MAISHA YA BIBI KHADIJA

MAISHA YA BIBI KHADIJA0%

MAISHA YA BIBI KHADIJA Mwandishi:
Kundi: Waheshimiwa wa Kidini

MAISHA YA BIBI KHADIJA

Mwandishi: Syed A .A .Razwy
Kundi:

Matembeleo: 23465
Pakua: 3002

Maelezo zaidi:

MAISHA YA BIBI KHADIJA
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 16 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 23465 / Pakua: 3002
Kiwango Kiwango Kiwango
MAISHA YA BIBI KHADIJA

MAISHA YA BIBI KHADIJA

Mwandishi:
Swahili

7

MAISHA YA BIBI KHADIJA

SURA YA KUMI NA MOJA

KUZINGIRWA KWA BANI HASHIM A.D. 616 - 619

Mwaka wa sita baada ya kutangazwa Uislamu ulikuwa unaelekea kwisha. Wapagani wa Makka walikwisha tumia miaka mitatu kufanya kampeni dhidi ya Uislamu. Walifaulu kusababisha machungu mengi na uadui dhidi ya Waislamu lakini hawakuwa na lolote la kuonyesha dhidi ya Waislamu, walitumia kila aina ya silaha ikiwa ni pamoja na kushaw-ishi, kupotosha, kutukana na kudhihaki. Waliishia kutumia nguvu na kwa hakika walitumia nguvu kuzuia Uislamu au angalau kwa kiwango fulani kuudhibiti, lakini juhudi zao zote zilishindwa. Waislamu wali-himili mashambulizi yao. Nguvu ya imani ya Waislamu viliwashangaza watesaji wao.

Kushindwa huko mara kwa mara kuliwalazimisha Maquraysh, hasa zaidi ukoo wa Umayya, kutathmini upya hali ya Muhammad na Uislamu na baadhi yao walijaribu kuliona tatizo lao kwa namna nyingine. Wakati wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa tatizo la kuchukiza walianza kuele-wa pole pole kwamba, adui yao alikuwa si kundi la Waislamu ambao ni masikini sana hapo Makka. Adui yao halisi - adui wa waabudu masana-mu na washirikina - alikuwa Abu Talib! Kwa vyovyote vile ni Abi Talib ndiye aliyekuwa anamlinda Muhammad na Uislamu kwa msimamo na ushupavu. Kwa upande mwingine, Waislamu walikuwa hawana uwezo wa kumlinda Muhammad. Hakika wao nao walikuwa wanahitaji sana ulinzi.

Uzoefu wa muda mrefu uliojaa mambo machungu kwa Quraysh, uli-wathibitishia kwamba mtu anayekwamisha vita yao dhidi ya Uislamu si mwengine isipokuwa Abu Talib. Kwa hiyo, waliamua kwamba hawangeweza kukivunja kipingamizi kilichowakabili, kwa kuwawinda au kulitesa kundi la Waislamu wakazi wa Makka ambapo adui halisi - Abu Talib - alikuwa huru na kuranda randa miongoni mwao, na kama vile anawakejeli. Hatimaye Maquraysh walifaulu kumtambua adui yao halisi.

Kufaulu huku "kumtambua adui" kulikuwa na athari ya ufunuo juu ya viongozi wa Maqurysh. Na waliamua kutengeneza mkakati mpya kati-ka vita yao dhidi ya Muhammad na Uislamu. Abdul - Al-Rahman Azzam.

"Hatimaye, utawala wa Makka uliamua katika hali ya kukata tamaa kumchukulia hatua Abi Talib. Kwa mawazo yao, alikuwa mlinzi halisi wa kufuru, ingawa bado alikuwa ana heshimiwa kama mtetezi wa taasisi za Makka na hajawa mfuasi wa imani ya Muhammad. Walikubaliana kumpelekea kauli ya mwisho..." (The Eternal Messege of Muhammad, London, 1964)

Siku za nyuma Quraysh walijaribu mara nyingi "kumtenga" Muhammad kutoka kwenye kabila lao, na walikuwa na matumaini kwamba wangeweza ama kumshawishi au kumdanganya Abu Talib asiendelee kumuunga mkono na kumpa ulinzi mpwa wake na Uislamu. kama wangemtenga Muhammad kutoka Bani Hashim, waliridhika kwamba, wangeweza kutatua tatizo ambalo liliwakera kwa njia rahisi ya "Kummaliza."

Lakini Abu Talib hakuwaruhusu Maquraysh "kumtenga" Muhammad. Si tu kwamba alikuwa anamlinda mpwa wake, alikwisha unganisha koo za Bani Hashim na Bani al-Muttalib na kuwa naye. Hizi koo mbili zilikuwa imara katika kumuunga mkono Muhammad, na makafiri wali-jikuta hawana uwezo dhidi yake.

Baada ya mjadala mrefu na mashauriano, Maquraysh walikubaliana kwamba kutotii na kutokukubali maafikiano kwa Bani Hashim palihita-jika kutumia hatua kali zaidi dhidi yao, na waliamua kumtenga si Muhammad tu lakini mlinzi wake, Abu Talib, pamoja na koo za Bani Hashim na Bani al-Muttalib. Ilikuwa ni jambo lenye mantiki kudhani kwamba jaribio lolote la kuwachokoza Bani Hashim lingesababisha mkingamo katika mshikamano wa makundi jijini Makka. Kila mtu Makka angetangaza ama kuwa pamoja au dhidi ya Bani Hashim. Lakini haikuchukuwa muda mrefu, ilijulikana wazi kwamba katika mapambano haya, Bani Hashim wangejikuta Arabia yote inawapinga.

Muhammad Husayn Haykal Ni karibu ya kutowezekana kwetu sisi kufikiria nguvu na kiwango cha juhudi ambacho Maquraysh walitumia katika jitihada zao dhidi ya Muhammad au uvumilivu wake katika kipindi cha miaka ya juhudi hiyo. Maquraysh walimtishia Muhammad na ndugu zake, hususan ami zake. Walimkejeli yeye na ujumbe wake, na walimtusi yeye halikadhalika na wafuasi wake. Waliwaagiza washairi wao wamuigize kwa kubeza kwa werevu wao na waelekeze miba yao mikali dhidi ya mafundisho yake. Ilimsababishia madhara na maumivu juu yake na wafuasi wake.

walijaribu kumpa rushwa ya fedha, ya ufalme na utawala, kwa hakika, katika yote yale ambayo yangemtosheleza mgumu aliye mgumu kabisa wa kuridhika miongoni mwa watu. Waliwafanya kuwa masikini Waislamu kwa kuharibu biashara zao, waliwafukuza na kuwatawanya kutoka nchi-ni mwao. Walimtahadharisha Muhammad na wao kwamba vita hiyo pamoja na matokeo yake ingewapata wao. Waliishia kwanza kuwasusa kama njia ya kuwashindisha na njaa. (The Life of Muhammed, Cairo, 1935).

