MAISHA YA BIBI KHADIJA

MAISHA YA BIBI KHADIJA0%

MAISHA YA BIBI KHADIJA Mwandishi:
Kundi: Waheshimiwa wa Kidini

MAISHA YA BIBI KHADIJA

Mwandishi: Syed A .A .Razwy
Kundi:

Matembeleo: 8467
Pakua: 640

Maelezo zaidi:

MAISHA YA BIBI KHADIJA
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 16 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 8467 / Pakua: 640
Kiwango Kiwango Kiwango
MAISHA YA BIBI KHADIJA

MAISHA YA BIBI KHADIJA

Mwandishi:
Swahili

8

MAISHA YA BIBI KHADIJA

SURA YA KUMI NA MBILI

KIFO CHA KHADIJATUL KUBRA NA ABU TALIB A.D. 619.

Mashujaa watano wa Makka waliukanyaga mkataba wa Maquraysh wa kuwasusia Banu Hashim. Shukurani kwa uungwana na ushujaa wao, Bani Hashim wameweza kurudi mjini, na kuishi kwenye nyumba zao kwa mara nyingine tena. Lakini, kabla hata hawajatulia na kuanza kusa-hau ugumu wa maisha ya maficho ya milimani kwa miaka mitatu, Khadija, mke, sahaba na rafiki wa Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mfadhili wa Uislamu na Waislamu aliugua. Ugonjwa wake ulikuwa wa muda mfupi lakini wa kufisha. Maisha yake yote aliyoishi katikati ya maisha ya kujitosheleza na ya anasa, lakin miaka mitatu aliyoishi uhamishoni ulikuwa wakati wa kushikilia sana maadili kwake ambao bila kuepukika uligharimu maisha yake.

Kama ambavyo imeandikwa kwenye kurasa za nyuma, Khadija alikuwa mwanamke wa kwanza kutangaza kwamba Muumbaji ni Mmoja na kwamba Muhammad alikuwa Mjumbe Wake. Utukufu na heshima ya kuwa Muumini wa Kwanza duniani pote, ni yake daima.

Wakati Uislamu ulipoanza kupata upinzani mkali kutoka kwa maadui zake, Khadija alijitolea kwa kusahau raha zake zote, utajiri na familia yake ili auhami Uislamu, na sasa ilionyesha kama vile alikuwa tayari kuyatoa mhanga maisha yake. Bila shaka kama angeishi kwenye nyum-ba yake ya starehe Makka, akiwa amezungukwa na watumishi wake, labda angeishi kwa miaka mingi. Lakini alipendelea kumsaidia mume wake na ukoo wake na kushiriki maisha machungu pamoja nao. Kipindi cha kuzingira Waislamu, si tu kwamba alivumilia uchungu wa njaa na kiu, bali na joto kali la kiangazi na baridi ya majira ya kipupwe, hata hivyo hakulalamika kwa mumewe kwa hayo yote. Ima hali iwe nzuri au mbaya; mahitaji ya kutosha au hakuna kabisa kitu, wakati wote alikuwa na furaha. Hali mbaya ya maisha na ufukara kamwe havikumkatisha tamaa. Mwenendo huu ndio ulikuwa chanzo imara cha raha, ujasiri, umadhubuti wa mume wake wakati mbaya sana katika maisha yake.

Katika kipindi cha kuzingirwa Waislamu. Khadija alitumia utajiri wake wote kwa kununua mahitaji muhimu kama chakula na maji kwa ajili ya ukoo wa mumewe. Aliporudi nyumbani kwake Makka, senti yake ya mwisho ilikwishatumika na alipofariki dunia hapakuwepo hata hela ya kununua sanda. Joho la mume wake lilitumika kama sanda.

Muhammad Mustafa kamwe hakuoa mke mwingine wakati wa uhai wa Khadija, na kama asingekufa, uwezekano ni mkubwa kabisa kwamba hangeoa kabisa. Endward Gibbon Katika kipindi cha miaka 24 cha ndoa yao, mume wa Khadija ambaye alikuwa bado kijana aliepusha na haki ya mitala, na fahari au upendo wa mjane kamwe haukufedheheshwa na jamii ya upinzani. Baada ya kifo chake, Mtume alimweka kwenye daraja la wanawake wanne ambao ni bora zaidi, dada wa Musa, mama wa Isa (Yesu) na Fatima, binti yake aliyependwa sana. (The Decline and Fall of the Roman Empire) Muhammad bin Ishaq, mwandishi wa maisha ya Mtume, anasema kwamba wakati Wahyi kutoka kwa Mungu uliponza tena baada ya kuko-ma kwa muda baada ya kutembelewa mara mbili na malaika Jibril katika pango la Hira, Khadija alipokea sifa na salamu za amani kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t). Ujumbe uliwasilishwa na malaika Jibril kupi-tia kwa Muhammad, na alipoufikisha ujumbe kwa Khadija alisema: "Mwenyezi Mungu ni Amani (as-Salaam), na Amani yote hutoka kwake na amani iwe kwa Jibril."

Muhammad alimkumbuka Khadija katika uhai wake kwa hisia za mapenzi, shukrani na upendo. Wakati Khadija anaugua, usiku kucha hakulala kwa kumuuguza, kumliwaza na kumwombea. Mumewe alimwambia kwamba Mwenyezi Mungu alimuahidi furaha kamili ya Milele na alikwisha mjengea kasri ya kifalme yenye kuta za lulu huko Peponi. Ilipokaribia asubuhi mwili wake uliodhoofika haukuweza kuhimili mauvivu ya homa na roho yake iliyotakaswa na uadilifu ilion-doka hapa duniani na kuelekea kwenye kituo chake - Mbinguni ambapo iliingia kwenye kundi la walio hai milele. Kifo chake kilimhuzunisha Muhammad sana.

Khadija alifariki tarehe kumi mwezi wa Ramadhani mnamo mwaka wa kumi baada yakutangazwa Uislamu. Khadija alizikwa Hujun sehemu ilioko jirani na Makka. Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, aliteremka ndani ya kaburi na kulala humo kwa dakika chake. Halafu akawasaidia waombolezaji wengine kuuteremsha mwili kaburini. Baada ya maziko alisawazisha ardhi juu ya Kaburi lake (Khadija). Kwa hiyo, Khadija alikufa akiwa mwanamke wa kwanza kuamini Upweke wa Muumbaji.

Amani iwe kwa Khadija ambaye alipelekewa salamu za amani na Mwenyezi Mungu (s.w.t). Amani iwe kwa Khadija ambaye alijengewa kasri ya kifalme yenye kuta za lulu huko Peponi. Amani iwe kwa Khadija, mbora sana miongoni mwa wanawake, na mkuu wa wanawake wote. Khadija alifariki mwaka wa 619 A.D. Mwezi mmoja baada ya kifo chake, Muhammad Mustafa alipata mshtuko mwengine wa kifo cha Abu Talib, ami yake na mlezi wake na ngao ya Uislamu. Kifo cha hawa marafiki wawili-Khadija na Abu Talib - kilikuwa mshtuko mkubwa zaidi ambao Mtume wa Mungu alitakiwa avumilie katika miaka hamsi-ni ya maisha yake. Taa mbili za maisha yake zilizimika. Alizidiwa na huzuni. Aliuita mwaka wa vifo vyao "Mwaka wa Huzuni."

