UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI0%

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Vitabu mbali mbali

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi: SHEIKH JA'AFAR SUBHANY
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 50398
Pakua: 5041

Maelezo zaidi:

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 24 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 50398 / Pakua: 5041
Kiwango Kiwango Kiwango
UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi:
Swahili

19

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

NINI LENGO LA HIJJA?

Kwanza Hijja ni Ibada: Hapana shaka kwamba jambo la kwanza ambalo Hijja inalilenga na ndiyo makusudio muhimu ya ibada zake, ni kuzidisha kumuelekeza mja kwa Mwenyezi Mungu na kumfanya kuwa mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na kuimarisha uhusiano kwake na kuiingiza kwa ndani zaidi imani katika moyo wake na kuithibitisha itikadi ndani ya dhamiri yake juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu. Kwa kifupi tunaweza kusema kwamba lengo muhimu la Hijja ni ibada na ni kwa kuanzia kuhirimia kwa ajili ya umra na kutufu al-Kaaba tukufu kisha kuswali na kwenda baina ya Safa na Marwa na kupunguza nywele, na kisha Ihramu ya pili ni kwa ajili ya Hijja na kusimama Arafah na kwenda Muz-dalifa na kusimama hapo, kisha kwenda Mina na kulala usiku kadhaa na kupiga Jamarat, kisha kuchinja ngamia au (ng'ombe, mbuzi au kondoo) halafu kunyoa kisha kutufu aI-Kaaba Tukufu na kumalizia kufanya Saayi baina ya Safa na Marwa pamoja na kufanya yanayoambatana nayo miongoni mwa dua na dhikri na kujizuwiya na yaliyoharamisha yanayohusika nayo, yote haya ni kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hiyo ni ibada iliyo katika ubora wa aina yake, na ni kuonyesha utumwa (mbele ya Mwenyezi Mungu) katika daraja iliyo juu ya ibada. Na kwa hakika ni (kuonyesha) unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika namna zilizo bora mno.

Ni ibada inayoonyesha udhalili (wa waja) mbele ya Mwenyezi Mungu kwa undani wa aina yake. Hivyo basi Hijja ni ibada inayokusanya kila misingi inayodhihirisha utumwa (mbele ya Mwenyezi Mungu, na (pia inadhihirisha) kila aina za unyenyekevu na utii kwa Mola Mtukufu, (miongoni mwake) ni kutosheka na dunia na kuyapuuza ma-tamanio na kujitolea kwa mali na kudhalilika na kufanya dhikri, na Tah-lili na Tasbihi, Tahmidi na Takbira na kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika kumtii na kumuomba msaada na kutoka kwenye uzio wa mapendekezo ya kimaada na kujisahaulisha kwa muda (furaha ya) mali mtoto mke na jamaa kwa ajili ya kuitumikia dini ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili yake Mwenyezi Mungu na kwa amri ya Mwenyezi Mungu na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kufuata hukmu ya Mwenyezi Mungu, na kutekeleza matakwa ya Mwenyezi Mungu, na kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu pekee asiye na mshirika. Bila shaka Hijja ni ibada, lakini je, lengo la Hijja linaishia kwenye matendo haya matukufu ya ibada tu? (au kuna zaidi)? Na Je, hivi Hijja ilifaradhishwa kwa Waislamu wote wanaume na wanawake, wazee na vijana na kila aina ya rangi (za watu) na jinsi (zao) ili watekeleze maamrisho yanayofungamana na uhusiano (wao) na Mola wao tu bila wajibu huu mtukufu (wa Hijja) kuwa na lengo la (maisha) ya kijamii na bila mafungamano yoyote na masuala ya maisha yao na mambo yao?

Na Je, hivi hata tendo dogo la kiibada ndani ya Uislamu huwa halina lengo la kijamli kiasi kwamba ibada hii kubwa ya Hijja ikose lengo hilo (la kijamii)? Na faradhi hii kubwa yenye vigawanyo na misingi mingi na yenye muundo wa kijamii kama swala ya Ijumaa (Iwe haina lengo lolote ndani yake)? Bila shaka aya za Qur'an na Sunna tukufu na sera za waliotangulia na kauli za wanachuoni zote zinaungana (kutambulisha) kwamba lengo la Hijja haliishii na kukoma katika hali ya kuwa ni jambo la ibada peke yake na unyenyekevu auonyeshao mja katika maisha yake ya kijamii, (Bali) makusudio yake ndiyo makusudio ya ibada zingine miongoni mwa faradhi za Kiislamu kama vile Swala, Saumu, Zaka, Jihadi na nyinginezo ambazo hazihusiani tu na mambo ya kuabudu peke yake, bali zinajumuisha malengo ya Kijamii na mambo ya kisiasa katika maisha ya Waislamu (kuanzia) mmoja mmoja na (hadi kufikia ngazi ya) Taifa. Na jambo hili (kwa maana iliyoelezwa) linaungwa mkono na akili iliyosalimika na kutiwa nguvu na fikra sahihi. Bila shaka Uislamu ni dini yenye kuenea (kila upande) yaani ina muongozo wa kiibada, kisiasa, kiuchumi na kijamii, nayo iko kinyume na Uyahudi na Ukristo wa leo na kanuni zilizowekwa na watu, na haukuwa Uislamu ila ni mkusanyiko uliopangika wa itikadi na kauni na mafunzo yanayohusu kila upande wa maisha, bali ni kila sehemu ya dini hii ni mchanganyiko uliyowekwa kimahesabu kutokana na malengo mbali mbali na ni mpango uliowekwa kwa usawa kwa mtu mmoja mmoja, jamii, ibada, siasa, uchumi, afya, dunia na akhera.

