• Anza
  • Iliyopita
  • 6 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 17445 / Pakua: 3988
Kiwango Kiwango Kiwango
UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

4

3

UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

Katika kipindi chote cha historia ya Kiislamu, tunaona watumwa wakipanda siyo tu katika nyadhifa za utawala bali hata katika Ufalme pia. Katika maneno ya Will Durant, "Inashangaza ni watoto wangapi wa watumwa wamepanda katika nafasi za juu katika usomi (kitaaluma) na Kisiasa, katika ulimwengu wa Kiislamu; ni wangapi, kama vile Mahmud na wale Mamelik wa mwanzo, walikuja kuwa Wafalme. o Subktagin wa Ghazni na mtoto wake, Mahmud (mfalme mpiganaji maarufu ambaye aliishambulia India mara kumi na saba) walikuwa watumwa na watoto wa watumwa mtawalia. Utawala wa kwanza wa Kinasaba wa Kiislamu wa nchini India nao pia uliundwa na utawala wa kinasaba wa watumwa. Kabla ya kuifunga sura hii, ni lazima nisisitize nukta moja: Wale wafungwa wote au watoto wa wafungwa ambao wali-fika kilele cha heshima kiroho au Kisiasa -hawakufanywa hivyo kamwe kwa sababu ya kuwa watumwa au watoto wa watumwa; bali walifikia daraja hizo kwa sababu walikuwa Waislamu waliokuwa na uwezo. Daraja zao za kiutumwa au kuachiwa huru kamwe halikuongezeka au kupunguza nafasi za mafanikio yao; kamwe haukurahisisha wala kuzuia kufikia lengo lao la maisha. Jamii ya Kiislamu, shukurani kwa sheria madhubuti za Uislamu na Mtume Muhammad, walikuwa vipofu-kirangi na vipofu-kihadhi (yaani Uislamu haufadhilishi rangi au hadhi ya mtu). Jambo moja tu lililo-husika lilikuwa ni uwezo wa kufanya jambo au kitu ambao mwanamume au mwanamke alikuwa nao.

Mafanikio haya, yaliyo patikana miaka 1400 iliyopita, ni kilio cha tofauti sana kutokaka na kushindwa kwa dhahiri 105. Durant, W., The Story of Civilization, j. 4, uk. 209. kwa Ukristo katika miaka hii ya 1960 ambako, katika nchi ya Kikristo ya Amerika (U.S.A) kama mtu mweusi (Mnegro) anakuwa Meya (wa Jiji) inaonekana ni habari kubwa; na wakati ambapo katika mwaka 1971 serikali ili-panga kumpandisha cheo mwanajeshi wake wa kwanza mtu mweusi kuwa admiral (mkuu wa jeshi la wana maji), aliyeitwa Kapteni Samwel Lee Granely. Unaona kidokezi cha habari hizi. Mtu fulani kutoka jamii ya watu weusi (Manegro) anachaguliwa na kupandishwa cheo kwa misingi ya kisiasa kwa sababu ni mtu mweusi (Mnegro). Lakini ingekuwa hasa hasa ni sifa zake tu za kib-inafsi, jina hili lisingekuwa ni jambo la kutangazwa na kuenezwa kila mahali! Aina kama hiyo ya ubaguzi wa rangi na kujiona ilikuwa, na hata sasa haifikiriki katika Uislamu.

Hivyo basi, ni dhahiri kwamba Uislamu ulifanikiwa mahali ambapo kila dini nyingine na mifumo imeshindwa mpaka sasa. Uislamu uliwachanganisha watumwa katika jamii ya Waislamu bila kujali rangi zao au asili. Kuamua kutokana nakumbu kumbu zake zenyewe (zilizo za kweli), hatuwezi ila kushanga mafanikio makubwa ya Uislamu katika uwan-ja wa nyanja hii.

CHIMBUKO LA WATUMWA WEUSI

Sasa tumeona msimamo wa Uislamu kuhusu utumwa, hebu ngoja tuuangalie Ukristo na wafuasi wake, na tuone wali-fanya nini kuhusu suala hili. Inashangaza kuona kwamba Wakristo, ambao kwa sababu wanazo zijua wao, siku hizi wanajifanya kama mabingwa wa uhuru wa mwanadamu, kumbe wao ndiyo mawakala wa dhahiri na watetezi wakub-wa wa mfumo huu wa utumwa. Walivumbua falsafa na uthibitisho wa kimaadili, kama sababu za kuwafanya watumwa watu "wasio staarabika." Mojawapo ya hoja zao ni kwamba walikuwa wana waokoa watu hao (watumwa) kutoka kwa majirani zao wanaokula watu hapa duniani, na kutoka kwenye fedheha ya daima milele baada ya uhai wa hapa duniani. Uislam na wafuasi wake kamwe hawakuwa na fikira kama hizo. Wingi mno wa maandiko ya Kiisilamu hauna kitu kama hicho, kutokana na aina hii ya jitihada ya uadilishi wa kusikitisha. Lakini waandishi wa Kikiristo kila mara hutaja biashara ya utumwa kama vile wao hawakuhusika kwa vyovyote vile na tatizo hili, na kwamba ni Uislam ndio ambao "ulihimiza na kuhalalisha utumwa" ambapo wao, Wakristo, kila mara walijaribu kukomesha mpango huu mbaya sana! Haya ndiyo maelezo ya waandishi wa Kikristo.

Ni jambo la kuvutia kuona kwamba wakati wanapo zungumzia kuhusu biashara ya watumwa ya Afrika ya Magharibi ambayo ilifanywa kikamilifu na Wakristo peke yao, waandishi na wanahistoria wa Kikristo, wameipa biashara hii jina la "West African Slave trade," Yaani biashara ya utumwa ya Afrika ya Magharibi au "Atlantic Slave - Trade" yaani biashara ya utumwa ya Atlantic, lakini wanapotoa maelezo kuhusu suala hili kwa upande wa Afrika ya Mashariki, hubadili maneno na kuandika "Arab Slave Trade" yaani biashara ya utumwa ya Waarabu. Ukristo, kwa kutumia propanganda ya udanganyifu wa jinsi hii, umefaulu kwa kiwango kikubwa kupanua uwanja wa athari zake miongoni mwa Waafrika ambao humo umeweka mkakati wa propaganda yake na wanafurahi sana lakini hawatambui ukweli kwamba makanisa ya Kikristo yalikuwa washiriki wenye bidii sana kwenye "African Slave Trade" (biashara ya utumwa ya Kiafrika). Sura zifuatazo zitaonye-sha picha ya kweli kwa wasomaji.

Mnamo mwaka wa 1492, ambapo Columbus, akiwakilisha ufalme wa Hispania aligundua "New World" (Dunia mpya), alianzisha mfululizo mrefu na mchungu wa ushindani wa kimataifa katika kujipatia makoloni, ambao hadi sasa baada ya karne nne na nusu, hakuna suluhu iliyopatikana. Ureno, ambayo ndio iliasisi kitendo cha kujipanua kimataifa, ilidai hizo nchi mpya kwa hoja ya kwamba zilikuwa kwenye eneo la madaraka ya amri ya baba mtakatifu (papal bull) wa 1455 inayowaruhusu wareno (ambao ni Wakristo) kuwafanya watumwa wapagani wote. Katika kujaribu kuepuka ubis-hani, mamlaka hizi mbili, zilitafuta suluhisho, na kwa sababu zote zilikuwa katika madhehebu ya Ukatoliki, zil-imwelekea Baba Mtakatifu - hatua ambayo ilikuwa ya kawaida na ya mantiki katika kipindi ambapo madai ya wakati wote ya Kipapa yalikuwa bado hayana upinzani ama kutoka kwa mtu binafsi au serikali ya nchi. Baada ya kuchunguza kwa makini madai ya washindani, Baba Mtakatifu, katika mwaka 1493, alitoa mfululizo wa amri za kipapa ambazo ziliweka mipaka ya kuaua kati ya makoloni yanayomilikiwa na dola hizo mbili za Ulaya: Mashariki ilichukuliwa na Ureno na Magharibi ilichukuliwa na Hispania. Mgawanyo huo, hata hivyo, haukukidhi mategemeo ya Ureno na mwaka uliofuata washindani hao wawili walifanikiwa kuhitimisha mwafaka wa maridhiano zaidi kwenye Mkataba wa Tordesillas ambao ulirekebisha uamuzi wa Baba Mtakatifu kuiruhusu Ureno kumiliki B 106. Williams, Dk. Eric, Capitalism and Slavery (London, 1964) P. 4. kama koloni lake.

Lakini maamuzi haya hayakuweza kuzifunga mamlaka zingine ambazo zilikuwa zina wania kunyakua makoloni mengi iwezekanavyo; Uingereza, Ufaransa, na hata Uholanzi zilianza kudai sehemu zao (makoloni) hapa duni-ani. Mtu mweusi, pia, alikuwa apate sehemu yake, licha ya kwamba hakuomba; ilikuwa uanzishwaji na upanukaji wa mashamba makubwa ya miwa, tumbaku na pamba ya ulimwengu Mpya. "Kwa mujibu wa Adam Smith, maendeleo ya koloni jipya yalitegemea jambo moja rahisi la kiuchumi- 'ardhi pana yenye rutuba.' Hata hivyo, umiliki wa makoloni wa Uingereza hadi 1776, kwa ujumla unaweza kugawanywa katika aina mbili. Aina ya kwanza ni wakulima wadogo wanao jitosheleza na kushughulika na uchumi wa bidhaa mbalimbali. Aina ya pili ni koloni ambalo limesheheni hali iwezeshayo mtu kuzalisha bidhaa kuu mbali mbali kwa wingi kwa madhumuni ya kuuza nje. Katika aina ya kwanza, yalikuwemo makoloni ya Kaskazini ya bara la Marekani; katika aina ya pili, yalikuwepo makoloni ya tumbaku na visiwa vya miwa vya Caribbean. Kwenye makoloni; ardhi na mtaji havikuwa na manufaa bila ya kuwepo nguvu kazi ya musuli. Kibarua, lazima awepo wakati wote na lazima afanye kazi, au ahimizwe kufanya kazi, katika kundi moja. Bila ya sharti hili, kibarua angeamua kuwa na mwelekeo wake binafsi na kufanya kazi katika ardhi yake mwenyewe. Hadithi moja inasimuliwa mara nyingi kuhusu kabaila mmoja wa Uingereza, Bwana Pell, ambaye alichukua pauni za Kiingereza elfu hamsini (50,000) na vibarua mia tatu akaenda nao kwenye koloni la Swan River huko Australia.