Mwaka wa 619 uligeuka kuwa mwaka wa huzuni kwa Muhammad Mustafa katika maana mbili. Kifo cha mpendwa wa wastu kwa kawaida ni tukio la huzuni. Lakini kwa hali ya Muhammad, kifo cha hawa marafiki wawili haikuwa tu tukio la huzuni kwake. Haikupita muda mrefu alifanywa atambue maana ya vifo vyao, kwa mfululizo wa matukio tofauti tofauti. Muhammad bin Ishaq. Khadija na Abu Talib walikufa mwaka mmoja, na kwa kifo cha Khadija matatizo yalikuja kwa haraka moja baada ya lingine. Alikuwa muumini wa kutegemewa naye katika Uislamu, na alikuwa anamsimulia kuhusu matatizo yake. Pamoja na kifo cha Abu Talib alipoteza chanzo cha nguvu ya maisha, ulinzi wa kabila lake. Abu Talib alifariki miaka mitatu kabla ya Muhammad hajahamia Madina, na hapo ndipo Maquraysh walipoanza kumfanyia mambo mabaya ambayo hawangeyafanya wakati wa uhai wa ami yake.

Kijana baradhuli alimtupia Mtume mchanga kichwani. Hisham kutoka kwa baba yake, Urwa, aliniambia kwamba Mtume aliin-gia nyumbani mwake na alikuwa anasema: Maquraysh kamwe hawaku-nifanyia hivi kabla Abu Talib hajafa." (The Life of the Messenger of Allah) Washington Irving. Baada ya kipindi kifupi, Muhammad alitambua hasara aliyopata kutokana na kifo cha Abu Talib. ambaye hakuwa tu ndugu mwenye upendo bali mlinzi madhubuti mwenye nguvu, kutokana na ushawishi wake mkubwa kule Makka. Baada ya kifo cha Abu Talib hapakuwepo mtu ambaye angezuia uchokozi wa Abu Sufian na Abu Jahl.

Mafanikio ya Muhammad yalianza kufifia pale Makka. Khadija, mfad-hili wa kwanza, swahiba wake aliyejitolea katika faragha na upweke wake, muumini mkereketwa wa imani yake, alikufa; vivyo hivyo Abu Talib, ambaye alikuwa mlinzi wake mwaminifu na makini. Kwa kukoseshwa kinga yenye ushawishi ya Abu Talib, Muhammad katika hali hiyo, alikuwa kama mtu mhalifu mjini Makka, aliwajibika kujificha na kuwa mzigo wa wema wa watu ambao imani yake mwenyewe ili-waingiza kwenye mateso (sic*). Kama manufaa ya dunia yangekuwa ndio lengo lake, aliweza vipi kufanikiwa? (The Life of Muhammed) Washington Irving amekosea kwa kusema kwamba Muhammad "alikuwa mzigo wa wema wa watu ambao imani yake mwenyewe ili- *Sic- Japo kwa makosa. Maana yake ni kukataa maneno ya mwandishi aliyenukuli-wa waingiza kwenye mateso."

Kamwe Muhammad hakuwa mzigo kwa yeyote. wakati wowote. Watu wa ukoo wake Bani Hashim waliona fahari na upendeleo kumlinda yeye na kuutetea Uislamu, vyote hivi vilikuwa hazina yao kubwa mno. Walitambua kwamba akiwepo Muhammad miongoni mwao, walikuwa wapokeaji wa neema za Peponi na hawakuwa na nia ya kuzipoteza neema hizo kwa jinsi yoyote ile. Ni nani mwengine isipokuwa ukoo wa Banu Hashim ambaye angemlin-da Muhammad na Uislamu? Muhammad alikuwa musuli na damu yake, na Uislamu ulikuwa uhai na mapenzi yake. Kosa lingine ambalo mtaalamu huyu mashuhuri wa historia amelifanya lipo ndani ya swali ambalo ameliuliza: "Kama manufaa ya dunia yangekuwa lengo lake, aliweza kuyapata jinsi gani?"

Manufaa ya dunia hayakuwa madhumuni ya Muhammad. Quraysh walikuwa tayari kumpa yeye manufaa ya dunia; walitaka kumpa utajiri, utawala na starehe. Vyote hivyo wangempa kama angevitaka. Lakini alivikataa katakata. Je, wangeweza kumpa chochote kingine zaidi ya hivyo? "Muhammad alikuwa na lengo moja tu, nalo ni kufanya kazi aliyoamri-wa na Mwenyezi Mungu (S.w.t), yaani kutangaza Uislamu - Dini ya Mwenyezi Mungu" Sir William Muir. Kujitoa muhanga ambako Abu Talib na familia yake walifanya kwa ajili ya mpwa wake, ingawa bado hajasadiki ujumbe wake, ameikiri tabia yake kuwa ni nzuri ya kipekee na ni mkarimu si mchoyo na mbinafsi. Hapo hapo wanadiriki kuhoji uthibitisho madhubuti wa uaminifu wa Muhammad. Abu Talib hangefanya hivyo kwa mpenda uwongo; na alikuwa na njia nyingi za kuchunguza. (The Life of Muhammed, London, 1877) Sir William Muir anasema kuhusu jambo hili: "Kama kweli isingekuwa kwa sababu ya ushawishi na ulinzi mkali wa Abu Talib, ni dhahiri kwamba nia ya uchokozi wa Maquraysh inge- hatarisha uhuru na pengine uhai wa Muhammed." (The Life of Muhammed, London, 1877).

Turji Zaydan. Sababu iliyomfanya Abdul Muttalib amshawishi Abu Talib kufanya kazi ya kumlea Muhammad, ilikuwa, Abu Talib na Abdullah walikuwa wato-to wa mama mmoja. Bila shaka, ulinzi wa Abu Talib ulikuwa sababu kubwa, si tu kwa ushindi wa ujumbe wa Muhammad lakini pia kwa sababu ya usalama wake mwenyewe. Abu Talib alikuwa na hadhi kwa Maquraysh, na mtu mwenye kuheshimika sana. Muhammad aliishi ndani ya nyumba yake kama mmojawapo wa watoto wake... (Complete Works, published by Dar. ul-Jeel, Beirut, Lebanon, Volume 1 page 91, 1981).

