• Anza
  • Iliyopita
  • 6 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 16306 / Pakua: 2208
Kiwango Kiwango Kiwango
UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

Mwandishi:
Swahili

5

UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

KWA NINI UTUMWA ULIKOMESHWA

Mtu anaweza akasema: "Hivi haikuwa Uingereza ya Kikristo hatimaye ndio iliyo komesha utumwa? Vema, kama mtu anafanya udhalimu si yeye ndiye anayetakiwa kuen-deleza udhalimu huo? Kama ambavyo imekwisha elezewa, Uingereza ilikuwa ndio mfanya bishara ya watumwa mkub-wa zaidi ya wote, na nguvu za kiuchumi zilipoilazimisha kukomesha biashara ya watumwa, ilifanya hivyo. Je! ni Uingereza inayostahili au Ukristo ndiyo unastahili kupewa shukurani zozote kwa tukio hilo? Kwa nini tusizishukuru nguvu za uchumi ambazo ndizo zililazimisha Uingereza kutokuendelea na biashara hiyo? Ukweli ni kwamba harakati dhidi ya utumwa hazikuon-gozwa na makanisa; kazi hiyo ilifanywa na watu waadilifu wachache ambao vilio vyao vilikuwa havisikilizwi hadi pale umuhimu wa kiuchumi ulipolazimisha Bunge kupitisha muswada mnamo mwaka wa 1870 dhidi ya biashara ya watumwa. Baada ya miaka 26, muswada mwingine ulipi-tishwa kukomesha utumwa katika makoloni ya Uingereza mnamo mwaka 1833. Kama Profesa D.W. Brogan alivyoandika kwenye utangulizi wa kitabu cha Dk. Eric Williams ambacho ni kizuri, kiitwacho "Capitalism and Slavery", "Kukomeshwa kwa biashara ya utumwa halafu kusitishwa kwa utumwa, hayakuwa tu matokeo ya kuboreka kwa kiwango cha mfumo wa maadili ya kisiasa humo Uingereza (ingawaje Dk. Williams hadharau kazi ya watu kama Clarkson kuwa ina umuhimu) lakini ilikuwa namna ya kupunguza hasara. Ukiritimba wa kilimo cha miwa cha visi-wa vya West Indies haukuvumilika kulinganishwa na jamii ya viwanda iliyokuwa inastawi haraka, yenye kujiamini kwa usahihi katika nafasi yake ya ushindani isio tetereka mnamo siku za mwanzo za mageuzi ya viwanda. "Kufupisha, kwa maneno ya Profesa Brogan, mpango wa utumwa ulikuwa "unavumiliwa, unatetewa, unasifiwa almuradi ulikuwa na faida."

"Mpango wa mtumwa ulikuwa na faida sana na kwa kipin-di kirefu. Mafanikio ya Bristol na Liverpool na kwa kiwango fulani, ya Glasgow yalitegemea faida ya mashamba ya miwa ya visiwa vya West Indies. Mkulima wa West Indies alikuwa mshindani wa ufahari wa tajiri mpenda anasa wa East Indies. Ilikuwa kama kupoteza muda kwa waadilifu kuonyesha kwamba kila tofali lililojenga maghala makubwa ya Bristol na Liver pool lilitokana na damu ya Mtu Mweusi. Lakini sauti ya waadilifu ilisikika mara chache sana mion-goni mwa mlio wa sarafu ya Uingereza Guine (jina hilo hilo linakumbusha biashara ya pembe-tatu baina ya Uingereza, Afrika na makoloni ya transatlantic)." "Biashara ya pembe tatu" maana yake ni nini? Kutoka Uingereza, bidhaa mchanganyiko "mfano halisi wa mzigo wa mfanya biashara ya watumwa" ulipelekwa Africa. Mavazi mazuri na umalidadi kwa Waafrika, vyombo vya nyumbani, nguo za kila aina, chuma na metali, pamoja na bunduki, pingu na minyororo." Kutoka Afrika mzigo wa binadamu ulichukuliwa kupelekwa visiwa vya West Indies na nchi za Amerika. Kutoka West Indes na makoloni mengine; sukari, tumbaku na rangi ya buluu, pamba, kahawa na malighafi zingine zilipelekwa nchi mama (yaani Uingereza) ambako yalitengenezwa kwenye viwanda na halafu yakaingizwa tena kwenye makoloni. 135.

Mashamba yalianzishwa kwa sababu ya kuwepo nguvu kazi ya utumwa na yakalindwa na ukiritimba. Halafu ukaja mtengano wa makoloni 13 ya Marekani ambayo yalifunga soko kubwa dhidi ya nchi iliyohuru makoloni ya Uingereza ya visiwa vya West Indies. Athari yake nyingine ilikuwa kwamba nchi iliyo huru sasa, ya Marekani (U.S.A.) iligeuka kwenye makoloni ya Ufaransa yaani Visiwa vya Saint Domingue (Haiti), Cuba na Brazil. Dk. Williams anaandika, "Ubora wa makoloni ya sukari ya Ufaransa ulikuwa kwa ajili ya wakulima wa Kiingereza, kubwa miongoni mwa maovu mengi ambayo yalijitokeza nje kutoka kwenye Pandora's box o (sanduku la Pandora) ilikuwa ni mapin-duzi ya Marekani. Kati ya mwaka 1783 na 1789 maendeleo ya sukari ya visiwa hususan vya Ufaransa, vya Saint Domingo (Haiti), hususan lilikuwa jambo la kushangaza katika maendeleo ya kikoloni. Rutuba ya udongo wa makoloni ya Ufaransa ilikuwa ni ya wazi mno, sukari ya Ufaransa iligharimu moja ya tano ( 1/5) chini zaidi ya ile ya Uingereza, mavuno ya wastani huko Saint Domingo na Jamaica yalikuwa tano kwa moja." 136 Athari iliyosababisha maafa kwenye makoloni ya Uingereza ya West Indies inaweza kuamuliwa na ukweli kwamba "mwaka 1775 Jamaica ilikuwa na mashamba 775; 135. Williams, Dr. Eric. Capitalism and Slavery uk. 65. **Pandora box ni maneno ya methali, maana yake ni mpango ambao ukihamasishwa huzalisha matatizo mengi yasiyodhibitika. 136. Ibid, uk. 122. hadi kufika 1791, katika kila mashamba mia moja, masham-ba ishirini na tatu yaliuzwa kwa ajili ya kulipa, kumi na mbili yalikuwa kwenye miliki ya wafilisi, wakati saba yali-achwa; na wakulima wa West Indies, wakiwa na deni la kiasi cha pauni milioni ishirini." Polepole, wakulima wa Kiingereza walipoteza moja kwa moja mamlaka yao ambayo waliyafurahia kwa kipindi kirefu katika soko la Ulaya. "Uuzaji wa bidhaa nje kutoka makoloni ya Ufaransa, uliingiza pauni za Kiingereza zaidi ya milioni nane, na Uingizaji bidhaa ndani ya nchi, zaidi ya pauni milioni nne, tani zilizo shughulikiwa 164,000 na wafanya kazi wa meli 33,600; uuzaji wa bidhaa nje kutoka makoloni ya Uingereza uliingiza pauni za Kiingereza milioni tano, na uingizaji bidhaa ndani ya nchi chini ya milioni mbili, tani zilizo shughulikiwa, 148,000 na wafanya kazi wa meli 14,000. Katika hali zote makoloni ya sukari yalikuwa na umuhimu mkubwa sana kwa Ufaransa kuliko yalivyokuwa kwa Uingereza."

