• Anza
  • Iliyopita
  • 4 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 8468 / Pakua: 3460
Kiwango Kiwango Kiwango
SHADA LA MAUA KUTOKA BUSTANI YA AHADITH

SHADA LA MAUA KUTOKA BUSTANI YA AHADITH

Mwandishi:
Swahili

1

1

BUSTANI YA AHADITH ZA MTUME (s.a.w.w) Na AHLUL - BAYT(A.S)

KUMWAMINI ALLAH NA KUIPATA FURAHA YAKE

32. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , Biharu al-Anwaar, J. 71, Uk. 208: "Baba yangu aliniambia kuhusu baba yake kuwa mtu mmoja kutoka mji wa Kufa alimwandikia baba yake viz. Al-Husayn ibn Ali(a.s) , akimwuliza(a.s) kumjulisha yeye kuhusu mema ya dunia hii na mema ya Akhera. Kwa hayo Imam(a.s) alimwandikia (katika majibu): "Kwa jina la Allah,aliye Rahmaan na Rahiim'. Baadaye akiendelea 'Kwa hakika yeyote yule atakaye furaha ya Allah swt hata wakati wa kutokuwafurahisha watu, Yeye humtosheleza katika masuala ya watu. Lakini, yule ambaye hutaka furaha za watu wakati anamuudhi Allah swt, basi Allah swt humwachia watu ( na yeye atakuwa mbali na baraka za Allah swt), Wassalaam'. "

33. Amesema Al-Imam Zayn Al-Abedin(a.s) , Al-Kafi, J.2, Uk.81: "Yeyote yule atendaye matendo yake kwa mujibu wa vile alivyoamrisha Allah swt, ni miongoni mwa watu bora. "

34. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , Al-Kafi, J.2, Uk. 124: "Yeyote yule aliye na mapenzi ya Allah swt,anachukia kwa ajili yake Allah swt, na anatoa msaada kwa ajili ya Allah swt, basi huyo ni miongoni mwa wale ambao Imani yao imekamilika. "

35. Amesema Al-Imam Al-Hasaan Al-Askari, Imam wa Kumi na Moja, a.s. , Biharu al-Anwaar, J.17, Uk. 218: "Hakuna sifa zaidi ya hizi mbili: Kuwa na Imani kwa Allah swt na kuwa mwenye manufaa kwa Waislamu. "

TAQWA NA UMUHIMU WAKE KWA WAISLAMU

36. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) , Bihar al- Anwar J. 71, Uk. 373: "Miongoni mwa kitu kilicho muhimu kabisa kwa kuwafikisha watu hadi kufikia Peponi ni taqwa na tabia njema ."

37. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) , Bihar al- Anwar ,J.77, Uk. 130: "Wakati wa kutoa uamuzi wa kitu, fikiria matokeo yake. Iwapo ni nzuri kwako wewe kuendelea na maendeleo, fuata hivyo, lakini iwapo inakupotosha, uiachilie mbali.. ".

38. Aliulizwa Al-Imam Sadique(a.s) kuhusu maana ya taqwa, na alijibu, Safinat ul-Bihar, J.2, Uk.678: "Allah swt hakukosi mahala pale alipokuamrisha wewe uwepo, na hakuoni pale ambapo amekuharamishia wewe kuwepo. "

39. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) , Mustadrak Al-Wasa'il-ush-Shi'h, J.8, Uk.466 no. 10027: "Onyesha heshima zako kwa ajili ya Allah swt kama vile utakavyoonyesha heshima zako mbele ya mtu mwema miongoni mwa ukoo wako. "

40. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Ali ibn Abi Talib(a.s) , Ghura-ul-Hikam, Uk. 321: "Kwa mtu kuinamisha macho yake kutamwia kama kizuizi dhidi ya matamanio (shahwa) yake. "

41. Al-Imam Amir-ul-Muminiin Ali ibn Abi Talib(a.s) amewaambia wana wake Al Imam Al-Hassan na Al-Husayn(a.s) wakati 'Abdur Rahman ibn Muljim (Allah amlaani) alipokuwa amempiga dharuba ya upanga kichwani mwake, katka Nahjul Balagha, Barua no. 47: "Ninawasihini nyote mumwogope Allah swt na nyinyi wala musiwe na uchu wa starehe za dunia hii hata kama itawakimbilia nyinyi. Wala musikisikitikie kitu chochote cha dunia hii ambacho mumekikosa. Semeni ukweli na mutende (kwa kutumai) malipo. Muwe adui wa mdhalimu na msaidizi wa mdhulumiwa. "

42. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Ali ibn Abi Talib(a.s) , Nahjul Balagha, Barua no. 31: "Ninawauusieni kumwogopa Allah swt, Ewe mwana wangu, kubakia katika Amri Zake, kuujaza moyo wako kwa ukumbusho Wake na kubakia katika kumtegemea Yeye tu. Hakuna Hakuna ushikamano unaotegemewa kuwa madhubuti baina yako na Allah isipokuwa wewe iwapo utaishikilia menyewe.

43. Abi Osama amesema kuwa alimsikia al-Imam Sadique a.s. akisema, Al-Kafi, J.2, Uk. 77: "Mujiepushe na adhabu za Allah, taqwa, ijtihadi,kusema ukweli, uaminifu katika amana,tabia njema na ujirani mwema. Muwaite wengine kwenu (kwa tabia zenu njema), wala si kwa maneno tu. Muwe watu wenye kupendeza na kamwe musiwe watu wa kutuaibisha. Ninawausieni murefushe rukuu' na sujuda zenu. Kwani kila mmoja wenu anaporefusha rukuu' na sujuda basi Sheitani hulia nyuma yenu kwa kusea ' Ole wako ! yeye ametii; amesujudu na mimi nilikataa. "

44. Imam Ali ibn il-Husayn(a.s) amesema, Bihar al- Anwar ,J.69, Uk. 277: "Kwa hakika marafiki wa Allah hawatakuwa na khofu yoyote juu yao wala hawatakuwa watu wenye kuhuzunika) iwapo watadumisha yaliyofaradhishwa na Allah swt, wakafuata Sunnah za Mtume (s.a.w.w), wakajiepusha na yale yaliyoharamishwa na Allah swt, wakawa wacha Mungu wema katika kile walichonacho katika utajiri na wadhifa wa humu duniani, wakajitahidi kujitafutia kile kilicho halali, wakaamua kutojifakharisha wala kutojilimbikia katika mali na utajiri isipokuwa katika kutoa misaada na kutoa malipo ya kulipa yaliyofaradhishwa kwake. Basi kwa hakika hao ndio waliobarikiwa katika mapato yao na watalipwa mema kwa yale waliyoyatanguliza huko Aakhera. "

45. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) , Mustadrak al-Wasa'il J. 12, Uk. 89: "Kwa hakika Wana wa Adam wapo sawa na meno ya kitana kuanzia zama za Mtume Adam (a.s) hadi leo, na wala hakuna utukufu wa Mwarabu juu ya asiye Mwarabu, wala Mwekundu juu ya Mweusi isipokuwa kwa Taqwa. "

46. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , Al-Kafi, J. 2, Uk. 76: "Kwa hakika, tendo dogo kabisa lifanywalo pamoja na Taqwa ni bora kabisa kuliko tendo kubwa (au matendo mengi) lifanywalo bila Taqwa. "

KUOMBA DUA

47. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , Al-Kafi J.2, Uk.493: "Dua yoyote inayoombwa kwa Allah swt, inakuwa imezuiwa na mbingu hadi hapo iwe imeshirikishwa na Salawat kumsaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na Ahlil Bayt (a.s )".

48. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , Al-Kafi J.2, Uk.491: "Muminiin ambao Dua zao hazikukubaliwa humu duniani watatmani kuwa dua zao hata moja zisingelikubaliwa pale watakapoonyeshwa hapo Aakhera, mema kupita kiasi ya thawabu (akipewa yeye kwa kutokujibiwa Dua zake na kwa mateso na shida alizozipata akiwa humu duniani). "

49. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Ali ibn Abi Talib(a.s) , Biharu al- Anwar , J.93, Uk. 295: "Tendo lipendwalo sana mbele ya Allah swt humu duniani ni Dua na ibada iliyo bora kabisa mbele Yake ni unyenyekevu na ucha-Mungu ."

50. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Ali ibn Abi Talib(a.s) , Al-Khisal cha Sadduq, Uk. 302: "Milango ya Peponi ipo wazi kwa nyakati tano: wakati mvua inyeshapo; wakati wa Vita vitukufu; wakati wito wa Sala utolewapo (wanapotoa Adhaan); wakati wa kusoma Qur'an Tukufu wakati ambapo jua linazama na linachomoza alfajiri. "

51. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Ali ibn Abi Talib(a.s) , Bihar al- Anwar ,J.93, Uk. 343: "Mujiweke tayari kuomba Dua katika nyakati tano: Wakati usomwapwo Qur'an; Wakati utolewapwo Aadhaan; Wakati unaponyesha mvua; Wakati wa kwenda kupigana katika vita vitakatifu kwa ajili ya kuwa shahidi; Wakati madhulumu anapoomba dua, kwa sababu yeye hana kizuizi cha aina yoyote chini ya mbingu. "

52. Amesema Al-Imam al-Husayn(a.s) ,katika Dua 'Arafah: "Ewe Mola Wangu ! Wewe U karibu kabisa wa kuombwa; Na mwepesi wa kujibu; na Wewe Mkarimu wa kutoa; na unamtosheleza umpaye; unamsikia vyema akuulizae; Ewe Uliye Rahmaan wa dunia na Aakhera na Mremehevu kote !".

