HIKAYA ZA B A H L U L MWENYE BUSARA

HIKAYA ZA B A H L U L MWENYE BUSARA0%

HIKAYA ZA B A H L U L MWENYE BUSARA Mwandishi:
Kundi: Waheshimiwa wa Kidini

HIKAYA ZA B A H L U L MWENYE BUSARA

Mwandishi: AMIRALY M.H.DATOO
Kundi:

Matembeleo: 2360
Pakua: 843

Maelezo zaidi:

HIKAYA ZA B A H L U L MWENYE BUSARA
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 8 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 2360 / Pakua: 843
Kiwango Kiwango Kiwango
HIKAYA ZA B A H L U L MWENYE BUSARA

HIKAYA ZA B A H L U L MWENYE BUSARA

Mwandishi:
Swahili

HIKAYA ZA BAHLUL MWENYE BUSARA

KIMEKUSANYWA NA KUTARJUMIWA NA: AMIRALY M. H. DATOO

MANENO MAWILI

Katika kuona haja ya kupata nasiha na mawaidha nimeonelea vyema kutumia mbinu hii ya kuchapa nasiha na mawaidha katika sura ya hekaya za Bahlul. Kwani maisha yake yanatuchekesha na kutu furahisha papo hapo tunapata mafundisho ndani mwake. Vile vile nimekikusanya na kukitarjumu kitabu kimoja chenye masimulizi na hadithi zilizopo katika Qur'an Tukufu. Hivyo ni matumaini yangu kuwa vitabu hivi na vingine vitatusaidia sisi sote katika kulenga maisha yetu vile ipasavypo.

Amiraly M.H.Datoo 28 Safar 1423

P.O.Box 838, 11.5.2002

BUKOBA

Tanzania.

datooam@hotmail.com

KATIKA KUMTAARUFISHA BAHLUL

BAHLUL ni kumaanisha kwa ujumla wa kucheka,uwema na pendeza. Majibu haya yanaweza kuwa mafunzo kwa watu wa kila aina hadi katika zama zetu na mbeleni. Watu wengi waliweza kutokezea kwa jina hilo, lakini mashuhuri ni lile la Bahlul aliyekuwapo katika zama za Harun al-Rashid. Bahlul alikuwa ni mmoja wa wanafunzi bora wa Imam Jaafar as-Sadiq(a.s) na vile vile alikuwa mpenzi wa Ahli-Bayt(a.s) ya Mtume(s.a.w.w) Vile vile inasemekana kuwa Bahlul alikuwa na undugu wa Harun Rashid kwa upande wa mama yake na riwaya nyingine imesemwa kuwa alikuwa jamaa wa karibu wa Harun. Qadhi Nurallah Shushtary anasema katika kitabu chake Majalis al-Muuminin Bahlul alikuwa ni mtu mwenye akili mno ambaye kwa sababu fulani fulani alijegeuza mwendawazimu.

Bahlul alizaliwa Kufa na jina lake la asili lilikuwa Wahabu bin Amru. Kwa mujibu wa riwaya moja, Harun Rashid alimwona Imam Musa bin Jaafer(a.s) kama tishio kubwa kwa kubakia utawala wake. Hivyo alijishughulisha katika mbinu za kutaka kumwua. Na aliweza kutafuta hila moja ya kumwua. Hivyo alimzulia dai la kuasi na hivyo aliwataka hukumu wacha Mungu ya kumwua Imam, ambamo Bahlul pia alikuwamo. Wote walitoa fatwa ya kuuawa kwa Imam(a.s) lakini Bahlul aliipinga. Bahlul alimwendea Imam(a.s) na kumjulisha yale yaliyokuwa yakitokea, na alimwambia Imam(a.s) ampatie ushauri na njia za kuyakabili hayo. Imam(a.s) alimwambia kuwa ajigeuze na awe mwenda wazimu.

Hii ndiyo sababu ya yeye kuwa mwenda wazimu kwa matakwa ya Imam(a.s) na hivyo aliweza kuepukana na adhabu na maangamizi ya Harun Rashid, aliyekuwa Khalifa wakati huo. Na hivyo bila ya woga wowote akijifanya mwenda wazimu, aliweza kukabili, kumsuta hata Khalifa na mawaziri wake na papo hapo aliwatetea wanyonge na wale wote waliokuwa wamedhulumiwa. Pamoja na hali yake hiyo, watu walimpenda kwa mioyo yao, hadi leo hekaya zake zinasimuliwa katika vikao na kujifunza mengi kutokana hayo. Kwa mujibu wa riwaya ya pili - ambayo inasadikiwa zaidi. Masahaba na wapenzi wa Imam(a.s) walikuwa wametingwa na udhalimu wa Khalifa na watawala wake. Hivyo wote walimwomba Imam(a.s) uongozi kuhusu swala hilo. Imam(a.s) aliwajibu kila mmoja kwa herufi moja tu. "Jim" kwa hivyo walielewa kuwa hapakuwapo na haja ya kuulizia ziada. Kila mmoja alielewa hilo herufi tofauti tofauti. Mmoja alielewa "Jila Watan" yaani kutoka nyumbani, mwingine alielewa 'Jabl yaani 'Mlimani' na Bahlul alielewa kuwa ikimaanisha 'Junuun' Yaani "Uenda wazimu" na hivyo alijigeuza hivyo na kwa hayo, wote waliweza kunusurika na janga hilo la kuteketezwa na udhalimu wa Khalifa.

Bahlul alikuwa akiishi maisha ya starehe na bora kabisa lakini baada ya ishara hiyo ya Imam(a.s) aligeuzia uso dunia na kuziacha starehe zote hivyo akaishi maisha ya utawa na akawa na mavazi yaliyokuwa yamechakaa. Yeye alipendelea kuishi uwanjani kuliko majumba ya Wafalme, vile vile aliishi kwa kipande kikavu cha mkate kuliko kutegemea misaada ya hisani ya Khalifa kwani alikuwa akijiona yu bora kuliko Khalifa Harun Rashid, mawaziri wake na Baraza lake zima.

Bahlul kwa hakika, alikuwa mcha Mungu na mpenzi wake, mwenye akili sawa na Aslim kamili. Yeye alikuwa ni mtu mwenye akili sana na fahamu zaidi na mwenye kutoa majibu ya papo hapo na mtatuzi wa masuala katika zama zake. Jina lake halikuwa mashuhuri tu miongoni mwa watu wenye akili tu bali kwa amri ya Imam(a.s) alijifanya mwenda wazimu na hivyo aliweza Din na Sharia na kuelezea uhakika na ukweli wa Ahli Bayt(a.s) Katika zama hizo hapakuwapo na njia nyyingine ila yeye kujifanya mwenda wazimu amasivyo Harun Rashid angalimwua. Kama vile Harun Rashid alisikiliza uthibitisho wa Uimam Musa ibn Jaafer(a.s) kutoka mwanafunzi mmoja wa Imam Jaafer as-Sadiq(a.s) Hisham bin Hikam, na akamwambia Waziri wake Yahya ibn Khalid Barki: "Ewe Yahya! Maneno ya mtu huyu, Hisham, kwangu mimi ni sawa na tishio la mapanga laki moja, lakini jambo la kushangaza ni kule kubainika kwake hai wakati mimi natawala!" Harun alibuni kila aina ya mbinu za kutaka kumwua Hisham. Na alipopata habari hizo, alitorokea Kufa ambako aliishi nyumbani (mafichoni) mwa rafiki yake, na katika kipindi kifupi alifariki.

