UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI0%

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Vitabu mbali mbali

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi: SHEIKH JA'AFAR SUBHANY
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 48034
Pakua: 4111

Maelezo zaidi:

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 24 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 48034 / Pakua: 4111
Kiwango Kiwango Kiwango
UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi:
Swahili

16

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

KUITAKIDI UWEZO WA GHAIB WA MAWALII WA MWENYEZI MUNGU

Je, kuitakidi kwamba Mawalii wa Mwenyezi Mungu wanao uwezo wa ghaib ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu? Bila shaka hakuna wasi wasi kwamba, mtu hawezi kuomba haja yake kwa yeyote yule ila atakapokuwa na uhakika wa uwezo wa huyo amuombaye kuwa atamtimizia haja yake na kutekeleza ombi lake. Uwezo huu umegawika sehemu mbili:

1. Uwezo wa kimaada unaoonekana kama vile kumuomba maji mtu fulani kisha akakujazia maji hayo kwenye chombo na akakupatia.

2. Uwezo wa ghaib uliojitenga na mazingira ya maada ulio nje ya matendo ya kimaumbile, kwa mfano mtu akaamini kwamba, Imam Ali bin Talib[a.s] anao uwezo wa kuung'oa mlango wa Khaibar, ambao kwa kawaida mtu hawezi kuung'oa bali yeye Imam Ali[a.s] anaweza kwa kutumia nguvu ya ghaibu ambayo iko juu kuliko uwezo wa watu. Au mtu akaamini kwamba Nabii Isa[a.s] kwa maombi yake ya kumponya mgonjwa ambaye ugonjwa wake umeshindikana kupona, lakini Nabii Isa anamponya mgonjwa huyo bila kutumia dawa yoyote au kufanya operesheni. Kama umeifahamu mifano hii, basi fahamu pia kwamba kuamini uwezo wa ghaibu ikiwa uliotegemezewa kwenye uwezo wa Mwenyezi Mungu na idhini yake na kutaka kwake, ni sawa na kuitakidi uwezo ulioko katika maumbile ya mazingira ya kimaada na wala siyo kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani yeye Mwenyezi Mungu ndiye muweza wa kumpa mtu uwezo wa mazingira ya kimaada na ndiye anayempa mwingine uwezo wa ghaibu. Na katika kuamini jambo hili inatakiwa pasiwe na imani kwamba, kiumbe aliyepewa uwezo huu yeye hahitajii msaada na uwezo wa Mwenyezi Mungu.

MAONI YA KIWAHABI

Wawahabi wanaitakidi kwamba, lau mtu atamuomba haja fulani mmoja wa Mawalii wa Mwenyezi Mungu, awe hai Walii huyo au aliyekwisha fariki, kwa mfano, akamuomba amponye maradhi yake au amrejeshee kitu chake kilichopotea, na au kumlipia deni lake na mengineyo, basi mtu huyo atakuwa ameamini kuwepo uwezo wa siri kwa huyo aliyemuomba kiasi cha kuwa anaweza kwa uwezo huo kukiuka kanuni za kimaumbile zitumkazo katika ulimwengu huu. Na kwa ajili ya kuitakidi uwezo huu kuwa anao mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi itakuwa ni kuamini uungu wa huyo asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kumuomba pamoja na itikadi hii ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa kufafanua ni kwamba: Kwa maoni ya Kiwahabi; lau mtu yuko jangwani na ana kiu ya maji, kisha akamuomba mtumishi wake ampe maji, ombi hili halikiuki kanuni za kimaumbile na linafaa na siyo shiriki. Ama ikiwa mtu ataomba ombi kama hili hili kumuomba Mtume au Imam ambaye amezikwa au anayeishi sehemu nyingine katika mji mwingine au akawa hayupo machoni mwake, basi ombi hilo ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kuwa ameitakidi kwamba Nabii huyo au Imam huyo anaweza kumtatulia shida ya maji kinyume na mfumo wa kanuni na sababu za kimaumbile, yaani kumpa uwezo wa siri. Na itikadi hii ni kuitakidi uungu kwa huyo anayeombwa ikiwa ni Nabii au Imam. Maoni haya ya Kiwahabi ameyafafanua zaidi mwandishi wa Kiwahabi aitwaye "Abul-aala Al-maududi" akasema: "Bila shaka sifa ambayo kwayo mtu humuomba Mola na kumtaka msaada na kumnyenyekea lazima itakuwa ni ile sifa ya kuwa kwake yeye Mola ndiye mwenye kumiliki uwezo wa kusimamia kanuni za maumbile".

