UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI0%

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Vitabu mbali mbali

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi: SHEIKH JA'AFAR SUBHANY
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 48390
Pakua: 4204

Maelezo zaidi:

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 24 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 48390 / Pakua: 4204
Kiwango Kiwango Kiwango
UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi:
Swahili

7

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

MATOKEO MAZURI YANAYOPATIKANA KUTOKANA NA KUWAZURU WATU MUHIMU WA KIDINI

Makaburi yanayopata hadhi ya kutunzwa na kuheshimiwa na watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu katika ulimwengu - hasa Waislamu ni yale ambayo mara nyingi yanakuwa ni makaburi ya watu ambao wamebeba ujumbe wa amani na kuufikisha kama ilivyotakiwa ufike. Watu hawa wamegawanyika sehemu tatu:

1. Manabii: Ambao ndiyo viongozi wa dini, walibeba mabegani mwao ujumbe kutoka mbinguni, walizitoa nafsi zao na mali zao pamoja na wanavyovipenda kwa ajili ya kufikisha ujumbe huo, na wakavumilia aina mbali mbali za taabu na matatizo ili wapate kuwaongoa watu.

2. Wanachuoni na wanafikra: Ambao ni kama mshumaa unaowangazia wengine wakati wenyewe unateketea.

Watu hawa waliishi maisha ya kichamungu na kujinyima na wakaupatia ulimwengu maelezo yenye thamani na uchambuzi mzuri, katika nyanja za elimu, fikra, tabia na elimu za maumbile na ufunuo kutoka mbinguni na elimu za ulimwengu, viumbe na mengineyo.

3. Mujahidina (wapiganaji Jihadi): Hawa ni wale wenye kupigania mabadiliko ambao walihuzunishwa na hali ya maisha ya jamii kutokana na dhulma na ubaguzi wa rangi na kabila na hawakuivumilia hali hiyo, wakapigana dhidi ya dhulma na ukandamizaji na wakadai heshima na haki za binadamu zilindwe, na wakajenga ngome ya uadilifu kwa kutoa damu zao zenye thamani kubwa. Mapinduzi yoyote au mabadiliko ya jamii hayalinganishwi na kitu chochote isipokuwa kwa kutoa kitu cha thamani ili mafaniko yapatikane. Na thamani ya mapinduzi inayoweza kubomoa tawala za madhalimu na kuwasonga koo, ni kutoa damu tukufu ambayo wapiganaji mashujaa hujitolea muhanga kwa damu hiyo ili kurejesha haki na uhuru kwenye nchi za Kiislamu.

Kwa hiyo watu huwa wanazuru makaburi ya watu wa aina hizi, na hutokwa machozi wawapo makaburini na huwa wanakumbuka ushujaa wao na kujitoa kwao muhanga, pia huziliwaza roho za mashujaa hao kwa kusoma Qur'an kisha kuwazawadia thawabu za visomo hivyo. Kadhalika huimba Qasida ambazo hutaja sifa zao na utukufu wao na kiwango cha daraja zao tukufu. Hakika kuzuru makaburi ya watu hawa muhimu ni moja katika aina ya kuwashukuru na kuwatukuza kwa kujitolea kwao na pia kujulisha kizazi kilichopo kuwa, hayo ndiyo malipo ya wale ambao hupita njia ya haki na uongofu na ubora, na ndiyo malipo ya wale wanaopigana na kulinda misingi ya itikadi (Uislamu).

Malipo yao ni kudumu kwa utajo wao, utajo ambao ni mwema na sifa nzuri hata kama ni muda mrefu umepita toka kufariki kwao. Mpaka hapa tumefahamu umuhimu wa kuhuyisha utajo wa watu hawa muhimu wa dini, na kwa msingi huu inapasa kufanya juhudi ili kuendelea kuzifanya kumbukumbu zao kuwa hai na kuzihifadhi na kusimamisha sherehe kubwa za kukumbuka siku za kuzaliwa kwao na kuvaa mavazi ya kuonyesha msiba na kufanya hafla za kuomboleza na kukumbuka kufa kwao, pia kufanya vikao na mikusanyiko mikubwa na kutoa hotuba za kuwatambulisha watu hao watukufu na itikadi zao zilizopelekea wao wajitoe muhanga. Kadhalika kuyaheshimu malazi yao (makaburi) na kujiepusha na kila linalotia dosari heshima yao, kwani kuyaheshimu makaburi yao ndiko kuheshimu ujumbe wao na itikadi zao.

