WAULIZE WANAOFAHAMU

WAULIZE WANAOFAHAMU0%

WAULIZE WANAOFAHAMU Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Misingi mikuu ya Dini

WAULIZE WANAOFAHAMU

Mwandishi: Muhammad Tijani As-samawi At-Tunisi
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 49402
Pakua: 4126

Maelezo zaidi:

WAULIZE WANAOFAHAMU
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 26 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 49402 / Pakua: 4126
Kiwango Kiwango Kiwango
WAULIZE WANAOFAHAMU

WAULIZE WANAOFAHAMU

Mwandishi:
Swahili

3

WAULIZE WANAOFAHAMU

KAULI YA AHLU-DHIKRI KUHUSU MTUME (S.A.W.W)

Imam Ali(a.s) anasema: "Mpaka karama za Mwenyezi Mungu zikamfikia Muhammad(s.a.w.w) , akamtoa kutoka kwenye maoteo yenye asili bora, na mahala penye mapandio yenye nasaba tukufu, (akamtoa) kutoka katika mti ambao Mitume wake wametokana nao, na kutokana na mti huo (Mwenyezi Mungu) ameteua wawakilishi wake, kizazi cha Mtume ndiyo bora kuliko vizazi vyote, na ukoo wake ndiyo bora kuliko koo zote, na mti wake ndiyo bora kuliko miti yote, umeota mahala patakatifu na ukachanua mahala pema, una matawi marefu na matunda yasiyodhurika kwa chochote kile. Basi yeye Mtume ndiyo kiongozi wa yeyote anayemcha Mungu, naye ndiye jicho la mwenye kuongoka, ni taa ing'arayo mwanga wake na ni miali ambayo nuru yake imechomoza, yeye ni mwenge ambao mng'ao wake ni wenye kumeta, mwendo wake ni wenye msimamo na Sunna yake ni uongofu, maneno yake ndiyo upambanuzi na hukumu yake ni yenye uadilifu. Mwenyezi Mungu alimtuma akiwa ni miongoni mwa Mitume katika muda muafaka kwani ulikuwa ni wakati wa upotofu na matendo ya kijinga miongoni mwa watu. Mtume akatoa nasaha kikamilifu, akapita katika njia (ya haki) na akalingania (watu) kwa hekima na mawaidha mazuri Makazi yake ni makazi bora na chimbuko lake ni chimbuko tukufu lililomo ndani ya asili bora na makazi ya amani. Kwa hakika nyoyo za (watu) wema zimegeuziwa upande wake na macho yamemwelekea. Kwa sababu yake Mtume, chuki baina ya watu zimezimwa na uadui nao umeangamizwa, na kwa ajili yake udugu (Kiislamu) umeunganika na ukabomolewa uhusiano (na kufru). Kupitia kwa Mtume mnyonge ameheshimika na amedhalilishwa mwenye kiburi, maneno yake ndiyo ubainifu na ukimya wake ni usemi (tosha). (Mwenyezi Mungu) amemtuma kwa hoja zilizokamilika, na mawaidha yenye kuponya, na wito ulio mzuri, kwa Mtume amezidhihirisha sheria zilizokuwa zimesahaulika na kwake yeye amekemea uzushi uliokuwa umeingizwa (katika dini) na kwake akazibainisha hukumu kwa ufafanuzi. Alimtuma pamoja na mwangaza, na akamtanguliza kwa kumtukuza kwake yeye Mtume, akaondosha maovu na akawashinda wenye kuipinga haki, na akayawepesisha yaliyo mazito na akazidhalilisha itikadi mbaya mpaka akautenga mbali upotovu kutokana na njia ya haki.

MLANGO WA TATU

YANAYOWAHUSU WATU WA NYUMBA YA MTUME (S.A.W.W)

SWALI LA TATU: AHLUL-BAIT (WATU WA NYUMBA YA MTUME) NI KINA NANI?

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا ﴿٣٣﴾

Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni baarabara. (Qar'an, 33:33).

Ahlu-Sunna Wal-Jamaa, wanasema kwamba aya hii ilishuka kwa ajili ya wake za Mtume(s.a.w.w) , na wanatolea ushahidi wa madai hayo kulingana na mfumo wa aya zilizo itangulia aya hii na zinazoifuatia. Kwa mujibu wa madai yao ni kwamba Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu wakeze Mtume na amewatakasa kikamilifu. Na miongoni mwa hao Ahli-Sunnah wapo wanaowaongeza juu ya wakeze Mtume(s.a.w.w) Imam Ali, Fatma, Hassan na Husein (a.s) . Lakini ukweli ulivyo na kama ulivyonukuliwa, kadhalika akili na historia vinaikataa tafsiri hii, kwani Ahlu-Sunnah haohao wanazo riwaya ndani ya vitabu vyao (zisemazo) kwamba aya hii ilishuka kuwahusu watu watano tu nao ni: Mtume Muhammad(s.a.w.w) , Ali, Fatma, Hasan na Husein(a.s) , na kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ndiye aliyewahusisha hao na nafsi yake tukufu kwenye aya hii pale alipomuingiza Ali, Fatma, Hasan na Hussein pamoja na yeye mwenyewe ndani ya kisaa (shuka) na akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu hawa ndiyo watu wangu basi waondolee uchafu na uwatakase kikamilifu." (Tafsiri) hiyo wameiandika wanachuoni wengi wa Kisunni, mimi nitawataja baadhi yao tu:

1) Muslim ndani ya Sahihi yake katika mlango wa Fadhail-Ahlil-Bait Juz. ya 2 uk. 368.

