UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI0%

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Vitabu mbali mbali

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi: SHEIKH JA'AFAR SUBHANY
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 48442
Pakua: 4223

Maelezo zaidi:

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 24 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 48442 / Pakua: 4223
Kiwango Kiwango Kiwango
UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi:
Swahili

12

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

NATIJA YA UTAFITI

Mpaka hapa kwa namna fulani tunaweza kufafanua uhakika wa Ibada na sasa ni lazima tueleze kwa kifupi matokeo ya utafiti huu na tunasema: Lau mtu atawanyenyekea watu wengine bila ya kumzingatia mmoja wapo kuwa ni Mungu au Rabbu au kuwa ni asili inayojitegemea kwa kutenda matendo ya Mwenyezi Mungu, bali amewaheshimu tu kwa kuwa wao ni:

عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ ﴿٢٦﴾ لَا يَسْبِقُونَهُ بِالْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِ يَعْمَلُونَ ﴿٢٧﴾

"Waja waliotukuzwa hawamtangulii Mwenyezi Mungu kwa neno (Lake asemalo) nao wanatenda amri zake" - Qur'an, 21:26.

Basi mtu huyo tendo lake hili la kunyenyekea haliwi ila kuwaheshimu na kuwatukuza, wala hakuna uhusiano wowote wa tendo hili na ibada kamwe. Bila shaka Mwenyezi Mungu amewataja baadhi ya waja wake kwa utajo mwema na amewasifu kwa namna inayoamsha raghba (hamu) ya kila mtu awatukuze na kuwaheshimu. Miongoni mwa utajo huo ni kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema:

إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ آدَمَ وَنُوحًا وَآلَ إِبْرَاهِيمَ وَآلَ عِمْرَانَ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٣٣﴾

"Bila shaka Mwenyezi Mungu alimchagua Adam na Nuh na kizazi cha Ibrahim na kizazi cha lmran juu ya walimwengu wote." Qur'an, 3:33.

Vile vile Qur'an inabainisha kwamba Mwenyezi Mungu alimchagua Nabii Ibrahim kwa ajili ya Uimamu anasema:

قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا ﴿١٢٤﴾

"(Mwenyezi Mungu) akasema bila shaka ninakufanya uwe lmamu kwa ajili ya watu. Qur'an, 2:124

Pia Mwenyezi Mungu katika Qur'an amewataja kwa utajo mwema Manabii Nuh, Ibrahim, Dawood, Seleiman, Musa, Isa na Muhammad, (Rehma za Mwenyezi Mungu ziwashukie wote). Na amewasifu kwa sifa tukufu kiasi kwamba kila sifa moja peke yake inatosha kuuvuta moyo na kuleta mapenzi ndani ya nafsi za watu. Na utaiona Qur'an Tukufu inatangaza ubora wa kizazi cha Mtume Muhammad[s.a.w.w] katika aya nyingi. Miongoni mwa aya hizo ni hizi zifuatazo:

إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا ﴿٣٣﴾

"Bila shaka Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Enyi watu wa nyumba (ya Mtume) na akutakaseni sana sana." Qur'an, 33:33

قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَىٰ ﴿٢٣﴾

"Waambie sikutakeni malipo yoyote juu ya utume wangu isipokuwa muwapende Al-Qurbaa". Qur'an 42:23

Na huwalisha chakula katika mahaba ya Mwenyezi Mungu, masikini, yatima na mateka hali ya kuwa wenyewe wanakipenda (chakula hicho) (nao husema moyoni mwao) tunakulisheni kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu (tu) hatutaki kwenu malipo wala shukurani, hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu hiyo siku yenye shida na taabu, basi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo na kuwakutanisha na neema na furaha na atawalipa mabustani ya pepo na (nguo) za hariri kwa sababu ya kusubiri (kwao)... mpaka mwisho wa Surat hii ya 76.[170] Basi lan watu wangesimama upande wa Mawalii hawa watukufu kwa matendo ambayo yanakubalika ikiwa ni pamoja na kuwatukuza na kuwaheshimu, sawa sawa katika zama za uhai wa Mawalii hao au baada ya kufa kwao, bila ya kuwaitakidi kuwa wao ni miungu na ni vyanzo vinavyojitegemea kwa matendo yanayomstahiki Mwenyezi Mungu, basi hapana mtu yeyote ambaye angeyaona matendo haya kuwa ni ibada wala anayeyasimamia asingeonekana kuwa ni mshirikina, bali kinyume chake angewaona kuwa ni watu wenyc mafanikio wanaoheshimu Mawalii wa Mwenyezi Mungu na kudumisha utajo wao na kuwafanya Mawalii hao kuwa ni kiigizo (chema) kwa watu hao.