Siku chache kabla ya kuanza mwaka wa saba, viongozi wa koo mbal- imbali za Maquraysh walikutana katika baraza la siri lenye umakini, kwenye ukumbi wa jiji la Makka, na waliandika na kutia saini zao katika mikataba ambayo ilisema kwamba, hadi hapo ambapo ukoo wa Bani Hashim utakapomwasilisha Muhammad kwao, wangeususa ukoo huo kiuchumi na kijamii. Waliahidi kutokununua chochote au kuuza chochote kwa watu wa Bani Hashim na walizuia kuoana.

Makubaliano haya yalipelekwa kwa makabila mengine kwa uthibitisho, na baada ya makabila mengine kukubali, mikataba hiyo ilitundikwa kwenye ukuta wa Al-Ka'aba kwa utaratibu wa mila yao. Uthibitisho wa makabila mengine wa makubaliano haya lilikuwa tendo la uchokozi!

Abu Talib aliitafakari hali hiyo. Aliona waziwazi kwamba mpangilio wa tatizo kubwa ulikuwa unawazunguka Bani Hashim. Baada ya makabila mengine kuthibitisha makubaliano ya kuwasusa Bani Hashim, hali huko Makka ilibadilika dhahiri, hali ilikuwa ilipuke wakati wowote hivyo kwamba walijikuta kwenye dhiki kubwa mno. Abu Talib alitam-bua kwamba ingekuwa ni hatari sana kwa ukoo wake kuishi jijini Makka ambapo wakati wowote adui angechoma moto nyumba zao. Kwa hiyo, kwa usalama wa ukoo huo, alitangaza kuondoka Makka, na kutafuta usalama wake pembezoni mwa jiji mahali penye korongo. Korongo lilikuwa na usalama wa kutosha katika hali yoyote ile. Hapo ilikuwepo salama ya Bani Hashim kuishi, kuliko kuishi kwenye nyumba zao ambazo zingeshambuliwa kwa urahisi.

Mnamo siku ya kwanza ya mwaka wa saba tangu Wito au Kutangazwa kwa Uislamu, koo mbili za Bani Hashim na Bani al-Muttalib, zilitoka nje ya Makka, na walianza kuishi kwenye korongo ambalo baadaye lilipewa jina - Shi'b Abu Talib. Sasa walikuwa katika hali ya kuzingirwa! Hali hii ingeendelea kwa kipindi kirefu. Muhammad Husayn Haykal Mkataba ambao uliwekwa na koo za Maquraysh kwa kumsusa Muhammmad na kuwakwamisha Waislamu uliendelea kutekelezwa kwa miaka mitatu mfululizo. (The Life of Muhammad, Cairo, 1935).

Marmaduke Picktha!! Kwa kipindi cha miaka mitatu, Mtume alikuwa amezuiliwa (amefungiwa) pamoja na ndugu zake katika ngome yao ambayo ilikuwepo katika moja ya mabonde membamba yateremkayo mpaka mjini Makka. (Introduction to translation of Holy Quran 1975) Maelezo kuhusu kuzingirwa kwa Bani Hashim ni hali inayotisha katika historia ya Uislamu, na imeelezewa na kila mwanahistoria kuhusu jambo hilo, miongoni mwao ni Muir na Margoliouth.

Sir William Muir. Maquraysh walisaini mkataba dhidi ya Banu Hashim - kwamba hawangeoa wanawake wao wala hawangewaruhusu wao kuoa wanawake wao, kwamba hawangewauzia chochote wala kununua chochote kutoka kwao, na kwamba shuguli za aina yoyote na wao lazima zisitishwe. Kikwazo hiki kiliandikwa kwa uangalifu sana na kupigwa mihuri mitatu. Wakati wote walipofungamana na mkataba huo, maandiko hayo yalining'nizwa juu ya Al-Kaaba na hivyo adhabu ya kidini kupatiwa kibali chake Banu Hashim hawakuweza kuvumilia maneno ya watu ambayo yalianza kuenea kwa fujo dhidi yao na kuelewa kwamba labda huo ulikuwa ni mwanzo wa mashambulio halisi yaliyo kuwa yanakuja na yangekuwa makali zaidi, walikwenda kuishi mahali pembezoni mwa mji wa Makka palipoitwa Shib Abu Talib. Ilikuwa ni sehemu ya korongo, ambapo majabali ya Abu Kubeis yalichomoza nje kidogo ya Makka.

Mnamo usiku wa kwanza wa Mwezi wa kwanza wa mwaka wa saba baada ya kutangazwa ujumbe wa Muhammad, Banu Hashim, pamoja na Mtume na familia yake, walikwenda kwenye makazi ya Abu Talib, na pamoja nao pia walifuata wazawa wa Al-Muttalib, ndugu wa Hashim. Mtafaruku wa kutengwa ulisimamiwa kikamilifu. Banu Hashim wali-jikuta wamezuiwa kupata mahitaji ya nafaka na vitu vingine vya muhimu na uhaba mkubwa wa vitu uliwakumba, akiba ya Banu Hashim ilikuwa inaongezewa tu mara kwa mara kwa njia za kichinichini na hatari, hali ambayo iliwafanya wawe watu walioishiwa na mahitaji. Raia wa Makka waliweza kusikia kilio cha watoto wenye njaa huko Shi'b. Miongoni mwa ndugu wa kundi lililotengwa, walionekana wakihatar-isha maisha yao kwa kupeleka chakula kwa siri kwenye makazi ya Abu Talib ingawa walitishiwa na Maquraysh.

Hakimu, mjukuu wa Khuwayled, alikuwa na mazoea ya kupeleka chakula kwa shangazi yake Khadija, ingawa ilikuwa hatari. (The Life of Muhammed, London, 1877) D.S. Margoliouth Mpango uliofahamika kwa wapagani wa Kiarabu ulikuwa kuwatenga, madhumuni ambayo yalifanya kuanzishwa kwa ushirikiano maalum. Hati za kukunja (scroll)[1] zilikuwa katika matumizi ya kawaida mjini Makka.

Mapatano na mkataba makini ulifanywa, uliandikwa kwenye hati ya kukunja na kutundikwa ndani ya Kaaba, ambao ndani yake viongozi wa Makka waliapa kuwatenga bani Hashim na Bani Muttalib ili wasipate haki hizi hadi hapo Muhammad atakapotangazwa kuwa ni mhalifu na akakabidhiwa kwenye mamlaka husika na kulipa kisasi. (Muhammed, and the Rise of Islam, London, 1931).

