WAULIZE WANAOFAHAMU

WAULIZE WANAOFAHAMU0%

WAULIZE WANAOFAHAMU Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Misingi mikuu ya Dini

WAULIZE WANAOFAHAMU

Mwandishi: Muhammad Tijani As-samawi At-Tunisi
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 49401
Pakua: 4126

Maelezo zaidi:

WAULIZE WANAOFAHAMU
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 26 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 49401 / Pakua: 4126
Kiwango Kiwango Kiwango
WAULIZE WANAOFAHAMU

WAULIZE WANAOFAHAMU

Mwandishi:
Swahili

14

WAULIZE WANAOFAHAMU

ABUBAKR ALIWAUA WAISLAMU WALIOKATAA KUMPA ZAKA

Bukhari amethibitisha katika sahih yake Kitabustitabatil Mar-taddina, Babu qatli man abaa qabulal-faraidhi wama nusibu ilar-ridah, na Muslim naye ndani ya sahih yake Kilabul-iman babul-amri biqitalin-nas. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah amesema: "Alipofariki Mtume(s.a.w.w) na Abubakar akatawazwa, na wakapinga waliopinga miongoni mwa Waarabu, Umar alisema: Ewe Abubakr vipi unataka kuwapiga watu na hali ya kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema kuwa, Nimeamrishwa niwapige watu mpaka waseme Lailaha Illallah, basi yeyote atakayesema Lailaha Illallah mali yake na nafsi yake imehifadhika kutokana nami isipokuwa kwa haki na hisabu yake ni juu ya Mwenyezi Mungu. Abubakar akasema: Wallahi nitampiga yeyote anayetenganisha baina ya sala na zaka kwani zaka ni haki inayostahiki katika mali, Wallahi lau wakinizuwilia mbuzi mdogo (wa zaka) waliyekuwa wakimtoa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) basi nitawapiga kwa kuizuwia (zaka hiyo). Umar akasema basi, Wallahi sikuona isipokuwa Mwenyezi Mungu alikifungua kifua cha Abubakr (ili awapige nami nikafahamu kuwa ni haki."

Na jambo hili si geni kwa Abubakar na Umar ambao walitishia kuichoma moto nyumba ya bibi Fatmah aliye mwanamke bora, pamoja na waliokuwemo miongoni mwa Masahaba waliokataa kutoa baia. Na kama itakuwa kuwachoma moto Fatmah, Ali, Hassan, Hussein na kundi la Masahaba bora ambao walikataa kutoa baia ni jambo jepesi kwa Abubakr na Umar, basi siyo jambo zito kwao kuwaua wanaokataa kutoa zaka. Wana thamani gani Mabedui wa mbali ukiwalinganisha na kizazi kitukufu cha Mtume na Masahaba hao wema? Na zaidi ya hapo ni kwamba hawa waliokataa kutoa baia walikuwa wanaona kuwa haki ya Ukhalifa ni yao kwa mujibu wa matamko ya Mtume(s.a.w.w) , na hata kama tutajaalia iwe hakuna tamko linalowahusisha katika haki waliyokuwa nayo, lakini walikuwa na haki ya kupinga, kukosoa na kutoa maoni kama kweli kulikuwa na mashauriano kama wanavyodai.

Pamoja na hayo kule kuwatishia kuwachoma moto ni jambo lililothibiti, na lau si kukubaliana kwa Ali na kuwaamuru wale Masahaba watoke wakatoe baia ili kuhifadhi kumwagika kwa damu ya Waislamu na umoja wa Uislamu, basi watawala hao wasingechelewesha kuwachoma moto. Ama kwa hakika mambo yaliwanyookea kina (Abubakr na Umar) na zikaimarika nguvu zao, na hapakuwepo mtu mwenye kuwapinga baada ya kufariki kwa bibi Fatmah na baada ya Imam Ali kufanya nao Sulhu, kwa hiyo ni vipi basi watayanyamazia baadhi ya makabila ambayo yalikataa kuwapa zaka yakidai kuwa yanasubiri mpaka jambo la uongozi na mambo yaliyotokea baada ya Mtume(s.a.w.w) yabainike, ikwemo ule Ukhalifa ambao Umar mwenyewe amekiri kuwa ulikuwa ni wa ghafla. Kwa hiyo basi haishangazi (kumuona) Abubakr na serikali yake wananyanyuka na kuwauwa Waislamu wasiokuwa na hatia yoyote na kuwavunjia heshima zao na kuwateka wanawake zao.

Kwa hakika wanahistoria wameeleza kwamba, Abubakar alimtuma Khalid ibn Walid akaliangamize kabila la Bani Sulaim, na akamtuma kwenda Al-Yamamah, na pia kwa Bani Tamim. Khalid aliwaua watu hao kwa hila baada ya kuwafunga mikono na kuzikata shingo zao hali ya kuwa wamefungwa, na akamuuwa Malik ibn Nuwairah sahaba mtukufu ambaye Mtume wa Mwenyezi Mungu alimtawalisha kusimamia sadaka za jamaa zake kwa kumuamini, kisha Khalid akamuingilia mke wa Malik katika usiku ule ule aliomuua mumewe!!! Lahaula Wala quwwata ilia billahil-aliyyil-adhim.

Malik na jamaa zake hakuwa na kosa lolote isipokuwa ni kwamba waliposikia mambo yaliyotokea baada ya kufariki kwa Mtume(s.a.w.w) ikiwa ni pamoja kutengwa kwa Imam Ali na kudhulumiwa kwa bibi Fatmah mpaka akafariki hali ya kuwa amewakasirikia (kina Abubakr). Si hayo tu bali upinzani wa kiongozi wa Ansari Saad ibn Ubbadah na kujitoa kwenye baia yao, na mengineyo waliyoyanakili Waarabu miongoni mwa habari zinazotia shaka juu ya kusihi kwa baia ya Abubakar, kutokana na yote haya Malik na jamaa zake walikataa kutoa zaka. Hivyo basi hukumu iliyotoka kwa Khalifa (Abubakr) na wasaidizi wake ikawa ni kuwaua na kuwateka wanawake zao na watoto wao kisha kuvunja heshima zao na kuwaangamiza kabisa ili kusije kukatokeza miongoni mwa Waarabu wenye maoni ya upinzani au kuhoji juu ya suala la Ukhalifa. Kwa kweli linalohuzunisha mno ni kule kumkuta mtu anamtetea Abubakar na utawala wake, na anayafanya makosa ya Abubakar kuwa ni sahihi, makosa ambayo yeye mwenyewe anakiri kuwa ni makosa, na katika kumtetea anasema kama ilivyokauli ya Umar aliposema: "Wallahi sikuona isipokuwa Mwenyezi Mungu alikifungua kifua cha Abubakar (alimuongoza) ili awapige, nikafahamu kuwa hiyo ni haki."