(1). BAHLUL NA CHAKULA CHA KHALIFA

Siku moja Harun al-Rashid alimpelekea Bahlul sinia iliyojaa vyakula mbalimbali. Mfanyakazi alipomwakilishia Bahlul vyakula hivyo, alimwambia: "Hivi ni vyakula makhususi vya Khalifa na amekutumia wewe uvile." Bahlul alimtupia mbwa aliyekuwa ameketi karibu, vyakula vyote alivyoletewa. Alipoyaona hayo, mfanyakazi wa Harun al-Rashid alighadhabika mno na kusema kuwa hiyo ilikuwa ni kumvunjia heshima Khalifa na angalimjulisha hivyo. Hapo Bahlul alimjibu: "K aa kimya! Iwapo na mbwa atafahamu kuwa vyakula hivyo vinatoka kwa Khalifa, naye pia ataacha kuvila!

Fundisho : Inatupasa kukataa zawadi kutoka kwa waonevu na madhalimu ili visituathiri sisi kutotimiza wajibu wetu wa ukweli na haki.

(2). BAHLUL KUKALIA KITI CHA KHALIFA

Siku moja Bahlul aliingia katika Qasri ya Khalifa na kukuta kiti chake tupu aliona hakuna mtu wa kumzuia, hivyo alikwenda moja kwa moja akaketi juu ya kiti cha Khalifa. Walipotokezea maaskari wa Khalifa, walijaribu kumwondoa Bahlul, lakini alikataa, hivyo waliweza kumwondoa kwa kumpiga. Hapo Bahlul alianza kulia kwa sauti, na alipotokea Harun Rashid alimwona Bahlul akilia kwa sauti na aliwauliza maaskari wake sababu. Wao walimwelezea yote yaliyotokea. Hapo Khalifa aliwakemea maaskari hao na kumpa pole Bahlul. Kwa hayo, Bahlul alisema: "Mimi sikililii kile kilichonipata, bali ninakulilia wewe Khalifa, kwani mimi nimeteswa kwa kuketi punde tu, je wewe utateswaje kwa kukikalia kiti hiki kwa miaka yote hiyo kwani kiti hiki cha Ukhalifa ni kwa ajili ya watu wengine na wewe umewadhulumu hao, na kukikalia kwa mabavu! "

(3). BAHLUL NA MFANYA BIASHARA

Siku moja mfanya biashara wa Baghdad alimwendea Bahlul kwa kutaka ushauri wake. Alimwambia: "Ewe Sheikh Bahlul ! Naomba ushauri wako katika ununuzi wa bidhaa ambazo zitanipatia faida nyingi."Bahlul alimjibu: "Chuma na Pamba" (mapokezi mengine yanataja tende na pamba) ." Mfanyabiashara huyo aliyafuata mashauri hayo, na akapata faida kubwa sana katika kipindi kifupi. Ikatokea tena kukutana na Bahlul. Hapo alirudia ushauri wake kwa kusema: "Ewe Bahlul Mwehu! Je ninunue bidhaa zipi ili nipate faida nyingi?" Safari hii Bahlul alimjibu: "Vitunguu na matiki ti maji ." Hapo mfanya biashara huyo alitumia fedha zake zote kwa kununulia bidhaa hizo akitarajia kupata faida zaidi. Baada ya kupita siku chache, bidhaa hizo zikaanza kuoza na hivyo kusababisha hasara kubwa mno. Hapo alitoka kumtafuta Bahlul na alipomwona alimwambia "Nilipokutaka ushauri mara ya kwanza ulinishauri kununua chuma na pamba (tende na pamba) kwa hiyo nilifaidika mno lakini mara ya pili, umenishauri kununua vitunguu na matikiti maji, maboga yote yameoza kwa hivyo nimefilisika kabisa........." Bahlul alimkatiza na kumwambia "Mara ya kwanza wewe uliniita "Ewe Sheikh Bahlul!" na kwa kuwa uliniamini mimi ni mtu mwenye akili hivyo nilikupatia mashauri ya akili. Na kwa kuwa mara ya pili uliniita 'Ewe Bahlul mwehu' na kwa kuwa uliamini mimi ni mwehu, basi nilikujibu kiwehu.....! . Hapo mfanya biashara alibung'aa kwa majibu hayo na alielewa maana na kujiondokea kimya kimya.

Fundisho : Uislam inasisitiza ushauri kama alivyosema Mtume(s.a.w.w) :- "Ushauri ni kinga dhidi ya tubu na usalama wa kutolaumiwa na watu...... na Atakaye ushauri husaidiwa...... "

(4). BAHLUL AMSHAURI HARUN

Siku moja Bahlul alimtembelea Harun al-Rashid, na aliombwa atoe nasaha.

Hapo Bahlul alianza: "Ewe Harun! Iwapo wewe utakuwapo porini ukashikwa na kiu ya maji ambayo hayapatikani, huku ukikaribia kufa. Je utalipa kiasi gani kwa kiasi cha kikombe kimoja cha maji?"

Harun: "Sarafu za dhahabu (Dinar)!" alijibu Harun.

Bahlul: "Iwapo mwenye maji asiporidhia sarafu hizo, je utampa nini badala yake?" aliendelea kusema Bahlul.

Harun: "Nitampatia nusu ya dola yangu" alikatiza Harun kwa haraka.

Bahlul: "Naam, baada ya kumalizia kiu chako, ukashindwa kupata mkojo (ukaziba) nawe usiweze kujitibu, je utampa nini yule atakaye kutibu huo ugonjwa?" Alisema Bahlul.

Harun akanena katika hali ya bumbuwazi: "Nitampatia sehemu ya nusu ya dola yangu iliyobakia.

Basi hapo Bahlul alisema kwa kupumua: "Ewe Harun! Usijivunie Ukhalifa wako ambao unajua thamini yake ni sawa na kikombe cha maji na uponyaji wa ugonwa wako. Hivyo, ni kheri yako iwapo utawatendea watu wako kwa upole na haki!"