2) At-Tirmidhi ndani ya Sahih yake Juzuu ya 5 uk. 30.

3) Musnadul-Imam Ahmad ibn Hanbal Juzuu 1 uk. 330.

4) Mustad-rak-Al-Hakim Juzuu 3 uk. 123.

5) Khasaisul-Imamin-Nasai uk. 49.

6) Tal-Khisud-dhahabi Juzuu 2 uk. 150.

7) Mu'ujamut-Tabrani Juzuu 1 uk. 65.

8) Shawahidut-Tanzil ya Al-Hakimul-Haskani Juz.2 uk.ll

9) Bukhari ndani ya Tarikhul-Kabir Juz. 1 uk. 69

10) Al-Isabah ya ibn Hajar Al-Asqalani Juzuu 2 uk. 502.

11) Tadh-Kiratul-Khawas ya ibn Al-jauzi uk. 233.

12) Tafsirul-Fakhrir-Razi Juz. 2 uk. 700.

13) Yanabiul-Mawaddah ya Al-Qanduzi Al-Hanafi

uk. 107.

14) Manaqibul-Khawar-Zami uk. 23.

15) As-siratul-Halabiyyah Juz.3 uk. 213.

16) As-siratud-dah-laniyyah Juz. 3 uk. 329.

17) Usudul-ghabah ya ibnul-Athir Juz. 2 uk. 12. jl8) Tafsirut-Tabari Juz. 22 uk.6.

19) Ad-durul-Manthur ya Suyuti Juz. 5 uk. 198.

20) Tarikhu ibn A'sakir Juz. 1 uk. 185.

21) Tafsirul-Kashaf ya Az-Zamakhshari Juz. 1 uk.193

22) Ah-kamul-Qur'an ya ibn Arabi Juz. 2 uk. 166.

23) Tafsirul-qur-Tubi Juz. 14 uk. 182.

24) As-sawaiqul-Muhriqah ya ibn Hajar uk. 85.

25) Al-Istiiabu ya ibn Abdibarri Juz. 3 uk. 37.

26)Al-Iqdul-Farid ya ibn Abd rabih Juz. 4 uk. 311.

27) Muntakhabu Kanzil-Ummal Juz. 5 uk. 96.

28)Masabihus-Sunnah ya Al-baghwi Juz. 2 uk. 278.

29)As-babun-nuzul ya Al-wahidi uk. 203.

30)Tafsiru ibn Kathir Juz. 3 uk. 483.

Wako wengine wasiokuwa hawa miongoni mwa wanachuoni wa Ahlul-sunnah Wal-jamaa, wengi tu hatukuwataja lakini tumetosheka na idadi hii. Sasa basi ikiwa wanachuoni wote hawa wanakiri kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ndiye aliyebainisha makusudio ya aya hii, je zina nafasi gani kauli za wengine wasiokuwa Mtume miongoni mwa Masahaba na Tabiina au wafasiri ambao wanataka kuipeleka maana ya aya hiyo kinyume na vile atakavyo Mwenyezi Mungu na Mtume wake eti kwa lengo la kutaka kumridhisha Muawiyah na kutumainia (mali) aliyonayo? Kama ambavyo Mtume(s.a.w.w) amepata kuwaashiria watu nyumba yake kwa mara nyingine na akawahusisha kwamba wao ndio Ahlul-bait na siyo wengine wasiokuwa wao, napo ni pale iliposhuka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo:

فَقُلْ تَعَالَوْا نَدْعُ أَبْنَاءَنَا وَأَبْنَاءَكُمْ وَنِسَاءَنَا وَنِسَاءَكُمْ وَأَنفُسَنَا وَأَنفُسَكُمْ ثُمَّ نَبْتَهِلْ فَنَجْعَل لَّعْنَتَ اللَّـهِ عَلَى الْكَاذِبِينَ ﴿٦١﴾

"Basi waambie njooni tuwaite wanetu na wanenu, na wanawake wetu na wanawake wenu na sisi wenyewe na ninyi wenyewe, kisha tuapizane na tuombe laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo" (Qur'an, 3:61).

Bwana Mtume alimwita Ali, Fatma, Hassan na Husein na akasema "Hawa ndiyo wanetu na sisi wenyewe na wanawake wetu, basi njooni ninyi wenyewe na wanenu na wanawake zenu."

Na katika riwaya ya Muslim amesema: "Ewe Mwenyezi Mungu hawa ndiyo watu wangu ."

Na wale wanachuoni wa Ahli-Sunna Wal-Jamaa ambao nimewataja katika rejea zilizotangulia vile vile wote wanakiri kuwa aya hii (Qur'an, 3:61), ilishuka kuwahusu watu watano hawa waliotajwa, rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwashukie wote. Ifahamike kwamba, wakeze Mtume(s.a.w.w) waliyafahamu makusudio ya aya hiyo tukufu, (Qur'an, 33:33).

Na ndiyo maana hakuna mmoja wao aliyedai kwamba yeye ni miongoni mwa Ahlul-Bayt(a.s) na hasa hasa wakitanguliwa na Ummu Salamah na mwana Aisha, kwani kila mmoja wao (wawili hawa) ameleta riwaya (isemayo) kwamba aya hii inamuhusu Mtume wa Mwenyezi Mungu, Ali, Fatma, Hassan na Husein(a.s) , na wameandika juu ya kukiri kwa wake za Mtume kuhusu aya hiyo, Muslim, Tir-midhi, Al-Hakim, Tabari, Suyuti na Ibnul- Athir na wengineo.