Bila shaka kuwatukuza Mawalii wa Mwenyezi Mungu ni kutukuza vitambulisho vya Mwenyezi Mungu kama ilivyokwisha onyeshwa hapo kabla, na kwamba Uislamu unavitukuza vitambulisho vya Mwenyezi Mungu. Mtume[s.a.w.w] alikuwa akilishika na kulibusu "Hajarul-Aswad" pamoja na yeye kufahamu wazi kwamba hilo ni jiwe tu. Na sisi pia tunamfuata Mtume[s.a.w.w] kwa tendo lake hilo, tunalibusu Hajarul Aswad na tunatufu nyumba ya Mwenyezi Mungu ambayo si kitu ila mkusanyiko wa mawe na udongo, na tunakimbia baina ya Safa na Marwah na si kitu ila vilima viwili. Hii ni (kana kwamba) tunatenda matendo yale yale yaliyokuwa yakitendwa na waabuduo sanamu kwa masamu yao, lakini hapana kabisa mtu yeyote ambaye imepata kumpitia katika fikra zake kwamba sisi tunaabudu udongo na mawe. Basi Je, ni kwa nini? Ni kwa sababu mawe hayo hayadhuru wala kunufaisha.

Ama tungetekeleza Ibada hizi hali ya kuwa tunaitakidi kuwa mawe haya na vilima hivi ni miungu na ndiyo chanzo cha athari za uungu, basi tungekuwa miongoni mwa wanaoabudu sanamu. Na kwa msingi huu, bila shaka kuubusu mkono wa Nabii au Imam au Mwalimu au wazazi wawili na pia kuibusu Qur'an na vitabu vya dini kama vile "Nahjul-Balagha" na kubusu Zariha na kila kile chenyc kuhusiana na waja wema wa Mwenyezi Mungu, hakuna kinachokusudiwa ila ni heshima na kuwatukuza, na kawatukuza wao si kitu kingine ila kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ndani ya Qur'an imekuja (Habari) ya Malaika kumsujudia Adam[a.s] na pia ndugu wa Nabii Yusuf kumsujudia Yusuf[a.s] , lakini hapana yeyote iliyempitia katika akili (yake) kwamba kusujudu (kwao hawa) ilikuwa ni kumuabudia Adam au Yusuf na hiyo ni kwa sababu hao waliomsujudia Adam na Yusuf hawakuwaitakidi wawili hao kuwa ni miungu na hawakuwazingatia kuwa wao ndiyo asili ya matendo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, bali jambo hilo lilikuwa ni heshima na utukufu na siyo ibada kama inavyoonekana.

Bila shaka Mawahabi wakati wanapokutana na aya hizi, wanagongana nazo, kwani utawaona wanachunguza huku na huko ili kuzikwepa na kuzificha na husema; "hakika kusujudu kwa watu hao ilikuwa ni amri ya Mwenyezi Mungu kwa hiyo haiwezi kuzingatiwa kuwa ni ibada." Ni sawa kwamba yote hayo na hata kusujudu kwa ndugu wa Yusuf[a.s] kulikuwa ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu au radhi yake, lakini kitu ambacho Mawahabi wanajisahaulisha na kujifanya hawakijuwi ni ule ukweli wa tendo lenyewe Ia Sajdah siyo ibada na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akaliamrisha. Na lau Sajdah ingekuwa ni ibada kwa anayesujudiwa, Mwenyezi Mungu asingeliamrisha kabisa, kwani amri haiwezi kuitoa ibada kwenye uhakika wake na wala haiwezi kuifanya shiriki kuwa Tauhidi. Mwenyezi Mungu anasema:

قُلْ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَأْمُرُ بِالْفَحْشَاءِ أَتَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢٨﴾

"Waambie, bila shaka Mwenyezi Mungu haamrishi maovu, Je, Mwasema juu ya Mwenyezi Mungu mambo msiyoyajua?" Qur'an, 7:28.

Kifupi ni kuwa, uhakika wa tendo lolote lazima uwe siyo wa kiibada kabla haijatolewa amwi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuliamrisha tendo hilo ili (itakapotoka amri) ipate kuihusisha ibada (kwenye tendo hilo) na wala hakuna namna yoyote ya amri itakayokuja kulitengua tendo hilo kutoka kwenye hukmu ya Ibada.

Bila shaka kujitakasa ambako Mawahabi wanategemea, kitu ambacho muda mrefu tumekuwa tukisikia toka kwa Masheikhe zao huko Maka na Madina, kunajulisha ukaidi walionao juu ya kufahamu maarifa ya Qur'an na kukosa kwao kuelewa kuwa "Ibada" inao uhakika wa pekee unaojitegemea na hupata ikatokeza amri kuamrisha ibada na wakati mwingine katazo kukataza. Hii ina maana kwamba, kitu ambacho kwa dhati yake ni ibada, Mwenyezi Mungu hukiamrisha au kukikataza, kama vile Sala na Saumu ambazo Mwenyezi Mungu amewaamrisha watu "Mukalafu" kazitekeleza na amemkataza (kufanya ibada hizo) mwanamke mwenye hedhi, ati kama vile kufunga siku ya Idi al-Fitri na Adh-haa ambazo Mwenyezi Mungu amewakataza watu wote "Wasifunge". Basi kama kusujudu kwa Malaika kumsujudia Adam[a.s] na ndugu wa Yusuf[a.s] na wazazi wake wawili kumsujudia Yusufu[a.s] ni kuwafanyia Ibada, basi ile amri ya kuamrishwa kwao kusujudu, hakuitoi sijda katika uhakika wa kuwa ni ibada bali hapana budi tuseme kuwa kuitakidi Uungu ndiko kutakakokiharamisha kitendo hicho na kukifanya kuwa ni ibada, au kuitakidi kuwa yule anayenyenyekewa ndiyo asili (chanzo) cha matendo ya Mwenyezi Mungu. Vipi tutapata msimamo?