Mpango wake ulikuwa kwamba vibarua hao wangefanya kazi kwake, kama iliyvokuwa Uingereza. Bwana Pell akawasili Australia ambapo ardhi ilikuwa pana sana vibarua wakapendelea kufanya kazi kwenye mashamba yao madogo kwa manufaa yao kama wamiliki wadogo, badala ya kufanya kazi chini ya kabaila kwa kulipwa ujira. Austaralia haikuwa Uingereza, na kabaila huyo alibaki hana mtumishi wa kumtandikia kitanda au wa kumchotea maji." CHIMBUKO LA WATUMWA WEUSI "Ni njia ya kuchukiza," ingawa inaweza kuwa hivyo, kama Merivalle alivyoiita, utumwa ulikuwa taasisi ya kiuchumi yenye muhimu wa kwanza. Utumwa ulikuwa ndiyo msingi wa uchumi wa Ugiriki na ukajenga Ufalme wa Kirumi. Katika zama hizi utumwa ulizalisha sukari kwa ajili ya chai, na vikombe vya kahawa vya dunia ya Magharibi. Ulizalisha pamba ikiwa ndiyo msingi wa Ukabaila mambo leo. Utumwa ulijenga Marekani (US) ya Kusini na visiwa vya Caribbean."108. "Ulaya ikiwa na watu wachache katika karne ya kumi na sita, hivyo kwamba, vibarua wa kulima bidhaa muhimu kama miwa, tumbaku na pamba katika Dunia Mpya hawangepatikana kwa idadi ya kutosheleza kuruhusu uzal-ishaji wa kiwango kikubwa. Utumwa ulikuwa muhimu kwa lengo hili na ili kuweza kuwapata watumwa, wazungu walianza kwanza kuwatumia Waaborigine kama watu- 107. Ibid uk. 4-5 108. Ibid 109. Ibid, uk. 6 Lakini utumwa wa Kihindi kamwe haukuwa mkubwa kwenye makoloni ya Uingereza... Kwa upande wa Wahindi... utumwa ulionekana kama jambo lilotokealo mara chache, kama kinga ya adhabu na si kama ndiyo hali ya kawaida na ya kudumu. Katika makoloni ya New England, utumwa wa Wahindi haukuwa na faida, kwani utumwa wa aina yoyote ulikuwa hauna faida kwa sababu haukustahili kwenye kilimo cha mazao mbalimbali ya makoloni haya. Juu ya haya, mtumwa wa Kihindi alikuwa hawezi kufanya kazi kwa bidii. Wahispania waligundua kwamba mtumwa mweusi mmoja alikuwa sawa na watumwa wanne wa Kihindi. Afisa mmoja mashuhuri wa Hispaniola alisisitiza mnamo mwaka 1581 kwamba itolewe ruhusa ya kuwaleta watu weusi, jamii iliyo kakamavu kwa kazi badala ya wazawa ambao ni dhaifu sana hivyo kwamba wanaweza kuajiriwa kwenye kazi ndogo zisizo hitaji matumizi ya nguvu nyingi kama vile kutunza mashamba ya mahindi.... Bidhaa za siku za usoni za "New World," yaani miwa na pamba, zilihitaji nguvu ambazo watumwa wa Kihindi walipungukiwa na wakataka "mtu mweusi wa pamba" aliye mkakamavu kama ambavyo miwa inahitaji nyumbu wenye nguvu ambao hupatikana Louisiana, wenye kisifa cha jina la 'nyumbu wa sukari.' Kwa mujibu wa Lauber, inapolinganishwa kiasi cha malipo kilichotolewa kwa mtu mweusi (Mnegro) kwa wakati huo huo na kwa mahali hapo hapo, utaona kwamba bei za watumwa wa Kihindi zinaonekana kuwa za chini mno.

Wingi wa nguvu kazi ya Kihindi, pia, ilikuwa ndogo, ambapo vibarua wa Kiafrika walikuwa hawaishi. Kwa hiyo, watu weusi (Manegro) waliibiwa kutoka hapa Afrika kwen-da kufanya kazi kwenye ardhi, iliiyoporwa (na kuibiwa) kutoka kwa wazalendo wa Kihindi (Wahindi wekundu) huko Marekani. Misafara ya baharini ya Prince Henry the Navigator (Mfalme Henry Baharia mvumbuzi) ilikamilisha ile ya Columbus, historia ya Afrika ya Magharibi ikawa kamilisho la historia ya West Indians." (Wahundi wa Magharibi)110.

WAKRISTO WANAPANGA BIASHARA YA UTUMWA

Watumwa walikuwa wanachukuliwa kutoka hata katika wakati wa Ufalme wa Kirumi, lakini "biashara halisi ya Utumwa" ilianza mnamo karne ya 16 baada ya ujio wa mataifa ya Kikristo ya Ulaya. Edward A. Alpers wa Chuo Kikuu cha Dar- es Salaam, anaandika kwamba; "kama tunavyoleta utofautisho baina ya biashara inayoambatana katika watumwa ambayo ilichuruzika katika sahara kutoka magharibi mpaka kaskazini ya Afrika kuanzia siku za nyuma sana za wakati wa utawala wa Ufalme wa Kirumi, kwa upande mmoja, na kioja tunacho kiita The West African Slave Trade kwa upande mwingine, kwa hiyo lazima tulete tofauti hiyo hiyo kwa Afrika ya Mashariki." 111 Walter Rodney pia wa Chuo, Kikuu cha Dar es Salaam, anaanza kuandika kijitabu chake "West Africa and the Atlantic Slave-Trade kwa maneno yafuatayo: - Wakati wote lazima ikumbukwe kwamba biashara ya utumwa iliyo;fanyi-ka katika bahari ya Atlantiki" lilikuwa ni tukio katika historia ya dunia, iliyo husisha mabara matatu - Ulaya, Afrika na Marekani. 110. Ibid, UK. 8-9 111. Alpers, Edward A., East Africa Slave-Trade (Dar-es-Salaam: The Historical Association of Tanzania, 1967) Watu walio toka kwa dhamira ya kutafuta watumwa walikuwa Wazungu waliotoka katika kila nchi kati ya Sweeden kwa upande wa Kaskazini na Ureno kwa upande wa magharibi. Wareno walifika Afrika ya Magharibi muda mfupi kabla ya kuingia nusu karne ya kumi na tano. Mara moja na kwa haraka sana walianza kukamata (watumwa) Waafrika na kuwapeleka kufanya kazi Ulaya kama watumwa, hususan katika Ureno na Hispania. Lakini maendeleo muhimu sana kwa biashara hii ya utumwa yalikuwa katika karne ya kumi na sita, ambapo mabepari wa Kizungu walitambua kwamba wangepata faida kubwa sana kwa kutumia nguvu-kazi ya Waafrika kuujenga na kuuen-deleza utajiri wa nchi zote za Amerika. Matokeo yake, Waafrika walipelekwa Amerika ya kaskazini, Amerika ya kati, Amerika ya kusini na Visiwa vya Caribbean kwa ajili ya kukidhi haja ya nguvu-kazi ya watumwa kwenye machimbo ya dhahabu na shaba, na kwenye mashamba ya kilimo cha mazao ya miwa, pamba na tumbaku. Biashara hii mbaya ya kununua na kuuza binadamu ilidumu kwa kipindi cha miaka (400) mia nne, kwani Atlantic slave-Trade (Biashara ya Utumwa wa kupitia bahari ya Atlantiki) ilikoma mwishoni mwa miaka ya 1870.

"Mambo mengi yanaweza kusemwa kuhusu jinsi Biashara ya Utumwa katika bahari ya Atlantiki ilivyopangwa huko Ulaya, na kuhusu faida kubwa iliyokusanywa na nchi kama Uingereza na Ufaransa. Mambo mengi yanaweza kusemwa kuhusu safari za kutisha kutoka Afrika hadi Marekani kuvu-ka bahari ya Atlantic. Waafrika walipangwa kama dagaa kwenye meli za kubeba watumwa, na matokeo yake walik-ufa wengi sana." 112. 112. Rodney, Walter., West African and the Atlantic slave-trade (Dares-Salaam: The Historical Association of Tanzania, 1967) Na dagaa walioje! Kwa maelezo zaidi kuhusu upakiaji huu wa watumwa kwenye meli, soma taarifa ifuatayo: -Moja ya hati yenye kuuvunja moyo sana katika nyaraka zote zinazotisha ni "Plan of the Brookes," mpango mbaya sana wa karne ya kumi na nane wa kupanga watumwa kwenye meli ya kubeba watumwa 'Brookes'... Kwa mahesabu sahi-hi, teknolojia ya kushtua ilitengenezwa - futi na inchi, chumba cha kusimama na nafasi ya kupumua iliwekwa kwa matumaini ya faida kubwa. Mtu mmoja Bwana Jones anapendekeza kwamba wanawake watano wahesabiwe kama wanaume wanne, na wavulana watatu au wasichana watatu wafanywe kuwa sawa na watu wazima wawili kila mtumwa mwanaume aruhusiwe futi sita kwa futi moja na inchi nne (1'4"x6') kama nafasi ya chumba chake, kila mwanamke alipewa nafasi ya upana wa futi tano na inchi kumi na futi moja na inchi nne.... (5'10"x1'4"); na inaen-delea hivyo mpaka kila mtu anapata nafasi - watumwa 451. Lakini Muswada wa Bunge unaruhusu watumwa 454. Kwa hiyo hati hiyo inahitimisha kwamba kama watumwa watatu zaidi wangeweza kuwekwa kwa kubanwa katikati ya wale waliotamkwa kwenye mpango, mpango huu ungeweza kuchukua idadi ile ile ambayo imeelekezwa kwenye muswada. 113.

Mara Waafrika walipofikishwa upande mwingine wa bahari ya Atlantic, kwa hakika walikuwa katika "Dunia Mpya", iliyojaa ukandamizaji na ukatili. Taarifa ifuatayo inaweza kusaidia kuelewa hali ilivyokuwa wakati huo. Rodney anaandika: 113. Newsweek (March 15, 1965) uk. 106 "Kuanzia wakati walipofika (Wakristo) Wazungu hadi 1600, takriban Waafrika milioni moja (1, 000,000) walichukuliwa kwenye meli za kubeba watumwa. Wakati wa kipindi hicho, Wareno walikuwa ndio wafanya biashara wakuu wa biashara ya watumwa huko Afrika ya Magharibi. Ama wali-wapeleka Waafrika huko Brazil, ambayo nchi hiyo ilikuwa koloni lao, au vinginevyo waliwauza kwa waloezi wa Kihispania huko Mexico, Amerika ya kati, Amerika ya Kusini na visiwa vya Caribbean. Mnamo karne ya kumi na saba, kiasi cha Waafrika wapatao milioni saba hadi nane kutoka Afrika ya magharibi walivushwa bahari ya Atlantic. Wadachi walijumuika na Wareno kama wafanya biashara wakuu wa biashara ya utumwa mnamo karne ya kumi na saba, na karne iliyofuata Waingereza wakawa wafanya biashara wakubwa kushinda wote wa biashara ya utumwa. Wakati biashara ya Utumwa katika bahari ya Atlantiki ilipofikia kileleni mnamo karne ya kumi na nane, meli za Kiingereza zilikuwa zinachukua zaidi ya nusu ya jumla yote ya watumwa na idadi iliyobaki iligawanywa baina ya Wadachi, Wafaransa, Wareno na Wadane (Danish).

"Ilipofika karne ya kumi na tisa, palikuwepo na mabadiliko mengine ya watu ambao walishika nafasi mbele katika kuinyonya Afrika. Nchi za Ulaya zenyewe hazikushiriki kikamilifu kwenye biashara ya utumwa, lakini badala yake Wazungu ambao waliloea Brazil, Cuba, na Amerika ya Kaskazini ndio ambao walipanga sehemu kubwa ya biashara. waamerika (U.S.A) ndiyo katika kipindi hicho hicho tu walipata uhuru kutoka kwa Waingereza, hili lilikuwa taifa jipya (U.S.A.) ambalo lilikuwa na mgawo mkubwa kabisa kuliko wote katika biashara ya watumwa katika biashara ya Atlantiki katika kipindi cha miaka hamsi-ni ya mwisho, kwa kuchukua kiwango kikubwa zaidi cha watumwa kuliko ambavyo imewahi kufanya huko nyuma. "Ilipoanza "biashara ya watumwa ya Atlantiki kwenye pwani ya Afrika ya Magharibi, ilichukua utaratibu wa kutu-mia nguvu moja kwa moja wa Wazungu kuwashambulia Waafrika waliokuwa wanaishi karibu na pwani. Mabaharia wa kwanza wa Kireno walipofika kwenye pwani inayoju-likana leo kama Mauritania, waliacha meli zao na kuanza kuwawinda watu waitwao, Moors watu walioishi katika jimbo hilo. Kwa kweli, hii haikuwa biashara hata kidogo -ilikuwa uvamizi wa nguvu. Hata hivyo, baada ya masham-bulizi kadhaa ya kushtukizwa, Waafrika wa pwani wakawa na kawaida ya kulinda kwa zamu na walijilinda kwa nguvu dhidi ya washambuliaji wao Wazungu. Katika kipindi kifupi tu, Wareno walitambua kwamba uvamizi haikuwa mbinu inayofaa na iliyo salama katika kujaribu kuwapata watumwa. Zaidi ya hayo, pia walitaka dhahabu na bidhaa zingine za Kiafrika, ambazo wangeweza tu kuzipata kwa njia ya kununuliana na kuuziana kwa amani.

