UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI13%

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Vitabu mbali mbali

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI
  • Anza
  • Iliyopita
  • 24 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 52164 / Pakua: 5895
Kiwango Kiwango Kiwango
UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi:
Swahili

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

KIMEANDIKWA NA SHEIKH JA'FAR SUBHANI

KIMETAFSIRIWA NA MUSABBAH SHAABANI MAPINDA

KIMETOLEWA NA AHLUL BAYT ASSEMBLY OF TANZANIA

Dar es Salaam - Tanzania

MUHTASARI

Afrika ya Mashariki imefaidi mazingira ya amani sana kiasi cha karne mbili zilizopita. Watu wa imani na itikadi zote waliishi pamoja kwa upendo na mapenzi. Kila mmoja akishiriki kwenye shughuli za mwenzake za kijamii na za Kidini. Ukiangalia kwenye Jumuiya za Kiislamu, wote wakihudhuria kwenye Misikiti ya kila mmoja, waliungana pamoja katika Maulidi na hafla za Muharram, na kupanua ushirikiano wao katika miradi ya kila mmoja. Kama Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi alivyosema katika hotuba moja ya hadhara; "Misikiti mingi ya Waislamu wa (Madhehebu ya) Shafi'i iliyoko Zanzibar na Pemba ilijengwa na kutolewa na Shia Ithna-ashariyya" Hatimaye Wahhabi walianza Tabligh (Mahubiri) yao hapa. Badala ya kujaribu kuwaleta mapagani au wasio waislamu kwenye boma ya Uislamu, nia yao kabisa ilikuwa na bado inakaziwa katika kuwabadilisha Mashafii wawe Mawahabi. Kwa lengo hili, hujifanya kama wao ni Masunni, na kuchanganyika pamoja na Masunni. Mawahabi hao wamepanda mbegu ya fitina na chuki kati ya Madhehebu mbali mbali za Kiislamu, na hususan kati ya Sunni na Shia. Wanazungumza dhidi ya Shia, na kusambaza vitabu na vijitabu (vya mambo ya dini) dhidi ya itikadi ya Shia ambavyo vimejaa mambo ya uwongo na uzushi. Kishawishi chao kiko wazi, kwa kuwatenganisha Masunni na Mashia, wakitumaini kupata urahisi wa kuingia katika jamii ya Sunni na Misikiti yao, ingawaje tumaini hili lingali bado kukamilishwa katika Tanzania.

Hebu tuangalie katika mzizi wa uovu wa kampeni hii. Huenda hapo nyuma katika mwaka 1979, ambapo Mapinduzi ya Ki-Islamu yalipotokea katika nchi ya Iran, na watawala wa Kiwahaabi wa Saudia walihadharishwa vikali mno, hata kabla ya tukio la Mapinduzi ya Kiislamu, wakati Ayatullah al-'uzma al-Khomeini (r.a.) akiwa bado Najaf (Iraq). Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Saudi Arabia, akizungumza katika hadhara moja ya Waarabu, aliuonya ulimwengu wa Waarabu kwamba kama Khomeini ataruhusiwa kuendeleza harakati zake kutoka Iraq kama hapo nyuma, sio tu kwamba utawala wa Shaha utaangushwa, lakini, hali katika eneo lote vile vile itakuwa imetibuliwa. Hivyo wakaishinikiza Iraq kuweka vikwazo juu ya Khomeini kwa hofu ya kwamba, kama juhudi zake zitafanikiwa katika Iran, zitatingisha tawala zao wenyewe zisizo imara. Haikushangaza kwamba mara tu Mapinduzi ya Kiislamu yalipoimarika nchini Iran, hawa Wahhabi wakuanza propoganda kali yenye chuki dhidi ya Khomeini, dhidi ya Iran na dhidi ya Ushia. Kalamu za kukodisha zikuanza mchakato kutoa vitabu, makala na vijitabu (vya mambo ya dini) dhidi ya Shia. Shia waliitwa Makafiri, na pengine mtu angeuliza: Kama ni Makafiri, basi kwa nini wanapewa viza kwa ajili ya Hija na Umra? Wairani waliitwa Majus (Waabudu Moto) kwa nini? Kwa sababu kabla ya kuja kwa Uislamu waliabudu moto. Kwa hoja hii nasi hatuna haki ya kuwaita Wahhabi Mushrikuna? Kwa sababu kabla ya kuja kwa Uislamu wata wa Najd walikuwa wakiabudu Masanamu.

Baadhi ya waajiriwa wao wa ngazi za juu walikuwa ni (marehemu) Ihsan Ilahi Zaheer wa Pakistan, na Manzoor Ahmad Nu'mani na Abul Hasan Ali Nadwi wa India. Sauti itokayo kwenye vinywa vyao ni katika watakiwayo na mabwana zao kuyasema, na jambia la uzayuni lilichovywa kwenye damu ya waislamu linatumika kama kalamu yao. Kitabu kinachoandikwa dhidi ya Shia na watumwa hawa, kwa miezi michache tu kinatarujumiwa katika lugha zote kubwa za ulimwengu wa Kiislamu; na hufanywa kipatikane kila mahali, kadhalika husambazwa bure miongoni mwa Mahujaji: Nimeandika majibu kwa kitabu kimoja kama hicho, ambacho kilichapishwa katika mwaka 1994 nchini Tanzania na Marekani kwa jina la "Wahhabi's Fitna Exposed". Kimevunja habari za uwongo wao wote na masingizio yasiyo na msingi dhidi ya Shia. Tarjuma yake ya Kiswahili (Fitina za Wahhabi Zafichuliwa) imechapishwa na Bilal Muslim Mission of Tanzania, Dar es Salaam.

Bado inahisiwa haja ya kuweko kitabu katika sehemu hizi za ulimwengu ambacho kitaangalia katika mawazo yote na mafundisho ya Uwahhabi na kushughulika nayo katika mwanga wa Qur'an na Hadithi, ili kufichua uwongo na itikadi yao na mtizamo wao juu ya vita vitakatifu vya Kiislamu. Ahlul-Bayt(a.s) Assembly of Tanzania, ina furaha kutoa kitabu kama hiki kwa wata wazungumzao Kiswahili. Nimechagua kwa ajili ya madhumuni haya kitabu (kitwacho) "Al-Wahhabiyah Fil-Mizan" kilichoandikwa na Mwanachuoni mashuhuri wa dini na mtunzi, aitwaye Shaykh Ja'far Subhani, Profesa wa Chuo cha dini Qum (Iran). Kitabu hiki kwa hakika (bila kupendelea) kinaangalia katika hoja zote zilizotolewa na Wahhabi na kutahini kusihi kwake kutoka kwenye Qur'an na Sunnah.

Shaykh Musabbah Shaabani Mapinda, wa Dar-es-Salaam kwa ushauri wangu amefanya tarjuma ya kitabu hiki kutoka Kiarabu kwenda kwenye Kiswahili, kinachoitwa "Uchunguzi juu ya Uwahhabi". Nimekikagua kwa utaratibu ili kuhakikisha kwamba mafuhumu ya Kiarabu kwa uaminifu na ukweli yametolewa kwenda kwenye Kiswahili. Hiki ni kitabu cha kwanza cha "Ahlul-Bayt(a.s) Assembly of Tanzania", na nina fahari kwa kushirikishwa katika kila hatua. Namuomba Allah Subhanahu Wa Ta'ala atoe malipo yake kwa Mtunzi, mtarjumi na wale wote ambao wamesaidia katika kuchapishwa kwake kwa njia yoyote ile. Wa Ma Tawfeeq Illa Billah

Syed Saeed Akhtar Rizvi

Mwenyekiti,

Ahlul-Bayt (A.S.) Assembly

P.O. Box 75215,

Dar- es- Salaam, Tanzania

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UTANGULIZI WA CHAPA YA KWANZA

KUHUSU MAWAHABI NA ITIKADI ZAO

Shukurani zote Anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye ni Mtangu na hapana kitu kilichokuwepo kabla yake, naye ndiye wa mwisho hapana baada yake chochote. Na yeye ni dhahiri hapana kilicho dhahiri kuliko yeye, naye ni batin hapana kilicho Batin kuliko yeye. Na Sala na Salamu zimshukie Mtume wake na mbora wa viumbe wake ambaye alimtuma katika kipindi ambacho watu walikuwa ndani ya upotevu wakihangaika na wamezama ndani ya Fitna, na wametekwa na matamanio yao na wamepotoshwa na ujeuri na akili zao zimepotoshwa na Ujahili uliopita kiasi, wakihangaika katika mambo yaliyovurugika na balaa linalotokana na ujinga, basi Mtume[s .a.w.w ] akatoa nasaha kwa upeo, akaitengeneza njia na akalingania kwa hekima na mawaidha mazuri.

Mwenyezi Mungu alimtuma kuitimiza ahadi yake na kukamilisha Utume wake. Alichukua ahadi yake toka kwa Manabii na alama zilikuwa Mashuhuri na mazazi yake yalikuwa matukufu hali ya kuwa walimwengu katika zama hizo wakiwa na mila tofauti tofauti, na fikra mbali mbali na ni vikundi vingi wakiwemo wanaomshabihisha Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake au walikuwa wakifanya kufuru na shiriki katika jina lake au wakimuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Basi Mwenyezi Mungu akawaongoa kupitia kwa Mtume[s.a.w.w] kutoka kwenye upotovu na akawaokoa kutokana na ujinga kwa njia yake na ni nguzo ya dini yake. Na Rehma za (Mwenyezi Mungu) zimshukie Mtume na kizazi chake (watu) ambao ndiyo wa ndani wake na ni tegemeo la dini yake na ni chombo cha elimu yake, na ni rejea ya hekima zake na ni hazina ya vitabu vyake.

