UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI0%

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Vitabu mbali mbali

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi: SHEIKH JA'AFAR SUBHANY
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 48467
Pakua: 4233

Maelezo zaidi:

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 24 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 48467 / Pakua: 4233
Kiwango Kiwango Kiwango
UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi:
Swahili

2

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

KIASI CHENYE MAKOSA

Tunakwenda sambamba na mwandishi huyu wa Kiwahabi katika kitabu chake kisichokuwa na maana, na tunamuona anamkosoa Imam Ali ibn Abi-Talib [a] kwa njia ya kutaka kufahamu na kuuliza sababu za kufanya haraka kumuuzulu Muawiyah mara tu Imam Ali[a.s] alipotawalia (Ukhalifa) na anajiuliza anasema: Kwa nini, kwa nini? Bila shaka kilichompelekea kupinga ni kule kumlinganisha kwake Imam Ali[a.s] na watawala wenye kujali maslahi ambao hawafikiri isipokua maslahi yao binafsi na kuyatanguliza kuliko hukumu za sheria na wajibu aliowajibisha Mwenyezi Mungu, bali huupinda upande wa sheria kwa lengo la kulinda uongozi na utawala wao, basi kwa mujibu wao "lengo lao in kujisafishia wasiIa." Fikra hii potofu ndiyo iliyomfanya mwandishi huyo wa Kiwahabi ampinge kiongozi wa wachamungu Ali[a.s] kwa njia ya kuuliza na kutaka kufahamu. Naam, lau Imam Ali[a.s] angekuwa kama watawala wengine wanaojali maslahi yao, basi upinzani wa Wahabi huyu ungekuja hapa na angetakiwa awaache watu wapotofu na mafasid kama vile Muawiyah na mfano wake waendelee kuwatawala Waislamu kama zipendavyo nafsi zao za kishetani, lakini Imam Ali[a.s] siyo kiongozi wa aina hiyo ya watawala hao sivyo kabisa.

Kwa hakika ni kiongozi mwenye Ikhlas, kwani anasema Imam Ali[a.s] akimjibu Mughira ibn Shu'bah na walio kama Mughira "Mimi sitaki Mwenyezi Mungu anione ni mwenye kuwafanya wanaopotosha kuwa ni wasaidizi (wangu)".[14] Ewe msomaji mpendwa: Mpaka hapa tunafupisha maneno, na tunachokitarajia ni kwamba jibu hili la haraka tulilolileta limekuwekea wazi msimamo wa huyu Wahabi mwenye chuki dhidi ya kizazi cha Mtume Muhammad[s.a.w.w] na wafuasi wao na (na vile vile limekuwekea wazi) kufilisika kwake (Wahabi huyu) katika maarifa ya Dini na Itikadi za haki za Kiislamu na kukosea kwake na upotofu wake alioufanya kwa makusudi na riwaya zake za nongo. Nao wanachuoni wa dini na wanachuoni wa sheria ya haki watazishughulikia hujuma hizi mbaya za Kiwahabi, nasi tunataraji hivi karibuni apendapo Mwenyezi Mungu, litatolewa jawabu thabiti dhidi ya uzushi wa Wahabi huyu mpotofu mwenye kupotosha.

MWITO WA KUFANYIKA KONGAMANO LA KIISLAMU

Kwa hakika ni muhimu sana kufanyika kongamano la Kiislamu ambalo ndani yake yatatatuliwa Masail yenye Khitilafu kwa mujibu wa muongozo wa kielimu na Mantiq na dalili, kwani wakati huu wa sasa ziko khitilafu kubwa mbili ambazo ni Uwahabi na madhehebu mengine ya Kiislamu juu ya Tauhidi na shirki, basi Je, kwa lengo la kukurubiana pande hizi mbili si inafaa kufanya mkutano wa kielimu ambao Masail haya yataaridhiwa katika meza ya uchunguzi na uhakiki kwa lengo Ia kuondoa batili na kuithibitisha haki, kwani huenda ikachomoza nuru ya kuonyesha njia kwa wanaobabaika? Inabidi kongamano hili lifanyike kwa msingi wa kutatua tatizo na siyo propaganda tu, na lisichukuliwe kama vile ni jambo Ia propaganda ya Serikali fulani.

