WAULIZE WANAOFAHAMU

WAULIZE WANAOFAHAMU0%

WAULIZE WANAOFAHAMU Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Misingi mikuu ya Dini

WAULIZE WANAOFAHAMU

Mwandishi: Muhammad Tijani As-samawi At-Tunisi
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 49404
Pakua: 4127

Maelezo zaidi:

WAULIZE WANAOFAHAMU
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 26 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 49404 / Pakua: 4127
Kiwango Kiwango Kiwango
WAULIZE WANAOFAHAMU

WAULIZE WANAOFAHAMU

Mwandishi:
Swahili

2

WAULIZE WANAOFAHAMU

MLANGO WA PILI KATIKA MAMBO YANAYOMUHUSU MTUME (s.a.w.w).

Swali la Pili : Isma ya Mtume(s.a.w.w) . Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema kuhusu ustahiki wa Mtume wake Muhammad(s.a.w.w)

"Na Mwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu . " (Qur'an, 5:67), na amesema tena:

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾

"Na wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake) isipokuwa ni ufunuo uliofunuliwa kwake." (Qur'an, 53:3).

Na akasema tena,

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ﴿٧﴾

"Na yale anayokupeni Mtume basi yachukuweni, na yale anayokukatazeni komeni (msiyafanye)." (Qur'an, 59:7).

Aya zote hizi zinajulisha wazi juu ya Isma (kuhifadhika) kwake Mtume(s.a.w.w) moja kwa moja katika kila kitu. Ama ninyi (Ahlus-Sunnah Waljamaa) mnasema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ni Maasum (amehifadhika) katika kufikisha Qur'an tu, na mambo mengine yeye ni kama watu wengine, anakosea na anapatia, na mnatolea ushahidi ili kuthibitisha kukosea kwa Mtume katika minasaba mbali mbali kwa hadithi mnazopokea ndani ya vitabu vyenu. Ikiwa hali ndiyo iko namna hii (kama mnavyodai) basi hoja yenu iko wapi na dalili yenu ni ipi kuhusu madai yenu ya kushikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake maadam Sunna hii kwenu ninyi haikuhifadhika na inawezekana kukawa na makosa ndani yake? Na kwa msingi huu basi, kushikamana na Kitabu na Sunna kwa mujibu wa itikadi zenu hakusalimiki kuwa na makosa, na hasa tutakapofahamu kwamba Qur'an yote imefasiriwa na kubainishwa na Sunna ya Mtume. Basi hoja yenu ni ipi inayothibitisha kuwa tafsiri yake (Mtume) na ubainishaji wake haukuwa umekwenda kinyume na kitabu cha Mwenyezi Mungu? Mmoja wa Masunni aliniambia alipokuwa akielezea maoni haya (akasema): "Bila shaka Mtume(s.a.w.w) alikhalifu hukumu nyingi zilizomo katika Qur'an kutegemeana na vile Maslahi yanavyopelekea."

Mimi nilisema katika hali ya kushangaa: "Nipe mfano mmoja juu ya yeye kuikhalifu Qur'an." Alijibu akasema: "Qur'an inasema:

الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا مِائَةَ جَلْدَةٍ ﴿٢﴾

Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume wapigeni kila mmoja wao mijeledi mia moja". (Qur'an, 24:2).

wakati ambapo Mtume aliwahukumu mzinifu mwanamume na mzinifu mwanamke wapigwe mawe jambo ambalo halimo ndani ya Qur'an." Mimi nilisema: "Bila shaka kupigwa mawe ni hukumu ya yule mwenye hifadhi (mwenye mke au mume) atakapozini awe mwanamume au mwanamke na mijeledi ni kwa mjane atapozini, awe mwanamke au mwanamume". Sunni yule akasema: "Ndani ya Qur'an haikutajwa mjane au aliyehifadhika, kwani Mwenyezi Mungu hakuhusisha (aina ya mzinifu) bali ametumia tamko mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume bila ya kuhusisha". Mimi nikasema: "Kwa hiyo kwa msingi huu basi kila hukumu ya moja kwa moja iliyomo katika Qur'an na Mtume akaihusisha hivi yeye Mtume atakuwa ameikhalifu Qur'an? Na kwa msingi huu ndiyo maana wewe unasema kuwa Mtume ameikhalifu Qur'an katika hukumu zake nyingi? Alijibu hali ya kuwa kachanganyikiwa: "Qur'an peke yake ndiyo imehifadhiwa kwa kuwa Mwenyezi Mungu amechukua jukumu la kuihifadhi, ama Mtume yeye ni mtu tu, anakosea na kupatia kama ambavyo Qur'an inasema juu ya stahiki yake, Waambie sikuwa mimi ila ni mtu mfano wenu ninyi." Nikasema: "Basi ni kwa nini tunaswali Asubuhi, Adhuhuri, Alasiri, Magharibi na I'sha, na hali ya kuwa Qur'an imetumia tamko Sala bila ya kuzihusisha nyakati zake?".

Alijibu: "Ndani ya Qur'an kuna (aya isemayo), Bila shaka sala imekuwa kwa waumini ni faradhi iliyowekewa wakati maalum. Na Mtume ndiye aliyebainisha nyakati za Sala." Nikasema: "Basi ni kwa nini unamsadiki katika (kubainisha) nyakati za sala na unampinga juu ya hukumu ya kumpiga mawe mzinifu?" Alijaribu kwa juhudi zake kunitosheleza kwa njia ya falsafa mbovu zinazopingana ambazo haziwezi kusimama kwenye dalili ya kiakili wala kimantik, kama pale aliposema: "Hatuwezi kuwa na mashaka juu ya Sala kwa sababu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alisali muda wote wa uhai wake tena kila siku mara tano, ama kumpiga mawe mzinifu hatuwezi kuwa na utulivu (wa nafsi) kwani hakufanya jambo hilo katika uhai wake isipokuwa mara moja au mara mbili." Na kama alivyosema (tena huyu Sunni) kwamba, "Mtume hakosei pale Mwenyezi Mungu anapomuamuru jambo fulani, ama wakati anapohukumu kwa fikra yake, basi yeye anakuwa hakuhifadhika kutokana na makosa, na kwa sababu hiyo basi Masahaba walikuwa wakimuuliza kila jambo kwa kumwambia, Je, jambo hilo linatoka kwake au ni linatoka kwa Mwenyezi Mungu, na pindi akiwaambia kuwa ni jambo lililotoka kwa Mwenyezi Mungu basi mara moja hulitekeleza bila ya kufanya mjadala. Ama akisema kuwa jambo hilo ni kutoka kwangu (yaani kwake Mtume), hapo humjadili na kumpa nasaha na yeye hukubali nasaha zao na maoni yao. Na wakati mwingine Qur'an hushuka kuafiki maoni ya baadhi ya Masahaba na kukhalifu maoni yake kama ilivyo katika qadhiya ya mateka wa Badri, na qadhiya nyinginezo mashuhuri".

Nilijaribu kwa kadiri ya uwezo wangu kumkinaisha lakini bila mafanikio, kwani wanachuoni wa Kisunni wanaamini hivyo (juu ya Isma) na vitabu vyao vimejaa maelezo kama haya yanayoifedhehesha Isma ya Mtume na kumfanya kuwa ni mtu mwenye kiwango cha chini kuliko mtu mwenye akili pevu au chini ya kiwango cha kamanda wa kiaskari au hata chini ya kiwango cha Sheikh wa Tariqa kwa masufi. Sintakuwa nazidisha nitakaposema kuwa wamemuweka Mtume(s.a.w.w) chini ya kiwango cha mtu wa kawaida, tutaposoma baadhi ya riwaya zilizomo ndani ya sihahi za Ahlus-Sunnah wal-Jamaa itatubainikia wazi ni kwa kiasi gani athari za Kibanu Umayyah zimekita mizizi yake katika akili za Waislamu tangu zama (walizotawala) na zimebakia mpaka nyakati zetu hizi.

Tukitafiti madhumuni na lengo la hayo, huenda tukatoa matokeo yasiyo na shaka na machungu, lakini kwa ufahamisho matukio yenyewe ni haya: Ni kwamba jamaa hao waliowatawala Waislamu katika zama za dola ya Bani Umayyah wakiongozwa na Muawiyyah ibn Abi Sufiyani hata siku moja hawakuamini kwamba Muhammad ibn Abdillah ni mjumbe aliyetumwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu au ni Nabii wa kweli wa Mwenyezi Mungu. Dhana yenye nguvu kwa (watu hao) walikuwa wakiitakidi kuwa yeye Mtume ni mchawi aliyewashinda watu na ameimarisha ufalme wake kwa msaada wa wanyonge miongoni mwa watu, na hasa hasa watumwa ambao waliutia nguvu wito wake na wakamsaidia. Hii siyo dhana tu kwani baadhi ya dhana ni dhambi, lakini tunaposoma ndani ya vitabu vya historia ili tupate kumfahamu Muawiya na mazingira yake, na yote aliyoyafanya muda wote wa uhai wake hasa muda wa utawala wake, basi inakuwa ni hakika (yaani ni kweli wala si dhana tena) hakuna njia ya kuikwepa. Sote tunafahamu kuwa Muawiya ni nani na baba yake Abu Sufiyan ni nani na mama yake (Muawiya) Hindu ni nani (katika historia yao dhidi ya Uislamu). Basi Muawiya ni muachwa huru mwana wa muachwa huru ambaye ujana wake aliumaliza akiwa chini ya malezi ya baba yake na (alikuwa) chini ya mafunzo ya majeshi yaliyoandaliwa kumshambulia Mtume na kuumaliza wito wake (ujumbe wa Uislamu) kwa juhudi zake zote mpaka mbinu zake zote ziliposhindwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu akamshinda (yeye Muawiya) na baba yake, akasalimu amri bila ya kuwa ni mwenye kuamini. Lakini Mtume(s.a.w.w) kwa ukarimu wake na utukufu wa tabia yake alimsamehe na akamwita kuwa ni muachwa huru. Na baada ya Mtume kufariki, baba yake Muawiyah (Abu Sufiyan) alijaribu kuzusha fitna ili aumalize kabisa Uislamu, hilo alilifanya pale alipomjia usiku Imam Ali(a.s) kumchochea afanye mapinduzi dhidi ya Abubakr na Omar na akawa anamtia tamaa ya mali na watu (wa kumsaidia), lakini Imam Ali(a.s) alifahamu makusudio yake akamfukuza. Hivyo basi (Abu Sufiyan) alibakia katika maisha ya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu katika uhai wake wote mpaka pale Ukhalifa ulipohamia kwa mtoto wa ami yake Bwana Uthman ibn Af-faan. Hapo ndipo alipodhihirisha yaliyokuwa (yamejificha) ndani ya nafsi yake ambayo ni ukafiri na unafiki akasema: "Enyi watoto wa Umayyah, udakeni (muung'ang'anieni) Ukhalifa kama udakwavyo mpira, amma hakika kwa yule ambaye Abu Sufiyan anamuapia, hakuna pepo wala moto." Ibn Asakir ameandika ndani ya kitabu chake juzuu ya sita ukurasa wa 407 kuwa, "Imepokewa kutoka kwa Anas kwamba, Abu Sufiyan aliingia kwa Uthman, baada ya kuwa amepofuka akasema: "Hivi hapa kuna yeyote (asiyekuwa miongoni mwetu Banu Umayyah)? Wakasema, Hapana, Abu Sufiyan akasema, "Ewe Mwenyezi Mungu lifanye jambo hili (la Uislamu) liwe ni jambo la kijahiliyyah, na Ufalme huu uwe ni Ufalme wenye kupokonywa, na uimarishe utawala wa Banu Umayyah."