1

HIKAYA ZA B A H L U L MWENYE BUSARA

(5). BAHLUL NA FAQIHI

Faqihi mashuhuri kutoka Khurasan alifika Baghdad, alialikwa na Harun Rashid katika Baraza lake na akimkalisha ubavuni mwake. Wakati alipokuwa akizungumza na Harun, alitokezea Bahlul ambaye naye alikaribishwa aketi karibu nao. Huyo mtu alimwona Bahlul yu kama mwehu na hivyo alimwambia Harun: "Nimestaajabishwa na heshima na mapenzi yako Khalifa, kwa kuwa unawastahi hata watu waliwehuka hadi kuwakaribisha karibu nawe?" Alipoyasikia hayo Bahlul, alielewa kuwa alikuwa akisemwa yeye tu na hapo akajikaza akamwambia: "Kwa nini waringia ilimu yako hiyo kidogo, usinidharau kwa udhahiri wangu bali jitayarishe kwa mabishano ili nami nimdhihirishie Khalifa kuwa wewe haujui lolote!" "Mimi nimesikia kuwa wewe u - mwehu na hivyo siwezi kubishana na wehu!" Aliyasema huyo Faqihi. Hapo Bahlul alimjibu akiwa ameghadhabika, "Mimi ninaukubalia uwehu wangu lakini wewe unakataa kuukubalia ujahili wako na kutokuwa na ilimu kamili." Harun alipoyasikia hayo, alijaribu kumtuliza Bahlul, lakini ilishindikana huku akidai kuingia mabishano na huyo Faqihi, iwapo anajiamini kwa ilimu kamili."

Basi Harun alimgeukia huyo Faqihi na kumwambia: "Je kuna kipingamizi gani katika kumwuuliza maswali?" Hapo huyo Faqihi alijibu: "Mimi nipo tayari kubishana naye iwapo atakubaliana na shuruti langu moja nalo ni, iwapo ataweza kunijibu basi nitampa Dinar elfu moja za dhahabu na akishindwa itambidi anilipe hivyo." Bahlul alimjibu: "Kwa kweli mimi huwa sina mali za kidunia na wala sina Dinar wala dhahabu, lakini nipo tayari kuwa mtumwa wake iwapo nitashindwa kumjibu, na iwapo nitamjibu basi nipatiwe hizo Dinar elfu moja za dhahabu ambazo nitazigawa miongoni mwa mafukara." Kwa hayo, huyo mtu alianza kumuuliza swali hivi: "Katika nyumba moja yupo mwanamke aliyeketi na mume wake halali kisheria na humo humo wapo watu wawili ambao mmoja wao anasali na mwingine yupo katika hali ya saumu. Ghafla anatokezea mtu kutokea nje na kuingia ndani ya nyumba hiyo. Kutokezea huku kwa mtu huyo, wale bibi na bwana wanakuwa haramu baina yao na sala na saumu za wale wawili zinakuwa batili. Je unaweza kuniambia huyo mtu aliyotokezea ni nani?" Bahlul bila ya kusita anamjibu: "Huyo mtu aliyeingia nyumbani kwa ghafla alikuwa ndiye bwana wa kwanza wa yule bibi kwani alikwenda safari na baada ya muda mrefu kupita, ilijulikana kuwa amefariki na hivyo huyo mwanamke akaolewa na bwana wa pili (aliyekuwa nyumbani) baada ya kupokea idhini ya hakimu sharia. Wale watu wawili walikuwa wamelipwa kwa ajili ya kusali na kufunga saumu zilizo za qadhaa za bwana wake aliyesadikiwa amekufa safarini.

Na kurejea kwake kutoka safari ndefu aliyosadikiwa amekufa, imebatilisha ndoa ya mke wake na yule bwana kwani yu hai bado, vile vile saumu na sala pia zinabatilika kwani kumsalia mtu aliye hai pia ni batili." Kwa hayo, Harun na wanabaraza wake wote walivutiwa na majibu ya Bahlul na walimsifu sana. Baada ya hapo, ilikuwa ni zamu ya Bahlul kuuliza swali: "Je niulize?" " Uliza tu!" alijibiwa. Bahlul aliuliza: "Iwapo ninayo kasiki moja ya siki (vinegar) na nyingine ya urojo wa sukari, na kwa ajili ya kutengeneza Sikanjabin (kinywaji cha Siki) nimeweka ili kuchanganya katika kasiki ya tatu na hapo tunakuja kumkuta panya amefia humo. Je unaweza kutuambia kuwa huyo panya alitokea kasiki ya Siki au Urojo wa Sukari? Hapo huyo mtu alijaribu kwa uwezo wake wote kumjibu Bahlul, lakini alishindwa. Kwa kuona hali hiyo, Harun alimwambia Bahlul "sasa wewe mwenyewe tujibu hayo." Bahlul alimwambia Harun: "Nitafanya hivyo iwapo huyu mtu atakiri kutoelewa majibu yake." Kwa masikitiko na aibu kubwa huyo Faqihi alikubali kushindwa kwake kwa kuling'amua hilo fumbo. Alianza Bahlul kulijibu: "itabidi sisi kumtoa huyo panya na kumwosha vizuri kwa maji safi halafu tupasue tumbo lake na humo iwapo tutakuta siki au urojo wa sukari, basi itatubidi tumwage kile kitakachothibitika kuwamo tumboni mwake." Wote waliokuwa wamehudhuria, walifurahishwa mno na majibu ya Bahlul na Faqihi alilazimika kutoa Dinar elfu moja za dhahabu ambazo Bahlul alizigawa miongoni mwa mafuqara wa Baghdad.

(6). BAHLUL NA MTUMWA ALIYEOGOPA MAJI

Mfanya biashara mmoja alikuwa akisafiri katika jahazi pamoja na mtumwa wake kuelekea Basrah. Kwa bahati na Bahlul alikuwamo humo pamoja na watu wengineo. Mtumwa huyo alianza kulia palipotokea machafuko hapo majini. Wasafiri wote walikerwa na sauti za kilio cha mtumwa huyo. Hapo Bahlul alimwomba ruhusa mfanyabiashara huyo ili atumie mbinu za kuweza kumkomesha mtumwa huyo, basi bila ya pingamizi alipewa ruhusa. Na hapo Bahlul alitoa amri ya kutupwa majini kwa utumwa na ilitekelezwa hivyo. Alipofikia wakati wa kutaka kufa, alitolewa nje. Baada ya kutolewa nje, mtumwa huyo aliketi kimya akitulia katika kona moja ya jahazi. Hapo baadaye, Bahlul alielezea: "Huyu mtumwa alikuwa haelewi raha na usalama wa jahazi inapokuwa majini. Pale alipotupwa majini ndipo alipotambua kuwa jahazi ni mahala pa raha na usalama."

Fundisho: Amesema mtume(s.a.w.w) : "Safirini na mutajitajirisha (kwa uzoefu na uelewano). "

(7). SWALI KUTOKA HARUN

Siku moja Harun alikuwa katika Qasri yake akiangalia mandhari iliyokuwa ikimzunguka na sauti ya mbubujiko wa maji ya mto Tegris. Na mara hapo akatokezea Bahlul, na Harun alimwambia Bahlul: "Ewe Bahlul! leo hii nakuuliza fumbo, iwapo utafumbua vyema basi nitakupa dinar elfu moja na iwapo utashindwa basi nitatoa amri ya kukutosa majini." Bahlul alimwambia Harun: "Mimi sihitaji dinar hizo, bali ninakubali kwa sharti moja." Na alipokubali Harun, Bahlul alisema: "Iwapo nitaweza kulijibu vyema basi itakubidi kuwaachia marafiki zangu mia moja - kutoka Gereza lako, na iwapo nitashindwa basi unao uhuru wa kunitupa majini."