1 3 7. Hivyo, gharama ya sukari (na hivyo hivyo kwa bidhaa zingine zote.) ilianza kwenda juu sana. Dk. Williams anaeleza, "Ukiritimba wa mkulima wa West Indies haukuwa tu jambo lisilofaa kinadharia, haukuwa na faida katika hali halisi. Mnamo mwaka 1828 ilikisiwa kwamba ili-wagharimu raia wa Uingereza zaidi ya pauni milioni moja na nusu kwa mwaka. Mnamo mwaka 1844, ulikuwa unagharimu nchi pauni 70,000 kwa juma moja na jiji la London peke yake pauni 6,000. Uingereza ilikuwa inalipa zaidi ya pauni milioni tano kwa ajili ya sukari yake kwa mwaka kuliko Bara lote la Ulaya... Mbili ya tano (2/5) ya bei ya ratili moja ya sukari iliyotumiwa Uingereza iliwaisha 137. Ibid, uk. 123. gharama ya uzalishaji, mbili ya tano ( /$) ilichukuliwa kama ushuru wa serikali, moja ya tano ( 1/5) shukurani kwa mkulima wa West-Indies..." o Pole pole, Saint Domingue (Haiti) koloni la Ufaransa, lili-ibuka kama mzalishaji muhimu sana wa sukari. Kwa mtazamo wa Waziri Mkuu wa Uingereza, William Pitt, hili lilikuwa jambo lenye uamuzi. Umri wa visiwa vya Uingereza vya sukari ulifika mwisho. Mpango wa West-Indian haukuwa na faida, na biashara ya watumwa ambayo ndio ilikuwa tegemeo lake, badala ya kuwa na manufaa kwa Great Britain... ni ya uharibifu mno ikilinganishwa na dhana ya maslahi. ^"- Kwa hiyo, Pitt aligeukia India kulima na kuzalisha sukari. Mpango wa Pitt ulikuwa na sehemu mbili: kurejesha soko la Ulaya kwa msaada wa sukari kutoka India, na kupata fursa ya kukomesha biasharra ya watumwa kimataifa tukio ambalo lingeiangamiza Saint Domingue. Kama haingekuwa ukomeshaji wa Uingereza. Wafaransa waliwategemea sana wafanyabiashara ya watumwa wa kimataifa, basi ingekuwa ukomeshaji wa Uingereza hivyo kwamba hata kama Uingereza peke yake ingepiga marukufu biashara ya watumwa, uchumi wa makoloni ya Ufaransa ungetetereka.

"Mpango wa Pitt ulishindwa kwa sababu mbili. Umuhimi wa sukari ya kutoka India ya Mashariki, kwa kiwango kili-chopangwa, haingewezekana kwa sabahu ya kodi ya ushuru kuwa juu iliyowekwa kwa sukari yote isipokuwa ile iliyoza-lishwa kwenye makoloni ya Uingereza ya West-Indies... Pili, Wafaransa, Wadachi na Wahispania walikataa 138. Ibid, uk. 138-9. 139. Ibid, uk. 146. kukomesha biashara ya utumwa. Ilikuwa rahisi kuona malengo halisi ya kisiasa yaliyoko nyuma ya pazia la ubi-nadamu la Pitt. Gaston-Martin, Mfaransa maarufu mwenye taaluma ya historia ya biashara ya watumwa na makoloni ya Caribbean, anamlaumu Pitt kwa kutaka kuwapa uhuru watumwa kwa kutumia propaganda, hapan shaka kwa kutu-mia jina la ubinadamu. lakini pia kuharibu biashara ya Ufaransa. Na anahitimisha kwamba kwenye propaganda hii ya kiihsani na kiubinadamu palikuwepo na malengo ya kiuchumi.

Halafu pakatokea tukio moja kubwa. Wakulima wa Kifaransa huko Saint Domingo, mwaka 1791, wakihofia matokeo ya Mapinduzi ya Ufaransa, waliwapa Uingereza visiwa hivyo; muda si mrefu Windward Island ilifuata mtin-do huo; Pitt alikubali kuvichukua visiwa hivyo mwaka wa 1793. Vikosi vya jeshi la Ufaransa vilipelekwa kimoja baada ya kingine mara kadhaa lakini havikufanikiwa kuvire-jesha visiwa hivyo kwenye miliki ya Ufaransa. Dk. William anafafanua: "Hii ni zaidi ya manufaa ya kiso-mi. Pitt hangeweza kumiliki Saint Domingo na kukomesha biashara ya watumwa wakati huo huo. Bila ya kawaida yake ya kuingiza watumwa 40.000 kwa mwaka, Saint Domingo ingekwisha filisika. Kitendo cha Pitt kukubalia kuchukua kisiwa hicho kimantiki kilikuwa na maana kwamba hangeendelea na mpango wake wa kukomesha biashara ya watumwa. Kwa wazi hakusema hivyo. Pitt alikwisha fika mbali sana katika kuwaahidi raia wa Uingereza. Aliendelea kuzungumza kuhusu kukomesha biashara ya watumwa hata hapo alipokuwa anaitumainisha biashara ya watumwa katika hali halisi... Sababu za Pitt zilikuwa za kisiasa na kwa kiwango kidogo kibinafsi. Pitt alipendelea biashara ya sukari: Ama ilikuwa lazima aivuruge Saint Domingo kwa kuingiza sukari nyingi sana Ulaya na ya bei rahisi kutoka India au kwa kukomesha biashara ya watumwa; au aichukue Saint Domingo iwe yake binafsi."

140. Hali hii ingeipatia Uingereza ukiritimba wa sukari, rangi ya buluu, pamba na kahawa... Lakini kama Pitt angeikamata Saint Domingo, biashara ya watumwa lazima ingeendelea. Wakati Saint Domingo ilipochukuliwa na Ufaransa, biashara ya watumwa ilichukua sura mpya ya kuwa kama vile suala la ubinadamu tu... Lakini kuharibika kwa Saint Domingo haikuwa na maana ya ukombozi kwa makoloni ya Uingereza ya visiwa vya West-Indies. Walijitokeza maadui wawili wapya kwenye uwanja. Cuba ilisonga mbele na kuziba pengo lililoachwa kwenye soko la dunia baada ya kutoweka Saint Domingo." 141. Wakati ule ule, chini ya mamlaka ya Marekani, sukari ya Cuba na wazalishaji wengine waliokuwa na msimamo wa kati, bado ilipata soko Ulaya, na sukari ya ziada kutoka British West Indian ililundikana Uingereza. Kufilisika kwa wakulima ilikuwa hali ya kawaida. Kati ya 1799 hadi 1807, mashamba 65 ya Jamaica yaliachwa, 32 yaliuzwa kufuta madeni, na malalamiko 1807 ya madai yalikuwa yana ngoja uamuzi dhidi ya 115. Mada zilizokuwa zinazungumziwa hapo kisiwani ni madeni, maradhi na vifo. Kamati ya bunge iliyoundwa mwaka 1807 iligundua kwamba mkulima wa British Indian alikuwa anazalisha kwa hasara. Mwaka wa 1800 faida ya mkulima ilikuwa asilimia 2.5 (2 '2 %), mwaka 140. Ibid uk. 146 -7, Ibid uk. 1487- 8. 141. Ibid, uk. 148-9. wa 1807 hakuna faida. Mwaka wa 1787 mkulima alipata 19/6d. faida kwa kila ratili mia na kumi na mbili; mwaka 1799, 10/9d; mwaka wa 1803, 18/6d; 1805, 12/-; katika kwaka 1809, hasara. Kamati ilidhani sababu kubwa ilikuwa hali mbaya ya soko la nje. Mwaka 1809 sukari ya ziada ya Uingereza ilikuwa tani 6,000. Uzalishaji ukasitishwa. Kuwekea mipaka uzalishaji, biashara ya watumwa lazima ikomeshwe." 1 Kwa hiyo, kwa maneno ya Dk. Williams, "Kukomeshwa kwa biashara ya watumwa moja kwa moja ilisababishwa na kuvurugika kwa uchumi huo.

