MASOMO YA KI-ISLAMU 3

MASOMO YA KI-ISLAMU 30%

MASOMO YA KI-ISLAMU 3 Mwandishi:
Kundi: Misingi mikuu ya Dini

  • Anza
  • Iliyopita
  • 9 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 1389 / Pakua: 726
Kiwango Kiwango Kiwango
MASOMO YA KI-ISLAMU 3

MASOMO YA KI-ISLAMU 3

Mwandishi:
Swahili

MASOMO YA KI-ISLAM

KITABU CHA TATU

DIBAJI

Ewe Ndugu Yangu!

Je, wajua nani Mwislamu? Mwislamu ni ambaye anaamini kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja na Muhammad ni Mtume wake wa mwisho. Kama ukiamini haya, basi wewe ni Mwislamu.

Lakini haitoshi kusema tu kuwa mimi ni Mwislamu; bali ni wajibu juu yako kutenda kwa mujibu wa kanuni za Ki-islamu, ili uwe Mwislamu wa ukweli, na uishi duniani katika raha, na upate utukufu Akhera[1] kwa kuingia peponi na kupata ridhaa za Mwenyezi Mungu.

Basi ni lazima juu yako kujitahidi kufanya hayo.

Na Uislamu una sehemu tatu:

(1) Asili (Mizizi) ya Dini

(2) Matawi ya Dini

(3) Tabia (Mwenendo) ya Dini

Basi anayekubali kwa ukweli Asili ya Dini, na kutumia Matawi ya dini, na akiishajipamba na tabia ya dini, basi yeye ni mbora duniani na akhera (Kiyama[2] .

Kitabu hiki Kimefasiriwa na Sheikh Muhammed Ali Ngongabure. na kimesahihishwa na kimepangwa na Ayatullah Allamah Al-Haj Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Muasisi na Muhubiri Mkuu wa Bilal Muslim Mission ofTanzania.

Wabillahi Tawfiq.

MASOMO YA KI-ISLAM

KITABU CHA TATU

SOMO LA KWANZA

MATAWI YA DINI

Tuliandika habari juu ya Mizizi ya 'Dini' katika kitabu cha kwanza. Sasa tunaanza maelezo machache juu ya Matawi ya Dini.

Maelezo haya ni kwa mujibu wa madhehebu ya Shia-Ithna-asheriya.

Na mashuhuri katika Matawi ya Dini ni kumi:

1. Sala

2. Funga{Saumu}

3. Zaka

4. Hija

5. Khumsi

6. Jihadi {Vita kwa aj ili ya Dini}

7. Kuamrisha Mema (Amr-bil Maaruf)

8. Kukataza Mabaya (Nahil-Anil Munkar)

9. Kuwapenda Mtume(s.a.w.w) na Ahli Bayti zake

10. Kujiepusha na maadui wa Mtume(s.a.w.w) na Ahli- bayti zake.

Na katika matawi ya dini mambo kama biashara na ndoa na kisasi na fidia na kadhalika.

SOMO LA PILI

NAMNA YA SALA NA KUTAWADHA

Sala zipo za aina mbili:

1. Sala za Wajibu.

2. Sala za Sunna.

Basi sala za wajibu ni namna mbali mbali, hapa tutaeleza sala za kila siku zote, nazo ni tano (5).

Jua kuwa utapotekeleza sala ni lazima utawadhe (ufanye Wudhu).

Na namna ya kutawadha ni kama ifuatavyo:

(a) Chukua maji mataharifu na ya halali, na viwe viungo vyako tohara.

(b) Kosha mikono yako vifundoni mara tatu.

(c) Sukutuwa na utie maji puwani, kila kimoj a mara tatu.

(d) Kisha kusudia kuwa "Mimi ninatawadha kwa kutaka ukaribu wa Mungu.

(e) Utie maji usoni kwako, kuanzia maoteo ya nywele za kichwa. na utakosha mpaka kidevuni, ndio urefu na ukati wa dole gumba na kidole cha shahada, ndio upana wa uso.

(f) Baadae utakosha mkono wa kulia, kuanzia juu ya kisigino, mpaka nchani mwa vidole.

(g) Kisha utaosha mkono wa kushoto vilevile.

(h) Kisha utapaka kwa kiganja chako cha kulia sehemu ya mbele ya kichwa.

(i) Baadae utapaka kwa mkono wako wa kulia juu ya mgongo wa unyayo wako wa kulia, kuanzia vidoleni mpaka katika kifundo.

(j) Baadae utapaka kwa mkono wako wa kushoto juu ya mgongo wa unyayo wa kushoto vilevile.

SOMO LA TATU

IDADI NA WAKATI WA SALA

Ujue kuwa sala za Wajibu za siku zote ni tano:

(a) Sala ya Asubuhi ni Rakaa mbili.

Na nyakati zake ni Alfajir kabla ya kuchomoza jua.

(b) Sala ya Adhuhuri ni Rakaa nne: na

(c) Sala ya Alasiri ni Rakaa nne.

Na nyakati zake sala hizi mbili ni dhuhuri hadi kuchwa jua.

(d) Sala ya Magharibi, nayo ni Rakaa tatu, na

(e) Sala ya Isha nayo ni Rakaa nne.

Na nyakati zake sala hizi mbili ni magharibi hadi nusu ya usiku.