Zaidi ya hayo ibada katika fikra ya dini hii, mipaka yake inatanuka mpaka inakusanya maisha yote na kuyaenea matendo yote ya watu kama yatatendwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, haikomei kwenye mambo ya ibada yaliyo mashuhuri kama vile Sala, Zaka na Hijja, bali inakusanya kila tendo ambalo kwalo kuna mafanikio ya maisha na kufaulu kwa watu. Na kwa ajili hii Mtume Mtukufu[s.a.w.w] amesema kumwambia Abu Dharri: "Uwe na nia njema kwa kila kitu (ukitendacho) hata katika usingizi"[247] Kwa hiyo basi, Hijja kama tunavyoibainisha kutoka katika Qur'an na Sunna na sera za waliotangulia, na kauli za wanachuoni wahakiki, (lengo lake) halikomei kwenye kuwa yenyewe ni msimu wa ibada kwa utambuzi uliozoeleka kwa watu wengi bali kwa upande mwingine ni mkutano wa kisiasa wa ulimwengu na ni mkusanyiko wa kijamii kwa jumla unaowapa Waislamu wanaokuja kutoka kila pande za miji fursa ya kufahamiana, kuzoweyana, kukutana na kunufaishana wao kwa wao na kubadilishana mambo yao na kutatua matatizo yao ya kisiasa, kiuchumi na kijamii wakiwa mahala pa amani na utukufu na upendo. Na haya ndiyo tunayotaka kuyaonyesha na kuyatolea ushahidi katika kurasa hizi chache pamoja na kuwa tunakiri ya kwamba Mas-ala haya (ya Hijja, na kuyasoma malengo ya Hijja ya kiibada na kisiasa na kijamii ni (somo) pana mno kuliko hili somo (tutakalolieleza) kwa ufupi. Kwa hiyo basi tunataraji kawa yatakayokuja katika mlango huu ni dalili tu siyo zaidi, na ni wajibu wa Waislamu wote na mahujaji kwa upande wao wajaribu kufahamu mafunzo zaidi katika nyanja hii, nayo ni kwa kuifanyia mazingatio faradhi hii na ibada zake na kuzitilia maanani aya za Qur'an na hadithi Tukufu katika njia hii.

MAKUSUDIO YA HIJJA KIJAMII NA KISIASA NDANI YA QUR'AN

Qur'an Tukufu imeitaja Hijja mahala pengi ya kuwa ndani yake mna mambo yenye manufaa kwa watu na inayo maslaha yao, pale Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema:

وَأَذِّن فِي النَّاسِ بِالْحَجِّ يَأْتُوكَ رِجَالًا وَعَلَىٰ كُلِّ ضَامِرٍ يَأْتِينَ مِن كُلِّ فَجٍّ عَمِيقٍ ﴿٢٧﴾ لِّيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ فِي أَيَّامٍ مَّعْلُومَاتٍ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّن بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ ﴿٢٨﴾ ثُمَّ لْيَقْضُوا تَفَثَهُمْ وَلْيُوفُوا نُذُورَهُمْ وَلْيَطَّوَّفُوا بِالْبَيْتِ الْعَتِيقِ ﴿٢٩﴾ ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّـهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ عِندَ رَبِّهِ وَأُحِلَّتْ لَكُمُ الْأَنْعَامُ إِلَّا مَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فَاجْتَنِبُوا الرِّجْسَ مِنَ الْأَوْثَانِ وَاجْتَنِبُوا قَوْلَ الزُّورِ ﴿٣٠﴾ حُنَفَاءَ لِلَّـهِ غَيْرَ مُشْرِكِينَ بِهِ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَكَأَنَّمَا خَرَّ مِنَ السَّمَاءِ فَتَخْطَفُهُ الطَّيْرُ أَوْ تَهْوِي بِهِ الرِّيحُ فِي مَكَانٍ سَحِيقٍ ﴿٣١﴾ ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّـهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ ﴿٣٢﴾ لَكُمْ فِيهَا مَنَافِعُ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ثُمَّ مَحِلُّهَا إِلَى الْبَيْتِ الْعَتِيقِ ﴿٣٣﴾

"Watangazie watu habari ya Hijja, watakujia watu kwa miguu na (wengine) wakiwa juu ya mnyama aliyekonda kutokana na machovu ya njiani, wakija kutoka njia ya mbali, ili washuhudie manufaa yao na kulitaja jina Ia Mwenyezi Mungu katika siku zinazojulikana - Juu ya yale aliyowaruzuku, nao ni wanyama wenye miguu minne, na kuleni katika wanyama hao na mumlishe mwenye shida aliye fakiri. Kisha wajisafishe taka zao na watimize nadhiri zao na waizunguke nyumba ya kale (Al-Kaaba). Namna hii iwe, na anayevitukuza vitu vitakatifu vya Mwenyezi Mungu basi (kufanya) hivyo ni kheri yake Mwenyewe mbele ya Mola wake, na mumehalalishiwa wanyama isipokuwa wale mnaosomewa humu (katika Qur'an kuwa wasiliwe), basi jiepusheni na uchafu wa masanamu na jiepusheni na usemi wa uongo, Mkhalisike kwa Mwenyezi Mungu bila kumshirikisha na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu ni kama kwamba ameporomoka kutoka mbinguni, kisha ndege wakamnyakua au upepo kumtupa mbali. Namna hivi, yeyote anayeziheshimu alama za (Dini ya) Mwenyezi, basi hilo ni jambo katika utawa wa nyoyo. Katika (wanyama) mnaowapeleka Makka kuchinjwa) mnayo (ruhusa kutumia) manufaa (yake) mpaka muda maalumu, kisha mahala pa kuchinjwa kwake ni (karibu na) ile nyumba kongwe". Qur'an, 22:27-33.