Zaidi ya yote hayo ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) aliondoa utatanishi na mush-keli huu, kwani yeye alifahamu kwamba Waislamu wataisoma Qur'an na kuwafahamu Ahlul-Bait kutokana na mtiririko wa aya zilizotangulia na zinazofuatia ambazo zinawaonya wake wa Mtume, hivyo akawahi kuufundisha umma (wake) makusudio ya aya ya kuwaondolea uchafu na kuwatakasa (watu wa nyumba ya Mtume) pale alipodumu kwa mfululizo wa muda wa miezi sita (baada ya kushuka aya hii) kwa kupita kwenye mlango wa (nyumba ya) Ali, Fatma, Hasan na Hussein kabla ya kuanza kusali kwa kusema: (Bila shaka Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba ya Mtume na kukutakaseni sana sana, basi amkeni mkasali Mwenyezi Mungu akurehemuni. Suala la Bwana Mtume kuwahi kuufundisha umma wake ni jambo aliloliandika Tir-midhi katika Sahih yake Juz. 5 uk. 31, Al-hakim katika Mustad-rak Juz. 3 uk. 158, Ad-dhahabi ndani ya Tal-khisi yake, Ahmad ibn Hanbal ndani ya Musnad yake Juz. 3 uk. 259, Ibnul-athir ndani ya Usudul-ghabah Juz. 5 uk. 521 na Al-Has-Kani katika Shawahidut-tanzil Juz. 2 uk. 11, As-suyutti ndani ya Ad-durul-manthur Juz. 5. uk. 199, Tabari katika tafsiri yake Juz. 22 uk. 6, Al-baladhuri ndani ya Ansabul-Ash-raf Juz. 2 uk. 104, ibn Kathir katika tafsiri yake Juz. 3 uk. 483 na Haithami katika Majmauz- zawaid Juz. 9 uk. 168 na wengineo.

Zaidi ya hawa wanachuoni wa Kisunni tukiwaongeza Maimamu wa nyumba ya Mtume na wanachuoni wa Kishia ambao hawana shaka juu ya kuhusika kwa Mtume, Ali, Fatma Hassan na Husein katika aya hii tukufu, basi hakuna nafasi yoyote ya kujitetea watakayokuwa nayo wapinzani miongoni mwa maadui wa Ahlul-Bait na wafuasi wa Muawiyah na Banu Umayyah ambao wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa kutumia vinywa vyao na Mwenyezi Mungu (bila shaka) ataitimiza nuru yake (ing'ae) japokuwa makafiri watachukia. Kwa hakika wamedhihirisha wazi hao wanaofasiri aya hizo kinyume cha tafsiri ya Mtume(s.a.w.w) kwamba, wao ni miongoni mwa wanaojipendekeza kwa watawala wa Banu Umayyah na Bani Abbas hapo zamani mpaka sasa, kwani (wafasiri) hao ni miongoni mwa watu wenye chuki ambao hawampendi Ali japo watajificha kwa mavazi ya Uanachuoni na Ufaqihi. Tunasema hivi kwa sababu akili peke yake tu inatosha kupata uamuzi wa kutokuwaingiza katika aya hii yaani (kuondolewa uchafu na kuwatakasa) wakeze Mtume(s.a.w.w) .

1) Kwa mfano tukimchukua Ummul-Muuminina Aisha ambaye yeye anadai kuwa ni kipenzi mno kwa Mtume kuliko wakeze wengine na ni wa karibu mno kwa Mtume kiasi kwamba wake wengine wa Mtume walimuonea wivu na wakamtumia ujumbe (Mtume) wa kumtaka awe muadilifu kwa sababu ya binti Abi Quhafah, kama tulivyotangulia (kueleza) hakuthubutu na wala hakuna aliyethubutu miongoni mwa watetezi wake na wampendao si miongoni mwa waliopita wala wale waliofuatia (hakuna aliyethubutu) kusema kuwa Bibi Aisha alikuwa ndani ya Kisaa siku iliposhuka aya hiyo. Basi ni utukufu ulioje wa Muhammad(s.a.w.w) katika maneno yake na vitendo vyake na ni utukufu ulioje wa hekima yake pale alipowafunika ndani ya Kisaa mpaka Ummul-Muuminina Ummu Salamah ambaye ni mke wa Mtume alitaka kuingia pamoja nao ndani ya Kisaa na akamuomba mumewe ambaye ndiye Mtume wa Mwenyezi Mungu (naye aingie), lakini Mtume akamzuwia kuingia na akamwambia, "Wewe uko kwenye kheri".

2) Kisha aya hii kwa maf-humu yake makh'sus na ile ya jumla inajulisha juu ya "Isma" (ambayo ni kuhifadhika kutokana na kila aina ya madhambi), kwani kuondolewa uchafu kunakusanya kila aina ya dhambi, maasi na uovu, madogo na makubwa, na hasa itakapoongezewa utakaso huo kuwa unatoka kwa Mola Mtukufu mwenye nguvu.

3) Na iwapo Waislamu hujitoharisha kwa maji na udongo tahara ya kimwili ambayo haivuki zaidi ya nje ya miwili, basi Mwenyezi Mungu amewatakasa Ahlul-Bait kwa tahara ya kiroho iliyosafisha akili na moyo, na haukuachiwa nafasi yoyote ushawishi wa shetani wala kutenda maovu. Kwa hiyo nyoyo zao (Ahlul-Bait) ni safi, zimetakasika, zenye ukweli wa dhati kwa Muumba wao katika kila harakati zao na utuvu wao.

