UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI0%

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Vitabu mbali mbali

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi: SHEIKH JA'AFAR SUBHANY
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 48465
Pakua: 4233

Maelezo zaidi:

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 24 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 48465 / Pakua: 4233
Kiwango Kiwango Kiwango
UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi:
Swahili

4

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

KUMBUKUMBU ZA KIISLAMU NI DALILI YA KUENDELEZA DINI

Hapana shaka kwamba kuhifadhi kumbukumbu za Manabii na hasa zile za Nabii Muhammad[s.a.w.w] pamoja na kaburi Ia Mtume[s.a.w.w] na makaburi ya wakeze, wanawe na masahaba wake, na vile vile nyumba walizokuwa wakiishi na misikiti walimokuwa wakisali, hapana shaka kabisa kwamba mambo haya yanazo faida nyingi na yanayo matokeo mazuri. Tunataja baadhi ya faida hizo kama ifuatavyo: Leo hii baada ya kupita karne ishirini tangu kuzaliwa Nabii 'Isa [a.s] yeye na mama yake na kitabu chake cha Injili pamoja na wale wafuasi wake maalum (Hawaariyyuun) kwa mtazamo wa watu wa magharibi wamegeuka kuwa kama masimulizi yasiyo na ukweli, na baadhi ya wataalamu wanatia shaka hata kuwa je, alikuwako mtu aitwaye Masih 'Isa au mama yake aitwaye Mariyam, au kitabu chake kiitwacho lnjili. Na habari za Nabii 'Isa[a.s] wanazichukulia kuwa ni mazungumzo tu yasiyo na ukweli na kwamba yanafanana na ngano za Laila Majnuun.

Basi kwa nini imekuwa hivyo? Hii ni kwa sababu hakuna athari yoyote inayoonekana kuhusu Nabii 'Isa[a.s] . Kwa mfano: Haifahamiki kabisa ni mahali gani Nabii 'Isa[a.s] alipozaliwa; na iko sehemu gani nyumba aliyokuwa akiishi, na hi mahali gani alipozikwa? (Kwa mujibu wa madai ya Wakristo kuwa Nabii 'Isa[a.s] aliuawa). Kwa upande wa kitabu chake kilichoteremshwa toka mbinguni, kitabu hiki kimeingiliwa na mikono ya watu waliokigeuza na kukibadilisha na kuzua mambo mbalimbali. Na hizi Injili nne zilizomo mikononi mwa watu hazina uhusiano wowote na Nabii 'Isa[a.s] , na wala siyo ile Injili yake; bali hizo ni Injili za kina Matayo, Yohana, Marko na Luka.

Ndiyo maana basi, utaviona mwishoni mwake vinataja kisa cha kuuawa kwa Nabii 'Isa[a.s] na kuzikwa kwake. Basi ukweli halisi ulivyo ni kuwa, lnjili hizo zimeandikwa baada ya Nabii 'Isa[a.s] kutoweka. Na kwa msingi huu basi wengi wa watafiti na wachunguzi wanaitakidi kwamba, Injili hizi nne ni miongoni mwa vitabu vya mafunzo tu ambayo historia yake inaanzia karnye ya pili ya masihiya. Na lau kama vingekuwepo vitu muhimu vinavyomuhusu Nabii Isa[a.s] vimehifadhiwa, vingelikuwa ndiyo dalili madhubuti ya kuthibitisha kuwepo kwake, na maisha yake yalivyokuwa; na pia vingeonyesha utukufu wake, na wala kusingekuwa na nafasi ya kuzusha mashaka na maswali mengi toka kwa wataalam wenye mawazo potofu.

Ama kwa upande wa Waislamu, wao wanaukabili ulimwengu bila ya hofu na wanasema: "Enyi watu, kwa hakika kuna mtu kutoka katika ardhi ya Hijazi aliyetumwa kuja kuiongoza jamii ya wanadamu tangu miaka elfu moja na mia nne iliyopita, na ameuthibitisha ushindi wenye mafanikio katika jambo lake hilo (la dini) na hizi hapa kumbukumbu za maisha yake zimehifadhiwa kikamilifu katika miji ya Makka na Madina". Wanaendelea kusema: "Hii hapa ndiyo nyumba alimozaliwa na hili hapa ni pango la Hiraa mahala ambapo Wahyi na ufunuo vilimshukia, na huu ndiyo Msikiti wake ambamo alikuwa akisalisha ndani yake, na hii hapa ndiyo nyumba alimozikwa na hizi ni nyumba za wanawe, wakeze, na jamaa zake, na makaburi haya ni ya kizazi chake na mawasii wake[a.s] ."

Sasa basi, iwapo sisi tutaziondosha kumbukumbu hizi zinazojulisha kuwa Mtume[s.a.w.w] alikuweko, na takaondosha dalili zinazoashiria utukufu wake na ukweli wake, tutakuwa tayari tumeandaa njia kwa maadui wa UisIamu waseme yale wayatakayo dhidi yetu na Uislamu wetu. Kwa hakika kubomoa kumbukumbu za Mtume[s.a.w.w] na zile za watu watukufu wa nyumba yake, siyo tu ni kuwakosea wao na kuvunja heshima yao, bali ni kufanya uadui dhahiri dhidi ya Utume wenyewe kwa nafsi yake na Mtume[s.a.w.w] mwenyewe na vitambulisho vya dini aliyokuja nayo. Ujumbe wa dini ya Kiislamu ni ujumbe wa kudumu milele; na Uislamu utaendelea kuwa ndiyo dini pekee inayowafaa wanaadamu mpaka siku ya Kiyama; na vizazi vijavyo havina budi kukiri ukweli wake na kuamini utukufu wa ujumbe huu.

Na ili litimie lengo hili, ni lazima kuzihifadhi kumbukumbu za Mtume[s.a.w.w] ili tupige hatua mbele katika njia za kuendeleza dini hii na kuifanya ibakie milele kiasi ambacho asiwe na shaka mtu ye yote juu ya kuwepo kwa Nabii wa Uislamu[s.a.w.w] kama ambavyo watu wamefanya shaka kuhusu kuweko kwa Nabii 'Isa [a.s] (kutokana na kupotea kwa kumbukumbu zake). Waislamu (kwa upande wao) wamelipatia umuhimu mkubwa jambo la uwekaji kumbukumbu za Nabii Muhammad[s.a.w.w] ikiwemo sera zake na mwenendo wake kiasi kwamba wameyasajili katika historia mambo yake madogo madogo yanayohusiana na maisha yake na athari zake za kipekee.