Kuna mambo matatu ya kuzingatia ndani ya aya ya pili miongoni mwa aya hizi: Kwanza: Manufaa yamewekwa upande wa kumtaja Mwenyezi Mungu na ndani yake inafahamisha kwamba Hijja inayo malengo mawili: Moja wapo ni la Kiibada na linachukua nafasi ya kumtaja Mwenyezi Mungu, lengo jingine siyo Ia kiibada kwa maana iliyozoweleka nalo linachukua mahala pa manufaa. Pili: Kuyatanguliza manufaa juu ya kumtaja Mwenyezi Mungu jambo linaloshika nafasi ya kiibada. Tatu: Kuyafanya manufaa yasiwe na ufupisho uliofungika bali yawe yenye kuingia katika nyanja nyingi, kwani Mwenyezi Mungu hakusema kuwa ni manufaa ya kiuchumi tu peke yake, jambo ambalo linafahamisha kwamba manufaa haya yanakusanya manufaa ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na mengineyo. Amesema Al-Mar-hum Al-Imam Sheikh Muhammad Shaltut ambaye alikuwa Sheikh wa Chuo Kikuu cha Az-Har, kuhusu tafsiri ya aya hii kama ifuatavyo: "Manufaa ambayo Hijja imefanywa kuwa ndiyo njia ya kuyashuhudia na kuyapata - nayo ndiyo yaliyotajwa mwanzo kuhusu hekima za Hijja, ni manufaa ya ujumla bila ya sharti, hayakufungiwa kwa aina moja pasina aina nyingine, wala upande mmoja bila upande mwingine, nayo kwa ujumla wake yanakusanya kila kinachomnufaisha mtu mmoja na jamii na kutengeneza mambo yao, kwani kuitakasa nafsi na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu ni manufaa na kushauriana kuweka mipango ya Elimu na Taaluma na kuungana kuimarisha Da'awa na kufanya juhudi kuutangaza Uislamu na hukmu zake bora ni manufaa, na kuandaa mikakati ili kuimarisha heshima ya Uislamu kutokana na ukandamizaji na unyonge ni manufaa, na hali kama hii manufaa yake ni mengi na yana aina nyingi kutegemeana na hali zinavyolazimu na nyakati zinavyotambulisha na mitazamo kati ya watu na watu"[248]

Na amesema tena: "Nayo Hijja kwa kuzingatia utukufu wake ndani ya Uislamu na lengo lake lililokusudiwa kwa mtu binafsi na jamii, bila shaka wanaikubali watu wa elimu na watu wanaohusika na mafunzo na taalauma pia wanaohusika na uendeshaji wa mambo na idara na wale wanaohusika na mali na uchumi na watu wa sheria na dini na wale wanaohusika na mambo ya vita na jihadi. Ukweli ni kwamba (ilipasa) wakaishuhudia watu wa aina mbali mbali wenye fikra na watatuzi wa matatizo (tofauti tofauti ya kijamii n.k.), wachunguzi na wenye juhudi (ya kutafuta amani) na wenye imani ya kweli na malengo ya kisiasa ambayo Waislamu wanawajibika kuyakusudia (yawe ni msimamo wao) katika maisha yao, inafaa waielekee Hijja watu wote hawa na Makka iko tayari kuwapokea na kuwaunganisha kwenye neno la Mwenyezi Mungu pembezoni mwa nyumba ya Mwenyezi Mungu, utawaona wakitambuana (kufahamiana huyu katoka wapi na ninani anafanya nini huko aliko) na wanashauriana na kusaidiana, hatimaye hurejea makwao hali ya kuwa ni umma mmoja (kitu kimoja) na nyoyo zilizoshikamana na mawazo na fikra za aina moja".[249]

Kwa hiyo ukweli ulivyo ni kwamba, aya hizi za Hijja zinaendelea mpaka zinamalizika na kuungana na kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

إِنَّ اللَّـهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ خَوَّانٍ كَفُورٍ ﴿٣٨﴾ أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا وَإِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ ﴿٣٩﴾ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِم بِغَيْرِ حَقٍّ إِلَّا أَن يَقُولُوا رَبُّنَا اللَّـهُ وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّـهِ النَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّهُدِّمَتْ صَوَامِعُ وَبِيَعٌ وَصَلَوَاتٌ وَمَسَاجِدُ يُذْكَرُ فِيهَا اسْمُ اللَّـهِ كَثِيرًا وَلَيَنصُرَنَّ اللَّـهُ مَن يَنصُرُهُ إِنَّ اللَّـهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ ﴿٤٠﴾

"Bila shaka Mwenyezi Mungu huwakinga wale walioamini, kwa hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila haini asiyeshukuru, wameruhusiwa (kupingana) wale wanaopigwa hiyo ni kwa sababu wamedhulumiwa, na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni muweza wa kuwasaidia wale waliotolewa majumbani mwao pasipo haki ila kwa sababu wamesema kuwa, Mwenyezi Mungu ndiye Mola wetu, na kama Mwenyezi Mungu asingeliwakinga watu baadhi yao kwa wengine, bila shaka yangelivunjwa mahekalu na makanisa na nyumba nyingine za ibada na misikiti ambamo jina la Mwenyezi Mungu hutajwa kwa wingi, na bila shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anayesaidia Dini yake, hakika Mwenyezi Mungu nimwenye nguvu na ni mwenye kushinda". Qur'an, 22:38-40.

Mtiririko huu haukuja kwa bahati tu bila kutegemea, haiwezekani kwa aya za Qur'an zipangike kwa mpangilio huu bila ya kuwepo mahusiano baina yake. Bila shaka mshikamano na mfumo wa namna ya aya hizi zilivyokuja kwa aina hii, kunaonyesha kuwepo maungamano yenye nguvu kati ya Hijja na matendo ya kisiasa.

Nasi hatukusudii kusema kuwa Hijja igeuke na kuwa uwanja wa mapigano, lakini kinachofahamika ndani ya mtiririko huo ni kuwa Hijja iwe ni hatua ya maandalizi ya mwelekeo (huo). Kwa hakika kinachowezekana kukipata na kufaidika nacho katika mtiririko huu ambao umekusanya baina ya aya zinazohusu Hijja na Jihadi na kupinga dhulma, na kuwemo msaada wa Mwenyezi Mungu kwa wanaodhulumiwa inajulisha kwamba Hijja ni mahala bora pa Waislamu kujiandaa kiroho na kinafsi kukabilina na dhulma na wanaodhulumu, na kupinga ukandamizaji na wakandamizaji na pia kupinga ukoloni na wakoloni. Bila shaka Hijja ni fursa nuzuri kwa Waislamu wanaokusanyika huko kutoka miji mbali mbali, kuonyesha nguvu waliyonayo na umoja wao, na watangaze msimamo wao wa umoja kisiasa na wawatamkie maadui mafunzo ambayo hawatayasahau pamoja nakuwa tendo hili haliishii kwenye Hijja tu kwani upinzani dhidi ya dhulma na wanaodhulumu na kutangaza chuki zao dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu ni jambo ambalo halina mipaka ya nyakati wala mahali. Ndiyo maana wafasiri wametafsiri "Manufaa" kuwa ni mambo yanayojumlisha mambo ya dunia na dini.

