UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI0%

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Vitabu mbali mbali

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi: SHEIKH JA'AFAR SUBHANY
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 48468
Pakua: 4233

Maelezo zaidi:

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 24 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 48468 / Pakua: 4233
Kiwango Kiwango Kiwango
UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi:
Swahili

14

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

KUOMBA MSAADA KWA KUPITIA ROHO ZA MAWALII WA MWENYEZI MUNGU

Mas-ala ya kuomba msaada kwa kupitia roho za Mawalii wa Mwenyezi Mungu baada ya kufa kwao na kutoweka katika maisha haya ya kimaada, ni jambo muhumi mno kulifanyia uchunguzi, na hakuna tofauti baina ya kuwa huko kutaka msaada ni kwa namna ya dua au kwa kuomba. Sababu ya umuhimu wa jambo hili kuliko yale yaliyotangulia ni kuwa, leo hii Waislamu hawako katika mahdhar (ushuhuda) wa Nabii au Imam ili wakamuombe msaada ana kwa ana, kwa sababu hiyo basi, Waislamu wanaomba msaada kupitia roho za Mawalii hao watukufu. Mpaka hapa yaonekana umuhimu wa kuyafanyia uchunguzi mkubwa mas-ala haya kuliko yale yaliyotangulia.

Ewe msomaji mtukufu, uchunguzi wa maudhui hii utazungumzia mambo manne, na wakati wa kuelezea na kuichambua maudhui hii, bila shaka kufaa kwa mas-ala ya kuomba msaada kupitia kwa roho tukufu za Mawalii kutaeleweka vizuri. Mambo hayo manne ni haya yafuatayo:

1) Roho huwa zinabaki hai baada ya mtu kufa.

2) Ukweli halisi wa mtu ni roho yake.

3) Kuwasiliana na ulimwengu wa roho ni jambo linalowezekana.

4) Hadithi sahihi zilizopokewa na wanachuoni wa hadithi zinazungumzia kusihi mas-ala ya kuomba msaada kupitia kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu na kwamba, sera ya Waislamu imekuwa hivyo toka hapo kabla. Na ufuatao ndiyo ufafanuzi wa mambo hayo manne:

MTU ANAPOKUFA HAINA MAANA KUWANDIYO AMETOWEKA KABISA

Aya nyingi za Qur'an zinajulisha wazi kwamba kufa siyo mwisho wa uhai, bali kufa ni moja ya kituo cha kuhamia kuelekea kwenye maisha mapya, na pia kufa kunamuingiza mtu kwenye ulimwengu mpya ulio bora kuliko ulimwengu huu wa kimaada. Kila anayeitakidi kwamba kufa ndiyo kutoweka kabisa, na ndiyo mtu huwa habakishi athari yoyote isipokuwa mwili usio na roho, mwili ambao hatimaye baada ya muda fulani hugeuka na kuwa udongo, mwenye itikadi hii huwa anafuata falsafa ya kimaada ambayo inapinga kuwepo kwa vitu visivyo vya kimaada, naye anafuata bila kujua anachokifanya. Watu wenye nadharia hii, hawauoni uhai isipokuwa ni matokeo ya kimaada yenye silsila ya utendaji wa kikemia na kifizikia unaopatikana ndani ya ubongo na mishipa ya fahamu. Na pindi mwili utakapokosa joto lake na chembe hai nazo zikakoma kufanya kazi basi uhai wa mtu nao hukoma vile vile na kugeuka kuwa mwili mkavu. Nadharia hii inakwenda mbele zaidi na kusema, eti roho ni matokeo ya vitu fulani vya kimaada na misingi yake, na inapokosekana misingi hiyo na athari zake, basi roho nayo hupotea na kuharibika kufuatia kuharibika kwa hivyo vitu vya kimaada. Kwa sababu hii basi watu hawa hawaitakidi kuwepo kwa ulimwengu mwingine ambao ni wa kiroho.

Hakika nadharia hii inategemea falsafa ya kimaada ambayo inamuona mtu kuwa ni kama mashine iliyounganishwa vipande vipande na sehemu tofauti tofauti, na kwamba utendaji wa baadhi ya viungu kuvifanyisha kazi viungo vingine ndiko kunakozalisha uwezo wa kufikiri na kufahamu ndani ya ubongo, na pindi viungo hivi vikisimama kutenda kazi, basi athari za kufikiri hukosekana na uhai nao hutoweka moja kwa moja. Wanafalsafa wakubwa na wanachuoni wa dini wanaipinga kabisa nadharia ya kimaada kuhusu roho, na wanasema kwamba, ni kweli mtu katika mwili wake anayo nidhamu ya kimaada inayotawala katika mwili wake na utendaji unaotegemeana na silsila ya viungo, lakini zaidi ya haya yote yeye anachokitu cha asili kinachoitwa roho. Na kitu hiki (yaani roho) kuna kipindi inakuwa pamoja na mwili kisha roho hutengana na mwili na kupaa ikaenda kwenye ulimwengu uitwao "Bar-zakh" ili iungane na mwili latifu. (Mwili latifu ni kitu chenye urefu, upana na kina lakini hakionekanai kama hewa). Kuizungumzia roho "ili kuifahamu" baada ya kufa inataka kitabu maalum kitakachohusika na suala la roho tu, na wala haiwezekani kuitafiti kwa upana ndani ya kurasa hizi chache, na hii ni kwa sababu aya za Qur'an na hoja za kifalsafa na majaribio ya wataalamu wa roho wamebainisha kubakia kwa roho ya mtu baada ya kufa.

