ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE0%

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE Mwandishi:
Kundi: Imam mahdi (a.s)

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

Mwandishi: Marehemu Mulla Muhammad Jaafar Sherif Dewj
Kundi:

Matembeleo: 20768
Pakua: 2971

Maelezo zaidi:

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 20 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 20768 / Pakua: 2971
Kiwango Kiwango Kiwango
ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

Mwandishi:
Swahili

16

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 24

WAJIBU WA WAUMINI NA DUA YA WAUMINI KATIKA KIPINDI CHA GHAIBA (KUGHIBU) KWA IMAM (A.S)

Ijapokuwa imam wetu(a.s) ameghibu machoni mwetu, lakini yeye ana habari zote kuhusu ibada zetu, vitendo, mashughuli yetu, matatizo na maafa tunayoyakabili. Mwumini yeyote wakati wa shida akiomba msaada kwa dhati hakosi kupata kutoka kwa imam(a.s) . Kuna masharti fulani ambayo waumini wanawajibika kutimiza ili kuthibisha ukweli wa itikadi yao:-

1. ni wajibu wa kila mwumini kwa dhati na kwa mapenzi kumkumbuka imam wake ambaye ni kiongozi wake wa kweli duniani na kesho akhera na kusoma dua mbali mbali katika kipindi hicho k.m. dua-ul-ahad kila siku baada ya swala ya asubuhi, dua-ul-nudba kila ijumaa na ziyarah (maamkizi).

2. ni wajiba wa kila mwumini kujikumbusha kwamba madhalimu wameghasibu haki ya imam(a.s) na kuwa yamefanyiwa mabadiliko na mageuzi katika kanuni za dini na kuwa wapenzi na wafuasi wa dhuria ya mtume mtukufu(s.a.w.w) ni wachache na wanadharauliwa, lazima huyo mwumini aombe mungu aondoshe hiyo balaa na aharakishe ukombozi wa mwisho.

3. Ni wajibu wa kila mwumini kuhakikisha kwamba dini inabaki,waumini wanaendelea kuimarisha imani yao na kujitahidi kadri ya uwezo wao kueneza dini pamoja na kuanzisha madarasa ya dini na kuchapisha vitabu vya dini.

4. Kama vile mtu hutoa sadaka kukinga balaa juu ya wazazi wake na familia yake, vivyo hivyo lazima atoe sadaka kwa ajili ya imam(a.s) kwa sababu yeye ni mtakatifu, hii ni alama ya mapenzi yakweli. kama ilivyoamrishwa kumswalia (salawat) mtume mtukufu(s.a.w.w) na aila yake ijapokuwa hawahitaji, lakini hiyo ni alama ya upendo na njia ya kujipatia jazaa kubwa, na vilevile utoaji wa sadaka kwa ajili ya imam(a.s) ni kuamini utukufu wake.

5. Ni lazima kila mwumini amfurahishe imam(a.s) kwa kusoma qur'an kila wikati, kuzuru pahala ptakatifu pa karbalaa na kwenda hajj kwa niaba yake na kadhalika. Imam(a.s) humwomba mungu awahifadhi na kuwasamehe waumini wake kwa sababu imam(a.s) huwa na taarifa kuhusu vitendo vyetu. mara moja abu muhammad adaji alimtuma mwumini mmoja kwenda kuhiji kwa niaba imam Mahdi(a.s) .

Huyo mtu alikuwa na wana wawili, mmoja wao mwumini na wa pili mpotovu. kutokana na pesa aliyopata kwenda kuhiji akampa fedha kidigo mwanawe mpotovu. alipofika arafah akakutana na mtu mwenye uso unaong'aa ambaye alimwambia, " Eh shekh, huni hata aibu? " huyo shekh akauliza, ' kwa sababu gani ?' huyo mtu akamjibu: 'Unajua kwamba huyo mtu uliokuja kuhiji kwa niaba yake ni imam wako na kwa hivyo anaelewa habari yote. Hata hivyo, katika pesa ulizopewa kufanyia hija ulimpa mwanao mpotovu. Utakuwa kipofu haraka sana' baada ya kusema hayo huyo mtu akaondoka. Siku chache baada ya kurudi nyumbani kwake akaumwa macho na kuyapoteza.