Luteni Generali Sir John Glubb ameandika kwenye kitabu chake, the Life and Times of Mohammad. Kwamba Abu Talib hafikiriwi na Waislamu kuwa shujaa kwa sababu alikufa kabla hajasilimu. Lakini anaongezea, "Hata hivyo, kama isingekuwa kwa ujasiri wa kumlinda mpwa wake, inawezekana Uislamu ungesambaratika ukiwa katika siku zake za mwanzo. Wote wawili, Sir William Muir na Sir John Glubb na wataalam wengine wengi wamejiingiza katika kusema kwamba Abu Talib alikufa kabla hajasilimu. Kama wakitakiwa kuthibitisha madai yao wangekimbilia kwenye maandishi ya Imam Bukhari. Bukhari anasema kwenye "hadithi" yake kwamba; wakati Abu Talib alipokuwa taabani kitandani, Mtume alimsisitizia asilimu, lakini alisema kwamba kufanya hivyo kungemuaibisha yeye na rafiki zake Maquraysh. Waandishi wa "hadithi" hii walisahau kitu kimoja. Abu Talib alikuwa anakufa na alijua kwamba hangewaona tena rafiki zake, Maquraysh.

Alitambua kwamba alikuwa anakwenda kukutana na Muumba wake. Kwenye kipindi kama hiki hangewajali Maquraysh. Shauku yake wakati wote ilikuwa kufuzu kumfurahisha Mwenyezi Mungu. Alithibitisha hilo kwa vitendo vyake zaidi kuliko mtu mwingine yeyote ambaye angeweza kuthibitisha kwa maneno yake kwamba imani yake kuhusu Upweke wa Mungu na kwenye ujumbe wa Muhammad kama mjumbe Wake, ilikuwa imani imara thabiti na ngumu kama mwamba usiotikisika.

Amin Dawidar, mtaalam wa historia wa zama za sasa wa Misri, anase-ma kwamba Abu Talib alikuwa kama ngome ya Muhammad ambayo ilimhifadhi yeye (Muhammad) kutokana na joto lote na baridi yote na shutuma na ukaidi wa walimwengu. "Na Abu Talib alipofariki," anase-ma: "Muhammad alijikuta ana kwa ana na adui kwa mara ya kwanza katika maisha yake. Bila shaka, kifo cha Abu Talib kilikuwa msiba kwake." Hakuwa na lingine la kufanya ila Abu Talib aliamua kuwa Mwislamu na Muumini. Hakuna mtu anayeweza kumpenda Muhammad na masana-mu kwa wakati mmoja; mapenzi hay a mawili hayaendi pamoja hata kidogo. Na hakuna mtu anayeweza kumpenda Muhammad na auchukie Uislamu. Kumpenda Muhammad na kuchukia Uislamu ni vitu visivy-oweza kuwekwa pamoja. Yeyote anayempenda Muhammad, lazima apende Uislamu. Kama kuna kitu chochote kisichokuwa na shaka katika historia ya Uislamu, ni mapenzi ya Abu Talib kwa Muhammad. Kama ambavyo imeandikwa kwenye kurasa za nyuma, Abu Talib na mke wake, walimpenda Muhammad zaidi ya walivyowapenda watoto wao. Mapenzi hayo yalikuwa na chemchem moja tu - yaani kukubali kwamba Uislamu chanzo chake cha asili ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Abu Talib alijivuna kwamba Mwenyezi Mungu alimteua Muhammad mtoto wa ndugu yake, Abdullah, katika Uumbaji wote, kuwa awe mjumbe Wake wa mwisho na Mjumbe mkubwa kabisa kwa watu wote. Muhammad alikuwa pendo kubwa kabisa na fahari kubwa kabisa ya ami yake, Abu Talib.

Kwenye Kitabu Chake, Mwenyezi Mungu (s.w.t) alitambua mwenyewe ulinzi ambao Abu Talib alimpa Muhammad Mustafa, kama ulinzi wake mwenyewe kama isemavyo Aya ifuatayo:

أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَآوَىٰ ﴿٦﴾

"Je! Hakukukuta yatima akakupa makazi (mazuri ya kukaa)" Qur'ani 93:6

Mwenyezi Mungu alimpa ulinzi na ulezi (uangalizi) Mtume Wake Muhammad Mustafa, kupitia kwa mtumishi Wake Abu Talib.

Abu Talib alifanya kazi Makka kwa ajili ya Utukufu na Uwezo wa Uislamu na alikuwa mlezi wa maadili. Kwa muda wa miaka 10 alikien-desha chombo cha Uislamu wakati wa ujinga na matatizo mbali mbali kwa ustadi, akiona mbali na imani ambayo iliwakasirisha walezi wa masanamu ya wapagani wa Arabuni. Matendo yake ni sehemu muhimu ya simulizi ya Uislamu, pia ni uthibitisho usiopingwa wa imani yake kwa Mwenyezi Mungu na mjumbe Wake - (imani ) ya Uislamu. Mwenyezi Mungu na awabariki waja wake wapendwa, Khadija na Abu Talib. Wote wawili waliuweka utii kwake Yeye mbele kuliko kitu cho-chote kingine katika maisha.

9

MAISHA YA BIBI KHADIJA

SURA YA KUMI NA TATU

KHADIJA MAMA WA WAUMINI KABLA YA UISLAMU

Khadija alikuwa Malkia wa Makka. Wakati jua la Uislamu lilipochomoza juu ya upeo wa macho, Mwenyezi Mungu ali-furahi kumfanya pia Malikia wa Uislamu. Mwenyezi Mungu pia alifu-rahishwa kumfanya yeye Mama wa Waumini, kama Asemavyo kwenye Kitabu chake.

النَّبِيُّ أَوْلَىٰ بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنفُسِهِمْ وَأَزْوَاجُهُ أُمَّهَاتُهُمْ ﴿٦﴾

"Nabii yu karibu zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao wenyewe, na wakeze ni mama zao. (33:6).

Maelezo ya mfasiri "Sura hii ya (33) inathibitisha hadhi na nafasi ya wakeze Mtukufu Mtume, ambao walikuwa na ujumbe maalum na wajibu kama Mama wa Waumuini. Hawakutakiwa kuwa kama wanawake wa kawaida: wali-takiwa kuwaelekeza wanawake katika mambo ya kiroho, kuwatembelea na kuwasaidia wagonjwa au wenye dhiki, na kufanya mambo mengine mema katika kusaidia ujumbe wa Mtume." (A.Yusuf Ali) Cheo cha Mama wa Waumini kinaonyesha kutayarishwa hususani kwa ajili ya Khadija. Bila Khadija, cheo hiki hakina maana. Yeye na yeye peke yake alionyesha mapenzi ya dhati ambayo yanatolewa na mama tu kwa waumini. Mama anaweza kuwa anahisi njaa lakini kama watoto wake wana njaa, atawapa chakula watoto wake kwanza. Kwa hakika, kama ni muhimu katika hali ya dharura atawalea na njaa huku akifurahi. Hali hii imetokea mara nyingi katika historia, hasa zaidi wakati wa vita na njaa. Ni jambo la uhakika kwamba watoto walioshiba na kutosheka, inatosha kumfanya mama afurahi na kutosheka, inatosha kumfanya yeye (mama) asahau njaa na kiu yake. Mapenzi ya mama hayana shar-ti; yanalenga hali zote na kujumuisha wote.