Hapa tunataja baadhi ya aya za Qur'an Tukufu zinazothibitisha kubakia kwa roho baada ya kufa.

QUR'AN NA KUBAKIA KWA ROHO

Aya za Qur'an zinafahamisha wazi kabisa kwamba roho huwa inabaki baada ya kiwiliwili kufa, na tunazitaja aya chache ili kufupisha maelezo.

وَلَا تَقُولُوا لِمَن يُقْتَلُ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتٌ بَلْ أَحْيَاءٌ وَلَـٰكِن لَّا تَشْعُرُونَ ﴿١٥٤﴾

(1) Na wala msiseme kuwa, wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu, bali wao wa hai lakini ninyi hamtambui. Qur'an, 2:154.

وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ ﴿١٦٩﴾ فَرِحِينَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا بِهِم مِّنْ خَلْفِهِمْ ﴿١٧٠﴾ يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ ...﴿١٧١﴾

(2) Wala usidhani wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wafu, bali wao wa hai wanaruzukiwa mbele ya Mola wao. Wanafurahia yale aliyowapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila zake na wanawashangilia wale ambao hawajajiunga nao.... Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi Mungu. Qur'an, 3:169, 170, 171.

إِنِّي آمَنتُ بِرَبِّكُمْ فَاسْمَعُونِ ﴿٢٥﴾ قِيلَ ادْخُلِ الْجَنَّةَ قَالَ يَا لَيْتَ قَوْمِي يَعْلَمُونَ ﴿٢٦﴾ بِمَا غَفَرَ لِي رَبِّي وَجَعَلَنِي مِنَ الْمُكْرَمِينَ ﴿٢٧﴾

(3) Bila shaka mimi nimemuamini Mola wenu, basi nisikilizeni. (Hawakusikiliza bali walimuuwa), akaambiwa ingia peponi, akasema laiti watu wangu wangejua. Jinsi Mola wangu alivyonisamehe na akanijaalia miongoni mwa walioheshimiwa. Qur'an, 36:25-27.

Makusudio ya Pepo aliyoamrishwa aingie ndani yake ni pepo ya barzakh[176] siyo ile ya akhera kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu pale aliposema "laiti watu wangu wangejua jinsi Mola wangu alivyonisamehe na akanijaalia miongoni mwa walioheshimiwa".

Bila shaka kutamani kwake kwamba watu wake wangefahamu cheo alichokipata, hakuna maana ya kuwa cheo hicho alichopata ni cha huko akhera kwa sababu huko akhera siri zote zitadhihirishwa wazi mbele ya macho ya watu na wala hapatafichikana hali za watu fulani kuwaficha wengine. Bali matarajio haya yanalingana na uhai wa dunia hii ambayo watu wanaishi bila ya kufahamu mambo ya barzakh na yanayotendeka huko na haya yanathibika katika aya hii tukufu. Zaidi ya hapo aya nyingine inayofuatia baada ya aya iliyotajwa, inaonyesha kwamba Qaumu ya mtu yule mwema aliyeingia Peponi, walikufa baada yake kutokana na ukelele mkali kutoka mbinguni na Mwenyezi Mungu anasema:

وَمَا أَنزَلْنَا عَلَىٰ قَوْمِهِ مِن بَعْدِهِ مِن جُندٍ مِّنَ السَّمَاءِ وَمَا كُنَّا مُنزِلِينَ ﴿٢٨﴾ إِن كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً فَإِذَا هُمْ خَامِدُونَ ﴿٢٩﴾

(4) "Na hatukuwateremshia watu wake jeshi kutoka mbinguni (kuwaangamiza) baada yake, wala hatukuwa ni wenye kuteremsha majeshi toka mbinguni, bali ulikuwa ni ukelele mmoja tu na mara moja wakazimika (wakafa)." Qur 'an, 36:28-29.

Ndani ya aya hizi mbili kinachofahamika ni kwamba, wale Qaumu ya yule mtu aliyeingia peponi walikuwa wakiishi hapa duniani kisha ghafla yaliwafikia mauti, kwa hiyo pepo iliyotajwa hapo si nyingine ila ni ile ya barzakh.

النَّارُ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا غُدُوًّا وَعَشِيًّا وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ أَدْخِلُوا آلَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ الْعَذَابِ ﴿٤٦﴾

(5) Adhabu za motoni wanadhihirishiwa asubuhi na jioni, na siku kitakapotokea Kiyama kutasemwa, 'Waingizeni watu wa Fir-aun katika adhabu kali zaidi". Qur 'an, 40:46.