4) Kwa yote hayo watu hawa wamekuwa kiigizo kwa watu wote katika ucha Mungu, ukweli, elimu, upole, ushujaa, utu, utakasifu, kuipa nyongo dunia na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na historia haikupata kuandika maasi au dhambi ya yeyote miongoni mwao muda wote wa uhai wao. Na kama mambo yako kama hivyo, hebu na turejee kwenye mfano wa kwanza unaohusu wakeze Mtume(s.a.w.w) na (tumuone) Mwanaisha ambaye amefikia daraja tukufu na cheo cha juu na umaarufu mkubwa ambao hakuna mke yeyote wa Mtume(s.a.w.w) aliyeufikia. Haiwezekani kabisa kuzifikia sifa kemkem za bibi Aisha binti Abubakr hata kama sifa zao (wake wengine wa Mtume) zitakusanywa pamoja, na hivi ndivyo wasemavyo Ahlus-Sunnah kuhusu sifa za Mwanaisha pia Ahlus-Sunnah wanaamini kwamba nusu ya dini inatokana kwake (Bibi Aisha) peke yake.

Tukishikamana na ukweli bila ya chuki wala kupendelea, hivi kweli inaingia akilini kwamba Mwanaisha ametakasika hana madhambi wala maasi? Au tuseme kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alimuondolea Mwanaisha hifadhi na kizuwizi (cha kutofanya dhambi) baada ya kifo cha mumewe (ambaye) ni Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ? Basi hebu na tuuangalie kwa pamoja ukweli halisi ulivyo. Bibi Aisha katika zama za uhai wa Mtume(s.a.w.w) Tunapoyafanyia uchunguzi maisha yake na mumewe, tunayakuta madhambi na maasi mengi (aliyoyatenda). Mara nyingi alikuwa akifanva njama yeye na bibi Hafsa dhidi ya Mtume(s.a.w.w) mpaka akamlazimisha Mtume kujinyima kitu alichohalalishiwa na Mwenyezi Mungu. Maelezo ya jambo hilo yamo ndani ya Bukhari na Muslim, na wawili hao walisaidiana dhidi ya Mtume(s.a.w.w) kama zilivyolithibitisha jambo hilo sihah na tafsiri zote, na Mwenyezi Mungu ameyataja matukio yote mawili ndani ya kitabu chake kitukufu.

Vile vile ni kama ilivyokuwa wivu ukitawala moyo na akili zake na akawa hana heshima wala adabu mbele ya Mtume(s.a.w.w) , kuna wakati alimwambia Mtume(s.a.w.w) pale Mtume alipomtaja bibi Khadija mbele yake, (bibi Aisha akasema) "Kuna uhusiano gani kati yangu na Khadija, hakika yeye alikuwa bibi Kizee mwenye midomo myekundu na Mwenyezi Mungu amekubadilishia (mke) bora kuliko yeye." Na kwa ajili hii Mtume wa Mwenyezi Mungu alikasirika mpaka nywele zake zikatikisika. Kuna wakati fulani mmoja kati ya wakeze Mtume(s.a.w.w) alimpelekea Mtume sahani ambayo ndani yake mlikuwa na chakula ambacho Mtume alikuwa akikipenda, bibi Aisha (kwa wivu aliokuwa nao) akaivunja sahani hiyo na chakula chake mbele ya Mtume(s.a.w.w) .

Kuna mara nyingine tena bibi Aisha alimwambia Mtume, "Hivi wewe ndiye unayedai kuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu? Pia ipo siku ambayo Mama Aisha alikasirika mbele ya Mtume na akamwambia Mtume, "Fanya uadilifu." Baba yake alikuwepo mahala hapo akampiga mpaka damu zikamtiririka. Na kutokana na wingi wa wivu (aliokuwa nao) alimdanganya Asmaa binti Nu'uman alipokuwa bi harusi nyumbani kwa Mtume akamwambia, "Mtume humfurahia sana mwanamke ambaye akiingia kwake amwambie, "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana nawe". Lengo la Mama Aisha ilikiwa kinyume cha hivyo, bali ni alitaka mwanamke huyo asiye na kosa aachike, na Mtume alimuacha kwa sababu ya maneno haya. Kutokana na adabu yake mbaya mbele ya Mtume(s.a.w.w) , ilifikia mahali ambapo Mtume alikuwa akiswali naye bibi Aisha amenyoosha miguu yake kwenye Qibla, na Mtume akisujudu huisogeza pembeni ndipo (bibi Aisha) huikunja, Mtume akisimama yeye huionyoosha miguu yake kwenye Qibla yake. Kuna kipindi fulani walikula njama yeye na Mama Hafsa dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ikapelekea (njama hiyo kumfanya Mtume) ajitenge na wakeze kwa sababu ya njama hiyo kwa muda wa mwezi mmoja kamili Mtume analala kwenye jamvi. Iliposhuka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo:

"Na umuahirishe umtakaye miongoni mwao na umsogeze umtakaye " (Qur 33:51). Aisha alimwambia Mtume bila hata aibu "Simuoni Mola wako isipokuwa anaweka mbele matamanio yako".

