ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE0%

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE Mwandishi:
Kundi: Imam mahdi (a.s)

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

Mwandishi: Marehemu Mulla Muhammad Jaafar Sherif Dewj
Kundi:

Matembeleo: 20636
Pakua: 2905

Maelezo zaidi:

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 20 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 20636 / Pakua: 2905
Kiwango Kiwango Kiwango
ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

Mwandishi:
Swahili

15

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 20

HADITHI KUHUSU KUJITOKEZA KWA IMAM MAHDI(A.S) NA ALAMA MAALUM ZITAKAZO TANGULIA

Vitabu vyote vya sunni vimehadithia hadithi juu ya kujitokeza kwa imam(a.s) . hii ni dalili kwamba imam(a.s) wa wakati huu yu hai, kwa sababu mtu atakayeweza kujitokeza lazima awe hai na aliyeghibu na si yule ambaye bado hajazaliwa.

1) Imenakiliwa katika juzuu la pili la tarikhe khamis kuwa: "wakati atakapojitokeza mehdi, muhammad bin hassan askari(a.s) malaika watatangaza kujitokeza kwake. Yeye ni khalifa aliyeteuliwa na mungu na katika kipindi cha utawala wake mbuzi watakuwa malishoni pamoja na mbwa mwitu na watoto wa binadamu watakamata nyoka na visusuli na kucheza nao."

2) Katika kitabu cha asafurraghbin, ukurasa 140, sheikh muhyiddin amenakili kutoka kitabu cha kiarabu futuhat kuwa: "hakuna shaka yoyote kwamba hadhrat imam mehdi(a.s) atatokeza, lakini wakati ule dunia nzima itakuwa imejaa udhalimu, ukandamizi, na dhambi na huyo imam as. atasafisha hayo yote na ataijaza dunia kwa insafu na usawa. "yeye atatokana na dhuria ya mtume mtukufu(s.a.w.w) kutokana na binti yake fatima(a.s) kwa utaratibu ufuatao: mwana wa fatima atakuwa imam hussein(a.s) atakayemzaa alia zainul abedin(a.s) ambaye atamzaa muhammad ai-baqhir(a.s) atakayemzaa jaffar sadiq(a.s) atakayemzaa musa(a.s) atakaye mzaa ali ridha(a.s) ambaye atamzaa hassn askari(a.s) ambaye mwanaye atakuwa muhammad mehdi(a.s) atakaye pokea kiapo cha utii katika kaaba takatifu".

3) Ibne abbas amearidhi katika faraidussimtayn kutoka mtume mtukufu(s.aw.w) kuwa: "watakuwa makhalifa 12 walioteuliwa na mungu, wa kwanza wao ni hadhrat ali(a.s) na mwisho atakuwa mwanangu mehdi(a.s) . nabii issa atakapoteremka kutoka mbinguni ataswali nyuma ya mehdi(a.s) . dunia nzima itang'aa kwa nuru ya mungu. utawala wa hadhrat mehdi(a.s) utaenea kutoka mashariki mpaka magharibi duniani kote (hadithi tatu hizi zote zilizotajwa zimehifadhiwa katika vitabu vya sunni).

vitabu hivyo vya kisunni vile vile vimethibitisha kwamba hadhrat mehdi(a.s) atakapojitokeza atastawisha uislam kuwa ni dini ya pekee duniani kote na kueneza insafu na huyo atakuwa mwana wa imam hassan askari(a.s). hao wote waliodai kuwa mehdi (kadiani mirza na wengineo) na wale ambao hudai kuwa imam wa wakati huu na mehdi hawakuweza kushinda dhuluma na ukandamizi kwa namna yoyote. alama zitakazoashiria kujitokeza kwa imam mehdi(a.s) alama zitakazotangulia kabla ya kujitokeza kwa imam hadhrat mehdi(a.s) na hali ya dunia itakavyokuwa imekwisha elezwa. Sasa tutazingatia alama maalum ambazo zitatangulia kabla imam hajajitokeza:

i) Dajjal atatokeza.

ii) Sauti kubwa itasikika kutoka mbinguni.

iii) Sufiani atatokea na ataanzisha vita vikali.

iv) Jeshi la sufiani ghafla litamezwa na mpasuko wa ardhi baina ya makkah na madina.

v) Seyyid mahshumu na mcha mungu atauawa makkah.

vi) Seyyid anayetokana na dhuria ya imam hassan(a.s) atatokeza na jeshi lake.

vii) Sura ya binadamu itaonekana mbinguni kabili ya juwa.

viii) Kutatokea kupatwa mwezi na juwa mara mbili katika mwezi mtukufu wa ramadhan kinyume cha hali ya kawaida na hesabu: kutakuwa kupatwa juwa

tarehe 15 na tarehe ya mwisho wa mwezi.

ix) Nyakati tatu itasikilizana sauti kubwa kutoka mbinguni katika mwezi mtukufu wa ramadhan. alama hizi zimekwishaelezwa bayana kwingineko.

Imam Jaafar Sadiq(a.s) amesema kwamba: kutakuwa kupatwa kwa jua na mwezi kinyume cha hali ya kawaida na kabla ya tukio hilo thuluthi mbili ya waislamu watakuwa wamegeuka makafiri.

