1
ROHO YA MATUMAINI
SAYYIDINA 'ALI BIN ABI TALIB
KIFO CHA MTUME(S.A.W.W)
Mtume baada ya miaka kumi ya kuishi mjini Madina ambapo Mtume(s.a.w.w)
aliugua kwa mara ya mwisho. Huu ulikuwa ni muda mbaya sana kwa familia yake. Hadhrat Ali
alikaa karibu na Mtume(s.a.w.w)
kwa wakati wote wa ugonjwa wake na Mtume(s.a.w.w)
hakupendelea Hadhrat Ali
aachane naye hata kwa muda mfupi tu. Hatimaye, Mtume(s.a.w.w)
aliaga dunia na kurudi kwa Bwana Wake. Kabla hajafa Mtume(s.a.w.w)
alimtaka Hadhrat Ali
asogee karibu naye, akamkumbatia na akazungumza naye kwa muda mrefu akiwa na madhumuni ya kumpa maagizo ya mwisho. Hata baada ya Mtume(s.a.w.w)
kumaliza mazungumzo yake na Hadhrat Ali
hakumwachilia aende, bali aliendelea kumshika mkono na kuuweka kifuani pake na roho ya Mtume(s.a.w.w)
ilipotoka mkono wa Hadhrat Ali
ulikuwa bado upo kifuani pake.
Baada ya Kifo cha Mtume(s.a.w.w)
: Vipi Hadhrat Ali
angeliweza kuuacha mwili wa Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
, baada ya kushirikiana naye kwa muda mrefu? Hivyo ibada za maziko ya Mtume(s.a.w.w)
ziliendeshwa na Hadhrat Ali
ambaye pia aliongoza na kushiriki katika kuteremsha maiti ya Mtume(s.a.w.w)
kaburini. Na Ali
alipoinua kichwa chake alikuta swali la kushika nafasi ya Mtume(s.a.w.w)
. Ukhalifa limekwisha kuamuliwa mara moja kwa watu wote, na wale ambao kwao swali hili lilikuwa swali muhimu sana baada ya kifo cha Mtume(s.a.w.w)
. Lakini kwa Hadhrat Ali
kuendelea kuueneza Uislamu ndilo jambo muhimu zaidi.
Baada ya kifo cha Mtume(s.a.w.w)
Hadhrat Ali
alijitenga akawa kimya kimya anaendelea kueneza Ujumbe, kwani alijua kuwa ilikuwa ni kazi yake ambayo aliifurahia kuifanya, na kila siku alikuwa tayari kutatua matatizo ya Waislamu waliyomletea kuyatatua. Hadhrat Ali
alitayarisha toleo la Qur'ani Tukufu na kuzipanga Aya zake kwa utaratibu wa kufunuliwa kwao, pamoja na maelezo ya aya zilizochukua mahali pa aya nyingine (Nasikh), zile zilizochukuliwa mahali pao (Mansuukh), zile aya zisizo eleweka vizuri (Mutashaabi haat) na zile zilizo wazi wazi kabisa. Hadhrat Ali
alianzisha ari ya utafiti na uandishi katika tabaka Ia Waislamu wasomi. Na yeye mwenyewe aliacha zana muhimu sana kwa ufafanuzi wa Qur'ani, lugha, fiqah na mambo mengine ya kidini. Aliwatayarisha wanavyuoni ili waweze kuiendeleza kazi ya kuwaelimisha Waislamu baada ya kufa kwake. Alizipanga vizuri kanuni za sarufi ya Kiarabu na elimu ya ufasaha wa kusema. Hivyo Hadhrat Ali
alitoa mafunzo kwamba wakati uwapo mbaya na ubora wa mtu hautambuliwi, basi mtu anaweza kubakia nyumbani mwake na anaweza kuwatumikia watu wake na aangalie mawazo yake yasimpoteze kutoka katika misingi ya utu.