Waislamu walio wengi Makka walikuwa masikini. Hawakuwa na vyan-zo vya mapato, na walikuwa hawana namna ya kuwawezesha kujipatia riziki kwenye jiji ambalo uchumi wake ulikuwa mikononi mwa makun-di ya siri ya waubudu masanamu. Wanachama wa makundi ya siri wal-itoa agizo kwamba Mwislamu asilipwe ujira wowote kwa kazi yoyote atakayofanya na ni marufuku kununua kitu chochote kutoka kwake. Walitambua kwamba ufukara wa mali uliathiri vibaya mwili na roho na walidhani kwamba wakati upinzani wa Waislamu utakaposhindwa, kutokana na kudhoofika kiuchumi, wangeukana Uislamu, na wangemkataa Muhammad. Lengo la sera hii ilikuwa ni kuwanyima chakula Waislamu. Lakini Khadija aliwalisha Waislamu masikini kila siku, hivyo kwamba hakuna hata mmoja miongoni mwao aliyedhikika kwa njaa, na aliwapa mahali pa kukaa. Kwake yeye, utoaji wa sadaka halikuwa jambo jipya lakini kipimo na uwezo wa msimamo ilikuwa kama ifuatavyo: alitumia fedha nyingi mno kwa ajili ya masikini na Waislamu wa Makka wasiokuwa na nyumba, hivyo alikwamisha mpango wa matajiri wa Makka waabuduo masanamu.

Msaada ambao Khadija aliutoa kwa jamii ya Waislamu wa Makka, ulikuwa muhimu kwa uhai wa Uislamu. Msaada wake kwa jamii ya Waislamu ulihakikishia uhai wa Uislamu wakati ulipokuwa katika hali ya mkwamo. Katika hali hii, alikuwa mtengenezaji wa historia - histo-ria ya Uislamu. Wake zake Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wote ni kina Mama wa Waumini; lakini kuna tofauti kubwa kati yao na Khadija. Wanawake wote walioolewa na Mtume Muhammad huko Madina walipokea ujira kutoka Hazina ya Umma. Baadhi yao walidai haki maalumu na marupurupu kutoka kwake. Walisema kwamba haki maalum zilizolipwa zilikuwa hazitoshi kwa mahitaji yao. Kwa upande mwengine, Khadija kamwe hakuomba kitu chochote kuto- ka kwa mume wake. Khadija aliamua mali yake iwe Hazina ya Umma kwa ajili ya Waislamu. Hapo Makka hapakuwepo Hazina ya Umma, ilikuwa ukarimu usio na mpaka na utajiri mwingi wa Khadija ambao ndio uliiokoa Jamii ya Waumini. Alikuwa anajihusisha sana na ustawi wa wafuasi wa mume wake, hivyo kwamba aliridhika kutumia fedha zake zote kwa madhumuni haya.

Mwenyezi Mungu ambariki mtumishi Wake, Khadija, Mama wa Waumini zaidi na zaidi. Khadija kama Mama. Dk. Sir Muhammed Iqbal (d. 1938) alikuwa Mshairi Mwana falsafa wa Indo Paksitan. Pia alikuwa kichocheo cha mwamko wa Waislamu karne ya 20. Anasema kwamba, mama anashika nafasi ya pili baada ya Mungu Mwenyewe.

Mama analeta maisha mapya hapa duniani, yaani anaumba; na tendo hilo tendo la kuleta maisha mapya hapa duniani au tendo la kuumba, linamtaka mtu ajitolee muhanga. Katika kuleta maisha mapya hapa duniani, mama huyaweka maisha yake hatarini. Kwa hiyo, mama anastahili hadhi na heshima kubwa sana. Kinachomfanya mama ayatoe muhanga maisha yake ni mapenzi-mapenzi kwa mwanawe.

Mapenzi kwa mwanawe ni mapenzi yaliyotakasika. Kwenye utakatifu, mapenzi ya mama kwa mwanae yanashika nafasi ya pili baada ya mapenzi ya Mungu Mwenyewe. Khadija alikuwa mama aliyejivunia watoto watatu - watoto wanaume wawili na mwanamke mmoja, kama ilivyokwisha onyeshwa huko nyuma. Watoto wawili wa kiume - Qasim na Abdullah walifariki dunia wakiwa wachanga. Mtoto wake wa mwisho na ndiye tu aliyebaki katika kuishi alikuwa Fatima Zahra. Kama Khadija alikuwa mama bora, Fatima Zahra alikuwa binti bora. Fatima Zahra, binti bora wa Muhammad Mustafa na Khadija, naye pia alipata kuwa mama bora. Alikuwa mama wa watoto wa kiume wawili -Hasan na Husain - na mabinti wawili- Zainabu na Umm Kulthum.

Khadija na Fatima Zahra - mama na bintiye - walikuwa wawili miongo-ni mwa wanawake wanne walio bora hapa duniani. Wote wawili wali-fanya umama utakasike. Waliufanya umama utukuke na kuheshimiwa. Kama ambavyo imesemwa huko nyuma, katika kitabu hiki wanawake hawakuwa na hadhi kabla ya Uislamu huko Arabuni. Kwenye jamii iliy-otawaliwa na mfumo dume walikuwa wana dhulumiwa kikatili na wal-ifanyiwa mambo kama wanyama. Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alikomesha dhuluma ya wanaume kwa wanawake, na aliwapa hadhi ambayo wanawake walikuwa hawajapewa katika nchi yoyote na wakati wowote. Kuhusu wakina mama alisema: "Pepo ya mtu ipo chini ya miguu ya mama ."

Maana yake ni kwamba hakuna mtu anayeweza kuwa na matumaini ya kupata pepo kama amemkasirisha mama yake. Mtu kuipata pepo lazi-ma awe na uwezo wa kufuzu kuupata wokovu, na hakuna mtu ambaye amemkasirisha mama yake akaupata wokovu. Hivyo Mtume wa Uislamu amefanya mtu kufuzu kupata radhi ya mama - mwanamke - sharti linalo tanguliwa kabla mtu hajapata wokovu na kuingia peponi.

SURA YA KUMI NA NNE

KHADIJA, MWANAMKE MKAMILIFU

Kumekuwepo na wanawake wengi katika historia ya ulimwengu huu ambao walipata kuwa wakubwa na maarufu kwa sababu ya matendo yao makubwa. Jamii ya kibinaadamu inaweza kujivunia kwa haki kabisa kutokana na (wanawake) hawa.