MAONI YETU JUU YAMANENO HAYA

Bila shaka kosa alilolifanya Maududi na wengineo kama yeye ni kwamba, yeye ameona kuwa kuamini kuwepo uwezo wa siri kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni kumshirikiisha Mwenyezi Mungu moja kwa moja, na hakutofautisha au hakutaka kutofautisha baina ya kuamini uwezo huo wa siri unaotoka kwa Mwenyezi Mungu na kumtegemea yeye na ule uwezo ambao haumuhitajii Mwenyezi Mungu, wakati ambapo ushirikina ni hii itikadi ya pili siyo ile ya kwanza (yaani uwezo wa kutokumuhitajia Mwenyezi Mungu). Nayo Qur'an Tukufu inataja wazi wazi majina ya watu ambao walikuwa nao uwezo wa siri, na matakwa yao yalikuwa yakienda kinyume na kanuni za kawaida na kuzibadilisha nyendo zake. Hebu angalia baadhi ya majina ya watu ambao Qur'an imewataja:

1). UWEZO WA SIRI WA NABII YUSUF[a.s]

Nabii Yusuf[a.s] aliwaambia nduguze:

اذْهَبُوا بِقَمِيصِي هَـٰذَا فَأَلْقُوهُ عَلَىٰ وَجْهِ أَبِي يَأْتِ بَصِيرًا وَأْتُونِي بِأَهْلِكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٩٣﴾

"Nendeni na kanzu yangu hii na muiweke usoni mwa baba yangu, yeye atafunuka macho aone; basi alipokuja mtoaji wa habari ujema akaiweka (kanzu ya Yusuf) usoni mwake mara aliona". Qur'an, 12:93 na 96.

Dhahiri ya aya inayoonyesha kwamba Nabii Yaaqub[a.s] macho yake yalirudi (akaona) kikamilifu kutokana na uwezo wa siri alioutumila Nabii Yusuf[a.s] ili kuyarejesha macho hayo. Ukweli ulivyo ni kwamba kurejea kwa macho ya Nabii Yaaqub[a.s] hakukutokana na Mwenyezi Mungu kwa sura ya moja kwa moja, bali liliwezekana jambo hilo kwa idhini yake Mwenyezi Mungu lakini kupitia kwa Nabii Yusuf[a.s] . Kwa hiyo basi, Nabii Yusuf[a.s] yeye alikuwa ndiye sababu ya kurudi macho ya baba yake kikamilifu, na lau si hivyo basi asingewaamuru nduguze waende na kanzu yake na kuiweka usoni mwa baba yake bali angemuomba Mwenyezi Mungu tu ili jambo hilo litimie. Hii bila shaka ndiyo nguvu ya siri iliyotoka kwa Nabil Yusuf[a.s] mmoja wa Mawalii wa Mwenyezi Mungu, na alibadilisha mwenendo wa kawaida kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na hapana yeyote awezaye kutenda hivi isipokuwa yule tu aliyepewa na Mwenyezi Mungu uwezo huo wa siri.

2). UWEZO WA SIRI WA NABII MUSA[a.s]

Mwenyezi Mungu alimpa Nabii Musa[a.s] uwezo wa siri pale alipolipiga jiwe kwa fimbo yake na zikapasuka chemchem kumi na mbili kufuatia idadi ya makabila ya wana wa Israil kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

فَقُلْنَا اضْرِب بِّعَصَاكَ الْحَجَرَ فَانفَجَرَتْ مِنْهُ اثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا ﴿٦٠﴾

"Tulimwambia (Musa) lipige jiwe kwa fimbo yako, basi (alipopiga) zilipasuka chemchem kumi na mbili". Qur'an, 2:60.

Nabii Musa[a.s] pia alitumia uwezo wake wa siri kwa mara nyingine pale alipoipiga bahari kwa fimbo yake ili afungue njia kumi na mbili zilizo kavu ndani ya bahari wapate kupita wana wa Israel na waivuke bahari hiyo, (baada ya kuipiga) maji yalijikusanya kama milima pembeni ya njia hizi bila ya kurukia japo tone dogo la maji njiani!!! Mwenyezi Mungu anasema:

فَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنِ اضْرِب بِّعَصَاكَ الْبَحْرَ فَانفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرْقٍ كَالطَّوْدِ الْعَظِيمِ ﴿٦٣﴾

"Basi mara tulimpelekea Musa ufunuo (Wahyi) tukamwambia, ipige bahari kwa fimbo yako, (alipopiga) ikatengana na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa". Qur'an, 26:63.