UNAFIKI WA WAKOMESHAJI WA BIASHARA YA WATUMWA

Kama mtu yeyote anataka kudhani kwamba sababu ya kukomeshwa kwa utumwa ni maendeleo ya unyofu wa maadili, basi anashauriwa kuangalia msimamo wa watu waliokuwa wanashughulikia suala la kukomesha biashara ya watumwa katika mfumo wa malengo yao ya kiuchumi. Hivyo tunaona kwamba wale wale washikiliaji wa maslahi ya West Indies ambao kabla ya tatizo lililotajwa, walikuwa ni waungaji mkono motomoto wa biashara ya watumwa sasa waligeuka kuwa "waungwana wenye huruma na shauku ya kuukomesha utumwa". Dk. Williams anasema, kwa kejeli kabisa, ilikuwa ni wamiliki wa watumwa wa siku za nyuma wa West Indies ambao sasa walishikilia tochi ya kuwahuru-mia binadamu. Wale ambao, katika mwaka wa 1807, kwa majonzi walikuwa wanatabiri kwamba kukomesha biashara ya 142. Ibid, uk 149. 143. Ibid, uk 150. watumwa ya Uingereza "ingesababisha kupungua kwa biashara, kupungua kwa ushuru wa kodi, na kupungua kwa safari za baharini; na hatimaye kudhoofisha na kuondoa kabisa msingi mkuu wa ustawi wa Uingereza, walikuwa, baada ya 1807, watu wale wale waliokataa 'mpango wa mtu' kuwaiba watu masikini na ambao hawana jinsi ya kujitetea." Manufaa ya West India katika mwaka wa 1830 yaliweka azimio la "kuchukua hatua madhubuti zaidi kusitisha biashara ya watumwa ya nje; kushughulikia suala la ukan-damizaji uliokwisha fanywa ambao kwamba ustawi wa makoloni ya Uingereza ya West Indes... hatimaye yali-utegemea. Wajumbe kutoka Jamaica, walopelekwa Uingereza mwaka 1823, walitangaza kwamba makoloni yangepatanishwa kwa urahisi kuhusu kukomeshwa kwa biashara ya kishenzi na ya kinyama, ambayo ustaarabu ulioendelea wa wakati huu hukuiruhusu tena kuwepo... Kundi kubwa la kukomesha biashara ya watumwa lilijidhi-hirisha nchini Jamaica katika mwaka 1849. Auj claplo, vyama na madhehebu viliunganishwa kuhusu suala la Africa kutendewa haki. Walilaani biashara ya watumwa na utumwa kama ni "kinyume cha ubinadamu iliyozalisha maovu mabaya sana Afrika - kuwadhalilisha wote walio-husika katika biashara hiyo, na kudhuru maadili na utashi wa kiroho wa watumwa, na kusihi kwamba neno la kuchuk-iza 'mtumwa' liondolewe kwenye msamiati duniani pote. UTUMWA LAZIMA UANGUKE, na utakapoanguka, JAMAICA ITASTAWI! walitamka kwa ukali, iliingia kwenye vita nyingi bila ya sababu zilizo halali." 144. 144. Ibid, uk 175-6.

Na palikuwepo na manufaa gani ya vifungu vya maneno vilivyo vikali na ambavyo vinaweza kuamuliwa kutokana na ukweli kwamba ubepari wa Uingereza, hata baada ya kuvu-ruga utumwa wa West Indian, "Uliendelea kustawi kutokana na utumwa uliokuwa unaendelea huko Brazil, Cuba na utumwa wa Amerika ya Kaskazini na Kusini." Kwa hiyo, kwa maneno ya Profesa Brogan, "tunapata mafumbo ya wajibu uliogeuzwa. Ilikuwa sawa kabisa kwa watetezi wa hoja ya kukomeshwa utumwa, kulaani matumizi ya sukari iliyo zalishwa na watumwa kutoka West Indes, lakini haku-na aliyependekeza kusimamisha matumizi ya pamba iliy-ozalishwa kutoka Marekani (U.S.A.). Hakika, hakuna mtu aliyependekeza kwa dhati kuacha kutumia sukari iliyozal-ishwa na watumwa kutoka Brazil au Cuba. Fedha sio hisia, hisia za uovu za uzuri, husokota na kupotosha njama." Dk. Williams anaandika, "Baada ya India, Brazil na Cuba, bila ya dhana yoyote. Je, muungwana yeyote angeweza kuhalalisha pendekezo lolote lililopangwa kuimarisha miny-ororo ya utumwa ambayo bado imewafunga Watu Weusi wa Brazil na Cuba. Kwa usahihi hiyo ndio ilikuwa maana ya biashara huru ya sukari. Kwani baada ya mwaka 1807 British West Indians walikataliwa na kunyimwa kuendesha biashara ya watumwa, na baada ya 1833 wakanyimwa nguvu kazi ya watumwa. Kama watetezi wa kukomesha utumwa walipendekeza sukari ya kutoka India, kwa makosa, kwa misingi ya ubinadamu kwamba ni sukari iliyolimwa na watumwa huru, ilikuwa ni wajibu wao kwa kanuni zao na dini yao kususia sukari iliyolimwa na watu wa Brazil na Cuba. Katika kuanguka kufanya hivi isiamuliwe kwamba hawakuwa sahihi, lakini si jambo la kukanusha kwamba kushindwa kwao kutumia njia hiyo ilivuruga hoja ya ubinadamu. Baada ya 1833, watetezi wa kukomesha utumwa, waliendelea kumpinga mkulima wa West Indian ambaye sasa aliajiri wafanya kazi huru. Ambapo, kabla ya hapo 1833, waliwagomea wamiliki wa watumwa wa Uingereza, baada ya 1833 waliunga mkono sababu ya wamiliki wa watumwa wa Brazil."

145. Kuondolewa kwa Watu Weusi kishenzi kutoka Afrika ni shughuli iliyoendelea kwa karibu miaka 25 tangu 1833, ambao walipelekwa kwenye mashamba ya miwa ya Brazil na Cuba. Uchumi wa Brazil na Cuba ulitegemea biashara ya watumwa. Msisitizo peke yake ulidai kwamba watetezi wa kukomesha utumwa wa Uingereza walipinga biashara hii. Lakini jambo hilo lingerudisha nyuma maendeleo ya Brazil na Cuba na matokeo yake kuzuia biashara ya Uingereza. Haja ya kupata sukari ya gharama ya chini baada ya 1833 ilishinda chuki yote ya utumwa. Tishio ambalo hapo mwan-zo lilichochewa na fikira ya mswaga watumwa wa Uingereza wa West Indies mwenye mjeledi; mswaga watumwa wa Cuba mwenye mjeledi, panga, jambia,. kisu na bastola na kufuatwa na mbwa mwitu, haikuamsha hata maoni ya watetezi wa kuzuia biashara ya watumwa." 146. Hivyo ni wazi kwamba sababu halisi yaubinadamu na uung-wana wa Uingereza wala haikuwa usawa wa kiunyofu au mwamko wa kimaadili bali ilikuwa ni kwa sababu ya shinikizo la kiuchumi na kuwaumiza washindani wao wa biashara. Kwa maneno ya Profesa Brogan, somo la Ubepari na Utumwa linavunja moyo na kufadhaisha kama si jipya. "Pale ilipo hazina yako ndipo moyo wako unapo lala.' 145. Ibid, uk 188. 146. Ibid, uk. 192.