53. Amesema Al-Imam Amirul Muminiin Ali ibn Abi Talib(a.s) , Nahjul Balagha, Msemo 135: "Anayejaaliwa vitu vinne hanyimwi vinne: Anayejaaliwa kuomba Dua hanyimwi kukubalika kwake; anayejaaliwa kufanya Tawba hanyimwi kukubalika kwake; anayejaaliwa kuomba msamaha hanyimwi kusamehewa kwake; anayejaaliwa kutoa shukuurani zake hanyimwi kuongezewa kwake. ".

54. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , Bihar al- Anwar , J. 78, Uk. 216: "Siku ya Qiyama, Allah swt atazihesabu Dua zote alizokuwa akiziomba Mja wake na kuuzibadilisha katika matendo mema na kwa hayo atawapandisha daraja katika Jannat (Peponi). "

55. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , At- Tahdhib, J. 4, Uk. 112: "Ponyesheni magonjwa yenu kwa kutoa sadaqah na mujiepushe na balaa za kila aina kwa Dua ".

56. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , Wasail-ush-Shi'ah J. 7, Uk. 60: "Mwombe Allah swt maombi yako na daima uwe ukisisitiza katika kumwomba kwani Allah swt mwenyewe anapenda mno kubakia kwa kumsisitiza miongoni mwa waja wake Muminiin. "

57. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , Al-Kafi, J. 2, Uk. 467: "Ninakuusieni muombe Dua', kwa sababu hamtaweza kumkaribia Allah swt kwa vinginevyo kama hivyo. "

58. Amesema Al-Imam Amirul Muminiin Ali ibn Abi Talib(a.s) , Ghurar-ul-Hikam, Uk. 185: "Inawezekana kuwa wewe umemwomba Allah swt Dua ya kitu fulani ambacho yeye hakukujaalia kwa sababu yeye anataka kukupa kitu kilicho bora zaidi ya kile ulichokuwa umekiomba, hapo mbeleni(unatakiwa kufanya subira. (mtarjum). "

AHLUL BAYT(A.S)

59. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) , Bihar al- Anwar ,J.27, Uk. 113: "Mfano wa Ahlul-Bayt yangu kwa Ummah wangu ni sawa na Safina ya Mtume Nuh (a.s) Wote wale watakaoipanda ndani yake basi wameokolewa na wote wale waupingao, basi wamezama na kupotea .".

60. Amesema Al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) , Imam wa tano, Bihar al- Anwar , J. 2, Uk. 144: "Ahadith zetu (za Alhul Bayt) zinahuisha nyoyo."

61. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w ), Bihar al- Anwar , j.38, Uk. 199: "Muhuishe mikutano na mikusanyiko yenu kwa makumbusho ya Ali ibn Abi Talib (a.s) ".

62. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) , Ikmal-ud-Din, j. 1, uk.253 na yenye maana yakaribiayo katikaYanabi-ul-Muwaddah, uk. 117: Ipo riwaya kupitia Jabiri Al-Ju'fi iliyopokelewa kutoka Jabir-ibn-Abdillah isemayo: Mimi nilisema: Ewe Mtume wa Allah swt, sisi tunamwelewa Allah swt na Mtume wake(s.a.w.w) Sasa jee hawa Ulul-Amr ni wakina nani ambao utiifu wao umefardhishwa sawa na wako?

Hapo Mtume(s.a.w.w) alisema: "Ewe Ja'abir! Wao ni, baada yangu, Makhalifa wangu na Ai'mmah wa Waisilamu; wa kwanza miongoni mwao ni Ali ibn Abi Talib(a.s) ; atafuatia (Imam) Hassan, na (Imam) Husayn; atafuatia Ali ibn il Husayn; atafuatia Muhammad ibn Ali; ajulikanaye katika Tawrati kama Baqir, ambaye utakutana naye, Ewe Ja'abir! Pale utakapomtembelea, umpe salaam zangu. Baada yake Musa ibn Ja'afar; atafuatia Ali ibn Musa, atafuatia Muhammad ibn Ali; atafuatia Ali ibn Muhammad, atafuatia Hassan ibn Ali; na baada yake (atakuja) Al-Qaim, ambaye jina lake ni sawa na jina langu. Yeye ndiye atakaye kuwa Mamlaka Ya Allah swt juu ya ardhi hii na Aliyebakia miongoni mwa Waja wake. Yeye ndiye mwana wa (Al-Imam) Hassan ibn Ali ( al-'Askari). Huyu ndiye shakhsiyyah ambaye Allah swt atafungua Dhikiri zake Mashariki na Magharibi na huyu ndiye Shakhsiyyah ambaye atakuwa ghaibu kwa wafuasi na wapenzi wake ambavyo hakuna nyoyo zozote zile zinazoweza kukubali isipokuwa nyoyo za wale tu ambao Allah swt ameshakwishakuzijaribu kwa ajili ya Imani." Ja'abir alisema: "Mimi nilimwuliza 'Ewe Mtume wa Allah swt! Je wafuasi wake watafaidika naye wakati akiwa ghaibu? Mtume(s.a.w.w) alijibu: 'Naam. Kwa kiapo cha Yule aliyenichagua kuwa Mtume, wao watafaidika kwa nuru yake na watafaidika kwa ibada akiwa ghaibu kama vile kufaidika kwa watu kutokana na nuru ya jua hata pale linapofunikwa kwa mawingu."

63. Amesema Malik ibn Anas kuhusu mema ya Imam Sadique(a.s) , Bihar al- Anwar J. 47. Uk. 28: "Hakuna macho yaliyowahi kuona, hakuna masikio yaliyokwisha kusikia, na wala hakuna moyo uliyokwisha shtushwa kwamba kunaweza kuwapo na mtu yeyote aliye bora zaidi kuliko (Imam) Ja'afar as- Sadique (a.s) katika Taqwa, elimu, ibada na Ucha-Mungu. ".

64. Amesema Al-Imam al-Husayn(a.s) , Al-Irshaad, uk. 204: "Kwa roho yangu, hakuna Imam isipokuwa ni Hakimu kwa Kitabu, anaimarisha uadilifu, anaamini katika Dini ya Ukweli, na anajizuia nafsi yake pamoja na njia ya Allah swt. ":

MAPENZI YA AHLUL-BAYT(A.S)

65. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) , Al-Jami'-ul-Saghir, J. 1 uk. 14: "Wafunzeni watoto wenu vitu vitatu: Mapenzi ya Mtume wenu, Mapenzi ya Ahlul-Bayt, usomaji wa Qur'an. "

66. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , Biharu al- Anwar , J. 74, uk. 354: "Mtu yeyote ambaye hawezi kutufanyia wema wowote sisi Ahlul-Bayt basi wawafanyie mema wafuasi wetu walio wema; na yeyote yule asiyeweza kutuzuru, basi wanaweza kuwazuru wafuasi wetu walio wema ambavyo thawabu za kutuzuru sisi zitaandikiwa yeye. ".

67. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) , Al-Kafi, J.1, uk. 187: "Kwa kile kilicho bora kabisa kwa mja kumkaribia Allah swt ni utiifu kwake Allah swt, utiifu kwa Mtume (s.a.w.w) na utiifu kwa ulil Amr ." Aliendelea kusema: "Mapenzi yetu (ya Ahlul-Bayt) ni Imani na chuki dhidi yetu ni kufr. "

68. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , Biharul- Anwar , j.27, uk.91: "Kwa hakika zipo daraja za ibada, lakini mapenzi yetu , Ahlul-Bayt, ni ibada iliyo bora kabisa.

SIFA NA TABIA ZINAZOKUBALIKA

69. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) Al-Kafi, j.2, uk.235: "Je niwatambulisheni Mumiin ni nani? Mumin ni yule ambaye waumini wengine wanamwamini kwa nyoyo zao na mali pia. Je niwatambulisheni Mwislamu ni nani? Mwislamu ni yule ambaye Waislamu wengine wanakuwa wamehifadhika kwa ulimi na mikono yake.. Ni haramu kwa Mumiin kumfanyia ubaya mumin mwenzake, au kumwacha katika hali ya shida, au kumsengenya au kumkataa kwa ghafla. "

70. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , Usul-i-Kafi,j.2, uk. 374: "Haimpasi Muislamu kuhudhuria au kushiriki katika mikutano au mikusanyiko ambapo Sharia za Allah swt zinavunjwa na kwamba yeye (huyo Muislamu) hana uwezo wa kuyazuia hayo. "

71. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , Khisal cha Saduq, j.1, uk. 88: "Yeyote yule kwa tabia yake husema ukweli, basi matendo yake yametakasika; Na allah swt humwongezea riziki yule aliye na nia njema; na yeyote yule awatendeaye mema familia yake, Allah swt humwongezea umri mrefu. ".

72. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Ali ibn Abi Talib(a.s) , Safinat ul-Bihaar, j.1, uk.599: "Mtume(s.a.w.w) alijiwa na mtu mmoja aliyeomba kufundishwa tendo kwayo ataweza kupendwa na Allah swt pamoja na watu, utajiri wake utaongezeka, mwili wake utakuwa na siha nzuri, umri wake utaongezeka na atainuliwa Siku ya Qiyama pamoja na Mtume(s.a.w.w)

Mtume(s.a.w.w) alimjibu: 'Hizi ndizo njia sita zinazohitaji sifa sita:

Iwapo wataka Allah swt akupende, lazima umwogope na ujiepushe na madhambi.

Iwapo wataka watu wakupende, lazima uwe mkarimu kwao na ukatae walichonacho mikononi mwao,

Iwapo wataka Allah swt akuongezee utajiri wako, hunabudi kutoa malipo yaliyofaradhishwa kwako i.e. Zaka, Khums, na zinginezo.

Iwapo wataka Allah swt aupatie mwili wako afya njema, basi uwe ukitoa sadaqa kila mara iwezekanavyo,

Iwapo wataka Allah swt aurefushe umri wako, basi uwe ukiwajali majamaa zako,

Iwapo wataka Allah swt akuinue pamoja nami Siku ya Qiyama, basi ni lazima urefushe sujuda zako mbele ya Allah swt, aliye Pekee na Mmiliki."

73. Amesema Al-Imam Ar-Ridhaa(a.s) Imam wa Nane, 'Uyun-ul-Akhbaar ur-Ridhaa, j.1,uk.256: "Mumin hawezi kuwa mumin kamili hadi hapo atakapokuwa na mambo matatu: Sunna za Allah swt, Sunna za Mtume(s.a.w.w) na Sunna za Imam(a.s) wake. Ama Sunna za Allah swt ni kuzificha siri zake; kama vile Allah swt anavyosema katika Sura Al-Jinn, 72, Ayah 26 Na 27. Na ama Sunna za Mtume(s.a.w.w) ni kule kupatana na kuelewana na watu, wakati ambapo Allah swt alimtuma Mtume wake kuwapenda watu na Amesema: 'Uzoee usamehevu na uwafundishe mema na ujiondoe kutoka majaheli Ama kuhusu Sunna za Imam a.s. (kuwa imara na) mwenye subira katika siku nzuri na siku mbaya na nzito, ambavyo Allah swt anatuambia katika Sura Al-Baqarah,2, Ayah 177. "

74. Amesema Al-Imam Muhammad ibn Ali(a.s) , al-Jawad, Imam wa Tisa, Muntah al-'Amal, uk.229 "Mumin anahitaji mambo matatu: mafanikio yatokayo kwa Allah swt, mwenye kujipa mawaidha, kukubaliwa na yule ampaye nasiha. ".

75. Imam 'Ali ibn il-Husayn(a.s) , Imam wa Nne, aliulizwa "Ewe mwana wa Mtume! Huanzaje siku yako?" Na Imam(a.s) alijibu, Bihar al- Anwar j.76, uk. 15: "Mimi huanza siku yangu huku nikitakiwa kutimiza mambo manane (8): Allah swt ananitaka nitimize yaliyafaradhiwa juu yangu; Na Mtume(s.a.w.w) ananitaka nitimize yale yaliyo Sunna yake; Familia yangu inanitaka mimi niwatimizie mahitaji yao kama chakula n.k.; Nafsi yangu inanitaka niitimizie matamanio yangu; Shaytani ananitaka mimi nitende madhambi; Malaika wawili wanaonihifadhi wananitaka mimi nitende matendo kwa moyo halisi, Malaika wa Mauti anataka roho yangu na Kaburi inautaka mwili wangu. Basi mimi ndivyo nilivyo baina ya mzunguko wa matakwa hayo."

76. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , Bihar al- Anwar, j. 67 uk.305: "Kwa hakika kila kitu kinashawishiwa na Mumin kwa sababu Dini ya Allah swt inamfanya yeye awe ni mtu mwenye nguvu, na wala yeye kamwe hashawishiwi na kitu chochote kile, na kwa hakika hii ndiyo dalili ya kila Mumin.

WAFUASI HALISI WA AHLUL-BAYT(A.S) NA SIFA ZAO

77. Imam Muhammad al-Baqir(a.s) alimwambia Ja'bir, Al-Kafi, j. 2, uk. 74: "Je inatosheleza kwa mtu kujiita Shia na mfuasi wetu ati kwa kudhihirisha mapenzi yetu, Ahlul Bayt? Kamwe sivyo hivyo!, Kwa kiapo cha Allah swt, huyo mtu kamwe hawezi kuwa mfuasi wetu isipokuwa yule ambaye amejawa khofu ya Allah swt na kumtii ipasavyo. Ewe Ja'abir! Wafuasi wetu hawawezi kutambuliwa isipokuwa kwa sifa zifuatazo watakazokuwanazo kama unyenyekevu, kujitolea; uadilifu; kumsifu Allah kupita kiasi; kufunga saumu na kusali; kuuwatii wazazi; kuwasaidia masikini, wenye shida, wenye madeni, na mayatima wanaoishi karibu naye; kusema ukweli; kusoma Qur'an; kuuzuia ulimi kusema chochote kuhusu watu isipokuwa kwa mapenzi; na kuwa mwaminifu kwa majamaa kwa maswala yote. "

78. Amesema Sulayman Ibn Mahran kuwa yeye alimtembelea Imam Ja'afer Sadique(a.s) wakati ambapo baadhi ya wafuasi (Mashiah) walikuwa karibu naye na alimsikia Imam(a.s) akiwaambia, Al-Amali, cha Saduq, uk. 142: "(Mujiheshimu) muwe kama vito vya thamani kwa ajili yetu na wala kamwe musiwe wenye kutuaibisha sisi. Waambieni watu kuhusu mema, na muizuie ndimi zenu zisizungumze mneno maovu na mambo yasiyo na maana. "

79. Amesema al-Imam Sadique(a.s) , Al-Kafi j. 2, uk. 56: "Kwa hakika, sisi huwapenda wale walio na busara, wenye kuelewa, wenye elimu, wenye kufanya subira, waaminifu na wenye imani. Kwa hakika Allah swt aliwajaaliwa Mitume (a.s) kwa tabia njema. Kwa hivyo yeyote yule aliye na sifa hizo basi amshukuru Allah swt, lakini yule ambaye hana hayo basi amlilie Allah swt,Aliye Mkuu na Mwenye uwezo, na Amwombe hayo. "

Ja'abir kwa unyenyekevu alimwuliza Imam(a.s) ndiyo yapi hayo, na Imam(a.s) alimjibu: "Nayo ni: Ucha-Mungu, kutosheka, subira, kushukuru, kuvumilia, tabia njema, furaha, hima, bidii,shauku, mkarimu, mkweli na mwaminifu katika amana. "

80. Amesema Al-Imam Muhammad al-Baquir(a.s) , Al-Kafi, j.2, uk.75: "Yeyote yule anamtii Allah swt basi ni mpenzi wetu, na yeyote yule asiyemtii Allah swt basi ni adui wetu (sisi Ahlul-Bayt) .."

MADHAMBI NA ATHARI ZAKE

81. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) , Biharu al- Anwar,j.77,uk.79: na Mustadrak Al-Wasail,j.11, uk. 330: "Msitazame udogo wa dhambi, lakini muangalie muliyemuasi (Allah swt). "

82. Amesema Al-Imam Amirul Muminiin Ali ibn Abi Talib(a.s) , Biharu al- Anwar ,j. 70, uk.18: "Iwapo mtu anapenda kujiona vile alivyo mbele ya Allah swt, basi ajitathmini kwa madhambi na maasi yake mbele ya Allah swt; basi kwa kipimo hicho ndivyo alivyo huyo mtu mbele ya Allah swt. ".

83. Al-Imam Sadique(a.s) aliwauliza watu ni kwa nini wanamwudhi Mtume(s.a.w.w) Basi mmoja wa watu alimwuliza Imam(a.s) vipi, naye Imam(a.s) aliwaambia, Usulu Al-Kafi , j.1, uk.219: "Je hamujui kuwa matendo yenu yapoyanajulishwa kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w) na pale aanapoona madhambi dhidi ya Allah swt miongoni mwao, basi husikitishwa mno. Kwa hivyo musimuudhi Mtume wa Allah swt na badala yake munatakiwa kumfurahisha (kwa kutenda mema). ".

84 Amesema Ali ibn Abi Talib(a.s) , Ghurur al-Hikam, uk. 235: "Kukosa kusamehe ni kasoro moja kubwa kabisa na kuwa mwepesi katika kulipiza kisasi ni miongoni mwa madhambi makubwa kabisa. ".