Kwao wao Mwenyezi Mungu aliimarisha dini yake, na ni watu ambao Mwenyezi Mungu amewaondoshea uchafu na kuwatakasa mno. Na (Pia) ziwashukie Masahaba wake ambao waliisoma Qur'an na wakazitumia hukmu zake na wakazizingatia faradhi kisha wakazisimamisha. Waliihuyisha Sunna na kuuwa Bid'a, walilinganiwa kwenye jihadi wakaitika, na walimuamini kiongozi wao (ambaye ni Mtume[s.a.w.w] , kisha wakamfuata. Wamekutana na Mwenyezi Mungu na akawalipa ujira wao, na amewapa makazi ya amani baada ya khofu waliyokuwa nayo, waliendelea katika njia ya Dini na wakaifuata haki, Rehma ziwashukie daima milele muda wote wa kudumu mbingu na ardhi. Amma baad, bila shaka umma wa Kiislamu tangu mwanzoni umeshikamana juu ya Tauhudi katika nyanja zake mbali mbali, ukaafikiana juu ya kuipwekesha dhati ya Mwenyezi Mungu na kwamba, yeye ni mmoja hana mshirika wake na ni mpweke hana mfano. Kama ambavyo umeafikiana ya kwamba, yeye ni uumba na hapana muumba asiyekuwa yeye. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Je, kuna muumba asiyekuwa Mwenyezi Mungu " Qur'an, 35:3.

Na Amesema tena: "Waambie, Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa kila kitu " Qur'an, 13:16.

Vile vile umekubaliana juu ya Tauhidi yake katika Rububiya yake na kwamba hapana Mola wala mwenye kusimamiya (mambo yao) asiyekuwa yeye. Amesema Mwenyezi Mungu: Yeye ndiye anayesimamia mambo yote hakuna muombezi ila baada ya idnini yake, huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu basi muabuduni yeye, Je, hamna kumbukumbu? Pia wamekubaliana kempwekesha Mwenyezi Mungu katika Ibada na kwamba, yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mola ambaye anastahiki kuabudiwa na hukuna wa kuabudiwa asiyekuwa Yeye. Mwenyezi Mungu Amesema:

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٦٤﴾

"Waambie, Enyi mliopewa Kitabu, njooni kwenye neno lililo sawa kati yetu na ninyi ya kwamba, tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, na wala tusimshirikishe na chochote, wala baadhi yeta tusiwafanye kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu". Qur 'an, 3:64.

Bali hizi ndizo nukta ambazo zenye kuafikiana baina ya sheria zote za mbinguni, na yote haya yanaonekana kuwa ni miongoni mwa mambo ya kipekee kwa baadhi ya wafuasi wa sheria zilizopita. Basi mtazamo uliyo kinyume na misingi hii ni miongoni mwa vitendo vya uchafuzi na kupotosha vinavyotokana na wanachuoni, Watawa na Makasisi (wao).

MAWAHABI NA MSIMAMO WAO KWA UNDANI KATIKA QADHIYYAH ZA TAUHID

Cha ajabu, (na midhali uhai utona maajabu zaidi) in kwamba, Uwahabi unatokana na fikia ya Sheikh mpotofu aitwaye Ibn Taimiyyah ambaye ametuarifisha maana ya Tauhidi katika kitabu chake aliposema: "Hakika Mwenyezi Mungu yuko juu ya mbingu yake kwenye arshi yake, yuko juu ya viumbe wake".[1] Na amesema tena: "Mola wete hushuka mpaka kwenye mbingu ya dunia kila siku inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku kisha husema; Nani ataniomba (saa hizi) nami nitamkubalia (maombi yake) nani ataniomba nami nitampa, ni nani atanitaka msamaha nami nitamsamehe".[2] Haya ndiyo maarifa ya mtu huyo (Ibn Taimiyyah) na huku ndiko kumtakasa kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu na (yote haya aliyoyasema) inajulisha wazi kabisa kuwa yeye anaitakidi kuwa Mwenyezi Mungu anao mwili na anapatikana upande fulani. Na (huyu Ibn Taimiyyah) amesema hayo kutokana na kung'ang'ania kwake dhahiri ya aya na hadithi za Mtume bila ya kuzitafiti kwa undani aya zilizokuja kuhusu maudhui hiyo, na bila ya kufanya uhakiki katika isnadi za hadithi na madhumuni yake.

Basi iwapo haya ndiyo maoni ya mwalimu (wa Mawahabi) basi itakuwaje hali ya watu wanaoramba vikombe vyake na wanakaa katika meza zake kama kina Ibn Al-Qayyim na Muhammad bin Abdul-Wahhab. Na cha ajabu ni kwamba, hawa nao wanataka wawe ni waalimu wa Tauhidi na walinganiaji wa Tauhid. Na Mwenyezi Mungu amrehemu mshairi aliyesema: "Katika maajabu ya duniani ni kwamba, mwenye ugonjwa wa manjano anadai kuwa ni mganga na mwenye macho mabovu awe mwenye kutengeneza dawa ya macho na kipofu awe mnajimu, na msomaji wetu wa Qur'an awe Mturuki na Khatibu wetu awe Muhindi, basi njooni tulie na tupige vifuajuu ya Uislamu, (Tuulilie kwa msiba uliyoufika). Hii ndiyo itikadi ya jamaa hawa kuhusu Mwenyezi Mungu, basi iwapo tutataka kuzipima fikra hizi, basi tunawajibika kulinganisha kati ya maelezo hayo na yale yaliyopokelewa kutoka kwa Maimamu wa nyumba ya Mtume[s.a.w.w] kuhusu makusudio hayo (ya Tauhid), kisha tuone ni lipi kati ya makundi haya mawili lenye haki ya kufuatwa.

Je, ni yule amsifuye Mwenyezi Mungu kwamba, yeye ana mwili na anakaa upande fulani na kuteremka mpaka mbingu ya dunia, (ndiye wa kufuatwa) au yule amsifuye Mwenyezi Mungu kwa kusema: "Shukurani zote anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye hawafikii kikamilifu sifa zake wenye kuzisema, wala hawazidhibiti neema zake wenye kuhesabu, na wala hawatekelezi ipasavyo haki yake wenye kujitahidi, Mwenyezi Mungu ambaye fikra hazimfikii hate ziende umbali kiasi gani, wala akili hazimfikii japo ziende ndani kiasi gani, ambaye sifa zake hazina mpaka, wala hakuna maneno yatakayoeleza sifa zake kikamilifu. Na yeye hana wakati uliohesabiwa wala muda uliopangwa, mwenye kumsifu Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa fikra zake atakuwa kamfanyia mwenza, na mwenye kumfanyia mwenza atakuwa kanifanya wawili na mwenye kumfanya wawili basi atakuwa kamgawa. Na mwenye kumgawa hakumjua, na asiyemjua atamuashiria na mwenye kumuashiria atakuwa kamuwekea mipaka, na mwenye kumuwekea mipaka atakuwa kamfanya kuwa zaidi ya mmoja, na atakayeuliza yuko katika kitu gani, basi yeye atakuwa kamuweka ndani ya kitu, na atakayemuuliza kuwa yuko juu ya kitu gani, basi yeye atapafanya mahala pengine pote kuwa Mwenyezi Mungu hayupo. Yeye yupo lakini si kwamba hapo kabla hakuwepo. Yupo pamoja na kila kitu, lakini si kwa kuambatana naye yu mbali na kila kitu lakini si kwa kuondoka.[3]

(Ndugu msomaji), utakapolinganisha yale yaliyonakiliwa kutoka kwa As-Habul-Hadithi kuhusu Tauhidi ya Mwenyezi Mungu na kumtakasa kwake utastaajabu, kwani Imam Al-Ash-Ari amenakili toka kwao kwamba, maana ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika kuomba ni kuwa: Maovu ya waja anayaumba Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa matendo ya waja anayeyaumba ni Mwenyezi Mungu na waja hawawezi kufanya chochote.[4] Bila shaka ibn Taimiyyah na wale walioko kama yeye wanajisifu wenyewe kuwa ni Ahlul-hadithi na wanaitafsiri Tauhidi inayohusu kuumba kwa maana hii. Basi Je, baada ya hali hii itawezekanaje kwao (kina ibn Taimiyyah) kumtakasa Mwenyezi Mungu kutokana na dhulma na ujeuri na kuvuka mipaka. Basi iwapo Mwenyezi Mungu ndiye anayeumba maovu ya waja, na waja hao wakawa hawana walichokifanya katika maovu hayo, si kwa uwezo wao wala kwa kuiga basi ni kwa nini Mwenyezi Mungu awaadhibu? Je, hali hii siyo miongoni mwa kauli za msemaji fulani aliposema: "Amefanya makosa mwingine nami ninaadhbiwa."

Nawe unatambua kwamba Tauhid inayohusu kuumba haimaanishi kama walivyoileza Ahlul-Hadithi, na kabla na baada yao (waliyasema kama hayo) Jabriyyah na ibn Taimiyyah na wafuasi wake. Bali maana yake ni kwamba: Muumba mwenye kujitosheleza na mtendaji asiyehitaji kitu chochote ni yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu. Lakini wako watendaji wanaotenda kwa idhini yake na wanaumba kwa amri yake na husimama na kukaa kwa uwezo wake na nguvu zake, hivyo basi mtu analo jukumu lake kutokana na matendo yake na kazi zake: "Kila nafsi itafungika kwa yale iliyoyatenda ". Qur'an, 74:38.