Na ili jambo hili lipate kukamilika kama inavyotakiwa, inapasa kuchunga sharti zifuatazo:

1. Mwito huo utolewe kwa wanafikra wa Kiislamu kutoka katika Madhehebu mbali mbali za Kiislamu ambao wanawakilisha Madhehebu hayo na wanafahamika khasa kuwa wao ni wanachuoni na ni wafikra wa dhehebu hilo (wanaloliwakilisha), na wasipelekewe mwito huu wanachuoni wa Pilato wa Saudia peke yao ambao wanapatikana India, Pakistani na Misri iliyodhulumiwa.

2. Na zaidi ya wawakilishi wa Madhehebu manne, ni lazima mwito huu utolewe kwa wanachuoni na wanafikra wa Shia Ithna-Asheriyyah na dhehebu la Zaydiyyah ili mkutano huo unenekane kwa muono wa pamoja na ujumla wa Waislamu wote.

3. Ni lazima utolewe uhuru kamili kwa wajumbe wa mkutano ili kila mmoja miongoni mwao aweze kujadili juu ya Masail yatakayokuwa yamearidhiwa kwenye uwanja (wa majadiliano), na awe na haki ya kuzitetea kwa uhuru fikra zake na itikadi zake, pia kongamano hilo lijiepushe na kila kitu kinachoharibu heshima ya wajumbe wake, miongoni mwa maneno ya matusi na dharau ambayo leo hii yameenea katika miji ya Saudia.

4. Na ni lazima idara inayoendesha kongamano isifungamane na upande wowote, na bora zaidi iwe imeundwa kutokana na Madh-hebu tofauti tofauti yanayoshiriki kwenye kongamano.

5. Utafiti wote unaofanyika kwenye kongamano usambazwe (kama ulivyo) bila ya mabadiliko yoyote ndani yake na utumwe kwenye vituo (vyuo) vya Elimu ulimwenguni ili wanaopenda kujua matokeo ya kongamano hilo wausome. Aina hii ya kongamano na kwa kuchunga sharti hizi, tunataraji Masail mengi mbali mbali yatatatuliwa, na kile kiini cha mafahamiano kitathibitika na maelewano baina ya Waislamu yatapatikana.

LENGO LA KITABU HIKI

Katika kitabu lilki tumejaribu kuchukua Masail ya msingi ambayo kuna hitilafu ndani yake baina ya Mawahabi na Madh-hebu mengine ya Kiislamu, na kuyatolea hukumu kwa mujibu wa Qur'an Tukufu na Sunna Tukufu ili tufahamu rai ya Uislamu katika Masail hayo. Na kitabu hiki siyo pekee ambacho tulichoandika kuhusu maudhui hizi, bali kimetanguliwa na vitabu vitatu na kila kimoja miongoni mwa hivyo kimebeba jukumu Ia kuchunguza na kuhakiki baadhi ya Masail haya, na vitabu hivyo ni:

1. Mafahimul-Qur'an: Na ndani yake kuna uchunguzi mpana juu ya Tauhidi katika ibada ndani ya juzuu ya kwanza ya kitabu hicho kutoka ukurasa wa 378 hadi 528, nayo ni mkusanyiko wa mihadhara iliyotolewa katika hauza ya elmu katika mji mtakatifu wa Qum, na akaiandika kwa kalamu Sheikh Jaafar al-Hadi na ikachapishwa nchini Iran na Lebanon.

2. At-Tawasul-Bil-Auliya: Ni uchunguzi unaohusu kujuzu kutawassal kwa Maimamu watakatifu (Amani iwashukie) na kutawassal kwa Mawalii wema wa Mwenyezi Mungu, na mas-ala haya ni miongoni mwa mas-ala muhimu ambayo Mawahabi wanaeneza Shub-ha (Utata) juu yake.

3. At-Tauhid Wash-Shirki Fil-Qur'anil-Karimu: Kwa hakika (ndani ya Kitabu hiki) nimejaribu kujihusisha na Mas-ail ya Tauhidi na shirki, na nimelitatua tatizo hili ambalo limekishughulisha kikundi hiki cha Mawahabi kwa muda wote wa karne mbili na nusu, na kimechapishwa katika nchi nyingi za ulimwengu.