6. Katika kipindi cha shida na matatizo imam(a.s) huja kutoa msaada. lakini, shuruti yule mtu anaeomba msaada kwa imam(a.s) awe anaswali kila siku, kufunga kama ilivyoamrishwa, lifanya kila bidii kuepukene na maasi, kuomba toba kwa maasi aliyotenda, kuwa na mapenzi kwa ajili ya imam(a.s) , kumkumbuka imam katika maombi, dhikiri na maamkizi. Mtume mtukufu amesema:

'Hata unapokuwa umewekewa kisu shingoni ukimkumbuka imam wako wa wakati (imam al-zaman) bila shaka imam (a.s) atakuja kukusaidia' . Kuna nyakati imam(a.s) alitoa misaada na hilo litazungumzwa katika sura zinazo husika.

7. Ni faradhi ya kila mwumini wakati anapotaja jina la imam(a.s) katika maombi, maamkizi au mazungumzo kusimama na kuweka mkono wake wa kiume juu ya kichwa chake. hii ni alama ya mapenzi, heshima na taadhima kwa imam(a.s) .

8. Kuna hadithi nyingi zinazoeleza namna mbali mbali ya kuomba msaada wakata wa dhiki na shida. hadithi moja ni hii ifuatayo:- kataka kipindi cha utawala wa shah fatehali huko iran kulitokea mafarakano baina ya wanazuoni mashuhuri kuhusu suala la waqfu. Wanazuoni walio husika walikuwa agha haji muhammad ebrahim na agha mirza muhammad mabdi. kwa hiryo, shah wa iran alimtuma mwanazuoni wake mashuhuri sana mulla kassam isafahani kwenda kusuluhisha mafarakano hayo. alifanya hivyo na kuwapatanisha wanazuoni hao. Katika safari yake siku moja alikwenda makaburini huko isfahan akifuatana na msaidizi wake. Siku hiyo madhali haikuwa "alhamisi hawakuwa watu wengi huko makaburini na mikahawa ilifungwa. Baada ya kusoma suratul fatiha huko makaburini akamwambia msaidizi wake, "hapa hakuna mkahawa. mimi ninatamani kuvuta rushba".

Msaidizi wake akamjibu, "ungeniambia hayo tulipokuwa mjini ningeleta huka." basi, mulla kassam akaenda kwenye kaburi la mwanazuoni mashuhuri hayati mirza muhammad baqir damad. kaburi hilo lilijengwa vizuri na alipoingia humo alimwona sheikh kaketi juu ya mswala. mulla kassim alisogelea hilo kaburi na kuanza kusoma fatiha. kuyo mtu akamwambia: "mulla kasam, nyinyi mulla inaonyesha hamna tabia nzuri. kwa nini hukunisalimu wakati ulipo ingia?" mulla kassim alishangazwa na haiba ya huyo mtu na akainamisha shingo yake na kusema kwa unyenyekevu: baada ya kumaliza kusoma fatiha ningefika kwako na kukusalimia". baada ya kusema hayo akamsalimia huyo mtu ambaye alijibu na kusema, "tafadhali kaa, baba yako alikuwa mwana mwadilifu. Alimwomba mungu amjaalie mwana mwadifu ambaye atakuwa mwanazuini. Dua yake mungu ameikubali na amejaaliwa mwana mwadilifu na mwenye elimu kama wewe."

Baadaye huyo mtu akamwuliza mulla kassim kama angependa kuvuta huka. mulla kassam akajibu kwamba alidhani kwamba huko makaburini kutakuwa maduka na hivyo hakuleta huka yake. Mtu huyo akasema: 'tafadhali nenda ukalete huka katika kikapu changu." mulla kassam akaangalia ndani ya mkoba akaona huka, tumbaku na makaa ya kutosheleza pamoja na kibiriti. Mulla kassam aliamua kumwita msaidizi wake amtayarishie huka. Huyo mtu alimkataza asimwite mhudumu wake bali atayarishe huka yeye mwenyewe. Basi mulla kassam akatoka nje kutayarisha huka na kuvuta huko huko. Baada ya kuvuta huka. Mulla kassam akasafisha na kuirudisha kwenye mkoba. huyo mtu tena akamwuliza kwamba alikuwa na haja yoyote". Mulla kassam akamwomba chakula kidogo lakini mtu huyo akamwambia, "usiombe kitu cha dunia". mulla kassam akasema kwamba alikuwa tayari kupokea kitu chochote atakachopewa. kwa hiyo, akasema: "mimi ninakufundisha dua mbili na usome hizo wakati wote unapohitaji chochote au unapohitaji msaada wangu katika dhiki na papo hapo mimi nitakuja kukusaidia. hata hivyo, dua mojawapo ni kwa ajili yako tu, na ya pili kwa ajili ya kila mwumini".