Alianza Harun kulielezea fumbo lake: "Iwapo mimi ninayo mbuzi mmoja, mbwamwitu, na fungu la majani.Je nitawezaje kuvivusha vyote hivyo, kwamba majani hayataliwa na mbuzi na wala mbuzi kuvamiwa na mbwamwitu?" Bahlul alianza kumjibu: "Kwanza utamvusha mbuzi kwenda ng'ambo ukimwacha mbwa mwitu na majani. Baadaye utachukuwa majani uyavushe huku ukirudi na mbuzi upande huu. Utamwacha mbuzi upande huu na utamchukua mbwamwitu ng'ambo.Mwishoni utampeleka mbuzi. Kwa hivi majani hayataliwa na mbuzi wala mbuzi kuvamiwa na mbwamwitu." Harun alifurahishwa mno kwa majibu ya Bahlul. Na hapo Bahlul alimpa orodha ya majini mia moja ya wafuasi na wapenzi wa Ali bin Abi Talib(a.s) . Lakini Harun alimgeuka Bahlul. Lakini Bahlul aliendelea kusisitiza, na hatimaye aliwaacha huru watu kumi tu na akimwamwuru Bahlul kuondoka.

(8). BAHLUL AUZA PEPO

Siku moja Bahlul alikuwa ukingoni mwa mto akicheza kwa udongo kwa kutengeneza nyumba na bustani. Hapo alitokea Zubeidah, mke wake Harun, akipita hapo. Alipomkaribia Bahlul, alimwuliza: "Ewe Bahlul! Je wafanya nini?" Bahlul alimjibu: "Najenga Pepo (Jannat) ." Zubeidah alimwambia: "Je wauza hizi Pepo ulizozijenga?" Bahlul alimjibu: "Naam ninaziuza!" Zubeidah alimwuliza: "kwa Dinar ngapi?" Bahlul alimjibu "Kwa Dinar mia moja tu!" Kwa kuwa Zubeidah alikuwa akitaka kumsaidia Bahlul, hivyo aliona hapo ndipo pahala pa kumsaidia na alimwamuru mfanyakazi wake amlipe Bahlul hizo fedha. Nao walimlipa hizo dinar mia moja. Usiku ule Zubeidah aliota ndoto akiwa Peponi ambamo kuna Qasri nzuri mno iliyopambwa mno na wapo wajakazi wamesubiri amri, wao walimwambia hiyo ndiyo Qasri aliyoinunua kutoka kwa Bahlul. Zubeidah alipoamka siku ya pili, akiwa amejawa na furaha, alimwelezea mume wake, Harun. Harun alimwita Bahlul, alipofika, Harun alimwambia, "Ewe Bahlul, chukua hizi Dinar mia moja na uniuzie Pepo mojawapo ya Pepo kama ile uliyomwuzia Zubeidah." Bahlul alicheka na kumwambia: "Zubeidah alinunua bila ya kuona ambapo wewe unataka kununua baada ya kujua ya kuwapo kwake. Hivyo sitakuuzia!"

(9). HARUN RASHID AMKASIRIKIA BAHLUL

Harun alimwajiri jasusi makhususi kwa ajili ya kuchunguza na kuripoti kwake juu ya imani na akida sahihi za Bahlul. Baada ya siku chache huyo jasusi alikamilisha uchunguzi wake na kuripoti kwa Khalifa kuwa Bahlul alikuwa ni mpenzi wa Ahl-al-Bayt ya mtume(s.a.w.w) na alikuwa mfuasi wa Imam Musa al-Kadhim(a.s) . Harun alimwita Bahlul na kumwambia: "Ewe Bahlul! Mimi nimepata habari za kuaminika kuwa wewe ni mmojawapo wa wapenzi na wafuasi wakubwa wa Musa ibn Jaafar na hivyo unafanya kila jitihada za kudhihirisha na hivyo umejidhihirisha u - mwehu ambapo sivyo ulivyo!" Bahlul alimjibu: "Iwapo hivyo ndivyo ilivyo, je utanifanya nini?" Kwa majibu hayo, Harun alighadhibika mno na kumwamuru Masrur, mfanyakazi wake, amvue nguo Bahlul akalishwe juu ya punda na kuzungushwa mjini na hatimaye kukatwa kichwa mbele yake Harun. Masrur, alitekeleza vile alivyoamrishwa na hatimaye kumleta mbele ya Harun katika hali hiyo ili aweze kuuawa. Mara, hapo akatokezea Jaafer Barmaki ambaye kwa kuiona hali hiyo ya Bahlul alimwuliza sababu ya hali yake hiyo: "Ewe Bahlul! Je umetenda kosa gani?" Bahlul alimjibu: "Kwa kuwa mimi nimesema ukweli, kwa hivyo Khalifa akanizawadia mavazi yenye thamani." Harun Rashid, Jaafar, na wote waliokuwepo walichekeshwa mno kwa majibu ya Bahlul, na papo hapo Harun alimsamehe Bahlul na kutoa amri ya kufunguliwa na apewe mavazi mapya na mazuri. Lakini Bahlul hakukubali hayo bali yeye alichukua kifurushi cha nguo zake kuukuu na kuondoka.

(10). BAHLUL NA HARUN KWENDA KUOGA PAMOJA

Ilitokea siku moja Bahlul na Harun Rashid kukutana katika Hammam (majumba ya kuogea). Khalifa alimfanyia mzaha kumwuliza Bahlul: "Je iwapo ningalikuwa mtumwa, ningalikuwa na thamani gani?" Bahlul alimjibu: "Dinar hamsini." Harun Rashid katika kughadhabika alisema: "Ewe Mwehu! itawezekanaje hivyo? Mavazi yangu tu yamezidi thamani hiyo!" Hapo Bahlul alimwambia: "Kwa hakika mimi nimesema kuwa hiyo ni thamani ya nguo zako tu ama Khalifa hana thamani yoyote!"

(11). MABISHANO PAMOJA NA ABU HANIFA

Abu Hanifa alikuwa akiwafundisha wafuasi wake na Bahlul alikuwa ameketi katika kona moja akisikiliza masomo hayo, baina ya mafunzo, Abu Hanifa alisema kuwa yeye hakukubaliana na mambo matatu yaliyoelezwa na Imam Jaafer Sadiq(a.s) , nayo ni:

Kwanza : Imam Jaafer Sadiq(a.s) amesema kuwa sheitani ataadhibiwa katika Jahannam (motoni). Kwa kuwa sheitani ameumbwa kwa moto sasa moto utamuumizaje moto huo?

Pili : Yeye amesema kwa sisi hatutaweza kumwona Allah (s.w.t) ambapo twajua kuwa kile kilichopo ni lazima kionekane. Hivyo Allah anaweza kuonwa kwa macho.