Kwa hiyo badala ya kuvamia, Wareno waliona afadhali kutumia bidhaa zilizo tengenezwa kiwandani ili kuwatia moyo Waafrika kubadilishana na bidhaa zao na hata kuweza kuwafikisha mateka wa Kiafrika kwenye meli za Wazungu kwa urahisi. Mpango huu haukufanywa na Wareno pekee, lakini hata wazungu wengine wote walitambua na kukubali kwamba huo ulikuwa mpango mzuri zaidi wa kupata bidhaa hapa Afrika; na ilikuwa kwa njia hii waliweza kupata mamilioni mengi ya Waafrika." 114 114. Rodney, op. cit., uk.4-5 Akifafanua juu ya kipengele hiki cha biashara ya watumwa, mwandishi anasema: "Moja ya vitu muhimu sana ni kutam-bua jambo liumalo sana na lisilo pendeza kwamba walikuwepo Waafrika ambao waliwasaidia na kushirikiana na Wazungu katika kuwafanya Waafrika wenzao kuwa watumwa. Maana yake ni kwamba hatuwezi kuchukua msi-mamo dhaifu na kusema kwamba watu weupe walikuwa wabaya sana na watu weusi walikuwa waathirika (katika kuangamia). Mfano unaofaa na sambamba ambao ungeweza kusaidia kuelewa yale yaliyotokea katika Afrika ya Magharibi wakati wa kipindi cha karne za biashara za watumwa unaweza kuonekana hapa Afrika leo, ambapo viongozi wengi wanashirikiana na mabeberu wa Ulaya na Marekani (U. S. A.) kwa lengo la kuwanyonya na kuwakan-damiza Waafrika walio wengi.

Hatimaye, Waafrika wa Afrika ya Magharibi walifikishwa kwenye hali ya "uza au uuzwe." Hapa suala la bunduki lilikuwa na umuhimu maalum. Kuwa na nguvu, serikali ili-hitaji bunduki, lakini ili kupata bunduki kutoka kwa wazungu, Waafrika ilibidi kuwapa Wazungu watumwa na wao kupewa bunduki. Watawala wa Kiafrika walijikuta wenyewe wanawauza watumwa ili wapate bunduki ambazo ziliwawezesha kuwakamata raia wao na kuwauza kama watumwa ili wanunue bunduki nyingi zaidi. Hali hii inaweza kuelezewa, kama "ubaya juu ya ubaya (mzun-guuko unaoashiria kukwama)." Watawala wa Kiafrika ambao waliwasaidia wazungu hawasameheki moja kwa moja, lakini inafafanua jinsi gani mwishoni hawakuwa washirika halisi wa Wazungu bali walikuwa watumishi au vibaraka wa Wazungu." 11 116. Ibid, uk. 7f.

Na kanisa lilikuwa linafanya nini wakati wote huo? Msikilize mwandishi huyu huyu anasema; "Kwa sababu faida kubwa sana ilikuwa inapatikana kwa kuwachukua watumwa kutoka Afrika, Wazungu walikataa kuzisikiliza dhamiri zao. Walifahamu kuhusu mateso yaliyo wapata watu katika Afrika, ndani ya meli za kubebea watumwa na kwenye mashamba yaliyokuwa yanalimwa na watumwa ya Waamerika, na walitambua kwamba kuwauza binadamu wenzao ni jambo ambalo halingethibitishwa kimaadili. Hata hivyo kanisa la Kikristo lilijitokeza na kutoa sababu nyingi likijitetea kuingia kwake katika biashara ya watumwa. Wachungaji wengi walifanya biashara ya watumwa, hasa katika Angola, na wengine wengi walimili-ki watumwa, katika nchi za Amerika. Sababu moja tu ambayo ilitolewa na kanisa Katoliki kuhusu vitendo vyake ilikuwa kwamba lilikuwa kinajaribu kuziokoa roho za Waafrika kwa kuwabatiza watumwa. Waprotestanti walikuwa wabaya zaidi, kwani wala hawakuweka wazi kwamba walikubali kwamba Waafrika walikuwa na roho. Badala yake, walikubaliana na fikira kwamba mtumwa wa Kiafrika alikuwa sehemu ya rasilimali kama fenicha au hayawani wa kufugwa. Hakuna sehemu ya historia ya Kanisa la Kikristo ambayo inafedhehesha zaidi kuliko kusaidia "Biashara ya Utumwa katika Bahari ya Atlantiki."116. Kwa mujibu wa orodha ya Lloyd, iliamuliwa kwamba watumwa walikuwa ni bidhaa, na wenye thamani sana. Hati za bima zilizochukuliwa kutoka Lloyd waliwakatia watumwa hati za bima hadi kufika kiasi cha pauni za Kiingereza 45 kila mtumwa - kiasi hicho cha fedha ni kikubwa katika kipindi hichi cha mwanzoni mwa karne ya 116. Ibid uk.22. 18 huko Uingereza.

Ili kuwazuia watumwa wasitoroke, au kuwaadhibu, nyenzo zisizo za kawaida kama zilivyoorodheshwa hapa zilitumiwa katika Afrika ya Magharibi na katika visiwa vya West-Indies. 117. Siku zote kulikuwepo watu wachache ambao walipinga Biashara ya Utumwa katika Bahari ya Atlantiki. tangu mwanzo; lakini serikali mbalimbali na wafanya biashara hawakuwajali, wakati wa karne ya kumi na tano, kumi na sita na kumi na saba. Haikuwa hivyo, hadi mwishoni mwa karne ya kumi na nane wakati majaribio ya dhati yalifanywa kwa lengo la kukomesha biashara hii. James Boswell, akijaribu kukana hoja za watu waliotaka biashara ya watumwa ikomeshwe, anaandika katika kitabu chake kiitwacho "Life of Johnson." Kwamba: Jaribio la kinyama na la hatari ambalo kwa muda fulani limeendelea kuwepo kwa lengo la kupata sheria ya bunge letu, ili kukomesha tawi la maana sana na muhimu la faida kibi-ashara, lazima lingekwisha amuliwa mara moja, kama isin-gelikuwa kundi lisilo na maana la washabiki waliokuwa msitari wa mbele kwalo bila kufaulu, ndilo ambalo linaunda kundi kubwa la Wakulima, Wafanya biashara na wengineo ambao rasilimali yao imetumbukizwa na kuhusishwa kwenye biashara hiyo, kwa sababu zao kujikinaisha, hufikiria kwamba hapangekuwepo na hatari. 117. Lloyd's list, 250th Anniversary (1734-1984) April 17,1984, London, uk. 149.

Ujasiri ambao jaribio hilo limepata msisimko mshangao wangu na hasira, na ingawa watu fulani wenye uwezo mkubwa wameliunga mkono, ama kwa sababu ya kutaka umaarufu wa muda mfupi, wakati wanao utajiri, au kupenda kujumuika kwenye fitina, wakati hawana kitu, maoni yangu hayatetereki. Kukomesha hali ya kuwepo utumwa ambayo katika zama zote, MUNGU ameruhusu, na binadamu akaen-deleza, haingekuwa unyang'anyi tu kwa tabaka la raia wetu wasio hesabika; lakini pia ingekuwa ukatili mno kwa Washenzi wa Kiafrika, ambao sehemu kutoka miongoni mwao inaokolewa kutoka kwenye mauaji ya kinyama, au kutoka kwenye utumwa isiyovumilika katika nchi yao wenyewe, na huwaingiza kwenye maisha ya hali ya furaha zaidi, hasa zaidi sasa kupita kwao kwenda katika visiwa vya West-Indies na wanavyotendewa huko katika hali ya udhibiti wa kibinadamu. Kukomesha biashara hiyo itakuwa sawa na kufunga milango ya huruma kwa binadamu."H -Marekebisho ya takrima ya kibinadamu wanayofanyiwa na huruma, hujionyesha yenyewe kwenye maelezo ya kina na picha iliyoonyeshwa hapo juu!

5

UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

KWA NINI UTUMWA ULIKOMESHWA

Mtu anaweza akasema: "Hivi haikuwa Uingereza ya Kikristo hatimaye ndio iliyo komesha utumwa? Vema, kama mtu anafanya udhalimu si yeye ndiye anayetakiwa kuen-deleza udhalimu huo? Kama ambavyo imekwisha elezewa, Uingereza ilikuwa ndio mfanya bishara ya watumwa mkub-wa zaidi ya wote, na nguvu za kiuchumi zilipoilazimisha kukomesha biashara ya watumwa, ilifanya hivyo. Je! ni Uingereza inayostahili au Ukristo ndiyo unastahili kupewa shukurani zozote kwa tukio hilo? Kwa nini tusizishukuru nguvu za uchumi ambazo ndizo zililazimisha Uingereza kutokuendelea na biashara hiyo? Ukweli ni kwamba harakati dhidi ya utumwa hazikuon-gozwa na makanisa; kazi hiyo ilifanywa na watu waadilifu wachache ambao vilio vyao vilikuwa havisikilizwi hadi pale umuhimu wa kiuchumi ulipolazimisha Bunge kupitisha muswada mnamo mwaka wa 1870 dhidi ya biashara ya watumwa. Baada ya miaka 26, muswada mwingine ulipi-tishwa kukomesha utumwa katika makoloni ya Uingereza mnamo mwaka 1833. Kama Profesa D.W. Brogan alivyoandika kwenye utangulizi wa kitabu cha Dk. Eric Williams ambacho ni kizuri, kiitwacho "Capitalism and Slavery", "Kukomeshwa kwa biashara ya utumwa halafu kusitishwa kwa utumwa, hayakuwa tu matokeo ya kuboreka kwa kiwango cha mfumo wa maadili ya kisiasa humo Uingereza (ingawaje Dk. Williams hadharau kazi ya watu kama Clarkson kuwa ina umuhimu) lakini ilikuwa namna ya kupunguza hasara. Ukiritimba wa kilimo cha miwa cha visi-wa vya West Indies haukuvumilika kulinganishwa na jamii ya viwanda iliyokuwa inastawi haraka, yenye kujiamini kwa usahihi katika nafasi yake ya ushindani isio tetereka mnamo siku za mwanzo za mageuzi ya viwanda. "Kufupisha, kwa maneno ya Profesa Brogan, mpango wa utumwa ulikuwa "unavumiliwa, unatetewa, unasifiwa almuradi ulikuwa na faida."

