ATAKAPOKUJA

ATAKAPOKUJA0%

ATAKAPOKUJA Mwandishi:
: S. Muhammad Ridha Shushtary
Kundi: Imam mahdi (a.s)

ATAKAPOKUJA

Mwandishi: Sayyid Mahdi Shuja'i
: S. Muhammad Ridha Shushtary
Kundi:

Matembeleo: 2909
Pakua: 1556

Maelezo zaidi:

Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 3 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 2909 / Pakua: 1556
Kiwango Kiwango Kiwango
ATAKAPOKUJA

ATAKAPOKUJA

Mwandishi:
Swahili

ATAKAPOKUJA

MTUNGAJI: SAYYID MAHDI SHUJA'I

MTARJUMI: S. MUHAMMAD RIDHA SHUSHTARY

Mwaridi mwekundu ulikuwa umefifia kwa huzuni. Mashina yake yalilegea na matawi yake yaliinama. Mwaridi uliopooza ulijikaza kuutazama mlangilangi na kuunong'oneza: "Nimechoka. Nimechoka sana." Kwa msaada wa upepo, mlangilangi uliyapepea matawi yake upande wa mwaridi na ukajiinamisha kidogo ili kuweza kusikia vizuri maneno yake: "Umesema umechoka? Nimesikia vizuri? Ina maana kwamba wewe umechoka kama mimi?" Mwaridi mwekundu ulishangazwa na jibu la mlangilangi, ukakiinua zaidi kikonyo chake kilichoinama na kuuliza: "Wewe? Kweli wewe umechoka pia? Kwa nini wewe?" Mlangilangi ukayaweka matawi yake juu ya matawi ya mwaridi kwa huruma na kusema: "Uchungu wangu hausemeki. Huzuni yangi si kisa cha leo wala cha jana. Tangu siku ile nilipojitambua mwenyewe, nilianza kuishi kwa majonzi. Lakini wewe je? Sema! Toa uchungu wako! Huenda moyo wako ukapoa. Huenda majonzi yako yakapungua kidogo." Waridi jekundu ambalo lilikuwa likijichanua, na umande ulikuwa ukilengalenga kwenye petali zake, likasema: "Majonzi yangu si madogo. Wala uchovu wangu si uchovu mdogo. Moyo wangu umevunjika mno kwa kadiri kwamba nyimbo za chiriku na zawaridi (zuwardi) haziwezi kuburudisha moyo wangu.

Mimi nimechoka mno na kupooza. Matumba na maua yamelegea katika mikono ya wapita njia. Kwa muda mrefu sasa ninamngojea yule ambaye hakuna ua lolote litakalopooza na kunyauka katika mikono yake ya huruma." Kwa ghafla, waridi likaangua kilio na umande ukaanza kuchururika. Kijito ambacho mpaka wakati huo kilikuwa kikipita polepole karibu na mwaridi, kilisikia maneno ya waridi jekundu bila ya kutaka. Kwa kudondoka chozi moja tu la waridi kwenye maji, maji yakachafuka, yakajisukuma na kutoka kwenye mkondo wake na kulikaribia ua la waridi. Kijito kikasema: "Rafiki yangu mpole! Kwa hakika umenisemea vizuri maneno yangu ya moyoni. Umeyaeleza vizuri majonzi yangu." Waridi likaelekea upande wa kijito (mto mdogo) likapangusa machozi yake kwa matawi yake na kuuliza: "Wewe! Kwani nawe pia una huzuni? Vipi? Wewe ambaye kutwa kucha unakwenda katika hali ya furaha na kuchangamka, na unapita katika ardhi pana na safi, vipi uwe na majonzi?