WANACHUONI WA KIWAHABI WANAJIPENDEKEZA KWA WATAWALA

Tunaona kwamba wanachuoni wa Kiwahabi nchini Saudia na sehemu zingine wanajipendekeza kwa watawala na Makhalifa wajeuri, wanajaribu kuyatakasa matendo ya dhulma ya watawala hao na msimamo wao wakijeuri, na wanajitahidi kutoa kibali cha kisheria kwa kila kinachotokana na watawala wao na wenye mamlaka juu yao (mtawala huyo) awe mwema au muovu. Na hilo siyo jambo la ajabu (kwao) kwani wao (Mawahabi) ndiyo wanaoona kuwa kusali nyuma ya kila Imam mwema au muovu sala inasihi, na kuwaombea wema viongozi wa Waislamu ni faradhi, na kuwapinga wanapopotoka ni haramu.[5] Wanaichukuliaje kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu [s.w.t] kama alivyoinakili toka kwake mjukuu wake Husein bin Ali[a.s] "Abu-Shuhadaa" pale aliposema: "Enyi watu, hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu [s.w.t] amesema; mtu yeyote atakayemuona mtawala muovu anayehalalisha haramu ya Mwenyezi Mungu, mwenye kutengua ahadi ya Mwenyezi Mungu, mwenye kwenda kinyume cha Sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, anawatendea uovu na uadui waja wa Mwenyezi Mungu, kisha mtu huyo akaacha kumkataza kwa kitendo au kauli, basi Mwenyezi Mungu atakuwa na haki ya kumuingiza motoni mtu huyo." [6] [6] Hebu niambie kweli, ni ipi baina ya kauli mbili na ni ipi baina ya njia mbili inayotokana na Uislamu halisi na inaonyesha picha ya nadharia ya Uislamu halisi?

Mwenyezi Mungu amesema: "Wala msiwategemee (mkawa pamoja nao) wale wanaodhulumu usije kukupateni moto ." Qur'an, 11:113.

MAPINDUZI YA KIISLAMU NA HUJUMA ZA KIWAHABI

Kwa hakika Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yameleta mshituko mkubwa katika ghuba, na kuzisononesha tawala zote zilizoko sehemu hiyo na hasa hasa zile zinazohusiana na mataifa makubwa na kuyategemea kwa kila hali, na kwa upande mwingine madola hayo ya kikoloni yanazitegemea nchi hizo na miongoni mwa tawala hizi ni ule utawala wa Kiwahabi unaotawala nchi kubwa miongoni mwa nchi za Kiislamu, nchi ambayo inasifika kwa utajiri mkubwa wa asili na inufaika kwa hali maalum ya kijiografia. Basi ukoloni mbaya na vibaraka wake na watendaji wake wakiongozwa na waliaganiaji wa Kiwahabi wamekusudia kupinga mapinduzi ya Kiislamu na kimbunga chake kwa njia mbali mbali, miongoni mwa upinzani huo ni kuzusha wasi wasi ndani yake na kuwasha mioto ya vita dhidi yake na kulazimisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya mapinduzi hayo. Na njama zote hizi za upinzani dhidi ya mapinduzi ziliposhindwa, wakakusudia kuleta picha mbaya ya utamaduni wa mapinduzi an kuondosha Mafhumu yake na kuuzushia uongo na kuupakazia uzushi ili kuwazuia watu kufuata muongozo wake na kumfuata kiongozi wa mapinduzi hayo. Kwa hakika njama hii ya kiadui dhidi ya utamaduni wa mapinduzi ya Kiislamu, inabainika katika mambo yafuatayo:

1. Kueneza matangazo na magazeti aina nyingi katika nchi mbali mbali za ulimwengu ili kuzungumzia dhidi ya mapinduzi na kufanya ushawishi dhidi yake na kuonyesha sura mbaya ya utamaduni wake halisi.

2. Kuchapisha vijitabu na vitabu vingi mno kuhusu utamaduni huo kwa kupitia mikono ya watu na waandishi ambao wameuza nafsi zao na hawajali isipokuwa mlo wao na pengine vyeo vyao vya kidunia, wakiongozwa na yule muongo mkubwa ih-Sa'an ilahi dhahiri[7] ambaye ni miongoni mwa watu wanaopata mali nyingi kutoka Saudia. Mtu huyu amesimama kidete kwa nguvu zake zote na kwa kila kile ambacho Suudia inakitoa ili kutoa picha mbaya ya taaluma ya mapinduzi miongoni mwa Waislamu.

Na huyu Bwana ni masikini kwa kila kitu hata katika madai yake kuwa anayafahamu madhhebu ya Shia Imamiyyah, basi anachanganya na kuvuruga na wala hapambanui baina ya Asili na Far-i. Wala baina ya Aqida na Riwaya, na anatoa ushahidi kwa kutumia riwaya kuwa eti ndiyo madhhebu ya Shia (yalivyo). Yapo mengi zaidi ya hayo, katika uongo wake na uzushi wake na natija mbovu atoazo, hivyo basi sisi tutahusika naye mahala pengine ndani ya kitabu pekee.

3. Kuyaeneza Madhhebu ya Kiwahabi miongoni mwa vijana katika Eneo hilo kwa njia mbali mbali huku wakibainisha wazi kuwa Mawahabi ndiyo Waislamu na kwamba wao ndiyo wanaompwekesha Mwenyezi Mungu na ndiyo wanaoitumia Qur'an na sunna kwa usahihi, na wasiyokuwa wao wako mbali mno na hayo. Basi kwa ajili hiyo tumeweka risala hiyo kuyabainisha madhhebu ya Kiwahabi, na kuweka bayana ndani yake upeo wa yale wayasemayo Mawahabi na upeo wa kuwa kwao mbali na Qur'an na Sunna na sera ya Waislamu.

Mwisho, tunatoa ushauri kwa wanachuoni wa Kiislamu walioko ulimwenguni kwanza, na pili kwa waandishi wa Kiwahabi, wasimamie kuitisha mkutano wa Ulimwengu wa Kiislamu, mkutano ambao utawakusanya wanachuoni wa Kiislamu kutoka vikundi vyote vya Kiislamu ili kuyachambua Mas-ala haya kwa mujibu wa Qur'an na Sunna na kuyasambaza matokeo ya mkutano huo kwa Waislamu wote ili haki iwabainikie kwa uwazi na ifuatwe, na iliyo haki ndiyo yenye haki mno kufuatwa, na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuwafikisha na ndiye msaidizi. Jaafar Subhani

Qum Takatifu

1/Mfunguo Tano/1405

3

TAFSIRI YA SUURAT YUUNUS

SURAT YUNUS 19-23

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Warahmatullahi Wabarakaatuh. Karibuni katika mfululizo mwingine wa Darsa ya Qur'an.

AYA YA 19

Hii ni darsa ya 310, na tukiwa tunaendelea kuizungumzia sura ya 10 ya Yunus, tunaianza darsa yetu kwa aya ya 19 ambayo inasema:

وَمَا كَانَ النَّاسُ إِلَّا أُمَّةً وَاحِدَةً فَاخْتَلَفُوا وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ فِيمَا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿١٩﴾

19. Wala watu hawakuwa ila umma mmoja tu. Kisha wakakhitalifiana. Na lau kuwa si neno lililo kwisha tangulia kutoka kwa Mola wako, bila shaka hukumu ingelikwisha katwa baina yao katika hayo wanayo khitalifiana.

Mwenyezi Mungu sw amewaumba wanaadamu wote wakiwa na fitra yaani maumbile safi ya tauhidi ya kukubali kuwepo kwa Mungu mmoja.

Hivyo hapo awali wanaadamu wote walikuwa ni sawa na umma mmoja. Lakini kwa kupita muda, na kuzainiwa na shetani kundi miongoni mwa watu wakatumbukia kwenye upotofu wa shirki na hivyo watu wakagawika katika makundi mawili ya wampwekeshao Allah na Mushrikina. Ama Mwenyezi Mungu hakutaka kuwateza nguvu waja wake, bali alitaka kila mtu achague kwa hiyari yake njia anayoamua kufuata. Na ni kwa sababu hiyo ndipo akaamua kuwapa fursa na muhula wale waliokhitari upotofu kufanya lolote lile watakalo.

Na lau si utaratibu huo aliouweka Mwenyezi Mungu basi angewaadhibu papa hapa duniani na kumaliza hitilafu kati ya waumini na makafiri. Funzo mojawapo tunalopata katika aya hii ni kuwa thamani na utukufu wa mwanadamu unapatikana kwa kule kufanya ayatakayo ikiwa ya thawabu au ya madhambi kwa hiyari yake. Vinginevyo hakuna fakhari yoyote kwa mtu kuamini na kufuata njia ya haki kwa kulazimishwa.

AYA YA 20

Ifuatayo sasa ni aya ya 20 ambayo inasema:

وَيَقُولُونَ لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَقُلْ إِنَّمَا الْغَيْبُ لِلَّـهِ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ ﴿٢٠﴾

20. Na wanasema: Kwa nini hakuteremshiwa kutoka kwa Mola wake miujiza (tunayoitaka)? Sema: Mambo ya ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu.Basi nyinyi ngojeni, na mimi ni pamoja na nanyi katika wanaongoja.

Nabii Muhammad(s.a.w.w) alikuja na miujiza mbali mbali kama walivyokuwa Manabii waliomtangulia. Tabaan muujiza mkuu wa Mtume huyo wa mwisho ni quran tukufu ambao washirikina walishindwa kukabiliana nao hata kwa kuleta walau aya moja mfano wake.

