ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE0%

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE Mwandishi:
Kundi: Imam mahdi (a.s)

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

Mwandishi: Marehemu Mulla Muhammad Jaafar Sherif Dewj
Kundi:

Matembeleo: 20778
Pakua: 2984

Maelezo zaidi:

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 20 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 20778 / Pakua: 2984
Kiwango Kiwango Kiwango
ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

Mwandishi:
Swahili

4

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 4

UIMAMU NA UKHALIFA

Uteuzi wa imam na khalifa ulifanywa na mtume mtukufu(s.a.w.w) kutokana na agizo la mungu peke yake. Kwa hiyo hakuna imkani yoyote ya kuwahusisha watu katika uteuzi huo. mwenyezi mungu amesema katika qur'an:

وَرَبُّكَ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَيَخْتَارُ مَا كَانَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ سُبْحَانَ اللَّـهِ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٦٨﴾

Na Mola wako Mlezi huumba na huteuwa atakavyo. Viumbe hawana khiari. Mwenyezi Mungu ametukuka na ametakasika na hao wanao washirikisha naye (28:68).

Katika qur'an tukufu allah amewateua manabii Adam na Daudi kuwa makhalifa tu; wawakilishi wake duniani

يَا دَاوُودُ إِنَّا جَعَلْنَاكَ خَلِيفَةً فِي الْأَرْضِ ﴿٢٦﴾

Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. (38:26).

Hata hivyo licha ya kumteua awe nabii na khalifa vile vile alimpa hadhi ya kuwa imam". kwa hakika mimi nitakufanya wewe imam". (2:124).

Kutokana na hadithi mashuhuri ya mtume(s.a.w.w) , watakuwa warithi kumi na wawili baada yake. Wanazuoni mashuhuri wa madhehebu ya kisunni wameukubali ukweli wa hadithi hiyo na kunakili katika vitabu vyao. vile vile katika historia ya kiislam, banu ummaya, na banu abbasi walikuwa watawala wa kidunia tu, wao kamwe hawakuteuliwa na mtume mtukufu(s.a.w.w) . kwa hakika kufuatana na hadithi zingine, mtume(s.a.w.w) mewaatangaza hao kuwa ni waghasibu wa ufalme.

Kwa hakika warithi na makhalifa wa mtume(s.a.w.w) ni maimam kumi na wawili ambao kama mtume(s.a.w.w) mwenyewe, ni katika kizazi bora cha hashim wa kabila la quraishi na kupewa madaraka juu ya viumbe vyote. walikuwa na elimu na uwezo wa kufanya (kuleta) miujiza na sifa zote alikuwa nazo mtume(s.a.w.w) . kama alivyo yeye (mtume) walikuwa wametakasika kwa kila uovu na dhambi. Hawa ni maimamu waliotajwa na allah katika qur'an tukufu kuwa ni "watu wa kweli wenye madaraka na walio takasika". mwanazuoni wa kisunni fak-ruddin Razi, katika kitabu cha Tafsir Al-kabir, juzuu ya 3, ukurasa 357, kilichochapishwa misri, ameeleza kwamba amri ya "kumtii mungu, mtume wake na wale wenye madaraka" (4:54). Inamaanisha kwamba: wale wenye madaraka ambao utii wao uliamrishwa katika qur'ani ni wale tu wasio kuwa na dhambi na wasioweza kukosa; la sivyo, inamaanisha kwamba mungu ametuam risha kuwafuata wale wanaoweza kukosa kueleza amri za mungu.

Utambulisho wa hao maimam kumi na wawili warithi wa mtume(s.a.w.w) , umethibitishwa na hadithi chache ambazo zimenakiliwa katika vitabu vya kisunni. Shaikhul islam, sheikh suleiman hanafi nehshabandi kanduzi balkhi aliyefariki 1294 (a.h.) na aliyekuwa mtakatifu mkuu wa sultani wa istanbul (uturuki) abdul aziz khan, ameandika katika kitabu cha: Yanabiu Al-mawaddah kurasa 369-71 (kama ilivyotafsiriwa katika kiingereza) "yahudi mmoja mwenye jina la naathal alikuja kuonana na mtume(s.a.w.w) na kutaka maelezo kuo.ndosha shaka alizokuwa nazo na kuahidi kwamba akipata maelezo ya kumtosheleza kutoka kwa mtume(s.a.w.w) atakubali dini ya uislam.

Mtume(s.a.w.w) alimruhusu kuuliza maswali yake. kwanza yeye (naathal) aliuliza juu ya upwekee wa allah na sifa zake, na kupata majibu ya kumtosheleza. baadaye akauliza maswali, juu ya urithi wa mtume(s.avw.w) na wa kila mtume na utangazaji wa warithi wao (warithi wa mitume kabla ya muhammad(s.a.w.w) , kabla kufariki dunia k.m. nabii moosa alimteua yushae bin noon, mtume(s.a.w.w) akajibu "mrithi wangu mimi ni ali ibn abi talib, baada yake watakuwa wajukuu wangu wawili hassan na hussein na baada ya hao watakuwa maimam tisa ambao watatokana na kizazi cha hussein (a.s) ; nao ni warithi wangu". hapa huyo yahudi aliuliza majina ya hao maimam tisa na mtukufu mtume alisema "baada ya hussein atakuwa mwanawe ali ibni hussein, na baada yake atakuwa mwanawe muhamedl bin ali (baqir)na baada yake jaffer sadiq na baada yake mussa kadhim na baada yake ali ridha na baada yake muhamad taki na baada yake ali naqi na baada yake hassan na baada yake mwanawe muhammad mehdi.

Hayo ndiyo majina ya warithi wangu kwa mpangilio huo". Myahudi yule tena alimwomba mtume(s.a.w.w) amweleze hao warithi wake watatu yaani ali, hassan na husein watafariki dunia namna gani. Mtume(s.a.w.w) akamjibu "hadhrat ali (a.s) atauawa na upanga, hassan atapewa sumu na hussein atauawa kwa (kuchinjwa) huku ana njaa na kiu ya siku tatu". myahudi tena akamwuliza mtume(s.a.w.w) kama hao mashahidi watakuwa na mtume(s.a.w.w) huko peponi. Na hapo mtume(s.a.w.w) akajibu "hao watakuwa na mimi peponi". Hapo myahudi akakiri shahada takatifu, na akawa mwislamu, na akasema "eh mtume wa mungu bila shaka hao uliowataja ni warithi wako. Hao wametajwa kwa kirefu katika vitabu vya manabii waliopita na vilevile katika maagano ya nabii mussa. Imeelezwa wazi humo kwamba atakuwa nabii katika kipindi cha mwisho akijulikana kwa majina ya ahmad na muhammad na ndiye wa mwisho wa manabii na baada yake hatakuwa nabii yeyote.