Je, tunaweza kumuuliza Umar siri ya yeye kutosheka juu ya mauaji haya ya Waislamu, Waislamu ambao yeye mwenyewe Umar ameshuhudia kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ameharamisha kuwauwa kwa sababu tu ya wao kusema Lailaha Illa llah? Ni huyu huyu Umar ndiye aliyemuhadithia Abubakar hadithi hii, ni vipi aligeuka ghafla na akatosheka wauawe? Alitambua kuwa hiyo ni haki eti kwa kuona Mwenyezi Mungu amemuongoza Abubakar, basi je ni vipi tendo la kuongozwa Abubakar lilitimia, na watu wengine wasilione? Ikiwa tendo la Abubakar kupewa muongozo lilikuja kimaana na siyo kwa kuthibitisha (kimaono) basi vipi Mwenyezi Mungu awaongoze watu kwenda kinyume na maamuzi yake ambayo ameyapitisha kwa kupitia ulimi wa Mtume wake(s.a.w.w) ? Na itakuwaje Mwenyezi Mungu awaambie waja wake kupitia ulimi wa Mtume wake kwamba yeyote atakayesema Lailaha Illallah ni haramu kwenu kumuua na malipo yake yako kwangu, kisha hatimaye ampe muongozo Abubakar na Umar wawaue Waislamu hao? Je, kuna ufunuo ulioshuka kwao baada ya Mtume Muhammad? Au ndiyo ijtihadi ambayo inayohukumiwa kwa kutegemea maslahi ya kisiasa, Ijtihadi ambayo imezitupilia mbali hukumu za Mwenyezi Mungu? Ama madai ya wanaowatetea yanasema kuwa, "Watu hawa walitoka katika Uislamu, basi ilikuwa ni lazima kuwaua."

Jambo hilo siyo sahihi, na yeyote ambaye anafuatilia kwa undani vitabu vya historia ataelimika kwa elimu yakinifu kwamba anayezuwia kutoa zaka huwa hajatoka katika Uislamu, basi vipi watakuwa walitoka katika Uislamu hali ya kuwa walisali pamoja na yeye Khalid na jamaa zake walipofika kwenye maeneo yao? Kisha Abubakar mwenyewe aliyabatilisha madai haya ya uongo kwa kutoa fidia (kutokana na mauaji) ya Malik kutoka ndani ya hazina ya Waislamu na akataka radhi kwa kumuua Malik? Na mtu aliyetoka katika dini hakuna kuomba radhi kwa kumuua na wala haitolewi fidia yake kutoka ndani ya hazina ya Waislamu!! Hapana yeyote miongoni mwa viongozi wema waliotangulia aliyesema kwamba wanaozuwia zaka wametoka katika Uislamu, isipokuwa haya yamesemwa katika zama za karibuni pale yalipokuwa yametokea madhehebu na tofauti nyingi miongoni mwa Waislamu.

Masunni wamejaribu juhudi zao bila ya mafanikio kuvitakasa vitendo vya Abubakr, lakini hawakupata njia isipokuwa ni kuwapakazia Waislamu hao kuwa waliritaadi (wakatoka katika Uislamu) na hii ni kwa kuwa Masunni wanafahamu kuwa, kumtukana Muislamu ni ufasiki na kumuua ni kufru, kama yalivyoelezwa hayo ndani ya sahih za Masunni. Hata Bukhari alipoiandika hadithi ya Abubakar na kauli yake aliposema, "Wallahi nitamuua yeyote anayetenganisha kati ya sala na zaka," aliufungua mlango kwa anuani isemayo: "Mwenye kukataa faradhi na wala hakusema kuwa wameritadi." Hiyo ni dalili ya kwamba Bukhari mwenyewe haamini kuwa waliritadi, kama inavyoonekana wazi. Na wengine (miongoni mwa Masunni) wamejaribu kuitolea tafsiri nyingine hadithi hii kama alivyoitafsiri Abubakar kwamba, zaka ni haki ya mali, na hii ni tafsiri iliyowekwa mahala ambapo si pake.

Kwanza : Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ameharamisha kumuua yeyote aliyesema Lailaha Illallah peke yake, na juu ya hilo ziko hadithi nyingi ambazo Sihah zimezithibitisha na tutakuletea hadithi hizo.

Pili : Japokuwa zaka ni haki ya mali, hadithi hii inamruhusu mtawala wa kisheria kuchukua zaka kwa nguvu kutoka kwa anayeizuwia bila kumwaga damu yake.

Tatu : Basi lau tafsiri hii ingekuwa sahihi, Mtume wa Mwenyezi Mungu angemuuwa Tha'alabah ambaye alikataa kutoa zaka kwa Mtume (kisa hiki ni mashuhuri hakuna sababu ya kukitolea maelezo).

Nne : Hebu angalia yale yaliyoandikwa na vitabu vya Kisunni kuhusu heshima ya mtu atakayesema Lailaha Illallah, nami nitatosheka na Bukhari na Muslim na baadhi tu ya hadithi ili nifupishe maelezo.

A: Muslim amethibitisha ndani ya sahih yake, Kitabul-iman Babu Tahrimi qatlil-kafir ba'ada an qala Lailaha illallah, Naye Bukhari ndani ya sahih yake, Kitabul-maghazi babu had-d thani Khalifatu anil Miq-dad ibnil-As-wad, kwamba yeye Miqdad alimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) : "Mtume waonaje ikiwa nitakutana na mtu miongoni mwa makafiri, tukapigana, kisha yeye akaupiga kwa upanga mmoja kati ya mikono yangu na akaukata, kisha akajikinga kutokana nami kwenye mti, halafu akasema, Nimesilim kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Je, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nimuue mtu huyo baada ya kusema kauli hiyo?" Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: "Usimuue." Miqdad akasema "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika yeye ameukata mmoja kati ya mikono yangu kisha amesema hayo baada ya kuukata." Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema, "Usimuue, kwani ukimuuwa yeye atachukua mahala pako ulipokuwa kabla hujamuua na wewe utachukua mahala pake alipokuwa kabla hajasema neno lake hilo alilolisema."