Ewe msomaji mpendwa inapasa ufahamu kuwa, kuondosha tofauti iliyopo kati ya Waislamu na Mawahabi ndani ya mambo mengi (wanayohitalifiana) inategemea kupata ufumbuzi wa maana ya ibada. Ikiwa haikubainishwa maana ya ibada kwa taarifu ya kimantiki, na ikawa hakuna maelewano na uadilifu katika pande mbili, basi hakuna faida ya kutafiti na kujadiliana. Kwa maelezo haya basi, hana budi mtu mwenye kutafuta ukweli afanye kila njia ya kuchunguza maudhui hii kwa undani na asihadaike na taarifu za kilugha zilizopungufu kuweza kutatua na kufafanua. Rejea iliyo bora atakayoirejea ni aya za Qur'an, hiyo ndiyo dalili inayoongoza (kufahamu) maudhui hii na kila maudhui. Na miongoni mwa mambo yanayohuzunisha ni kwamba, waandishi na watunzi wa Kiwahabi na walioandika kuwajibu Mawahabi, wamefanya utafiti na uchunguzi kwa urefu katika nukta zingine na wala hawakuitilia maanani nukta hii muhimu (ya Ibada) kwa kuisherehesha na kuithibitisha. Basi Mawahabi wanasema, "Matendo mengi muyafanyayo Enyi Waislamu kumhusu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu[s.a.w.w] na Maimamu wa nyumba yake ni kumuabudia, na hali hiyo inalazimu kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika ibada." Kwa hiyo basi inabidi Waislamu walete ufafanuzi na maelezo ya kina kuhusu ibada ili kuiondoa dalili yao ya upuuzi. Kwa hakika Mawahabi wanayaona mambo mengi wayatendayo Waislamu kwa maiti kuwa ni kumuabudia. Kwa mfano:

1). Kuomba Shafaa kwa Mtume[s.a.w.w] na watu wema.

2). Kuomba uponyo kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu.

3). Kuomba kutekelezewa haja toka kwa viongozi wa Dini.

4). Kumheshimu na kumtukuza mwenye kaburi.

5). Kutaka msaada kwa Mtume[s.a.w.w] na wengineo.

Basi wao (Mawahabi) wanasema, "Hakika Shafaa ni katika matendo ya Mwenyezi Mungu na vile vile kuponya ni kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuomba mojawapo ya mawili haya kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu kunapelekea kumuabudu huyo (aombwaye).

NI KIPI KITENDO CHA MWENYEZI MUNGU?

Katika kitabu hiki kidogo tunatanguliza uchunguzi juu ya matendo ya Mwenyezi Mungu na maana yake ili maudhui hii ipate kufahamika na tunasema: "Ikiwa ambaye anasimamaia Shafaa na kuponya kwa uwezo wake mwenyewe na kwa kutaka kwake hali ya kujitegemea bila ya kuipata haki ya Shafaa kutoka kwa yeyote yule na bila ya kutegemea uwezo wa aliye juu zaidi kuliko yeye kiuwezo) basi haya ni miongoni mwa matendo ya Mwenyezi Mungu yanayomuhusu peke yake. Na kuomba Shafaa kwa yeyote yule hali ya kaitakidi (kama tulivyosema hivi punde) maana yake ni kuamini Urabbi na Uungu wa huyo anayeombwa. Ama ikiwa kuomba Shafaa na uponyo kumesalimika kutokana na itikadi hii, na mtu akaomba Shafaa kwa mtu anayemuitakidi kuwa ni mja wa Mwenyezi Mungu, pia anatenda kwa msaada na uwezo wa Mwenyezi Mungu na idhini yake, basi Shafaa hii na uponyo huu havilazimiani na itikadi ya Uungu na siyo kuomba tendo la Mwenyezi Mungu kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu." Qur'an Tukufu inasema ikimnukuu Nabii Isa[a.s] :

وَأُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ وَأُحْيِي الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِ اللَّـهِ ﴿٤٩﴾

"Na ninaponya vipofu na wenye mbaranga, na ninafufua wafu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu". Qur'an, 3:49

Na ufafanuzi kama huu unakuja pia ndani ya munasaba wa kuomba kukidhiwa haja toka kwa mmoja wa Mawalii wa Mwenyezi Mungu au kumuomba msaada. Basi kutaka kukidhiwa haja na Walii huyo kuna namna mbili:

1). Kumuomba mja pamoja na kuitakidi kuwa anao uwezo wa kujitegemea Mwenyewe, hii itakuwa ni Ibada.