Hii ni kwa mwenye kuwa mkazi wa mji au kama mkazi wa mjini. Lakini msafiri husali sala za rakaa nne (Adhuhuri, alasiri na Isha) kwa rakaa mbili mbili kama sala ya Asubuhi.

MASOMO YA KI-ISLAM

KITABU CHA TATU

SOMO LA NNE

ADHAAN

Ukitaka kusali elekea kibla na usimame. Baadae Uadhini kama hivi:-

1.Allahu Akbar (mara nne)

(MWENYEZIMUNGU NI MKUBWA)

2.Ash-hadu allailahailla-Llah {marambili}

(NAKIRI KUWA HAKUNA MOLA ILA MWENYEZI MUNGU)

3. Ash hadu anna Muhammadar Rasulullah {mara mbili}

(NAKIRI KUWA NABII MUHAMMAD NI MJUMBE WA MWENYEZI MUNGU)

4.

[3] Ash-hadu anna Amiral Muuminiin Aliyyan Waliyyu-llah (mara mbili)

(NAKIRI KUWA AMIRAL MU-UMINIINA ALI NI WALII WA MWENYEZI MUNGU)

5. Hayya alas-Salaah (marambili)

(NJOONI KATIKA SALA)

6. Hyya alal-Falaah {marambili}

(NJOONI MFUZU KHERI YA DUNIA NA AKHERA)

7. Hayyaalaa Khairil-Amal {marambili}

(NJOONI KWENYE KITENDO BORA KABISA KULIKO VITENDO VYOTE).

8. AllahuAkbar {marambili}

(MWENYEZI MUNGU NI MKUBWA)

9. Lallaha llla-Llah (marambili).

(HAKUNA MOLA ILA MWENYEZI MUNGU).

SOMO LA TANO

IQAMAH

Baada ya Adhana ni bora sana kusema Iqamah. Namna yake ni kama hivi:

1. AllahuAkbar (marambili)

(MWENYEZI MUNGU NI MKUBWA)

2. Ash-hadu allailaha illah-Llah (marambili)

(NAKIRI KUWA HAKUNA MOLA ILA MWENYEZI MUNGU)

3. Ash-hadu-anna Muhammadar "Rasuulullah {mara mbili}

(NAKIRI KUWA NABII MUHAMMAD NI MJUMBE WA MWENYEZI MUNGU)

4.[4] Ash-haduAnnaAliyyan Waliyyullah (marambili).

(NAKIRI KUWA ALI NI WALII WA MWENYEZI MUNGU)

5. Hayya alas-Salaah (mara mbili)

(NJOONI KWENYE SALA).

6. Hayya alal-Falaah {mara mbili}

(NJOONI MFUZU KHERI YA DUNIA NA AKHERA)

7. Hayya Ala Khairil-amal (mara mbili)

(NJOONI KWENYE KITENDO BORA KABISA KULIKO

VITENDO VYOTE)

8. Qad-qaamatis -Salaah (mara mbili)

(SALA INAANZA SIMAMA)

9. AllahuAkbar {marambili}

(MWENYEZI MUNGU NI MKUBWA)

10.La-ilaha illa-Lllah (mara moja)

(HAKUNA MOLA ILA MWENYEZI MUNGU)

SOMO LA SITA

SALA YA ASUBUHI (i)

1. Baada ya kusema Iqamah, utanuwia sala kama hivi:-

Nasali Sala ya Asubuhi Rakaa mbili kurbatan ilallahi Taala

2. Utasema' Allahu Akbar'

3. Utasoma sura ya Al-hamdu:

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿١﴾ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٢﴾ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿٣﴾ مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ ﴿٤﴾ إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾ اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿٦﴾ صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ ﴿٧﴾

Kwa jina la Allah Mwenye rehema za dunia na rehema za Akhera

Kila sifa nzuri inamstahili Alla {Mungu} mlezi wa viumbe vyote

Mwenye rehema za dunia na akhera Mfalme wa siku ya Kiyama

Wewe tu ndie tunae kuabudu, na wewe tu ndio tunae kuomba msaada.

Tuongoze katika njia iliyo nyooka sawa. Njia ya ambao ulio waneemesha, isiokuwa ya wale ulio waghadhibikia juu yao wala wale walio potea.

4. Baadae utasoma, sura nyingnine yoyote kamili.

Afadhali usome sura ya Tawheed:

BISMILLAHIR RAHMANIR RAHIIM

QUL HUWA LLAHU AHAD*ALLAHUSSWAMAD*LAM YALID WALAM YUULAD*WALAM YAKULLAHUU KUFUWAN AHAD.

Tafsiri yake ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Allah Mwenye Rehma za dunia na Rehma za Akhera

Sema, yeye Mungu ni mmoja. Mungu, Asiye hitaji, ambaye wote wanahitaji kwake.

Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hakuwa anaye fanana naye hata mmoja.

5.Kisha utasema' Allahu Akbar' na utainama mpaka vifike viganja vyako magotini, utaweka juu yake na utasema:-

SUBHANA RABBIYAL - ADHWIMI WA BIHAMDIHI

ALLAHUMMA SWALLI ALA MUHAMMADIN WA AALI MUHAMMAD

(Ninamtukuza Mola wangu Aliye mkubwa na ninataja sifa zake njema)

(Ewe Mwenyezi Mungu. Mrehemu Muhammad na Ahli zake.)