Wameandika pia maelezo yanayohusu pete yake na viatu vyake, mswaki wake na upanga wake, deraya yake, mkuki wake na farasi wake, ngamia wake na hata mtumishi wake na mpaka wameandika visima alivyokunywa maji na ardhi aliyoitoa wakfu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. (Waislamu) wameandika pia aina ya chakula ambacho Mtume[s.a.w.w] alikuwa akikipenda na zaidi ya hayo wameandika hata namna ya kutembea kwake na kula kwake na kunywa kwake na pia namna ya ndevu zake zilivyokuwa na alivyokuwa akizipaka hina na mengineyo. Na baadhi yakumbukumbu hizo bado zimebakia mpaka katika siku zetu hizi.[31]

Na kila inaporejewa historia ya Uislamu na kuichunguza hali ya miji ya Kiislamu na kumbukumbu zilizomo, inadhihirika wazi kabisa kwamba, kujenga juu ya makaburi ili kuyahifadhi yasitoweke ni jambo lililokuwa likifanyika kwa Waislamu wote katika sehemu mbali mbali za miji mikubwa ya Kiislamu, na mpaka sasa yako madhariha yaliyowekwa kwenye makaburi ya Manabii na ya watu wachamungu kiasi kwamba Waislamu wanakwenda kufanya ziyara kwenye sehemu hizo na kuomba dua. Na Makaburi hayo yanahesabiwa (kuwa ni miongoni mwa kumbukumbu za kihistoria za Kiislamu. Vile vile katika sehemu hizo kuna waqfu nyingi zilizowekwa ambazo kipato chake hutumika katika kuimarisha hifadhi ya kumbukumbu hizo na kusafisha mazingira yake na mengineyo.

Ukweli ulivyo ni kwamba makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu yalikuwa yamejengewa hata katika nchi ya Hijazi yenyewe, na kabla fitana hii ya Mawahabi haijaingia na kuikalia Haram ya Makka na Madina pamoja na pembezoni mwake, kulikuwa na makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu katika kila upande wa nchi ya Hijazi yamejengewa yakipata hadhi kutokana na kupewa heshima na Waislamu wote, na wala hapakuweko mwanachuoni yeyote aliyekemea kubakia kwa makaburi hayo au aliyepinga kujenga juu yake. Wala siyo kwamba nchi ya Iran peke yake ndiyo ambayo kunapatikana makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu yaliyojengewa juu yake, bali hali hii imeenea katika nchi za Kiislamu, hasa hasa Misri, Syria, Iraq, Morocco, Tunisia na Jordan.

Katika miji hiyo kuna makaburi ya wanachuoni wakubwa wa Kiislamu yamejengewa, na Waislamu wanayatembelea kwa wingi na kusoma Qur'an wafikapo hapo, hasa Surah al-Fatiha na kumuomba Mwenyezi Mungu azipeleke thawabu za kisomo chao kwa roho za walioko kwenye makaburi hayo. Vile vile kwenye makaburi hayo wapo wafanyakazi wanaosimamia ulinzi, huduma, usafi na hifadhi ya sehemu hizo. Baada ya maelezo yaliyotangulia, itakuwaje ni haramu kuyajengea makaburi wakati desturi iliyokuwa ikifuatwa tangu mwanzo wa kuja Uislamu hadi leo inaendelea kutumika kitu ambacho wanachuoni wanakiita kuwa ndiyo sera ya Waislamu ambayo mizizi yake inakwenda hadi kuzifikia zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu, au zama za Maimamu watukufu wa nyumba ya Mtume[s.a.w.w] .

Kwa hakika sera hii imesimama kwenye msingi wa ruhusa ya kujenga juu ya makaburi; bali inathibitisha umuhimu na kupendekezwa kwa jambo hili; na halikupata kupingwa na upinzani wa aina yoyote muda wote wa kuwepo kwake kitu ambacho kinaonyesha kuwa linayo asili kwa Waislamu na linafaa wakati wote, na kwamba limekuwa katika sunna zenye kufuatwa kwa Waislamu. Mwandishi mmoja wa Kiwahabi anakiri uasili wa jambo hili alipoandika akasema: "Jambo hili limeenea katika miji na limeenea ulimwenguni mashariki na magharibi kiasi kwamba hapana mji katika miji ya Kiislamu isipokuwa yamo makaburi na maziyara, zaidi ya hapo misikiti mingi haikosi kuwa na kaburi na ziyara; na wala haingii katika akili ya mtu kabisa kwamba jambo hili ni baya, kiasi cha ubaya nilioutaja, na kisha wanachuoni wa Kiislamu wanyamaze kimya."[32]

Ni ajabu kwamba mwandishi huyu wa Kiwahabi anakiri kuwa sera ya Waislamu inao msimamo wa kujenga juu ya makaburi ya watu wacha Mungu na kuyatukuza, lakini utamuona kuwa hakuacha uovu wake na dhamira yake mbaya, na utamuona analiona jambo hili kuwa ni baya na anawalaumu wanachuoni kwa kukaa kwao kimya na anadai kwamba kimya cha wanachuoni hao wa kale kwa muda mrefu hakiwazuwii wanachuoni wa zama hizi kulikemea jambo hilo. Lakini jibu lake liko wazi mno. Basi ni vipi wanachuoni wanyamaze muda wote wa karne saba wasitamke chochote? Je, wote hawa katika karne hizo zilizopita walikuwa wakilinyamazia jambo baya na wakijizuwiya kulikataza kama anavyodai Wahabi huyu? Katika zama za Khalifa Omar bin Khattab Waislamu walipoiteka Bait-al-Muqaddas, ni kwa nini Omar hakuamrisha makaburi ya Manabii yaliyoko hapo yabomolewe? Basi je, enyi Mawahabi mwamuona Omar kwamba ni mwenye kukubaliana na washirikina?

JAWABU LA WANACHUONI WA MADINA

Jambo la ajabu katika maudhui haya ya kujenga juu ya makaburi ni lile jawabu linalonasibishwa kuwa limetoka kwa wanachuoni wa Madina, waliposema: "Ama kujenga juu ya makaburi, ni jambo Iililokatazwa kwa ijma'i, na hii ni kutokana na hadithi sahihi zilizokuja kuzuwiya jambo hili, na kwa ajili hii wametoa fatwa wanachuoni wengi kuwa ni wajibu kuyabomoa". Lakini ni vipi madai ya Ijma'i yatasihi katika kuharamisha kujenga juu ya makaburi, wakati VVaislamu walimzika Mtume[s.a.w.w] katika nyumba aliyokuwa akikaa Bibi Aisha kisha baadaye wakawazika katika nyumba hiyo hiyo Abubakar na Omar; tena karibu kabisa na Mtume kwa nia ya kupata baraka, na hatimaye walijenga ukuta uliotenganisha, sehemu moja ikawa ni makazi ya Bibi Aisha na sehemu nyingine ikawa ni makaburi ya Mtume[s.a.w.w] na Abubakar na Omar.

Ilipokuwa ukuta huo wa kutenganisha sehemu hizo mbili ni mfupi, uliongezwa urefu katika zama za Abdallah bin Zubair, na kisha nyumba hii yenye makaburi haya ikawa hujengwa upya kila zama na karne zinavyopita kwa ujenzi wa kitaalam ulivyo katika kila zama. Na katika wakati wa utawala wa Banu Ummaya na Banu Abbas ujenzi wa kaburi Ia Mtume[s.a.w.w] ulipewa umuhimu na heshima kubwa na uliendelea kujengwa upya kwa mujibu wa utaalamu uliokuwepo katika zama zile. Jengo Ia mwisho lililojengewa kaburi tukufu la Mtume[s.a.w.w] ambalo mpaka leo lipo, ni lile lililojengwa wakati wa Sultan Abdul Hamid (wa Uturki) mwaka 1270 A.H. sawa na mwaka 1869 A.D., na ujenzi huu ulimalizika kwa muda wa miaka minne.