ILIKUWA NI VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE YA MAREKANI

Je, ni ya kuwakomboa watumwa? Nadhani itakuwa kwa manufaa ya wasomaji kutizama kwa umakini hadithi isemayo kwamba vita ya Marekani ya wenyewe kwa wenyewe ilitokea kwa lengo la kuwakomboa watumwa. Ni ngano ambayo iliyobuniwa na haina uhusiano wowote na hali halisi ya ukweli. Nina nukuu hapa kutoka kwenye sura ya 22 ya "Lincoln, the Unkown" kilichoandik-wa na mwandishi wake maarufu Dale Carnegie. 1 Anaanza na maneno haya: - "Muulize raia wa kawaida wa Kimarekani leo kwa nini Waamerika walipigana vita ya wenyewe kwa wenyewe, atakacho kuambia ni kwamba, 'Kuwakomboa watumwa.' "Ni kweli hivyo?" "Hebu tuangalie. Hapa ni sentenso ambayo imechukuliwa kutoka kwenye hotuba ya kwanza ya Lincoln ya kuzindua urais wake. 'Sikusudii kuingilia kati, taasisi ya utumwa, moja kwa moja au kuzunguuka kwenye majimbo ambayo utumwa bado upo. Nina amini sina haki ya kisheria kufanya hivyo, na sipendelei kufanya hivyo." Ukweli ni kwamba mzinga ulikuwa unanguruma na majeruhi wanatoa sauti ya kulemewa kwa takribani miezi kumi na nane kabla Lincoln hajatoa tangazo la "Ukombozi wa watumwa." 147. Carnegie, Dale, Lincoln: The Unknwown (Surrey, U.K.: The World Work Ltd. 1948) Sura ya 22 Wakati wote huo watu wenye msimamo Mkali na Watetezi wa kukomesha utumwa walimsihi achukue hatua haraka, walimshambulia kupitia kwenye magazeti na kumshutumu kwenye majukwaa ya mikutano. "Wakati mmoja ujumbe wa mawaziri wa Chicago ulikwen-da Ikulu ya Marekani na kile walichokitangaza kwamba ilikuwa ni amri ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu Mweza wa Yote kuwaachia watumwa kuwa huru haraka sana. Lincoln aliwaambia kwamba alidhani kwamba kama Mweza wa Yote alikuwa na ushauri wowote wa kutoa, Angekuja moja kwa moja makao makuu na ushauri huo, badala ya kuwasilisha kwa mzunguuko wa kupitia Chicago." Zaidi ya hayo, Dale Carnegic anaendelea kunukuu kutoka kwenye jibu la Lincoln alipojibu makala ya Greedy, 'The Prayer of Twenty million.'('Sala ya milioni ishirini).

"Kusudio langu kubwa katika mapambano haya ni kuokoa Muungano, na wala si kuokoa au kukomesha utumwa. Kama ningeokoa Muungano bila kumpa uhuru mtumwa hata mmoja, ningefanya hivyo; na kama ningeokoa Muungano kwa kuwapa uhuru wa watumwa wote ningefanya hivyo, na kama ningeuokoa Mungano kwa kuwapa uhuru baadhi yao na kuwaacha wengine, pia ningefanya hivyo. Ninachofanya kuhusu watumwa na machotara, ninafanya hivyo kwa sababu ninaamini inasaidia kuokoa Muungano, na kile ninachovumilia, ninavumilia kwa sababu siamini kama ingesaidia kuokoa Muungano. Sitafanya yote wakati wowote nitakapoamini kile ninachokifanya kitadhu-ru lengo; na nitazidisha juhudi nitakapoamini kufanya hivyo itasaidia lengo." Akifafanua jibu hilo Dale Carngie anaandika: "Majimbo manne yamebakia na watumwa pamoja na Kaskazini, na Lincoln alitambua kwamba kama angetoa tangazo la "ukombozi wa watumwa" mapema mno katika mzozo huu, angewafukuzia kwenye Shirikisho, kuimarisha kusini, na pengine kuvunja Muungano daima milele. Palikuwepo na methali wakati huo ambayo Lincholn angependa kuwa na Mungu Mweza wa Yote upande wake, lakini lazima aipate Kentucky. "Hivyo alisubiri wakati mzuri, na kufanya mambo kwa tahadhari" "Lincoln mwenyewe alioa kwenye familia yenye kumiliki watumwa, ya Jimbo la mpakani. Sehemu fulani ya fedha ambayo mke wake Lincoln alipokea ilitoka kwenye urithi wa shamba la baba yake ambayo ilitokana na mauzo ya watumwa. Na rafiki mmoja tu wa karibu sana na wa kweli ambaye Lincoln alikuwa naye, alikuwa Joshua Speed ambaye alitoka kwenya familia yenye watumwa. Lincoln aliwahurumia watu wa Kusini kwa maoni yao. Kwa upande mwingine, alikuwa na desturi ya kumshehimu mwanasheria Mkuu kuhusu Katiba na sheria na rasilimali. Hakutaka kus-ababisha shida kwa mtu yeyote. (ila kwa watumwa)

"Lincoln aliamini kwamba majimbo ya kaskazini yalistahili kulaumiwa sana kwa kuendelea kuwepo kwa utumwa "Marekani (U.S.A) " kama ilivyo huko kwenye majimbo ya Kusini; na kwamba kuliondoa tatizo hilo, sehemu zote lazima zivumilie mzigo sawa kwa sawa. Kwa hiyo hatimaye alitengeneza mpango ambao ulikuwa karibu sana na moyo wake. Kwa mujibu wa mpango huo, wamiliki wa watumwa waliokuwa kwenye mipaka ya majimbo yenye uaminifu walipewa dola mia nne kwa kila Mtu Mweusi. Watumwa walitakiwa kuachiwa huru polepole, polepole sana. Mlolongo wa mambo haya haukutakiwa kumalizika kikamilifu hadi Januari 1, 1900. Lincoln aliwaita wawakil-ishi kutoka kwenye Majimbo ya mipaka wamuone huko Ikulu White House, akawasihi wakubali pendekezo lake. "Lincoln alihoji na kusema, mabadiliko yaliyomo kwenye pendekezo lake, yanakusudiwa kuja polepole kama umande unavyo dondoka kutoka mbinguni, bila kupokonya au kuvunja matarajio ya watu. Kwa nini msikubali pendekezo hili? Mambo mengi sana mazuri bado hayajafanyika kwa jitihada moja, katika wakati wote uliopita, kama ilivyo katika upaji wa Mungu sasa hivi ni upendeleo wenu wa juu kutekeleza. Muda mwingi ujao na upana wake usije ukalalamika kwamba ulipuuzia jambo hili."

Msomaji angekumbuka kwamba mpango huu wa kuwapa watumwa uhuru "kwamba ulikuwa karibu mno na moyo wake Lincoln" ulikuwa sawa na mpango ambao tayari ulik-wisha wekwa na kutekelezwa miaka 1300 iliyopita katika Uislam na ambao ulitoa matokeo ya kushangaza katika ulimwengu wa Kiisilamu. Kama mpango huo ungekubaliwa na ndugu zake Lincoln, hapange kuwepo na chuki kubwa baina ya mataifa, migongano ya ndani, mageuzi ya kijamii na udhaifu wa hisia ambao bado unaendelea kuwepo nchini Marekani (U.S.A.) karne moja baada ya kile kilichoitwa Ukombozi wa watu weusi (Emancipation of Negroes). Bahati mbaya, wawakilishi wa Majimbo hayo yaliyokuwa yanapakana walikataa mpango huo. Carnegie anasema, "Lincoln mara moja alikasirika sana. Lazima niiokoe serikali hii, kama inawezekana, alisema na inaweza ikaeleweka, kwa mara zote, kwamba sitakubali kuacha mchezo huu, na kuacha kadi yoyote ile ipatikanayo iwe hai-jachezwa.... Ninaamini kwamba kuwapa uhuru watumwa na kuwapa silaha watu weusi sasa imekuwa jambo la msin-gi na muhimu kivita. Nimesukumwa kwenye uchaguzi ama kutekeleza hilo au kuuwachia) Muungano (usambaratike). "Ilibidi Lincoln ashughulike haraka, kwani Ufaransa na Uingereza walibakia kidogo watambue Shirikisho. Kwanini? Sababu zilikuwa rahisi. Tuchukue mfano wa Ufaransa kwanza."