Idadi ya watu wa ukoo wa Hashim na al-Muttalib, wateja wao na watumwa wao ambao waliondoka Makka kwenda kutafuta makazi kwenye korongo walikuwa mia nne. Mara tu walipotulia kwenye makazi yao, waliangalia mandhari ya ardhi ya hapo, waliweza kuona kwamba walikabiliwa na changamoto ya hali ngumu isiyoelezeka kwa urahisi. Ambapo siku za nyuma walikuwa wanapambana na uadui wa binadamu, sasa walishindana pia na uadui wa maumbile. Waligundua pia kwamba makazi yao mapya hayakuwa na mpangilio unaofaa kutege-meza maisha.

Kwa hiyo, walifahamu tangu siku ya mwanzo kabisa kwamba wangewajibika kwa kutumia ujasiri wao, ustadi wao, ubunifu wao na uamuzi wao kukubali mazingira mapya. Walijua kwamba uhai wao ungetegemea uwezo wao wa jinsi ya kutumia makazi hayo. Khadija alizaliwa kwenye familia ya kiungwana na alilelewa katika raha na starehe. Kwa hiyo alikuwa mgeni kabisa kwenye maisha magumu na ya upweke. Lakini ilipotokea dharura, aliambiwa aache nyumba yake yenye nafasi kubwa mjini, aende kuishi ndani ya korongo lenye hali ngumu, alifanya hivyo kwa hiyari yake mwenyewe akiwa na furaha. Korongo lilikuwa linatia majonzi hivyo kwamba roho ya mtazamaji ilikata tamaa lakini Khadija hakuonyesha dalili ya kufadhaika alipoingia humo. Ingawa makazi mapya yalikuwa si mazuri, alijizoesha haraka sana kuishi humo. Aliangalia mateso mbele yake, akajikaza na kuvu-mila na kutumia uhodari wake. Uimara wa roho yake, kweli ulis-hangaza.

Mwanzoni mwa kuzingirwa, Ali alikuwa na umri wa miaka kumi na sita. Alikabiliwa na kazi ngumu na hatari ya kukusanya akiba ya chaku-la kwa ajili ya koo mbili. Alifanya kazi hii katika hali ya hatari kwa maisha yake; alileta maji na nafaka kutoka popote. Kiriba kimoja cha maji walinunua kwa kipande kimoja cha dhahabu, na alijihisi anayo bahati kama alifaulu kufikisha kwenye makazi mapya. Juhudi zake, zilileta nafuu kidogo kwenye koo zilizozingirwa.

Abu Talib alikuwa halali usingizi usiku. Kwake yeye usalama binafsi wa Muhammad ulipewa kipaumbele. Muhammad alipolala, Abu Talib alimnyanyua na akamweka kwenye kitanda cha mmoja wa watoto wake wanne na akamuamuru alale kwenye kitanda cha Muhammad. Baada ya muda kidogo akamweka kwenye kitanda cha mmoja wa watoto wake. Usiku wote Abu Talib alifanya kazi ya kumyanyua Muhammad kutoka kitanda hiki na kumpeleka kitanda kingine. Hakutaka kudanganyanyika kuhusu maadui zake, alitambua kwamba walikuwa wang'ang'anizi sana, wasaliti, fisadi, wapenda kulipa kisasi.

Kwa hiyo hakufanya kosa la kudhani wangeshindwa. Kama mmoja wao angetambaa chini na kuingia kwenye makazi yao kwa nia ya kumuua Muhammad, basi uwezekano mkubwa ungekuwa kwamba, angemuua mmojawapo wa watoto wake Abu Talib akidhani kwamba ni Mtume.

Abu Talib na mkewe walikuwa tayari kujitolea maisha ya watoto wao kwa ajili ya kumwokoa Muhammad. Kwa hakika wangefurahi sana kujitolea maisha yao wenyewe kwa sababu ya Muhammad kama ingekuwa lazima. Si tu kwamba walimlinda Muhammad, walihakikisha kila mtu mzima kwenye makazi hayo mapya anawajibika kumlinda Mtume.

Kuna wakati ambapo Ali, pamoja na ujasiri wake, alishindwa kupata mahitaji yoyote au kama alipata chochote hakuweza kuleta hapo kwenye makazi, kwa kushindwa kuwakwepa Maquraysh. Nyakati kama hizo, watoto na wakubwa walisumbuliwa na njaa na kiu. Lakini njaa na kiu hapo kwenye korongo ilikuwa hali ya kawaida. Wanawake walichemsha majani na magamba ya miti na kuwapa watoto wanywe ili watulize njaa.

Kilio cha watoto wenye njaa kilisikika nje ya makazi hayo ya muda na Maquraysh walijibu kwa kicheko cha kejeli. Walichekelea na huku wakiwabeza kuhusu ushindi wao wa kuwafanya watoto wa Bani Hashim walie kwa sababu ya njaa na kiu. Maquraysh walidhamiria kufanya makusudi ili Banu Hashim waathirike.

Zawadi yenye thamani kubwa sana kwa koo zilizozingirwa katika kipin-di cha miaka mitatu ilikuwa maji. Watu wa koo hizi; wateja wao na watumwa, walipata maji kutoka kwa Khadija. Alimpa Ali vipande vya dhahabu ambavyo alitumia kununua maji. Kuhusika kwake kwa watu waliokuwa pale kulijionyesha kwa namna nyingi. Alimwomba Mwenyezi Mungu Awahurumie. Sala ilikuwa shughuli ya muhimu sana kwake, na ilikuwa ni lengo lake la kuhimili dhiki. Baada ya muda mfupi alitambua kwamba ilikuwa lengo rahisi na lenye umuhimu.

Sala ilimwezesha Khadija kukabiliana na changamoto zisizoepukika kila siku wakati wa kuzingirwa, na alifaulu. Alikuwa malaika kiongozi wa kabila, na kila mmoja alihisi tabia ya kupendeza ya kuwepo kwake na kuungwa mkono na uwezo wa nguvu yake ya kiroho.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٣﴾

" Enyi mlioamini! Jisaidieni (katika mambo yenu) kwa subira na Sala; Bila ya shaka Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaosubiri"Qur'an 2:153.

Khadija alitafuta msaada wa Mwenyezi Mungu kwa uvumilivu na sala. Aliposali, hakupata msaada tu bali, ujasiri, nguvu, amani na utulivu na kutosheka.