Ama mwanawe Abu Sufiyan yaani Muawiyah, na huyo Muawiya ni nani? Simulia wazi wazi wala hakuna kosa (kumueleza Muawiya alivyo) na matendo yake aliyoyafanya dhidi ya ummati wa Muhammad(s.a.w.w) katika muda wote wa ugavana wake huko Shamu na baadaye alipoukalia Ukhalifa kwa nguvu na shinikizo, na mengineyo waliyoyataja wanahistoria ikiwa ni pamoja na (yeye Muawiyah) kuidhalilisha Qur'an na Sunnah na kuchupa kwake mipaka ambayo imewekwa na sheria. Hakika Muawiyah alitenda matendo ambayo kalamu inastahi kuyaandikia na ulimi nao unastahi kuyatamka kutokana na ubaya na uchafu wa matendo hayo. Kwa hakika tumeacha kuyataja (matendo yake) kwa kuzingatia hisia za ndugu zetu miongoni mwa Ahlus-Sunnah wal-Jamaa na wale ambao nyoyo zao zimeyeyushwa na mapenzi ya kumpenda Muawiyah na kumtetea mtu huyu. Lakini hapa hatujaacha kutaja undani wa mtu (huyu) na itikadi yake kumhusu Mtume(s.a.w.w) kwani itikadi yake haiko mbali na ile itikadi ya baba yake, na itikadi hiyo aliinyonya ndani ya maziwa ya mama yake aliyekuwa akiitwa Hindu mla maini (ya Sayyidna Hamza ibn Abdul-Mut-Talib) tena (Mama huyo) alikuwa mashuhuri kwa uzinifu na uchafu, kama ambavyo alivyoyarithi hayo toka kwa baba yake ambaye ni mkuu wa wanafiki ambaye Uislamu haukupata njia ya kuingia moyoni mwake. Na kama tulivyokwisha ufahamu undani wa baba yake, basi huyu hapa mwanawe naye anaeleza undani wake kwa maelezo yale yale lakini kwa njia yake (inayoonyesha) ujanja na unafiki.

Amepokea Zubair bin Bakar kutoka kwa Mutawaf bin Mughirah bin Shuuba At-Thaqafi amesema: "Niliingia mimi na baba yangu kwa Muawiyah, na baba yangu alikuwa akienda kwa (Muawiya) na kuzungumza kwake kisha huja akamtaja Muawiyah na akili yake na hupendezwa na mambo ayaonayo kwake. Basi usiku mmoja alikuja (kutoka kwa Muawiyah) akakataa kula chakula cha jioni, na nikamuona ni mwenye huzuni. Nikamsubiri kwa muda na nikahisi kuna jambo lililotokea juu yetu au katika kazi yetu nikamwambia, mbona nakuona ni mwenye huzuni tangu usiku ulipoingia?" Akasema: "Ewe Mwanangu, hakika nimetoka kwa mtu mbaya kuliko watu wote". Nikamwambia, "Ni nani huyo?" Akasema, "Nimemwambia Muawiyah na nilikua naye faragha ya kwamba, Hakika wewe umekwisha fikia lengo lako ewe Amriul-Muuminina, lau utaonesha uadilifu na ukaeneza wema, kwani wewe sasa hivi ni mtu mzima na lau utawaangalia nduguzo Bani Hashim, ukashirikiana vyema na kizazi chao, Wallahi leo hii hawana cho chote unachokiogopa toka kwao, na kwa kufanya hivyo kwako utabakia utajo (mwema) na thawabu zake."

Muawiyah akanijibu, "Haiwezekani kabisa, ni utajo gani ninaotarajia kuwa utabakia (baada yangu)? Alitawala ndugu wa kizazi cha Taim akafanya uadilifu na akatenda aliyoyatenda, lakini alipokufa basi na utajo wake nao ukafa, isipokuwa ikawa husema msemaji, Abubakr. Kisha alitawala ndugu wa kizazi cha Adiyyi, akajitahidi na kuimarika kwa miaka kumi, basi Wallahi alipokufa na utajo wake nao ukafa isipokuwa aseme msemaji, Umar. Hatimaye alitawala ndugu yetu Uthman, akawa ametawala mtu ambaye hakuwepo yeyote mwenye mfano katika nasaba yake, akatenda aliyoyatenda naye akatendewa, Wallahi alipokufa utajo wake nao ulikufa ikawa yanatajwa aliyofanyiwa. Lakini kwa hakika ndugu wa kizazi cha Hashim anapigiwa makelele kila siku mara tano (katika adhana) Ash-hadu Anna Muhammadan Rasulullah. Sasa basi, ni tendo gani na ni utajo gani utakaobakia sambamba na utajo huu? Koma (kunishauri jambo kama hilo) na Wallahi (hakuna kingine kitakachobaki) isipokuwa kuwaangamiza tu." Umepata hasara na umefedheheka ewe muovu uliyetaka kuuangamiza utajo wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa juhudi zako zote,lakini juhudi zako zimeshindwa kwa sababu Mwenyezi Mungu anakufuatia nyendo zako na ni yeye aliyesema: "Na tumeutukuza utajo wako". Basi kamwe wewe si mwenye uwezo wa kuufuta utajo wake ambao Mwenyezi Mungu ameutukuza, Mola mwenye nguvu na utukufu, basi fanya vitimbi vyako na uwakusanye jamaa zako, wewe huna uwezo wa kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa mdomo wako na Mwenyezi Mungu ataikamilisha nuru yake licha ya chuki za unafiki wako, uliimiliki nchi mashariki mpaka magharibi na wakati ulipokufa na utajo wako nao ukafa ila akutaje mwenye kukutaja kwa matendo yako maovu ambayo kwayo ulitaka kuubomoa Uislamu kama yalivyokuja hayo kupitia kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) . Na umebakia utajo wa Muhammad ibn Abdillah ndugu wa (kizazi cha) Hashim kwa karne na zama zote mpaka hapo Mwenyezi Mungu atakapoiondosha ardhi na vilivyoko juu yake. Na kila amtajapo Mtume (yeyote) mwenye kumtaja humsalia yeye na kizazi chake licha ya chuki zako na chuki za Banu Umayyah ambao walijaribu kwa kuongozwa na wewe kukiangamiza kizazi cha Hashim na utukufu wao, basi (njama hizo) hazikuwaongezea isipokuwa utukufu na utajo mwema. Amma ninyi (enyi Banu Umayyah) mtakutana na Mwenyezi Mungu siku ya Qiyama hali ya kuwa amekukasirikieni kwa yale mliyoyazusha ndani ya sheria yake na atakulipeni mnachostahiki.

Tukiongeza juu ya hawa (tuliokwisha wataja) ni mtoto wao Yazid ibn Muawiyah asiye na haya, muovu mnywa pombe na anayedhihirisha ufasiqi na uovu wazi wazi, basi yeye tunamkuta ndiye wa mwisho aliyebeba itikadi ile ile ambayo ameirithi kwa baba yake Muawiyah na babu yake Abu Sufiya, kama ambavyo amerithi kutoka kwao ukatili na uovu na kunywa pombe na kutopea katika uzinifu na kucheza kamari. Na lau hata asingekuwa na sifa zote hizi mbaya, Muawiya hakustahiki kumrithisha (Yazid) Ukhalifa na kumtawalisha juu ya shingo za Waislamu, na hali ya kuwa wote wanamfahamu fika. Muawiyah alifanya hayo hali ya kuwa (akijua) miongoni mwa Waislamu walikuwemo masahaba watukufu kama vile Hussein ibn Ali Bwana wa vijana wa peponi. Na hapana shaka kwamba Muawiyah alimaliza muda wa uhai wake (katika) kutoa mali yake ambayo aliipata kwa njia za haramu ili auangamize Uislamu na Waislamu wa kweli. Bila shaka tumekwisha ona ni jinsi gani alikuwa akitaka kuufuta utajo wa Muhammad(s.a.w.w) na hilo hakuweza ndipo alipowasha moto wa vita dhidi ya Imam Ali ambaye ni ibn ammi ya Mtume na ni wasii wake mpaka akamuua na akaushika Ukhalifa kwa nguvu, udanganyifu na unafiki. Aliweka Sunna yake chafu na akawaamuru wawakilishi wake katika kila nchi wamlaani Ali(a.s) pamoja na watu wa nyumba ya Mtume(s.a.w.w) kwenye mimbari na ndani ya kila Sala.Kwa kufanya hivyo (bila shaka) alikuwa akikusudia kumlaani Mtume wa Mwenyezi Mungu, na hila zake ziliposhindwa alikufa bila kulitimiza lengo lake isipokuwa alimuweka mwanawe na akamtawalisha juu ya Ummah ili aendeleze malengo yake aliyoyaweka yeye Muawiyah na baba yake Abu Sufiyan. Ni malengo gani hayo? Hapana kingine bali ni kuuangamiza Uislamu na kurudisha mambo kwenye zama za ujinga.

Yazid muovu asiye na haya aliukumbatia Ukhalifa na akaziimarisha nguvu zake kwa ajili ya kuuangamiza Uislamu kama yalivyokuwa mapenzi ya baba yake. Hivyo basi alianza kwa kulihalalishia jeshi lake kuuvamia mji wa Mtume(s.a.w.w) , jeshi lake la kikafiri likafanya lilivyofanya, na kwa muda wa siku tatu yalifanyika mauaji makubwa kwa maelfu ya Masahaba wema na baada ya hapo alifuatishia kumuua Bwana wa vijana wa peponi na kiliwazo cha Mtume(s.a.w.w) na watu wote wa nyumba ya Mtume ambao ndiyo nuru ya ummahma akawateka wanawake watukufu wa nyumba ya Mtume. "Hakika sisi ni Milki ya Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea." Na lau Mwenyezi Mungu asingempunguza umri wake, angeumaliza Uislamu na Waislamu. Jambo muhimu (tunalolikusudia) katika utafiti huu ni kuidhihirisha wazi itikadi ya Yazid kama tulivyoidhihirisha wazi itikadi ya baba yake na babu yake.