Napoleon wa III alikuwa mfalme wa Ufaransa. Alikuwa na shauku kubwa ya kutaka utukufu wa mamlaka ya utawala, kama alivyokuwa ami yake mtukufu, Napoleon Bonaparte, alivyo fanya. Kwa hiyo, alipoona majimbo yanapigana, na alitambua kwamba walikuwa na shughuli nyingi mno kuweza kufikiria kuhusu utekelezaji wa sheria ya "Momoe Doctrine," aliamuru jeshi kwenda Mexico, huko likaua wazalendo elfu kadhaa, likashinda nchi, ikaitwa Mexico iliyo chini ya himaya ya Ufaransa, na likamweka Archduke Maximilian kukalia kiti cha enzi. "Napoleon aliamini na si bila sababu, kwamba kama kundi linalotaka shirikisho lingeshinda, lingependelea ufalme wake mpya; lakini kama kundi linalotaka shirikisho lingeshinda, United States ingechukua hatua za haraka za kuifukuza Ufaransa huko Mexico. Kwa hiyo, ulikuwa ni upendeleo wake Napoleon, kwamba Kusini ifaulu kujitenga, na alitaka kuisaidia kutekeleza kujitenga huko kwa kadiri ya uwezo wake. Mwanzoni mwa vita, jeshi la majini la Kaskazini lilifunga bandari zote za Kusini, bandari 189 zikawa chini ya ulinzi wao na walifanya doria kwenye eneo la maili 9,614 za uwanda wa pwani, njia nyembamba za maji zinazoungan-isha bahari na zinazounganisha bahari na maziwa, vinamasi na mito. Hiki kilikuwa kizuizi kikubwa mno ambacho ulimwengu haujapata kuona. Kundi lililotaka Muungano lilikuwa lina haha. Halikuweza kuuza pamba yake, wala kuweza kununua bunduki, risasi, viatu, madawa au chakula. Watu hawa walianza kuchemsha karanga na mbegu za pamba kuwa mbadala wa kahawa, na walianza kuchemsha majani ya miti ya matunda mithili ya mibuni na kuchuja maji yake na kuwa mbadala chai. Magazeti yalianza kuchapishwa kuwekwa kwenye matangazo. Nyumba zenye sakafu za udongo na zenye kufuka moshi, zililoweshwa dabwa dabwa kwa mafuta ya wanyama, zikachimbuliwa na kuchemshwa ili kupata chumvi. Kengele za makanisa ziliyeyushwa na kutiwa katika mizinga. Reli za magari madogo mitaani katika mji wa Richmond zilikatwa katwa na kufanywa silaha katika mashua za kivita zenye bunduki.

Watu wa Muungano hawakuweza kuzifanyia matengenezo reli zao au kununua vifaa vipya, kwa hiyo usafiri ulibakia kidogo sana; nafaka ambayo ilinunuliwa kwa dola mbili, pishi tisa huko Geogia, ilinunuliwa kwa dola kumi na tano Richmond. Watu waishio Virgini walikuwa wanashinda na njaa. Ilibidi utaratibu fulani ufanywe haraka sana. Kwa hiyo, Kusini walikubali kumpa Napoleon wa III dola milioni 12 kama angeutambua Muungano na atumie meli za Kifaransa kuondoa kizuizi. Kwa upande mwingine, waliahidi kumzidishia nguvu kwa amri ambayo ingeanzisha moshi kwenye kila kiwanda huko Ufaransa usiku na mchana. Kwa hiyo Napoleon akazisihi Urusi na Uingereza kuungana naye katika kuutambua Muungano. Utawala wa makabaila uliokuwa madarakani, wahusika wake waliweka sawa miwani zao, wakanywa toti kadhaa za Scotch Whisky, na wakasikiliza kwa hamu kubwa mazungumzo ya awali ya Napoleon. Marekani (U.S.A.) ilianza kutajirika sana na kuwa na uwezo mkubwa wa kuwaridhisha, Walitaka kuona taifa linagawanyika, Muungano unavunjika. Kwa upande mwingine, walitaka pamba ya Kusini. Viwanda kadhaa vya Uingereza vilifungwa, na watu milioni moja hawakuwa tu hawana kazi, bali pia kuwa fukara na kushuka chini kuwa omba omba halisi. Watoto walikuwa wanalia njaa, mamia ya watu walikuwa wanakufa kwa sababu ya njaa. Michango ya raia kwa ajili ya kununua chakula cha wafanya kazi wa Uingereza ilichukuliwa na kupelekwa kwenye vijiji vya ndani kabisa ya dunia hata India ilioko mbali sana na China ambayo ilibanwa na umasikini. Palikuwepo na njia moja, na njia moja tu, kwamba Uingereza ingeweza kupata pamba na hiyo ilimaanisha waungane na Napoleon III katika kuutambua Muungano na kuondoa kizuizi. "Kama hilo lingefanyika, nini kingetokea Marekani? Kusini wangepata bunduki, baruti, mkopo, chakula vifaa vya njia ya reli, na msaada mkubwa sana wa hali na mali.

"Na Kaskazini wangepata nini? Wangepata maadui wawili wapya na wenye nguvu. Hali hiyo kuwa mbaya kiasi hicho sasa, hapangekuwepo na matumaini. "Hakuna aliyejua hilo vizuri zaidi kumzidi Abraham Lincoln. "Ni kama vile tumecheza kadi yetu ya mwisho', aliungama hivyo katika mwaka 1892. Ama lazima tubadili mbinu zetu au tukubali kushindwa mchezo.' Kama ilivyoona Uingereza, makoloni yote yalikwisha jitoa kutoka kwenye utawala wake tangu mwanzo. Sasa makoloni ya Kusini nayo yamekwishajitoa kutoka makoloni ya Kaskazini; na Kaskazini ilikuwa inapigana kuilazimisha na kuitiisha Kusini. Je, pangekuwa na tofauti gani kwa mtu wa kawaida huko London au mwana mfalme huko Paris kama Tenessee na Texas zingetawaliwa kutoka Washington au Richmond? Hakuna. Kwao vita haikuwa na maana yoyote na yenye kuleta hatari bila madhumuni ya maana. 'Nilikuwa sijapata kuona vita imepamba moto kama hiyo katika uhai wangu', aliandika Carlyle, 'iliyokuwa inaonekana zaidi kama ya kipumbavu. Lincoln aliona kwamba msimamo wa Ulaya kuhusu vita hiyo lazima ubadilike, na alijua jinsi ya kufanya. Watu mil-ioni moja huko Ulaya walikwisha soma "Uncle Toms Cabin" walikisoma kisa hicho na wakalia na wakajifunza kuchukia michomo ya moyo na udhalimu wa utumwa. Kwa hiyo Abraham Lincoln alitambua kwamba kama angetoa tangazo lake la "ukombozi wa watumwa", watu wa Ulaya wangeiona vita kwa namna tofauti. Haingekuwa tena ugomvi wa kumwaga damu kwa sababu ya kudumisha Muungano ambao haukuwa na maana yoyote kwao. Badala yake, ingetukuzwa kuwa vita takatifu ya kutokomeza utumwa. Serikali za Ulaya hazingeitambua Kusini. Maoni ya watu hayangestahamili kuwasaidia watu ambao wanapi-gana kwa lengo la kuendeleza utumwa wa kibinadamu.