lbn Jaririt-Tabari, baada ya kunakili kwake kauli nyingi kuhusu tafsiri ya "manufaa" ameandika kama ifuatavyo: "Na kauli bora miongoni mwa kauli iliyo sawa, ni kauli ya yule aliyesema: Akikusudia hilo (yaani) "Ili washuhudie manufaa yao" ni miongoni mwa matendo anayoyaridhia Mwenyezi Mungu na biashara, na hiyo ni kwamba Mwenyezi Mungu ameyajumlisha manufaa yao yote yanayoshuhudiwa na kipindi cha Hijja na huiletea Makka katika siku za msimu huo manufaa ya dunia na akhera na hakuhusisha kitu fulani miongoni mwa manufaa yao kwa kupitia riwaya yoyote au akili, basi manufaa hayo ni ya jumla."[250] Kisha Qur'an imeieleza AI-Kaaba Tukufu kuwa imefanywa iwe ni Qiyam (Kisimamo) kwa ajili ya watu pale iliposema:

جَعَلَ اللَّـهُ الْكَعْبَةَ الْبَيْتَ الْحَرَامَ قِيَامًا لِّلنَّاسِ ﴿٩٧﴾

"Mwenyezi Mungu ameifanya Al-Kaaba nyumbaTukufu kuwa ni kisimamo kwa ajili ya watu. Qur'an, 5:97.

Na ndani ya Qur'an tamko "Qiyam" limekuja kuhusu mahali pale pale Mwenyezi Mungu anaposema:

وَلَا تُؤْتُوا السُّفَهَاءَ أَمْوَالَكُمُ الَّتِي جَعَلَ اللَّـهُ لَكُمْ قِيَامًا ﴿٥﴾

"Wala musiwape wapumbavu mali zenu ambazo Mwenyezi Mungu amezijaalia kuwa ni Qiyam kwenu. Qur'an, 4:5.

Na hii inafahamisha namna ya kufanana baina ya Hijja na mali, kama ambavyo uchumi na mali vinaendesha maisha ya watu na kulinda maslahi ya umma na Kiislamu. Basi hivyo hivyo Hijja nayo ndivyo ilivyo, na hii ikiwa na maana kwamba mkusanyiko wa mambo yaliyomo ndani ya Hijja hauishii kwenye ibada na kuabudu peke yake na kuneynyekea tu, bali unayo nafasi pana kiasi cha kujumlisha kila kitu chenye mafungamano na maslahi ya Waislamu miongoni mwa mambo yanayoendesha maisha yao na mazingira yao. Na kitu chochote kinachoendesha maisha yao (kitu hicho) ni bora kuliko matendo ya kisiasa ambayo yanalengo Ia kupinga ukoloni na utumwa na kunyonywa na kuthibitisha uhuru wao katika kila nyanja, na kuwazindua Waislamu kutokana na kuendelea kwa mambo yanayowazunguka ikiwemo njama na vitimbi na hatimaye kuwaelekeza kushika msimamo mmoja na kumpiga adui na kumzuia. Kisha ikiwa haifai kuwapa mali watu wapumbavu ambao hawajui jinsi ya kuitumia kwa kukosa kwao kuwa na upeo wa maarifa au upungufu wa akili zao, basi haifai kabisa kwa njia ambayo inastahiki mno kuachwa Hijja ikawa mikononi mwa watu wasiotambua utukufu wake na uzito wake na umuhimu wake katika maisha ya umma wa Kiislamu.

Hebu tazama waliyoyasema baadhi ya wafasiri kuhusu aya hii: Amesema Ibn Jaririt-Tabari: Mwenyezi Mungu anasema: "Mwenyezi Mungu ameifanya Al-Kaaba nyumbaTukufu kuwa ni yenye kuwatengenezea mambo yao watu ambao hawana cha kuwatengenezea mambo yao kutokana na kiongozi ambaye anamzuwia mwenye nguvu dhidi ya mnyonge na muovu miongoni mwao dhidi ya mwema na dhalim dhidi ya anayedhulumiwa na akaifanya kuwa ndiyo utambulisho wa dini yao na maslahi ya mambo yao.[251] Na ndani ya Tafsirul-Manar amesema kama ifuatavyo: "Bila shaka (Mwenyezi Mungu) ameifanya Kaaba kuwa ni kisimamo kwa watu kuhusu mambo ya dini yao na ni yenye kurekebisha nyendo zao, na ni yenye kuzitakasa nafsi zao kwa yale aliyoyafaradhisha kwao katika Hijja, ambayo ni miongoni mwa nguzo kubwa za dini, kwani hiyo ni ibada ya kiroho na kimali na kijamii".

Na amesema tena: "Hakika uwekaji wa Mwenyezi Mungu wa mambo haya (Yaani Ibada za Hijja) ni kuweka kulikohusisha maumbile na sheria kwa pamoja na uwekaji huu unajumlisha kusimamia na kuyathibitisha maslahi ya dini yao na dunia yao".[252] Na lau tutayafumbia macho yote hayo basi Je, ni kweli itawezekana kuifumbia macho sura ya Bara'ah ambayo inatangaza wazi msimamo wa kisiasa kuwahusu washirikina, ilishuka (Sura hii) ili isomwe ndani ya siku za Hijja nalo ni tendo la kisiasa bila ya shaka yoyote. Basi hebu na tuisikilize Qur'an Tukufu inasema:

بَرَاءَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ إِلَى الَّذِينَ عَاهَدتُّم مِّنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١﴾ فَسِيحُوا فِي الْأَرْضِ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِي اللَّـهِ وَأَنَّ اللَّـهَ مُخْزِي الْكَافِرِينَ ﴿٢﴾ وَأَذَانٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ إِلَى النَّاسِ يَوْمَ الْحَجِّ الْأَكْبَرِ أَنَّ اللَّـهَ بَرِيءٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ وَرَسُولُهُ فَإِن تُبْتُمْ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ وَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِي اللَّـهِ وَبَشِّرِ الَّذِينَ كَفَرُوا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٣﴾

"(Hili ni) tangazo la kujitoa katika dhima, litokalo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa washirikina (Makafiri) - (waambieni) basi tembeeni katika nchi kwa miezi minne na mtambue kwamba ninyi hamuwezi kumshinda Mwenyezi Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuwadhalilisha makafiri. Na ni tangazo litokalo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwenda kwa watu kuwajulisha siku ya Hijja kubwa kwamba, Mwenyezi Mungu yu mbali na washirikina na pia Mtume wake (yu mbali nao) basi kama mkitubu ndiyo kheri kwenu na mkikengeuka basi jueni kwamba ninyi hamuwezi kumshinda Mwenyezi Mungu, na wapashe waliokufuru habari ya adhabu iumizayo: Qur'an, 9:1-3. Na zinazofuatia.