Mama Aisha alipokuwa akikasirika (na ni mara nyingi alikuwa akikasirika) huacha jina la Mtume(s.a.w.w) na hutaja jina la Muhammad na hupata akasema: "Ewe Mlezi wa Ibrahim. (Kwa kweli) Aisha alimuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu mara nyingi na kumpa taabu, lakini Mtume(s.a.w.w) ni mpole mwenye huruma, na tabia yake ni tukufu na subira yake ni kubwa, mara nyingi alikuwa akimwambia Aisha, "Ewe Aisha shetani wako kisha kukuvaa" na mara nyingi alikuwa akisikitika kutokana na makemeo ya Mwenyezi Mungu kwake Aisha na Hafsa binti Umar, na ni mara nyingi Qur'an ilishuka kwa sababu yake, Mwenyezi Mungu amesema kuwaambia Aisha na Hafsa:

إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا ﴿٤﴾

"Iwapo mtatubia kwa Mwenyezi Mungu itakuwa kheri kwenu kwa hakika nyoyo zenu zimepotoka" (Qur'an 66:4). Aya hii inamaanisha kwamba amepotoka na kuiacha haki na amesema tena Mwenyezi Mungu:

وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ ﴿٤﴾

"Na kama mtasaidiana dhidi ya (Mtume) basi Mwenyezi Mungu ndiye msaidizi wake na Jibril na Waislamu wema, na zaidi ya hayo Malaikapia watasaidia". (Qur'an, 66:4).

Ni onyo la wazi kutoka kwa Mola Mtukufu (kuwaonya) Mama Aisha na Hafsa ambaye mara nyingi alikuwa akimfuata Aisha na kutekeleza anayomuamrisha. Na amesema tena Mwenyezi Mungu kuwaambia wawili hawa

عَسَىٰ رَبُّهُ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَاتٍ مُّؤْمِنَاتٍ ﴿٥﴾

"Mtume akikupeni talaka Mola wake atampa badala yenu wanawake wengine walio bora kuliko ninyi Waislamu tena waumini." (Qur'an, 66:5).

Aya hizi zilishuka kumuhusu Mama Aisha na Hafsa kwa ushahidi wa Umar ibn Khatab kama ilivyokuja katika Bukhari. Basi aya hii pekee inajulisha kuwa, kuna wanawake waumini miongoni mwa Waislamu ambao ni bora kuliko Aisha. Kuna wakati fulani Mtume(s.a.w.w) alimtuma Aisha pale Mtume alipotaka kumposa dada wa kiongozi wa kabila la Kalbi, Mtume akamtaka Aisha aende akamtazame mwanamke huyo, na aliporudi wivu ulikuwa umeusonga moyo wake, Bwana Mtume(s.a.w.w) akamuuliza, "Umemuonaje ewe Aisha? Aisha akasema "Sikuona uzuri wowote." Mtume(s.a.w.w) akamwambia Aisha, "Hakika umeona uzuri, hapana shaka umemuona msichana bora na umesisimka ukamuogopa." Basi Aisha akasema; "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kwako wewe hapana siri na ni nani mwenye kukuficha." Yote aliyoyafanya Aisha kumfanyia Mtume(s.a.w.w) miongoni mwa njama (mbali mbali) mara nyingi alikuwa akimshirikisha Hafsa binti Umar, na la kushangaza ni kwamba tunakuta kuwa maelewano na mtiririko kamili kati ya wanawake wawili Aisha na Hafsah ni kama ulivyo mtiririko (wa ushirikiano) na maelewano baina ya baba zao Abubakr na Umar, isipokuwa kwa wanawake Aisha mara nyingi alikuwa na nguvu na hana woga na ndiye mwenye kuharakia (mambo), na yeye Aisha ndiye aliyekuwa akimkokota Hafsah nyuma yake katika kila kitu, wakati huo huo baba yake (Aisha) Abubakr alikuwa dhaifu mbele ya Umar, ambapo Umar alikuwa na nguvu na hana woga na ndiye mwenye kuchukua hatua ya mwanzo katika kila kitu.

Kwa hakika tumeona katika maelezo yaliyopita kwamba (Abubakr) hata katika ukhalifa wake, Umar ndiye aliyekuwa mtawala mtendaji. Wanahistoria wamesimulia ya kwamba, Aisha alipokusudia kutoka kwenda Basra kumpiga Imam Ali(a.s) katika vita ambayo iliitwa vita ya Jamal, aliwapelekea ujumbe wakeze Mtume(s.a.w.w) akiwataka watoke pamoja naye, basi hakuna aliyekubali mwito huo miongoni mwao isipokuwa Hafsa bint Umar ambaye alijiandaa na akaazimia kutoka, lakini kaka yake Bwana Abdallah ibn Umar akamkataza na akaenda kumwita ndipo akavunja safari yake.[47] Kwa ajili hiyo basi Mwenyezi Mungu alikuwa akiwaonya Aisha na Hafsa kwa pamoja katika kauli yake aliposema: "Na kama mtasaidiana dhidi yake (Mtume) basi Mwenyezi Mungu ndiye msaidizi wake na Jibril na Waislamu wema, na zaidi ya hayo Malaika pia watamsaidia." Na vile vile kauli yake aliposema: "Iwapo mtatubia kwa Mwenyezi Mungu (itakuwa kheri kwenu) kwa hakika nyoyo zenu zimepotoka." Kwa hakika Mwenyezi Mungu aliwapigia (Aisha na Hafsa) mfano wa hatari sana katika Surat-tahrim ili Mwenyezi Mungu awafahamishe Waislamu wengine ambao wanaamini kwamba Mama huyu wa waumini ataingia peponi bila ya hesabu wala adhabu, eti tu kwa kuwa ni mke wa Mtume(s.a.w.w) . Sivyo kabisa, Mwenyezi Mungu amewajulisha waja wake wanaume kwa wanawake kwamba hali ya kuoana hainufaishi wala haidhuru mbele ya Mwenyezi Mungu, bali ni matendo ya mtu mwenye we (ndiyo yatakayomsaidia).