Yeye (nabii) atakuwa na warithi kumi na wawili; wa kwanza ni binamu yake na mkwewe; wa pili na watatu watakuwa ndugu. Mrithi wa kwanza atauawa kwa upanga, wa pili kwa sumu na watatu atauawa jangwani pamoja na wanawe na masahaba wake wakiwa na njaa na kiu ya siku tatu. watakabili misiba yote kwa subira na watapewa jazaa na mungu na kutukuzwa na uwezo wa kuokoa marafiki na wafuasi wake kutoka kwenda motoni. walio biki lisa watatokana na kizazi chake (hussein) na kwa ujumla watakuwa kumi na wawili kama idadi ya "asbat". Mtume mtukufu(s.a.w.w) baadaye akamwuliza kama anajua habari za asbat. Yeye akajibu "ndiyo walikuwa kumi na wawili na katika hao lawa bin barkhya alighibu na kujitokeza tena na kupigana na mfalme wa karastya na kumwua". Mtume mtukufu(s.a.w.w) akaendelea kusema: "kwa hakika yale yaliyo wakabili mayahudi yatajiri kwa wafuasi wangu. Mrithi wangu wa kumi na mbili ataghibu. katika siku hizo uislam utabakia kwa jina tu . Qur'an itasomwa kama kawaida ya dini lakini bila kufuatwa kwa vitendo.

Wakati dhulma (kufuru) itakapokuwa imetawala mrithi wangu wa kumi na mbili atajitokeza na kuufufua tena uislam, haki na insafu. watao bahatika ni wafuasi wale ambao wataomtii yeye (mehdi) na ghadhabu ya mungu itawasubiri wale ambao watamhalifu yeye (mehdi)." tena katika kitabu hicho, ukurasa 371, sura ya 77, kuhusu hadithi ya mrithi wa kumi na mbili ameeleza chini ya kichwa cha 'tahkik' (uthibitisho) kuwa: "imesimuliwa kwamba jabir bin saamra, mmojawapo wa masahaba wa mtume(s.a.w.w) , amesema kwamba uislam utadumu kwa sababu mrithi wangu wa kumi na mbili atakuwepo na warithi wangu wote watatokana na nambari ya qureish." vitabu vilivyo andikwa na bukhari, muslim na tirmidhi vinaeleza hadithi hiyo ilivyo. Zaidi ya hayo yahya bin hassan katika kitabu chake umdah ameelezea kwamba kuna hadithi 20 za mtume mtukufu(s.a.w.w) za kusimulia kwamba warithi wake kumi na wawili wote watatokana na mbari ya quraish.

Vitabu mashuhuri vya sunni kama vile vya bukhari na hamid vimesimulia hadithi tatu na. Tirmidhi vile vile kaandika hadithi moja juu ya jambo hilo. Muslim aandika kwamba abdi saad, sahaba wa mtume(s.a.w.w) alimwandikia samra kumwuliza kwamba alisikia hadithi yoyote kutoka kwa mtume(s.a.w.w) . samra katika jibu akaeleza kwamba siku ya ijumaa ambayo aslami alipigwa mawe mpaka akafariki, mtume(s.a.w.w) alisema uislam utaendelea mpaka siku ya kiyama na watakuwa warithi wake kumi na wawili baada yake na wote watatokana na ukoo wa quraishi. Hadithi nyingi zilizoandikwa katika vitabu vya sunni zathibitisha kuwapo kwa warithi kumi na wawili waliotajwa na mtume(s.a.w.w) wanatokana na ukoo wa quraishi. Kwa hakika warithi kumi na wawili waliotajwa hawawezi kuwa wengine ila wale tu wanaokubaliwa na mashia ithnaasheri. hawawezi kuwa na uhusiano wowote na makhalifa wa bani umayya kwa sababu hawakuwa kumi na wawili na ambao walikuwa wadhalimu ila mmoja omar bin abdulaziz ambaye alikuwa mwema. Vile vile hao bani umayya hawakuwa katika kizazi cha hashim kama ilivyoelezwa katika hadithi nyingi za mtume(s.a.w.w) . vile vile hawawezi kuwa makhalifa wa bani abbas kwa sababu hawakuwa kumi na wawili na walikuwa madhalimu na maadui wa ahlul-bait wa mtume(s.a.w.w) .

Hivyo, uhakika ni kuwa warithi kumi na wawili waliotangazwa (tajwa) na mtume(s.a.w.w) ni maimam kumi na wawili kutokana na dhuria ya mtume(s.a.w.w) na katika uhai wao hawakuwa na mtu yeyote aliyelingana nao katika elimu, ibada, atakuwa na ushujaa. hakuna wengine wanaostahili sifa zilizoelezwa kutokana na hadithi za mtume(s.a.w.w) isipokuwa hao maimam kumi na wawili. tena katika kitabu hicho hicho sura ya 78, ukurasa 374, mwandishi amenakili: "katika kitabu faraedussimtayn imeelezwa kwamba mtume mtukufu(s.a.w.w) ameeleza bayana kwamba yeyote asiye amini katika kujitokeza kwa mehdi ni kafiri na yeyote asiye amini kuja kwa nabii issa kutoka mbinguni vile vile ni kafiri na yeyote asiye amini kujitokeza kwa dajjal mwenye jicho moja tu vile vile ni kafiri."

zaidi ya hayo, katika kitabu hicho hicho imesimuliwa hadithi kutoka kwa mtume mtukufu(s.a.w.w) iliyo andikwa na ibnu abbas kwamba yeye (mtume) amesema "watakuwa warithi kumi na wawili baada yangu ambao watakuwa hujjah (dalili) ya mungu juu ya viumbe wake. Wa kwanza atakuwa hadhrat ali(a.s) na wa mwisho hadhrat mehdi(a.s) . wakati huo wa mehdi(a.s) ardhi itang'aa na utawala wake utaenea kote kote duniani".

Waislamu wote, mashia na masunni, huamini kwamba watakuwa warithi kumi na wawili wa mtume(s.a.w.w) . hivyo imebainika kutokana na hadithi mashuhuri kwamba warithi wa kweli kumi na wawili kufuatana na hadithi za mtume(s.a.w.w) ni wale kumi na wawili wanao kubaliwa na shia ithnaasheri; wa kwanza ni ali ibn abi talib (a.s) na wa mwisho wao ni imam wa kumi na mbili imam hadhrat muhammad mehdi(a.s) . hata hivyo, kuna hadithi mbili katika vitabu vya sunni zinazonakili majina ya maimam kumi na wawili. Itabainika kuwa kukamilisha idadi hiyo ya kumi na wawili, hadithi hizo zinamtaja muawiyya pamoja na mwanawe yazid n.k. ambao hawastahili kuitwa warithi wa mtume(s.a.w.w) . mulla alikari katika kitabu cha 'sharhe mishkat' na tena katika kitabu 'sharhe akber' amenakili majina kumi na mbili y amakhalifa wanao aminiwa na masunni.

