WAULIZE WANAOFAHAMU

WAULIZE WANAOFAHAMU0%

WAULIZE WANAOFAHAMU Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Misingi mikuu ya Dini

WAULIZE WANAOFAHAMU

Mwandishi: Muhammad Tijani As-samawi At-Tunisi
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 49405
Pakua: 4127

Maelezo zaidi:

WAULIZE WANAOFAHAMU
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 26 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 49405 / Pakua: 4127
Kiwango Kiwango Kiwango
WAULIZE WANAOFAHAMU

WAULIZE WANAOFAHAMU

Mwandishi:
Swahili

11

WAULIZE WANAOFAHAMU

KAULI YA AHLUL-DHIKRI KUHUSU BAADHI YAMASAHABA

Imam Ali(a.s) amesema akiwazungumzia Masahaba hawa wanaohesabiwa kuwa ni miongoni mwa (watu) wa mbele:

"Niliposimamia Ukhalifa, kuna kundi lililotengua (kiapo chake) na kundi jingine lilitoka, na wengine wakafanya ujeuri, kama kwamba wao hawakuyasikia maneno ya Mwenyezi Mungu aliposema, Hayo ni makazi ya akhera tunawapa wale wasiotaka ukubwa katika nchi wala uovu, na marejeo (mema) ni kwa ajili ya wamchao Mwenyezi Mungu. Bila shaka Wallahi Wallahi, waliyasikia maneno hayo na wakayafahamu, lakini dunia imewapendeza machoni mwao na mapambo yake yamewafurahisha .[19] ".

Na amesema tena Imam Ali(a.s) kuwahusu hao Masahaba: "Wamemfanya shetani kuwa ndiyo msimamizi wa mambo yao, naye amewafanya wao kuwa ni washirika (wake) basi ametaga (mayai) na kuyaangua ndani ya nyoyo zao na anatambaa ndani ya akili zao, basi (shetani) anaona kwa kutumia macho yao na anazungumza kwa kupitia ndimi zao, akawapoteza na kuwapambia maovu yakawa ndiyo matendo ya yeyote aliyeshirikishwa na shetani ndani ya utawala wake na akazungumza batili kwa ulimi wake ."[20]

Na amesema tena Imam(a.s) juu ya Sahaba mashuhuri Amri ibn Al-'as:

"Anashangaza mwana wa Nnabighah, hakika amesema (mambo) batili na ametamka uovu, ama (na ifahamike kwamba) kauli mabaya ni kusema uongo, hakika yeye akizungumza husema uongo, na akiahidi huenda kinyume na ahadi, na akiomba (kitu) hulazimisha (apewe) na anapoombwa ni bakhili, ana hiyana kwenye ahadi na anakata udugu. "[21]

Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema(s.a.w.w) :

"Alama za mnafiki ni tatu: Akizungumza husema uongo, na akiahidi huenda kinyume na ahadi na akiaminiwa hufanya khiyana ."

Ewe msomaji fahamu kwamba: machafu yote haya na zaidi kuliko haya yanapatikana kwa Amru ibn Al-'as.

Na amesema Imam Ali(a.s) akimsifu Abu Dharri Al-Ghifari na wakati huo huo akamshutumu Uthman ibn Affan pamoja na washirika wake ambao walimfukuza Abudharri na kumpeleka mahala paitwapo Ar-rabdhah kisha kutomruhusu kurudi Madina mpaka akafa huko akiwa peke yake.

"Ewe Abudharri, hakika wewe umechukizwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi mtarajie huyo ambaye kwa ajili yake umechukizwa, bila shaka jamaa hawa walikuogopa juu ya dunia yao, nawe uliwachelea kwa ajili ya dini yako, kwa hiyo viache mikonini mwao vitu ambavyo kwavyo walikuogopa na uwakimbie ukiwa na kile ambacho wewe uliwachelea wao kwa ajili yake, hakika wanakitaka mno hicho ulichowazuwia, nawe umetosheka mno na hicho waliochokuzuwilia, na hivi karibuni utajua ni nani atakayepata faida kisha (ni nani) mwingi wa husuda, na lau mbingu na ardhi zingekuwa zimeshikana juu ya mja kisha (mja huyu) akamcha Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu angemjalia mja huyo njia katika mbingu na ardhi. Usiwe na kiliwazo kingine isipokuwa haki, na kisikufanye mpweke chochote isipokuwa batili, basi lau ungeikubali dunia yao wangekupenda na lau ungekata sehemu (katika dunia) wangekupa amani ."[22]

Amesema Imam Ali(a.s) kuhusu Mughirah ibn Al-akhnas ambaye naye ni miongoni mwa Masahaba wakubwa:

"Ewe mwana wa aliyelaaniwa aliyekatikiwa, na (ewe mwana wa) mti ambao hauna mizizi wala matawi, Wallahi Mwenyezi Mungu hajamtukuza yule ambaye wewe unamtetea, na wala hatosimama yule ambaye wewe unamnyanyua, hebu tuondokee, Mwenyezi Mungu ayaangamize makazi yako, kisha azidishe mashaka yako, kamwe Mwenyezi Mungu asikubakishie muda wa kubakia kwako ."[23] Na amesema Imam(a.s) kuwahusu Tal-ha na Zubair, ambao ni Masahaba mashuhuri waliompiga vita Imam Ali baada ya kuwa wamempa baia na hatimaye wakatengua baia yao:

"Wallahi hawakunikuta na aibu ya aina yoyote ile, na wala hawakufanya uadilifu kati yangu na wao, na kwa hakika wao wanaitetea damu ambayo wao ndiyo walioimwaga...Hapana shaka hilo ndilo kundi lililoasi, ndani yake yumo jamaa (wa karibu yangu (yaani Zubair) na yumo nyoka, madai yao si kweli bali kuna jambo walitakalo, hapana shaka mambo yako wazi na hakika uovu umeondoka toka mahala pake na ulimi wake umekatika kutoka mahala pake pa uchochezi Ni nyie mlionijia mbio mbio kama mwanamke mwenye watoto anavyowakimbilia wanawe na huku mnasema, "Baia Baia" lakini mimi nikakikunja kiganja changu ninyi mkakinyoosha, nikautoa mkono wangu nanyi mkauvuta, Ewe Mwenyezi Mungu hakika wawili hawa wameniasi na wamenidhulumu, wametengua kiapo chao kwangu, wamewavuruga watu dhidi yangu, nakuomba uyafungue waliyoyafunga na wala usiwakubalie waliyoyaamua na uwaoneshe ubaya wa waliyoyategemea na kuyafanya. Niliwataka wajirekebishe kabla ya mapambano, na hapo vitani niliwataka wawe mbali wakanipinga na kuukataa msamaha wangu.

Na amesema Imam Ali(a.s) ndani ya barua aliyowaandikia Zubair na Tal-ha: "Enyi Masheikh wawili badilisheni maoni yenu (mujisahihishe) kwani sasa hivi jambo kubwa litakalowafika ni aibu kabla ya fedheha na moto havijakutana... Was-salaam. "[24]

Na amesema kuhusu Marwan ibn Al-hakam wakati alipomteka katika vita ya Jamal kisha akamwachia huru, na huyu Marwan ni miongoni mwa watu waliombai Imam Ali kisha akatengua baia yake: Anasema Imam Ali: "Sina haja na baia yake, hakika kiganja chake ni kiganja cha Kiyahudi, lau atanibai kwa kiganja chake hatimaye atatengua kimya kimya, ama huyu (Marwan) atamiliki uongozi kama mbwa arambavyo pua yake (muda mchache) naye ni baba wa watawala wanne, na kutokana naye na wanawe hao umma (wa Kiislamu) utakumbana na siku nyekundu. matatizo na umwagaji damu. "

Na amesema Imam(a.s) kuhusu Masahaba ambao walitoka pamoja na bibi Aisha kwenda Basrah katika vita ya Jamal na katika hao walikuwemo Talha na Zubair: "Wakatoka hali ya kuwa wanaikokota heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kama akokotwavyo mjakazi anaponunuliwa wakaielekeza Basra, wao wakawazuwia wake zao majumbani mwao, na wakamtoa nyumbani kwa ajili yao na wasiokuwa wao mtu ambaye Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alimzuwia asitoke, wakiwa ndani ya jeshi ambalo hapana mwanaume yeyote aliyekuwa ndani ya jeshi hilo isipokuwa (hapo kabla) alikuwa amenitii na kunipa kiapo cha utii kwa hiyari yake mwenyewe bila kulazimishwa. Wakamshambulia muwakilishi wangu na muweka hazina wa nyumba ya mali ya Waislamu hapo Basra na wengineo miongoni mwa wakazi wa mji huo, wakauwa watu kadhaa hali yakuwa wamefungwa. na wengine wakawauwa baada ya kuwahadaa. Basi Wallahi lau wasingemuuwa miongoni mwa Waislamu isipokuwa mtu mmoja ambaye kumuuwa kwake iwe kuwa ametenda kosa lolote, hakika ingenihalalikia mimi kulipiga jeshi hilo lote, kwani walipomfikia hawakupinga (kuuawa kwake) wala hawakumtetea kwa ulimi wala kwa mkono, achilia mbali ile hali ambayo wao wamewauwa Waislamu kwa kiasi cha idadi ambayo waliyoingia nayo dhidi yao .[25]

Na amesema Imam(a.s) kuhusu bibi Aisha na wafuasi wake miongoni mwa Masahaba katika vita ya Jamal: "Ninyi mmekuwa askari wa mwanamke na wafuasi wa mnyama, akipiga kelele ninyi mnaitikia na akijeruhiwa mnakimbia, tabia yenu ni mbaya, ahadi yenu ni yenye kuvunjika na dini yenu ni unafiki ."[26]

"Ama fulani umemtangulia mtazamo wa wanawake wenziwe, anayo chuki inayotokota kifuani mwake mfano wa chungu kinachotokota, lau angeitwa ili atende kwa mwingine kama haya yaliyomleta kwangu asingefanya, na kwangu mimi anayo heshima yake ile ile ya mwanzo (kwa kuwa ni mke wa Mtume) na malipo (yake) yapo kwa Mwenyezi Mungu ." (Nahjul-Balagha uk. 334).

Pia Imam Ali(a.s) alisema kuhusu Maquraishi wote, na hapana shaka alikuwa akiwakususudia Masahaba.