Mwenyezi Mungu anasema: "Mwenyezi Mungu amewapigia mfano wale waliokufuru kwa mkewe Nuhu na mkewe Lut, walikuwa chini ya waja wetu miongoni mwa waja wetu wema wawili hao (Nuh na Lut) basi (wanawake hao) wakawafanyia hiyana waume zao, hawakuweza kuwakinga kwa lolote (kutokana na adhabu) mbele ya Mwenyezi Mungu, na wakaambiwa ingieni motoni pamoja na wenye kuingia (humo). Surat-tah-riim, aya ya kumi. Mwenyezi Mungu amepiga mfano kwa wale walioamini (akamtaja) mke wa Firaun pale aliposema:

رَبِّ ابْنِ لِي عِندَكَ بَيْتًا فِي الْجَنَّةِ وَنَجِّنِي مِن فِرْعَوْنَ وَعَمَلِهِ وَنَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿١١﴾ وَمَرْيَمَ ابْنَتَ عِمْرَانَ الَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهِ مِن رُّوحِنَا وَصَدَّقَتْ بِكَلِمَاتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِ وَكَانَتْ مِنَ الْقَانِتِينَ ﴿١٢﴾

"Ewe Mola wangu! nijengee nyumba peponi na uniokoe kutokana na Firaun na matendo yake (machafu) na uniokoe kutokana na watu madhalimu. Na Mariamu binti wa Imran aliyejihifadhi tupu yake, tukampulizia humo roho yetu (inayotoka kwetu) na akayasadikisha maneno ya Mola wake na vitabu vyake na alikuwa miongoni mwa (watu) wanyenyekevu." (Qur.66:ll-12).

Kutokana na hali hii basi inabainika kwamba kuoana na urafiki japokuwa kuna ubora mwingi lakini hausaidii (chochote) kuepukana na adhabu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa (kuoana huko na urafiki) kutakapo jitambulisha kwa matendo mema, vinginevyo basi adhabu itakuwa maradufu, kwani uadilifu wa Mwenyezi Mungu ni kutomuadhibu aliye mbali ambaye hakusikia wahyi (kwa kiwango) kama cha yule ambaye Qur'an inashuka nyumbani mwake, na haitakuwa sawa adhabu ya mtu aliyeifahamu haki kisha akaipinga aadhibiwe kama mjinga ambaye hakutambua haki. Ewe msomaji sasa hivi hebu angalia baadhi ya riwaya zenye ufafanuzi ili upate kumfahamu vyema mwanamke huyu aliyechukua nafasi kubwa ya kumtenga Imam Ali kutoka kwenye Ukhalifa na akampiga vita kwa kila aina ya nguvu na vitimbi. Vile vile ili upate kufahamu kwamba ile aya ya kuondolewa uchafu na kutakaswa haimhusishi kabisa Mama Aisha kwa umbali wa masafa ya mbingu na ardhi, na kwamba Ahlu-Sunnah wengi wao ni mateka wa uharibifu na uzushi (wa Banu Umayyah) na wanawafuata Banu Umayyah hali yakuwa wao hawafahamu.

4

WAULIZE WANAOFAHAMU

UMMUL-MU'MININA AISHA ANAISHUHUDIA NAFSI YAKE

Hebu na tumsikie bibi Aisha mwenyewe analeta riwaya (inayomuhusu) na ni namna gani (tutaona) wivu ulivyo mkosesha lengo lake na kisha ni jinsi gani alionesha tabia mbaya mbele ya Mtume(s.a.w.w) .

Anasema bibi Aisha: "Safiyah mkewe Mtume alimletea Mtume(s.a.w.w) chakula alichomtengenezea wakati Mtume akiwa nyumbani mwangu, nilipomuona mjakazi (analeta chakula hicho) nilianza kutetemeka na nikashindwa kujizuwia, kisha nikaipiga sahani (ya chakula) na nikaitupa (chini). Mtume wa Mwenyezi Mungu akaniangalia na nilifahamu hasira (iliyojitokeza) usoni mwake, basi nikasema, Najilinda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu asije nilaani leo hii." Mtume akasema: "Badilisha." Nikasema, kafara yake ni kitu gani ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?" Mtume akasema, "Ni chakula kama chakula chake (kilichokuwa humu) na chombo kama chombo chake". Na kuna mara nyingine ameleta riwaya inayomuhusu yeye mwenyewe amesema: "Nilimwambia Mtume, anakutosha Safiyyah (kwa jambo) kadha wa kadha," Mtume akaniambia, "Kwa hakika umesema jambo (ambalo) lau litachanganywa na maji ya bahari lingeyaharibu." Subhanallah!!!. Ana hali gani Ummul-Muminina, yuko mbali mno na tabia njema na haki ambazo Uislamu umezifaradhisha katika kuharamisha kuteta na uzushi? Na hapana shaka kwamba kauli yake aliposema, "Anakutosha Safiyyah (kwa jambo) kadha wa kadha, na kauli ya Mtume aliposema kuwa neno hilo lau litachanganywa na maji ya bahari lingeyaharibu," jambo hilo alilolisema Aisha kuhusu mke mwenziwe Bibi Safiyyah inaonesha lilikuwa ni jambo la kutisha na lilikuwa jambo la hatari. Mimi naamini kwamba wapokezi wa hadithi waliliona kuwa ni baya na la kutisha basi wakalibadilisha kwa ibara ya "kadha wa kadha" kama ilivyo kawaida yao kwa mambo kama haya.