2). Kumuomba mja hali ya kuitakidi kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu na nguvu zake zinatoka kwa Mwenyezi mungu, basi hali hii haihusiani kabisa na ibada. Kwa Hakika ufafanuzi huu siyo tu ndiyo ukomo wa kutenganisha baina ya ibada na kisichokuwa ibada kwa munasaba wa matendo haya, bali ni kanuni ya ujumla inayotenganisha baina ya Shirki na Tauhidi katika kila vinavyo athiri na sababu. Bila shaka kuitakidi athari (matokeo) ya 'Asprini' (kwa mfano) katika kutuliza maumivu, na kuitakidi kuwa ikiwa athari hiyo inatokana na uwezo wake wa kujitegemea na kwamba hakuna mafungamano na uwezo uliyo juu zaidi ambaye ni Mwenyezi Mungu, basi maana yake ni kuitakidi Uungu wa hiyo 'Asprini'. Ama kuitakidi kwamba Mwenyezi Mungu ndiye aliyeyaweka matokeo haya na athari hii ndani ya Asprini na pia dawa hii si lolote ila ni sababu ya kutuliza maumivu na vile vile haiwezi kutuliza maumivu isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, bila shaka itikadi ya namna hii inatokana na Tauhidi yenyewe khasa, kwani hapana mwenye kuathiri ila yeye Mwenyezi Mungu.

Na kwa sababu hii tumesema kwamba "Kuondosha tofauti mbali mbali kunaegemezewa kwenye ufafanuzi wa maana ya Ibada na kuitakasa Tauhidi kutokana na shirki na matendo ya Mwenyezi Mungu kutokana na mengineyo na kuutakasa uungu kutokana na Ubudiyyah. Na hapo kabla imeonyeshwa kuwa Waarabu wa zama za Jahiliyya walikuwa wakiitakidi itikadi hii yenye makosa, kwamba Masanamu (hayo hayo) ndiyo yaliyokuwa yanaendesha baadhi ya mambo ulimwenguni kwa kujitegemea na yalikuwa yakimiliki Shafaa na mambo mengineyo. Itikadi hii ndiyo iliyowafanya wawe washirikina. Kwa hiyo, iwapo utataka ufafanuzi wa kielimu juu ya maudhui hii rejea vitabu hvi viwili vifuatavyo vilivyoandikwa na Mwandishi wa kitabu hiki.

1). Maalimut-Tauhidi Fil-Qur-'anil-Karim.

2). At-Tauhidu Was-Shirku Fil-Qur-anil-Karim.

MANENO YA AL-QUDHAI AL-MISRI

Baada ya kuwa nimeyahariri (maelezo yaliyotangulia) na kubainisha ufafanuzi wa ibada niliyaangalia kwa makini maneno ya mmoja wa wachunguzi miongoni mwa wanachuoni wa chuo cha Az-har, yaani Ustadh Sheikh Salamah Al-Qudhai Al-Izami As-Shafii ambaye ndiye Mwandishi wa kitabu kiitwacho "Fur-Qanul Qur'an Baina Sifatil-Khaliq Wa Sifatil-Ak-Waan.[171] Yeye amesema: Mwenyezi Mungu aing'arishe hoja yake: (Sasa tutazame maana ya Ibada kisheria, na ninataraji mahala hapa patatoa uzinduzi uliyo bora, kwa hakika kosa lililomo ni kuteleza kukubwa na ni kosa kubwa ambalo zilimwagwa damu (za watu) zisizoidadi ya kudhibitiwa na heshima za watu zilizovunjwa hazina hesabu, na jamii zikatenganishwa mahala ambapo Mwenyezi Mungu ameamuru ziunganishwe Mwenyezi Mungu atulinde kutokana na makosa na fitna hasa hasa fitna za Shubuhati - basi fahamu kwamba wao yaani Mawahabi waliifasiri ibada kuwa ni "Kufanya unyenyekevu ulio katika daraja ya juu sana", na wakakusudia ndani ya tafsiri hiyo maana ya kilugha tu. Ama maana ya kisheria inatoa maana iliyo finyu kuliko hii (ya kilugha) kama itakavyodhihiri kwa mchunguzi mwenye kuvumilia katika utafiti iwapo ataangalia kila mahali ambapo neno ibada limekuja katika sheria, kwani maana yake ni "kufanya unyenyekevu wa hali ya juu kwa moyo kwa kuitakidi Uungu wa anayenyenyekewa, au kwa mwili pamoja na itikadi hiyo.

Basi ikiwa itikadi hii itakuwa haipo, unyenyekevu wa dhahiri alioufanya (Mwenye kunyenyekea) hauwezi kuwa ni ibada kisheria, ikiwa kanyenyekea sana au kidogo na kwa namna yoyote hata kama ni kusujudu na hata kama hakuamini Rububiya kwa yule anayemnyenyekea lakini akaamini kuwa anazo khususiyah fulani za Rububiyah, basi hii pia itakuwa ni ibada. Kwa mfano kama ataitakidi kwamba huyo mwenye kunyenyekewa anajitegemea katika kunufaisha au kudhuru na kama vile kupitisha matakwa yake japokuwa kwa njia ya Shafaa kumshufaia huyo mwenye kumuabudia mbele ya Mola ambaye ni mkuu kuliko huyu mwenye kuabudiwa. Kwa hakika washirikana walikufuru kwa sababu ya kuyasujudia masanamu yao na kuyaomba na mambo mengineyo miongoni mwa aina za unyenyekevu kwa sababu ya sharti hii kwani washirikina waliitakidi umola wa hayo wanayoyanyenyekea au wakayahusisha na khususiyyat za Rububiyah kama utakavyokujia ufafanuzi wake. Na haiwezekani kusema kwamba kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu bila itikadi hii ni ibada kisheria ukiachilia mbali aina zingine za unyenyekevu ambazo ni duni kuliko Sijda. Na kama tutasema, Sijda hii ni Ibada itakuwa ni kufru, na chochote kilicho kufru hakitofautiani kutokana na tofauti ya sheria wala amri ya Mwenyezi Mungu kwa kitu hicho wala Mwenyezi haamrishi kitu kama hicho: "Waambie Mwenyezi Mungu haamrishi mambo mabaya " Qur'an, 7:28