Na mihadhara hii (iliyomo kitabuni humu) ni uchunguzi wa mara ya nne ambao tunautoa kwa ulimwengu wa Kiislamu, na tunawaita Mawahabi walioko Riyadhi na katika Haram mbili Tukufu na waandishi walioajiriwa na Mawahabi ambao wanaandika kwa Maslahi yao, waikubali haki wala usiwadanganye upinzani wa kijinga na wazinyenyekee dalili, na iwapo hawatakubali isipokuwa (kuendelea na) uadui na kupinga haki, basi sisi tunawapa changa moto ya kukijibu kitabu hiki kwa jawabu madhubuti linalokubalika, linalotegemea mantiki na siyo (jibu la) udanganyifu na uzushi. Na, Mawahabi wanalazimika kuwaacha huru Waislamu katika Haram mbili tukufu watende mambo yao matukufu ya dini, na wasiwakabili kwa uovu ndani ya Haram ya amani ya Mwenyezi Mungu na waache propaganda za Kiwahabi ambazo haziongezi chochote ndani ya Waislamu isipokuwa utengano, fitna na bughudha. "Bila shaka huu ni ukumbusho, basi yeyote atakaye na aishike njia kwenda kwa Mola wake". Jaafar Subhani

Chuo cha Elimu - Qum Tukufu

26 / Mfunguo Mosi /1406 A.H.

VIDOKEZO JUU YA MAISHA YA MUASISI WA UWAHABI

Madhehebu ya Kiwahabi yanahusishwa kwa Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi kuwa ndiyo muanzilishi wake. Madhehebu ya Sheikh huyu yameitwa "Wahabiyya" kwa munasaba wa jina lababa yake aliyekuwa akiitwa "Abdul-Wahabi". Ama sababu zilizofanya Madhehebu ya Kiwahabi yasiitwe "Muhammadiyya" kwa munasaba wa jina la muanzilishi wake, ni kama wasemavyo baadhi ya Wanachuoni kwamba, palifanywa tahadhari ya kuepusha kufanana baina ya hao wafuasi wa Kiwahabi na Waislamu wengine ambao ni wafuasi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Muhammad bin Abdillahi).[15] Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab alizaliwa mwaka 1115 A.H. katika mji wa Uyainah ambao ni miongoni mwa miji ya Najdi; na mzazi wake alikuwa kadhi wa hapo Uyainah. Tangu utotoni, Muhammad bin Abdul-Wahab alikuwa na shauku sana ya kusoma vitabu vya tafsiri, hadithi na mambo ya ambaye alikuwa ni miongoni mwa wanachuoni wa Kihanbal. Na tangu akiwa kijana, Muhammad bin Abdul-Wahabi alikuwa akiyakosoa mambo mengi ya Dini waliyokuwa wakiyatenda watu wa Najdi.

Sheikh huyu hakutosheka na Najdi peke yake katika upinzani wake huo, bali alivuka mipaka hadi Madina alikokwenda wakati akitoka Hija na kuendelea kusambaza upinzani huo. Kwa hakika hapo Madina, alikuwa akiwakemea wata waliokuwa wakitawasal kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu [s.w.t] kwenye kaburi lake tukufu. Baadaye alirejea Najdi na hatimaye akaenda Basra kwa lengo la kwenda Shamu. Alipokuwa Basra alianza kuwakemea watu na kuwakataza wasitende mambo yao ya dini, wenyeji wa Basra walipoiona hali hii, wakamtimua na kumfukuzilia mbali kutoka katika mji wao. Muhammad bin Abdul-Wahabi akakimbia na kuelekea katika mji wa Az-Zubair. Wakati akiwa njiani kuelekea Az-Zubair, Muhammad bin Abdul-Wahabi alichoka sana kutokana na mwendo wasafari hiyo, hivyo basi joto kali la jua lilimsababishia kiu kali kiasi cha kukaribia kufa; (Afadhali angekufa). Kwa bahati mtu mmoja kutoka Az-Zubair alimuona akamhurumia hasa kwa kuwa mavazi aliyokuwa amevaa yalikuwa ni mavazi ya watu wa dini basi mtu huyo akamnywesha maji Muhammad bin Abdul-Wahab; na akampandisha kwenye kipando chake na kumfikisha mjini.