"Ama sisi kuwekwa kando kuhusiana na cheo hiki (cha Ukhalifa) wakati sisi ndio watukufu kwa nasaba na watu wa karibu mno na Mtume kimafungamano, yote hayo ni kwa sababu ya choyo na chuki katika nafsi za watu lakini hukumu ya yote hayo iko kwa Mwenyezi Mungu na marejeo ni kwake siku ya Kiyama Kwa hakika mambo ya dunia hii yananichekesha na kuniliza, hasa kuhusu huyu mwana wa Abu Sufiyan, hapana shaka ametenda mambo yanayoshangaza na kuzidisha mashaka. Jamaa hawa walitaka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kutoka kwenye taa yake na kuziba mbubujiko toka kwenye asili yake, na wakanichanganyia kinywaji kibaya, iwapo yataondoka matatizo kwetu na kwao nitawapasha ukweli halisi, vinginevyo basi usiwajutie kwani hakuna shaka Mwenyezi Mungu anayajua wayatendayo ."[27] Na alisema katika maana kama hii maneno yafuatayo alipokuwa akimzika bibi Fatma hali yakuwa akimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu. "Binti yako atakueleza namna Umma wako walivyosaidiana kuubomoa (Ukhalifa), basi muulize akueleze jinsi ya hali (ilivyokuwa) hali hii (imetokea) hata haujapita muda mrefu (toka kufariki kwako) na wala utajo wako haujatoweka.. ."[28]

Na amesema Imam Ali(a.s) ndani ya barua aliyomuandikia Muawiya:

"Wewe bila shaka neema zimekupa kiburi na shetani amechukua sehemu ya kwako wewe na amefikia malengo yake kupitia kwako, anazunguka (mwilini mwako) mzunguko wa roho na damu, tangu lini enyi kina Muawiyah, mmekuwa viongozi wa raia na watawala wa mambo ya Umma pasina kuwa kuna unyayo uliotangulia wala heshima tukufu? Tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na kushikilia mwenendo wa waovu waliotangulia, nakuonya kuwa wewe ni mwenye kuendelea kudanganyika kwa matamanio umekuwa tofauti kati ya nje yako na ndani yako, kwa hakika wewe Muawiyah umeitaka vita, basi hebu waache watu pembeni unitokee mimi, na yaache makundi haya mawili (langu na lako) yasipigane (utoke wewe na mimi) ili apate kutambulikana ni yupi kati yetu aliyemzoefu moyoni mwake na ambaye macho yake yamefumbwa. Basi (fahamu ya kwamba), mimi ndiye baba Hasan, ndiye niliyemuua babu yako, mjomba wako na nduguyo, nikawavunja vunja siku ile ya Badri, na ule upanga (niliowavunjia bado) ninao, na moyo ule ule (wa siku ile) nilipopambana na adui yangu (bado ni ule ule) kamwe sijabadili dini wala sijazusha Mtume mwingine (zaidi ya Muhammad) na ni bila shaka nipo kwenye dini ambayo mliikataa kwa hiyari yenu na mkaingia bila kupenda... "[29] Imam(a.s) anaendelea kusema:

"Ama kauli yako (kusema) kwamba, sisi ni kizazi cha Abdu Manafi ni kweli, sisi ndio wao, lakini Umayyah halinganishwi na Hashim, na wala Harbu (babu yake Muawiyah) yeye si kama Abdul-Mutalib, na wala Abu-Sufiyan si (sawa kwa ubora) kama Abu Talib, wala Muhajir (aliyetoka Maka mwanzoni anajikusudia yeye mwenyewe Imam a.s) si kama muachwa huru (anamkusudia Muawiyah) wala mwenye nasaba takatifu si kama mwenye nasaba ya kubandikizwa, wala atendaye haki si sawa na mpotoshaji, wala Muumini si sawa na muovu, kwa kweli badali mbaya ni ya yule anayefuata waliomtangulia ambao wameporomokea ndani ya moto wa Jahannam.

Mikononi mwetu (tumeshika) utukufu wa Utume ambao kwao tumemuinamisha mwenye nguvu na tukamnyanyua mnyonge, na pale Mwenyezi Mungu alipowaingiza Waarabu ndani ya dini yake kwa wingi, basi Umma huu ulijisalimisha kwa hiyari yake na wengine kwa kulazimika, hivyo ninyi mlikuwa miongoni mwa walioingia katika dini ima kwa matumaini fulani au kwa kuogopa, na (kwa kweli) wamefaulu wale waliotangulia kwa sababu ya kutangulia kwao na Muhajirina wa mwanzo wamejichukulia ubora wao."[30]

"Kwa hakika umetuita kwenye usuluhishi wa Qur'ani na wewe si miongoni mwa watu wa Qur'ani, (fahamu kwamba) sisi hatukukuitikia wewe (matakwa yako) lakini tumeiitika Qur'ani katika hukumu yake Wassalaam.... "[31]

"Waambie, ukweli umekwisha fika na bila shaka uongo ni wenye kuondoka ." (Qur'ani, 17:81).

12

WAULIZE WANAOFAHAMU

MLANGO WA TANO

UNAWAHUSU MAKHALIFA WATATU ABUBAKR, UMAR, NA UTHMAN

Bila shaka Masunni kama tulivyotangulia kueleza, hawakubali kabisa kumkosoa Sahaba yeyote kati ya Masahaba wa Mtume(s.a.w.w) na wanaamini kwamba, Masahaba wote ni waadilifu. Na iwapo kuna mwanataaluma yeyote aliye huru ataandika juu ya kukosoa matendo ya baadhi ya Masahaba, basi Masunni humshutumu, si hivyo tu, bali humkufurisha japo mwanataaluma huyo atakuwa ni miongoni mwa wanachuoni wao. Hali hii ndiyo iliyowapata baadhi ya wanachuoni huru wa Kimisri na wasio Wamisri, na mfano wa wanachuoni hao ni Sheikh Mahmud Abur-rayyah mwandishi wa kitabu kiitwacho Adh-wau Alas-sunnatil-Muhammadiyyah na kitabu kingine kiitwacho, Shaykhul-Mudhirah, na mwingine ni Qadhi Shaykh Muhammad Amin Al-antaki mwandishi wa kitabu kiitwacho, Limadha Ikhtartu Madh-haba Ahlil-Bait na mwingine ni Sayyid Muhammad ibn Aqil, ambaye alitunga kitabu kiitwacho, An-nasaihul-hafiyah liman yatawallaa Muawiyah. Bali zaidi ya hapo, baadhi ya waandishi wa Kimisri walifikia kiasi cha kumkufurisha Sheikh Mahmud Shal-tut, ambaye alikuwa ni Sheikh wa Chuo cha Azhar, pale tu alipotoa fat-wa kuruhusu kufanya ibada kwa mujibu wa Madhehebu ya Ja'afariyyah.