Lakini katika kutafuta visingizio, washirikina hao kila siku walikuwa wakitaka waonyeshwe muujiza mpya ikiwa ni pamoja na kumtaka Bwana Mtume awaletee kila wanachotaka. Ndipo katika kuwajibu Bwana Mtume akawaambia muujiza ni suala lililoko kwenye mamlaka ya Mwenyezi Mungu na wala haliko mikononi mwangu mimi, na ni kila pale anapotaka yeye ndipo muujiza unapoletwa, ama mnachotaka nyinyi si kitu kingine ghairi ya kutafuta visingizio tu.

Ukweli wa haya wapenzi wasomaji unashuhudiwa pia kama tulivyoona katika aya zilizotangulia pale washirikina wa kikureishi walipomtaka Bwana Mtume azibadilishe aya za quran au hata ikiwezekana awaletee qurani nyingine mpya badala ya ile aliyoteremshiwa na Mola wake.

Pamoja na mambo mengine aya hii inatufunza kuwa chanzo na chimbuko la shirki na ukafiri si kutokuwepo muujiza na hoja za kuthibitisha ukweli wa risala ya haki, isipokuwa ni tabia ya ukaidi, inda na inadi mbele ya haki.

AYA YA 21

Tunaiendeleza darsa yetu kwa aya ya 21 ambayo inasema:

وَإِذَا أَذَقْنَا النَّاسَ رَحْمَةً مِّن بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُمْ إِذَا لَهُم مَّكْرٌ فِي آيَاتِنَا قُلِ اللَّـهُ أَسْرَعُ مَكْرًا إِنَّ رُسُلَنَا يَكْتُبُونَ مَا تَمْكُرُونَ ﴿٢١﴾

21. Na tunapowaonjesha watu rehma baada ya shida iliyowapata, mara huanza kutunga hila (za kutaka kupinga) Aya zetu. Sema: Mwenyezi Mungu ni mwepesi zaidi wa kupanga. Hakika wajumbe wetu wanayaandika mnayoyapanga.

Historia inasimulia kuwa ilitokea wakati mmoja mji wa Makka ulikumbwa na ukame mkubwa lakini Mwenyezi Mungu kwa baraka ya kuwepo Nabii Muhammad(s.a.w.w) akateremsha mvua zake za rehma na kuuletea faraja mji huo.

Ama washirikina wao walidai kuwa kunyesha kwa mvua hizo kulitokana na baraka za masanamu yao.

Ndipo aya tuliyoisoma ikashuka na kuwatanabahisha kuwa kama nyinyi ni wenye kutaka hakika ya mambo, basi tambueni kuwa mvua hizo ilikuwa ni muujiza utokao kwa Mwenyezi Mungu. Hata hivyo inadi yenu imekufanyeni muzue hila hizi na zile za kuzinasibisha na masanamu yenu rehma hiyo iliyotoka kwa Mola wenu.

Pamoja na hayo tambueni kuwa malaika wa Mwenyezi Mungu ambao hutumwa kwa watu wanayanakili na kuyarekodi yote yanayotendwa na waja na hivyo mushirikina wajiandae na majibu ya kwenda kumpa Mola wao siku ya kiyama kwa yote wanayoyatenda.

Tabaan katika dunia hii pia Mwenyezi Mungu atawapa jaza ya vitimbi na hila zao, nao katu hawawezi kusimama dhidi ya irada ya Allah s.w.t.

AYA ZA 22 NA 23

Aya za 22 na 23 ndizo zinazotuhitimishia darsa yetu hii. Aya hizo zinasema:

هُوَ الَّذِي يُسَيِّرُكُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ حَتَّىٰ إِذَا كُنتُمْ فِي الْفُلْكِ وَجَرَيْنَ بِهِم بِرِيحٍ طَيِّبَةٍ وَفَرِحُوا بِهَا جَاءَتْهَا رِيحٌ عَاصِفٌ وَجَاءَهُمُ الْمَوْجُ مِن كُلِّ مَكَانٍ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ أُحِيطَ بِهِمْ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ لَئِنْ أَنجَيْتَنَا مِنْ هَـٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ ﴿٢٢﴾

22. Yeye ndiye anayekuendsheni bara na baharini. Hata mnapokuwa majahazini na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri wakaufurahia, mara upepo mkali ukawazukia na yakawajia mawimbi kutoka kila upande na wakaona wameshatingwa, hapo ndipo wanapomwomba Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia utii (wakisema): Ukituokoa na haya bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.

فَلَمَّا أَنجَاهُمْ إِذَا هُمْ يَبْغُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّمَا بَغْيُكُمْ عَلَىٰ أَنفُسِكُم مَّتَاعَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُكُمْ فَنُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٢٣﴾

23. Lakini akishawaokoa mara wanafanya jeuri tena katika ardhi bila ya haki.Enyi watu! Jeuri zenu zitakudhuruni wenyewe. Ni starehe (chache tu) za maisha ya dunia. Kisha marejeo yenu ni kwetu, na hapo tutakuambieni mliyokuwa mkiyatenda.

Bila shaka mngali mnakumbuka wapenzi wasomaji kuwa tulisema mwanzoni mwa darsa yetu hii kuwa Mwenyezi Mungu amewaumba wanaadamu wote katika fitra na maumbile safi ya tauhidi ya laa ilaha illa llah, yaani kukana waungu wengine wote bandia na kuthibitisha hakika ya kuwepo kwa Mola mmoja tu wa haki.

Baada ya kueleza hayo, aya hizi tulizosoma hivi punde zinabainisha kuwa mapumbao haya na yale ya kidunia huwa mithili ya utando unaogubika na kufililiza nuru hiyo ya tauhidi ndani ya nafsi ya mtu na kumfanya mja aghafilike na Mola wake.

Ama pale mtu anapotingwa na kupatwa masaibu yanayomfanya akate tamaa ya kupata nusra kupitia njia yoyote ile hapo ndipo utando ule unapotoweka mithili ya vumbi lililosukumwa na upepo na kuiamsha fitra na maumbile ya tauhidi, na kumshuhudia mja akimlingana na kumwomba kwa ikhlasi na unyenyekevu Mola wake aliyemuumba msaada wa nusra na uokozi.

Lakini kama tulivyowahi kuashiria katika moja ya darsa zilizopita baada ya kupata nusra ya Allah mwanadamu husahau kila kitu mara moja, akighafilika kwamba maisha haya ya dunia ni mafupi na ya kupita tu, na kwamba sisi sote mwisho wetu na marejeo yetu ni kwa Mwenyezi Mungu, na huko kila mmoja atasimamishwa mbele ya mahakama ya uadilifu ili kuwajibika kwa yote aliyoyafanya hapa duniani.

Aya hizi zinatuoenyesha kuwa majanga ya kimaumbile husaidia kuondoa ghururi na kiburi cha mwanadamu na kuamsha hisia za kumtambua na kumnyenyekea Mola wake.

Aidha aya zinatutaka tuelewe kuwa imani ya msimu na ya mazingira fulani haina faida; imani ya kweli ni ya kudumu na ya katika kila hali, awe mtu katika raha na neema au shida na nakama.

Darsa ya 310 inaishia hapa. Tunamwomba Mwenyezi Mungu atujaalie kuwa miongoni mwa wale wanaomwamini na kuikiri tauhidi katika hali zote. Amin. Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

SURAT YUNUS 24-27

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kutuwafikisha kukutana tena katika darsa yetu hii.

AYA YA 24

Sura ya 10 ya Yunus ndiyo tunayoizungumzia kwa sasa, na hii ni darsa ya 311 tunayoianza kwa aya ya 24 ambayo inasema:

إِنَّمَا مَثَلُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ مِمَّا يَأْكُلُ النَّاسُ وَالْأَنْعَامُ حَتَّىٰ إِذَا أَخَذَتِ الْأَرْضُ زُخْرُفَهَا وَازَّيَّنَتْ وَظَنَّ أَهْلُهَا أَنَّهُمْ قَادِرُونَ عَلَيْهَا أَتَاهَا أَمْرُنَا لَيْلًا أَوْ نَهَارًا فَجَعَلْنَاهَا حَصِيدًا كَأَن لَّمْ تَغْنَ بِالْأَمْسِ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٢٤﴾

24. Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama maji tuliyoyateremsha kutoka mawinguni, kisha mimea ya ardhi wanayoila watu na wanyama ikachanganyika nayo (maji hayo, ikastawi). Hata ardhi ilipokamilika uzuri wake na ikapambika, na wenyewe wakadhani wameshaiweza, iliifikia amri yetu usiku au mchana na tukaifanya kama iliyofyekwa, kama kwamba haikuwako jana. Namna hivi tunazipambanua aya (zetu) kwa watu wanaofikiri.

Katika kubainisha baadhi ya masuala, Mwenyezi Mungu ametumia ndani ya quran lugha ya tamthili na tashbihi. Aya tuliyoisoma ni miongoni mwa aya hizo ambayo imelinganisha na kushabihisha hali ya kupita na kumalizika haraka dunia kuwa ni sawa na ardhi iliyonawiri kutokana na kunyeshewa na mvua lakini pale inapokuja kukumbwa na kimbunga au mafuriko tahamaki kila kitu kilichopandwa katika ardhi hiyo kinatoweka kana kwamba havukiwepo hapo kabla.

Aya hii wapenzi wasomaji inatuelimisha kuwa umri wa mwanadamu katika dunia hii ni mfupi mithili ya umri wa mimea na maua hivyo tusihadaike tukadhani kuwa tutabaki milele katika ulimwengu huu.