85. Kutokea Asbaghi bin Nabatah kutokea kwa Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema, Al-Khisal,cha Sadduq, j.2, uk. 360: "Amesema Mtume (s.a.w.w) kuwa Allah swt anapoikasirikia Ummah na kama hakuiadhibu basi bei za vitu vitapanda juu sana yaani maisha yatakuwa ghali, maisha yao yatakuwa mafupi, biashara zao hazitaingiza faida, mazao yao hayatukuwa mengi, mito yao haitakuwa imejaa maji, watanyimwa mvua (itapungua), na watatawaliwa na waovu miongoni mwao." (Yaani Hadith hiyo juu inatubainishia kuwa iwapo kutakuwa na jumuiya ambayo imejitumbukiza katika madhambi basi wanabashiriwa kupatwa na mambo saba hayo yaliyotajwa. )

86. Al-Imam al-Baqir(a.s) amesema kuwa amekuta katika kitabu cha Al-Amir al-Muminiin Ali ibn Abi Talib(a.s) akisema kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema: Safinatu Bihar, j.2, uk.630: "Wakati zinaa itakapokithiri katika jumuiya basi idadi za mauti za ghafla zitakithiri; na patakapokuwa na uovu basi Allah swt atawatumbukiza katika maisha ya ghali na hasara. Wakati watu watakapoacha kulipa zaka, basi ardhi itazinyakua baraka zake kutokea mazao, matunda, madini na vitu vyote kama hivyo. Wakati watakapotenda bila haki kwa mujibu wa Shariah, basi itakuwa sawa na kumsaidia dhalimu na ugaidi. Na watakapozikiuka ahadi zao, basi Allah swt Allah swt atawafanya maadui wao kuwasaliti na kuwakandamiza. Wakati watakapoacha uhusiano pamoja na ndugu na jamaa zao, basi yote yale wayamilikiayo yatakwenda mikononi mwa waovu. Na wakati watakapojiepusha na kutoa nasiha ya mambo mema na kuyakataza maovu na kama hawatawafuata waliochaguliwa Ahl-ul-Bayt (a.s), basi Allah swt atawasalitisha kwa walio wenye shari miongoni mwao na katika hali hii, wataomba duaa lakini hazitakubalika. "

87. Amesema Al-Imam Ali ibn Abi Talib(a.s) , Biharu al- Anwar, j.70,uk.55: "Machozi hayaishi illa kwa nyoyo kuwa ngumu, na nyoyo haziwi ngumu illa kukithiri kwa madhambi. "

88. Allah swt alimwambia Mtume Dawud(a.s) : Ithna-Ashariyyah, uk.59: "Ewe Dawud! Wabashirie habari njema wale watendao madhambi kuhusu msamaha wangu, ambayo inajumuisha kila kitu kilichopo humu duniani, ili wasikate tamaa ya msamaha wangu; na waonye wale watendao mema kwa adhabu zangu ili wasije wakajifanyia ufakhari kwa utii wao, kwani ufakhari ni dhambi mbaya kabisa. "

6

ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

UCHAMBUZI WA MADA

Madda muhimu katika uchambuzi: Imebakia madda moja muhimu ndani ya uchambuzi wote huu, madda ambayo inataka kuangaliwa kwa makini na kusomwa, na huenda hiyo pekee ndiyo kikwazo ambacho huwachemua wapinzani pale wanaposhinikizwa kwa hoja nzito. Utawaona wanashangaa na kutokuamini ya kuwa Masahaba wapatao laki moja walihudhuria kutawazwa kwa Imam Ali (kuwa Khalifa wa Mtume) na hatimaye hao hao Masahaba wakaafikiana wote kumkhalifu Imam Ali na kumpuuza na miongoni mwao wamo Masahaba wakubwa.

Hali hii (ya kushangazwa kwa wapinzani) imepata kunitokea mimi mwenyewe wakati nilipoingia kikamilifu ndani ya utafiti, sikuamini na haiwezekani kwa mtu yeyote kuamini pindi tukio hili linapoaridhiwa kama lilivyo, lakini wakati tunapolisoma tukio hili kwa pande zote basi kule kushangaa kunaondoka kwani hali halisi haiko kama tunavyoitazamia sisi au kama wanavyoiaridhi Masunni (ya kuwa) haiwezekani Masahaba laki moja wakaenda kinyume na amri ya Mtume, hivyo basi ilikuwaje mambo yakatokea kama yalivyotokea?

Kwanza Siyo kila aliyehuduria Baia ya Ghadir alikuwa akiishi Madina, bali ilikuwa kama ambavyo hali halisi ilivyokuwa kwamba kwa kiasi kikubwa itakuwa ni watu elfu tatu au Nne tu miongoni mwa Masahaba hao ndiyo waliokuwa wakiishi Madina.Na tutakapofahamu ya kwamba wengi wa hawa walikuwa ni watumwa na walioachwa huru na wanyonge ambao walimfikia Mtume (s.a.w.) kutoka sehemu mbali mbali na hapo Madina hawakuwa na uwenyeji wala jamaa (kwa mfano watu wa As-Safah) basi haitabakia isipokuwa nusu yao yaani watu elfu mbili tu, na hata hawa nao ni watiifu kwa viongozi wa makabila na muongozo wa kidugu ambao ndiyo wanaohusika nao na Mtume aliwakubalia (kuwa watiifu kwa viongozi wao) kwani ulipokuwa ukimfikia ujumbe wa kabila fulani, Mtume (s.a.w.) humtawalisha juu yao kiongozi wao, na kwa ajili hiyo ndiyo tumekuta katika Uislamu Istilahi ya kuitwa kwao kuwa ni Ahlul-Hilli wal-Iqdi, watu wanaotumainiwa kutowa maamuzi katika jamii au nchi.

Kadhalika tunapoutazama mkutano wa Saqifah ambao ulikutana mara tu baada ya kufariki Mtume (s.a.w.), tunawakuta waliohudhuria ambao waliuthibitisha uchaguzi wa Abubakar kuwa ni khalifa, idadi yao haizidi watu mia moja kwa makadirio ya juu, kwani katika Ansari ambao ndiyo wenyeji wa Madina hawakuhudhuria isipokuwa viongozi wao kama ambavyo Muhajirina ambao ni wenyeji wa Maka waliohama pamoja na Mtume (s.a.w.) hawakuhudhuria isipokuwa watu watatu au wanne wakiwakilisha Maquraishi. Hali hii itoshe basi kuwa ni dalili ya kupima ukubwa wa hiyo Saqifah ikoje, Saqifah ambayo ilikuwa haina nafasi ya kutosha, kwani haikuwa inakosa kuwa karibu katika kila nyurnba.

Kwa hiyo haikuwa uwanja wa maadhimisho wala siyo jumba la mikutano, na tunaposema kuwa watu mia moja walihudhuria hapo Saqifah bani Saida basi idadi hiyo sisi ndiyo tunaoizidisha ili tu, mwenye kutafiti aweze kufahamu kwamba wale Masahaba laki moja hawakuwepo wala hata hawakusikia mazungumzo yalivyofanyika ndani ya Saqifah isipokuwa baada ya muda mrefu kupita, .kwani hapo zamani hapakuwa na mawasiliano ya anga wala simu au Satellite.

Na baada ya mabwana wakubwa hawa kuafikiana juu ya Abubakar pamoja na upinzani wa bwana wa Kiansari Saad bin Ubbadah ambaye ni kiongozi wa kabila la Khazraj na mwanawe Qais, lakini wengi mno miongoni mwao (kama isemwavyo hii leo) walipitisha makubaliano hayo na kumpa Abubakar mkono wa Baia, wakati ambapo Waislamu wengi hawakuwepo hapo Saqifah, na baadhi yao walikuwa wameshughulika kumuandaa Mtume (s.a.w.) kwa mazishi au walihamanika kutokana na khabari za kifo chake, ambapo Umar bin Al-Khatab naye alikuwa amewatisha na kuwatia khofu iwapo watasema kuwa Mtume amefariki. Taz: Sahih BukhariJuz. 4 -195.

Zaidi ya hayo wengi wa Masahaba wa Mtume walikuwa amewateua wawemo ndani ya Jeshi la Usamaha na wengi wao walikuwa wameweka kambi mahala paitwapo Jorfi wakiwa tayari kwenda vitani na jeshi la Usamah hawakuwepo Mtume alipofariki wala hawakuhudhuria mkutano wa Saqifah. Basi je, inaingia akilini baada ya haya yaliyotokea kwamba mtu fulani katika kabila au ukoo kumpinga kiongozi wake kwa lile alilolipitisha na hasa inapokuwa hilo alilolipitisha lina ubora na utukufu mkubwa ambao kila kabila linaukimbilia? Ni nani ajuwaye ya kwamba huenda siku moja naye atawatawalia Waislamu wote, maadamu mwenye haki hiyo kisheria amekwisha tupwa mbali na mambo sasa yanakwenda kwa kushauriana wanabadilishana kwa kuachiana, basi ni kwa nini wasilifurahie hilo, na ni kwa nini wasiliunge mkono?