6.Kisha utanyanyua kichwa chako na utasimama, na kusema:

Samiallaahu liman Hamida. Allahu Akbar.

(Mwenyezi Mungu Anamsikia kila anayemshukuru).

7.Kisha utasujudu; utawekapaji lako la uso juu ya kidongo twahara au mfano wake, na hivyo hivyo utaweka vitanga vyako na magoti na vidole gumba vya miguu ardhini, na kusema:

'SUBHANARABBIYAL A'LAWABIHAMDIHI ALLAHUMMA SWALLI ALAA MUHAMMADIN WA AALI MUHAMMAD'

(Nataja Utukufu wa Mwenyezi Mungu, Bwana wangu alie juu ' kabisa, na ninamshukuru).

8.Kisha utanyanyua kichwa chako na kukaa, na kusema: -

ALLAHU AKBAR, ASTAGH FIRU LLAHA RABBI WA ATUBU ILAYHI, ALLAHU AKBAR'

(Naomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu, Bwana wangu, na ninatubu kwake).'

9.Kisha utasujudu sijda ya pili kama ya mwanzo, utakaa baada yake,kisha utasimama kwa Rakaa ya pili, utasema utaposimama.

BIHAULILLAHI WA QUWWATIHI AQUMU WA AQ-UD

(Kwa msaada na nguvu ya Mwenyezi Mungu nainuka na nakaa.)

SOMO LA SABA

SALA YA ASUBUHI (ii)

1.Baada ya kusimama kutoka Rakaa ya kwanza, utasoma sura ya Al-Hamdu na sura nyingine katika Rakaa ya pili kama ulivyosoma katika Rakaa ya kwanza.

2.Baada ya kusoma Al-Hamdu na sura, utaomba Dua na kunyanyua mikono mkabala wa uso, na utasema:-

'RABBANAA AATINA FIIDDUN'YAA HASANATAN WA FIL AAKHERATI

HASANATAN WAQINA ADHABAN-NAR.'

(Ewe Mola wetu; Tupe hapa duniani kila yaliyo mema, na utupe Akhera kila yaliyo mema, na utukinge na adhabu ya moto.)

3.Kisha utarukuu, kama ulivyofanya katika Rakaa ya kwanza, na utasujudu sijda mbili kama mwanzo.

4.Baada ya kukaa kutoka sijda ya pili, utasoma Tashaahud kama ifuatavyo:

ASH - HADU AL LAA ILAAHA ILLALLAHU WAHDAHU LA SHARIKA LAHUU WA ASH - HADU ANNA MUHAMMADAN ABDUHU WA RASULUH ALLAHUMMA SWALLI ALAA MUHAMMADIN WA AALI MUHAMMAD.

Tafsiri yake ni hii:

Nakiri kuwa hapana Mola ila Mwenyezi Mungu, yeye tu wala hana mshirika yeyote.

Na nakiri kuwa Muhammad(s.a.w.w) ni mtumwa na mjumbe wake.

Ewe Mwenyezi Mungu mpelekee rehma Mtume wako Muhammad naAhali zake.

5. Kishautasoma Salaam:

ASSALAAMU ALAYKA AYYUHANNABIYYU WARAHMA TULLAHI WA BARAKATU ASSALAAMU ALAYNA WA ALA IBADILLAHISSALIHIIN.

ASSALAAMU ALAYKUM WARAHAMA TULLAHI WA BARAKATUH.

Tafsiri yake ni kama ifuatavyo:

Amani juu yako Ewe Mtume Mtukufu, na Rehmaya Mwenyezi Mungu na baraka zake; Amani juu yetu na juu ya viumbe wa Mungu watenda mema:

Amani juu yenu na Rehma ya Mwenyezi Mungu na Baraka zake.

6. Kisha utasema ALLAHU AKBAR, ALLAHU AKBAR ALLAHU AKBAR.

7. Baada ya sala ni bora mno kusoma Tasbihi kama hivi: -ALLAHU AKBAR (marathelathini na nne) AL-HAMDU LILLAH (mara thelathini na tatu) SUB HANA LLAH (mara thelathini na tatu).

MASOMO YA KI-ISLAM

KITABU CHA TATU

SOMO LA NANE

SALA ZINGINE ZA SIKU

(a) SALA YA ADHUHURI

1. Namna ya Sala ya Adhuhuri ni kama sala ya Asubuhi, ispokuwa wewe utanuwia hivi: 'Nasali sala ya Adhuhuri Rakaa nne Qurbatan ila llahi Taala.

Kisha utaenda kusali kama sala ya Asubuhi.

2. Utapokaa baada ya sajda ya Rakaa ya pili, utasoma Tashahhud:

lakini Salamu hautasoma, ispokuwa utasimama kwa ajili ya rakaa ya tatu.

3. Utasoma ndani ya rakaa ya tatu {badala ya alhamdu na sura}:

SUBHANALLAHI WAL-HAMDULILLAHI WA LAAILAHA ILLALLAHU WALLAHU AKBAR (mara tatu).

4. Baadae utasimama kwa Rakaa ya nne, na utafanya kama ulivyo fanya katika rakaa ya tatu; kisha utarukuu na utasujudu.

5.Kisha utasoma Tashahhud na Salaam kama sala ya Asubuhi. Sala yako imetimia.