Wanahistoria wamesimulia kwamba, baada ya tukio baya la kuuvamia mji wa Madina na kuwauwa Waislamu wema elfu kumi isipokuwa wanawake na watoto, na (katika tukio hilo) bikra za kiasi cha wasichana elfu moja ziliharibiwa na wanawake wapatao elfu moja walishika mimba bila ya kuwa na waume. Kisha watu waliobakia walifanya Baiah wakiwa ni watumwa wa Yazid na aliyekataa aliuawa. Yazid zilipomfikia habari za maovu hayo ambayo yanamfanya mtu alie (kwa uchungu) na wala historia haijapata kuyashuhudia ambapo hata Wamongolia na Watataar... na Waisraeli (hawajapata kutenda hayo), Yazid alifurahi na akaonesha kufurahia msiba uliompata Mtume wa Uislamu na ndipo aliposema kauli ya Ibn Az-Zub-ari, kauli ambayo aliisema baada ya tukio la Uhd akasema: "Laiti wazee wangu (waliouawa) siku ya Badri wangeshuhudia khofu (iliyowapata) Khaz-Raji kutokana na tukio la vita, basi wangejitokeza wakafurahi, kisha wangesema, Ewe Yazid usihuzunike, bila shaka tumemuuwa Bwana Mtukufu miongoni mwa watukufu wao na tumelipa kisasi cha Badri na tumelingana".Aliendelea akasema, "Iwapo sintaacha kuwaadhibu kizazi cha Ahmad (Muhammad) kwa yale yaliyotendeka (hapo kabla). Bani Hashim walicheza (mchezo wa) Ufalme, hakuna habari yoyote iliyokuja wala hapakushuka Wahyi."

Basi ikiwa babu wa Yazid (Abu Sufiyan) ambaye ndiye adui wa kwanza wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake anasema wazi wazi kwamba, "Udakeni (Ukhalifa) enyi Banu Umayyah kama udakwavyo mpira, basi kwa yule ambaye Abu Sufiyan anamuapia. hakuna pepo wala moto." Na iwapo baba wa Yazid (Muawiyah) ambaye ni adui wa pili wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake (naye) anasema wazi wazi (pale anapomsikia Muadhini anashuhudia kwamba Muhammad ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu) yeye aseme "Ni utajo gani utakaobakia (kwangu) sambamba na (utajo) huu, basi koma Wallahi nitaendelea kuwaangamiza tu." Kama mtoto (wao) Yazid ambaye ni adui wa tatu wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake naye anasema wazi wazi kwamba "Banu Hashim walicheza (mchezo wa) Ufalme, hakuna habari iliyokuja wala Wahyi ulioshuka." Nasi tunapokuwa tumezifahamu itikadi za watu hawa juu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na (itikadi zao) juu ya Uislamu, na tukawa tumefahamu matendo yao maovu ambayo kwayo walitaka kubomoa nguzo za Uislamu na kumchafua Mtume wa Uislamu. Isitoshe hali hiyo, bali matendo mengine tumeacha kuyataja kwa nia ya kufupisha maelezo, kwani lau tungetaka kupanua zaidi tungejaza mkusanyiko mkubwa (wa kitabu) kinachohusu matendo ya Muawiyah peke yake ambayo yamebakia kuwa ni aibu na fedheha kwake wakati wote japokuwa walijaribu kuyaficha. Baadhi ya wanachuoni waovu ambao walikuwa wakikirimiwa na Banu Umayyah, macho yao yalipofuka wakaiuza akhera yao kwa thamani ya dunia yao, na haki wakaifunika kwa batili hali yakuwa wanafahamu na Waislamu wengi walibakia kuwa mateka wa uovu huu na uzushi huu. Na lau mateka hawa wangefahamu ukweli kabisa wasingemtaja Abu Sufiyan na Muawiyah na Yazid isipokuwa kwa kuwalaani na kujitenga nao. Lakini jambo muhimu katika utafiti huu mfupi ni kufikia kwenye kiwango cha namna zilivyo athari za watu hawa (Banu Umayyah) na wafuasi wao na vipenzi vyao (katika kuuvuruga Uislamu), ambao waliwatawala Waislamu kwa muda wa miaka mia moja Hapana shaka kwamba athari ya wanafiki hawa ilikuwa kubwa kwa Waislamu, kwani waliwageuza itikadi zao, mienendo yao, tabia zao na mahusiano yao mpaka ibada zao, kiasi kwamba ni namna gani tutaweza kueleza ni jinsi gani umma wa Kiislamu uliacha kuitetea haki na kuwafanyia uhaini Mawalii wa Mwenyezi Mungu na (kinyume chake ikawa ni) kusimama pamoja na maadui wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake(s.a.w.w) .

Ni jinsi gani tutaweza kueleza namna Muawiya aliyeachwa huru, mtoto wa muachwa huru na mwenye kulaaniwa mtoto wa aliyelaaniwa alivyoweza kuufikia Ukhalifa ambao unawakilisha cheo na Ukhalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , tutawezaje kulieleza hili wakati wanahistoria wanatupotosha eti kwamba watu walikuwa wakimwambia Omar ibn Khatab, "Lau tungekuona unapotoka tungekurekebisha kwa panga zetu." Ni wanahistoria hao hao ndiyo wanaotueleza habari za Muawiyah aliyetwaa cheo cha Ukhalifa kwa nguvu na mabavu, na hotuba yake ya kwanza anayoisema mbele ya Masahaba wote kama ifuatavyo; "Bila shaka mimi sikuwapigeni eti kwa ajili mswali wala kwa ajili mfunge, lakini (nimekupigeni) ili niwatawaleni na sasa mimi huyu hapa ni mtawala wenu."

Hakuna (Sahaba) yeyote miongoni mwao anayejaribu kutingishika wametulia tulii, wala hapana aliyempinga (Muawiyah kwa kauli hiyo) bali anatamba kiasi kwamba wanahistoria wanauita mwaka huo aliotawala Muawiya kuwa ni mwaka wa umoja, na kwa kusema kweli huo ulikuwa ndiyo mwaka wa kusambaratika kwa Waislamu. Kisha tunawaona Masahaba baada ya hayo (aliyowatendea Muawiya) wanakubali awatawalishie mwanawe muovu Yazid ambaye anafahamika kwao wote, hawakupinga wala kujitetea isipokuwa wachache ambao Yazid aliwauwa katika tukio la uvamizi wa Madina na akachukua baia kwa wale waliobakai (tena kwa nguvu) akawafanya kuwa watumwa wake. Basi ni jinsi gani tutayaeleza yote hayo, kwani tunachokikuta baada ya hayo ni kwamba waovu wa kibanu Umayyah kama Marwan ibn Al-Hakam na Walid ibn Uqbah na wengineo waliutwaa Ukhalifa kwa niaba ya kuwaongoza waumini. Kwa kupitia viongozi wa aina hiyo mambo yaliharibika yakafikia hatua ya kuushambulia mji wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na wakatenda mjini humo matendo machafu, na vitu vitakatifu vikavunjiwa heshima zake, (kama hayo hayakutosha) bali waliiunguza nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu (Al-Kaaba) na waliwauwa ndani ya Haram hiyo Masahaba wema. Kwa amri ya hao (waitwao kuwa) viongozi wa waumini mambo yalifikia hata kuimwaga damu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu pale walipomuuwa kiliwazo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) Husein ibn Ali(a.s) na kizazi chake na wakawateka mabinti zake, (basi kwa yote hayo) hakuna yeyote aliyeshituka miongoni mwa watu wa umma wa Kiislamu wametulia na wala Bwana wa vijana wa peponi Imam Husein(a.s) hakupata wa kumtetea.

Na kwa hao waliojiita viongozi wa waumini walifikia hatua ya kukichana kitabu cha Mwenyezi Mungu na kisha wakakiambia, "Utakapokutana na Mola wako siku ya ufufuo mwambie ewe Mola wangu Walid alinichanachana." Tendo hili alilitenda Walid wa ukoo wa Banu Umayyah. Mambo hayakuishia kupitia kwao hao viongozi wa waumini, bali walimlaani Ali ibn Abi Talib juu ya minbari na wakawaamuru watu wamlaani katika kila nchi, na hali hakuna wanachokikusudia kwa tendo hilo isipokuwa kumlaani Mtume wa Mwenyezi Mungu, wakati yote haya yanatendeka watu walitulia kimya hakuna aliyeshtuka miongoni mwao, na aliyekataa kumlaani Ali(a.s) aliuawa, akasulubiwa na kuteswa kama onyo kwa wengine. Mambo yalifikia kwa viongozi hao wa waumini kunywa pombe hadharani na kuzini, kufanya mambo ya upuuzi, kuimba na kucheza n.k Basi ikiwa mambo ya umma wa Waislamu yalifikia kiwango kama hiki cha kuporomoka katika maadili yao na udhalili kama huu, basi hapana budi kuna mambo ambayo yaliathiri itikadi yao, na hili ndilo jambo muhimu katika utafiti huu kwani linafungamana na maudhui ya Ismah na heshima ya Mtume Mtukufu(s.a.w.w) . Jambo la kwanza linalotufanya tuwe waangalifu hapa ni kwamba, Makhalifa watatu Abubakr, Umar na Uthman walizuwia hadithi za Mtume(s.a.w.w) zisiandikwe wala kusimuliwa.

Basi huyu hapa Abubakr anawakusanya watu na anawaambia, "Hakika ninyi mnasimulia hadithi toka kwa Mtume(s.a.w.w) ambazo ndani yake mnatofautiana, na watu watakaokuja baada yenu watahitilafiana mno. Hivyo basi msisimulie cho chote toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, na yeyote atakaye kuulizeni mwambieni kuwa baina yetu kuna Kitabu cha Mwenyezi Mungu, ihalalisheni halali yake na muiharamishe haramu yake." Kama alivyofanya Abubakr, Umar bin Khatab naye aliwazuwiya watu wasisimulie hadithi za Mtume(s.a.w.w) . Qur-Zatu ibn Kaab anasema: "Umar bin Khatab alipotutuma kwenda Iraq alitushindikiza na akatuambia; Je, mnafahamu ni kwa nini nimekushindikizeni? Wakasema, bila shaka kwa kutuheshimu tu. Umar akasema: Pamoja na hilo, bila shaka ninyi mtawafikia watu wa kijiji (fulani) wanao mvumo kwa kusoma Qur'an kama mvumo wa nyuki, basi msiwazuwiye kwa hadithi mtawashughulisha isomeni Qur'an na mpunguze maelezo ya hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu, nami niko pamoja nanyi." Mpokeaji wa hadithi hii anasema: "Basi sikunakili hadithi yoyote kamwe baada ya maneno ya Umar." Alipofika Iraq watu walimkimbilia wakimuuliza juu ya hadithi (za Mtume), Qur-zah akawaambia, "Umar alitukataza kufanya hivyo." Kama ambavyo Abdur-Rahman ibn Auf alisema kwamba, "Umar bin Khatab aliwakusanya masahaba toka sehemu mbali mbali kwa ajili ya kuwazuwia kuzizungumza hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa watu na akawaambia, "Bakieni hapa kwangu na wala msiachane nami muda wote wa uhai wangu." Masahaba hao hawakuondoka mpaka alipokufa. Vile vile amelieleza jambo hili Al-khatib Al-bagh-dadi na Addhahabi ndani ya Tadh-kiratul-hufadh kwamba Umar ibn Khatab aliwafunga jela Masahaba watatu hapo Madina nao ni, Abud-dir-dai na ibn Mas-ud na Abu Masud Al-ansari kwa kosa la kunakili kwa wingi hadithi (za Mtumes.a.w.w ). Pia Umar aliwaamuru Masahaba wamletee kila kitabu kilichomo mikononi mwao miongoni mwa vitabu vya hadithi, basi wao wakadhani kwamba yeye anataka kuvisahihisha viwe katika hali ambayo hapatakuwa na tofauti ndani yake, wakamletea vitabu vyao yeye akavichoma moto vyote. Kisha baada yake alikuja Uthman akaiunganisha sera yao kwa kuwatangazia watu wote kwamba "Si halali kwa mtu yeyote kueleza hadithi ambayo hakuisikia katika zama za Abubakr wala katika zama za Umar!!"