Kufuatana na maana iliyomo katika aya hizi inatudhihirikia kwamba, watu wa Firaun wako hai katika ulimwengu wa barzakh; kwa kuwa wanadhihirishiwa adhabu za moto asubuhi na jioni mpaka siku ya kiyama, na kiyama kitakaposimama, wataingizwa kwenye adhabu kali zaidi ya Jahannam. Basi lau si kauli ya Mwenyezi Munga aliposema "Na siku kitakapotokea kiyama" makusudio ya aya hii yasingedhihiri, lakini sasa inathibitisha kwamba maneno kabla ya siku ya kiyama yanarejea kwenye ulimwengu wa Bar-zakh. Zaidi ya hayo ni kule kutamka kwa "asubuhi na jioni" kunaonyesha kwamba adhabu hiyo siyo ya sika ya kiyama kwa kuwa siku hiyo hakuna asubuhi wala jioni. Msomaji mtukufu, maelezo yaliyotangulia yalikuwa ni uchunguzi kwa kifupi kuthibitisha kuwepo kwa uhai baada ya kufa na sasa tuzungumzie jambo la pili.

UHAKIKA WA MTU NI ROHO YAKE

Mtu kwa mara ya kwanza hufikiria kwamba ameungamana kwa roho na mwili vikiwa pamoja, lakini ukweli halisi wa mtu ni ile roho yake inayopatikana katika mwili wake. Sasa hivi sisi hatufanyi uchunguzi wa maudhui haya kafuatana na mtazamo wa falsafa ya Kiislamu na ile ya Kiyunani, isipokuwa lengo letu ni kuyafahamu maudhui haya kwa mujibu wa kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho hakina shaka ndani yake. Bila shaka tukifanya mazingatio kwenye aya zinazomzungumzia mtu, kutatudhihirishia wazi kabisa kwamba ukweli halisi wa mtu ni ile roho yake. Hebu soma aya hii ifuatayo:

قُلْ يَتَوَفَّاكُم مَّلَكُ الْمَوْتِ الَّذِي وُكِّلَ بِكُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ ﴿١١﴾

Waambie; "Atakufisheni Malaika wa mauti aliyewakilishwa kwenu kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu". Qur'an, 32:11.

Ilivyo sahihi ni kwamba neno "tawafaa" halina maana ya kufisha inavyodhaniwa na watu bali maana yake ni kuchukua, kwa ajili hiyo basi kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema "yatawafaakum" maana yake ni "anakuchukuweni".[177] Kwani roho ni sehemu moja ya dhati ya mtu, na sehemu ya pili ni kiwiliwili chake, basi ibara hii itakuwa ni "Majaz"; kwani Malaika wa mauti huwa anachukua sehemu moja ambayo ni roho tu, na ama ile sehemu ya pili ambayo ni kile kiwiliwili hukiacha na kikabakia duniani kisha huzikwa kaburini wala Malaika wa mauti huwa hajishughulishi nacho.

Msomaji mpendwa, aya zinazozungumzia roho na mahala pake katika utu ni nyingi mao, sisi tumetaja moja tu kama mfano. Na jambo Ia mwanzo tuliloliashiria yaani "kubaikia kwa roho baada ya mauti" maelezo yetu yaliyotangulia yanaonyesha wazi kuwa roho ndiyo mtu mwenyewe halisi na ndiyo asili ya kukamilika kwake kinafsi na kiroho kama ambavyo mwili unachukua nafasi ya vazi ambalo huifunika roho. Qur'an Tukufu haizingatii mauti kuwa ndiyo kutoweka kwa mtu na kuwa eti ndiyo mwisho wa uhai wake, bali inasisitiza "hasa kwa mashahidi na watu wema" na hata kwa watu wenye dhambi pia kwamba, wanao uhai mwingine kabla ya siku ya Kiyama na kwamba uhai huo ima utakuwa ni wa furaha na kushangilia au utakuwa ni wa adhabu kali. Na kama itakuwa kwamba uhakika wa mtu umo katika mwili wake, hapana shaka mwili wake huo baada ya kufa na kazikwa utaoza na kugeuka kuwa udongo n.k. Iwapo haii itakawa namna hivi basi utakuwa wapi huo ulimwengu wa barzakh?

MAWASILIANO NA ULIMWENGU

Je, inawezekana kuwasiliana na ulimwengu wa kiroho? Jawabu linasema kuwa: Ndiyo bila shaka upo uwezekano huo, nasi tutatoa dalili kwa mujibu wa Qur'an tukufu na pia dalili za kielimu. Kuthibitika kubakia kwa roho isiyokuwa ndani ya mwili, hakatoshelezi kukubalisha kufaa kuomba msaada kupitia kwenye roho hiyo mpaka uthibiti uwezekano wa kuwepo mawasiliano baina ya roho hiyo na ulimwengu wa duniani. Ndani ya Qur'an kuna aya nyingi zinathibitisha kwamba, mtu kuwasiliana na ulimwengu wa kiroho ni jambo linalowezekana, isitoshe jambo hili limethibitika kwa vitendo kwa mfano:

1). NABII SALEHE [a.s] ALIZISEMESHA ROHO ZA WATU WA QAUMU YAKE

Mwenyezi Mungu anasema:

فَعَقَرُوا النَّاقَةَ وَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ وَقَالُوا يَا صَالِحُ ائْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٧٧﴾ فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٧٨﴾ فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا قَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَةَ رَبِّي وَنَصَحْتُ لَكُمْ وَلَـٰكِن لَّا تُحِبُّونَ النَّاصِحِينَ ﴿٧٩﴾

"Wakamchinja yule ngamia na wakaiasi amri ya Mola wao na wakasema: Ewe Saleh tuletee hayo unayotuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa Mitume. Mtetemeko wa ardhi ukawanyakuwa (roho zao) na wakawa wamekufa humo katika nyumba zao. Basi akawaacha na huku anasema: Enyi kaumu yangu nilikufikishieni ujumbe wa Mola wangu na nikakupeni nasaha lakini ninyi hamuwapendi wenye kutoa nasaha". Qur'an, 7:77, 78, 79.

Ziangalie aya hizi kwa makini: Aya ya kwanza inaashria kwamba watu wa Nabii Saleh walipokuwa hai duniani walimtaka awaletee adhabu ya Mwenyezi Mungu iliyoahidiwa. Aya ya pili inaashiria kushuka kwa adhabu juu yao na kufa kwao wote. Aya ya tutu inaashiria usemi wa Nabii SaIeh[a.s] aliousema baada ya watu wake kufa, akawahuzunikia kwa matokeo hayo ya kutisha waliyoyachagua wenyewe akawaambia: "Enyi watu wangu nilikufikishieni ujumbe wa Mola wangu na nikakunasihini lakini ninyi hamuwapendi wanaotoa nasaha". Na dalili inayoonyesha kwamba khitabu (usemi) hii ilitoka kwa Nabii Saleh baada ya watu wake kufa ni kama ifuatavyo: a) Mpango na mfumo wa aya kama zilivyopangika zaonyesha wazi jambo hilo. b) Herufi ya "FAA" katika neno "FATAWALAA" ambalo linajulisha kuwepo utaratibu "yaani baada ya hiki kinakuja hiki" na tamko "FATAWALAA" limekuja baada ya kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo "Wakawa wamekufa humo katika nyumba zao", kitu ambacho kinajulisha kwamba Khitabu ya Nabii Saleh[a.s] kwa watu wake ilikuja baada ya kuwashukia adhabu. Pia inafahamika kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu kwamba, watu hao walikuwa wamekithiri katika ujeuri na uovu kiasi kwamba hata baada ya kufa kwao roho zao zilikuwa bado zikipinga mawaidha na nasaha. Na inafahamika katika kauli yake aliposema: "Lakini ninyi hamuwapendi wanatoa nasaha".

2) NABII SHUAIBU [a.s] ALIZISEMESHA ROHO ZA WATU WAKE

Soma aya hizi:

فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٩١﴾ الَّذِينَ كَذَّبُوا شُعَيْبًا كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا الَّذِينَ كَذَّبُوا شُعَيْبًا كَانُوا هُمُ الْخَاسِرِينَ ﴿٩٢﴾ فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا قَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَنَصَحْتُ لَكُمْ فَكَيْفَ آسَىٰ عَلَىٰ قَوْمٍ كَافِرِينَ ﴿٩٣﴾

"Basi mtetemeko wa ardhi uliwatoa roho zao wakawa hawajimudu (wamekufa) katika nyumba zao. Wale waliompinga Shuaib wakawa kama kwamba hawakuwako, (mahala hapo) waliompinga Shuaib ndiyo waliokula khasara. Basi akawaacha akaenda zake na akasema: Enyi watu wangu nimekufikishieni ujumbe wa Mola wangu na nimekupeni nasaha; basi ni vipi nihuzunike kwa watu waliokufuru". Qur'an, 7:91, 92, 93.

Kutolea ushahidi aya hizi ni sawa na zile aya zilizotangulia kutokana na mafungamano yaliyopo kwa Nabii Saleh[a.s] .

3) MTUME MUHAMMAD [s.a.w.w] PAMOJA NA MANABII WENGINE

Mwenyezi Mungu anasema:

وَاسْأَلْ مَنْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رُّسُلِنَا أَجَعَلْنَا مِن دُونِ الرَّحْمَـٰنِ آلِهَةً يُعْبَدُونَ ﴿٤٥﴾

"Na waulize Mitume wetu tulio watuma kabla yako: Je! Tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Rah'mani?" Qur'an, 43:45.

Hakika dhahiri aya hii inajulisha kwamba, upo uwezekano wa Mtume[s.a.w.w] (Ambaye anaishi katika ulimwengu huu) kuwasiliana na Manabii wanaoishi kwenye ulimwengu mwingine ili apate kuwathibitishia washirikina ya kwamba, Manabii wote na katika kila zama walikuwa wakilingania kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumuabudu.