Tatu : Yeye amesema kila mtenda tendo ndiyo mhusika mwenyewe atawajibika kujibu kwani ametenda mwenyewe. Ambapo sisi (wakina Abu Hanifa) twaamini kuwa kila kitendo kitatokana na Allah na wala mtu hawajibiki. Abu Hanifa alipoyamaliza kuyasema hayo, Bahlul alichukua rundo moja la udongo na kumlenga Abu Hanifa. Alipoutupa, ulimpiga Abu Hanifa juu ya uso wake, ulileta maumivu makubwa mno. Na hapo ndipo Bahlul alipotimua mbio, lakini wanafunzi wa Abu Hanifa waliweza kumshika Bahlul. Kwa kuwa Bahlul alikuwa akipatana mno na Khalifa, alipelekwa mbele yake, ambapo Khalifa alielezwa hali yote. Bahlul alisema: "Aletwe Abu Hanifa ili niweze kumjibu!" Alipoitwa Abu Hanifa, Bahlul alimuuliza, "Je, dhambi gani nililokufanyia? Abu Hanifa alisema: "Kichwa changu chaumwa sana kwa sababu ya wewe kunipiga rundo la udongo." Bahlul alimjibu: "Je waweza kunionyesha maumivu hayo?" Hapo Abu Hanifa alimwambia: "Je na maumivu pia yanaweza kuonyeswa?" Basi Bahlul alianza kumjibu kwa busara: "Wewe mwenyewe umedai kwa kila kitu kilichopo lazima kionekane na umekuwa ukimpinga tena Imam Jaafer Sadiq(a.s) na vile vile unadai kuwa itawezekanaje kwa Allah kuwapo na asiweze kuonekana? "Pili madai yako hayafai, kwani itawezekanaje kuwa kitu cha jinsi moja kiwezi kukiumiza kitu cha jinsi hiyo (sheitani hana dhambi wala kuchomwa moto) kwani wewe umeumbwa kwa udongo na udongo niliokupiga ni vitu vya jinsi moja." Tatu, kila tendo linatokana na Allah, hivyo kwanini wewe unilaumu na kunishtaki mbele ya Khalifa na kudai kisasi kwani humlaumu Allah aliyenisababisha mimi kukupiga?" Kwa hayo, Abu Hanifa aliaibika na hakuwa na chaguo lolote isipokuwa kuondoka hapo.

(12). BAHLUL NA WAZIRI

Siku moja Waziri mmoja wa Harun alimwambia Bahlul, "Ewe Bahlul, Khalifa amefanya wewe uwe mtawala na Hakimu wa ufalme wa mbwa, kuku na nguruwe wote." Bahlul alimjibu: "Basi kuanzia hivi sasa, wewe hauna budi kuzitii amri zangu kwani wewe pia upo miongoni mwa raia wangu." Wote waliokuwa pamoja na Waziri walicheka mno na kulimfanya aondoke kimya kwa kuaibishwa.

(13). BAHLUL AMSIHI ABDULLA MUBARAK

Siku moja Abdulla Mubarak alimwendea Bahlul kwa kutaka nasaha. Alipofika kwa Bahlul, alimkuta kichwa wazi na miguu wazi akisema Allah! Allah..... Alimwendea na kumtolea salaam na Bahlul alimjibu. Baadaye Abdulla alisema: "Ewe Sheikh! Naomba unipatie nasaha na naomba unionyeshe njia itakayonionyesha vile niishi maisha yangu pasi na madhambi kwani mimi ni mtu mwenye madhambi ambayo nafsi yangu potofu imenighalibu. Hivyo nionyeshe njia hiyo mwokovu."

Bahlul alimwambia Abdullah: "Mimi mwenyewe nimehangaika mno, sasa wawezaje kunitegemea? Iwapo ningelikuwa mwenye akili, basi watu wasingaliniita mwehu na wewe watambua kuwa maneno ya mwehu hayana athari yoyote yakuweza kukubaliwa na watu. Kwa hivyo, nakuomba umtafute mtu ambaye ni mwenye akili ili akushauri vyema."

Abdullah akasema: "Ewe Sheikh mara nyingi wehu wanatokezea kusema mengi yenye busara." Kwa hayo Bahlul alinyamaza. Hapo tena Abdullah akaanza kumwomba kwa kumbembeleza. "Ewe Sheikh, tafadhali sana usinivunje moyo kwani nimekuja kwa matumaini makubwa."

Bahlul alimjibu: "Ewe Abdullah! Tafadhali sana kwanza kabisa kubali sharti zangu nne ili usiyageukie maneno ya mwehu, ndipo hapo nitakupa nasaha zangu ambazo zitakuokoa.

Abdullah akasema: "Je masharti hayo manne ni yapi ili niweze kuyakubali."

Bahlul akasema: "Sharti la kwanza ni hili: iwapo utatenda dhambi yolote ile, na kupinga hukumu ya Allah, basi uache kula riziki itokayo kwa Allah."

Abdullah akamwambia: "Nisipokula riziki ya Allah, je nitakula riziki ya nani?

Bahlul akasema: "Wewe ukiwa mtu mwenye akili umedai kuwa unafanya ibada ya Allah na kula riziki yake Allah na pepo hapo unafanya maasi ya kutozitii amri zake. Tafadhali sana jaribu kuamua mwenyewe iwapo hii ndio haki ya ibada?"

Abdallah akasema: "Ewe Sheikh wewe umesema kweli na yaliyo sahihi na sharti la pili ni ipi?" Bahlul akasema: Sharti la pili ni kwamba, unapotenda dhambi lolote, basi jitoe katika milki ya Allah." Abdullah akasema: "Ama kusema ukweli sharti hili la pili ni gumu kuliko hata lile la kwanza, kwani kila mahala pana ardhi ya Allah na utawala wake, sasa nitakwenda wapi?" Bahlul alimwambia: "Kwa kweli hili ni jambo baya mno kwani wewe unakula riziki yake na kuishi katika milki yake na papo hapo unakana kutii kwa amri yake. Fanya maamuzi yako wewe mwenyewe kuwa hiyo ndiyo sharti ya ibada?" Hapo Abdullah aliuliza: "Je sharti la tatu ni lipi?" Bahlul alijibu: "Sharti la tatu ni kwamba iwapo wewe wataka kutenda madhambi yoyote, basi uende ujifiche mahala pale ambapo Allah hataweza kukuona, wala kuona hali yako, na hapo ndipo utende vile upendavyo." "Sharti hilo ni gumu zaidi!" alisema Abdullah, kwani Allah anafahamu na kuona kila kitu, yupo kila mahala. Chochote kile akitendacho mja, Allah hukiona na kukielewa."