الَّذِينَ آمَنُوا وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُم بِذِكْرِ اللَّـهِ أَلَا بِذِكْرِ اللَّـهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ ﴿٢٨﴾ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ طُوبَىٰ لَهُمْ وَحُسْنُ مَآبٍ ﴿٢٩﴾

"(Nao) ni wale walioamini na zikatulia nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Sikilizeni! Kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu nyoyo hutulia. Wale walioamini na kufanya vitendo vizuri raha itakuwa yao, na marejeo mema." Qurani (13:28,29)

A. Yusufu Ali amefafanua "kuneemeshwa" kama ifuatavyo: "Kuneemeshwa: hali ya kutosheka katika nafsi, furaha ya ndani ambayo hujionyesha katika maisha ya mtu mzuri, bila kujali raha na taabu. Na halafu, kila mara huwa kuna lengo la mwisho ambako macho ya mhusika huelekea, Makazi mazuri ya kupumzika huko Peponi, baada ya shughuli za maisha haya (hapa duniani) kwisha. Lengo ni Mwenyezi Mungu Mwenyewe." Katika kumkumbuka Mwenyezi Mungu, Khadija, mtumwa Wake mwenye imani kali, walipata kutoshelezwa na kuneemeshwa.

Mara kwa mara, wale marafiki wachache waliokuwa nao Bani Hashim Makka, walijaribu kupeleka chakula kwa siri kwenye makazi ya muda ya Banu Hashim, lakini wapagani waliwanyang'anya endapo wali-waona. Mmoja wapo wa marafiki wa Banu Hashim huko Makka alikuwa Hashim bin Amr al-Amiri. Alikuwa anawapelekea chakula na maji mara nyingi kadiri alivyoweza. Alijua kwamba kupeleka mahitaji huko kwenye Makazi ni shughuli iliyotakiwa kufanywa kwa siri - tahadhari kubwa, usahihi na bila vurugu. Kwa hiyo, muda aliochagua wa kupeleka chakula na maji kwa Waislamu waliozingirwa, ulikuwa saa chache kabla ya alfajiri. Lakini siku moja wapagani walimkamata na wal-imtishia kumuua kama angeendelea kuwapelekea Bani Hashim mahitaji.

Rafiki mwingine wa Banu Hashim huko Makka alikuwa Hakim bin Hizam, mpwa wa Khadija. Yeye na rafiki yake, Abul Bukhtari, walipeleka mahitaji muhimu kwa Bani Hashim. Siku moja, wote wawili walikuwa wanapeleka chakula na maji na nguo kwa Banu Hashim ambapo Abu Jahl aliwashtukiza na aliwaambia kwamba alikuwa anawanyang'anya ngamia na mahitaji. Abu Bukhtari alijaribu kuele-wana naye lakini hakutaka kusikia lolote. Aliwazuia wasifike kwenye Makazi Mapya ya Waislamu. Abu Bukhtari alijaribu kumpita kwa nguvu. Walipigana ngumi. Ugomvi wa namna hii ulitokea mara kwa mara karibu na makazi lakini marafiki wa Banu Hashim wa Makka hawakukata tamaa, na walijitahidi kila wawezalo kupeleka msaada.

Hashim bin Amr al-Aamiri, na Hakim hawakuwa Waislamu lakini hawakutaka kuona mtoto au hata mtumwa yeyote wa Banu Hashim anaangamia kwa njaa au kiu na walihatarisha maisha yao mara kwa mara kwa kupeleka mahitaji huko Shib Abu Talib. Pia walifurahi kuli-pa gharama za shuguli za kuhami kama hizo kwa miaka mitatu, na wali-chotaka wao ni usalama wa koo zilizozingirwa.

Lazima ieleweke kwamba katika kipindi hiki mahsusi, chuki na hasira za ukoo wa Umayya wa Quraysh hazikuelekezwa kwa Waislamu tu, bali zilielekezwa kwa ukoo wa Banu Hashim. Lengo lao ilikuwa kuangamiza Uislamu bila kumuua Muhammad. Walijaribu mara nyingi kumuua lakini walishindwa kwa sababu hawakuweza kumfikia. Alikuwa salama na mwenye furaha akiwa na ulinzi wa ukoo wake - Banu Hashim.

Kama ilivyo andikwa kwenye kurasa za nyuma, Banu Umayya kwa uhakika walimlenga Abu Talib mkuu wa Banu Hashim, kuwa yeye ndiye aliye sababisha kushindwa kwa vita yao ya kipumbavu dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mjumbe Wake, Muhammad. Kamwe hawakum-samehe kwa yale aliyokuwa anayafanya kwenye jitihada hiyo.

Kwa Waislamu ambao hawakuwa wa ukoo wa Banu Hashim, walikuwa wengi na wote walikuwa wanaishi mjini Makka. Baadhi yao walitangazwa kuwa wenye ushawishi, uwezo na tajiri, na wote walidai kwamba walikuwa wanampenda Mtume wao. Lakini jambo la kushangaza ni kwamba hakuna hata mmoja miongoni mwao aliyekwenda kumuona Mtume au hata kumpelekea msaada wowote. Walifurahia starehe na usalama wa nyumba zao kwa miaka mitatu ambapo Mtume wao, Muhammad Mustafa, aliishi, na aliowapenda, akiyumbayumba, kama ilivyokuwa, kwenye makali ya upanga, akiwa amezungukwa na maadui ambao walikuwa na kiu ya damu yake na wafuasi wake.

Inaweza ikaonekana kama vile familia ndogo ya Khadija yenye mume wake Muhammad Mustafa, mtoto wake mdogo wa kike, Fatima Zahra na mtoto wake wa kambo, Ali bin Abi Talib, waliishi katika hali ya wasi-wasi wakati wote kama watu wengine kwenye ukoo huo, bila kujua kabisa vitisho vya siku iliyofuata au usiku huo. Kila siku ilisongwa na hatari. Lakini hata kidogo hakukosekana kuwa na akiba mpya katika Imani yake na Tabia, kuiimarisha kama kitu kamili. Aligundua kwamba hakuna kitu kingine alichokitaka zaidi ya kujihisi yu karibu na Mwenyezi Mungu. Kwa kujihisi kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, ali-weza kuondoa wasiwasi.

Kwa Khadija, chanzo cha dukuduku kilikuwa njaa na kiu ya watoto. Pale Ali au Hakim bin Hizam au Hashim bin Amr alipokuwa akileta mahitaji kwenye Makazi, yeye (khadija) aliwaangalia. Watoto walimzunguka na aliwapa chakula na maji. Walimtazama kwa furaha na mshangao. Aliyapa kipaumbele mahitaji ya watoto halafu ya wazazi wao, na alishughulikia mahitaji ya wazazi wa watoto kabla ya kwake. Alikuwa na kipaji cha kupanua familia hadi kwenye kabila lote.