AYA YA 25

Ifuatayo sasa ni aya ya 25 ambayo inasema:

وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَىٰ دَارِ السَّلَامِ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٢٥﴾

25. Na Mwenyezi Mungu anaita kwendea nyumba ya amani, na humuongoa amtakaye kwenye njia iliyonyooka (maadamu anakubali uwongofu).

Mkabala wa maisha haya ya mafupi na ya kupita ya dunia kuna maisha mengine ya milele ya akhera ambayo Mwenyezi Mungu amewataka waja wake wayapiganie hayo na akawapelekea Mitume pia wa kuongoza watu kuelekea kwenye makazi ya utulivu wa kweli.

Ni wazi kuwa watu wanaoshikamana na kamba ya uongofu ni wale ambao Mwenyezi Mungu amewahisi kuwa wana ustahili wa kufikia makazi hayo na ambao matendo na amali zao hapa duniani hazikuwa sababu ya kujiweka mbali na njia iliyonyooka.

Aya hii inatufunza kuwa raha na uzima wa dunia ni vitu vya kupita tu, kinyume chake raha na uzima wa akhera ni za kudumu na za milele. Funzo jengine tunalolipata katika aya hi ni kuwa njia pekee ya kufikia kwenye utulivu na raha za kweli ni kupiga hatua kuelekea kwenye njia ya iliyonyooka ya Allah, ambayo hapa duniani huupa moyo wa mja utulivu na huko akhera humuongoza kuelekea kwenye pepo ya saada.

AYA YA 26

Tuitegee sikio sasa aya ya 26 ambayo inasema:

لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ قَتَرٌ وَلَا ذِلَّةٌ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٦﴾

26. Wale waliofanya wema watapata (jaza ya) wema (wao) na ziada; Wala vumbi halitawafunika nyuso zao wala madhila. Hao ndio watu wa Peponi; humo watakaa milele.

Baada ya aya iliyotangulia kuashiria juu ya pepo, aya hii inasema Mwenyezi Mungu ameiandaa pepo hiyo kwa wale waja wake waliofanya mema, na kwamba jaza na malipo watakayopata waja hao iwe ni kwa sura ya wingi au ubora, yatakuwa makubwa na bora zaidi kuliko amali walizotenda hapa duniani, .kama ambavyo katika aya nyinginezo Allah s.w.t anasema yeyote atendaye jema moja hupata thawabu na malipo mara kumi ya jema hilo, ambapo kwa upande wa utoaji, malipo ya mja hufikia hata mara mia saba ya kile alichotoa.

Baadhi ya yale tunayojifunza katika aya hii ni kuwa ikiwa Mwenyezi Mungu ametuita tuifuate njia yake ya uongofu kisha akatuonyesha njia ya kuifikia, na kisha akatushajiisha na hata kuwalipa thawabu na malipo bora kabisa wale wanaoifikia njia hiyo, ni kitu gani basi cha kutufanya tuache kuitikia mwito wa Mola wetu na kuwafuata wengine wasiokuwa yeye?

AYA YA 27

Aya inayotuhitimishia darsa yetu ni aya ya 27 na ambayo inasema:

وَالَّذِينَ كَسَبُوا السَّيِّئَاتِ جَزَاءُ سَيِّئَةٍ بِمِثْلِهَا وَتَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ مَّا لَهُم مِّنَ اللَّـهِ مِنْ عَاصِمٍ كَأَنَّمَا أُغْشِيَتْ وُجُوهُهُمْ قِطَعًا مِّنَ اللَّيْلِ مُظْلِمًا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٧﴾

27. Na wale waliochuma maovu, malipo ya uovu ni mfano wake vile vile; na yatawafika madhila. Hawatakuwa na awezaye kuwalinda na (adhabu ya) Mwenyezi Mungu. Zitakuwa nyuso zao kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wa giza. Hao ndio watu wa Motoni; humo watakaa daima.

Wakati ambapo wale waliotenda matendo mazuri watakuwa na mwisho mwema huko akhera, wale waliokhitari kufuata upotofu kwa kumkufuru na kumwasi Mola wao hawatapata jaza nyingine ghairi ya adhabu ya Allah, na wala hawatoweza, wala kupata pa kukimbilia, ambapo ukali wa adhabu watakayopata utazifanya nyuso zao zititie na kupiga weusi.

Tabaan adhabu hiyo italingana kabisa na uzito na kiwango cha madhambi waliyofanya, ama kwa upande wa watenda mema wao watapata fadhila zake Mola za kulipwa malipo ya kheri yaliyo makubwa zaidi ya mema waliyotenda.

Aya hii pamoja na mambo mengine inatuelimisha kuwa Mwenyezi Mungu amewaumba wanaadamu akiwa amewapa uhuru na hiyari ya kuchagua njia ya kufuata. Na ndiyo maana kundi moja linaamua kufuata mema na jengine linakhitari kufuata maovu.

Halikadhalika aya inatufunza kuwa katika mfumo wa malezi wa Uislamu siku zote ushajiishaji kwa kutoa hidaya na zawadi unapewa kipaumbele kuliko utiaji adabu na utoaji adhabu.

Darsa ya 311 inaishia hapa. Tunamwomba Allah ajaalie bora ya amali zetu ziwe ni zile za lahadha ya mwisho ya uhai wetu, na siku bora kwetu iwe ni ile ya kukutana na yeye. Amin

Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

SURAT YUNUS 28-33

Assalaamu Warahmatullahi Wabarakaatuh. Karibuni katika mfululizo mwingine wa Darsa ya Qur'an.

AYA ZA 28 NA 29

Hii ni darsa ya 312, na tukiwa tunaendelea kuizungumzia sura ya 10 ya Yunus, tunaianza darsa yetu kwa aya za 28 na 29 ambazo zinasema:

وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا مَكَانَكُمْ أَنتُمْ وَشُرَكَاؤُكُمْ فَزَيَّلْنَا بَيْنَهُمْ وَقَالَ شُرَكَاؤُهُم مَّا كُنتُمْ إِيَّانَا تَعْبُدُونَ ﴿٢٨﴾

28. Na siku tutakapowakusanya wote, kisha tutawaambia wale walioshirikisha: 'Simameni mahali penu nyinyi na wale mliowafanya washirika wa Mungu.' Kisha tutawatenga baina yao. Na hao waliowashirikisha watasema: 'Nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi.

فَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ إِن كُنَّا عَنْ عِبَادَتِكُمْ لَغَافِلِينَ ﴿٢٩﴾

29. Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yetu na baina yenu. Hakika sisi tulikuwa hatuna habari ya ibada yenu.

Aya hizi zinabainisha jinsi hali itakavyokuwa siku ya Kiyama, ambapo Mwenyezi Mungu atawasimamisha mushirikina na wale waliokuwa wakiwaabudu na kuliuliza kila kundi peke yake; kwa nini nyinyi mlikuwa mkiyaabudu masanamu na miungu wa kubuni? Na nyinyi pia ilikuwaje mkaridhia kuabudiwa na watu hawa? Hapo ile miungu ya masanamu isiyo na uhai itapewa uhai kwa amri ya Mwenyezi Mungu na kuwakana wale waliokuwa wakiwaabudu na kutamka kuwa, "sisi hatukuwa tukijihesabu kuwa washirika wa Mwenyezi Mungu, bali nyinyi mlijitengenezea taswira akilini mwenu, na kuziabudu na sisi kutufanya kama kisingizio tu".

Aya ya 41 ya suratu Sabaa pia imeashiria maudhui hii na kueleza kuwa malaika nao ambao walikuwa wakiabudiwa wanadhihirisha, kuchukizwa kwao na kitendo hicho cha Mushrikina.

Nukta yenye mguso wa aina yake hapa ni kuwa katika aya hizi Allah s.w.t amewataja waabudiwa hao kuwa ni washirika wa Mushrikina kwa maana kwamba, hao hawakuwa waungu wanaoshirikishwa na Mwenyezi Mungu, bali ni washirika wenu nyinyi mushirikina mliojibunia na kujitengenezea wenyewe.

Miongoni mwa yale tunayojifunza katika aya hizi ni kuwa siku ya Kiyama, mbali ya wanaadamu, miungu na waabudiwa bandia yakiwemo masanamu yatapewa uhai ili kutoa ushahidi katika mahakama ya uadilifu dhidi ya mushirikina.

AYA YA 30

Ifuatayo sasa ni aya ya 30 ambayo inasema:

هُنَالِكَ تَبْلُو كُلُّ نَفْسٍ مَّا أَسْلَفَتْ وَرُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٣٠﴾

30. Huko kila mtu atayajua aliyoyatanguliza. Na watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa haki. Na yatawapotea yale waliyokuwa wakiyazua.

Baada ya masanamu na waabudiwa wengine kuwakana mushirkina, hapo makundi mawili hayo yatatenganishwa na mushirikina hawatoweza kuwaomba msaada hao waliokuwa wakiwafanya washirika wa Mwenyezi Mungu hapa duniani, na badala yake watarejea kwa Mola wao wa haki yaani Allah sw na hapo ndipo watapata jaza na malipo ya amali zao.

AYA YA 31

Tunaiendeleza darsa yetu kwa aya ya 31 ambayo inasema:

قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَمَن يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ الْأَمْرَ فَسَيَقُولُونَ اللَّـهُ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٣١﴾

31. Sema: 'Ni nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na katika ardhi. Au ni nani anayemiliki kusikia na kuona? Na ni nani amtoaye mzima katika mfu na kumtoa mfu katika mzima?Na nani anaye yadabiri mambo yote?' Watasema: 'Ni Mwenyezi Mungu.' Basi sema: 'Je Hamuogopi?

