ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE0%

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE Mwandishi:
Kundi: Imam mahdi (a.s)

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

Mwandishi: Marehemu Mulla Muhammad Jaafar Sherif Dewj
Kundi:

Matembeleo: 4790
Pakua: 526

Maelezo zaidi:

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 20 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 4790 / Pakua: 526
Kiwango Kiwango Kiwango
ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

Mwandishi:
Swahili

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

MUANDISHI: MAREHEMU MULLA MUHAMMAD JAAFAR SHERIF DEWJI

DIBAJI

kitabu hiki kinatoa ufafanuzi wa hadithi maarufu ya mtume muhammad(s.a.w.w) ambaye amesema:

"Yeyote atakayekufa pasina kumtambua imamu wake atakufa mauti ya mpagani." kila mwislamu mwenye kuamini kauli ya bwana mtume(s.a.w.w) hana budi kufanya kila juhudi ya kumtambua imamu wake wa wakati huu maana dunia hii haiwezi kubaki hata sekunde moja bila ya hujjah ya mwenyezi mungu (s.w.t) kuwapo. ama kwa hakika, kuwa na imani katika imami ni mzizi mmoja wapo wa dini, maana kazi ya kuiongoza na kuihifadhi dini ni wajibu wa imamu baada ya kuondoka duniani bwana mtume(s.a.w.w) .

Ndipo kitabu hiki kinafaa kisomwe na kila mwislamu! na kutafakari aya za kurani, hadithi za bwana mtume(s.a.w.w) za maimamu waliotajwa na mtume(s.a.w.w) na maelezo ya kihistoria yaliyomo ndani yake. kila neno lina maana na maarifa yake.

Mwalifu wa kitabu hiki, marehemu mulla muhammad jaafar sherif dewji, amefanikiwa kueleza kwa uwazi dhana ya uimamu ambaye ni usuli unaofafanuliwa kwa masimulizi kuhusu kuzaliwa, na kughibu na maisha yake marefu, ungojaji wa waumini kutokeza kwake, mahala aishipo, na ishara na dalili za kujitokeza kwa imam mehdi. vilevile ameeleza faradhi za waumin miongoni mwa mambo mengine mengi ya msingi na muhimu. mtarjumi wa kitabu hiki kwa lugha ya kiingereza kutoka lugha ya kigujarati ni alhajj murtaza a. lakha na alhaj z; m. s. lakha amekitarjumi kwa kiswahili chepesi na chenye ufasaha.

Maulana seyyid sabir husein musawi, qibla, ametilia shime kitabu hiki kichapishwe kwa kiswahili na mkarimu mmoja amejitolea kugharimia uchapishaji wa hiki kitabu.

Alla subhanahu wa taala kwa wasita wa mtume muhammad(s.a.w.w) na mwanae imam mehdi(a.s) atawajazi kila lililo jema mchapishaji huyo na wengine waliosaidia kwa dhati dhamira , hali na mali kueneza habari hizi muhimu zinazohusu imani na amali za waumini wa dini ua uislaam. miye, al-hakiri, ninashukuru kupewa fursa hii ya kuandika dibaji na ninaamini kuwa nami pia nitakubaliwa na imamu wangu kuwa mmojawapo wa mfuasi wake na kupata shifaa yake siku ya kiyama na pia hadhi ya kukutana naye hapa duniani.

alhaji muhsin m.r.alidina

Dare -es-Salaam

25 shawwal, 1409.

SHUKRANI

kitabu hiki kimetarjumiwa kutoka lugha ya kiingereza. kama ilivyoelezwa katika dibaji, sina budi kumshukuru alhaj muhsin m. ali dna ambaye alinihamasisha kuendelea kukitarajumi baada ya kukatishwa tamaa ya kumpata mtu wa kusahihisha na kunyoosha lugha. ijapokuwa alhaj muhsin m.r. alidina alipitia muswaada kikamilifu na kutoa mapendekezo muafaka au naksi yoyote iliyobaki ni 'dhima yangu. ninatumai wasomaji watazisamehe kasoro za lugha na kujali zaidi ujumbe uliomo katika kitabu hiki. alhaj zakirihusein m.s lakha mtarjumi. imam al zaman (imam wa wakati huu) hadhrat mehdi(a.s) kwa jina la mwenyezi mungu mwenye rehema na huruma

1

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE SURA 1

UTANGULIZI

Kitabu hiki hakikuandikwa kwa ajili ya kuleta majadiliano au mabishano na waumini wa dini zingine au madhehebu mengine ya kiislamu, bali kimeandikwa kwa ajili ya waumini wa jamii yangu, hasa kwa ajili ya vijana wanaokua ili waweze kufahamu na kutambua vema manufaa na ukweli wa imam wa wakati, hadhrat mehdi(a.s) , uongozi wake wa kiimamu, kughibu na hatimaye kuonekana kwake tena mara ya pili. ni katika kuthibitisha ukweli na uhakika wa imam huyo na maimamu kumi na wawili ndipo kitabu hiki kimenukulu-kauli kutoka vitabu vya madhehebu mbalimbali ya kiislamu na dini zingine.

Kwa vile uimamu ni mojawapo wa maadili matano ya dini yetu (shia ithnaashery) mwumini wa madhehebu shurti awe na yakini na imani juu ya itikadi hii kama vile shurti afahamu na kuamini kwa makini upweke wa mungu,uadilifu wa mungu, manabii walioletwa na mungu na siku ya kiyarna. kwa hivyo ni lazima mtu awe na yakini juu ya uimamu. hivyo hamna budi mtu kufahamu, kukubali na kuamini kwamba maimamu hao ni warithi na makaimu wa mtume wa mwisho. katika hao maimamu kumi na wawili ni imam wa kumi na mbili, imam wa wakati huu, hadhrat mehdi(a.s) ambaye yungali hai, bali kwa sababu mbalimbali ameghibu. wakati mungu atakapo mwamrisha, imam mehdi(a.s) atajitokeza na atatawala ardhi (dunia) hii kwa kueneza usalama na uadilifu kadri ile hivi inavyotawaliwa na dhuluma na maonevu, na ataeneza dini ya uislam.

Kiini cha hitilafu kati ya madhehebu 73 katika dini ya uisla ni suala la uimamu. Juu ya suala la upweke wa mungu, manabii, korani takatifu, na siku ya kiyama madhehebu yote yanaafikiana katika imani zao (isipokuwa makadiani, mabahai na madhehebu machache yaliyojitokeza katika karne mbili zilizopita). Lakini suala la uimamu ni jambo muhimu mno.

Waislamu wote wanaamini kwa kauli moja hadithi ya mtume mtukufu(s.a.w.w) kwamba "yeyote anayefariki bila kumtambua imamu wa wakati hufa kifo cha upagani (kutokuwa na imani ya dini), yaani, kifo cha kutokuwa mwislamu." vile vile hadithi ya mtume(s.a.w.w) inayokubalika kwa waislamu kwamba "wafuasi wangu watagawanyika katika makundi 73, na watapotoka kwenda motoni ila kundi moja tu ambalo iitakuwa katika njia ya haki." Haiyumkiniki kwamba firka zote 73 ziwe kwenye sirat-al-mus takim. kadhalika kila firka inamwona mwingine kapotoka. Hivyo kila mwislamu anawajibika kutafuta na kukubali madhehebu ya kweli na ya haki. kwani kwa mujibu wa hadithi ya mtume(s.a.w.w) "Mtu anayekufa bila kumtambua imam wake wa wakati hufa kifo cha kutokuwa na dini na vitendo vyake vyote, swala saumu zake zote huwa hazina thamani yoyote ." Kwa vile imani katika uimamu hufarakanisha madhehebu mbalimbali, basi hilo ni suala muhimu na zito sana.

Uislam umeweka maadili matano ya kuthibitisha ukweli wa mahehebu. kwa hivyo kila mwislamu anayejibidiisha kwa dhati kujipatia ridhaa ya mwenyezi mungu na uokovu wake na aliye jiandaa na yuko tayari kuacha ukaidi wake na dhana alizofuga bila shaka ataweza kutambua dini iliyokuwa ya haki na yenye ukweli. mwenyezi mungu amesema katika kitabu chake:

وَالَّذِينَ جَاهَدُوا فِينَا لَنَهْدِيَنَّهُمْ سُبُلَنَا وَإِنَّ اللَّـهَ لَمَعَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٦٩﴾

"Wale ambao wanajitahidi kwa ajili yetu kwa hakika wataongozwa kwenye njia yetu ya haki na iliyonyooka." (29:69).

maadili matano hayo ni:

1) Qur'ani takatifu.

2) Hadithi sahihi za mtume ambazo hazipingani na au kuwa kinyume cha Qur'ani takatifu

3) Tawarikh (historia).

4) Uhakikawatukio.

5) Utumiaji wa akili (urazini)

Katika kufahamu na kuelewa maana halisi ya qur ani takatifu, ujuzi wa hadithi sahihi, historia, uhakika wa matukio na utumiaji wa akili ni muhimu sana. udogo wa kitabu hiki hauruhusu majadiliano bayana juu ya mambo hayo. tangu kughibu kwa imam mehdi(a.s) , zaidi ya miaka elfu moja iliyopita, mamia ya waislamu wamedai utume, uimamu na hata kuwa mehdi(a.s) . wadanganyifu wengi walidai kuwa mehdi wametoka bara arabu, iran, bara hindi na afrika. lakini kwa hakika hata mmoja wao hakuwa mehdi wa kweli kama ilivyoelezwa katika kitabu kitakatifu. hadithi na historia huthibitisha kwamba atakuwa mehdi mmoja tu. kwa hivyo wenye. kudai kuwa mehdi ni wazushi, waongo na kwa udanganyifu wao wamemkebehi mungu na mtume wake. Aidha dalili moja muhimu katika kutafuta madhehebu ya haki ambayo itamletea uokovu mwanadamu ni kwamba kila firka ya uislarnu hukubali atukufu wa aila ya mtume(s.a.w.w) .

Yeye mwenyewe, Ali, Fatima, Hassan na Hussein (rehma ya mungu iwe juu yao), ni watu waliotakasika kikamiliru na walio juu ya siratul-mus-taqim (njia ya haki) na ambao wanastahiki utukufu na taadhima ya haki. Kwa hivyo, bila pingamizi lolote, amri zao, hadithi zao na mafunzo yao yanapatia watu uokovu. Hakuna mwislamu yeyote ambaye anaweza kuyapinga mafunzo ya hao watano. Kila mwislamu anawajibika kutafiti maisha waliyo ishi hao watano, maagizo na mafundisho yao ili kuweza kufuata madhehebu ya haki.

Inawezekana kujua namna ya maisha yao, vitendo vyao maagizo ya hao "watano" sio tu kutoka katika vitabu vya madhehebu ya shia ithnaashery, bali pia katika vitabu vilivyoandikwa na waandishi maarufu wa madhehebu ya sunni. Wafuasi wa kila madhehebu ya kiislam huwakubali hao watano ambao walikuwa juu ya haki na mfuasi wa madhehebu hudai kwamba ni mfuasi wa hao watano. Aidha madai hayo ya firka mbali mbali kuhusu maagizo yanayohitilafiana, ni kinyume cha busara na hayawezi kukubaliwa. Kitabu hiki kitajaribu kubainisha maelezo ya watano hao pamoja na maelezo kuhusu madhehebu ya kweli na ya kumtambua imamu mehdi(a.s) , imam wa wakati huu.

Zaidi ya hayo kuhusu hao watukufu watano kuna hadithi mashuhuri ya mtume(s.a.w.w) ambayo inakubaliwa na wote; nayo ni:"Mimi ninawaachieni vitu viwili muhimu (vizito) mno: kitabu cha mungu na dhuriya yangu (Ahlul-bait). kama mtashikamana na vyote viwili hamtapotea kamwe."

Familia tukufu ya mtume mtukufu(s.a.w.w) imetajwa katika kitabu kitukufu na mwenyezi mungu kuwa ni yenye watu watakatifu na waliotakasika kutokana na kila uovu. bila shaka, licha ya kuwa katika njia ya haki, watu hao pia ni viongozi wa umma kwenye njia ya uokovu. kwa hivyo wafuasi wanaowapenda watano, huzingatia na kufuata mafunzo pia maagizo yao na kuwa maadui wa wauaji wa Ahlul Bayt, kwa hakika ni wafuasi wa dini ya haki na wanastahili uokovu.

Madhehebu yote ya kiislam hukubali kwamba qur'ani ni neno la mwisho la allah lililoteremshwa juu ya mtume(s.a.w.w) kuwa yanawajibika kufuata maagizo yake (ila makadiani ambao wanashaka na qur'ani kwa sababu imo katika lugha ya kiarabu kwa hivyo ni kwa ajili ya waarabu tu). Iwayo yote itakavyokuwa mgeni anapozuru jiji, ikiwa mchana jua linapowaka, au usiki taa zinapomeremeta kama haujui huo mji hataweza kufika kokote bila mwongozi. Vivyo hivyo, qur'ani ni mfano wa mwanga wa jua; kwa hivyo, tunahitaji mwongozi kutuongoza kwenye siratul mustakiim (ajia ya haki). kama vile mwongozi anahitajika kuwa mwenyeji na kufahamu mambo yote katika jiji hulo,vivyo hivyo, hainabudi kwa maimamu kuwa na ujuzi kamili na wa kweli wa qur'ani iliyoteremshwa kwao na mwenyezi mungu mwenyewe. Kwa hiyo Mtume(s.a.w.w) katika hadithi yake madhukura amesema kwamba ameachia vitu viwili vizito: kitabu cha mungu na dhuriya wake, na yeyote atakayeshikamana na hivyo viwili hatapotoka kabisa.

Hoja inayotolewa na wapinzani wa imamu wetu ni kwamba imam lazima awe anaonekana siku zote na kuwa awe hadharani mwa watu na kwamba imam aliyejificha hawezi kuwa imam au hawezi kutoa mwongozo mwema au kusaidia si hoja thabiti. Iwapo hatuwezi kumkubali imam tusiyemwona, basi kuwepo kwa mungu mwenyewe ambaye hatumwoni bapa duniani na hata baadaye (siku ya akhera) vile vile, naudhubillah, hubatilisha kuwepo kwake. hata hivyo, kukubali kuwepo kwa mungu ni imani muhimu katika dini zote. licha ya hayo viumbe wengi wa mungu ambao hawaonekani, lakini kuwepo kwao hakupingwi. Mathalan roho ya binadamu inayoingia katika kijusi kilichopo tumboni mwa mama na roho inapotoka mwilini mwa binadamu vile vile haionekani. kuongezea hayo, hewa na malaika hawaonekani, lakini hatuvikanushi.

Mtume adhimu wa uislamu alilazimika kujificha na kuishi katika pango kwa muda wa miaka mitatu. Vile vile manabii mussa, suleiman, ibrahim na issa kwa baadhi za nyakati waliona dharura ya kujificha. Kadhalika manabii khidhri na elias wapo hapa duniani kwa muda wa maelfu ya miaka na huo ni ukweli unaokubaliwa na waislamu wote.

licha ya hayo, shetani "iblis"na wafuasi wake na majini wapo hai duniani na hawaonekani. Dajjal na yajuj majuj (agog na magog) na mataifa yao yanakubaliwa kuwa wapo hai lakini hawaonekani. Qur'an takatifu yenyewe imeeleza juu ya imani ya ughaibu na tutaeleza aya hizo za qur'an pahala pengi katika kitabu hiki. Hali itakayokabiliwa katika kaburi, siku ya hukumu (kiyama) pepo, moto, mizani, sirat (njia nyembamba siku ya kiyama) arsh na kiti cha enzi (kursy) na kadhalika havionekani. Licha ya waislam kuwa na itikadi juu ya hayo yote, hata wakristo, mayahudi na mabaniani pia huyaamini. kwa hivyo hakuna sababu ya kusaili kutoonekana kwa imam.

Jamii ya kibohora huamini kwamba imam wao tayyab ametoweka tangu 524 a.h. na kwa muda wa miaka 876 haonekani. Kwa hivyo wao hawawezi kusema kwamba kutoonekana kwa imam wetu wa kumi na mbili haimkiniki. Vile vile ismailia, wafuasi wa agakban, "wamesimulia katika vitabu vyao kuwa baadhi ya maimam wao walikuwa hawaonekani. Hivyo kuzaliwa kwa imam wa wakati, imam Mahdi(a.s) , na kuwa hai na kughibu kunathibitika na aya za qur'an, hadithi za mtume mtukufu, historia na akili na hakuwezi kubatilishwa kwa kisingizio hicha kutoonekana kwake. Kwa hiyo suala muhimu linalojitokeza si kwamba, je, iwapo imamu haonekani au kufikiwa anawezaje kuutumikia uislam na waislamu na kwa nini asijitokeze kuondoa ukafiri? hayo ni masuala ambayo yatajadiliwa kwa makini katika kitabu hiki katika sura zinazofuata ili idhihirike kwamba ijapokuwa imam haonekani lakini uislam na waislamu hupata manufaa na fadhila nyingi kutoka kwake imam(a.s) .

Maismailia wanaomfuata agakhan pamoja na viongozi wa dini hiyo wanasema kuwa maneno ya qur'ani "imaulmubin" yanamaanisha imam aliyekuwa mbele ya macho yetu, na siyo imam aliyejificha. walakini neno "mubin" halimaanishi tu "kitu kinachoonekana bayana". neno hilo limetumiwa pahala pengi katika qur'an takatifu kwa maana anuwai k.m.

1) Kifungu "imamul mubin" kimetumiwa katika sura ya 36 (surat-yasin) aya 12 "na sisi tumehifadhi kila kitu katika imamu aliyebainika". Katika kamusi za kiarabu kiingereza neno "mubin" humaanisha, "bayana", "dhahiri" na "wazi wazi".

2) Katika sura hiyo hiyo ya yasin, neno la "mubin" limetumiliwa katika muktadha wa "yeye ni adui dhahiri" (36:60). Aya hiyo bila shaka inamzungumzia shetani kuwa ni adui anayejulikana waziwazi na hakuna ushahidi wa aina yoyote wa kusema shetani anaonekana. kwa hiyo imedhihirika kwamba neno "mubin" halimaanishi "dhahiri" kwa macho tu. katika sura hiyo hiyo, aya 24 inasema, "nikifanya hivyo nitakuwamo katika upotofu bayana". Katika aya hii upotofu unasibishwa na sifa "mubin" (bayana). Hapo tena inakubalika kwamba kosa sio kitu kinachoonekana.

3) Katika sura ya "nyuki", sura ya 16, mwisho wa aya 35, kuna maneno yafuatayo: "basi kunawajibu'. Mwingine wa mitume pia kufikisha ujumbe waziwazi?" neno "mubin" hapa limenasibi- shwa na ufikishaji ambao ni kitu kisichoweza kuonekana.

4) Neno hili pia limetumika katika sura 26 kuhusu washairi ambamo katika aya 195 inasomeka: "katika lugha ya kiarabu dhahiri", lugha siyo kitu kinachoweza kuonekana kwa macho.

5) Katika sura ya yasin, aya ya 17: "na hakuna kitu kinachowapasa ila ufikishaji wa ujumbe bayana". ujumbe sio kitu kinachoweza kuonekana kwa macho. 7) tena katika sura ya "nyuki" aya ya 4:" amemuumba binadamu kutokana na chembe ya uhai bali anakuwa mpinzani bayana." kwa hivyo, ni dhahiri kwamba kukubali kwamba neno la "mubin" linamaanisha tu kuweza kuonekana kwa macho ni uwongo na udanganyifu. Wakati huo huo imethibitika kwamba hata mitume waliishi maisha ya kutoonekana bayana. mabohora na waismailia pia huamini kama baadhi ya maimam wao walijificha. katika mpangilio wa kurithiana, maimamu watatu wa kiaghakhan, wafi ahmed, taki mohamed na raza abdullah waliishi maisha ya mafichoni. licha ya hayo hakuna habari yoyote juu ya maisha na wasifu wa wengi wa maimamu wao 48.

Mwisho :

Sifa za imam zimeelezwa bayana katika qur'an na katika hadithi za mtume(s.a.w.w) . sifa hizo zitajadiliwa katika kitabu hiki katika sura zijazo. kitu muhimu cha kuzungumzia hapa ni mazingira au hali inayohitajika kufanya imam mehdi(a.s) kujitokeza. iwapo hali zilivyoelezwa katika qur'an tukufu na hadithi za mtume(s.a.w.w) hazikutimia, basi mdai veyote hatakubaliwa na mwislamu kuwa yeye ndiye mehdi. sifa zinazohusu ni zifuatazo:

1. Jina tukufu la mehdi ni hadhrat muhammad(a.s) . ukweli wa maneno hayo umethibitishwa kutokana na hadithi na historia ya uislam. kwa hivyo, wenye majina ya gulam ahmed, mohamedali bab, bahauddin au mwenye jina lolote lingine hawezi kukubalika kuwa mehdi.

2. Hadhrat mehdi'(a.s) yungali hai hadi hii leo na hakujitokeza kwa sababu ishara zinazohusika na wakati wa kujitokeza kwake kama zilivyo elezwa katika qur'an na hadithi hazikudhihirika.

3. Ishara moja muhimu kabla ya kujitokeza kwake ni kuonekana kwa dajjal ambaye atauliwa na imam(a.s) . japokuwa baadhi ya watu waliodai kuwa mehdi wameshajitokeza na kupotea, lakini mpaka leo dajjal hajaonekana. (mirza wa kadiani alieleza kuwa kampuni ya gari la moshi ya uingereza (british railways) ni punda wa dajjal asiyekuwa na mkia, lakini baadaye yeye mwenyewe na wafuasi wake walimpanda huyo punda (gari moshi).

4. Kitambo tu baada ya kujitokeza kwa mehdi duniani kutakuwa na uadilifu na amani. hali kama hiyo bado haijapatikana hadi leo ingawa wadanganyifu wengi waliodai umahdi wamejitokeza. kinyume cha hayo uonevu, uovu na dhuluma umezagaa. nabii issa atateremka kutoka mbinguni na atafika kwa hadhrat mehdi(a.s) . jambo hilo bado halijatokea. mirza kadiani na mithili yake wengine vile vile walidai kuwa wao ndio nabii issa.

Kufuatana na kauli ya wanahistoria na wanahadithi wa kiislamu, hadhrat mehdi(a.s) atajitokeza wakati uliopangwa na mungu, na ni mwana wa imam wa kumi na moja, imam hassan askari(a.s) na anatokana na dhuria (kizazi) ya imam hussein(a.s) mwana wa mwana-fatima(a.s) , binti wa mtume mtukufu(s.a.w.a) . yeye atakuwa kwenye kizazi cha tisa cha imam hussein(a.s) na imam wa kumi na mbili katika urithi huo.

5. Pia hadhrat mehdi(a.s) atakuwa ni mwana wa wazazi walio wacha mungu wa hali ya juu na watakatifu na atakubaliwa na waislamu wote. kwa hivyo, kwa vile wadanganyifu wote kutoka bara arabu, pakistan, iran na punjab waliodai kuwa mehdi hawakutokana na kizazi hicho kamwe. kwa hiyo hawakubaliki.

6. hadhrat mehdi(a.s) atakuwa na vitu maalum vya wadhifa wake kama mitume walio pita k.m. pete ya nabii suleiman, fimbo ya nabii mussa, jiwe la nabii mussa ambalo alipolipiga fimbo yake liliibua chemchem kumi na mbili na bendera ya mtume(s.a.w.w) . wadanganyifu waliodai kuwa wao ni hadhrat mehdi(a.s) hawakuwa na hata kitu kimoja kati ya vile vilivyo tajwa hapo. Vile vile maayari hao wataweza kuwa na daawa hiyo?

2

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 2

AYA ZA QUR'ANI KUHUSU UIMAMU, KUGHIBU NA KUONEKANA TENA KWA IMAM WA WAKATI WETU HADHRAT MEHDI(A.S)

"Alif laam mim. kitabu hiki, bila shaka ni mwongozo kwa wale wanaoepukana na maovu. wale ambao wanaamini visivyoonekana".

kuna aya nyingi katika qur'an tukufu kuhusu kuwa na imani ya mambo yasiyoonekana. "mwenyezi mungu ameahidi baina yenu kwa wale ambao hutenda vitendo vyema kwamba bilashaka atawateua wraithi juu ya ardhi (duniani) kama alivyo teua warithi, kabla ya hao na bilashaka atastawisha dini wanayo fuata (uislam) aliyoichagua yeye (mungu) na kwa hakika baada ya hali ya hofu kubadilika kuwa pa imani ili wanaomwabudu mungu na kutomshirikisha yeyote nayeye (mungu) na yeyote ambeye hataleta imani baada ya hayo,hao ndio ambao ni waovu." (55).

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ ﴿٩﴾

"Ni yeye (mungu) ndiye alie mtuma mtume wake pamoja na mwongozo na dini ya haki ili ishinde dini zote japokuwa washirikina watakasirihishwa na hilo. " (61:9).

Mtume mtukufu(s.a.w.w) katika uhai wake hakuweza kushinda dini zote wala kuwashinda washirikina. Kwa hivyo ahadi hiyo itatimizwa na kukamilishwa katika kipindi cha utawala wa hadhrat mehdi(a.s) .

Katika ufafanuzi wa aya hiyo mwanazuoni mashuhuri sana wa kisunni, imam fakhruddin razi, anasimulia kutoka kwa Abu hureira kwamba mtume(s.a.w.w) amesema kwamba: Ahadi hiyo iliyotolewa na Allah kuupa uislam ushindi juu ya dini zote itatekelezwa na hadhrat mehdi(a.s) atakapojitokeza na watu wote kukubali dini ya uislam.

Hadithi nyingi kuhusu hadhrat mehdi(a.s) zimo katika vitabu vya kisunni.

وَلَقَدْ كَتَبْنَا فِي الزَّبُورِ مِن بَعْدِ الذِّكْرِ أَنَّ الْأَرْضَ يَرِثُهَا عِبَادِيَ الصَّالِحُونَ ﴿١٠٥﴾

"Na kwa hakika tuliandika katika zaburi baada ya ukumbusho ya kwamba waja wangu watakatifu watarithi (watatawala) ardhihii".(21:105).

وَلَقَدْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَبَعَثْنَا مِنْهُمُ اثْنَيْ عَشَرَ نَقِيبًا ﴿١٢﴾

"Na bilashaka allah amewaahidi wana wa israil kwamba amewateua viongozi kumi na wawili" (5:12).

Sahih Bukhari na Sahih Muslim ambavyo ni vitabu vinavyo aminiwa sana na masunni, vinasimulia hadithi ya mtume(s.a.w.w) kuwa:

"Hadi hapo itakapo kamilika silsila ya warithi wangu kumi na wawili dunia hii itaendelea, nao watakuwa maimam kumi na wawili."

"(Kumbukeni) siku ambayo kila watu wataitwa pamoja na imam wao." (17:71).

وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا وَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِمْ فِعْلَ الْخَيْرَاتِ وَإِقَامَ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءَ الزَّكَاةِ وَكَانُوا لَنَا عَابِدِينَ ﴿٧٣﴾

"Na sisi tumewateua maimam miongoni mwao watakao ongoza binadamu kwa amri yetu (amri ya mungu) ya kutenda mema, kuendeleza swala na kutoa sadaka na walitutumikia sisi peke yetu" (21:73).

Maimamu wameagizwa kutenda vitendo vyema, kuendeleza swala, kulipa zaka, kumwabudu mungu na kuwaongoza watu kufuatana na maagizo ya mungu. Kwa hiyo, ni watu hao tu ambao waliojiwajibisha - kutenda hivyo na kuwaongoza wengine kufuatana na maagizo ndiyo wanaoweza kuwa maimam; na sio wale ambao hutenda kinyume (kuasi amri ya mungu). 8)

وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يُنصَرُونَ ﴿٤١﴾ وَأَتْبَعْنَاهُمْ فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ هُم مِّنَ الْمَقْبُوحِينَ ﴿٤٢﴾

"Na sisi tumewafanya maimam ambao huwavuta watu motoni; na siku ya kiyama hao hawatasaidiwa. na sisi tumesababisha maafa kuwazingira duniani na siku ya kiyama hao watakuwa katika kikundi cha watu wataotisha." (28:41-42)

لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ ﴿٣﴾ تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ ﴿٤﴾ سَلَامٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ ﴿٥﴾

Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu. Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo. Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri!" (97:3-5).

Malaika huteremka kwa idhini ya mola kwa ajili ya kila amri. lakini malaika hao huenda wapi na hayo mambo huelekezwa wapi na je, hao wanaoteremka hawakamilishi ujumbe? hivyo inathibitika kwamba duniani kuna mwakilishi wa mungu na ni mrithi wa mtume(s.a.w.w) anayetimiza wajibu wa imam. kila mwaka katika usiku huo mtukufa malaika huteremka na kumkabidhi ujumbe wa mungu. Kutokana na hoja za aya za qur'an, hadithi za mtume(s.a.w.w) na akili, mtu aliyekamilika na anayestahili heshima hiyo na kutembelewa na malaika hawezi kuwa yeyote mwingine ila hadhrat mehdi (a.s) katika kitabu hiki kwingineko tutaelezea kwamba hawezi mtu mwingine kudai hadhi hiyo ila hadhrat mehdi(a.s) .

3

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 3

UTEUZI WA MAIMAMU, SIFA ZAO NA WAAJIBU WA VEEO VYAO

Imam ni neno la kiarabu linalomaanisha, "mkuu", "kiongozi", na "mwongozi."

Uteuzi wa imam hufanywa na mungu na kumjulisha mtume wake, ambaye hutangaza uteuzi wa imam huyo kwa wafuasi wake. mwenyezi mungu amesema katika qur'an "na bwana wenu anayeumba na kumchagua anayempenda, na siyo hiari yao, na kutukuzwa ni yeye ambaye ni juu ya vyote anavyo shirikishwa nae" kuna aya nyingi katika qur'an zinazoeleza kwamba uteuzi wa imam ni wa mungu na hufanywa na mungu mwenyewe. kwa mfano kuhusu nabii adam:

وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ﴿٣٠﴾

Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa ...(2:30).

Kuhusu Nabii Daudi, Mungu amesema katika Qur'an:

يَا دَاوُودُ إِنَّا جَعَلْنَاكَ خَلِيفَةً فِي الْأَرْضِ فَاحْكُم بَيْنَ النَّاسِ بِالْحَقِّ ﴿٢٦﴾

Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. Basi wahukumu watu kwa haki... (38:26).

Kuhusu Nabii Ibrahim, Qur'an imeleza:

وَإِذِ ابْتَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ رَبُّهُ بِكَلِمَاتٍ فَأَتَمَّهُنَّ قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِي قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ ﴿١٢٤﴾

Na Mola wake Mlezi alipo mjaribu Ibrahim kwa kumpa amri fulani, naye akazitimiza, akamwambia: Hakika Mimi nitakufanya uwe mwongozi wa watu. Akasema: Je, na katika vizazi vyangu pia? Akasema: Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu." (2:124).

Kutokana na aya hizo imedhihirika kwamba mtume(s.a.w.w) humteua (tangaza) imam kutokana na amri ya mungu tu. La sivyo, yeye hana uwezo wa kumteua imam kwa sababu imam lazima awe mwenye hekima yote na. awe maasum (asiyekosa, asiye na dhambi na kuwa taahir).

Qur'an inazungumzia maimam aina nyingi, k.m.

وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا وَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِمْ فِعْلَ الْخَيْرَاتِ وَإِقَامَ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءَ الزَّكَاةِ وَكَانُوا لَنَا عَابِدِينَ ﴿٧٣﴾

"Na sisi tumewafanya kuwa maimam wanao ongoza watu kwa amri yetu na tumewaamrisha kutenda wema, kuimarisha swala na kutoa zaka na sisi peke yetu tu wao hututumikia." (21:73).

وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يُنصَرُونَ ﴿٤١﴾

"Na sisi tumewafanya maimam ambao huwaongoza watu kwenda motoni, na siku ya hukumu hao hawatasaidiwa." (28:41).

Yafuatayo ni madondoo machache ya wanazuoni mashuhuri wa kisunni kuhusu imam na sifa zake. aalim mashuhuri wa kihindi katika kitabu chake madhahibul islam katika ukurasa 106 aandika:

Imam ni mwakilishi wa mtume(s.a.nv.w) na kwa niaba yake ni mtawala na mhifadhi wa mambo yao duniani na mtoaji mwongozo kuhusu mambo ya kidini, kudumisha elimu ya dini, kutekeleza maagizo ya kiislam, kuamrisha watu kutenda mema, na kuwakataza watu waache maasi, kupingana na makafiri na kuwapa adhabu wahalifu kufuatana na mwongozo wa dini."

licha ya hayo, katika madhehebu ya sunni neno la "imam" hutumika katika maana ya kawaida tu. Mtu yeyote ambaye ni mtaalamu katika hadithi na sheria ya kiislam vile vile huweza kuitwa imam. k.m.

Imam ghazali, imam shafi, imam abu hanifa. lakini hata hivyo wanaamini kwamba kuwa mrithi (mwakilishi) wa mtume(s.a.w.w) na faradhi za mtume(s.a.w.w) imam lazima awe na masharti yafuatayo.

Imam lazima awe:

1) Mwislam.

2) Mwanamume.

3) Mtu huru (asiwe mtumwa)

4) Awe na akili timamu.

5) Awe amebaleheghe (siyo mtoto mdogo)

6) Awe mcha mungu (asiwe mtenda maasi)

7) Awe anatokana na kabila la quraishi.

8) Asiwe na kilema cha aina yoyote; kiziwi, bubu au kipofu.

9) Awe mtaalam katika sheria ya kiislam.

Imam wa 32 wa ismaili (wafuasi wa aga khan) shah mustansir billah, ameandika sifa za watakatifu katika kitabu chake kiitwacho "fidi aad jawan mardi".

Kitabu hiki kinahesabika kuwa ni cha uhakika wa hali ya juu kwa waismailia na vile vile kuna makala ya watakatifu. toleo moja la kitabu hiki kilichapishwa katika mwaka wa hindoo 1961 na laljibhai devraj katika lugha ya kiajemi (persian) lakini katika hija ya kihindi. katika ukurasa wa 94 sifa za watakatifu zimeelezwa "eh waumini, jueni kwamba "peer" (mtakatifu) huwa mtu thabiti, pili humkumbuka na kuamini mungu, na wajibu wake ni kutafakari, kuhubiri na kuhutubia juu ya ukweli.

Yeye lazima kwanza hujitaradhia nafsi yake kabla ya kuwasihi wengine." "tena katika kurasa 94-96 anaendelea: "mtakatifu wa haki ni yule ambaye ni mwenye matamanio katika makuu ya dunia, huepuka kwenda pahala pasipo pazuri na vitendo vya fuska, mwenye subira, makini, mkweli na mcha mungu". mwishowe tunasimulia hadithi moja kuhusu sifa za imam, kutoka kitabu cha shia ithnaasheri. hassan bin fadhal asimulia kutoka kwa baba yake kwamba Imam Ali-ridha(a.s) , imam wa nane, ameeleza sifa 30 zinazo mhusu imam, nazo ni:

1. Imam lazima awe na elimu zaidi kuliko watu wote wa wakati huo.

2. Awe kiongozi na mwamuzi wa watu wote.

3. Awe ni mtu mwenye subira zaidi kuliko wote katika karne

anayoishi.

4. Awe mcha mungu zaidi kuliko watu wote wa wakati wake.

5. Awe shujaa kuliko wote.

6. Awe mtu mwenye dini na mwabudu mungu zaidi kuliko wote.

7. Awe mkarimu kuliko wote.

8. Awe amezaliwa akiwa ametahiriwa.

9. Huzaliwa msafi na huwa mcha mungu.

10. Huweza kuona nyuma yake kama anavyoona mbele bila kugeuka nyuma.

11. Hawi na kivuli cha mwili wake.

12. Anapozaliwa papo hapo huweka viganja vyake juu ya ardhi

(Sakafu).

13. Hutoa shahada juu ya upekee wa mungu na utume (unabii) wa

Mtume muhammad(s.a.w.w)

14. Hapati ndoto za unyevunyevu.

15. Hata akiwa amelala huwa macho kifahamu.

16. Malaika huja kumwamkia na kuzungumza naye.

17. Deraya ya mtume(s.a.w.w) humtosha barabara.

18. mkojo au kinyesi chake hakionekani na mtu yeyote. hunyonywa

(mezwa) na ardhi, haiwi na harufu mbaya lakini hutoa harufu ya

ambari na miski."

19. Hudhibiti maisha ya watu.

20. Huwa na huruma zaidi juu ya watu kuliko wazazi wao.

21. Huwa mnyenyekevu mno katika swala zake na ibada ya mungu.

22. huwa wa kwanza katika kutekeleza amri za mungu.

23. Hujizui kwa dhati na juhudi kuepuka na maasi.

24. Dua zake zote hutakabaliwa na allah na hakuna kitu anachomwomba mola hukataliwa na mungu, akimwomba mungu jiwe gumu lipasuke hupasuka.

25. Huwa anamiliki deraya ya mtume(s.a.w.w) pamoja na upanga wake dhulfikar.

26. Huwa na daftari lenye orodha ya wafuasi wake wote pamoja na

wale ambao watakao zaliwa mpaka siku ya hukumu.

27. Huwa na kitabu chenye orodha ya maadui wake wote.

28. Huwa na jaamiah yenye urefu wa yadi 70 ambamo kuna maelezo kamilifu kuhusu mambo ya dunia.

29. Huwa na nyaraka kubwa iliyo tengenezwa kwa ngozi ya mbuzi na nyingine ndogo iliyotengenezwa kwa ngozi ya kondoo ambazo huitwa jafar kuu na jafar ndogo ambazo zinaeleza kanuni zote za kidini hata kuhusu mambo madogo kama vile sheria inayomhusu mtu akimcho mamwezie kwa ukucha.

30. Huwa na kitabu alicho rithishwa kutoka mwana fatima(a.s) binti muhammad(s.a.w.w) .

Ikiwa mtu hana hizo sifa 30, basi kwa mujibu wa itikadi ya shia ithnaashery hawezi kamwe kukubaliwa kuwa imam.

Kwa hakika ni wajibu wa mtume(s.a.w.w) na warithi wake kumi na wawili kuishi maisha kwa mujibu wa amri za mola na kanuni zilizoandikwa katika qur'an tukufu na kuongoza waislamu ili kuishi maisha ya kidini bila kuleta mabadiliko ya aina yoyote katika amri takatifu. kuhusu jambo hilo tunakumbusha aya chache zinazohusika za qur'an:

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾

Wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa (53:3- 4).

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ ﴿٤٤﴾

"Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri." (5:44).

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٤٥﴾

"Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhaalimu." (5:45).

ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٍ مِّنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٨﴾

"Kisha tukakuweka wewe juu ya Njia ya haya mambo, basi ifuate, wala usifuate matamanio ya wasio jua kitu". (45: 18)

وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الْأَقَاوِيلِ ﴿٤٤﴾ لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ ﴿٤٥﴾ ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ الْوَتِينَ ﴿٤٦﴾ فَمَا مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَاجِزِينَ ﴿٤٧﴾

Na angalikuwa amezua chochote kinyume cha amri zetu, kwa hakika tungelimtwaa upande mkono wa kuume na baadaye tungelikata mishipa yake ya damu upande wa kushoto wa moyo. Na hakuna hata mmoja katika nyinyi angeweza kumkinga." (69:44-47).

Wakati hata mtume mtukufu(s.a.w.w) hana madaraka ya kuongeza au kupungu za, kubadilisha au kugeuza yaliyoteremshwa (wahyi) na allah kama ilivyoelezwa katika qur'an tukufu. Basi kwa hakika imam(a.s) pia hana uwezo wa namna hiyo. Maimam wote(a.s) ni viongozi wa wafuasi, huwafunza amri za mungu kama alivyofunza mtume(s.a.w.w) .

Kwa hiyo ni jambo la lazima kuwa elimu ya maimam(a.s) kuhusu qur'an tukufu na hadithi iwe bora kuliko ya waislam wote.