Na Mtume Mtukufu[s.a.w.w] alimuamrisha Imam Ali[a.s] alifikishe onyo hili na tangazo hili kwa washirikina ndani ya siku za Hijja, basi Imam Ali akafanya hivyo na liii ni kwa ushahidi wa wana tafsiri wote na wanahistoria na wanahadithi wote. Ndani ya tafsiri ya Tabari kuna hadithi yenye Isnad kama ifuatavyo: "Ilipofika siku ya kuchinja (siku ya kumi mfunguo Tatu) Ali bin Abi Talib (r.a) alisimama akawatangazia watu kile alichoamuriwa na Mtume na Mwenyezi Mungu[s.a.w.w] akasema: "Enyi watu nimeamuriwa mambo manne:

(1) Asiikurubie nyumba hii baada ya mwaka huu mshirikina yeyote.

(2) Na wala asitufu uchi yeyote.

(3) Na haitaingia peponi isipokuwa nafsi iliyosilimu.

(4) Na atimize ahadi yake kila aliye na ahadi. Katika Riwaya nynigine imesema: "Na yeyote aliye na ahadi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu[s.a.w.w] basi na aitimize kwa muda wake.[253] Na ukipenda unaweza kusema kwamba kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema: "(Hili ni) tangazo la kujitoa katika dhimma, litokalo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa washirikina". Na kauli yake aliposema: "Na ni tangazo litokalo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwenda kwa watu kuwajulisha siku ya Hijja kubwa kwamba Mwenyezi Mungu yu mbali na washirikina na pia Mtume wake (yu mbali nao)", bila shaka kujitenga kulikotajwa ndani ya aya hizi mbili hakuhusiani tu na washirikina wa Kiquraishi au washirikina wa Bara Arabu peke yao bali kujitenga kulikokusudiwa ndani ya aya hizo mbili ni tangazo la Kiungu linalokusanya washirikina wa ulimwengu mzima, waliokuwepo katika zama zake Mtume[s.a.w.w] na baada ya hao mpaka siku ya Kiyama.

Qur'an Tukufu inafunza umma wa Kiislamu na kufafanua daraja yao ya kidini na inawalazimisha kujibari (kujitenga) na washirikina wote katika zama zote, na kwa sababu hiyo lau wageni wa Mwenyezi Mungu wote watajibari kutokana na walahidi na washirikina wanao wakandamiza, basi watakuwa wametekeleza wajibu wao kwa pamoja. Na huenda ikafikiriwa kwamba, kujibari na kuwapinga (washirikina) kulikokuja katika aya hizi, kunahusika na zama aliyoishi Mtume[s.a.w.w] wala haikuvuka baada ya hapo, kwa hakika hiyo ni kauli isiyo na dalili, nayo ni mfano wakauli ya watu waovu ambao wanataka kuuhusisha ujumbe wa Mtume[s.a.w.w] na mwongozo wa Qur'an Tukufu katika zama maalum pasina zama zingine. Nami sifikiri kwamba Muislamu aliye huru atakuwa na shaka kwamba, wakomunisti na wanaowaunga ni wabaya mno kuliko washirikina ambao ufunuo wa Mwenyezi Mungu umewajibisha kujitenga nao, kama ambavyo sifikirii mtu mwenye insafu atakuwa na shaka kwamba shetani mkubwa (Amerika) ni mbaya mno na ni mwenye madhara mno kuliko washirikina. Kama ambavyo imekuja ndani ya vitabu ya pande mbili (Sunni na Shia) kwamba Hisham Ibn Abdil-Malik alihiji katika zama za Ukhalifa wa Baba yake na akatufu, kisha akataka aibusu "Hajar-al-Aswad, "lakini hakuweza kutokana na msongamano (wa watu) basi akatengenezewa mimbar na akakaa juu yake, mara akaja Ali bin Husein [a.s] akiwa amevaa Ihram, akiwa ni mwenye uso mzuri kuliko watu wote na mwenye harufu nzuri na kwenye paji lake la uso kuna athari ya Sijda inaonekana kama koti la kondoo, akaanza kutufu Al-Kaaba na anapofika kwenye Hajar al-Aswad watu humpisha ili aibusu kwa kumheshimu na kumtukuza, basi jambo hilo likamchukiza Hisham, na mtu mmoja katika watu wa Sham akamuuliza Hisham "Ni nani mtu huyu ambaye watu wamemuheshimu kwa heshima hii na wamempisha kwenye Hajar al-Aswad?

Hisham akasema: "Simjui", Alijibu hivyo ili tu watu wa Shamu wasije wakampenda Imam Ali bin Husein. Basi Farazdaq aliyekuwepo hapo akasema: "Lakini mimi namjua". Yule mtu wa Shamu akamwambia "Ni nani huyu Ewe Abu Faras"? Farazdaq akasoma Qasida, nasi tunataja hapa sehemu ya beti zake. "Huyu ndiyo yule ambaye Makka inatambua sauti ya nyayo zake, nayo Al-Kaaba na nje ya Makka na Haramu ya Makka zote zinamtambua. Huyu ni mwana wa mmbora wa waja wa Mwenyezi Mungu wote. Huyu ndiye mcha Mungu mtakasifu mwenye tahara na ni bendera ya uongofu. Huyu ndiye ambaye mzazi wake ni Ahmad mteule, Mola wangu amsalie mpaka siku ya Qiyama". (Aliendelea) mpaka akasema: "Babu yake ni miongoni mwa Quraishi katika nasaba yake ni Muhammad kisha Ali ambaye ni bendera ya viongozi mashahidi wake ni vita vya Badri na pango la mlima wa Uhdi na vita vya Khandaq na wote walijulikana siku ya Fat-hi Makka, na Khaybar na Hunayn zinamshuhudia na siku ya Quraydha".[254] Namna hivi ndivyo mshairi huyu mkubwa wa Kiislamu anavyomkabili khalifa huyo mjeuri kwanjia ya kaswida hii ya kishujaa na anamuarifisha Imam wa haki kutoka katika kizazi cha mtume katika mkabala wenye changamoto la kisiasa.