Ndani ya sehemu mbili hizi haiwezekani kabisa kujifanya hatujuwi nafasi ya Nabii Musa [a.s] katika kupasua chemchem na kufungua njia ndani ya bahari, na kufaidika kwa nguvu yake ya siri, yote haya yalithibitika kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na kutaka kwake.

3). UWEZO WA SIRI WA NABII SULEIMAN[a.s]

Ni mara nyingi Nabii Suleiman[a.s] alikuwa akinufaika kwa uwezo wa siri, na ameielezea zawadi hiyo tukufu ya Mwenyezi Mungu ambayo amepewa kwa kauli yake mwenyewe kama ilivyo ndani ya Qur'an Tukufu. "Na tumepewa kutokana na kila kitu ". Qur'an, 27:16.

Ufafanuzi wa maelezo ya zawadi na uwezo aliopewa Nabii Suleiman[a.s] umo ndaji ya sura ya An-namli kuanzia aya ya 16 hadi aya ya 44, na sura Sabai aya ya 12, pia sura Anbiyaa aya ya 81 na sura Saad kuanzia aya ya 36 hadi aya ya 40. Bila shaka kufanya mazingatio katika aya hizi kutatudhihirishia wazi zawadi hizi tukufu na uwezo wa siri ambao Mwenyezi Mungu amempa mja wake na Nabii wake Suleiman[a.s] . Na kabla hujaifungua Qur'an ili kuzisoma aya zilizoashiriwa, hapa tunakutajia baadhi ya aya hizo ili ikukalie wazi hali ya utukufu wa uwezo huo wa siri, na uone kwa macho yako kwamba Qur'an Tukufu inavyouthibitisha uwezo huo wa siri kwa baadhi ya waja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nabii Suleiman[a.s] alikuwa na mamlaka juu ya majini na ndege, pia alikuwa akifahamu semi za ndege na lugha za wadudu. Mwenyezi Mungu anasema:

وَوَرِثَ سُلَيْمَانُ دَاوُودَ وَقَالَ يَا أَيُّهَا النَّاسُ عُلِّمْنَا مَنطِقَ الطَّيْرِ وَأُوتِينَا مِن كُلِّ شَيْءٍ إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْفَضْلُ الْمُبِينُ ﴿١٦﴾ وَحُشِرَ لِسُلَيْمَانَ جُنُودُهُ مِنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ وَالطَّيْرِ فَهُمْ يُوزَعُونَ ﴿١٧﴾ حَتَّىٰ إِذَا أَتَوْا عَلَىٰ وَادِ النَّمْلِ قَالَتْ نَمْلَةٌ يَا أَيُّهَا النَّمْلُ ادْخُلُوا مَسَاكِنَكُمْ لَا يَحْطِمَنَّكُمْ سُلَيْمَانُ وَجُنُودُهُ وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿١٨﴾ فَتَبَسَّمَ ضَاحِكًا مِّن قَوْلِهَا وَقَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ ...﴿١٩﴾

"Na Suleiman alimrithi Daudi na akasema, Enyi watu tumefundishwa (hata kutambua) semi za ndege na tumepewa kutokana na kila kitu, hakika huu ni ukarimu wa Mwenyezi Mungu uliyo wazi, na alikusanyiwa Suleiman majeshi yake miongoni mwa majini na watu na ndege nayo yakapangwa makundi makundi, hata walipofika katika bonde la wadudu "chungu" alisema mdudu chungu (kuwaambia wenziwe) ingieni majumbani mwenu asikupondeni Suleiman na majeshi yake hali ya kuwa hawana khabari, basi (Suleiman) akatabasamu akilichekelea neno lake (yule chungu) na akasema Ee Mola wangu, nipe nguvu nikushukuru neema yako uliyonineemesha mimi na wazazi wangu...." Qur'an,27:16, 17, 18, 19 na kuendelea.

Ewe msomaji mtukufu lau utaisoma Qur'an juu ya kisa cha ndege "Hud-Hud" ambaye Nabii Suleiman[a.s] alimtuma kwa Malkia wa Sabai apeleke barua kutoka kwake kwenda kwa Malkia huyo, utakupata mshangao kutokana na nguvu hiyo ya siri aliyokuwa nayo Nabii Suleiman[a.s] . Kwa hiyo tunataraji utafanya mazingatio katika aya ya 20 mpaka ya arobaini na nne ndani ya Surat An-namli ili upate nguvu ya kuyakanusha na kuyabatilisha madhhebu ya Kiwahabi yanayopingana na Qur'an. Isitoshe zaidi ya hayo ni kwamba Nabii Suleiman[a.s] kwa mujibu wa ufafanuzi wa Qur'an alikuwa na mamlaka juu ya upepo ambao ulikuwa ukivuma apendavyo kwa amri yake. Mwenyezi Mungu anasema:

وَلِسُلَيْمَانَ الرِّيحَ عَاصِفَةً تَجْرِي بِأَمْرِهِ إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا وَكُنَّا بِكُلِّ شَيْءٍ عَالِمِينَ ﴿٨١﴾

"Na kwa Suleiman (tukaupa utii) upepo wa nguvu ukavuma kwa amri yake katika ardhi ambayo tumeibarikia nasi ndio tunaokijua kila kitu". Qur'an, 21:81.

Yeyote mwenye kuweka mazingatio kwenye aya hii "unavuma kwa amri yake", ambayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu, (ataona) inajulisha uwezo wa siri wa Nabii Suleiman[a.s] juu ya upepo na kuuhukumu kwake katika njia zake na nyendo zake.

4). NABII ISA[a.s] NA UWEZO WA SIRI

Tunaweza kuufahamisha uwezo wa siri wa Nabii Isa[a.s] kwa kupitia mazingatio tunayoweza kuyapata katika aya za Qur'an zinazomzungumzia Nabii Isa[a.s] na uwezo huo. Miongoni mwa aya hizo ni kauli ya Mwenyezi Mungu akimnakili Nabii Isa[a.s] :

أَنِّي أَخْلُقُ لَكُم مِّنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ فَأَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِ اللَّـهِ وَأُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ وَأُحْيِي الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِ اللَّـهِ وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأْكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمْ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٤٩﴾

"Bila shaka mimi nakuumbieni kutokana na udongo kama sura ya ndege, kisha nampulizia na mara anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ninawaponyesha vipofu na wenye mbaranga, ninawafufua (baadhi ya) waliokufa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na nitakwambieni mtakavyovila na mtakavyoweka akiba katika nyumba zenu, bila shaka katika haya imo hoja kwenu ikiwa ninyi ni watu wa kuamini". Qur'an, 3:49.

Katika aya hii neno "kwa idhini ya Mwenyezi Mungu" limerudiwa mara mbili ili kutia mkazo kwamba matumizi ya uwezo wa siri ambao Mawalii wa Mwenyezi Mungu huutumia, huwa yanatokana na uwezo wa Mwenyezi Mungu na kutaka kwake. Ndiyo maana unamuona Nabii Isa[a.s] katika aya hii anauzingatia uwezo wake wote kuwa umo ndani ya udhibiti wa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Basi hali ni kama hii hii kwa Manabii wa Mwenyezi Mungu na Mawalii. Mwenyezi Munga anasema:

وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأْتِيَ بِآيَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ﴿٣٨﴾

"Na haiyumkiniki kwa Mtume kuleta muujiza isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu". Qur'an, 13:38.

Pamoja na hayo, utamuona Nabii Isa[a.s] anayanasibisha matendo yake yote ya uwezo huo wa siri kwenye nafsi yake tukufu anasema, "Naumba" "Napuliza" "Naponya" "Nafufua" 'Nakwambieni" yote ameyatamka kwa dhamiri ya msemaji mmoja. Kwa hiyo basi, Manabii Yusuf, Musa, Isa na Suleiman [a] siyo wao peke yao ambao walikuwa na uwezo wa siri, bali wako Manabii wengi ambao walikuwa na bado wanaminiliki uwezo huo, na kulitafiti jambo hili kwa upana kunahitaji kitabu makhsusi kuzungumzia jambo hili, nasi tumelizingumzia kwa upana katika kitabu kiitwacho "Al-qudratul-maanawiyya Lil-anbiyaa" na kimechapishwa mara nyingi.

5). UWEZO WA SIRI WA MALAIKA

Bila shaka Malaika nao pia wananufaika kuta uwezo wa siri. Hii hapa Qur'an inamsifu Malaika Jibril kwa kusema, "Mwenye nguvu sana ". Qur'an, 53:5.

Na inawasifu baadhi ya Malaika inasema: "Wakazitengenezea mambo yake " Qur'an, 79:5. Na aya nyingine zaidi ya hizo mbili ambazo zimeeleza wazi wazi au zinaashiria kwamba, Malaika wanasimamia uendeshaji wa mambo ya ulimwengu ikiwa ni pamoja na kutoa roho na kuwalinda watu na kuandika matendo (ya watu) "waandishi watukufu" na kuangamiza nyumati zenye maovu na mengineyo miongoni mwa majukumu ya ulimwengu huu. Bila shaka kwa kiIa mwenye kuifahamu vyema Qur'an japo kidogo anafahamu kwamba Malaika wanao uwezo wa siri na kwamba wanautumia kimuujiza kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na nguvu zake. Basi lau kuamini nguvu hizo za siri kungelazimiana kuamini uungu (wa mwenye nguvu hizo) basi Mitume wote na Malaika wangekuwa ni waungu kinyume cha Mwenyezi Mungu, jambo ambalo haliwezekani kabisa.