Huyu hapa tena Aisha Ummul-Muminina anaeleza kwa mara nyingine wivu wake kwa wakeze Mtume anasema: "Sikumuonea wivu mwanamke yeyote isipokuwa wivu huo utakuwa chini ya wivu niliomuonea "Mariyah" na hiyo ni kwa sababu alikuwa mzuri mno na Mtume wa Mwenyezi Mungu alimpenda, mwanzoni alipokuja naye alimfikishia kwenye nyumba ya Harithah ibn Nuuman, na tulitishika kutokana naye lakini mimi nilishindwa kuvumilia, ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipomuhamishia Aliyah, kisha akawa huenda huko. Jambo hilo lilikuwa zito mno kwetu sisi na Mwenyezi Mungu akamruzuku (Mtume) kutokana na Mariyah mtoto wa kiume nasi akatunyima". Kama ambavyo wivu wa bibi Aisha ulivuka mipaka kutoka kwa mke mweziwe bibi Mariyah hadi kwa mtoto mdogo Ibrahim. Aisha amesema: "Ibrahim alipozaliwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuja naye kwangu akasema, Hebu muangalie namna alivyofanana nami, basi mimi nikasema, Sioni kufanana kokote, Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: Hivi huoni weupe wake na mwili wake? Nikamwambia, Yeyote aliyenyweshwa mazima ya kondoo huwa mweupe na hunenepa". Wivu wa Mwanaisha ulivuka mipaka yote na hauelezeki hasa pale ulipomfikisha kumdhania vibaya na kumtilia wasi wasi na mashaka Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , kwani mara nyingi alikuwa akijifanya kalala wakati Mtume anapolala nyumbani kwa Aisha, lakini kumbe humchunga mumewe na kumchunguza mahali alipo katika giza na kumfuatilia popote anapokwenda. Hebu ione riwaya hii inayotoka ulimini mwa Mama Aisha riwaya ambayo ameiandika Muslim ndani ya sahihi yake na Imam Ahmad ndani ya Musnad yake na wengineo.

Amesema: "Ilipokuwa ni usiku wangu ambao Mtume(s.a.w.w) alikuwa kwangu, alirudi akaweka nguo zake, akavua viatu vyake akaviweka mbele ya miguu yake na akakunjua shuka yake juu ya kitanda chake kisha akalala, basi muda si mrefu alidhani mimi nimepitiwa na usingizi, alichukua nguo zake taratibu na akavaa viatu vyake taratibu halafu akafungua mlango akatoka kisha akaufunga mlango taratibu. Pale pale nami nikavaa nguo yangu na nikafunga shuka yangu nikatoka kumfuata nyuma yake mpaka akafika Baqii. Hapo akasimama kwa muda mrefu kisha akanyanyua mikono yake mara tatu, kisha akageuka nami nikageuka, akakaza mwendo nami nikakaza mwendo, akaongeza mwendo nami nikaongeza mwendo, alifika nami nimeshafika nikawa nimemtangulia nikaingia ndani, hakuna nilichofanya ila nililala, basi akaingia na akasema, Una nini ewe Aisha mbona unahema namna hii?. Nikamwambia, "Hapana lolote." Mtume akasema: "Lazima utaniambia vinginevyo Mwenyezi Mungu atanieleza." nikasema, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, namuapia baba yangu na mama yangu, basi nikamueleza hali ilivyokuwa. Akasema, "Wewe ndiyo ule weusi niliouona mbele yangu"? Nikasema, "'Ndiyo." Akanipiga kifuani pigo lililonipa maumivu, kisha akasema, "Hivi ulidhani Mwenyezi Mungu na Mtume wake watakudhulumu..."? Na kuna mara nyingine bibi Aisha alisema, "Nilimkosa Mtume wa Mwenyezi Mungu basi nikadhani amekwenda kwa baadhi ya wajakazi wake, basi nikamtafuta, ghafla nikamuona amesujudu hali ya kuwa anasema, "Ewe Mola nisamehe" Na mara nyingine amesema, "Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu alitoka nyumbani mwangu usiku, basi nikaona wivu, aliporudi akayaona mambo ninayoyafanya, Mtume akasema, Una nini ewe Aisha je, umeona wivu? Nikasema, kwa nini mtu kama mimi nisione wivu kwa mtu kama wewe?! Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: Hivi shetani wako kisha kuchukua? Riwaya hii ya mwisho inajulisha wazi kwamba, bibi Aisha kila alipokuwa na wivu alikuwa anabadilika kutoka katika hali yake ya kawaida na kufanya mambo ya ajabu kama vile kuvunja vyombo au kuchanachana mavazi.