Lakini katika historia ya ulimwenguni wote, wako wanawake wanne tu ambao wangeweza kufikia vipimo vya daraja ya juu vya ukubwa wa kweli na ukamilifu uliowekwa na Uislamu. Walifikia kwenye vipimo hivi kutokana na huduma zao kubwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Muhammad Mustafa, Mtume wa Uislamu, Mpokeaji wa Ufunuo (Wahyi) kutoka mbinguni, na Mfasiri wake, aliwatambua. Nao ni:

1. Asiya, mke wa Firauni,

2. Maryam, mama wa Isa, (Yesu)

3. Khadija, binti wa Kuwaylid na

4. Fatima Zahra, binti ya Muhammad Mustafa(s.a.w.w)

Muhammad Mustafa aliwaona wanawake wanne tu walio bora katika jamii ya dunia nzima. Baina ya hao wanne, wawili wa mwisho wanato-ka nyumba moja; wao ni Khadija, mama wa Fatima, na binti yake, Fatima. Khadija alikuwa mfano kwa roho iliyo bora na iliyokamilika.

Katika jamii iliyosalia hapa duniani, wanawake wengine tu ambao wanaweza kufuzu kuwa wanawake wenye sifa ya ubora, wangekuwa ni wake zake wengine wa Muhammad Mustafa. Lakini yeye mwenyewe alitoa hukumu kuhusu jambo hili, na hukumu yake haifutiki haibadili-ki. Alimtaja Khadija tu miongoni mwa wake zake kwamba ni mwanamke bora, na kwa hiyo aliwatenganisha - kwa amri wake zake wengine kutoka kwenye kundi la wanawake bora. Khadija alikusanya katika utu wake sifa zote hizo zinazo mfanya mtu kuwa bora. kama angepungukiwa na yoyote katika sifa hizo, mume wake hangemweka kwenye kundi la walio bora. Na hakuna ushahidi wowote kwamba alikuwa na kasoro hizo, ambazo zinasemekana kwa kanuni kuwa ni tabia za kimaisha ya wanawake. Tabia mojawapo ya udhaifu wa wanawake ni wivu. Khadija hakuwa na wivu wa aina yoyote. Alikuwa mwanamke aliyeona ukamilifu, furaha na kutosheka katika kutoa msaada. Alikuwa mlezi karimu wa masikini. Alikuwa anajisikia mwenye raha wakati anawapa chakula wenye njaa na huzuni. Matendo ya kuwalisha na kuwaliwaza wenye njaa na huzuni haikulazimu juhudi ya dhamira kwa upande wake; kwake matendo hayo yalikuwa kawaida yake.

Kama vile ambavyo Khadija alivyokuwa hana wivu, pia alikuwa habezi. Kitu kimoja ambacho kamwe hakukifanya, ni kuumiza hisia za mtu. Hakumtania mwanamke yeyote, hakujaribu kumdhalilisha mtu yeyote; kamwe hakumdharau mtu yeyote; kamwe hakukasirika na kuchukia na hakujiingiza katika kutoa maamuzi. Hakutamka neno baya au neno la kashfa dhidi ya mtu yeyote. Alikuwa na moyo wa kuelewa, alikuwa mtu wa kujihusisha sana na hisia za wanawake wanyenyekevu na masikini sana, na alidhikika kwa sababu ya dhiki ya wengine.

Kuna wakati ambapo Khadija aliitwa Binti wa Wafanyabiashara na Binti wa Makka. Halafu kuna wakati ambapo aliamua mali yake nyingi imi-likiwe na Uislamu. Alikuwa tajiri sana lakini baadaye akawa masikini kwani hakuwa na kitu. Alibadilisha mfumo wa maisha ya starehe na kuendesha maisha ya dhiki. Lakini hakuna kilichobadilika katika tabia yake. Alikuwa mwenye furaha, karimu, mkamilifu kama mwanzo. Alitumia muda mwingi sana kujitolea kumtumikia Mwenyezi Mungu, na Mjumbe Wake, na kama ilivyo kawaida, kamwe hakusahau ustawi wa umma wa Waumini. Aya ifuatayo inatoa maelezo kuhusu alivyo:

وَمِنْهُمْ سَابِقٌ بِالْخَيْرَاتِ بِإِذْنِ اللَّـهِ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَضْلُ الْكَبِيرُ ﴿٣٢﴾

"Na wako wanaokwenda mbele kabisa katika mambo ya kheri, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo fadhila kubwa."Qur'an 35:32

Khadija, aliyemkamilifu, alikuwa mstari wa mbele kufanya "Matendo mema." Alikuwa na hali ya msukumo wa utakatifu ndani mwake. Kupitia "matendo yake mema" akawa mpokeaji wa neema za hali ya juu kutoka Mbinguni. Khadija alikuwa mwanamke aliyekamilika, mke aliyekamilika wa Muhammad Mustafa, Mama aliyekamilika wa watoto wao, na Mama aliyekamilika wa Waumini. Imani kwamba Mwenyezi Mungu ni mwingi wa huruma ilikuwa kama springi ambapo ndipo Khadija alipata majibu ya mafanikio ya maisha yake. Yeye aliyepewa kile Quran inachokiita Qalb Salyim (moyo mtulivu) aya ya 89 kwenye Sura ya 26. Qalb Salyim au moyo mtulivu, A. Yusuf Ali mfasiri na mfafanuzi wa Quran Majid ametoa maana ifu-atayo: "Moyo uliotakasika, na usio athiriwa na maovu yanayotesa wengine. Kwa sababu kwa lugha ya Kiarabu moyo unaeleweka kama kiini cha hisia maono na akili, na matokeo ya tendo, ina jumuisha tabia yote."

Ulinganifu wa tabia ya Khadija ilikuwa ishara ya Qalb Salyim yake. Khadija alizaliwa na "Qalb Salyim" (moyo mtulivu) kama vile tu wale wateule wa Mwenyezi Mungu wanavyo zaliwa nayo. Ni moyo uliokuwa unabubujika imani, kuutumikia Uislamu. Mapenzi na shukurani kwa Mwenyezi Mungu.

SURA YA KUMI NA NA TANO

UKARIMU WA KHADIJA

Khadija Bint wa Arabuni, na Muhammad Mustafa, walioana mwaka wa A.D. 595. Miaka kumi na tano baadaye, Muhammad aliteuliwa na Mwenyezi Mungu kuwa Mjumbe Wake. Kama Mjumbe wa Mungu, kazi yake ilikuwa kutangaza Uislamu hapa duniani. Kuanzia hapo, kila kitu kilibadilika kwa Khadija. Alitoa wakfu utajiri wake wote kwa ajili ya Uislamu. Wakfu huo ulipatikana katika kipindi mwafaka kwa Uislamu. Khadija alimwambia mumewe kwamba utajiri wake wote umekuwa mali yake, na atumie utajiri huo kwa jinsi apendavyo.