Ewe msomaji, unaweza kurejea kitabu kiitwacho Wafa'ul-wafa cha As-samhudi, kutoka ukurasa 383 hadi ukurasa 390 ili upate maelezo kwa urefu juu ya kujengewa kaburi la Mtume[s.a.w.w] na kufanywa upya na kuimarishwa ujenzi wake katika historia ya Uislamu mpaka kufikia zama za huyu As-samhudi katika vitabu vya historia ya mji wa Madina.

C. HADITHI YA ABUL-HAYYAJ

Hivi sasa umefika wakati wa kuichunguza hadithi wanayoitegemea Mawahabi kuharamisha kujenga juu ya makaburi. Kabla ya yote tunaitaja hadithi yenyewe kwa sanadi aliyoipokea Muslim katika kitabu chake. "Ametusimulia Yahya ibn Yahya, na Abubakar ibn Abi Shaiba na Zuhayr ibn Harb, Yahya ametusimulia; (na watu wawili wa mwisho wamesema): Ametusimulia Waki'i, amepokea kutoka kwa Sufyan, toka kwa Habib bin Abi Thabiti, naye kapokea kwa Abi Wa'il ambaye kapokea toka kwa Abil Hayyaj Al Asadi' amesema: "Ali ibn Abi Talib alimambia: Je, nikutume kwa jambo ambalo Mtume wa Mwenyezi Mungu alinituma kwamba, usiache sanamu yoyote ila uiondoshe wala kaburi lolote lile lililonyanyuka isipokuwa ulisawazishe".[33] Hadithi hii Mawahabi wameifanya kuwa ndiyo dalili ya kuharamisha kujenga juu ya makaburi bila hata ya kufanya uchunguzi wowote kwa watu walioipokea na Sanadi yake.

KUIJADILI HADITHI

Kwa ujumla tunapotaka kutoa ushahidi kwa kutumia hadithi ili tutoe hukmu miongoni mwa hukmu za Mwenyezi Mungu, hapana budi hadithi hiyo itimize masharti haya mawili:

1) Kusihi kwa Sanadi: Hii ikiwa na maana kwamba, wapokezi na watu wahusikao kwenye hadithi yenyewe katika kila ngazi wawe ni waaminifu kiasi ambacho iwezekane kuwategemea katika maneno yao.

2) Ushahidi wa hadithi: Maana yake ni kwamba, matamko na sentensi zilizomo katika hadithi hiyo ziwe zimetimia katika kuelekeza makusudio yetu kwenye hadithi hiyo, kiasi waweze kuifahamu na wengine wanaofahamu vizuri lugha iliyomo katika hadithi hiyo, na wazifahamu pia kanuni zake kama tunavyozifahamu sisi na waweze kutoa matokeo tunayoweza kuyatoa.

Na kwa bahati nzuri, hadithi ya Abul-Hayyaj imekosa sharti zote mbili na hasa ile ya pili, kwani hakuna mahusiano yoyote kabisa ya kujenga juu ya makaburi katika hadithi hiyo.

UFAFANUZI WA MAMBO HAYA

(A) Ama upande wa Sanad, ndani ya hadithi hii wamo wapokezi ambao wanachuohi wa hadithi hawakuafikiana juu ya uaminifu wa wapokezi hao, tin hapa chini tunataja majina ya wapokezi waliomo katika hadithi hii ambao wanachuoni wa hadithi wamezikataa hadithi zao:

1) Waki'

2) Sufyan Ath-Thauri

3) Habib ibn Abi Thabit

4) Abu Wai'l Al-Asadi.

Wapokezi hawa wanne amewatia kasoro Al-Hafiz ibn Hajar Al-'Asqalani katika kitabu chake kiitwacho "Tahdhibut-Tahdhib, na amewataja kwa sifa ambazo zinaondoa uaminifu katika hadithi yao hii tuliyotaja hapo kabla na pia kwenye hadithi zao nyingine.

1. Kwa upande wa huyu Waki' anapokea Al-Hafiz Al- 'Asqalani kutoka kwa Ahmad bin Hanbal (Imam wa Madhhebu ya Kihambal) amesema: "Hakika Waki' amefanya makosa katika hadithi mia tano".[34] Anasema tena Al-'Asqalani akimnakili Muhammad bin Nasr Al-Marwazi "Waki' alikuwa akisimulia hadithi kwa mujibu wa maa'na yake' isitoshe hakuwa mtaalam wa lugha".[35]

2. Na kwa upande wa "Sufyan At-Thauri" AI-'Asqalani anasema kwa kumnakili ibn Mubarak: "Sufyan alikuwa akisimulia hadithi, basi mimi nikafika kwake na yeye alikuwa anafanyia Tadlis hadithi hiyo (kufanya udanganyifu katika hadithi), basi aliponiona aliona haya (kwa tendo lake hilo).[36]

Kitendo cha kudanganya katika hadithi kwa namna yo yote ile, kinajulisha kwamba yule msimulizi alikuwa hana tabia ya uadilifu na ukweli, kwa hiyo alikuwa akikifanya kitu kisicho cha kweli kionekane kuwa ni kweli, kama ilivyo maana ya tadlis katika lugha ya Kiarabu.

3. Ama huyu "Habib ibn Abi Thabit", Al-Asqalani ameandika akimnakili Abu Habbani: "Kwa hakika Habib: Alikuwa mdanganyifu."[37] Na ameandika Al-Asqalani akimnakili Qat-tan: "Hakika Habib siyo mtu wa kufuatwa."

4. Ama huyu Abu Wa'il, yeye alikuwa mpinzani wa Imam Ali[a.s] na ni miongoni mwa watu waliomfanyia uadui na kero Imam Ali[a.s] .[38] Basi vipi atategemewa mtu kama huyo, wakati Mtume[s.a.w.w] amesema; "Ewe Ali, hatakupenda wewe isipokuwa mtu muumini, na hatakubughudhi isipokuwa mtu mnafiki".[39]

Na inafaa kusema kwamba mpokeaji wa hadithi ya Abul-Hayyaj hana hadithi hata moja katika sihahi zote sita isipokuwa hadithi hii tu tunayoizungumzia. Basi utasema nini kuhusu mtu ambaye hakusimulia ila Riwaya moja? Jambo hili kwa hakika linajulisha kwamba mtu huyu hakuwa mpokeaji wa hadithi, na kwa msingi huu basi kumtegemea katika hadithi yake ni jambo lenye mushkili. Ewe msomaji mpendwa, hii ndiyo Sanad ya hadithi ya AbulHayyaj; na umefahamu udhaifu wa wapokezi wake, na kwamba wanachuoni wa hadithi hawakuafiki ukweli wa wapokezi hao. Basi iwapo hadithi itakuwa imezungukwa na matatizo kama haya mengi haitawezekana kwa faqihi yeyote kuitegemea hadithi hiyo kwa ajili ya kufahamu hukmu ya shari'ah au kutoa fatwa. Ama utambulisho wa hadithi hi, hautaepukana na matatizo licha ya ile Sanad yenyewe, kwani ile nukta muhimu wanayoitolea ushahidi Mawahabi ni hii ifuatayo: "Walaa qabran mush-rifan illa Sawwaitahu".