وَمَنْ أَرَادَ الْآخِرَةَ وَسَعَىٰ لَهَا سَعْيَهَا وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ كَانَ سَعْيُهُم مَّشْكُورًا ﴿١٩﴾

"Na anayetaka akhera na akazifanyia jitihada amali zake, na hali ya kuwa ni Mwislamu, basi hao jitihada yao (hiyo) itakuwa ni yenye kushukuriwa." Qur'ani 17:19.

Usalama wa koo zilizozingirwa hapo Makazi ya Waislamu haukutishi-wa na Banu Umayyad tu, na si tu na tishio la njaa na maji, lakini pia na joto na baridi kali. Wakati wa siku ndefu wa majira ya kipupwe, anga ilitema cheche duniani, na majabali na miamba ya korongo yalizirudisha zilikotoka, hivyo kufanyiza kitu kama tanuru. Khadija aliwapa maji wenye kiu mara kwa mara kwa kadri alivyoweza ( kujaaliwa). Wakati wa majira ya baridi, usiku mrefu ulikuwa na baridi kali sana. Mama wenye watoto walifanya jitihada nyingi sana bila matumaini kuwalinda watoto wao wasiumizwe na baridi kali. Khadija aliwagawia nguo na kuni..

Hali hiyo ya muda mrefu ilivuruga mwenendo wote wa maisha ya watu wa ukoo wa Hashim na al-Muttalib. Kila siku ilileta mateso ya kutisha au hatari mpya kwao. Lakini hawakukata tamaa. Kwa hakika, walifurahi. Kuwepo kwa Muhammad, kipenzi cha Mwenyezi Mungu, miongoni mwao ilitosha kuwafanya wasahau hofu yao na kuwapa furaha. Walitambua kwamba Mwenyezi Mungu aliwateua wao kwa kazi ya kumlinda Muhammad, Mtume Wake, kutoka kwa maadui zake. Ilikuwa ni heshima ambayo hawangetaka kubadilisha hata kwa kupewa utawala. Khadija aliwatia moyo kwa mfano wake. Utukufu na uwezo wa Imani yake uliwapa msukumo, na walipita kwenye shida nzito za miaka ya uhamishoni kwa heshima na kujiamini.

Khadija alikuwa na furaha kutoka mwanzo wa kuzingirwa hadi mwisho. Roho ya Kweli na Ukarimu ilikuwa maajabu ya utu wake. Alitambua ulinzi wa Mwenyezi Mungu kwa kabila la Banu Hashim, kwa hiyo, lilikuwa salama. Siri ya utulivu wake ipo kwenye aya za Qur'an zifuatazo:

"Basi watakaofuata uongozi wangu huo haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika" Qur'ani 2 : 38;

"Sikilizeni! Vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na khofu (siku ya Kiyama) wala hawahuzuniki" Quran 10: 62

"Hakika wale waliosema: Mola wetu ni Mwenyezi Mungu," kisha wakatengenea, hawatakuwa na khofu (siku ya kufa kwao wala baadaye) wala hawatahuzunika."Quran 46; 13. Maelezo ya Mfasiri.

"Kujitolea na kufanya kazi ya Mwenyezi Mungu husababisha roho kuwa huru na huondoshewa woga na huzuni, kuhusu yaliyopita, yaliy-opo na yajayo, kama tukichukua mfano wa kulinganisha na wakati wa hali isiyo na wakati. Kujitolea huko na kufanya kazi, huonyeshwa na (1) Kuamini Dalili za Mwenyezi Mungu, ikimaanisha kuelewa na kukubali Radhi Yake na (2) kwa kushikamanisha utashi wetu moja kwa moja na Utawala Wake wa ulimwengu, maana yake: kuwa katika mlingano pamoja na hali isiyo na ukomo, na kutenda katika mambo yote ili kuen-deleza Ufalme Wake." (A. Yusuf Ali). Kwa upande wa Khadija hapakuwepo na woga na huzuni. Alionyesha namna Ujumbe wa Mungu ulivyo ndani ya kazi zake za kila siku. Imani ya Khadija, wema na kutoa sadaka ni mambo yaliyojulikana na kila mtu. Hakuna mtu aliyejua kiwango cha uvumilivu wa mateso na uwezo wake wa kuvumilia hadi hapo alipoanza kuishi uhamishoni. Khadija alivumilia usumbufu kwa ukakamavu, na alipambana na hali ya kukata tamaa na kufa moyo, na alishinda.

Maisha ya Khadija yalishikamanishwa na matumaini kama msokoto wa kamba. Matumaini yangetoweka kutoka kwenye mazingira aliyoishi Khadija. Lakini hali hiyo haikumhusu yeye. Matumaini yake yalikuwa hayaonekani lakini yalikuwa yanaambukiza." Yaani yaliwatia moyo watu ambao walikuwa wanakata tamaa.

يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٧١﴾

"Wanashangilia neema ya fadhila za Mwenyezi Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wanaoamini" Qur'ani 3:171.

Khadija alifurahia kwenye Rehema na neema za Mungu na Ukarimu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Alibarikiwa nazo kwa wingi.

Yafuatayo ni maelezo mafupi yaliyokusanywa kutoka vyanzo mbalim-bali, kuhusu kisa cha Muhammad Mustafa na Khadija, na Banu Hashim na Bani al-Muttalib, walipokuwa wamezingirwa huko Shib Abu Talib mwaka 616-619. Mambo mengi muhimu hayakusimuliwa kikamilifu. Lakini yapo matumaini kwamba utafiti wa wataalamu wa historia na wasomi wenye kujitolea kwa dhati utadhihirisha mambo mapya. Mambo haya mapya yatawawezesha wataalamu wa historia ya Uislamu wa siku zijazo kuandika historia iliyokamilika na kueleweka zaidi kuhusu kipindi ambapo Uislamu ulikuwa umezingirwa.

Kuzingirwa kwa Bani Hashim na Bani al-Muttalib kulidumu hadi mwaka wa A.D. 619. Mnamo mwaka huo, koo zote zilirudi jijini Makka. Kuzingirwa kwao na Quraysh hakukufanikisha lengo lililotarajiwa. Watu wa Banu Hashim hawakujali kabisa na ari yao ilikuwa imara. Kwa upande wao, ilikuwa ni jambo lisilofikirika, katika mwisho wa kipindi cha kuzingirwa, kama ilivyokuwa hapo mwanzoni, kumtoa Muhammad - kipenzi chao kwa maadui zake..