UKHALIFA
Baada ya muda mrefu upatao miaka 25, mnamo mwaka wa 35 Hijirya, Waislamu walimwomba Hadhrat Ali
akubali kuwa Khalifa, lakini kwa masharti kwamba atatawala kufuatana na Qur'ani Tukufu na Sunnat za Mtume(s.a.w.w)
. Waislamu waliyakubali masharti haya lakini wakati ulikwisha badilika, hivyo Waislamu wengi hawakuweza kuona haki ikifuatwa na wakakaa kimya. Ukoo wa Bani Umayyah waliiona hatari kwa faida zao katika utawala wake wa kidini. Hadhrat Ali
aliona kuwa ni wajibu wake kuyapiga vita mawazo haya na vita vya "Jamal", "Siffin", na Nahrawan", vilishuhudia kuwa mishipa ya Hadhrat Ali
ilikuwa na damu ya aina ile ile iliyofanya kazi kishujaa chini ya uongozi wa Mtume(s.a.w.w)
katikati ya safu za askari maadui katika vita vya "Badr", "Uhud", "Khandaq" "Khaibar". Vipingamizi vya Bani Umayyah havikumruhusu kutawala na kuwarekebisha watu wake.
Lakini hata hivyo, kwa muda mfupi wa maisha yake aliobakia kuendelezea Uislamu, aliifufua misingi ya Uislamu ambayo ni usawa maisha rahisi na kuishi kiaminifu. Akiwa na madaraka ya juu kabisa katika Uislamu, alikuwa na kawaida ya kukaa kando ya barabara akiuza tende, na rafiki yake Bwana Misam aliondoka kwenda kufanya kazi nyingine. Kila mara Hadhrat Ali
alivaa nguo za zamani na zenye viraka na alikuwa na mazoea ya kukaa chini na kula chakula pamoja na maskini. Kila mara aIigawanya pesa za 'Baitul-Mal' (Hazina ya Serikali) sawa sawa kati ya wale waliostahili. Siku moja ndugu yake aitwaye Aqil aliomba apewe pesa kidogo zaidi ya wengine. Hadhrat Ali
alikataa na akamwambia "Ingekuwa hivyo kama zingelikuwa pesa zangu. Lakini hii ni Mali ya Waislamu wote, hivyo huwezi kupendelewa zaidi kuliko wengine". Wakati fulani alipokuwa akikagua mahesabu ya pesa za 'Baitul-Mal' mtu mmoja kila mara alimjia kwa mazungumzo ya kibinafsi Hadhrat Ali
alikuwa kila mara akizima taa na kusema, "Taa ya 'Baitul-Mal' lazima itumike kwa kazi iwahusuyo Waislamu wote, siyo shughuli zingine". Kila wakati Hadhrat Ali
alijaribu kugawa pesa za 'Baitul Mal' kwa wale wanaostahili haraka iwezekanavyo. Hakupenda kuiacha kwanza.
Shahaadah yake: Lakini ole wao wale wabaya wa ulimwengu ambao hawakuweza kuyavumilia maisha ya Mchamungu huyu na kuwa bingwa wa amani, usawa, udugu na ubinadamu, Hadhrat Ali
alipata pigo la bapa lenye sumu la upanga uliolaaniwa na Abdul Rahman lbn Muljim. Ilikuwa mnamo tarehe ya Mwezi wa Ramadhani wa mwaka wa 40 Hijiriya, kuwa Hadhrat Ali
alipata pigo hili kali sana alipokuwa akisali sala ya Alfajiri katika Msikiti wa mji wa Kufa (nchini Iraq). Muuaji huyo alipoletwa mbele yake, huruma za sahaba huyu wa Mtume(s.a.w.w)
zilimjia na akawaambia wanawe, "Huyu ni mateka wenu. Wala msimtaabishe. Mpeni chakula kile kile mnachokula ninyi wenyewe. Nikipona nitaweza kumuadhibu au kumsamehe lakini kama nikifa, na ikiwa mnataka kumwadhibu basi mpigeni dharuba moja tu kwa sababu yeye alinipa dharuba moja tu. Msimkatekate viungo vyake kwani kufanya hivyo ni kinyume na mafundisho ya Uislamu. Sumu kali ilifanya kazi yake na mnamo tarehe 21 mwezi wa Ramadhani, Hadhrat Ali
alifariki dunia. Wanawe Hasan na Husain (Amani ya Mwenyezi Mungu na iwe juu yao wote) walimfanyia ibada za maziko na lile ua la utu lililazwa kwenye mapumziko yake ya milele katika ardhi ya Najaf, nchini Iraq.