Hadithi hii inafidisha kwamba, kafiri aliyesema Lailaha Illallah, japokuwa baada ya kumtendea ubaya Muislamu kwa kumkata mkono wake, ni haramu kumuua, na hapo hakuna (sharti ya) kukiri kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu wala kusimamisha sala wala kutoa zaka na wala kufunga Ramadhani wala kuhiji Makka. Basi ni wapi mwendako (katika kutetea uovu aliofanya Abubakr) na ni kitu gani mnachokitetea? B: Bukhari ameandika ndani ya sahih yake, Kitabul-Maghazi babu baathin-nabiyyi(s.a.w.w) Usama ibn Zaid ilal-hir-qaat min juhainah, na Muslim ndani ya sahih yake, Kitabul-iman babu tahrimi qatlil-kafir ba 'ada an qaala Lailaha illa llah.

Imepokewa kutoka kwa Usamah ibn Zaid amesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu alitutuma kwenda Al-Hurqah, asubuhi tukawafika kwa jamaa hao na tukawashambulia, mimi na mtu fulani miongoni mwa Ansar tukakutana na mtu katika jamaa hao, basi tulipomvamia akasema Lailaha illa llah "Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu." Yule Muansar akamuacha asimshambulie yule mtu, mimi nikamchoma kwa mkuki wangu nikamuua. Tuliporudi, habari hizo zikamfikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: Ewe Usamah umemuua baada ya kusema Lailah illa llah? Nikasema, alikuwa akijitetea tu. Basi Mtume hakuacha kukariri usemi wake huo mpaka nikatamani kuwa nisingekuwa nimesilimu kabla ya siku ile." Hadithi hii moja kwa moja inafidisha kwamba yeyote atakayesema Lailaha illa llah ni haramu kumuua, ndiyo maana unamuona Mtume(s.a.w.w) anamkemea mno Usamah mpaka Usamah anatamani kwamba asingekuwa amesilimu kabla ya siku ile ili impate ile hadithi isemayo kuwa, Uislamu unafuta yaliyopita kabla yake, ili awe na matumaini ya kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu kuhusu dhambi hii kubwa aliyoifanya. C: Bukhari ameandika ndani ya sahih yake, Kitabul-libasi babut-thiyabil-biidh. Kadhalika Muslim ndani ya sahih yake Kitabul-imani babu man maata laa Yushriku billahi shaian dakhalal-jannah.

Imepokewa kutoka kwa Abu Dharri Al-ghifari (r.a) amesema: "Nilikwenda kwa Mtume(s.a.w.w) akiwa amejifunika nguo nyeupe amelala, kisha nikamwendea akawa ameamka akasema, Hapana mja yeyote atakayesema Lailaha illa llah kisha akafa hali ya kuwa yuko katika hali hiyo isipokuwa ataingia peponi. Nikasema japo atazini na ataiba? Akasema: Japo atazini na ataiba. Nikasema japo atazini na ataiba? Akasema japo atazini na ataiba hata kama Abudharri atachukia." Abudharri kila alipoisimulia hadithi hii alikuwa akisema "Hata kama Abudharri atachukia ." Na hii ni hadithi nyingine inayothibitisha kuingia peponi kwa mtu yeyote atakayesema Lailah Illa llah na akafa. Katika hali hiyo basi haifai kumuua, na hata kama Abubakar na Umar watachukia na wote wanaowatetea ambao wanaugeuza ukweli kwa kulinda heshima ya viongozi wao waliopita na wakubwa zao ambao walizibadilisha hukumu za Mwenyezi Mungu. Ukweli halisi ulivyo ni kwamba Abubakar na Umar wanazifahamu hukumu zote hizo, kwani wao wako karibu mno kuliko sisi katika kufahamu hukumu hizo na wako karibu mno na Mtume kuliko wengineo, lakini watu hawa kwa ajili ya (tamaa ya) uongozi walibadilisha hukumu nyingi za Mwenyezi Mungu na Mtume wake(s.a.w.w) hali ya kuwa wanajua wazi.

Na huenda Abubakr alipoazimia kuwaua waliozuwia kutoa zaka, na Umar akampinga kwa hadithi ya Mtume(s.a.w.w) ambayo inaharamisha jambo hilo, basi Abubakr alimkatiza jamaa yake kwa kumwambia kuwa (akumbuke kwamba) yeye ndiye aliyebeba kuni kwenda kuichoma nyumba ya Fatmah na kwamba Fatmah alipopeleka madai yake alikuwa akishuhudia kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, (pamoja na hali hiyo Umar akataka kwenda kuichoma nyumba ya Fatmah) kisha (Abubakr) akamkinaisha Umar kwamba, Fatmah na Ali hawakuwatendea (kina Abubakr) jambo lolote kubwa (la kuhatarisha) katika Ukhalifa, wakati ambapo makabila haya yalikataa kutoa zaka, kwa hiyo lau wangewaacha na jambo lao hilo likaenea katika miji ya Kiislamu, basi bila shaka pangetokea athari kubwa kwao kwenye makao makuu ya Ukhalifa. Basi hapo ndipo Umar alipoona kuwa eti Mwenyezi Mungu amemuongoza Abubakr awapige na akakiri kuwa hiyo ni haki.

Abubakr alikataza kuandikwa Sunna ya Mtume, pia Umar na Uthman nao walifanya hivyo baada yake. Bila shaka mtu anayetafiti akisoma vitabu vya historia na akafuatilia baadhi ya mambo ambayo utawala wa Makhalifa watatu ulikuwa umeyakusudia kuyafanya, atafahamu vilivyo kwamba wao ndiyo waliokataza kuandikwa hadithi za Mtume Mtukufu, bali walikataza hata kuzisimulia na kuzinakili kuwajulisha watu, kwani Makhalifa hao bila shaka walifahamu kwamba hazitatumikia maslahi yao au zitapingana na maamuzi yao mengi na yale waliyoyageuza kufuatia juhudi zao na kwa maslahi yao. Hadithi za Mtume(s.a.w.w) ambazo ndiyo msingi wa pili wa sheria ya Kiislamu, na ndizo zenye kufasiri na kuubainisha msingi wa kwanza ambao ni Qur'ani Tukufu, zilibakia ni marufuku na ni haramu (kuziandika na kuzizungumza) katika kipindi chao cha utawala na ndiyo maana wameafikiana wanachuoni wa hadithi na wale wa historia kuwa mwanzo wa kukusanywa hadithi na kuandikwa ilikuwa katika zama za Umar ibn Abdil-aziz (r.a) au baada yake kwa kipindi kifupi.