Ukarimu wa Khadija ulikuwa mng'aro wa kiwenyewe. Muhammad Mustafa "aliwekeza" utajiri wa Khadija kwenye Uislamu. Hapajafanyika "uwekezaji" mzuri kama huo katika historia ya binadamu. "Uwekezaji" huu ulikuwa hakikisho kwamba mwendo wa Uislamu hautsimamishwa au hata kudumazwa kwa sababu ya kusefu wa matumizi muhimu na msaada. Ulikuwa ni uwekezaji ambao, mpaka hii leo, unalipa "migawanyo" mingi na utalipa "migawanyo" kwa kila kizazi cha Waislamu, mpaka mwisho wa muda.

Lakini nyenzo ya utajiri haikuwa ya uwekezaji pekee ambao Khadija alifanya kwa ajili ya Uislamu. Vilevile aliwekeza muda wake, kipaji, nguvu na juhudi na moyo katika Uislamu, uwekezaji unaojulikana vinginevyo kama msimamo wa kujituma. Alitambua ndoto na matu-maini ya mume wake na alishiriki yote pamoja naye. Nia ya Khadija kusaidia Uislamu ilikuwa dhahiri mno hivyo kwamba Mwenyezi Mungu(s.w.t) alifurahi na kuuita utajiri huo wa Kwake Mwenyewe katika ay a ifuatayo:

"Na akakukuta fakiri akakutajirisha" Qur'an 93:8

Maelezo ya mfasiri: "Mtukufu Mtume hakurithi utajiri wowote na alikuwa masikini. Mapenzi ya kweli, safi, na ya dhati ya Khadija si tu kwamba yalimwon- dosha na kumweka juu ya tamaa ya kupata, bali yalimfanya ajitegemee kwa mahitaji ya kidunia, mnamo siku za usoni za maisha yake, yal-imwezesha yeye kutumia muda wake wote kumtumikia Mwenyezi Mungu." (A.Yusuf Ali).

Mwenyezi Mungu alimtajirisha mtumishi wake, Muhammad, kwa mali ya Khadija. Khadija na makundi mawili ya Wahamiaji Waislamu kwenda Abyssinia (Uhabeshi) Makundi mawili ya Waislamu yaliondoka Makka mwaka wa 615 na 616 kuepuka mateso ya Maquraysh na walitafuta hifadhi Abyssinia. Jumla ya idadi ya wanaume na wanawake katika makundi yote mawili ilikuwa takriban mia moja. Wakitolewa wachache katika kundi kama Uthmani na Zubayr, wakim-bizi wengine wote walikuwa masikini mno kiasi cha kushindwa kumudu gharama za usafiri kwenda Abyssinia. Nani aliyefanya mipango yote ya misafara kuipatia vifaa muhimu ikiwa ni pamoja na chakula na maji na gharama nyengine zote za kuwezesha kusafiri? Wataalamu wa historia hawajatoa jibu la swali hili. Lakini kuna uwezekano mkubwa kwamba Khadija aliipatia misafara vifaa na kulipa gharama za usafiri, na Waislamu wakawa na uwezo wa kukimbilia Abyssinia. Hapa Makka ni Khadija peke yake ndiye aliyekuwa na uwezo wa kudhamini uhamaji wa Waislamu wa kiwango hicho.

SURA YA KUMI NA SITA

KHADIJA NA MUHAMMAD MUSTAFA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA KUMI NA TANO YA MWANZO WA NDOA YAKE

kazi za Khadija zilikuwa zile hasa za mke na mama wa nyumbani. Mwaka wa A.D. 610 Mwenyezi Mungu (S.w.t) alimteua Muhammad kuwa Mjumbe Wake, na tangu hapo kazi za Khadija ziliongezeka. Zaidi ya kuwa mume wake, Muhammad alikuwa kiongozi na mlezi wake katika malimwengu yote mawili hapa duniani na Akhera. Khadija alikuwa makini sana katika utendaji wa kazi zake kama mke na mama; na pia, sasa akajitambua katika kazi zake kama Mwislamu na Muumini wa kweli. Alifurahi kwamba Mwenyezi Mungu alimteua mume wake kuto-ka miongoni mwa viumbe wote kuchukua ujumbe wa Uislamu kuufik-isha duniani, na yeye alijitolea nafsi yake, kwa moyo, akili na roho, kuhakisha kwamba kazi hiyo inatekelezeka ipasavyo na kuleta mafanikio Wazazi wa Khadija, kama wale wa Muhammad Mustafa, walifariki akiwa bado mdogo sana. Kwa hiyo hakuwa nayo mapenzi ya huruma na upole wa wazazi kama ilivyokuwa kwa Muhammad. Khadija na mume wake walikuwa mayatima lakini hatimaye wote wawili wangekuwa watu wa kuwapa mapenzi na huruma mayatima wa dunia yote. Kile walichopoteza kutoka kwenye mapenzi na huruma ya wazazi wao, walifanikiwa kupata mapenzi na huruma kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe (s.w.t) za milele na milele.

Khadija alipoingia nyumba ya Muhammad baada ya kuolewa, hakuonyesha kupenda kujikwatua kwa kutumia vipodozi, kuvaa mapambo ya gharama kubwa yaliyoingizwa kutoka nchi za nje na kad-halika. Baada ya ndoa yake, alikuwa na mapenzi ya kufanya kitu kimo- ja tu, nacho ni kumpa mume wake starehe na furaha. Aliweza kufanik-isha hayo kwa kutumia nguvu zake zote kwa uthabiti. Alistarehe pale ambapo mume wake alikuwa na starehe na alifurahi tu ikiwa mume wake alikuwa na furaha. Furaha ya mume wake ilikuwa furaha yake. Alipewa kipaji hicho adimu na ule mkono stadi uliofanya nyumba ya mume wake kufana kama Pepo hapa duniani.

Wajibu aliofanya Khadija baada ya mume wake kutangaza ujumbe wake kama mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ulikuwa muhimu sana katika his-toria ya Uislamu. Mara alipotoka nyumbani mwake, alipambana na matatizo. Wapagani walimtesa kwa matusi na walimuumiza kwa mikono yao. Kazi yake ilijaa matatizo, ugomvi na jirani wasio na adabu waliifanya kuwa ngumu zaidi. Lakini mara alipoingia nyumbani mwake, Khadija alimsalimia kwa tabasamu iliyomfanya afurahi. Alisema maneno ya kuchangamsha yenye matumaini na starehe na wasiwasi na woga wake wote ulitoweka.

Tabasamu na maneno ya Khadija yalikuwa kama kitulizo cha mateso aliyofanyiwa Muhammad na waabudu masanamu kila siku. Na kila siku Khadija alimtia moyo na kurejesha ari yake. Uchangamfu wake ulipun-guza shinikizo baya lililosababishwa na matukio wakati wa shughuli zake, na aliweza kupambana na maadui zake tena akiwa mwenye kuji-amini. Khadija alikuwa ndio chanzo pekee cha furaha yake wakati wa vitisho na hofu. Huzuni na majonzi yalikuja kwa mfululizo kama maw-imbi, yakimtishia kumshinda, lakini mke wake alikuwepo wakati wote na kumwezesha apate ujasiri na ushupavu zaidi kuendelea na kazi yake. Kwake yeye mke wake alikuwa ngao ya kisaikolojia dhidi ya vurugu za Maquraysh zilizokuwa zinaongezeka mara kwa mara.