Baada ya aya zilizotangulia ambazo zimeonyesha unyonge na udhalili utakaowapata washirikina siku ya Kiyama, Mwenyezi Mungu anamwambia Mtume wake awaulize watu hao kuwa nyinyi ambao mnamkubali Mwenyezi Mungu, na mnajua kuwa ni yeye ndiye anayekuruzukuni, na ni yeye ndiye anayesimamia mambo yenu yote, kwa nini basi badala ya kumwabudu yeye mnayaabudu masanamu na kuyafanya wasita na waunganishi wa mambo yenu kwa Mwenyezi Mungu?

Kama ambavyo katika aya nyingine za quran imeelezwa kuwa mushirikina wa enzi za ujahiliya walikuwa wakikubali kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wao na Muumba wa ulimwengu, ama katika suala la kuendesha mambo, mamlaka hayo yako mikonnoni mwa malaika na vitu vingine vya maumbile, kama kwamba Mwenyezi Mungu ameumba tu kisha akakaa kando na kulikabidhi kwa viumbe hao suala la uendeshaji wa ulimwengu.

Fikra ya aina hii imeelezwa na quran tukufu kuwa ni batili na aina mojawapo ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Funzo mojawapo tunalopata katika aya hii ni kuwa uendeshaji wa ulimwengu unahitajia tadbiri isiyobadilika, na hili halingewezekana kama kungekuwepo na Muumba zaidi ya mmoja.

AYA ZA 32 NA 33

Aya za 32 na 33 ndizo zinazotuhitimishia darsa yetu hii. Aya hizo zinasema:

فَذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمُ الْحَقُّ فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ ﴿٣٢﴾

32. Basi huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu wa haki. Na kipo kitu gani baada ya haki isipokuwa upotofu tu? Basi huwaje mkageuzwa?

كَذَٰلِكَ حَقَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى الَّذِينَ فَسَقُوا أَنَّهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٣٣﴾

33. Hivi ndivyo kauli ya Mola wako itakavyowathubutikia wale walioasi, ya kwamba hawataamini.

Baada ya aya zilizotangulia kubainisha mifano ya ishara za adhama ya Mwenyezi Mungu katika uumbaji wa mbingu na ardhi pamoja na kukiri kwa washirikina kuhusu uumbaji wa Mwenyezi Mungu.

aya hizi zinabainisha wazi kuwa Mungu huyu ndiye Mola wenu, na vile vile ndiye muendeshaji mambo yenu; na si kwamba yeye ni muumba wenu lakini masanamu yakawa ndio waendeshaji wa mambo yenu.

Kisha aya zinaendelea kwa kutoa kauli ya mkato kwamba, hakuna hali ya tatu baada ya haki na batili. Kwa maana kwamba kila kitu ima ni haki au ni batili, na kwa hivyo kwa kuwa Mwenyezi azza wa jal ndiye haki, basi bila shaka masanamu na miungu wenu wengine wa kubuni hawawezi kuwa haki, na hivyo wale watu wanaoamua kuipa mgongo haki kwa inadi, ubishi na ukaidi hawawezi kupata taufiki ya kuufikia uongofu.

Baadhi ya yale tunayojifunza kutokana na aya hizi ni kuwa hakuna njia ya tatu baada ya haki na batili. Na kwa hivyo yanapothibitika mawili hayo, hakuna nafasi ya mtu kudai kuwa yeye hayuko huku wala huku bali ni mtu wa kati na kati.

Kwa haya machache tunaifunga darsa yetu hii. Tunamwomba Allah atuepushe na shirki na kuijenga imani kamili na safi ya tauhidi ndani ya nyoyo zetu. Amin

SURAT YUNUS 34-38

AYA ZA 34 NA 35

Sura ya 10 ya Yunus ndiyo tunayoizungumzia kwa sasa, na hii ni darsa ya 313 tunayoianza kwa aya za 34 na 35 ambazo zinasema:

قُلْ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ قُلِ اللَّـهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٣٤﴾

34. Sema: Je Yupo katika miungu yenu ya ushirikina, aliyeanzisha kuumba viumbe kisha akavirejesha? Sema: Mwenyezi Mungu ameanzisha kuumba viumbe kisha ndiye atakayevirejesha. Huwaje basi mkadanganywa?.

قُلْ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ قُلِ اللَّـهُ يَهْدِي لِلْحَقِّ أَفَمَن يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ أَحَقُّ أَن يُتَّبَعَ أَمَّن لَّا يَهِدِّي إِلَّا أَن يُهْدَىٰ فَمَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ ﴿٣٥﴾

35. Sema: Je Yupo katika miugu yenu ya ushirikina anayeongoa kuendea Haki? Sema: Mwenyezi Mungu anaongoa kwendea Haki. Basi je anayestahiki kufuatwa ni yule Mwenye kuongoa kwendea Haki au asiyeongoa ila aongozwe yeye? Basi nyinyi mna nini? Mnahukumu namna gani?.

Zikiendelea kuzungumzia yale yaliyokuja katika aya zilizotangulia kuhusu kutoa changamoto kwa mushrikina ya kuwaonyesha jinsi miungu yao bandia isivyo na uwezo wa kufanya lolote, aya tulizosoma zinasema, ikiwa mtatupia jicho na kuzingatia uumbaji ulivyo mtabaini kuwa hakuna yeyote ghairi ya Mungu Mmoja awezaye kuumba kila kilichopo na kukipa uhai mpya, na hayo masanamu yenu mnayoyaabudu na viumbe vingine vyote vilivyoko, vyote hivyo vimeumbwa na vinamhitajia Muumbaji, basi yawaje vitu hivyo viweze navyo kuwa waumbaji wa ulimwengu?

Kama nyinyi ni wenye kutafuta uongofu na kutaka kuifikia saada tambueni kuwa miungu wenu hao wenyewe hawana cha kumuongoza mtu hata muweze kupata muongozo wa kufuata kutoka kwao, na kama ni suala la kupata uongofu, inalazimu wao wenyewe kwanza wawe na sifa hiyo ya kuweza kuufikia huo uongofu kisha ndipo waweze kukuonyesheni nyinyi pia njia ya kuufikia. Hali ya kuwa Mwenyezi Mungu ndiye muongozaji wenu wa kukufikisheni kwenye njia iliyonyooka. Tabaan uongofu wa Mwenyezi Mungu unapatikana kupitia Mitume wake na vitabu vya mbinguni walivyokuja navyo ambavyo kila kilichomo ndani yake ni maneno yake Mola Muumba.

Miongoni mwa yale tunayojifunza kutokana na aya hizi ni kuwa kutumia mfumo wa masuali na majibu ni mojawapo ya mbinu bora kwa ajili ya kujadiliana na wapinzani wa kiitikadi na kifikra, mbinu ambayo Allah sw amewafunza Mitume wake. Aidha aya zinatuelimisha kuwa Mwenyezi Mungu si Muumbaji wa ulimwengu tu, bali baada ya kuwaumba viumbe wake hakuwaacha kama walivyo, ila amewaonyesha pia njia yao ya uongofu itakayowafikisha kwenye saada ya duniani na akhera.

AYA YA 36

Ifuatayo sasa ni aya ya 36 ambayo inasema:

وَمَا يَتَّبِعُ أَكْثَرُهُمْ إِلَّا ظَنًّا إِنَّ الظَّنَّ لَا يُغْنِي مِنَ الْحَقِّ شَيْئًا إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِمَا يَفْعَلُونَ ﴿٣٦﴾

36. Na wengi wao hawafuati ila dhana tu. Na dhana haifai kitu mbele ya haki. Hakika Mwenyezi Mungu anajua yote wanayoyatenda.

Aya hii wapenzi wasomaji inaashiria chanzo na chimbuko la upotofu wa kifikra la wale wanaomkanusha na kumkufuru Mwenyezi Mungu na kueleza kuwa kufuata dhana na mambo ya udhanifu yasiyo na msingi ambayo kwa hakika ni njozi za kifikra ndiyo yaliyowafanya watu hao waipe mgongo haki na kung'ang'ania fikra na itikadi batili.

Hali ya kuwa katika masuala ya kifkra na kiitikadi, dhana na mambo ya udhanifu hayana nafasi wala itibari yoyote, na ukweli ni kuwa hakika na yakini ndiyo mambo yanayoweza kumfikisha mtu kwenye haki.

Mbali na hayo chimbuko la itikadi nyingi za zama za ujahilia lilikuwa ni watu kufuata yale waliyowakuta nayo babu zao na kushikilia na kuyanng'ang'ania mambo kwa sababu ya taasubi tu za kikabila, mambo ambayo hayakuwa na thamani wala itibari yoyote ya kielimu na kifikra.

Baadhi ya yale tunayojifunza kutokana na aya hii ni kuwa katika masuala ya kiitikadi na kimaadili wingi hauwi kipimo cha kuonyesha haki. Kwani si hasha walio wengi katika watu wakawa wamepotoka kifikra na kimatendo.

AYA ZA 37 NA 38

Tunaihitimisha darsa yetu ya juma hili kwa aya za 37 na 38 ambazo zinasema:

وَمَا كَانَ هَـٰذَا الْقُرْآنُ أَن يُفْتَرَىٰ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِن تَصْدِيقَ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ الْكِتَابِ لَا رَيْبَ فِيهِ مِن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٣٧﴾

37. Na haiwezekani Qurani hii kuwa imetungwa, na haitoki kwa Mwenyezi Mungu. Bali inayasidikisha yaliyotangulia, na ni mfafanuo wa Kitabu kisicho na shaka ndani yake kutoka kwa Mola wa walimwengu wote.

أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ قُلْ فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّثْلِهِ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٣٨﴾

38. Je! Ndiyo wanasema ameizua? Sema:" Hebu leteni sura moja mfano wake na muwaite (kukusaidieni) muwawezao isipokuwa Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi mnasema kweli.

Quran tukufu imetoa changamoto mara kadhaa ya kuthibitisha kuwa ni maneno ya mbinguni na kuonyesha kwamba si majini wala binaadamu walio na uwezo wa kuleta kitu kilicho mfano wake.

Bali ikafika mbali zaidi na kueleza kwa kujiamini kwamba, si kuleta mfano wa Quran yote au moja ya sura zake tu, bali kama wana uwezo, wapinzani wa muujiza huo wa Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu na walete walau aya moja tu iliyo mfano wa Quran.

Hata hivyo licha ya maadui na wapinzani wengi ambao Uislamu na Quran imekabiliana nao katika kipindi cha karne 14 zilizopita, hadi leo hii hakuna aliyethubutu kujitokeza kukabiliana na changamoto hiyo iliyotolewa na kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.

Magwiji wa kila zama wa nahau na balagha pamoja na fani nyinginezo za lugha ya kiarabu wasio waislamu, wote hao wameshindwa kubuni walau aya moja tu iliyo na sifa za aya ya Quran tukufu.

Wapenzi wasomaji quran tukufu ina miujiza na maajabu ya aina kwa aina, machache kati ya hayo ni haya yafuatayo:

Kwanza : ni utamu wa maneno yake na mvuto wa ajabu yalionao, kiasi kwamba hata kama mtu ataisoma mara elfu hahisi kuwa amesoma kitu cha kushosha na kilichopitwa na wakati. Si hayo tu, bali vibwagizo vya maneno yake, mianguko yake ya sauti na mahadhi yake yamejipambanua na maneno mengine yote ya lugha ya kiarabu.

Ujumuishaji wa quran wa kila kipengele cha maisha ya mwanadamu vikiwemo vya masuala ya mtu binafsi, familia, jamii, masuala ya kisheria, kiuchumi, kisiasa na kiakhalqi ni wa namna ambayo, ni muhali kwa mwanaadamu yeyote kuweza kuufikia upeo wake.

Wapenzi wasomaji darsa ya 313 imefikia tamati. Tunamwomba Mwenyezi Mungu aturuzuku kuisoma quran usiku na mchana, kwa namna airidhiayo yeye, na kutuwafikisha kutekeleza kivitendo yaliyomo ndani yake ili tuweze kupata uombezi wa quran siku ya kiyama. Amin.

SURAT YUNUS 39-44

Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

Karibuni katika mfululizo huu wa 314 wa darsa ya quran, tukiwa tunaendelea kuizungumzia sura ya 10 ya Yunus.

AYA ZA 39 NA 40

Tunaianza darsa yetu kwa aya za 39 na 40 ambazo zinasema:

بَلْ كَذَّبُوا بِمَا لَمْ يُحِيطُوا بِعِلْمِهِ وَلَمَّا يَأْتِهِمْ تَأْوِيلُهُ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الظَّالِمِينَ ﴿٣٩﴾

39. Bali wameyakanusha wasiyoyaelewa ilimu yake kabla hayajawajia maelezo yake. Namna hivi walikanusha waliokuwa kabla yao. Basi angalia jinsi ulivyokuwa mwisho wa madhalimu hao.

وَمِنْهُم مَّن يُؤْمِنُ بِهِ وَمِنْهُم مَّن لَّا يُؤْمِنُ بِهِ وَرَبُّكَ أَعْلَمُ بِالْمُفْسِدِينَ ﴿٤٠﴾

40. Na miongoni mwao wapo wanaoiamini. Na miongoni mwao wapo wasioiamini. Na Mola wako anawajua vyema waharibifu.

Katika darsa iliyopita tulisema kuwa kutokana na dhana tu na bila kuwa na ushahidi mushirikina na makafiri walikuwa walivurumiza tuhuma kuwa Quran ni maneno ya Bwana Mtume na kukanusha kwa kudai kuwa kitabu hicho kitukufu hakina uhusiano wowote na Mwenyezi Mungu.

Aya tulizosoma zinasema kuwa kinachofanywa na makafiri na mushirikina hao ni kukariri yale yaliyosemwa na wenzao waliotangulia, kwani mitume wa kabla ya Nabii Muhammad(s.a.w.w) walikabiliwa na tuhuma sawa na hizo.

Hii ni pamoja na kuwa ukadhibishaji wao hauna mashiko yoyote ya kielimu, hivyo kitendo chao hicho ni sawa na kujidhulumu nafsi zao na pia ni dhulma kwa dini ya haki ya mbinguni na mitume waliotumwa na Allah kuitangaza dini hiyo kwa watu.

Lakini katika upande mwingine, kuna watu wanaoitambua na kuiamini haki, na hivyo, kama tulivyowahi kuashiria mara kadhaa, ndivyo alivyokadiria Allah s.w.t, kwamba: kila mtu kwa hiyari mwenyewe aamue ima kuwa muumini au kafiri. Baadhi ya yale tunayojifunza kutokana na aya hizi ni kuwa chanzo cha ukafiri, ukanushaji na ukadhibishaji haki ni kukosa utambuzi wa kuielewa haki hiyo. Kwani wale wanaokusudia kwa dhati kuitafuta na kutaka kuijua haki hufika mahali wakaitambua risala ya tauhidi waliyokuja nayo Mitume wa Mwenyezi Mungu na wakaiamni.

Aidha aya zinatuelimisha kuwa kuyakanusha na kuyapa mgongo mafundisho ya manabii wa Allah ndiyo chanzo cha dhulma na ufisadi tunaoushuhudia ulimwenguni.

AYA YA 41

Ifuatayo sasa ni aya ya 41 ambayo inasema:

وَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل لِّي عَمَلِي وَلَكُمْ عَمَلُكُمْ أَنتُم بَرِيئُونَ مِمَّا أَعْمَلُ وَأَنَا بَرِيءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٤١﴾

41. Na wakiendelea kukukadhibisha sema: Mimi nina amali yangu na nyinyi mna amali yenu. Nyinyi hamna dhima kwa niyatendayo, wala mimi sina dhima kwa mnayotenda nyinyi.

Aya hii inabainisha jinsi ya kuamiliana na makafiri na wapinzani wa haki na kueleza kuwa jukumu lenu nyinyi kwa watu hao ni kuwaonyesha tu na kuwatambulisha uongofu; si kuwalazimisha wao waufuate kwa nguvu, wala nyinyi kutaka kuwakumbatia wao ili kiwe kishawishi cha kuwafanya wavutiwe na haki.

Ikiwa wao watakuwa wamekaidi na kukataa kata kata kuiamini haki, dhima yenu kwao imeshaondoka, kwani imani ni jambo la moyoni na la hiyari, na hivyo watu hao ni kwamba wameshaamua hawataki kuielewa haki, na kama wameielewa, basi hawataki kuiamini.

Katika suala hili hutokezea baadhi ya Waislamu wakahisi kuwa labda ikiwa wao wenyewe wataamua kuacha kushikamana na baadhi ya mambo ya msingi ya dini huenda hilo linaweza kuwavutia wale wanaowalingania waikubali haki. Hali ya kuwa mtu hana haki yoyote ya kufanya hivyo kwa sababu tu ya kutaka kupata idadi kubwa zaidi ya watu walioukubali uongofu.

Na ndiyo maana tunaona katika aya hizi Bwana Mtume Muhammad saw anatakiwa awaambie makafiri kwamba, madamu nyinyi hamko tayari kuyaamini maneno yangu, tambueni kuwa mimi najiweka mbali kabisa na matendo yenu na wala sina dhima wala jukumu lolote kwenu.

Funzo mojawapo tunalolipata katika aya hii ni kuwa Uislamu ni dini ya hoja, maadili na msimamo. Inatangaza na kuweka wazi msimamo wake; na kama ambavyo haimlazimishi mtu kuifuata, ndivyo vivyo hivyo nayo haiko tayari kulegeza msimamo katika misingi ya mafundisho yake.

AYA ZA 42, 43 NA 44

Darsa ya 314 inahitimishwa na aya za 42, 43 na 44 ambazo zinasema:

وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُونَ إِلَيْكَ أَفَأَنتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ وَلَوْ كَانُوا لَا يَعْقِلُونَ ﴿٤٢﴾

42. Na wako miongoni mwao wanaokusikiliza. Je wewe unaweza kuwafanya viziwi wasikie ijapokuwa hawafahamu?.

وَمِنْهُم مَّن يَنظُرُ إِلَيْكَ أَفَأَنتَ تَهْدِي الْعُمْيَ وَلَوْ كَانُوا لَا يُبْصِرُونَ ﴿٤٣﴾

43. Na wapo miongoni mwao wanaokukodolea macho. Je wewe utawaongoa vipofu ingawa hawaoni?

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ النَّاسَ شَيْئًا وَلَـٰكِنَّ النَّاسَ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٤٤﴾

44. Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu chochote; lakini watu wenyewe wanajidhulumu nafsi zao.

Katika kuendeleza yale yaliyokuja katika aya zilizotangulia kuhusu jinsi wapinzani wa haki walivyokuwa wakiamiliana na Bwana Mtume, aya hizi zinasema, si hasha baadhi ya wapinzani hao wakawa ni watu wanaohudhuria vikao vya Bwana Mtume, wakimwona kwa macho yao mtukufu huyo na kuyasikia yale anayoyasema; lakini yote hayo hayazipi athari yoyote nafsi zao. Na sababu ni kuwa yote hayo waliyokuwa wakiyashuhudia na kuyasikia hayakuwa yakipenya kweli kwenye masikio yao na kukita kwenye fikra na nyoyo zao.