Hadhrat Ali(a.s) amesema kwamba kabla ya kujitokeza kwa hadhrat mehdi(a.s) kutamwagika damu kwa uwingi, vifo kwa tauni vitakithiri na mchwa watatokeza kwa wingi mara mbili.

SURA 21

KAFIRI DAJJAL CHONGO

siku moja hadhrat Ali(a.s) mwishoni mwa hotuba yake katika msikiti wa kufa aliwaomba watu wamwulize maswali wanayotaka kabla yeye kufariki dunia. Sasa bin sawhan akasimama na kuuliza: "eh kiongozi wa waumini! Wakati gani hadhrat hujjat atatokeza"? Imam Ali(a.s) akajibu: "kwanza zitatokeza alama nyingi moja baada ya moja. Sikiliza kwa makini kuhusu hizi alama na uzikumbuke. Watu watapotosha dhana ya ibada, watakhini amana, watahalalisha uongo, watakula riba, watakuwa waovu, na waasharati na hawatawapenda jamaa zao, wataona fahari kufanya dhuluma, watapamba Qur'an tukufa, misikiti yenye minara mirefu itajengwa, wataheshimiwa waovu na wadhalimu, misikiti itajaa watu wa kuswali lakini watu hao hawatakuwa na umoja, watawashirikisha wake zao katika biashara ili kupata utajiri, wataamini maneno ya waasi na kuwatii, waovu na wapotovu watakuwa viongozi wa majamii, wataweka vifaa vya ghina (muziki) (gita na piano), wanawake watapanda farasi (baiskeli) na kuwaiga wanaume (kwa mavazi ya kiume), watu watajishughulisha na kutekeleza mambo ya dunia kabla ya kuswali faradhi na kuonekana waungwana lakini mioyo yao itakuwa imejaa ufasiki".

Alipofika hapo asbag bin nabata akauliza, dajjal ni nani? imam ali(a.s) akajibu: "jina la Dajjal ni sayad bin sed. Waovu tu ndio watamfuata na waungwana watamkimbia. Dajjal atatokea yahudiyya mjini isfahan Iran. atakuwa na jicho moja na hilo jicho litakuwa kwenye paji la uso na litang'aa sana. Mboni ya jicho lake litakuwa wekundu na karibu na jicho lake litakuwa limechorwa neno kafiri ili lisomeke na wote. Mbele yake kutaonekana mlima wa moshi na kisogoni kwake kutaonekana kilima cheupe. Yeye atatokeza wakati wa njaa kali, watu watababaika na vilima hivyo kufikiria hiyyo ni vyakula na kumkimbilia huyo dajjal. Atapanda punda rangi ya majivu ambaye hatua yake moja itakuwa sawa na masafa ya maili moja.

Akipita karibu na mto wowote maji yake yatakauka. kwa sauti kubwa itayosikika na watu na majini wote yeye atanadi, "eh nyinyi rafiki zangu, njooni kwangu mbio. Mimi ni muumba wa vyote ulimwenguni. Nimeumba vitu katika maumbile mbalimbali na mimi ndiye mtoa riziki mimi ninawaita kwenye maongozi yangu kwa sababu mimi ni mungu na nina uwezo juu ya vitu vyote."

Imam Ali(a.s) tena aliendelea kuwatahadharisha watu kwamba yule adui wa mungu ni mdanganyifu wa nafsi yake kwa sababu yeye anakula na kunywa. zaidi ya hayo mungu wenu siye chongo, wala hali wala kunywa, hana mwili na haondoki kutoka pahala pamoja na kwenda pengine. mjitahadhari! wafuasi wa huyo mwovu watakuwa watoto wa haramu na mayahudi. hadhrat mehdi(a.s) atamwua dajjal huko sham kwenye mlima mkubwa unaoitwa tallu affik siku ya ijumaa saa tatu baada ya jua kuchwa. baadaye kutatokeza tukio kuu. akasoma aya kutoka qur'an tukufu isemayo:

"Na sisi tuliwasimulia kwamba kuna mtu hutembea kwa wepesi na kuzungumza nao ". (27.28).

Mtu huyo (Imam a.s) atatokeza kutoka mlima wa saffa uliopo makkah. atakuwa amevaa pete ya nabii suleiman na kushika asa ya nabii mussa.

Atagusa paji la uso la waumini kwa pete hiyo na papo hapo kutachoreka maneno "hadha mu'min" (huyu ni mtu aliyeamini). Atagusa paji la uso la makafiri na papo hapo patachoreka maneno "hadha kafir (huyu kafiri). Juwa litachomoza kutoka magharibi na yeye atanyanyua kichwa mbele ya juwa na watu wote duniani wataweza kumwona. wakati huo mlango wa toba utafungwa na vitendo havipatiwi jazaa ila vya wale walio amini kabla ya tukio hilo kwa sababu imani bila amali haikamiliki."

Katika kitabu kimoja cha kisunni, kamaluddin, abdulla bin umar amesimulia kwamba siku moja baada ya swala ya asubuhi mtume mtukufu(s.a.w.w) pamoja na masahaba zake walikwenda kutembea mjini. mtume(s.a.w.w) akasimama karibu na nyumba moja na kugonga mlango wa nyumba hiyo. alitoka mwanamke mmoja aliyemtambua mtume(s.a.w.w) na kumwuliza kwamba angeweza vipi kumsaidia mtume(s.a.w.w) . mtume akamjibu kwamba alitaka kuonana na mwanae, abdulla. mama huyo alijibu kwamba mwanae alikuwa mgonjwa wa akili na kwa hivyo huchafua nguo zake na kuzungumza maneno ya kiburi mara kwa mara. mtume(s.a.w.w) akaomba ruhusa ya kuingia ndani kumwona huyo mgonjwa. mama huyo akamruhusu mtume(s.a.w.w) lakini aliomba asamehewe ikiwa mwanawe huyo atazungumza vibaya na mtume.(s.a.w.w) .

Mtume(s.a.w.w) akaingia ndani pamoja na masahaba. yule maluuni alikuwa amevaa nguo nene na kuzungumza peke yake. mama yake akamwambia anyamaze kwa sababu mtume mtukufu(s.a.w.w) alikuja kuonana naye. kusikia hivyo akanyamaza. mtukufu mtume(s.a.w.w) akasema: "ingelikuwa huyo mama asingemwambia kunyamaza, mngelisikia anayosema na mngeelewa hali nilivyoeleza". tena mtume(s.aw.w) akamwuliza kwamba anaona nini. alijibu, "mimi ninashuhudia haki na ubatili na nina ona arsh ya mungu inaelea juu ya maji". bwana mtume(s.a.w.w) akamsihi atoe shahada juu ya upweke wa mungu na unabii wake. naye akajibu, "ninatoa shahada juu ya upekee wa allah na mimi mwenyewe ni mtume wa mungu kwa sababu wewe hustahili utume zaidi yangu." mtume(s.a.w.w) akaondoka.

Siku ya pili mtume mtukufu(s.a.w.w) , pamoja na masahaba wake walikwenda kumwona tena nyumbani kwake. kwa idhini ya mama akaingia ndani na wakamwona amekaa juu ya mtende anapayukapayuka tena mama yake akamgombeza na kumwambia akae kimya na kuteremka chini. siku hiyo tena mtume akachukiwa na akasema "ingekuwa mama yake asingemwambia kunyamaza, nyinyi mngeamini kwamba huyo ni dajjal mfasiki, ambaye nimekwisha watahadharisheni naye" mtume(s.a.w.w) akaondoka. mtume(s.a.w.w) tena pamoja na masahaba wake akaenda kumwona siku ya tatu na alipoingia ndani akamwona huyo abdulla akicheza na mbuzi waliokuwa karibu naye.

Mtume(s.a.w.w) akamsihi akubali upekee wa mungu na unabii wake na akamwambia aseme mtume(s.a.w.w) alikuwa na wazo gani. huyo akasema "addhukh adhukh" (dukh maana yake mvuke na siku hiyo hiyo suratul dukhan iliteremshwa na mtume(s.a.w.w) alisoma sura hiyo aliposwalisha swala ya alfajiri. mtume(s.a.w.w) akamjulisha 'atakayo mungu ' ndivyo huwa na wewe hutafikia mradi wako." mtume mtukufu(s.a.w.w) baadaye akawaeleza masahaba "wake kwamba huyo abdulla ndiye dajjal mfasiki ambaye habari zake alikwishawaeleza. atatokeza duniani siku za mwisho na kabla ya hapo mungu atakuwa amemweka mahabusu katika kisiwa kimoja. atawaletea watu utatanishi mkubwa siku za mwishoni. manabii wote kabla ya mtume mtukufu(s.a.w.w) waliwatahadharisha wafuasi wao kuhusu dajjal. kadhalika, mtume wetu(s.a.w.w) ametutanabahisha sisi kuhusu huyo dajjal na akaongeza "msidanganyike na huyo: mungu wetu siyo chongo, wala hana mwili na huyo mwovu (dajjal) atajitokeza siku za mwisho amepanda punda".

Dajjal atajitokeza siku za mwisho na ataishi kwa muda wa siku arubaini na atatembelea kila sehemu ya dunia juu ya punda wake. mwisho atauliwa huko syria kwa mikono ya imam mehdi(a.s) .

SURA 22

HAKIKA KUHUSU KUJITOKEZA KWA IMAM WA KIPINDI HIKI

Imam Mahdi(a.s) wakati uliopangwa wa kujitokeza kwa hadhrat mehdi(a.s) utapowadia upanga wake "dhulfiqar" utajitokeza nje ya ala yake na kwa kudra ya mungu utapata kauli na kusema: "Eh hujjat wa Mungu, wakati wa kujitokeza kwako umewadia. tafadhali jidhihirishe mbele ya watu duniani" Imam jaafar Sadiq(a.s) amesema: "Atakapojitokeza imam mehdi (a.s) ataingia katika jiji la makkah. atakuwa amevaa mavazi ya mtume (s.a.w.w). kilemba cha njano, na atashika fimbo na kuvaa viatu vya mtume (s.a.w.w). mbele yake watakuwa mbuzi wachache waliodhoofika ".

Hakuna mtu katika makkah atakayeweza kumtambua imam mehdi(a.s) . ataingia kaaba akionekana kijana kabisa. ataignia katika kaabah tukufu usiku wa manane. Jibriil, Mikaiil na malaika wengine katika vikundi vikubwa watateremka kutoka mbinguni kuja ka’aba na kumwamkia imam Mahdi(a.s) . Jibril atampasha imam habari kuhusu maagizo ya Mungu Subhana wa taala kwamba chochote atakachopenda na kuamrisha kitakuwa. Imam(a.s) hapo atachukua mkono wake wa kulia na kuweka juu ya uso wake na kusema:

وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي صَدَقَنَا وَعْدَهُ وَأَوْرَثَنَا الْأَرْضَ نَتَبَوَّأُ مِنَ الْجَنَّةِ حَيْثُ نَشَاءُ فَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿٧٤﴾

"Nao watasema: Alhamdulillah, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye tutimizia ahadi yake, na akaturithisha ardhi, tunakaa katika Bustani popote tupendapo. Basi ni malipo mazuri yaliyoje ya watendao!." (39: 74).

Baadaye hadhrat hujjat(a.s) atasimama kwenye pembe moja ya kaaba tukufu na kutangaza "Eh nyinyi mlioteuliwa mahsusi na allah kunisaidia mimi tafadhali mje kwangu" sauti hiyo itasikika katika kila nchi lakini khassa na waumini 313 katika asia, afrika na china. baadhi ya hao waumini watakuwa juu ya miswala, wengine watakuwa wamelala, lakini wote watafunga safari kwenda makkah na katika muda mfupi mno watajikuta wamekwisha fika kwa imam(a.s) .

Wakati huo Jibreel atabusu mkono wa Imam(a.s) na kula kiapo cha utii kwa imam(a.s) . na kufuatwa na malaika wengine. baadaye viongozi wa majini na hao waumini 313 watakula kiapo cha utii. watu wa makkah kutahamaki hayo watashangazwa na watauliza hao watu ni nani na wanatokea wapi? vile vile watajiuliza kwa sababu gani usiku huu umekuwa marini na kwa miujiza mingi inaonekana. wengi wao watajibu kwamba hawajui; ila watu wanne kutoka madina ambao watawajulisha kwamba kiongozi wao mwenye uso marini ni imam(a.s) .

Baada ya kupambazuka kutasikika sauti (mwito) katika lugha ya kiarabu duniani kote ikitangaza: "eh nyinyi viumbe mliokuwa mbinguni na ardhini, shaksi aliyejitokeza ni mehdi anayetokana na dhuria ya mtume(s.a.w.w) . baadaye hiyo sauti (tangazo) itaeleza majina kamili ya hadhrat mehdi na nasaba yake mpaka imam hussein(a.s) na itawataka watu kula kiapo cha utii kwa imam(a.s) na kuwaonya kwamba kuhalifu ni kugeuka kafiri. malaika, majini na wale 313 pamoja na waumini wengine watadhihirisha imani yao na utii kwa imam(a.s) .

Huo mwito utasikika vizuri mno katika nchi zote, misitu na milima yote na wanaume kwa wake na watoto wote watashangazwa nao. Wakati wa machweo kutasikika mwito mwingine ukitangaza: "Eh watu, sikilizeni. mungu wenu amejitokeza kutoka misitu ya yabis (palestine) na jina lake ni othman bin amsasah anayetokana na ukoo wa umayyah na dhuria ya yazidi bin muawiyah. Mwelekee kwake na kula kiapo cha utii mwongozwe njia ya haki". Malaika majini na waumini halisi watabatilisha tangazo hilo kuwa ni uzushi na uwongo mtupu. Makafiri wanafiki na wasioamini dini watababaishwa na tangazo hilo na kupotoshwa.

Baadaye imam Mahdi(a.s) akishikilia kaaba tukufu atanadi "Eh viumbe vyote wa mungu nisikilizeni! mimi nimejaliwa na wema, uwezo na miujiza yote ya mitume wote, pamoja na sifa zote za mtume mtukufu (s.a.w.w) na maimam na elimu ya vitabu vitakatifu vyote. " waumini wote watakubali tamko hilo. hapo tena mtu mmoja ajulikanaye kama dabbatul ardh atatokeza baina ya rukn na maqam akishika fimbo na pete mkononi. huyo. (dabbatui ardh) atapoiweka pete hiyo kwenye paji la uso wa waumini papo hapo maneno "huyu mwumini" yatajitokeza na atapoiweka hiyo pete juu ya paji la uso wa makafiri maneno "huyu kafiri" yatajitokeza.

Baada ya hapo mtu mwenye uso wake uliogeuka nyuma atafika kwa imam(a.s) na kusema, "eh bwana wangu! Mimi na ndugu yangu tulikuwa katika jeshi la sudani na tulivamia ardhi yote baina ya damascus na baghdad kusababisha hasara na maangamizi. Baadaye tulielekea madina na makkah na jeshi la watu 300,000 tukikusudia kuingia makkah kubomoa kaaba tukufu na kuua umati mzima wa jiji.

Tulifika usiku jangwa la bayadana lililopo baina ya madina na makkah. Baada ya usiku wa manane tulisikia sauti: "Eh bayadana, waangamize makafiri wadhalimu. Papo hapo kwa amri ya allah ardhi ikapasuka na maaskari wetu 300,000, mali zetu pamoja na wanyama wetu wakamezwa na ardhi, haikubakia alama yoyote. Mimi na ndugu yangu tu tulisalimika. akatokea malaika mmoja na kutupiga makofi kwa nguvu mno na kusababisha nyuso zetu kuelekea nyuma (migongoni). Hapo huyo malaika akinielekea mimi akaniambia, "eh bashir elekea makkah na mpe imam(a.s) taarifa njema kuhusu maangamizi ya jeshi la sufiani. Tena baadaye alimwelekea ndugu yangu na kusema: "eh nazir elekea damascus na mwarifu sufiani kuhusu kuangamia jeshi lake na vilevile mpe taarifa ya kujitokeza kwa hadhrat mehdi(a.s) huko makkah. Msihi aje ajisalimishe kwa imam(a.s) na kuomba msamaha kwa maovu yake na akifanya hivyo toba yake itakubaliwa. (lakini hata hivyo huyo mtu mwovu hataomba msamaha na atajitumbukiza jahanam). Baada ya kusikia hayo yote imam(a.s) kwa mikono yake iliyo barikiwa ataurudisha uso wake uwe sawa. hadhrat mehdi(a.s) ataelekea kufa kutoka makkah na jeshi kubwa la malaika na majini. msikiti wa kufa utakuwa mahakama na msikiti wa sahlah makazi yake.

Mtume mtukufu(s.a.w.w) amebashiri kwamba imam Mahdi(a.s) . atapata ushindi katika usiku mmoja na kukamilisha malengo yake. Hadithi hii ya mtume mtukufu(s.a.w.w) ni ushahidi kamili wa kubatilisha daawa ya wale wote waliojidai kuwa wao ni mehdi(a.s) na vilevile ya wale ambao watafanya daawa ya kuwa mehdi(a.s) . Mji mkuu wa utawala wa imam(a.s) utakuwa kufa ambao utakuwa umepanuka hata kumeza jiji la najaf. kila inchi ya ardhi hiyo itathaminika sana na waumini kutoka kote kote dumanai watakutana huko (kufa). Jiji la kufa litakuwa na urefu wa maili 54 na kuungana na mji wa kerbala, katika zamana hiyo mwenyezi mungu subhana wa taala atatimiza kila matilaba ya waumini.

Imam(a.s) hapo atatuma jeshi kubwa kwenda damascus ambalo litashinda jeshi la sufiani na kumwua sufiani. Sawia ya hapo imam husein(a.s) pamoja na masahaba wake 72 ambao waliuawa karbalaa pamoja na waumini halisi watarudi duniani kwa amri ya mola. Hao watu watafika mbele ya imam mehdi hadhrat ali(a.s) na maimam wengine watarudi duniani. Mtume mtukufu(s.a.w.w) pamoja na masahaba wake waliouawa vitani (jihadi) vilevile watarudi duniani. wale ambao hawakumwamini mtume(s.a.w.w) , kumsumbua, kumzulia kuwa ni mchawi na kumtuhumu maovu mengine watarudishwa duniani na kuadhibiwa kwa dhuluma na uonevu waliotenda. vilevile atarudi nabii issa na mitume wengine pamoja na waumini. Hakutakuwa dini ila moja tu, uislaam, ulimwenguni kote. Dunia hii itajaa baraka za mungu. hali itakayokuwa wakati huo imekwisha elezwa katika vitabu vingine.

16

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 23

MAREJEO (RAJ'AAT)

raj'aat maana yake ni kurudi duniani (kupata maisha mapya) kwa wale waliokufa. Ni lazima kuamini kuwa baada ya kujitokeza kwa hadhrat mehdi(a.s) wenye sifa nzuri na hata wadhalimu, maadui wa aila ya mtume mtukufu(s.a.w.w) watapatiwa uhai mara ya pili. Kuna aya nyingi za qur'an kuhusu raj'aat na vilevile hadithi nyingi za mtume mtukufu(s.a.w.w) zimenakiliwa katika vitabu vya kisunni kuthibitisha ukweli wa raj'aat. Sio hivyo tu, bali hata vitabu vya wakristo, mayahudi, waabudu moto na mahindoo vimetaja dhana hiyo. Katika sura hii tunaeleza kwa ufupi itikadi hiyo kutokana na aya za Qur'an tukufu na hadithi.

وَيَوْمَ نَحْشُرُ مِن كُلِّ أُمَّةٍ فَوْجًا مِّمَّن يُكَذِّبُ بِآيَاتِنَا فَهُمْ يُوزَعُونَ ﴿٨٣﴾

1. "Na Siku tutapo kusanya kutoka kila umma kundi katika wanao kadhibisha Ishara zetu, nao watagawanywa mafungu mafungu. " (27.83).

kwa upande wa pili kuhusu siku ya kiyama qur'an tukufu imearidhi.

وَحَشَرْنَاهُمْ فَلَمْ نُغَادِرْ مِنْهُمْ أَحَدًا ﴿٤٧﴾

"Na tukawafufua - wala hatutamwacha hata mmoja kati yao ." (18:47).

Aya hii inatuthibitisha kwamba siku ya kiyama viumbe wote watahuishwa bali katika aya iliyotangulia baadhi ya wafuasi wa kila mtume watapatiwa uhai. kwa hiyo, hii ishara ya dhahiri kuwa wachache watarudi duniani baada ya kufa.

وَحَرَامٌ عَلَىٰ قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا أَنَّهُمْ لَا يَرْجِعُونَ ﴿٩٥﴾

2. "Na haiwi kwa wana-mji tulio uangamiza, ya kwamba hawatarejea".(21:95).

Aya hii inathibitisha bayana kurudi tena duniani kwa sababu siku ya kiama, mwenyezi mungu atawapa uhai viumbe wote.

قَالُوا رَبَّنَا أَمَتَّنَا اثْنَتَيْنِ وَأَحْيَيْتَنَا اثْنَتَيْنِ فَاعْتَرَفْنَا بِذُنُوبِنَا فَهَلْ إِلَىٰ خُرُوجٍ مِّن سَبِيلٍ ﴿١١﴾

3. "Wao watasema: "bwana wetu ametufisha mara mbili na umetuhuisha mara mbili". (40:11)

aya hii inazungumzia kufa na kupatiwa uhai mara mbili, kwa hivyo humaanisha kurudi duniani baada ya kufa.

فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ أُولَاهُمَا بَعَثْنَا عَلَيْكُمْ عِبَادًا لَّنَا أُولِي بَأْسٍ شَدِيدٍ فَجَاسُوا خِلَالَ الدِّيَارِ وَكَانَ وَعْدًا مَّفْعُولًا ﴿٥﴾

4. Basi itapo fika ahadi ya kwanza yake tutakupelekeeni waja wetu wa kali kwa vita. Watakuingilieni ndani ya majumba. Na hii ilikuwa ahadi iliyo timizwa.." (17:5).

إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ ﴿٥١﴾

5. "Kwa hakika sisi tunawaauni mitume wetu, na wale walioamini katika maisha ya dunia hii." (40:51).

6. Kuna aya nyingi katika qur'an tukufu kuhusu kuwapa uhai (kuwarudisha duniani) waliofariki. zaidi ya hayo, "kurudishwa" (kupatiwa uhai mara ya pili) kulitokea katika baadhi ya wafuasi wa mitume waliopita na katika wale waliokufa walipatiwa uhai mara ya pili, kwa hivyo kuamini kwamba waliofariki duniani hawatapatiwa uhai mpaka siku ya kiyama ni hoja isiyo na uzito.

1. Nabii musa aliwachukua masahaba 70 wateule kumwomba mungu na kusikia maagizo ya mungu. walidai kutaka kumwona mungu kwa macho yao. Kwa hivyo wote walikumbwa na kifo. Kwa dua ya nabii musa, mungu aliwarudisha duniani hao wote waliokufa. Hiyo imeelezwa katika qur'an tukufu.

2. Katika qur'an tukufu sura ya pili ya Al-baqarah (Ng'ombe) aya 243 huaridhi.

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ خَرَجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَهُمْ أُلُوفٌ حَذَرَ الْمَوْتِ فَقَالَ لَهُمُ اللَّـهُ مُوتُوا ثُمَّ أَحْيَاهُمْ﴿٢٤٣﴾

"Hukuwaona wale walio toka majumbani kwao kwa maelfu kwa kuogopa mauti? Mwenyezi Mungu akawaambia: Kufeni! Kisha akwahauisha.".

Aya hii inasimulia kisa cha nabii hizkil na wafuasi wake wenye familia 70,000. wakati ugonjwa wa tauni ulipoenea jijini kwao wote waliacha jiji. kabla kupata makazi mengine kulitokea amri ya mungu, wote wafe na papa hapo wakafa na miili yao ikaanza kuozeana na kubaki mifupa tu. siku moja nabii mmojawapo wa bani israil akapita hapo (mtume armiya au hizkil) na kumwomba mungu awapatie uhai hao kutokana na uwezo wake ili jiji hilo lipate watu wa kumwabudu yeye (Mungu). Mwenyezi Mungu akamwamrisha huyo nabii anyunyizie maji juu ya hiyo mifupa. siku hiyo ilikuwa ya nairuzi. mtume akatekeleza hivyo na hao wote wakawa hai na kuingia jijini kwa mara ya pili. wakawa wafuasi wa mtume na wakafanya ibada na kuwa watiifu wa allah.

Katika kipindi cha raj'aat ("kurudi") waumini thabiti na makafiri waovu watahuishwa. vile vile baadhi ya manabii, mtume wetu mtukufu, maimam kumi na mmoja na baadhi ya masahaba wake na mashahidi wa karbala vile vile watarudi. kuna hadithi nyingi kuhusu jambo hili lakini tunaeleza machache tu.

1. Imam Jaafar Sadiq(a.s) amearidhia kwamba: katika kipindi cha raj'aat baada ya kujitokeza kwa Imam Mahdi(a.s) , kwanza imam Hussein(a.s) pamoja na masahaba wake waliouawa karbala watarudi tena duniani. pamoja na imam hussein(a.s) watakuwa manabii 70. Wakati umri wa hadhrat mahdi(a.s) utakapomalizika atamkabidhi pete yake imam hussein(a.s) ambaye atashungulikia mazishi ya hadhrat mehdi(a.s) baada ya kufa kwake.

2. zaidi ya hayo imam jaffar sadiq(a.s) amesema "baada ya raj'aat, imam mahdi(a.s) ataingia kufa na kutokea makaburini ya najaf panapoitwa waadis-ssalam allah atawapa uhai waumini thabiti 70,000 ambao watamsaidia hadhrat mahdi(a.s) .

3. vile vile imam(a.s) amesema kwamba wakati atakapojitokeza hadhrat mahdi(a.s) malaika mmoja atakwenda kwenye kaburi la kila mwumini na kumjulisha kujitokeza kwa hadhrat mahdi(a.s) na kumwambia asimame ikiwa anataka kufika kwa imam(a.s) wakati huo kila mwumini apendaye kwenda kwa imam(a.s) atatoka nje ya kaburi lake.

4. imam jaffar sadiq(a.s) vile vile amesema kwamba mwumini yeyote ambaye husoma Duaul-Ahad (dua inayohusu maamkizi kwa imam mahdi(a.s) atakuwepo miongoni mwa masahaba wa hadhrat mahdi(a.s) na akiwa amefariki Imam Mahdi(a.s) kudhihiri atapewa uhai na kuamshwa kutoka kaburini mwake.

5. Baada ya masimulizi hayo, imam(a.s) amesema kwamba kabla ya dhuhur (kujitokeza kwa mara ya pili) ya imam mabdi(a.s) kwa muda wa siku arubaini kuanzia mwezi mzima wa jamadiul akhir (mfungo tisa) hadi siku kumi za mwanzo wa mwezi wa rajab mvua zitanyesha kwa wingi mno kiasi ambacho hazikunyesha kamwe kabla ya hapo, napo ndipo mwenyezi mungu ataunganisha mifupa na nyama za wafu. waumini watajitokeza makaburini mwao huko wakijipangusa mchanga kichwani. kuna hadithi nyingi kuelezea hali hiyo lakini hatutaeleza hapa.

6. Haras bin Abdallah Rabai anahadithia kwamba: safari moja alikaa pamoja na khalifa mansur kwenye daraja la baghdad. ubavuni mwa khalifa alikuwa waziri mkuu wake sawaar. pamoja nao alikuwa mshairi seyyid hamyari ambaye alikuwa anasoma shairi alilotunga kumsifu huyo khalifa ambaye alifurahishwa sana na hilo shairi. waziri mkuu alipogundua kwamba khalifa alinogewa sana aliingiwa na husda na kusema, "eh kiongozi wa waumini, huyu seyyid kwa hakika hakupendi, bali anawapenda na kuwaheshimu viongozi wake: familia ya mtume(s.a.w.w) . licha ya hayo yeye hawakubali makhalifa na masahaba wa mtume(s.a.w.w) na ni adui yako."

Huyo Seyyid akajitetea: "huyu waziri wako hulalamika dhidi yangu kwa sababu ya husda. jamii yake nzima kabla ya kusilimu na kukubali dini ya uislam walikuwa na uadui dhidi ya nasaba yako. hata Mungu alimjulisha hivyo mtume(s.a.w.w) katika qur'an.

إِنَّ الَّذِينَ يُنَادُونَكَ مِن وَرَاءِ الْحُجُرَاتِ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿٤﴾

"Hakika hao wanao kuita nawe uko nyuma ya vyumba, wengi wao hawana akili." (49:4)

katika hao mmojawapo ni huyu waziri wako. khalifa akatabasamu na kusema: "hayo ni kweli". waziri mkuu hapo akapandwa na ghadhabu zaidi na kusema "huyu seyyid huamini katika raj'aat". seyyid akajibu "kwa hakika mimi ninaamini raj'aat kwa sababu allah amezungumzia juu ya raj'aat katika qur'an tukufu (na huyo seyyid akasoma aya tulizotaja za qur'an na vile vile hadithi nyingi za mtume mtukufu(s.a.w.w) kuhusu jambo hili.

Hapana shaka kuwa hadithi nyingi za mtume mtukufu(s.a.w.w) kwamba siku ya kiyama wenye kiburi watakuwa na sura ya chungu. aliendelea kusema kuwa katika siku za mwisho duniani wafuasi wake wengi watamezwa na ardhi na wengine watageuka kuwa na sura ya kima na nguruwe na kadhalika, itikadi yangu kuhusu raj'aat ni ya hakika na hutokana na agizo la qur'an tukufu na hadithi nyingi na kunithibitishia kwamba katika raj'aat huyu waziri atapatiwa uhai mara ya pili lakini atageuka sura ya mbwa, nguruwe au kima. kwa jina la allah, huyu waziri ni mdhalimu, mstakadhari na kafiri. kusikia maneno hayo machungu khalifa akatabasamu na kusema : "unayosema wewe ni kweli."

Katika kipindi cha raj'aat hadhrat mahdi(a.s) atalipiza kisasi kikamilifu dhidi ya wakatili wa imam hussein(a.s) na maimam wengine na waumini. wale waliouliwa bila kosa watarudishwa duniani ili waweze kumaliza umri waliojaaliwa na watapatiwa haki zao kutoka wakatili wao na hao wakatili vile vile watauliwa. Katika siku hizo hadhrat mahdi(a.s) atatawala kwa uadilifu kutokana na uwezo aliojaliwa na allah, hatahitaji mashuhuda. kipindi hicho kitajulikana kama kiyamat-al-sughra (kiyama-ndogo).

7. Imam Muhamad Baqir(a.s) amesema kwamba: siku ya ashura (siku ambayo imam Hussein(a.s) pamoja na aila masahaba zake waliuawa huko karbala) imam hussein(a.s) aliwaarifu masahaba wake kabla ya kuanza vita kwamba mtume mtukufu(s.a.w.w) alimjulisha kwamba baada ya kufariki kwake (mtumes.a.w.w ) maadui wake watamwalika imam Hussein (a.s) kwenda iraq na kumwua pamoja na masahaba wake. Imam Hussein(a.s) akaendelea: "mimi ninaona kuwa hawa makafiri watatuua sisi sote. kwa hakika baada ya kifo chetu sisi tutaonana na mtume mtukufu(s.a.w.w) na tutakaa naye kwa muda mfupi. tena katika kipindi cha raj'aat mimi (imam) nitakuwa wa kwanza kutoka kaburini mwangu. sisi tutapigana na hao maadui wa allah tukisaidiana na malaika ambao hawajawahi kuteremka ardhini nao watateremka pamoja na jibraeel, mikaeel na israfeel kuungana nasi. wakati huo mtume mtukufu(s.a.w.w) , Imam Ali (a.s) , ndugu yangu imam hassan(a.s) pamoja na maimam wote wanaotokana na dhuria yangu watakuwa nasi mtume mtukufu(s.a.w.w) atatweka bendera yake pamoja na upanga wake na kumkabidhi Imam Mahdi(a.s) . Masahaba wangu wote watakuwa na mimi na wataishi duniani kwa muda aliopanga allah.

Baadaye hadhrat ali(a.s) atanikabidhi mimi upanga wa mtume mtukufu(s.a.w.w) na atanituma pamoja na jeshi kwenda mashariki ya dunia (bara la asia). Huko nitapigana na maadui wa dini na kuwaua wote, nitafika barahindi na kuiteka na kuisafisha na kuondoa makafiri na washirikina. Nitawaua wanyama wote ambao nyama zao ziliharamishwa. nitawasihi wakristo, wayahudi na washirikina waje kwenye njia ya haki. Wale watakaobakia bila dini nitawaua. Katika kipindi hicho mwenyezi mungu atawahifadhi waumini kutoka kila balaa na ugonjwa na kuwajalia baraka na rehema. Matawi ya miti yatakuwa yamejaa matunda. Yale matunda yanayopatikana katika msimu wa joto yatapatikana katika kipupwe na yale ya kipupwe vile vile atapatikana katika msimu wa joto".

Baadaye imam Hussein(a.s) akawaambia masahaba wake kwamba allah amesema katika qur'antukufu kwamba

وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَىٰ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم بَرَكَاتٍ مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَـٰكِن كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُم بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٩٦﴾

"Na lau kama watu wa mji wangeliamini na kuepukana na maovu, sisi tungewapatia baraka kutoka mbinguni na aridhi, lakini walikadhibisha; kwa hivyo sisi tumewahukumu kufuatana na vitendo vyao." (7:96).

8. Nabii Idris alighibu kwa muda wa miaka ishirini. Alipojitokeza akaonyesha miujiza kwa kumrudisha duniani mtu aliyefariki. Mama wa huyo mtu aliyepatiwa uhai mpya akawajulisha jamii yake na wote wakaja kwa nabii kuomba msamaha na kumlalamikia awaondoshee hiyo gumba iliyowakabili kama bidhaa ya uhalifu wao. Nabii akawaombea msamaha kwa Mwenyezi Mungu na wote wakaokoka. Kwa hiyo, kuna mifano mingi ya watu waliokufa na kuhuishwa mara ya pili na ambao waliishi muda mrefu, kufunga ndoa na kuzaa watoto, udogo wa kitabu hiki haurulmsu kueleza kwa urefu mifano hlyo. Lakini lazima ieleweke bayana kwamba idadi maalum ya watu waliopatiwa uhai (kurudi duniani) baada ya kufariki kwa amri ya allah hujulikana kama raj'aat. kwa hivyo hakuna chochote cha kustaajabisha kwamba wakati wa zuhuru (kujitokeza baada ya kughibu) ya imam mahdi(a.s) kutakuwa raj'aat ya manabii, maimam(a.s) waumini thabiti na wadhalimu wakatili.