Kijito kikatazama kwa mtazamo wake wenye unyevu kwenye macho yenye machozi ya waridi na kusema: "Kwenda, kukimbia na kutafuta kwangu si kwa sababu ya furaha, bali ni kwa sababu ya kutoona raha na kutovumilia kwangu. Kwani mimi sioni ukame? Kwani mimi sina habari ya kiu ya miti? Kwani mimi sijui kwamba maua mengi yanakauka na kufa kila siku kwa sababu ya kukosa maji? Babangu, babu yangu na baba wa babu yangu walikuwa wakisema: 'Atakuja mtu ambaye atakapoosha mikono yake katika kijito au mto, maji yatakuwa na baraka na mengi mno kwa kadiri kwamba hautakuwepo mti au mmea wowote ardhini ambao utaona kiu.'" "Mimi siku zote ninamngojea yeye. Kila siku tangu asubuhi mpaka usiku na tangu usiku mpaka asubuhi ninamtafuta, na ninapita mikondo hiyo yote kumtafuta. Tazama! Miguu yangu imejaa malengelenge! Mimi sijakuwa na furaha wakati wowote, wala sitakuwa na furaha mpaka aje." Waridi ambalo mpaka wakati huo lilikuwa likisikiliza maneno ya kijito kwa mshangao, likahisi kwamba lina maneno mengi ya kusema, lakini lilipomwona paa akija kwa kuchchemea, likapiga kelele: "Marafiki! Tazameni kule!"

Mlangilangi na kijito, vyote vilielekea upande ulioonyeshawa na waridi jekundu, na vilishangaa kumwona paa mzuri akija huku macho yake yakimlengalenga machozi na mguu wake ukitoka damu. Njia aliyokuwa akijia paa ilikaa alama za damu ya mguu. Paa akaja kwa kijito huku akilia. Akaamkia kisha akakaa hapohapo kwa sababu ya kuchoka sana. Kijito kikajisukuma juu zaidi ili paa anywe maji na apumzike. Mlangilangi ukaanza kumpepea kwa matawi yake yaliyokuwa yakining'inia, na waridi likamwuliza kwa upole: "Rafiki mpenzi! Ni nani aliyekuumiza mguu wako?" Paa akayafumba macho yake, akapiga kite na kusema: "Maumivu yangu si ya mguu, ni maumivu ya moyoni. Jeraha langu hasa si hili la mguu, ni la maini..." Mlangilangi ukayatikisa matawi yake juu ya paa na kumwuliza: "Kwani wewe una jeraha jingine mbali na jeraha hili la mguu?" Waridi baada ya kuvitazama viungo vyote vya paa, likajiinua na kusema kwa mshangao: "Sioni jeraha jingine mwili wala viungo vyako." Kijito kikayatazama macho ya paa na kuuliza: "Ni nani aliyekutia uchungu moyo wako?"

Paa akautazama mguu wake uliorowa damu na akasema: "Maumivu yangu si maumivi mapya. Ikiwa nitapata nafasi kabla ya kuja mwindaji, nitakuambieni huzuni yangu ni ya nini." Mlangilangi ukasema: "Basi niache kwanza nilifunge jeraha lako ili kwamba ikiwa mwindaji atatokea, uweze kukimbia." Kijito kikaanza kuliosha jeraha la mguu wa paa na kusema: "Kwa bahati nzuri, jeraha lako si kubwa. Mshale umeukwaruza mguu wako na kuuumiza." Paa ambaye alipata maumivu zaidi kwa kuoshwa kwa maji, alilia na kusema: "Sijui kwa taabu gani nilivyoweza kumkimbia mwindaji." Kijito kilipokwishaosha barabara jeraha la paa, waridi likaweka petali chache juu ya jeraha, na mlangilangi ukafunga jeraha hilo kwa majani na vijiti vyake laini. Paa akavuta pumzi ndefu na akahisi kwamba maumivu ya mguu wake yamepungua. Waridi likatabasamu na kusema: "Basi sasa tuambie maumivu yako hasa ni nini? Maumivu ambayo ulisema yanakuuma daima." Paa akaunyosha mguu wake ulioumia, akauegemea mlangilangi na akasema: "Jana mbwa mwitu alimrarua mtoto wangu wa pekee na kumla." Shina la mlangilangi likainama kidogo kusikia habari hiyo, kijito kikachafuka na machozi yakalengalenga machoni mwa waridi jekundu. Paa akaendelea kusema kabla ya wengine kusema au kuuliza: "Alikuwa ni mwanangu wa pekee niliyekuwa nikimpenda sana. Lakini maumivu yangu yote si hayo." Waridi, mlangilangi na kijito vikauliza kwa pamoja: "Basi hayo soi maumivu yako yote? Msiba mkubwa kama huu..."