BASI NINI UFUMBUZI WAKE NA NI IPI KAULI ILIYO SAWA

Hakika tumekwisha taja kuwa ufumbuzi na kauli ya sawa, ni kutenganisha baina ya uwezo wa kujitegemea na ule wa kupewa. Kuamini kuwa uwezo wa kujitegemea kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, wakati ambapo kuamini uwezo wa kupewa (na Mwenyezi Mungu) katika nyanja yoyote ile, hiyo ndiyo Tauhidi yenyewe. Mpaka hapa ewe msomaji, imekubainikia kwamba, kuamini kuwepo uwezo wa siri kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu haiwezi kuwa ni shirki, bali hiyo ndiyo Tauhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) hasa, lakini kwa sharti kwamba mtu aitakidi uwezo huo umetegemezewa kwa Mwenyezi Mungu ambao ni uwezo wa milele, na katika hali kama hii imekubainikia vile vile kwamba, maana ya Tauhidi siyo kuviegemezea vitendo vya kimaumbile kwa mtu na vile vya siri kuviegemezea kwa Mwenyezi Mungu, bali Tauhidi halisi ni kuviegemeza vitendo vyote kwa Mwenyezi Mungu na inafahamika kuwa nguvu na uwezo vyote vinaanzia na kumalizikia kwake Mwenyezi Mungu. Na sasa ndiyo umefika ule wakati wa kuzungumzia ile nguzo ya pili katika mlango huu, nayo ni ile inayozungumzia kufaa kuwaomba Mawalii wa Mwenyezi Mungu mambo ya siri yasiyowezekana (katika maumbile yetu ya kawaida).

KUWAOMBA MAWALII MATENDO YA GHAIBU

Je, inafaa kumuomba mmoja wa Mawalii wa Mwenyezi Mungu matendo ya muujiza? Na je, ombi kama hilo ni ushirikina? Kwa kuanza tunasema: "Kila tukio linayo sababu yake", kini ambacho hakuna khitilafu yoyote ulimwengu mzima, hivyo basi kila kitu hakiwezi kuwa ila ni kwa sababu, kwani maisha tunayoishi ni maisha ya sababu na visababishwaji, zaidi ya hapo ni kwamba hakipatikani chenye kupatikana ulimwenguni kote ila kutakuwa na sababu yake. Vile vile miujiza ya Manabii na karama za Mawalii haziwezi kutokea pasina sababu, isipokuwa sababu zake siyo za kimaumbile, bali zimefichikana na ziko nje ya maada na ziko juu ya kiwango (chetu) cha maarifa. Kwa mfano, ilipogeuka fimnbo ya Nabii Musa na kuwa nyoka, au Nabii Isa alipokuwa akifufua wafu naye Mtume[s.a.w.w] mwezi uliposuka kwa ajili yake na zilifanya Tasbihi tembe za mchanga mkononi mwake na miujiza mingineyo ya Manabii, yote hii haikutoka bila ya sababu yoyote, lakini sababu iliyosababisha kutokea kwake kama tulivyokwisha sema siyo sababu ya kimaumbile tunayoweza kuidiriki (kuiona) kwa macho yetu lakini siyo kwamba yote haya yamefanyika bila sababu, bali sababu yake iko nje ya maada.

Baada ya maelezo haya mafupi, sasa tuzungumzie maudhui inayohusika, nayo ni ile ya kuwaomba Mawalii wa Mwenyezi Mungu matendo ambayo ni ya kimiujiza yaliyo kinyume na maumbile ya kawaida. Bila shaka Mawahabi wapotofu na kwa upotevu wao wanapoteza (umma) wanadai kwamba, kuomba (kwa Mawalii) matendo ambayo yako kinyume na maumbile ni kumshirkisha Mwenyezi Mungu, lakini kuomba mambo ya kawaida katika maumbile (yetu) siyo ushirikina. Basi Je, nini maoni ya Uislamu juu ya madai haya? Jawabu: Qur'an hii tukufu ndiyo muongozo bora ambao tutapata kwayo uamuzi kwani utaiona Qur'an mahala pengi tu imeweka wazi jambo hili kwa kuwataka Manabii na wengineo wasimamie mambo yaliyo nje ya kanuni za kawaida ya maumbile. Kwa mfano: Watu wa Nabii Musa[a.s] walimuomba awape maji na mvua na awaokoe kutokana na ukame ambao ulikuwa ukiwasumbua, na hapo ikatoka amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuitikia maombi yao akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ إِذِ اسْتَسْقَاهُ قَوْمُهُ أَنِ اضْرِب بِّعَصَاكَ الْحَجَرَ ﴿١٦٠﴾