Baadaye ilifika zamu ya Muawiyah ibn Abi Sufiyan alipokalia cheo cha Ukhalifa, akapanda kwenye mimbar akasema, "Enyi watu ole wenu kusimulia hadithi toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , msisimulie isipokuwa zile hadithi zilizotajwa katika zama za Umar." Kwa hiyo basi hapana budi kwamba kuna siri ya kuzuwia hadithi alizozisema Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) (hasa) zile ambazo hazikubaliani na malengo ya zama hizo (za watawala hao), vinginevyo basi ni kwa nini hadithi za Mtume ziendelee kuzuwiwa kuandikwa kwa muda huu mrefu na isipatikane ruhusa ya kuziandika mpaka zama za Umar ibn Abdil-Aziz (r.a) ndipo ilipopatikana ruhusa ya kuziandika. Kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia kutokana na uchunguzi kuhusu maelezo halisi yaliyo bayana juu ya Ukhalifa, ambayo Mtume(s.a.w.w) aliyatangaza mbele ya ushuhuda wa watu wengi tunapata matokeo yanayomaanisha kwamba, Abubakr na Umar -walizuwia mapokezi ya hadithi kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) kwa kuhofia kusambaa kwa maelezo hayo (ya Mtume kuhusu Ukhalifa) katika miji au katika vijiji vya jirani na yangewadhihirishia ukweli huo. Hapo kabla tumekwisha zungumza katika maudhui haya na tumeuweka wazi ukweli huu ndani ya kitabu chetu Liakuna Maas-Sadiqin, basi na arejee (kitabu hicho atakaye) ili kuong,eza uthibitisho.

La kushangaza miongoni mwa mambo ya Umar ibn Al-Khatab ni ile misimamo yake inayopingana hasa katika kila jambo linalohusiana na suala la Ukhalifa. Kuna wakati tunamkuta yeye ndiye aliyeisimamia baia ya Abubakar na akawalazimisha watu wautii (Ukhalifa huo) kwa nguvu, na akauhukumu kuwa eti ulitimia pasipo kutegemea bali Mwenyezi Mungu aliikinga shari yake. Wakati mwingine (tunamkuta Umar) anateua watu sita kwa ajili ya Ukhalifa anasema, "Lau watamtawalisha Alah (akiwa na maana ya Ali ibn Abi Talib) basi atawaongoza kwenye njia ya sawa." Basi maadam (Umar) anakiri kwamba Ali ndiye mtu pekee ambaye atawapeleka watu kwenye haki, basi ni kwa nini hakumbainisha wazi wazi na mambo yakamilike na kwa ajili hiyo awe ametoa mchango mzuri kwa umma wa Muhammad? Lakini kinyume chake, tunamuona anajichanganya na kukipa uwezo mkono wa Abdur-rahman anaposema, "Lau Salim aliyeachwa huru na Abu Hudhaifah angekuwa hai ningemtawalisha juu yenu." Na la kushangaza zaidi kuliko yote katika mambo ya Abu Hafsah (Umar) ni kule kuzuwia kwake kuzungumzwa hadithi za Mtume(s.a.w.w) na kuwafunga Masahaba hapo Madina kwa kuwazuwia wasitoke nje ya mji huo, na pia kuwakataza wajumbe watokao kwake kwenda miji mingine wasiwazungumzie watu sunna ya Mtume, na (miongoni mwa aliyoyatenda) ni kuvichoma moto vitabu vilivyokuwa mikononi mwa Masahaba ambavyo vinazungumzia hadithi za Mtume(s.a.w.w) .

Je, Umar ibn Khatab hakufahamu kwamba Sunna ya Mtume ndiyo inayobainisha Qur'an Tukufu? Je, hakusoma kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema:

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ ﴿٤٤﴾

"Na tumekuteremshia wewe ukumbusho (Qur'an) ili uwabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwao." (Qur'an, 16:44).

Au (yeye Umar) alifahamu yaliyomo ndani ya Qur'an ambayo, Mtume(s.a.w.w) aliyeteremshiwa hiyo Qur'an hakuyafahamu? Mambo kama haya ndiyo wayatakayo watu waliochanganyikiwa ambao wanasema kwamba eti Qur'an mara nyingi ilikuwa ikishuka kuunga mkono maoni ya Umar, na iliyapinga maoni ya Mtume(s.a.w.w) . "Ni maneno mabaya yatokayo vinywani mwao, bila shaka hawana wanachokijua." Siku zote nilikuwa nikishangaa nisomapo ndani ya Bukhari juu ya upinzani wa Umar kutokubali riwaya za Ammar ibn Yasir hasa hasa ile ya mafunzo ya Mtume kwake (Ammar) juu ya nama ya kutayammamu. Kama ambavyo ninashangaa kutokana na kauli ya Ammar kwa kumuogopa Umar anasema, "Ukitaka sitaisimulia hadithi hiyo." Basi inabainika wazi kwamba Umar alikuwa mkali dhidi ya kila anayesimulia hadithi za Mtume na humtaabisha. Ikiwa Masahaba miongoni mwa Maquraishi wanamuogopa Khalifa huyo, kiasi kwamba hawatoki nje ya Madina na wakitoka hawanakili (na kusimulia) hadithi za Mtume, kisha Khalifa huyo anavichoma vitabu vyao ambavyo ndani yake walikusanya hadithi (za Mtume) na pasiwepo mtu hata mmoja wa kusema kitu (kutokana na tendo hilo), basi Ammar ibn Yasir ana thamani gani? Ni mgeni, mtoka mbali, na alikuwa akichukiza mbele ya Maquraishi kwa kusimama kwake pamoja na Ali ibn Abi Talib na kumpenda kwake Ali ibn Abi Talib (a.s) ?

Tunaporudi kidogo kwenye uchunguzi (wa Mas-ala yanayostaabisha), na hasa ile siku ya Al-Khamisi ambayo ilikuwa kabla ya kufariki kwa Mtume(s.a.w.w) na siku hiyo ndiyo ile ambayo Ibn Abbas ameiita kuwa ni "Siku ya Msiba". Ameiita hivyo kwa sababu, wakati Mtume(s.a.w.w) alipowaamuru waliokuwepo mbele yake wamletee karatasi na kidau cha wino ili awaandikie maandiko ambayo kwayo kamwe hawatapotea, tunaona katika siku hiyo Umar ibn Khatab ndiye aliyempinga Mtume(s.a.w.w) na kumtuhumu kwamba "Anaweweseka" Mungu apishe mbali. Na akasema yeye Umar "Kinatutosha kitabu cha Mwenyezi Mungu." Tukio hili ameliandika Bukhari na Muslim, ibn Majah, An-Nasai, Abu Dawud na Imam Ahmad na wengineo miongoni mwa wana historia wengi. Sasa basi, iwapo Umar anathubutu kumzuwiya Mtume wa Mwenyezi Mungu asiandike hadithi zake mbele ya watu wengi wakiwemo Masahaba na watu wa nyumba ya Mtume na kumtuhumu kuwa anaweweseka, na kisha (kuonesha) ushupavu huo ambao historia haijapata kutambua mfano wake, basi hiyo haishangazi na wala siyo ajabu kwa Umar ibn Khatab kuendelea tena kwa nguvu baada ya kufariki Mtume(s.a.w.w) kuwazuwiya watu kunakili hadithi za Mtume(s.a.w.w) kwa juhudi zake zote hali ya kuwa ni Khalifa mwenye nguvu na anamiliki uwezo, na hapana shaka kwamba alikuwa nao wasaidizi miongoni mwa Masahaba wengi ambao wanao uwezo katika makabila na jamaa wa kutosha, na ni katika wale ambao walimfuata Mtume kwa sababu ya tamaa au khofu au unafiki, tumekwisha waona hawa kutokana na wingi wao wanaunga mkono ile kauli ya Umar eti kwamba Mtume anaweweseka, walishiriki kumzuia Mtume(s.a.w.w) kuandika maandiko yake.

Mimi naamini kwamba hiyo ndiyo iliyokuwa sababu ya msingi kwa Mtume kunyamaza asiandike maandiko hayo kwani yeye alifahamu kwa kupitia Wahyi kutoka kwa Mola wake kwamba, kuna njama zenye nguvu na huenda zitatishia ukamilifu wa malengo ya Uislamu iwapo maandiko hayo yataandikwa. Maandiko hayo aliyotaka kuyaandika Mtume(s.a.w.w) yalikuwa na lengo la kuulinda Umma wake usiingie katika upotevu, lakini kumbe walikuwepo wenye njama (dhidi yake) wakageuza lengo (lililokusudiwa) na ikawa kama kwamba maandiko hayo yakiandikwa itakuwa ni sababu ya kupotea na kuacha Uislamu. Basi ni kwa nini Mtume wa Mwenyezi Mungu asibadilishe (hivyo alivyotaka kuandika yaani akaacha kuandika) na wakati yeye yuko katika hali hiyo ya maradhi juu ya kitanda cha mauti (akaacha kuandika) kutokana na Wahyi toka kwa Mola wake, Wahyi ambao unasikika katika masikio yake, na kuujaza moyo wake masikitiko na huzuni juu ya Umma wake ambao umefikwa na kauli yake (Mwenyezi Mungu). "Basi ikiwa (Muhammad) atakufa au atauawa mtarudi nyuma kwa visigino vyenu?" Hii aya haikushuka bure bure tu bali ni matokeo ya kweli ambayo Mwenyezi Mungu alikwishafahamu uovu wao na magenge yao na vitimbi vyao. Mwenyezi Mungu yeye ndiye anayefahamu hiana ya macho na yale yaliyojificha katika nyoyo............... Bali Mwenyezi Mungu amemwambia Mtume wake toka hapo mwanzo kama ifuatavyo:

وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ يَقُولُ يَا لَيْتَنِي اتَّخَذْتُ مَعَ الرَّسُولِ سَبِيلًا ﴿٢٧﴾ يَا وَيْلَتَىٰ لَيْتَنِي لَمْ أَتَّخِذْ فُلَانًا خَلِيلًا ﴿٢٨﴾ لَّقَدْ أَضَلَّنِي عَنِ الذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَاءَنِي وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِلْإِنسَانِ خَذُولًا ﴿٢٩﴾ وَقَالَ الرَّسُولُ يَا رَبِّ إِنَّ قَوْمِي اتَّخَذُوا هَـٰذَا الْقُرْآنَ مَهْجُورًا ﴿٣٠﴾ وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا مِّنَ الْمُجْرِمِينَ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ هَادِيًا وَنَصِيرًا ﴿٣١﴾

"Na siku ambayo dhalimu atajiuma mikono yake na huku anasema; Laiti ningelishika njia pamoja na Mtume, Ee Mola wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki, amenipoteza nikaacha ukumbusho baada ya kunifikia na kweli shetani ni mwenye hiana kwa mwanadamu. Na Mtume alikuwa akisema: Ewe Mola wangu! hakika watu wangu wameifanya hii Qur'ani ni kitu kilichohamwa, na vivi hivi tumemfanyia kila Nabii adui miongoni mwa waovu na Mola wako mlezi anatosha kuwa mwenye kuongoa na mwenye kunusuru." (Qur'an, 25, 27-31).