Bahlul alisema: "Wewe mwenyewe u - mtu mwenye akili. Inakubidi wewe uelewe kuwa Allah yupo kila mahala na kumwona kila mtu. Hivyo ni jambo la kustaajabisha ni kule kutumia riziki yake kuishi katika milki yake na vitendo wazi katika utawala wake ambavyo yeye anakuona na kufahamu. Baada ya yote hivyo unadai kufanya ibada yake. Abdullah alisema: "Kwa hakika umesema ukweli kabisa. Na sharti la nne ni lipi?" Bahlul alimwambia: "Wakati utakapoijiwa na Malakul Maut (Malaika atoae roho) ili kuitoa roho yako, basi umzuie asifanye hivyo hadi hapo utakapokuwa umekwisha agana na ndugu na rafiki zako wote na kuweza kutenda matendo mema ambayo yatakusaidia hapo baadaye." Abdullah alijibu: "Lo! Sharti hili ni gumu zaidi kuliko masharti yote. Huyo Malakul Mauti hatanipa hata fursa ya kupumua!" Hapo ndipo Bahlul alipomjibu: "Ewe mtu mwerevu! Wewe watambua vyema kabisa kuwa mauti hayana hila yoyote, na hauwezi kamwe kujitenga nayo na hautapatiwa muhula wowote ule. Na inawezekana pia ikatokea mauti katikati mwa hali ya madhambi na hautapata hata muhula wa kupumua kama vile Allah (s.w.t) alivyosema. Kwa hiyo ewe Abdullah! Pokea nasiha hata kwa mwehu na uamke kutoka usingizi wako!" Jihadhari na ghururi na ulevi wako na uwazie akhera kwani safari yako ndefu ipo mbele yako na umri wako upo mdogo kabisa. Kazi ya leo usiiweke kesho kwani kesho hiyo labda hautaiona. Muda huu uliopo uthamini. Kazi za Aakhera usizicheleweshe kwani usichokitenda leo utakijutia hapo kesho na kujuta kwako hakutakufaidisha."

Abdullah alipoyasikia hayo alianza kuwaza huku akiwa amekiinamisha kichwa chake. Mara Bahlul alianza kusema: "Ewe Abdullah! Wewe umenitaka nikusihi ili uweze kufaidika nayo kesho, sasa baada ya kuyasikia hayo mbona wainamisha kichwa chini?" Siku ya Qiyama, katika uwanja wa Hisabu na Kitabu, utawajibu nini Malaika watakao kuhoji. Yeyote yule atakayekuwa na hisabu yake safi humu duniani, hatakuwa na khofu yoyote ile hapo Aakhera! Hatimaye,Abdullah alikiinua kichwa chake na kusema: "Ewe Sheikh! Mimi nimeyasikia yote uliyoyazungumza. kwa moyo wangu wote na nimelikubali hili sharti la nne pia, naomba unisihi zaidi na kunifanya niwe mmoja wenu. Bahlul alisema: "Ewe Abdullah! Mwanadamu afanyalo lolote inambidi aweke mbele maamrisho yake Allah (s.w.t) na hata katika hali ya kusema au kusikiliza, kwani kwa kila hali yu mwumba wa Allah (s.w.t)" Bahlul alikuwa ni mtu ameelimika kwa Imam Jaafer as-Sadiq(a.s)

2

HIKAYA ZA B A H L U L MWENYE BUSARA

(14). BAHLUL AMSIHI HARUN

Harun Rashid alikuwa akipita njia moja na alimkuta Bahlul akicheza mbio na watoto, hapo alimpigia sauti ya kumwita. Bahlul alipofika alisema: "Je una kazi gani?" Harun alimwambia, "Nataka nasiha zako!" Hapo Bahlul alimwambia: "Tazama kwa makini mno majumba ya Wafalme yaliyokuwa ya fahari na sasa yalivyo na vile vile makaburi yao. Hayo pia yanatosha kukutanabahisha. Wewe waelewa vyema kabisa vile wafalme hao walivyokuwa wakiishi katika majumba hayo kwa starehe na fakhari na kiburi chao, lakini leo walipo (makaburini mwao) hawana la kufanya ila wao wanajuta kwa yale waliyoyafanya wakiwa na uwezo. Uelewe vyema kabisa kuwa nasi pia karibuni tutaungana nao." (tutakufa). Kwa hayo, Harun alitetemeka, na hakusita kuuliza: "Sasa, je nifanyeje ili mola aniwie radhi?" Bahlul alimjibu, "Watendee matendo mema viumbe vya Mwenyezi Mungu kwa hayo utaweza kupata radhi yake Mwenyezi Mungu." Harun aliuliza, "Je ni kama matendo gani?" Bahlul alimjibu: "Utawale kwa haki na uadilifu. Chochote kile ukionacho kibaya kwako ndivyo hivyo hivyo kiwe kwa ajili ya wengineo. Kilio cha aliyedhulumiwa na maombi yake uyasikilize vyema na kuyajibu kwa utukufu na uyafanyie uchunguzi kwa makini na utoe maamuzi na hukumu zako kwa haki na uadilifu." Harun alisema: "Hongera ewe Bahlul! Kwa hakika umenipatia nasiha nzuri mno. Mimi natoa hukumu kuwa deni zako zote zilipwe." Bahlul alimjibu: "Deni haliwezi kamwe kulipa deni. Chochote kile ulichonacho wewe ni mali ya Umma,uwarejeshee mali yao. Usinifanyie hisani kwa mali iliyodhulumiwa." Harun alimwambia: "Fanya ombi lako lingine." Bahlul alimjibu: "Ombi langu ni kuwa wewe ujaribu kutimiza nasiha zangu, lakini nasikitika mno kuona kuwa roho na nafsi yako imeshakuwa ngumu kutokana na tamaa na starehe za dunia na hivyo nasiha zangu hazitakuathiri chochote." Kwa hayo, Bahlul akipeperusha kifimbo chake na kusema: "Sogea, kwani farasi wangu hupiga teke pia." Kwa maneno hayo, alijiondokea na safari yake.

(15). BAHLUL AMSIHI FADHIL IBN RABI'I

Siku moja Waziri wake Harun Rashid, Fadhil ibn Rabii alikuwa akipita njia moja hapo alimkuta Bahlul ameketi akiwa ameinamisha kichwa chini akiwa anawaza. Fadhil alisema kwa sauti, "Ewe Bahlul! Je, wafanyaje?" Bahlul alikiinua kichwa na alipomwona Fadhil, alisema: "Nimekuwa nikiwazia yatakayokupata kwani yaliyompata Jaafer Barki ndiyo hayo hayo yatakayokupata wewe." Kwa hayo, moyo wake Fadhil ulitingisika, na akasema: "Ewe Bahlul! Mimi nimeweza kusikia hali hiyo kutoka watu tofauti lakini sijawahi kukusikia wewe, hivyo nitapenda kukusikia, juu ya kuuawa kwa Jaafer." Bahlul akaanza kuelezea:"Katika zama za Ukhalifa wa Mahdi, mwanamke Mansur, mwanamke Khalid Barki, Yahya, aliteuliwa kuwa Katibu na mshauri wa Harun Rashid. Katika kipindi kifupi, Harun, Yahya na Jaafer walishikamana mno. Harun na Jaafer walipendana mno hadi Harun dada yake Abbasa, kuolewa na Jaafer. Lakini pamoja na ndoa hiyo, alimpa sharti la kutomwingilia dada yake. Lakini Jaafer alimwingilia kimwili, na hapo Harun alipopata habari hizo aligeuza urafiki wake katika uadui na upingamizi. Kila wakati alikuwa akibuni mbinu za kumwua na kuuteketexa ukoo wao mzima. Usiku mmoja alimwambia mtumwa wake Masrur: "Mimi nataka usiku wa leo uniletee kichwa cha Jaafer."Kwa hayo, Masrur alishtushwa na kukiinamisha kichwa chake chini. Hapo Harun alimwambia: "Je kwa nini umenyamaza na wawaza nini?" Mansur alimjibu: "Loh! Kazi hii ni kubwa mno, lau ingeliniijia mauti kabla ya kuamriwa kazi kama hii."