"Na tukampelekea wahyi Musa, pale watu wake walipomuomba maji (tukamwambia) lipige jiwe kwa fimbo yako." Qur 'an, 7:160.

Iwapo mtu atasema "Hapana kizuwizi kumuomba muujiza mtu aliye hai, basi utafiti ufanywe juu ya kumuomba maiti". Je, Inafaa? Jawabu litakuwa: Bila shaka uhai na kifo haviibadili hakika ya Tauhidi na shirki, kiasi kwamba kitu kiwe ni Tauhidi wakati wa uhai na kiwe ni shirki katika hali ya ufu, au kinyume cha hivi, bali hakika ya Tauhidi inabaki pale pale katika hali zote". Naam,..... inawezekana kukawa na athari Fulani kwa uhai na mauti katika (kupatikana) faida ya maombi au kukosekana, kitu ambacho hakiathiri ukweli wa Tauhidi na shirki.

NABII SULEIMAN[a.s] ANAOMBA (KULETEWA) KITI CHA BIL-QIIS

Qur'an Tukufu inatusimulia kwamba Nabii Suleiman[a.s] aliwaomba waliokuwa wamehudhuria mbele yake kwamba, mmoja wao amletee kiti cha enzi cha Bil-qiis kwa kutumia uwezo wa ghaibu na kinyume cha maumbile. Nabii Suleiman[a.s] akawaambia kama ilivyo ndani ya Qur'an: "Nani kati yenu atakayeniletea kiti chake cha enzi kabla hawajaja kwangu hali ya kuwa wamekwisha silimu? Mjasiri mmoja miongoni mwa majini akasema, mimi nitakuletea kabla hujainuka mahali pako hapo, na bila shaka ninazo nguvu za (kutenda) hayo na nimuaminifu. Akasema yule aliyekuwa na elimu kutoka katika kitabu; "Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako," basi alipokiona kimewekwa mbele yake, (Nabii Suleiman) alisema "Haya yote ni kwa fadhila za Mola wangu ". Qur'an, 27:38-40.

Ikiwa madh-hebu ya Mawahabi yatasihi kuharamisha kumuomba yeyote asiyekuwa Mwenyezi Mungu kutenda matendo yanayokwenda kinyume na kawaida ya maumbile, basi Nabii Suleiman[a.s] atakuwa alifanya kufru na ushirikina kuwaomba waliohudhuria mbele yake wamletee kiti cha enzi cha Bil-qiis!!! Vile vile kumuomba muujiza mtu aliyedai Utume katika zama zozote na mahala popote itakuwa ni tendo la ukafiri na ushirikina. Lakini tunajua kwamba watu walikuwa wakimuomba muujiza kila aliyedai Utume akiwa mkweli au muongo ili iwe ni dalili ya kuthibitisha ukweli wa madai yake na kama kweli anayo mawasiliano na ulimwengu wa juu. Yote haya hawakumuomba Mwenyezi Mungu ambaye ndiye aliyemtuma bali walikuwa wakisema:

"Kama umekuja na alama (muujiza) basi ilete iwapo wewe ni miongoni mwa wasemao kweli ". Qur'an, 7:106.

Na hii ndiyo kawaida ya mataifa yote na nyumati zote ulimwenguni, kwani kila walipotaka kupambanua baina ya Nabii wa kweli na muongo mwenye kujipachika Unabii walikuwa wakimuomba muujiza utakaojulisha uwezo wake wa ghaibu, nao Manabii katika kutekeleza wajibu wao walikuwa wakiwaita watu waje kushuhudia miujiza yao inayojulisha ukweli wao. Bila shaka Qur'an Tukufu imesajili baadhi ya matukio ambayo yalipita baina yao Manabii na nyumati (zao) kuhusu maudhui hii, bila ya kuwakosoa waombaji wa mijuza kwa Manabii, jambo ambalo linajulisha kwamba Qur'an inakubaliana na maombi haya. Hebu natutaje mfano mmoja kwamba: Lau umati fulani unaotafuta ilipo haki utamwijia Nabii Isa[a.s] na kumwambia, "Kama wewe ni mkweli kwa madai yako ya Unabii basi hebu mponye kipofu huyu na umrudishie macho yake na mponye huyu mwenye mbaranga, umati huu hauwezi kuzingatiwa kuwa umefanya shirki bali utahesabiwa kuwa ni miongoni mwa nyumati bora ambao unatafuta ukweli na kwa ajili hiyo utasifiwa.