4) SALAMU ZA QUR'AN KWA MANABII

Qur'an Tukufu inawatolea salamu Manabii mahala pengi, na wala hapana shaka kwamba salamu hii siyo salamu ya juu juu isiyo na uhakika bali ni salamu na maamkizi ya hakika ambayo Qur'an inayaelekeza kwa Manabii na Mitume wa Mwenyezi Mungu. Siyo uadilifu iwapo mtu atajaribu kuzifasiri aya za Qur'an kwa tafsiri ya juu juu bila ya undani wake, basi atakuwa amezigeuza aya za Qur'an na kuwa matamko matupu yasiyo na maana. Kwa hakika watu wasioamini Mwenyezi Mungu, ambao hawaamini kuwepo kwa roho, huwatolea salamu viongozi wao kwa kutumia ibara zisizo na maana. Ama kwa upande wetu sisi Waislamu, tunanufaika kutokana na itikadi sahihi kuhusu suala la roho, na haifai kuzifasiri maana za maneno ya Qur'an kuhusu roho kwa tafsiri ya juu juu kwa sababu mafuhum ya Qur'an inategemea hakika na misingi ya ukweli. Basi hatuwezi kusema kwamba, maamkizi yaliyomo katika Qur'an ambayo tunayasema usiku na mchana ni maamkizi ambayo hayana hakika wala maana sawa sawa na maamkizi ya watu wasioamini. Hebu itazame Qur'an namna inavyowatolea salamu Manabii:

1. "Salamu zimshukie Nuhu katika walimwengu".

2. "Salamu zimshukie Ibrahim"

3. "Salamu zimshukie Musa na Harun"

4. "Salamu ziwashukie kizazi cha Yasin" 5. "Salamu ziwashukie Mitume". Quran, 37:79, 109, 120, 130, 181.

MAAMKIZI KWA MTUME [s.a.w.w] MWISHONI MWA SWALA

Waislamu wote ulimwenguni, bila kujali tofauti za Madhhebu yao katika furui za dini humsalimia Mtume[s.a.w.w] ndani ya swala zao mwishoni na huwa wanasema: "Salamu zikushukie Ewe Nabii, na Rehma na Baraka za Mwenyezi Mungu". Imam Shafii na wengineo wametoa Fat-wa kuwa ni wajibu kuitoa salamu hiyo baada ya 'TASHAHUD", na wengine nao wametoa Fat-wa wakasema kuwa ni Sunna, lakini wote wameafikiana kuwa Mtume[s.a.w.w] amewafundisha salaam hiyo. Pamoja na tofauti hii katika salamu hiyo na kwamba Sunna ya Mtume huwa inathibiti katika uhai wake na baada ya kufa kwake. [178] Suala ambalo sasa hivi tunalazimika kujiuliza ni hili lifuatalo: "Ikiwa maungamano na mawasiliano yetu na Mtume[s.a.w.w] yalikatika baada ya kufa kwake basi kuna maana gani kumsemesha na kumsalimia kila siku (katika Sala zetu)?" Imepokewa kutoka kwa Mtume[s.a.w.w] kwamba yeye amesema: "Yeyote mwenye kunitakia Rehma kwenye kaburi langu nitamsikia, na yeyote atakayenitakia rehma kutoka mbali, nitafikishiwa salamu yake". [179] Tumezungumza kwa ufafanuzi kuhusu maudhui ya kuwepo maungamano na roho zilizoko katika huo ulimwengu mwingine ndani ya kitabu maalum, na humo tumetaja aya nyingi kulihusu jambo hilo, hapa tunatosheka na aya hizi ili kufupisha maelezo. Kwa kumaliza inafaa kutambulisha kwamba, tumeleta dalili za kutoa salamu wakati wa 'Tashahud' tulipokuwa tukizitafiti zile aya tulizozitaja hapo kabla na hii ni kwa sababu jambo hili limethibiti bila ya shaka yoyote.

Sasa hivi hebu angalia mifano iliyomo katika tarekh (Historia) inayozungumzia uwezekano wa kuzisemesha roho (za watu waliokufa).

1. Imepokewa kutoka kwa Mtume[s.a.w.w] kwamba yeye alisimama kwenye kisima cha Badri na akawasemesha washirikina ambao waliuawa na miili yao ikatoswa kisimani humo: "Ninyi mlikuwa ni majirani wabaya kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mlimtoa nyumbani mwake na mkamfukuza, kisha mkaungana dhidi yake mkampiga vita, basi mimi nimeyapata aliyoniahidi Mola wangu". Basi mtu mmoja akamwambia Mtume[s.a.w.w] "Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu namna gani unavisemesha vichwa vilivyooza?" Mtume[s.a.w.w] akasema: "Wallahi wewe siyo msikivu kuliko wao, na hapana (kizuwizi) baina yao na kuadhibiwa kwao na Malaika kwa mijeledi ya chuma ila inwageuzie uso wangu hivi". [180]

2. Na imepokewa kwamba Imam Ali bin Abi Talib [a] alipanda mnyama wake baada ya kumalizika vita vya Jamal huko Basra, kisha akawa anapita katikati ya watu waliouawa mpaka akapita mahali alipokuwa kaangukia Kaab bin Suur ambaye alikuwa Qadhi wa Basra tangu zama za Omar bin Khatab na Uthman, na ilipotokea fitna huko Basra, Bwana huyu na watu wake na mwanawe walitaka kupigana dhidi ya Imam Ali[a.s] ambaye alikuwa Khalifa wa Mtume na Imam wa zama zake na wote wakauawa.