Hatimaye, kwa hiyo, mnamo Julai, 1862, Lincoln akiwa amedhamiria kutoa tangazo lake, lakini McClellan na Papa mnamo siku chache za nyuma waliliongoza jeshi la Kusini kwenye fedheha ya kushindwa mara kadhaa. Seward alimwambia Rais kwamba muda huo haukuwa mwafaka, hivyo angelazimika kungoja na kutoa tangazo kwenye kilele cha ushindi wao. "Ushauri huo ulionekana wa hekima. Kwa hiyo Lincoln akangojea na miezi miwili baadaye ushindi ukapatikana." Na kwa hiyo, kuendeleza Vita ya Muungano, tangazo la "Ukombozi wa Watumwa" lilichapishwa mnamo Septemba 1862, ambalo lilitakiwa lianze kutekelezwa tarehe Moja, Januari 1863. Ninampa Abraham Lincoln heshima ya juu sana na amekuwa mmoja wapo wa mashujaa ninao wapenda tangu nilipokuwa mdogo. Lakini heshima hiyo msingi wake ni kwenye ukweli na hali halisi, si kwenye mambo ya kubuni-wa. Lincoln alikuwa na ubinadamuna, na yeye, kutoka ndani ya moyo wake alikuwa dhidi ya utumwa. Lakini haina maana kwamba tumtukuze kwa propaganda za uwon-go. Uhalisi wa jambo hili ni kwamba hakupigana vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa lengo la kuwapa watumwa uhuru, kwa usahihi zaidi aliwapa watumwa uhuru kwa lengo la kushinda vita na kuokoa Muungano.

UTUMWA WA KIMAJIMBO

Hadi sasa tumechambua aina moja tu ya utumwa, yaani utumwa wa utumishi wa nyumbani kwa mtu. Lakini ilita-jwa kwenye sura ya kwanza kwamba utumwa ni wa aina mbili, aina ya pili ni Utumwa wa Kimajimbo au taifa moja kutumikisha taifa lingine. Licha ya kwamba utumwa wa nyumbani sasa hivi unajulikana kwamba ulikomeshwa, utumwa wa kitaifa bado upo unaendelea. Moyo ukiwa umejaa huzuni mtu anaona uharibifu wa maisha ya binadamu kwa mpango maalum na hadhi ya binadamu inaendelezwa na ustaarabu wa Kikristo karibu katika kila nchi hapa duniani. Wahindi Wekundu walikuwa wakazi wa mwanzo wa Nchi mpya. Wapo wapi sasa? Walitolewa polepole kutoka kwenye ardhi yao na wamelazimishwa kuishi kwenye ardhi yenye rutuba hafifu ambayo haiwezi kuzalisha mazao, vishamba vilivyoko ndani ya Marekani (U.S.A). Waaborigine wa Australia walipitishwa kwenye uonevu wa aina hiyo hiyo. Wahindi Wekundu na Waaborigine walikuwa wanawindwa kama wanyama pori: yaani, nyati na kadhalika na sasa hivi idadi yao inakaribia kufutika kabisa katika uso wa dunia hii. Dk. Eric Williams ananukuu maelezo ya Mkuu wa wahindi wekundu, Hatuey, ambaye alipewa adhabu ya kifo kwa kuwawekea pingamizi wavamizi, alikuwa imara katika kukataa imani ya Kikristo kama njia ya kwenda kwenye wokovu alipotambua kwamba wauaji wake, nao pia walikuwa na matumaini ya kwenda Peponi. 148. Lakuhuzunisha zaidi ni hatima ya Waafrika wa Afrika ya Kusini. Wareno wakiwa na tangazo la Papa "Walazimisheni makafiri kuwa watumwa" wanang'ang'ania kuiweka Angola na Msumbiji chini ya nira ya Utumwa wa kitaifa. Ni jambo la kushangaza kweli kuona Papa Paulo wa VI mara nyingi hutoa matamshi kuhusu matatizo ya kisiasa ya dunia; akini kamwe hata siku moja hajaona umuhimu wa kuishauri Ureno kuzungumza na "raia" wake hapa Afrika na 148. Williams, op. cit., uk. 8. kwingineko.

Badala yake Mapapa wamekuwa wakien-deleza uhusiano maalum na Ureno na Hispania, nchi hizi mbili za Kanisa Katoliki ambazo zinakataa kuyaacha huru makoloni yake ya Afrika. Katika mwezi wa July, 1970, Papa Paulo VI aliwapokea viongozi fulani wa wapigania uhuru wa makoloni ya Ureno katika Afrika. Mkutano huu uli-ikasirisha sana Ureno, ambayo ilitoa tamko la pingamizi; Vatican katika hali ya wasi wasi ilitoa maelezo. Akieleza kuhusu jambo hili, barua ifuatayo yenye kichwa cha habari "Muhtasari wa Papa ni Faraja: ilichapishwa katika gazeti la "Standard Dar es Salaam (Tanzania) na muunini mweusi wa Roman Katoliki, aliposema: "Kipengee cha habari; 'Muhtasari wa Papa waifariji Ureno' (Standard, July 11) yahusika. Ninanukuu sentenso muhimu: Muhtasari wa Vatican ulisema kwamba Papa alipowapokea (yaani viongozi wa vyama vya ukombozi katika Afrika walioko chini ya utawala wa Kireno) wakiwa kama Wakatoliki na Wakristo, bila ya kuangalia shughuli zao za kisiasa. Aliwakumbusha kuhusu mafundisho ya Kanisa kwamba njia za amani siku zote zitumike hata katika kutafuta kile mtu akionacho kuwa ni haki yake mtu.

"Habari za mapema zaidi kwamba Baba Mtakatifu ame-pokea viongozi hao waliosemwa, zimenisumbua na kunitia wasi wasi sana. Sasa ufafanuzi huu umefanya wasi wasi wangu kutulia. Ngoja nieleze kwa nini. Lilikuwa Kanisa la Roman Katoliki ambalo ndilo lililoleta ukoloni wa Kimagharibi kwa kuigawa ardhi yote na nchi zote mpya zili-zogunduliwa hivi karibuni katika mafungu mawili; kuwapa Wahispania nusu ya Magharibi (kama nchi za Amerika) na kuwapa Wareno nusu ya Mashariki (kama nchi ya Afrika na India). Makoloni ya Ureno katika Afrika yameundwa imara sana juu ya lile Agizo la Papa. Niliposoma mapema kwam- ba Papa Paulo VI aliwapokea viongozi wa vyama vya Ukombozi, nilishangaa iliwezekana vipi. Kwa mujibu wa imani yetu ya kutokukosea kwa Papa, Paulo VI analazimi-ka kuchukua na kuhalalisha kila kitu kilichoamriwa na kua-gizwa na wale watakatifu waliokwisha mtangulia. Kwa hiyo, kwa mujibu wa kufikiria kwangu asingewatia moyo viongozi hao.

"Sasa ufafanuzi wake umenifariji mimi sana kiroho. Sasa naweza kulala kwa amani na kuwa ujuzi wa uhakika kwamba Kanisa halikujilaumu lenyewe kwa kuonyesha kwamba Mapapa walikosea katika kuuweka na kuunga mkono "mwanga" wa bara hili jeusi chini ya Ubepari wa Kireno. "Pia ushauri wake kwa hawa waitwao 'Waathirika kutokana na Ukoloni' kubakia katika amani (yaani kuvinyang'anya silaha vikundi vya wapigania uhuru) ni sawa na mvinyo wa zamani ndani ya chupa mpya. Inanikumbusha maombi ya mapadre wa Kanisa la Romani Katoliki wakati wa kuen-deshwa meli zenye watumwa kutoka bandari za Ureno kwenda katika visiwa vya West Indes. Waliomba kwa Mola Mwenye Uwezo na nguvu zote kuhakikisha usalama wa meli hizo na siku zote waliwaamuru watumwa weusi wawe na tabia za kiungwana na utii. Kwa hakika, hawakufikiria kwamba ni lazima kuwashauri mabwana (wamiliki) wa watumwa kuwafikiria nao kuwa ni wanaadamu. Nina furaha kwamba Kanisa langu halijabadilika katika kipindi chote hiki cha karne ndefu." Sera ya Afrika ya Kusuni ya Ubaguzi wa rangi inalaumiwa ulimwenguni pote na Baraza la Umoja wa Mataifa (UN) na kila mahali. Lakini Makanisa siku zote yalifuata mstari huo huo. Ilikuwa baada tu ya "mabadiliko ya Upepo" katika Afrika na kutokea kwa haraka uhuru wa nchi za Kiafrika kwamba makanisa yalitambua haja ya kuupinga mfumo ulio mbaya kabisa ambao hukatilia wenyeji wa asili (wazawa) wa nchi husika haki ya kufanya kazi, kutembea, kukaa, kupanda vipando vya kusafiria, kuchuma au kulala katika ardhi yao wenyewe. Na hata pia wakati Makanisa mengine yote, yalipolazimishwa na haja muhimu za Kisiasa, walionyesha upinzani wao kwa aina hii ya utumwa, Kanisa la Kidini la Mageuzi- 'The Dutch Reforned Church' bado linaunga mkono mfumo huu wa kinyama.