"Mpango wa mtumwa ulikuwa na faida sana na kwa kipin-di kirefu. Mafanikio ya Bristol na Liverpool na kwa kiwango fulani, ya Glasgow yalitegemea faida ya mashamba ya miwa ya visiwa vya West Indies. Mkulima wa West Indies alikuwa mshindani wa ufahari wa tajiri mpenda anasa wa East Indies. Ilikuwa kama kupoteza muda kwa waadilifu kuonyesha kwamba kila tofali lililojenga maghala makubwa ya Bristol na Liver pool lilitokana na damu ya Mtu Mweusi. Lakini sauti ya waadilifu ilisikika mara chache sana mion-goni mwa mlio wa sarafu ya Uingereza Guine (jina hilo hilo linakumbusha biashara ya pembe-tatu baina ya Uingereza, Afrika na makoloni ya transatlantic)." "Biashara ya pembe tatu" maana yake ni nini? Kutoka Uingereza, bidhaa mchanganyiko "mfano halisi wa mzigo wa mfanya biashara ya watumwa" ulipelekwa Africa. Mavazi mazuri na umalidadi kwa Waafrika, vyombo vya nyumbani, nguo za kila aina, chuma na metali, pamoja na bunduki, pingu na minyororo." Kutoka Afrika mzigo wa binadamu ulichukuliwa kupelekwa visiwa vya West Indies na nchi za Amerika. Kutoka West Indes na makoloni mengine; sukari, tumbaku na rangi ya buluu, pamba, kahawa na malighafi zingine zilipelekwa nchi mama (yaani Uingereza) ambako yalitengenezwa kwenye viwanda na halafu yakaingizwa tena kwenye makoloni. 135.

Mashamba yalianzishwa kwa sababu ya kuwepo nguvu kazi ya utumwa na yakalindwa na ukiritimba. Halafu ukaja mtengano wa makoloni 13 ya Marekani ambayo yalifunga soko kubwa dhidi ya nchi iliyohuru makoloni ya Uingereza ya visiwa vya West Indies. Athari yake nyingine ilikuwa kwamba nchi iliyo huru sasa, ya Marekani (U.S.A.) iligeuka kwenye makoloni ya Ufaransa yaani Visiwa vya Saint Domingue (Haiti), Cuba na Brazil. Dk. Williams anaandika, "Ubora wa makoloni ya sukari ya Ufaransa ulikuwa kwa ajili ya wakulima wa Kiingereza, kubwa miongoni mwa maovu mengi ambayo yalijitokeza nje kutoka kwenye Pandora's box o (sanduku la Pandora) ilikuwa ni mapin-duzi ya Marekani. Kati ya mwaka 1783 na 1789 maendeleo ya sukari ya visiwa hususan vya Ufaransa, vya Saint Domingo (Haiti), hususan lilikuwa jambo la kushangaza katika maendeleo ya kikoloni. Rutuba ya udongo wa makoloni ya Ufaransa ilikuwa ni ya wazi mno, sukari ya Ufaransa iligharimu moja ya tano ( 1/5) chini zaidi ya ile ya Uingereza, mavuno ya wastani huko Saint Domingo na Jamaica yalikuwa tano kwa moja." 136 Athari iliyosababisha maafa kwenye makoloni ya Uingereza ya West Indies inaweza kuamuliwa na ukweli kwamba "mwaka 1775 Jamaica ilikuwa na mashamba 775; 135. Williams, Dr. Eric. Capitalism and Slavery uk. 65. **Pandora box ni maneno ya methali, maana yake ni mpango ambao ukihamasishwa huzalisha matatizo mengi yasiyodhibitika. 136. Ibid, uk. 122. hadi kufika 1791, katika kila mashamba mia moja, masham-ba ishirini na tatu yaliuzwa kwa ajili ya kulipa, kumi na mbili yalikuwa kwenye miliki ya wafilisi, wakati saba yali-achwa; na wakulima wa West Indies, wakiwa na deni la kiasi cha pauni milioni ishirini." Polepole, wakulima wa Kiingereza walipoteza moja kwa moja mamlaka yao ambayo waliyafurahia kwa kipindi kirefu katika soko la Ulaya. "Uuzaji wa bidhaa nje kutoka makoloni ya Ufaransa, uliingiza pauni za Kiingereza zaidi ya milioni nane, na Uingizaji bidhaa ndani ya nchi, zaidi ya pauni milioni nne, tani zilizo shughulikiwa 164,000 na wafanya kazi wa meli 33,600; uuzaji wa bidhaa nje kutoka makoloni ya Uingereza uliingiza pauni za Kiingereza milioni tano, na uingizaji bidhaa ndani ya nchi chini ya milioni mbili, tani zilizo shughulikiwa, 148,000 na wafanya kazi wa meli 14,000. Katika hali zote makoloni ya sukari yalikuwa na umuhimu mkubwa sana kwa Ufaransa kuliko yalivyokuwa kwa Uingereza."

1 3 7. Hivyo, gharama ya sukari (na hivyo hivyo kwa bidhaa zingine zote.) ilianza kwenda juu sana. Dk. Williams anaeleza, "Ukiritimba wa mkulima wa West Indies haukuwa tu jambo lisilofaa kinadharia, haukuwa na faida katika hali halisi. Mnamo mwaka 1828 ilikisiwa kwamba ili-wagharimu raia wa Uingereza zaidi ya pauni milioni moja na nusu kwa mwaka. Mnamo mwaka 1844, ulikuwa unagharimu nchi pauni 70,000 kwa juma moja na jiji la London peke yake pauni 6,000. Uingereza ilikuwa inalipa zaidi ya pauni milioni tano kwa ajili ya sukari yake kwa mwaka kuliko Bara lote la Ulaya... Mbili ya tano (2/5) ya bei ya ratili moja ya sukari iliyotumiwa Uingereza iliwaisha 137. Ibid, uk. 123. gharama ya uzalishaji, mbili ya tano ( /$) ilichukuliwa kama ushuru wa serikali, moja ya tano ( 1/5) shukurani kwa mkulima wa West-Indies..." o Pole pole, Saint Domingue (Haiti) koloni la Ufaransa, lili-ibuka kama mzalishaji muhimu sana wa sukari. Kwa mtazamo wa Waziri Mkuu wa Uingereza, William Pitt, hili lilikuwa jambo lenye uamuzi. Umri wa visiwa vya Uingereza vya sukari ulifika mwisho. Mpango wa West-Indian haukuwa na faida, na biashara ya watumwa ambayo ndio ilikuwa tegemeo lake, badala ya kuwa na manufaa kwa Great Britain... ni ya uharibifu mno ikilinganishwa na dhana ya maslahi. ^"- Kwa hiyo, Pitt aligeukia India kulima na kuzalisha sukari. Mpango wa Pitt ulikuwa na sehemu mbili: kurejesha soko la Ulaya kwa msaada wa sukari kutoka India, na kupata fursa ya kukomesha biasharra ya watumwa kimataifa tukio ambalo lingeiangamiza Saint Domingue. Kama haingekuwa ukomeshaji wa Uingereza. Wafaransa waliwategemea sana wafanyabiashara ya watumwa wa kimataifa, basi ingekuwa ukomeshaji wa Uingereza hivyo kwamba hata kama Uingereza peke yake ingepiga marukufu biashara ya watumwa, uchumi wa makoloni ya Ufaransa ungetetereka.

"Mpango wa Pitt ulishindwa kwa sababu mbili. Umuhimi wa sukari ya kutoka India ya Mashariki, kwa kiwango kili-chopangwa, haingewezekana kwa sabahu ya kodi ya ushuru kuwa juu iliyowekwa kwa sukari yote isipokuwa ile iliyoza-lishwa kwenye makoloni ya Uingereza ya West-Indies... Pili, Wafaransa, Wadachi na Wahispania walikataa 138. Ibid, uk. 138-9. 139. Ibid, uk. 146. kukomesha biashara ya utumwa. Ilikuwa rahisi kuona malengo halisi ya kisiasa yaliyoko nyuma ya pazia la ubi-nadamu la Pitt. Gaston-Martin, Mfaransa maarufu mwenye taaluma ya historia ya biashara ya watumwa na makoloni ya Caribbean, anamlaumu Pitt kwa kutaka kuwapa uhuru watumwa kwa kutumia propaganda, hapan shaka kwa kutu-mia jina la ubinadamu. lakini pia kuharibu biashara ya Ufaransa. Na anahitimisha kwamba kwenye propaganda hii ya kiihsani na kiubinadamu palikuwepo na malengo ya kiuchumi.

Halafu pakatokea tukio moja kubwa. Wakulima wa Kifaransa huko Saint Domingo, mwaka 1791, wakihofia matokeo ya Mapinduzi ya Ufaransa, waliwapa Uingereza visiwa hivyo; muda si mrefu Windward Island ilifuata mtin-do huo; Pitt alikubali kuvichukua visiwa hivyo mwaka wa 1793. Vikosi vya jeshi la Ufaransa vilipelekwa kimoja baada ya kingine mara kadhaa lakini havikufanikiwa kuvire-jesha visiwa hivyo kwenye miliki ya Ufaransa. Dk. William anafafanua: "Hii ni zaidi ya manufaa ya kiso-mi. Pitt hangeweza kumiliki Saint Domingo na kukomesha biashara ya watumwa wakati huo huo. Bila ya kawaida yake ya kuingiza watumwa 40.000 kwa mwaka, Saint Domingo ingekwisha filisika. Kitendo cha Pitt kukubalia kuchukua kisiwa hicho kimantiki kilikuwa na maana kwamba hangeendelea na mpango wake wa kukomesha biashara ya watumwa. Kwa wazi hakusema hivyo. Pitt alikwisha fika mbali sana katika kuwaahidi raia wa Uingereza. Aliendelea kuzungumza kuhusu kukomesha biashara ya watumwa hata hapo alipokuwa anaitumainisha biashara ya watumwa katika hali halisi... Sababu za Pitt zilikuwa za kisiasa na kwa kiwango kidogo kibinafsi. Pitt alipendelea biashara ya sukari: Ama ilikuwa lazima aivuruge Saint Domingo kwa kuingiza sukari nyingi sana Ulaya na ya bei rahisi kutoka India au kwa kukomesha biashara ya watumwa; au aichukue Saint Domingo iwe yake binafsi."

140. Hali hii ingeipatia Uingereza ukiritimba wa sukari, rangi ya buluu, pamba na kahawa... Lakini kama Pitt angeikamata Saint Domingo, biashara ya watumwa lazima ingeendelea. Wakati Saint Domingo ilipochukuliwa na Ufaransa, biashara ya watumwa ilichukua sura mpya ya kuwa kama vile suala la ubinadamu tu... Lakini kuharibika kwa Saint Domingo haikuwa na maana ya ukombozi kwa makoloni ya Uingereza ya visiwa vya West-Indies. Walijitokeza maadui wawili wapya kwenye uwanja. Cuba ilisonga mbele na kuziba pengo lililoachwa kwenye soko la dunia baada ya kutoweka Saint Domingo." 141. Wakati ule ule, chini ya mamlaka ya Marekani, sukari ya Cuba na wazalishaji wengine waliokuwa na msimamo wa kati, bado ilipata soko Ulaya, na sukari ya ziada kutoka British West Indian ililundikana Uingereza. Kufilisika kwa wakulima ilikuwa hali ya kawaida. Kati ya 1799 hadi 1807, mashamba 65 ya Jamaica yaliachwa, 32 yaliuzwa kufuta madeni, na malalamiko 1807 ya madai yalikuwa yana ngoja uamuzi dhidi ya 115. Mada zilizokuwa zinazungumziwa hapo kisiwani ni madeni, maradhi na vifo. Kamati ya bunge iliyoundwa mwaka 1807 iligundua kwamba mkulima wa British Indian alikuwa anazalisha kwa hasara. Mwaka wa 1800 faida ya mkulima ilikuwa asilimia 2.5 (2 '2 %), mwaka 140. Ibid uk. 146 -7, Ibid uk. 1487- 8. 141. Ibid, uk. 148-9. wa 1807 hakuna faida. Mwaka wa 1787 mkulima alipata 19/6d. faida kwa kila ratili mia na kumi na mbili; mwaka 1799, 10/9d; mwaka wa 1803, 18/6d; 1805, 12/-; katika kwaka 1809, hasara. Kamati ilidhani sababu kubwa ilikuwa hali mbaya ya soko la nje. Mwaka 1809 sukari ya ziada ya Uingereza ilikuwa tani 6,000. Uzalishaji ukasitishwa. Kuwekea mipaka uzalishaji, biashara ya watumwa lazima ikomeshwe." 1 Kwa hiyo, kwa maneno ya Dk. Williams, "Kukomeshwa kwa biashara ya watumwa moja kwa moja ilisababishwa na kuvurugika kwa uchumi huo.

