• Anza
  • Iliyopita
  • 4 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 4227 / Pakua: 719
Kiwango Kiwango Kiwango
SHADA LA MAUA KUTOKA BUSTANI YA AHADITH

SHADA LA MAUA KUTOKA BUSTANI YA AHADITH

Mwandishi:
Swahili

SHADA LA MAUA KUTOKA BUSTANI YA AHADITH ZA MTUME (s.a.w.w) NA AHLUL - BAYT(A.S)

ZIMEKUSANYWA NA KUTARJUMIWA NA: AMIRALY M.H.DATOO

UTANGULIZI

Allah swt anatuambia katika Al-Qur'an tukufu: Sura al-Nahl, 16 Ayah 43 na Sura Al-Ambiya,21 Ayah:7, Ayah hii Tukufu inawasihi Waumini kujielekeza kwa Ahl-Dhikr; yaani watu wenye busara na Wanazuoni wa Ummah ili kuweza kubainisha baina ya haki na batili, wakati ambapo Waumini wanapokumbana na shida au ugumu katika masuala mbalimbali, kwa sababu Allah swt baada ya kuwafundisha ilimu, aliwachagua hao kwa hayo. Hivyo, wao wamebobea katika ilimu na ambao ndio watu halisi wanaoielewa, kuifundisha na kuitekeleza kwa usahihi mafunzo ya Qur'an. Ayah hii iliteremshwa kwa ajili ya kuwatambulisha Ahlul-Bayt(a.s) nao ni Mtume Muhammad(s.a.w.w) , Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , Fatimah(a.s) , Al-Imam Hassan ibn Abi Talib(a.s) na Al-Imam Husayn ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , ambao kwa ujumla wanaitwa Watukufu watano au 'Ali-'Aba ambapo pamoja na hao wameongezeka Ma-Imamu(a.s) wengine tisa kutokea kizazi cha al-Imam Husayn ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) Mtume(s.a.w.w) mara nyingi katika nyakati mbalimbali aliwatambulisha hao kuwa ni Ma-Imam waongozi, nuru katika kiza, na ni wale ambao wamebobea katika ilimu na bila shaka Allah swt amewajaalia Ilimu ya Kitabu Kitukufu.

Ukweli huu, kama ilivyorejewa mahala pengi katika Ahadith mbalimbali kuanzia zama za Mtume(s.a.w.w) kuanzia ufunuo hadi leo hii, na vile vile wanazuoni wengi na Wafasiri kutokea Ahl-Sunnah wamekiri waziwazi katika vitabu vyao kuwa Ayah hizi za Qur'an zilikuwa zimeteremshwa hususan kwa ajili ya kuelezea na kuwatambulisha Ahl-ul-Bayt(a.s) Baadhi ya mifano ya vitabu vyenyewe ni kama ifuatavyo:

1. Imam Tha'labi katika tafsiri ya kitabu chake juu ya Ayah hiyo ya 42 kutokea Sura An-Nahl, namba 16.

2. Tafsir ibn Kathir, j.2, uk.591.

3. Tafsir at-Tabari, j.14, uk.75.

4. Tafsir-i-Alusi, ijukanavyo kama: Rahul-Bayan , j. 14, uk. 134.

5. Tafsir-i-Qartabi, j.11, uk. 272.

6. Tafsir-i-Hakim, au Shawahid-ut-Tanzil, j. 1, uk. 334

7. Tafsir-i-Shabistrary, au: Ihqaq-ul-Haq, j.3, uk.482

8. Yanabi'-ul-Muwaddah, cha Ghanduzi Hanafi, uk. 119

Kwa kutegemea ukweli huu, sisi lazima tujielekeze kwa Wananyumba ya Ahlul-Bayt(a.s) , na kutekeleza maneno yatuongozayo ili kuelekeza maisha yetu mema. Kwa sura hii, Imamul-Hadi(a.s) anasema katika Man la Yahdhuruhul-Faqih, Tahdhib na 'Uyuni-Akhbarur-Ridha: "Maneno yenu yenye busara yanatupa nuru, maamrisho yenu ni hidaya kwa watu na usia zenu ni Taqwa na usawa. "