Pili Ikiwa wenye uwezo wa kuamua ni wakaazi wa Madina na wamepitisha jambo fulani, basi watu walio mbali katika sehemu mbali mbali za bara Arabu hawawezi kupinga na hali ya kuwa hawajui yanayopita wakati hawapo kwani vifaa vya mawasiliano kwa zama hizo vilikuwa ni vile vya kizamani kisha wao walikuwa wakifahamu kwamba wakazi wa Madina ndiyo waliokuwa wakiishi na Mtume wa Mwenyezi Mungu hivyo basi hao ndiyo wajuao mno mambo mapya miongoni mwa hukmu, kwani huenda ukashuka Wahyi wakati wowote au siku yoyote. Kisha kama kuna kiongozi wa kabila lolote lililo mbali na makao makuu basi jambo la Ukhalifa kwake si muhimu sana sana iwapo Abubakr atakuwa Khalifa au Ali au mtu mwingine yeyote, kwani watu wa Maka ndiyo wajuao zaidi utaifa wao, na cha muhimu kwao ni kubakia kwenye uongozi wa ukoo wake ambapo hakuna anayemkera katika uongozi huo.

Basi ni nani ajuwaye kwamba huenda baadhi ya watu waliulizia juu ya jambo hilo (la Ukhalifa) na walitaka kufahamu mambo yalivyokwenda lakini vyombo vya mtawala viliwanyamazisha sawa iwe kwa njia ya kuwapa tamaa ya mali au vyeo au vitisho, na huenda kisa cha Malik bin Nuwairah ambaye alikataa kutoa zaka kwa Abubakr ni utokea jambo hilo. Na yeyote mwenye kufuatilia matukio hayo yaliyotokea katika vita ya wanaokataa kutoa zaka katika zama za Abubakr atakuta kuna kupingana (kwa maelezo), wala hawezi kutosheka kwa maelezo yaliyoelezwa na baadhi .ya wanahistoria kwa lengo la kulinda heshima ya Masahaba na hasa wale watawala.

Tatu Kiini cha tatizo hili ni kule kushitukizwa ghafla kupatikana kwa Khalifa, hili ni jambo lililochangia mno kukubalika kwa kile ambacho leo kinaitwa kuwa "Hali halisi iliyopo". Kwani mkutano wa Saqifah ulifanyika ghafla kwa kuwashitukiza baadhi ya Mashaba ambao walikuwa wakimshughulikia Mtume (s.a.w.), na miongoni mwao alikuwa Imam Ali na Abbas na wengine miongoni mwa Bani Hashim, Miq-dad, Salman, Abu Dharri, Ammar, Zubair na wengineo wengi. Ama wale waliokuwa Saqifah walipotoka huko hali ya kuwa wakimshangilia Abubakr walielekea msikitini huku wakitoa mwito kwa watu wafanye baia ya jumla na watu wakaipokea baia hiyo kwa wingi watake wasitake kipindi hicho Imam Ali na wafuasi wake walikuwa hawajamaliza wajibu wao Mtukufu ambao tabia zao (mwenendo wao) mwema uliwalazimisha (wautimize) basi haikuwezekana kwao kumuacha Mtume (s.a.w.) bila ya kumkosha, kumvisha sanda, kumtayarisha na kumzika eti badala yake wakimbilie Saqifah kugombea Ukhalifa.

Walipomaliza wajibu wao huo, mambo yalikuwa yamekwisha kamilika kwa Abubakr na yeyote mwenye kwenda kinyume na baia hiyo akawa anahesabiwa kuwa ni miongoni mwa watu wenye fitna ambaye anabomoa umoja wa Waislamu, hivyo ni wajibu kwa Waislamu kumpinga au hata kumuuwa ikiwa itabidi, na ndiyo maana tunamuona Umar alimuonya Saad bin Ubbadah kuwa atauawa pale alipokataa kumbai Abubakr, Umar akasema, "Muuweni hakika yeye ni mtu wa fitna"[52] na baada ya hapo Umar aliwatishia wote waliobaki ndani ya nyumba ya Ali ya kuwa atachoma moto nyumba hiyo na wote waliomo humo. Tukishakufahamu vyema maoni ya Umar bin Al-Khatab kuhusu baia tutatambua mengi baada ya hapo miongoni mwa mambo yanayotatanisha.

Kwa hakika Umar anaona kuwa baia inatosha kusihi pale mmoja miongoni mwa Waislamu anapowahi, basi hapo inakuwa ni lazima kwa wengine kumfuata na yeyote atakayeasi miongoni mwao huyo atakuwa ametoka nje ya mshikamano ya Waislamu na ni wajibu kumuuwa. Basi hebu na tumsikilize yeye mwenyewe hasa kuhusu baia, kama alivyoeleza Bukhar ndani ya Sahih yake juzuu ya nane ukurasa wa ishirini na nane, Babu Rajmi Al-Hubla Minaz-Zinaa Idha-Ah-Sanat amesema: akisimulia yale yaliyotokea ndani ya Saqifah. "Basi fujo ikazidi na sauti zikapaa mpaka nikatishika kuwa kutatokea kuhitilafiana, nikasema, Ewe Abubakr kunjua mkono wako, Abubakar akakunjua mkono wake nikambai nao muhajirina wakambai[53] Ansari (nao wakambai) na tukamruka Saad bin Ubbadah, akasema msemaji miongoni mwao, "Mmemuuwa Saad bin Ubbadah" Mimi nikasema:

"Mwenyezi Mungu amuuwe Saad bin Ubbadah" Umar akasema: "Wallahi sisi hatujakutana na jambo gumu katika yote tuliyohudhuria kuliko kumbai Abubakar, tulichelea kuwa hawa jamaa tukiwaacha bila kupitisha baia, basi watambai mtu miongoni mwao baada yetu, hivyo imma tuwape madaraka, jambo ambalo hatulikubali, au tuwapinge itokee uharibifu, (naonya) yeyote atakayetoa baia bila ya kushauriana na Waislamu asifuatwe yeye wala yule aliyembai ili asiuawe. Basi jambo lililovyo kwa Umar siyo uchaguzi wala hiyari wala mashauriano, bali inatosha pale Mwislamu mmoja anapoiwahi baia hiyo iwe ni hoja kwa wengine na ndiyo maana alimwambia Abubakr, "Kunjua mkono wako Ewe Abubakar," na Abubakr naye akakunjua mkono wake akambai bila ya mashauriano tena haraka haraka kwa kuchelea kutanguliwa na mwingine na kwa hakika Umar amekwisha ieleza rai hii pale aliposema:

"Tulichelea lau tutawaacha watu hawa bila ya kuipitisha baia, watambai mtu miongoni mwao baia yetu (Umar aliwachelea Maansar wasimtangulie wakambai mtu miongoni mwao), na kinachomuongezea ufafanuzi zaidi ni pale anaposema: "Basi imma tuwape Baia jambo ambalo hatulikubali na au tuwapinge patokee uharibifu."[54]

Na ili tuwe waadilifu katika maamuzi na wenye kuchunguza kwa undani, inatupasa tukiri kwamba Umar bin Al-Khatab alibadilisha mtazamo wake kuhusu baia mwishoni mwa uhai wake na hilo ni pale mtu mmoja alipomjia Umar mbele ya Abdur-Rahman bin 'Auf katika Hijja yake ya mwisho aliyohiji, yule mtu akamwambia: "Ewe Amirul-Muuminina unayo habari kuwa fulani anasema, bila shaka Umar akifa hakika nitambai fulani kwani wallahi baia ya Abubakar haikuwa isipokuwa kwa kushitukiza tu na ilitimia". Umar alikasirika na kwa ajili hii alisimama akawahutubia watu alipokuwa akirudi Madina, miongoni mwa aliyoyasema katika khutba yake ni haya yafuatayo:

"Kwa hakika nimepata habari kwamba kuna asemaye miongoni mwenu kuwa, Wallahi lau Umar atakufa nitambai fulani, basi na asijidanganye mmoja wenu kusema kuwa baia ya Abubakar ilikuwa hivyo lakini Mwenyezi Mungu aliikinga shari yake.."[55] Kisha Anasema: "Yeyote mwenye kumbai mtu bila mashauriano kutoka kwa Waislamu, basi huyo asipewe baia yeye wala huyo aliyembai kuhofia asije uwawa.[56]

Basi laiti Umar angekuwa na mtazamo huu siku ya Saqifah na asiwalazimishe Waislamu kumbai Abubakr ambako kulikuwa kwa kushitukiza, na Mwenyezi Mungu aliikinga shari yake kama alivyoshuhudia yeye mwenyewe, lakini imekuwaje Umari awe na rai hii mpya katika mtazamo huu mpya, hakika atakuwa amejihukumia kifo yeye mwenyewe na rafiki yake (Abubakr) kwa kuwa kwenye mtazamo wake mpya anasema: "Yeyote mwenye kumbai mtu bila ya mashauriano toka kwa Waislamu basi asipewe Baia yeye wala huyo aliyembai ili asije uwawa."

Imebakia juu yetu kufahamu ni kwa nini Umar alibadilisha maoni yake mwishoni mwa uhai wake pamoja na kwamba yeye anafahamu mno kuliko mwingine ya kuwa mtazamo wake mpya unatengua baia ya Abubakar iliyotimia bila ya mashauriano toka kwa Waislamu na ilikuwa ni baia ya kushitukiza? Pia mtazamo wake huu mpya unatengua baia yake yeye aliyopewa, kwani aliupata ukhalifa kwa tamko la Abubakar wakati wa kufa bila ya makubaliano kutoka kwa Waislamu, kiasi baadhi ya masahaba walikwenda kwa Abubakar wakamkemea kwa kuwatawalishia mtu msusuavu tena mgumu wa tabia.[57] Na Umar alipotoka ili awasomee watu maandiko ya Abubakr kuna mtu alimuuliza: "Ewe Baba Hafs kuna nini ndani ya waraka huo?" Umar akasema, Sijuwi, lakini mimi nitakuwa wa kwanza kusikiliza na kutii." yule mtu akasema: "Lakini Wallahi mimi najua kilichomo, wewe ulimtawalisha (Abubakar) kipindi cha mwanzo naye amekutawalisha kipindi hiki".