Makusudio ya Muhammad bin Abdul-Wahabi ilikuwa ni kwenda mpaka Shamu, lakini kutokana na kukosa kwake chakula na mali ya kuweza kumudu safari hiyo, alisafiri mpaka Al-Ahsaa; kisha akaenda Huraimala ambao ni mji katika miji ya Najdi, na huo ulikuwa ni mwaka 1139 A.H. Katika mwaka huo huo, baba yake alihama kutoka Uyainah akaenda Huraimala. Hapo Muhammad bin Abdul-Wahabi akaungana na mzazi wake na akaendelea kusoma kwake. Katika kipindi hicho hicho, yeye aliendelea kueneza upinzani wake dhidi ya ibada mbali mbali za kidini katika nchi ya Najdi, jambo ambalo lilisababisha machafuko na kutokuelewana baina yake na baba yake kwa upande mmoja, na baina yake na watu wa Najdi kwa upande wa pili. Hali hii ya vurugu na kutoelewana iliendelea hadi mwaka 1153 alipofariki baba yake.[16] Kufariki kwa baba yake kulimpa nafasi nzuri Muhammad bin Abdul-Wahabi kutangaza wazi wazi itikadi zake za pekee. Alitembea huku na kule kueneza Aqida yake potofu, akawa anawakemea watu kutenda matendo ya dini, na kuwataka wajiunge katika kundi lake na wawe chini ya uongozi wake. Baadhi ya watu walihadaika na mwenendo wake, na wengine walimpinga.

Pamoja na hali hii, mambo yake yalijulikana wazi kwa watu wa mji wa Huraimala, na baada ya muda Muhammad bin AbdulWahabi alifunga safari kurudi Uyainah mahala alipozaliwa. Wakati huu Athumani bin Hamad alikuwa ndiyo mtawala wa hapo Uyainah, na alimpokea Muhammad bin Abdul-Wahabi na akamkaribisha kwa wema. Muhammad bin Abdul-Wahabi na mtawala huyo wa Uyainah walifanya makubaliano ya kila mmoja kumlinda mwenzake; ili mmoja wao awe na nguvu za kisheria na mwingine awe na nguvu za utekelezaji wa maamuzi yanayoamuliwa.

Kwa hiyo basi mtawala wa Uyainah akawa anamsaidia Muhammad bin Abdul-Wahabi kutekeleza malengo yake kwa kutumia nguvu za kiutawala, naye Muhammad bin Abdul-Wahabi humsaidia mtawala huyo kwa kutoa fatwa zinazowataka watu wamtii mtawala huyo na kuzifuata amri zake. Habari zilimfikia mtawala wa Al-Ahsaa kwamba, Muhammad bin Abdul-Wahabi anawalingania watu kwenye rai zake na uzushi wake, na pia kwamba mtawala wa Uyainah ndiye anayempa nguvu ya kufanya hayo. Mtawala huyu wa Al-Ahsaa alimwandikia barua kiongozi wa Uyainah kumuonya kwa kumsaidia kwake Muhammad bin Abdul-Wahabi. Barua hiyo alipoisoma, akamwita Muhammad bin Abdul-Wahabi na kumfahamisha kuwa yeye hatomsaidia tena.

Muhammad bin Abdul-Wahabi akamwambia mtawala wa Uyainah, "Iau ungenisaidia katika mwito wangu huu, ungeitawala Najdi yote". Mtawala huyo alikataa rai hiyo na akamuamuni Muhammad bin Abdul-Wahabi aondoke hapo Uyainah. Hivyo basi Muhammad bin Abdul-Wahabi akafukuzwa kutoka Uyainah hali ya kuwa mwenye kufedheheka. Tukio hili la kufukuzwa kwa Muhammad bin Abdul-Wahabi lilitokea mwaka 1160 A.H. na aliondoka hapo Uyainah akaelekea Dir'iyyah, mji ambao ulikuwa mashuhuri miongoni mwa miji ya Najdi. Mtawala wa hapo alikuwa in Muhammad bin Saud ambaye ndiye babu mkuu wa kizazi cha Saud (wafalme wa Saudi Arabia). Muhammad bin Abdul-Wahabi alipofika hapo, akatembelewa na mtawala huyo na akakirimiwa vizuri na kuahidiwa kutendewa mema. Naye kwa upande wake alimpa bishara mtawala huyo kwamba, ataitawala miji yote ya Najdi. Hivyo ndivyo yalivyotimia maafikiano ya wawili hawa, katika kutekeleza maovu yao dhidi ya Uislamu.