Kinyume cha hivyo ni kuyadharau na kuyapuuza makaburi yao, na itakuwa ndiyo kuudharau ujumbe wao na ni kuwadharau wao wenyewe. Katika siku zetu hizi, mtu anapoingia katika makaburi ya Baqii ili akazuru makaburi ya watu wa kizazi cha Mtume[s.a.w.w] na makaburi ya viongozi wa Kiislamu na watetezi wa dini na Masahaba, atayaona makaburi hayo yako katika hali inayohuzunisha kutokana na dharau yaliyofanyiwa, jambo ambalo linatetemesha nafsi na kuifanya ishangazwe na uovu wa kikundi cha Mawahabi ambao wanadai kuwa wao ndiyo watetezi wa Uislamu. Ajabu ni kwamba, kwa upande mmoja Mawahabi huwataja masahaba kwa wema na kuwasifu katika majukwaa ya hotuba zao, lakini kwa upande wa pili wanayaacha makaburi ya Masahaba bila ya heshima yoyote, na katika hali ya kusikitisha katika kuyadharau na kuyapuuza makaburi hayo, Mawahabi hawayajali kabisa hata kama wanyama wataingia na kuharibu sehemu ya makaburi ya Masahaba. Zawadi ya pekee ambayo Mawahabi huwapatia mahujaji na wanaozuru (makaburi ya Baqii) ni kuwaita kuwa ni washirikina na tendo lao la kuyazuru makaburi hayo ni tendo la shirki.

Mawahabi wanawaambia Waislamu maneno (haya machafu) kwa sababu tu Waislamu hao wanawaheshimu viongozi wa dini, na wanawatukuza Mawalii wa Mwenyezi Mungu. Hali hii inaonyesha kwamba, Mawahabi wanaficha mioyoni mwao chuki na kero waliyonayo dhidi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu na viongozi wa dini yake. Na sasa umefika wakati wa kuzungumzia ziyara ya kaburi la Mtume[s.a.w.w] kwa mujibu wa mtazamo wa dalili za Kiislamu.

KUZURU KABURI LA MTUKUFU MTUME

Katika maelezo yafuatayo tutatoa baadhi ya aya za Qur'an na hadithi tukufu za Mtume[s.a.w.w] ambazo zinahimiza kulizuru kaburi lake. Na tunataraji kuwa msomaji atapata maelekezo zaidi na kufahamu.

USHAHIDI WA QUR'AN

Qur'an tukufu inawaamrisha wenye madhambi wafike mbele ya mjumbe wa Mwenyezi Mungu na wamuombe awaombee msamaha kwa Mwenyezi Mungu, kwani dua au maombi ya Mtume yatakubaliwa kwa ajili yao. Mwenyezi Mungu anasema:

وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذ ظَّلَمُوا أَنفُسَهُمْ جَاءُوكَ فَاسْتَغْفَرُوا اللَّـهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُوا اللَّـهَ تَوَّابًا رَّحِيمًا ﴿٦٤﴾

"Na lau wangelikuja kwako walipojidhulumu nafsi zao wakaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu, na Mtume pia akawaombea msamaha, bila shaka wangelinikuta Mwenyezi Mungu ni mwenye kupokea toba tena mwenye kurehemu. (Qur'an, 4:64).

Lau aya hii ingekuwa ndiyo pekee katika mada hii, basi tungelisema kuwa inahusika tu katika zama za uhai wa Mtume[s.a.w.w] na ni kwa kipindi kile tu cha yeye kuwepo miongoni mwa watu. Lakini sisi tunachukua hukmu ya jumla inayoenea, ambayo haimuwekei Mtume mpaka wa mwisho kwa maisha yake ya dunia. Hukmu hiyo iko katika maelezo yafuatayo:

Kwanza : Qur'an inabainisha kuwa, Manabii, Mawalii na baadhi ya watu wengine wako hai katika Bar-zakh (uhai baada ya kufa) na inawazingatia kuwa wanaona na wanasikia katika huo ulimwengu wa Barzakh.

Tutazionyesha hizo aya zinazobainisha jambo hili katika sehemu ya kuzungumzia kutawasal kwa roho tukufu.

Pili : Hadithi tukufu zinabainisha kwamba, Malaika humfikishia Mtume[s.a.w.w] salamu za yeyote anayemsalimia. Imekuja hadithi katika Sihah: "Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Hapana yeyote atakayenisalimia, isipokuwa Mwenyezi Mungu hunirudishia roho yangu mpaka nami nimrudishie salamu ". [89] Na amesema Mtume[s.a.w.w] : "Niswaliyeni, kwani swala zenu zinanifikia (kutoka) popote mlipo ." [90]

Tatu : Waislamu wamefahamu tangu siku hizo kwamba maana ya aya tuliyotangulia kuitaja inaendelea kutumika na wala haikomi kwa kufariki Mtume[s.a.w.w] , kiasi kwamba kuna baadhi ya mabedui (kwa mujibu wa fikra zao nzuri) walikuwa wakilikusudia kaburi Ia Mtume na wanalizuru na wanaisoma aya hii kaburini kwa Mtume na kumuomba awatakie msamaha.

Ametaja Taqiyyud-din As-Subaki katika kitabu kiitwacho "Shifaus-siqami" na pia As-Samhudi katika kitabu kiitwacho "Wafa-ul Wafa" mifano mbali mbali ya Waislamu kuzuru kaburi la Mtume[s.a.w.w] na kusoma kwao aya hii mbele ya kaburi lake tukufu. Tunataja baadhi ya mifano kama ifuatavyo: Amepokea Sufyan bin Anbar kutoka kwa Al-Utbi, na wawili hawa ni Masheikh wa Imamu Shafii na ni wallimu wake, kwamba yeye amesema, "Nilikuwa nimekaa kwenye kaburi la mjumbe wa Mwenyezi Mungu[s.a.w.w] , mara akaja bedui mmoja akasema: "As-Salaamu Alaika ya Rasulallah, nimemsikia Mwenyezi Mungu akisema: "Na lau wangelikuja kwako walipojidhulumu nafsi zao wakaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu na Mtume pia akawaombea msamaha, bila shaka wangelimkuta Mwenyezi Mungu ni mwenye kupokea toba tena mwenye kurehemu". Nami nimekujia mwenye kutaka msamaha kutokana na dhambi zangu mwenye kutaka Shafaa kwako (uniombee) kwa Mola wangu". Kisha bedui yule akalia, na akawa anasema:

"Ewe mbora wa waliozikwa ardhini, kwa uzuri wako ardhi na mimea (iliyopo hapa) vimependeza, nafsi yangu iwe fidia ya kaburi ulilomo, ndani yake kuna utakatifa na kuna kila ukarimu na ubora". Kisha bedui yule akaomba msamaha na akaenda zake.[91] Naye Abu Said As-Sam-ani anapokea kutoka kwa Imam Ali bin Abi Talib[a.s] kwamba, bedui mmoja alikuja Madina baada ya siku tatu tangu Mtume[s.a.w.w] azikwe, akajitupa kwenye kaburi tukufu la Mtume akajipaka udongo wa kaburi kichwani mwake na akasema: "Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ulisema nasi tukaisikia kauli yako, umepokea kwa Mwenyezi Mungu mambo ambayo tumeyapokea kwako na katika aliyokuteremshia Mwenyezi Mungu ni "Na lau wangelikuja kwako walipojidhulumu nafsi zao.... nami nimedhulumu nafsi yangu na nimekuja ili unitakie msamaha kwa Mola wangu"[92] Yote haya yanajulisha cheo kikubwa alichokitoa Mwenyezi Mungu kwa Mtume[s.a.w.w] kama ilivyobainisha aya hii kwamba cheo hicho siyo makhsusi katika uhai wake tu, bali inatia mkazo kuwa kinathibiti hata baada ya kufa vile vile.

Kwa ujumla Waislamu wanazizingatia aya zote zilizoshuka kwa ajili ya kumtukuza Mtume[s.a.w.w] kwamba, zinakusanya kipindi cha uhai wake na baada ya kufa, na hapana yeyote anayezihusisha katika wakati wa uhai wake tu. Na katika historia imekuja kwamba: Alipouawa Imam Hasan bin Ali[a.s] na mwili wake Mtukufu ukaletwa ndani ya msikiti wa Mtume[s.a.w.w] , Banu Ummayya walidhani kwamba Banu Hashim wanataka kumzika karibu na kaburi la Babu yake, wakaeneza fitna na makelele ili asizikwe karibu na Babu yake. Imam Husein[a.s] akasoma kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Enyi mulioamini, musipaze sauti zenu kuliko sauti ya Mtume . Qur'an, 49:2.

Hakuna mtu yeyote aliyempinga Imam Husein[a.s] eti kuwa aya hii inahusu zama za uhai wa Mtume[s.a.w.w] , hata hao Banu Ummayya hawakuthubutu. Na leo hii utawaona Mawahabi wameiandika aya hii na kuiweka kwenye ukuta unaokabiliana na kaburi la Mtume[s.a.w.w] hali ya kuwa wanakusudia kuzuwiya watu wasipaze sauti zao mahala hapo. Na kwa mtiririko huu tunaweza kutoa maana pana zaidi ya aya hii, nayo ni kwamba, ni juu ya Waislamu wa leo kusimama mbele ya kaburi la Mtume[s.a.w.w] na wamuombe Mtume awatakie msamaha kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo kumzuru Mtume[s.a.w.w] hakuna maana isipokuwa kufanya yale ambayo yamo katika aya hii na zinginezo. Aya hii inajulisha maudhui mbili nazo ni:

1. Mtu anawajibika kusimama kwenye kaburi la Mtume[s.a.w.w] baada ya kufa kwake na kumuomba Mtume amtakie msamaha kwa Mwenyezi Mungu.

Tutafafauna maudhui haya wakati wa uchambuzi kuhusu kutawassal kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu, Insha-Allahau Taala.

2. Aya hii inashuhudia kuweko ruhusa ya kuzuru kaburi la Mtume[s.a.w.w] kwani ukweli wa ziyara huwa hauna maana isipokuwa mwenye kuzuru afike pale alipo anayemzuru. Basi ikiwa kusimama mbele ya kaburi la Mtume[s.a.w.w] na kumuomba atutakie msamaha kwa Mwenyezi Mungu ni jambo linalojuzu, bila shaka yatathibiti mambo mawili:

1. Tutakuwa tumemuomba atuombee msamaha kwa Mwenyezi Mungu.

2. Tumefika mbele yake na tumemsemesha.

Na maana ya ziyara hakuna isipokuwa mambo haya mawili.

DALILI NYINGINE

lj-mai ya Waislamu juu ya hukmu fulani miongoni mwa hukmu za kisheria katika zama mbali mbali, huwa inazingatiwa kuwa ni dalili iliyo wazi kabisa ya kusihi kwa hukmu hiyo na kuthibiti kwake. Na ziyara kwenye kaburi la Mtume[s.a.w.w] ni miongoni mwa mambo haya na unadhihiri ukweli wa mambo iwapo tutarejea vitabu vya hadithi, Fiqhi, Akhlaq na Historia na hasa sehemu zinazohusu ibada ya Hija katika vitabu hivyo. Ameutaja ubora wa kuzuru kaburi la Mtume[s.a.w.w] Al-Marhum Al-Allama AI-Amini kutoka katika rejea arobaini na mbili zikiwa ni miongoni mwa rejea muhimu za elimu za Kiislamu. Ndani ya kitabu chake kiitwacho Al-Ghadir kwenye juzuu ya tano ukurasa wa 106 mpaka ukurasa wa 129, amezitaja nassi na ibara zinazohusu maudhi hii kwa undani sana. Miongoni mwa vitabu ambavyo tumevitegemea kutolea ushahidi kuhusu mada hii ni kama ifuatavyo:

1. Shifaus-siqami fi Ziyarati Khairil-Anami, kilichoandikwa na Taqiyyud-din As-Subaki as-Shafii, aliyefariki mwaka 706 A.H. Ndani ya Kitabu chake hiki ametaja mkusanyiko wa maneno ya wanachuoni walioboresha ziyara ya kuzuru makaburi na kuisisitiza sana.

2. Wafa-ul Wafa, kilichoandikwa na As-Samhudi aliyefariki mwaka 911 A.H., naye ametaja katika kitabu chake maneno ya wanachuoni katika kuboresha na kupendekeza ziyara.

3. Al-Fiqhu Alal-madhahibil-ar-baa, kilichotungwa na wanachuoni wanne wa Madhehebu manne, na wamekusanya ndani ya kitabu hicho Fatwa za Maimamu wa Madhehebu manne mashuhuri kwa Masunni. Wanachuoni hawa wanasema: "Kulizuru kaburi la Mtume[s.a.w.w] ni sunna iliyo bora kuliko Sunna zote kwani hadithi nyingi zimekuja juu ya jambo hili".[93] Sasa umefika wakati wa kutaja baadhi ya hadithi zilizopokelewa na wanahadithi kuhusu kuzuru kaburi Ia Mtume[s.a.w.w]

HADITHI TUKUFU JUU YA KUZURU KABURI LA MTUME [s.a.w.w]

Hadithi tukufu ambazo wanachuoni wa hadithi wamezipokea kuhusu kumzuru Mtume[s.a.w.w] ni nyingi mno kiasi kufikia daraja ya Mutawatir, kwa hiyo hatuoni sababu ya kuzihakiki katika Sanadi zake wala wapokezi wake. Mahafidh kutoka Madh-hebu zote za Kiislamu wameziandika katika vitabu vyao na Sihahi zao, na hadithi zote kwa ujumla zinajulisha kwamba, kulizuru kaburi la Mtume ilikuwa ni sunna iliyothibiti kwa wanachuoni hao wa hadithi. Na lau tungetaka kuzitaja zote ingechukuwa nafasi kubwa, kwa hiyo tunatosheka kutaja baadhi yake kama ifuatavyo:

1. Imepokewa toka kwa Abdallah bin Omar kwamba: Mtume[s.a.w.w] amesema: "Ye yote mwenye kuzuru kaburi langu, yamemuwajibikia maombezi yangu ". Hadithi hii imekuja katika kitabu cha Al-fiqhi Alal-madhahibil-ar-baa, Juz. 1 uk. 590.

Wanachuoni wa madhehebu manne wametoa fatwa kwa mujibu wa hadithi hii. Ili kufahamu rejea zilizotumika, rejea kitabu kiitwacho Wafa-ul Wafa, Juz. 4 uk. 1336. Katika mambo yasiyo na shaka ni kwamba, hadithi wanayoipokea mahafidh na maulamaa tangu nusu ya karne ya pili Hijiriya mpaka leo haiwezekani kuwa ni uzushi na eti haina msingi. Sheikh Taqiyyud-din As-Subaki, ameandika uchunguzi wa hadithi hii na Sanadi zake na wapokezi wake katika kitabu chake Shifaus-siqami na akathibitisha kuwa ni hadithi sahihi. (Na kitabu hiki ni kitabu bora mno kilichoandikwa na masunni dhidi ya Ibn Taymiyyah kuhusu kuharamisha kwake Safari ya kwenda kuzuru kaburi la Mtume[s.a.w.w] .

2. Amesema Mtume[s.a.w.w] : "Ye yote atakayenijia kwa lengo la kunizuru na ikawa hakuna kingine kilichomfikisha kwangu ila kunizuru mimi tu, basi nitakuwa na wajibu wa kuwa muombezi wake siku ya Qiyama ". Hadithi hii imetajwa na mahafidh na wanachuoni wahadithi kumi na sita ndani ya vitabu vyao. Naye Taqiyyud-din As-Subaki ameizungumzia hadithi hii katika kitabu chake tulichokwisha kitaja juu ya sanadi zake na wapokezi wake, na vile vile As-Samhudi ameitaja katika kitabu chake Wafa-ul Wafa Juz. 4, uk. 1340.

3. Amesema Mtume[s.a.w.w] "Mwenye kuhiji nyumba tukufu (Al-Kaaba) na asinizuru, basi mtu huyo amenidhulumu ". Hadithi hii wameipokea Masheikh na Mahafidh wa hadithi tisa, na As-Samhudi amewataja kwa ufafanuzi katika kitabu chake Juz. 4, uk. 1342.

4. Mtume[s.a.w.w] amesema "Mwenye kuhiji kisha akalizuru kaburi langu baada ya kufa kwangu, atakuwa kama amenizuru katika zama za uhai wangu ". Wameipokea hadithi hii watu kumi na tano miongoni mwa wanahadithi na mahafidhi mashuhuri. Sheikh Taqiyyud-din As-Subaki katika kitabu chake amezungumzia Sanadi za hadithi hii, kama ambavyo As-Samhudi ameitaja katika kitabu chake Juz. 4, uk. 1340.

5. Mtume[s.a.w.w] amesema: "Mwenye kuzuru kaburi langu au mwenye kunizuru, nitakuwa muombezi wake". Hadithi hii imepokewa na wana hadithi na mahafidhi kumi na watatu, As-Samhudi amewataja ndani ya kitabu chake Juz. 4, uk. 1347. 6. Amesema Mtume[s.a.w.w] : "Mwenye kunizuru baada ya kufa kwangu ni kama amemzuru wakati wa uhai wangu ". Hii ilikuwa ni mifano ya hadithi nyingi ambazo zimepokelewa kutoka kwa Mtume[s.a.w.w] zinazowataka watu na kuwahimiza kulizuru kaburi tukufu la Mtume(s.a.w.w) . Mar-hum Sheikh Al-Amini katika kitabu chake kiitwacho "Al-Ghadir" amekusanya hadithi ishirini na mbili juu ya maudhui hii. As-Samhudi katika kitabu chake, yeye ametaja hadithi kumi na saba na amezungumzia sanadi zake na wapokezi wake kiasi kwamba hakuna Ia kuongeza. [94] Ikiwa Mtume[s.a.w.w] amewataka watu walizuru kaburi lake tukufu, basi bila shaka ni kutokana na matokeo na athari na faida za kimaada na kimaana zinazoambatana na kumzuru yeye na kuwazuru watu wengine mashuhuri wa kidini. Kwa hakika, kutokana na kuzuru kaburi la Mtume[s.a.w.w] Waislamu hupata fursa ya kukifahamu kituo cha Uislamu na pia kuyafahamu matukio yaliyopata kutokea na yanayotokea kwa kipindi hicho na kutoka huko huwa wanajipatia elimu na maarifa ya Kiislamu ambayo huyachukua na kuyasambaza kila pembe ya dunia.

DALILI ZA MAWAHABI KATIKA KUHARAMISHA SAFARI ZA KUZURU MAKABURI

Kinachojitokeza kwa Mawahabi ni kwamba, asili ya kufanya ziyara wanaruhusu, lakini wanaharamisha kufanya safari kwa nia ya ziyara. Muhammad Abdul-Wahabi anasema katika risala yake ya pili miongoni mwa risala za "Hadiyatus-saniyyah" kama ifuatavyo: "Inasuniwa kumzuru Mtume[s.a.w.w] , isipokuwa haiwezi kufungwa safari ila kwa (nia ya) kuzuru msikiti na kuswali ndani yake". Na dalili wanayoshikilia katika kuharamisha ziyara ni ile hadithi iliyotajwa katika Sihahi zao kutoka kwa Abu Huraira!! Kwamba Mtume[s.a.w.w] amesema, "Haifungwi safari isipokuwa kwa Misikiti mitatu: Msikiti wangu huu na Masjidil-haram (Makka) na Masjidil-Aqsaa (Baitul-Muqadas). Na imepokewa tena hadithi hii kwa namna nyingine kama ifuatavyo: "Hakika hufanywa safari kwenda kwenye Misikiti mitatu: Msikiti wa Al-Kaaba, na msikiti wangu na msikiti wa Il-Yaa. Vile vile imepokewa kwa namna ya tatu nayo ni hii: "Hufungwa safari kwenda kwenye Misikiti mitatu..."

Hadithi zote hizi tatu amezileta Muslim ndani ya Sahih yake.[95] Hapana shaka yoyote kwamba hadithi hii imo katika Sihahi lakini sasa hivi sisi hatuko katika uwanja wa kuijadili hadithi hii, hasa kwa kuwa katika sanadi hii yako Bwana Abu Huraira (ambaye hali yake inaeleweka kwa wanachuoni) bali makusudio yetu ni kutazama hadithi hii inamaanisha nini. Basi hebu na tukadirie kwamba Nassi ya hadithi hii iko kama ifuatavyo: "Haifungwi safari ila ya kwenda kwenye Misikiti mitatu...." Ukweli unaothibiti ni kwamba harfu ya "Il-la" ni "Adatustith-Nai" kwa hiyo hapana budi awepo "Mustathna minhu" na ni wajibu afahamike. Na kwa kuwa hapa katika Nassi hayupo, basi hapana budi kumkadiria kuwa yupo katika maneno haya.

Na kabla ya kuonyesha dalili zinazopatikana inawezekana kumkadiria Mustath-na Min-hu kwa namna mbili:

1. Haifungwi safari kwenda kwenye Msikiti miongoni mwa Misikiti isipokuwa Misikiti Mitatu...

2. Haifungwi safari kwenda sehemu miongoni mwa sehemu yoyote isipokuwa kwenye misikiti mitatu... Kuifahamu hadithi hii na kuichunguza maana yake kutategemea moja ya makadirio haya mawili. Basi iwapo tutachagua makadirio ya kwanza, maana ya hadithi itakuwa kutokufungwa safari kwenda msikiti wowote isipokuwa misikiti ile mitatu, wala haitakusudia kutoruhusu kufungwa safari kwenda sehemu yoyote hata kama sehemu hiyo siyo msikiti. Kwa hiyo katazo lililopo hapa halimhusu yule anayefunga safari kwa ajili ya kuwazuru Manabii, Maimamu Watukufu na wachamungu, kwani mahala panapofanyiwa uchambuzi ni ufungwaji wa safari za kuzuru misikiti kwa kuwa misikiti iliyovuliwa ni mitatu. Ama anayefunga safari kuyazuru maziyara matukufu hatahusika na katazo hili wala haingii katika maudhui hii. Maelezo haya ni kwa mujibu wa makadirio ya kwanza.

Tukija kwenye makadirio ya pili ni lazima zihusike safari za aina zote za kidini isipokuwa safari za kwenda sehemu hizo tatu zilizotajwa, sawa sawa kama safari hizo zitakuwa ni kwa ajili ya kuzuru msikiti au kuzuru sehemu nyinginezo. Lakini qarina na dalili zinaelekeza kwamba makadirio ya mwanzo ndiyo sahihi kama tutakubali kwamba sanadi ya hadithi hii ni sahihi. Ama qarina zinazoonyesha kusihi kwa makadirio ya kwanza ni kama ifuatavyo: Kwanza: Misikiti iliyovuliwa ni mitatu na hiyo Istith-nai ni Mut-tasil kama inavyoonekana wazi, basi hapana budi mustathnaminhu awe ni misikiti na wala siyo mahala. Kama mtu atasema: "Majaa Il-la Zaidun" yaani "hakuja isipokuwa Zaidi" basi "Mustath-na Min-hu" katika sentensi hii atakuwa ni mtu au watu na wala haliwezi kuwa ni tamko la ujumla kwa mfano kitu. Pili: Lau kama lengo lingekuwa ni kuzuwiya safari zote basi Istith-nai ya misikiti mitatu tu haitosihi kwani mtu hukusudia safari katika msimu wa hija na akafanya safari kwenda "Arafa" na "Mash-ari na Mina".

Kwa hiyo kama safari za dini zisizokuwa za misikiti mitatu zingekuwa haramu, basi ni kwa nini zinafanywa katika sehemu hizi tulizozitaja? Tatu: Qur'an Tukufu na hadithi tukufu vinaashiria kuwepo kwa safari zingine za kidini na kumekuja msukumo wa kuhimiza na kusisitiza kuhusu safari hizo, kama vile safari kwa ajili ya kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kutafuta elimu na kuunganisha udugu, kuwazuru wazazi na mfano wa hayo. Na miongoni mwa hayo yapo ambayo Mwenyezi Mungu ameyazungumzia aliposema:

وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَائِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ ﴿١٢٢﴾

"Kwa nini halitoki kundi katika kila Taifa miongoni mwao liende likajifundishe vyema dini na kisha wakaja kuowaonya wenzao (waliosalia) ili wapate kujihadharisha". Qur'an, 9:122.

Na kwa sababu ya aya hii wafasiri wakubwa na wahakiki wa hadithi wameifasiri hadithi hii kama tulivyoonyesha sisi.

Kwa mfano: Ghazali anasema katika kitabu chake Ih-yaau Ulumid-din: Sehemu ya Pili: Nayo ni kuwa, asafiri kwa ajili ya ibada ima ya Hija au Jihadi na inaingia katika jumla ya hayo, kuzuru makaburi ya Manabii[a.s] , na kuzuru makaburi ya Masahaba na Tabiina na wanachuoni na Mawalii na kila ambaye (watu) hutabaruku kwake zama za uhai wake, basi watatabaruku kwa kumzuru baada ya kufa kwake." "Na inajuzu kufunga safari kwa lengo hili na wala halizuwiliki hili kutokana na kauli ya Mtume[s.a.w.w] aliposema: "Haifungwi safari isipokuwa kwenda kwenye misikiti mitatu, musikiti wangu huu na masjidil-haram na masjidil-Aqsa: Kwa sababu hadithi hii inahusu misikiti tu kwani misikiti yote ni sawa sawa katika ubora isipokuwa misikiti mitatu na hakuna tofauti baina ya kuzuru makaburi ya Mitume, Mawalii na wanachuoni katika asili ya ubora japo katika daraja kuna tofauti kubwa kutegemea vyeo vyao mbele ya Mwenyezi Mungu.[96] Kwa hiyo kilichokatazwa katika hadithi ni kufungwa safari kwenda kwenye Misikiti yoyote isiyokuwa hiyo mitatu, na haihusiki safari ya kuzuru au kwa malengo mengine ya dini.

Na kwa kumalizia, hapana budi tuonyeshe kwamba Mtume[s.a.w.w] wakati aliposema "Haifungwi safari isipokuwa kwenda kwenye Misikiti mitatu", alikuwa hana maana kwamba kufunga safari kwenda kwenye Misikiti mingine ni haramu, bali maana yake ilikuwani kwamba haistahiki mtu kufunga safari na kupambana na mashaka ya safari kwa ajili ya kuzuru Misikiti hiyo kwani Misikiti hiyo haitofautiani katika ubora kwa tofauti kubwa, sawa sawa kama Msikiti uko mjini an kijijini au schemu fulani hapana tofauti kubwa, na kwa ajili hiyo hapana kinachomlazimisha mtu kuifungia safari Misikiti hiyo. Ama akifunga safari kwa ajili ya Misikiti yoyote basi tendo la mtu huyo haliwi ni haramu wala lenye kwenda kinyume cha sunna tukufu, hilo linajulishwa na kile walichokipokea As-habus-sihah Wassunan: "Mtume[s.a.w.w] alikuwa akienda kwenye msikiti wa Qubaa hali akiwa kwenye kipando au kwa miguu, basi (akifika) huswali rakaa mbili msikitini. [97] Sisi tunawajibika kujiuliza ni vipi itawezekana kuwa haramu kufunga safari na kukata masafa marefa kwa ajili ya kusimamisha sala katika moja ya nyumba miongoni mwa nyumba za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Ikiwa kuswali msikitini ni Mustahabu basi kilichodhahiri ni kuwa kitangulizi cha Mustahabu ni Mustahabu vile vile.