Taz: Al-Imam Was-Siyasah cha Ibnu Qutaibah Juz. 1 uk. 25Mlango unaohusu maradhi ya Abubakri na kumtawalisha kwake Umar. Kauli hii inafanana na kauli ya Imam Ali kumwambia Umar pale alipomuona anawalazimisha watu kwa nguvu wambai Abubakr akasema "Nifanye jambo ambalo wewe utakuwa na hisa (wanitaka) leo nilikazanie jambo lake ili kesho akurudishie"? Taz: Al-Imamah Was-Siyasah cha ibnu Qutaiba Juz. 1 uk. 18. Cha muhimu ni kufahamu ni kwa nini Umar alibadilisha mtazamo wake kuhusu Baia?

Mimi ninakurubia kuamini kwamba, wakati alipowasikia baadhi ya Masahaba wanataka kumbai Ali bin Abi Talib baada ya kufa Umar jambo ambalo yeye Umar kamwe hakubaliani nalo, kwa kuwa yeye ndiye aliyezipinga maagizo ya Mtume yaliyobayana, na akapinga Mtume (s.a.w.) asiwaandikie yale maandiko[58] kwa kuwa yeye alilifahamu lengo lake kiasi kwamba akamtuhumu Mtume kuwa anaweweseka na akawatisha watu wasiseme kuwa Mtume amekufa[59] yote hayo ni kwa sababu wasije wakawahi kumbai Ali. Umar alitilia mkazo baia ya Abubakr na akawalazimisha watu kwa nguvu waikubali baia hiyo na kisha kumuonya kila atayepinga kuwa atamuua[60] ili tu kumtenga mbali Ali na ukhalifa.

Hivi itawezekana Umar aridhie aseme msemaji kwamba fulani atapewa baia lau Umar atakufa? Hasa pale msemaji huyu ambaye jina lake limebakia kuwa halijulikani na hapana shaka kuwa alikuwa miongoni mwa Masahaba wakubwa? Msemaji huyu alitumia hoja ya kitendo alichokitenda Umar mwenyewe alipombai Abubakar pale anaposema: "Wallahi Baia ya Abubakr haikuwa isipokuwa ya kushitukiza na ikatimia", yaani pamoja na kuwa ilitokea kwa kuwashitukiza Waislamu na bila kupata ushauri wao lakini ilitimia na likawa jambo lililothibitika, kwa hiyo ilifaa kwa Umar kulifanya kwa Abubakr kwa nini isifae kwake kulifanya yeye mwenyewe kwa njia ile ile kwa mwingine? Na hapa tunaona kwamba ibn Abbas na Abdur-Rahman bin Auf na Umar bin Khatab wanakwepa kulitaja jina la huyu msemaji kama ambavyo wanakwepa kulitaja jina la mtu anayetaka kupewa baia msemaji huyu. Na ilipokuwa wawili hawa wanao umuhimu mkubwa kwa Waislamu, tunamuona Umar alikasirika kwa usemi huu na haraka katika Ijumaa ya kwanza aliwahutubia watu na akaieleza maudhui ya Ukhalifa itakavyokuwa baada yake na akawaonesha maoni yake mapya kuhusiana na Ukhalifa, ili azuwie njia ya huyu anayetaka kurudisha ile ghafla iliyokwisha tokea kwani njia hiyo itamnufaisha mgomvi wake, kwani kwa kupitia uchunguzi tumefahamu kuwa usemi huo haukuwa ni maoni ya fulani tu peke yake, bali ulikuwa ndiyo mtazamo wa Masahaba wengi, na ndiyo maana Bukhari anasema: "Umar alichukia na kisha akasema bila shaka apendapo Mwenyezi Mungu mimi nitasimama usiku huu miongoni mwa watu niwaonye hawa ambao wanataka kuwapora mambo yao..." [61]

Basi kubadilisha kwa Umar mtazamo wake kuhusu Baia ilikuwa ni kuwapinga hawa ambao wanataka kuwapokonya watu mambo yao na wambai Ali, na hili ni jambo ambalo Umar hakubaliani nalo kwani yeye anaitakidi kuwa Ukhalifa ni miongoni mwa mambo ya watu na siyo haki ya Ali bin abi Talib, na itikadi hii itapokuwa ni sahihi, basi ni kwa nini yeye Umar aliruhusu kuwapokonya watu mambo yao baada ya kufariki Mtume (s.a.w.) na haraka haraka akambai Abubakar bila ya makubaliano na Waislamu. Na msimamo wa Abu Hafs (Umar) dhidi ya Abul-Hasan (Ali) unaeleweka na ni mashuhuri mno, nao ni kumtenga Ali kwenye utawala kwa kutumia njia yoyote inayowezekana.

Na matokeo haya hatukuyafahamu kutokana na hotuba yake (Umar) iliyotangulia hapo kabla peke yake, lakini yeyote mwenye kufuatilia historia atafahamu kuwa Umar bin Al-Khatab alikuwa ndiye mtawala mtendaji hata katika Ukhalifa wa Abubakr na ndiyo maana tunamuona Abubakr anamuomba Usamah bin Zaid amuachie Umar bin Al-Khatab ili amsaidie kuhusu suala la Ukhalifa kama alivyoeleza hilo Ibn Saad ndani ya Tabaqat yake na pia wanahistoria wengi walioelezea jeshi la Usamah - pamoja na hayo tunamuona Ali bin Abi Talib anabakia mbali na majukumu, hawakumpa cheo chochote wala utawala wowote wala kumpa uamiri wa jeshi lolote lile na wala hawakumuamini kuwa mweka hazina na yote haya ni kwa kipindi cha Ukhalifa wa Abubakr, Umar na Uthman, nasi sote twamjua Ali bin Abi Talib ni nani.

Cha kushangaza kuliko yote haya ni kuwa, sisi tunasoma ndani ya vitabu vya historia kwamba kifo kilipomfikia Umar alisikitika kwamba lau Abu Ubaidah bin Al-Jarrah au Salim Huru wa Abu Hudhaifah wangekuwa hai angewatawalisha baada yake. Lakini hapana shaka Umar alikumbuka kuwa hapo kabla alikwisha badilisha mtazamo wake juu ya baia kama hii na akaiona kuwa ni ya kushitukiza na ni kupokonya mambo ya Waislamu, basi hapana budi kwake aweke njia mpya kuhusu baia ili kati kwa kati asije yeyote akafaulu kumbai amuonaye kuwa anafaa na kuwalazimisha watu kumfuata kama alivyofanya yeye kwa Abubakr na kama alivyofanya Abubakar kwake Umar au kama atakavyofanya fulani ambaye anangoja kufa kwa Umar ili ambai jamaa yake.Basi hili haliwezekani baada ya Umar kuwa ameuhukumia Ukhalifa kuwa ni jambo lililofanyika ghafla na kuwa linataka kuwa ni jambo la kupora, na haiwezekani pia kwake kuliacha jambo hili liwe la makubaliano baina ya Waislamu. Na ule mkutano wa Saqifah uliofuatia kufariki kwa Mtume (s.a.w.) yeye Umar alihudhuria na akajionea mwenyewe hitilafu iliyotokea ambayo karibu zitoke roho za watu na damu imwagike.

Basi baadaye alitoa fikra ya watu wa mashauriano au (tuseme) watu sita ambao peke yao ndiyo wenye haki ya kumchagua Khalifa na Muislamu mwingine yeyote hana haki ya kushirikiana nao katika jambo hilo, na Umar alikuwa akitambua kwamba tofauti baina ya watu hawa sita haiwezi kuepukwa, ndiyo maana aliusia ikiwa watatofautiana basi wawe kwenye upande alioko Abdur-Rahman bin Auf hata kama itapelekea kuwauwa watu watatu ambao watamkhalifu Abdur-Rahman bin Auf wakati watakapogawika watu hawa sita makundi mawili, na hilo ni muhali kwani Umar anafahamu kwamba Saad bin Abi Waqas ambaye ni ibn Ammi ya Abdur-Rahman bin Auf na wawili hawa ni ukoo wa Bani Zuhrah, na alifahamu pia kwamba Saad hampendi Ali na moyoni mwake kulikuwa na chuki kwani Ali ndiye aliyewauwa wajomba zake wa ukoo wa Abdis-Shams, kama ambavyo Umar alikuwa akifahamu kwamba Abdur-Rahman bin Auf ni shemeji wa Uthman kwani mkewe aliyekuwa akiitwa Ummu Kul-thum ni dada wa Uthman. Si hivyo tu kadhalika alifahamu kuwa Tal-hah akimpenda Uthman kutokana na mahusiano yaliyokuwepo baina yao kufuatana na maelezo ya baadhi ya wapokezi wa khabari, na hakika ilitosha kwa Tal-hah kumpenda Uthman kutokana na kumpinga kwake Ali kwani yeye Tal-hah ni katika ukoo wa Bani Taym, na kulikuwa na chuki fulani baina ya Bani Hashim na Bani Taym kutokana na Ukhalifa wa Abubakar.