MUWE TAHADHARI ENYI WASOMAJI

Kwa kupitia Watuku hawa ndipo sisi tunaweza kuokoka humu duniani na Aakhera na maisha yetu yakawa mema na salama. Twapata katika Man la Yahdhuruh-ul-Faqih, Tahdhib na 'Uyuni Akhbar-ur-Ridha: "Ni kwa sababu yenu Allah swt ametutoa nje ya upotofu (wa ukafiri), ametufanya huru kutoka huzuni na masikitiko, na kutuchukua pa usalama dhidi ya maangamizo ya dunia na mioto ya Jahannam pia. "

Katika katika Man la Yahdhuruhul-Faqih, Tahdhib na 'Uyuni Akhbarur-Ridha twasoma: "Ni kwa sababu ya Ukuu na uongozi wenu kuwa Allah swt ametufundisha ilimu ya kanuni za Dini , na kuweka sawa na vyema yale yote yaliyovurugika na kufasidika katika dunia. (Naye ametuepusha na umasikini, udhalilifu na ujahili, na kututunukia ilimu, heshima na hadhi.) Kwa hakika, iwapo sisi tutawaacha hawa watukufu waliobarikiwa na kutukuzwa na Allah swt, basi hakuna shaka kuwa tutatumbukia katika upotoshi na maangamizi katika kila hali. Ndipo Mtume(s.a.w.w) amesema: "Mfano wa Ahlul-Bayt (a.s) wangu ni sawa na Safina ya Mtume Nuhu (a.s) Yeyote yule atakaye ipanda basi kwa hakika ameokoka na yeyote yule atakayekhilafu kuipanda, basi kwa hakika amezama na kutokomea mbali ."

Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Inawezekana nikaitwa hivi karibuni nami nikaitikia. Hivyo, mimi ninawaachieni vizito viwili: Kitabu cha Allah swt (yaani Qur'an) ni kamba iliyovutika kutoka mbinguni hadi ardhini, na Ahlul-Bayti (a.s) wangu; kwa hakika Allah swt, Mrehemevu, Mwenye kuwa Makini, amenijulisha kuwa kamwe, kamwe vitu hivi viwili havitatengana hadi kukutana na mimi hapo Hawdh-Kauthar (Chemchemi ya milele). Hivyo, muwe waangalifu mutakavyojishikiza navyo wakati ambapo mimi sitakuwapo. "

Na vile vile katika Hadith nyingineyo imeongezeka: "Kamwe, kamwe, hamtapotoka iwapo mutakuwa mumeshikamana navyo hivi vitu viwili. " Hivyo, je ni heshima gani itakayopita kuliko Qur'an, Mtume(s.a.w.w) na Ahlul-Bayt (a.s) vikawa ni mifano yetu, waalimu na viongozi wetu ? Na kwa sababu hizi ndipo sisi kwa moyo halisi na unyenyekevu tunasema: Sisi tumefadhilika kwa sababu sisi ni wafuasi wa Madhehebu ambayo muasisi wake Mtume Muhammad(s.a.w.w) na Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) (mja ambaye amekombolewa kutokana na minyororo ya udhalili na kuchaguliwa kuwa mkombozi wa binadamu wote kutoka utumwa mbali na ule wa Allah swt ) kwa kufuata mwongozo kutoka Allah swt.

Sisi tumetukuzwa kwa kuwa na kitabu kitakatifu cha Nahjul-Balagha, ambacho ni kitukufu baada ya Qur'an Tukufu, chenye maandiko matukufu kwa ajili ya maisha yetu wanaadamu, ni kitabu kikubwa kwa ajili ya ukombozi wa mwandamu na maelekezo yake ya kiroho na kisiasa yanayo thamani kubwa kwa ukombozi na kimeandikwa na Ma'sum Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) Vile vile tumebarikiwa kwa Imam Al-Mahdi(a.s) atokanaye na Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) yu bado hai na kwamba anahabari na kujua habari zetu zote. Sisi tumebarikiwa kuwa na Doa ambazo ndizo zilizofunzwa na Ma-Imam(a.s) kama Dua za Sha'baniyyah, Dua ya 'Arafah ya al-Imam Husayn ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , Sahifa-i-Sajjadiyah ya al-Imam Zaynul-'Aabediin(a.s) , na Sahifa - Fatimah. Vile vile sisi tumebarikiwa kuwa na Mwanazuoni mkubwa katika zama zetu ambaye hawezi kueleweka kwa watu wengine isipokuwa Allah swt, Mtume(s.a.w.w) na Ma-Imamu(a.s) kwa sababu ya kipaji chake kikubwa cha ilimu na hekima.