Hapa ni lazima kutulia na kufanya mazingatio na uchunguzi kwenye maneno mawili:

1) Mushrifan

2) Sawwaitahu.

1. Tamko Al-Mushrif manna yake ni kitu kuwa juu na chenye

kunyanyuka. Amesema katika Munjid: Al-Mushrif minal-amakin: Al-aali Wal-mutilu ala Ghairih. Maana yake: Mahali Mush-rif, ni pale palipo juu na pamejitokeza kuliko mahali pengine. Naye mwenye Al-Qamus ambaye ni mpangaji bora wa utaratibu wa maana za matamko amesema: "As-Sharaf: Al-Uluwu, Waminal-Ibili Sanaamuhu".

Yaani As-Sharafuni kuwa juu; na likitumika kwa ngamia maana yake ni nundu yake". Kwa hiyo basi maana ya "Mushrif' ni kuwa kitu chenye muinuko (kutokeza); na hasa muinuko ulio katika umbile Ia nundu ya ngamia. Basi hapa niwajibu pamoja na kuzirejea dalili na qarina, tufanye uchambuzi kuhusu nini lengo la neno "Al-Mush-rif" lililoko katika hadithi tunaoizimgumzia.

2. Tamko "Sawwaitahu" maana yake ni, kukifanya kitu kuwa sawa (kukisawazisha) na kurekebisha kiwe sawa sawa. Sawwas-Shaia: Maana yake amekifanya kiwe sawasawa; husemwa: Nimesawazisha kitu kilichopinda kikasawazika, (Nimekitengeneza sawasawa). Katika Qur'an tukufu kuna aya isemayo Al-ladhii Khalaqa Fasawwaa (Aliyeumba Akasawazisha). Surah Al-Aalaa,aya ya 2. Baada ya kuangalia maana ya maneno mawili tofuati, tunawajibika kufahamu nini makusudio ya maneno haya katika hadithi. Kwa hakika hadithi hii ina mielekeo miwili, na ni lazima kuchagua mmojawapo kwa mujibu wa maana zitumikazo kwenye maneno haya pamoja na dalili nyingine.

MWELEKEO WA KWANZA

Ni kwamba Imam Ali[a.s] alimuamuru Abul-Hayyaj kuyabomoa makaburi yaliyoinuliwa na kuyasawazisha kabisa na ardhi. Lakini mwelekeo huu ambao ndio wanaoushikilia Mawahabi haukubaliki kutokana na sababu nyingi.

Ya Kwanza: Neno "At-Taswiyya" katika lugha ya Kiarabu halikuja kwa manna ya kubomoa; na lau makusudio yake hapa ingekuwa ni kubomoa basi ilitakiwa hadithi hiyo isemwe hivi: "Wala Qabran Illa Sawwaitahu bil ardhi" Yaani "Wala (usiache) kaburi ila ulisawazishe na ardhi". Lakini hadithi haikuja namna hiyo.

Ya Pill: Lau kama makusudio katika hadithi yangekuwa ni kubomoa, basi ni kwa nini hakutoa fatwa mwanachuoni ye yote wa Kiislamu kuyabomoa? Zaidi ya hapo ni kwamba, kulisawazisha kaburi na ardhi ni kinyume cha sunna ya Kiislamu na mapendekezo ya kisheria; kwani inapendekezwa na sheria kaburi linyanyake kuliko ardhi, na hii ndiyo fatwa waliyoitowa mafaqihi wote wa Kiislamu kwamba kaburi liinuke kutoka katika ardhi kiasi cha shibri moja. Katika kitabu cha Al-Fiqhu Alal-Madhaahibil-arba'ah (Fiqhi kwa mujibu wa madhehebu manne) kuna maelezo yafuatayo: "Ni Sunna kuinua udongo juu ya kaburi kiasi cha shibri moja".[40] Basi itapokuwa muelekeo huu wa kwanza haukubaliki itakuwa ni lazima kuifasiri hadithi hii kwa kutumia muelekeo wa pili ufuatao.

MUELEKO WA PILl

Makusudio ya neno "Tas-wiyatu l-Qabri" itakuwa ni kulisawazisha kaburi likawa sawa kwa sawa kinyume na makaburi ambayo hujengwa kwa umbile Ia samaki au nundu ya ngamia. Kwa msingi huu hadithi itakuwa inakusudia kwamba, sehemu ya juu ya kaburi iwe imetandazwa sawa sawa, na haifai kuwa kama mgongo wa samaki au nundu ya ngamia, kama wafanyavyo baadhi ya Waislamu wa Madhehebu ya Kisunni. Maimamu wa Madhehebu ya Kisunni (isipokuwa Imam Shafi'i) wametoa fatwa kwamba inapendekezwa kulifanya kaburi kama nundu.[41] Na kwa ajili hii basi hadithi hii inathibitisha ukweli wa fatwa ya wanachuoni wa Kishia na Kishafi'i ambao wanasema kwamba, "Inapasa kulisawazisha kaburi na kuliinua kuliko ardhi". Muslim katika sahihi yake ameileta hadithi hii ya Abul-Hayyaj pamoja na hadithi nyingine (ambayo tutaitaja) kwenye Babul-Amri Bitas-wiyatil-Qabri, na vile vile At-Tir-midhi na An-Nasai katika Sunan zao wameileta hadithi hii kwenye hiyo hiyo Babul-Amri Bi Tas-Wiyatil-Qabri.

Na makusudio ya Babul-Amri Bitas-wiyatil-Qabri ni (kujulisha) kwamba kaburi linatakiwa liwe ni lenye kusawazishwa, na lau ingekuwa makusudio ni kulisawazisha na ardhi basi ingekuwa lazima kuuita mlango huu kuwa ni "Babul-Amri bi TakhiriibilQuburi Wahadmiha" yaani mlango wa kuharibu na kubomoa makaburi. Manna tuliyoieleza juu ya neno Tas-wiyah lililo ndani ya hadithi ndiyo unayoweza kuikuta katika lugha ya Kiarabu, kwani neno Tas-wiyah linapotumika kwenye kitu kama kaburi, manna yake huwa ni kwamba, hilo kaburi lisawazishwe na siyo lilinganishwe na kitu kingine kama vile ardhi. Hebu tuangalie hadithi nyingine aliyoitaja Imam Muslim katika Sahihi yake, hadithi ambayo inayo madhumuni yale yale tuliyoyateuwa: "Kunnaa Maa Fadhaalah Ibn Ubaid Biardhir Ruum, Biraudasi, Fatuwufiyya Sahibun lana, Faamara Fadhaalah Ibn Ubaid Biqabrihi Fasuwwiya Thumma Qaala, Samitu Rasulallahi Ya'muru Bitas-wiyatiha". Maana Yake: Tulikuwa pamoja na Fadhaalah ibn Ubaid huko Ruum (katika sehemu iitwayo) Raudas; basi mwenzetu (mmoja) akafishwa; na Fadhaalah ibn Ubaid akaamuru lichimbwe kaburi lake (kisha tulipokwisha mzika) akalisawazisha halafu akasema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akiamuru kuyasawazisha makaburi.[42] .