Jambo ambalo hatuwezi kulikwepa katika uchunguzi huu ni hayo matokeo yenye uchungu tuliyoyafikia, nayo ni kwamba Abu Sufiyani na Muawiyah wasingekuwa wajeuri dhidi ya Mtume(s.a.w.w) lau si msimamo wa Umari wa kijeuri aliokuwa akiufanya mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu hasa tunapouchunguza mwenendo wake muda wote wa uhai wa Mtume(s.a.w.w) na upinzani wake aliokuwa akiuonesha katika matukio mbali mbali. Kwa hali hii hatuna budi kupata matokeo yanayomaanisha kwamba, kulikuwa na njama kubwa zilizoandaliwa ili kuudhalilisha utu wa Mtume Mtukufu na kumtia doa, pia kumfanya aonekane mbele ya watu wasiomfahamu kwamba yeye ni mtu wa kawaida tu au chini kuliko hapo na kwamba yeye wakati mwingine anatawaliwa na ubinafsi na matamanio yake yanampotosha na kumtoa kwenye haki. Yote hayo lengo lake ni kuwapotosha watu wamuone kwamba yeye siyo Maasumu (yani hakuhifadhika kutokana na madhambi).

Dalili ya hilo ni kwamba Umar amempinga Mtume mara nyingi na eti Qur'ani ikaja kumuunga mkono Umar mpaka ikafikia Mwenyezi Mungu kumkemea Mtume wake naye Mtume akalia na kusema:"Lau Mwenyezi Mungu angelituteremshia maangamizo basi asingeokoka kutokana na maangamizo hayo isipokuwa mwana wa Khatab (yaani Umar) Tukio hili linahusu mateka wa Badri. Au kama isemwavyo kwamba, Umar alikuwa akimwamuru Mtume wa Mwenyezi Mungu kuwaweka wake zake kwenye hijabu, wakati Mtume alikuwa hafanyi hivyo mpaka Qur'an ikamuunga mkono Umar na kumwamrisha Mtume wa Mwenyezi Mungu awaweke wake zake kwenye hijab. Au kama isemwavyo kwamba shetani hakumuogopa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu lakini alimwogopa Umar na kumkimbia na mengineyo miongoni mwa riwaya potofu zinazoangusha heshima ya Mtume(s.a.w.w) na kupandisha juu heshima ya Masahaba. Kwa hakika Umar alifanikiwa mno katika lengo lake hili mpaka watu wamesimulia (Mwenyezi Mungu awafedheheshe watu hao) Eti wanasema kwamba; mjumbe wa Mwenyezi Mungu alikuwa akiutilia mashaka utume wake na hilo limo ndani ya hadithi wanayoisimulia isemayo kuwa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amesema: "Jibril alikawia kuja kwangu mpaka nikadhani kwamba yeye sasa atashuka kwa Umar bin Khatab. "

Mimi naamini kwamba hadithi kama hizi na nyingine mfano wa hizi, ziliwekwa katika zama za Muawiyah ibn Abu Sufiyan aliposhindwa kufuta ukweli unaomhusu (fadhila za) Ali ibn Abi Talib akaona azushe fadhila za Abubakr, Umar na Othman ili anyanyue zaidi daraja zao mbele ya macho ya watu kuliko daraja ya Ali, na alilifanya hilo kwa malengo mawili:

1) Ni kuirudisha chini heshima ya Ali ibn Abi Talib (Abu Turab) kama alivyomwita yeye ili kuwapotosha watu na kuwafanya Makhalifa watatu waliomtangulia kuwa wao ni bora zaidi kuliko yeye.

Lengo la pili la kuzua kwake hadithi ilikuwa ni kuwafanya watu wakubali kinyume na maamrisho ya mjumbe wa Mwenyezi Mungu na usia wake unaohusu suala la Ukhalifa ambao ni haki ya watu wa nyumba ya Mtume, hususan Hassan na Husein ambao waliishi katika kipindi cha Muawiyah. Basi ilipokuwa imewezekana kwa Makhalifa watatu wa mwanzo kwenda kinyume na maamrisho ya Mtume kuhusu (ukhalifa wa) Ali je, ni kwa nini isiwezekane Muawiyah ambaye ni wanne wao naye asiweze kwenda kinyume na maamrisho ya Mtume juu ya watoto wa Ali? Kwa hakika mwana wa Hindu (Muawiyah) amefanikiwa sana katika mipango yake, na dalili (ya mafanikio yake) ni kuwa leo hii sisi tunapozungumzia elimu ya Ali(a.s) na ushujaa wake na udugu alionao kwa Mtume na ubora na fadhila zake kwa Uislamu na Waislamu, basi mbele yetu husimama mtu ambaye husema, "Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema, Lau itapimwa imani ya umma wangu kulinganisha na imani ya Abubakr basi imani ya Abubakr itakuwa nzito." Na mwingine naye atatuambia, "Umar Al-Faruq ndiye aliyetenganisha baina ya haki na batili". Na mwingine naye atasimama mbele na kutuambia, "Uthman Dhun-Nurain ndiye ambaye Malaika wa Mwenyezi Mungu walimstahi."

Yeyote mwenye kufuatilia uchunguzi huu atakuta kwamba, Umar ibn Al-Khatab amechukua nafasi ya simba katika mlango wa ubora, na hayo hayakuja ghafla bali ni kutokana na misimamo yake ya upinzani wa mara kwa mara dhidi ya Mtume(s.a.w.w) . Maquraish walimpenda na hasa kwa mchezo alioucheza katika kumtweza Amirul-Muuminina na Bwana wa Mawasii Ali ibn Abi Talib kwa kumnyang'anya Ukhalifa, na kuwapa Maqureish walitolee uamuzi vile wapendavyo kiasi cha kupupiwa na waachwa huru na waliolaniwa miongoni mwa Bani Umayyah, na hapana shaka Maquraish wote wakiongozwa na Abubakr wanafahamu kwamba shukurani zote zinarejea kwa Umar katika kuwatawalisha wao juu ya Waislamu. Hivyo basi Umar ndiye shujaa wa upinzani dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na ndiye aliyemzuwia Mtume wa Mwenyezi Mungu asimuandikie Ali usia wa Ukhalifa, na ni yeye aliyewakemea watu na kuwatia shaka juu ya kifo cha Mtume wao ili wasije kumtangulia kwa kumpa baia Ali. Si hivyo tu bali Umar ndiye shujaa wa Saqifa aliyethibitisha baia ya Abubakr na huyo huyo Umar aliyewaonya wale waliopinga (Baia ya Abubakr) na wakajizuwia ndani ya nyumba ya Ali (akawaonya) kwa kwaambia kwamba, "Ataiunguza nyumba hiyo na waliomo ndani, ikiwa tu hawatatoka kwenda kula kiapo cha utii kwa Abubakr". Ni yeye pia aliyewalazimisha watu wampe baia Abubakr kwa nguvu na shinikizo, na ndiye ambaye alikuwa akiteua magavana na kuwapa vyeo wakati wa Ukhalifa wa Abubakr, bali hatutakuwa tumetia chumvi tutakaposema kwamba yeye ndiye alikuwa mtawala mtendaji hata katika Ukhalifa wa Abubakr mwenyewe. Wanahistoria wamesimulia kwamba, wenye kuimarishwa imani zao katika dini (Muallafatul-Qulubi) walipomjia Abubakar ili wachukue sehemu yao ambayo Mwenyezi Mungu ameifaradhisha kwa ajili yao kufuatana na mazowea waliyokuwa nayo wakati wa Mtume(s.a.w.w) , Abubakar aliwaandikia barua juu ya jambo hilo wakaenda kwa Umar ili wakapokee (sehemu hiyo) kutoka kwake, basi (Umar) akaichana barua hiyo na akasema, "Hatuna haja nanyi kwani Mwenyezi Mungu amekwisha uimarisha Uislamu na hana haja nanyi, kwa hiyo mkislimu (mtasalimika) vinginevyo upanga ndiyo utakaoamua baina yetu na ninyi".

Watu hao walirudi kwa Abubakr wakamwambia, "Hivi wewe ndiyo Khalifa au yeye? Akasema: "Bali ni yeye apendapo Mwenyezi Mungu". Kisha akayapitisha aliyoyaamua Umar. Na mara nyingine Abubakar aliwaandikia barua Masahaba wawili (kuwapa) sehemu ya ardhi na akaituma barua hiyo kwa Umar ili aipitishe, Umar akaitemea mate na kuifuta, wale wakamshutumu na wakarudi kwa Abubakar huku wanalaumu na wakamwambia Abubakar "Sisi hatufahamu, hivi wewe ndiyo Khalifa au Umar?" Abubakar akasema, "Ni yeye." Baadaye Umar alikuja hali amemkasirikia Abubakar na akamwambia, "Huna haki ya kuwapa ardhi hawa." Abubakr akamwambia Umar, "Hakika nilikwisha kuambia kwamba wewe ndiwe mwenye nguvu kuliko mimi juu ya jambo hili hakika wewe umenishinda nguvu." Mpaka hapa inatubainikia siri ya cheo alichokuwanacho Umar ibn Khatab mbele ya Maquraish wote na mbele ya Bani Umayyah kwa upande wao, kiasi kwamba wamemuita shujaa na mwenye kupata Il-Ham na kuwa ndiyo Faaruq na muadilifu bila mipaka hadi wakamboresha juu mno kuliko hata Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) . Bila shaka tumekwishaona itikadi ya Umar juu ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kuanzia siku ya mapatano ya Hudaibiyah hadi siku ya msiba (wa siku ya Al-Khamisi) basi ongeza juu ya hayo kwamba, yeye aliwazuwia Masahaba kutabaruku kwa athari za Mtume wa Mwenyezi Mungu, akaukata mti wa Baiyatur- Ridh-wan, kama ambavyo alitawasali kupitia kwa Abbas ambaye ni ammi yake Mtume(s.a.w.w) ili awaoneshe watu kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alikwisha kufa na mambo yake yamemalizika hakuna faida hata kumkumbuka. Basi hapana lawama juu ya Mawahabi wasemao maneno kama haya, kwani siyo maneno mapya kama baadhi ya watu wanavyodhani. Mpaka hapa (utaona) mlango umefunguliwa kwa maadui wa Uislamu na Mustashrikina "Orientalists" ili waone kuwa Muhammad alikuwa mtu hodari tu, aliyewafahamu watu wake kuwa ni waabudu sanamu wamelelewa ndani ya ibada ya Masanamu, basi akawaondolea masanamu na kuwabadilishia jiwe jeusi (Hajarul-As-Wad).