Jambo ambalo linajulisha kwamba jambo hili ni sheria (kufanyika) katika msimu wa Hijja na kujuzu kwake ni kutokana na kutopingwa na Mwislamu yeyote siyo zama hizo wala baada ya hapo. Na kwa maneno mengine tunaweza kusema kwamba, mshairi huyo analazimika kufanya munadhara huo wa kisiasa wenye nguvu iii amtambulishe Imam mbele ya mkusanyiko wa Mahujaji waliofika kwenye nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, kwa kumzingatia kuwa ndiyo mrithi wa haki wa kizazi cha mjumbe wa Mwenyezi Mungu[s.a.w.w] , na tukio hili linatupatia dalili iliyo wazi kwamba, tendo la kisiasa katika msimu wa Hijja linazingatiwa kwa mujibu wa kanuni na sheria, na hiyo ni kwa sababu hakuna kizuwizi au uharamu wa kutekeleza matendo kama haya, sawa sawa ni katika siku hizo, au miaka iliyofuatia siku hizo.

MALENGO YA HIJJA YA KIJAMII NA KISIASA KATIKA SUNNAH

Kwa hakika Sunna na sera tukufu ya Mtume na kitu kingine kinachoashiria kwamba, Mtume[s.a.w.w] alifanya matendo ya kisiasa katika Hijja, na zaidi ya hapo kuna hadithi zinazofidisha kwamba Hijja ni aina ya jihadi pale Mtume[s.a.w.w] aliposema: "Jihadi iliyo bora ni Hijja ". [255] Na kauli yake Mtume[s.a.w.w] isemayo: "Hijja ni Jihadi " Na pia kauli yake Mtume[s.a.w.w] : "Hijja ni Jihadi ya kila mnyonge " Hadithi hizi mbili za mwisho zinapatikana katika: Sunan lbn Majah: Al-Manasik, na Sunan an-Nasai: Al-Haj, Na Musnad ya Ahmad bin Hanbal. Na kauli yake Mtume[s.a.w.w] alipokuwa akiwajibu wanawake walipomtaka waende katika Jihadi akasema: "Jihadi yenu ni Hijja " Na katika baadhi ya hadithi Mtume[s.a.w.w] amelinganisha Hijja na Jihadi kinyume cha faradhi zingine hakuzilinganisha nayo, aliposema: "Mwenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuhiji na mwenye kufanya umra niwageni wa Mwenyezi Mungu aliowaita ". [256]

Na hadithi hii inaonyesha kupatikana kwa maungamano na wajihi wa kufanana katika athari na malengo baina ya faradhi hizi mbili na ukitaka unaweza kusema: "Hakika hadithi hii inaonyesha kwamba Hijja si mujaradi wa ibada kwa maana inayoelekeweka, bali ni tendo linalofanana na jihadi yaani ni ibada na ni tendo Ia kisiasa, basi Hijja ni msimu wa tendo la kisiasa kama ambavyo ni msimu wa ibada na unyenyekevu na kumuelekea Mwenyezi Mungu kwa kumuabudu." Kisha ni kwamba, sera inatusimulia kuwa Mtume Mtukufu[s.a.w.w] alihutubu mahala pawili (yaani) Arafah na Mina na akatangaza katika hotuba yake misimamo na hukumu muhimu za Kiislamu, za kiuchumi, kisiasa na za kijamii, hapa tunataja sehemu ya hotuba hiyo: Katika Sunan At-Tirmidhi: Imepokewa toka kwa Jabir ndani ya mlango wa Hijja ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu[s.a.w.w] amesema: Ilipofika siku ya Tarwiyyah (siku ya nane ya mfunguo Tatu) na wakaelekea Mina na wakasoma Tal-Biya ya Hijja, Mtume[s.a.w.w] pia alikusudia na akasali Mina Adhuhuri na Alasiri na Magharibi, na I'sha na Asubuhi, kisha akakaa kidogo mpaka jua likachomoza na akaamuru khema lake lililotengenezwa kwa manyoya lisimikwe Namirah, Mtume akaenda mpaka Arafat akakuta hema lake limesimikwa, akateremka mpaka jua likapanda juu, akaamuru ngamia wake aletwe, na akaletwa basi akapanda mpaka akafika

Bat-Nul-Wadi na akawahutubia watu akasema:

1) Bila shaka Damu yenu na mali zenu ni vitu vyenye heshima juu yenu, kama ilivyo na heshima siku yenu hii ya leo katika mwezi wenu katika mji wenu huu.

2) Fahamuni ya kwamba kila kitu katika mambo ya kijahiliya kiko chini ya nyayo zangu hizi (yaani vimebatilishwa).

3) Na Damu za wakati wa Jahiliyah zimeondolewa, na damu ya kwanza ninayoiondoa ni ya Rabia Ibn Al-Harith (Ibn Ammi ya Mtume, alikuwa amepelekwa kulelewa katika Bani Saad watu wa kabila la Huzail wakamuua)

4) Na riba ya Jahiliyah imeondolewa na riba ya kwanza ninayoindoa ni riba ya Abbas Ibn Abdil-Muttalib, hii imeondolewa yote.

5) Hakika kila Muislamu ni ndugu wa Muislamu na kwamba Waislamu wote ni ndugu, basi hakiwi halali chochote kwa mtu kutoka kwa nduguye isipokuwa kile alichompa kwa moyo safi.

6) Vitu vitatu moyo wa Muislamu usifanye hadaa juu ya vitu hivyo: Kufanya ikhlasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu katika matendo, kuwa na moyo safi kwa Maimamu wa haki na kushikamana na jamaa ya waumini.

7) Katika Uislamu watu wote ni sawa, watu wote wanatokana na Adam na Hawa hapana ubora kwa Muarabu juu ya asiyekuwa Muarabu isipokuwa kwa kumcha Mwenyezi Mungu.

8) Bila shaka Muislamu nduguye ni Muislamu, asimdanganye nduguye wala asimfanyie khiyana wala asimtete wala damu yake haiwi halali kwake wala kitu chake chochote hakiwi halali kwake isipokuwa kwa radhi ya nafsi yake.