Kwa kifupi ufunguo wa kuifahamu hadithi liii umejificha katika tamko Ia "Sawwaitahu", na ndani yake mna uwezekano wa kupatikana maana tatu. Pamoja na kuzifahamu dalili na Qarina hapana budi kuchagua maana moja tu. Maana hizo tatu ni hizi zifuatazo: Ya Kwanza: Maana yake iwe ni kuyabomoa majengo yaliyojengwa juu ya kaburi. Na maana hii ni batili kwa sababu makaburi yaliyokuwepo Madina zama hizo hayakuwa na maqubba au madharih. Ya Pili: Iwe maana ya "Tas-wiyah" ni kulisawazisha kaburi na ardhi. Maana hii pia haikubaliki kwa kuwa Sunna iliyothibiti inaamuru kuliinua kaburi kiasi cha shibri moja. Ya Tatu: Maana yake iwe ni kulisawazisha kaburi na kurekebisha (likae sawa) na wala isiwe kuliinua kama ngongo wa samaki au nundu ya ngamia. Na maana hii ndiyo maana inayokusudiwa. Kwa hiyo haina uhusiano na makusudio wanayoyatolea ushahidi Mawahabi. Sasa hivi ndugu msomaji, hebu muangalie Al-Allamah Annawawi ambaye ndiye aliyeandika Sharhi ya Sahihi Muslim na uone ni vipi alivyoisherehesha hadithi hiyo:

Anasema: "Innas-Sunnata Annal-Qabra la Yurfa'u Anil Ardhi Kathiran wala Yusannamu, bal Yurfau Nahwa Shibrin wayusattahu."[43] Maana Yake: Iliyo sunna ni kwamba, kaburi lisiinuliwe (muinuko) mkubwa kutoka ardhini bali liinuliwe kiasi cha shibri lizawazishwe. Katika ibara hii inadhihiri kwamba mshereheshaji wa Sahih Muslim amefahamu maana ile ile tuliyofahamu katika hadithi hii, kwamba Imam Ali[a.s] alimuusia Abul-Hayyaj kuyabadilisha makaburi yenye kunyanyaliwa mno au yale yenye maumbile kama mgongo wa samaki yasawazishwe na wala hakuamuru kuyasawazisha na ardhi. Na sisi katika kutoa maana hii ndani ya hadithi hii hatuko peke yetu bali amesema pia Al-Hafiz Al-Asqalani katika kitabu chake Irshaad as-sraari fi sharhi Sahihil-Bukhari. Baada ya yeye kutaja kwamba iliyo sunna katika kaburi ni kulisawazisha; na kwamba haifai kuiacha sunna hii eti tu kwa sababu kufanya hivyo imekuwa ni alama ya marafidhi (anakusudia Mashia) kwani hakuna upinzani baina ya kusawazisha kaburi na hadithi ya Abul-Hayaj. Al-Hafiz Al-Asqalani anasema kama ifuatavyo:

"....Ni kwamba (katika hadithi hiyo) hapakukusudiwa kusawazishakaburi na ardhi bali alichokusudia ni kulisawazisha (yaani kuliweka sawa) na kwa hiyo tunakusanya maana za haadithi zote." Baada ya yote haya lau ingekuwa maana ya wasia wa Imam Ali[a.s] kwa Abul-Hayyaaj ni kubomoa maquba na majengo yaliyojengwa kwenye makaburi, basi ni kwa nini Imam[a.s] hakuamuru kuyabomoa maquba ambayo yalikuwa kwenye makaburi ya Manabii katika zama zake? Pamoja na kwamba inaeleweka kuwa yeye Imam Ali[a.s] alikuwa ndiyo mtawala wa nchi zote za Kiislamu na alikuwa akiyafahamu maquba yaliyojengwa kwenye makaburi ya Manabii huko Palestina, Syria, Iraq, Misri, Iran na Yemen, (lakini hakuyabomoa). Na tukiyafumbia macho maelezo yaliyotangulia hivi punde, na tukakadiria kwamba Imam Ali[a.s] alimuamuru Abul-Hayyaj kuyabomoa makaburi yaliyoinuliwa na ayasawazishe kabisa na ardhi, basi ndani ya hadithi hiyo hakuna kinachojulisha wajibu wa kubomoa majengo yaliyojengwa kwenye makaburi, kwa kuwa Imam Ali[a.s] alisema (iwapo tutakadiria kuwa hadithi hiyo imesihi):

"Wala Qabran illa Sawwaitahu" (wala kaburi ila ulisawazishe); na wala hakusema "wala Binaan Wala Qubbatan Illa Sawwaitahuma" (yaani wala jengo wala quba isipokuwa uyabomoe). Kwa kuwa uchunguzi wetu katika maudhui haya hauhusu kaburi lenyewe, bali majengo yaliyojengwa juu ya kaburi, kwa kuwa majengo haya yaliyoko kwenye makaburi waumini huwa wanapata kivuli kwa ajili ya kusoma Qur'an, dua na kusali, basije, katika sentensi hii (wala Qabran 1lla Sawwaitahu) kuna chochote kinachojulisha kuyabomoa majengo haya na kumbukumbu ambazo zinawasaidia wenye kuzuru makaburi hayo kufanya ibada na kuwakinga kutokana na joto au baridi?

UWEZEKANO WA MAANA MBILI MWISHONI

Mwisho wa uchunguzi kuna maana mbili nyingine hatuwezi kuepuka kuzitaja ili kukamilisha maudhui hayo. Ya Kwanza: Ni kwamba hadithi hii (ya Abul-Hayyaj na nyinginezo zinazofanana) ni ishara ya yale yaliyokuwa yamezoweleka kwa baadhi ya nyumati zilizopita ikiwa ni pamoja na kuyafanya makaburi ya wachamungu kuwa ndiyo kibla chao wakayaelekea wakati wa ibada. Watu hao pia walikuwa wakiweka picha kwenye kaburi, kwa hiyo waliacha kuelekea kibla aliyowaamuru Mwenyezi Mungu wakati wa ibada na wakayaelekea makaburi hayo. Na kwa maana hii basi, haiwezekani kwa hadithi hii kuwa na uhusiano wowote na makaburi ya Waislamu, na wala haijapata kuonekana kwa Muislamu yeyote kuyaelekea makaburi katika swala au kuyasujudia; isipokuwa mwenendo wa Waislamu ni kuswali jirani ya makaburi bila ya kuwa yenyewe ndiyo kibla chao, bali nyuso zao zinaelekea upande iliko Al-Kaaba, nao husimamisha swala na kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu huku wakiwa karibu ya makaburi. Na kama Waislamu wanakwenda kuzuru makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu, na wakatumia huko muda mrefu kufanya ibada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu karibu na malazi hayo matukufu, basi si kwa jingine ila ni kwa sababu ya utukufu uliyopatikana kwenye ardhi hizo kwa kuwepo watu watukufu waliozikwa mahali hapo.