Harun alimjibu: "Iwapo hutaitekeleza amri yangu hii, basi utanaswa na ghadhabu na adhabu zangu na utambue wazi wazi kuwa nitakuua vile hadi wanyama pia watakuhurumia." Masrur kwa khofu ya mdhalimu huyo aliingia nyumbani mwa Jaafer na kumwelezea vile hukumu ilivyokuwa. Jaafer alimwambia: "Labda hukumu hii ameitoa akiwa katika hali ya ulevi na kutakapokucha atajuta, hivyo nakuomba uende kwa Khalifa na umjulishe kuuawa kwangu. Iwapo utakuta hakuna athari zozote za kujuta na kusikitika hadi asubuhi basi, utambue kuwa nitakuwekea kichwa changu tayari kwa upanga wako." Masrur hakuweza kusadiki maneno ya Jaafer, na alimwambia: "Nataka wewe ufuatane nami hadi kwake Harun Rashid, labda inawezekana akakusamehe kwa upendo wako alionao." Jaafer aliyakubalia maneno ya Masrur na alijitolea kwa maangamizi yake. Basi Masrur alitokezea mbele ya Harun akiwa anatetemeka. Harun aliuliza: "Masrur, je umetekeleza?" Masrur alimjibu:"Nimemleta Jaafer, yupo nyuma ya pazia amesimama."

Khalifa akawa amekasirika, alisema: "Iwapo utachelewa hata punde kutekeleza amri yangu, basi nitahakikisha kuwa wewe uuawe kwanza." Baada ya mazungumzo hayo, hapakuwapo na fursa ya kupoteza. Masrur alimkimbilia Jaafer, kijana mrembo, na mwema, na kumkata kichwa na kukileta mbele ya Harun. Khalifa huyu aliyekosa huruma, hakukomea hapo tu, bali aliamrisha kuuangamiza ukoo mzima na mali na vitu vyao vyote kuchukuliwa. Mwili wa Jaafer usio na kicwa ulininginizwa katika jumba la Khalifa na baada ya siku chache ukachomwa moto. Sasa ewe Fadhil! Mimi nahofia matokeo yako. Nahofia matokeo yako pia yasiwe kama yale yaliyompata Jaafer." Fadhil alishtushwa mno kwa mazungumzo ya Bahlul, na alimwambia Bahlul kuwa "Niombee usalama wangu!"

(16). KISA CHA KUJENGA MSIKITI

Fadhil ibn Rabii aliujenga Msikiti katika mji wa Baghdad. Ilipofika siku ya kubandika kibao, aliulizwa kitu gani kiandikwe juu yake. Naye alishauri kuwa jina lake liandikwe kwani yeye ndiye aliyeugharamia ujenzi wake. Wakati hayo yalipokuwa yakitokea, Bahlul pia alikuwapo hapo, naye hakusita kumwuliza: "Je umejenga msikiti huu kwa ajili ya nani?" Fadhil alijibu: "Kwa ajili ya Allah (s.w.t)" Bahlul alisema: "Iwapo ni kwa ajili ya Allah (s.w.t) basi usiandikishe jina lako." Kwa hiyo, Fadhil alikasirika na akatamka: "Kwa nini nisibandike jina langu? Je watu watamjuaje mtu aliyejenga?" "Je kwa nini usiandike jina langu?" Akasema Bahlul. "Loh! Hayo kamwe hayawezi kuandikwa." akamjibu Fadhil. "Iwapo umejenga huu Msikisti kwa ajili ya kujionyesha kujifaharisha, basi utambue wazi kuwa thawabu zako kwa Allah (s.w.t) zimepotea." Hayo ndiyo aliyoyasema Bahlul. Kwa hayo, Fadhil aliaibika na akanyamaza na kusema: "Fuateni lile alisemalo Bahlul." Hapo Bahlul akawaambia "andikeni Aya moja ya Quran tukufu na kuitundika mlangoni mwa Msikiti."

(17). BAHLUL NA MWIZI WA VIATU

Siku moja Bahlul alikwenda Msikitini akiwa amevaa viatu vipya, na huko alimuona mtu mmoja akiviangalia mno viatu vyake, hivyo akaelewa kuwa ataweza kuviiba. Basi Bahlul akavichukua viatu vyake na kuviweka mbele yake huku akisali. Yule mwizi akamwambia: "Sala haisihi katika hali hiyo!" Bahlul akamjibu: "Iwapo sala itanitoka basi viatu vitabaki."

(18). BAHLUL NA RAFIKI YAKE

Siku moja rafiki yake Bahlul alichukua ngano kwenda kusaga, na baada ya kusagiwa alipakia juu ya punda na kuondoka. Alipokaribia nyumba ya Bahlul, yule punda alianza kufanya machachari na akajibwaga chini. Hivyo huyo mtu alimwita Bahlul na kumwomba msaada wa punda wake ili aweze kuufikisha mzigo wake nyumbani. Bahlul alikuwa ameishakwisha kula kiapo cha kutomwazima mtu yeyote punda wake, na hivyo alimwambia rafiki yake: "Mimi sina punda!" Ikatokea kuwa punda akalia kwa sauti. Na hapo rafiki yake akamwambia:"Kumbe punda wako yupo nyumbani na wewe waniambia kuwa hauna punda!" Bahlul akamwambia: "Loh! wewe rafiki wa kiajabu kweli! Sisi tupo marafiki kwa muda wa miaka hamsini, lakini nashangaa kuona kuwa hautaki kuamini nikuambiayo na huku unayaamini yale akuambiayo punda."

(19). BAHLUL NA MGANGA WA HARUN

Harun Rashid alimleta mganga kutoka Ugiriki Khususan katika Baraza lake. Alipowasili Baghdad, alipokelewa na kupewa heshima za kila aina. Kila mtu wa mji wa Baghdad walikwenda kumuona mganga huyo, na siku ya tatu Bahlul pia alikwenda kumuona pamoja na watu wachache. Wakati mganga akiwa anasifiwa na kutukuzwa, mara Bahlul akamwuliza swali : "Je unafanya kazi gani?" Kwa kuwa mganga alikwisha kuelewa vile Bahlul alivyo na uwehu wake, hivyo akataka kuleta kichekesho kwa kumjibu: "Mimi ni mganga wa huisha wafu." Bahlul akamjibu: "Tafadhali usiwaue hai na kumhuisha maiti ni fidia yake." Kwa majibu hayo ya Bahlul, Harun Rashid pamoja na watu wote katika Baraza lake waliangua kicheko hadi yule mganga akauhama mji wa Baghdad kwa aibu.