(b) SALA YA ALASIRI

Namna ya sala ni kama sala ya Adhuhuri, ispokuwa wewe utanuwia hivi: 'Nasali sala ya Alasiri rakaa nne, Qurbatan ilallahi taala'

(c) SALA YA MAGHARIBI

1.Namna ya sala ya Magharibi ni kama sala ya Adhuhuri, isipokuwa wewe utanuwia hi vi:

'Nasali sala ya Magharibi Rakaa tatu Qur batan ila llahi taala'

2.Na utaponyanyua kichwa chako sijda ya pili katika rakaa ya tatu utakaa na kusoma Tashaahhud na Salaam, na sala yako itakuwa imetimia.

(d) SALA YA ISHA

Namna ya Sala ya Isha ni kama sala ya Adhuhuri, ispokuwa wewe utanuwia hivi: 'Nasali Sala ya Isha Rakaa nne Qurbatan ilallahi Taala'

Maelezo muhimu

Wanawake watasoma katika Sala zote kwa sauti ya chini ispokuwa wasikie wao wenyewe yale maneno wanayosema. Rakaa ya kwanza na ya pili ya sala ya Asubuhi, Magharibi na Isha kwa sauti ya juu kidogo, pamoja na sala za Adhuhuri na Alasiri na Rakaa ya tatu na ya nne za Magharibi na Isha kwa sauti ya chini.

SOMO LA TISA

SALATUL-AAYAT

Tulizo zitaja ni sala za siku zote. Na sala nyingine za wajibu ni nyingi, tutaitaja kati ya hizo' Salat-ul-Ayat'.

Sala ya Ayaat ni wajibu zama linapopatwa jua au mwezi, wakati wa mtetemeko na kimbunga na radi, na vizuko vingine vya mbinguni au ardhini.

Na namna ya kusali kwake ni kama hivi:

1. Utanuwia, hali ya kuwa umesimama na umekabili Qibla: Nasali Salatul-Ayaat Rakaa mbili Qurbatan Ila llahi Taala.

2. Utasoma sura ya Al-Hamdu na sura nyingine, kisha utarukuu.

3. Utainuka kutoka katika rukuu; utasoma Al-Hamdu na sura nyingine, halafu utasoma Qunuti na utarukuu.

4.Utainuka kutoka rukuu. Na utasoma AI-Hamdu na sura, na utarukuu:

5. Utainuka kutoka rukuu, na utasoma Al-Hamdu na sura, halafu utasoma Qunut, na utarukuu.

6. Utainuka kutoka rukuu, na utasoma Al-Hamdu na sura, na utarukuu.

7. Utainuka kutoka rukuu, kisha utasujudu sijda mbili kisha utasimama kwa rakaa ya pili.

8. Utasoma Al-Hamdu na sura, na utasoma Qunut, halafu utarukuu.

9. Utainuka kutoka rukuu, utasoma Al-Hamdu na sura, na utarukuu.

10. Utainuka kutoka rukuu, utasoma Al-Hamdu na sura, na utasoma Qunuut, na utarukuu.

11. Utainuka kutoka rukuu, utasoma Al-Hamdu na sura, na utarukuu.

12. Utainuka kutoka rukuu, utasoma Al -Hamdu na sura, na utasoma Qunuut na utarukuu.

13. Baada ya hapo utainuka kutoka rukuu na kusujudu sijda mbili, na utasoma Tashaahhud na Salaam.

Itakuwa Sala ya Aayat ni rakaa mbili kwa Qunuut tano, na rukuu kumi, nasijda nne.

SOMO LA KUMI

SALA ZA SUNNA

Jua Ewe! Ndugu yangu, Sala zilizo Sunna ni nyingi. Na zilizo muhimu sana ni sunna za siku zote. Nazo ni kama hizi:

Sunna ya Asubuhi, rakaa mbili, kabla ya kusali Sala ya Asubuhi. Sunna ya Adhuhuri, rakaa nane, husaliwa rakaa mbilimbili, kabla ya Sala yaAdhuhuri.

Sunna ya Alasiri, rakaa nane, husaliwa rakaa mbilimbili, kabla y a Sala ya Alasiri.

Sunna ya Magharibi, rakaa nne, husaliwa rakaa mbilimbili, baada ya Sala ya Magharibi.

Sunna ya Isha, rakaa mbili mbili, husaliwa hizo kitako, baada ya Sala ya Isha.

Sunna ya Usiku rakaa kumi na moja; husaliwa rakaa mbilimbili, na ya kumi na moja husaliwa pekee. Na sala hii inajulikana pia kwa jina la Tahajjud. Na wakati wa sala hizi ni nusu ya usiku mpaka Alfajiri.

Sunna zote husaliwa namna ya Sala ya Asubuhi, ispokuwa tofauti ni katika nia.

Inafaa kwa mtu katika Sala za Sunna kusoma Al-Hamdu pasi na sura, au kusoma sehemu ya sura. au kusoma sura mbili za zaidi baada ya Al-Hamdu.

SOMO LA KUMI NA MOJA

KUFUNGA (SAUMU)

Saumu inamlazimu mtu balehe kama hakuwa mgonjwa au msafiri au katika hali ya hedhi na mengineyo.