Na sasa tena, lau tutakadiria kifo cha Nabii Isa[a.s] na kisha umati wake ukaiomba roho yake tukufu, imponye kipofu na mwenye mbaranga, basi ni kwa nini umati huu uonekane kuwa umefanya shirki pamoja na kufahamu kwamba mauti na uhai wa Nabii huyu havina athari yoyote katika Tauhidi na shirki? (Ili kuifahamu miujiza ya Nabii Isa[a.s] rejea aya ya 49 Sura ya 3 na aya ya 100 na 101 Sura ya 5.

KHULASA YA MAELEZO

Kwa kufupisha maelezo, Qur'an Tukufu inabainisha majina ya baadhi ya Mawalii aliowachagua Mwenyezi Mungu na akawapa uwezo huo wa siri ili watekeleze matendo ambayo yamefichikana yaliyo kinyume na maumbile ya kawaida, nao Mawalii hawa walikuwa wakitumia uwezo huu katika nyakati zinazofaa kama ambavyo kulikuwa na watu ambao walikuwa wakienda kwa Mawalii hao na kuwaomba kuwasaidia kwa uwezo huu. Kwa hiyo basi ewe msomaji imekudhihirikia kwamba, aya nyingi za Qur'an ziko wazi kabisa katika kuyapinga madhehebu ya Kiwahabi na zinavunja rai yao hiyo ya pekee. Lau Mawahabi watasema, "Kuomba muujiza Mawalii ni shirki." Sisi tutasema, "Kwa nini basi Nabii Suleiman[a.s] na wengineo aliomba matendo yaliyo kinyume cha maumbile kwa wengine"? Na iwapo watasema: "Bila shaka kuwaomba haja fulani Mawalii wa Mwenyezi Mungu kwa njia ya muujiza kunalazimu kuitakidi uwezo wao wa ghaibu". Sisi tutasema, "Kuamini uwezo wa ghaibu kuna namna mbili, ya kwanza itakuwa ndiyo Tauhidi yenyewe, na ile ya pili itakuwa inalazimu kupatikana shirki". Na iwapo watasema: "Hakika kuomba karama kutoka kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu katika zama za uhai inafaa, lakini kuziomba hizo karama kwa Walii aliyekwisha fariki haifai".

Sisi tutasema, "Hakika mauti na uhai vyote viwili siyo msingi wa Tauhidi na shirki wala hivi haviwezi kubatilisha ukweli wa kimojawapo." Na iwapo wao watasema, "Hakika kuomba uponyo kwa mgonjwa na kuondosha deni kwa njia isiyo ya kawaida ni kuomba kwa asiye Mwenyezi Mungu afanye tendo la Mwenyezi Mungu". Sisi tunasema, "bilashaka sharti ya kupatikana shirki ni kuitakidi uungu kwa yule unayemuomba au kuamini kuwa yeye ndiyo mfanyaji wa matendo ya Mwenyezi Mungu, kwa kujitegemea na kwamba kuomba matendo yasiyo ya kawaida kimaumbile maana yake siyo kuomba matendo ya Mwenyezi Mungu kutoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, kwani kipimo cha matendo ya Mwenyezi Mungu hakipimwi kwa kuwa matendo hayo yako nje ya kanuni za kimaumbile ili ombi hili liwe ni ombi Ia kuomba kitendo kinachostahiki kutendwa na Mwenyezi Mungu ambacho ameombwa mja akitende. Sivyo kabisa, bali kipimo cha matendo ya Mwenyezi Mungu ni kuwa mtendaji ni mwenye kujitegemea kule kufanya matendo hayo na kuyatekeleza. Ama ikiwa mtendaji anafanya kitendo fulani kwa kutegemea uwezo wa Mwenyezi Mungu basi kumuomba yeye hakuwi na maana ya kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu kutenda tendo la Mwenyezi Mungu. Na wala hapana tofauti katika uombaji ikiwa tendo hilo ni miongoni mwa matendo ya kawaida au ni yale yaliyo kinyume na kawaida. Majibu kama haya pia yatakuwa sawa sawa kuhusu kuomba uponyo kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu kwani kuna baadhi ya watu ambao wanapinga jambo hili kwa kutolea ushahidi aya ya Qur'an isemayo: "Na ninapoumwa yeye ndiye aniponyaye ". Qur'an aya ya 80 Surat As-shuaraa.