(20). BAHLUL AULIZWA SWALI

Siku moja Bahlul alikwenda katika Baraza la Harun Rashid na akaketi mbele yake. Kwa hayo, Harun aliudhika mno na alitaka amuaibishe Bahlul mbele ya wote waliokuwapo hapo. Alimwuliza: "Je Bahlul yu hadhiri? Nataka jibu la fumbo langu." Bahlul alisema: "Ni lazima kwanza uniambie sharti lako na utoe ahadi ya kutonigeuka katika kutimiza ahadi hiyo." Kwa hayo, Harun alisema: "Iwapo utanijulisha jawabu papo hapo basi nitakupa Ashrafi elfu moja na iwapo utashindwa kunijibu basi nitatoa amri ya kunyolewa kwa ndevu na masharubu yako, kisha utembezwe katika mitaa na vichochoro vya Baghdad kwa kuaibishwa na kudhalilishwa." Bahlul alimjibu "Ah! Mimi sijali wala sihitaji hizo Ashrafi zako, bali ninalo sharti moja iwapo nitaweza kulijibu fumbo lako." Hapo Harun akasema: "Je sharti lipi hilo?" "Iwapo nitaweza kukujibu basi nitataka uwatolee amri inzi wasinisumbue" alisema Bahlul. Harun alifikiri kwa kitambo, kisha akasema: Hili jambo haliwezekani kwani inzi sio katika utii wangu." Kwa hayo Bahlul aliangusha kichekesho na kwa mshangao akasema: Je kunaweza kutegemewa nini kutoka mtu ambaye hawezi hata kudhibiti kitu kidogo mno kama inzi?" Kwa hayo, Bahlul aliwaacha wote katika hali ya mshangao. Kwa majibu hayo, uso wa Harun ulianguka na Bahlul alipoyaona hayo, alisema: "Nipo tayari kujibu swali lako bila sharti lolote." Basi Harun alijikaza, na kuuliza: "Je ni mti upi ule ambao umri wake ni mwaka mmoja na unao matawi kumi na mawili na majani thelathini ni siku ambazo sehemu moja ni usiku na wa pili ni mchana." Harun alistajabishwa kwa majibu. Na wote waliokuwapo pia walifurahishwa mno kwa busara ya Bahlul.

(21). SADAKA YA KHALIFA

Siku moja Harun Rashid alimpatia Bahlul kiasi fulani cha fedha ili awagawie masikini, mafukara na wenye mahitajio. Bahlul alizipokea fedha hizo, na baada ya kitambo, alimrejeshea Khalifa fedha hizo. Harun Rashid alistaajabishwa kwa hatua hiyo ya Bahlul na hivyo alitaka kujua sababu. Bahlul alimjibu katika hali ya kumhurumia Khalifa: "Ewe Khalifa! Mimi kwa hakika nimejaribu mno kumtafuta mustahiki wa sadaka yako hiyo, lakini nimeona kuwa hapa mjini petu hakuna mtu mwingine isipokuwa ni wewe tu! Kwani nimewaona wanaokukusanyia kodi wewe, wakiwa wanawapiga mijeledi raia ili kukukusanyia fedha wewe ambazo unazihitaji katika hazina yako. Hivyo nimefikia uamuzi huo wa kukupa fedha hizo wewe tu unayestahiki mbele ya macho yangu kuliko raia yoyote yule

(22). NEEMA BORA YA ALLAH S.W.T

Siku moja Harun Rashid alimwuliza Bahlul: "Je ni neema ipi ya Allah (s.w.t) iliyo bora?' Bahlul alimjibu: "Neema bora kabisa ya Allah (s.w.t) ni Akili (Agl). Khawaja Abdullah Ansari pia amesema katika munajat: "Ewe Allah! Kwa yule aliyepewa nawe Akili je ni kipi tena ulichomnyima na yule asiyepewa akili umempa nini?" Imepatikana katika riwaya moja kuwa Allah SWT amepata kumwondoshea mja wake neema zake, basi humwondoshea akili yake. Akili (Agl) inahisabiwa katika kikundi cha riziki.

(23). BAHLUL NA MWIZI

Bahlul alikuwa akiishi katika nyumba iliyokuwa tupu. Mbele ya nyumba yake kulikuwa na duka la mshona viatu ambaye dirisha lake lilikuwa likifunguka mbele ya nyumba ya Bahlul alikusanya fedha kidogo na akazifukia ardhini na kila alipokuwa akipata dharura, alikuwa akifukua kiasi alichokuwa akikitaka na kufukia kiasi kilichobakia. Siku moja alipopata dharura ya fedha, alikwenda kufukua, na akakuta hakuna chochote shimoni, na hapo aling'amua kuwa fedha hizo zimeibiwa na mshona viatu tu kwani dirisha lake lilikuwa likifungukia mbele yake. Basi yeye bila ya kuonyesha dalili zozote zile alikwenda dukani mwa mshona viatu na akaketi kimya, na alianza mazungumzo ya kila aina hadi mshona viatu akafurahi na kuvutiwa. Hapo ndipo Bahlul aliposema: "Ewe rafiki mpenzi! Hebu naomba unijumlishie hesabu yangu!" Mshona viatu akasema: "Haya anza nami nitakujumlishia." Bahlul alianza kutaja majumba mengi na pamoja na kila jumba alikuwa akiisemea na fedha. Hadi kutaja na nyumba anamoishi kuwa ameficha kiasi fulani cha fedha. Mwishowe, mshona viatu akamwambia kuwa jumla ya sarafu alizozitaja ni dinar elfu mbili.

Bahlul akawaza kwa kitambo, na akaanza kusema: "Ewe rafiki mpenzi! Mimi na kuomba ushauri mmoja." Mshona viatu akasema: "Ndiyo sema tu!" "Mimi nafikiri kuwa dinar hizo elfu mbili nizilete hapo kwangu na kuzifukia shimoni." Mshona viatu alimjibu "Loh! wazo zuri kabisa. Ndiyo, kusanya fedha zako zote kutoka kote ulikoficha na uzifukie hapo unapoishi." "Kwa hakika mimi nasakiki maneno yako tu! Na nakwenda kuzichukua fedha zote zilipo ili nizifukie humu mwangu! "Alimjibu Bahlul. Baada ya kusema hayo Bahlul aliondoka.

Baada ya kuondoka kwake, yule mshona viatu akawaza kuwa itakuwa vyema iwapo hizo fedha kidogo alizoziiba akazirudishe mahala pake ili atakaporudi Bahlul kufukia zingine azikute zipo na hivyo asiingiwe na shaka ya kuibiwa. Hivyo ataweza kupata fedha zaidi kwa mara moja. Hivyo yeye alikwenda kurudisha zote alizokuwa ameziiba. Baada ya masaa machache, Bahlul alirudi nyumbani mwake na akazikuta zile fedha zake zilizokuwa zimeibiwa na mshona viatu. Basi alizifukua zote na kumshukuru Mwenyezi Mungu, na aliacha nyumba hiyo akahamia mahali pengine. Mshona viatu alikuwa akimsubiri kwa hamu lakini hakuweza kumwona tena. Na baada ya kupita kipindi fulani, hivyo aliweza kung'amua kuwa Bahlul alimdanganya kwa hayo ili aweze kuzirudisha fedha zake!.