Inamlazimu afunge mwezi wa Ramadhani.

Na funga maana yake ni kujizuia na vinavyo funguza saumu tangu alfajiri mpaka kuchwa jua kwa kisharia[5] . Inalazimu kunuwia kabla ya kuchomoza alfajiri, kama hivi:

Ninafunga kesho kutaka ukaribu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu."

Na yanayofunguza saumu ni haya:

1. Kula

2. Kunywa

3. Kuingilia mwanamume na mwanamke

4. Kujitoa manii (Shahawa).

5. Kutia bomba la dawa ya maji katika tundu ya nyuma

6. Kufikisha vumbi zito mpaka kooni

7. Kubaki na j anaba mpaka asubuhi

8. Kuogelea {kuzama mbizi}

9. Kumzulia Mungu au Mtume au Ma-Imam

10. Kufanya kusudi kujitapisha

MASOMO YA KI-ISLAM

KITABU CHA TATU

SOMO LA KUMI NA MBILI

UTHIBITISHO WA MWEZI

Kuthibitisha kwa mwezi wa Ramadhani kuandama na mfungo mosi ni kwa njia tano:

1. Kuona mwezi mwenyewe.

2. Kushuhudia watu wawili waadilifu.

Kuonekana na watu wengi wa kutosha Kutimia siku thelathini Shaaban au Ramadhani.

SOMO LA KUMI NA TATU

MAELEZO MATATU

(a) KAFFARA

Aliyefungua mwezi wa Ramadhani makusudi ni wajibu juu yake moja wapo katika mambo matatu:

i. Kufunga miezi miwili mfululizo

ii. au kuwalisha maskini sitini

iii. au kumpa mtumwa uhuru wake

(b) ZAKA YA FITIRI

Ni lazima kwa mtu baleghe kutoa 'fitri siku au Iddi (ya mfungo mosi)

Ajitolee mwenyewe na watu wa nyumbani kwake, na kumtolea kila mmoja kilo tatu ya chakula cha kawaida.

Ni bora kutoa ngano au tende au zabibu au mchele au unga.

Inafaa atoe kima chake.

Na anayepewa ni fakiri asiyekuwa na matumizi ya mwaka mzima.

(c) SALA YA IDI

Ni sunna kwa mtu kusali siku ya Idul Fitri (Sala ya Iddi). Na vilevile sala ya Iddi ya mfungo tatu (yaani Iddi ya Adh-ha).

SOMO LA KUMI NA NNE

VITU VYA ZAKA

1. Tende 4. Shairi 7. Ng'ombe

2. Zabibu 5. Ngamia 8. Dhahabu

3. Ngano 6. Mbuzi 9. Fedha

Kisha ni sunna kwa mtu kutoa zaka ya rasilimali ya biashara yake: tena atapopata faida katika biashara atatoa zaka ya faida yake. na Zaka hii inafaa kwa kuzidisha mali.

Inalazimu nia katika kutekeleza Zaka. utanuwia kama hivi:-"Mimi ninatoa zaka kwa kutaka ukaribu wa Mwenyezi Mungu".

SOMO LA KUMI NA TANO

MATUMIZI YA ZAKA

Wanaopewa zaka ni wafuatao:

1. Mafakiri

2. Masikini

3. Wanaofanya kazi ya Zaka

4. Wenye nyoyo nyepesi katika Uslamu

5. Kuwanunua watumwa kuwapa uhuru

6. Kuwalipia madeni ya wasiojiweza kulipa

7. Kutengeneza mambo ya Dini

8. Msafiri aliyeishiwa pesa zake ijapokuwa kwake ni tajiri.

SOMO LA KUMI NA SITA

VITU VYA KHUMSI

Khumsi maana yake ni moja kwa tano.

Kutoa Khumsi ni haki iliyo wajibu katika vitu saba. Ni lazima kutoa moja katika kila tano.

Navitu sabani hivi:

1. Ghanima ilyochukuliwa kwa makafiri wakati wa kupigana nao vita.

2. Migodi. kama dhahabu. fedha mafuta.chuma na chumvi na mengineyo.

3.Mali iliyofukiwa. Na kila mwenye kupata mali iliyofukiwa (kwa sharti zake) ni wajibu juu yake kutoa Khumsi yake.

4. Kinachotolewa baharini. kama lulu na marjani na vinginevyo.

5. Ikiwa mali ya halali ilichanganyika na mali ya haramu. kama

hakujulikana mwenyewe mali wala haijulikani kiasi cha haramu lakini unayo hakika kuwa mali ya haramu si zaidi kuliko ishirini katika mia. basi ni wajibu kutoa khumsi yake na zilizobaki zitakuwa halali kwako.

6. Kila kinachopatia faida mtu katika biashara au kilimo au chumo au kwa kupangisha milki yake na mfano kama huo, baada ya kutoa gharama yake ya mwaka. inampasa kutoa khumsi katika faida halisi.