Imam Ali[a.s] alipofika hapo alipolala Bwana huyu akasimama akawaambia watu waliokuwa karibu naye: "Mkalisheni Kaab bin Suur". Wakamkalisha huku watu wawili wamemshikilia. Imam Ali[a.s] akasema: "Ewe Kaab bin Suur hakika mimi nimeyakuta aliyoniahidi Mola wanga kuwa ni ya kweli, basi je wewe umeyakuta aliyokuahidi Mola wako kuwa ni ya kweli?" Kisha Imam Ali[a.s] akasema: "Mlazeni". Akaenda mbele kidogo akafika mahali alipokuwa ameangukia Tal-ha bin Abdallah akasema: "Mkalisheni Tal-ha". Wakamkalisha na akasema tena Imam Ali[a.s] "Ewe Talha hakika mimi nimeyakuta aliyoniahidi Mola wangu kuwa ni ya kweli, basi je wewe umeyakuta aliyokuahidi Mola wangu kuwa ni ya kweli?" Kisha akawaambia; "Mlazeni Tal-ha". Mtu mmoja akamwambia Imam Ali[a.s] "Ewe Amirul Muuminina yanafaida gani maneno yako uliyowaambia maiti hawa wawili hali wao hawakusikii?" Imam Ali[a.s] akasema: "Ewe mtu, Wameyasikia maneno yangu kama vile watu wa kisima (cha Badri) walivyoyasikia maneno ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu".[181]

MATOKEO YA UCHUNGUZI

Yafuatayo ni maelezo kwa kifupi juu ya uchunguzi wa maudhui hii:

1. Tumethibitisha ndani ya ile maudhui ya kwanza kwamba kifo siyo mwisho wa uhai, wala haimaanishi kuwa ndiyo kutoweka kwa mtu, bali kifo ni njia apitayo mtu kuelekea ulimwengu mwingine.

2. Tumethibitisha ndani ya maudhui hii ya pili kwamba, uhakika wa mtu ni roho yake, na kwamba mwili si chochote bali ni vazi linaloifunika roho. Na kubakia kwa roho maana yake ni kubakia kwa utu wa mtu na ukamilifu wa maana halisi ya mtu, ukiondoa uwezo wa kimatendo ambao hutoweka kwa kutoweka mwili. Na kwa msingi huu, iwapo nafsi ya mtu na roho yake itakuwa inao uwezo wa kuomba na kufanya mambo ya muujiza wakati wa uhai wake (duniani) basi roho yake vile vile inao uwezo wa kuyatenda matendo yote hayo baada ya kufa kwake kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

3. Na katika maudhui ya tatu tumethibitisha kuwepo uwezekano wa maungamano na ulimwengu mwingine, isitoshe tumethibitisha kuwepo maungamano hayo duniani na kwamba roho zilizoko huko zinauwezo wa kusikia maneno yetu tunapozisemesha, na wala hakuna tofauti kati ya roho za watu wema na waovu katika kusikia maneno kama ambavyo tumeeleza matukio ya aina hiyo katika Qur'an na historia. Baada ya kuyafahamu mambo haya matatu inathibiti kwamba Mawali wa Mwenyezi Mungu wanasikia maneno yetu tunapowasemesha, na pindi Mwenyezi Mungu anapowapa idhini ya kutujibu basi huwa wanaturudishia majibu. Swali lililopo hapa sasa hivi ni: Je, inafaa kwa mujibu wa sheria kuzisemesha roho za Mawalii wa Mwenyezi Mungu na kuziomba msaada? Insha-Allah jawabu litakujia katika jambo la nne lifuatalo.

WAISLAMU NA KUZIOMBA MSAADA ROHO TAKATIFU

Ibnu Taimiyya na wafuasi wake walifanya pupa kutoa hukmu pale walipopinga wakasema, "Masahaba na Tabiina hawakumuomba msaada Mtume[s.a.w.w] ". Watu hawa (Ibn Taimiyya na wafuasi wake) wanasema, "Hapana mtu yeyote miongoni mwa salafu wa umma huu waliotangulia katika zama za Masahaba wala zile za Tabiina wala wale waliofuatia baada ya Tabiina waliokuwa wa kiswali na kuomba dua kwenye makaburi ya Manabii au kuwaomba Manabii hao wala hawakuomba msaada wao wanapokuwa hawapo, wala kwenye makaburi yao.[182] Huenda mtu asiyefahamu historia ya Masahaba na Tabiina akahadaika kwa maneno haya na akayaona kuwa ni ya kweli na sahihi. Lakini iwapo ataiangalia historia kwa makini na akasoma juu ya Masahaba na wengineo kutawas-sal kwa Mtume[s.a.w.w] na kumuomba kwao msaada, utamthibitikia uongo wa madai haya. Hebu tazama mifano ifuatayo:

1. Watu walipatwa na ukame katika zama za Omar bin Al-Khatab, mtu mmoja akaenda kwenye kaburi Ia Mtume[s.a.w.w] na akasema, "Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, waombee umati wako kwa Mwenyezi Mungu wapate mvua, kwani wemekwisha angamia, basi Mtume alimjia mtu huyo usingizini akamwambia, nenda kwa Omar mwambie watapata mvua".[183]

Baada ya kutaja kisa hiki As-samhudi anasema: "Mahali penye ushahidi ni pale Mtume alipoombwa awaombee watu wake mvua hali akiwa katika ulimwengu wa Bar-zakh, na Mtume kumuomba Mola wake akiwa katika hali hiyo siyo jambo lisilowezekana, na imekuja katika hadithi kwamba Mtume anafahamu ombi Ia anayemuomba basi hakuna kizuiwizi kumuomba awaombee mvua na mengineyo kama alivyokuwa akifanya zama za uhai wake duniani.[184]

2 As-samhudi amepokea vile vile kutoka kwa Al-hafidh Abu Abdillahi Muhammad bin Musa bin Nuuman kwa Sanad inayoishia kwa Imam Ali[a.s] : "Hakika bedui mmoja alikuja Madina baada ya siku tata tangu kuzikwa Mtume[s.a.w.w] , akajitupa kwenye kaburi la Mtume na akajipaka udongo wa kaburi hilo kichwani na akasema, ewe Mtume ulisema tukasikia maneno yako na ulipokea toka kwa Mola wako nasi tukapokea toka kwako, na miongoni mwa yaliyoteremshwa kwako ni "Na lau wangekujia walipojidhulumu nafsi zao wakaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu na Mtume naye akawaombea msamaha bila shaka wangemkuta Mwenyezi Mungu ni mwenye kupokea toba na mwenye kurehemu", nami nimeidhulumu nafsi yangu, na nimekujia (Ewe Mtume) uniombee msamaha".[185] Ewe msomaji mtukufu, As-Samhudi anataja katika kitabu chake kiitwacho Wafaul-wafai ndani ya mlango wa nane, matukio mengi na yote yanajulisha kwamba kumuomba msaada Mtume[s.a.w.w] ulikuwa ni mwenendo unaoendelea kwa Waislamu kiasi amesema huyu Samhudi kwamba, Imam Muhammad bin Nuuman ameandika kitabu juu ya maudhui haya kiitwacho: Misbahudhalami fil-mustaghithina Bikhairil-anam".

3. Muhammad bin Al-munkadir anasema: "Mtu mmoja aliwekeza kwa baba yangu Dinari thamanini, kisha akaenda kwenye Jihadi na akamwambia baba yangu, iwapo utakuwa na haja nazo basi zitumie mpaka nitakaporudi, baadaye watu walipatwa taabu ya kupanda thamani ya vitu baba yangu akazitoa Dinari zile na yule mtu aliporudi alitaka apewe Dinari zake. Baba yangu akamwambia njoo kesho, (baba yangu) alilala msikitini, akawa mara analikumbatia kaburi la Mtume[s.a.w.w] na wakati mwingine kwenye mimbari ya Mtume[s.a.w.w] mpaka karibu ya kupambazuka, hali akiomba msaada kwenye kaburi Ia Mtume[s.a.w.w] . Wakati akiwa katika hali hiyo ghafla alitokea mtu katika giza akasema chukua ewe Abu Muhammad, basi baba yangu akanyoosha mkono na akapokea mfuko ambao ndani yake ulikuwa na dinari themanini". "Kulipokucha yule mtu alikuja na akampa dinari zake". [186]

4. Anasema Abubakar Al-muqri: "Nilikuwa mimi na At-tabrani na Abus-shaikh katika msikiti wa mjumbe wa Mwenyezi Mungu[s.a.w.w] na tulikuwa katika hali fulani na njaa ilikuwa imetuathiri, siku hiyo tukaimaliza na ulipofika wakati wa I'sha nilikwenda kwenye kaburi la Mtume[s.a.w.w] nikasema, Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (nahisi) njaa.... Basi alikuja mlangoni sharifu akagonga na tukamfungulia, kumbe alikuwa pamoja na vijana wawili ambao kila mmoja wao ana kikapu ndani yake mna vita vingi tukakaa tukala na tukadhani kwamba vilivyobaki vitachukuliwa na mmoja wa vijana hao, lakini aliondoka na kutuachia hivyo vilivyobakia. Tulipomaliza kula akasema yule Sharifu, Je, Nyie watu mmemlalamikia mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Kwani mimi nimemuona Mtume[s.a.w.w] usingizini akaniamuru nikuleteeni chochote". [187]