"Na wala haridhii kufru kwa waja wake ." Qur'an, 39:7

Na haya yako wazi (yanaeleweka) kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Na (sasa) hebu msikilize Mwenyezi Mungu Mtukufu alipowaambia Malaika:

"Msujudieni Adam, wakasujudu wote isipokuwa Ibilisi alikataa na akapinga " Qur'an, 2:34 Na alisema Iblisi: "Mimi ni bora kuliko yeye": Qur'an,7:12

"Na alisema tena: Je, Nimsujudie Uliyemuumba kwa Udongo ?" Qur 'an, 17:61

Na kusema kwamba Adam alikuwa ndiyo Qibla (cha Malaika walipamuriwa kumsujudia) ni usemi ambao haukubaliwi na ukweli na pia uchunguzi (wa jambo hili) katika kuifahamu aya inavyopasa kuifahamu unapinga kauli hiyo. Na kama fahamu zako zitashindwa kulifahamu jambo hili, basi huyu hapa Nabii Yaqub na mkewe na watoto wao kumi na mmoja ambao Mwenyezi Mungu amesema kuhusu wao,

"Wakaporomoka kumsujudia ". Hapa inamaana walimsujudia Yusuf[a.s] . Qur'an, 12:100.

Mwanachuoni Al-Hafidh Ibn Kathir amesema katika Tafsiri ya aya hii, "Walimsujudia (Yusuf) wazazi wake wawili na ndugu zake na walikuwa watu kumi na moja, na tendo lao hili lilikuwa ni desturi inayokubalika kufanywa katika sheria zao wanapomsalimia mkubwa humsujudia. Na desturi hii ilikuwa imeruhusiwa tangu kwa Nabii Adam[a.s] hadi kwenye sheria ya Nabii Isa[a.s] , kisha iliharamishwa katika mila hii ya Kiislamu na kuifanya Sijda ni makhsusi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na haya ndiyo madhumuni ya kauli ya Qatada (juu ya Qadhiya hii na wengineo). Na kuna mapokezi katika hadithi kwamba: "Muadhi alifika Shamu akawakuta watu wa huko wakiwasujudia Maaskofu wao, naye aliporudi (Madina) akamsujudia Mtume[s.a.w.w] , Mtume akasema "Nini hiki (ukifanyacho) Ewe Muadhi"?

Muadhi akasema: "Mimi nimewaona (Huko Shamu) wanawasujudia Maaskofu wao, nawe unastahiki mno mimi nikusujudie." Mtume akasema: Lau ningekuwa mwenye kumuamrisha yeyote kumsujudia mwingine, basi ningemuamuru mke amsujudie mumewe kutokana na haki kubwa aliyonayo kwake." Na katika hadithi nyingine inasemwa kwamba: "Salmaan alikutana na Mtume[s.a.w.w] katika baadhi ya njia za Madina, na huyu Salmaan alikuwa kasilimu hivi karibuni, basi akamsujudia Mtume[s.a.w.w] , Mtume akasema, "Ewe Salmaan usinisujudie bali msujudie (Mwenyezi Mungu) aliye hai ambaye hatakufa". Lengo katika maelezo haya ni kuonyesha kuwa (Desturi ya kusujudia wakubwa) ilikuwa ikiruhusiwa katika sheria zao, (mwisho wa kauli ya Ibn Kathir).

Naye Imam Abu Jaafar (At-Tabari) katika tafsiri yake amesema mfano wa maelezo haya. Bila shaka umekwisha fahamu kwamba (Kitendo) kilicho cha kufru hakitofautiani kwa kutofautiani sheria, wala Mwenyezi Mungu hakiamrishi kuwa kitendwe wakati fulani miongoni mwa nyakati, basi kusujudu kwa Malaika kumsujudia Adam wala sijda aliyosujudiwa Yusuf[a.s] hazikuwa ni kufru kwa kuwa waliosujudu hawakuwa wameitakidi itikadi ya mambo ambayo yanamuhusu Mwenyezi Mungu peke yake wakati walipowasujudia hao waliosujudiwa, bali Malaika waliposujudu (kumsujudia Adam) kwao ilikuwa ni ibada kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaamuru kufanya hivyo waliomsujudia Yusuf kwao ilikuwa ni maamkizi yaliyoruhusiwa, na ruhusa hiyo ilifutwa katika sheria yetu (ya Kiislamu). Na wanachuoni wamehukumu kuwa, ni kufuru kwa yeyote mwenye kusujudia jua, au mwezi au sanamu, kwa kuwa kufanya hivyo ni alama za kufru ambayo ni kupinga mafunzo ya msingi katika dini kama ambavyo wamehukumu kuwa, mwenye kutamka shahada mbili ni muumini kwa hivyo ndizo dalili za imani, na imani ni kitu cha moyoni. Wamehukumu hivi sio kwa kuwa eti kile kitendo cha kwanza yaani kusujudia mwezi na jua kwa dhati yake ndiyo kufru na kile cha pili (kutamka shahada mbili) ndiyo imani.