7. Ardhi aliyoinunua Kafir dhimmi kwa Mwislamu.

SOMO LA KUMI NA SABA

UGAWIKO WA KHUMSI

Khumsi hugawika sehemu mbili:

1. Nusu hutolewa kwa Mujtahidi mwenye elimi, mwadilifu. Ili aturnie katika maslaha ya Uislamu.

2. Nusu hupewa masharifu wahitaji.

Lau wangalitoa watu hizi wajibu mbili. Zaka na Khumsi. asingalibaki fakiri duniani wala kubakia maslaha ya Kiislamu ispokuwa itatima. kama inavyotuonyesha tarehe zama walipokuwa wa-Islamu wanafuata kanuni za Ki-Islamu zenye kupendeza.

Na kama tukinena kuwa haki mbili hizo hazitoshi kwa matumizi ya dola ya Ki-Islamu katika maendeleo ya wa- Islamu. basi ni lazima juu ya Dola ya ki-Islamu kutafuta njia nyingine za kupata mali. kama kilimo na biashara na kuchimbua migodi na vinginevyo. Si vizuri kwa dola ya Ki-Islamu kutia mkono katika mali ya watu. kwani Uislamu unaharamisha hayo. Soma Aya ya Qur'ani tukufu inayosema:

WALAA TA'AKULU AM-WALAKUM BAINAKUM BIL BATWILI:

"Wala msile mali zenu kati yenu kwa ubatilifu (Yaani kudhulumiana), "Kwani Uislamu una njia maalum ya uchumi kwa njia bora mno.

SOMO LA KUMI NA NANE

HIJJA (HAJJ) (i)

Moja miongoni mwa nguzo za Uislamu ni Hija.

Nayo ni wajibu kwa mtu baleghe mwenye kuweza hivyo kwenda Makka tukufu, mara moja kwa maisha yake kwa kufanza mambo ya Hija.

Nayo ni sehemu mbili: Sehemu ya kwanza ni Umra Na wajibu wa Umra ni kama ifuatavyo:

1. Kuhirimiya, maana yake ni kuondosha nguo zake za kawaida na kuvaa rubega kwa nguo mbili za kuhirimiya (za Ihram).

2. Tawwaf: Kuzunguka Kaaba tukufu mara saba.

3. Kusali rakaa mbili za tawwaf kama sala ya Asubuhi.

4. Sai: Kukimbia mara saba kati ya Safa na Marwa (na hivyo ni vilima viwili).

5. Taqseer: Kupunguza nywele na kukata sehemu za kucha.

SOMO LA KUMI NA TISA

HIJA (HAJJI) (ii)

Sehemu ya Pili ni Hajj

1. Kuhirimiya (Ihram)

2. Waquuf (Kusimama) katika Arafaat; napo ni mahala karibu na Makka.

3. Kusimama katika Mashar; napo ni mahala karibu na Makka.

4. Kwenda Mina kwa kufanya aamali tatu:

(a) Kutupia jamra (vijiwe), navyo ni sehemu ya mlima

(b) Kuchinja mbuzi au ngamia au ng'ombe

(c) Kunyoa nywele

5. Mzunguko wa kuzuru pembeni ya Kaaba

6. Kusali Rakaa mbili za Tawwafu

7. Kwenda mbio mbio kati ya Safaa na Marwaa

8. Mzunguko wa wanawake (Tawafun-Nisa) pembeni mwa Kaaba

9. Rakaa mbili za Tawaafu ya wanawake

10. Kupitiwa na usiku mbili Mina na kutupia Jamra tatu za huko.

Haya nimatendo ya Hija ya Tamattui nayo ni faradhi kwa mtu ambaye si mkazi wa Makka. Kisha ni sunna Hijja kwa asiyeweza, na kwa aliyeweza ambaye katekeleza wajibu wake. Na kwa Hija pana Thawabu kubwa sana.

MASOMO YA KI-ISLAM

KITABU CHA TATU

SOMO LA ISHIRINI

JIHADI (VITA VYA DINI)

Ya sita katika matawi ya Dini ni Jihadi. Na maana yake ni kupigana kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Jambo hili linahitaji maelezo mafupi hapa. Uislamu haupendi kuwaua wenye makosa. isipokuwa inataka kuondoa makosa yao. Vitendo viovu kama hivyo ni kama maradhi. Huhitaji matibabu na kila tabibu hutibu kwa kutumia madawa kadri itakavyowezekana kuponya yale maumivu,

Lakini wakati mwingine, maradhi hayo hufikia kiasi ambacho hata madawa huwa hayafai kitu; ndipo tabibu anapoonelea kwamba sharti mgonjwa apasuliwe au kukatwa ili kuokoa maisha yake.

Anapoamua hivyo hafanyi kwa furaha ispokuwa kwa shingo upande. Ijapokuwa mgonjwa anapata maumivu makubwa katika kumkata sehemu ile mbaya, lakini si kuadhibu bali ni kuponya.

Vivyo hivyo, tufanye kundi la watu ni kama kiwiliwili kimoja, ambacho baadhi ya sehemu zake zimepatwa na maradhi ya roho, na iwapo kila njia ya nasaha iliyotumiwa imeshindwa, huku sehemu nyingine zikiwa katika hatari ya kuambukizwa na kuleta tena shida katika sehemu hizohizo; basi tabibu wa roho, yaani Mtume au Imam, ambao ndio waganga wa kutibu roho, na ambao huongozwa na Mwenyezi Mungu, waahakikisha kama sehemu hizo zinahitaji kupasuliwa ili kuokoa sehemu zile za binadamu ambazo ni nzima kutokana na shida hizo. Kisha, na ndivyo vile, ambavyo ataamrisha Vita Vitakatifu na vita hivyo viwe katika sehemu zile tu ambazo hazina budi kuondolewa.