Paa akasema: "Msiba huu ni mkubwa, lakini jeraha langu hasa ni kubwa zaidi. Maumivu yangu na ya kungojea. Maumivu ya aisha haya yamechanganyika na kukimbia. Kila siku tangu asubuhi mpaka usiku sina raha, ninakimbia kwa kumwogopa mwindaji au wanyama wakali. Usiku hujitupa pembeni kwa sababu ya kuchoka sana. Lakini hata usiki sipati usingizi kwa kuogopa." "Mimi ninajua kwamba hali hii haitaendelea daima." "Mimi ninajua kwamba itakuja siku moja ambapo atakuja mtu mmoja atakayeleta utulivu na raha." "Nimesikia kwamba atakapokuja yeye hakuna mbwa yeyote atakayemla mtoto wa paa, wala hakuna msahle wowote utakaompiga paa." Ninajua kwamba kuna siku atakayokuja mtu huyo, lakini sijui huyo ni nani na lini atakuja." "Na kungojea huko kunaniumiza."

Mlangilangi ambao ulikuwa ukimpepea paa polepole kwa matawi yake laini, ulisema: "Ni mkasa wa ajabu! Wewe pia, na kijito na waridi, nyote mna maumivu yaleyale niliyonayo mimi. Nyinyi mnangojea kama mimi ninavyogojea. Sisi milangilangi mwanzoni hatukuwa kama hivi tulivyo sasa tumechoka. Maumivu ya kungojea yametuzeesha. Afadhali tungejua ni nani huyo." Ua la waridi jekundu likajipangusa machozi na kusema: "Angalau tungejua ni nani huyo tunayemngojea." Kijito kikatulia kidogo, kisha kikasema: "Ni vizuri tungejua lini atakuja."

Paa akatazama jeraha la mguu wake, kisha akasema: "Ni bora tungejua inatupasa tufanye nini ili yeye aje mapema zaidi." Baada ya wote kuuliza maswali hayo, wakanyamaza kimya kwa masikitiko. Ukapita muda kidogo katika ukimya huo. Mara kijito kikakumbuka kitu. Kikaruka bila ya mwenyewe kufahamu, na maji yake yakaruka kwenye uso wa paa na waridi. Shina la mlangilangi likarowana kutokana na kuruka kwa ghafla maji ya kijito. Wote wakauliza kwa pamoja: "Nini tena!?" Kijito kikasema kwa msisimko: "Mimi nimekumbuka jambo moja. Katika njia hii ambayo naipita kila siku, hupita kandoni mwa banda moja anamoishi mzee mmoja mwnye busara. Hapana shaka yeye anajua majibu ya maswali mengi. Kila siku ninawaona watu wakienda kwake kumwuliza maswali. Twendeni bandani kwa mzee huyo." Paa akasema: "Ni fikra nzuri. Mimi niko tayari kwenda njia hii yote kwa kuchechemea mpaka nifike bandanai kwa mzee." Mlangilangi ukajitazama shina lake na kusema: "Ni fikra nzuri lakini nitawezaje kuja nanyi kwa mzee hali mizizi yangu ima ardhini?" warid jekundu likasema: "Mimi pia na kama mlangilangi, nimefungika ardhini. Lakini napenda sana kumwona mzee mwenye busara."

Paa akasema: "Hakuna njia nyingine. Mimi na kijito wenye kuweza kwenda tutakwenda kwake. Tutamwuliza maswali na tutakuleteeni majibu yake." Mlangilangi na waridi vikatazamana na kusema: "Basi bora mfanye hivyo, kwani hakuna njia nyingine." Paa akajitayarisha kuondoka pamoja na kijito. Lakini kabla ya kuondoka, mwaridi ukakipa kijito maua yake kadhaa yasiyochanua na kukiambia: "Nisalimie mzee mwenye busara na mpe mawaridi haya kama ni zawadi kutoka kwangu." Mlangilangi pia ukaweka shada la langilangi pamoja na mawaridi mekundu na ukasema: Vilevile mpe salamu zangu mee mwenye busara." Kijito na paa wakaondoka. Njiani, kijito kilimwagazia paa kwamba watakapofika tu kwenye banda achukue mawaridi na shada la langilangi kutoka kwake, kwa kuwa kijito hakiwezi kuvishika kwa muda mrefu.