Baada ya yote haya tunamuona Umar kuwa ndiyo shujaa wa kupinga kuandikwa kwa hadithi za Mtume kiasi kwamba anawafunga Masahaba hapo Madina na wengine anawazuwia kusimulia hadithi na anavichoma moto vitabu vya hadithi kwa pupa yake kwamba Sunna ya Mtume isije ikasambaa miongoni mwa watu. Kadhalika kwa kupitia hali hiyo tunafahamu kwamba ni kwa nini Imamu Ali(a.s) alibakia nyumbani (mwake) hatoki ila pale anapoitwa kwenda kutatua swali gumu lililowashinda Masahaba, na wala Umar hakumshirikisha Imamu Ali(a.s) katika madaraka wala utawala na hata katika majukumu ya kutuma ujumbe (wala jeshi) na alizuwiwa hata mirathi ya bibi Fatma(a.s) na akawa hana cho chote ambacho kingewafanya watu wawe na hamu naye, na kwa ajili hiyo basi, wanahistoria wanataja kuwa alilazimika kutoa baia baada ya mauti ya bi Fatma(a.s) baada ya kuwaona watu wamempuuza. Ni kwa nini watu wasikubughudhi (ewe Ali) hali ya kuwa uliwauwa mashujaa wao (wa kikafiri) na ukausambaratisha umoja wao, ukazibomoa ndoto zao, na hukuwaachia heshima yo yote katika jamii yao wala hukuwachia chochote katika nyanja za wema. Pamoja na yote hayo wewe ndiye mwana wa ammi ya mteule wa Mwenyezi Mungu na mtu wa karibu mno kwake, nawe ndiye mume wa Fatma (binti yake Mtume ambaye ni) mwanamke bora kuliko wanawake wote ulimwenguni pia (wewe) ni baba wa wajukuu wawili (wa Mtume) mabwana wa vijana wa peponi, isitoshe wewe ndiwe wa mwanzo wao kusilimu na mwenye elimu nyingi kuliko (Masahaba) wote.

Si hivyo tu bali ammi yako Hamza ndiye bwana wa mashahidi, na Jaafar At-tayyar ni nduguyo kwa baba na mama, pia baba yako ndiye mlezi wa Mtume(s.a.w.w) , kadhalika Maimamu waliobarikiwa wote wanatokana na kizazi chako. Umewatangulia.wenye kutangulia na umewazidi waliodhaniwa kuwa wao ndiyo, ulikuwa ni simba wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na ulikuwa ndiyo upanga wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake(s.a.w.w) , na uliaminiwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake(s.a.w.w) uende ukaifikishe Suratul-baraa, kwani hakuaminiwa mwingine (kuipeleka sura hiyo) asiyekuwa wewe. Wewe ulikuwa ndiyo Sid-diqul-Akbar, hawezi kudai sifa hiyo mtu mwingine baada yako ila atakuwa ni muongo, kama ambavyo wewe ndiyo yule Faruqul-Akbar ambaye huiweka haki mahali pake, na kisha haki hiyo ikafahamika kutoka katikati ya rundo la batili. Ni wewe ambaye ulikuwa ndiyo elimu iliyo wazi na minara inayong'ara, hufahamika kwa akupendaye imani ya muumini na kwa yule anayekubughi (hufahamika) unafiki wa munafik. Wewe ndiyo mlango wa mji wa elimu, mwenye kukujia ataufikia mji huo, hivyo basi hapana shaka kwamba, yeyote atakayedai kuingia mjini kupitia kwa asiyekuwa huyo ni muongo. Je, ni nani miongoni mwao anayo hisa mfano wa hisa uliyonayo wewe ewe Abul-hasan, na ni nani miongoni mwao ana ubora kama ubora wako ndiyo dalili? Kwa hiyo, iwapo utukufu unachokitambulisho hapana shaka wewe ndicho kitambulisho chake, kwani ubora wako uko kwenye ngazi ya juu. Bila shaka walikuhusudu kwa yale aliyokujaalia Mwenyezi Mungu miongoni mwa fadhila zake, na kwa hakika walikutenga wakati Mwenyezi Mungu alipokuhusisha kuwa karibu naye. Basi watafahamu wale waliodhulumu ni mgeuko gani watakaogeuka(siku hiyo).

Sasa hivi kalamu imetusogeza karibu ili tuweze kuzungumza na Amirul-Muuminina (Ali ibn Abitalib) aliyedhulumiwa akiwa hai au amekufa ambaye ni kiigizo chema kwa nduguye Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kwani naye ni mwenye kudhulumiwa akiwa hai au amekufa, kutokana na yeye kuyamaliza maisha yake ya Utume hali akipigana jihadi na kuunasihi (umma), huku akiwahangaikia waumini, alikuwa mpole kwao tena mwenye huruma. (Lakini katika hao), wako waliomkabili kwa maneno machafu katika ile saa ya mwisho (wa uhai wake) wakamtuhumu kuwa anaweweseka na wakamjibu majibu yaliyomchukiza walipomuasi na kumpinga wakati alipompa uongozi wa jeshi Usama, si hivyo tu bali wakakimbilia Saqifa kwa ajili ya (kugombea) Ukhalifa na wakauacha mwili wa Mtume (alipofariki) na wala hawakujishughulisha na maandalizi ya kumkosha Mtume wala kumvalisha sanda. Baada ya kufariki kwake Mtume(s.a.w.w) walimfanyia mambo ya kumdhalilisha mbele za watu na kuiporomosha heshima yake pia kumuondolea "Isma" ambayo Qur'an na hali halisi vinashuhudia yote hayo, (na walifanya) haya yote kwa ajili ya kutafuta utawala usiodumu na dunia yenye kutoweka. Kwa hiyo basi, kwa kupitia utafiti huu, tumeufahamu msimamo wa baadhi ya masahaba dhidi ya utukufu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) katika lengo lao la kuufikia Ukhalifa.

Bila shaka watawala wa Bani Umayyah wakiongozwa na Muawiyyah ibn Abi Sufiyan, wao waliupata Ukhalifa kwa kurithiana na wakaimarika kwa Ukhalifa huo na wala yeyote miongoni mwao hakupata kufikiri kwamba siku moja Ukhalifa utawatoka. Sasa basi ni kwa nini Banu Umayyah waliendelea kuitweza heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) na kuzua riwaya za kuporomosha cheo chake? Mimi ninaamini kuwa, kuna sababu mbili za msingi nazo nihizi zfuatazo: Sababu ya Kwanza: Bila shaka lengo la kuitweza heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ilikuwa ni kuwadhalilisha Bani Hashim ambao walikuwa wamejipatia heshima na utukufu miongoni mwa makabila ya Kiarabu kwa kupatikana Nabii anayetokana na Bani Hashim, hususani pale tunapofahamu ya kwamba Umayyah (Babu wa Bani Umayyah) alikuwa akishindana na nduguye Hashim (Babu wa Bani Hashim), na (huyu Umayyah) akimhusudu (Hashim) kwa kufanya kila mbinu ili amuuwe. Ongeza zaidi ya hilo ni kwamba, Ali (a.s) ndiye Bwana wa Bani Hashim baada ya Mtume(s.a.w.w) bila kupingwa, na Waislamu wa pande zote wanafahamu kero ya Muawiyah dhidi ya Ali(a.s) na vita alivyopigana (Muawiyah) dhidi ya Ali ili amnyang'anye Ukhalifa. Na baada ya Ali kuuawa Muawiyyah akaendelea kumtukana na kumlaani Ali juu ya mimbari (misikitini), kwa hiyo ili kumuondolea Mtume(s.a.w.w) heshima yake, kwa mujibu wa imani ya Muawiyah ilikuwa ni, kwanza aiangushe heshima ya Ali kama ukweli wenyewe ulivyo ya kuwa, kumtukana na kumlaani Ali ni kuelekeza (matusi na laana) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) .

Sababu ya Pili: Bila shaka kuivunja heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ndani yake iko namna inayowatakasa watawala wa Banu Umayyah kutokana na matendo ya aibu na maovu waliyokuwa wakiyatenda kama yalivyoandikwa katika historia (na kueleza namna walivyokuwa). Iwapo Mtume wa Mwenyezi Mungu (kama wamtazamavyo wao Banu Umayyah) ni mtu mwenye kupenda mambo ya upuuzi na wanawake kiasi kwamba hali hiyo inampelekea kusahau wajibu wake, na (eti Mtume) alikuwa anampenda mmoja wa wanawake hao mpaka anafikia kushindwa kuwa muadilifu baina yao, nao (wakeze) wanamtumia ujumbe kumtaka afanye uadilifu. Baada ya yote hayo. watu wa kawaida (wasiokuwa Mitume) kama vile Muawiya na Yazid na wengine mfano wa hao hawana lawama (kwa kutenda hayo maovu waliyoyatenda). Ndani ya hii sababu ya pili, inajificha hatari ya kuwa Banu Umayyah walitengeneza hadithi nyingi zinazodaiwa kuwa zilisimuliwa kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) ambazo zimekuwa miongoni mwa hukumu (za sheria) zinazotumika ndani ya Uislamu, na Waislamu wamezichukulia moja kwa moja kuwa ni miongoni mwa kauli na matendo ya Mtume(s.a.w.w) na zimekuwa ni sunna ya Mtume kwa Waislamu. Nitatoa baadhi ya mifano kuhusu hadithi hizo miongoni mwa hadithi chafu ambazo ziliwekwa ili kuudhalilisha Utukufu wa Mtume na kuangusha daraja yake, na wala sitaki kuifanya maudhui hii iwe pana, bali nitafupisha tu kwa yale waliyoyaandika Bukhari na Muslim katika vitabu vyao nazo ni hadithi zenye fedheha kwa lengo la kumuaibisha Mtume(s.a.w.w) .

1). Bukhari ameandika katika kitabul-Ghusli mlango usemao, Atakapojamii kisha akirudia, Amesema Anas, "Mtume alikuwa akiwazungukia wakeze usiku katika saa moja pia mchana na walikuwa kumi na moja. Akasema: Nikamwambia Anas: Je, alikuwa akiweza kufanya hivyo? Akasema: Tulikuwa tukizungumza kwamba yeye alipewa nguvu za watu thelathini". Hebu tuiangalie sote kwa pamoja hadithi hii yenye fedheha ewe msomaji, hadithi ambayo inatuonyesha kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alikuwa katika hali ya uroho wa kujamii (kwa kiasi hiki), anawajamii wanawake kumi na moja kwa saa moja na anawajamii usiku na mchana tena kwa haraka namna hii kisha bila hata ya kukoga josho la jimai ya kwanza bali anamjamii mke wa pili akiwa na maji ya yule wa kwanza. Ni juu yako ewe msomaji upime na ufikiri itakuwaje mtu kumvamia mkewe kama mnyama bila kuwepo vitangulizi wala maandalizi, na tunashuhudia hata kwa wanyama kwamba suala la jimai huchukua muda mrefu na linahitaji vitangulizi na maandalizi, basi iweje kwa Mtume huyu Mtukufu afanye kama hivyo (ilivyoelezwa ndani ya hadithi hiyo bila kuwepo maandalizi ya jimai n.k.)? Kwa hakika Mwenyezi Mungu awalaani (waliozuwa mambo haya dhidi ya Mtume) ni waongo tena wamepotea. Na kwa kuwa Waarabu katika zama hizo na wanaume (kwa jumla) walikuwa hawajaacha kujifakhirisha kwa nguvu za jimai na waliliona jambo hilo kuwa ni alama ya uanaume ndiyo maana waliweka kisa hiki dhidi ya Mtume(s.a.w.w) .