Na ndiyo maana katika riwaya hii anasema, "Mtume alipokuja na akaona ninayoyafanya akasema, hivi shetani wako kisha kuchukua"? Hapana shaka kwamba shetani wa Aisha alikuwa akimchukua na kumzingira mara nyingi, na (shetani huyo) aliukuta moyo wa Aisha kuwa ni njia miongoni mwa njia za wivu. Imepokewa toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema kwamba: "Wivu kwa mwanamume ni imani na kwa mwanamke ni kufru. " Tafsiri yake ni kwamba: mwanamume anamuonea wivu mkewe kwa kuwa kisheria haifai awe na mshirika yeyote kwa mke huyo, ama mwanamke hana haki ya kuwa na wivu kwa mumewe kwa kuwa Mwenyezi Mungu amemruhusu mwanamume kuoa zaidi ya mke mmoja. Basi mwanamke mwema anayefuata hukumu za Mwenyezi Mungu Mtukufu humpokea mke mwenziwe kwa moyo mkunjufu, kama isemwavyo leo hii hasa pale mumewe akiwa muadilifu mwenye msimamo na anamuogopa Mwenyezi Mungu. Je, nini fikra yako kuhusu uadilifu na msimamo wa Bwana aliyembora wa utu na kigezo cha ukamilifu, uadilifu na tabia njema? Sisi tunakuta kuna tofauti bayana kuhusu penzi la Mtume kwa Aisha na vile wasemavyo Ahlus-sunnah Wal-jamaa, eti kwamba Aisha alikuvva ni kipenzi mno kwa Mtume kuliko wakeze wengine, na kwamba alikuwa bora mno mbele yake mpaka kiasi wanaleta riwaya kwamba baadhi ya wake za Mtume walizitoa nauba zao (siku anazostahiki Mtume kuwa kwao) kwa Aisha walipofahamu kwamba Mtume(s.a.w.w) anampenda mno bibi Aisha na havumilii kumkosa!!!. Je, hivi kweli inawezekana katika hali kama hii (tuliyoeleza juu ya Mama Aisha tukampata mtu kuutakasa na kuupa tafsiri (nyingine) wivu wa bibi Aisha usiokuwa na kipimo?

Ukweli unavyoonekana, ni kinyume cha alivyokuwa akifanya bibi Aisha, kwani wake wengine wa Mtume wao ndiyo wangestahiki kumuonea wivu Aisha kwa kuwa Mtume kampenda mno na kuegemea kwake kama wanavyodai na kueleza katika riwaya. Sasa, ni kitu gani kinachohalalisha wivu wa bibi Aisha.?

Historia haikusimulia isipokuwa hadithi zake na vitabu vya Sirah vimejaa sifa zake na kwamba yeye ndiye kipenzi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu, mwenye kujipendekeza ambaye Mtume alikuwa hawezi kutengana naye. Mimi naitakidi kwamba, yote hayo yametokana na Banu Umayyah ambao walimpenda bibi Aisha na wakamtukuza pale alipoyatumikia maslahi yao na akawatengenezea riwaya za yale wayapendayo, pia alimpiga vita adui yao Ali ibn Abi Talib(a.s) . Mimi naamini kwamba, Mtume(s.a.w.w) hakuwa akimpenda Aisha kutokana na hayo aliyomtendea, kama tulivyotangulia kueleza!! Basi itakuwaje Mtume wa Mwenyezi Mungu ampende mtu ambaye ni muongo, anateta, kufitinisha na kumtilia mashaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kuwadhania kuwa wanafanya dhulma? Itakuwaje basi Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ampende mtu ambaye anampeleleza na anatoka nyumbani mwake bila ruhusa ya Mtume ili tu atake kufahamu Mtume anakwenda wapi?

Itakuwaje kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ampende mtu ambaye anawatukana wakeze mbele yake japokuwa wamekwisha kufa? Ni vipi Mtume atampenda mtu ambaye anamchukia mwanawe Ibrahim na kumsingizia mama wa Ibrahim bibi Mariyah kuwa katenda dhambi?" Ni vipi Mtume wa Mwenyezi Mungu atampenda mtu anayejiingiza kati ya Mtume na wakeze kwa kuzua uongo na mara nyingine kueneza chuki na kusababisha Mtume kuwataliki wakeze? Itakuwaje basi Mtume wa Mwenyezi Mungu ampende mtu ambaye anamchukia binti yake Fatmah, na anamchukia nduguye Mtume na mtoto wa ami yake Ali ibn Abi Talib kiasi kwamba (bibi Aisha anashindwa kulitamka jina la Imam Ali, na wala tu nafsi yake haimfurahii Ali kwa wema. Yote haya na zaidi ya haya yalifanyika katika zama za uhai wa Mtume(s.a.w.w) , ama baada ya kufa kwake, na ni haki yasimuliwe wala hapana ubaya. Matendo yote haya Mwenyezi Mungu na Mtume wake waliyachukia na wala hawakumpenda aliyeyatenda, kwani Mwenyezi Mungu yeye ndiye haki na Mtume wake alikuwa akiitekeleza haki hiyo, hivyo basi hawawezi kumpenda mtu asiyekuwa kwenye haki.

Hapo baadaye kwa kupitia utafiti uliotangulia tutafahamu kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alikuwa hampendi Bibi Aisha, bali alipata kuutahadharisha ummati wake kutokana na fitina ya bibi Aisha. Kuna wakati fulani niliwauliza baadhi ya Masheikh sababu za Mtume(s.a.w.w) kumpenda kupita kiasi Bibi Aisha peke yake kuliko wake wengine, walinipa majibu mengi na yote hayo hayakuwa na maana yeyote. Mmoja wao alisema: "Kwa kuwa Aisha alikuwa mzuri kisha mdogo na ndiye bikra pekee ambaye Mtume alimuoa na nakushirikiana na mwingine kwa bibi Aisha ila yeye Mtume peke yake". Mwingine akasema, "Kwa kuwa alikuwa ni binti ya Abubakris -Sidiq ambaye alikuwa pamoja na Mtume pangoni". Wa tatu alisema: "Hiyo ni kwa sababu Mama Aisha alihifadhi nusu ya dini kutoka kwa Mtume, kwa hiyo ni mjuzi mwenye kufahamu". Na wanne alisema, "Ni kwa sababu Jibril alipata kuja akiwa katika sura yake (bibi Aisha) na Jibril alikuwa haji kwa Mtume ila Mtume awapo nyumbani kwa Aisha".