Sasa ikiwa Sheikh wa Azhar na Mufti wa miji ya Misri anashutumiwa kwa kiasi tu cha kuyakubali kwake Madhehebu ya Kishia ambayo yananasibishwa kwa mwalimu wa Maimamu wa Kisunni ambaye ni Imam Jaafar As-sadiq, basi unafikiri atakuwa na hali gani mtu aliyeyakinai (akaingia) ndani ya Madhehebu haya baada ya kuchunguza na kutosheka na akayakosoa Madhehebu ambayo hapo kabla yeye alikuweko na aliyarithi kutoka kwa baba zake na babu zake? Basi jambo kama hili ndilo ambalo Masunni hawalipi nafasi kabisa, na wanaamini kabisa kuwa (kumkosoa Sahaba) ni kutoka katika dini na ni kutoka katika Uislamu, na hali hii inaleta maana kwa mujibu wa madai yao kwamba, Uislamu umo ndani ya Madhehebu manne tu na mengine yote ni batili. Bila shaka fikra hizo ni fikra zilizoganda, zinafanana na akili ambazo Qur'an inatusimulia, akili za watu ambao walipinga wito wa Mtume tena kwa nguvu, pale Mtume alipowaita wampwekeshe Mwenyezi Mungu na waache kuabudia miungu mingi mbali mbali. Mwenyezi Mungu anasema:

وَعَجِبُوا أَن جَاءَهُم مُّنذِرٌ مِّنْهُمْ وَقَالَ الْكَافِرُونَ هَـٰذَا سَاحِرٌ كَذَّابٌ ﴿٤﴾ أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عُجَابٌ ﴿٥﴾

"Walishangaa alipowafikia muonyaji kutoka miongoni mwao, na makafiri wakasema huyu ni mchawi tena muongo, hivi kweli anawafanya miungu wengi awe Mungu mmoja, bila shaka hili ni jambo la kushangaza." (Qur'ani, 38:4 - 5).

Kutokana na yote hayo, mimi naamini kwamba kuna mashambulizi mabaya ambayo yataelekezwa kwangu kutoka kwa hao wang'ang'anizi (wa fikra za Kisunni) ambao wamejifanya kuwa wao ndiyo wanaowasimamia wenzao, basi ikawa kwamba hana haki yeyote yule kutoka kwenye mambo ambayo yamezoweleka kwao japo mazowea haya kama yatakuwa hayana uhusiano wowote na Uislamu. Sasa kama si hivyo ni vipi mtu anayewakosoa Masahaba katika matendo yao ahukumiwe kuwa ni kafiri na ametoka katika dini, wakati ambapo misingi ya dini na matawi yake havina kabisa uhusiano na suala la kuwakosa Masahaba? Baadhi ya watu wenye chuki za Kimadh-heb walikuwa wanaeneza uvumi katika mawazo yao eti kitabu changu kiitwacho Thummah-Tadaitu kinafanana na kitabu cha Sal-man Rushdie, ili tu wawazuwie watu kukisoma, bali zaidi ya hayo wakiwahimiza kumlaani mwandishi wake.

Bila shaka huo ni uchafuzi na ni uzushi na uongo mkubwa ambao Mwenyezi Mungu atamuadhibu mtu kwa ajili hiyo, kwani itakuwaje akilinganishe kitabu (changu) Thummah-Tadaitu ambacho kinaligania kwenye kauli ya Isma ya Mtume(s.a.w.w) na kumtakasa na kuwafuata Maimamu wa nyumba ya Mtume ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na amewatakasa mno? Iweje yeye akilinganishe na kitabu cha Aya za Shetani ambacho mwandishi wake mwenye kulaaniwa anaushutumu Uislamu na Mtume wa Uislamu(s.a.w.w) ndani ya kitabu hicho, pia anaiona dini ya Kiislamu kuwa ni maneno ya Shetani? Mwenyezi Mungu anasema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاءَ لِلَّـهِ وَلَوْ عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ ﴿١٣٥﴾

"Ehyi mlioamini kuweni wenye kusimamia' uadjlifu, wenye kushuhudia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu japokuwa (ushahidi huo) ni dhidi ya nafsi zenu." (Qur'an, 4:135).

Na kwa ajili ya aya hii tukufu, mimi sijali isipokuwa (nataka) radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu na siogopi lawama ya mwenye kulaumu maadamu ninatetea Uislamu sahihi na ninamtakasa Mtume wake Mtukufu kutokana na kila kosa japokuwa kwa kufanya hivyo italazimu kuwakosoa Masahaba (waitwao kuwa) watukufu na hata kama watakuwa ni wale Makhalifatur-rashiduna kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ndiye bora mno anayestahiki kutakaswa kuliko kiumbe mwingine yeyote. Msomaji yeyote mwenye akili iliyohuru atafahamu kutoka katika vitabu vyangu viwili nilivyoandika kwamba, lengo lililokusudiwa ni nini, kwani siyo suala la kuwakosoa tu Masahaba, bali ni kwa kiwango cha kumtetea Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) na Isma yake na kuondoa mashaka ambayo (watawala wa) Banu Umayyah na Banu Abbas wameyaambatanisha kwenye Uislamu na kwa Mtume wa Uislamu katika kipindi cha karne za mwanzoni ambazo waliwatawala Waislamu katika kipindi hicho kwa nguvu na wakaigeuza dini ya Mwenyezi Mungu vile ambavyo yalivyowatuma malengo yao mabaya, siasa zao butu na matamanio yao machafu.