Paa akasikia maagizo ya kijito na wakaendelea na safari. Walipofika kwenye banda la mzee, paa akapokea mawaridi mekundu na shada la langilangi kutoka kwa kijito na akagonga mlango wa banda. Banda la mzee lilkuwa katikati ya ardhi lakini halikuwa na ua. Mlango wake ulikuwa wazi lakini paa hakutaka kuigia ndani bila ya ruhusa. Muda si muda, mzee mwenye ndevu nyeupe na uso wa nuru akatopa bandani akienda kwa fimbo. Paa akamtolea salamu na mzee akamsogelea paa polepole, akaweka mkono wake juu ya kichwa na shingo ya paa na akasema: "Salamu aleikum, paa mzuri! Hapana shaka umeumia na umekuja kwangu kwa sababu hiyo. Njoo, njoo ndani ya banda upumzike ili niweze kukupa dawa." Paa akasema: "Ahsante sana mzee mpole! Mimi sikuja hapa kwa sababu ya jeraha langu. Ikiwa si taabu kwako tafadhali njoo karibu na kijito ili mimi na kijito tukuulize maswali yetu. Vilevile mlangilangi na mwaridi mwekundu ilitaka kuja kwako lakini haikuweza. Imekutumia salamu na kukupelekea zawadi hizi." Mzee akanyosha mkono wake kwa kushangaa na akapokea zawadi hizo. Akamtazama paa kwa mshangao na kusema: "Ahsante sana paa mpenzi! Nakushukuru wewe na mlangilangi na mwaridi pia. Ni zawadi nzuri sana! Moyo wangu haukutaka wakati wowote kuchuma maua au kukata tawi. Mimi nitapanda mwaridi na mlangilangi hapahapa mbele ya banda langu ili iwe makumbusho kwangu na niwakumbuke daima." Mzee akaweka mawaridi kwenye dirisha la banda na akaenda kwa kijito pamoja na paa. Kijito kikamwamkia mzee. Kikampa mkono na kuubusu uso wake unaongara. Maji ya kijito yakang'ara kama lulu kwenye ndevu za mzee.

Mzee akakaa karibu na paa na kijito na akauliza kwa kustaajabu: "Ni maswali gani yaliokutaabisheni mje mbali hadi hapa?" kijito kikajibu" "Mimi kila siku hupita karibu na banda lako, na kila usiku husikia sauti yako ya kuomba dua. Lakini sijafikiria hata mara moja kwamba ninaweza kukuuliza maswali yangu. Mimi ninajua kwamba wewe unatawadha katika chemchemi iliyopo upande ule wa banda. Maji unayotawadhia hupita katika njia nyembamba pembeni mwa banda na hujiunga nami. Mimi nikatambua kwamba hakuna maji yoyote yanayonukia uturi kama maji ya udhu wako." Kijito kikasita kidogo kisha kikaendelea kusema: "Leo nilipojua kwamba paa, mwaridi mekundu na mlangilangi vina maumivu na maswali kama yangu, nikakumbuka kwa ghafla kwamba tuje kwako kukuuliza maswali hayo." Kijito kikajaribu kujisogeza karibu zaidi na mzee: "Sisi tunamngojea mtu ambaye hakuna ua lolte litakalopooza mkononi mwake. Mtu ambaye atakapokuja, wanyama wote wanyonge watakimbilia kwake. Sisi tunajua kwamba hapana shaka yoyote yeye atakuja tu, lakini hatujui yeye ni nani, yuko wapi na lini atakuja. Na hatujui tufanye nini ili aje upesi zaidi."

Kijito hakijamaliza kusema wakati paa alipokiashiria kisite kusema na badala yake kiangalie uso wa mzee. Mzee alikuwa akisikiliza maneno ya kijito huku machozi yakimtoka polepole. Kila kijito kilivyozidi kusema ndivyo mzee alivyozidi kulia. Wakamwuliza: "Swali letu limekuhuzunisha? Sisi hatujataka..." Mzee akatabasumu pamoja na kulia kwake, na akasema: "Hapana, wapenzi wangu! Mimi sikuhuzunishwa na swali lenu..... Lakini....lakini nyinyi mmenikumbusha tena uchungu wangu. Angalau wanadamu wangekuwa na maarifa kiasi chenu..." Mzee akavuta pumzi ndefu, akapangusa machozi yake, kisha akaendelea kusema: "Kwa kweli maumivu ya kungojea si maumivu yenu peke yenu. Mimi pia ninamngojea kwa miaka mingi. Atakapokuja, ulimwngu utajaa suluhu, amani na mapenzi. Atakapokuja, udhalimu utaondoka, ubaya utaondoka na ulimwnegu utajaa uzuri na wema.[1] "Atakapokuja, hakuna atakayelala na njaa usiku."