Khadija alikuwa na uelewa sawa ujumbe huu kama Muhammad alivy-ouelewa, na yeye alikuwa na shauku ileile aliyokuwa nayo mume wake kuona Uislamu unashinda upagani. Zaidi ya kuwa na shauku ya kuona Uislamu unashinda, yeye aliongeza msimamo na uwezo. Alifanya hivyo kwa kuhakikisha mume wake anafanya kazi ya kutangaza Uislamu tu, na kazi ya kutafuta riziki alifanya yeye. Kwa hiyo Khadija alimwezesha mume wake kuelekeza uangalifu wake wote, nguvu zake zote na muda wake wote katika kuendeleza Uislamu. Huu ni mchango wake muhimu alioufanya katika kazi ya mume wake kama mjumbe wa Mungu. Khadija alikuwa tegemeo ambalo alihitaji, kwa maneno yake A. Yusuf Ali, "miaka yote ya matayarisho yake." Miaka ile kabla ya kutangazwa Uislamu, ilikuwa "miaka ya matayarisho" kwa utume wake. A.Yusuf Ali.

Mchana na usiku Muhammad alikuwa ndani ya pango la Hira na Mola wake Mlezi. Matatizo magumu aliyoyatafakari akilini mwake, magumu zaidi kuliko jiwe la kito jekundu litokanalo kwenye jabali lililomzungu-ka, matatizo ambayo si yake, lakini matatizo ya watu wake, ndio, na ya hatima ya mwanadamu, ya huruma ya Mungu na mgongano wa miaka mingi ya uovu na wema, dhambi na Rehema nyingi. (The Holy Qur'an Introduction) Inawezekana sana kwamba Muhammad, Mtume - Mteule, aliupangilia na kuuwekea msimamo Uislamu ndani ya pango la Hira. Sura ya Uislamu ilikuwa dhahiri na kuonekana wazi ndani ya maisha yake binafsi muda mrefu kabla hajatangaza kwamba alikuwa mjumbe wa Mungu. Hatujui kwa ufasaha "miaka ya matayarisho" ilidumu kwa muda gani hadi hapo alipofikisha umri wa miaka 40, msingi wa Uislamu ulikuwa akilini mwake.

Muda ulikuwa jambo la msingi katika mpangilio wa Uislamu, na Khadija alijua umuhimu wake kwa mume wake katika kazi yake kwa hiyo Khadija alitengeneza mazingira bora ambamo mume wake angepata mafaniko ya muda, na kusababisha matokeo mazuri. Khadija alikuwa na kipaji cha kusoma hisia za mtu mwengine. Alikuwa anategemea matamshi yasiyotamkwa kutoka kwa mume wake na aliendelea kufanya kile alichotaka kufanya. Miaka ishirini na tano ya maisha ya ndoa, aliyafanya mawasiliano sahihi kabisa na ya karibu sana baina yake na mume wake.

Mnamo mwaka wa 10 baada ya Tangazo la Uislamu, Khadija alifariki dunia. Kifo cha mpendwa huonyesha jinsi mapenzi ya binadamu yanavyoathiriwa na tukio hilo lakini mapenzi ya Muhammad na Khadija hayakuwa ya kusitishwa na kifo; yalikuwa mapenzi ya milele daima. Khadija alipofariki, mapenzi ya Muhammad kwake hayakukatika. Kwa hakika, mapenzi yake kwa Khadija yaliendelea kuongezeka hata baada ya kutoweka duniani. Hata kuwapo kwa wake zake tisa haikuwa sababu ya kuzuia ongezeko la mapenzi kwa Khadija, na mapenzi yake kwa marehemu, wakati wote yalikuwa yanatafuta namna ya kujionyesha. Kama Khadija alimfanyia wema mtu wakati fulani na hata kama ali-fanya hivyo mara moja tu, Muhammad Mustafa alikumbuka na aliji-tahidi kuonyesha wema wa aina ileile kwa mtu huyo hata baada ya kifo chake, na alifanya hivyo mara nyingi iwezekanavyo.

Huko Madina, ilitokea Bibi kizee alikuja kumuona Muhammad Mustafa na akampa maombi fulani. Alimsalimia kwa upole, na alionyesha kuhusika sana na tatizo lake, na alimtimizia ombi lake hapohapo. Alipoondoka Bibi kizee huyo, Aisha ambaye alikuwa mmojawapo wa wake zake, alitaka kujua mtu huyo ni nani. Alisema: "Wakati Khadija na mimi tulipokuwa Makka, mwanamke huyu alikuwa na mazoea ya kuja kumuona mara kwa mara." Wakati wa uhai wake, Khadija alionyesha ukarimu na wema kwa watu wengi sana. Baada ya kifo chake, Muhammad Mustafa hakuwasahau watu hao waliokuwa wanapokea ukarimu na wema kutoka kwa Khadija, baada ya kifo chake, waliendelea kufanyiwa hayo na mume wake.

Kuhusu haya Aisha alisema: "Wakati alipochinjwa mbuzi au kondoo (nyumbani kwa Mtume), mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliamuru nyama ipelekwe kwa wanawake ambao walikuwa marafiki zake Khadija. Siku moja nil-imuuliza kwa nini alifanya hivyo na alisema: Nawapenda watu wote ambao walimpenda Khadija."(Isaba, Vol. 4, P. 283) Mwenyezi Mungu (s.w.t) Alimpa heshima mtumishi wake ampendaye, Khadija, kwa kutokuchangia mapenzi ya mume wake na wake wengine. Kipindi chote cha robo karne cha maisha ya ndoa, ni Khadija pekee ndiye alikuwa sahaba na rafiki wa mume wake, Muhammad Mustafa. Kila mmoja aliishi kwa ajili ya mwenzake na walipata machungu na matamu ya maisha wote pamoja.

Mwenyezi Mungu alimpa mtumishi Wake Khadija nafsi na tabia yenye sifa nyingi. Kama alivyoneemeshwa kwa wingi mno kupewa sifa hizo, yeye aliziimarisha kwa kuutendea wema Uislamu. Khadija alizipamba sifa hizo kwa kumpenda Mwenyezi Mungu kwa kumtii mume wake na kuutumikia Uislamu. Upendo na kutumika kwake ni sifa zilizo mnyanyua Khadija na kumweka kwenye nafasi ambayo hakuna mke mwingine wa Muhammad Mustafa aliyeweza kuifikia. Khadija peke yake, kwa kemikali ya tabia yake aliifanya nyumba ya Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kuwa kama kisi-wa cha amani, kutosheka na furaha katika bahari ya mapambano na ugomvi.