Kama Abu Jahl na Banu Umayya walisitisha (waliacha) mpango wa kuwazingira Banu Hashim, haikuwa kwa sababu ya badiliko la moyo lolote lile kwa upande wao; walikuwa makafiri na azma yao mbovu isiy-ojenga, ya kuangamiza Uislamu. Walijaribu kuendeleza mzingiro huo na kuyazunguukia magofu ya Bani Hashim. Lakini walilazimika kusitisha mpango huo kwa sababu palikuwepo na nguvu nyingine inayofanya kazi dhidi yake. Yafuatayo ni maelezo yaliyotolewa katika kitabu cha mwanzo kabisa kilichopo mpaka leo, katika wasifu wa Mtume na Muhammad bin Ishaq, kuhusu matukio ya kilele katika kurudi kwa Banu Hashim na Bani al-Muttalib kutoka Shi'b Abu Talib, baada ya miaka mitatu ya uhamishoni.

Nukuu: "Kusitishwa kwa Mpango wa Kuwasusa Bani Hashim." Bani Hashim na Bani al-Muttalib waliishi mafichoni kwenye mlima baada ya Maquraysh kufanya mapatano ya kuwatenga wao. Halafu, baadhi ya watu ndani ya kundi la Maquraysh walichukua hatua za kuyapinga na kuyakataa mapatano yale. Miongoni mwao, hakuna aliye-jitahidi kumzidi Hisham Bin Amr katika jambo hili kwa sababu alikuwa mtoto wa kaka yake Nadla b. Hashim b. Abd Manaf upande wa kikeni, na alikuwa karibu sana na Bani Hashim. Alikuwa ana heshimiwa sana na watu wake. Wakati koo hizi mbili zilipokuwa uhamishoni, Shi'b mara nyingi alikuwa anawapelekea mahitaji wakati wa usiku kwa kutu-mia ngamia, alipofika mwanzo wa uchochoro aliondoa hatamu na aliusukuma mzigo ambao uliporomoka hadi kwenye makazi. Mara nyengine aliwapelekea nguo kwa kutumia njia hiyohiyo.

Hisham alikwenda kumuona rafiki yake, Zuhayr bin Abu Umayya bin al-Mughira ambaye mama yake alikuwa anaitwa Atika mtoto wa Abdul Muttalib, na alisema; "Wewe unaridhika kula chakula na kuvaa nguo nzuri ambapo unajua hali walionayo wajomba zako? Hawawezi kununua au kuuza au kuoleana. Kwa Jina la Mungu, kama wangekuwa wajomba wa Abul Hakam bin Hisham (Abul Jahl) na ukamwomba afanye kile ambacho amekuambia wewe ufanye, kamwe hangefanya."

Zuhayr alisema "Inashangaza, wewe Hisham, nifanye nini? Mimi nipo peke yangu. Kwa jina la Mungu kama ningekuwa na mtu mwengine wa kuniunga mkono, ningesitisha mgomo huu. "Alisema "Nimekutafutia mtu kwa ajili yako" (mimi mwenyewe)." "Tafuta mwengine;' Zahyr alisema. Hivyo Hisham alikwenda kwa al-Mutim bin Adiy na akamwambia "Wewe unaridhika kwamba koo mbili za Bani Abd Manaf ziangamie ambapo wewe unaafiki kuwafuata Maquraysh? Baada ya muda watakufanya hivyohivyo." Mutim alitoa jibu kama la Zuhyr na akadai mtu wa nne. Hisham alikwenda kwa Abul Bukhtari bin Hisham na akamuomba mtu wa tano na halafu kwa Zamaa bin Al-Aswad bin Al-Muttailb bin Asad, na akamkumbusha kuhusu uhusiano wao wa kindugu na kazi zao.

Alimuuliza endapo wengine walikuwa tayari kushirikiana katika kazi hii, na alimpa majina ya wengine. Wote walisema wangekutana usiku karibu na Hujun nje ya Makka na walipokutana, walikubaliana kutafakari kati ya mkataba na kusitishwa kwake. Siku iliyofuata, wahusika walipokutana pamoja, Zuhary alivaa kanzu na aliizunguuka Al-Kaaba mara saba.

Halafu akawageukia wenzake, akasema: "Enyi watu wa Makka, tutaku-la na kuvaa ambapo Banu Hashim wanaangamia, hawawezi kununua au kuuza? Kwa jina la Mungu sitapumzika hadi hapo uovu huu wa mkataba wa mapatano ya Maquraysh kuwasusa Banu Hashim na Bani al-Muttalib umeharibiwa." Abu Jahl aling'aka: "Umekosea. Hautaharibiwa kamwe." Zama'a alimjibu kwa ukali: "Wewe ndiye unayekosea. Mkataba huu wa udhalimu utaharibiwa. Hatukuutaka hata hapo ulipotayarishwa na kusainiwa."

Abul Bukhtari alisema: "Zama'a yuko sahihi. Hatukuupenda mkataba huu tangu ulipoandikwa na hatuutaki hivi sasa." Al-Mutim aliongeza: " Wote Zamaa na Zuhayr wako sahihi, na yeyote anayesema vinginevyo, anakosea. Tuna mtaka Mwenyezi Mungu awe Shahidi wetu kwamba sisi tunajitoa kwenye jambo hili, na yale yaliy-omo ndani ya mkataba huo." Hisham pia alisema, na aliwaunga mkono marafiki zake. Halafu Al-Mutim alikwenda kuuchukuwa ule mkataba na kuuchana vipande vipande. Alikuta mchwa ulikwisha kula sehemu kubwa isipokuwa maneno: "Kwa jina Lako Ee Mwenyezi Mungu." Huu ulikuwa utaratibu wa desturi na mila za Maquraysh za kuandika mambo yao. Mwandishi wa mkataba alikuwaa Mansur bin Ikrima.

Ifuatayo sio nukuu: Al-Mutim Bin Adiy aliupasua mkataba wa Quraysh vipande vipande. Vipande hivyo vilipeperushwa na upepo na hakuna alama iliyobaki. Kitendo hiki kilikuwa cha imani na ujasiri - imani kwamba Banu Hashim hawakuwa na hatia ila walikuwa wahanga wa dhuluma; na ujasiri kwa kuwadharau Maquraysh. Kitendo chake cha ushupavu ilikuwa dalili kwamba huo ulikuwa mwisho wa kuwasusa Banu Hashim, na kwamba wahusika walikuwa huru kurudi jijini Makka. Mutima yeye mwenyewe na vijana mashujaa wa ukoo wake waliovalia kijeshi walik-wenda kwenye korongo. Walimsindikiza Muhammad Mustafa, Khadija na watu wote wa koo mbili za Banii Hashim na Bani Al-Muttalib, kurudi Makka, na hadi majumbani mwao. Dr. Muhammad Hamidullah ameandika kwenye ukurasa wa 10 wa kitabu chake: Mafunzo ya Awali ya Uislamu.