Njama zao hizi kubwa kwa kweli zimeiathiri sehemu kubwa ya Waislamu ambao waliwafuata kwa nia njema na wakakipokea kila kile kilichosimuliwa (katika hadithi) miongoni mwa riwaya ambazo ni zenye kubadilisha (ukweli) na zingine za uongo zikawa ndizo za kweli na kwamba huo ndiyo Uislamu na ni wajibu kwa Waislamu kufanya ibada zao kwa mujibu wa riwaya hizo bila ya kuzihoji. Na lau Waislamu wangetambua ukweli wa mambo ulivyo wasingewathamini kabisa watawala hao na riwaya zao. Kisha lau historia ingetuletea riwaya zisemazo kwamba Masahaba walikuwa wakitekeleza amri za Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) na kuacha makatazo yake" bila ya kumjadili wala kuyapinga maamuzi yake, na kwamba hawakumuasi zama za mwisho wa maisha yake, basi tungewahukumu kuwa ni waadilifu wote na wala tusingefanya uchunguzi juu ya suala hili (la Masahaba) wala tusingesema chochote.

Ama ukweli ulivyo ni kwamba, miongoni mwao (Masahaba) wamo waongo na wanafiki na miongoni mwao wamo mafasiki kwa mujibu wa Qur'ani na Sunna sahihi iliyothibiti. Pia wamo Masahaba waliohitilafiana mbele ya Mtume(s.a.w.w) na wakamuasi kuhusu amri (yake) ya kuwaandikia maandiko mpaka wakamtuhumu kwamba anaweweseka, na wakamzuwia kuandika (maandiko hayo). Hawakufuata maamrisho yake pale alipompa uamiri wa jeshi Usamah, na walihitilafiana juu ya suala la Ukhalifa baada yake mpaka wakapuuza kumkosha Mtume na kumuandaa na kumzika, na wakagombana kwa sababu ya Ukhalifa, baadhi yao wakaridhia na wengine wakapinga. (Masahaba) walikhitilafiana katika kila kitu baada ya Mtume(s.a.w.w) mpaka wakafikia kukufurishana wao kwa wao na kulaaniana wao kwa wao na kujitenga baadhi yao kuwatenga wengine.

(Na kutokana nao) Dini ya Mwenyezi Mungu ambayo ni moja ikawa na madhehebu mengi na maoni yanayotofautiana, kwa hali hii hapana budi tufanye uchunguzi juu ya kiini (cha yote haya) na migawanyiko ambayo imeuchelewesha umma bora uliotolewa kwa watu na kuuporomosha chini ukawa ni umma dhalili usiojua kitu na unaodharaulika mno duniani. Leo hii unavunjiwa heshima yake na sehemu zake takatifu kukaliwa (kwa mabavu), mataifa yake kufanywa makoloni na wananchi wake kufukuzwa na kutawanywa (huku na huko) kutoka katikati ya nchi zao, na wala umma huu hauwezi kuwazuwia wavamizi hawa wala hata kujitoa aibu usoni pake. Ufumbuzi pekee ninavyoamini mimi kuhusu tatizo hili sugu ni kujikosoa kikweli kweli, tuache kuridhika na kujitapa kwa yale yasemwayo kufanywa na hao waliotutangulia ambao hawakubaliki na wamechakaa, wamekuwa ni makumbusho ambayo yako tupu hayana faida hakuna hata anaye yazuru. Ukweli unatuita tukafanye uchunguzi wa kina juu ya sababu za maradhi yetu, kubakia kwetu nyuma, kufarikiana kwetu na kushindwa kwetu mpaka tuweze kuugundua ugonjwa na kisha tuutafutie dawa itakayotuponyesha kabla ya kutumaliza sisi na kuwapata wenzetu wanaokuja.

Hili ndilo lengo linalokusudiwa, na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye mwenye kuabudiwa naye ndiye mwenye kuwaongoa waja wake kwenye njia iliyonyooka maadamu lengo letu ni sahihi. Basi una maana gani upinzani wa wale wanaopinga na wale wenye kung'ang'ania ambao hawafahamu isipokuwa kutukana na kushutumu eti kwa hoja ya kuwatetea Masahaba? Watu hawa sisi hatuwalaumu wala hatuwachukii, bali tunawahurumia kwa hali yao hiyo, kwani wao masikini kilichowazuwia (kufahamu) ni dhana zao njema kwa Masahaba. Dhana hiyo imewazuwia wasiweze kuufikia ukweli, wamefanana mno na watoto wa Mayahudi na Wakristo ambao wamefanya dhana njema kwa baba zao na babu zao, na hawakuzilazimisha nafsi zao kufanya juhudi ya kuchunguza ukweli wa Uislamu, wamebakia wanaamini tu yasemwayo na viongozi wao waliotangulia kwamba Muhammad ni muongo na wala siyo Nabii. Mwenyezi Mungu anasema:

وَمَا تَفَرَّقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَةُ ﴿٤﴾

"Na hawakufarakana wale waliopewa kitabu ila baada ya kuwafikia ukweli" (Qur'an 98:3).