Ukweli ulivyo kuhusu watu wa Dir'iyya ni kwamba, watu hawa walikuwa ni masikini mno mpaka kipindi alichofika Muhammad bin Abdul-Wahabi na kufanya mapatano ya kusaidiana baina yake na Muhammad bin Saud. Anasema Ibn Bishri An-Najdi kama alivyopokea kutoka kwake Al-Alusi: "Watu wa Dir'iyya zama hizo (kabla ya kufika huko Muhammad bin Abdul-Wahab) walikuwa katika dhiki na taabu ya maisha, kwa hakika nilipata kushuhudia dhiki yao ya maisha hapo mwanzoni, na kisha baadaye katika utawala wa Suud, niliwaona wakaazi wale wale wa Dir'iyya wakiwa na mali nyingi na silaha zilizorembeshwa kwa dhahabu na fedha. Pia nikawaona wakiwa na farasi wazuri, vyombo vizuri na mavazi ya fahari na mambo mengine ambayo ni katika kuonyesha kuwa hali yao ya utajiri sasa imekuwa bora kiasi cha kushindwa kutaja kila kitu kwa ubainifu. "Wakati fulani niliona katika kipindi cha mkusanyiko mkubwa wa watu wa Ad-Dir'iyya (siku ya soko) makundi ya wanaume wakiwa upande mmoja, na makundi ya wanawake yakiwa upande mwingine. Basi katika makundi haya niliona vitu mbali mbali ikiwemo dhahabu, fedha, silaha, ngamia, mbuzi, farasi na mavazi ya fahari pamoja na vitu vingine vingi visivyoweza kutajwa kutokana na wingi wake, isitoshe uwingi wa watu waliokuwepo hapo ulikuwa unatazamika hadi upeo wa macho.

Nami nilikuwa nazisikia sauti za wauzaji na wanunuzi zikivuma kama mvumo wa kundi Ia nyuki.[17] Sasa basi, utajiri huu mkubwa wa Ad-Dir'iyya umetokea wapi? Ibn Bishri An-Najdi hakufichua siri hii; lakini historia inaonyesha kuwa Muhammad bin Abdul-Wahab ndiye aliyekuwa akizipata mali hizo kwa kupitia mashambulizi yake ya kuvizia yeye na wafuasi wake dhidi ya miji ya Kiislamu ambayo ilikuwa ikipinga kukubaliana naye na kumtii. Hivyo basi, akawa anapora mali na milki ya miji hiyo na kuigawa kwa watu wa Ad-Dir'iyya. Katika kugawa mali alizozipora kutoka kwa waislamu waliokataa kumtii, Muhammad bin Abdul-Wahabi alikuwa akitumia njia ya pekee aliyojipangia, kwani ugawaji wake ulikuwa ni kwa namna apendavyo yeye. Wakati mwingine alikuwa akigawa mali hiyo baina ya watu wawili na watatu miongoni mwa wafuasi wake ijapokuwa mali hiyo ilikuwa nyingi. Ama mtawala wa Najdi yeye alikuwa akichukua fungu lake kwa ridhaa ya Muhammad Bin Abdul-Wahab mwenyewe.

Na katika mambo muhimu yanayoonyesha uasi wa Muhammad bin Abdul-Wahab, ni sera hii mbaya aliyowafanyia Waislamu waliokataa kutii matamanio yake na rai zake; akawa anawatendea nambo yanayostahiki kufanyiwa kafiri anayeupiga vita Uislamu. Bwana huyu alihalalisha mali za Waislamu ziporwe na heshima zao zivunjwe. Kwa kifupi, Muhammad bin Abdul-Wahabi alikuwa akilingania watu Tauhidi ya Mwenyezi Mungu, lakini Tauhidi aliyokuwa akiilingania yeye ilikuwa isiyo na maana sahihi; kwa sababu ilitokana naye mwenyewe, wala siyo ile Tauhidi inayolinganiwa katika Qur'an.