Iliamriwa huko Mbinguni kwamba Muhammad Mustafa lazima aoe mwanamke mwenye malezi mazuri na mwenye kuelewa sana katika Arabu yote. Hapakuwepo mwanamke wa aina hiyo isipokuwa Khadija. Mwenyezi Mungu alikuwa na madhumuni ya pekee ambayo yange-timizwa na Khadija. Kwa hiyo, ndoa yao ilitengenezwa Mbinguni. Abbas, Mahmud al-Akkad wa Misri anasema kwenye kitabu chake, "Aisha": "Ilikuwa amri maalumu ya Mwenyezi Mungu kwamba mke wa mjumbe wake anatakiwa awe mwanamke mpole sana, mwema na aliyetakasika kama Khadija."

Khadija alikuwa mfano halisi wa uchaji Mungu, utakatifu na alikuwa mlezi wa ukamilifu wa kiwango cha juu na maadili ya juu sana. Inaelekea kwamba kama Muhammad Mustafa hakutokea, Khadija angeishi maisha ya pekee bila mume. Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wakati fulani alisema kuhusu binti yake Fatima Zahra, kwamba hakuna mtu mwengine ambaye angemuoa isipokuwa Ali bin Abi Talib: Ingekuwa kweli kabisa kusema kwamba hapana mtu mwengine ambaye angestahili kumuoa Khadija isipokuwa Muhammad.

Kuhusu suala hili, A. Yusuf Ali, mfasiri na mfafanuzi wa Qur'an Majid anasema: Ilikuwa baina yake na Hadhrat Khadija, mwanamke na mke bora kuliko wote. Alimuoa miaka kumi na tano kabla ya kupewa Utume; maisha yao ya ndoa yalidumu miaka ishirini na tano, na mapen-zi yao yalikuwa ya kiwango cha juu sana, yakilinganishwa katika kipi-mo cha kiroho na kijamii. Wakati wa uhai wa Khadija mume wake hakuoa mke mwingine, jambo ambalo si la kawaida kwa mtu mwenye hadhi kama yake miongoni mwa jamii yake. Mkewe alipokufa, yeye alikuwa na umri wa miaka hamsini (50), na kwa sababu mbili tu, inaelekea kamwe hangeoa tena, kwa kuwa alikuwa anajiepusha sana katika maisha ya kidunia.

Mambo mawili yaliyotawala ndoa zake zilizofuata ni:

1. Aliwaonea huruma na kuwaonyesha upole wajane walio na dhiki na hawangesaidiwa kwa namna nyingine yoyote katika hali ya jamii ile, baadhi yao, kama Sauda, walikuwa na watoto katika ndoa zao za zamani, hivyo walihitaji ulinzi;

2. Msaada katika kazi yake ya uongozi, kutoka kwa wanawake ambao walipewa maelekezo na kuwekwa pamoja katika familia kubwa ya Waislamu, ambapo wanawake na wanaume walikuwa na haki sawa za kijamii. Muhammad Mustafa, Mtume wa Mwenyezi Mungu, alitumia fursa zote kuonyesha kuvutiwa kwake na mapenzi kwa Khadija na kutambua ukubwa wa kiwango alicho utumikia Uislamu. Alifanya hivyo, kwanza kabisa kutii amri ya Mwenyezi Mungu kama Kitabu chake kinavyose-ma kwenye Ay a zifuatazo:

1 "... Na kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu...." (Sura Al-Baqara 2:231)

2. " ...Na neema za Mola wake Mlezi zisimulie..." (Sura 93:11 ).

Muhammad Mustafa mtumishi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alipokea upendeleo na ukarimu mwingi kutoka Kwake kupitia kwa Khadija - alizikariri na kuzitangaza. Halafu, pili, Muhammad Mustafa alipenda kutaja matendo mema, makubwa ya Khadija aliyoyafanya katika kumtumikia Mwenyezi Mungu na Uislamu, kwa sababu ya kuonyesha mapenzi kwake (Khadija). Hii ilikuwa njia mojawapo ya kuonyesha mapenzi. Ilikuwa pia namna nyingine ya kujikumbusha muda waliyotumia yeye na Khadija wakiwa pamoja Makka. Mtu anaweza akaona waziwazi kwam-ba katika kumbukumbu zake, fikra zake zilikuwa zinayatembelea maisha yake ya zamani; na pia mtu anaweza kugundua humo dalili za mambo aliyozoea zamani. Palikuwepo na muda katika maisha ya kila mtu ambapo alizidiwa na kumbukumbu ya mambo aliyoyazoea.

Waandishi wa vitabu viwili mashuhuri, Isaba na Istiab, wamemnukuu Bi Aisha akisema: "Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu akiondoka kwenda popote, alimkumbuka, alimsifu na kumrehemu Khadija." Jinsi muda wa maisha ya ndoa ulivyopita, mapenzi ya Muhammad na Khadija yalizidi kupenya kwenye mioyo yao kwa nguvu zaidi. Kwa mapenzi yake, aliondoa wasiwasi wake wote, woga na huzuni kama ilivyoelezwa hapo kabla. Kwa kutumia istiari ya mashariki: Khadija aling'oa miba yote katika maisha ya Muhammad Mustafa, badala yake, alipanda maua ya waridi ya mapenzi.

Maua hayo kamwe hayakunyau-ka; rangi, harufu na ubichi wao ulikuwa wa daima milele. Kama palikuwepo na ndoa iliyopendeza wakati wote, ndoa hiyo ilikuwa ni ile ya Muhammad na Khadija; ndoa hiyo ilikuwa mpya siku ya mwisho wake kama ilivyokuwa siku ilipoanza. Khadija alikuwa hai moyoni mwake daima milele. Jina la Khadija lilikuwa mdomoni mwake wakati wote, na mapenzi ya Khadija yalijaa moyoni mwake. Hata kuzungumza juu yake na kumsifu kulimfanya Mtume afurahi.

Kila neno na tendo la Khadija lilidhihirisha busara zake. Katika kuch-agua mume wake, alionyesha uwezo wa kushangaza na wepesi wa kuelewa wa hali ya juu. Lakini uwezo na wepesi wa kuelewa ni vipaji ambavyo wanawake wengine vile vile wanaweza kuwa navyo, na Khadija hakuwa mwanamke pekee aliyepewa vipaji hivi. Maelezo kuhusu uamuzi wenye msukumo wa kimungu uliofanywa na Khadija kukubali kuolewa na Muhammad Mustafa ni kwamba kulifanywa chini ya mwongozo wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) Mwenyewe. Kwa hiyo, hangeamua vibaya. Alipokutana na Muhammad, Mtume mteule, Khadija aliona Utukufu kwa mbali sana ndani yake, na alikabidhi hati-ma yake kwenye mikono yake iliyobarikiwa. Mikono hiyo ilinyanyua hatima yake, na kuifanya tukufu.