Ikiwa kuna uzito wa kufahamu maelezo haya ambayo siyo mazito kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, hebu iangalie nafsi yako mwenyewe, huenda heshima na adabu uliyonayo kwa baba yako ikakuzuwia kukaa au kulala mbele yake, hivyo ukawa umesimama au kuketi kiasi saa moja au zaidi, na (kufanya hivi) haitakuwa ni ibada uliyomfanyia. Kwa nini basi? Hii ni kwa sababu tendo lako hili halikuambatana na itikadi ya mambo ambayo ni maalum kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na utaposimama kiasi cha kusoma Sura Al-Fatihah, na ukakaa kiasi cha kusoma Tashahudi kwa kiasi cha dakika moja au mbili hivi, na ikahesabiwa kuwa umefanya ibada kwa huyo uliyemsalia. Siri ya kuwa matendo haya ni ibada, ni kule kunyenyekea kwako kulikofanyika ndani ya kisimamo chako na kukaa kwako kulikoambatana na itikadi ya Uungu wa yule uliyemnyenyekea ambaye ni Mwenyezi Mungu.

Na (kwa mfano) unamwita kiongozi wako katika kazi au amiri wako ili akusaidie dhidi ya mtu aliyekudhulumu, au akusaidie kutokana na shida iliyokufika na hali wewe hukuitakidi kuwa huyo umwitaye ana uwezo wake wa kujitegemea kuleta manufaa au kuondosha madhara lakini tu Mwenyezi Mungu amemfanya awe ndiyo sababu ya kupitishia mambo ya kawaida mikononi mwake kwa yale ayapendayo yeye Mwenyezi Mungu. (Basi kuomba kwako msaada kwa kiongozi wako au amiri wako) haiwezi kuwa ni ibada kwa yule uliyemuomba kama tulivyokwisha eleza. Lakini iwapo utamwita (akusaidie) hali ya kuwa unaitakidi kwamba yeye ndiye anayenufaisha kwa dhati yake au kudhuru au kupitisha maamuzi bila kupingwa kwa ombi hilo, itakuwa wewe ni mwenye kumuabudia yeye, na kwa ibada hii umemshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kuwa umeitakidi ndani ya tendo hilo mambo yanayomuhusu Mwenyezi Mungu, kwani bila shaka kujitegemea kwa dhati, kuleta manufaa au kuondoa madhara na kupitisha maamuzi bila kipingamizi ni katika matendo makhususi ya Mwenyezi Mungu.

Na washirkina walikufuru kwa kuyasujudia masanamu na mfano wake kwa sababu ya kuyaitakidi masanamu hayo kuwa na uwezo wa dhati wa kujitegemea kunufaisha au kudhuru na kupitisha maamuzi bila kuyatenganisha na Mwenyezi Mungu japo kwa njia ya uombezi mbele yake kwani wao wanamuitakidi Mwenyezi Mungu kuwa ndiyo Mungu mkubwa na vile wanavyo viabudia ni waungu chini ya Uungu wa Mwenyezi Mungu, na kwa sababu ya uungu walionao imebidi wapitishe maamuzi wao na Mwenyezi Mungu bila kipingamizi. Aya nyingi za Qur'an zinajulisha kama tulivyoeleza na kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

أَمَّنْ هَـٰذَا الَّذِي هُوَ جُندٌ لَّكُمْ يَنصُرُكُم مِّن دُونِ الرَّحْمَـٰنِ إِنِ الْكَافِرُونَ إِلَّا فِي غُرُورٍ ﴿٢٠﴾

"Ni nani huyu ambaye ni mlinzi wenu atakayekusaidieni pasipo (Mwenyezi Mungu) mwingi wa Rehma, hawako makafiri ila katika kudanganyika". Qur'an, 67:20

Na kauli yake nyingine aliposema:

أَمْ لَهُمْ آلِهَةٌ تَمْنَعُهُم مِّن دُونِنَا لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَ أَنفُسِهِمْ وَلَا هُم مِّنَّا يُصْحَبُونَ ﴿٤٣﴾

"Je, wanao Miungu wanaowalinda badala yetu, hawawezi kujisaidia wenyewe na wala hawatahifadhiwa katokana nasi." Qur'an, 21:43

Na Istif-hami iliyoko katika aya hizi mbili ni ya makemeo kwanjia yakuwalaumu katokana na yale waliyoitakidi. Pia Mwenyezi Mungu amesimulia habari za watu wa Nabii Huud[a.s] walipomwambia: "Hatusemi ila ni kuwa baadhi ya Miungu yetu imekwisha kukutia katika balaa". Qur'an, 11:54 Naye Nabii Huud alipowaambia:

"Basi nyote nifanyieni hila (kunidhuru) na musinicheleweshe ". Qur'an, 11:55-56.