Ingawa utaona kuwa kuna lazima ya mgonjwa kutibiwa kwa njia hiyo, hutaamini kamwe kumkabidhi mtu ambaye hastahili kufanya kazi yenye hatari kama hiyo. Utakuwa ni upumbavu mno na kitendo cha ujinga. Huwezi kuridhika kuwa utabibu huo ni wa dharura. mpaka umeambiwa na mganga mtaalamu.

Kwa hiyo. kufuatana na sheria za Ki-Ithnaasheriya, vita haviwi kamwe mpaka vimeamrishwa na Mtume au Imam mwenyewe, na viwe kwa kadiri maalum ambapo vile vile imeamrishwa na Naibu wa Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, maisha yameumbwa na Mwenyezi Mungu na hayafai kuyabomoa (kuyaua) ispokuwa imeruhusiwa kufanya hivyo. kwa amri ya Naibu wa Mwenyezi Mungu.

Vivyo hivyo siku hizo. ambapo Imam wetu wa mwisho haonekani, kupigana jihadi hakuruhusiwi: kwa sababu yetu anayo madaraka ya kuwaita watu kwa ajili ya vita vya dini.

Lakini kama makafiri wakihujumu nchi ya Waislamu, basi Waislamu wameruhusiwa kupigana nao kwa ajili ya kujilinda.

SOMO LA ISHIRINI NA MOJA

KUAMRISHA MEMA

Nalo ni tawi la Uislam lililo muhimu sana. Na kila jambo lililoamrishwa na Mwenyezi Mungu ni jema; Kama Sala. kufunga, kutoa haki za makafiri na kusimamia mambo muhimu ya Uislamu au la kupendelea Uislamu. kama kulisha na kupokea wageni na kufunza tabia lizuri na kufunza yanayofanana na hayo.

Na kumwamrisha mtu jambo jema mara ya kwanza ni wajibu. Na mara ya pili ni Sunna.

Na kuamrisha mema ni wajibu kwa sharti nne:

1.Mwenye kuamrisha awe anajua mambo mema na mabaya.

2.Yeye anatumai kwamba maneno yake yatafuatwa.

3. Mtu ambaye ameacha mema anadumu kuacha.

4.Mwenye kuamrisha anatumai kuwa kuamrisha mema kwake hakutaleta madhara juu yake mwenyewe.

Lakini itapokuwa misingi ya imani ya wa-Islamu hatarini, au msimamo wa Uislamu umo ndani ya hatari (mfano: mapendekezo ya dola inataka kubadili itikadi za watu, au inataka kueneza ulevi au kamari katika makusanyiko) basi ni wajibu kwa kila mtu kuamrisha mema na kukataza mabaya, ijapokuwa yapo madhara; kama walivyofanya ma-Imamu watwaharifu na watu bora zaidi.

SOMO LA ISHIRINI NA MBILI

KUKATAZA MABAYA (i)

Nalo ni tawi la Uislamu lililo muhimu sana.

Umekuwa ubora wa Umma kushikama na haya mambo mawili; kama alivyosema Mungu Mtukufu:-

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ﴿١١٠﴾

"Mmekuwa bora kuliko Umma wote uliotolewa kwa watu, mnaamrisha mema na mnakataza mabaya."

Na Munkar ambayo waliokatazwa Waislamu kutenda: kama ulevi, kamari, riba. zinaa, kula mali ya watu na mengineyo.

Na lolote linalochukiza Uislamu, kama ubatilifu, na kulala baada ya alfajir, na kuacha kuweka sawa wafanyakazi na mengineyo.

Na kukataza mtu kufanya mabaya ni wajibu mara ya kwanza, na mara ya pili inakuwa ni Sunna.

Yanalazimika kwa kukataza mabaya kama yale yaliyomo katika kuamrisha mema. Na inayo sharti nne. kama tulivyoeleza katika kuamrisha mema.

SOMO LA ISHIRINI NA TATU

KUKATAZA MABAYA (ii)

Na kukataza mabaya kuna daraja nne:

1. Makatazo ya moyoni.

2. Kudhihirisha usoni (kukunja uso) na kukosa kumjali anayetenda mabaya.

3.Kukataza kwa ulimi, kama kuwaidhi na vizuri, au kukemea na mifano mingine kama hii.

4.Kukataza kwa mkono, kwa kupiga na mfano ya hivyo, akiwa mwenye kukataza hivyo anadhani kuwa hayatakuwa madhara juu yake.

Hapanabudi kujua kuwa wajibu hizo mbili (kuamrisha mema na kukataza mabaya) heshima zake ni kubwa.

Akasema Mtukufu Mtume(s.a.w.w) .

"Havipo vitendo vizuri vyovyote vya Dini kulingana na Jihadi {katika njia ya Mungu ila kama pulizo ndani yabahari yenye mawimbi, na havipo vitendo vyema vyote pamoja na Jihadi {katika njia ya Mwenyezi Mungu} kulingana na kuamrisha mema na kukataza mabaya ila kama pulizo ndani ya bahari yenye mawimbi."