Bukhari amenakili ndani ya sahih yake, Kitabul-ilmi, babu kaifa yuqbahd-ilm, amesema, "Umar ibn Abdul-aziz alimwandikia Abubakar ibn Hazmi akamwambia, Ziangalie hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) uziandike, hakika mimi nachelea kuhusu elimu na kutoweka kwa wanachuoni, na isikubaliwe isipokuwa iwe ni hadithi ya Mtume(s.a.w.w) na elimu ienezwe na watu wakae ili kila asiyejua afundishwe, kwani elimu haipotei mpaka pale inapofichwa. Basi hebu msikilize Abubakr anawahutubia watu baada ya kufariki Mtume(s.a.w.w) anawaambia: "Bila shaka ninyi mnasimulia hadithi kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) ambazo mnakhitilafiana katika hadithi hizo, na watu watakaokuja baada yenu watahitilafiana mno, hivyo basi msisimulie chochote kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, yeyote atakayekuulizeni semeni kuwa, Baina yetu na ninyi kipo Kitabu cha Mwenyezi Mungu, halalisheni halali yake na mharamishe haramu yake.

Wallahi Abubakr ana mambo ya ajabu, ni yeye huyo huyo baada ya siku chache tangu siku ile ya kusikitisha ambayo iliitwa kuwa ni msiba wa siku ya Al-hamisi anaafikiana moja kwa moja na yale aliyoyasema jamaa yake Umar ibn Khatab pale aliposema "Bila shaka Mtume wa Mwenyezi Mungu anaweweseka, kinatutosha Kitabu cha Mwenyezi Mungu." Sasa (Abubakr) naye anasema: "Msisimulie chochote kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, yeyote atakayekuulizeni semeni kuwa, kati yetu na ninyi ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, halalisheni halali yake na muharamishe haramu yake." Ashukuriwe Mwenyezi Mungu (kwa sababu Abubakr) amekiri wazi kwamba, wao waliitupa mgongoni Sunna ya Mtume wao na wakaifanya kuwa ni kitu kilichosahaulika kabisa. Swali lililopo hapa ni linawaelekea Masunni ambao wanawatetea Abubakr na Umar. na kuwaona kuwa wao ndiyo viumbe bora mno baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) nini hili lifuatalo: Iwapo Sihah zenu (vitabu vyenu sahihi) kama mnavyoitakidi vinaandika riwaya isemayo kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Nimekuachieni Makhalifa wawili ambao mkishikamana nao hamtapotea kamwe, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna zangu. " Sisi tunajaalia kuikubali hadithi hii kuwa ni Sahihi, lakini ilikuwaje kwa hao wabora wa viumbe kwenu ninyi kuikataa sunna (ya Mtume) na wala hawakuipa uzito unaostahiki, bali wakiwazuwia watu kuiandika na kuisimulia? Je, kuna mtu atakayemuuliza Abubakar ni katika aya gani amekuta (ruhusa ya) kuwaua Waislamu wanaokataa kutoa zaka na kuwateka nyara wake zao na watoto wao?

Kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho ndicho kilichopo kati yetu na Abubakr kinasema wazi kuhusu watu wanaokataa kutoa zaka.

وَمِنْهُم مَّنْ عَاهَدَ اللَّـهَ لَئِنْ آتَانَا مِن فَضْلِهِ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٧٥﴾ فَلَمَّا آتَاهُم مِّن فَضْلِهِ بَخِلُوا بِهِ وَتَوَلَّوا وَّهُم مُّعْرِضُونَ ﴿٧٦﴾ فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِي قُلُوبِهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ يَلْقَوْنَهُ بِمَا أَخْلَفُوا اللَّـهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ ﴿٧٧﴾

"Na miongoni mwao wapo waliomuahidi Mwenyezi Mungu kuwa, Akitupatia katika fadhila zake, tutatoa sadaka na tutakuwa miongoni mwa wanaotenda mema, lakini alipowapa hizo fadhila zake, walizifanyia ubakhili na wakakengeuka, kwa hiyo akawalipa unafiki ndani ya nyoyo zao mpaka siku ya kukutana naye kwa sababu ya wao kukhalifu waliyomuahidi Mwenyezi Mungu na kwa sababu ya kusema kwao uongo." (Qur'ani, 9:75-77).

Na kwa maafikiano ya wafasiri wote (wa Qur'an) aya hii ilishuka kumuhusu Tha'alabah, ambaye alikataa kutoa zaka katika zama za Mtume(s.a.w.w) , hivyo basi fahamu kwamba Tha'alaba alizuwia kutoa zaka na akakataa kumpa Mtume(s.a.w.w) hiyo zaka, kwani aliipinga na akasema kuwa hiyo ni kodi. Bila shaka Mwenyezi Mungu ameshuhudia ndani ya aya hizi juu ya unafiki wake (huyu Tha'alabah), pamoja na hayo Mtume(s.a.w.w) hakumshambulia, na wala hakuchukua mali zake kwa nguvu na hali ya kuwa Mtume alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Ama Malik ibn Nuwairah na watu wake hawakuipinga zaka kama faradhi miongoni mwa faradhi za dini, bali walimpinga Khalifa alieukalia Ukhalifa baada ya Mtume(s.a.w.w) kwa nguvu na shinikizo na kuchukua (kwake) nafasi hiyo. Hakika mambo ya Abubakr ni ya kushangaza mno, bwana huyu alikipuuza kitabu cha Mwenyezi Mungu, wakati bibi Fatmah alipotoa kitabuni humo hoja dhidi ya Abubakr, na akamsomea masikioni mwake aya zilizowazi kutoka ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho kinathibitisha kurithiwa kwa Mitume, lakini Abubakr hakukubali na akazitengua aya zote kwa kutumia hadithi aliyoileta yeye ili kutimiza matamanio ya nafsi yake.

