Hadith Ya Mufazzal

Hadith Ya Mufazzal0%

Hadith Ya Mufazzal : Mohammed Kanju
Kundi: Vitabu mbali mbali

Hadith Ya Mufazzal

: Mohammed Kanju
Kundi:

Matembeleo: 8303
Pakua: 2270

Maelezo zaidi:

Hadith Ya Mufazzal
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 4 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 8303 / Pakua: 2270
Kiwango Kiwango Kiwango
Hadith Ya Mufazzal

Hadith Ya Mufazzal

Swahili

HADITHI YA MUFAZZAL

UTANGULIZI

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

Sifa zote njema ni zake Yeye ambaye ameumba bila ya Yeye mwenyewe kuumbwa. Nilfikiriya mwenyewe kuwa ni mwenye bahati sana kwa kupewa fursa hii ya kuchapisha na kupanga tena upya kitabu hiki. Ningependa kuhakikisha pande zote kwamba hakuna kishawishi chochote cha pesa kwenye uchapishaji huu, na kwamba imefanywa tu kwa kutaka radhi za Allah (s.w.t).

Namshukuru pia Akhiy Mohammed Kanju aliyegeusha kitabu hiki kwenye Kiswahili. Mtumishi wa Allah

Bashir Alidina

ASILI YA HADITHI

Muhammad Bin Sanah anasimulia kwamba Mufazzal Bin Umar alimsimulia hivi: "Siku moja baada ya Sala ya Alasiri nilikaa baina ya Mimbari na Kuba la Mtukufu Mtume(s.a.w.w) nikitafakari juu ya ukubwa wa vyeo vitukufu, ambavyo kwamba Allah (s.w.t) amenijalia Maulana Bwana wetu Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ambavyo kwa ujumla Ummah ulikuwa hauna habari wala kwa ule ukubwa wa fadhila wala kwa sifa zake zilizo kamili wala kwa utukufu wake wa pekee. Nikiwa nimezama katika kuwaza huko, mara alitokea Bin Abi Al Auja, kafiri mshirikina na akakaa umbali wa kuweza kumsikia. Sahiba wake alimfuata na akakaa kwa utulivu ili kusikiliza.

Bin Ali Auja alianza mazungumzo kwa kusema: "Mwenye Kuba hili amepata fadhila kubwa za pekee kwa ukamilifu wa heshima kuu katika yote aliyoyafanya." Sahaba wake aliongeza kwa kuthibitisha akasema: "Alikuwa filossofa na alifanya dai kubwa likiungwa mkono na miujiza ambayo kwamba ilishangaza akili za kawaida. Waliojifanya ni wenye hekima walizama kwa undani wa vina vya akili zao kupenya kwenye maajabu hayo (ili kuyajua) lakini bila mafanikio. Ujumbe wake ulipokubaliwa na watu wastaarabu, wenye maarifa na wasomi watu kwa ujumla waliingia katika imani yake makundi kwa makundi. Sehemu za ibada na Misikiti ya sehemu zote ambako popote ulipofika wito wa utume wake ulianza kusikika kwa nguvu na kueleweka pamoja; na jina lake (kutajwa) sambamba na lile la Allah (s.w.t) bila ya tofauti yoyote ya bahari na bara, mlima na tambarare, bonde, siyo mara moja lakini mara tano kwa siku wakati wa Adhana na Iqamah. Lilipata jina lake (limepata) kuambatanishwa na lile la Allah (s.w.t) na maelezo yenye lengo la kuendeleza kumbukumbu yake na kuuweka ujumbe wake uwe ni wenye elimu ya kuendelea." Bin Ali Auja akasema: "Weka kando habari za kumtaja Muhammad(s.a.w.w) ambaye kuhusu yeye, akili yangu ina shangazwa vikubwa na mawazo yangu yamefadhaishwa.

Hebu tuongelee ukweli katika msingi wa watu kukubali imani ya Muhammad(s.a.w.w) - Mwenye Rehema kwa ulimwengu. Je, kuna kiumbe wa namna hiyo au hapana?" Kisha alirejea katika asili na uumbaji wa mpangilio mkubwa wa ulimwengu. Alifanya dai lisilosadikika kwamba hakuna aliyeviumba na hakuna Muumba, wala Msamii wala Mtengenezaji - Ulimwengu umejitokeza wenyewe. Katika kuwepo na ataendelea kuwepo na kwa hiyo hauna mwisho." Nilijisikia vibaya umno kusikia hivi na nikamwambia : "Ewe usiye amini! Huwamini katika imani ya Allah (s.w.t) kwa kukanusha moja kwa moja kuwepo kwake ambaye amekuumba wewe katika umbo zuri, akakugeuza kutoka hali moja kwenda hali nyingine, mpaka ukafikia katika umbo ulionalo sasa? Lau ungejifikiria wewe mwenyewe na lau akili zako nzuri zingekusaidia kiukweli, ungeweza kutambua katika nafsi yako mwenyewe hoja hizi za wazi za kuwepo kwa Allah Mtukufu Ishara ya vitu vyake vyote anavyoviruzuku na ushahidi wa Usanii wake usio na mipaka.

Alisema, "Tutajadili suala hili kama utapanga kwa utaratibu misingi ya kusadikisha hoja ambazo tutazikubali, vinginevyo huna haki ya kutia maneno yasiyo kuwemo bila ujuzi wa majadiliano. Kama wewe ni mfuasi wa Ja'far Bin Muhammad(a.s) haikupasi wewe kuzungumza katika tabia ambayo unaifanya kwani yeye si mwenye mtindo wa kuzungumza hivi wala habishani na sisi katika hali ya utovu wa adabu namna hii. Amesikia zaidi maneno yetu kuliko ulivyofanya wewe, lakini kamwe hajatumia maneno yoyote yasiyo adabu, wala kamwe kujibu kwa ukali kuanzisha ugomvi.

Ni mwenye kuvumilia sana, mwenye heshima, mwenye akili (za kuhoji) na mwanachuoni aliyepevuka. Yeye kamwe si mkali wala si mwenye hasira. Anayasikiliza maneno yetu kwa usikivu sana. Huvuta hoja zetu kiasi kwamba wakati tunapomaliza kabisa silaha zetu (hoja) na kufikiri kwamba tumemnyamazisha yeye kwa maneno machache huibuka tena, kuyavunja maoni yetu yote na kutufanya kuwa mabubu hivyo kwamba tukaachwa bila kuwa na uwezo wa kujibu hoja za Mtukufu Mstahiki. Kama wewe ni mfuasi wake, basi zungumza nasi katika tabia hiyo hiyo.

Kwa hili, nilitoka nje nikiwa na huzuni mno na mawazo tele kwasababu ya kutokuamini kwao katika Allah (s.w.t) na matokeo ya huzuni na majonzi ya Uislamu na Wachaji wake, kwasababu ya kutokuamini kwao na usahifi usio na maana wa ulimwengu huu. Nilikwenda mwenyewe kwa Bwana wangu, Imam Ja'afar Al Sadiq(a.s) . Aliponiona nimehuzunika, aliniuliza sababu ya kuwa hivyo. Nilimsimulia mazungumzo ya wale mushirikina na jinsi nilivyo jaribu kuoenyesha uongo wa hoja zao.

Aliniambia nije siku inayofuatiya (yaani kesho yake) wakati atakapo weka wazi kwangu ustadi mkubwa mno wa mwenye nguvu zote msanifu aliyedhihirika katika ulimwengu wote ulio na wanyama, na ndege, wadudu, vitu vyote vilivyo hai ama viwe ni wanyama au jamii ya mimea, miti izaayo matunda au dufu na ile isiyo na matunda, mboga zinazolika na zisizolika - maelezo ya kiustadi yatakayokuwa kama kifungua macho kwa wale ambao watakubali maelekezo; faraja kwa waumini na fadhaa kwa wazushi. Niliposikia haya, nilirudi kutoka sehemu yake tukufu nikiwa katika hali ya furaha. Ujio wa usiku ule ulionekana kuwa mrefu kwasababu ya shauku yangu kubwa ya kujifunza kutoka kwa Mwanachuo mstahiki huyo, mambo aliyoahidi kuyaeleza kesho yake.

BARAZA LA KWANZA MWANADAMU

Asubuhi na mapema niliwasili mwenyewe na baada ya kukaribishwa vizuri, nikisimama kiheshima mbele ya sehemu yake tukufu, na kushukua nafasi yangu ya kukaa ambayo nimepewa. Kisha yeye(a.s) alikwenda kwenye chumba cha faragha ambacho mara kwa mara huenda kujipekesha. Na mimi vile vile nilinyanyuka baada ya kuamrishwa, nilimfuata. Aliingia chumba kile cha faragha na miminilikaa chini mbele yake. Akasema, "Mufazzal! Nahisi kwamba umekuwa na usiku mrefu kwa sababu ya shauku yako kwa ajili ya kesho. Nilithibitisha maneno yake kiheshima. Alianza, "Allah (s.w.t) alikuwepo kabla hakujakuwa na kitu chochote na utakuwepo kiroho kupindukia milele. Atukuzwe Yeye kwa vile Ameufanya ufunuo wake kwetu. Kwake Yeye Anastahiki shukurani zetu za dhati kwa sababu ya tunu yake kwetu. Ametupa sisi daraja kubwa pamoja na elimu bora na akatuanisha sisi pamoja na utukufu wa cheo (kwani kwa vile tu) kizazi cha Hadhrat Ali Ibne Abu Talib(a.s) kupita viumbe vyote kwa elimu yake, ikiwa ni dhamana tukufu, pamoja nasi ya upambamizi wa (mambo) ya ulimwengu huu. Niliomba ruhusa aweke picha kamili yale yote yaliyotoka mdomoni (kinywani) mwake, kwa vile nilikuwa na kila kitu muhimu kwa kuandikia, kitu ambacho alikubali kwa furaha.

Akasema: "Ewe Mufazzal! Wababaishaji wameshindwa kufahamu siri na sababu zilizo msingi wa asili ya viumbe, na akili zao zimebaki kutokuwa na habari ya ustadi usio na kosa uendeleao kuwepo chini ya uumbaji wa jamii mbali mbali (za viumbe) wa bahari na bara, tambarare na miinuko miinuko. Wakawa makafiri, na kwa sababu ya kasoro ya elimu yao na ufinyu wa akili, wakaanza ulaghai ushindanao pamoja na ukweli, kiasi kwamba waliukataa uumbaji na kudai kwamba ulimwengu wote huu hauna maana yoyote ni bure tu, bila kuwa na ustadi wowote wa usanii juu ya uhusikaji na usanii au Muumba - bila kusudio usio na mwisho bila uwiyano au utulivu.

Allah (s.w.t) yu mbali mno na yale yote wanayomhusisha nayo. Na wapotelee mbali! Kulioje Kupotoka kwao! katika upofu wao wa kupotoka na bumbuazi, wako kama watu vipofu wapapasao kulia na kushoto katika nyumba iliyopambwa vizuri, iliyojengwa vizuri pamoja na mabusati mazuri, vitu vitamu vya chakula na vinywaji, aina mbalimbali za nguo na vitu vingine muhimu vya matumizi ya lazima, vyote vimewekwa kwa kutosheleza kwa kiasi kizuri na kuwekwa kwa ukamilifu makini na ustadi wa kusanii. Katika upofu wao wameshindwa kuliona jengo hilo na mapambo yake. Wanapita kutoka chumba kimoja kwenda kingine, wakiendelea mbele na kurudi nyuma. Kama kwa bahati yeyote mmoja kati yao atakuta kitu chochote katika mahali pake kinatoa hitaji, na asijue kusudio la kuwekwa pale na asijue (usitajwe) usitadi ulio chini yake, huenda akaanza kumlaumu Mjenzi wa (hilo) jengo kwa chuki zake na hasira, wakati ambapo, kusema kweli, makosa ni yake kwa kutokuwa na uwezo wa kuona.

Kutokulingana huku kwa tabia hushikilia vizuri katika kadhia ya tapo, ambalo hukataa nguvu iumbayo na hoja hiyo ipendeleayo usanii wa Kiungu. Hushindwa kutambua ubora wa riziki zao, ukamilifu wa uumbaji na uzuri wa Usanii, wanaanza kutangatanga katika mapana ya dunia, wakifadhaishwa kwa kutokuweza kwao kufahamu kwa akili zao sababu na misingi iliyo chini yake. Hutokea hivyo wakati mwingine kwamba mmoja miongoni mwao anayo habari ya kitu, lakini katika ujinga wake juu ya ukweli wake, kusudio na mtaji, huanza mara moja kulitafutia kosa akisema, "Ni kosa lisilothibitika."

Wafuasi wa Mani (Mtu aliyeanzisha Dhehebu la Zorasti wakati wa Mfalme Shapur mwana wa Urdisher, ambaye aliamini Utume wa Isa(a.s) lakini akaukataa ule wa Musa(a.s) na ambaye aliamini katika Uwili wa Uungu kama Waumbaji wa vizuri vyote na viovu katika ulimwengu huu - Nuru moja kama Muumba wa vitu vizuri, nyingine ya giza, kama ile ya wanyama wakali na viumbe vyenye madhara) ambao, kama valivyo washupavu katika kundi potovu la uovu, wameanza kutangaza waziwazi upotofu wao. Mbali na haya, baadhi ya watu wengine ambao waliopotoka nao pia wamepotea kutoka fadhila za Kiroho (Kiungu) kwa kutamka tu kama yakini halisi isiyothibitika au isiyowezekana.

Inampasa mtu ambaye Allah (s.w.t) amemjaliya na elimu ya maajabu ya Kiroho ya ukweli na ambaye amemuongoza kwenye imani yake, na ambaye amepewa kuona na kutafakari juu ya ujuzi wa usanii ulio chine ya uumbaji, na ambaye ametunukiwa uelezaji wa sifa wa vitu hivyo, juu ya msingi wa akili isadikishayo na sifa nzuri. Inampasa mtu kama huyo kumtukuza Allah (s.w.t) kwa ukamilifu kama Mola wake na fadhila za Kimbinguni, na kumuomba Yeye kwa kumzidishia elimu ya mambo ya Kiroho na msimamo imara ndani yake, na uwezo wa juu wa maelezo juu ya hayo. Yeye (s.w.t) asema, "Nitaongeza fadhila zangu, kama mtakuwa ni wenye kushukuru, na adhabu yangu ni kali kama hamtakuwa wenye kushukuru." Muundo wa Ulimwengu huu ni mwongozo wa juu zaidi na hoja ya kuwepo Allah (s.w.t) jinsi sehemu zake (huo ulimwengu) zilivyounganishwa pamoja na kuwa na ufundi mzuri wa Usanii.

Hali ya kufaa kutafakari na akili kuangalia kuhusu sehemu moja moja hudhihirisha kwamba ulimwengu huu unalinganishwa na nyumba iliyopambwa na vitu vyote muhimu kwa ajili ya mwanadamu. Mbingu hii ni kama chandalua; ardhi imetandazwa kama busati ambapo nyota zimewekwa katika safu juu ya safu zikijitokeza kama taa zilizowashwa katika sehemu zao. Vito vya thamani vimehifadhiwa kama kwamba ni nyumba yenye mkusanyo wa vitu vingi. Mbali na hivi kila kitu kiko tayari kupatikana kukidhi mahitaji ya mtu binafsi.

Mtu, katika Ulimwengu huu, ni kama bwana mmiliki mwenye nyumba, akiwa ni mwenye kumiliki kila kitu ndani yake. Na siyo jamii tofauti za mimea zipatikanazo kukidhi mahitaji ya mtu binafsi - baadhi ni chakula cha wanyama, nyingine ni dawa kwa Wanadamu; baadhi ni kwa mapambo tu, baadhi ni kumpatia mtu manukato kwa burdani yake, baadhi ni dawa kwa wanyama, baadhi ni lishe kwa Mwanadamu, baadhi kwa ndege tu na nyingine kwa wanyama wa miguu miine peke yao na kuendelea. Jamii tofauti za wanyama zimepangiwa kazi kwa mahitaji na faida maalum.

KUUMBWA KWA MWANADAMU

Tunaanza sasa na maelezo ya kuumbwa Mwanadamu kabla hujajifundisha somo litokanalo humo. Hatua ya kwanza katika kuumbwa kwa Mwanadamu hurejea kwenye hali wakati Kijusu (Mimba) kinapowekwa kimpango katika tumbo la uzazi, ingawa imefungwa ndani ya aina tatu za sitiri zilizo wazi na aina tatu za viza. Ya kwanza ikiwa ni ile ya ukuta wa nje, ya pili ni ya tumbo la uzazi na ya tatu ni ya Kondo la nyuma. Huu ni wakati ambapo kijusu hakiwezi kujilisha wala kuondoa madhara yoyote yatokanayo nayo.

Mtiririko wa Heidh umeadilishwa ili kutoa lishe kwa ajili yake, kama vile maji yanavyochukua lishe kupeleka kwenye mimea. Hivyo mpango huu huendelea mpaka kufikia wakati ambao viungo vyake vimekamilishwa, ngozi juu ya mwili wake huwa imara kiasi chakustahimili hali ya hewa - hivyo kwamba haiwezi kupata madhara yoyote kutoka kwenye hewa na macho yake yanapata uwezo wa kustahimili mwanga. Wakati vyote hivi vinapokuwa vimekwisha fanyika, mama yake hupatauchungu wa uzazi, ambao kwa ukali humtikisa kumfikisha kwenye kuhangaika, kufikia upeo wa kuzaliwa mtoto. Na kwa kuzaliwa mtoto, mtiririko wa heidhi uliokuwa ukipeleka lishe kwenye tumbo la uzazi unabadilishwa kwenda kwenye matiti ya mama. Ladha yake inabadilishwa hivo hivo na rangi yake, na kuwa lishe aina ya pekee tofauti ambayo hufaa hasa kwa hali ya mtoto, kama na wakati ahitajiayo (hayo) hayo, kulinganishwa na mtiririko wa damu.

Wakati ule ule wa kuzaliwa kwake anaanza kutikisa na kulamba midomo yake kwa ulimi wake kuonyesha hamu yake ya (kunyonya) maziwa hukuta jozi ya matiti ya mama yake matamu mno yaliyohifadhiwa yakining'inia tayari kwa kumpatia lishe kwa ajili yake. Hupata lishe yake kutoka maziwa katika njia hii mpaka wakati huo, kwa vile mwili wake bado ni mororo, viungo vyake na matumbo yake ni laini na dhaifu.

MENO NA NDEVU

Kama aanzavyo kutembea na kuhitaji chakula kigumu kujenga mwili weneye nguvu, magego yake hutokeza kutafuna vyakula kurahisisha uyeyushaji wachakula tumboni. Huendelea na lishe hiyo mpaka anapofikia balehe. Mwnaume anaota nywele katika uso kama alama ya uume kupata heshima kama mwanaume, hivyo kupita hatua ya utoto na kufanana na wanawake. Mwanamke huuweka uso wake safi, upendezao na bila nywele, kuuweka umaridadi wake na umbo zuri. Kama mvutio kwa wanaume katika huduma ya kulifanya Taifa liishi. Je, unaweza ukafikiria hali ambayo mtu katika kupitia kwenye hatua zote hizi tofauti ameongozwa na kukamilishwa, zinaweza zikatoka bila ya kuwa na Msanii na Muumba? Je, unafikiri kama mtiririko wa heidhi usingegeuzwa kwake wakati ni kijusu katika tumbo la uzazi,je, asingeweza kukauka kama vile mimea ikaukavyo, ikinyimwa maji? Na je, kama isingekuwa ni kusukumwa kwa uchungu wa uzazi baada ya kukomaa kwa uzazi, je, asingezikwa katika tumbo la uzazi kama vile mtoto anaeishi anavyozikwa katika ardhi?

Na je, kama asingepatiwa aina nzuri ya maziwa, je, asingekufa kwa njaa? kama asingelishwa na lishe nzuri zenye kulingana na hali ya uwezo wake ya kuukamilisha mwili wake na kama meno yake yasingetoka katika wakati mahususi, je, isingekuwa matatizo kwake kula, kutafuna na kuyeyusha chakula chake? Na kama asingepitia kipindi cha utoto cha kunyonya, mwili wake usinge umia katika sulubu na kudhoofika kwa kazi yoyote kwa matokeo ya mabadiliko ya kudumu juu ya mama yake kwa kumfanya ashughulike na silika yake tu na kumlea, bila muda wa kutafuta mtoto wa pili? Uso wake usingeota nywele katika wakati mahususi, je asingekuwa yu ngali katika hali yautoto na maumbile ya wanawake, bila ya murua wowote au sifa kama vile matoashi ambao wana sura mbaya kwa kukosekana ndevu? Ni nani basi huyo, ambaye amemuumba mtu bure bure tu, ambaye amekuwa mjenzi wa thamani yake, ambaye daima ni mwenye hadhari kumpatia mahitaji yake wakati wote?

UPUUZI WA ULAHIDI

Kama kujitokeza kwa uumbaji bila Msanii maalum kuna weza kukubalika chini ya masharti ya kawaida hii, basi matilaba ya Kizazi na uwiano thabiti wa uumbaji unaweza kuwa chanzo cha kosa na fadhaa, kwa vile viwili hivi vinapingana na kujitokeza kwa uumbaji bila usanii maalum. Maelezo kama hayo ni ya upuuzi wa hali ya juu kwamba mpango na kurekebisha kwa pasa kutokea hivi bila Muumba, na mpango mbaya na usio faa wa usanii na maumbile vingepaswa kuhusishwa na Muumba. Asemaye hivi ni juha kwa sababu kitu chochote kilicho tengenezwa bila usanii kamwe hakiwezi kuwa sawa na kulingana ambapo visivyo mpango na ukaidi haviwezi kuepo pamoja na usanii wa mpango. Allah (s.w.t) yuko mbali na wanayo sema wapotofu. Na kama mtoto angezaliwa na akili pevu, angepumbazishwa na ulimwengu huu jinsi ulivyo mgeni kwake, katika mazingira yasiyoeleweka yaliyo zunguukwa na wanyama na ndege wa kila aina pande zote, ambavyo vingeonekana katika macho yake kila muda wa siku.

Ifikirie katika hali ya mtu anayehamia nchi nyingine kutoka jela ya nchi nyingine, kama ana akili timamu, utamwona akiwa ametatazika na kufadhaika. Hawezi kujifundisha lugha ngeni kiasi cha kutosha kwa mara moja, wala kuupata mwenendo na tabia za mahali hapo. Kwa upande mwingine, yule ambaye anachukuliwa kama mfungwa kupelekwa nchi ngeni katika siku zake za mwanzo wakati akili yake ni changa, mara moja atajifundisha lugha hiyo, mwenendo na tabia za sehemu hiyo.

Hivyo hivyo, kama mtoto angezaliwa na akili pevu angeshangazwa katika kufumbua macho yake na kuona vitu mbali mbali vilivyopangwa kwa mpango namna hiyo, aina mbali mbali ya maumbile na mawazo yaliyo wazi ya umoja na faraka. Kwa muda mrefu, asingeelewa ni lini amekuja na ni wapi alipofikia na iwapo yale yote aliyokuwa akiyaona ni ndoto. Kisha, kama angezaliwa na akili pevu angejisikia kinyaa na kushushwa hadhi, kujiona yeye mwenyewe ni mwenye kupakatwa huku na huku miknoni, akilishwa kwa maziwa, kufungwa ndani ya vitata (desturi ya Waarabu) na kulazwa katika susu - hatua zote hizi zikiwa za muhimu kwa mtoto wachanga kwasababu ya umororo na ulaini wa miili yao.

Yasingekuwepo haya, kama wangezaliwa na akili pevu, kudekezwa huku, wala kudekezwa kule, wala upole huu kwa watoto wachanga katika akili za watu wazima ambako kikawaida huonekana kutokana na huba kwa watoto ambao hawakufundishwa kwa sababu ya unyofu wao hujenga hadhari maalum kw ajili yao. kwa hivyo anazaliwa katika ulimwengu huu bila kuelewa kitu chochote, bila kuelewa kabisa ulimwengu na kila kilichomo humo. Anayaangalia mambo yote haya na akili yake changa na upungufu wa kuelewa, na hivyo hajiskii kutatazika.

Akili yake na kuelewa kidogo kidogo, polepole muda hadi muda, kukua kidogo kidogo, hivyo ili kumuingiza kwa taratibu kwenye vitu vilivyo mzunguuka na kuizoeza akili yake ipasavyo ili kumzoesha kwa hayo bila kuhitaji udadisi zaidi na maajabu, hivyo kumwezesha kutafuta riziki yake kwa utulivu pamoja na kuelewa na kupanga, kuweka juhudi zake humo, na kujifunza masomo ya utii, makosa na utovu na adabu.

Na tazama! Kuna sehemu nyingine za mambo. Kama mtoto mchanga angezaliwa na akili pevu pamoja na kuelewa kazi zake, kungelikuwa na nyakati chache za deko lihisiwalo katika kawaida ya mtoto mdogo, na mahitaji, ambayo kwamba wazazi wanajikuta nyakati zote tangu mwanzo wanajishughulisha kwa mambo ya vijana wao, yasingejitokeza. Pendo na huba, vihisiwavyo kwa watoto wa kawaida, kufuatia taabu walizopitia kwa ajili yao, isingekuwepo baina ya wazazi na vizazi vyao. Kwa sababu ya akili zao pevu, watoto wasingehitaji matunzo ya wazazi. Mtengano ungeanza punde tu baada ya kuzaliwa kwa mtoto mchanga kutoka kwa wazazi wake. Hata mama au dada wangekuwa wageni kwake na kwa hivyo (pia) katika mipaka ya ndoa. Huoni kwamba kila kitu kikubwa au kidogo kimeumbwa katika mpango usio kombo bila dosari au kosa?

MACHOZI

Hebu tizama faida ya matokeo kwa watoto itokanayo na kulia. Kuna maji katika ubongo wa mtoto ambayo kama hayakutolewa, huweza kusababisha matatizo au maradhi, hata pengine jicho kupotea. Kutoka kwa maji kutoka katika ubongo wake huliacha kuwa na afya na macho kuwa na mng'aro zaidi, mtoto anafaidika kwa kulia, ambapo wazazi wake katika kutokojua kwao, hujaribu kuzuia kulia kwake kwa kumpatia matakwa yake, bila kujua faida ya huko kulia. Ziko faida nyingine kama hizo ambazo walahidi wameshindwa kuzifahamu, na kama wangeweza kuzifahamu, wasingeweza kukanusha kuwepo kwa faida hizo katika hili. Watu wenye elimu ya kiroho wanaelewa ni nini kisichotambulikana kwa wakanushaji hawa. Hutokea hivyo wakati mwingine kwamba viumbe hawajui hekima iliyoko humo, ingawa iko katika elimu ya Muumba.

MATE

Udende utokao midomoni mwa watoto huweza kusababisha uharibifu mkubwa kama hautaruhusiwa kutiririka. Hii inaweza kuonekana kwa wale wenye mate mengi ambao huzama chini katika hali ya mabaradhuli, mapunguani na wapumbavu, na kuwa chambo cha magonjwa mengine kama kiharusi - (kupooza) mwili nzima na (kiharusi cha) uso. Allah Azza Wa Jalla, ameamrisha kwamba maji haya yanapasa kutolewa kwa njia ya mdomo ili kumweka katika siha nzuri kwa uzuri wake wa baadae. Majaaliwa yametoa fadhila hii, ya uzito ambao wao hawajui. Wanaruhusiwa nafasi hii kupata elimu ya hekima iliyomo ndani yake, ili kwamba wawe wenye elimu ya Kiroho na kama watu hawa wangeshukuru fadhila zote hizi, wasingebakia katika dhambi kwa muda mrefu hivi. Hivyo sifa zote na utukufu ni wake Yeye. Ukubwa ulioje wa rehema zake. Baraka zake ni kwa wote wawe wamestahiki au hawastahiki, Yuko mbali, ametukuka juu ya yale wanayosema watu hawa waliopotoka.

VIUNGO VYA JINSIA

Hebu fikiria viungo vya mwanaume na mwanamke vya ngono. Kiungo cha mwanaume kina uwezo wa kuamka (kwa ashiki) na kuongezeka ili kuweza kuutolea manii mfuko wa uzazi - hiyo ikiwa ndiyo kazi yake, ikiwa chenyewe hakina uwezo wa kukuza kilenga na kwa hivyo kuhitaji uhamisho wa manii kwenda mfuko wa uzazi wa mwanamke - mfuko ulio ndani ulinganao na kuhifadhi kiufanisi matone mawili ya mbegu za uzazi, kukuza kilenga kwa kutanuka kikadiri kwa kuongezeka ukubwa wake, kuzuia shinikizo lolote juu yake, kukihifadhi mpaka kinaimarishwa na kufanywa imara. Je, haikusanifiwa hivyo na msanii aonae kwa undani zaidi? Je, kazi zote hizi za ustadi, au kadiri hizi jamala (uzuri) zimejitokeza hivi hivi zenyewe? Allah Azza Wa Jalla Yu mbali, ametukuka juu ya upotofu wa Washirikina.

VIUNGO VYA JUMLA

Hebu fikiria viungo mbali mbali vya mwili, kazi zitakiwazo kwa kila kimoja kufanya na ukamilifu wa usanii uliomo ndani ya kila kiungo. Mikono yote imekusudiwa kutumika kwa shughuli, miguu yote imekusudiwa kwa mwendo, macho kwa kuona kwayo, mdomo ni kuchukua chakula ndani, tumbo ni kukiyeyusha, ini ni kusindika lishe yake kwa kusambaza kwenye sehemu mbali mbali za mwili baada ya chakula hicho kufanyizwa kuwa damu, nyongo, maji ya tezi, belghamu, tundu za mwili zimekusudiwa kuondoa uchafu mwilini na utaona kwamba kila kiungo, kimelinganishwa barabara kufanya kazi zake maalum, kimefanyizwa kwa usanii kamili." Nilisema: "Maulana! Baadhi ya watu huwamini kwamba yote haya ni matokeo ya kazi ya maumbile - kila kiungo hujitokeza na kuwepo kama na wakati kihitajiwapo na maumbile."

Yeye(a.s) akasema, "Hebu waulize kama maumbile yanayofanya kazi katika mpango mzuri namna hiyo na uzuri wa taratibu za umbo vile vile huhitaji kuwa na elimu na uwezo au ni pasipo akili na sababu, bila uwezo na bila elimu?" Kama wakikubali kwamba inahitaji kuwa na elimu na uwezo, kipi basi kinawazuia katika imani ya kuwepo muumba? Tunachosema ni kwamba vitu vyote vimeumbwa na mmoja ambaye ni Bwana wa Elimu na Uwezo. Wanasema kwamba hakuna Muumba na bado wanakubali kwamba Maumbile yamefanya hivi kwa ustadi na mpango. Kana kwamba maumbile hayo ndiyo sababu ya kuumbwa kwao, ambapo wanamkana Muumba.

Kama watasema kwamba maumbile hufanya vitu kama hivi bila ya elimu na uwezo - bila kujua inachokifanya wala bila kuwa na uwezo wakukifanya katika uhusiano pamoja na aina na usanii na ustadi ule unaendelea kuwamo katika mambo yote, inashangaza kwamba kitu kinaweza kufanywa bila ulinganifu wa uwezo wa kukifanya na bila ya elimu ya kufanya hicho kitu. Kwa hivyo ni wazi kwamba kitendo huanzia kutoka kwa Muumba mwenye kujua yote, Ambaye amepanga kama njia ya pekee katika Uumbaji wake kutokana na Ujuzi wake, ambao watu hawa huita Maumbile. Kwa maneno mengine Allah (s.w.t) Ameamuru njia ya kutengeneza kila kitu kutokana na sababu halisi na kanuni. Kama kwa mfano, mbegu huhitaji maji kuchipua hakuna mvua hakuna nafaka; mtoto anazaliwa kwa muungano na Mume na Mke, na bila mpago huu wa muungano na kukutana kwa mbegu za uzazi; hakuna mtoto awezaye kuzaliwa; maji hugeuka hewa kusababisha wingu, wingu hilo husukumwa na upepo huku na huko na kuleta mvua; hakuwezi kuwepo na mvua bila taratibu hii.

Walahidi hawa huchukulia sababu hizi na maumbile kama ndiyo Muumba haswa, wakikanusha kuwepo kwa Muumba juu ya yote haya. Hili ni kosa la dhahiri, kwa kuwa maji hayana uhai, na mpaka yapatishwe uhai na mtoaji wa uhai, vipi yatatoa nafaka? Na inawezekana vipi manii isyokuwa na akili, igeuke kuwa mtoto mchanga, ila itiwe nguvu na Mwenye Enzi zote Kuumba kichwa kutoka sehemu moja, mikono na miguu kutoka sehemu zingine, mifupa kutoka sehemu nyingine? Maumbo mengine ya uumbaji yanaweza kufikiriwa ipasavyo.

LISHE

Hebu fikiria lishe isambazwavyo katika mwili, na mpango wa kistadi uliomo ndani yake. Hebu ona kwamba kifikapo tumboni, chakula kinaratibiwa kuwa mseto wa matibabu na mseto huo unahamishiwa kwenye ini na kapilari mororo zifanyazo kimia katika kiungo hicho. Tumbo linageuzwa kuwa kama mrekebishaji kwa kuhamisha vitu kwenda kwenye ini katika hali iliyo safishwa sana, kuzuia madhara katika umbo hili laini. Kisha ini huchukuwa mseto huo wa lishe ulioingizwa ndani yake, na kwa ustadi usiofahamika huubadili kuwa damu ili kusukumwa na moyo kwenda sehemu zote za mwili kwa kutumia mishipa ya damu, katika hali kama ya mifereji ya kunyweshea ionekanavyo katika mabustani na mashamba kusambaza maji kwenda sehemu yoyote ihitajikayo kunyweshwa.

Uchafu wote na sumu hutolewa na kupelekwa kwenye viungo vilviyokusudiwa kutoa nje uchafu na sumu hizo, kama kibofu cha nyongo, utumbo, tezi za jasho za makwapa na nyonga, na kadhalika. Jauhari ya nyongo huenda kwenye kibofu cha nyongo, baadhi ya jauhari huenda kwenye bandama na unyevunyevu huenda kwenye kibofu cha mkojo. Hebu fikiria ustadi ambao umefanywa katika kuujenga mwili! Uzuri ulioje uliounganishwa kwa viungo hivi! Jinsi mishipa (ya damu na maji), utumbo na kibofu n.k. vimepangwa kukusanya uchafu wa mwili ili kwamba kuuzuia kutokana na kutawanyika mwili wote na kusababisha magonjwa na uchafu. Basi utukufu ni wake yeye ambaye ameumba viungo hivi kutokana na mpango wneye sifa na ustadi. Sifa zote ni zake Yeye, Ambaye anastahiki kwayo."

MAENDELEO YA JUMLA YA MWILI WA MWANADAMU

Nilisema. "Kunradhi Maulana! Nieleze kukua kwa mwili kidogo kidogo, hatua kwa hatua mpaka kufikia ukamilifu wake." Yeye(a.s) akasema, "Hatua ya kwanza ya kukua huku ni kijusu ndani wa mfuko wa uzazi - isiyooenekana kwa jicho na isiyofikiwa kwa mkono. Kukua kwake hutokea kwa kasi, mpaka anakamilishwa katika mwili pamoja na viungo vyote na sehemu kukamilika kwa kila jambo, moyo, ini, utumbo na sehemu zote zifanyazo kazi, mifupa, misuli, nono, mishipa ya ubungo, mishipa ya damu, mifupa laini n.k. vyote vimekuzwa kikamilifu. Anaingia ulimwengu huu, na unaona jinsi anvyoendelea kukua pamoja na viungo vyake katika uwiyano, wakati huo huo akihifadhi maumbo yake yote bila ongezeko lolote au upungufu wowote. Hakuna mtengano wowote wa sehemu, kuongezeka chochote katika nyama au kuondolewa chochote kilichozidi. Mwili huendelea kukua, huku ukihifadhi umbo lake lililoumbwa vema, mpaka kukomaa kwake, iwe muda wake wa uhai umerefushwa au kufupishwa mapema. Je, si mpango wake wa maana sana na ustadi mzuri uliosanifiwa na Msanii mweny kujua yote?"

1

HADITHI YA MUFAZZAL

UBORA WA MTU JUU YA WANYAMA

Hebu fikiria ubora wa uumbwaji wa mtu juu ya wanyama. Anasimama wima na kukaa sawa sawa kumuwezesha kushika vitu mikononi mwake, kuvipata kwa viungo vyake, kufanya kazi kwa mpango. Kama mtu angekunjwa kama wanyama, asingeweza kufanya kazi azifanyazo sasa.

HISIA TANO ZA FAHAMU

Hisia tano za fahamu ni bora zaidi, tofauti na zile za wanyama kwa maana ya hulka na ufanisi ili kwamba kumjaalia sifa maalum kwa sababu hii. Macho yamewekwa katika kichwa kana kwamba ni taa iliyowekwa juu ya nguzo kumuwezesha kuona kila kitu. Hayakuwekwa katika sehemu za chini za miguu kuilinda salama dhidi ya majeraha na ajali wakati wa kazi au mwendo, ambao ungeweza kuyadhuru na kudhoofisha ufanisi wake. Yangewekwa katikati ya sehemu ya mwili kama vile tumboni, mgongoni au kifuani, ingekuwa vigumu kuyazunguusha au kuona vitu kwa mgeuko wa haraka. Kichwa ni kivutio - sehemu bora kabisa kwa hisia hizi za fahamu, pakufaa kulinganisha na kiungo kingine chochote. Hisia hizi za fahamu ziko tano kwa idadi kujibu aina zote za vichokoo na bila kukiacha kichokoo chochote kutogundulika. Macho yamehulkiwa ili kutofautisha kati ya rangi. Rangi zingelikuwa hazina maana bila kuwa na welekevu huu wa macho, kwa vile rangi hizi zipo kwa njia ambayo kwamba vitu vyaweza kutofautishwa kutoka kimoja na kingine, au macho hayo yangepata burudani kwayo.

Masikio yamewekwa katika kichwa kutambua sauti, ambazo kwamba zisingekuwa na maana bila uwelekevu huu wa masikio. Kadhalika ni sawa na hali ya hisia nyingine za fahamu - bila welekevu wa hisia ya fahamu ya kuonja, vyakula vyote vitamu vingekuwa visivyokolea, bila hisia ya fahamu ya kugusa, hisia ya joto, baridi, ulaini, ugumu, ingekuwa sawasawa tu kana kwamba hazipo; na bila hisia ya kunusa, manukato yote yangekuwa kama kifu. Na hivyo hivyo, kama kungekuwa hakuna rangi, macho yangekuwa hayana nguvu. Bila sauti, masikio pia yasingekuepo. Hivyo hebu fikiria jinsi ilivyoamrishwa kwamba kuna uafikiano wa dhahiri baina ya kiungo cha hisia ya fahamu na hisia - kichokoo kuingiliana - kiutendaji kazi zao kiuafikiano. Hatuwezi kusikia kwa macho yetu, wala kutofautisha rangi kwa masikio yetu, wala kunusa ila kwa pua zetu, na kadhalika.

Kisha kuna vijumbe (media) viunganishavyo vilivyowekwa kati ya kiungo cha hisia na kichokoo cha hisia, ambapo bila hivyo kiunganisho (baina ya viungo) kisingewekwa. Kama kwa mfano kutokuepo nuru kuinga'risha rangi, macho hushindwa kutambua rangi na bila hewa kufanya mawimbi ya sauti, masikio yasingekuwa na uwezo wa kutambua sauti yoyote.

Basi yaweza kufichika, kutoka kwa ambaye amejaliwa na akili nzuri na mtu ambaye hutumia akili yake sawa sawa, baada ya maelezo yote haya niliyotoa kuhusu mwingiliano wa viungo vya hisia, hisia- kichokoo na vijumbe (media) viunganishavyo kukamilisha hatima hii, kwamba kazi yote hii imepangwa na kutekelezwa na mjuzi wa yote mwenye nguvu zoto Allah (s.w.t). Yawezekana utratibu huu, ustadi huu utokee to wenyewe? Vipi maumbile yenyewe yataweza kufahamu namna gani jicho au sikio liumbwe, na kazi zipi kila kimoja izifanye na kijumbe (medium) gani kitakifaa kila kimoja kama njia kwa mfungano sahihi ili kukiumba kila kimoja?

Je, ni yenye kuwazika katika maumbile yasiyo na akili, isipokuwa Msanii Mwenye nguvu zote avipangilie juu ya Msingi wa ujuzi wa Mwenye kujua yote? Hebu fikiria hali ya mtu ambaye amepofuka macho yake na hasara anayopata katika kazi zake za kila siku. Hawezi kufahamu pa kuweka mguu wake, iwapo miguu yake itaangukia katika bonde katika muinuko, wala hawezi kuona mbele, wala kutambua rangi, wala hawezi kufahamu uso wa furaha au wakuchukizwa. Hatakuwa na uwezo wa kujua penye shimo, wala kujua adui na upanga (mkononi) uliofutwa, wala hawezi kufanya kazi yoyote ya mikono kama kuandika, biashara au utengenezaji wa kipambo kidogo. Ubongo wake hudokeza njia fulani kumuwezesha kutembea huku na huku au kula chakula chake, ambapo bila hivyo angelikuwa sawa na jiwe lililotulia.

Kadhalika ni sawa nahali ya mtu mwenye kasoro katika kusikia. Hupata hasara juu ya mambo mgeni. Hana furaha ya kusema katika maongezi, wala fahamu ya kuhisi sauti ya kupendeza au mbaya. Watu wanapata tabu ya kuongeya naye, hujichukia mwenyewe. Ingawa yu hai, yuko kama aliyekufa kwa upande wa kuongea. Ingawa yupo, bado ni kama mtu aliye mbali sana asiye na habari za aina yoyote. Mtu asiye na akili ni mwenye hali mbaya sana kuliko ng'ombe, kwani hata ng'ombe hutambua mambo mengi yasio na maana kwake. Je, huoni kwamba viungo hivi, mambo haya akili hizi na kila kitu kingine kihitajiwacho kwa marekebisho yake na ambapo bila hivyo yuko katika hasara kubwa katika hali ya ukamilifu wa kuumbwa kwake, amevipatiwa ipasavyo? Je, vyote hivi vimetengenezwa bila uwiyano, owezo na elimu? Hakika sivyo! Kiumuhimu hivi ni matokeo ya Usanii halisi na mpango wa Msanii Mwenye nguvu zote."

Niliuliza, "Maulana! Vipi inakuwa kwamba baadhi ya watu wanapungukiwa katika viungo hivyo na mambo hayo na wanapatwa na hasara hizo ambazo umezieleza?" Yeye(a.s) akasema: "Ni kwa ajili ya ukumbusho kwa mtu aliyepungukiwa viungo na watu wengine hali kadhalika. Mfalme anaamrisha raia zake katika njia za namna hii, amri kama hiyo haichukiwi, bali inafurahiwa kwa hila na kusifiwa. Watu hao ambao wameumizwa hivyo watafidiwa baada ya kufariki, maadamu ni wenye shukurani kwa Allah (s.w.t) na kugeukia kwake kiukarimu hivyo kwamba shida zote walizopata kutokana na upungufu wa viungo hivyo kuonekana duni katika ulinganifu (kwa fidia walizopata). Kiasi kwamba kama baada ya kufariki watapewa nafasi ya kurudi tena kwenye shida hizo, wangeikaribisha fursa hiyo ili kupata fidia kubwa zaidi.

MAUMBO KATIKA JOZI NA KIMOJA KIMOJA

Hebu fikiria ustadi na usanii uliooanishwa katika msingi wa Uumbaji wa viungo na maumbo katika jozi au kitu kimoja. Hebu fikiria kichwa ambacho kimeumbwa ni kitu kimoja na hii si kwasababu nyingine, bali kuweka kwa kusudi fulani tu, kisiwe kimeumbwa kwa zaidi ya kitu kimoja. Kichwa cha pili ingekuwa ni ongezeko la uzito tu, usio na umuhimu kabisa, kwa kuwa kichwa kimoja hukusanya hisia zote za fahamu zihitajiwazo kwa mtu. Vichwa viwili ingekuwa na maana ye sehemu mbili za watu. Hivyo kama angetumia kimoja kuzungumzia, kingine kingekuwa hakina kazi. Kutumia vyote kwa pamoja kwa mazungumzo hayo hayo kusingekuwa na maana yoyote kwani hakuna kusudi la zaidi lipatikanalo kwayo.

Mtu angekuwa amekwazishwa mno katika shughuli zake anazopaswa kufanya, kama angaliumbwa na mkono mmoja badala ya miwili. Je, huoni kwamba fundi seremala au fundi mwashi angeshindwa kuendelea na kazi yake kama mmoja wa mikono yake umepooza? Na hata kama angejaribu kufanya kazi yake kwa mkono mmoja hawezi kuifanya kiustadi na kiufanisi kama ambavyo angefanya kwa mikono miwili.

SAUTI

Hebu fikiria sauti ya mtu na mazungumzo, na kuumbwa kwa viungo vinavyohusika na hii sauti. Kongomeo, ambalo hutoa sauti ni kama mrija ambapo ulimi, midomo na meno hutengeneza sauti kuwa herufi na maneno. Je, huoni kwamba kibogoyo hawezi kutoa sauti ya erufi ya 'S', ambaye midomo yake imekatwa hawezi kutamka 'F', ambapo ulimi mzito hauwezi kutoa sauti ya 'V'? Zumari hufanana mno nalo (hilo kongomeo). Kongomeo hufanana na Mfuko ambamo hewa hupulizwa humo, kulingana na mapafu yenye hewa. Misuli inayowezesha mapafu kutoa sauti hufanana na vidole vinavyo bonyeza hewa ya mfuko kwenda kwenye bomba. Midomo na meno ambayo hutengeneza sauti kuwa herufi na maneno hulingana na vidole katika tundu zabomba na kutoa muziki na wimbo.

Kongomeo hapa linachukuliwa kuwa sambamba na zumari kwa njia ya maelezo, ambapo kwamba kiuhakika zumari ni ala (ya muziki) iliyotengenezwa katika mfano wa kiungo cha asili, kongomeo. Viungo vya kunena vilivyo fafanuliwa hapa, yatosha kuwa mfano sahihi wa herufi. Iwayo yote, viungo hivi, matumizi mengine yamefanyizwa anwani na hivi. Kongomeo kwa mfano, limebuniwa hivyo kuingiza hewa safi kwenye mapafu kwa kusambaza kwenye damu na moyo, ambapo kama likishindwa hata kwa muda mdogo tu, ingeleta kifo.

ULIMI NA MDOMO

Ulimi umefanyizwa kutofautisha kati ya mionjo mbalimbali ya vyakula kimoja kutoka kingine, kitamu kutoka kichungu, kichungu halisi kutoka kitamu, kichungu cha chumvikutoka kitamu. Ulimi vile vile husaidia kuhisi uzuri wa maji na chakula. Meno hutafuna chakula kuwa laini vyakutosha kuyeyushwa. Vilevile huzuia midomo kubonyea ndani ya kinywa. Kibogoyo anaonekana kuwa na ndomo iliyolegea. Midomo husaidia kunyonya maji ndani, hivyo kuruhusu kiasi cha kufaa kuingia tumboni kama yahitajiwavyo, sio kuvimbiza kwa kulingana kwake na kuleta kusongwa roho katika koo, au kuacha uvimbe kwa baadhi ya vitu vya ndani kwa uwezo wa kutiririka kwake kwa nguvu. Zaidi ya hapa, midomo miwili inafanya kazi, kama mlango kuweka mdomo kufunga upendapo. Tumekueleza namna mbali mbali za matumizi yaliyofanywa na hiyo midomo na ulimi na matokeo ya faida (za kimaumbile) kutoka kwayo, kama vile chombo cha aina moja kiwezavyo kufanya miradi tofauti. Kwa mfano shoka ambayo fundi seremala anaweza kuitumia na ambayo yaweza kutumika kuchimba ardhi na kwa matumizi mengine.

MAUNGO YA KUHIFADHI

Kama ukiangalia kwenye ubongo, utaona umefunikwa katika ngozi nyembamba moja juu ya nyingine kuuhifadhi kutokana na madhara na mtikisiko. Fuvu la kichwa huuhifadhi kama kofia ya chuma dhidhi ya kuvunjwa vipande pande kwa kugonga au mshindo kwenye kichwa. Fuvu limefunikwa na nywele kama mfuniko wa manyoya ya kondoo kuulinda salama dhidhi ya joto na baridi. Nani, basi, isipokuwa Allah Mwenye Nguvu zote ameujalia ubongo na usalama huo na kifuniko, na ambaye amekifanya ni asili ya hisia za fahamu, na ambaye amefanya mipango kwa hifadhi yake ya ajabu katika kulinganisha na sehemu nyingine zote za mwili kwa sababu ya kiwango cha umuhimu wake katika uwelekevu wa mwili?

Hebu fikiria ukope, jinsi ulivyoundwa kama pazia la jicho pamoja na kope zake kama kitani, kwa kunyanyulia na kuteremshia pazia. Hebu angalia mboni ilivyowekwa kwenye tundu ikifunikwa na kivuli cha pazia na nywele. Nani ameustiri moyo ndani ya kifua na kuufunika na pazia ambalo mnaliita utando? Nani aliyepanga hifadhi yake kwa njia ya mbavu, misuli na nyama zilizosokotwa katika njia ambayo ni ya kuzuia kitu chochote kisiingie ndani yake na kusababisha mchubuko? Nani aliyezifanyiza tundu mbili katika koo, moja kwa utoaji wake wa sauti imewekwa kwa ukaribu na mapafu na niyingine inaitwa umio inaelekea kwenye tumbo kwa upitishaji wa chakula. Na ni nani aliyeyweka kilango, kimio, (kidaka tonge) juu ya tundu inayoelekea kwenye kongomeo, kuzuia chakula kuingia kwenye mapafu, ambacho kingesababisha kifo kama kama isinge dhibitiwa hivyo? Nani aliyefanya mapafu kupuliza hewa kwenye moyo pasipokuchoka bila kupumzika kuondoa sumu ambazo vinginevyo zingeuaribu?

Nani aliyetengeneza misokoto ya misuli, izuiyao mkojo na kinyesi kutoka nje, kama vigwe vya mfuko, kufunguliwa au kufungwa kwa kupenda sio kuchurizika wakati wote wenyewe, na kuwa matokeo ya udhia wa kudumu katika maisha? Kadhalika kuna mambo ambayo kadiri ingekadiria, lakini mengine ambayo mtu hana elimu nayo, yako mbali na ukadiriaji. nani amejaalia kunepa huku kwa misuli ya tumbo ambalo limeamrishwa kuyeyusha chakula cha ukakasi? Na ni nani aliyeifanya ini laini na mororo kupokea lishe iliyochujwa na katika hali ya kusfishwa sana na kufanya kazi kwa uborazaidi kuliko tumbo? Yawezekana kazi zote hizi kufanywa na yoyote isipokuwa na Mwenye Enzi yote Mwenye Nguvu zote? Unaweza ukufikiria kwamba yote haya yaweza kufanywa na maumbile mfu? Hakika sivyo! Vyote hivi ni mpango wa Mwenye nguvu zote msanii Mwenye Enzi zote, ambaye ana elimu iliyojaa na ana ukamilifu wa Enzi zote kabla ya uumbaji. Yeye ni Allah, Mjuzi wa yote Mwenye nguvu zote.

Hebu fikiria kwa nini ute mororo wa mfupa ulivyowekwa kwa hifadhi ndani ya Mirija ya mfupa - kwa ajili tu ya kuuhifadhi dhidhi ya kuharibika kwa kuathiriwa na joto la jua ambalo linge uyeyusha, au kule (kuathirika) kwa baridi ambako kungeufanya ugande, ambapo maisha yangeangamia - ute wa mfupa ni kichanganyiko muhimu cha asili kitoleacho nishati kwa mahitaji ya mwili. Na kwa nini huu mzunguko wa damu umewekwa katika mishipa ya damu, isipokuwa ni kwamba ifanye kazi ndani ya mwili na sio kutiririka nje? Kwa nini hizi kucha zimewekwa kwenye vidole isipokuwa ni kwamba ziweze kuvihifadhi dhidhi ya madhara, na kusaidia katika ufanisi mzuri, kwani bila kuwa nazo, kuwepo kwa nyama peke yake kusingemuwezesha mtu kuokota kitu kwa kufinya kutumia kalamu kwa kuandika au kuweka uzi kwenye sindano? kwa nini sikio limewekwa sehemu nyingi kama nyumba ya jela, isipokuwa ni kwamba sauti zingechukuliwa kwenda kwenye utando (ngoma ya sikio) kwa utambuzi bila madhara kwalo kwa mshindo na mgongano wa hewa?

kwa nini nyama hizizisokotwe juu ya nyonga na matako ya mtu, isipokuwa ni kwamba, asipate kutaabika kwa ugumu wa sakafu katika kukaa kama ilivyo kwa mtu mwembamba na mwenye umbo lililodhoofika, mpaka kitu kiwekwe kati yake na sakafu kupunguza ugumu, kama mto au tandiko? Nani aliyeumba taifa la kibinadamu kama mwanaume na mwanamke? Ni Yeye Ambaye ameamrisha taifa kustawi kwa njia ya muungano wa jinsia mbili au iwayo yote kudumisha wingi wa nguvu zake kwa njia wa utofautishaji wa jinsia hizo mbili. Na ni nani aliyemfanya kuwa yeye ni Mzazi wa kizazi? Kwa hakika ni Yule Ambaye alitia tumaini ndani yake. Isingekuwa shauku hii kusuka suka kifua chake, kwa nini kuwe na chagiza (hamu ya ndani) ya wao kwa wao kuungana. Tizama uzazi wa vitu vinavyoishi kati yao ambavyo havikuwekwa ulazima (wa kuzaa) kwa muungano na kijinsia, lakini huletwa kwa hatua fulani ya kukua ya uke. Havina utofautishaji wa ume na uke kabisa. Je, yawezekana mtu yoyote, kwa mfano, kueleza kati ya ume na uke wa nyigu?

Nani aliyempa yeye (mtu) viungo kwa kufanya kazi? Hakika ni yule ambaye amemfanya (kuwa) mfanya kazi. Na ni nani aliyemfanya mfanyakazi? Hakika ni yule ambaye ameuumba kuwa mhitaji kwani mtu asingelifanya kazi kama hanahaja ya kukidhi. Kama asinge kuwa na haja kukidhi njaa yake, kwa nini ajitaabishe, kwa nini ajitie katika shighuli na utendaji. Angelikuwa hana haja ya kulinda nwili wake salama dhidhi ya joto na baridi, kwa nini impase kujifundisha kushona, kutengeneza sindano,kusokota nyuzi, kufuma, ukulima wa pamba na kadhalika. Na kutowepo kwa yote haya, ni matumizi gani yangelikuwa kwa viungo vya kufanya kazi na vidole? Na ni nani aliyemuumba yeye fukara? Hakika ni Yule Ambaye ameumba kwa ajili yake hali ya ufukara. Na ni nani aliyemuumba kwa ajili yake hali ya ufkara? Hakika ni Yule Ambaye amejichukulia juu yake mwenyewe jukumu la kumpatia mahitaji.

Nani amemjaalia yeye (mtu) kuwa na akili? hakika ni Yule Ambaye amefanya malipo na adhabu kama kanuni kwa ajili yake. Asingelihitaji akili kama asingelipasika kwa malipo na adhabu. Mwenye Nguvu zote Muumba amemjalia yeye kuwa na akili ili kutofautisha kati ya jema na ovu, Akiwa ameamua juu ya malipo na adhabu kama kanuni kwa ajili yake kupata malipo kwa wema na adhabu kwa uovu. Viumbe hai ambavyo havipasiki malipo na adhabu havina hisia ya jema na ovu, wala havijui kutofautisha baina ya haramu na halali, na aina ya matendo yaliyokatazwa na yaliyo ruusiwa. Walakini hutambua mambo yahitajiwayo nao kwa ajili ya kuishi kwa jamii yao au kiupweke. Kama kwa mfano, ndege anayo lazima ya kutambua kwamba (yeye) ndege ni mawindo ya tai, na hivyo kumuona kwake tu, humfanya aruke kwa kasi, au kulungu hujua vizuri kwamba simba angemchanilia mbali, hivyo kule kumuona kwake tu, hukimbia kuokoa maisha yake.

Nani aliye mjalia kuwa na maarifa na fahamu? Hakika ni Yule Ambae amembariki yeye kwa nishati. Na ni nani aliye mbariki yeye kwa nishati? Hakika ni Yule Ambaye ameamuru uthibitisho wa kuongoza juu yake. nani anamsaidia yeye katika shughuli zote hizi ambazo kwayo mipango yake hushindwa? hakika ni yule, ambaye anastahili shukurani zetu za juu mno. hebu fikiria mambo niliyo kwisha kukuelezea. Je, yawezekana kuwepo na mpangilio na taratibu kama hizi bila ya kuwepo upangaji? Hakika sivyo! Allah Mwenye Nguvu zote yu mbali na ametukuka juu ya mambo wanayoyasema watu hawa. Iwapo ungeona ubao mmoja wa mlango ukiwa na komeo lililokazwa juu yake. Je, unaweza kufikiria kwamba limefungwa hapo bila ya kusudio lolote? Hakika utatanabahi kwamba liko pale kuunganishwa kwenye ubao mwingine kwa faida ya dhahiri. Kadhalika utaona kiumbe wa kiume kama mmoja katika jozi kimeumbwa kwa ajili ya kiumbe mwanamke kwa muungano kuendeleza taifa.

Allah (s.w.t) awaangamize wale ambao wanadai kuwa ni mafilosofa, lakini ni wadhaifu wa kuona katika kuyaendea maajabu haya ya uumbaji na hulka ambazo wamezikana katika uumbaji wa ulimwengu, usanii wa Msanii mwenye Nguvu zote na Kupenda kwa Bwana Mpangaji. Hebu tizama kwa macho ya uheshima katika fadhila kubwa ya Allah Mwenye nguvu zote katika kutulia kwa taabu baada ya kula chakula na kinywaji. Je, huu siyo uzuri wa mpango katika ujenzi wa nyumba kwamba choo chapaswa kuwa sehemu iliyotengwa kwa hii nyumba? Katika njia kama hiyo, Allah Mwenye Nguvu zote ametengeneza tundu kwa ajili ya uchafu utokao katika mwili wa mtu katika sehemu ya faragha. Siyo katika uwazi wala haikujitokeza, bali imewekwa hivyo kwa kufichika kikamilifu kwa muunganiko wa nyonga na matako na nyama zao. Wakati mtu anataka kukidhi haja na akawa katika hali ya kuchutama, tundu huruhusu uchafu kutoka. Hebu fikiria seti ya meno katika kinywa cha mtu, baadhi ni makali, ambayo huchanja na kupasua chakula. Mengine ni butu ambayo utafuna na kufunda. Kwa vile aina zote zinahitajika, amepatiwa ipasavyo.

NYWELE NA KUCHA

Hebu fikiria na tambua ustadi uliomo ndani kwa nini ni sahihi kunyolewa nywele na kucha kupunguzwa. Zinakua na kuongezeka na hivyo huhitaji kukatwa. Kwa ajili hiyo hazina hisia kuepusha maumivu kwa mtu. kama kukata hivyo kungesababisha maumivu, ima zingeachwa zikue bila mpangilio na kuwa mzigo wa kuudhi, au ingelitia maumivu katika kukatwa." Niliuliza, "Maulana! Kwa nini zisirekebishwe bila ya kutononeka kufikia kwamba kukatwa kwao kuwe lazima?" Yeye(a.s) alisema: "naam, ziko baraka zisizo na idadi za Allah Mwenye Nguvu zote kwa Viumbe vyake zifahamikazo kwao, na ambazo kama wangelizijua, wangeshukuru kwayo.

Elewa kwamba matatizo na maradhi ya mwili yanatulizwa kwa njia ya nywele hizi zitokazo nje ya vinyweleo. Vidole hupata nafuu ya maradhi yao kupitia kwenye kucha. hiindiyo sababu ukataji wa kucha kwa juma, kunyoa kichwa na kuondoa nywele zilizozidi lazima kufanywe, ili kwamba kucha na nywele ziweze kukua haraka na kutuliza maradhi na matatizo, kama sivyo, maradhi hubaki yamezuiwa mwilini kufuatiwa na maumivu na magonjwa.

Hakuna ukuaji wa nywele uanoruhusiwa kwenye sehemu za mwili ambako zingeleta madhara kwamtu. Kama nywele zingeota ndani ya macho angepofuka. kama zingeota ndani ya kinywa, je, maji na chakula visingezuiwa? kama zingeota kwenye matumbo ya viganja vya mikono, je, zisingepunguza uwezo wa hisia ya kugusa na hali hiyo isingeingilia ufanyaji sahihi wa kazi nyingi na utambuzi wa ugusaji halisi? Kuna ustadi mkubwa uliomo ndani kuweka sehemu makhsusi za mwili bila nywele. Je, maumbile yangeweza kuwa na utambuzi wa busara nzuri au mipango ya usanii huu mzuri ingeweza kuhusishwa na haya maumbile?

Msiba uwapate walahidi hawa na upumbavu wao. hii habari ya uumbaji, na tizama ilivyo kosa na madhara kwa hayawani na manyama wengine, ambao uzazi wao hutegemea ngono, wanafananishwa hivyo hivyo. Unaona kwamba miili yao yote imefunikwa na nywele, isipokuwa sehemu maalum kwa sababu hizo hizo. hivyo fikiria habari hii ya uumbaji na tizama jinsi gani njia za makosa na madhara zilivyoepukwa ambapo maadili na faida vimewekwa salama.

Wakati wafuasi hawa wa mani na wale wa namna yao walipojaribu kukana imani hii katika uumbaji wa kimadhumuni, waliona kosa la uotaji wa nywele katika kinena na makwapa. Walishindwa kufahamu kwamba kuota huko kumetokea kwa sababu ya unyevunyevu unaochuruzika kwenye sehemu hizo. nywele hizo huota pale kama vile majani yaotavyo katika sehemu ambayo maji hujikusanya. Je, huoni namna gani sehemu zinavyotayarishwa kwa kukusanya uchafu na kuuzuia? bado busara nyingine iliyomo ndani yake, ni kwamba, inaondoa udhia mmoja zaidi mtu engediriki, kuhusiana na mwili wake, na yeye ni, mbali na hayo, kwa vile ameshughulishwa na usafi wa mwili wake na uondaji wa nywele zake, kazuilika kufanya matendo ya uchoyo, ukatili, kiburi na ufedhuli, ambayo kwamba hangepata fursa ya kuyafanya.

Hebu fikiria mate katika kinywa na ona hekima iliyomo ndani yake. Yamefanyizwa hivyo ili kuhakikisha mchirizi wa kudumu kuweka unyevu katika koo na kaa la kinywa siyo kuruhusu ukavu kwayo ambao ungesababisha kifo. Bila hayo chakula kisingeweza kutafunika wala kisingemezeka. Yote haya ni wazi na kuthibitishwa kwa uchunguzi. Na elewa kwamba maji haya chimbuko lake nikutokana na chakula na yakifika ndani husaidia kazi ya nyongo.

KUFUNIKWA KWA TUMBO

Baadhi ya wabishanaji wajinga na wadai wenye akili pungufu katika filosofia, kwa sababu ya uelewaji wao wenye kasoro na elimu potofu, wamesema, "Ingelikuwa vizuri zaidi kama tumbo la mtu lingekuwa kama joho kumuwezesha daktari kulifngua apendapo, kuangalia vitu vyake vya ndani na kuingiza mkono wake ndani kwa ajili ya matibabu, na sio kama jinsi lilivyo (kuwa na ukuta wa nyama na ngozi), limefichwa ki-ajabu kwa kuonekana na macho na kufikiwa na mkono. Magonjwa ya ndani yanaweza tu sasa kupimwa kwa dalili za ugonjwa kwa uchunguzi wa mkojo, mapigo ya mishipa na kadhalika, ambapo haziko katika kosa na shaka kufikia kwamba kosa kama hilo katika uchunguzi wa mapigo ya mishipa na mkojo laweza kusababisha kifo.

Lau kama wangejua wadai hawa wajinga katika Filosofia na washindani, kwamba ingeondoa hofu yote ya ugonjwa na kifo. Basi mtu angepumbazika na maisha yake ya umilele na ya siha nzuri, ambayo yangemfanya kuwa mkaidi na mwenye majivuno. Tumbo lililo wazi lingeruhusu mchuruziko wa daima wa unyevunyevu, hivyo kuharibu kikao chake, kitanda na mavazi yake mazuri; kwa ufupi, maisha yake yote yangekuwa katika hali hizo. Tumbo, ini na moyo hufanya kazi sawasawa kutokana na joto muhimu, ambalo lingeathiriwa na hewa ya nje ipitayo kwenye tumbo lifanyiwalo matibabu, lililowazi lionekanalo na jicho na kufikiwa na mkono. Hii ingesababisha kifo. Huoni kwamba udhanifu wote juu ya asili ya kweli ya uumbaji na muundo usio na maana ni wa upuuzu?

MATAMANIO

Hebu fikiria jambo la kulisha, kupumzika na ngono, ambavyo vimeumbwa kwa ajili yake na manufaa yaliyomo ndani yao. Kila kimoja katika hivyo kinasukumiwa tamanio, ambalo husababisha hamu na msisimko kwayo. Njaa huhitaji chakula ambacho huleta uhai na nishati katika mwili na uimara wake. Usingizi huhitaji kupumzika kwa ajili ya afya ya mwili kuondoa uchovu. Kama mtu angekula chakula kwa ajili tu ya mahitaji ya mwili wake bila tamanio kutoka ndani limlazimishalo kula, inawezekana kwamba angeupa mwanya ulegevu kwa sababu ya uchovu au shinikizo, mwili wake ungedhoofika na kusababisha kifo, kama vile mtu aachavyo kunywa dawa ambayo ndiyo pekee ahitajiayo kustawisha hali yake. Na hii ingesababisha kifo chake.

Kadhalika angeacha usingizi kwa ulegevu na kwa hiyo kudhoofisha mwili wake, kama angekusudia tu kwa sababu hii ya kupumzika kwa ajili ya mwili wake na uondoshaji wa uchovu wa viungo vyake. Kama kuzaa kungekuwa ndiyo lengo pekee la muungano kwa jinsia isingekuwa yamkini kwa upande wake kuzembea, na kutokea kupungua kwa idadi ya watu na mwisho wa kukoma kwao, kwani kuna watu hawana hamu ya kuwa na Kizazi (Watoto) wala haja yoyote kwayo. Angalia, basi kwamba tendo lile lile linalohusu siha ya mtu na ustawi limetiliwa nguvu kwa tamanio lishurutishalo lililowekwa ndani yake katika asili yake likimwongoza kwayo.

STADI ZA MAUMBO YA MWILI

Na elewa kwamba umbo la mwili lina Stadi nne :

(1) Stadi ivutayo - Hii hupokea chakula na kukisukuma ndani ya tumbo.

(2) Stadi ya kuhifadhi - Hii hukihifadhi chakula kwa ajili ya kufanyiwa taratibu za kawaida juu ya chakula hicho.

(3) Stadi ya kugeuza - Hii hufanya chakula kutoa mseto wake ili kuusambaza katika mwili.

(4) Stadi ya kuondosha - Hii huondoa uchafu baada ya Stadi ya kugeuza kukamilisha kazi yake.

Hebu fikiria mrekebisho huu uliofanywa mwilini baina ya Stadi hizi nne. Hizi zimefanywa kutosheleza mahitaji ya mwili kama sehemu ya Usanii wa Mwenye Kujua Yote.

Bila Stadi ya kuvuta, angewezaje kukitumia chakula hicho ambacho ni muhimu kwa ujenzi na ustawi wa mwili wake? Bila Stadi ya kuhifadhi, vipi chakula hicho kingehifadhiwa tumboni kwa kuyeyushwa? Bila Stadi ya kugeuza, vipi chakula kingetengenezwa kupata mseto kwa kusambazwa mwilini bila usumbufu? Na bila Stadi ya kuondosha, vipi uchafu, uliotolewa na tumbo ungeweza kuondoshwa kila wakati? Je, huoni jinsi Mtukufu Mwenye Nguvu zote Allah Ameamuru na kuzipanga Stadi hizi kwa ajili ya kazi na sharti la kuleta Afya ya mwili kwa kutimiza Ufundi wake na Enzi Kuu ya Mamlaka?

Hebu ngoja tuonyeshe kwa mfano. Hebu chukulia mwili kama Ikulu ya Kifalme, pamoja na watumishi wake na jamaa wakaao humo. Wako wafanya kazi wakihusika na uendeshaji wake. Mmoja wao amepewa jukumu la kuleta vyakula kwa jamaa. Wa pili amepewa jukumu la kukihifadhi ili kiweze kuwekwa kwa kubadilishwa kuwa lishe. Wa Tatu ni mwenye kukitengeneza na kukisambaza. Wa nne kufagia uchafu ulioachwa. Mfalme wa Ikulu hiyo ni Mwenye Kujua Yote, Mwenye Nguvu zote, Mola wa Ulimwengu Wote. Ikulu ni Mwili wa Mtu, jamaa ni viungo vya mwili, ambapo Stadi Nne zile ni Wafanyakazi. Huenda, pengine, ukafikiria maelezo niliyoyatoa kuhusu Stadi hizi nne na kazi zao kama nyingi mno zisizo na umuhimu. Bado maelezo yangu hayafuati mpango wa Vitabu uliotolewa na Madaktari, wala 0mahadhi ya mazungumzo yangu hayafuati ya kwao, Watu hao wamezitaja Stadi hizi nne katika msingi wa kwamba unahitajika katika fani ya uganga kwa ajili ya kuponyesha. Tunautaja kutoka mtizamo wa hitaji lake la kuimarisha imani na matengenezo ya watu vichwa ngumu, kama yalivyo maelezo yangu machache yenye ufafanuzi mpana na mfano, kuonyesha Usanii wa Mwenye Kujua Yote.

STADI ZA SAIKOLOJIA

Fikiria juu ya Stadi zilizowekwa ndani ya nafsi ya mwanadamu na jinsi zilivyopangwa katika kuelewa, kuamua, kudhania, kuhoji, kukumbuka n.k. Ingekuwa vipi hali ya mtu kama angenyimwa Stadi ya kumbukumbu, na kwa kiasi gani mambo yake ya maisha yangevurugika - mambo yake ya kiuchumi, na biashara yake. Asingekumbuka anachowiwa na watu wengine na anachowia wengine. Maafikiano ya bei aliyofanya, alichosikia na alichosema:- Asingekumbuka aliyemfanyia tendo jema na aliyemtendea tendo ovu, na kipi kilichomnufaisha na kipi kilichomdhuru. Asingekumbuka njia aliyopita mara nyingi. Asingekumbuka kitu chochote hata kama angeendelea kujifunza Sayansi maisha yake yote, wala asingeliweza kuamua juu ya itikadi au imani, wala kuweza kulinganisha kitu kimoja na kingine kwa muafaka. Kwa kweli, angeliambuliwa nje ya utu moja kwa moja. Hebu ona faida iliyoje ya Stadi hizi kwa mtu. Ukiziacha nyingine, hebu fikiri juu ya moja na nafasi ichukuayo katika maisha yetu.

Hata fadhila kubwa zaidi ambayo kumbukumbu ni yenye usahaulifu, bila huo mtu hangepata faraja katika huzuni yoyote, wala daima hangeondokana na maudhi, wala ansigeondokana na uovu. Angeshindwa kupendezwa na chochote katika vitu vya ulimwengu huu, kwa sababu ya kumbukumbu za huzuni zenye nguvu, wala kamwe hangekubali tumaini lolote la kudhoofisha nadhari ya Mamlaka yake ya husuda ya wenye kuhusudu. Je, huoni jinsi Stadi zikinzanazo za kumbukumbu na usahaulifu zilivyoumbwa ndani ya mtu, kila moja imeamrishwa kwa lengo maalum? Na watu wale, kwa mfano wafuasi wa Mani, ambao huamini katika Waumbaji wawili tofauti wa ulimwengu wote hawawezi kwa njia yoyote kutegemewa kufikiria vitu viwili tofauti kama waumbaji wa Stadi hizi mbili tofauti, kwani stadi hizi mbili zinazo faida ambazo unaziona kutokana nazo.

Hebu fikiria ubora ambao kwamba mtu peke yake amejaaliwa na hakuna kiumbe kingine ashirikianae nao (huo ubora) - Stara. Bila hiyo (Stara), hakuna mtu ambaye angeonyesha ukarimu kwa mgeni, wala yoyote kuweza kutekeleza ahadi yake, wala haja ya mtu yoyote kuweza kutekelezwa, wala wema wowote kupatikana. Kuna Wajibati nyingi zinafanywa tu kwa Stara. Yule ambaye anaacha Stara, hakiri haki za wazazi wake, wala wajibati za ndugu wa damu, wala kuheshimu dhamana yake, wala kuepuka ufedhuli. Je, huoni jinsi yote haya yalivyo jaalia katika mtu kiukamilifu hivyo ili kumnufaisha yeye na kukamilisha mambo yake?

UZUNGUMZAJI NA UANDISHI

Fikiria baraka ya uzungumzaji ambao kwamba amejaaliwa na Allah Azza wa Jallah, ambao ni chombo cha kuelezea wazo lake la ndani (moyoni) na hisia zake kunjufu zichipukazo kutokana na fikira yake na ambao kwa huo pia huelewa maana za ndani za wengine. Bila Stadi hii angelikuwa kama wanyama wa miguu minne si wa kuweza kupeleka wazo lake mwenyewe la moyoni kwa wengine wala kuelewa maneno ya mzungumzaji. Na hivyo ndivyo ilivyo katika fani ya uandishi ambayo ni njia ya kujua habari za watu waliopita na kwa kuwafikishia wale wote waliopo kwa vizazi vijavyo. Kutokana na fani hiyo hiyo, mafanikio ya Sayansi na maandiko yanahifadhiwa katika vitabu kwa muda mrefu. Kutokana na fani hiyo hiyo, huhifadhiwa mijadala na taarifa kati ya mtu mmoja na mwingine. Bila fani hii, muda mmoja usingelijulikana kabisa kutoka mwingine; wala zisingepatikana habari zozote kutoka kwa wale walio mbali na nchi zao.

Sayansi pia zingetoweka. Taarifa juu ya uadilifu na uungwana zingelipotea na madhara makubwa katika mambo ya mwanadamu yangelitokea kama vile pia katika mafundisho ya dini na simulizi, ambayo watu huhitaji kujua na elimu hiyo ingekuwa isiyowezekana. Pengine ungefikiria kwamba, hoja hii imetimizwa na mtu kwa msaada wa kubuni kwake mwenyewe na akili zake. Hairithiwi katika maumbile ya mtu. Na hali ni hiyo hiyo katika kuzungumza na lugha, kwani hili pia ni jambo la istilahi na azimio, huamuliwa na watu kufuatana na maafikiano yao ya kuelewana katika kuzungumza. Hivyo ndiyo sababu makundi tofauti yana lugha tofauti na maandishi yao, kwa mfano, Kiarabu, Kishamo, Kiebrania, Kirumi n.k.; ambayo kila moja ni tofauti na nyingine, kila moja ikiwa imeamua juu ya istilahi zake yenyewe ya lugha na maneno.

Kwa ambaye anafanya dai kama hilo, jibu litakuwa kwamba ingawa katika mambo yote haya kupanga kwa mtu na kutenda kume changia katika lengo, bado njia ambazo kwayo kupanga kwake na kutenda kumefikiliza lengo, ni kipaji katika ukarimu wa Allah Azza Wajalla uliyomo kwayo. Iwapo asingetunukiwa mahadhi ya kuzungumza, au akili isingeliwekwa juu yake kumwongoza katika harakati hizo, asingelikuwa na uwezo wa kuzungumza, na kama asingebarikiwa kuwa na Kiganja na vidole, kamwe isingeliwezekana kwake kuandika. Na huo ni msingi uliowekwa na Mwenye Nguvu zote Muumbaji na Asili ya Maumbile ya mtu kama fadhila maalum, kwa fadhila hiyo yoyote mwenye kushukuru kwayo atapata malipo ya Mbinguni, ambayo yoyote atakaye ikanusha atapuuzwa, kwani Allah Azza Wa Jallah ni Mwenye Kujitegemea kwa ulimwengu wote.

MIPAKA YA ELIMU

Fikiria mambo ambayo kwamba elimu amejaaliwa nayo mtu na yale ambayo hakupewa elimu nayo. Amejaaliwa na Elimu kwa mambo yote haya ambayo humpelekea kwenye mema yake kwa upande wa imani hali kadhalika na maisha yake hapa duniani. Elimu ya Kiroho ya Allah Azza Wa Jallah Muumba inapatikana kwa njia za hoja na ushahidi upatikanao katika kuwepo kwa uumbaji. Na pia elimu ya mambo ya wajibu juu yake, kwa mfano, haki kwa Wanadamu wote, upendo kwa wazazi, kutekeleza dhamana, huruma kwa wanao onewa na kudhulumiwa n.k. elimu na ruhusa ambayo Mataifa yote wanayo kimaumbile ni ukweli na mambo, ima kwa kupatana nasi au dhidi yetu.

Kadhalika amepewa elimu ya vitu vile ambavyo ni vya manufaa kwa maisha yake kidunia, kwa mfano ukulima, uendelezaji wa kilimo cha bustani, ufugaji, kutoa maji kutoka kwenye visima na chemchemi, utafiti wa miti shamba kwa ajili ya matumizi ya uganga, uchimbaji wa aina mbalimbali za mawe ya thamani, uzamiaji katika bahari, mipango aina mbalimbali ya kuwinda wanyama na ndege, uvivu, viwanda, kazi na mbinu za biashara na mambo mengine ambayo yanahitaji maelezo marefu, ambamo mna utekelezaji wa mambo ya maisha ya kidunia ya mtu, uboreshaji wa mambo ya dini yake na ya ulimwengu wake. Elimu kama hiyo imefanywa ipatikane kwake kama ilivyo bora kwa faida zake.

Mambo, ambayo elimu iko nje ya uwezo wake, wala hali yake haiihitaji, hayafanuliwi kwake, kwa mfano, elimu ya ghaibu, mambo ambayo yatatokea baadae au baadhi ya mambo yaliyotokea wakati uliopita, yale yanayo fungamana kwa yaliyo ndani ya bahari na katika eneo kubwa la ulimwengu, au yaliyo katika akili za watu yaliomo katika tumbo la uzazi n.k. Watu waliodai kuwa na elimu ya hayo madai yao yalibatilishwa kufuatia matukio yao kuwa kinyume chake. Hivyo hebu angalia, kwamba elimu ya vitu aliyopewa mtu ni ya muhimu kwa mambo yake ya Kilimwengu na ya Kidini. Amezuiliwa kujua vitu visivyo vya lazima kumvuta katika ubora wake na kasoro yake katika yote haya mna uzuri wake. Hebu fikiria kwa nini mtu hakupewa elimu ya muda wa maisha yake.

Kama angejua muda wa maisha yake duniani kuwa mfupi maisha yake yote yangechukiza, kwa kujua hivi angelingojea muda wake wa kufa. Hali yake ingekuwa ya mtu ambaye mali yake yote imepotea au karibuni sana itapotea. Na angehisi umasikini wake na uhitaji. Jinsi gani angehofia katika kutazamia kuharibika kwa mali yake na ufukara wa mwisho, huzuni na uchungu ambao angeuona kwa tazamio la kifo ungekuwa mkubwa zaidi kuliko ule wa tazamio la kuharibika kwa mali yake, kwani mwenye kupoteza mali yake wakati wote hubakia na tumaini kwamba huenda atapata zaidi ya hiyo na hilo lingempatia faraja katika akili yake Kinyume chake yule ambaye amesadikishiwa mwisho wa maisha yake atakuwa amevunjika moyo zaidi.

Kama angelikuwa na muda mrefu wa kuishi, tumaini hili katika kuishi kwake kungempa tumaini lisilofaa. Angeweza kuelemezwa na anasa na ufisadi juu ya dhana kwamba angeomba toba katika siku za mwisho za maisha zilizobakia kwa anasa hizi za sasa zinazo mshughulisha. Hili ni jambo ambalo Allah (s.w.t) halitaki kutoka kwake wala halitaki kwa viumbe vyake. Iwapo unaye mtumishi ambaye anaendelea kukukosea kwa mwaka mzima, na anatumaini husamehewa dhidi ya utumishi mzuri wa siku moja au mwezi mmoja. Hakika usingeipenda na mtumishi huyu asingekuwa na sifa sawa na mtumishi mzuri ambaye daima yuko tayari kutii amri yako.

Unaweza kuleta kinzano kwa hili kwa kusema kwamba haitokei kwamba mtu hupita njia ya upotofu, kisha akatubia na toba yake ikakubaliwa. Jibu letu kwa hili ni kwamba hii hutokea tu wakati mtu ameshindwa na ashiki yake kufikia hali isiyoweza kuzuilika, lakini wakati wote hana uamuzi katika utii wake juu ya dhana kuonyesha toba baadae wakati anajiingiza katika hawaa kwa sasa Allah (s.w.t) hamsamehi nje ya Rehema Zake zisizo na mwisho (yaani anasamehewa ndani ya Rehema za Allah (s.w.t).

Lakini katika Suala la yule ambaye ameamua juu ya upotofu kiasi atakachopenda, akitegemea msamaha katia hatua ya baadae, anajaribu kwa sababu hii kumdanganya Yeye, ambaye hawezi kudanganywa, akifikiria kupata anasa zaidi za muda huu huku akitegemea kusamehewa kwa sababu ya toba yake ya baadae. Pia, kwa hali hii ya jambo hili, kwamba kwa sababu ya aina fulani ya mfumo wa maisha wa kujiingiza katika anasa huenda usingemruhusu hata nafasi kwa ajili ya toba hususan katika uzee, wakati mwili umepita kiasi kikubwa cha udhaifu umzuiao kuyatekeleza mategemeo yake. Na mwenye kutafuta visingizio katika kutoa toba yake, isingewezekana kwake katika kifo cha shambulio la ghafla na angeutoka ulimwengu bila kutubia. Angekuwa kama mdaiwa ambaye ana bidii ya kulipa madeni yake lakini huahirisha mara kwa mara mpaka kifo kumfikia mali yake huharibika na madeni yake husimama dhidi yake, kwa hiyo ni katika usawa wa mambo kwamba elimu ya muda wa kuishi mtu ifanywe ni siri kwake ili kwamba ategemee kifo kumtokea wakati wowote na katika hofu hiyo, aepuke uasi na kuchagua kufanya tendo jema.

Unaweza kuleta Kinzano nyingine kwamba ikiwa muda wake wa kuishi ni siri kwake, na daima yuko kwenye wasiwasi kuhusu kifo chake, hufanya maovu na matendo ya haramu. Majibu yetu kwa hili ni kwamba mpango uko katika kulingana na hali ijitokezayo. Kama mbali na haya yote mtu hajizuii na uovu, ni dalili ya tabia yake kupoteka na ugumu wa moyo wake. Hakuna kosa katika kupanga kama mgonjwa baada ya kujulishwa kikamilifu faida za dawa makhsusi na makosa ya mambo maalum mabaya, haitamfaa kutumia taarifa kwa kuto heshimu maelekezo ya Daktari. Daktari si wa kulaumiwa bali mgonjwa aliyekengeuka kufuata agizo la mganga.

Mbali na wasiwasi kuhusu kifo ambao anao kwa sababu ya kutokujua kwake kuhusu muda wa maisha yake, haachi kufanya maasi. Angekakamia katika fisadi na uovu sana wa dhambi zisizoelezeka, iwapo angeipata elimu kamilifu ya muda wa maisha yake na kuishi. Kwa ajili hiyo wasiwasi kuhusu kifo kwa namna yoyote ni bora kwake kuliko tumaini lake la kuishi maisha marefu. Kama kuna jamii ya watu ambao, mbali na wasiwasi wao kuhusu kifo, ni wazembefu na hawafaidiki kwa ushauri, kuna jamii nyingine hufaidika kwa ushauri, hujiepusha kutenda dhambi na badala yake kutenda mema. Huwapa wenye kuhitaji na masikini kwa kutoa Sadaka ya vitu vyao vizuri. Isingekuwa haki kuinyima jamii hii kutokana na kupata faida kwayo.

NDOTO

Hebu fikiria kdoto na ustadi wake uliomo ndani yake. Kuna ndoto zinazotokea kuwa kweli na ndoto ambazo hazitokei kuwa kweli, zote zimechanganyika. Kama ndoto zote ni za kweli watu wote wangelikuwa Mitume. Kama ndoto zote zingekuwa za urongo zingalikuwa hazina faida bali huzidi na kutokuwa na maana. Ndoto wakati mwingine ni za kweli ambazo humnufaisha katika shughuli zake za maisha chini ya mwongozo wao, au kuepusha, hasara ambayo amejulishwa kwayo. Zaidi siyo za kweli isiwe watu wakazitegemea.

KUWAPATIA WANADAMU MAHITAJI

Hebu fikiria vile vitu ambavyo unaviona viko duniani vimewekwa kukidhi mahitaji ya mwanadamu. Udongo kwa kujenga nyumba, Chuma kwa ajili ya Kiwanda, mbao kwa kujengea, mashine n.k. Jiwe kwa matumizi kama kijaa, shaba kwa ajili ya vyombo vya nyumbani, dhahabu na fedha kwa ajili ya shughuli za biashara, johori kwa ajili ya hazina, nafaka kwa ajili ya chakula, vitu vya manukato kwa ajili ya burdani, madawa kuponya ugonjwa, wanyama wa miguu minne kama wanyama wa kubeba mizigo, miti mikavu kama nishati, majivu kwa ajili ya dawa (kemikali) mchanga kwa manufaa ya ardhi na inawezekana mtu kuhesabu vitu vyote hivi ambavyo havina idadi? Unafikiri kwamba kama mtu ataingia nyumba na kuiona imewekewa mahitaji yote ya mwanadamu; nyumba nzima imejaa hazina na kila kitu kimewekwa kwa madhumuni halisi, anaweza akafikiria vitu vyote hivyo vimejipanga vyenyewe bila ya yeyote kuupanga (mpango huo)? Sasa vipi itawezekana mtu yeyote mwenye akili akadokeza kwamba ulimwengu huu na vitu vyote hviti vimejitokeza vyenyewe?

Jifunze somo kutokana na vitu ambavyo vimeumbwa kukidhi mahitaji ya mwanadamu na ustadi mkubwa uliomo ndani yao. Nafaka zimezalishwa kwa ajili yake lakini amepewa jukumu la kazi ya kuzisaga, kuukanda unga na kupika. Sufi imezalishwa kwa ajili yake ambayo lazima aichambue, kusokota nyuzi na kuzitengeneza nguo. Mti umetengenezwa kwa ajili yake lakini lazima apande mbegu, ainyweshe na kuichunga. Miti shamba imeumbwa kama madawa kwa ajili yake lakini lazima aitafute aichanganye na kuifanyiza dawa.

Kadhalika utaona vitu vyote vilivyotengenezwa na Muumba kukidhi mahitaji ya mwanadamu katika njia ambayo kwamba hakuna mpango wa mtu ungeweza kufanya kazi kwa kutoshelezea kazi yao na kutumia kwayo. Haja na hali kwa kazi hiyo imeachwa juu yake kwa faida yake. Kama Allah (s.w.t) angefanyiza vifaa vyote hivi na mtu hana la kufanya kwa njia ya mshughuliko wake, angeanza kuzunguuka juu ya ardhi katika pande zote nne na ardhi isingeweza kuvumilia udhia wake. Mtu asingekuwa na maisha ya raha kama mahitaji yake yote yangetimizwa bila juhudi na, wala asinge furahia kitu kama hicho. Huoni kwamba mgeni akaae kwa muda na mahitaji yake yote yakitekelezwa kama kawaida na mwenyeji, bila juhudi yoyote kwa upande wake kuhakikisha ulaji wake, kinywaji, malazi au kikao, anachoka kwa kukaa kwake bure na kutokushughulika. Anahitaji baadhi ya shughuli, ingekuwa vipi hali yake kama kutokushughulika kwake kungekuwa ni kwa maisha yake yote?

Hii basi imeamriwa kwa mtu kuhodhi mipaka yake kufanya shughuli zake kwa faida zake, isiwe ulegevu na kutokushughulika kukamsababishia unyong'onyevu. Zaidi ya hayo angezuiwa kutokana na kufanya kazi hizo kwa vile ziko nje ya uwezo wake, na ambazo hazina faida kwake hata kama zimekamilishwa. Elewa kwamba haja ya msingi ya mtu ni chakula na maji. Ona mpango ambao umo humo. Mtu anahitaji zaidi maji kuliko mkate, kwa sababu anaweza kuvumilia njaa kwa muda mrefu kuliko kiu. Anahitaji maji kwa kunywa, kutawadha, kufua nguo, kunywesha wanyama wa miguu minne, kunywesha mimea. Kwa hiyo maji, yametolewa kwa wingi bila kuhitaji kuya-nunua kumwokoa mtu kwa haja ya kuyatafuta.

Mkate lazima upatikane kwa juhudi na kupanga kumfanya mtu ashughulike na kazi yake na kumzuia kutokana na majivuno na kiburi na kazi zisizo na maana. Huoni kwamba mtoto katika umri wake wa mwanzo anapelekwa kwa mwalimu kwa ajili ya maelekezo kumzuilia na michezo wakati wake wote, ambayo ingempelekea yeye au Mzazi wake kwenye matatizo. Kadhalika kama mtu angewekwa bila shughuli angejitwalia majivuno na kiburi na angejiingiza katika matendo ambayo yangemdhuru vibaya sana. Mtu aliyezaliwa na kulelewa katika malezi ya anasa chini ya masharti ya ukwasi na jamaa wake wengi, ni wazi atatumbukia kwenye tabia hizo, kufafanisha hali hiyo.

KUFAFANULIWA KWA MAUMBO

Elewa kwa nini mtu mmoja hafanani na mwingine kama walivyo ndege na wanyama n.k., wakiwa wamefanana mmoja na mwingine. Unaona kundi la kulungu na kundi zima la kwale kila moja akifanana na mwingine bila tofauti kubwa kati yao, ambapo kwamba watu, kama unavyoona, wana maumbo yenye kupambanulika na hulka, kiasi kwamba hakuna watu wawili wanaofanana kwa mfumo ule ule. Sababu ni haja ya kila mmoja inatakikana atambuliwe mwenyewe kwa umbo mahsusi na sura, kwa vile wataendesha biashara miongoni mwao ambayo haiwahusu wanyama. Huoni kwamba mshahaba wa wao kwa wao miongoni mwa wanyama na ndege hakuwaletei madhara? Sivyo ilivyo kwa mtu, kwani ikiwa kwa bahati jozi ya mapacha watafanana katika umbo, watu wanahisi kuchanganyikiwa kwa kiasi kikubwa katika kushughulika nao ambacho angepasa apewe huyu kinatolewa kwa mwingine kwa makosa. Mmoja anashikiliwa pahala pa mwingine katika adhabu (au kisasi).

Hutokea hivyo katika mambo mengine hivyo hivyo kwa sababu ya mshabaha. Mshabaha wa wanadamu unaweza kuwa na madhara zaidi. Nani basi, aliyetoa ufasaha huu na ukamilifu, ambao una pumbaza mawazo? Hakika ni Yeye yule aliye umba yote haya, ambaye Rehema zake zimeenea kwa vitu vyote. Je, utamwamini mtu asemae kwamba picha iliyoko ukutani, ambayo unaiona, imejitokeza yenyewe bila msaada wa msanii? Hakika sivyo, utamcheka. Vipi basi unaweza kuamini kwama mtu anayeishi akiwa na stadi za uzungumzaji na mwendo anaweza kujitokeza na kuwepo mwenyewe, ambapo huko tayari kukubali imani hiyo kuhusu picha isiyo na uhai?.

KADIRI YA UKUAJI

Kwa nini inatokea kwamba miili ya watu haikui kuupita mpaka mahsusi mbali na ukweli kwamba wanaendelea kuishi na kula? Hii ni kwa sababu gani kama si kwa utambuzi wa ndani? Mwenye Nguvu zote Allah Ameamuru hivyo kwamba kila jamii zote za viumbe vyenye uhai vyapaswa kuwa na ukomo maalum wa kukua si ukubwa zaidi wala udogo zaidi. Vimeendelea kukua mpaka kufikia ukomo huo na kisha husimama kukua, ingawa, ulishaji unaendelea bila kusimama. Kama isingeamuriwa hivyo vingeendelea kukua mpaka miili yao ingekuwa nje ya mipaka itambuliwayo.

UCHOVU NA MAUMIVU

Kwa nini katika suala hususan la wanadamu kwamba mwendo na shughuli huleta uchovu kwao na wanaepuka kazi laini kwa sababu tu mahitaji yake kama mavazi n.k., huhitaji juhudi zaidi? Kama mtu hakupata shida na maumivu, vipi angeweza kuepuka matendo ya uovu, kusujudi mbele za Allah (s.w.t) au kuwahurumia watu? Huoni kwamba mara tu mtu anapopatwa na maumivu, basi hugeuka kumuelekea Allah (s.w.t) kwa unyenyekevu kamili, akioma mbele ya Mola wake ili arejeshewe Afya yake na kufungua mikono yake katika ukarimu? Kama mtu asingepata maumivu kwa kupigwa, vipi Serikali zingewarudi wakaidi? Vipi atoto wangefundisha Sayansi na Sanaa? Vipi watumwa wangejisalimisha kwa Mabwana zao kwa hiari? Je, hakuna onyo katika yote haya kwa Ibn Abi Al Auja na Sahaba zake ambao wanakana madhumuni, na wafuasi wa Mani ambao wanakana Ustadi ulio ndani ya Kazi na maumivu?

Iwapo Viumbe vya Kiume tu au vya Kike tu vingeumbwa katika viumbe hai, je, Jamii yao isingetoweka? Hivi ndiyo sababu ya kuhifadhi jamii zao, kwamba mchanganyiko wa viumbe vya Kiume na vya Kike umeletwa kwa viumbe katika uwiano ulio sawa. Kwa nini inakuwa kwamba wanaume na wanawake wanapofikia baleghe, ni Wanaume peke yao tu huota ndevu? Je, haiko katika kawaida na amri ya Usanii? Hii ni kwa sababu mwanaume ameumbwa kama Bwana ma Mwanamke kama Mtunzaji wa Nyumba. Mwanambe huyo ndiye msimamizi wa maslahi ya Mume na msiri wake. Mwanaume, kwa hivyo, amepewa ndevu kumpa sifa na kuonekana Bwana wa Heshima. Mwanamke anaruhusiwa urembo na uzuri badala yake kama mvuto kwa muungano. Je, huoni sifa hizi kamili kwamba uumbaji huu unapatikana kwa Usanii wa Mwenye Kguvu zote Allah?

Kila kitu kinapasika kwa kipimo halisi. Hakuna kinachotolewa ambacho hakihitajiki."

Sasa ilikuwa ni adhuhuri, Bwana wangu alinyanyuka kwa ajili ya Sala akaniambia nije kwake siku ifuatayo (kesho). Insha Allah. Nikiwa nimejawa na furaha kwa maelezo niloyo yapata, nilirudi na moyo wa shukurani kwa Allah (s.w.t) kwa ajili ya Baraka niliyopatiwa juu yangu. Nilikuwa na usiku mzuri kwa ajili ya maelekezo yenye thamani yaliyowekwa juu yangu na Bwana wangu.