Taz: Shark Najul-Balaghah ya Muhammad Abdoh, Juz. 1 uk. 88.

Umar alikuwa akiyajuwa yote hayo na kwa ajili hii ndiyo maana akawachagua hawa peke yao. Umar aliwachagua hawa watu sita na wote wakiwa ni Maquraish na wote ni kutoka katika Muhajirina na hakuna yeyote kati yao ambaye ni kutoka miongoni mwa Ansar na wote hawa kila mmoja wao akiwakilisha na kuongoza kabila lenye umuhimu wake na athari yake.

1. Ali bin Abi Talib, kiongozi wa Bani Hashim.

2. Uthman bin Affan kiongozi wa Bani Umayyah

3. Abdur-Rahman bin Auf, kiongozi wa Bani Zuhrah

4. Saad bin Abi Waqqas, yeye ni kutoka katika Bani Zuhrah na wajomba zake ni Bani Umayyah.

5. Tal-ha bin Ubaidullah, Bwana wa Bani Taym.

6. Zubair bin Al-Awwan, yeye ni mtoto wa Safiyyah ambaye ni shangazi yake Mtume na ni mume wa As-maa binti Abubakr.

Basi hawa ndiyo wenye kutoa maamuzi, na hukmu yao ikubaliwe na Waislam wote, sawa sawa wakiwa ni wakaazi wa Madina (Makao Makuu ya Ukhalifa) au wengineo katika ulimwengu wote wa Kiislamu na ni wajibu wa Waislamu yeyote atakayetoka miongoni mwao akawa kinyume cha maamuzi yao basi damu yake imwagwe (auawe). Na hili ndilo jambo pekee tulilokuwa tunataka kulisogeza katika akili ya msomaji kuhusiana na kunyamaziwa kwa tamko la Ghadir katika maelezo yaliyotangulia.

Na ikiwa Umar anaufahamu undani, mapenzi na mtazamo wa watu hawa sita, basi bila shaka yeye alikuwa kisha mpendekeza Uthman bin Affan kuwa Khalifah au alikuwa anajua kuwa wengi miongoni mwa hawa sita hawamkubali Ali, vinginevyo ni kwa nini na ni kwa haki gani Umar anatilia nguvu upande wa Abdur-Rahman bin Auf dhidi ya Ali bin Abi Talib wakati ambapo Waislamu tangu hapo zamani na mpaka leo wamekuwa wakishindana juu ya ubora wa Ali na Abubakar na hatujamsikia yeyote akimlinganisha Ali na Abdur-Rahman bin Auf.

Na hapa hapana budi nisimame kidogo ili niwaulize Masunni ambao wanatetea msingi wa mashauriano na pia (niwaulize) watu wenye fikra iliyohuru wote kwa ujumla, nawauliza wote hawa, ni vipi mnaafiki baina ya mashauriano kwa maana yake ya Kiislamu na baina ya fikra hii ambayo kama itajulisha kitu fulani basi haitajulisha isipokuwa ni maoni ya ki-dikteta, kwani yeye Umar ndiye aliyewachagua watu hawa sita na siyo Waislamu, na iwapo kuufikia kwake Ukhalifa lilikuwa ni jambo la ghafla, basi ni kwa haki ipi anawalazimisha Waislamu wakubali mmoja wa hawa sita?

Kinachojitokeza kwetu ni kwamba Umar anauona Ukhalifa kuwa ni haki ya Muhajirina peke yao na mwingine yeyote hana haki ya kuwakorofisha kwenye jambo hili, bali zaidi ya hivi ni kuwa Umar anaitakidi kama anavyoitakidi Abubakar kwamba Ukhalifa ni milki ya Maquraish, bali wamo pia wasiokuwa Waarabu, hivyo basi haistahiki kwa Sal-man Al-Farisi wala Ammar bin Yasir wala Bilal wa Uhabeshi wala Suhayb Mrumi, wala Abu Dharri Al-Ghifari wala maelfu ya Masahaba ambao siyo Maquraish (haistahiki kwao) kujitokeza kwa ajili ya Ukhalifa. Na haya siyo madai ya hivi hivi tu sivyo kabisa, bali hiyo ndiyo itikadi yao ambayo historia na wataalamu wa hadithi wameisajili kutoka vinywani mwao (kina Abubakar na Umar) na hebu tuirudie khutba yenyewe ambayo Bukhari na Muslim wameieleza ndani ya Sahih zao:

Umar bin Al-Khatab anasema:

"Nilitaka kusema, na nilikuwa nimetunga vizuri usemi ambao ulinifurahisha nikitaka niutamke mbele ya Abubakr na nilikuwa nikimzunguka karibu. Basi nilipotaka kusema Abubakr akasema, tulia (ewe Umar), na sikupenda kumkasirisha. Abubakar akazungumza, na alikuwa mpole mno kuliko mimi na mtulivu mno, Wallahi hakuacha neno lolote katika maneno nilioyaandaa isipokuwa aliyasema vizuri zaidi mpaka aliponyamaza kisha akasema, nilichokieleza kwenu katika wema ninyi ndiyo mnaostahiki (akiwaambia Maansari) na wala jambo hili halitatambulika isipokuwa kwa upande huu wa Maquraish. Taz: Sahih Bukhar Babul-Wasiyyah.

Kwa hiyo inatubainikia wazi- kwamba Abubakr na Umar hawaamini mashauriano na hiyari, na baadhi ya wanahistoria wanasema kwamba Abubakar alitoa hoja dhidi ya Maansar kwa hadithi ya Mtume (s.a.w.) isemayo kuwa "Ukhalifa uko kwa Maquraish" Na hadithi hiyo hapana shaka ni sahihi (kama walivyoitaja Bukhar na Muslim na Sahih zote kwa Masunni na Mashia) Mtume (s.a.w.) amesema: "Makhalifa baada yangu ni kumi na wawili na wote ni kutoka kwa Maquraishi" na hadithi iliyo wazi zaidi kuliko hii ni ile kauli ya Mtume (s.a.w.) aliposema:

"Jambo hili (la Ukhalifa) halitakoma kwa Maquraish muda wote hata wakibakia watu wawili"[62] pia kauli yake isemayo "Watu ni wafuasi wa Maquraishi katika kheri na shari[63].

Basi ikiwa Waislamu wote wanaziamini hadithi hizi, ni vipi mtu aseme kuwa Mtume aliliwacha suala la Ukhalifa liwe la mashauriano baina ya Waislamu wamchague wamtakaye? Na haiwezekani kwetu sisi kukwepa kupingana huku, isipokuwa tutakapoyachukua maneno ya Maimamu wa nyumba ya Mtume na wafuasi wao na baadhi ya wanachuoni wa Kisunni ambao wanasisitiza kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwataja Makhalifa na akawabainisha kwa idadi yao na majina yao, na hapo ndipo utakapoweza pia kuufahamu msimamo wa Umar na kuuthibiti Ukhalifa kwa Maquraish na huyu Umar ni mtu aliyefahamika kwa Ijtihadi yake dhidi ya maagizo ya Mtume hata katika uhai wake mwenyewe Mtume (s.a.w.), kwani matukio ya Sul-hu ya Hudaybiyah[64] kuwasalia wanafiki,[65] msiba wa siku ya Al-Khamis,[66] na kuzuwiya kwake kubashiria watu pepo[67] ni ushahidi mkubwa wa haya tuyasemayo.

Basi haishangazi kwa Umar kufanya Ij-tihad baada ya kufariki Mtume dhidi ya hadithi inayohusu Ukhalifa, haoni ulazima wa kukubali agizo linalomuhusu Ali bin Abi Talib ambaye ni Quraish, mdogo kwa umri. Ni yeye aliyeidhibiti haki ya kumchagua Khalifa kwa Maquraish peke yao, na ni yeye ambaye alilazimisha peke yake kuchagua watu sita miongoni mwa watukufu wa Kiquraishi kabla hajafa ili ikubaliane kati ya hadithi ya Mtume (s.a.w.) na vile aonavyo yeye juu ya haki ya Maquraishi peke yao kuhusika na Ukhalifa. Huenda kumuingiza Ali katika kundi hilo hali yakuwa akifahamu kwamba wao hawatamchagua, ni udhibiti wake kwa Umma ili amlazimishe Ali kuingia pamoja nao ndani ya mchezo wa Kisiasa kama wanavyouita leo hii na ili pasibakie kwa Ali na wafuasi wake na wapenzi wake ambao walikuwa wakidai kuwa yeye ndiye wa mwanzo (pasibakie kwao) hoja yeyote. Lakini Imam Ali aliyazungumza yote hayo katika hotuba yake mbele ya watu wote akasema kuhusu jambo hilo:

"Nilivumilia muda wote wa taabu na majaribu mpaka alivyoondoka akauweka (Ukhalifa) chini ya maamuzi ya kikundi cha watu sita akidhania kuwa mimi nafanana nao oh! hayawi sawa ya Mungu na mashauriano! Toka lini nikatiliwa mashaka na wa kwanza miongoni mwao mpaka imebidi nilinganishwe na watu kama hawa! lakini nilitua walipotua na niliruka waliporuka (yaani, niliishi nao kwa hekima).