Ikawa yule anayekubali Tauhidi yake husalimika nafsi yake na mali yake, ama anayekataa basi huambiwa kuwa ni kafiri anayeupiga vita Uislamu, na kumwaga damu yake na kuchukua mali yake inatangazwa kuwa ni halali. Wafuasi wa Muhammad Abdul-Wahab wakawa wanazusha vita katika Najdi na nje ya Najdi, kama vile Yemen, Hijaz na sehemu za Syria na Iraq. Na kila mji waliyouteka, walikuwa wakiruhusu kufanya katika mji huo mambo yoyote wayapendayo; kiasi kwamba kila walipoweza kuiunganisha miji hiyo kwenye utawala wao waliiunganisha, na kama hawakuweza basi walitosheka na uporaji wa mali peke yake.[18]

Vile vile Muhammad ibn Abdul-Wahab alimuamuru kila aliyehadaika na wito wake huo wa Tauhidi potofu afike kwake na kula kiapo cha utii (Bai'ah); na yeyote atakayekataa ni lazima auawe na mali yake igawiwe. Na kwa sababu hii, aliwashambulia watu wa kijiji cha Al-Fusul kilicho pembezoni mwa Al-Ahsa, akawaua watu mia tatu na akapora mali zao. [19] [19] Ulipofika mwaka 1206 A.H. Muhammad ibn Abdul-Wahab alifariki dunia lakini wafuasi wake waliendeleza uzushi wake na upotovu wake. Na ilipokuwa mwaka 1216 Wahabi Amir Suud aliandaa jeshi kubwa lipatalo watu elfu ishirini, wakafanya mashambulizi ya kinyama katika mji mtukufu wa Karbala nchini Iraq. Mji wa Karbala ni mji mtukufu tangu hapo zamani mpaka sasa, na unao umaarufu mkubwa na mapenzi kwa waumini, na watu haukusudia kwa ajili ya ziyara kutoka sehemu mbali mbali na mataifa tofauti tofauti wakiwemo Wairan, Waturuki, Waarabu na wengineo.

Majeshi hayo ya Kiwahabi, yaliuzingira mji huu mtukufu na kufanya mauaji mengi na kupora mali, kuubomoa na kufanya kila aina ya uovu. Kwa hakika Mawahabi kwa kuishambulia Karbala tukufu walitenda jinai kubwa na walileta msiba usio mfano, kwani waliwaua watu wapatao elfu tano au zaidi, mpaka yasemekana waliwauwa watu wapatao elfu ishirini. Baada ya Amir Suud kumaliza mashambulizi ya kivita dhidi ya wakazi wa mji wa Karbala, alielekea kwenye Haram Tukufu ya Imam Husein bin Ali[a.s] , ambayo ilikuwa imejaa hazina mbali mbali nzuri na zawadi nyingi za thamani zilizotolewa na wafalme mbali mbali na Maamiri pamoja na watu wengine kwenye uwanja mtukufu wa Kaburi Ia Imam Husein[a.s] nazo akazipora.

Baada ya msiba huu unaoumiza roho, mji wa Karbala ulionekana wazi kuwa umekumbwa na huzuni kubwa na masikitiko kutokana na unyama uliofanywa na Mawahabi. Hali hii iliwatawanya washairi wengi wa Kiislamu watunge Mashairi ya kuomboleza msiba ulioufika mji huu Mtukufu wa Karbala.[20] Siyo tu kwamba Mawahabi walitosheka na shambulio hilo la kwanza dhidi ya mji wa Karbala na viunga vyake, bali waliendelea kufanya mashambulizi mara kwa mara karibu muda wa miaka kumi na miwili. Pia Mawahabi walikuwa wakiushambulia mji Mtukufu wa Najaf na kufanya uporaji, na kama tulivyokwisha sema, shambulio la mwanzo dhidi ya Karbala lilikuwa mwaka 1216 A.H.

Waandishi wa Kishia wameafikiana kwamba, tukio hilo Ia mashambulizi dhidi ya mji wa Najaf lilifanyika siku ya kumbukumbu ya Ghadir ambayo Mtume[s.a.w.w] alimbainisha Imam Ali bin Abi Talib kuwa ndiyo Khalifa wake baada ya kuondoka kwake yeye Mtume[s.a.w.w] . Ili kuifahamu kumbukumbu ya Ghadir, rejea: Kitabu cha Al-Ghadir cha Al-Aminiy, Juz. 1. Anasema Marhum Al-Allamah As-Sayyid Jawad Al-'Amili kuhusu mauaji yaliyofanywa na Mawahabi huko Karbala na Najaf: "Hakika Mwenyezi Mungu kwa hisani yake na fadhila zake pia kwa baraka za Mtume Muhammad na kizazi chake amejalia kutimia kwa Juzuu hii ya kitabu, "Miftah Al-Karamah" "usiku wa manane kuamkia tarehe tisa ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka 1225 A.H. kwa mkono wa mwandishi wake..... (kazi hii ya kuandika kitabu hiki nimeifanya kutokana na ushawishi wa kimawazo pia kutokana na hali ya mambo kuharibika". Anaendelea kusema:

"Kwa hakika mabedui wenye imani za Kiwahabi kutoka Unaizah, (ambao wamekwisha toka katika Uislamu) waliuzingira mji mtukufu wa Najaf na kaburi la Imam Husein[a.s] katika Karbala, wakazifunga njia zote kisha wakawapora watu waliokuwa wakitoka kumzuru Imam Husein[a.s] katika ziyara ya nusu ya mwezi wa Shaaban, wakawaua watu wengi, na wengi waliouawa walikuwa Waajemi. Yawezekana idadi ya watu waliouawa ilikuwa mia moja na hamsini na pengine chini ya idadi hiyo kama inavyosemekana."[21]

Kwa ujumla, Tauhidi aliyokuwa akiilingania Muhammad ibn Abdul-Wahabi na kundi lake ilikuwa ni ile isemayo kwamba "Mwenyezi Mungu ana mwili wenye viungo na anapo mahala pake maalum (na walikuwa wanahalalisha damu na mali za wenye kupinga kauli yao hiyo)". Bwana Al-Alusi anasema kuhusu Tauhidi ya Mawahabi: "Mawahabi wanaziamini hadithi zisemwazo kuwa zimetoka kwa Mtume[s.a.w.w] kwamba, Mwenyezi Mungu hushuka hadi kwenye mbingu ya dunia kisha hauliza, "Je, kuna yeyote mwenye kutaka msamaha?"[22] .

Al-Alusi anaendelea kusema: "Mawahabi wanaitakidi pia kwamba, Mwenyezi Mungu atakuja siku ya Qiyama kama alivyosema katika Qur'an "Waja'a Rabbuka Wal Malaku Saffan Saffa", na wanaammi kwamba Mwenyezi Mungu hujisogeza kwa viumbe vyake namna apendavyo kama alivyosema katika Qur'an: "Nasi tuko karibu mno na binadamu kuliko mshipa wa shingo yake".[23] Katika kitabu cha Ibn Taymiyyah kiitwacho "Ar-Radd AlalAkhnaiy", kana ushahidi ulio wazi kwamba, yeye Ibn Taymiyyah alikuwa akiitakidi hadithi zilizopokelewa kuhusu fadhila za kumzuru Mtume[s.a.w.w] kuwa ni za uzushi, na kwamba anyeitakidi kuwa mjumbe wa Mwenyezi Mungu yu hai baada ya kufariki kwake kwa uhai kama ule wa zama alipokuwa duniani, basi mtu huyo atakuwa katenda dhambi kubwa. Na hivi ndivyo anavyoitakidi Muhammad ibn Abdul-Wahabi na wafuasi wake; lakini hawa wamezidi mno kuliko Ibn Taimiyyah katika upotovu na kuvuruga. Itikadi hizo mbovu za Kiwahabi zimekuwa ni sababu ya kuwafanya watu wanaotafiti juu ya dini ya Kiislamu kwa kupitia vitabu vya Mawahabi, wauone Uislamu kuwa ni Dini isiyo ya maendeleo na wala haiwezi kutegemewa kukidhi mahitaji ya maisha ya watu katika nyakati zote.