(Introduction to Islam) kilichochapishwa na International Islamic Federation of Student Organizations, Salimiah, Kuwait (1977). "Baada ya miaka mitatu, watu wanne au watano wasio Waislamu, ambao walikuwa na ubinadamu zaidi kuliko wengine na waliotoka kwenye koo tofauti, walitangaza hadharani kukataa mkataba wa ususaji."

Dr. Hamidullah amehusisha kushindwa kuendelea kwa mkataba wa ususaji wa koo mbili na ubinadamu wa watu wasio Waislamu wanne au watano. Anasema watu hao walikuwa na "ubinadamu zaidi kuliko wengine." Anasema kweli. Watu hao walikuwa na ubinadamu zaidi kuliko wengine ambao hawakuwa Waislamu hapo Makka. Lakini walikuwa na ubinadamu zaidi kuliko hata Waislamu ambao walikuwa wakazi wa Makka? Inashangaza na maajabu," jibu la kihistoria la swali hili lenye kero ni "ndio." Ni hali yenye kejeli. Hata hivyo, zaidi ya hawa watu watano -wote wasio Waislamu - ubinadamu haukumlazimisha mkazi yeyote wa Makka asiye Mwislamu au Mwislamu - kuwadharau Maquraysh na kuwasaidia Banu Hashim! Kuna swali moja zaidi: kwa nini Zuhayr alihisi yupo peke yake?

Hisham alipoanzisha mada ya kusitisha Mkataba wa wapagani kwa mara ya kwanza kwa rafiki yake Zuhayr, alimsuta kwa kutokufikiria matatizo yao, na alimlaumu kwa kushindwa kusitisha tatizo hilo. Zuhayr alisema: "Inashangaza wewe Hisham, nifanye nini? Mimi nipo peke yangu. Kwa Jina la Mungu, kama ningekuwa na mtu mwengine wa kuniunga mkono, ningesitisha mgomo huu." Jibu la Zuhayr ni fumbo. Kwa nini alijihisi hana mtu wa kumsaidia? Hakujua kwamba walikuwemo Waislamu wengi Makka? Kwa nini hakujaribu kuwashawishi ili waondoe tatizo hili? Ilikuwa muhimu kwake kuomba msaada wao. Hata kama wangekataa, hapangeharibika jambo.

Kwa mujibu wa wanahistoria, baadhi ya Waislamu wa Makka walikuwa watu wenye hadhi na mashuhuri na walikuwa na ushawishi katika jamii ya Maquraysh. Lakini kwa sababu zisizoeleweka, haikutokea kwa Zuhayr au rafiki yake yeyote kuwahamasisha Waislamu. Waliamua kuwapuuza Waislamu. Waliendelea na mpango na kuchukuwa hatua za upande mmoja kusikitisha ususiaji kwa Banu Hashim.

Zuhary na marafiki zake walifaulu katika juhudi zao za kuwarudisha Banu Hashim mjini Muhammad Mustafa, Khadija, Ali, Abu Talib na jamaa wengine wote wa Banu Hashim na Bani al-Muttailb, walirudi kwao. Lakini kwa kitendo chao, Zuhayr na marafiki zake walionyesha kwamba Waislamu wa Makka, hawakuwa watu wa lazima kwa Muhammad na Uislamu.

Ni moja ya mafumbo makubwa ya historia ya Uislamu kwamba mkono ambao ulifikia ukuta wa Al-Kaaba na kuung'oa mkataba wa Maquraysh wa kuwatenganisha Banu Hashim, na kuupasua vipande vipande, haukuwa mkono wa "Mumin" bali ulikuwa mkono wa "asiyeamini" -Mutim bin Adiy! Wala hakuna yeyote katika marafiki zake aliyekuwa Mwislamu yaani; Hisham bin Amr, Zuhayr bin Abu Umayya, Abul Bukhtari bin Hisham na Zamaa bin al-Aswad. Lakini wote watano walikuwa watu waliojaa ubinadamu ambao hawakukubali kuonewa kwa Banu Hashim. Hawakupunzika hadi hapo haki ilipotendeka huko Makka. Hawa watu watano wenye msimamo mkali hawakuwa Waislamu kama ilivyo onyeshwa hapo juu. Lakini wao peke yao waliokuwa na ujasiri na busara za kuunga mkono na kutetea kanuni ambazo ni za Kiislamu, yaani; kanuni ya Haki. Walitetea haki na kwa tendo lao la kijasiri wal-ifuzu kupata uzima wa milele katika nyanja za Uislamu.

Kwa upande mwengine si tu kwamba Waislamu hawakuchukuwa hatua yoyote; hata ile ya kupinga dhidi ya ubezi na ukiburi wa Maquraysh. Walidumisha kwa muda wa miaka mitatu mtengo makinifu na ukimya usioshawishika. Wote walikuwa watu wenye busara. Kwa hiyo, yote hayo waliyo yafanya ilikuwa ni kukawiza mambo na kuangalia mwelekeo wa matukio. Bani Hashim walisuswa kwa muda wa zaidi ya siku elfu moja. Kinacho shangaza katika tukio hilo la kugomewa ni kwamba uimara wa Bani Hashim na al-Muttalib haukuonyesha ufa wowote ingawa wakati wote walikuwa kwenye mfadhaiko na wasiwasi kutoka mwanzo hadi mwisho. Quraysh hawakumpata hata msaliti mmoja kwenye koo, hata mtumwa aliyekuwa radhi kuwasaliti mabwana zake; wala hawakuona dalili yoyote ya mtu mwenye moyo mwepesi, hata kwa mtoto mdogo.

Kule Shi'b Abu Talib walikuwepo watu mia nne: wanaume, wanawake na watoto. Watu hao walikuwa wanapata uzoefu wa kuishi uhamishoni wakiwa na Muhammad na Khadija, na hakuna hata mmoja wao aliye-fanya utoro, ama kuokoa maisha yake au kutosheleza njaa na kiu au kuepuka joto na baridi kali au kuepuka kizuizi kisichokuwa na mwisho. Hawakuwa na njia ya kujua vipi na lini, kama ingetokea mwisho wa mgomo huo, na kama ingetokea wao warudi makwao. Uhamishoni siku zilipita kuwa majuma, majuma yalipita kuwa miezi, na miezi kuwa miaka. Kulikuwa hakuna kabisa kitu cha kupoteza matumaini. Na bado matumaini ndicho kitu kilicho waendeleza hadi mwisho.