Kamwe Mtume hakutenda hayo, kwani yeye ndiye aliyesema kuwa "Musiwavamie wake zenu kama wanyama, wekeni mjumbe baina yenu na wao." Basi mfano wa riwaya kama hizi ndizo ambazo maadui wa Uislamu huzichukulia kuwa hoja dhidi ya Mtume(s.a.w.w) na kumuelezea kuwa yeye alikuwa mtu aliyezama katika mambo ya kijinsia, kujamiana na kupenda wanawake na tuhuma nyinginezo. Hebu tumuulize huyo Anas ibn Malik aliyekieleza kisa hiki. "Je, ni nani aliyemuambia kisa hicho? Ni nani aliyemjulisha kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ana jamii wakeze kumi na moja kwa saa moja? Je, ni Mtume ndiye aliyemueleza jambo hilo? Na je, inakubalika kwa mmoja wetu kuwasimulia watu namna anavyomjamii mkewe? Au wakeze Mtume ndio waliokuambia hayo (ewe Anas)? Basi je, inakubalika kwa mwanamke Muislamu kuwaelezea wanaume namna anavyojamiiwa na mumewe? Au Anas yeye ndiye aliyempeleleza Mtume na kufuatilia faragha zake na wakeze na akachungulia kupitia matundu ya milango (akagundua hilo)? Namuomba Mwenyezi Mungu aniepushe na mawazo ya kishetani, na Mwenyezi Mungu awalaani wazushi hao. Mimi sina shaka kwamba watawala wa Banu Umayyah na Banu Abbas ambao ni mashuhuri kwa kuwa na wanawake na vijakazi wengi, wao ndiyo walioweka visa vyenye mfano kama huu ili kuhalalisha matendo yao (maovu).

2) Bukhari ameandika katika Sahihi yake ndani ya juzuu ya tatu ukurasa wa 132 na pia Muslim ndani ya Sahihi yake katika juzuu ya saba ukurasa wa 136 wamesema: "Bibi Aisha amesema, Wakeze Mtume(s.a.w.w) walimtuma Fatma binti ya Mtume(s.a.w.w) aende kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, alipofika akabisha hodi, na wakati huo Mtume alikuwa amelala pamoja nami ndani ya shuka yangu, Mtume akamkaribisha binti yake, Fatima akasema, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika wakezo wamenituma kwako wanakutaka uwe muadilifu kutokana na (kuegama kwako upande) binti ya Abu Quhafa, wakati huo mimi nimenyamaza tu: bibi Aisha akasema: Mtume akamwambia bibi Fatma; Ewe binti yangu hukipendi nikipendacho mimi, bibi Fatma akasema kwa nini (nisikipende) Mtume akasema basi mpende huyu (Aisha).."

Kisha hadithi inaendelea na inasema, "Mpaka wakeze Mtume wakamtuma kwa mara ya pili bibi Zainab binti Jahshi ambaye ni mke wa Mtume, wakimuelekeza afanye uadilifu (kwa kuegama kwake) kwa binti ya Abu Quhafah (yaani Aisha) na akaingia kwa Mtume na hali Mtume kalala pamoja na Aisha na amejifunika shuka ya Aisha na akiwa katika mazingira kama yale aliyomkuta nayo bibi Fatma, basi akamtaka Mtume awe muadilifu kuhusu binti ya Abu Quhafah kwa niaba ya wakeze Mtume. Hatimaye (bibi Zainab) akamrukia bibi Aisha na kumtukana, naye bibi Aisha akajitetea nafsi yake akamtukana Zainab mpaka Mtume akamnyamazisha na kisha Mtume akatabasamu na akasema: L'Bila shaka huyo ndiye binti Abubakr." Nasikitika sana kusema kwamba, hadithi hizi chafu ambazo zinamfanya Mtume wa Mwenyezi Mungu kuonekana kuwa ni mtu anayefuata matamanio ya nafsi yake na hana uadilifu baina ya wakeze, wakati ambapo Qur'an iliyokuja kwa kupitia ulimi wake inasema "Na mkichelea kuwa hamtafanya uadilifu basi mke mmoja anatosha, au wekeni wajakazi ambao mikonoyenu ya kuume imewamiliki". Itakuwaje basi Mtume(s.a.w.w) amkaribishe binti yake ambaye ni mwanamke bora kuliko wanawake wote aingie (chumbani) kwake na Mtume yuko katika hali ile amelala na mkewe na amejifunika shuka ya mkewe, na Mtume asinyanyuke akakaa au kusimama bali anabaki kalala hata amwambie, "Ewe binti yangu hukipendi nikipendacho?" Pia wakati mkewe Zainab anapoingia na kumtaka awe muadilifu (matokeo yake) Mtume anatabasamu na kusema: "Bila shaka huyo ndiyo binti Abubakr."

Ewe msomaji mpendwa hebu iangalie fedheha hii wanayomsingizia Mtume wa Mwenyezi Mungu ambaye ni kiigizo chema kwa uadilifu na usawa, na wakati huo huo wanasema eti uadilifu ulitoweka alipokufa Umar ibn Khattab na wanamfanya Mtume wa Mwenyezi Mungu kuwa ni mtu asiyejali tabia njema, hafahamu jambo la aibu ni lipi wala utu ni kitu gani. Kuna hadithi nyingi mno ndani ya vitabu vya Kisunni, mfano wa hii (iliyotangulia) ambazo makusudio ya wapokezi wake kwa undani ni kuonyesha ubora wa Sahaba au bibi Aisha mwenyewe kwa kuwa tu yeye ni binti ya Abubakr, na kwa hali hii wanamdhalilisha Mtume hali ya kuwa wanajua au hawajui. Na kama ilivyotangulia ndani ya uchunguzi (huu) kwamba hadithi hizi zimewekwa ili kuaibisha utukufu wa Mtume(s.a.w.w) . Sasa hebu itazame hadithi ya tatu inayofanana na hii (iliyotangulia).

3) Muslim ndani ya kitabu chake katika mlango unaohusu fadhila za Uthman ibn Affan ameandika hadithi toka kwa Aisha mkewe Mtume(s.a.w.w) na yeye Uthman, wawili hawa wameeleza kwamba, Abubakr alibisha hodi nyumbani kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) na hali Mtume kalala kitandani kwake amejifunika shuka ya Aisha, Mtume akamkaribisha Abubakar na Mtume akabakia kama alivyokuwa na akamtekelezea Abubakr shida yake (iliyomleta) kisha akaondoka, halafu Umar alibisha hodi na Mtume akamkaribisha hali ya kuwa katika hali ile ile ya mwanzo na akamtimizia shida yake akaondoka, Uthman akasema; hatimaye nilibisha hodi mimi basi Mtume akakaa na akamwambia Aisha; jifunike nguo zako, mimi nikamaliza shida yangu kwa Mtume kisha nikaondoka, Aisha akasema, Ewe Mtume wa Mwenyezi mungu mbona sikukuona ukibabaika (walipoingia) Abubakr na Umar (r.a) kama ulivyobabaika kwa Uthman? Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema, bila shaka Uthman ni mtu mwenye haya nami nilichelea lau ningemkaribisha nikiwa katika hali ile asingenifikishia shida yake". Hadithi hii inafanana na hadithi nyingine iliyo andikwa na Bukhari na Muslim kuhusu fadhila za Uthman ibn Affan na inaeleza kwamba, "Mapaja ya Mtume wa Mwenyezi Mungu yalikuwa wazi bila nguo, mara akabisha hodi Abubakr, Mtume hakuyafunika mapaja yake na ndivyo alivyofanya alipoingia Umar, hatimaye alipobisha hodi Uthman, Mtume akayafunika mapaja yake na kuziweka vizuri nguo zake, bibi Aisha alipomuuliza Mtume juu ya jambo hilo, Mtume akamwambia Aisha, kwa nini nisimstahi mtu Malaika wa Mwenyezi Mungu wanamstahi?"

Mwenyezi Mungu awalaani Banu Umayyah ambao wamemdhalilisha Mtume wa Mwenyezi Mungu ili wamtukuze bwana wao.

4) Muslim ameandika ndani ya sahih yake katika mlango wa Wujubul-Ghusli Bil-tiqail-khitaanain, kwamba imepokewa kutoka kwa bibi Aisha mke wa Mtume(s.a.w.w) amesema: "Kuna mtu mmoja alimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kuhusu mtu aliyemuingilia mkewe kisha akakidhi haja yake, je, wote wawili wanawajibika kukoga (wakati swali linaulizwa) bibi Aisha alikuwa kakaa (hapo anasikiliza), basi Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema, "Hakika Mimi na huyu (Aisha) huwa tunafanya hivyo kisha tunakoga." Nakuachia wewe ewe msomaji uichunguze mwenyewe hadithi hii, hivi ni kweli ilifikia kiasi cha Mtume kumpenda mkewe Aisha akawa anasimulia namna ya jimai yake kwa watu mahsusi na kwa kila mtu? Kuna hadithi chungu nzima za Aisha binti Abubakr kama hizi ambazo ndani yake zinagusa heshima ya Mtume na kuiangusha thamani yake, kwani mara nyingine anaeleza kwamba Mtume alikuwa akiweka shavu lake juu ya shavu la (Aisha) ili achungulie ngoma inayochezwa na Msudani (yaani mtu mweusi). Na mara nyingine (Mtume) humbeba begani kwake, na wakati mwingine hushindana naye na Aisha humshinda Mtume kisha Mtume anasubiri mpaka Aisha aliponenepa ndipo alipomshinda na hatimaye akasema: "Ushindi huu niliokushinda ni kwa zile mara mbili ulizonishinda". Na kuna wakati mwingine Mtume alilala chali huku wanawake wakipiga madufu na zumari za shetani nyumbani kwake na Abubakr akawakaripia. Zipo hadithi chungu nzima zenye mambo ya aibu mfano wa hizi ambazo hazina lengo isipokuwa kumuabisha Mtume wa Uislamu. Kwa mfano hadithi isemayo kwamba, Mtume(s.a.w.w) alifanyiwa uchawi kiasi kwamba akawa hajui akifanyacho wala akisemacho mpaka akawa anadhani kwamba anawaendea wakeze wakati hawaendei" na kama riwaya zisemazo kuwa Mtume(s.a.w.w) alikuwa akiamka na janaba mwezi wa Ramadhani na kwamba hulala Mtume mpaka anakoroma usingizini kisha husimama akaswali bila kutawadha. Mtume huwa anasahau ndani ya sala yake kiasi kwamba hajui ni rakaa ngapi ameswali na Mtume wa Mwenyezi Mungu hafahamu nini hatima yake siku ya Qiyama na atafanyiwa nini na kwamba yeye Mtume alikuwa akikojoa wima na Sahaba anasogea mbali kisha Mtume humwita Sahaba huyo asogee karibu mpaka amalize kukojoa. Naam (miongoni mwa hadithi hizo) kutoka kwa mkewe Aisha binti Abubakr zimefikia hatua mbaya ya kumdhalilisha Mtume wa Mwenyezi Mungu eti kwamba yeye alijizuwia nafsi yake mwenyewe na akawazuwia Waislamu waliokuwa pamoja naye ili watafute mkufu wa mwana Aisha, ulimpotea na (Waislamu) wakiwa hawana maji mpaka ikabidi watu wamshitaki Aisha kwa Abubakr, ikamlazimu baba yake Aisha aje kumkemea Aisha na kumlaumu na wakati yote haya yanatendeka Mtume amelala usingizi mapajani kwa mkewe. Hebu isome riwaya hii kwa urefu.