Mmarekani mmoja aitwaye "Lutrub Studard" anasema: 'Walisimama katika misingi hiyo watu wengi wanaoukosoa Uislamu, wakayafanya Madh-hebu ya Uwahabi kuwa ni ushahidi wa maneno yao wakasema, 'Hakika Uislamu kwa asili yake na mazingira yake, haukubali mabadiliko kulingana na wakati, wala haukubali maendeleo na mabadiliko ya hali, na Uislamu hauwezi kuwa tumaini katika maisha".[24]

Inapasa kusemwa kwamba wanachuoni wa Madh-hebu ya Hanbal tangu hapo mwanzo walimpinga Muhammad ibn Abdul Wahab na kupitisha uamuzi kuwa yeye amepotea, na kwamba hizo itikadi zake siyo sahihi. Na mtu wa kwanza kumpinga Muhammad ibn Abdul-Wahabi na kutangaza vita dhidi yake, alikuwa ni baba yake, kisha ndugu yake aliyekuwa akiitwa Sheikh Suleiman, na wawili hawa walikuwa ni wanachuoni wa Kihanbal. Ama huyu Sheikh Suleiman yeye aliandika kitabu cha kuzipinga itikadi za Muhammad ibn Abdul-Wahabi kiitwacho "As-Sawaiqul-llahiyyah Fi Araddi Al-Wahabiyyah". Ndani ya kitabu hicho amezipinga itikadi potofu na uzushi wa nduguye. Mufti wa Kis-Shafi'i katika Makka, Ash-Shaykh Zaini Dahlan, anasema kama ifuatavyo:- "Mzazi wa Muhammad ibn Abdul-Wahab ambaye ni Sheikh Abdul-Wahab, alikuwa ni mtu mcha Mungu miongoni mwa wanachuoni, naye Sheikh Suleiman ambaye ni ndugu wa Muhammad ibn Abdul-Wahab vile vile alikuwa miongoni mwa wanachuoni. Kwa kuwa Sheikh Abdul-Wahab na Sheikh Suleiman, toka hapo mwanzo walikuwa wakizifahamu fikra potofu za Muhammad ibn Abdul-Wahab hasa pale alipokuwa akiendelea na masomo yake huko Madina, walikuwa wakimlaumu na kuwatahadharisha watu kutokana naye." [25] .

Naye Abbas Al-'Aqqad Al-Misri anasema: "Mpinzani mkubwa wa Muhammad ibn Abdul-Wahab ni nduguye aliyekuwa akiitwa Sheikh Suleiman, ambaye ndiye mwandishi wa kitabu kiitwacho "As-Sawaiqul Ilahiyya". Sheikh Suleiman hakukubaliana kuwa nduguye (Muhammad ibn Abdul-Wahab) eti alikuwa amefikia daraja ya ijtihadi na akaweza kuifahamu Qur'an na Sunna. Na kwa maoni ya Sheikh Suleiman ni kwamba, zile bid'ah ambazo maimamu walikuwa wakiziona karne baada ya karne na hawamkufurishi mwenye kuzitenda, basi sisi hatuna haki ya kumkufurisha mtu kwa sababu ya hizo bid'ah wala hatuwezi kuhalalisha vita dhidi ya watu wanaotenda matendo hayo.

Anasema tena Sheikh Suleiman: "Mambo haya yalikuwepo sika nyingi hata kabla ya Imam Ahmad ibn Hanbal katika zama za Maimamu wa Kiislamu, na wenye kuyapinga waliyapinga miongoni mwa maimamu hao, na yaliendelea kuwepo mpaka yakaenea katika miji yote ya Kiislamu. Na matendo yote haya ambayo ninyi Mawahabi mnawakufurisha watu kwa kuyatenda, haikupokewa kutoka kwa Maimamu wa Waislamu kwamba, wao walimkufurisha mtu kwa ajili hiyo, wala hawakusema eti watendao matendo haya wameritadi, na wala maimamu hao hawakuamuru kuwapiga vita watendao mambo haya, wala hawakuiita miii ya Waislamu kuwa ni miji ya shirki na vita kama msemavyo ninyi; bali ninyi mmezidi mno kiasi cha kumkufurisha hata mtu asiyewakufurisha watu watendao haya japokuwa yeye mwenyewe hakuyatenda".[26]

Ni wazi kabisa kwamba, Muhammad ibn Abdul-Wahab siyo mtu wa mwanzo kutoa hizo rai zake na fikra zake azitoazo, bali yule aliyemtangulia tangu karne nyingi zilizopita ambaye ni Ibn Taymiyyah al-Harrani pamoja na mwanafunzi wake aitwaye Ibnul-Qayyim Al-Jauziyyah, na wengineo kama hawa, fikra za wote hawa hazikuanzisha madhehebu kama alivyozusha jambo hilo mwana wa Abdul Wahab.