Jambo hili ufafanuzi wake utakuja baadaye. Maana ya Pili: Ni kwamba, makusudio ya kauli ya Imam Ali[a.s] kwa Abul-Hayyaj aliposema: "Anlaa Tada'a Timthaalan Illa Tamastahu, Wala Qabran Mushrifan Illa Sawwaitahu", makusudio yake kusema "At-Timthal" ni mapicha na masanamu, na "Al-Qabr" ni makaburi ya washirikina ambayo yalikuwa yakienziwa na kuheshimiwa na wahusika. Kwa kifupi ni kwamba hadithi ya Abul-Hayyaj haina uhusiano wowote kabisa na kujenga juu ya makaburi, isipokuwa inahusu makaburi yaliyoinuliwa mno (kama ilivyoelezwa hapo kabla) au makaburi ya washirikina na masanamu. Maelezo yafuatayo tunataja fatwa ya Maimamu wa Madhehebu manne ya Kisunni kuhusu kujenga juu ya makaburi."

"Yukrahu An-yubnal-qabru Bibaytin au Qubatin au Madrasatin au Masjidin."[44] Maana Yake: Ni karaha kulijengea kaburi katika nyumba au Qubbah au chuo au msikiti. Basi maadamu Maimamu wa Madh-hebu nne za Kisunni wameafikiana kuwa ni karaha tu kuyajengea makaburi basi ni vipi Qadhi wa Najdi anathubutu kutoa fatwa ya uharamu wa kuyajengea? "Kwa hakika huu ni uzushi. Tena tunajua kwamba fatwa ya ukaraha wa kujenga juu ya makaburi haitegemei dalili sahihi yo yote, na hasa itapokuwa jengo hilo linamsaidia mwenye kuzuru hapo aweze kusimamisha mambo ya faradhi ya dini na kusoma Qur'an kwenye jengo hilo.

D. HADITHI YA JABIR

Hadithi ya Jabir inafahamika kuwa ni miongoni mwa hadithi wanazozitegemea Mawahabi kuharamisha kujenga juu ya makaburi; na imepokewa hadithi hii katika Sihah na Sunan kwa matamko tofauti tofauti, na wanapatikana katika Sanadi zake zote na mapokezi yake wanapatikana watu wawili.

1. Ibnu Juraih

2. Abuz-Zubair.

Na ili kuthibitisha kusihi kwa hadithi hii itategemea kuzifahamu hali za wapokezi wake na watu wa Sanad yake. Katika maelezo yafuatayo tutaitaja hadithi hiyo kwa matamko mbali mbali tena tofauti: Imekuja katika Sahihi Muslim (Babun-Nahyi 'An Tajsisil-Qabri Wal-Bina'i Alaih) Hadithi ya Jabir iliyopokelewa kwa njia tatu na katika aina mbili:

1. Ametusimulia Abubakar ibn Abi Shaiba, ametusimulia Hafsu ibn Ghiyath, kutoka kwa Ibn Juraih, naye toka kwa Abuz-Zubair kutoka kwa Jabir, amesema: "Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kulipaka kaburi jasi (aina ya chokaa) na kulikalia na kujengea juu yake."

2. Amenisimulia Harun ibn Abdillah, ametusimulia Hajaaj ibn Muhammad, na amemsimulia Muhammad ibn Raafi', ametusimilia 'Abdur-Razzaq, wote hawa wamepokea toka kwa Ibn Juraih, amesema: Alinieleza Abuz-Zubair kwamba yeye alimsikia Jabir ibn Abdillah anasema, "Nilimsikia Mtume..... (kama ilivyo hadithi ya hapo awali).

3. Ametusimulia Yahya ibn Yahya, ametusimulia Isma'il ibn Ulayyah kutoka kwa Ayyub, naye toka kwa Abuz-Zubair toka kwa Jabir; amesema: Amekataza kuyapaka makaburi jasi.[45] Na imekuja katika Sahihi Tirmidhi hadithi moja na kwa njia moja (kwenye Babu Karahiyyati Taj-sisil-Quburi Wal-Kitabati Alaiha) kama ifuatavyo:

4. Ametusimulia 'Abdur-Rahman ibn Al-Aswad, ametueleza Muhammad ibn Rabi'ah, kiltoka kwa Ibn Juraih naye toka kwa Abuz-Zubair kutoka kwa Jabir; amesema: Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amekataza kuyapaka jasi makaburi na kuyaandika juu yake na kuyajenga juu yake na kutembea juu yake.

Kisha baada ya kuandika hadithi hii At-Tirmidhi anaeleza kwamba imepokewa kwa al-Hasan Al-Basri na Shafi'i, kuwa wao wametoa fatwa kuruhusu kuyapaka makaburi jasi.[46] Na katika Sahih Ibn Majah, imekuja (katika Babu Ma Ja'a fin-nahyi Anil-Bina'i Alal-Quburi Wataj-sisiha Wal-Kitabati 'alaiha) hadithi hii kwa njia mbili na aina mbili, nazo ni hizi zifuatazo:

5. Ametusimulia Azhar ibn Marwan na Muhammad ibn Ziyad, wamesema: Ametusimulia 'Abdul Warith kutoka kwa Ayyub naye toka kwa Abuz-Zubair naye toka kwa Jabir; amesema: "Amekataza Mtume wa Mwenyezi Mungn kuyapaka makaburi jasi."

6. Ametusimulia Abdallah ibn Said ametusimulia Hafsi kutoka kwa Ibn Juraih naye toka kwa Suleiman ibn Musa kutoka kwa Jabir, amesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu amekataza kuandikwa chochote juu ya kaburi".[47]

Na baada ya kuitaja hadithi hii As-Sindi aliyeisherehesha anaandika akimnukuu Al-Hakim An-Nishapuri kwamba hadithi hii ni sahihi lakini haifuatwi, kwani viongozi wa Uislamu mashariki ya dunia na magharibi yake sera yao imekuwa ni ya kuandika juu ya makaburi kizazi baada ya kizazi.

Na imekuja hadithi hii katika Sahih An-nasa'i (katika Babul-Bina'I Alal-Qabri) kwa njia mbili na kwa namna mbili zifuatazo:

7. Ametueleza Yusuf ibn Sa'id amesema: Ametusimulia Hajjaj kutoka kwa Ibn Juraih amesema, amenieleza Abuz-Zubair kwamba yeye alimsikia Jabir anasema: "Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amekataza kuyapaka makaburi jasi au kujenga juu yake au yeyote yule kuyakalia."