Vile vile sisi tumebarikiwa kwa kuitwa Madhehebu ya Ja'afariyyah na kwamba Fiqh ambayo ni bahari isiyo na mwisho (ya ilimu), ambayo ni mchango mmojawapo wa al-Imam(a.s) Sadique(a.s) Vile vile sisi tunafakhari kubwa sana kwa kuwa na Ma-Imamu(a.s) wote, na tunawafuata kikamilifu. Sisi tumebarikiwa kwamba Maimam(a.s) wetu walikuwa wameteswa, kuwekwa mahabusu na vile vile kutolewa makwao kwa sababu wao walikuwa daima wamejitolea muhanga kuutetea ubinadamu na kuinua hali ya Dini ya Islam na kuyatekeleza maamrisho ya Qur'an yakiwemo maamrisho ya kutengeneza Serikali adilifu na hatimaye hao Ma-Imamu a.s. waliuawa katika harakati zao za kutokomeza serikali dhalimu na Taghuti katika kila zama. Sasa, ewe mpenzi kaka na dada! Wewe ni shahidi wa macho, katika dunia hii ndogo, ndogo zaidi kuliko kijiji katika ulimwengu, unajionea kuwa hali ya binadamu inaendelea ipo inateketea katika jangwa la dhuluma na pasi na haki, wakati mwanadamu huyo yupo anatumbukia chini zaidi katika matingatinga ya kutokuhurumiwa na kukosekana kwa uadilifu.

Wale wote wanaojidai kuhusu uhuru na raha ya mwanadamu wanashuhudia kwa makini kumomonyoka kwa maadili katika mazingira waliyoyaumba wao wenyewe. Wao hawana tena uwezo wa kudhibiti hali hiyo isipokuwa kuangamia kwa binadamu na ubinadamu. Lakini, je ni kweli kuwa huo ndio mwisho wa mstari huo?

Jibu kwa kushangaa litakuwa ndiyo, hadi hapo mwanadamu atakaporejea katika uumbwaji kwake wa kimungu, akimulika makosa na kasoro zake zilizopita kama ndiyo tochi kwa maisha yake ya mbeleni na akiitumia Islam kama ndiyo dawa ya matatizo yake yote. Katika zama hizi, Islam ambayo ndiyo tukufu, na bora kabisa katika kutuongoza, bora katika katika historia, imetoa mikono yake kwa ajili ya kumnusuru mwananadamu ili asije akazama na kughalibiwa na maovu na kwa baraka za Allah swt, imesimama imara kumtibu mwanadamu dhidi ya magonjwa maovu kabisa ya maovu.

Islam ipo kwa ajili ya kutuliza kiiu cha mwanadamu anayezurura katika majangwa ya chumvi kali zisizo na taqwa kwa kumnywisha maji matamu na baridi ya itikadi zilizonurishwa kwa ilimu na maarifa na utukufu wa Ahlul-Bayt(a.s) , ambayo ndiyo sura halisi ya tafsiri kamili ya ufunuo ambayo kamwe haikuwa na kosa au kasoro ya aina yoyote ile. Inatoa mwanga kwa hali zote na kimwili na kiroho ya maisha ya mwanandamu. Hivyo, imefungua milango kikamilifu kwa mwanadamu kukamilika kikamilifu. Lakini Ewe rafiki mpendwa Ni jambo la muhimu na kwanza kabisa kwa kutaka kujua habari za shule yoyote ile pamoja na mafunzo yake, inatubidi sisi kutazama kwa undani maandiko na kuelewa mazungumzo na maneno ya viongozi wake. Na kwa njia hii ndipo sisi tutakapoweza kujua kuhusu itikadi na imani na malengo ya shule hiyo kuhusu dunia na matatizo yake na hivyo kuweza kufikia maamuzi na makisio ya upeo wake. Al-Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) amesema katika Bihar al- Anwar j.2, uk.40; Ma'aniy-ul-Akhbaar, cha Saduq, uk.180; na WasAilu al-Shiah', j. 27, uk. 92: "Rehema za Allah swt zimfikie mja ambaye huisha maamrisho yetu " Nami nilimwuliza ni vipi mtu anaweza kuziweka hai maamrisho yenu? Imam(a.s) alijibu: "Yeye anaweza kujifunza ilimu na maarifa yetu na kuwafundisha wengineo. Kwa hakika, iwapo watu watazijua faida na mema za miihadhara na misemo yetu, basi kwa hakika watazifuata kuzitekeleza. "