Lakini zama zetu hizi wachache wanafanya mambo mawili haya ya wajibu muhimu.

Akasema Imam Muhammad Al-Baqir(a.s) : "Watakuwepo mwisho wa zama watu ambao hawataamrisha mema na kukataza mabaya ispokuwa wakiona hayatakuwa madhara: wanajitakia wenyewe ruhusa na uzuru. Wakati huo ghadhabu ya Mwenyezi Mungu itatimia juu yao. Na itawaenea adhabu yake Mwenyezi Mungu juu yao."

Hadithi hii inaonyesha hali ya Waislamu siku hizi, kwani wengi wao wameacha kuamrisha mema na kukataza mabaya. Kwa hivyo wamepambanishwa na makafiri.

Makafiri wakanyang'anya vitu vyao; wakamiliki nchi zao; wakabadilisha Dini yao. Na Waislamu wakawa wanyonge baada ya kuwa wakunjufu ulimwenguni.

SOMO LA ISHIRINI NA NNE

KUMPENDA MTUKUFU MTUME NA AHLIBAITI ZAKE NA KUJIEPUSHA NA MAADUI ZAO

Tawalla, maana yake ni kuwapenda Mwenyezi Mungu na Mtumewe na Ujumbe wake na Maimamu.

Tabarra, maana yake ni kujiepusha na maadui wa Mwenyezi Mungu na Mtume na Maimamu.

Na hivyo kwa sababu unapopenda mtu utamfuata mwenendo wake, kama ukimchukia mtu utajiepusha na vitendo vyake.

Basi mapenzi ya Mungu na mawalii wake yanasababisha utii wa Mwenyezi Mungu na mawalii wake katika mambo ya dini na thawabu za akhera.

Na uchukivu wa maadui wa Mungu na mawalii wake, hulazimisha kwa kuepukana nao, na kuviacha vitendo vyao na maneno yao.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU

YALIYOMO

MASOMO YA KI-ISLAM 1

KITABU CHA TATU 1

DIBAJI 1

MASOMO YA KI-ISLAM 2

KITABU CHA TATU 2

SOMO LA KWANZA 2

MATAWI YA DINI 2

SOMO LA PILI 2

NAMNA YA SALA NA KUTAWADHA 2

SOMO LA TATU 3

IDADI NA WAKATI WA SALA 3

MASOMO YA KI-ISLAM 4

KITABU CHA TATU 4

SOMO LA NNE 4

ADHAAN 4

SOMO LA TANO 4

IQAMAH 4

MASOMO YA KI-ISLAM 8

KITABU CHA TATU 8

SOMO LA NANE 8

SALA ZINGINE ZA SIKU 8

(a) SALA YA ADHUHURI 8

(b) SALA YA ALASIRI 8

(c) SALA YA MAGHARIBI 8

(d) SALA YA ISHA 8

SOMO LA TISA 8

SALATUL-AAYAT 8

SOMO LA KUMI 9

SALA ZA SUNNA 9

SOMO LA KUMI NA MOJA 9

KUFUNGA (SAUMU) 9

MASOMO YA KI-ISLAM 11

KITABU CHA TATU 11

SOMO LA KUMI NA MBILI 11

UTHIBITISHO WA MWEZI 11

SOMO LA KUMI NA TATU 11

MAELEZO MATATU 11

(a) KAFFARA 11

(b) ZAKA YA FITIRI 11

(c) SALA YA IDI 11

SOMO LA KUMI NA NNE 11

VITU VYA ZAKA 11

SOMO LA KUMI NA TANO 11

MATUMIZI YA ZAKA 11

SOMO LA KUMI NA SITA 12

VITU VYA KHUMSI 12

SOMO LA KUMI NA SABA 12

UGAWIKO WA KHUMSI 12

WALAA TA'AKULU AM-WALAKUM BAINAKUM BIL BATWILI: 12

SOMO LA KUMI NA NANE 13

HIJJA (HAJJ) (i) 13

SOMO LA KUMI NA TISA 13

HIJA (HAJJI) (ii) 13

MASOMO YA KI-ISLAM 14

KITABU CHA TATU 14

SOMO LA ISHIRINI 14

JIHADI (VITA VYA DINI) 14

SOMO LA ISHIRINI NA MOJA 15

KUAMRISHA MEMA 15

SOMO LA ISHIRINI NA MBILI 15

KUKATAZA MABAYA (i) 15

SOMO LA ISHIRINI NA TATU 15

KUKATAZA MABAYA (ii) 15

SOMO LA ISHIRINI NA NNE 16

KUMPENDA MTUKUFU MTUME NA AHLIBAITI ZAKE NA KUJIEPUSHA NA MAADUI ZAO 16

SHARTI YA KUCHAPA 16

MWISHO WA KITABU 16

YALIYOMO 17


[1] . Akhera: Ufufuo.

[2] . Kiyama: Siku ya kufufuliwa.

[3] . Hii si sehemu ya Adhana, lakini ni bora kusoma.

[4] . Hii si sehemu ya Iqama lakini ni bora kusoma.

[5] . Kisheria: Kwa kawaida Magharibi ni wakati jua linapozama na kufichika upeo wa macho. na kwa sharia ni wakati ule wekundu unao onekana upande wa mashariki baada ya kuzama jua ufike sawa na utosi mbinguni.