Na ikiwa yeye Abubakr anasema: "Hakika ninyi mnasimulia hadithi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na mnahitilafiana ndani ya hadithi hizo, na watu watakaokuja baada yenu watahitilafiana mno, basi msisimulie chochote kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, yeyote atakayekuulizeni mwambieni kati yetu na ninyi ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, ihalalisheni halali yake na muiharamishe haramu yake." Iwapo haya ndiyo maneno yake, basi ni kwa nini yeye hakufanya kama asemavyo pale yeye na Binti ya Mtume(s.a.w.w) walipohitilafiana kuhusu ile hadithi ya Mtume isemayo kuwa: "Sisi Manabii haturithiwi ." Bali mbona hakuhukumiana na Bibi Fatmah kwa mujibu wa kitabu cha Mwenyezi Mungu, ili apate kuihalalisha halali yake na kuiharamisha haramu yake? Jawabu liko wazi: Katika hali hiyo (lau angekubali) bila shaka angekikuta kitabu cha Mwenyezi Mungu kiko dhidi yake, na bibi Fatmah angepata ushindi katika madai yake dhidi ya Abubakr. Na kama siku hiyo bibi Fatmah angepata ushindi, basi huenda bibi Fatmah angekuja kumuuliza Abubakr kwa kutumia maneno ya Mtume kuhusu Ukhalifa wa Ibn ammi yake (Imam Ali), na hapo Abubakr asingeweza kumpinga, na kuhusu hali hii Mwenyezi Mungu anasema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ ﴿٢﴾ كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ ﴿٣﴾

"Enyi mlioamini mbona mnasema msiyoyatenda, ni jambo linalochukiza mbele ya Mwenyezi Mungu kusema msiyoyatenda. (Qur'ani,61:2-3).

Naam, kwa ajili ya yote hayo, Abubakr asingestarehe iwapo hadithi za Mtume(s.a.w.w) zingebakia zikisambaa miongoni mwa watu, na kupeana kutoka mji huu kwenda mji ule na hali ya kuwa ndani ya hadithi hizo yamo maelezo wazi yanayopingana na siasa ambazo dola yake ilisimama (kwa kupitia siasa hizo). Kwa hiyo hapakuwa na njia aliyoiona isipokuwa ni kuzikandamiza na kuzificha bali kuzifuta na kuzichoma moto hadithi (za Mtume(s.a.w.w) . Huyu hapa bibi Aisha binti yake Abubakr anashuhudia hilo dhidi ya Abubakr. anasema: "Baba yangu alizikusanya hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu, zilikuwa hadithi mia tano akawa anazigeuza geuza, nikasema anazigeuza geuza kwa kuwa ana mashaka fulani yaliyomfikia? Basi kulipokucha akasema: Ewe binti yangu niletee hadithi ulizonazo, nikamletea, akazichoma moto."

Umar ibn Khatab anakuwa mkali zaidi kuliko mwenzake, dhidi ya wanaosimulia hadithi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na anawazuia watu kuzinakili hadithi. Bila shaka tumeona siasa ya Abubakar juu ya kuzuwia hadithi kiasi kwamba alifikia wakati akazichoma moto hadithi zilizokuwa zimekusanywa katika zama zake, na zilikuwa mia tano. Kufanya hivyo ni kwa kusudio la kwamba zisije zikaenea miongoni mwa Masahaba na Waislamu wengineo ambao walikuwa na hamu kubwa ya kuifahamu sunna ya Mtume wao. Umar alipotawalia Ukhalifa kutokana na amri ya Abubakr, aliwajibika kuendeleza siasa ile ile, lakini kwa kutumia mfumo wake unaoeleweka ambao ni ukali na ususuavu. Hakuacha kuzuwia na kukataza kuandikwa hadithi na kuzitawanya tu, bali alionya na kukemea, kupiga na alitumia (njia ya) kuwadhibiti.

Ibn Majah ameeleza ndani ya Sunan yake katika juzuu ya kwanza Babut-tawaqqi fil-hadith amesema: "Imepokewa kutoka kwa Qurzah ibn Ka'ab kwamba Umar ibn Khatab alituma kwenda Kufah na akatushindikiza, alikwenda pamoja nasi mpaka mahala paitwapo Siraar akasema, Je, mnafahamu ni kwa nini nimetembea pamoja nanyi? Tukasema ni kwa ajili ya haki ya kusuhubiana kwako na Mtume wa Mwenyezi Mungu na ni kwa ajili ya haki ya Maansari. Umar akasema, Mimi nimetembea pamoja nanyi ili nipate kuwazungumzeni mazungumzo niliyotaka kukuzungumzeni. Nimekusudia kwa ajili ya mwendo wangu huu muyahifadhi mazungumzo hayo, bila shaka ninyi mtafika kwa watu ambao wanayo Qur'an vifuani mwao ikitingishika kama unavyotingishika mtungi wenye maji, watakapokuoneni watanyoosha shingo zao kwenu na watasema (hao ni) Masahaba wa Muhammad!! Basi punguzeni kuwapa riwaya zitokazo kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kisha kwa jambo hili mimi nitakuwa pamoja nanyi." Basi Qur'zah ibn Ka'ab alipofika huko watu hao wakasema: Tusimulie, Akasema, Umar ametukataza."

Kama alivyoeleza Muslim ndani ya sahihi yake Kitabul-adab babul isti-idhaan kwamba: Umar alimuonya Abu Musa al-Ash'ari kwamba, angempiga kwa sababu ya kusimulia hadithi aliyoipokea kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) . Abusaid Al-khudri amesema: "Tulikuwa katika kikao kwa Ubayyi ibn Ka'ab, basi akaja Abu Mussa Al-ash'ar akasimama hali ya kuwa amekasirika akasema: Nakuapieni Mwenyezi Mungu hivi kuna yeyote miongoni mwenu aliyemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema, Kubisha hodi ni mara tatu ukikaribishwa (uingie) vinginevyo basi rudi."