Baada ya kupita karne nyingi imekuwa ni vigumu leo hii kwa Muislamu kumtosheleza Myahudi au Mkristo juu ya itikadi ya Kiislamu, basi unafikiriaje juu ya mtu atakayewaambia kwamba Taurati na Injili ambazo wanapokezana (ni vitabu) vilivyobadilishwa na kisha akawatolea juu ya hilo ushahidi wa Qur'an, basi je, Muislamu huyu atampata mwenye kumsikiliza kutoka kwao? Hali ni hiyo hiyo kwa Muislamu wa kawaida ambaye anaamini kuwa Masahaba wote ni waadilifu na akaing'ang'ania fikra hiyo bila ya dalili yoyote, basi je itawezekana kwa mtu yeyote kumkinaisha kinyume cha hivyo? Ikiwa watu hawa (Masunni) hawawezi hata kumkosoa Muawiyah na mwanawe Yazid na wengine wengi kama hawa ambao wameuharibu Uislamu kwa matendo yao machafu, basi utakuwa na hali gani iwapo utakapowasemesha kuhusu Abubakar, Umar na Uthman ambao ni As-sidiq na Al-faruq na yule aliyestahiwa na Malaika, au (ukawasemesha) kuhusu Aisha Ummul-Muuminina mke wa Mtume(s.a.w.w) na ni binti ya Abubakar, (Aisha) ambaye tumemzungumzia katika mlango uliopita kwa mujibu wa mapokezi yaliyopokelewa juu yake na waandishi wa sihahi zinazotegemewa kwa Masunni? Na sasa imefika zamu ya kuwazungumzia Makhalifa watatu ili tupate kuonesha baadhi ya matendo yao ambayo yamesajiliwa na Sihahi za Kisunni na Musnad zao na vitabu vya historia vinavyotegemeka kwao, kwanza tubainishe kwamba usemi wa kuwa Masahaba wote ni waadilifu siyo sahihi, na kwamba uadilifu haupatikani hata kwa Masahaba (wanaozingatiwa kuwa ni) wema.

Hatimaye tutawaonesha ndugu zetu Masunni kwamba kukosoa (tunakokusudia) siyo kwa kutukana na kushutumu, bali (makusudio) ni kiasi cha kuweza kuondoa pazia ili kuufikia ukweli kama ambavyo (maelezo hayo ya kukosoa) siyo miongoni mwa uzushi na uongo wa wapinzani (wa dini) kama wanavyodai watu wengi bali yote ni kutoka ndani ya vitabu ambavyo (wao Masunni) wamevihukumu kuwa ndiyo vitabu sahihi na wakashikamana navyo. Abubakr Sidiq katika zama za uhai wa Mtume(s.a.w.w) Bukhari amethibitisha ndani ya sahihi yake juzuu ya sita ukurasa arobaini na sita Kitabu Tafsir Surah Al-Hujurat amesema: "Ametusimulia Nafii ibn Umar, naye amepokea kwa Ibn Abi Mulaikah amesema: Ilikuwa karibu watukufu wawili waangamie, Abubakar na Umar (r.a), walipaza sauti zao mbele ya Mtume(s.a.w.w) pale ulipokuja msafara wa Bani Tamim, mmoja wao alimuashiria Aqraa ibn Habis ndugu wa Bani Mujashi'i, na mwingine akamuashiria mtu mwingine, Nafii akasema, jina lake silikumbuki, basi Abubakar akasema kumwambia Umar hakuna ulichokusudia ila kunipinga, Umar akasema sikukusudia kukupinga, basi sauti zao zikapaa katika majibizano hayo, Mwenyezi Mungu akateremsha aya isemayo, Enyi mlioamini msipaze sauti zenu, Ibn Zubair amesema basi Umar alikuwa hamsikilizishi Mtume(s.a.w.w) baada ya kushuka aya hii mpaka Mtume amuulize na hilo hakulieleza toka kwa baba yake yaani Abubakar."

Kama ambavyo Bukhari ameandika ndani ya sahihi yake juzuu ya nane ukurasa wa 145 Kitabul-I'tisami Bil-kitabu Was-sunnah Babu Mayukrahu minat-ta'amuq Wat-tanazu'u amesema: "Ametueleza Waqi'i kutoka kwa Nafii ibn Umar kutoka kwa Abu Mulaikah amesema: Ilikuwa karibu watukufu wawili waangamie (yaani) Abubakar na Umar pale ujumbe wa Bani Tamim ulipofika kwa Mtume(s.a.w.w) , mmoja wao akamuashiria Aqraa ibn Habis At-tamimi Al-handhali ndugu wa Bani Mujashi'i, na mwingine akamuashiria mwingine, basi Abubakar akasema kumwambia Umar, bila shaka umekusudia kunipinga, Umar akasema, Sikukusudia kukupinga, basi sauti zao zikapaa mbele ya Mtume(s.a.w.w) , ikashuka aya isemayo: Enyi mlioamini musipaze sauti zenu zaidi ya sauti ya Mtume na wala msiseme naye kwa sauti ya nguvu kama mnavyosemezana ninyi kwa ninyi visije kuporomoka vitendo vyenu na hali ninyi hamjui, kwa hakika wale wanaoangusha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao ndiyo Mwenyezi Mungu amezisafisha nyoyo zao kwa kumcha Mungu, basi wanayo maghfira na ujira mkubwa."