UNAFIKI WA WAKOMESHAJI WA BIASHARA YA WATUMWA

Kama mtu yeyote anataka kudhani kwamba sababu ya kukomeshwa kwa utumwa ni maendeleo ya unyofu wa maadili, basi anashauriwa kuangalia msimamo wa watu waliokuwa wanashughulikia suala la kukomesha biashara ya watumwa katika mfumo wa malengo yao ya kiuchumi. Hivyo tunaona kwamba wale wale washikiliaji wa maslahi ya West Indies ambao kabla ya tatizo lililotajwa, walikuwa ni waungaji mkono motomoto wa biashara ya watumwa sasa waligeuka kuwa "waungwana wenye huruma na shauku ya kuukomesha utumwa". Dk. Williams anasema, kwa kejeli kabisa, ilikuwa ni wamiliki wa watumwa wa siku za nyuma wa West Indies ambao sasa walishikilia tochi ya kuwahuru-mia binadamu. Wale ambao, katika mwaka wa 1807, kwa majonzi walikuwa wanatabiri kwamba kukomesha biashara ya 142. Ibid, uk 149. 143. Ibid, uk 150. watumwa ya Uingereza "ingesababisha kupungua kwa biashara, kupungua kwa ushuru wa kodi, na kupungua kwa safari za baharini; na hatimaye kudhoofisha na kuondoa kabisa msingi mkuu wa ustawi wa Uingereza, walikuwa, baada ya 1807, watu wale wale waliokataa 'mpango wa mtu' kuwaiba watu masikini na ambao hawana jinsi ya kujitetea." Manufaa ya West India katika mwaka wa 1830 yaliweka azimio la "kuchukua hatua madhubuti zaidi kusitisha biashara ya watumwa ya nje; kushughulikia suala la ukan-damizaji uliokwisha fanywa ambao kwamba ustawi wa makoloni ya Uingereza ya West Indes... hatimaye yali-utegemea. Wajumbe kutoka Jamaica, walopelekwa Uingereza mwaka 1823, walitangaza kwamba makoloni yangepatanishwa kwa urahisi kuhusu kukomeshwa kwa biashara ya kishenzi na ya kinyama, ambayo ustaarabu ulioendelea wa wakati huu hukuiruhusu tena kuwepo... Kundi kubwa la kukomesha biashara ya watumwa lilijidhi-hirisha nchini Jamaica katika mwaka 1849. Auj claplo, vyama na madhehebu viliunganishwa kuhusu suala la Africa kutendewa haki. Walilaani biashara ya watumwa na utumwa kama ni "kinyume cha ubinadamu iliyozalisha maovu mabaya sana Afrika - kuwadhalilisha wote walio-husika katika biashara hiyo, na kudhuru maadili na utashi wa kiroho wa watumwa, na kusihi kwamba neno la kuchuk-iza 'mtumwa' liondolewe kwenye msamiati duniani pote. UTUMWA LAZIMA UANGUKE, na utakapoanguka, JAMAICA ITASTAWI! walitamka kwa ukali, iliingia kwenye vita nyingi bila ya sababu zilizo halali." 144. 144. Ibid, uk 175-6.

Na palikuwepo na manufaa gani ya vifungu vya maneno vilivyo vikali na ambavyo vinaweza kuamuliwa kutokana na ukweli kwamba ubepari wa Uingereza, hata baada ya kuvu-ruga utumwa wa West Indian, "Uliendelea kustawi kutokana na utumwa uliokuwa unaendelea huko Brazil, Cuba na utumwa wa Amerika ya Kaskazini na Kusini." Kwa hiyo, kwa maneno ya Profesa Brogan, "tunapata mafumbo ya wajibu uliogeuzwa. Ilikuwa sawa kabisa kwa watetezi wa hoja ya kukomeshwa utumwa, kulaani matumizi ya sukari iliyo zalishwa na watumwa kutoka West Indes, lakini haku-na aliyependekeza kusimamisha matumizi ya pamba iliy-ozalishwa kutoka Marekani (U.S.A.). Hakika, hakuna mtu aliyependekeza kwa dhati kuacha kutumia sukari iliyozal-ishwa na watumwa kutoka Brazil au Cuba. Fedha sio hisia, hisia za uovu za uzuri, husokota na kupotosha njama." Dk. Williams anaandika, "Baada ya India, Brazil na Cuba, bila ya dhana yoyote. Je, muungwana yeyote angeweza kuhalalisha pendekezo lolote lililopangwa kuimarisha miny-ororo ya utumwa ambayo bado imewafunga Watu Weusi wa Brazil na Cuba. Kwa usahihi hiyo ndio ilikuwa maana ya biashara huru ya sukari. Kwani baada ya mwaka 1807 British West Indians walikataliwa na kunyimwa kuendesha biashara ya watumwa, na baada ya 1833 wakanyimwa nguvu kazi ya watumwa. Kama watetezi wa kukomesha utumwa walipendekeza sukari ya kutoka India, kwa makosa, kwa misingi ya ubinadamu kwamba ni sukari iliyolimwa na watumwa huru, ilikuwa ni wajibu wao kwa kanuni zao na dini yao kususia sukari iliyolimwa na watu wa Brazil na Cuba. Katika kuanguka kufanya hivi isiamuliwe kwamba hawakuwa sahihi, lakini si jambo la kukanusha kwamba kushindwa kwao kutumia njia hiyo ilivuruga hoja ya ubinadamu. Baada ya 1833, watetezi wa kukomesha utumwa, waliendelea kumpinga mkulima wa West Indian ambaye sasa aliajiri wafanya kazi huru. Ambapo, kabla ya hapo 1833, waliwagomea wamiliki wa watumwa wa Uingereza, baada ya 1833 waliunga mkono sababu ya wamiliki wa watumwa wa Brazil."

145. Kuondolewa kwa Watu Weusi kishenzi kutoka Afrika ni shughuli iliyoendelea kwa karibu miaka 25 tangu 1833, ambao walipelekwa kwenye mashamba ya miwa ya Brazil na Cuba. Uchumi wa Brazil na Cuba ulitegemea biashara ya watumwa. Msisitizo peke yake ulidai kwamba watetezi wa kukomesha utumwa wa Uingereza walipinga biashara hii. Lakini jambo hilo lingerudisha nyuma maendeleo ya Brazil na Cuba na matokeo yake kuzuia biashara ya Uingereza. Haja ya kupata sukari ya gharama ya chini baada ya 1833 ilishinda chuki yote ya utumwa. Tishio ambalo hapo mwan-zo lilichochewa na fikira ya mswaga watumwa wa Uingereza wa West Indies mwenye mjeledi; mswaga watumwa wa Cuba mwenye mjeledi, panga, jambia,. kisu na bastola na kufuatwa na mbwa mwitu, haikuamsha hata maoni ya watetezi wa kuzuia biashara ya watumwa." 146. Hivyo ni wazi kwamba sababu halisi yaubinadamu na uung-wana wa Uingereza wala haikuwa usawa wa kiunyofu au mwamko wa kimaadili bali ilikuwa ni kwa sababu ya shinikizo la kiuchumi na kuwaumiza washindani wao wa biashara. Kwa maneno ya Profesa Brogan, somo la Ubepari na Utumwa linavunja moyo na kufadhaisha kama si jipya. "Pale ilipo hazina yako ndipo moyo wako unapo lala.' 145. Ibid, uk 188. 146. Ibid, uk. 192.

ILIKUWA NI VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE YA MAREKANI

Je, ni ya kuwakomboa watumwa? Nadhani itakuwa kwa manufaa ya wasomaji kutizama kwa umakini hadithi isemayo kwamba vita ya Marekani ya wenyewe kwa wenyewe ilitokea kwa lengo la kuwakomboa watumwa. Ni ngano ambayo iliyobuniwa na haina uhusiano wowote na hali halisi ya ukweli. Nina nukuu hapa kutoka kwenye sura ya 22 ya "Lincoln, the Unkown" kilichoandik-wa na mwandishi wake maarufu Dale Carnegie. 1 Anaanza na maneno haya: - "Muulize raia wa kawaida wa Kimarekani leo kwa nini Waamerika walipigana vita ya wenyewe kwa wenyewe, atakacho kuambia ni kwamba, 'Kuwakomboa watumwa.' "Ni kweli hivyo?" "Hebu tuangalie. Hapa ni sentenso ambayo imechukuliwa kutoka kwenye hotuba ya kwanza ya Lincoln ya kuzindua urais wake. 'Sikusudii kuingilia kati, taasisi ya utumwa, moja kwa moja au kuzunguuka kwenye majimbo ambayo utumwa bado upo. Nina amini sina haki ya kisheria kufanya hivyo, na sipendelei kufanya hivyo." Ukweli ni kwamba mzinga ulikuwa unanguruma na majeruhi wanatoa sauti ya kulemewa kwa takribani miezi kumi na nane kabla Lincoln hajatoa tangazo la "Ukombozi wa watumwa." 147. Carnegie, Dale, Lincoln: The Unknwown (Surrey, U.K.: The World Work Ltd. 1948) Sura ya 22 Wakati wote huo watu wenye msimamo Mkali na Watetezi wa kukomesha utumwa walimsihi achukue hatua haraka, walimshambulia kupitia kwenye magazeti na kumshutumu kwenye majukwaa ya mikutano. "Wakati mmoja ujumbe wa mawaziri wa Chicago ulikwen-da Ikulu ya Marekani na kile walichokitangaza kwamba ilikuwa ni amri ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu Mweza wa Yote kuwaachia watumwa kuwa huru haraka sana. Lincoln aliwaambia kwamba alidhani kwamba kama Mweza wa Yote alikuwa na ushauri wowote wa kutoa, Angekuja moja kwa moja makao makuu na ushauri huo, badala ya kuwasilisha kwa mzunguuko wa kupitia Chicago." Zaidi ya hayo, Dale Carnegic anaendelea kunukuu kutoka kwenye jibu la Lincoln alipojibu makala ya Greedy, 'The Prayer of Twenty million.'('Sala ya milioni ishirini).