Inaonyesha kwamba uamuzi wa pamoja, lakini wa kimya kimya wa hawa mashujaa "Mia Nne" ulikuwa ni wa "kuzama au kuogelea" (yaani, kuangamia au kunusurika) pamoja na Muhammad. Waliamua kuwa wafungwa lakini wawe naye Muhammad kuliko kuwa huru lakini asi-wepo. Kwa maoni yao ni kwamba, maisha bila Muhammad hayangekuwa na thamani ya kuishi kabisa. Abu Talib na watu wengine wa Banu Hashim na Bani al-Muttalib waliuona mgomo kama mtihani wa kuwapima kama kweli wanampenda Muhammad. Mgomo ulikuwa pia mtihani kwa hamasa yao, ujasiri wa kimwili na ujasiri wa kimaadili, uthabiti wao, uvumilivu wao usta-hamilivu wao kwenye matatizo, na nguvu zao. Walifuzu mitihani yote. Mwenyezi Mungu alikabidhi usalama binafsi wa Muhammad MustafaMjumbe Wake, kwao. Walikuwa na msimamo wa kumlinda yeye na walileta utukufu na heshima kwenye msimamo wao.

Katika miaka mitatu ya uhamishoni, utajiri mwingi wa Khadija ulik-wisha. Sehemu kubwa ya utajiri huo ulitumika kununua maji. Alifurahi kwamba utajiri wake ulikuwa njia ambayo Mwenyezi Mungu aliokoa maisha yenye thamani sana katika Uumbaji wote - maisha ya Muhammad Mustafa na Ahlul Bayt - na alimshukuru kwa kumpa yeye heshima hii. Katikati ya misukumo na mabadiliko yaliyomzunguka Khadija, imani ilibakia katika kiwango hichohicho na iliendelea kuwa chanzo cha nguvu isiyo shindwa kwake na wale aliokuwa nao. Imani yake iliendelezwa na sala kama ilivyoonyeshwa huko nyuma. Imani ya Khadija ilikuwa kitu kinachoonekana na kuguswa. Wakati wote alikuwa anawasiliana na Mwenyezi Mungu - kwa njia ya sala ambayo ndio chanzo cha Imani. Pia sala ilikuwa ndio siri ya ujasiri wake wa kimya kimya. Tabia yake ya amani na utulivu popote alipo, haikuruhusu imani ya kabila kudhoofika wakati wote wa mgomo. Alikuwa kama nanga ya meli ya kabila lote katika miaka yote ya fujo na majonzi.

Kushindwa kwa kugomewa Banu Hashim na Bani al-Muttalib, na wapa-gani wa Makka, na kurudi kwa koo mbili majumbani mwao, ilikuwa njia panda katika historia ya Uislamu. Ilikuwa uthibitisho wa uhakika na nguvu ya imani mpya. Mwanzoni mwa mgomo, wapagani walikuwa na uhakika kwamba wal-iumaliza Uislamu na kwamba sasa ulitegemea huruma yao. Juhudi zao za kufutilia mbali Uislamu hazikuwa nusu nusu au za hapa na pale, na hawakutaka kubahatisha. Walining'iniza tishio la njaa mbele ya koo zilizosuswa. Walidhani kwamba wakati wa mabalaa mawili kwa wakati mmoja unaoendelea, yaani njaa na kiu, na hali ya hatari inayoendelea, upinzani wa koo zilizogomewa nao, ungelazimika kumuwasilisha Muhammad kwao (wapagani). Bila shaka, uvumilivu wa binadamu una upeo wake, njaa na kiu isiyo na mwisho ni njia rahisi ya kudhoofisha imani ya mtu, hata kama angekuwa jasiri namna gani. Lakini wapagani hawakujua kwamba imani ya Banu Hashim kwa Mwenyezi Mungu ilikuwa na nguvu zaidi kuliko woga wa njaa na kiu na kwa hakika ilikuwa na nguvu zaidi kuliko woga wa kifo.

Watu wa ukoo wa Banu Hashim hawakuwa na woga wa kifo. Wakati Muhammad Musatafa aliposimamisha Bendera ya Tauhid na kuwasha Taa ya Imani humo Arabuni, mara moja alipewa changamoto na waabuduo masanamu. Waabudu masanamu walichukia kuona Bendera ya Tauhid inapepea hadi upeo wa macho na walipeleka vikosi vyao kwa msongamano ili waing'oe. Lakini vikosi hivyo vilikuta Bendera imezunguukwa na kulindwa na wana wa Banu Hashim. Bendera ilizunguukwa na walinzi na katika kuilinda ilibidi wadharau kifo kila sekunde! Vikosi vilifanya mashambulizi makali mara nyingi dhidi ya Bendera lakini wapiganaji hao walirudishwa nyuma. Wana wa Banu Hashim waliwashinda na kuwafukuza maadui. Taa ya Imani iliyowashwa na Muhammad Mustafa ilitishiwa na dhoru-ba ya upagani na ushirikina. Lakini wana wa Banu Hashim walifaulu kuilinda taa hiyo. Upagani ulitumia nguvu zake zote kuizima taa hiyo na ulishindwa.

Katika kulinda Bendera ya Tauhid na Taa ya Imani wapiganaji wengi wa Banu Hashim walikufa. Lakini kama ambavyo imeandikwa kwenye kurasa za nyuma, askari wa Banu Hashim hawakuogopa kifo. Tauhid na Imani ni vitu vilivyokuwa na thamani zaidi kwao kuliko uhai wao. Walijivunia kifo wakiwa wanailinda Tauhid na Imani. Waliamini kwamba bendera na Taa vyote vilikuwa urithi wenye thamani kubwa, na ilikuwa ni kazi yao ya kuheshimiwa sana kuvilinda vitu hivyo, na walifanya hivyo. Abu Jahl na Banu Umayya walifanya majaribio yasiyohesabika kuuzima mwanga wa Uislamu. Lakini walishindwa. Mwanga wa Uislamu uliangaza zaidi wakati wote. Wangewezaje kuuzima ambapo ulikuwa na walinzi wanao onekana na wasio onekana. Kama Banu Hashim walikuwa walinzi wa mwanga wa Uislamu walioonekana, Mwenyezi Mungu alikuwa Mlinzi wake. Asiye onekana. Kama tunavyosoma kwenye aya zifuatazo za Qur'an 9:32,33.

يُرِيدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّـهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ ﴿٣٢﴾

"Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, lakini Mwenyezi Mungu amekataa isipokuwa kuitimiza nuru yake ijapokuwa makafiri wanachukia." Qur'ani 9:32.

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ ﴿٣٣﴾

"Yeye ndiye aliyemleta mtume wake kwa uongofu na Dini ya haki ili ajaalie (dini hii) kushinda dini zote; ijapokuwa watachukia hao washirikina." (Quran 9:33).