Matumaini mema Twategemea kuwa msomaji kwa kuyasoma na kuyazingatia maneno yenye thamani isiyosemekana, kuwa kwa kupitia maneno na maongozao ya Ahlul-Bayt(a.s) vizazi vyetu hususan vijana wataongoka na kamwe hawatapotoka wala kuvutiwa na mavutio yanayotuongoza kuelekea maangamizo ya milele na kwamba utamaduni wetu hautamomonyoka siku baada ya siku na badala yake tutatengeneza utamaduni wetu uwe utamaduni wa Kiislamu kwa baraka na miongozo za Ahlul-Bayt(a.s) na kwamba tutakuwa washupavu na maaskari kulinda imani na Din ya Islamu dhidi ya maadui wake walio ndani na nje. Tutakuwa Waislamu bora na mfano kwa watu wote. Amani na Salaam ziwafikie wale wote waliongoka.

HADITH YA UFUNGUZI

1. Amesema al-Imam Zayn al-'Aabidiin(a.s) katika Bihar al- Anwar, j.90, uk 187, na Sahifah as-Sajjadiyyah, uk. 572: "Sifa zote ni za Allah swt, na kusiwa Kwake ni haki Yake: sifa zisizo na kifani ndizo zinazomstahiki Yeye. Na mimi najiepusha kwa msaada wake dhidi ya shari za nafsi yangu: Kwa hakika mwanadamu yupo katika kutenda madhambi isipokuwa wale waliobarikiwa na Mola wao. Naomba msaada wake Allah swt dhidi ya maovu ya Shaitani ambaye daima ananiongezea dhambi moja juu ya lingine. Naomba msaada wake Allah swt dhidi ya watawala waovu, watawala katili, na maadui wa nguvu." "Ewe Mola! Naomba unifanye mimi kuwa mmoja wa Majeshi yako, kwa sababu kwa hakika Majeshi Yako tu ndiyo yenye kushinda; na unifanye miongoni mwa wanachama Wako, kwani kwa hakika, chama Chako tu ndicho kitakachofanikiwa; na unikubalie kama mmoja wa wapenzi Wako, kwani kwa hakika, wapenzi wa Allah swt hawana hofu na kamwe hawatahuzunika. "

"Ewe Mola! Naomba uniimarishie Dini kwa ajili yangu, kwani hiyo ndiyo hifadhi ya matendo yangu yote; na unitengenezee Aakhera yangu, kwa sababu hakuna shaka kuwa hiyo ndiyo mwisho wangu wa kudumu na kuepukana na watu wenye dharau na dhihaka, na uyafanye maisha yangu yawe ya kuniongezea mema, na mauti yangu yawe ndiyo kujitoa huru kutokana na kila aina ya kasoro za magonjwa." "Ewe Mola! Mbariki Mtume Muhammad(s.a.w.w) , Mtume wa mwisho katika jamii ya Mitume yote, na Ahli Bayti(a.s) tukufu, na vile vile Masahaba wake wema, na naomba unijaalie mahitaji matatu kwa leo: Usinibakizie dhambi lolote lile isipokuwa umenisamehe na wala huzuni yoyote ile isipokuwa umeniondolea, wala kusikwapo na adui isipokuwa wewe umemwondosha kwa jina lako tukufu la Allah ambayo ni jina bora kabisa i.e.Bismillah, Mola wa Mbingu na Ardhi .."