Bukhari ameandika ndani ya Sahihi yake katika Babut-tayamum, na Muslim naye vile vile kaandika ndani ya Sahih yake katika Babut-tayammum imeelezwa toka kwa bibi Aisha kwamba yeye amesema, "Tulitoka pamoja na Mtume(s.a.w.w) katika baadhi ya safari zake hata tulipofika jangwani pasipo maji mkufu wangu ulikatika, Mtume wa Mwenyezi Mungu akasimama kuutafuta, watu wote wakasimama pamoja naye na walikuwa sehemu isiyo na maji na hawana (akiba ya) maji, basi watu wakamjia Abubakr wakasema: Je, huyaoni aliyoyafanya Aisha, amemsimamisha Mtume wa Mwenyezi Mungu na watu alionao hali ya kuwa wapo mahala pasipo na maji na wala wao hawana (akiba ya) maji. Basi Abubakr akaja na (akamkuta) Mtume wa Mwenyezi Mungu ameweka kichwa chake mapajani mwangu amelala akasema, Umemzuwia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) hali ya kuwa watu wako mahala pasipo na maji na hawana maji? Bibi Aisha anasema, Abubakr akanikemea na akasema aliyoyataka Mwenyezi Mungu ayaseme kiasi kwamba akawa ananichokoa kiunoni nami sikujizuia kutikisika isipokuwa mahala alipolala mjumbe wa Mwenyezi Mungu (yaani) mapajani mwangu. Basi Mtume alilala mpaka asubuhi bila ya maji na ndipo Mwenyezi Mungu alipoteremsha aya ya kutayammam. Usaid ibn Al-Hudhair ambaye ni miongoni mwa watu wenye haiba akasema, Hii siyo baraka yenu ya kwanza enyi kizazi cha Abubakr. Aisha akasema tukaagiza (aletwe) yule ngamia niliyekuwa nimepanda tukaukuta mkufu chini yake." Basi hivi kweli muumini anayeufahamu Uislamu ataamini kwamba Mtume(s.a.w.w) anapuuza jambo la Sala kwa kiwango hiki, na anawazuwia Waislam hali ya kuwa hawako mahala penye maji na hawana maji na yote hayo kwa ajili ya kutafuta mkufu wa mkewe ambao umempotea? Si hivyo awaache Waislamu wanasikitikia kupotea (kwa wakati wa) Sala na (hatimaye) wamshitakie kwa Abubakr na katika kipindi hicho hicho Mtume amekwenda kulala mapajani kwa mkewe na usingizi umemkolea hata asitambue kuja kwa Abubakr na kumkemea Aisha na kumchokoa kiunoni? Basi vipi itawezekana kwa Mtume huyu kuwaacha watu wakihangaika kwa ajili ya kukaribia (ibada ya) Sala hali yeye amelala mapajani kwa mkewe?

Hapana shaka kwamba hadithi hizi zilizuliwa katika zama za Muawiya ibn Abi Sufiyan na kwa kweli hazina chimbuko lolote (ndani ya Uislamu), vinginevyo basi tutalieleza namna gani tukio kama hili ambalo lilihudhuriwa na masahaba wengi na Umar akawa halijui tukio hili wakati alipoulizwa namna ya kutayammam, kama walivyoandika Bukhari na Muslim ndani ya vitabu vyao katika mlango wa kutayammam? Jambo muhimu katika utafiti wote huu ni kutaka kufahamu kwamba njama dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) zilikuwa ni njama mbaya na chafu zinazotumika kumuaibisha na kuporomosha hadhi yake mpaka kufikia kiwango cha mmoja wetu leo hii hawezi kuridhia binafsi yake aonekane kuwa na mwenendo kama huu na vitendo kama hivi (ukiachilia mbali uovu ambao umeenea kila mahali). Basi sisi Waislamu tunamuangalia vipi Mtume huyu mtukufu ambaye historia ya wanaadamu imemtambua (kwa wema) na anashuhudiwa na Mola mwenye nguvu na utukufu kwamba yeye ni mwenye hadhi kubwa mno kwa tabia njema? Kwa hakika ninavyoamini mimi ni kwamba, njama hizi zilianza baada ya Hija ya kuaga na hasa baada ya Mtume(s.a.w.w) kumsimika Imam Ali (a.s) kuwa Khalifa wake siku ya Ghadir khum. Hapo ndipo wale wenye tamaa ya ukubwa walipofahamu ya kwamba sasa hakuna lakufanya isipokuwa ni upinzani na ukaidi dhidi ya agizo (yaani uteuzi huo) kwa gharama yoyote ile japokuwa itapelekea kurudi nyuma kwa visigino vyao (yaani kutoka katika dini). Hiyo ni tafsiri ya matukio iliyoanza kujitokeza kwa kumpinga Mtume(s.a.w.w) katika kila maamrisho yake (aliyoyatoa) na inathibitika hali hiyo kuanzia pale Mtume alipoandika maandiko ya kumpa Usamah uongozi wa jeshi, na matokeo yake ni watu kutokwenda kwenye jeshi aliloliandaa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) mwenyewe, na pia matukio yaliyofuatia baada ya Mtume kufariki. Miongoni mwa matukio hayo ni kuwalazimisha watu wale kiapo cha utiifu kwa nguvu na kuwatishia kuwachoma moto wale waliogoma, wakiwemo Ali, Fatma, Hassan na Hussein (a.s) . Bali hali ilikuwa mbaya mno kiasi cha kuwazuwia watu kunakili hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kiasi kwamba vitabu ambavyo ndani yake tayari Sunna ya Mtume(s.a.w.w) ilikwisha andikwa vilichomwa moto. Si hivyo tu bali wako baadhi ya masahaba walitiwa gerezani ilimradi wasisimulie hadithi za Mtume(s.a.w.w) , mpaka ikafikia (kiwango) cha kuwauwa Masahaba ambao walikataa kutoa zaka kwa Abubakr kwa sababu yeye siye Khalifa waliyempa kiapo cha utii katika zama za Mtume wao kabla hajafariki.

(Haikuishia hapo tu bali) ilifikia kiwango cha kupora haki za bibi Fatma binti ya Mtume(s.a.w.w) ikiwa ni pamoja na shamba la Fadak, mirathi, Khums na kisha kumtuhumu kwamba yeye ni muongo kutokana na madai yake yanayohusu haki zake. Ilifikia wakati ambapo Imam Ali(a.s) alitengwa mbali mno na kila aina ya majukumu ya Kiislamu, na badala yake walitawalishwa juu ya shingo za Waislamu watu waovu na wanafiki miongoni mwa Bani Umayyah, na mambo yalivuka mpaka kwani Masahaba walizuiliwa kutabaruku kwa kumbukumbu za Mtume(s.a.w.w) . Utadhani hayo hayatoshi,. bali ilifikia hatua ya kufanya jaribio la kulifuta jina la Mtume(s.a.w.w) kwenye Adhana na kuushambulia mji wa Madina yenye Nuru kwa jeshi la kikafiri, jeshi ambalo lilifanya namna litakavyo mjini humo. Na ilifikia kuipiga nyumba tukufu (ya Mwenyezi Mungu) kwa mizinga, kuichoma moto na kuwauwa humo Masahaba, na ikafikia kukiua kizazi kitukufu cha Mtume(s.a.w.w) na kukitukana, kukilaani na watu kuwalazimisha kufanya hivyo, na hatimaye ilifikia kuwaua na kuwasambaratisha wote wanaowapenda watu wa nyumba ya Mtume kwa kuwafuatilia, mpaka ikafikia kuwa dini ya Mwenyezi Mungu ni jambo la mchezo na ni upuuzi na Qur'an ikawa inachanwa na kupuuzwa.

Njama hizo bado zinaendelea mpaka leo na athari zake na nguvu zake zinatembea ndani ya umma wa Kiislamu, na maadam kuna Waislamu wanaomtakia radhi Muawiyah na Yazid, na wanayatakasa matendo yao kuwa eti walifanya jitihada katika dini na kwamba watalipwa ujira kwa matendo hayo mbele ya Mwenyezi Mungu, na maadam wapo watu wanaoandika vitabu na makala mbali mbali dhidi ya wafuasi wa nyumba ya Mtume, kisha kuwavurumishia kila aina ya shutuma na matusi watu hao, na maadam kuna watu wanaohalalisha kuwaua wafuasi wa nyumba ya Mtume ndani ya nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu tena katika msimu wa Hija, basi njama hizo (dhidi ya Mtumes.a.w.w ) bado zinaendelea na zitabakia kuendelea mpaka hapo atakapotaka Mwenyezi Mungu. Nami siwezi kuzionesha zote au kuzidhibitisha kwa ufafanuzi wake kila upande, lakini ninajaribu juhudi yangu tena kwa unyenyekevu ili kumtakasa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kutokana na riwaya zenye fedheha ambazo amesingiziwa na ninamtetea yeye na Isma yake, na ninajaribu kuwatosheleza Waislamu wenye maarifa na walio huru (kifikra) kwamba, Mtume huyu ambaye Mwenyezi Mungu alimtuma ili awaongoe wanadamu wote na akamfanya kuwa mwangaza na taa inayong'ara, ni Mtume Mtukufu mno na ni mbora mno aliyetakasika sana sana, ni mkamilifu mno kuliko watu (wengine). Mwenyezi Mungu ndiye aliyemuumba (kwa sifa hizo) hivyo basi haiwezekani kwetu sisi kuzinyamazia riwaya ambazo undani wake hazikulengwa isipokuwa kuivunja heshima yake na kuporomosha utukufu wake.

Haiwezekani na haitawezekana kwetu sisi kuzikubali riwaya hizi japokuwa Ahlu-Sunnah Wal-Jamaa wamezikubali na wakaziandika ndani ya Sihahi zao na Musnad zao, haiwezekani (tukazikubali) hata kama wataafikiana (kuzikubali) walimwengu wote, kwani kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema, "Hakika wewe uko juu ya labia tukufu" hiyo ndiyo kauli ya ufumbuzi na uamuzi wa msingi, na baada ya kauli hiyo hapana kingine isipokuwa ni upotofu na uzushi. Na hii ifuatayo ndiyo kauli ya Mashia kumhusu Bwana wa viumbe wote ambaye ni muokozi wa wanaadamu kutokana na upofu na upotofu (uliozushwa dhidi ya) kiongozi wa umma anayeongoza watu kwenye amani na usalama, basi enyi wenye akili hebu fanyeni mazingatio.