Ibn Abi Mulaikah amesema, "Zubair amesema: Basi Umar baada ya hapo na hakumueleza hilo baba yake yaani Abubakar, akawa akizungumza na Mtume(s.a.w.w) humzungumza kama ndugu ampaye siri hakumsikilizisha jambo Mtume mpaka amuulize. Kama ambavyo Bukhari amethibitisha ndani ya sahihi yake juzuu ya tano ukurasa 116 Kitabul-maghazi Wafdu Bani Tamim amesema: "Ametusimulia Hisham ibn Yusuf kwamba Ibn Juraij aliwasimulia kutoka kwa Ibn Abi Mulaikah kwamba, Abdallah ibn Zubair aliwaeleza kuwa ulifika kwa Mtume(s.a.w.w) , ujumbe kutoka kwa Bani Tamim, Abubakar akasema, Mpe Uamiri Al-Qa'aqa'a ibn Ma'abad ibn Zurarah, Umar akasema Hapana, mpe uamiri Aqra'a ibn Habis, Abubakar akasema huna nia nyingine ila kunipinga. Umar akasema; sikukusudia kukupinga, wakajibizana mpaka sauti zao zikapaa juu ikashuka aya kuhusu tukio hilo isemayo: Enyi mlioamini, msitangulize kusema lenu mbele ya (neno la) Mwenyezi Mungu na Mtume wake . Mpaka mwisho wa aya.

Kinachoonekana wazi hapa kupitia riwaya hii ni kwamba Abubakar na Umar hawakufanya heshima mbele ya Mtume(s.a.w.w) kwa mujibu wa adabu za Kiislamu, na walijitanguliza mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake bila idhini, wala Mtume hakuwaomba watoe maoni yao kuhusu kumpa uamiri mtu yeyote miongoni mwa Bani Tamim, kisha wasitosheke na hali hiyo mpaka wakazozana mbele ya Mtume na zikapaa sauti zao mbele yake bila ya heshima wala kujali mambo yanayowalazimu katika (kuonesha) tabia na adabu (njema) ambazo haiwezekani kwa yeyote miongoni kwa Masahaba kukosa kuzifahamu au kujifanya hazifahamu baada ya Mtume kumaliza muda wa uhai wake akiwalea na kuwafundisha. Lau tukio hili lingekuwa limetokea mwanzoni mwa kuja kwa Uislamu tungewatakia samahani Masheikh hawa wawili juu ya tendo lao hilo, na tungejaribu kupata baadhi ya tafsiri. Lakini riwaya hizi zinathibitisha mambo ambayo hayatoi nafasi ya kuwa na mashaka kwamba tukio hili lilitokea mwishoni mwa uhai wa Mtume(s.a.w.w) , kwani ujumbe wa Bani Tamim ulifika kwa Mtume(s.a.w.w) mwaka wa tisa wa Hijra, na baada ya hapo Mtume hakuishi isipokuwa miezi michache, kama ambavyo wanashuhudia pia wanahistoria na wanachuoni wa hadithi ambao wameeleza juu ya kufika kwa ujumbe huo kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Isitoshe hili ni tukio ambalo Qur'ani imelizungumza ndani ya sura za mwisho pale inaposema: "Utakapokuja msaada wa Mwenyezi Mungu na ushindi, utawaona watu wanaingia katika dini ya Mwenyezi Mungu kwa wingi."

Ikiwa mambo yako namna hii, ni vipi wenye kutoa udhuru wanatoa udhuru kuhusu msimamo wa Abubakar na Umar (namna ulivyokuwa) mbele ya Mtume(s.a.w.w) , na lau riwaya ingeishia kueleza msimamo waliouonesha Masahaba hawa wawili, basi tusingepata nafasi ya kukosoa, lakini Mwenyezi Mungu ambaye hastahi chochote katika haki amelisajili tukio hilo na akateremsha Qur'ani kuhusiana nalo itakayokuwa ikisomwa, na ndani yake yamo maonyo na makemeo kwa Abubakar na Umar kwamba, matendo yao yataporomoka iwapo watarudia tendo kama hilo, kiasi kwamba mpokezi wa riwaya ya tukio hili ameanza maneno yake kwa kusema: "Karibu watukufu wawili waangamie, (akimaanisha) Abubakar na Umar."

Mpokezi wa riwaya inayohusu tukio hili ambaye ni Abdallah ibn Zubair anajaribu kutukinaisha kwamba Umar baada ya kushuka aya hii kuhusu tendo lake kwamba yeye Umar anapomzungumza na Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) akawa hamsikilizishi sauti yake mpaka Mtume humuuliza pamoja na kwamba hakumwambia babu yake Abubakar. Lakini historia na matukio ambayo wameyataja wana hadithi yanathibitisha kinyume cha hivyo, na inatosha ukumbuke ile siku ya alhamisi kabla ya kufariki Mtume(s.a.w.w) kwa siku tatu, tunamkuta Umar mwenyewe alitamka ile kauli yake mbaya akasema: "Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu anaweweseka, kinatutosha kitabu cha Mwenyezi Mungu." Kwa sababu yake watu wakahitilafiana, wapo wanaosema sogeeni kwa Mtume akuandikieni, na wengine wanasema kama alivyosema Umar, basi walipozidisha vurugu na kukhitilafiana, Mtume wa Mwenyezi Mungu akawaambia, Ondokeni haifai kufanya makelele mbele yangu." Maana ya wingi wa fujo, makele, kuhitilafiana na kugombana inajulisha kwamba, wao walivuka kila mipaka ambayo Mwenyezi Mungu aliwawekea katika suratul-huj-rati kama ilivyotangulia.

Haiwezekani kututosheleza kwamba, kutofautiana kwao na vurugu zao eti zilikuwa kwa kunong'ona kwenye masikio, bali inafahamika kutokana na yote hayo kwamba wao walipaza sauti zao mpaka hata wanawake ambao walikuwa nyuma ya pazia na hijabu walishiriki katika fujo na wakasema: "Sogeeni kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) akuandikieni maandiko." Umar akawambia: "Ninyi ndiyo kama wale wanawake waliomfanyia vitimbi Yusuf, anapokuwa (Mtume) mgonjwa mnalia na akipona mnamfanyia vitimbi."