"Kusudio langu kubwa katika mapambano haya ni kuokoa Muungano, na wala si kuokoa au kukomesha utumwa. Kama ningeokoa Muungano bila kumpa uhuru mtumwa hata mmoja, ningefanya hivyo; na kama ningeokoa Muungano kwa kuwapa uhuru wa watumwa wote ningefanya hivyo, na kama ningeuokoa Mungano kwa kuwapa uhuru baadhi yao na kuwaacha wengine, pia ningefanya hivyo. Ninachofanya kuhusu watumwa na machotara, ninafanya hivyo kwa sababu ninaamini inasaidia kuokoa Muungano, na kile ninachovumilia, ninavumilia kwa sababu siamini kama ingesaidia kuokoa Muungano. Sitafanya yote wakati wowote nitakapoamini kile ninachokifanya kitadhu-ru lengo; na nitazidisha juhudi nitakapoamini kufanya hivyo itasaidia lengo." Akifafanua jibu hilo Dale Carngie anaandika: "Majimbo manne yamebakia na watumwa pamoja na Kaskazini, na Lincoln alitambua kwamba kama angetoa tangazo la "ukombozi wa watumwa" mapema mno katika mzozo huu, angewafukuzia kwenye Shirikisho, kuimarisha kusini, na pengine kuvunja Muungano daima milele. Palikuwepo na methali wakati huo ambayo Lincholn angependa kuwa na Mungu Mweza wa Yote upande wake, lakini lazima aipate Kentucky. "Hivyo alisubiri wakati mzuri, na kufanya mambo kwa tahadhari" "Lincoln mwenyewe alioa kwenye familia yenye kumiliki watumwa, ya Jimbo la mpakani. Sehemu fulani ya fedha ambayo mke wake Lincoln alipokea ilitoka kwenye urithi wa shamba la baba yake ambayo ilitokana na mauzo ya watumwa. Na rafiki mmoja tu wa karibu sana na wa kweli ambaye Lincoln alikuwa naye, alikuwa Joshua Speed ambaye alitoka kwenya familia yenye watumwa. Lincoln aliwahurumia watu wa Kusini kwa maoni yao. Kwa upande mwingine, alikuwa na desturi ya kumshehimu mwanasheria Mkuu kuhusu Katiba na sheria na rasilimali. Hakutaka kus-ababisha shida kwa mtu yeyote. (ila kwa watumwa)

"Lincoln aliamini kwamba majimbo ya kaskazini yalistahili kulaumiwa sana kwa kuendelea kuwepo kwa utumwa "Marekani (U.S.A) " kama ilivyo huko kwenye majimbo ya Kusini; na kwamba kuliondoa tatizo hilo, sehemu zote lazima zivumilie mzigo sawa kwa sawa. Kwa hiyo hatimaye alitengeneza mpango ambao ulikuwa karibu sana na moyo wake. Kwa mujibu wa mpango huo, wamiliki wa watumwa waliokuwa kwenye mipaka ya majimbo yenye uaminifu walipewa dola mia nne kwa kila Mtu Mweusi. Watumwa walitakiwa kuachiwa huru polepole, polepole sana. Mlolongo wa mambo haya haukutakiwa kumalizika kikamilifu hadi Januari 1, 1900. Lincoln aliwaita wawakil-ishi kutoka kwenye Majimbo ya mipaka wamuone huko Ikulu White House, akawasihi wakubali pendekezo lake. "Lincoln alihoji na kusema, mabadiliko yaliyomo kwenye pendekezo lake, yanakusudiwa kuja polepole kama umande unavyo dondoka kutoka mbinguni, bila kupokonya au kuvunja matarajio ya watu. Kwa nini msikubali pendekezo hili? Mambo mengi sana mazuri bado hayajafanyika kwa jitihada moja, katika wakati wote uliopita, kama ilivyo katika upaji wa Mungu sasa hivi ni upendeleo wenu wa juu kutekeleza. Muda mwingi ujao na upana wake usije ukalalamika kwamba ulipuuzia jambo hili."

Msomaji angekumbuka kwamba mpango huu wa kuwapa watumwa uhuru "kwamba ulikuwa karibu mno na moyo wake Lincoln" ulikuwa sawa na mpango ambao tayari ulik-wisha wekwa na kutekelezwa miaka 1300 iliyopita katika Uislam na ambao ulitoa matokeo ya kushangaza katika ulimwengu wa Kiisilamu. Kama mpango huo ungekubaliwa na ndugu zake Lincoln, hapange kuwepo na chuki kubwa baina ya mataifa, migongano ya ndani, mageuzi ya kijamii na udhaifu wa hisia ambao bado unaendelea kuwepo nchini Marekani (U.S.A.) karne moja baada ya kile kilichoitwa Ukombozi wa watu weusi (Emancipation of Negroes). Bahati mbaya, wawakilishi wa Majimbo hayo yaliyokuwa yanapakana walikataa mpango huo. Carnegie anasema, "Lincoln mara moja alikasirika sana. Lazima niiokoe serikali hii, kama inawezekana, alisema na inaweza ikaeleweka, kwa mara zote, kwamba sitakubali kuacha mchezo huu, na kuacha kadi yoyote ile ipatikanayo iwe hai-jachezwa.... Ninaamini kwamba kuwapa uhuru watumwa na kuwapa silaha watu weusi sasa imekuwa jambo la msin-gi na muhimu kivita. Nimesukumwa kwenye uchaguzi ama kutekeleza hilo au kuuwachia) Muungano (usambaratike). "Ilibidi Lincoln ashughulike haraka, kwani Ufaransa na Uingereza walibakia kidogo watambue Shirikisho. Kwanini? Sababu zilikuwa rahisi. Tuchukue mfano wa Ufaransa kwanza."

Napoleon wa III alikuwa mfalme wa Ufaransa. Alikuwa na shauku kubwa ya kutaka utukufu wa mamlaka ya utawala, kama alivyokuwa ami yake mtukufu, Napoleon Bonaparte, alivyo fanya. Kwa hiyo, alipoona majimbo yanapigana, na alitambua kwamba walikuwa na shughuli nyingi mno kuweza kufikiria kuhusu utekelezaji wa sheria ya "Momoe Doctrine," aliamuru jeshi kwenda Mexico, huko likaua wazalendo elfu kadhaa, likashinda nchi, ikaitwa Mexico iliyo chini ya himaya ya Ufaransa, na likamweka Archduke Maximilian kukalia kiti cha enzi. "Napoleon aliamini na si bila sababu, kwamba kama kundi linalotaka shirikisho lingeshinda, lingependelea ufalme wake mpya; lakini kama kundi linalotaka shirikisho lingeshinda, United States ingechukua hatua za haraka za kuifukuza Ufaransa huko Mexico. Kwa hiyo, ulikuwa ni upendeleo wake Napoleon, kwamba Kusini ifaulu kujitenga, na alitaka kuisaidia kutekeleza kujitenga huko kwa kadiri ya uwezo wake. Mwanzoni mwa vita, jeshi la majini la Kaskazini lilifunga bandari zote za Kusini, bandari 189 zikawa chini ya ulinzi wao na walifanya doria kwenye eneo la maili 9,614 za uwanda wa pwani, njia nyembamba za maji zinazoungan-isha bahari na zinazounganisha bahari na maziwa, vinamasi na mito. Hiki kilikuwa kizuizi kikubwa mno ambacho ulimwengu haujapata kuona. Kundi lililotaka Muungano lilikuwa lina haha. Halikuweza kuuza pamba yake, wala kuweza kununua bunduki, risasi, viatu, madawa au chakula. Watu hawa walianza kuchemsha karanga na mbegu za pamba kuwa mbadala wa kahawa, na walianza kuchemsha majani ya miti ya matunda mithili ya mibuni na kuchuja maji yake na kuwa mbadala chai. Magazeti yalianza kuchapishwa kuwekwa kwenye matangazo. Nyumba zenye sakafu za udongo na zenye kufuka moshi, zililoweshwa dabwa dabwa kwa mafuta ya wanyama, zikachimbuliwa na kuchemshwa ili kupata chumvi. Kengele za makanisa ziliyeyushwa na kutiwa katika mizinga. Reli za magari madogo mitaani katika mji wa Richmond zilikatwa katwa na kufanywa silaha katika mashua za kivita zenye bunduki.

Watu wa Muungano hawakuweza kuzifanyia matengenezo reli zao au kununua vifaa vipya, kwa hiyo usafiri ulibakia kidogo sana; nafaka ambayo ilinunuliwa kwa dola mbili, pishi tisa huko Geogia, ilinunuliwa kwa dola kumi na tano Richmond. Watu waishio Virgini walikuwa wanashinda na njaa. Ilibidi utaratibu fulani ufanywe haraka sana. Kwa hiyo, Kusini walikubali kumpa Napoleon wa III dola milioni 12 kama angeutambua Muungano na atumie meli za Kifaransa kuondoa kizuizi. Kwa upande mwingine, waliahidi kumzidishia nguvu kwa amri ambayo ingeanzisha moshi kwenye kila kiwanda huko Ufaransa usiku na mchana. Kwa hiyo Napoleon akazisihi Urusi na Uingereza kuungana naye katika kuutambua Muungano. Utawala wa makabaila uliokuwa madarakani, wahusika wake waliweka sawa miwani zao, wakanywa toti kadhaa za Scotch Whisky, na wakasikiliza kwa hamu kubwa mazungumzo ya awali ya Napoleon. Marekani (U.S.A.) ilianza kutajirika sana na kuwa na uwezo mkubwa wa kuwaridhisha, Walitaka kuona taifa linagawanyika, Muungano unavunjika. Kwa upande mwingine, walitaka pamba ya Kusini. Viwanda kadhaa vya Uingereza vilifungwa, na watu milioni moja hawakuwa tu hawana kazi, bali pia kuwa fukara na kushuka chini kuwa omba omba halisi. Watoto walikuwa wanalia njaa, mamia ya watu walikuwa wanakufa kwa sababu ya njaa. Michango ya raia kwa ajili ya kununua chakula cha wafanya kazi wa Uingereza ilichukuliwa na kupelekwa kwenye vijiji vya ndani kabisa ya dunia hata India ilioko mbali sana na China ambayo ilibanwa na umasikini. Palikuwepo na njia moja, na njia moja tu, kwamba Uingereza ingeweza kupata pamba na hiyo ilimaanisha waungane na Napoleon III katika kuutambua Muungano na kuondoa kizuizi. "Kama hilo lingefanyika, nini kingetokea Marekani? Kusini wangepata bunduki, baruti, mkopo, chakula vifaa vya njia ya reli, na msaada mkubwa sana wa hali na mali.

"Na Kaskazini wangepata nini? Wangepata maadui wawili wapya na wenye nguvu. Hali hiyo kuwa mbaya kiasi hicho sasa, hapangekuwepo na matumaini. "Hakuna aliyejua hilo vizuri zaidi kumzidi Abraham Lincoln. "Ni kama vile tumecheza kadi yetu ya mwisho', aliungama hivyo katika mwaka 1892. Ama lazima tubadili mbinu zetu au tukubali kushindwa mchezo.' Kama ilivyoona Uingereza, makoloni yote yalikwisha jitoa kutoka kwenye utawala wake tangu mwanzo. Sasa makoloni ya Kusini nayo yamekwishajitoa kutoka makoloni ya Kaskazini; na Kaskazini ilikuwa inapigana kuilazimisha na kuitiisha Kusini. Je, pangekuwa na tofauti gani kwa mtu wa kawaida huko London au mwana mfalme huko Paris kama Tenessee na Texas zingetawaliwa kutoka Washington au Richmond? Hakuna. Kwao vita haikuwa na maana yoyote na yenye kuleta hatari bila madhumuni ya maana. 'Nilikuwa sijapata kuona vita imepamba moto kama hiyo katika uhai wangu', aliandika Carlyle, 'iliyokuwa inaonekana zaidi kama ya kipumbavu. Lincoln aliona kwamba msimamo wa Ulaya kuhusu vita hiyo lazima ubadilike, na alijua jinsi ya kufanya. Watu mil-ioni moja huko Ulaya walikwisha soma "Uncle Toms Cabin" walikisoma kisa hicho na wakalia na wakajifunza kuchukia michomo ya moyo na udhalimu wa utumwa. Kwa hiyo Abraham Lincoln alitambua kwamba kama angetoa tangazo lake la "ukombozi wa watumwa", watu wa Ulaya wangeiona vita kwa namna tofauti. Haingekuwa tena ugomvi wa kumwaga damu kwa sababu ya kudumisha Muungano ambao haukuwa na maana yoyote kwao. Badala yake, ingetukuzwa kuwa vita takatifu ya kutokomeza utumwa. Serikali za Ulaya hazingeitambua Kusini. Maoni ya watu hayangestahamili kuwasaidia watu ambao wanapi-gana kwa lengo la kuendeleza utumwa wa kibinadamu.