Nne: Hakika Imam Ali (a.s.) alitoa hoja dhidi yao kwa kila namna lakini bila mafanikio, na je, Imam Ali aombe baia ya watu ambao walimgeuzia nyuso zao na nyoyo zao zikawaelekea wengine imma kwa husuda dhidi yake kutokana na yale aliyompa Mwenyezi Mungu miongoni mwa fadhila zake, na imma kwa chuki dhidi yake kwani yeye ndiye aliyewaua mabwana zao, akawabomoa mashujaa wao, akawakatisha tamaa, akawadhalilisha na kuvunja ujeuri wao kwa upanga wake na ushujaa wake mpaka wakasilimu na kujisalimisha hali ya kuwa Imam Ali akiwa ni Mtukufu akimtetea mwana wa ammi yake (Mtume s.a.w.) na alipokuwa akifanya hayo haikumzuwia kuyatenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu lawama ya mwenye kulaumu na wala hakurudi nyuma kwenye azma yake kutokana na tamaa ya dunia. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) naye alikuwa akiyajua vema hayo na kila tukio alikuwa akitilia mkazo fadhaila za nduguye na mwana wa ammi yake ili kuwafanya wampende. Mtume alikuwa akisema "Kumpenda Ali ni (dalili ya) imani na kumchukia (ni dalili ya) unafiki"[68] Na pia husema "Ali anatokana nami, nami natokana na Ali."[69] Na alikuwa akisema: "Ali ni mtawala wa kila muumini baada yangu"[70] na husema kuwa, "Ali ni mlango wa mji wa elimu yangu na ni baba wa wanangu."[71] Pia Mtume alikuwa akisema, "Ali ni Bwana wa Waislamu na ni Imamu wa wachamungu na ni kiongozi wa waumini wenye kutowa mwanga na nuru."[72]

Lakini inasikitisha kwamba yote hayo hayakuwazidishia isipokuwa chuki na husuda na kwa ajili hiyo Mtume alimuita Ali kabla ya kufariki akamkumbatia kisha akalia na akamwambia: "Ewe Ali bila shaka mimi nafahamu kwamba ndani ya nyoyo za jamaa hawa kuna shinikizo la chuki dhidi yako, na hapo baadaye watakudhihirishia baada yangu mimi, iwapo watakupa baia kubali vinginevyo basi subiri mpaka hapo utapokutana nami hali ya kuwa mwenye kudhulumiwa". Taz: Ar-Riyadun-Naz-Rah Fi Manaqibil-Asharah cha Tabari Babu Fadail Ali ibn Abi Talib. Basi ikiwa Abul-Hasan (a.s.) ilimlazimu kuvumilia baada ya baia ya Abubakr, hilo ni kutokana na usia wa Mtume kwake yeye na ndani ya hilo muna hekima ambayo iko wazi.

Tano: Zaidi ya yote hayo yaliyotangulia ni kwamba, Muislamu ataposoma Qur'an Tukufu na kuzizingatia aya zake, atafahamu kwa kupitia masimulizi yake kuhusu mambo ambayo yaliwafika watu na mataifa yaliyopita kwamba, kwao yalitokea mengi kuliko yale yaliyotokea kwetu sisi. Basi mwangalie huyu Qabil anamuuwa nduguye Habil kwa dhulma na uadui tu, na huyu hapa Nuh ambaye ni babu wa Manabii, baada ya miaka elfu moja ya jihadi hakuna aliyemfuata katika watu wake isipokuwa wachache tu, isitoshe mkewe na mwanawe walikuwa miongoni mwa makafiri.

Mtazame Nabii Lut haikupatikana katika kitongoji chake isipokuwa nyumba moja tu ya Waumini. Nao Mafirauni ambao walikuwa wenye kiburi katika nchi wakawafanya watu kuwa watumwa, hapakuwepo miongoni mwao isipokuwa Muumini mmoja anayeficha imani yake. Hawa hapa nduguze Yusuf watoto wa Yaaqub nao ni kikundi, wanakula njama kumuuwa ndugu yao mdogo asiye na kosa lolote lakini (wanafanya hivyo) kwa kumhusudu kwa kuwa yeye ni kipenzi kwa baba yao. Watazame wana wa Israel ambao Mwenyezi Mungu aliwaokoa kupitia kwa Musa na akawapasulia bahari na kumuangamiza adui yao Firauni na askari wake bila ya kuwakalifisha taabu yoyote ya vita, basi mara walipotoka baharini na nyayo zao hata hazijakauka, wakawafikia watu wanaoabudia sanamu (wana wa Israel) wakasema:

"Ewe Musa tutengenezee Mungu kama wao walivyo na Miungu, Musa akawaambia hakika ninyi ni watu msiojua." Na alipokwenda kwenye ahadi ya Mola wake na kumuacha nduguye Harun, walifanya njama dhidi yake karibu wamuuwe, wakamkufuru Mwenyezi Mungu, na wakamuabudia ndama kisha baadaye waliwauwa Manabii wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema: "Kila walipokufikieni Mitume kwa yale ambayo nafsi zenu haziyapendi mlijivuna, kundi moja mlilipinga na kundi jingine mkaliua".(Qur'an, 2:87)

Huyu hapa naye Bwana wetu Yahya bin Zakariya naye ni Nabii na Mtawa miongoni mwa watu wema anauwawa na kichwa chake anazawadiwa mtu muovu miongoni mwa waovu wa Kibani Israel. Mayahudi na Wakristo nao walikula njama kumuua na kumsulubu bwana wetu Isa. Nao ummati wa Muhammad wanaandaa jeshi la kiasi ya watu elfu thelathini ili kumuuwa kipenzi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu na Bwana wa vijana wa peponi ambaye hawakuwa pamoja naye isipokuwa watu Sabini miongoni mwa wafuasi wake, wakawauwa wote ikiwa ni pamoja na mwanawe mchanga. La ajabu ni lipi baada ya yote haya? Lipi litashangaza baada ya kauli ya Mtume kuwaambia Masahaba wake yakuwa: "Mutafuata nyendo za wale waliokuwa kabla yenu shubiri baada ya shubiri na dhiraa baada ya dhiraa mpaka hata wakiingia kwenye shimo la kenge nanyi mutaingia". wakasema, "Wadhani kuwa hao ni Mayahudi na Wakristo"? Mtume akasema, "Ni kina nani basi (kama si hao)"?

Taz: Sahih BukharJuz. 4 uk. 144 na Juz. 8 uk. 151. Ni kipi cha ajabu basi, nasi twasoma ndani ya Bukhar na Muslim kauli ya Mtume (s.a.w.) isemayo: "Siku ya Kiyama Masahaba wangu watapelekwa upande wa kushoto nami nitasema wanapelekwa wapi? Patasemwa Wallahi Motoni, nitasema, Ewe Mola wangu Masahaba wangu hao, patasemwa, Hakika wewe hujuwi waliyoyazusha baada yako, nitasema atengwe mbali aliyebadilisha baada yangu, na sitamuona anaokoka miongoni mwao isipokuwa kikundi kidogo kama cha ngamia waliotelekezwa".

Tax: Sahih Bukhar Juz. 7 uk. 209 na Sahih Muslim Babul-Haudh. Basi lipi la ajabu baada ya kauli yake Mtume (s.a.w.) aliposema: "Umati wangu utagawanyika makundi sabini na tatu na yote yataingia motoni isipokuwa kundi moja". Taz: Sunan Ibn Majah Kitabul-Fitan Juz. 2 hadith Na. 3993, Ahmad Juz. 3 uk. 120, Sunan Tirmidhi Kitabul-Iman. Amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola mwenye nguvu na Utukufu, mjuzi wa undani wa nyoyo pale aliposema: "Na watu wengi hawataamini japo utapupia" (Qur'an, 12:103)

"Bali amewajia na ukweli na wengi wao wanaichukia kweli" (Qur'an,23:70)

"Bila shaka tumekujieni na ukweli lakini wengi wenu hawaupendi ukweli" (Qur'an 43:78)

"Fahamuni ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli lakini wengi wao hawafahamu" (Qur'an, 10:55)

"Wanakuridhisheni kwa vinywa vyao na nyoyo zao zinakataa, na wengi wao ni mafasiki (Qur'an, 9:8)

"Bila shaka Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila juu ya watu, lakini watu wengi hawashukuru" (Qur'an, 10:60)

"Wanaitambua Neema ya Mwenyezi Mungu kisha wanaipinga na wengi wanakataa ila kukufuru tu" (Qur'an, 25:50)

"Na wengi wao hawawezi kumuamini Mwenyezi Mungu ila hali ya kuwa wanamshirikisha" (Qur'an, 12:106)

"Bali wengi wao hawaijuwi haki basi wao wanapinga" (Qur'an, 21:24)

"Hivi mwashangazwa na mazungumzo haya na mnacheka wala hamlii hali ya kuwa ninyi mmeghafilika (mmejisahau)" (Qur'an, 53:61