8. Ametueleza Imran ibn Musa amesema, ametusimulia 'AbdulWarith amesema, ametusimulia Ayyub kutoka kwa Abuz-Zubair nayr kutoka kwa Jabir amesema: "Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amekataza kuyapaka jasi makaburi.[48] Na hadithi ya Jabir imekuja katika Sunan Abi Dawuud (Juzuu ya tatu ukurasa 216), "Babul-Bina'I Alal-Qabr) kwa njia mbili na namna mbili zifuatazo:

9. Ametusimulia Ahmad ibn Hanbal, ametusimulia 'Abdur-Razzaq, ametusimulia Ibn Juraih, amenieleza Abuz-Zubair kwamba yeye amemsikia Jabir anasema, nimemsikia Mtume amekataza kukalia kaburi, na kupakwa jasi na kujenga juu yake."

10. Ametusimulia Musaddad na Uthman bin Abi Shaibah amesema: Ametusimulia Hafsu ibn Ghiyath kutoka kwa lbn Juraih naye toka kwa Sulaiman ibn Musa na kutoka kwa Abuz-Zubair kutoka kwa Jabir amenisimulia hadithi hii (iliyotajwa kabla). Amesema Abu Daud: Amesema Uthman "au kuliongeza", na akaongeza Suleiman ibn Musa "au kuandikwa juu yake". Ama Ahmad ibn Hanbal (Imam wa madhehebu ya Kihanbal) yeye ameipokea hadithi hii katika Musnad yake kwa namna ifuatayo:

11. Imepokewa toka kwa 'Abdur-Razzaq naye kapokea kwa Ibn Juraih: Amenieleza Abuz-Zubair kwamba yeye amemsikia Jabir ibn Abdilahi anasema: Nimemsikia Mtume akikataza mtu kukalia kaburi na kulipaka jasi na kulijenga juu yake.[49] Haya ndiyo mapokezi yaliyopokelewa toka kwa Jabir kuhusu maudhui haya, na tumeitaja hadithi hii kwa mapokezi tofauti tofauti na Sanad zake mbali mbali. Sasa hivi umefika wakati wa kuitafiti na kuichunguza ndani yake ili tuone je, hadithi hii inafaa kutolea ushahidi au hapana?

DALILI ZA UDHAIFU NDANI YA HADITHI HII

Hadithi hii ya Jabir ma mkusanyiko mkubwa wa nukta mbali mbali za udhaifu, kiasi kwamba nukta hizo zinaiangusha isiwezekane kuitolea hoja na kuizingatia, na haiwezekani kabisa kuitolea ushahidi kwa namna yoyote ile. Maelezo yafuatayo tutataja nukta za udhaifu uliyomo katika hadithi hii: Kwanza: Katika sanad zote za Hadithi hii yamo majina ya Ibn Juraih (Abdul-Malik ibn Abdul-Aziz ibn Juraih AI-Amawi) na Abuz-Zubair (Muhammad ibn Muslim Al-Asadi) kwa pamoja au likawepo Ia mmoja wao. Tutakapofahamu mazingira ya hawa wapokezi wawili na hali zao, basi hakutakuwa na sababu ya kutaka kuwafahamu wapokezi wengine waliomo katika hadithi hii, ambao baadhi yao hawatambuliki na wengine wanaosababisha hadithi hii iwe dhaifu. Katika kitabu kiitwacho Tahdhibut-Tahdhib cha Ibn Hajar Al-'Asqalani utasoma maoni ya wanachuoni wa Rijal (wanaotambua wapokezi wa hadithi) juu ya ibn Juraih kama ifuatavyo:

Yahya ibn Said aliulizwa kuhusu hadithi za Ibn Juraih, akasema: "Ni dhaifu;" akaambiwa: "Hata kama akisema kuwa amenieleza fulani?" Akasema, "Usihadaike; si lolote; zote ni dhaifu".[50] Naye Ahmad ibn Hanbal amesema: "Iwapo Ibn Juraih atasema kuwa fulani amesema na fulani amesema, nami nimeambiwa, basi haya yote ni uzushi". Maana yake ni kuwa hadithi zake hazitambuliwi au ni za uzushi. [51] [51] Naye Malik ibn Anas amesema: kuwa Ibn Juraih alikuwa akisenya kuni usiku (akikusanya kila kitu bila kuchagua kilicho sahihi na kisicho sahihi kama msenya kuni asenyeaye usiku hawezi kuona ni zipi kuni na wepi nyoka). Ama Ad-Daruqutni yeye amesema: Jiepushe na tadlisi ya Ibn Juraih, kwani tadlisi yake hi mbaya sana, yeye alikuwa hafanyi tadlisi isipokuwa kwa yale aliyoyasikia toka kwa mtu Majruh. (Mpokezi ambaye ubaya wake umebainishwa).

Ibnu Hibbaan amesema: "Ibn Juraih alikuwa akidanganya katika hadithi"[52] Ewe msomaji, nakuapia Mwenyezi Mungu, hivi kweli inafaa kuchukuwa mapokezi ya mtu huyu pamoja na kuwa wanachuoni wa hadithi wamemshutumu na kuonyesha unyonge wake? Na je, inafaa kuacha sera ya Waislamu ya kujenga juu ya makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu na kuyaheshimu kwa kutegemea hadithi za mpokeaji huyu mdanganyifu? Na je, inafaa tuwashutumu Waislamu kwa ushirikina na ukafiri na upinzani kwa kuwa wanaupenda mwenendo wa Kiislamu na wanafuata sera ya watu wema waliopita ya kujenga juu ya makaburi na kuyazuru na kuyaheshimu? Maelezo haya yaliyopita ndiyo baadhi ya yalioandikwa kuhusu Ibn Juraih.

Ama Abuz-Zubair, msikilize lbn Hajar huyu hapa anataja kauli za wanachuoni wa Rijal wasemavyo: "Imepokewa kutoka kwa Abdullah ibn Ahmad ibn Hanbal, naye amepokea toka kwa babaye (Imam wa Kihanbal) naye toka kwa Ayyub kwamba yeye alikuwa akimfahamu Abuz-Zubair kuwa hi mpokezi dhaifu. Na imepokewa toka kwa Shu'bah kwamba, Abuz-Zubair alikuwa hawezi hata kuswali vizuri. Na imepokewa tena toka kwa Shu'bah amesema: Hapakuwepo katika dunia mtu nimpendaye mno kuliko yule ajaye kisha nikamuuliza habari za Abuz-Zubair; basi nilifika Makka nikawa napokea toka kwake, ghafla nikiwa nimekaa kwake alikuja mtu na akamuuliza swali fulani, basi alimjibu lakini alizusha uongo; basi mimi nikasema: "Ewe Abuz-Zubair, unamwambia uzushi mtu Mwislamu?" Akajibu:- "Hakika yeye amenikasirisha".

Nikasema: "Basi yeyote anayekukasirisha unamzushia? Basi kamwe sitapokea hadithi yoyote toka kwako". Na imepokewa toka kwa Warqaa amesema: "Nilimwambia Shu'bah, vipi mbona umeziacha hadithi za Abuz-Zubair"? Akasema: "Nilimuona akipima, na anapunguza kipimo". Ibn Abi Hatima amesema: "Nilimwuliza baba yangu kuhusu Abuz-Zubair; akasema: "Hadithi zake zinaandikwa lakini hazitolewi ushahidi." Anasema tena: Na nilimwuliza Abu-zar'ah kuhusu Abuz-Zubair. Akasema: "Watu wanapokea toka kwake". Nikasema: "Hadithi zake hutolewa ushahidi?"