Hatimaye, kwa hiyo, mnamo Julai, 1862, Lincoln akiwa amedhamiria kutoa tangazo lake, lakini McClellan na Papa mnamo siku chache za nyuma waliliongoza jeshi la Kusini kwenye fedheha ya kushindwa mara kadhaa. Seward alimwambia Rais kwamba muda huo haukuwa mwafaka, hivyo angelazimika kungoja na kutoa tangazo kwenye kilele cha ushindi wao. "Ushauri huo ulionekana wa hekima. Kwa hiyo Lincoln akangojea na miezi miwili baadaye ushindi ukapatikana." Na kwa hiyo, kuendeleza Vita ya Muungano, tangazo la "Ukombozi wa Watumwa" lilichapishwa mnamo Septemba 1862, ambalo lilitakiwa lianze kutekelezwa tarehe Moja, Januari 1863. Ninampa Abraham Lincoln heshima ya juu sana na amekuwa mmoja wapo wa mashujaa ninao wapenda tangu nilipokuwa mdogo. Lakini heshima hiyo msingi wake ni kwenye ukweli na hali halisi, si kwenye mambo ya kubuni-wa. Lincoln alikuwa na ubinadamuna, na yeye, kutoka ndani ya moyo wake alikuwa dhidi ya utumwa. Lakini haina maana kwamba tumtukuze kwa propaganda za uwon-go. Uhalisi wa jambo hili ni kwamba hakupigana vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa lengo la kuwapa watumwa uhuru, kwa usahihi zaidi aliwapa watumwa uhuru kwa lengo la kushinda vita na kuokoa Muungano.

UTUMWA WA KIMAJIMBO

Hadi sasa tumechambua aina moja tu ya utumwa, yaani utumwa wa utumishi wa nyumbani kwa mtu. Lakini ilita-jwa kwenye sura ya kwanza kwamba utumwa ni wa aina mbili, aina ya pili ni Utumwa wa Kimajimbo au taifa moja kutumikisha taifa lingine. Licha ya kwamba utumwa wa nyumbani sasa hivi unajulikana kwamba ulikomeshwa, utumwa wa kitaifa bado upo unaendelea. Moyo ukiwa umejaa huzuni mtu anaona uharibifu wa maisha ya binadamu kwa mpango maalum na hadhi ya binadamu inaendelezwa na ustaarabu wa Kikristo karibu katika kila nchi hapa duniani. Wahindi Wekundu walikuwa wakazi wa mwanzo wa Nchi mpya. Wapo wapi sasa? Walitolewa polepole kutoka kwenye ardhi yao na wamelazimishwa kuishi kwenye ardhi yenye rutuba hafifu ambayo haiwezi kuzalisha mazao, vishamba vilivyoko ndani ya Marekani (U.S.A). Waaborigine wa Australia walipitishwa kwenye uonevu wa aina hiyo hiyo. Wahindi Wekundu na Waaborigine walikuwa wanawindwa kama wanyama pori: yaani, nyati na kadhalika na sasa hivi idadi yao inakaribia kufutika kabisa katika uso wa dunia hii. Dk. Eric Williams ananukuu maelezo ya Mkuu wa wahindi wekundu, Hatuey, ambaye alipewa adhabu ya kifo kwa kuwawekea pingamizi wavamizi, alikuwa imara katika kukataa imani ya Kikristo kama njia ya kwenda kwenye wokovu alipotambua kwamba wauaji wake, nao pia walikuwa na matumaini ya kwenda Peponi. 148. Lakuhuzunisha zaidi ni hatima ya Waafrika wa Afrika ya Kusini. Wareno wakiwa na tangazo la Papa "Walazimisheni makafiri kuwa watumwa" wanang'ang'ania kuiweka Angola na Msumbiji chini ya nira ya Utumwa wa kitaifa. Ni jambo la kushangaza kweli kuona Papa Paulo wa VI mara nyingi hutoa matamshi kuhusu matatizo ya kisiasa ya dunia; akini kamwe hata siku moja hajaona umuhimu wa kuishauri Ureno kuzungumza na "raia" wake hapa Afrika na 148. Williams, op. cit., uk. 8. kwingineko.

Badala yake Mapapa wamekuwa wakien-deleza uhusiano maalum na Ureno na Hispania, nchi hizi mbili za Kanisa Katoliki ambazo zinakataa kuyaacha huru makoloni yake ya Afrika. Katika mwezi wa July, 1970, Papa Paulo VI aliwapokea viongozi fulani wa wapigania uhuru wa makoloni ya Ureno katika Afrika. Mkutano huu uli-ikasirisha sana Ureno, ambayo ilitoa tamko la pingamizi; Vatican katika hali ya wasi wasi ilitoa maelezo. Akieleza kuhusu jambo hili, barua ifuatayo yenye kichwa cha habari "Muhtasari wa Papa ni Faraja: ilichapishwa katika gazeti la "Standard Dar es Salaam (Tanzania) na muunini mweusi wa Roman Katoliki, aliposema: "Kipengee cha habari; 'Muhtasari wa Papa waifariji Ureno' (Standard, July 11) yahusika. Ninanukuu sentenso muhimu: Muhtasari wa Vatican ulisema kwamba Papa alipowapokea (yaani viongozi wa vyama vya ukombozi katika Afrika walioko chini ya utawala wa Kireno) wakiwa kama Wakatoliki na Wakristo, bila ya kuangalia shughuli zao za kisiasa. Aliwakumbusha kuhusu mafundisho ya Kanisa kwamba njia za amani siku zote zitumike hata katika kutafuta kile mtu akionacho kuwa ni haki yake mtu.

"Habari za mapema zaidi kwamba Baba Mtakatifu ame-pokea viongozi hao waliosemwa, zimenisumbua na kunitia wasi wasi sana. Sasa ufafanuzi huu umefanya wasi wasi wangu kutulia. Ngoja nieleze kwa nini. Lilikuwa Kanisa la Roman Katoliki ambalo ndilo lililoleta ukoloni wa Kimagharibi kwa kuigawa ardhi yote na nchi zote mpya zili-zogunduliwa hivi karibuni katika mafungu mawili; kuwapa Wahispania nusu ya Magharibi (kama nchi za Amerika) na kuwapa Wareno nusu ya Mashariki (kama nchi ya Afrika na India). Makoloni ya Ureno katika Afrika yameundwa imara sana juu ya lile Agizo la Papa. Niliposoma mapema kwam- ba Papa Paulo VI aliwapokea viongozi wa vyama vya Ukombozi, nilishangaa iliwezekana vipi. Kwa mujibu wa imani yetu ya kutokukosea kwa Papa, Paulo VI analazimi-ka kuchukua na kuhalalisha kila kitu kilichoamriwa na kua-gizwa na wale watakatifu waliokwisha mtangulia. Kwa hiyo, kwa mujibu wa kufikiria kwangu asingewatia moyo viongozi hao.

"Sasa ufafanuzi wake umenifariji mimi sana kiroho. Sasa naweza kulala kwa amani na kuwa ujuzi wa uhakika kwamba Kanisa halikujilaumu lenyewe kwa kuonyesha kwamba Mapapa walikosea katika kuuweka na kuunga mkono "mwanga" wa bara hili jeusi chini ya Ubepari wa Kireno. "Pia ushauri wake kwa hawa waitwao 'Waathirika kutokana na Ukoloni' kubakia katika amani (yaani kuvinyang'anya silaha vikundi vya wapigania uhuru) ni sawa na mvinyo wa zamani ndani ya chupa mpya. Inanikumbusha maombi ya mapadre wa Kanisa la Romani Katoliki wakati wa kuen-deshwa meli zenye watumwa kutoka bandari za Ureno kwenda katika visiwa vya West Indes. Waliomba kwa Mola Mwenye Uwezo na nguvu zote kuhakikisha usalama wa meli hizo na siku zote waliwaamuru watumwa weusi wawe na tabia za kiungwana na utii. Kwa hakika, hawakufikiria kwamba ni lazima kuwashauri mabwana (wamiliki) wa watumwa kuwafikiria nao kuwa ni wanaadamu. Nina furaha kwamba Kanisa langu halijabadilika katika kipindi chote hiki cha karne ndefu." Sera ya Afrika ya Kusuni ya Ubaguzi wa rangi inalaumiwa ulimwenguni pote na Baraza la Umoja wa Mataifa (UN) na kila mahali. Lakini Makanisa siku zote yalifuata mstari huo huo. Ilikuwa baada tu ya "mabadiliko ya Upepo" katika Afrika na kutokea kwa haraka uhuru wa nchi za Kiafrika kwamba makanisa yalitambua haja ya kuupinga mfumo ulio mbaya kabisa ambao hukatilia wenyeji wa asili (wazawa) wa nchi husika haki ya kufanya kazi, kutembea, kukaa, kupanda vipando vya kusafiria, kuchuma au kulala katika ardhi yao wenyewe. Na hata pia wakati Makanisa mengine yote, yalipolazimishwa na haja muhimu za Kisiasa, walionyesha upinzani wao kwa aina hii ya utumwa, Kanisa la Kidini la Mageuzi- 'The Dutch Reforned Church' bado linaunga mkono mfumo huu wa kinyama.

Rhodesia inafuata nyayo za Afrika ya Kusini. Msemo ulio-zoeleka na maarufu wa kuchekesha wa Kiafrika katika sehe-mu hizi za dunia unaelezea kuhusu Mwafrika mmoja aki-umwambia (rafiki yake) Mzungu: "Ulipokuja ulikuwa na Biblia na sisi tulikuwa na ardhi. Sasa hivi sisi tunayo Biblia na wewe una ardhi, (unaimiliki). Mbali na utumikishaji huu wa kijeuri na dhahiri, bado upo udanganyifu mwingine ambao biashara ya utumwa wa Kitaifa hudhihirisha uso wake. Ukiwa kama kinyonga, hubadilisha rangi yake kwa kutegemea mazingira. Ukoloni wa dhahiri sasa umebadilika na kuwa ukoloni mamboleo; lakini inafikia pale pale kwenye utumikishaji na watu na yale mataifa makubwa yenye nguvu kwa kutumia mbinu zenye utata zaidi au zisizokuwa na utata sana. Tumekwisha ona nini kilitokea kuhusu league of Nations (Shirikisho la Mataifa). Imeondolewa na badala yake ni UNO, lakini wakati mataifa dhaifu yanapolia na kuomba kuwepo na haki, usawa na uadilifu, shinikizo la kidiplomasia hutumika na madai yao ya haki kuhusu haki zao za msingi huondole-wa na kuwekwa kando au huahirishwa. Kuna usaliti wa kisiasa, na rangi ya ngozi bado ndio kiumacho. Kwa kweli nchi zitawalazo au zile ambazo zina nguvu na zimejizatiti vyema kwa vyombo na uwezo wa kuleta maangamizi makubwa na uharibifu, bado zinashikilia utawala wao.