5. lbn Jal-laad anasema: "Niliingia Madina mji wa Mtume[s.a.w.w] hali ya kuwa nina njaa, basi nikaenda kwenye kaburi la Mtume[s.a.w.w] nikasema mgeni wako, (baada ya muda) nikasinzia na nikamuona Mtume[s.a.w.w] akinipa mkate nikaula nusu yake, nilipozinduka nikaiona ile nusu nyingine iko mkononi mwangu." [188] Sasa hivi hatujadili matukio haya yaliyotajwa na kubainisha usahihi wake au makosa yake, bali tunachozungumzia ni kuwa, matukio yote haya kwa ujumla yanashuhudia kwamba kumuomba msaada Mtume[s.a.w.w] ni jambo ambalo lilikuwa likitendeka miongoni mwa Waislamu. Na lau lingekuwa ni uzushi na ni haramu au ni shiriki au ni kufuru hata hao wazushi wa hadithi wasingelisema kwa kuchelea kuharibu heshima zao miongoni mwa watu. Na kutokana na ukweli wa jambo hili sisi tumeandika kitabu makhususi kuhusu jambo hili kiitwacho: "Isalatur-ruuh" na humo tumezungumza kwa upana kila kinachofungamana na maudhui haya, na tumeleta hadithi na mapokezi mengi, na yote yanajulisha juu ya kusihi kuomba mahitaji kupitia kwenye roho tukufu na pia kusihi kuomba kutekelezwa kwa jambo ambao likokinyume na maumbile ya kawaida. Na kwa kukamilisha mlango huu tunaleta uzindushi kwenye mambo yafuatayo:

1. Kuwaomba msaada Mawalii wa Mwenyezi Mungu kamwe siyo kuwaabudu, na hasa baada ya kuwa tumeieleza kwa upana maana ya neno Ibada, na linavyotumika neno lenyewe na kwamba kuitakidi uungu (katika kutenda) ndiyo jambo ambalo hulipa picha ya Ibada tendo linalotendwa. Na jambo lililo wazi ni kwamba mtu anaye tawa-sal kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu huwa hana itikadi kwamba Mawalii hao ni Miungu na wala haitakidi kwamba wao ndio wanaosimamia mambo ya ulimwengu na wala kutenda matendo ya Mwenyezi Mungu kwa uhuru bila kumtegemea Mwenyezi Mungu bali anawafahamu tu kuwa wao ni waja watukufu walio wema mbele ya Mwenyezi Mungu wasiotenda japo dhambi ndogo au maasi.

2. Mambo manne yaliyotajwa hapo kabla yamethibitisha tena kwa hoja na dalili kwamba, Mawalii wa Mwenyezi Mungu wanao uwezo wa kukidhi haja ya mwenye kutawas-sal kwa kuwa wao wako hai mbele ya Mwenyezi Mungu, na kwamba kila kinachotoka kwao huwa ni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa hiyo basi wao ndio thibitisho la kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema "Na hamtataka (kitu kiwe) mpaka Mwenyezi Mungu atake (kiwe kitakuwa). Kwa mfano: Nabii Isa[a.a.w.w] ambaye katika zama za uhai wake na maisha ya duniani alikuwa akimuomba Mwenyezi Mungu amjaalie kheri mtu amtakaye, au kuwaponya vipofu na wenye mbaranga kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, vile vile Nabii Isa[a.s] anao uwezo wa kufanya hivyo baada ya kuhamia kwenye ulimwengu wa Bar-zakh kwa kuwa roho yake inaendelea kubakia, nayo ndiyo hakika yake yeye Nabii Isa[a.s] .

3. Kuheshimu na kunyenyekea mbele ya makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu ni kumheshimu Mwenyezi Mungu, japokuwa dhahiri inaonekana kuwa ni kumheshimu walii aliyezikwa hapo, lakini lau tutaufungua moyo wa huyu mwenye kutoa heshima na unyenyekevu huo tungemuona anamnyenyekea Mwenyezi Mungu kupitia kwa Walii huyo mwema, na kwamba yeye anaomba maombi yake kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwa Walii huyu. Kwa hiyo basi, kutawas-sal kwa kupitia sababu ndiyo huko huko kutawas-sal kwa aliyesababisha sababu hizo ziwepo naye ni Mwenyezi Mungu Mtukufu. Jambo hili liko wazi kwa watu wenye kuchunguza na kufahamu.

Nawe msomaji lau utamuuliza huyu anayetawas-sal kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu kwamba ni jambo gani limemfanya atawas-sal kwa Walii? Haraka sana atakujibu kuwa "Walii huyo ni wasila (njia) ya kumfikisha kwa Mwenyezi Mungu kama alivyosema Mwenyezi Mungu, "Enyi mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu na mutafute wasila wa kukufikisheni kwake, na mupiganie katika njia yake ili mupate kufaulu".[189] Hali ni ile ile mtu anapotawas-sal kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwenye Sala, Saumu, Ibada na mengineyo ya wema, ndiyo hivyo hivyo anavyotawas-sal kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mawalii wema waliotukuzwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Kwa ufupi, muumini anaitakidi katika nafsi yake kuwa, kutawas-sal kwake kupitia kwa Mtume[s.a.w.w] na wengineo miongoni mwa maasumina na watu wema huwa kunamfanya huyo anayefanyiwa tawasuli hiyo kumuomba Mwenyezi Mungu akubali maombi ya yule aliyetawas-sal, sawa sawa kama tawasuli hiyo itakuwa ni kutaka kusamehewa madhambi au kulipa deni, kuponya maradhi, au kupata maisha mazuri na mengineyo.