Ubayyi akasema kuna nini (kimetokea)? (Abu'Musa) akasema nilibisha hodi kwa Umar ibn Khatab jana mara tatu lakini sikuitikiwa nikarudi, kisha leo nilimwendea nikaingia kwake na nikamwambia kwamba mimi jana nilikuja na nikasalimia mara tatu kisha nikaondoka, yeye akasema, Hakika tulikusikia lakini katika kipindi hicho sisi tulikuwa tumeshughulika, lau ungeendelea tu kubisha hodi mpaka tukukaribishe. Mimi nikamwambia nilibisha hodi kama taratibu ile niliyomsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (akifundisha). Basi Umar akasema (kuniambia) Wallahi nitaujeruhi mgongo wako na tumbo lako au vinginevyo uniletee watakaokushuhudia juu ya jambo hili (ulisemalo). Ubayyi ibn Ka'ab akasema, Wallahi hatosimama pamoja nawe isipokuwa aliye mdogo wetu kwa umri, simama ewe Abu Said, nikasimama nikamwendea Umar nikasema: Bila shaka nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema jambo hili." Naye Bukhari amelielezea tukio hili, lakini yeye kama kawaida yake amelikata na akaondosha maonyo ya Umar kuwa atampiga Abu Mussa Al-ash'ari, kama ilivyo desturi yake kutetea heshima ya Umar.

Pamoja na hayo, Muslim ndani ya sahihi yake ameongeza kauli ya Ubayyi ibn Ka'ab kumwambia Umar, "Ewe mwana wa Khatab usiwe mwenye kuwaadhibu Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ." Naye Ad-dhahabi amepokea ndani ya Tadh-kiratul-huffaadh, katika juzuu ya kwanza ukurasa wa nne. Kutoka kwa Abu Salamah amesema: "Nilimwambia Abu Hurairah, Je, katika zama za Umar ulikuwa ukiyasimulia haya? (yaani hadithi za Mtume) akasema, Lau ningekuwa nasimulia katika zama za Umar kama ninavyokusimulieni Wallahi angenipiga kwa fimbo yake." Ni kama ambavyo Umar baada ya kuzuwia kusimulia hadithi na kuonya kumpiga atakayesimulia, pia yeye alichoma moto maandiko hadithi (za Mtumes.a.w.w ). yaliyoandikwa na Masahaba.

Siku moja aliwahutubia watu akasema: "Enyi watu hakika imenifikia habari kwamba, kumeonekana mikononi mwenu vitabu, (mimi nasema), kitabu kipendezacho mbele ya Mwenyezi Mungu ni kile chenye uadilifu na sahihi, kwa hiyo asibakishe mmoja wenu kitabu chochote ila aniletee ili nitoe maoni yangu ndani ya kitabu hicho. Watu wakadhani kwamba yeye anataka kuvisahihisha ili pasiwe na kutofautiana ndani yake, wakamletea vitabu vyao, yeye akavichoma moto."[135] Ni kama alivyoandika ibn Abdilbarri ndani ya Kitabu jaami'i hayaanil-Ilmi wafadhlih kwamba, Umar ibn Khatab alitaka kuiandika Sunna ya Mtume(s.a.w.w) kisha ikamdhihirikia kuwa asiandike, na hatimaye akawaandikia kwenye miji (ya Kiislamu) kwamba, "Yeyote aliyemiliki chochote kile (katika sunna ya Mtume) basi na akifute." Na alipokuwa hana njia yoyote ile pamoja na kuonya kwake, kukemea kwake, kuzuwia kwake na kuvichoma moto vitabu vya hadithi, walibakia baadhi ya Masahaba wakihadithia waliyoyasikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) pindi wakutanapo na watu katika safari zao nje ya Madina kila wanapowauliza juu ya hadithi za Mtume(s.a.w.w) . Hapa ndipo Umar alipoona awafungie watu hawa mjini Madina na awawekee vizuwizi na akaimarisha ukandamizaji dhidi yao.

Amepokea ibn Is-haq kutoka kwa Abdur-rahman ibn Auf amesema: "Wallahi Umar hakufa mpaka pale alipokuwa amewatumia ujumbe kuwaita Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu akawakusanya kutoka sehemu mbali mbali, (na aliowakusanya walikuwa ni) Abdallah ibn Hudhaifah, Abud-dirdai, Abudharri Al-ghifari na U'qbah ibn Amir, Umar akawaambia: Imekuwaje ninyi mmezisambaza sehemu mbali mbali hizi hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu" Wakamwambia: Je,unatukataza kufanya hivyo? Akasema: Hapana, lakini bakieni kwangu (hapa hapa Madina), naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba, hamtaachana nami muda wote wa uhai wangu.[136] Kisha baada ya Umar alikuja Khalifa wa tatu Uthman ambaye alifuata nyayo zile zile na akipita pale alipotengenezewa na jamaa yake aliyetangulia, akapanda kwenye mimbari na akatangaza bayana aliposema: "Si halali kwa yeyote yule kuleta hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ambayo mimi sikuisikia katika zama za Abubakr na Umar.

Basi hivyo ndivyo ulivyoendelea udhibiti (dhidi ya hadithi za Mtume) kwa muda wote wa uhai wa Makhalifa hao watatu, na hicho kilikuwa ni kipindi cha miaka ishirini na tano, na laiti angalau udhibiti huo ungekuwa katika kipindi hicho peke yake lakini uliendelea baada ya hapo. Kwani alipokuja Muawiyah kwenye utawala, naye akapanda juu ya minbar akasema: "Ole wenu kusimulia hadithi, isipokuwa (simulieni hadithi) zilizokuwepo wakati wa Umar, kwani Umar alikuwa akiwakhofisha watu kuhusu Mwenyezi Mungu Mtukufu." Hadithi hii ameiandika Muslim ndani ya sahih yake katika Kitabuz-zakati babun-nahyi anil-mas-allah juzuu ya tatu. Mwenendo wa Makhalifa wa Kibani Umayyah uko katika mfumo huu, wao walizuwia hadithi sahihi za Mtume na wakabobea katika fani ya kuzusha hadithi za uongo dhidi ya Mtume(s.a.w.w) kiasi kwamba, Waislamu leo hii wameingia ndani ya mtihani wakati wote kutokana na (balaa la) hadithi zinazopingana na uzushi ambao kabisa hauna uhusiano wowote na Uislamu.