Aina hii ya utumwa inafanywa leo hii siyo tu na mataifa bepari ya Kikristo bali na Wakomonist pia, na itaendelea hivi kwa kipindi kirefu maadam jamii ya kibinadamu inabakia katika kugawanyika katika makundi ya walio na mguvu na walio dhaifu au mpaka kuwepo na kutambuliwa kwa Mwenye Kudra na Mwenye Nguvu zote, Mwenyezi Mungu (atambuliwe), na Himaya (Enzi) yake katika Ulimwengu wote iwe imeaminiwa kabisa na kupokewa. Hata sasa wakati Karne ya ishirini inaelekea kufika mwisho wake na Waamerika wakiwa wanajifaharisha wenyewe katika yale waliyoyapata, suala la "Watu Weusi-Manegro" liko mbele kabisa na bado halijapatiwa ufumbuzi. Kwa kukata tama, O.A Sherrad anasema: Utumwa umekuwepo kutoka mwanzo na utamalizika katika mfumo mmoja au mwingine, kwa kadiri ambavyo mwanadamu ana tamaa ya madaraka. Matokeo yake yamekuwa katika taabu zaidi, mauaji zaidi, kushuka heshima zaidi, huzuni zaidi, mateso zaidi na dham-bi kuliko asasi yoyote nyingine ya mwanadamu. Inaangamiza mtu mmoja mmoja na jamii nzima ya mwanadamu. Hutia chachu katika maingiliano ya mwanadamu, kwani alama aonekanayo mtu ni hofu... imeshughulika na wakati uliopita katika hali ya kiovu na iliyojaa makosa, na pengine ni yenye uovu zaidi na makosa zaidi katika wakati wa sasa. Utumwa kama si wa dhahiri sana lakini ni wenye kutapakaa zaidi na hofu yake ni yenye kuenea kote. Hofu ya kinyonge, dhalili na ya kitumwa iji-tokezayo miongoni mwa vibaraka vyake inaitembelea na kuyaandama Makao ya Utawala wa Urusi; hofu ya maangamizi ya mtumwa mnyonge huzidisha uhasama kati ya Mashariki na Magharibi; hofu ya lipizo la mnyonge hujizalisha katika Afrika ya Kusini na kuyafunika majimbo; hofu ya mafedhuli kutia kasumba mateso, vifo vya ghafula, hunyonyesha makundi makubwa ya watu ulimwenguni pote. 149. Lakini hatushirikiani katika mtazamo huu ulio mbaya kabisa. Tunatambua kwamba tatizo lenyewe ni kubwa kabisa, lakini tunajua pia kwamba Uislam ni Dini iliyoletwa na Allah, Aliye Muweza juu ya kila kitu. Uislam, miaka 1400 ulileta mpango wa sura tatu (three sided programme) kwa ajili ya kuondoa utumwa.

Kuzuia njia za kupatia watumwa wapya, kukomboa watumwa, na kuirudisha na kuiweka heshima ya kibi-nadamu kwa watumwa. Na ukweli ni kwamba ingawa Banu Ummayya waliuhujumu upande mmoja wa mpango huo kwa kuingiza utumwa kwa njia ya kuwanunua, hawakuweza kupunguza athari ya pande hizo nyingine mbili zilizobaki. Na watumwa katika ulimwengu wa Kiislamu walipata tena heshima yao ya kibinadamu iliyopotea. Mfumo ambao umeonyesha manufaa yake, na ambao umepata mafanikio katika nyanja, ambako mifumo mingine imeshindwa kabisa, kwa hakika utapata ukomeshaji wa jumla wa kila aina ya mgawanyiko, mtengano, tofauti na dhuluma kama utapewa nafasi. Ameer Ali anaandika: "inabakia kwa Waislamu (sic. - japo kwa makosa) kuonye-sha uwongo wa kashifa juu kumbukumbu za Mtume mkub-wa na Mtukufu (zinazofanywa na wazushi na maadui wa 149. Sherrard, op. cit., uk. 188-189.

Uislam) kwa kutamka kwa maneno ya wazi kwamba Utumwa (utumwa katika sura ya aina yoyote ile na tofauti za mataifa na rangi) unachukiwa na dini yao, na umekatazwa na sheria yao. Na tuna uhakika kwamba Uislam utape-wa fursa na Allah ili kuleta haki yote na kamili katika ulimwengu. Maimamu wa Kishia, Viongozi waliochaguliwa na Mwenyezi Mungu, waliiendeleza kazi ya Mtukufu Mtume na waliingiza katika wafuasi wao ile roho ya kweli ya Uislam. Wao kwa mifano yao na kwa kupitia kwenye dua, wameuhifadhi Uislam asilia (wenyewe) kwa ajili ya wafuasi wao. Na Imamu wa mwisho wa Mwenyezi Mungu, Imamu Muhammad al-Mahd (amani iwe juu yake) Anayengojewa, atadhihiri tena wakati ulimwengu huu utakapokuwa umejaa dhuluma, ukatili na kutokuaminika. Wakati yeye Anayengojewa atakapotokea kutoka katika Ghaibati (Alikofichwa na Allah) ataujaza ulimwengu na Haki, Uadilifu, Uaminifu na Rehema. Tumeamini katika ulimwengu ulio bora zaidi (wa kesho -Akhera) na tunajua kwamba katika hali yoyote ile utumwa utavyojitokeza katika kuji-ficha kwake katika wakati wa kudhihiri tena kwa Imamu wa Kumi na mbili, yeye anayengojewa, (utumwa huo) utalaz-imika kutoweka na kuicha nafasi yake kwenye undugu na heshima ya kibinadamu kwa watu wote. 150. Ameer Ali, Spirit of Islam, uk. 267

MAELEZO YA NYONGEZA (POST SCRIPT)

Mheshimiwa Mwandishi (wa kitabu hiki) aliandika nyongeza ya maelezo katika mwaka wa 1987 wakati Afrika ya Kusini ilikuwa bado ni Taifa la kibaguzi (ubaguzi wa rangi) na shirikisho la Urusi (Sovieti Union) ilikuwa bado ni taifa lenye nguvu sana. Licha ya mabadiliko haya muhimu katika uwanja wa kisiasa ulimwenguni, maelezo ya mwandishi kuhusu utumwa wa kitaifa (taifa moja kutumikishwa na lingine ) bado ni halali wakati huu wa mwanzo wa karne mpya. Ukoloni mambo leo bado upo katika mifumo mbalimbali tofauti na sasa Baraza la Umoja wa Mataifa (UNO) linatu-miwa kama mhuri wa kibali cha kuendelezwa zaidi shabaha na malengo ya mataifa yenye nguvu sana yaliyobaki katika ulimwengu huu. Nchi ya Marekani (USA) na washirika wake wa Ulaya walitumia "Kadi ya demokrasia," demokrasi ya kuteuliwa katika Ulimwengu wa Tatu inavumilika tu kama itahakikisha faida na maslahi ya nchi za Magaribi, kama ilivyoonekana katika suala la Algeria na Uturuki. Baraza la Usalama, Baraza pekee lishughulikalo na maa-muzi ya Baraza la Umoja wa Mataifa (UNO), linaendesha shughuli zake katika misimamo isiyokuwa ya kidemokrasia. Inatumika kwa kuchaguliwa tu au kuteuliwa katika kuhalal-isha maslahi ya matajiri na wenye nguvu juu ya mataifa yaliyo dhaifu ya ulimwengu. Nchi ambayo iko ndani ya 'vitabu vibaya' vya nchi za Magharibi kamwe nchi hiyo hai-wezi kupatiwa uamuzi ulio sawa na haki wakati nchi ya Iraq ilipoivamia Iran, hakukuwepo na dhoruba kali la jangwani, lakini wakati nchi hiyo hiyo, yaani Iraq ilipoivamia Kuwait na kuitishia Saudia (Saudi Arabia) na washirika wengine katika eneo hilo. "majeshi ya ushirika huo" yaliungana kwa kibali cha ridhaa ya Umoja wa Mataifa (UNO). Jinai hiyo katika hali zote lilikuwa sawasawa na kutendwa na mhalifu yule yule, lakini bado hali iliyooneshwa kwa mhalifu ilikuwa tofauti kwa sababu tu muathirika wa pili (yaani Kuwait) alikuwa mshirika wa upande wa nchi za Magharibi wakati ambapo huyo muathirika a kwanza (Iran) hakuwemo ndani ya vitabu vizuri vya nchi ya Marekani (USA).

The New World Order (mpango wa Marikani) kwa hakika ni zama ya unafiki: Mataifa yenye nguvu za kijeshi bado yanaendelea kulundika na kutengeneza zaidi silaha za kisasa zenye maangamizi makubwa na wakati huo huo wanaende-lea kuhubiri kwa mataifa dhaifu kuhusu kujizuia wasiten-geneze silaha kama hizo! Wakiwa mbele kwa masuala ya mazingira; wachafuzi wakubwa kabisa wa mazingira ni mataifa yenye viwanda vingi: lakini bado ni nchi ya Marekani (USA) ambayo ndiyo inakataa kutia sahihi mkata-ba wa kuzuia momonyoko wa ukanda wa hewa safi katika anga-hewa. Kanuni ya uadilifu ya haki kwa wote siyo kawaida katika mpango huu wa Marikani (New World Order). Maslahi binafsi ya matajiri na nchi zenye nguvu, katika istilahi yake zaidi ya kistaarabu ya "maslahi ya kitaifa" bado ndio ufun-guo unaofanya kazi katika mchezo huu. Pengo lililopo kati ya nchi za Kaskazini na Kusini linakuwa kwa haraka sana. Serikali za nchi masikini haziko huru kutekeleza sera zao wenyewe; ni Benki ya Ulimwengu, chombo kingine cha Ukoloni mambo leo, ambayo ndiyo inayowaundia sera za kiuchumi watu wan chi hizo. Sera hizi haziboreshi wengi wa watu katika nchi za Afrika na Asia.

Kwa masikitiko sana, hata katika suala la utambuzi wa mis-iba ya watu inaonyesha kunakuwepo na ubaguzi; msiba wa kundi moja la watu ambao waliteseka katika mikono ya Wanazi unafahamika kwa mapana sana (na Pia wakaza-wadiwa kuwa na "Nchi ya kuishi" ambayo baadaye inageu-ka kuwa "taifa") wakati ambapo utambuzi wa msiba wa mamilioni ya Waafrika ambao walichukuliwa na kupelekwa katika nchi za Amerika na kunyang'anywa jina lao, utambulisho, dini, lugha na haki za msingi za kibinadamu bado ni jambo lilioko katika kujadiliwa. Na tukiwa pamoja na mwandishi, tunamwomba Muumba Mwenye Nguvu Zote aharakishe kudhihiri kwa Mahdi, aliye Masihi, ambaye atauondolea ulimwengu na uonevu na kuieneza haki na amani katika ulimwengu. Amin. "Enyi watu! Hakika Adamu hakuzaa mtumwa mwanaume au mtumwa mwanamke, wanadamu wote wako huru."

Imamu Ali(a.s) Maoni ya watu kuhusu utumwa ni kwamba umetupwa kwenye mapipa ya takataka ya historia, wakati bado athari za ushenzi huu wa kuchukiza ambao mwanzo wake ulikuwa dhidi ya Waafrika, unajitokeza wenyewe kwa sura mpya na mbaya zaidi kwenye karne ya 21. Tangu kupigwa marufuku kwake rasmi katika mwaka wa 1863, utumwa umechukuwa sura ya uovu na ya kuchukiza zaidi, katika muundo wa utumwa uliopakazwa mafuta kwa mgongo wa chupa. Utandawazi kupitia umiliki wa nguvu za kuzalisha unao-fanywa na "Muungano wa Kimataifa wa Wakiritimba" (Multi National Cartels) ni muundo mpya wa utumwa. Allamah Rizvi anaelezea suala hili la biashara ya utumwa kwa muktadha wake halisi. Allamah Sayyid Saeed Akhtar amekiandika kitabu hiki kwa uwezo mkubwa na jitihada. Kama ilivyo kwa msomi mtafiti kama yeye, ameshuhgulikia mada ya kitabu hiki bila upendeleo, Ameupanga ukweli baada ya ukweli kutoka kwenye historia; amenukuu kutoka kwenye Qur'an, Hadithi na waandishi wa zama za leo kuhusu somo hili, na ameonyesha sheria za Kiislamu na zile zilizotumika kabla ya Uislam. Ameonyesha waziwazi kwamba ustaarabu wa Kimagharibi sio bingwa mkubwa kiasi hicho wa kuwaokoa watumwa kama unavyojionyesha na kujigamba. Kwa kweli kitabu hiki kitathibitisha kuwa kifungua macho kwa wale ambao hukubali bila kuchunguza kuhusu propaganda ya ubinadamu wa Kimagharibi.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU


7