9) Msije mkarudia kuwa makafiri wenye kupotea baada yangu, baadhi yenu wasiwakandamize wengine.

10) Kwa hakika ninyi mutaulizwa, basi aliyepo na amfikishie asiyekuwepo.

Kisha Mtume[s.a.w.w] aliwashuhudisha mara tatu mambo aliyoyabalighisha, nao masahaba wakashuhudia kwake juu ya hayo.[257] Na bila shaka mapokezi sahihi yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume[s.a.w.w] miongoni mwa dua na dhikri zinazohusu Hijja, mambo ambayo yameshikamana na maana za kisiasa pamoja na maana za Tauhidi. Ni ushahidi bora juu ya kuwa Hijja ni msimu unaonasibu (unaostahiki) kwa Waislamu kudhihirisha msimamo wao kwa maadui wa Mwenyezi Mungu na Uislamu na pindi tutakapofahamu kuwa ni mustahabu kuzikariri dua hizi wakati wa ibada kwa mfano dua ifuatayo: "Lailaha-illa-llah Wahdahu la Sharika Lahu Lahul Mulku Walahul-Hamdu Yuhyi Wayumitu Wahuwa Ala kulli shain Qadir." Lailah illa-llah Wahdahu Wahdahu Anjaza Waadahu Wanasara Abdahu Wahazamal-Ah-Zaba Wahdah.[258] Haya ni pamoja na ishara zinazopatika katika Manasikul Haj. Kila ibada iliyomo ndani ya ibada hizi inaashiria kwenye jambo la kijamii na kisiasa na kiakhlaq (Muenendo) zaidi ya kuwa kwake ni ibada na ni kutii japokuwa hatuwezi kujua kwa ukamilifu kila mama zilizomo katika Ibada hizi. Wanachuoni wengi wa Kiislamu na wanafikra wa Kiislamu wameyaashiria mambo yanayoelekezwa na ibada hizi, miongoni mwake yamo mambo ya kiroho, kiuchumi, kijamii na kisiasa, nasi tunamfupishia msomaji mtukufu ili kufanya mukhtasari.

Kwa hiyo kuna zaidi ya mambo ambayo yanajulisha kuwa Mtume[s.a.w.w] aliyachanganya matendo ya kiibada na matendo ya kisiasa katika Hijja. Ndani ya Bukhari, imepokewa kwa Said bin Jubair kutoka kwa Ibn Abbas amesema: "Pindi Mtume[s.a.w.w] alipofika katika mwaka aliopewa amani (mwaka wa saba Hijiriya) akasema, ongezeni mwendo (katika Saayi)". Mtume alifanya hivyo iii awaonyeshe washirikina nguvu za Waislamu. Ibn AI-Athir amesema ndani ya An-Nihayah, Mtume aliwaamuru Masahaba wake kuongeza mwendo katika Tawafu wakati wa umrah ya Qadhaa (mwaka wa saba Hijiriya) ili kuwaonyesha washirikina nguvu za Waislamu, kwa sababu washirikina walikuwa wakisema, "Limewadhoofisha joto la Madina" na ni sunna katika baadhi ya tawafu tu. Na pindi Uislamu ulipoimarika na kupata nguvu, Umar akasema, "Kuna haja gani sasa hivi kuongeza mwendo, yaani kutufu kwa aina ile, au kuacha wazi mabega, na Mwenyezi Mungu amekwisha yasawazisha mambo ya Waislamu na ameifukuza kufru na makafiri".

Ibn al-Athir amesema tena: "Muradi wa Umar kusema, Ramalani, maana yake ni tawafu pekee iliyosuniwa kwa ajili ya kuwaonyesha makafiri". Na hii inaashiria kuwa inajuzu kuziunganisha ibada za Hijja kwenye makusudio ya kisiasa na malengo yake ya Jihadi, kwa mfano kuwakhofisha maadui kama vile kuwaogopesha maadui na kupinga matendo yao na kuziangamiza njama zao na kuiumbua mipango yao. Kisha Je, hivi Mtume[s.a.w.w] kuzichagua Suratut-Tauhid "Qul-Huwallahu Ahad" na Suratul-Kafiruna katika Sala ya kutufu na kuzipendekeza zisomwe na muislamu anayehiji wakati kuna Sura nyingine na aya nyingine ambazo zinazo maana na malengo ya kiakhlaq na mafunzo zaidi na kushuhudia kwamba Hijja ni mkusanyiko wa Kiislamu wa ulimwengu na kwamba mkutano huu ni wakati mzuri wa kutangaza msimamo uliyo wazi dhidi ya nguvu za kufru na ubeberu kama ambavyo inajulisha hivyo (kwa mapokezi yasemayo) kwamba Umar Ibn Khattab pindi akipiga Takbira na kulibusu jiwe alikuwa akisema: "Bismillahi Wallahu Akbaru ala Mahadana, Lailaha illa llahu la Sharika lahu Amaantu Billahi Wakafartu Bittaghuti"[259]

Maana ya maneno hayo: "Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa juu ya aliyotuongoza, hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu asiye na mshirika, nimemuamini Mwenyezi Mungu na nimeyakufuru mataghuti". Kisha ni kwamba Imam Jaafar bin Muhammad As-Sadiq[a.s] amesema katika kubainisha falsafa ya Hijja kama ifuatavyo: "Bila shaka Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaumba viumbe si kwa ajili yoyote isipokuwa alitaka na akafanya, akawaumba mpaka ulipofika muda fulani akawaamuru na kuwakataza, kuhusu mambo ambayo yatakuwa ni miongoni mwa mambo ya utiifu katika dini na maslahi yao miongoni mwa mambo ya dunia yao, basi akafanya ndani yake mkusanyiko wa (watu) kutoka mashariki mpaka magharibi ili wafahamiane.... Na ili athari za mjumbe wa Mwenyezi Mungu[s.a.w.w] zitambulike na habari zake nazo zijulikane zisije zikasahaulika, na lau kila watu wangelitegemea miji yao na yaliyomo basi wangeangamia na miji ingeharibika na mapato na faida vingeanguka na khabari zingepotea na wasingefahamu chochote, basi hiyo ndiyo sababu (ya kuweko kwa) Hijja".[260]