Baadhi ya Hadithi za Hadhrat Ali
: Hizi zifuatazo hapa chini ni baadhi tu ya Hadithi (Semi) nyingi za Hadhrat Ali bin Abi Talib
:
1.Ulimwengu unapomsikiliza mtu, humpa mtu huyo wema wa watu wengine, lakini unapompa mtu huyo kisogo unamwondolea mtu huyo wema wake yeye mwenyewe
.
2.Muadhibu ndugu yako (kwa makosa yake) kwa wema na mlipe madhara yake kwa ukarimu (wako)
.
3.Ye yote yule ajiwekaye katika hali ipasiwayo na masengenyo, asimlaumu mtu ye yote ajengaye wazo baya juu yake.
4.Wapende watoto wa watu wengine na utawatengenezea watoto wako maisha yao ya baadaye.
5.Dhambi mbaya sana ni ile inayodharauliwa na mtenda dhambi.
6.Kuridhika ni hazina isiyofilisika.
7.Jinsi mtu azidivyo kuwa mwenye hekima, ndio jinsi apunguzavyo mazungumzo yake.
8.Yule mwenye uwezo mkubwa wa kuadhibu huwa mvumilivu zaidi.
9.Cho chote kile mtu akifichacho hufichuliwa katika midomo ya ulimi wake na hall ya uso wake.
10.Watu wengi wenye elimu wanapata matatizo kwa ajili ya ujinga wao, na elimu yao hubakia bila faida yo yote.
11.Kufaulu hakumshindi mwenye subira ingawaje kuje baadaye kabisa.
12.Ng'oa uovu kutoka katika nyoyo za wengine kwa kuung'oa kutoka katika moyo wako wewe mwenyewe.
13.Kama mtu ana wazo zuri kuhusu wewe, basi thibitisha kuwa unastahili kufikiriwa hivyo.
14.Majivuno ni moja ya maadui wa busara.
15.Siri ya uongozi ni kuwa na huruma sana.
16.Choyo ni utumwa wa milele.
17.Kama unaogopa kitu fulani cho chote kile, basi kikabili; kwa maana taabu ya hofu yako ni kubwa kuliko ile ya taabu zenyewe.
18.Kama kupotea kwa utajiri wako kunakufanya uwe mwenye busara, basi hiyo si hasara.
19.Thawabu ya kwanza kwa mwenye kuvumilia ni kuwa watu humtetea dhidi ya wakaidi.
Mwenyezi Mungu Anasema:(Ikumbuke) Siku Tutakapowaita kila watu na Imamu wao" (Banii-Israil,
17:710.
HADITH THAQALAINI
MtuIwfu Mtume alihutubia akisema: "(Enyi Waislamu!) Nimeitwa na Mola wangu na nimeitika amri yake (Yaani hivi karibuni nitafariki)". "Ninakuachieni miongoni mwenu Vitu viwili vyenye thamani zaidi (Thaqalain). Kimoja miongoni mwao ni kikubwa kuliko kingine –
(1) Kitabu cha Allah, ambacho ni kamba ya Allah illyotanda kutoka mbinguni hadi nchini, na kingine ni
(2) Dhuria wangu, ambao ni Ahlul-Bait wangu. Vitu hivi havitatengana hadi vitakaponijia vyote kwa pamoja kwenye Hodhi ya kawthar (huko Peponi) Kisha akamwinua Bwana 'Ali bin Abi Talib
na akasema: "Ye yote yule ambae mimi ni Bwana wake, basi huyu 'Ali nae yu Bwana wake
". (Sahih ya Tirm idhii, Khasais cha Imamu Nasai, Kanzul Ummal cha Sheikh Ali Muttaqi n.k.).
SHARTI YA KUCHAPA
Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein
Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini
ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.
MWISHO WA KITABU