Kana kwamba watu hao walikuwa ni vipofu wasioona au viziwi wasioweza kusikia chochote. Kimsingi ni kwamba kitu kinachompambanua mwanadamu na mnyama ni uwezo wake wa kufikiri na kutafakari, vinginevyo mnyama naye anaona na anasikia, bali hata uwezo na nguvu zake zake za kuona na kusikia ni kubwa zaidi kuliko za binaadamu. Hivyo linalomstahikia mwanadamu ni kuyatia kwenye tafakuri yale ayaonayo na ayasikiayo, kwa kupambanua la haki na la batili, kisha kushikamana na lile la haki na kujiweka mbali na lile la batili. Funzo mojawapo tunalolipata kutokana na aya hizi ni kuwa kuona na kusikia, ni utangulizi wa kutafakari na kuifahamu haki.

Wapenzi wasomaji darsa yetu ya juma hili inaishia hapa. Tunamwomba Allah atuwafikishe kuitambua haki na kuifuata, na kuielewa batili na kuiepuka. Amin.

SURAT YUNUS 45-49

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutuwafikisha kukutana tena katika darsa yetu hii.

AYA YA 45

Sura ya 10 ya Yunus ndiyo tunayoizungumzia kwa sasa, na hii ni darsa ya 315 tunayoianza kwa aya ya 45 ambayo inasema:

وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ كَأَن لَّمْ يَلْبَثُوا إِلَّا سَاعَةً مِّنَ النَّهَارِ يَتَعَارَفُونَ بَيْنَهُمْ قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِلِقَاءِ اللَّـهِ وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿٤٥﴾

45. Na siku atakapowakusanya, itakuwa kama kwamba hawakukaa (duniani) ila saa moja tu ya mchana. Watatambuana. Hakika wamekhasirika wale waliokanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, wala hawakuwa wenye kuongoka.

Ijapokuwa makafiri wamekadhibisha na kukanusha kuwepo kwa siku ya kiyama, hata hivyo watake wasitake ni kwamba wao pia kama ilivyo kwa wanaadamu wote watafufuliwa tu na kuishuhudia siku hiyo.

Uzito wa siku hiyo utakuwa hauna mfano wake kiasi cha kuwafanya wale waliokufuru wahisi kwamba umri wao wote walioishi hapa duniani, pamoja na kipindi chote cha maisha ya barzakh huko makaburini, ulikuwa ni sawa na muda wa saa moja tu ya mchana mzima.

Pamoja na wanaadamu kupitiwa na miaka bali pengine karne nyingi za baada ya kufa kwao, lakini watahisi kana kwamba wameamka tu kutoka kwenye usingizi wa kawaida. Katika hali hiyo watu watatambuana vizuri na wala hawatokumbwa na usahaulifu.

Ni wazi kwamba katika lahadha hiyo wale ambao hapa duniani walikanusha kuwepo kwa kiyama, wakati kweli itakapodhihiri na kujiona wamesimamishwa katika uwanja wa siku ya kiyama, hapo ndipo watakapobaini kuwa wao ni watu waliokhasirika kwa kufika mahala hapo wakiwa mikono mitupu, huku kukiwa hakuna tena fursa ya kurudi walikotoka.

Baadhi ya mafunzo tunayopata kutokana na aya hii ni kuwa umri tunaoishi hapa duniani ni mfupi, kiasi kwamba siku ya kiyama mtu atajuta na kujihisi amekhasirika na kupata hasara kubwa kwa kutoitumia fursa hiyo ya uhai wa kupita aliojaaliwa hapa duniani.

Halikadhalika inatubainikia kutokana na aya hii ni kuwa hasara ya kweli ni ile ya mtu kuhitari na kufadhilisha starehe za kupita za hapa duniani kwa raha na neema za milele za huko akhera.

AYA YA 46

Tunaiendeleza darsa yetu kwa aya ya 46 ambayo inasema:

وَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ الَّذِي نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ اللَّـهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ ﴿٤٦﴾

46. Na vyovyote vile, tukikuonyesha baadhi ya tunayowaahidi au tukakufisha kabla yake, marejeo yao ni kwetu. Kisha Mwenyezi Mungu ni shahidi wa wanayoyafanya.

Aya hii inamliwaza Bwana Mtume na waumini kwa kuwaambia kuwa ikiwa mnaona Mwenyezi Mungu hawashushii adhabu kamili makafiri hapa duniani ni kwa sababu malipo hasa ya waja iwe ni adhabu ya moto au neema ya pepo wataipata huko akhera pale wote watakaporejea kwa Mola wao.

Hata hivyo sio kwamba adhabu ya kila ovu itasubiri huko akhera tu bali baadhi ya adhabu zitawashukia wakanushaji hapo papa hapa duniani, nawe Mtume utashuhudia kwa macho yako; na baadhi ya adhabu zitawashukia hata baada ya wewe kuaga dunia.

Funzo mojawapo tunalopata katika aya hii ni kuwa waislamu wasikate tamaa kuona muda unapita bila makafiri kupatwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu.

Hiyo ni ahadi ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni mtimizaji wa ahadi anayotoa, tabaan kulingana na hikima yake mutlaki.

AYA YA 47

Ifuatayo sasa ni aya ya 47 ambayo inasema:

وَلِكُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولٌ فَإِذَا جَاءَ رَسُولُهُمْ قُضِيَ بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٤٧﴾

47. Na kila umma una Mtume. Alipowajia Mtume wao walihuhukumiwa baina yao kwa uadilifu; wala hawakudhulumiwa.

Mitume wa Mwenyezi Mungu walikuwa katika makundi mawili. Wale waliopewa vitabu na sheria, na wale ambao walikuwa wafikishaji na walinganiaji tu wa risala za Mitume waliopewa vitabu na sheria. Kutokana na aya za quran inabainika kuwa katika kipindi cha historia, na katika umma na kaumu mbali mbali za wanaadamu wamekuwepo watu waliokuwa wakiwafikishia wanadamu wenzao mafundisho ya mitume na yale yaliyokuja katika vitabu vya mbinguni.

Na ujumbe mkuu katika risala za manabii ulikuwa ni kusimamisha haki na uadilifu na kupambana na dhulma na uonevu. Na hivyo siku ya kiyama Allah sw ataawafufua watu wa kila kaumu na umati pamoja na Mtume wao na kuwasimamisha na kuwahukumu kwa uadilifu katika mahakama ya siku hiyo ya malipo.

Funzo mojawapo tunalopata kutokana na aya hii ni kuwa: hakuna uma au kaumu yoyote ambayo Mwenyezi Mungu ameiwacha vivi hivi bila ya kuhakikisha imefikiwa na ujumbe wa mafundisho ya Mitume wake.

AYA ZA 48 NA NA 49

Tunaihitimisha darsa yetu kwa aya za 48 na na 49 ambazo zinasema:

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٨﴾

48. Na wanasema: Ni lini ahadi hii ikiwa mnasema kweli?

قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي ضَرًّا وَلَا نَفْعًا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ لِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ إِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ فَلَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ ﴿٤٩﴾

49. Sema: Sijimilikii nafsi yangu shari wala kheri, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Kila umma una muda wao waliowekewa. Ukifika muda wao hawakawii saa moja wala hawatangulii.

Makafiri ambao waliamua kukanusha hakika ya kuwepo kwa siku ya kiyama waliamua kuzusha visingizio vya kila aina alimradi kuutia shaka uhakika huo.

Hivyo wakaibuka na suali kwamba ikiwa ni kweli kiyama kitatokea na wewe Muhammad unayoyasema ni kweli kuhusu hilo, tuambie basi kujiri kwake kutakuwa lini hasa! Walizusha hoja hiyo ilhali uhakika wa kutokea jambo haushurutishi kujua wakati halisi wa kutokea kwake. Mfano wa hili ni sawa na mauti.

Kila mmoja wetu ana hakika kuwa iko siku ataiaga dunia tu, lakini hakuna yeyote kati yetu ajuaye ni lini hasa atafikwa na mauti. Kwa upande wa Bwana Mtume, naye pia kupitia wahyi alioushushiwa na Mola wake aliwapa khabari watu wa umati wake kwamba baada ya kumalizika dunia itawadia siku ya Kiyama, hata hivyo Allah s.w.t hakumbainishia Mtume wake ni wakati gani hasa litajiri tukio hilo kubwa kabisa la kutikisa nyoyo.

Baadhi ya mafunzo tunayoyapata kutokana na aya hizi ni kuwa Mitume walikuwa ni waja wateule wanaozungumza na watu kwa uwazi na ukweli mtupu; na hivyo wakiwaeleza bayana kuwa binafsi hawana nguvu na uwezo usio wa kawaida wala mamlaka ya kujiamulia kupata manufaa fulani au kujilinda na kujiepusha na shari yoyote ile ila kwa uwezo na idhini ya Allah s.w.t

Wapenzi wasomaji, kwa haya machache tunaifunga darsa hii ya 315. Inshaallah Mwenyezi Mungu atujaalie kuwa miongoni mwa wanaoyakinisha kiimani juu ya kuwepo kwa siku ya kiyama kutokana na amali zao na matendo yao.

Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh

4

5

6

7

8

9

10

11

12

13

14

15

16

17

18

19

20

21

22

23