Hebu angalia (mifano) aliyoinakili Al-madaini jidani ya kitabu chake kiitwacho, Al-ahdath amesema: "Muawiyah aliwaandikia watendaji wake (yaani magavana) makala moja baada tu ya mwaka ule wa jamaa (akasema ndani ya makala hiyo), "Simchukulii dhamana mtu yeyote atakayeeleza kitu chochote miongoni mwa fadhila za Abu Turab ( yaani Ali) na watu wa nyumba yake." Hapo ndipo makhatibu waliposimama kwenye mimbar katika kila mji (misikitini na sehemu nyinginezo) wakawa wanamlaani Ali(a.s) na kumtukana yeye na watu wa nyumba yake." Hatimaye Muawiyah aliwaandikia tena watendaji wake sehemu zote kwamba, wasikubali ushahidi wa yeyote miongoni mwa wafuasi wa Ali(a.s) na watu wa nyumba yake, akawaandikia akasema, "Waangalieni vema (muwatunze) wafuasi na wapenzi wa Uthman walioko kwenu, ambao wanamtawalisha (Uthman) na wale wanaosimulia fadhila zake na ubora wake, yasogeleeni makazi yao na muwasogeze karibu, muwakirimu na muniandikie kila kile akisimuliacho mtu miongoni mwao, jina lake na jina la baba yake na la ukoo wake."

Basi wakafanya hayo mpaka riwaya zinazohusu ubora na utukufu wa Uthman zikawa nyingi mno. Muawiyah alikuwa akiwapelekea (magavana wake) zawadi mbalimbali ikiwemo mavazi na kuwapa nyadhifa, na aligawa mali nyingi kuwapa Waarabu. Jambo hilo likaenea kwa wingi katika kila mji, na watu wakashindania vyeo na kuipata dunia, ikawa hawezi kuja mtu kwa hawa watendaji wa Muawiyah akarudishwa bure. Kwa ajili hiyo basi walikuwa wakisimulia fadhila na ubora wa Uthman, kisha (gavana) humwandika jina (mtu huyo) na humkaribisha vizuri halafu humzawadia. Hali hiyo ilibakia kwa muda fulani, kisha Muawiyah aliwaandikia watendaji wake akasema: "Hadithi juu ya Uthman zimeshakuwa nyingi na zimetapakaa kila mji na kila mahali, basi barua yangu itakapokufikieni watakeni watu wasimulie kuhusu ubora wa Masahaba na Makhalifa wa mwanzoni, na msiiache habari yoyote inayosimuliwa na Muislamu yeyote kuhusu Abu Turab isipokuwa leteni hadithi kinyume chake kuhusu Masahaba, kwani jambo hili mimi nalipendelea mno na ndiyo nipatapo utulivu na litazima hoja ya Abu Turab na wafuasi wake na litawavunja nguvu kutokana na fadhila za Uthman na utukufu wake (tulioutengeneza).

Barua zake zikasomwa mbele ya watu, na hapo ndipo zilipoanza kusimuliwa habari nyingi kuhusu Utukufu wa Masahaba, habari ambazo ni za kuzusha zisizokuwa na ukweli wowote, na watu walifanya kila juhudi kuleta riwaya zinazokubaliana na mtazamo huu mpaka wakapata umashuhuri kwa kuyataja hayo katika mimbar na yakapelekwa kwa waalimu wa vyuoni nao wakawasomesha vijana wao na watoto wao kiasi cha kuzipokea habari hizo na kuzisoma kama isomwavyo Qur'ani. Si hivyo tu bali wanawake wao, watumishi wao na jamaa zao nao waliishi katika mazingira hayo kwa muda mrefu. Hatimaye Muawiyah aliandika nakala nyingine moja akaipeleka kwenye miji yote (akasema ndani ya nakala hiyo): "Muangalieni yeyote ambaye utathibiti ushahidi kwamba anampenda Ali na watu wa nyumba yake, basi mumfute jina lake ndani ya diwani (daftari) na muliondoshe pato lake na riziki yake." Kisha Muawiyah alifuatisha nakala nyingine tena akasema: "Yeyote mtakayemtuhumu kuwa anawatawalisha watu hawa (Ali na watu wa nyumba yake), muadhibuni adhabu (itakayokuwa ni fundisho kwa wengine) na muibomoe nyumba yake."

Balaa hili kubwa liliwakumba watu wa Iraqi na hasa mji wa Kufah, kiasi kwamba mtu yeyote katika wafuasi wa Imam Ali alikuwa akifikiwa na mtu hamuingizi ndani mpaka awe anamuamini na kumpa siri yake, na mtu akawa anamuogopa hata mtumishi wake na mtumwa wake, na hamsimulii chochote mpaka amuapishe kiapo kizito kuthibitisha kwamba atamfichia siri yake. Kipindi hiki zilidhihiri hadithi nyingi za uzushi na uongo na zikaenea, nao wanachuoni na maqadhi na watawala wakazikubali. Watu waovu mno juu ya balaa hili (katika kuenea kwake) ni wasomi wenye kujipendekeza (kwa watawala) na wanyonge ambao huonesha unyenyekevu na ucha Mungu, hawa walikuwa wakizitumia hadithi hizo ili wapate vyeo mbele ya watawala wao, na wapate kuyakaribia mabaraza ya watawala na wapate mali, mashamba na majumba kiasi kwamba hadithi hizo za uongo zikasambaa sana mbele za watu wa dini wasiojua uzushi na uongo, nao wakazikubali hadithi hizo na kuzieleza hali yakuwa wanadhani kuwa ni za kweli, na lau wangetambua kuwa siyo za kweli wasingezipokea wala wasingezitumia. Mimi nasema kwamba, jukumu la yote hayo linabebwa na Abubakr, Umar na Uthman, hawa ndiyo ambao walizuwia hadithi sahihi za Mtume wa Mwenyezi Mungu zisiandikwe kwa madai ya kuchelea kuchanganyikana Sunna na Qur'an. Huu ndiyo usemi wausemao wanaowatetea na kuwasaidia, na madai kama hayo yanamchekesha hata mwenda wazimu.

Na je, hivi Qur'ani na Sunna ni kama sukari na chumvi ambavyo vikichanganyika inakuwa hakuna uwezekano wa kukitenganisha kimoja wapo kutokana na mwenziwe na hata hiyo sukari na chumvi havichanganyikani kwani kila kimoja huhifadhiwa ndani ya kopo lake maalum. Je, Makhalifa hawa hawakutambua kuwa waiandike Qur'an ndani ya Msahafu wake na Sunna nayo waiandike ndani ya Kitabu chake maalum kama hali ilivyo kwetu leo hii.? Na tangu hadithi zilipoandikwa katika zama za Umar ibn Abdil-azizi (r.a), basi ni kwa nini Sunna na Qur'an hazikuchanganyikana pamoja wakati ambapo vitabu vya hadithi vinahesabika kwa mamia. Sahih Bukhari haikuchanganyikana na Sahihi Muslim, na hii nayo haikuchanganyikana na Mus-nad ya Ahmad wala Muwataa ya Imam Malik, sembuse Qur'an Tukufu ichanganyikane na Hadithi? Bila shaka hii ni hoja dhaifu mfano wa nyumba ya buibui haisimami kuwa ni dalili bali kinyume chake ndiyo dalili iliyo wazi.