KUMJUA ALLAH SWT, UKUU NA BARAKA ZAKE

2. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) katika Al-Khisal, 322 "Enyi Watu ! Kwa hakika hakutakuwapo na Mtume baada yangu, na wala hakutakuwapo na Ummah baada yenu (Waislamu). Hivyo, Muwe waangalifu katika kumwabudu Allah swt, musali sala tano za siku, mufunge saumu katika mwezi uliowekwa (Ramadhaan al-Mubarak), mufanye Hijja ya Nyumba ya Allah swt (Al-Ka'aba huko Makkah al-Mukaramah), mutoe Zaka kutoka mali zenu kwa ajili ya kuitakasisha nafis zenu kwa hayo, na mutii amri za Wale wenye mamlaka, ili muweze kuingia Pepo ya Mola wenu. "

3. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema katika Nahjul-Balagha,Semi no.129: "Kwa kuwa na tasawwuri ya Ukuu wa Mola wako basi itakufanya wewe utambue udogo wa viumbe katika mitazamo yako. "

4. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema katika Bihar al- Anwar, j. 77, uk. 289: "Tawba ni kwa ajili ya yule ambaye ametakasisha kwa ajili ya Allah swt matendo, ilimu, mapenzi, bughudha, kuchukua, kutoa, misemo, ukimya, matendo na asemavyo. "

5. Amesema al-Imam Sadique(a.s) katika Bihar al- Anwar, j. 70, uk. 25: "Moyo ni mahala pa takatifu ya Allah swt, hivyo, basi hakikisha hapawi kitu kingine chochote isipokuwa Allah swt tu. " (Moyo mtukufu ni wa Allah swt tu. Hivyo mapenzi ya dunia isivyo sahihi, lazima iwekwe mbali.)

6. Amesema al-Imam Sadiq(a.s) katika Bihar al- Anwar,j. 93, uk. 162: "Wafuasi wetu ni wale ambao wanapokuwa peke yao, wanamkubuka Allah swt kwa kupita kiasi. " (Kwa hivyo, wao hujiepusha kutenda madhambi wanapokuwa peke yao wakati ambapo kuna hakuna kizuizi cha kuwazuia wao wasitende madhambi na badala yake humkumbuka Allah swt kwa kupita kiasi.).

7. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) katika Al-Kafi, j.2, uk. 426: "Kwa kiapo cha Allah swt! Yeye, aliyetukuka, huwategemea kwa mawili:wao waungame na kushukuru Kwake kwa neema ili Yeye awaongezee wao; na waungame kwa madhambi yao ili kwamba Yeye awasamehe madhambi yao. "

8. Amesema al-Imam Husayn ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) katika Safinat-ul-Bihar, j.2, uk. 180: "Kwa hakika, Allah swt, aliye Mkuu, hakuwaumba wanadamu isipokuwa kwa kumjua Yeye na baada ya kumjua Yeye kumwabudu kwa kumjua Yeye; na wakati wanapomwabudu basi kusikuwepo na haja tena ya kumwabudu yeyote mwingine isipokuwa Yeye peke yake. "

9. Amesema al-Imam Zayn-al-'Aabediin(a.s) katika Safinat-ul-Bihar, uk. 517 "Hakuna maangamizo (Jahannam au Motoni ) kwa ajili ya Mumiin aliye na sifa tatu : Kuungama na kukubali kuwa hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu peke yake, pekee ambaye hana mshiriki; Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni mtetezi; ukubwa usio na kipimo cha Rehema za Allah swt. "

SALA NA ATHARI ZAKE

10. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) , katika Man la Yahdhurul Faqihi, J.1, Uk. 206: "Mtu yeyote aichukuliaye sala pasi na uzito wake, basi si hatokani nami. Hapana, Kwa kiapo cha Allah swt, mtu kama huyo hatafikia chemchemi ya Haudh Kawtha. "

11. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , katika Bihar al-Anwaar, Juzuu 82, Ukurasa 236: "Iwapo kutakuwapo na mto unaopita nyumbani mwa mtu ambamo mtu huyo anaoga mara tano kwa siku, je kutabakiapo aina yoyote ya uchafu mwilini mwake? Kwa hivyo sala ndivyo ilivyo mfano wa mto huo. Mtu ambaye anasali sala zake basi hujiondolea madhambi yake yote isipokuwa kutabakia madhambi yale ambayo yanamtoa katika Imani yake .

12. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) , katika Bihar-ul-Anwaar, J.99, uk. 14: "Sala iliyofaradhishwa kwa Allah swt ni sawa na kutimiza Hajj elfu moja na 'Umrah elfu moja ambazo ni sahihi na zilizokubalika. "

13. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) , katika Bihar-al-Anwaar, J.83, Uk. 14: "Kamwe musizipoteze sala zenu, kwa hakika, mtu yeyote anayezipoteza nyakati za sala zake atainuliwa pamoja na Qarun na Hamaan na itamwia haki Allah swt awatumbukize katika moto wa Jahannam pamoja na Munafiqiin (wanafiki) .

14. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) , katika Bihar-ul Anwaar,Juzuu 69, Uk. 408: "Musali sala zenu kama kwamba hiyo ndiyo sala yenu ya mwisho ".

15. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Ali ibn Abi Talib(a.s) ,katika Tasnif-I- Gurar ul-Hikam, uk.175: "Iwapo mwenye kusali angalikuwa akifahamu kiasi alichozungukwa na rehema za Allah swt, basi kamwe asingaliinua kichwa chake kutoka hali ya kusujudu ".

16. Amesema Al-Imam Al-Muhammad al-Baqir(a.s) , katika Bihar al-Anwaar, J.7, Uk. 267: "Siku ya Qiyama, jambo la kwanza litakalo hisabiwa ni kuhusu sala; kwa hivyo, iwapo itakuwa imkubaliwa, basi matendo mengine pia yatakuwa yamekubaliwa (amasivyo matendo yake mengine mema hayatamnusuru) ".

17. Amesema Al-Imam Al-Sadiq(a.s) , Bihar Al-Anwaar, J.82, Uk. 236: Katika siku za mwishoni mwa maisha yake, Imam As-Sadiq(a.s) aliwaita jamaa na wafuasi wake na kuwaambia "Kwa hakika, Uokovu wetu hautamfikia yule aichukuliaye sala kiepesi (bila ya kuichukulia kuwa ndiyo fardhi na lazima)".

18. Amesema Al-Imam Al-Muhammad al-Baqir(a.s) , Al-Khisaal cha Sadduq, uk. 432: "Yapo mambo kumi ambayo mtu atakapokutana na Allah swt siku ya Qiyama ataingia Peponi: Kuamini na kukiri kuwa hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt, Na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah swt Kukiri na kuamini kuwa kile kilichoteremshwa juu ya Mtume Muhammad(s.a.w.w) kutokea Allah swt ni Qur'an tukufu, Kutimiza sala Kutoa Zaka Kufunga saumu mwezi wa Ramadhani, Kuhiji Makkah, Kuwatendea mema wale wampendao Allah swt, Kujiepusha na maadui wa Allah swt, Na kujiepusha mbali na ulevi wa kila aina.

19. Amesema Al-Imam Amirul-Muminiin Ali ibn Abi Talib(a.s) katka Nahjul Balagha, Msemo 136: "Kwa kila mwenye kusali, sala ndiyo sababu kubwa ya kumfanya amkaribie Allah swt,; na kwa yule aliye dhaifu, Hajj - kuhijji Makkah - ni sawa kabisa na Jihadi - kupigana katika njia ya Allah swt. Kwa kila jambo kuna zaka yake, na hivyo zaka ya mwili ni saumu. Jihadi ya mwanamke ni kuwa mwenzi mwema wa mume wake. "

20. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) , 'Irshad-ul-Qulub, uk. 53: "Hakuna usiku unaopita isipokuwa Malaika wa Mauti huwaita 'enyi watu wa maqaburi!' na huwauliza kile kinachowasikitisha kwa siku hiyo kwa yale waliyoyaona na maisha yajayo. Kwa hayo wafu husema 'kwa hakika, sisi twasikitika na kuwaonea wivu muminiin wale ambao wapo misikitini mwao ambapo wao wapo wansali wakati sisi hatusali; wao wanatoa zaka wakati sisi hatutoi; wao wanafunga mwezi wa Ramadhan wakati ambapo sisi hatufungi; wao wanatoa misaada kwa kile walichonacho ziada ya familia yao, wakati sisi hatufanyi hivyo . "

21. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) , Mustadrakul-Wasa'il, J.3, Uk.102: "Kwa kila wakati uliyofanywa muayyan kwa ajili ya sala , mimi huwa ninamsikia mpiga mbiu ambaye huita na kusema 'Enyi wana wa Adam ! Dumisheni sala ili muweze kuuzima moto ambao nyinyi wenyewe muliuwasa kwa ajili yenu (kwa kutenda madhambi). "

22. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) Bihar-ul-Anwaar, J.82, Uk.202: "Lazima muwe waangalifu wa Sala, kwani siku ya Qiyama Allah swt atakapomsimamisha mja wake (kwa hisabu) basi jambo la kwanza la kuulizwa litakuwa ni kuhusu Sala. Iwapo mtu atakuwa amekujanayo kamilifu, basi atakuwa miongoni mwa watu waliookoka, ama sivyo, atatupwa Motoni (Jahannam). "

23. Abu Basir amesema kuwa yeye alimtembelea Ummi-Hamidah (mama yake Imam Musa ibn Ja'afar(a.s) kwa ajili ya kumpa pole kwa kifo cha Ja'afar ibn Muhammad(a.s) Yeye alilia na hivyo yeye pia alilia kwa sababu ya kilio cha mama huyo. Baadaye, mama yake al-Imam(a.s) alisema: "Ewe Aba Muhammad! Iwapo ungalikuwa umemwona Ja'afar ibn Muhammad alipokuwa kitandani wakati wa kufariki, basi ungalikuwa umejionea mambo ya ajabu kabisa: Yeye alifumua macho yake na kutaka majamaa wote wakusanywe.' Na hapo yeye aliendelea kusema kuwa majamaa wote walikusanyika bila ya kubaki mtu. Hapo al-Imam (a.s) alisema kwa kuwaangalia wote: "Kwa hakika, Uokovu wetu hautamfikia yule aichukuliaye Sala kiepesi (bila ya kuichukulia kuwa ndiyo fardhi na lazima) " Wasa'il-ush-Shiah, J.4, Uk. 26.

24. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) , Bihar-ul-Anwaar, J.84, Uk.258: "Ibada ya yule mtu ambaye mapato yake yanatokana na njia zilizo haramu ni sawa na kujenga nyumba juu ya mchanga. "

SALA ZA USIKU WA MANANE

25. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) , Bihar-ul-Anwaar, j.77, uk. 20: "Heshima ya Mumiin ipo katika kukesha kwake usiku na utukufu wake upo katika kujitawala mwenyewe miongoni mwa watu. "

26. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Ali ibn Abi Talib(a.s) , Ghurar-ul-Hikam, uk. 289: "Yeyote yule alale zaidi wakati wa usiku, lazima atapoteza kitu mujimu kabisa katika matendo yake (sala ya usiku) ambayo hataweza kuipata wakati wa mchana. ".

27. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , Bihar al- Anwar , J. 13, Uk. 329 Allah swt katika ufunuo wake kwa Mtume Musa(a.s) , mwana wa 'Imran(a.s) alisema: "Ewe Mwana wa 'Imran! Wale tu ambao wanadai kunipenda mimi, wasema uongo, kwani usiku unapoingia wao hulala huku wakiniacha mimi. ".

28. Amesema al-Imam as- Sadique(a.s) , Bihar al- Anwar ,J.83, Uk. 127: "Kamwe usiikose Sala ya usiku wa manane! Kwa sababu, ukweli ni kwamba, mpotezaji ni yule anayeikosa (faida zake) Sala za usiku wa manane. "

29. Amesema al-Imam as- Sadique(a.s) , Khisal cha Sadduq, Uk. 72 Mtume(s.a.w.w) alimwambia Jibrail amwambie chochote, naye alimwambia: "Ishi utakavyo huku ukitambua kuwa utakuja kufa; penda chochote kile utakacho lakini utatengana nacho; tenda utakavyo lakini utakutana nacho ( na kulipwa malipo yake). Heshima ya Mumin ni Sala yake ya Layl (usiku wa manane), na utukufu wake upo katika kujiepusha (na kuangamiza) sifa za watu. "

30. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , Bihar al- Anwar , j.75, Uk. 107 "Vipo vitu vitatu ambavyo ndivyo sifa za Muumin na ndivyo vito vya thamani kwake humu duniani na Aakhera. Navyo ni: Sala katika sehemu ya mwisho wa usiku (Salat ul-Layl), kutotamani au kuwa na wivu kwa kile kidogo kilicho mikononi mwa watu, na mapenzi (na uongozi ) wa Imam kutokana na kizazi cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) "

31. Amesema al-Imam Muhammad ibn Ali al-Jawad ul-'A'immah(a.s) , Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 79 "Yeyote yule aliye na imani kamili juu ya Allah swt, anaona furaha; na yeyote amwaminiaye, basi anatosheleza matendo yake. "