Na vile vile imepokewa toka kwake Imam Jaafar As-Sadiq[a.s] amesema: "Hapana uwanja wowote unaopendwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko Mas-aa (Mahala pa Saayi baina ya Safa na Marwa) kwani mahala hapo hudhalilika kila mwenye nguvu.[261]

MALENGO YA HIJJA YA KISIASA NA YA KIJAMII KATIKA SERA YA SALAFU

Bila shaka historia inatusimulia kwamba Salafus-Salih hawakufupizika na matendo ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na ibada tu katika Hijja, bali munasaba huu wa Hijja waliutumia kwa ajili ya matendo ya kisiasa kuwa ni sehemu ya asili katika faradhi hii na siyo kitu chenye kuzidi juu yake au kilicho nje yake. Basi huyu hapa Imam Husein Ibn Ali ambaye ni mjukuu wa Mtume[s.a.w.w] anatoa hoja cihidi ya mtawala jeuri miongoni mwa watawala wa zama zake hapo Mina katika kipindi cha Hijja. Hakika Imam[a.s] aliwakusanya Bani Hashim wanaume na wanawake na wafuasi wao wenye kuhiji na wale wasiohiji na Ansari ambao ni wafuasi wake na watu wa nyumba yake, kisha hakumwacha yeyote miongoni mwa Masahaba wa mjumbe wa Mwenyezi Mungu[s.a.w.w] na watoto wao na (Tabiina) na Maansari waliokuwa mashuhuri kwa uchamungu na ibada. Basi wakakusanyika hapo Mina zaidi ya watu elfu moja na wengi wao walikuwa Tabiina na watoto wa Masahaba, na Imam Husein[a.s] akatoka kwenye hema lake akasimama kuhutubia, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamtukuza kisha akasema: "Amma baad, kwa hakika ujeuri huu tumefanyiwa sisi jambo ambalo nyote munalijua, mumeliona, mumelishuhudia na limekufikieni, nami kwa hakika nataka kuwaulizeni vitu fulani basi iwapo nitakuwa mkweli nisadikisheni, na nikiwa muongo, basi nikadhibisheni, sikilizeni usemi wangu na mufiche kauli yangu kisha murudi kwenye miji yenu na makabila yenu, yeyote mutayemuamini na mukawa na imani naye mwiteni (mumjulishe) yale muyajuayo kwani mimi naogopa haki hii itafutwa na kutoweka na Mwenyezi Mungu ndiyo mwenye kutimiza nuru yake japokuwa makafiri watachukia.[262]

Basi Imam Husein[a.s] hakukiacha chochote alichokiteremsha Mwenyezi Mungu ndani ya Qur'an kuhusu Ahlul Bait ila alikisema..... Na alisema: "Nakuombeni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mukirudi msimulieni yeyote munayemuamini". Kisha alishuka na watu wakatawanyika. Naye Uthmani lbn Affan anaiandikia miji yote ya Kilslamu zama za ukhalifa wake barua ambayo ndani yake alisema kama ifuatavyo: "Hakika mimi ninawalazimisha magavana wangu wanifikie katika kila msimu (wa Hijja) na kwa hakika umma umepewa madaraka ya kuamrisha mema na kukataza maovu, basi hapana chochote kitakachodaiwa dhidi yangu au dhidi ya magavana wangu ila nitampa anayestahiki, na sina mimi wala magavana wangu haki upande wa raia isipokuwa imeachwa kwao, na kwa hakika watu wa Madina wameniletea mashitaka kwamba kuna watu wanashutumu na kupiga (wenzao) basi yeyote mwenye kudai chochote katika hayo na aje kwenye msimu (wa Hijja) achukue haki yake ikiwa ni kutoka kwangu au kwa magavana wangu au msamehe kwa hakika Mwenyezi Mungu anawalipa wenye kusamehe.[263]

Bali hata wasiokuwa Waislamu walipata fursa ya kuaridhi mashtaka yao kwa Khalifa katika Hijja, basi Khalifa husimama kuwapatanisha ndani ya kipindi cha Hijja na siyo baada ya kipindi hicho, basi sote tunakijua kisa cha mtoto wa Kimisri aliyefanya mashindano na mtoto wa Amri bin Aas (gavana wa Misri) na yule Mmisri akashinda, mtoto wa Amri akampiga yule mtoto wa Kimisri, basi baba wa mtoto wa Kimisri akaeleza mashtaka yake kwa Umar, Umar akamchukulia kisasi katika msimu wa Hijja mbele ya macho na masikio ya maelfu ya mahujaji kisha akamwambia Liwali Amri lbn Al-Aas mbele ya ushuhuda wa mkusanyiko mkubwa: "Ewe Amri ni lini mumewafanya watu kuwa watumwa na hali ya kuwa mama zao waliwazaa wakiwa huru".[264] Na hapa inafaa tuashirie mambo aliyoyaandika mwandishi wa Kiislamu wa zama hizi muheshimiwa Dr. Yusuf Al-Qar-dhawi katika kitabu chake muhimu kuitwacho, 'Al-lbadatu-fil-Islam", kuhusu lengo hili.

"Makhalifa walitambua umuhimu wa msimu huu wa kiulimwengu, wakaufanya kuwa ndiyo nafasi ya kukutana baina yao na wanachi wanaokuja kutoka masafa ya mbali, na baina yao na magavana wao kutoka katika miji, basi yeyote miongoni mwa watu mwenye kudhulumiwa au mwenye mashitaka na ayalete kwa Khalifa mwenyewe bila ya wasita wowote wala kizuwizi, na huko wananchi wamkabili gavana mbele ya Khalifa bila ya woga wala kificho, basi hapo husaidiwa mnyonge na haki kupewa aliyedhulumiwa na haki kurejeshwa kwa mwenyewe hata kama haki hii ni ya gavana au Khalifa." Basi iwapo Hijja ni msimu wa kuibainisha dhulma na malalamiko yatendwayo na watawala na wasimamizi wa Kiislamu, je, haiwi ni bora zaidi kujulisha ndani yake malalamiko kwa wakoloni na wafuasi wao na watumishi wao na kuwasaidia Waislamu dhidi yao? Na Je, inajuzu kumlalamikia mtawala Muislamu anapovuka mipaka yake lakini haijuzu kumlalamikia mkoloni dhalimu mvamizi aliyetoka nje na hali yakuwa anafanya maovu na mauaji?.