Amepokea Az-zuhri kutoka kwa Ur-wah kwamba, Umar ibn Khatab alitaka kuandika Sunna (ya Mtume) akataka maoni ya Masahaba wa Mtume(s.a.w.w) wao wakamuelekeza kuwa aiandike. Basi Umar akawa anamuomba ushauri Mwenyezi Mungu kuhusu jambo hilo kwa kadiri ya mwezi mmoja, kisha siku moja alipoamka asubuhi akasema: "Hakika mimi nilikuwa nataka kuiandika Sunna (ya Mtumes.a.w.w ) nami nimekumbuka kwamba, watu waliokuwa kabla yenu waliandika vitabu kisha 'WakaVithamini mno wakakiacha kitabu cha Mwenyezi Mungu 'nami kwa hiyo Wallahi siwezi kamwe kukichanganya kitabu cha Mwenyezi Mungu na kitu chochote kile. Ewe msomaji ingalie riwaya hii, ni namna gani Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu walivyomuelekeza Umar kwamba aiandike Sunna ya (Mtumes.a.w.w ) naye akawapinga wote na akayategemea maoni yake kwa madai eti watu waliokuwa kabla yao waliandika vitabu kisha wakavithamini mno na wakakiacha kitabu cha Mwenyezi Mungu. Basi kama ni hivyo, yako wapi basi madai ya kuwepo mashauriano (shuuraa) ambayo Masunni wanajivunia? Kisha wako wapi hao watu waliothamini vitabu vyao na kukiacha Kitabu cha Mwenyezi Mungu? Hatujapata kuwasikia watu hao isipokuwa kutoka katika mawazo ya Omar ibn Khat-tab. Hebu tukadirie kuwepo kwa watu hawa, lakini hatuna sababu ya kuwalinganisha kwani wao waliandika vitabu vyao wenyewe ili kukipotosha kitabu cha Mwenyezi Mungu, imekuja ndani ya Qur'an Tukufu kama ifuatavyo:

فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَـٰذَا مِنْ عِندِ اللَّـهِ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا يَكْسِبُونَ ﴿٧٩﴾

"Adhabu kali itawapata wale wanaoandika kitabu kwa mikono yao kisha wakasema, Hiki kinatoka kwa Mwenyezi Mungu ili wapate thamani ndogo ya ulimwenguni, basi ole wao kwa yale iliyoyaandika mikono yao na ole wao kwa yale wayatendayo. (Qur'an, 2:79).

Ama kuziandika Sunna za Mtume sivyo kama hivyo, kwani zenyewe zinatokana na Nabii aliyehifadhiwa, ambaye hasemi kwa matamanio yake isipokuwa ni wahyi unaofunuliwa kwake, na hii Sunna ndiye mbainishaji na mfasiri.wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema:

بِالْبَيِّنَاتِ وَالزُّبُرِ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٤٤﴾

"Na tumekuteremshia mawaidha ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao." (Qur'an, 16:44).

Naye Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Nimepewa-Qur'an na kilicho mfano wa Qur'an pamoja nayo. " Jambo hili halipingiki kwa kila aliyeifahamu Qur'an, kwani ndani ya Qur'an hizo sala tano (kwa namna tunavyozisali), na zaka kwa viwango vyake, hukumu za saumu na hakumu za hijja na hukumu nyingine nyingi tu zote amezibainisha Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , na kwa ajili ya yote haya Mwenyezi Mungu amesema: "Anachokupeni Mtume kichukueni, na anachokukatazeni kiacheni." Na amesema: "Waambie, ikiwa ninyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni Mwenyezi Mungu atakupendeni."

Ilikuwa jambo jema kwa Umar kufanya bidii ili apate kujifunza na kukifahamu kitabu cha Mwenyezi Mungu na kufuata maamrisho ya Mtume wala asingeyajadili na wala kuyakosoa. Na laiti Umar angekifahamu kitabu cha Mwenyezi Mungu na akafanya bidii kujifunza hukumu ya mirathi ya ndugu kwa upande wa mama ambayo Umar hakuifahamu mpaka akafariki, (lakini masikini hakufanya hivyo) na akahukumu katika zama za Ukhalifa wake kwa hukumu mbali mbali zinazopingana. Laiti angekifahamu Kitabu cha Mwenyezi Mungu na akafanya bidii ili ajifunze hukumu ya kutayammamu ambayo hakuifahamu hata katika siku za Ukhalifa wake, bali alitoa fat-wa kwamba mtu ambaye hakupata maji asisali.

Na laiti Umar angekifahamu kitabu cha Mwenyezi Mungu na akafanya bidii ili ajifunze kutokana na kitabu hicho ile hukumu ya talaka kuwa ni mara mbili, basi imma kukaa kwa wema au kuachana kwa wema (lakini kwa kuwa hakujifunza) Umar akaifanya kuwa ni moja na akazipinga hukumu za Mwenyezi Mungu kwa maoni yake na ijtihadi yake, kisha hukumu za Mwenyezi Mungu akazitupilia mbali.

Ukweli uliopo ambao haukwepeki ni kwamba, Makhalifa (hao) walizuwia kuenea kwa hadithi (za Mtume) na wakamuonya yeyote anayezisimulia na kuziwekea vikwazo, kwani hadithi hizo zilikuwa zinaumbua mipango yao na njama zao, na walikuwa hawana njia ya kuziawili kama walivyoiawili Qur'ani, kwani Kitabu cha Mwenyezi Mungu kimebeba namna nyingi. Amma Sunna ya Mtume yenyewe ni maneno na vitendo vya Mtume(s.a.w.w) haiwezekani kwa mtu yeyote kuibadilisha, na ndiyo maana Amirul-muuminina Ali(a.s) alimwambia Ibn Abbas wakati alipomtuma aende akawatolee hoja Makhawariji (akasema): "Usijadiliane nao kwa Qur'an, kwani Qur'an imebeba mengi na namna nyingi, wewe utasema na wao watasema, lakini jadiliana nao kwa Sunna (ya Mtume) basi hapo hawatapata njia ya kukwepa.