mengine mengi miongoni mwa dhuria wa Miytham yametajwa kwenye vitabu vya hadithi na wasifu.