Rhodesia inafuata nyayo za Afrika ya Kusini. Msemo ulio-zoeleka na maarufu wa kuchekesha wa Kiafrika katika sehe-mu hizi za dunia unaelezea kuhusu Mwafrika mmoja aki-umwambia (rafiki yake) Mzungu: "Ulipokuja ulikuwa na Biblia na sisi tulikuwa na ardhi. Sasa hivi sisi tunayo Biblia na wewe una ardhi, (unaimiliki). Mbali na utumikishaji huu wa kijeuri na dhahiri, bado upo udanganyifu mwingine ambao biashara ya utumwa wa Kitaifa hudhihirisha uso wake. Ukiwa kama kinyonga, hubadilisha rangi yake kwa kutegemea mazingira. Ukoloni wa dhahiri sasa umebadilika na kuwa ukoloni mamboleo; lakini inafikia pale pale kwenye utumikishaji na watu na yale mataifa makubwa yenye nguvu kwa kutumia mbinu zenye utata zaidi au zisizokuwa na utata sana. Tumekwisha ona nini kilitokea kuhusu league of Nations (Shirikisho la Mataifa). Imeondolewa na badala yake ni UNO, lakini wakati mataifa dhaifu yanapolia na kuomba kuwepo na haki, usawa na uadilifu, shinikizo la kidiplomasia hutumika na madai yao ya haki kuhusu haki zao za msingi huondole-wa na kuwekwa kando au huahirishwa. Kuna usaliti wa kisiasa, na rangi ya ngozi bado ndio kiumacho. Kwa kweli nchi zitawalazo au zile ambazo zina nguvu na zimejizatiti vyema kwa vyombo na uwezo wa kuleta maangamizi makubwa na uharibifu, bado zinashikilia utawala wao.

Aina hii ya utumwa inafanywa leo hii siyo tu na mataifa bepari ya Kikristo bali na Wakomonist pia, na itaendelea hivi kwa kipindi kirefu maadam jamii ya kibinadamu inabakia katika kugawanyika katika makundi ya walio na mguvu na walio dhaifu au mpaka kuwepo na kutambuliwa kwa Mwenye Kudra na Mwenye Nguvu zote, Mwenyezi Mungu (atambuliwe), na Himaya (Enzi) yake katika Ulimwengu wote iwe imeaminiwa kabisa na kupokewa. Hata sasa wakati Karne ya ishirini inaelekea kufika mwisho wake na Waamerika wakiwa wanajifaharisha wenyewe katika yale waliyoyapata, suala la "Watu Weusi-Manegro" liko mbele kabisa na bado halijapatiwa ufumbuzi. Kwa kukata tama, O.A Sherrad anasema: Utumwa umekuwepo kutoka mwanzo na utamalizika katika mfumo mmoja au mwingine, kwa kadiri ambavyo mwanadamu ana tamaa ya madaraka. Matokeo yake yamekuwa katika taabu zaidi, mauaji zaidi, kushuka heshima zaidi, huzuni zaidi, mateso zaidi na dham-bi kuliko asasi yoyote nyingine ya mwanadamu. Inaangamiza mtu mmoja mmoja na jamii nzima ya mwanadamu. Hutia chachu katika maingiliano ya mwanadamu, kwani alama aonekanayo mtu ni hofu... imeshughulika na wakati uliopita katika hali ya kiovu na iliyojaa makosa, na pengine ni yenye uovu zaidi na makosa zaidi katika wakati wa sasa. Utumwa kama si wa dhahiri sana lakini ni wenye kutapakaa zaidi na hofu yake ni yenye kuenea kote. Hofu ya kinyonge, dhalili na ya kitumwa iji-tokezayo miongoni mwa vibaraka vyake inaitembelea na kuyaandama Makao ya Utawala wa Urusi; hofu ya maangamizi ya mtumwa mnyonge huzidisha uhasama kati ya Mashariki na Magharibi; hofu ya lipizo la mnyonge hujizalisha katika Afrika ya Kusini na kuyafunika majimbo; hofu ya mafedhuli kutia kasumba mateso, vifo vya ghafula, hunyonyesha makundi makubwa ya watu ulimwenguni pote. 149. Lakini hatushirikiani katika mtazamo huu ulio mbaya kabisa. Tunatambua kwamba tatizo lenyewe ni kubwa kabisa, lakini tunajua pia kwamba Uislam ni Dini iliyoletwa na Allah, Aliye Muweza juu ya kila kitu. Uislam, miaka 1400 ulileta mpango wa sura tatu (three sided programme) kwa ajili ya kuondoa utumwa.

Kuzuia njia za kupatia watumwa wapya, kukomboa watumwa, na kuirudisha na kuiweka heshima ya kibi-nadamu kwa watumwa. Na ukweli ni kwamba ingawa Banu Ummayya waliuhujumu upande mmoja wa mpango huo kwa kuingiza utumwa kwa njia ya kuwanunua, hawakuweza kupunguza athari ya pande hizo nyingine mbili zilizobaki. Na watumwa katika ulimwengu wa Kiislamu walipata tena heshima yao ya kibinadamu iliyopotea. Mfumo ambao umeonyesha manufaa yake, na ambao umepata mafanikio katika nyanja, ambako mifumo mingine imeshindwa kabisa, kwa hakika utapata ukomeshaji wa jumla wa kila aina ya mgawanyiko, mtengano, tofauti na dhuluma kama utapewa nafasi. Ameer Ali anaandika: "inabakia kwa Waislamu (sic. - japo kwa makosa) kuonye-sha uwongo wa kashifa juu kumbukumbu za Mtume mkub-wa na Mtukufu (zinazofanywa na wazushi na maadui wa 149. Sherrard, op. cit., uk. 188-189.