Wanasema; "Basi vipi itafaa kusema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu niponye"? Na mengineyo katika matendo yaliyo kinyume na ada kawaida)? Jawabu lake: Bila shaka wale wanaoitakidi itikadi hii kwa bahati mbaya hawakutenganisha baina ya matendo ya kiungu na yale ya kiutu, na ndiyo maana wanaona kwamba kila kitendo ambacho kina kwenda kinyume na njia za kawaida kiutendaji, basi hicho ni miongoni mwa matendo ya Mwenyezi Mungu na kitendo kinachopita katika utendaji wakawaida, basi hicho ni miongoni mwa matendo ya watu. Bila shaka watu hawa hawakufahamu au wanajifanya kutokufahamu kipimo kinachotenganisha kati ya matendo ya Mwenyezi Mungu na yale yasiyo yake. Kama ingekuwa kila kitendo kilicho kinyume cha maumbile kinazingatiwa kuwa ni miongoni mwa matendo ya Mwenyezi Mungu, basi matendo yanayofanywa na watawa wa huko India yangekuwa ni matendo ya kiuungu na wote hao wanaoyatenda wangekuwa ni "Miungu". Tumekwisha taja zaidi ya mara moja kwamba, kipimo katika matendo ya Mwenyezi Mungu nikule "kujitegemea katika utendaji" na kutokutegemea aina ya uwezo mwingine wowote ule, wakati ambapo matendo yatendwayo na watu ni kinyume cha hivyo. Kwa hakika mtu (siku zote) anamtegemea Mwenyezi Mungu na hutaka msaada kwa uwezo wake katika kila jambo sawa sawa likiwa ni Ia kimaumbile (yetu) au lililovuka mipaka ya kimaumbile, na watu wengi hupata uwezo (huo) na kuutumia kufikia malengo yao wayatakayo. Basi je, kuomba jambo fulani kwa watu hawa ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu?

Kwa hakika kuenda kinyume cha Tauhidi kumo udani ya itikadi iliyoambatanishwa na ombi (la mtu), basi iwapo muombaji aombapo kitu kwa mmojawapo wa Mawalii wa Mwenyezi Mungu hali ya kuwa anaamini kwamba Walii huyo ni mwenye kujitegemea (katika matendo yake) basi atakuwa kamfanya Walii huyo kuwa ni mtu anayejitosheleza kwa dhati yake, na maana ya kujitosheleza ni kwamba atakuwa amemzingatia Walii huyo kuwa ni mtu asiyemuhitajia Mwenyezi Mungu kwa lolote, na hii ndiyo shirki kwa kuwa hakuna anayejitosheleza kwa dhati yake isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake. Na hapo kale wengi wa washirikina katika zama za jahiliya na mwanzo wa kuja Uislamu walikuwa wakiitakidi itikadi hii kuhusu Malaika na nyota, na kwamba Mwenyezi Mungu ameviumba viumbe hivi na akaviegemezea uwezo wa kuendesha ulimwengu na kuuangalia kwa muegemezo wa viumbe hivyo kujitegemea kikamilifu na au kwa uchache, washirkina waliamini kuwa viumbe hivyo vinamiliki shafaa (uombezi) na kuutumia uwezo huo wa shafaa wapendavyo.

SHIRKI NA JINSI WASEMAVYO MUUTAZILA

Ama kundi Ia Muutazila wao wanamuona mtu katika hali ya kuwepo kwake kuwa yeye ni kiumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, lakini Muutazila hao hao kwa wakati huo huo wanamuona mtu kuwa ni mwenye kujitegemea katika kutoa athari kwenye vitu na kutekeleza matendo. Lau hawa Muutazila wangefanya mazingatio kidogo katika kauli yao hii wangeona kuwa kuna aina fulani yashirki iliyofichikana, lakini wao wameghafilika nayo. Bila shaka shirki hii iliyojificha haifikii ule ushirikina wa washirikina (hao) na tofauti iliyopo katika shirki mbili hizi ni kwamba washirikina wanadai kuwa masanamu yao yanajitegemea kiuwezo katika kuendesha mambo ya ulimwengu na matendo yanayomstahikia Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nao Muutazila wandai kuwa mtu anao uwezo wa kujitegemea katika matendo yake. Al-mustalahat Al-arbaa, uk. 18.