"Atakapokuja, urafiki na mapenzi yatachukua nafasi ya uadui na uhasama." "Kila mtu anayependa wema humngojea yeye. Mitume wote wamesema kwamba atakuja." "Yeye anajulikana kwa jina la Mahdi, lakini jina lake hasa ni Muhammad. Hakuna mtu anayejua Mahdi yuko wapi na lini atakuja. Wale wenye sifa nzuri zaidi wanaweza kumwona mara kwa mara." "Yeye mwenyewe huenda kuonana na marafiki zake..." Mzee alipofika hapa, machozi yakamlengalenga tena. Akatazama huku na huko na akasema polepole: "Hata mimi ambaye sistahili, nimewahi kumwona mara moja." Mzee akaangua kilio. Kijito kikauliza kwa mshangao: "Basi ni kwa sababu hiyohiyo ndiyo maana maji hunukia manukato kwa kutawadha kwako?" Na paa akasema: "Na moyo hutulia kwa kukutazama wewe?" Mzee akaendelea kusema kana kwamba hakuyasikia maneno yao: "Lakini jambo lililo muhimu kabisa ni tufanye nini ili aje mapema zaidi."

Paa na kijito wakasema pamoja: "Ndiyo! Tufanye nini?" Mzee akasema: "Ni lazima sis wenyewe na wengine tujiandae kwa ajili ya kuja kwake. Tusipojiandaa..." Kijito na paa wakakata maneno ya mzee kwa kuuliza: "Vipi tujiandae?" Mzee akasema: Ni lazima tuwe vile ambavyo yeye atatupenda. Tuwe vile ambavyo yeye atafurahika nasi. Yeye yu hai na yuko. Anakwenda kwenye ardhi hiihii, na anavuta pumzi katika hewa hiihii. Yeye anaona kazi zetu zote." Ni lazima tufanye mambo ambayo yatamridhisha. Nyinyi mmekwenda masafa marefu sana. Huko kumgojea kwenu kuja kwake; huko kupinga kwenu udhalimu na ubaya; huko kupenda na kujitahidi kwenu kuja kwake; huko kupinga kwenu udhalimu na ubaya; huko kupenda na kujitahidi kwenu wengine wote wawe wazuri kama nyinyi; na huko kupendana kwenu - kote huko ni aina moja ya kujiandaa. Mimi nina yakini kwamba yeye anakupendeni na yuko radhi nanyi." Mzee akatazama juu kisha akasema: "Vema! Sasa ni wakati wa kusali, na marafiki zenu wanakungojeeni."

Kisha mzee akasimama kwa fimbo yake na akasema: "Ehee! Pamoja na yote hayo, msisahau kitu kimoja." Kijito na paa wakauliza kwa kustaajabu: "Kitu gani tusikisahau?" Mzee mwenye busara akatazama juu na kusema: "Dua! Ombeni dua aje upesi zaidi."

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU

YALIYOMO

ATAKAPOKUJA 1

MTUNGAJI: SAYYID MAHDI SHUJA'I 1

MTARJUMI: S. MUHAMMAD RIDHA SHUSHTARY 1

SHARTI YA KUCHAPA 5

MWISHO WA KITABU 5

YALIYOMO 6


[1] . Mtume Muhammad (s.a.w.w) amesema: "Siku moja bwana wa ulimwengu huu atakuja, ambaye atatokana na kizazi changu na jina lake litakuwa kama langu. Ataujaza ulimwengu uadilifu na usawa kama ulivyojaa udhalimu na maonevu."

Al-Jami'u 's-Saghir, uk. 104. Al-Mustadrak 'ala 's-Sahihayn, jz. 4, uk. 464-465. Muntakhab Kanzu 'l- 'Ummal, uk. 32.