Uislam) kwa kutamka kwa maneno ya wazi kwamba Utumwa (utumwa katika sura ya aina yoyote ile na tofauti za mataifa na rangi) unachukiwa na dini yao, na umekatazwa na sheria yao. Na tuna uhakika kwamba Uislam utape-wa fursa na Allah ili kuleta haki yote na kamili katika ulimwengu. Maimamu wa Kishia, Viongozi waliochaguliwa na Mwenyezi Mungu, waliiendeleza kazi ya Mtukufu Mtume na waliingiza katika wafuasi wao ile roho ya kweli ya Uislam. Wao kwa mifano yao na kwa kupitia kwenye dua, wameuhifadhi Uislam asilia (wenyewe) kwa ajili ya wafuasi wao. Na Imamu wa mwisho wa Mwenyezi Mungu, Imamu Muhammad al-Mahd (amani iwe juu yake) Anayengojewa, atadhihiri tena wakati ulimwengu huu utakapokuwa umejaa dhuluma, ukatili na kutokuaminika. Wakati yeye Anayengojewa atakapotokea kutoka katika Ghaibati (Alikofichwa na Allah) ataujaza ulimwengu na Haki, Uadilifu, Uaminifu na Rehema. Tumeamini katika ulimwengu ulio bora zaidi (wa kesho -Akhera) na tunajua kwamba katika hali yoyote ile utumwa utavyojitokeza katika kuji-ficha kwake katika wakati wa kudhihiri tena kwa Imamu wa Kumi na mbili, yeye anayengojewa, (utumwa huo) utalaz-imika kutoweka na kuicha nafasi yake kwenye undugu na heshima ya kibinadamu kwa watu wote. 150. Ameer Ali, Spirit of Islam, uk. 267

MAELEZO YA NYONGEZA (POST SCRIPT)

Mheshimiwa Mwandishi (wa kitabu hiki) aliandika nyongeza ya maelezo katika mwaka wa 1987 wakati Afrika ya Kusini ilikuwa bado ni Taifa la kibaguzi (ubaguzi wa rangi) na shirikisho la Urusi (Sovieti Union) ilikuwa bado ni taifa lenye nguvu sana. Licha ya mabadiliko haya muhimu katika uwanja wa kisiasa ulimwenguni, maelezo ya mwandishi kuhusu utumwa wa kitaifa (taifa moja kutumikishwa na lingine ) bado ni halali wakati huu wa mwanzo wa karne mpya. Ukoloni mambo leo bado upo katika mifumo mbalimbali tofauti na sasa Baraza la Umoja wa Mataifa (UNO) linatu-miwa kama mhuri wa kibali cha kuendelezwa zaidi shabaha na malengo ya mataifa yenye nguvu sana yaliyobaki katika ulimwengu huu. Nchi ya Marekani (USA) na washirika wake wa Ulaya walitumia "Kadi ya demokrasia," demokrasi ya kuteuliwa katika Ulimwengu wa Tatu inavumilika tu kama itahakikisha faida na maslahi ya nchi za Magaribi, kama ilivyoonekana katika suala la Algeria na Uturuki. Baraza la Usalama, Baraza pekee lishughulikalo na maa-muzi ya Baraza la Umoja wa Mataifa (UNO), linaendesha shughuli zake katika misimamo isiyokuwa ya kidemokrasia. Inatumika kwa kuchaguliwa tu au kuteuliwa katika kuhalal-isha maslahi ya matajiri na wenye nguvu juu ya mataifa yaliyo dhaifu ya ulimwengu. Nchi ambayo iko ndani ya 'vitabu vibaya' vya nchi za Magharibi kamwe nchi hiyo hai-wezi kupatiwa uamuzi ulio sawa na haki wakati nchi ya Iraq ilipoivamia Iran, hakukuwepo na dhoruba kali la jangwani, lakini wakati nchi hiyo hiyo, yaani Iraq ilipoivamia Kuwait na kuitishia Saudia (Saudi Arabia) na washirika wengine katika eneo hilo. "majeshi ya ushirika huo" yaliungana kwa kibali cha ridhaa ya Umoja wa Mataifa (UNO). Jinai hiyo katika hali zote lilikuwa sawasawa na kutendwa na mhalifu yule yule, lakini bado hali iliyooneshwa kwa mhalifu ilikuwa tofauti kwa sababu tu muathirika wa pili (yaani Kuwait) alikuwa mshirika wa upande wa nchi za Magharibi wakati ambapo huyo muathirika a kwanza (Iran) hakuwemo ndani ya vitabu vizuri vya nchi ya Marekani (USA).

The New World Order (mpango wa Marikani) kwa hakika ni zama ya unafiki: Mataifa yenye nguvu za kijeshi bado yanaendelea kulundika na kutengeneza zaidi silaha za kisasa zenye maangamizi makubwa na wakati huo huo wanaende-lea kuhubiri kwa mataifa dhaifu kuhusu kujizuia wasiten-geneze silaha kama hizo! Wakiwa mbele kwa masuala ya mazingira; wachafuzi wakubwa kabisa wa mazingira ni mataifa yenye viwanda vingi: lakini bado ni nchi ya Marekani (USA) ambayo ndiyo inakataa kutia sahihi mkata-ba wa kuzuia momonyoko wa ukanda wa hewa safi katika anga-hewa. Kanuni ya uadilifu ya haki kwa wote siyo kawaida katika mpango huu wa Marikani (New World Order). Maslahi binafsi ya matajiri na nchi zenye nguvu, katika istilahi yake zaidi ya kistaarabu ya "maslahi ya kitaifa" bado ndio ufun-guo unaofanya kazi katika mchezo huu. Pengo lililopo kati ya nchi za Kaskazini na Kusini linakuwa kwa haraka sana. Serikali za nchi masikini haziko huru kutekeleza sera zao wenyewe; ni Benki ya Ulimwengu, chombo kingine cha Ukoloni mambo leo, ambayo ndiyo inayowaundia sera za kiuchumi watu wan chi hizo. Sera hizi haziboreshi wengi wa watu katika nchi za Afrika na Asia.

Kwa masikitiko sana, hata katika suala la utambuzi wa mis-iba ya watu inaonyesha kunakuwepo na ubaguzi; msiba wa kundi moja la watu ambao waliteseka katika mikono ya Wanazi unafahamika kwa mapana sana (na Pia wakaza-wadiwa kuwa na "Nchi ya kuishi" ambayo baadaye inageu-ka kuwa "taifa") wakati ambapo utambuzi wa msiba wa mamilioni ya Waafrika ambao walichukuliwa na kupelekwa katika nchi za Amerika na kunyang'anywa jina lao, utambulisho, dini, lugha na haki za msingi za kibinadamu bado ni jambo lilioko katika kujadiliwa. Na tukiwa pamoja na mwandishi, tunamwomba Muumba Mwenye Nguvu Zote aharakishe kudhihiri kwa Mahdi, aliye Masihi, ambaye atauondolea ulimwengu na uonevu na kuieneza haki na amani katika ulimwengu. Amin. "Enyi watu! Hakika Adamu hakuzaa mtumwa mwanaume au mtumwa mwanamke, wanadamu wote wako huru."

Imamu Ali(a.s) Maoni ya watu kuhusu utumwa ni kwamba umetupwa kwenye mapipa ya takataka ya historia, wakati bado athari za ushenzi huu wa kuchukiza ambao mwanzo wake ulikuwa dhidi ya Waafrika, unajitokeza wenyewe kwa sura mpya na mbaya zaidi kwenye karne ya 21. Tangu kupigwa marufuku kwake rasmi katika mwaka wa 1863, utumwa umechukuwa sura ya uovu na ya kuchukiza zaidi, katika muundo wa utumwa uliopakazwa mafuta kwa mgongo wa chupa. Utandawazi kupitia umiliki wa nguvu za kuzalisha unao-fanywa na "Muungano wa Kimataifa wa Wakiritimba" (Multi National Cartels) ni muundo mpya wa utumwa. Allamah Rizvi anaelezea suala hili la biashara ya utumwa kwa muktadha wake halisi. Allamah Sayyid Saeed Akhtar amekiandika kitabu hiki kwa uwezo mkubwa na jitihada. Kama ilivyo kwa msomi mtafiti kama yeye, ameshuhgulikia mada ya kitabu hiki bila upendeleo, Ameupanga ukweli baada ya ukweli kutoka kwenye historia; amenukuu kutoka kwenye Qur'an, Hadithi na waandishi wa zama za leo kuhusu somo hili, na ameonyesha sheria za Kiislamu na zile zilizotumika kabla ya Uislam. Ameonyesha waziwazi kwamba ustaarabu wa Kimagharibi sio bingwa mkubwa kiasi hicho wa kuwaokoa watumwa kama unavyojionyesha na kujigamba. Kwa kweli kitabu hiki kitathibitisha kuwa kifungua macho kwa wale ambao hukubali bila kuchunguza kuhusu propaganda ya ubinadamu wa Kimagharibi.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU