Hadith Ya Mufazzal

Hadith Ya Mufazzal0%

Hadith Ya Mufazzal : Mohammed Kanju
Kundi: Vitabu mbali mbali

Hadith Ya Mufazzal

: Mohammed Kanju
Kundi:

Matembeleo: 8355
Pakua: 2348

Maelezo zaidi:

Hadith Ya Mufazzal
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 4 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 8355 / Pakua: 2348
Kiwango Kiwango Kiwango
Hadith Ya Mufazzal

Hadith Ya Mufazzal

Swahili

2

HADITHI YA MUFAZZAL

BARAZA LA PILI UFALME WA WANYAMA

UFALME WA WANYAMA

Asubuhi na mapema niliwasili kwa Bwana wangu, na baada ya kupata ruhusa ya kuingia katika vyumba vyake niliketi kwa ruhusa yake. Yeye(a.s) alianza: Sifa zote njema zamstahiki Yeye Ambaye ni Muumba wa mabadiliko ya nyakati Ambaye huleta hatua moja baada ya nyingine na hali moja baada ya nyingine ya miongo ya muda, kuwalipa wema na kuwaadhibu waovu, kwa sababu ni Mwenye Haki. Majina yake yote yametukuzwa. Baraka zake ni adhimu. Hafanyi dhuluma hata ndogo kwa viumbe wake, walakini, mtu anajifanyia udhalimu mwenyewe! Maneno ya Allah (s.w.t) mwenyewe yanathibitisha ushuhuda kwa haya:

فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾ وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ ﴿٨﴾

"Basi atakayefanya kheri (jema) uzani wa mdudu chungu atauona. Na atakayefanya uovu uzani wa mdudu chungu (pia) atauona" (Qur'an 99:7 - 8).

Kuna Aya nyingine katika Kitabu Kitukufu katika maana hii hii zikitoa kinaganaga maelezo ya mambo yote. Uwongo hauwezi kuja mbele yake wala nyuma yake. Ni kitabu kilichofunuliwa na Mwenye Nguvu zote Mwenye Kustahiki Shukurani Allah. Ni kwa maelezo haya kwamba Mtukufu Mtume(s.a.w.w) amesema kwa jambo hili kwamba: "Matendo yenu yatarudishwa kwenu. "

Imam(a.s) aliinamisha chini kichwa chake kwa muda na akasema: "Ewe Mufazzal! Mwanadamu amefadhaika na kupotea, ni kupofu, amepumbazika katika ukaidi wake, kufuatia mashetani yao na vioja. Wana macho lakini hawaoni, wana ndimi lakini ni mabubu na hawaelewi. Wana masikio lakini hawasikii. Ni wenye furaha katika ufisadi wao duni. Wanadhania wameongozwa vema. Wamepotoshwa kutoka sifa za viumbe vyenye akili. Wanakula juu ya mboga zilizonajisiwa na uchafu wa watu wachafu. Wanadhani wenyewe wako salama kutokana na msiba wa kifo cha ghafla na adhabu ya matendo. Ole! Ajali mbaya iliyoje iwapatao watu hawa !".

Hii ilinifanya mimi nitoe machozi, na Imam(a.s) alinifariji kwa kusema kwamba nimeokolewa, kwa sababu ya kuikubali iman na elimu ya kiroho,na nimepatiwa wokovu.

ULIMWENGU WA WANYAMA

Yeye(a.s) aliendelia: Sasa napenda kukuelezea kuhusu ulimwengu wa Wanyama, ili kwamba upate maelezo zaidi kuhusu (Ulimwengu) huo kama ulivyopata kuhusu mengine. Hebu fikiria umbile la mwili na mfumo wa muundo uliomo katika uumbaji wao. Siyo wagumu kama mawe, kwani wangekuwa hivyo, wasingeweza kufanya shughuli, wala siyo laini kwani kwa hali hiyo wasingeweza kuzunguusha vichwa vyao au wenyewe kusimama wima bila mhimili. Wamefanyizwa na misuli hiyo ya kupinda kama kuinama na kujikunja. Wametengenezwa kwa mifupa migumu ambayo imeshikwa kwa misuli na ambayo imefungwa pamoja kwa makano juu ya kila mfupa. Ifunikayo mifupa hii na misuli hii ni ngozi yao ambayo huenea juu ya mwili vote. Wanasesere wa miti na matambara yaliyo zunguushwa juu yao na kufungwa na vigwe na Sandarusi ya gundi ju ya umbo lote, itafafanisha jambo hili, ifanye mbao iwe kama mifupa, matambara kama misuli, vigwe kama makano no sandarusi kama ngozi.

Kama inawezekana katika hali ya viumbe vyenye uhai na mwendo kujitokeza kuwepo kwa vyenyewe, ingekuwa busara kutegemea kutokea maumbo haya yasio na uhai. Na kama haiwezekani kwa wanasesere hawa, itakuwa ni upuuzi zaidi kwa wanyama. Kisha angalia kwa uangalifu sana kwenye miili yao, imefanyizwa kwa misuli na mifupa kama ya wanadamu. Wamejaaliwa macho na masikio, ili kwamba kumuwezesha mtu kupata huduma kutoka kwao, wasingaliweza kutekeleza lengo lake (huyo mtu) kama wangekuwa vipofu au viziwi. Wamenyimwa Stadi za akili na hoja, ili kwamba wabakie ni wenye kutii kwa watu na wasije wakawa wasiotii hata kama akihusishwa na kazi nzito isiyovumilika na kuelemea.

Kinzano laweza kuletwa katika hali ya watumwa wanadamu, wenye akili na hoja, hutii mabwana zao kiunyonge japokuwa ni dhiki na kazi ngumu. Jibu kwa hili ni kwamba watu wa aina hii ni wachache kiidadi. Wengi wa watumwa ni wafanyaji kazi ngumu bila kupenda, ambapo wanyama ni watii hata katika kulemewa kuzito na wakati wa kuzunguusha kijaa n.k. hawawezi kuathirika kwa mfadhaiko kama kazi zao mahsusi zihusikavyo kwa mtu. Kama mtu angefanya kazi ya ngamia mmoja au nyumbu, watu wengi wangehitajika, na kusababisha kizuizi katika shughuli nyingine. Majukumu haya rahisi yangechukua wafanyakazi wote, bila kuacha watu wowote kando kwa ajili ya Sanaa na Taaluma. Zaidi ya hayo watu wangepatwa na uchovu wa akili. Hebu fikiria miundo ya aina tatu ya viumbe hai ifuatayo, na Sifa ambazo kwamba wamejaaliwa nazo.

(1) Mtu, akiwa ameamriwa kuwa na akili na hoja kufanya kazi hizo za ufundi kama useremala, uashi, uhunzi, kushona n.k. amejaaliwa kuwa na viganja vipana na vidole vinene kumwezesha kushika aina zote za ala zilizo muhimu kwa ajili ya taaluma hizi.

(2) Wanyama walao nyama, wakiwa wameamriwa kuishi kwa kula wanyama (nyama) wametunukiwa viganja laini na makucha yawezekanayo kufichika ndani. Ni wazuri kwa kuwinda lakini hawafai kwa kazi za sanaa za kitaaluma.

(3) Wanyama walao majani, wakiwa wameamriwa si kwa sanaa za kitaaluma wala kwa uwindaji, wametunukiwa, baadhi na kwato zilizopasuliwa kuwasaidia kutokana na ugumu wa ardhi wakati wa kulisha ambapo wengine wana kwato imara kuwawezesha kusimama sawa sawa juu ya ardhi kwa ulinganifu mzuri kama wanyama wa mizigo.

Wanyama walao nyama katika mfumo wao wa kuumbwa wana meno makali, kucha ngumu, na vinywa vipana kuwasaidia katika lishe yao kwa chakula cha mnyama kama ilivyoamriwa kwao, na wameumbwa ilivyo. Wamepewa silaha hizo na vyombo vya kazi kwa kuwafaa katika uwindaji. Kwa ulinganifu wa sawa, utaona mdomo na kucha vikiwafaa kwa kazi zao mahsusi. Kama kucha hizo wangepewa wanyama walao majani, zingekuwa mbaya zaidi kuliko manufaa kwani kamwe hawawindi wala kukamata kiwiliwili. Na wanyama walao nyama wangepewa kwato badala ya kucha wangeshindwa kupata mahitaji yao katika kukosekana vifaa vya kufaa kwa mahitaji hayo. Huoni kwamba aina zote hizi za wanyama wametunukiwa sawasawa na vitu vyenye kufaa (kwa kusudi la kila mmoja) kwa ulinganifu na haja zao, humo kwayo mna kuishi kwao.

Sasa watazame wanyama wa miguu minne na angalia jinsi wanavyowafuata Mama zao. Kamwe hawahitaji kubebwa wala kulishwa kama ilivyo kwa watoto wa kibinadamu. Hii ni kwasababu kwamba mama wa watoto hao hawana nyenzo ambazo mama wa watoto wa Kibinadamu wanazo. Wana Upendo, Huba na Elimu ya Sanaa ya Maumbile na Mikono maalum na Vidole vya kuwanyanyulia. Wamefanyizwa hivyo ili kuwasaidia katika aina zote za kazi. Utaona namna hiyo hiyo katika ndege, kwa mfano, Vifaranga vya Kuku, Kwale na jamii ya Kuku (k.v. Kanga) huanza kuokota nafaka na kwenda huku na huko mara tu vinapoanguliwa kutoka kwenye mayai. Ndege ambao vifaranga vyao ni dhaifu, bila nguvu ya kusimama, kwa mfano wale wa porini na njiwa wa nyumbani, wana mama wenye silika zaidi za kimama, ili kwamba wawaletee lishe kwenye vinywa vya vifaranga vyao waliyoiweka kwenye maumio yao.

Malisho aina hiyo huendelea mpaka vifaranga viweze kujikimu vyenyewe. Njiwa hana makinda wengi kama kuku, kuwezesha majike kuyalea kiutoshelezaji bila kuwaua kwa njaa. Hivyo kila kimoja hupata mgao wa kutosha kutoka baraka za Mwenye Nguvu zote Mwenye Kujua yote Allah (s.w.t) Hebu tizama jinsi miguu ya wanyama ilivyoumbwa katika jozi kuwawezesha kutembea kwa urahisi, ambapo ingekuwa vigumu, kama ingeliumbwa katika idadi ya witir. Mnyawa atembeaye hunyanyua mguu mmoja ambapo mwingine anautuliza juu ya ardhi. Wenye miguu miwili ananyanyua mmoja na kupata msaada juu ya mwingine. Wa miguu minne hunyanyua jozi moja na kutulia juu ya pande tofauti. Kama mnyama wa miguu minne angenyanyua jozi ya miguu katika upande mmoja, tutusa kwa jozi ya upande mwingine kungekuwa kugumu kama ambavyo ubao hauwezi kusimama juu ya miguu miwili. Mguu wa mbele wa upande wa kulia na mguu wa nyuma wa upande wa kushoto inanyanyuliwa pamoja, na kinyume chake. Kwa ajili ya mwendo thabiti.

Je, huoni kwamba punda anaendesha Kijaa kama kazi nyongeza ya ubebaji mizigo, kwa kuwa farasi anaruhusiwa pumziko na faraja kwa kulinganishwa na punda? Na ngamia anafanya kazi zaidi, ambayo haiwezi kumalizwa na idadi ya watu. Ingekuwa hali gani kama angekataa kutii amri? Husalimu Amri hata kwa mtoto aliyepo hapo! Vipi Maksai anasalimu amri kwa Bwana wake akilima Shamba na mhimili shingoni mwake? Farasi wenye asili bora hukimbia kuelekea makali ya panga na mikuki kama wafanyavyo mabwana zao wakati wa mapigano. Mtu mmoja anaweza akachunga kundi la kondoo. Kama kondoo wangetawanyika kila mmoja akaenda njia yake, vipi mtu angeweza kuwatafuta? Kadhalika, Jamii nyingine za wanyama ni zenye kufaa kwa mtu, kwa nini? Hii ni kwa sababu hawana akili yoyote, wala uwezo wowote wa kuhoji mambo. Kama wangelikua na akili, wangejitoa katika kutekeleza kazi nzuri ya mahitaji ya mtu.

Ngamia angekataa kusalimu amri, na fahali angeasi dhidi ya bwana wake, kondoo wangetawanyika na kadhalika. Kama wanyama wa kuwindwa wangekuwa na akili na hoja wangeshindana kwa ajili ya vitu vya kula na watu. Nani basi angeweza kushindana na ushauri wao wa pamoja dhidi ya watu? Je, huoni jinsi walivyozuiwa kutokana na kufanya hivyo? Wanaogopa makazi ya watu na kumkimbia mwanadamu, badala ya mwanadamu kuwaogopa wao (na kuwakimbia). Hawatoki nje wakati wa mchana kutafuta chakula, bali wakati wa usiku. Wanaogopa watu na utukufu wao wote utishao bila kupata dhara lolote au onyo kutoka kwao. Kama hii isingeamriwa hivyo, wangekuja wakirukaruka kwenye makazi ya wanadamu na kufanya maisha yao kuwa ya mashaka.

Mbwa, (akiwa) miongoni mwa hayawani, amejaaliwa tabia maalum, utii kwa bwana wake, utumishi wake kwake na ulinzi wake kwake. Huweka ulinzi wakati wa usiku wa giza, hubweka huko na huko katika nyumba akilinda usalama dhidi ya wezi. Yuko tayari kujitoa mhanga maisha yake ili kumwokoa mtu na watu wake. Huo ndio utii wake kwa bwana wake. Anaweza kujiweka na njaa na maumivu kwa ajili ya bwana wake.

Kwa nini, mbwa ameumbwa katika mfumo huu, isipokuwa tu amtumikie na kumlinda mtu, na meno yake imara, kucha madhubuti, ubwekaji wa kutisha, kwa nini? Ni kwa kuwatisha wezi na kuwazuia kukaribia mali iliyo dhaminiwa kwa ulinzi wake. Tizama katika nyuso za wanyama wa miguu minne na angalia vipi zilivyoumbwa. Utaona kwamba macho yao yamewekwa mbele, wasije wakagonga ukuta au kutumbukia shimoni. Utaona vinywa vyao vimepasuliwa chini ya pua. Kama vingekuwa kama vile vya watu wasingeweza kuokota chochote kutoka ardhini. Huoni kwamba mtu haokoti chakula chake kwa kinywa chake? Hufanya hivyo kwa mikono yake.

Huu ni ubora wa pekee kwa mtu katika mlingano na walishi wengine. Kwa kuwa wanyama wa miguu minne hawakupata mikono kama hiyo kuwawezesha kuokota majani, sehemu ya chini ya pua imepasuliwa humwezesha kuokota majani na kuyatafuna. Anasaidiwa zaidi na midomo iliyo refushwa kufikia vitu vilivyoko mbali zaidi kama vile afikiavyo vilivyo karibu zaidi. Fikiria mikia ya wanyama na faida zilizoamriwa kwayo. Ni aina fulani ya mfuniko kwa viungo vyake vya siri vya kutolea uchafu. Vilevile husaidia kufukuza inzi na mbu ambao hutua juu ya uchafu katika miili yao. Mkia yao imefanyiwa mfano wa mapanga boi ambayo kwa hiyo hufukuzia inzi na mbu. Vile vile hupata afueni kwa kupungia mikia yao daima.

Wanyama hawa husimama juu ya migu yote minne, hawana muda wa kuitembeza huku na huku, kwa hivyo, huhisi kufarijika kwa kupungia mikia yao. Kuna faida nyingine hata hivyo ambazo mawazo ya mwanadamu si yenye kuweza kuzishika na ambazo zinajulikana tu inapotokea haja, miongoni mwa faida hizi, mkia ni silaha ya zaidi sana mkononi kwa kuunyongotoa kumtoa mnyama anasapo kwenye matope. Mwengo wa mkia unaweza vile vile kutumiwa na watu kwa manufao kadhaa. Kiwiliwili cha wanyama hawa kimefanywa bapa kwa kulala juu ya miguu yote minne kurahisisha ngono kwa sababu ya hali ya sehemu zao zinazohusiana.

TEMBO

Fikiria mkonga wa tembo na ustadi mkubwa uliopo katika muundo wake. Unasaidia dhumuni la kuchukua chakula na maji kupeleka ndani tumboni, kama mkono wa mtu. Bila huo tembo hawezi kunyanyua chochote kutoka ardhini, kwa kuwa shingo yake siyo ndefu vya kutosha, ambayo angeweza kuinyoosha mbele kama wanyama wa miguu minne. Kwa kutokuwepo kwa shingo ndefu amepewa mahala pake mkonga mrefu ili kwamba aweze kuunyoosha na kukidhi haja yake. Nani aliyempa kiungo hiki kufidia kwa kutokuwepo kwa kile kilicho kosekana? Hakika, Yeye Ambaye ni Mwenye Huruma Sana juu ya Viumbe Vyake. Na hii itawezekana vipi bila kupanga Usanii kama ilivyojitokeza kwa Wataalam wapotofu na walahidi?

Kwa kinzano kwamba kwa nini hakujaaliwa kuwa na shingo sawa kama ile ya wanyama wengine, jibu ni kwamba kichwa na masikio vya tembo vikiwa ni vizito sana vingeweza kusababisha mvuto mkubwa wa nguvu, hata pia kuvunjika, hivyo kichwa chake kimeungwa moja kwa moja na mwili kukikinga dhidi ya matokeo hayo na badala yake kwa ajili hiyo mkonga umefanyizwa kushughulikia madhumuni yote hayo inayohitaji, pamoja na yale ya kulisha.

TWIGA

Hebu fikiria umbo la twiga na asili mbalimbali ya viungo vyake vifananavyo na wanyama wengine mahsusi. Kichwa chake hufanana na ile cha farasi, shingo kama ile ya ngamia, kupasuka kwato kama zile za ng'ombe, na ngozi yake kama ile ya chui. Baadhi ya watu wajinga wamedhania kwamba haya ni matokeo kutokana na muungano wa aina mbalimbali za wanyama wajao sehemu za kunyweshea, jamii moja binafsi huingia katika muungano wa ngono na jamii nyingine binafsi, na kutokea uzao wa namna hii. Na kwa hiyo unakuwa mfano wa umbo mbalimbali.

Kusema hivi ni kuudhihirisha ujinga, na ukosefu wa elimu ya kiroho ya Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t) utukufu uwe kwake. Hakuna mnyama aingiaye kwenye muungano ufanyikao kati ya farasi na ngamia jike au ngamia na ng'ombe. Muungano wa ngono unaweza kuwepo (au kutokea) tu kati ya wanyama wenye umbo linalofanana katika kuumbwa, kwa mfano farasi na punda jike hutokea (kuzaliwa) kwa nyumbu, au mbwa mwitu na mbweha hutokea (kuzaliwa) chotara. Hata hivyo, kamwe haitokei kwamba uzao wa muungano wa namna hiyo unaweza kuchukua kiungo kimoja kutoka mmoja wa mwenzi mwingine.

Twiga ana kiungo kimoja kifananacho na kile cha farasi, mwingine na kile cha ngamia ukwato wa mwingine na ule wa ng'ombe. Lakini unaona kwamba nyumbu kichwa chake, masikio yake, mgongo wake, mkia na kwato zake vi katikati baina ya vile vya punda na vya farasi, na ndivyo ulivyo mlio wake u katikati baina ya mlio wa farasi na mlio wa punda. Hoja hii yaonyesha kiutoshelezaji kwamba twiga si uzao wa muungano wa jamii inayojifanyia tu, bali ni ajabu moja ya uumbaji wa ajabu wa Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t) kuthibitisha Enzi yake Kuu.

Yapasa pia ifahamike kwamba Muumba wa jamii za Wanyama zisizo idadi Huumba viungo vyovyote vile Apendavyo ya hivyo vilivyo sawa kimoja na kingine na vile vingine ambavyo havifanani. Anaongeza katika uumbaji chochote apendacho na hukataza humo namna Apendavyo. Hii ni kwamba Enzi Yake Kuu iweze kuthibitishwa na hakuna kitu kinachoweza kumzuia katika lolote Apendalo. Kwa nini shingo yake ni ndefu na faida gani zipatikanazo kwake kutokana nayo? Faida ipo katika kumwezesha kufikia majani na matunda ya miti mirefu kwa lishe yake ambapo anaishi, anakaa, na amezaliwa na sehemu zake za kujilishia, ni misitu minene.

KIMA

Hebu fikiria uumbaji wa Kima na ufanano ambao upo kati ya viungo vyake na vile vya mtu, kichwa, mabega yote, kifua na viungo vya ndani. Zaidi ya hayo, amepewa akili na utambuzi/uwelekevu kwa sababu ya hizo huelewa ishara na maelekezo ya bwana wake. Kwa ujumla huiga matendo ya mtu kama anavyomwona. Yuko karibu sana na mtu katika ubora wake, tabia na asili ya kuumbwa. Inapasa iwe kama ni onyo kwa mtu kwamba azingatie akilini kwamba katika asili na umbo ni sawa na wanyama akifanana nao kwa ukaribu sana na kama asingepewa akili, ujuzi/utambuzi na uzungumzaji angekuwa sawa tu kama wanyama.

Kuna maongezeko kidogo katika muundo wa (kuumbwa) kima umtofautishao na mtu k.m. kinywa, mkia mrefu, nywele zifunikazo mwili mzima. Tofauti hizi, hata hivyo, zisingemzuia kuwa mwanadamu, kama angelipewa stadi za hoja, akili na uzungumzaji kama mtu. Tofauti yenyewe hasa ya mpaka baida yake na mtu, kwa hiyo, ni kwa ajili (ya kukosa) tu njia za hoja, akili na uzungumzaji.

NGOZI YA MNYAMA

Hebu fikiria Rehema za Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t) kwa wanyama hawa katika kuipa miili yao mfuniko wenye aina mbali mbali za nywele kuwalinda dhidi ya misukosuko/matatizo ya kipupwe. Na wamepewa kwato, zilizopasuliwa na zisizopasuliwa, au miguu fumba kwa kuwahifadhi. Si wenye mikono, wala viganja wala vidole kusokotea nyuzi na kufuma, na kwa hiyo mavazi yao yamefanywa ni pamoja na sehemu ya umbo la miili yao, kuwahifadhi maisha yote bila kutengeneza na kubadilisha.

Mtu, iwayo yote, ana mikono na ufundi wa kufuma nguo na kusokota nyuzi. Hutengeneza nguo na mara kwa mara huibadilisha kwa faida nyingi upande wake. Miongoni mwa hizo hujishughulisha na utengenezaji nguo zake na kwa hiyo akaepukana kutokana na shughuli (mbaya) zenye kudhuru na uvivu. Huiacha kazi yake ya kushona wakati apendapo kuwa nyumbani. Anaweza kutengeneza aina mbalimbali za mavazi kwa burdani apatayo katika kubadili kwa njia ya fahari na kadhalika. Hutayarisha soksi na viatu kwa njia ya utendaji mzuri kuhifadhi miguu yake. Vibarua, na wafanya biashara kwayo hupata riziki zao na riziki za jamaa zao. Hizi aina tofauti za nywele huwasaidia wanyama kama mavazi ambapo kwato zao na miguu - fumba kama viatu.

KUZIKA MFU

Hebu fikiria tabia hii ya asili ya wanyama, nayo ni, ufichaji wa miili ya wafu wakati inaokufa kama vile watu wanavozika maiti wao. Hakuna hata mwili mfu mmoja wa hayawani na wanyama unaoonekana. Hawako mbali sana kiasi cha kutokuonekana. Kwa ukweli idadi yao ni kubwa zaidi kuliko ile ya watu. Yatazame makundi ya kulungu, nyati, punda wa porini, mbuzi mawe na paa na pia jamii mbali mbali za wanyama na hayawani kama vile simba, nyumbu, mbwa mwitu, chui n.k., na aina aina za wadudu waishio ndani ya matumbo ya ardhi na kutembea juu take, katika majangwa na milima, na kadhalika ndege warukao kama kunguru, kwale, bata, korongo, njiwa, na ndege wa mawindo. Hakuna mizoga yao tunayoiona isipokuwa michache ambayo mwindaji huipata, kama mawindo au ile inayonyafuliwa na hayawani. Likiwa ni jambo la ukweli, wakati wanyama hawa wanapopata hisia za kukaribia kifo (kufa), ujificha katika baadhi ya sehemu za siri na kufia humo.

Zitazame sanaa ambazo mtu (mwanadamu) amejifunza kutoka wanyama hawa - mfano wake wa kwanza. Aliona kunguru wawili wakipigana. Mmoja akamuua mwingine na kisha akauzika mwili wake mfu, hivyo Kabil akajifundisha kuchimba shimo na kuzika maiti ya ndugu yake Habil. Hayo yalifanyika chini ya mwongozo wa Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.). Wanyama hawa walipewa hisia hizi kumwokoa mwanadamu (mtu) kutokana na msiba wa matatizo hayo na milipuko ya magonjwa ambayo yangeweza kuja (kutokea).

SILIKA ZA WANYAMA

Fikiria silika ambazo kwazo (wanyama) kwa desturi wamepewa na Mwenye Kguvu zote Allah kwa Rehema zake zisizo na mwisho ili kwamba asiache kiumbe chochote kunyimwa Rehema zake ingawa hii haiko chini ya Stadi za kufikiria hali ya usawa. Paa humeza nyoka lakini hanywi maji hata kama kiu yake itakavyokuwa kali namna gani, kwa kuchelea sumu inayosambaa ndani ya mwili wake ambayo kwa sababu ya maji ingemuua. Huzunguukia mapipa ya maji. Hupiga kelele kwa sababu ya ukali wa kiu lakini hagusi maji kwa kuchelea (kuogopa) kifo. Unaona kujizuia kukubwa huku ambako wanyama hawa wanako bila kujali kiu kali kwa sababu ya hofu au dhara katika hali ambayo mtu mwenye akili na busara hawesi kustahimili.

Mbweha nae, asipopata chakula kwa njia yoyote ile hujifanyia "kifo cha hadaa na kulitanua tumbo lake kuwadanganya ndege waamini kuwa kafa. Maru tuu ndege wakija kumzunguuka kwa kutaka kuunyofoa mwili uonekanao kama mzoga, huwashambulia na kufanya mlo mzito wa nyama zao. Sasa, sema, nani aliyetoa wlekevu huu kwa mbweha asiyezungumza na asiye na akili? Hakika ni Yeye Yule Ambaye amechukua juu Yake Mwenyewe Jukumu la kumlisha. Kwa vile mbweha hawezi kufanya shughuli zile ambazo hayawani wengine wanaweza, k.m. shambulio la moja kwa moja juu ya mtesi, amepewa werevu na hadaa kama njia za kujipatia riziki (maisha).

Dolfin (Samaki kama nyangumi mdogo) huhitaji ndege kama watesi. Humkamata samaki na kumuua na kumuweka ili kwamba aelee juu ya maji ambapo yeye mwenyewe akijificha chini yake akiyavuruga maji wakati wote kuufanya mwili wake ufichike. Mara tuu ndege anapomrukia ghafla yule samaki, huruka kwa ghafla juu yake na kumshikilia yule ndege. Kwa werevu huu humpata mtesi wake (riziki)."

CHATU NA WINGU

Kisha niliomba maelezo kuhusu chatu na wingu. Imam(a.s) akajibu kwamba: "Wingu ni mfano wa Malaika kumkamatia (kumshikilia) chatu wake popote atakapomwona, kama vile jiwe la sumaku linavyoshikilia chuma. Hanyanyui kichwa chake kutoka ardhini kwa sababu ya kuchelea (kuogopa) wingu hilo, isipokuwa katika (majira ya) kiangazi wakati anga ni nyeupe bila dalili ya wingu na kisha litokeapo tu (hilo wingu) mara moja hutoweka." Niliuliza, "Kwa nini wingu limefanywa mtawala wa chatu kumshililia popote litakapomwona?" Imam(a.s) akajibu,"Kumwokoa mtu (mwanadamu) kutokana na madhara yake."

SIAFU

Nilisema, "Maulana! umetoa maelezo ya ulimwengu wa wanyama kwa ukamilifu kufanya kama kifungua macho kwa kila mtu. Tafadhali hebu toa baadhi ya maelezo kuhusu Siafu na ndege". Imam(a.s) akasema: "Tizama katika taya za siafu huyu mdogo. Je, unaona kasoro yoyote ndani yao inayoathiri faida yake? Je, umetoka wapi ulinganifu huu na hadhari? Hakika ni kutokana na ustadi uleule na usanii ambao umetomika katika ujenzi wa uumbaji wote, mkubwa au mdogo. Hebu tizama siafu jinsi wanavyokusanyika pamoja kukusanya chakula kwa ajili yao. Utaona kuwa wakati siafu wengi wakiazimia kuchukua nafaka kupeleka kwenye nymba zao wanafanana na watu wengi wanaojishughulisha na kupeleka nyumbani nafaka zao .

Siafu kwa kweli huonyesha juhudi na shughuli ambazo watu hawawezi kuzifanya. Huoni jinsi wanavyosaidiana kila mmoja katika kuchukua nafaka kama watu? Wanazivunja nafaka vipande vipande zisije zikachipua na kuwa zisizo na maana kwa dhumuni lao. Kama zikipata unyevu nyevu, huzisambaza zipate kukauka. Siafu hotoboa mashimo yao sehemu zilizonyanyuka, mbali kutokana na hatari ya mafuriko. Shughuli zote hizi, iwayo yote, hazipo bila uamuzi wa hoja, wenye silika halisi, ambazo kwazo miundo yao imejaaliwa nazo, kwa ukarimu wa Mwenye Nguvu zote Allah.

BUIBUI

Hebu mtizame mdudu aitwae "Lais" (aina ya buibui) kwa kawaida huitwa simba wa inzi. Ukubwa ulioje wa werevu na ustadi na upole aliojaaliwa mao kwa utafutaji wa riziki zake. Uatona kwamba wakati ana hisia ya kufikiwa na inzi humpuuza kwa muda kujifanya kama kamba vile mwili wenyewe ni usio na uhai (umekufa). Wakati akihisi kwamba inzi hayupo katika hofu yoyote ya kukamatwa na hana habari kabisa ya kuwepo kwake (buibui) huanza kunyemelea kuielekea katika mwendo wa kunyata pole pole hatua kwa hatua mpaka amfikie karibu kiasi cha kuweza kuikamata, akiwa yu ngali ameishikilia, huikumbatia na kuizingira kwa mwili wake wote kuzuia kuponyoka kwake. Hushikilia hivyo mpaka ahisi kuwa inzi huyo ameishiwa nguvu na viungo vyake vimetulia, na hapo sasa huigeukia za kuila. Hii ndiyo njia aitumiayo kwa kuishi.

Buibui wa kawaida hutanda utando wake na kuutimia kama mtego kwa kukamatia inzi. Hukaa amejificha ndani yake. Mara tu inzi anaponaswa humrukia kumkamata na kumkata kata katika vipande. Huendelea kuishi katika njia hii. Na hali hii indivyo ilivyo kwa mbwa, simba muwinda na mtengo wa kunasia wakati wa kuwinda. Hebu angalia mdudu huyu mnyonge jinsi alivyotunukiwa na silika (akili) ya kukamatia windo lake ambalo mtu hawezi kufanya bila kutumia matengo na ala (vyombo vya kazi).

Usitoe kasoro katika kitu chochote, kwani kila kitu kina funzo (Somo) la kufundisha kama vile siafu n.k. Maana nzuri mara nyingi huelezewa kwa kitu kidogo bila kupunguza thamani yake kama vile dhahabu haipunguki thamani kama itapimwa dhidi ya (vipimo) vitu vitokanavyo na chuma.

NDEGE

Hebu fikiria umbo la mwili wa ndege kama alivyoamriwa kwamba angeruka juu angani. Ametunukiwa mwili mwepesi na kiulinganifu muundo imara. Ana miguu miwili badala ya minne, vidole vinne badala ya vitano, tundu moja kwa kutolea uchafu badala ya mbili. Ametunukiwa kifua kilichochongoka (kumuwezesha) kuruka angani kama vile mashua ilivyojengwa kupasua majini. Ana manyoya marefu magumu katika mbavu zake na mkia kumsaidia kuruka juu. Mwili wote umefunikwa na manyoya kwa kujazwa hewa ya kurukia juu angani.

Kwa kuwa imeamriwa kwake kwamba lishe yake itakuwa ya nafaka na nyama ambazo atameza bila ya kutafuna, meno yamekosekana katika umbo lake na amepewa mdomo imara kwa kutafutia chakula ambao kwa huo anaweza kuokotea chakula. Hauumizwi wakati aokotapo wala kuvunjika amegapo nyama. Kwa vile hana meno lakini hula nafaka na nyama mbichi, joto jingi hufanyizwa ndani ya tumbo lake ambalo hufanya kazi ya kupika chakula chake bila kuhitaji kutafuna. Ni kama vile mfano wa mbegu za zabihu hutoka nje ya tumbo la mtu kama zilivyo ambapo zinapikika kabisa/kikamilifu katika tumbo la ndege.

Wameumbwa hivyo kwamba watage mayai badala ya kuzaa watoto ili kwamba wasije wakapata uzito wa aina yoyote wa kuvumilia wakati wa kuruka kwa sabubu ya kilengwa katika mfuko wa uzazi kikaacho humo ili kikuzwe kikamilifu. Kila kitu katika muundo wake kimeumbwa hivyo ili kiwe cha kutosheleza kufaa kwa hali yake katika maisha. Iliamriwa pia kwamba ndege ambao ni wenye kuruka juu angani wakae kwa juma moja au juma mbili au juma tatu wakilalia mayai, kwa kutotoa vifaranga vyao. Kisha huvigeukia kwa hadhari yao yote. Analo gole kubwa la kutosha kuwaletea vifaranga vyake na chakula ambacho kwama kwa hicho pia anaweza kujilisha.

Nani aliyemuwekea majukumu kwanza ajaze gole lake kwa nafaka zilizochumwa shambani, na kisha aweke mavuno hayo katika umio la vifaranga? Kwa nini anachukua taabu yote hiyo ingawa hana stadi ya kuhoji wala hana mategemeo yoyote ambayo mtu hawazia kuhusu watoto wao - heshima, kuishi kwa jina, na urithi n.k. Hii ni shughuli ambayo huonyesha kwamba ni fadhila maalum kwa vifaranga vyake chini ya mgawo maalum wa Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t) ambao udege mwenyewe hawezi kujua, wala kuhoji juu yake. Na ni nini hicho? Ni mpango kwa ajili ya kuishi kwa taifa.

KUKU

Hebu mtizame kuku na uone jinsi alivyo na wasiwasi wa kutaga mayai na kutotoa vifaranga ingawa hana kiota chochote mahsusi wala si mayai kutoka jamii hiyo hiyo. Hupiga kidoko (mlio wa kuku mwenye vifaranga au anayetaka kutaga), hutimua manyoya yake, huacha lishe yake, isipoluwa ipewe mayai ya kulalia na kutotoa vifarange, kwa nini? Ni hivyo ili kuhifadhi taifa. Isingeamriwa hivyo kiasili, nani ambaye angeifadhili kwa hifadhi ya taifa, ingawa haina stadi ya akili au ya kuhoji? Hebu tizama kwenye umbo la yai na jauhari nyeupe na njano ndani yake. Sehemu moja ni kwa ajili ya kufanyizwa kifaranga ambapo inyingine ni ya kukipatia lishe mpaka wakati huo kitakapolitoka yai.

Hebu fikiria ustadi ulio ndani yake kwa vile umbo la kifaranga lilikuwa libebwe humo kiusalama ndani ya ganda (kaka) bila kuruhusu zahama yoyote ya nje, lishe yake imewekwa ndani yake ambayo ni ya kutosha mpaka kitoke nje. Mtu ambaye amefungwa (jela) kiusalama bila ya fikio lolote kwake huwa anapatiwa chakula cha kadiri kumtosha mpaka kuachiliwa kwake.

UMIO LA NDEGE

Hebu fikiria gole/umio la ndege na ustadi ulio ndani yake. Tumbo limekaribiwa na mrija mwembamba kuruhusu lishe kufika ndani yake kwa kiasi kidogo kidogo. Bila gole/umio nafaka ingalichukua muda kufika tumboni. Ndege katika ujuzi wake wa kuhisia hali ngumu ya baadae, hujaza gole/umio lake kwa haraka. Gole/umio lake limeumbwa katika muundo wa shanti (aina ya mkoba) iliyoangikwa mbele yake, ili kwamba ijae kwa haraka kwa chochote kile ikipatacho, kisha pole pole hukihamishia tumboni. Kuna faida nyingine katika gole/umio. Baadhi ya ndege hushughulika na kuhamisha chakula kuwapelekea watoto wao. Goleumio huwasaidia kukihamisha kwa urahisi.

MANYOYA YA NDEGE

Baadhi ya watu wa mafundisho haya ya maumbo ya asili hudai kwamba rangi kuwa mbalimbali na maumbo tofauti ya ndege vimetokana tu na mchanganyiko wa vitu vya asili na tabia katika linganifu mbalimbali. Havikutokea kuwa hivyo kutokana na Usanii wowote mahsusi. Urembo huu unaouona kwenye tausi au kwale na uzuri halisi, kama kwamba msanii fulani mwenye brashi nzuri ameitimiza sanaa ya uzuri wa picha. Utaweza vipi mchanganyiko huu usio wa akili uulete uzuri huo wenye kuonekana bila kombo yoyote?

Ikiwa vitu hivi vya sanaa vimejitokeza kuwa viumbe bila ya Msanii Mwenye Nguvu zote, ni vipi uzuri huu na mfanano ungehifadhika? Hebu tizama kwa makini katika manyoya ya ndege, utayaona kama nguo iliyofumwa na nyuzi nzuri. Unywele mmoja umesokotwa na mwingine kama vile kipande kimoja cha uzi kinavyosokotwa na kingine.

Tizama katika umbo lake. Kama unalifungua, hufunguka bila kuchanika kuruhusu kewa kujazwa ndani na kuruhusu ndege kuruka wakati apendao. Ndani ya unyoya utaona ufito madhubuti uliofunikwa na kitu kama unywele ili kwamba, kwa sababu ya umadhubuti wake huyashikilia (manyoya haya). Ufito u wazi ndani (kama mrija) ili kwamba usiwe mzigo kwa ndege huyo na kuzuia urukaji wake.

NDEGE WA MIGUU MIREFU

Je, umewahi kuona ndege wa miguu mirefu na ukadiriki kufikiria faida aliyonayo kwa miguu mirefu hiyo? Mara nyingi (ndege huyo) huonekana kiulinganifu katika maji ya kina kifupi. Utamwona kana kwamba yuko katika lindo mahali alipo akiwa amesimama juu ya miguu yake mirefu. Hufanya lindo kwa vipitavyo katika maji. Akiona kitu chochote chenye kulika pole pole hukisogelea na hudaka na kumshikilia mtesi wake. Kama miguu yake ingekuwa mifupi zaidi, tumbo lake lingegusa maji katika nyendo zake za kumnyemelea mtesi wake na pengine lingevimba na kushindwa kumkamata mtesi wake. Kwa hiyo ametunukiwa na mihimili (miguu) miwili mirefu kukidhi/kutimiza haja yake bila kikwazo.

UPATIWAJI RIZIKI

Hebu fikiria kazi nyingine za umahiri (ufundi) ambazo zimetumika katika kuumbwa kwa ndege. Unaona kila ndege mwenye kinga ya miguu mirefu amepewa shingo ndefu vilevile kumuwezesha kuokota chakula chake kutoka ardhini. Wakati mwingine hutokea kwamba mdomo mrefu unatengenezwa kufanya kazi ya shingo ndefu ikipelekea kwenye urahisi utakiwao. Je, huoni kwamba uumbaji wowote unaofikiria utauona barabara na umejaa ustadi?

Tizama kwenye mimea ambayo ndege hawa wanaitafuta nyakati za mchana. Haitokei kamwe kwamba haipatikani lakini hawaipati ikiwa imekusanyika mahali pamoja. Wanaipata kwa kuitafuta na kwenda huku na huko. Hali kama hii hujitokeza katika viumbe wengine Utukufu ni wake Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t). Ambaye amegawanya riziki na akapanga njia mbalimbali za namna ya kuisambaza.

Haikupangwa katika hali ya kwamba isifikiwe (isipatikane hiyo riziki) kwa viumbe ambavyo huihitaji wala haikupangwa, kwamba njia ya kuifikia iwe nyepesi na kwamba ipatikane bila juhudi zozote kufanyika kwani kuwa hivyo kungekuwa hakuna maana kama chakula kingelipatikana kwa wingi katika sehemu moja yoyote ile wanyama wangekuwa walafi, kamwe wasingeitoka sehemu hiyo, ingepelekea kutokuyeyushwa chakula tumboni na (kutokea) maangamizi. Watu pia, kwa sababu ya uwingi (wa riziki) wangepatwa na hali ya kuwa na kiburi na majivuno na matokeo ya misiba na matendo maovu."

NDEGE WA USIKU

Imam(a.s) aliniuliza: "Unajua kuhusu ndege kama vile bundi na popo ambao hutoka nje wakati wa usiku tu, na kuhusu vitu walavyo kama chakula chao?" Nilijibu,"Sijui." Yeye(a.s) akasema: "Chakula cha hawa ni mchanganyiko wa aina mbalimbali za wadudu waliotawanyika katika anga, k.m. mbu, nondo, wadudu walio kama nzige na buibui n.k. Siku zote wako kwenye anga, hakuna sehemu ilivyo huru bila wao kuwepo. Kama ukiwasha taa usiku juu ya paa au sehemu yoyote ya eneo la nyumba, wengi wa aina mbalimbali za wadudu hao hujikusanya kuizunguuka taa (hiyo) .

Wametokea wapi? Hakika wametokea sehemu za karibu tu. Kama mtu yoyote atasema kwamba wanatokea misituni na mashambani, atajibiwa kwa kuulizwa kwamba ni vipi wanafika upesi sana na vipi wanaweza kuiona taa iliyowashwa ndani ya nyumba iliyozunguukwa na nyumba nyingine nyingi, ambapo kusema kweli hawachukui muda mrefu kuja kuizunguuka hiyo taa. Ni wazi kutokana na hili kwamba wote hawa wametawanyika kila mahali katika anga na ndege wale wanaotoka usiku kuwakamata na kujilisha kwa hao.

Tizama vipi lishe ilivyoandaliwa kwa ajili ya ndege ambao wanatoka usiku kwa njia ya wadudu hawa, waliotawanyika katika anga. Jaribu kuelewa madhumuni ya uumbaji wa viumbe hivi vyenye uhai, isije ikawa mtu fulani akafikiria kwamba vimeumbwa bure bila faida yoyote. Popo ni kiumbe wa ajabu, yu katikati baina ya ndege na mnyama wa miguu minne, kwa kweli amejamiika zaidi kwa mnyama wa miguu minne, na masikio mawili yatokezayo, meno na nywele nzuri. Huzaa watoto wake, ambao huwalisha kwa maziwa yake. Hukojoa na kunya.

Hutembea katika misimu yote minne. Tabia hizi zote ni kinyume (tofauti) na zile za ndege. Hujitokeza nje usiku tu na kujilisha kwa wadudu waliosambaa katika anga. Baadhi (ya watu) husema hali chochote, bali huishi tu kwa hewa fufutende (vuguvugu) kama lishe. Hii siyo sahihi kwa sababu mbili, kwani kukojoa na kunya, ni vithibitisho vya matumizi ya chakula kigumu. Kisha ana meno, kama asingekuwa anakula, meno yangekuwa hayana maana, ambapo kwamba hakuna kitu katika uumbaji kisicho na maana.

huyu ana sifa zijulikanazo vizuri. Kinyesi chake kimechanganyika na vitu vingine. Umbile lake la kushangaza lenyewe ni la ajabu. Huruka huku na huko kama apendavyo kwa faida yake mwenyewe - ishara ya Ujuzi Mkuu wa Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t). Ndege afumae (kiota) hujenga kiota chake wakati mwingine katika miti. Kama akiona nyoka mkubwa anaelekea kwenye Kiota chake, hupatwa na wasiwasi. Hutafuta huku na huko njia za usalama Mara tuu anapopata mbegu yenye miba huichuma na kuitupa kutokea kwa juu kwenye mdomo uliowazi wa nyoka.

Nyoka huanza kugaragara kwa uchungu na humsukasuka mpaka kufikia kifo. Kama nisingekuelezea hivi, je, ungeweza kudhania kwamba mbegu yenye miba ingeweza kuwa na faida kama hizi, au mtu yoyote angeweza kufikiri kwamba ndege mkubwa au mdogo, angeweza kufanikisha mpango kama huo? Jifunze somo kutokana na hili. Yako mambo mengine mengi yenye faida zisizojulikana ambazo huhitaji maelezo ya matukio mapya au habari zitakiwazo kufahamika.

NYUKI

Hebu fikiria kuhusu nyuki na juhudi za pamoja za kuzalisha asali na kundi la nyuki la pande sita, na werevu mwingi wa silika uliowekwa ndani (yake). Utaona ni wa kustaajabisha mno na wa kutatanisha, wakati ukifikiria kazi zake. Utaona uzalishaji wao (wa asali) ni mkubwa kabisa na ni tumizi zuri kwa wanadamu. Na kama utamtizama fundi huyo (nyuki) utamuona hana akili, asingeweza kujitambua mwenyewe, nini la kusema kuhusi mengine. Hivyo kuna hoja iliyo wazi katika hili kwamba usahihi katika ufundi na ustadi si vyenye kutokana na nyuki (mwenyewe) bali ni (Ufundi na Ustadi) Wake Yeye Mwenye Kuweza yote, Ambaye amemuumba katika umbo hilo na akamtiisha kwa kuwahudumia wanadamu.

NZIGE

Hebu mtizame nzige alivyo mnyonge, lakini aliye imara. Hakuna yoyote awezaye kujikinga dhidi ya kundi la nzige, kama litauvamia mji. Je, hujui kwamba kama yeyote yule katika Wafalme wa ulimwengu mzima atoke na majeshi na jamaa zake kuwapiga nzige, asingeshinda? Je, hii siyo hoja yenye kudhihirisha Uwezo Mkuu wa Mwenye Ngugu zote Allah (s.w.t) kwamba (viumbe) vyenye nguvu nyingi kabisa katika uumbaji wake visingeweza kuhimili shambulio la viumbe vilivyo dhaifu kabisa katika Viumbe Vyake? Watazame jinsi wanavyoifunika ardhi yote kama mafuriko, wakizagaa juu mlimani, jangwani, uwandani na mjini, wote kwa umoja, hivyo kwamba kundi lao huzuia hata mwanga wa jua. Sasa kadiria ni miaka mingapi ingehitajika kutengeneza kundi hilo kwa mkono (wa mtu). Mwenye Nguvu zote Allah ametoa hapa hoja nyingine ya uwezo Wake Mkuu ambao hakuna kiwezacho kuupunguza na kwa huo hakuna kiwezacho kuuongeza.

SAMAKI

Hebu fikiria samaki na hili ambazo zipo chini ya mazingira iliyo amriwa kuendelea kupelekea maisha yake. Haina miguu, kwa kuwa makazi yake ni katika maji na haihitaji kutimbea (na miguu). Haina mapafu, kwa vile haiwezi kuvuta hewa. Imewekwa (iishi) chini ya uso wa maji. Badala ya miguu, imejaaliwa na mapezi madhubuti ambayo kwayo hupazua maji katika pande zote; kama vile baharia wa mashua akatavyo maji katika pande zote kwa makasia yake. Ina mfuniko wa magamba mazito yaliyounganishwa na kile lingine kama pete za koti la deraya kujilinda dhidi ya ajali.

Ina stadi kali ya kunusa, kama fidia kwa uoni dhaifu usababishwao hivyo na maji. Hunusa kitu chake kutoka kwa mbali na (hapo) hukifuatia. Ni kwa njia ipi nyingine ingeweza kutumia kufahamu asili na mahali kilipo chakula (chake)? Na, elewa vilevile, kwamba inazo tundu sehemu zote kuanzia kinywani mpaka masikioni, ambazo kwazo maji hupita na kuipa stawisho la kuburudika sawasawa kama lile linalopatikana kwa wanyama wengine kwa kuvuta kewa halisi iliyopoa ya upepo wa asubuhi.

Sasa, fikiria tabia zake za kiuzazi. Idadi ya mayai ndani ya samaki ni zaidi ya kadiri. Sababu ni kuongeza chakula kiwezekanacho kuwa kwa viumbe vingine hai kwa vile wengi zaidi katika wao wanaishi kwa kula samaki pembezoni mwa madimbwi ya maji, katikati ya mapori. Mara tu samaki apitapo, humrukia juu yake. Kwa vile samaki ni mawindo ya hayawani, ndege, watu na hata samaki wengine, mambo yamepangwa kwa namna kuiweka idadi ya samaki kuwa juu.

Hebu fikiria aina za wanyama wenye rangi mbalimbali, ma-kaka (maganda), maisha ya majini na jamii mbalimbali za samaki, kupata fununu ya ustadi mkubwa mno wa Mwenye nguvu zote Allah kwa upande mmoja na silika (maumbile) dhaifu ya elimu hii imilikiwayo na viumbe. Hawana mpaka katika idadi wala sifa zao hauziwezi hujulikana, isipokuwa kwamba asijue moja baada ya nyingine kwa fursa ziwezazo kutokea.

Kama kwa mfano "Cochineal" (vitu vyenye rangi angavu nyekundu iliyofanywa kutokana na miili iliyokauka ya aina fulani ya wadudu), rangi yake ilisomwa yote na watu, imeelezwa mbweha azururaye ufukweni mwa bahari, alimpata na kumla Halzuuni (mdudu mwenye rangi). Mdomo wake ulipatwa na rangi. Rangi hiyo iliwavutia watu ambao walianza kumtumia mdudu "Cochineal" kama rangi ya kuchovyea vitu. Viko vitu vingine vingi ambavyo tabia zao huja kujulikana kwa watu mara kwa mara."

Ilikuwa adhuhuri. Bwana wangu aliamka kwa ajili ya Sala, akiniambia nije kwake (tena) mapema asubuhi ijayo. Nilirejea nyumbani nikiwa nimefurahishwa maradufu kwa tunu ya maelekezo katika elimu niliyopata kutoka kwake. Kwa shukurani nyingi kwa Mwenye Nguvu zote Allah niliupitisha usiku huo kwa kufurahia sana.

3

HADITHI YA MUFAZZAL

BARAZA LA TATU MAZINGIRA

MAZINGIRA

Niliwasili mapema asubuhi ya siku ya tatu, na kwa kuruhusiwa, niliingia, na nilipoombwa kukaa nilikaa. Yeye(a.s) alianza, "Ewe Mufazzal! nimekuelezea kwa kina na ukamilifu zaidi kuhusu uumbaji wa mwanadamu na usanii ustaajabishao wa Mwenye Nguvu zote Allah ambao umepelekea kwenye ukamilifu wake na masomo ya kujifunza kutokana na mabadiliko kidogo ya manzili zake. Vilevile nimeshughulika na maelezo ya ulimwengu wa Wanyama. Sasa natoa maelezo yenye kuhusu anga, jua, mwezi, nyota, mbingu, mchana na usiku, kiangazi na kipupwe, pepo, kanuni za misimu minne, mvua, miamba, milima, ulimwengu wa mimea, mitende na miti ya kawaida kuonyesha kwayo ishara na masomo ya kujifundisha humo.

MBINGU

Hebu itizame rangi ya mbingu na ona jinsi Usanii ufaavyo kwa makusudio (ya mambo). Rangi hii mahsusi ni dawa ifaayo kuliko zote kwa kutia afya na nguvu ikilinganishwa na rangi nyingine zote. Hata madaktari humuelekeza mtu kuangalia kwenye rangi ya kijani au katika rangi nyingine iliyozidi katika kijani kibichi kwa ajili ya maradhi fulani ya jicho. Madaktari walio wafanisi (hodari) humuelekeza mtu mwenye udhaifu wa kuona kuangalia kwenye beseni la rangi ya kijani lililojazwa maji. Hebu tizama jinsi Mwenye Nguvu zote Allah alivyoiumba mbingu kwa rangi ya kijani ikageuzwa kuonekana nyeusi ili isije ikasababisha upungufu fulani, kwa kule kurudia rudia kuangalia. Hali hii hii ambayo watu wameigundua kitokana na kufikiri na kufanya majaribio ni hali halisi ili kwamba wale ambao wangejifunza somo kutoka humo, na wapotofu - Allah (s.w.t) awaangamize, wanapotoka.

MAWIO NA MACHWEO (YA JUA)

Hebu fikiria kuchomoza na kuchwa kwa jua katika kuingia kwa mchana na usiku. Bila kuchomoza jua, shughuli zote za ulimwengu zingesimama. Ulimwengu ungezama katika giza bila kuwepo uwezekano wa kazi au maisha (riziki). Kungekuwa hakuna raha (furaha) katika maisha bila ya athari nzuri ya mwanga wa jua. Faida za mawio ya jua ziko wazi kabisa na hazihitaji simulizi nyingi. Hebu fikiria kuchwa kwa jua. Kama lisinge tua, watu wasingepata wasaa wala pumziko lolote. Watu bila kukosa, huhitaji kupumzika na kupata faraja ili kuziponya stadi ya kuyeyusha na utumiaji mzuri wa chakula (mwilini) na kutuliza na kupumzisha mishipa ya fahamu ya mwili.

Tamaa yao, kwa kutaka kuendelea kufanya kazi (bila ya kupumzika), kungesababisha matatizo makubwa kimwili, kwani wengi wameazimia na kukakamia kwamba mpaka usiku uwafunike, hawatakuwa na faraja na pumziko, katika utafutaji wa maisha (riziki) na ulimbikizaji wa mali. Kuendelea kuwaka kwa jua daima, nako kungeipasha ardhi kwa joto kali sana na (hivyo) kurudishwa nyuma kwa maisha ya wanyama na mimea. Mwenye Nguvu zote Allah kwa ajili hiyo, ameamuru kwamba kutakuwa na vipindi vya kuwaka jua na vya giza, kama taa ambayo huwashwa na watu wa nyumbani pindi tu wanapoihitaji, na huzimishwa isipohitajika, ili kuwapa faraja na pumziko. Nuru na giza vinakinzana vyenyewe kwa vyenyewe na bado vyote vimefanywa kufaa kwa faida za uboreshaji wa ulimwengu na mtengenezo mzuri.

MISIMU MINNE YA MAJIRA YA MWAKA

Kisha hebu fikiria misimu minne ya majira ya mwaka, kwa matokeo ya upandaji juu wa jua na utelemkaji wake (kutua) na faida na mpango uliomo humo. Miti na mimea hupata mchipuko (muinuko)wa uhai ndani ya vipindi viwili muhimu vya mwenendo wa jua. Ugandaji wa mvuke katika anga husababisha kufanyika mawingu hatimae kuleta mvua. Wanyama huimarika miili yao na kupata nguvu katika msimu huu. Kuna upatikanaji wa joto muhimu la uhai katika kiangazi na vile vile pia kukua kwa vitu ambavyo hukomaa katika kipupwe, mimea hupata maua na matunda katika msimu huu. Wanyama hupata msisimko wa kufanya ngono.

Anga hupatishwa joto katika kiangazi ambalo hupelekea katika kuiva kwa matunda. Taka za mwili hukazwa. Ardhi hukauka na kufaa kwa ujenzi na shughuli nyingine. Hewa husafika wakati wa kipupwe, maradhi hupitishwa (huepushwa). Miili hupata afya. Usiku huwa mrefu zaidi na hivyo kusaidia katika kufanya majukumu fulani kwa sababu ya vipindi virefu. Hewa katika msimu huu hufaa shughuli nyingi na vile vile, ambazo zitachukua muda mrefu kusimulia.

JUA

Sasa fikiria mwendo wa jua kupitia mafungu kumi na mbili ya Zodiac (Burji) kuukamilisha mwaka na ustadi uliomo ndani yake. Hiki ni kipindi ambacho kina misimu hii minne ya majira - Kipupwe Kiangazi, Masika na Demani ("Spring") katika ukamilifu wao. Nafaka na matunda huiva katika mwendo huu wa jua katika mwaka kukidhi haja za wanadamu. Mafuatano ya nyakati hizi za mwaka ni muendelezo unaojirudia rudia Je, hujui kwamba kupita kwa jua hili katika kanda za mbinguni, kutoka ukanda wa Samaki (pisces) na mpaka kuurudia tena, hufanya mwaka mmoja? Miaka hii n.k. imeendelea kuwa kama vipimo vya kukadiria muda tangu mwanzo wa dunia katika nyakati zote zilizopita. Watu wanakadiria kwayo vipindi vya muda wa maisha, mikopo, mikataba, na mambo mengine ya biashara. Ni katika mwenendo wa jua hili kwamba mwaka hukamilika na ukadiriaji sahihi wa wakati ukaanzishwa.

Hebu tizama jinsi jua litoavyo mwanga wake katika ulimwengu na ustadi gani jua hili limeamriwa kwayo. Kama lingeangaza daima kwenye sehemu moja ya "Zodiac", bila kubadilisha sehemu yake, faida za mionzi yake isingepenya katika pande zote kwa sababu ya kuwepo milima na kuta. Kwa hiyo, limeumbwa hivyo kwamba linachomoza kutoka Mashariki katika wakati wa kabla ya adhuhuri, likitoa mwanga wake juu ya vitu vilivyoko upande wa Magharibi, huenda hivyo daima, likieneza mwanga wake kutoka upande huu kwenda upande huu mpaka kuelekea upande wa Magharibi kutoa na kutawanya mwanga wake juu ya vitu ambavyo vilishindwa kuupata wakati wa kabla ya adhuhuri, hivyo ili kutoruhusu pembe yoyote kubakia bila faida na dhumuni lililokusudia kufanya.

Kama kwa mwaka mzima au sehemu yake tu hali ingebadilika kuwa kinyume, unaweza ukafikiria msiba wa wanadamu. Kwakweli ni njia ipi wangeweza kuitumia kwa kuishi? Je, mtu hachunguzi mpango huu adhimu ambamo humo taratibu zake zingeshindwa kabisa? Zinafanya kazi kwa kujiendesha zenyewe bila kuzembea, wala hazichelewi nyuma ya muda uliowekwa kwa uendeshaji wa utaratibu wa ulimwengu huu na ustawi (wake).

MWEZI

Kuna ishara iliyofunuliwa na Mwenye Nguvu zote Allah katika uumbaji wa mwezi -kielekezo kizuri. Watu kwa ujumla wanakadiria miezi katika msingi wake, lakini mwaka haukuanzishwa kisawasawa nao. Mwendo wake haukufanyizwa mabadiliko ya msimu wala nyakati za kuchanua maua na kuiva kwa nafaka. Hii ndiyo maana hesabu ya miezi na miaka ya miezi iwakaya hutofautiana kutoka hesabu ya miezi na miaka ya jua. Mieze ya miezi iwakayo hubadilika, hivyo kwamba wakati mwingine mwizi ule ule una angukia katika majira ya Kiangazi na wakati mwingine katika kipupwe. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa miezi mingine. Kwa mfano mwezi wa Muharram unaweza ukachukua kipindi ndani ya majira ya Kiangazi wakati mwingine, (na) ndani ya majira ya msimu wa mvua kwa nyakati nyingine na ndani ya majira ya Kipupwe katika wakati mwingine. Hii huonyesha kwamba hesabu ya miezi kwa miezi iwakayo na hesabu ya miezi ya jua huendelea kubadilika na hailingani kwa kila mwingine.

Fikiria kwa nini mwezi huwaka usiku na ustadi uliomo ndani yake. Viumbe hai huhitaji ubaridi kidogo upatikanao kutokana na giza ili kupata pumziko na faraja. Kukosekana kabisa kwa mwanga na giza leusi kusingekuwa na ubora wowote, hata hivyo, bila ya uwezekano kwa kazi ya aina yoyote. Watu huhitaji kufanya kazi kidogo kwa kutaka kupata burdani la kupumzika wakati wa mchana. Inaweza ikawa kwamba kwa ajili ya ukomo (ukali) wa joto (la jua) anaweza akafanya kazi katika mwanga wa mwezi kwa mfano, kilimo, ukamuaji wa maziwa, ukataji kuni n.k.

Mwanga wa Mwezi huwasaidia watu kufanya kazi kwa kutafuta maisha yao (riziki) wakati wowote wanapopenda kufanya hivyo. Wasafiri huuona ni mvutio katika safari zao. Kuchomoza mwezi kumeamriwa kwa vipindi mbali mbali vya usiku ambao unafanywa kuwa na mwanga mdogo zaidi kuliko wa jua kwa wakati wa kipindi sawa, wasije watu wakaanza kufanya kazi katika taratibu ile ile kama wanavyofanya wakati wa mchana bila kupumzika hata kulazimisha kifo.

Katika awamu tofauti za mwezi, kutokea kwake kama mwezi mwandamo, kutoweka kwake wakati wa mausiku ya mwishoni mwishoni, kufifia kwake na kupungua na kupatwa kwake, kuna vielekezo mahsusi kwamba mabadiliko yote haya yameamriwa kwa faida ya ulimwengu na Mwenye Nguvu zote Muumba Allah (s.w.t) ambavyo vinaweza vikasaidia kama mwongozo kwa mtu yoyote apendae kuufuata mwongozo huo.

NYOTA

Hebu fikiria kuhusu nyota na nyendo zao zenye kupambanulika. Kuna baadhi miongoni mwao ambazo hazisogei kutoka maeneo yaliyokusudiwa kwa ajili yao. Ziko nyingine ambazo husogea kutoka eneo mpaka eneo na zina nyendo zao zenye kupambanulika. Kila moja katika hizo ina nyendo mbili moja kwa sababu ya taratibu ya mwendo wa ulimwengu mzima kwa muelekeo wa upande wa magharibi, na mwingine ni mwenndo wake yenyewe kwa muelekeo wa upande wa mashariki. Hii hufananishwa kwa nyendo mbili za mdudu chungu akiwa upande wa juu wa Kipande cha Kijaa. Kijaa huzunguuka kwa upande wa kulia na mdudu chungu huenda upande kinyume (kushoto). Katika hali hii mdudu chungu atakuwa na nyendo mbili - moja ni ya mwendo wake mwenyewe, mwelekeo wa mbele na mwingine usiokusudiwa, pamoja na Kijaa.

Sasa hebu ulizia kutoka watu hawa ambao hudai kwamba nyota hizi zimejitokeza kuwepo zenyewe bila ya Usanii wa Msanii Mwenye Nguvu zote, ya kwamba ni kitu gani kilichokuwa pingamizi kwa maumbo yao haya yote yawe ni yenye kusimama tu mahali pamoja au yote kuwa yenye kuzunguuka (kutembea)? Uumbaji bila Muumba huthubutu mfumo mmoja, kwa nini kutokee nyendo aina mbili tofauti juu ya mfumo mahsusi na uliopendelewa? Yote haya huonyesha wazi kabisa kwamba mwendo wa namna mbili za nyota kama unavyoendelea sasa, ni matokeo ya dhumuni halisi, Usanii na Ustadi, siyo kitu cha bure kisicho na maana kama wanavyodai Walahidi hawa wapendao vitu vya kidunia tu.

Kama Kinzano litaletwe kwamba kwa nini baadhi ya nyota zimetulia ambapo nyingine zina sogea, jibu letu litakua kwamba kama zote zingekuwa zimetulia, ishara pambanuzi ambazo zinaonyeshwa sasa na nyendo zao kutoka eneo mpaka eneo (lingine) zisingekuwepo. Siri nyingi hufahamika kwa matukio yaliyohusishwa na juu na nyota nyingine kwa sababu ya nyendo zao katika njia zao mahsusi. Faida ipatikanayo sasa katika suala la msimu wa nafaka na hata bashirio n.k. katika nyendo za nyota chache kwa sasa, isingeweza kufikiwa.

Kama zote zingekuwa na msogeo, kituo chao cha kufika kisingekuwa na doria za kuweza kutambuliwa. Mwenendo wa Sayari zisogeazo katika maeneo yao yalizopangiwa, huwezesha kupatikana taarifa muhimu, kama kadiri ya mwendo wa msafiri inavyopimwa kwa kipimo cha umbali. Kwa kutokuwepo vipimo vya maili, au hatua, kadirio la kiasi cha mwendo lingekuwa vigumu (kufanyika).

Kadhalika, kama nyota zote hizi zingekuwa na msogeo na misogeo ya matakwa tofauti wakati huo, kadirio la kiasi cha msogeo wao lisingewezekana, kwa sababu katika mahali pa kwanza zilikuwa hazina idadi kuwezekana kufanya hesabu kwa chombo chochote kile cha kufanyia hesabu au mnajimu, na pili kwa sababu ya mahali pao ziliopo - baadhi ziko upande wa mashariki, nyingine upande wa magharibi, bado nyingine ziko pande wa kasikazini na tena nyingine katikati au katika ncha (mbili za dunia) au hapa, pale na kila mahali. Maeneo yao yangekuwa vigumu kwa kweli kupangika, na tatu kwa sababu ya ugumu utakanao na nyota zote kupitia katika safu kumi na mbili. Kisha ingekuwa haiwezekani kufanya upambanuzi wa aina yoyote, na kwa sababu hii dhumuni lote la msogeo wao na kuwepo kungebatilishwa.

Kama zote zingesogea kwa kiasi cha mlingano mmoja wa usogeo, lengo lililomo lingefanywa kuonekana bila faida yoyote kwa mchanganyiko wa makundi yao (nyota). Kinzano katika hali hiyo kutoka kwa fundi mtoa makosa lingepata nafasi kwa kusema kwamba ulinganifu wa mwendo (msogeo) juu ya mfumo mmoja huonyesha kutokuwepo kwa Msanii - Muumba, kama tulivyokwisha kubalisha kwa ushahidi wa maelezo kuwepo kwa uhai wa Mwenye Nguvu zote Alah (s.w.t). Ndiyo maana ni wazi kabisa kwamba nyendo zao tambuzi, mabadiliko na mizunguuko yao ikiwa ni yenye malengo, ni kazi ya usanii na upambanuzi.

Hebu fikiria nyota ambazo hutokea vipindi fulani fulani katika mwaka na hupotea wakati wa vipindi vingine vya mwaka, kwa mfano, kilimia (Pleides), Mpini kata (Orion), jozi ya nyota za "Sirius" na "Canopus". Kama zote zingetokea kwa pamoja, hakuna hata moja ingejitokeza kuwa kama alama maalum kwa watu kuipambanua, kuijua na kupata mwongozo, kama watu wapatavyo maarifa kutokana na kupotea kwa "Orion" na "Taurus" (thaura). Kutokea huku na kupotea kwa lika kimoja katika nyakati mahsusi kuliamriwa kwa faida ya wanadamu. Kama vile nyota za kilimia ziliamriwa kutokea na kupotea katika nyakati tofauti kwa faida mahsusi za watu, kadhalika kundi la nyota la "Bear" limeamriwa kwa mandhari isiokoma kamwe isipotee, kwa vile ina jukumu lingine la kufanya, ikiwa kama boya kwa ajili ya watu kutafuta njia zao katika vijia katikati ya msitu na bahari.

Kwa vile nyota za kundi hili (la falaki) daima ziko kwenye mandhari (zinaonekana), watu huzitizama mara tu wanapohitaji kujua kijia kwa upande wowote. Mambo yote haya mbalimbali hutekeleza faida za wanadamu. Mbali na hayo, ndani yake mna mwelekezo wa wakati, kwa ajili ya kilimo, (jumla), kilimo cha bustani, usafiri katika nchi kavu na baharini. Vilevile kuna udhahiri wa mambo mengine ambayo yana rejea kwenye nyakati tofauti, kwa mfano kunyesha mvua, kuvuma kwa pepo majira ya misimu ya Kiangazi na Kipupwe. Zaidi ya hayo, watu hupata njia yao kwa msaada wao (nyota) ndani ya Safari (zao) katika nyanda zinazotisha na bahari zinazoogofya wakati wa masaa ya masiku ya giza. Juu ya hayo, kuna masomo mengi makubwa ya kujifundisha kutoka nyota hizi ambazo sama huenda mbele, baadhi hurudi nyuma katika muelekeo wa upande wa Mashariki au wa Magharibi.

Mambo ya Kimbinguni, mwezi na jua husogea kwa haraka sana, na kama yangekuwa karibu zaidi nasi na mwendo wao ungekuwa ni wa kusikiwa kiusawasawa kama ilivyo je, hufikiri kwamba macho yangekuwa kiwi kwa mng'aro wao na miali kama vile yanavyokuwa kiwi kwa miali ya radi wakati inapoanza kutoa miali moja kwa moja, ikiiwasha anga iliyoko kati ya nchi na mbingu kama moto? Mfano mwingine wa hili ni nyumba yenye dari lake lililofungwa na mishumaa mingi iwakayo ikikizunguuka kichwa kwa nyendo za kasi sana. Maho yatalazimika kupofuka na mhusika kuanguka chini kifudifudi. Hebu angalia jinsi ilivyoamriwa kwamba (jua na mwezi) vingetembea kwa kasi yao iliyopo sasa katika umbali mkubwa mno kutoka sisi ili kuuzuia uwezo wetu wa kuona dhidi ya uharibifu na ugonjwa, wakati bado zinakuwa na masafa yao ya ajabu kwa dhumuni yatakayo yahudumia.

Nyota ni zenye kung'ara tu kutoshako kutoa mwanga wakati wa ukosekanaji wa mwezi na kutuwezesha sisi kutembea huku na huko katika vimulimuli vyao. Mtu nyakati nyingine huhitaji kusafiri wakati wa usiku, na katika kukosekana kumetameta kwao, angeona ni vigumu kujisogeza katika njia yake. Hebu fikiria upole na ustadi ulioamriwa katika uumbaji huu. Giza nalo pia lilihitajika na kwa hiyo kipindi kimewekwa, na kuongezeka kwa vimuli muli, ili kutekeleza malengo tuliyokwisha yashughulikia.

ULIMWENGU

Hebu fikiria ulimwengu pamoja na jua lake, mwezi wake, nyota zake na "Zodiac"' ambazo daima zinazunguuka kwa kupasika na amri halisi na hukumu ili kuleta humo faida nyingi kwa wakazi wa ardhini, kwa mnyama wa rangirangi na falme za mimea katika mabadiliko ndani ya misimu minne ya majira, siku na mausiku, ambavyo (vyote hivi) vimeelezewa kwako. Je, mtu yeyote mwenye akili timamu anaweza kufikiri kwamba mpango huu ulioratibishwa na usanii ambao hutegemea kanuni na utaratibu wa ulimwengu unaweza kujitokeza na kuwepo hivi hivi bila ya Msanii Mwenye Kujua Yote?

Kama mtu mmoja atasema kwamba ni bahati tu ndiyo iliyosababisha hivi (ulimwengu huu kujitokeza na kuwepo), ni kwa nini hasi hasemi jambo lile lililo sawa katika uhusiano kwa gurudumu la Kiajemi ambalo analiona likizunguuka, (na) likinyweshea shamba lililooteshwa kwa miti na mboga? Anaona vipuli vyake vyote vimetengenezwa kupasika na mpango halisi, kila kipuli kimeunganishwa kwa kupatana na kingine kwa mfumo wa kutekeleza mahitaji ya vifao vyake.

Na kama akitoa maelezo kama hayo kuhusu gurudumu la Kiajemi basi maoni gani kumhusu yeye watu watamuazia kwa kuyasikia maneno yake? Hakika huyu ni asiye na akili mtu mpumbavu aliyepungukiwa na akili. Je, haoni jinsi jauhari na asili ya gurudumu la Kiajemi, ambalo lenyewe ni kufu na lisilo na akili, lingeweza kujitokeza lenyewe likiwa pakoja na ukusudiaji kamili kwa mahitaji ya shamba? Je, yawezekana kweli mtu yeyote mwenye akili timamu kulikubali hili?

Je, atalikataa hili katika suala la gurudumu la mbao la Kiajemi ukiwemo mpango na ustadi mdogo, kwamba siyo sehemu ya uhunzi iliyopangwa na kusaniwa, na bado ataweza kusema kwamba ulimwengu huu mkubwa mno na wa ajabu ambao umejaa miradi iliyo nje ya ufahamu wa mwanadamu, ukifanya kazi kwa uso wote wa dunia na vitu vyote vilivyomo ndani yake uwe umejitokeza kuwepo kwa bahati bila ya ujuzi na ustadi au kipimo? Je, mtu anazo njia au mbinu za kuonea usawa kama kitu chochote kile kinaiendea mrama mbingu, kama vile vipuli vya mbao vinapotoka nje ya taratibu (kuharibika).

MCHANA NA USIKU

Hebu fikiria uhusiano wa saa za mchana na usiku. Zimerekebishwa kwa faida ya uumbaji. Saa za mchana au za usiku hazizidi saa kumi na tano. Je, unajua kwamba kama masaa ya mchana yangerefushwa kufikia masaa mia moja au mia mbili, uhai wa wanyama na mimea ungetoweka? Kipindi hicho kirefu bila pumziko na wasaa (faraja) kingewaua hayawani, ambapo wanyama wa miguu minne wangeendelea tu kujilisha. Watu, vilevile, wangeendelea kufanya kazi tu bila kusimama na kutokezea kuhatarika kwa maisha. Uhai wa mimea ungeteketea kabisa kwa kuathiriwa na kipindi kirefu cha joto la mchana. Kadhalika, kama usiku ungerefushwa ukalingana kiusawa, jamii zote za viumbe hai vingezuilika kutembea huku na huko kutafuta lishe na matokeo ni kufa njaa. Mimea ingepoteza joto lao muhimu, kukawia na kutoweka, kama vile unavyoona ile mimea ambayo imewekwa hivyo kwa kupata mwanga mdogo tu wa jua.

JOTO NA BARIDI

Fikiria mzunguuko wa joto na baridi kuhusu ongezeko, punguko na usawa, na kutokea misimu minne ya majira ya mwaka ifuatanayo mmoja baada ya mwingine katika ulimwengu na ikishughulika kwa faida yetu. Zaidi ya hayo, miili husitawi na kutiwa afya kwayo. Hii hupelekea kwa afya zao na maisha marefu, kwani kukosekana kwa athari ya joto na baridi moja baada ya ingine kwa mawumbo yenye mwili wangeumia kwa uharibifu, mvunjiko na udhoofu.

Hizi mbili (joto na baridi), kimoja kuchukua nafasi ya kingine kidogo kidogo na pole pole. Utaona kwamba mipunguko inatoa nafasi kidogo kidogo kwa mfuatio wa muongezeko wa mwingine. Ikiwa mmoja ghafla umeingilia kati utaratibu wa mwingine. Ungepelekea kwenye madhara makubwa, kwenye ugonjwa kwa viumbe vyenye mwili kama vile mtu awezavyo kupata dhara na ugonjwa, kama kwa ghafla atajitoa kutoka ndani ya bafu yenye maji moto na kujiingiza katika sehemu ya baridi. Mwenye Nguvu Zote Allah (s.w.t) ameamuru badiliko la joto na baridi kidogo kidogo kumzuia mtu kutokana na dhara la ghafla wa badiliko.

Kama yeyote yule atadai kwamba ukidogo kidogo huu na kawio, katika mjio wa matokeo ya joto na baridi hufanya mzunguuko wa jua na mwinamo wake ukivutia sana muda wa mchana, anaweza kuulizwa kama sababu ipi kuhusu msunguuko wa jua na mwinamo wake wa kidogo kidogo ukivutia sana kawio na ukidogo kidogo. Kama atajibu kwamba ni kwa sababu ya anga za pande za Mashariki na Magharibi, anaweza kuulizwa kama kwa nini iwepo hivyo. Maswali katika kusudio hili yataendelea kurudiwa rudiwa kuulizwa mpaka alazimike kukubali umuhimu wa kuwepo Mwenye Kujua yote, Mwenye Dhumuni na Msanii.

Bila joto, matunda mabichi, machachu yaliyo magumu yasingeweza kupevuka yakawa na utamu na maji mengi yatumikayo kwa kiungo au viungo, vibichi au vikavu. Bila baridi, vikonyo visingechipua masikio ya punje kwa usaaji mwingi mno kwa utoshelezaji wa lishe na mbegu. Je huzitambui faida za joto na baridi, pamoja na sifa zao zote ni chanzo cha matatizo kwa miili vile vile? Mna fundisho kwa wale ambao wangetafakari juu ya hili na uthibitisho kwamba taratibu zote hizi ni kwa faida ya ulimwengu na, kila kimoja katika viumbe kuna faida kwayo kutokana na Usanii wa Mwenye Nguvu zote Mwenye kujua yote.

HEWA

Ngoja nikufahamishe kuhusu baraka za hewa. Je, huoni wakati inapoacha kuvuma kuna udhia ukaribiao msongo wa roho? Watu wenye afya kamili huanza kuugua wanaoumwa hudhoofika, matunda huharibika, mboga mboga huoza, maumbo ya mwili huambukizwa na nafaka huozeshwa? Hii huonyesha kwamba kuvuma kwa hewa ni kwa faida ya uumbaji wa mpango wa Mwenye Nguvu zote Mwenye Kujua yote. Tabia (sifa) nyingine ya hewa imeelezwa hapa. Sauti hufanyizwa kwa mgongano wa vitu, kimoja juu ya kingine. Inapeperushwa na hewa mpaka kuyafikia masikio. Watu wote huendelea kuongea sehemu ya kipindi cha usiku au cha mchana kuhusiana na mahitaji ya shughuli za kila siku. Kama hutuba hii ingeacha alama yake katika hewa kama ambavyo maandishi yaachavyo chapa kwenye karatasi, anga yote iizunguukayo dunia ingejazwa kwayo, na kufuatia mashaka na fadhaa. Wangehitaji badiliko katika anga - hewa. Hoja kwa ajili hii ingekuwa kubwa zaidi kuliko ile ya badiliko la karatasi, kwa kiasi kwamba hutuba ya kuongea imependekezwa zaidi kuliko maelezo ya kuandikwa.

Mwenye Nguvu zote Muumba, Utukufu ni wake, ameumba njia hii ya ajabu, ambayo huhifadhi fikira (chapa) kwa muda utoshao tu kuhudumia mahitaji ya watu wa dunia na hufanya hali nzuri itengenezwe kwa fikira mpya kupatikana nayo, ambayo ungesababisha mgongano kwayo. Kupata fundisho kutokana na baraka za upepo uliopoa uitwao hewa ni lenye kukutosha. Hii hewa ni msingi wa uhai kwa maumbo yenye miili. Husaidia kupata uhai wakati tunaivuta ndani kutoka mahali pasipoeleweka na kuiruhusu na kuhusikana na roho ndani ya mwili. Hewa hii hii ni njia au chombo kwa kupeleka mawasiliano katika mfumo wa mawimbi ya sauti kwenda sehemu za mbali. Hewa hii hii huchukua harufu nzuri kutoka sehemu hadi sehemu. Hebu angalia vipi hewa hupeperusha aina mbalimbali za manukato kwenye pua yako. Na vilevile sauti. Hewa hii hii ni chombo cha kuchukulia joto na baridi, ambavyo hupishana kimipango kwa faida ya ulimwengu.

Hewa inayovuma ni upepo ambao huondoa maradhi mengi ya mwili. Huhamisha mawingu kutoka mahali fulani mpaka mahali pengine kwa faida ya jumla kwa njia ya kuganda mvuke na kuleta mvua. Kisha huyakaza na yanatawanyika mbali. Husababisha mimea kutoa maua na matunda. Hufanya milo laini matunda kuwa na maji mengi. Hupoza maji kuwa baridi. (Hewa) Inawasha mioto na kukausha unyevunyevu. Kwa ufupi, husaidia na kuhuisha vitu vyote vya ardhini. Bila kuvuma huku kwa hewa (upepo) mboga mboga zingekauka, uhai wa wanyama ungetoweka na kila kitu kingepotea.

ARDHI

Fikiria vitu vinne vilivyopo vya asili vilivyoumbwa na Mwenye Nguvu zote Allah kukamilisha dhumuni la kuumbwa kwao kiutoshelezaji. Miongoni mwao ni ardhi na eneo lake. Je, ingetosheleza vipi kwa mahitaji ya mwanadamu kuhusu ujenzi wa nyumba, kilimo, mashamba ya majani, misitu, vichaka, miti shamba (kwa kutengenezewa dawa) na madini ya thamani, kama isingekua kubwa mno? Mtu asingependezwa na angelaumu kuhusu nyanda zisizo na miti na sehemu zenye kutisha zisizokalika na kuhoji utumikaji wake. Hizi ni sehemu za kuishi wanyama pori, (ni) makazi yao na mbuga za kujilishia.

Watu wana eneo kubwa mno la kuhamia kama wakihitajia kufanya hivyo. Sehemu nyingi za uwanda zisizokalika zimegeuzwa kuwa bustani za matunda na majumba makubwa kwa kuyafanya makazi ya kudumu ya wanadamu. Kama ardhi isingekuwa kubwa kno, watu wenweye wangejiona (wangejikuta), kama waliojengewa ukuta ndani kwa ngome nyembamba, kwani wasingeweza kutoka kwenye nyumba zao hata kama wangeshinikizwa na hali ngumu.

Tena, fikiria silika iliyopewa ardhi nayo ni kwamba imewekwa sawa vizuri mno ili kutolekeza kuwa makazi yenye kufaa kwa viumbe vyote. Mtu amewezeshwa humo kutembea huku na huko, apate pumziko na wasaa (faraja) ajihusishe katika kilimo na biashara kwa uthabiti halisi. Kama ingeelekezwa katika muinamo ingekuwa vigumu kusimamisha majengo na kufanya biashara na kazi n.k. chini ya hali hizi za matetemeko ya mara kwa mara, maisha yao yangekuwa mbali mno na yale ya kupendeza.

Hebu yaelewe haya kutokana na matetemeko ya ardhi ambayo hudumu kwa muda tu na bado watu wanaopatwa nayo huyakimbia makazi yao. Wangepataje basi pumziko na wasaa kama hali ya ardhi ingekuwa ya tetemeko wakati wote? Kama mkinzani akiuliza kwamba ni kwa nini tetemeko la ardhi hutokea, atajibiwa kwamba tetemeko la ardhi na misiba mingine kama hiyo iko katika asili ya ilani na maonyo kwa watu kuchukua hadhari dhidi ya matendo maovu.

Kadhalika matatizo ya misiba ambayo huipata miili yao na mali zao yana dhumuni lilelile kimaoni, wawe tayari kufanya matengenezo yao na uboreshaji. Kama wakiwa wema, malipo watakayopata akhera yatazidi thamani ya vitu vyote vya kidunia. Hutokea wakati mwingine kwamba kuna malipo yapatikanayo hapa hapa katika ulimwengu huu, kama malipo hayo ni yenye faida katika ujumla wa watu. Ardhi katika asili yake ni baridi na kavu, hayo ndivyo yalivyo mawe. Je, unaweza kuona kwamba kama ardhi ingepewa asili ya ukavu zaidi kidogo kuwa ngumu kama jiwe ingeweza kuzalisha mimea yoyote ambayo kwama ni tegemeo la uhai wa wanyama? Je, kilimo cha aina yoyote kingewezekana au aina yoyote ya ujenzi kuwezekana?

Je, huoni kwamba inakushikana shikana kidogo zaidi kuliko jiwe? Mgeuko wa ulaini kutokana na asili yake ni kwa ajili ya kutegemewa. Sura nyingine ya asili ya ardhi kama ilivyoamriwa na Mwenye Nguvu zote Allah; Utukufu ni Enzi Yake Kuu, ni mwinamo wake wa kidogo kidogo kutoka kaskazini kuelekea kusini. Kwa nini Mwenye Nguvu zote Allah, Utukufu uwe kwake, ameiamuru hivyo? Hakika ni kwa kuruhusu ziada ya maji baada ya kuinywesha nchi yatiririkie baharini, kama vile paa (la nyumba) limefanywa kuinama kutoka upande mmoja kuelekea mwingine kuzuia maji kujikusanya na kuruhusu upitaji wake kuwa rahisi. Nchi imefanywa kuinama kwa sababu hiyo. Kama isingekuwa hivyo, ardhi yote ingejazwa na maji yaliyosimama na kutokea kuzuiwa katika biashara na mawasiliano ya barabarani.

HEWA

Kadhalika, kama hewa isingepatikana kwa wingi mno, watu wangesongwa roho kwa sababu ya moshi na mvuke kuisongasonga. Kama anga isingekuwa kubwa mno, isingefanya kazi kama kijumbe kwa ajili ya mwanga na mawingu mazito, ambayo sasa yanajikusanya kidogo kidogo kwa kufyonza maji. Maelezo ya hii hewa yamekwisha tolewa ambayo yanapasa kutosha.

MOTO

Na hiyo ndiyo hali ya moto. Ungekuwa mwingi kama maji na hewa, ungeteketeza kila kitu katika ulimwengu, bila kuacha njia yoyote ya kuanzisha kudhibitiwa kwa moto huo, kwani, ni wenye faida kwa mtu kama ilivyo kazi. Kwa namna hiyo umetunzwa kwenye kuni. Unaweza kutumika wakati inapotokea haja. Umehifadhiwa kwa njia ya kuni. Hauruhusiwi kuzimishwa wote kabisa bali baadhi yake unahifadhiwa. Kwa namna hiyo huuhitajiki kuweka bila kikomo kwani kufanya hivyo kungeleta usumbufu sana. Wala si wa kutawanyika sana kufanya uteketeze kila kitu katika ujirani wake. Imeumbwa tu katika kipimo sawa huepusha upungufu. Una sifa nyingine, kuridhia, umekusudiwa kwa faida ya wanadamu tu. Wanyama hawana haja nao. Uchumi wa wanadamu ungeridhika vikubwa katika kukosekana kwa moto. Ama kwa wanyama wa miguu minne wao hawana matumizi nao.

Kama Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t) alivyoamuru matumizi yake (huo moto) yawe kwa ajili ya wanadamu peke yao mtu amejaaliwa kuwa na viganja na vidole ili kwamba aweze kuuwasha na atumie, wakati ambapo wanyama hawakutunukiwa na viungo hivyo. Hana hivyo, wamewezeshwa kuvumilia kwa utulivu kutokana na usumbufu wa ushari wa tumbo na kuwaokoa kutokana na matatizo ambayo mtu atayapata kwa kukosekana moto. Ngoja nikuambie sifa ndogo ya moto, ambayo ni bora sana na ya kufaa, kukuelewesha, ni taa hii ambayo watu huiwasha kupata mahitaji maalum ya usiku kama watakavyo. Bila huo maisha ya wanadamu, yangefananishwa na kuzikwa kaburini. Angewezaje mtu kusoma, kuandika, kufuma, kushona kwa mashine au kushona kwa mkono katika giza la usiku? Nini ingekua taabu ya mtu anayeumwa kutokana na maumivu ya ugonywa akihitajia kutaka kuweka dawa ya kusugua au kunyunyizia daw ya uvumbi kama uganga uponyao?

MAJI

Kama maji haya yasingekuwa mengi mno yakitiririka kutoka kwenye chemchem, mabonde na mifereji, yangesababisha udhia mkubwa mno kwa watu, ambao huyahitajia wenyewe, kunywesha wanyama wao wa miguu minne na hayawani, kwa kilimo chao, mimea yao na mashamba yao ya nafaka. Na wakati huo huo wanyama wakali, ndege na hayawani au samaki na viumbe hai vyenye asili ya nchi kavu na majini vinavyoishi majini vingeumia kiasi kikubwa mno. Mbali na hayo, yana faida nyingine ambazo una habari nazo, lakini thamani kubwa sana na sifa kwayo wewe huzijui. Kisha hebu ona, mbali na faida za jumla na zenye thamani zilizomo kwayo, kukubali ukweli, uhai wote wa hayawani na mimea katika uso wote wa ardhi una asili katika maji, yanatumika katika taratibu nyingine za vinywaji kuvifanya mororo kwa ladha ya kupendeza. Hutumika kuondoa uchafu mwilini hali kadhalika na kufulia nguo. Udongo huloweshwa kwayo kuufanya ufae kwa kutengezea vyombo vya nyumbani n.k. yanatumika kuzimishia moto kama utawaka kusababisha madhara. Mtu hupata kuburudika baada ya uchovu na utumishi. Vili vile kuna vitu vingine vihudumiwavyo na maji, ubora mkubwa na thamani iliyomo humo huweza kujulikana tu wakati wa kuhitajika.

Pamoja na kuhusu haya yote, unatia shaka juu ya thamani ya wingi huu wa maji yatiririkayo katika mito na bahari, basi elewa kwamba maji haya haya ni makazi ya uhai kwa jamii nyingi ya wanyama waishio majini na samaki. Hii ni nyumba ya hazina ya lulu, rubi, mawe njano na vitu aina mbalimbali ya vito vya thamani ambavyo hutolewa kutoka katika mito na bahari. Sehemu zinazozunguuka hifadhi za maji hukutwa kukiwa na harufu nzuri za "aloes". Miti pamoja na harufu nzuri ya vitu vya rangi rangi na miti shamba (itengenezwayo dawa).

Zaidi ya hayo, ni njia ya usafirishaji. Ni njia itumikayo kwa kubadilishana biashara kati ya nchi za mbali kutoka kila nchi nyingine k.m. kutoka nchi ya Irak kwenda nchi ya Uchina na kinyume chake (toka Uchina kwenda Irak) na Irak yenyewe. Biashara ingeharibika kwa kutokuwepo kwa njia hizi, mbali na hayo uchukuzi juu ya migongo ya wanyama na ya wanadamu na bidhaa za biashara vingebakia kwenye nchi zalishaji na pia kubakia katika mikono ya walaji wenyeji. Usafirishaji wao ungegharimu zaidi kuliko gharama zao za uzalishaji. Hakuna mtu ambaye angethubutu kudiriki kuyasafirisha.

Hii ingepelekea kwenye upungufu wa aina mbili. Vitu vingi vya (matumizi ya) lazima visingepatikana. Wazia kwamba yichanganyiko vya matumizi ya dawa kuhitaji "henna" au "aloes" au matunda kama zambarau au baadhi ya dawa ya tiba au dawa ya lishe kutoka miji ya Asia au Ulaya, kama vingekuwa visafirishwe juu ya migongo tu bila njia ya mashua kupitia kwa kujitia kati ya bahari, vipi zingefika Uhindini (India) na vipi Wahindi wangefaidika nazo. Na kwa upande wa pili watu ambao sasa wanaendesha maisha yao kwa faida zipatikanazo kutokana na safari zao (za kibiiashara), wangepoteza tegemeo lao la kiuchumi.

Faida nyinginezo ni katika kupikia, kupashia mwili joto, juzikia vitu vya umajimaji na kuyeyushia vitu vigumu n.k. ni nyingi mno kiasi kwamba haziwezi kuhesabika. Ziko wazi kiasi kwamba haziwezi kuelezeka.

MVUA

Fikiria anga wakati ni nyeupe na wakati mvua inyeshapo. Hupishana kwa faida ya ulimwengu. Endeleo la hali moja yoyote kungesababisha machafuko (na matatizo). Huoni kwamba inapoanza kunyesha mfululizo, mboga mboga na mimea huanza kuoza. Miili ya hayawani hupata misukosuko. Anga - hewa huzidiwa na baridi na kufuatia maradhi, barabara na njia huharibika. Wakati anga inapokuwa nyeupe kwa muda mrefu, ardhi hukaushwa, mimea hunyauka. Hapo mtu hupatwa na madhara kwayo. Hewa hupata UKAVU na kufuatia magonjwa. Wakati (hali) zikipishana hivi kiutaratibu, hali ya hewa huwa sawasawa. Kila moja kwa zamu yake hufidia upungufu wa (hali) nyingine. Kila kitu huenda sawa.

Mkimzani angeuliza kwa nini haikuamriwa kwamba kusiwe na athari za madhara. Jibu likakuwa kwamba hii ni hivyo ili kwamba mtu mara kwa mara asumbuliwe ili kumuepusha na kutenda maovu. Mtu mgonjwa, kwa mfano, anapewa dawa chungu na isiyopendeza ili kumponya. Kadhalika wakati mtu mwenyewe hujichukulia katika makuu na kiburi huhitaji kupewa kitu ambacho kitamsumbua ili kumkinga kutokana na hasara na madhara yaletwayo makusudi na muhuweka juu ya ukarimu na utengeneko mzuri. Kama mfalme atawafanyia ukarimu watu wake, je, ukarimu wake huu hautavuta akili zao kwa heshima yake na mshangao? Wakati ambapo ukifikiria ni mfananisho gani walio nao yale mamilioni na mvua ambayo ni chanzo cha upatikanaji wa chakula na hali ya kustawi kwa sehemu zote za ulimwengu kwa unyweshaji wake wa mashamba ya nafaka.

Huoni, baraka kubwa iliyoje ya mvua hii ndogo kwa wanadamu? Bado watu ni wenye kuzembea kwayo. Mara nyingi wakati kiasi cha haja ndogo ya mtu kikizuiliwa, huanza kunung'unika na kufanya ufadhuli. Hupendelea zaidi haja yake ndogo kuliko zile faida kubwa zenye matokeo mazuri. Hii ni kwasababu ameshindwa kuthamini kuikamilifu sifa za fadhila hii bora. Fikiria ustadi uliomo ndani ya myua ilinyesha na kumwagikia chini kutoka juu (na) kunywesha kila mahali na uwanda wa juu pia. Kama ingekuwa ije kutoka kwa pembeni, ingeziwacha nyanda za juu zimenywesheka, (lakini) bila kuwepo eneo la kilimo. Nchi zenye unywesheaji wa mifereji (ambao siyo kwa njia za asili) ni pungufu kwa eneo. Maji ya mvua huienea ardhi yote. Mara nyingi kilimo kinaweza kikaendeshwa katika sehemu kubwa ya majangwa na maeneo ya milimani na kutokea kupatikana wingi wa nafaka.

Watu wanaepushiwa taabu ya kuchukua maji kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Mashambulizi mengi ya kikabila huibuka kutokana na umilikaji wa sehemu zenye maji ukifanywa na Mfalme mmoja na kulinyima kundi dhaifu. Matukio kama hayo vile vile huzuiliwa. Basi kwa kuwa iliamriwa, imepangwa hivyo ili kufanya hazi kama marasha rasha juu ya ardhi kuifanya ilowane na kuinywesha. Kama ingekuja na wepesi wa haraka kama mafuriko, isingenywea ndani. Katika hali ya mfuriko (mafuriko) ingeng'oa nafaka zote zilizosimama. Kwa hiyo, basi imeamriwa kunyesha katika manyunyu mepesi, ili kuziwezesha mbegu kuchipua, nchi iweze kunywesheka na mimea iliyosimama ipate kustawishwa. Kuna baraka nyingine katika unyweshaji huu. Hutuliza miili, huisafisha anga, kuiondolea uvundo uliosababishwa na usimamaji wa maji. Mimea ya bustani huponywa ugonjwa na njano na kadhalika.

Kama mkinzani atasema, iwapo mvua nyakati nyingine husababisha hasara kubwa kwa uwingi wake au katika hali ya mvua za mawe, husababisha nafaka kuteketea na anga kupata unyevunyevu mwingi usiofaa kwa afya na hatimae kutokea magonjwa na matatizo. Jibu litakuwa kwamba hasara hii pia wakati mwingine inakusudiwa kwa kumboresha mtu (na) kumkinga (au kumzuilia) kutokana na kujitumbukiza katika kuvuka mipaka ya Allah (s.w.t).

Faida ambayo atakuja ipata katika uboreshaji wa imani yake itapita hasara aliyoipata katika mali zake za kilimwengu (alizomiliki). Tizama kwenye milima hii iliyofanyizwa kwa udongo na mawe, ambayo mtu asiyojua hufikiri kama isiyo na maana na isiyo na umuhimu wowote. Hufanya umbo lenye manufaa yenye kuonekana. Miongoni mwao ni theluji ambayo huanguka na kubakia juu ya vilele vyao. Yeyote yule anaweza kunufaika nayo, wakati ikiyeyuka hufanya chanzo cha chemchem za kububujika maji na vijito vya ajabu. Hutoa mitishamba (ya dawa) na mimea ambayo haiwezi kukua sehemu tambarare na katika nyanda za chini. Ina matundu na mapango kwa ajili ya hayawani wanyama wakali wawindao. Hutumika kwa jinsi zilivyo ngome za muundo wa hali ya juu kiujenzi kama vituo vya ulinzi. Huweza kuchangwa na kufanywa makazi. Inakatwa na kufanywa vijaa. Ina madini ya mawe ya thamani ya rangi rangi namna mbalimbali.

Mbali na haya, ina sifa nyingine, ambazo Yeye Pekee Ambaye ameiumba katika vipimo halisi, hujua kwa Elimu Yake ya asili ya umilele wote. Fikiria aina mbambali za madini ambazo huchimbwa kwenye migodi kwa mfano, chkaa, chokaa malighafi (lime) itengenezwayo Saruji na chokaa (mortar), jipsa (gypsum), sumu mrututu (sulphurate of carsenicum), risasi (lead oxide), zebaki (mercury), shaba (copper), bati (tin), fedha (silver), dhahabu (gold), kito cha kijani (beryl), kito cha kundu (ruby), kito nyekundu (garmet) na aina mbambali za mawe na kadhalika vikitokezea kupatikana lami (tar), mafuta mgando (vaseline), mrututu (Sulphur), mafuta ya taa (kerosene) hutumiwa na watu. Je, basi hili ni fumbo kwa kiumbe mwenye akili kwamba hazina zote hizi zimewekwa kwa matumizi ya mtu ambazo anaweza kuzichimbua kama na wakati akizihitaji?

Watu hata hivyo, ni wenye tamaa na wanataka vitu vyenye thamani ndogo kuwa dhahabu na fedha. Wanafanya juhudi kubwa katika upande huo lakini zaidi sana bila mafanikio. Mipango yao haitoi faida. Kama watu hawa wangefanikiwa katika kutafuta kwao elimu, ingekuwa elimu ya kawaida. Dhahabu na fedha zingechimbuliwa kwa wingi mno kwamba zingepoteza thamani yao mbele ya macho ya watu. Manufao yaliyopatikana kutokana na shughuli za madini na biashara yangepotea na si wafalme wala mtu yeyote yule angeweka bohari za mali hizo.

Walakini, watu walipewa elimu ya (kuwawezesha) kuibadilisha shaba kuwa shaba bandia na kuwa kioo, bati kuwa fedha na fedha kuwa dhahabu, ambayo haifanyi madhara sana. Hebu tizama uone kwamba elimu ilitolewa mahali ambapo ikitumika haileti madhara sana, ambapo kwamba ile ambayo ni ya kudhuru imezuiwa. Na wakati mtu akiingia kwenye mgodi anaweza akakuta ndani yake vijito visivyotambulika vya maji yatiririkayo na mawe yenye rangi ya kifedha. Fikiria Usanii uliomo katika hili la Mwenye Nguvu zote Mwenye Kujua yote. Yeye (s.w.t) anataka kuwapa watu wazo la kujua uwingi wa hazina zake na ukubwa wa Enzi Yake Kuu ili waelewe kwamba kama Yeye (s.w.t) Akipenda, Yeye (s.w.t) anaweza kutupa susu fedha uwingi na ukubwa wa viwango sawa na milima. Yeye (s.w.t) anaweza kufanya hilo, hata hivyo, kungekuwa na kipato kidogo kwa sababu uwingi wa johari ungepunguza thamani yao, kama ilivyoelezwa kabla. Wachache wangenufaika kwayo.

Kuielezea kwa mfano, fikiria mtu amegundua kitu kipya, kwa mfano, vyombo au vitu vingine vya matumizi. Ni vyenye ubora, vikubwa na vyenye thamani maadamu tu vipatikane kwa uchache na adimu. Na wakati vitu hivyo vitazidi hitajio na kufidia kila mfuko (kila mtu) hupunguka katika thamani na huwa visivyo na maana. Kila kitu hufikiriwa kuwa kizuri pale tu kinapokuwa adimu.

MIMEA

Fikiria mimea na mahitaji mbalimbali inayotimiza. Tunda hutumika katika lishe, majani makavu kama chakula kwa wanyama, kuti kama nishati, mbao hutumika kwa (kazi ya) useremala wa kila aina. Kuna faida mbalimbali zipatikanazo kutokana na maganda yao, majani, mizizi mikubwa na midogo na gundi. Fikiria matunda tunayotumia kwa lishe yetu. Kama yangekuwa yanapatikana sehemu moja badala ya kuwa yamening'inizwa kwenye matawi ambayo huyazaa, mchafuko ulioje wa mpango ungesababishwa katika maisha yetu! Lishe ingepatikana bila shaka yoyote, lakini vipi kuhusu manufaa yenye thamani tuyapatayo kutoka mbao za miti, majani makavu na sehemu nyingine tulizozitaja. Zaidi ya hayo, furaha ambayo huletwa na uzuri wa kimandhari na hewa safi ya mimea kiulinganifu ni bora zaidi kwa anasa na furaha za ulimwengu wote.

NAFAKA

Hebu fikiria jinsi kilimo kilivyoamriwa kustawi. Mia au zaidi ya nafaka zinatoka kwenye mbegu moja. Nafaka moja kutoka kwenye mbegu moja kungekuwa na mantiki. Kwa nini basi kuongezeka huku? Hakika ni kuizidisha nafaka ili kwamba hiyo hiyo isaidie kwa chakula kufikia vuno lingine mbali na uwekaji wa nyingine kama mbegu kwa wakulima. Fikiria Mfalme akusudiaye kuujaza mji na watu. Hupanga kutoa kiasi kikubwa cha nafaka ambacho kitatoshelezea wakazi kuwasaidia kwa chakula mpaka mavuno yajayo mbali na kuweka nyingine kwa ajili ya mbegu. Angalia jinsi mpango huu unavyosimamiwa katika taratibu za Mwenye Nguvu zote Allah Utukufu uwe kwake, kwamba kilimo kingepelekea kwenye ongezeko kubwa sana kama hili ili kuhudumia vyote viwili, hitajio la lishe na vile vile kwa lile la mbegu. Ni sawasawa hali hiyo katika miti, mimea na mtende. Huzaa matunda mengi mno. Unaona kwamba kuna mzizi mmoja, lakini kuna machipukizi mengi. Kwa nini? Hakika kwa ajili ya dhumuni la kuzalisha zaidi kizazi kutokana na mbegu, baada ya watu kuziweka kwa matumizi yao.

Kama kungekuwa na mzizi mmoja bila ya matawi kuchipua kwa wingi hivyo, isingeyamkinika kuchukua chochote kutoka kwenye mimea kwa kupanda au kwa shughuli yoyote nyingine. Katika hali ya kutokea maafa ya ghafla mimea ya asili ingetoweka bila ya kuwepo uwezekano wa mmea mwingine kuchukua nafasi yake. Fikiria nafaka za kunde, choroko, dengu na maharage. Zote hukua kwenye maganda kama hifadhi ya madhara, mpaka zinapokomaa kwenye ugumu, kama vile kondo la nyuma. Nafaka za ngano na nafaka nyingine kama hizo zimepangwa tabaka kwa tabaka katika maganda magumu, zikiwa na ncha kali kwenye miishilizo yao kama mikuki kuwazuia ndege na kuongeza mazao kwa wakulima.

Kama mkinzani akiuliza iwapo ndege hawapati kitu katika nafaka za ngano n.k. jibu kwake litakuwa kwamba hapana shaka wanazipata nafaka na imeamriwa hivyo kwao, kwa kuwa ndege nao vilevile ni katika viumbe vya Mwenye Nguvu zote Allah. Yeye (s.w.t) Amewaamria sehemu ya mazao ya ardhi. Nafaka hizi zimehifadhiwa katika mifuniko wasije wakapata kumiliki nafaka yote kupelekea kwenye hasara ya dhahiri kwa upotezaji ulio tukutu.

Katika kukosekana kwa hifadhi kama hii ndege wangeruka juu ya nafaka na kufanya kazi nyepesi (na ndogo) ya wao wote. Wangeumia kutokana na uyeyushaji dhaifu wa chakula katika tokea jingine, kwa dhahiri ya madhara yao, Wakulima vile vile, wangekuwa wenye hasara. Mifuniko hii ya hifadhi kwa hiyo, imetokea kupewa ili kwamba ndege wapate kiasi chao cha kuwatosha tuu kwa chakula, wakiacha sehemu kubwa kwa matumizi ya wanadamu. Wanayo haki kubwa zaidi kwayo kwa sababu ya kazi iliyofanywa na wao, na hitaji lao la nafaka ni kubwa kuliko lile la ndege.

UZAO WA MIMEA

FIkiria uzao wa mimea na jamii mbalimbali za miti. Huhitaji lishe sawa kama wanyama. Hata hivyo haina vinywa vya kujilishia, wala haiwezi kwenda huku na huko kutafuta chakula chao. Kwa hiyo, imetnikiwa mizizi chini ya ardhi, kupokea lishe yao kwa upelekaji kwenye matawi yao, majani na matunda. Ardhi huihudumia kama mama ambamo kutoka humo inanyonya lishe yao kupitia mizizi yao ambayo huitumikia (kikazi) kama vinywa kuipatia chakula chao. Kama vile watoto wadogo wa wanyama hujilisha kwa maziwa kutoka matiti ya mama zao. Je, huoni hizi mambo zilivyohimilishwa wima bila hofu au kuanguka au kuinamisha mahema na kutiwa ngvu kwa njia ya kamba zilizfungwa imara? Kadhalika, utauona kila mmea umesimikwa katika ardhi kwa mizizi iliyosambaa kila upande kuupa nguvu. Vipi miti mikubwa ya mitende yote ingesimama imara dhidi ya dhoruba?

Angalia! Ustadi wa uumbaji ulivyo tangulia mbele umahiri wa utendaji kazi. Umahiri uliotumika katika kusimamisha mahema na kutiwa nguvu na mafundi, ulitumika nyuma kabla katika usanifishaji wa mpango wa usimikaji miti ambao hutangulia uhitaji wa mahema kwa mambo na nguzo vyote vikiwa vimepatikana kutokana na miti. Ni wazi kwamba umahiri huu umeigizwa kutoka ustadi uliotumika katika kusimika miti.

MAJANI

Fikiria utokaji wa majani ya mimea kwa uangalifu na utaona yametanda katika misokoto yake kitu kifananacho na mfumo wa mizizi itambaayo sehemu zake zote za marefu na mapana. Baadhi yao ina kapilari nyororo iliyounganishwa na iliyo minene, yote ina nguvu sana na mizuri. Kama ingetayarishwa kwa mkono mtu asingeweza kuwa na uwezo wa kufanya kazi juu ya mti mmoja katika muda wa mwaka. Angelihitaji ala (zana), nia, kielelezo na mafunzo katika kuifanya. Katika siku chache za majira ya msimu wa demani majani mengi mno hujitokeza kiasi kwamba milima na maeneo ya mabonde ya ardhi hujazwa nayo bila ya neno kusemwa au kufanywa shughuli yoyote kama vile tu katika matokeo ya wangwa kuenea vitu vyote - ruhusa ya mgawo mmoja usiodhuru.

Elewa, tena, jambo la asili linalohusikana na kapilari nyororo. Zimefumwa katika misokoto ya majani ili kuinyweshea kama vile kimia cha kapilari katika mwili kichukuavyo lishe kupeleka sehemu zote. Kuna ustadi mwingine katika vena (chelewa) nene za majani. Kwa sababu ya uwezo wao wa kujirudi haraka na nguvu, hushikilia kwa nguvu msokoto wa jani kuyakinga kutokana na kuchanika. Majani haya ni sawa na majani bandia yanayo tengenezwa kutokana na nguo na ambayo yametengenezwa kwa marefu na mapana na kushikishwa kwa nguvu dhidi ya uchakavu. Kwa hiyo majani bandia yafanywayo kwa mkono hufuata yale ya asili, ingawa kamwe hayawezi kuweka uhai wa kweli.

MBEGU

Fikiria kokwa ya mbegu iliyochimbiwa ndani ya tunda, ambayo itawezesha kuzalisha nyingine iwapo mti utapotea kwa ajili ya baadhi ya majangwa. Ni zao zuri tu la matumizi ya kudumu, linahifadhiwa katika sehemu witri liweze kupatikana katika sehemu nyingine kama hii ikipata ajali katika sehemu moja. Kisha kwa sababu ya kurudi upesi kwenye hali zao za kawaida (baada ya kunyofolewa) na ugumu huzuia tunda kuwa laini sana na utovu mwingi. Bali bila kokwa hizi matunda yangepasuka na kuwezesha udhaifu.

Baadhi ya kokwa zinalika na mafuta hukamuliwa kutoka nyinginezo kwa matumizi katika kazi tofauti. Na kwa kuwa umejifunza dhumuni lifanywalo na kokowa, yakupasa ufikirie nyama ya tunda iliyofungika ndani ya mbegu ya tende na ile inayozunguuka kokwa ya zabibu, ubora kwayo na sababu gani ya umbo lake, ambapo kwamba ilikuwa inawezekana kutoa/kuzalisha badala ambayo isingekuwa ya kulika kama vile miti ya "cypress" na miti (mingine) maarufu. Hakika ni hivyo kwamba mtu akute lishe tamu, afurahi.

Fikiria sifa, nyingine za mimea. Utaona kwamba inaathiriwa na majira ya msimu wa masika, hivyo kwamba joto lao muhimu huhifadhiwa katika vitawi vyao, na malighafi kwa uzalishaji wa tunda hutengenezwa. Majira ya msimu wa demani huivalisha majani na kupata aina zote za matunda, kama vile unavyopanga aina mbalimbali za vyakula vitamu mbele yako ambavyo vimepikwa kwa zamu. Hebu ona vitawi vitoavyo matunda yao kwako kwa mikono yao.

Na unayatazama kwa furaha maua ambayo yanakuja mbele yako juu ya vikonyo vyao kama kwamba vinajiwakilisha vyeme kwako? Nani amepanga hivi? Hakika ni Yeye Ambaye ni Mwenye kujua yote Mwenye Kuamuru. Na ni dhumuni gani linakusudiwa kwayo? Hakika, ni kwamba mtu afurahie matunda na maua. Ajabu ilioje, kwamba badala ya shukurani kwa baraka hizi, watu humkana Mtoaji moja kwa moja.

KOMAMANGA

Hebu fikiria Komamanga na umahiri na ustadi ambao umetumika katika uzalishaji wake. Utaona, ndani yake lote ni duara na madoido ya nafaka zilizowekwa tabaka juu ya tabaka, kama vile zimepangwa kwa mkono. Nafaka hizi zimegawanywa kwenye sehemu tofauti na kila sehemu imefunikwa katika kitani, zimefanyizwa katika hali iliiyo bora sana ya kipekee. Zote hizi zimezunguukwa na ganda la nje.

Ustadi wa Kisanii uliomo humo ni kwamba kwa kuwa nafaka haziwezi kusaidiana kila moja katika ukuaji wa nyama ya tunda, utando umewekwa ndani ya Komamanga ya kulisha katika huo, unaona zote nafaka na nyama ya tunda zimetiwa ndani sana na kukazwa imara. Tando hizi husaidia kuziweka mahali pamoja zisizosogezeka. Juu ya yote haya, mfunika wenye nguvu umewekwa kuziweka salama kutokana na madhara ya nje. Hizi ni nukta chache kuhusu Komamanga, ambalo yoyote ambaye hupenda maelezo zaidi (kwa urefu) anaweza kuongeza mengi zaidi. Maelezo yaliyotolewa hapa ni, hata hivyo, yenye kutosha kwa dhumuni la hoja na funzo.

MIMEA ITAMBAAYO

Hebu ona mtambaazi huu mnyonge (dhaifu). Mitambaazi hii hutoa nje (huzaa) mamung'unya makubwa mno, matango na mitikiti -maji. Ustadi ulioje umeendelea katika Usanii wake! Kwa kuwa imeamriwa kwamba itazaa matunda makubwa mno, mmea huu umesanifiwa utambae juu ya ardhi. Ingekuwa kama mimea mingine isimamayo wima, usingeweza kuhimili mavumo yakushangaza ungevunjika na kuanguka chini kabla (ya mazao yake) hayajawa. Angalia jinsi unavyojitandaza (na kuenea) juu ya udongo kuweka uzito wa mazao yake juu ya ardhi. Pengine ungeweza kuona kwamba mizizi ya mitambazi mmung'unya na tikiti-maji husambaa katika ardhi na mazao yake (matunda) yakilala juu ya ardhi pande zote, kama vile paka alalae chini akinyonyesha watoto wake (maziwa) - matunda.

Fikiria ukweli kwamba mitambaazi hii hukua tu katika majira maalum ya misimu iliyowekwa kuifaa (mimea hii) katika joto kali la Kiangazi, kwa mfano, wakati watu huikaribisha kwa furaha. Kama ingestawi katika kipupwe, watu wasingevumilia kuonekana kwao. Kwa nyongeza inaweza kusababisha maradhi wakati wa kipupwe. Hutokea wakati mwingine kwamba matango yanazaliwa katika kipupwe. Watu kwa ujumla huyaepuka, isipokuwa walafi pamoja na hisia ya madhara na magonjwa.

MTENDE

Fikiria mitende. Kuna miti ya Kike miongoni mwao. Kwa uzazi wao miti ya kiume huzaliwa pia, ambayo huzalisha bila ya kupangwa kilimo cha bustani. (Miti) dume, kama yale (madume) ya wanyama, huzalisha, lakini yenyewe ni gumba. Fikiria kiuangalifu shina la mtende. Utaona kwamba limefumwa kama utando, ingawa hakuna nyuzi ndefu. Liko kama vile kipande cha nguo kimefumwa na mkono kulifanya kuwa na nguvu na kunyooka kuweza kustahamili pepo zenye nguvu na ubebaji wa vichala vikubwa vya matunda, katika kukomaa, na kisha mwishowe kutumika kwa kupauliwa na madaraja. Utaona ndani yake nyuzi zimesokotwa kwa marefu na mapana. Liko imara vya kutosha kutumika katika utengenezaji wa ala (zana).

Kama lingekuwa gumu kama jiwe, lisingetumika katika majengo kama mbao, kwa mfano, milango kazi ya kimia, mbao za miti na makasha n.k.

MBAO

Kuna sifa moja kubwa katika mbao. Inaelea juu ya maji. Kila mtu anaijua hii lakini hatambui thamani yake kwa ukamilifu. Kutokuwepo kwa tabia hii, vipi mashua zingetengenezwa, ambazo hubeba milima ya bidhaa za biashara kutoka mji kwenda mji kwa juhudi kubwa? Shida zilioje ambazo zingekuwa zistahimiliwe katika kusafirisha bidhaa za biashara? Vitu vingi vya matumizi vingetoweka sokoni au vingepatikana kwa bei ya aghali sana.

MITI SHAMBA

Fikiria hii miti shamba na tabia ambazo kila mmoja amejaaliwa nazo kama madawa. Hupenyeza chini kwenye viungio, huteketeza takataka na jauhari za sumu kutoka humo, kwa mfano, ugonjwa uitwao, Shahtra, baadhi ya mitie mingine hutuliza ulegevu wa moyo, kwa mfano mti wenye dawa iitwayo "ateemoon", baadhi ya mingine huondoa riahi, kwa mfano siki, baadhi ya mingine hutuliza uvimbe, kwa mfano zabibu pori na kadhalika kwa ufanisi wao. Nani basi ameijaalia kuwa na sifa kama hizi? Hakika Yeye Ambaye ameiumba na dhumuni. Nani amewapa watu elimu kwayo? Hakika Yeye ambaye ameyajaalia madawa haya na hali kama hizi. Vipi mambo haya yangefika kwenye fahamu za mwanadamu kwa bahati na yenyewe tu kama wale waaminio mambo ya bahati nasibu wanavyodai?

Haya, hebu natukubali kwama mtu amejifunza yote haya kutokana na akili yake na hoja, taamuli na majaribio ya kimaabara. Lakini ni nani amewafundisha wanyama? Baadhi ya hayawani, wanapojeruhiwa (na kuumia), hutumia miti shamba kujiponyeshea, na baadhi ya ndege wakiumwa kutokana na kufunga choo hupata afueni kwa kuharisha kwa kutumia maji ya bahari na kadhalika?

Unaweza, pengine, kutia shaka manufaa (faida) ya uhai wa mimea au faida za nchi zilizoachwa (vihameni) na za tambarare ambako hakuna uhai wa binadamu upatikanao na kuufikiria kuwa wote ni bure na hauna maana. Sivyo hivyo vilivyo. Wanyama pori hujilisha kwayo na nafaka yao inatumiwa na ndege kwa chakula. Vitawi vyao na kuni hutumiwa na watu kama nishati. Kuna nukta nyingine vile vile zenye faida kuzijua. Ina tumika kwa madawa ya kutibu (kuponya). Ngozi hudubaiwa kwayo. Nguo hutiwa rangi na kadhalika. Inazo sifa nyinginezo pia.

VITU VISIVYO THAMANI

Je, hujui kwamba mti wa chini kabisa kwa daraja na uliodharauliwa ni (ule uitwao) "Khairya Baradi?" Pia hiyo ina sifa mbalimbali. Karatasi hutengenezwa kwayo kwa matumizi ya Wafalme na watu wa kawaida. Hutengenezwa kuwa mikeka/busati kwa matumizi ya wote na vyote. Hutumika katika kutengeneza vifniko vya kufunikia vyombo vya nyumbani vilivyotengenezwa kwa kioo n.k. ambavyo hujazwa nayo kuzuia kuvunjika. Ina sifa nyingi nyinginezo kwa nyongeza ya hizi.

Kisha jifunze somo kutoka namna nyingi na faida ambazo hupatikana kutokana na viumbe vidogo na vikubwa kama vile pia kutoka vitu vile ambavyo havina thamani na vile ambavyo vina thamani. Isiyo na thamani zaidi ya yote haya ni kinyesi cha ng'ombe na uchafu utokao mwilini ambao ni taka zisizo na thamani, na fikiria faida ambazo hupatikana kutokana nazo kwa kilimo na mboga. Zina faida hivi kiasi kwamba hazina kifani. Hakuna mboga mboga inayeweza kuwa na thamani isipokuwa iwe imewekewa mboji ambayo ni ya kuchukiza kiasi kwamba mtu haikaribii kwa kuona kinyaa.

Elewa hili nalo, kwamba thamani ya bidhaa haitegemei juu ya thamani ya pesa peke yake. Ina thamani mbili tofauti katika masoko mawili tofauti. Hutokea wakati mwingine kwamba bidhaa haina thamani katika soko la uchumi na bado bidhaa hiyo hiyo ina thamani katika soko la elimu. Inaweza kuwa kwamba unaweza kufikiria kitu kwamba hakina faida kwa sababu ya thamani yake yu chini kifedha. Hebu angalia ni thamani kubwa kiasi gani ingekuwa kwa uchafu wa wanadamu (kinyesi na mkojo) kama hali/sifa zake zingefahamika kwa mkemia. Ni ukweli kwamba majaribio mahsusi ya kemia hayawezi kufanywa bila uchafu wa wanadamu."

Ilikuwa sasa ni wakati wa Sala za adhuhuri, na Imam(a.s) aliniambia kuja siku ifuatayo (yaani kesho), Insha - Allah! Nilirudi mwenye furaha kwa sababu ya maelezo niliyopata kutoka kwa Imam(a.s) . Nilimshukuru Allah (s.w.t) kwa maelezo yenye thamani niliyopokea. Nilipitisha usiku kwa amani halisi.