Nyingine ni kauli yake Mwenyezi Mungu atakayosema kuwalaumu washirikina siku ya Qiyama kutokana na itikadi walizoziitakidi kwa masanamu ikiwa ni pamoja na kuamini kuwa yana uwezo wa kunufaisha na kupitisha maamuzi kama yapendavyo:

وَقِيلَ لَهُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ ﴿٩٢﴾ مِن دُونِ اللَّـهِ هَلْ يَنصُرُونَكُمْ أَوْ يَنتَصِرُونَ ﴿٩٣﴾

"Wako wapi mliokuwa mkiwaabudu, badala ya Mwenyezi Mungu, Je, wanaweza kukusaidieni au kujisaidia wenyewe? Qur'an, 26:92-93.

Nao washirkina watasema hali wakiwa motoni wakizozana na kuwaambia hao waliowaitakidi kuwa ni Miungu na wanazo khususiya za kiungu:

تَاللَّـهِ إِن كُنَّا لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٩٧﴾ إِذْ نُسَوِّيكُم بِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٩٨﴾

"Wallahi bila shaka tulikuwa katika upotofu uliodhahiri, tulipokufanyeni sawa na Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote". Qur'an, 26:97-98.

Hebu angalia kulinganisha walikokiri (washirikina) kiasi kwamba muongo anasema kweli na muovu naye anajuta wakati majuto yake hayamsaidii kita. Bila shaka kulinganisha kulikotajwa ikiwa ni kwa ajili ya kuthibitisha kitu katika sifa za Uungu, basi hilo ndilo lengo na kutokana na hali hii ndipo unapatikana ushirikina wao na kufru yao, kwani sifa za Mwenyezi Mungu zinawajibisha upweke kwa maana ya kutokuwa na mfano wake kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kama ilivyotangulia kuelezwa. Na kama kulinganisha huko ni katika kustahiki kwake ibada, basi italazimu kuitakidi ushirika katika yale ambayo ndani yake kuna ustahiki wa ibada, na huo ustahiki ni sifa za Uungu au baadhi ya sifa hizo, na ikiwa (kulinganisha) ni katika nafsi ya ibada yenyewe basi kitendo hicho hakifanywi na mtu mwenye akili ila kwa yule anayeitakidi kustahiki huyo mwenye kuabudiwa kama vile anavyostahiki Mola wa ulimwengu. Basi ni vipi itakanushwa itikadi yao ya Uungu kwa miungu yao hali ya kuwa waliifanya kuwa niwashirika wa Mwenyezi Mungu na wakaipenda kwa mapenzi anayostahiki kupendwa Mwenyezi Mungu kama alivyosema yeye Mwenyezi Munga akieleza habari zao:

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ﴿١٦٥﴾

"Na miongoni mwa watu kuna wanaowafanya miungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu, wanawapenda kwa mapenzi anayostahiki kupendwa Mwenyezi Mungu". Qur'an, 2:165.

Na neno "Andaad" lililotumika kwenye Aya hiyo hapo juu ni uwingi wa "Nidd" na maana yake ni kama walivyosema wataalam wa tafsiri na lugha. Ama kauli ya Mwenyezi Mungu akiwazungumzia washirikina akasema:

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٨٧﴾

"Na ukiwauliza ni nani aliyewaumba, bila shaka watasema, ni Mwenyezi Mungu". Qur'an, 43:87.

Kauli hii na nyinginezo mfano wa hii maana yake siyo kwamba wao (washirikina) hawauthibitishi uungu wa miungu yao na yale mambo maalum yanayohusu uungu, bali maana yake ni kwamba, wanapohojiwa hukiri kutokana na ukweli ambao Mwenyezi Mungu ameziumbia nafsi (kumtambua). Lakini ni kwa kiasi gani wao hurejea haraka katika itikadi zao za waungu wa uongo kwa miungu yao, hurudi na katumbukia humo kama alivyosema Mwenyezi Mungu katika aya nyingine.

يَعْرِفُونَ نِعْمَتَ اللَّـهِ ثُمَّ يُنكِرُونَهَا وَأَكْثَرُهُمُ الْكَافِرُونَ ﴿٨٣﴾

"Wanazijua neema za Mwenyezi Mungu kisha wanazikanusha na wengi wao ni makafiri". Qur'an, 16:83.

Na kauli nyingine ya Mwenyezi Mungu akizungumzia kikundi miongoni mwao: "Kila wakirudishwa katika fitna, huangushwa humo ". Qur'an, 4:91

Kurudishwa katika fitna na kuangushwa humo siyo jambo la ajabu kutokea kwa wale walioyafanya matamanio yao kuwa miungu yao, nawe msomaji utawaona hao wenye matamanio hayo iwapo utamjadili katika Bid'a zake, atakusikiliza kwa makini na atakinaika (atatosheka) wakati wa majadiliano na atakiri kuwa amekwenda kinyume cha haki na ataonyesha dalili za uadilifu (katika majadiliano na matokeo yake). Kinapomalizika kikao cha mjadala hurudi kule kwenye mazoea ya matamanio na kurudia Bid'a yake kama kwamba hapakuwa na mjadala baina yako na yeye (isipokawa waliorehemewa na Mwenyezi Mungu). Na hali kama hii tumeiona mara nyingi kwa wale tuliokutana nao miongoni mwa wanaofuata matamanio. Tunamuomba Mwenyezi Mungu kwa fadhila zake atupe mafanikio. Pamoja na yote haya, lau itakubalika kwamba (washirikina) hawakuitakidi kwa miungu yao kuwa na uwezo wa kuumba, kuruzuku wala kuendesha mambo, lakini wanaitakidi ndani ya miungu hiyo mambo yasiyokuwa hayo ambayo yanahusu mas-ala ya uungu nao ni wajibu wa kupitisha maamuzi wayatakayo. Basi wao wanaona kuwa shafaa ya masanamu hayo inakubaliwa moja kwa moja hairudishwi na haitegemei idhini ya Mwenyezi Mungu. "Ametakasika sana Mwenyezi Mungu na yale wayasemayo wajinga." Kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu amesema katika Qur'an akijibu madai yao haya:

مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ﴿٢٥٥﴾

"Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake (Mwenyezi Mungu) bila idhiniyake? Qur'an, 2:255

Amesema Qadhi Nasirudin Al-Baidawi katika tafsiri ya aya hiyo, "Ni ubainifu wa utukufu wa mambo yake, na hiyo ni kwa sababu hakuna anayeungana naye au kumkurubia awezaye kutoa akitakacho iwe kwa shafaa au kunyenyekea, basi itakuwaje iwezekane kwa njia ya kumpinga": Hivyo basi iangalie kauli ya Baidawi aliposema; "Awezaye kutoa akitakacho ikiwa ni kwa Shafaa" utakuta ni dhahiri kuwa inahusu wajibu wa matakwa yake yakubalike kwanza kwa Mwenyezi Mungu na wajibu wa kupitisha maamuzi ni miongoni mwa mambo yanayohusu uungu kama inavyofahamika. Na aina hii ya Shafaa ni Shafaa ya shirki ambayo Qur'an imeibatilisha, kwani kuiamini Shafaa ya aina hii ni kufru kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

"Au ndiyo wamejifanyia waombezi kinyume cha Mwenyezi Mungu?" Qur'an, 39:43 Na kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

قُلْ مَن ذَا الَّذِي يَعْصِمُكُم مِّنَ اللَّـهِ إِنْ أَرَادَ بِكُمْ سُوءًا أَوْ أَرَادَ بِكُمْ ﴿١٧﴾

"Waambie, ni nani ambaye anaweza kukulindeni kutokana na Mwenyezi Mungu kama akikutakieni ubaya au (nani anayeweza kuzuwiya Rehma yake) kama akikutakieni Rehma?" Qur'an, 33:27.

Ama Shafaa ambayo wanaiitakidi watu wa Tauhidi na ndiyo iliyoletwa na Qur'an na Sunna, yenyewe iko mbali na itikadi ya Shafaa inayoitakidiwa na washirikina kama ulivyo umbali wa imani na kufru na umbali wa mwangaza na kiza. Na Shafaa ya watu wa Tauhidi ni maombi ya mwenye kushufaiya kumuombea mwenye kushufaiwa, na Mwenyezi Mungu kwa fadhila zake humkubalia amtakaye na hiyo ndiyo maana ya Istith-nai katika kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema: "Isipokuwa kwa idnini yake". Na maana ya idhini hapa ni kuridhia kama alivyosema kwenye aya nyingine: "Wala hawamuombei yeyote ila yule aliyeridhiwa (na Mwenyezi Mungu) . Qur'an, 21:28. Na nyingine tena:

وَكَم مِّن مَّلَكٍ فِي السَّمَاوَاتِ لَا تُغْنِي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا إِلَّا مِن بَعْدِ أَن يَأْذَنَ اللَّـهُ لِمَن يَشَاءُ وَيَرْضَىٰ ﴿٢٦﴾

"Na wako Malaika wangapi mbinguni ambao uombezi wao hautafaa chochote isipokuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia". Qur'an, 53:26.

Na kwa maelezo haya inakubainikia tofauti baina ya yale iliyoyathibitisha Qur'an katika Shafaa na yale iliyoyakanusha (ambayo hayana idhini yake na radhi yake.) Mwenyezi Mungu ni mkubwa, hakifanyiki kitu katika ufalme wake ila yeye atake. Ama Shafaa kwa idhini yake na radhi yake inayotokana na waja wake wema walio wateule kuwaombea wenye kuasi katika watu wa Tauhidi inafaa, na limethibiti hilo kwa njia ya mutawatir wala hapana kizuizi ndani yake na kuitakidi hivyo ni katika mambo ya dini, kwani jambo hili liko katika mlango wa Dua, naye Mwenyezi Mungu huwakubalia waaminio na wakatenda mema na huwazidishia fadhila zake. Tunataraji itakuwa imeeleweka kwako msomaji (Insha-Allah) nini maana ya ibada kisheria, na wakati huo huo utakuwa umefahamu kuwa siyo ibada ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu pale Mwislamu anapotaka wasila kwa Mwenyezi Mungu.[172] Basi haya yalikuwa ndiyo maneno yaliyoandikwa na Al Allamah Al-Qudhai, nasi tumeyaleta kutokana na faida nyingi zilizomo, na bila shaka tumeifafanua hali yake, ni juu yako ewe msomaji muadilifu kufanya uchunguzi.