1) Abu Bakar

2) Omar

3) Othman

4) Ali bin Abi Twalib(a.s)

5) Muawiyya

6) Mwana wa muawiya Yazid

7) Abdul Malik bin Marwan na wanawe wane

8) Walid

9) Suleiman

10) Hisham

11) Yazid

12) Omar bin Abdulaziz.

Suyut katika kitabu 'tarikhul khulafaa' (historia ya makhalifa) amenakili kutoka sahihi bukhari na sheikhul islam ibnu hajar kuwa: "kutokana na hadithi zinazo kubalika, waislamu wanakubaliana kuwepo makhalifa wafuatao:

1. Abubakar

2. Omar

3. Othman

4. Ali bin Abi Twalib(a.s) na baadaye hapakuwa na makubaliano juu ya urithi wa imam hassan(a.s) kulikuwa na mapatano ya kumkubali

5. Muawiya na baadaye imam hussein(a.s) ambaye hakurithi kwa sababu aliuawa "shaheed", kwa hivyo

6. Yazid alikubaliwa na watu wakala kiapo cha utii kumkubali yeye yazid. baada ya kifo cha yazid kulikuwa na mafarakano juu ya urithi lakini wengi wakamkubali abdul malik baada ya kuuawa ibnu zubeir. (baada ya yazir marwan alitawala kwa muda ya miezi sita tu na mwanawe abdul malik aliendelea kwa miaka 21 lakini wote wawili hao hawakuorodheshwa).

katika orodha ya makhalifa kutoka taarifa tuliyotaja kwanza abdul malik ametajwa ni khalifa wa saba lakini katika orodha ya pili ya makhalifa hakutajwa kabisa.

7. Baada ya yazid wana wanne wa abdul malik wanakubaliwa kuwa warithi, nao ni walid

8. Suleiman

9. Yazid

10. Hashim na baada ya hao

11. omar bin abdulaziz (kama alivyoorodheshwa wa kumi na mbili katika orodha ya kwanza kutokana na hadithi)

12. walid ibnu yazid ibnu abdul malik bin marwan (ambaye kutokana na hadithi iliyotajwa atakuwa khalifa wa kumi na tatu).

kwavyo, huthibitika kutokana na maandishi ya waislamumashuhuri na hadithi za kuaminika kwamba maimam kumi na wawili wanaofuatwa na shia ithnaasheri ni warithi wa kweli. katika hao wa kwanza ni hadhrat aii ibn abi talib(a.s) na wa mwisho ni hadhrat mehdi(a.s) ..

5

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 5

HADITHL KUHUSU KUWEPO KWA IMAM WA ZAMA HIZI

Hadhrat Mahdi(a.s) wanazuoni wengi mashuhuri wa madhehebu ya kisunni wameandika kuhusu kuwapo kwa hadhrat mehdi(a.s) katika vitabu vyao. kati ya hao tunaorodhesha majina ya wanazuoni 14:

1) Shaikh Kamil Abdul Wahab Sharam.

2) Mulla Ali Asadullah Akbar bin Mawdudi.

3) Mulla Nurdin bin Abdulrahman bin Ahmad jamii.

4) Khaja muhammad parsa, Ahmad bin Mahmoud Al hafizi.

5) Sheikh Abdul Haqi Muhadith Dehlawi,

6) Allama Sheikh Nuruddin bin Sabag Maliki.

7) Shah Waliyullah Muhaddis Dehlawi.

8) Allam Hamwayn Shafi'i mwandishi wa Faraidu Simtayn.

9) Sheikh ata Naishapuri.

10) Sheikh Kabir Shamshudin Tabrizi.

11) Sheikh Neimkillah Al Walli.

12) Sheikh Kamil Arif Matuk Misri.

13) Sheikh Saad bin Hamawi.

14) Shaik Suleiman bin Ibrahim Balkhi Kunduzi sheikhul islam wa Istambul (uturuki) na mwandishi wa wa kitabu kinacho julikana sana katika madhehebu ya sunni Yanabiu Al-Mawaddah.

Waandishi hao wote wameandika katika vitabu vyao kuwa mwana wa hadhrat Imam hassan askari(a.s) , hadhrat Mahdi(a.s) yu hai na ameghibu.

Licha ya hayo wanazuoni wengi wengine wamenakili taarifa kama hizo katika vitabu vifutavyo:

1. Kitabu cha Jaamiul- Usul, kikitumia ushuhuda uliopo katika Bukhari, Muslim. Abu Dawood na Tirmidhi wamenakili matamshi ya Abu Hureira kwamba: Mtume(s.a.w.w) alisema:"Miongoni mwa wafuasi wangu kikundi kimoja kitatangaza jihadi ya kushinda vita vyote. hapo nabii Issa atateremka kutoka mbin guni na kiongozi wa hicho kikundi hadhrat mehdi (a.s) atamkaribisha nabii Issa kuongoza swala ya jamaa lakini nabii Issa atajibu "wewe ndiye mwenye mamlaka (madaraka) juu ya viumbe wa Mungu na kutokana na dhuria ya mtume Muhammad (s.a.w.w) Mwenyezi Mungu amekutunukia heshima na ubora kuliko waumini wote wa wakati huu". kanji, mfuasi wa ushafi'i, vile vile amenakili hadithi hii na ametilia mkazo kwamba hadithi hiyo ni sahihi.

2. Hafidh Abu Nairn na Tabarani katika kitabu chao Muazamu -akber wamenakili kwamba mtume muhammad(s.a.w.w) amesema: "Baada yangu watakuja makhalifa ambao baadhi yao watakuwa watawala na baadhi yao watakuwa wafalme dhalimu.

Baada ya hapo atakuja mehdi kutokana na kizazi changu kama mungu alivyoahidi na atatokeza na kueneza unyoofu na uadilifu katika dunia hii.

3. mwanazuoni anaye aminiwa sana katika madhehebu ya sunni huko india obeidullah amratsari, amenakili katika kitabu chake arjahul ma talib, ukurasa 472, kwamba sheikh abu abdullah na muhammad bin yusufu kanji shafi katika kitabu chao al bayan fi akhbare-sahibuz-zaman ameandika kwamba hadhrat mehdi(a.s) yu hai na ameghibu na kuna sababu nyingi za kuthibitisha hayo. Kwa mfano nabii issa, nabii idris na nabii ilyas ni mitume ambao wamekuwa hai kwa miaka maelfu na vile vile katika maadui wa mungu, dajjal na iblis watakuwa hai mpaka muda maalum; kwa hivyo hakuna cha kustaajabisha kwamba hadhrat mehdi(a.s) yuna umri wa miaka 1100.

4. Ibnu hajar hanafi makki katika kitabu chake sawaikul muhrika, ukurasa 481, ameandika kwamba jina la hadhrat mehdi(a.s) ni muhammad na majina mengine yake maarufu yanayo julikana ni: abul qasim na lakabu ni mehdi, saleh, qaaim, muntadhar, na sahibuz-zaman. wakati alipofariki baba yake hadhrat imam hassan askari(a.s) , imam mehdi(a.s) alikuwa na umri wa miaka mitano tu. mwenyezi mungu alimjaalia elimu hekima katika utoto wake. sababu ya kupatiwa lakabu ya qaaim ni kuwa yupo hai lakini ameghibu na maskani yake hayajulikani.

5. Katika kitabu hicho hicho, ukurasa 102, imeandikwa kwamba hadhrat mehdi(a.s) atajitokeza kabla kurudi (kuteremka kutoka mbinguni) nabii issa. katika hadithi nyingi mtume mtukufu(s.a.w.w) amesisitiza kwamba hadhrat Mahdi(a.s) atatokana na kizazi chake na baada ya kujitokeza atatawala kwa muda wa miaka saba na kustawisha insafu duniani na baada ya muda mfupi tu nabii issa atateremka kutoka mbinguni na hadhrat mehdi(a.s) atamwua dajjal.

Kuna hadithi nyingi kuhusu hadhrat mehdi katika vitabu vinavyojulikana sana katika madhehebu ya sunni lakini bado baadhi ya wanavyuo wa kisunni wanaamini kwamba hadhrat medhi hajazaliwa bado na baadaye ndiyo ataeneza insafu duniani. ijapokuwa hiyo ni baadhi ya imani ya maulamaa wa kisunni, lakini kutokana na wingi wa hadithi na ushahidi wa kihistoria ni dhahiri kwamba hadhrat mehdi(a.s) alikwisha zaliwa tarehe 15 shaban 255 a.h. kwa hiyo, si jambo la kubishana tena juu ya kuzaliwa kwake. mwanazuoni wa kuaminika mno wa kisunni, muhammad yazeed hafiz bin maajah (aliyefariki dunia 273 a.h.) katika kitabu chake sunan ibni maajah ameandika (kurasa 518/519) kwamba zipo hadithi nyingi za mtume muhammad(s.a.w.w) kuhusu hadhrat mehdi(a.s) kuwa atatokana na dhuria yake na kizazi cha binti wake fatima(a.s) . atakuwa ameteuliwa kwa amri ya allah na atakuwa mrithi wake. Mtume mtukufu(s.a.w.w) tena amewataradhia waislamu wote kwamba wakipata bahati ya kuonana naye (kuwa hai katika karne ya hadhrat mehdi(a.s) basi wamtii yeye. vile vile ameeleza kwamba hamza, jaffar, ali, hassan, hussein na mehdi watakuwa viongozi huko peponi.

Imam Ahmad bin Hambal (aliyefariki 240 a.h.) mwandishi maarufu wa vitabu vya kisunni amearidhia katika sehemu ya kwanza ya kitabu chake musnad, ukurasa 99, kwamba imesimuliwa kuwa "mwenyezi mungu atamleta mehdi(a.s) aliyetokana na dhuria yangu kutoka mafichoni kabla ya siku ya kiyama, japokuwa ikibakia hata siku moja kabla mwisho wa dunia, naye ataeneza haki, usawa na usalama duniani na kutokomeza dhuluma na ukandamizaji." sheikh-ul-islam wa istanbul, sheikh suleiman nakshbandi hanafi, katika kitabu cha yanabeeul-mawaddah, katika ukurasa wa 494, amenakili masimulizi kutoka kwa jabir bin abdullah ansari kuwa Mtume(s. a.w.w) amesema: "Baada yangu watakuwa maimam 12; wa kwanza ni Ali, na watakaofuata baada ya Ali ni Hassan, Hussein, Ali bin Hussein, Muhammad bin Ali(a.s) (Baqir). Eh! Jabir wewe utabahatika kuonana na huyo Baqir(a.s) , tafadhali mpe salam zangu. Na baada yake, Jaffar bin Muhammad. Mussa bin Ali bin Muhammad, Hassan bin Ali na Baada yao atakuja msubiriwa Mahdi(a.s) . Mahdi atakuwa mrithi wa kumi na mbili na wa mwisho. yeye atakuwa na jina langu na lakabu ya kassim. atakuwa mwana wa Hassan bin Ali, Al-Askari.

ahmad bin hajar makki katika kitabu chake sawaikulmuh-rika, ukurasa wa 116, na vile vile tirmidhi katika kitabu chake jame-a, ukurasa wa 33, wamenakili kwamba mtumemtukufu(s.a.w.w) amesema, "baada yangu watakuwa warithi wangu kumi na wawili ambao watakuwa makhalifa wangu na hao wote watatokana na mbari ya quraishi".

Sheikhul-kamil, Abdul Wahab, amearidhia katika kitabu chake yawakit wa jawahir kuwa, "wakati dunia itapojaa ukandamizaji na ukafiri ndipo hadhrat mehdi(a.s) atatokeza. yeye (hadhrat mehdi(a.s) ni mwana wa hadhrat hassan al- askari(a.s) , alizaliwa tarehe 15 shaaban 255 a,h. na yupo hai duniani. wakati nabii issa atapoteremka kutoka mbinguni yeye (mehdi a.s.) atatokeza na kuishi naye; wakati wa kuandika kitabu hiki umri wake (hadhrat mehdi a.s.) ulikuwa umekwisha timia miaka 1146."

Abu Abdullah muhammad bin muhammad bin yusuf muhammad bin kanji shafii amenakili katika kitabu chake "kifayya tut-talib" kuwa: "haiwezi kupingwa kwamba hadhrat mehdi(a.s) yu hai hadi leo. Dalili kwamba yeye anaweza kuwa hai kwa muda mrefu inatokana na uhakika kwamba manabii issa, khidhr na elias wapo hai duniani kwa miaka elfu kwa maelfu. Hao ni manabii wa mungu, lakini maadui wake (mungu) pia kama dajjal mwenye jicho moja na lblis aliye laaniwa wapo hai hadi leo kama ilivyo thibitishwa katika qur'an.

6

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 6

HADHRAT MAHDI (A.S.) NI IMAM WA KUMI NA MBILI

Kuna hadithi nyingi mno katika madhehebu ya shia ithnaasheri kuthibitisha kwamba hadhrat mehdi(a.s) ni imam wa kumi na mbili. katika sura hii tutanakili mateuzi machache kutoka vitabu vya kisunni na vya ismaili, wafuasi wa agakhan, kuthibitisha ukweli huo. Waislamu wote wanakubaliana kwa kauli moja ukweli wa hadithi ya mtume mtukufu(s.a.w.w) kwamba baada yake idadi ya warithi wake itakuwa kumi na wawili. mwandishi wa kisunni abdul wahab katika kitabu chake "Al- yawaqit wal Jawahir" amenakili kuwa "wakati dhuluma na kufuru itapozagaa duniani hadhrat mehdi(a.s) atatokeza, yeye ni mwanae imam hassan askari(a.s) alizaliwa tarehe 15 shaaban mwaka 255 (a.h) na ataishi mpaka atapokutana na nabii issa."

Shaikhul islam, mwanazuoni wa kisunni Ahmed Jami, katika kitabu chake 'nafsatulanas' katika lugha ya kiajemi amesimulia kishairi, kwa mapana na marefu majina ya maimam kumi na wawili na ameeleza kwamba: "hadhrat imam Hassan askari(a.s) ni mwanga unaoongoza dunia na mwanae hadhrat mahdi(a.s) hana kifani duniani. molvi jallaludin rumi katika tenzi zake za "divan" ametaja majina ya maimam kumi na wawili na kuthibitisha kwamba hadhrat mehdi(a.s) ni imam wa kumi na mbili.

Katika 'Tadhkiratul Kiram' ya Molavi shah mohamed kabir, ukurasa 270, imearidhiwa kutoka masimulizi sahihi kwamba kutakuwa na urithi wa namna mbili: moja bayana na moja ya kisiri (kufichika), urithi wa namna moja tu utaendelea mpaka

Imam Hassan Al-askari(a.s) , lakini baada yake namna zote mbili zitatokeza na hapo baadaye imam wa kumi na mbili atafuata.

Shah Abdul Aziz na imam ghazali katika' Ihyaul-uloomm. mulla moin katika 'dirasatul labib na ibne Hajar As-kalani katika 'FAthul Bari wote ambao wanazuoni mashuhuri wa kisunni wanakubaliana kwa pamoja kwamba elimu ya maimam kumi na wawili hutoka kwa allah moja kwa moja. maimam kumi na wawili pamoja na mtume mtukufu(s.a.w.w) na binti yake fatima(a.s) ni watakatifu kikamilifu (masumin) na kuhusu hao kumi na wanne kuna makubaliano ya kauli moja baina ya waislam kwamba tokea kuzaliwa mpaka kufa kwao hawakutenda dhambi ya aina yoyote wala kukosea. (tarikhul islam, .juzu 1, ukurasa 29).

Katika kitabu chake kiitwacho 'Kanzul Masaib" kurasa 9-10 na 22 na 23, aga khan, his highness hassanali shah saheb amearidhia juu ya imani ya maimam kumi na wawili. uthibitisho wa ziada umeelezwa katika hukumu iliyotolewa na jaji maarufu wa kiparisi katika daawa ya "mahuwa commission" ambayo imenakiliwa kwenye ukurasa wa 56 kuwa: "kanzul Masaib" ni kitabu cha lugha ya kiajemi (irani) na imeandikwa kwa amri na msaada wa muadham muhammad hassan el husseini. Mualifu wa kitabu hicho ni Ibrahim Isfahani na kitabu hicho kilichapishwa mwaka 274 a.h. katika kurasa 22 na 23 za. kitabu hiki majina ya maimam kumi na wawili yametajwa bayana".

Ibratulafza' ni kitabu katika lugha ya farsi kilicho andikwa na agakhan i kuhusu maisha yake mwenyewe. mateuzi hayo yalitafsiriwa katika lugha ya gujarati mwaka 1865 b.k. na bawana karim dadaji na kuchapishwa na oriental press bombay. Katika ukurasa 19, ameandika, "kwa karne nyingi baba zangu walikuwa na vyeo vya uwaziri katika serikali ya misri. wao walikuwa wanafuata kanuni za imani ya jaafery na sheria zilizowekwa na maimam kumi ria wawili."

Aga Jahangir shah mwana wa aga khan i, amechapisha risala yake kuhusu ibada katika farsi. Hiyo ilichapishwa na datprasad printers bombay mwaka 1313 a.h. humo yeye ameandika kwamba: mimi natoa ushahidi kwamba hadhrat ali murtadha(a.s) na wanawe (watoto wake kutokana na kizazi chake) kumi na moja ni warithi wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) na kila mmoja ni imam wa kweli (haki). kutokana na mateuzi hayo matokeo ya 'mahuwa commission ukurasa 57 imearidhia kuwa: "aga khan wa karne hii amekubali mahakamani ukweli wa mateuzi hayo. zaidi ya hayo kulikuwa na ushahidi kwamba mama yake aga khan bibi alishah na mkewe vile vile wakiamini maimam kumi na wawili.

Aga Khan wa pili, his highness aga ali shah, alitoa mateuzi yake kuhusu kanuni za swala na mfungo wa ramadhani katika lugha ya kisindhi. kwenye ukurasa wa 15, mstari wa 17 katika "mahuwa commission report," kumeelezwa kuhusu maamkizi kwa imam wa kumi m mbili(a.s) . vile vile mstari wa 17 ukurasa 34 kuna maagizo kuhusu maamkizi kwa imam hussein(a.s) .kadhalika, katika mstari wa 6 ukurasa 35 kumeelezwa juu ya maamkizi kwa imam wa kumi na mbili. kwenye ukurasa huohuo, mstari wa kumi, unatoa amri ya kum womba mungu kwa kutaja majina ya "Muhammad, Ali, Fatima, Hassan, Hussein watakatifu mahsusi na pamoja na maimam tisa walio tokana na dhuria ya imam hussein. zaidi ya hayo mtu ataka dalili (uthibitisho) gani?

Varas wa Junaghat (india) kassambhai ismail alimwandikia barua mfawidhi wa jamnagar (india) kassambhai devji kuthibitisha kwamba siku hizo makhoja ismaili wafuasi wa aga khan wakiamini maimam kumi na wawili na watakatifu kumi na nne na vile vile wakitoa maamkizi kwa imam wa nane. mateuzi halisi katika barua hiyo ni yafuatayo "jamnagar 927-55 shah peer amjalie mfawidhi kassam devji raha milele. kutoka varas kassam vares ismail wa jamnagar na tafadhali kubali salaam zake. pili, khudavand, maadham, his highness, ameandika barua kutoka zanzibar tarehe 19 shravan kwamba khudavand ataondoka zanzibar kwenda mombasa tarehe 20 septemba na baadaye atawasili india na ameamrisha jumuia zote na kamadia wote wajulishwe kwamba:

a) Maelezo kuhusu tukio la karbala yasisomwe kila mara, lakini yasomwe katika siku za muharram tu, na maamkizi kwa imam hussein baada ya hotuba yaendelee, lakini maamkizi mawili kwa imam ar-ridha(a.s) na muhammad mehdi(a.s) yasiendelee.

b) Baada ya majlis maamkizi moja tu yaendelee kuelekea magharibi.

c) katika kumbukumbu na vitabu vinavyowekwa na jamati (jumuiya) au kumbukumbu za hesabu zinazo hifadhiwa na mfawidhi au katika kumbukumbu za ndoa, majina ya maimam kumi na wawili pamoja na watakatifu kumi na wanne yasitumike tena. Juma mosi tarehe 17 bhardva 1956 kassam ismail.

katika mwaka 1941 wa hindoo; aladin gulamhusein, mfuasi madhubuti wa aga khan, alichapisha kitabu chake kisindhi, katika gulamhussein press ambacho sasa hakipatikani (kimezuiliwa). imeandikwa: "huko mtume, amirul mumiiin mola murtadha Ali na maimam kumi na wawili pamoja na malaika jibraeel na israel watahudhuria." (kurasa 18-19). Katika kitabu hicho ukurasa 43 imearidhiwa "nuru ya pepo itamfikia yule ambaye atakuwa na imani juu ya upekee wa mungu na unabii wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) na atayefuata Ahlul-Bait na kutambua maimam kumi na wawili na hadhi ya waumini hao itakuwa ya juu.' (kimenakiliwa kutoka Risala ya Imam Ja’afer Sadiq. uk. 43).

Kwa kweli ijapokuwa sifa nyingi mno ziliturnika kwa ajili ya his highness, yeye hakukubaliwa kama ni imam wa wakati huu katika barua iliyoandikwa na varas kassam ismail. hii inathibitisha pasi shaka kwamba mpaka wakati huo aga khan hakuhesabiwa kuwa ni imam, bali ni peer tu (kiongozi). varas: ni cheo katika jumuia ya makhoja wafuasi wa aghakhan. majlisi: mkutano maalum panapodhikiriwa kisa cha karbalaa.

7

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 7

KUTAJWA KWA HADHRAT MAHDI (AS.) KATIKA GINAN ZA PEER (VIONGOZI) (NYIMBO ZA DINI ZA WATAKATIFU WA KIISMAILI)

Katika kitabu cha Sala ya waismailia, wafuasi wa Aga Khan, kiitwacho so ginan, sehemu ya kwanza ukurasa 70, katika sala ya nne ya peer shams imeandikwa kwamba huyo mehdi aliyetakasika atakuja amepanda farasi duldul.

Katika kitabu hicho hicho, sehemu 2, ukurasa wa 3, katika sala ya peer ismaili shah yafuatayo yameandikwa: "yeyote asiyemtambua mehdi shah atahesabika hakuelimika (mjinga) na atakabiliwa na hasara duniani na akhera na hataokoka. mehdi ataua makafiri wote na atafundisha qur'an na kufuta ujinga."

Katika kitabu hicho hicho sehemu ya 6, kuna sala za peer hassan kabirdin ambaye amearidhia "imam wa mwisho imam Mahdi(a.s) atakuja. Yeye (Mahdi) ni mtakatifu mno na watakaomfuata watakuwa wamebahatika. Wa kwanza ni ali(a.s) , mwisho ni mehdi(a.s) ambaye ni imam mtukufu. Yeyote atayemkataa na kutomfuata yeye (Mahdi) aamali (sala zake) hazitakubaliwa."

Sala nyingine ya peer Hassan Kairdin, katika kitabu hicho hicho inasema: "Mahdi aliye shujaa atafundisha kiarabu na jina lake litakuwa Mahdi Shaah. yeye atawaua iblis na Dajjal na kutawala bara zote duniani."

Tanbihi: wadanganyifu wote waliodai kuwa wao ni mehdi hawakuweza kutawala hata kijiji kidogo licha bara zote duniani. Kutokana na hizo sala zote nne zilizotajwa uhai wa hadhrat mehdi(a.s) umethibitika na kuja kwake kutawala ulimwengu na kuleta usawa na amani vile vile kumebitika.

SURA 8

KUZALIWA KWA HADHRAT MEHDI (A.S)

Mwenyezi Mungu amesema katika qur'an:

يُرِيدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّـهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ ﴿٣٢﴾

" Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia."(9:32).

Maadui wa allah hawakuacha jambo lolote katika jitihada zao za kumwumbua mtume mtukufu(s.a.w.w) na ahlul-bait wake(a.s) . wamewaua kwa kuwachinja au kwa kuwapa sumu dhuria ya mtume(s.a.w.w) moja baada ya mmoja, iakini "nuru" imeendelea kuangaza na itaangaza hadi siku ya kiyama. khalifa mo'tamid aliyekuwa katika makhalifa wa bani abbas alimweka kizuizini imam wa kumi na moja, hadhrat imam hassan askari(a.s) , miaka mingi gerezani. alikuwa ana habari kamili juu ya hadithi ya mtume muhammad(s.a.w.w) kwamba imam hassan .askari atapata mwana hadhrat mehdi(a.s) na huyo ataanzisha na kustawisha utawala wa dhuria ya mtume(s.a.w.w) ulimwenguni na kuangamiza maadui wa Ahlul-Bait na wa mtume(s.a.w.w) . kwa hivyo alimweka imam hassan askari (a.s) gerezani kwa muda mrefu sana ili kuzuia bishara ya mtume(s.a.w.w) .

Firaun alidai kwamba yeye mungu. wanajumi walimshauri kwamba kutokana na kizazi cha bani israel atazaliwa mtoto ataye angamiza ufalme wake, kumwua yeye (firaun), wafuasi na masahaba wake. kwa hiyo firaun aliweka ulinzi mkali juu ya wanawake wa bani israel. kila mtoto akizaliwa akiuliwa ili kuzuia kuzaiiwa kwa nabii musa. Hata hivyo, alivyotaka mungu ikawa. nabii musa alizaliwa katika nyumba hiyo hiyo ya firaun. Licha ya kuzaliwa tu, hata kalelewa nyumbani mwa firaun. kama vile alivyo firaun, mo'tamad alitaka hadhrat mehdi(a.s) asizaliwe. Lakini hakuna mtu anayeweza kufaulu kuzuia amri ya mungu.

Katika kipindi imam hassan askari(a.s) alipokuwa kizuizini kulitokea ukame mkali sana samarra. kwa muda mrefu hapakunyesha hata tone moja la mvua. waislamu waliswali swala maalum ya kuomba mvua inyeshe lakini hawakufanikiwa.

Wakati waislamu wote walipokusanyika nje ya jiji la samarra, padri mmoja wa kikristo akanyanyua mikono yake kuomba mungu na papo hapo mawingu yakakusanyika na myua ikanyesha kidogo. Kuona hivyo waislamu wote walibabaika. Wakaanza kupatwa na wasiwasi kwamba labda ukristo ni dini ya kweli. Khalifa papo hapo akaitisha baraza lake na kuchukua ushauri wa wanavyuo, mawaziri na maofisa wake. Wote walipigwa butaa. Mmoja wa washauri wake akatoa wazo kwamba yuko mwokozi mmoja tu ambaye anaweza kuwaokoa, naye ni imam hassan askari(a.s) ambaye alifungwa gerezani. khalifa alikuwa na hakika (yakini) juu ya elimu, ukweli na uimam wa imam hassan askari(a.s) na haki yake ya utawala (ukhalifa). akamwita imam hassan askari katika baraza la kifalme.

Hadhrat imam hassan askari(a.s) alipofika kasri, khalifa akasimama kwa taadhima, akamkaribisha, na akamkalisha karibu na kiti cha kifalme na kumweleza mambo yote. Imam akasema "usiwe na wasiwasi. Hilo si jambo kubwa. Waamrishe waislamu wote wakusanyike nje ya jiji kesno ili waswali na kuomba mvua inyeshe. Na wakati huo huo mwamrishe huyo padri wa kikristo alike". Kesho yake waislamu wote pamoja na yule mkristo walikusanyika huko. Imam akamwambia huyo padri aombe mungu na papo hapo mawingu yakakusanyika. Irnam akamwomba khalifa kumtuma mtu akalete kile kitu padri huyo alichoficha katikati ya vidole vyake. Khalifa aliamrisha afisa wake akamnyang'anye mfupa uliofichwa katikati ya vidole vya padri, na akamkabidhi imam hassan askari(a.s) . imam Hassan Askari(a.s) akaufunika huo mfupa katika leso na kuiweka hiyo leso mfukoni mwake. papo hapo mawingu yaliyokusanyika yakatawanyika. Hapo hadhrat akamwambia huyo padri amwombe mungu ili inyeshe mvua. Padri huyo alijitahidi sana kumwomba mungu lakini hakufanikiwa hapo imam akamjulisha khalifa kwamba ule mfupa ulikuwa wa nabii mmojawapo na wakati wowote unapowekwa chini ya mbingu basi mawingu hukusanyika imam akiwaongoza waislamu katika swala akanyanyua mikono yake mitakatifu. Papo hapo mawingu yakakusanyika pande zote. Imam akawaamuru watu waende makwao na baadaye mvua kubwa ikanyesha. imam na khalifa walirudi kitaluni na hilo lilikuwa jambo pekee likizungumzwa na kila mtu. Khalifa alifurahi mno kwa sababu uislam ulinusurika.

Khalifa na watu wote waliamini mafaa ya swala, ukweli na utawala wa imam. Baada ya muda imam(a.s) akaondoka. Khalifa alipomwuliza alikokuwa anaelekea imam akamjibu kuwa alikuwa anarudi kifungoni alimo wekwa na khalifa. Kusikia hayo, khalifa aliona haya sana na akasema, "eh mjukuu wa mtume, tafadhali rudi nyumbani kwako". Hapo imam alirudi nyumbani kwake. Katika muda huo narjis-khatun (mama yake imam wa kumi na mbili akawa mja mzito).

يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّـهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ ﴿٨﴾

"Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia." (61:8).

Jina la mama yake hadhrat mehdi(a.s) hasa lilikuwa narjis khatun. majina yake mengine yalikuwa malika, sausan na 'rayhana. Yeye ni mjukuu wa mfalme wa utawala wa uturuki. Historia ya kuvutia ya narjis khatun kufika samarra ni kama ifuatavyo: imesimuliwa na bashir bin suleiman kuwa: "niliitwa na imam ali naqi (baba yake imam hassan askari(a.s) , imam wa kumi na kuambiwa: 'wewe ni katika kizazi cha wasaidizi wetu na marafiki zetu. Nitakupa shughuli muhimu kwa sababu mimi nina imani na wewe: mimi nilimwomba aniamrishe tu kwa sababu nilijiandaa kutimiza anachotaka. ameniambia kwamba anahitaji kumnunua kijakazi.

Akaniamrisha niende baghdad kwa ajili ya shughuli hiyo, na nitapofika huko niende kwenye ukingo wa mto. Huko mimi nitaona majahazi mengi na mateka wa kike wakiuzwa. Mimi niende kwa mtu mmoja aitwaye omar bin yazid ambaye atakuwa na mtekwa wa kike aliyevaa nguo mbili za hariri. yeye (huyo mtekwa wa kike) atakataa kuuzwa kwa mnunuzi yeyote na atakuwa anazungumza lugha ya kituruki. Imam ali naqi akanipa dinar 120 akaniambia kwamba mwuzaji atakubali kumwuza huyo mtekwa kwa hiyo bei. Vile vile alinipa barua ya kumpa huyo mtekwa wa kike.

Mimi nilikwenda baghdad kama nilivyoagizwa na kwa alama nilizo elezwa na imam ali naqi, nilimtambua huyo mtekwa na nikampa barua. kusoma barua hiyo tu huyo bibi machozi yalimjaa machoni mwake na akamwambia maliki wake kwamba hatakubali kununuliwa na mtu yeyote ila miye (bashir bin suleiman). Kwa hivyo nilirudi nyumbani (huko baghdad) na huyo mtekwa ambaye aliweka barua hiyo juu ya macho yake na kulia sana. Nilimwuliza kwa nini anabusu hiyo barua na kulia wakati yeye ni mgeni kutoka uturuki na hamjui mwandishi wa barua hiyo. Yeye akasema: "Sikiliza, mimi ni mjukuu wa kaisar, mfalme wa uturuki na jina langu ni malika.

Jina la baba yangu ni yashua na jina la mama yangu ni shamunusafaa. baba yangu aliandaa mipango niolewe na mpwa wake. Siku moja aliwaita mapadri wote, mawaziri, viongozi na wafuasi wake, na kumkalisha mpwa wake juu ya kiti cha enzi ambacho kilipambwa na almasi na kumwomba padri afunge ndoa yetu. Padri alipoanza kufungua kitabu kutaka kufunga ndoa masanamu waliotundikwa ukutani waliporomoka na mwana mfalme (mpwa wa babu yangu) akazirai na kuanguka na kiti cha enzi kilivunjika vipande vipande. mapadri walitetemeka na kumwomba msamaha baba yangu mfalme, kwa sababu hawakutarajia kutatokea balaa hiyo.

Mfalme alihuzunika sana. Akaona ndoa hiyo ilikuwa na nuksi na kwa hivyo aliagiza kiti kingine cha enzi na kutundika masanamu tena ukutani. padri tena akaanza kufunga ndoa na tukio hilo hilo likatokea tena. waliohudhuria wote walishtuka sana na wakaondoka papo hapo. baba yangu alifedheheshwa sana na siku nyingi alikuwa hakutoka nje ya kasri.

Usiku huo huo nilimwona nabii issa katika ndoto. Yeye alikuwa pamoja na masahaba wake waliokuwa wamehudhuria sherehe ya ndoa yangu. kiti kirefu cha enzi kiliwekwa pahali palipo wekwa kiti cha mwana wa mfalme (aliyetaka kunioa) na kilikaliwa na mtu mkubwa mwenye uso uliojaa nuru. Baada ya muda mfupi tu niliwaona watu wenye nyuso za nuru na hapo nabii issa alisimama kuwakaribisha na kuwapa nafasi karibu yake. Nilimwuliza mtu mmoja anijulishe hao waliokuja walikuwa nani? nikaarifiwa kwamba hao ni mtume wa uislam pamoja na mrithi wake na maimam kumi na moja wanaotokana na dhuria yake.

Mtume mtukufu hapo akamwomba nabii issa kumcchumbia malika binti wa shamunusaafa mjukuu wake imam H assan askari ambaye uso wake uking'aa kwa nuru (ombi hilo lilifanywa kwa nabii issa kwa sababu malika alitokana na kizazi cha hadhrat shamoon mrithi wa nabii issa). Nabii issa akamwomba hadhrat shamoon atoe kibali chake na papo hapo hadhrat shamoon akakubali kwa kuona hiyo ni heshima kuu. Kwa hiyo ndoa yangu ikafungwa na imam hassan askari(a.s) . macho yangu yakafunguka ghafla na mimi nilijawa na furaha. Nilikumbuka hiyo ndoto. Hata hivyo niliogopa sana na sikumhadithia ndoto hiyo mtu yeyote. Hapo baadaye mimi nikaanza kuwa mgonjwa ona kumkumbuka imam hassan askari na hali yangu ikaanza kudhoofu. Safari moja nilimwona binti wa Mtume(s.a.w.w) mwana Fatima(a.s) na katika ndoto mimi nilisimama kwa taadhima na nikamweleza hali yangu na kutomwona imam hassan askari(a.s) . aliniamrisha nisome "shahada", nikawa mwislamu na baadaye kila usiku nilimwona imam hassan askari katika ndoto akinituliza. Mara moja imam hassan askari aliniambia kwamba babu yangu atatuma jeshi kuivamia nchi ya waislamu na mimi nibadilishe mavazi yangu niungane na jeshi kama mtumishi mmojawapo. Waislamu watashinda vita hivyo, na mimi nitatekwa na kwa hivyo niungane na mateka wengine, mpaka baghdad."

Mimi (bashir bin suleiman) niliposikia hayo nilijawa na furaha na nilimleta bibi narjis khatun samarra kwa imam ali naqi(a.s) . imam Ali naqi(a.s) alimkaribisha pia akamkabidhi kwa dada yake Halima Khatun. Baadaye imam ali naqi(a.s) alimwozesha bibi narjis khatun na mwanawe imam Hassan Askari(a.s) akawabashiria kwamba watampata mwana ambaye atakuwa hujjat (dalili) duniani wa kuthibitisha kuwepo kwa mungu. Wakati dunia itapokuwa imeghariki katika ukandamizi, uovu na ulaghai yeye atakuja kutawala na kuleta insafu na usawa. Imam Mahdi(a.s) alizaliwa samarra iraq alfajiri siku ya ljumaa tarehe 15 shaaban 255 a.h. nyumbani kwa baba yake mtukufu. Alizaliwa tohara na amekwishatahiriwa na uso wake ulivyojaa na nuru ambayo ilipenya paa na kuelekea mbinguni. Alipozaliwa tu, kwanza alisujudu na huku akiwa amenyosha kidole chake cha shahada kuelekea samawati na kuthibitisha upweke wa mungu na unabii wa mtume muhammad(s.a.w.w) na uimamu wa Ali(a.s) pamoja na warithi wake kumi kuwa ni maimam wa kweli. Hapo baadaye akamwomba mungu atimize ahadi yake.

Halima khatun, binti wa imam wa tisa, hadhrat imam mohammed taqi(a.s) , shangazi yake imam hassan askari(a.s) , akamnyanyua mtoto aliyezaliwa na kumpa baba yake ambaye alimpakata. Imam Mahdi(a.s) papo hapo akamwamkia baba yake ambaye alimjibu na akamwambia aendelee kusema kwa amri ya mungu. hapo tena hadhrat mehdi(a.s) akarudia kuthibitisha upweke wa mungu, utume wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) urithi wa maimam kumi na moja na kusoma aya ya qur'ani "tumekusudia kuwajalia jamala yetu wale ambao waliofikiriwa ni wanyonge duniani na kuwateua maimam na kuwafanya warithi duniani" (28:5). Hapo baadaye imam Hassan askari(a.s) akamrudisha huyo mwana kwa bibi Halima Khatun na Halima Khatun akamrudisha mtoto kwa mama yake. Mwana huyo alimwamkia mama yake vile vile. Katika Sherehe ya akika imam Hassan Askari(a.s) alimwamrisha wakili wake Othman Saidi Omari kuwagawia maskini nyama ya mbuzi 10,000 na mikate 10,000.

Kuna marejeieo mengi katika vitabu vya kisunni kuhusu kuzaliwa kwa hadhrat mehdi(a.s) . tuna nakili madondoo machache pamoja na ushahidi. mwanazuoni wa kisunni, ubeidullah amrat-sari katika kitabu chake sawanahe umry hadhrat Ali(a.s) ukurasa 433, kuhusu imam hassan askari(a.s) . ameandika, "hakuna mwana yeyote aliyeishi baada yake ila mwanawe aabdal qassim mohammad al-hujjat tu" zanabl katika kitabu chake tarikhul islam ameandika kwamba imam wa kumi na mbili amezaliwa katika mwaka 256 a.h.

Sheikhul Sislam wa istanbul, sheikh suleiman balkhi kanduzi, katika kitabu chake yanabiul mawaddah ameeleza bayana kuhusu kuzaliwa kwa hadhrat mehdi(a.s) kama vile maelezo yaliyomo katika vitabu vya ithnaasheri. Yeye ameandika kuwa hadhrat mehdi(a.s) alizaliwa mwaka 250 a.h. ambayo nitofauti kidogo na hiyo ilisababishwa na kosa la uchapishaji. katika kitabu maarufu sana cha kisunni tarikh ibnul khaladun juzuu la pili, ukurasa 24, mwandishi anaeleza "Mahdi(a.s) anaye subiriwa alizaliwa siku ya ijumaa tarehe 15 shaaban 255 a.h. na baba yake ni imam hassan askari (a.s.). 5) mulla abdur-rahman jami katika shawahidu Nubakhat, ukurasa 247, ameandika kuwa "mwana wa imam ridha ni muhammad, na mwanawe ni ali na mwanawe hassan na mwanawe ni muhammad mehdi(a.s) , huyu wa mwisho alizaliwa samarra 255 a.h.