Akasema: Hutolewa ushahidi hadithi za watu waaminifu. (Akiwa na maana kuwa Abuz-Zubair siyo mwaminifu.)[53] Naam! Ewe ndugu yangu hii ndiyo hali ya Ibn Juraih na Abuz-Zubair; nao ndiyo miongoni mwa wapokezi wa hadithi ya Jabir katika Sanad zake zote. Basi, je inawezekana kutolea ushahdi hadithi ambayo ndani yake wamo wapokezi wawili hawa? Na hapo kabla ilitangulia ishara kwamba ndani ya Sanad za hadithi hii wamo wapokezi wanyonge zaidi ya Ibn Juraih na Abuz-Zubair, kama vile Abdur-Rahman ibn Aswad anayetuhumiwa kuwa ni mwongo tena mzushi. Basi je, inafaa kubomoa athari za watu wa nyumba ya Mtume[a.s] na athari za Masahaba na kuwanasibisha Waislamu kuwa wamepotea kwa muda wa karne zote kumi na nne kwa kutegemea hadithi hii dhaifu isiyokubalika? Nukta ya Pili: Hakika hadithi ya Jabir inamvurugano sana katika matamko na matni yake, na mvurugano huu unajulisha kuwa wapokezi wa hadithi hii walikuwa hawana uwezo wa kudhibiti na kufuatilia riwaya (mapokezi), pamoja kuwa na uwezo wa kudhibiti ni moja ya masharti anayotakiwa kuwa nayo Rawii (mpokeaji).

Kwa mvurugano uliyomo kwenye hadithi hii, uaminifu unakosekana, na pia imani na mategemeo ya hadithi hii vinaondoka. Hebu endelea kuona ufafanuzi zaidi katika kuitafiti hadithi hii: Hadithi hii ya Jabir imepokewa katika namna saba, pamoja na kuwa Mtume[s.a.w.w] aliitamka kwa tamko la aina moja tu. Angalia namna hizo saba zilivyo:

1. Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kulipaka kaburi jasi na kuliegemea. Hadithi Na. 1, 2 na 9.

2. Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kulipaka kaburi jasi. Hadithi Na. 5 na 8.

3. Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kulipaka kaburi jasi na kuliandika na kujenga juu yake na kutembea juu yake. Hadithi Na. 4.

4. Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kuandika juu ya kaburi. Hadithi Na. 6.

5. Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kukaa juu ya kaburi na kulipaka jasi na kulijenga na kuliandika juu yake. Hadithi Na. 10.

6. Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kukaa juu ya kaburi na kulipaka jasi na kujenga juu yake. Hadithi Na. 11.

Hapa iko tofauti baina ya hadithi hii na ile ya kwanza, kwani ile ya kwanza imekataza kuliegemea kaburi na hii inakataza kukaa juu ya kaburi.

7. Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kukaa juu ya kaburi na kulipaka jasi na kujengea juu yake na kuliongeza na kuliandika.

Tunaona katika sura hii kumeongezwa kwenye kukaa, kupaka jasi na kujenga kuna ziada ya kuliongeza kaburi na kuandika juu yake. Baada ya yote haya utaona kuna hitilafu katika matni za hadithi na sentensi zake, kwani katika namna ya kwanza anasema (Al-'itimadu) kuegemea, na ya tatu (Al-wat'u) kutembea, na ya tano na ya sita: (Al-qu'udu) kukaa. Hivyo basi hakuna uwezekano wa kuikubali hadithi hii na kuitegemea kwa mwanachuoni yeyote kutokana na mvurugano uliyomo.

Nukta ya Tatu: Hadithi hii iwapo itakadiriwa kuwa ni sahihi na kupuuza mvuragano uliyomo, haijulishi zaidi ya kuwa Mtume[s.a.w.w] alikataza kujenga juu ya makaburi, lakini haijulishi kuwa jambo hilo ni haramu kwani kukataza (Nah-yi) kumegawanyika vigao viwili: Kuna Nahyi Tahriim na Nahyi Karaha. Yaani kukataza kwa kuharamisha na kukataza kwa karaha. Na hiki kigawo cha pili kimekuja mara nyingi mno katika hadithi za Mtume[s.a.w.w] na Maimamu watukufu [a.s] . Ni kweli kwamba nahyi kwa asili yake inajulisha kuharamisha na tahriim ndiyo inayothibiti kwanza mpaka ije dalili ya kugeuza uharamu na kuwa karaha, lakini wanachuoni hawakufahamu katika hadithi hiyo isipokuwa karaha tu. Kwa mfano utamwona At-Tirmidhi ameitaja hadithi hiyo katika Sahihi yake chini ya anuani isemayo, "Karahiyyatu Taj-sisilqubur " (Ukaraha wa kupiga lipu makaburi.).

Na ushahidi uliyo wazi zaidi ni kuwa As-Sindi aliyesherehesha Sahih Ibn Majah amemnakili Al-Hakim An-Nishapuri amesema kwamba, "Hajalitumia katazo hili Mwislamu yeyote;" kwa hiyo hakulizingatia kuwa ni Nahyi Tahriim kwa dalili kuwa, sera ya Waislamu iko kwenye kuandika juu ya makaburi. Kingine ambacho ni ushahidi vile vile kuwa Nahyi hiyo ni Nahyi karaha ni maafikiano ya madhehebu za Kiislamu kuwa inafaa kujenga juu ya kaburi isipokuwa ardhi iliyowekwa wakfu kisheria. Anasema mashereheshaji wa Sahih Muslim alipokuwa akifafanua hadithi hii: "Ama suala la kujenga juu ya kaburi, iwapo (ardhi) ni mali ya mjengaji basi ni karaha (kujenga) na kama ni (ardhi) ya wakfii basi ni haramu (kujenga).[54]

Katika mambo yasiyohitaji maelezo marefu ni kuwa kitu kinapokuwa karaha basi ukaraha wake huondoka kwa kuyazingatia baadhi ya mambo fulani muhimu. Kwa mfano: Ikiwa kujenga juu ya kaburi itakuwa ni sababu ya kuhifadhi asili ya Uislamu na kudhihirisha mapenzi kwa mwenye kaburi hilo ambaye Mwenyezi Mungu amefaradhisha kumpenda au kujenga huko kutakuwa ni sababu ya kuhifadhi athari za Uislamu au itafanya wakusanyike wenye kuzuru mahali hapo chini ya jengo hilo ili wasome Qur'an na kuswali na kusoma dua, basi moja kwa moja karaha hiyo itaondoka. Si hivyo tu bali jambo hilo litakuwa ni mustahab, lenye kupendekezwa kufanywa, na litakuwa katika mlango wa kuhuyisha desturi na urithi wa dini na ni kuimarisha mambo matukufu ya Kiislamu.