Mtume akasema kumwambia Umar, "Waacheni, kwani wao ni bora kuliko ninyi." Na tunachokifahamu katika yote haya ni kwamba, wao hawakufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu katika kauli yake aliposema: "Enyi mlioamini msitangulize (kusema lenu) mbele ya (neno la) Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wala msipaze sauti zenu zaidi ya sauti ya Mtume." Hawakukiheshimu cheo cha Mtume na wala hawakufanya adabu pale walipomtuhumu kuwa anaweweseka. Hapo kabla Abubakr alikwisha kutamka maneno machafu mbele ya Mtume(s.a.w.w) pale alipomwambia Ur-wah ibn Mas-oud, "Amsas bibidhril-laab." Na Al-QastaJani ambaye ndiye aliyeisherehesha sahihi Bukhari amesema katika kuifafanua ibara hii kwamba, suala la kufyonza Bidhri ni miongoni mwa matusi makubwa mno kwa Waarabu.

Sasa basi, ikiwa maneno kama haya yanatamkwa mbele ya Mtume(s.a.w.w) basi nini maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema: "Na wala msiseme naye kwa sauti ya nguvu kama mnavyosemezana ninyi kwa ninyi.?" Na ikiwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ana tabia njema ya hali ya juu kama alivyomsifu Mola wake, na itakapokuwa Mtume ni mwingi wa haya kuliko mwali aliye ndani kama walivyoyathibitisha haya Bukhari na Muslim. Masheikh hawa wawili Bukhari na Muslim wamebainisha wazi kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) hakuwa muovu wala mwenye kueneza maovu na alikuwa akisema: "Hakika mbora wenu ni mzuri wenu kwa tabia." Basi imekuwaje Masahaba wake hao waliokuwa karibu yake mno hawakuathirika kwa tabia hii tukufu? Zaidi ya yote haya ni kwamba, Abubakr hakutekeleza amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) pale Mtume alipompa uamiri Usamah bin Zaid na Abubakr akawa miongoni mwa askari walio chini ya uamiri wa Usamah (lakini Abubakar hakutii amri hiyo) na Mtume(s.a.w.w) aliwakemea mno wale waliobakia nyuma (wasiende pamoja na Usamah katika jeshi hilo) mpaka akasema: "Mwenyezi Mungu amlaani yeyote atakayebaki nyuma asitoke na jeshi la Usamah." Haya aliyasema baada ya kumfikia habari yeye Mtume juu ya upinzani wa wapinzani dhidi yake kutokana na kumpa uamiri Usamah ibn Zaid, jambo ambalo wanahistoria wengi wamelitaja.

Hali ni kama hiyo kwamba, Abubakr alikimbilia Saqifah na akashiriki kumtenga Ali ibn Abi Talib kutoka kwenye Ukhalifa, na (yeye Abubakar alipokuwa akikimbilia Saqifah) aliuacha mwili wa Mtume na wala hakuona umuhimu wa kumkosha na kumvisha sanda na kufanya maandalizi (yanayohusika) na hatimaye kumzika, bali aliyaacha yote hayo kwa kugombea cheo cha Ukhalifa na uongozi ambao ndiyo iliyokuwa hamu yake. Kama ni hivyo uko wapi huo usahaba na urafiki unao daiwa (kuwa alikuwa nao Abubakar kwa Mtume)?

Na je, iko wapi tabia njema (anayostahiki kuwa nayo)? Mimi unanishangaza sana msimamo wa Masahaba hawa kuhusu Mtume wao ambaye alimaliza muda wa uhai wake akiwaongoza na kuwalea (malezi bora), na kuwapa nasaha mbali mbali Mtume ambaye "Yanamuhuzunisha yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni na ni mpole na mwenye huruma kwa walioamini." Matokeo yake walimuacha juu ya kitanda cha mauti na wao wakakimbilia Saqifah ili kumchagua mmoja wao awe Khalifa wao. Na sisi leo hii tunaishi katika karne ya ishirini, karne ambayo tunaisema kuwa ni karne mbaya, na kwamba eti tabia za watu zimeharibika na miongozo nayo imetelekezwa. Lakini pamoja na hayo hapana shaka Waislamu (wa leo hii) anapokufa jirani yao hufanya haraka kumshughulikia mpaka wanamsitiri kaburini mwake hali ya kuwa wakitekeleza kauli ya Mtume(s.a.w.w) aliposema: "Kumkirimu maiti ni kumzika."

Bila shaka Amirul-Muuminina Ali ibn Abi Talib aliyaumbua matukio hayo waliyoyatenda pale aliposema: "Amraa Wallahi, hakika mwana wa Abu Qahafah (Abubakr) aliuvaa (aliutwaa) Ukhalifa hali ya kuwa anafahamu kwamba nafasi yangu juu Ukhalifa ni sawa na mkono (mshikio) ulioko kwenye jiwe la kusagia." Kisha baada ya hapo, Abubakr aliruhusu nyumba ya bibi Fatmah ihujumiwe na kutishiwa kuchomwa moto ikiwa hawakutoka humo kwenda kumbai Abubakr wale wote waliopinga (Ukhalifa wake) na yalitokea yaliyotokea miongoni mwa mambo ambayo wanahistoria wameyataja ndani ya vitabu vyao na wapokezi nao wakayanakili zama hadi zama nyingine. Nasi tutakubainishia ewe msomaji sehemu tu ya hayo, na ni juu ya mwenye kutaka ziyada kuvisoma vitabu vya historia.