Mulla kassam akaomba msamaha kwa sababu ya kutokuwa na karatasi au kalamu. Mtu huyo akamwelekeza akachukue kutoka mkobani. Mulla kassam alipoangalia mkobani aliona hakuna huka aliouweka humo yeye mwenyewe. aliona dawati, kalamu na karatasi tu. Akachukua hizo na kuanza kuandika. Kwanza huyo mtu akamwandikisha dua iliyokuwa kwa ajili yake tu. baadaye akamwandikisha dua nyingine ya kusoma mara sabini ambayo inamhusu kila mwumini akiwa na haja au anakabiliwa na dhiki "ya allah, ya muhammad, ya ali, ya fat1ma, ya sahibuzzaman adrikny wala tuhlikny". mulla kassam alipofikia neno la mwisho alisita maana katika vitabu vingine vimeandikwa adrikuuny 'katika uwingi' (nyinyi wote njooni kwa kunisa1dia). Huyo mtu akasema: "kwa nini huandiki. adrikny katika umoja ni sahihi kwa sababu mimi peke yangu naja kusaidia na mimi ni hujjat (khalifa) wa mungu katika muda huu na nina uwezo wote. kwa hivyo msaada wangu tu unaombwa. majina ya mungu, mtume mtukufu 'hadhrat ali(a.s) na fatima(a.s) yanatajwa kwa pamoja, kwa sababu wao ni wasila.

Mwombaji msaada ameomba msaada wangu kwa kutumia majina yao". kwa hivyo mulla kassam aliandika hivyo na kurudisha wino na kalamu mkobani. Akainua kichwa chake kutaka kusoma hizo dua il kuangalia kama kuna kosa. aliponyanyua kichwa chake hakumwona mtu yeyote, mswala wala mkoba. Papo hapo akaelekea mlangoni na kuangalia kote lakini hakumwona mtu yeyote. akamwuliza msaidizi wake, naye akajibu hakumwona mtu yeyote. mulla kassam hapo akaamini kwamba huyo mtu alikuwa imam wake(a.s) naye alionyeshwa miujiza na imam wake. kwanza imam(a.s) alijua alichotamani mulla kassam, katika mkoba wake hakikuwemo kitu chochote, tena kuona vifaa vya kuandika na hiyo huka kutoweka. akamshukuru mungu kwa nafasi hiyo aliyopatiwa lakini alisikitika kukosa fursa ya kumwuliza imam(a.s) masuala mengine.

9. Mwanazuoni mtakatifu seyyid ibne tawoos alimwusia mwanawe wa kwanza yafuatayo:- "mimi nakujulisha wewe, ndugu zako na yeyote atakayefahamu yaliyomo katika wasia huu kwamba mwenyezi mungu na mtume wake mtukufu(s.a.w.w) ametujulisha kuhusu bwana wetu imam wa wakati huu hadhrat imam mehdi(a.s) na vilevile kuhusu heshima, taadhima, misaada na manufaa wanayopata wafuasi wake kutoka kwake. sisi tusiwe tunamsahau na kutokumbuka kwa mapenzi hata kwa muda mfupi. ikiwa mtu atajishughulisha katika mambo ya dunia tu, utajiri, watoto, majumba na biashara basi atapendelea vitu duni vya dunia badala ya kumpenda imam wake."

Zaidi ya hayo, ikiwa mtu anajishughulisha nafsi yake na wafalme, wakuu duniani na viongozi, na kila saa anajibidiisha kuwafurahisha hao, kwa matumaini ya kunufaika kutoka kwao, basi naye daima atapenda uongozi na utawala wa wakuu hao uendelee. kwa hivyo, hatapata kujitokeza kwa imam(a.s) na utawala wake uanze kwa sababu utawala huo hautompendeza. kiini cha itikadi yetu ni kuwa imam wa wakati huu ni mtawala mstahilifu wa falme zote, na mali yote ni yake. Utawala na madamaa yote ni yake aliyopewa na mwenyezi mungu. Hata baada ya kuwa na itikadi kama hiyo ikiwa mwumini hachukizwi na hali ilivyo duniani na haombi mungu kuwa udhalimu wa haki za imam ukome basi huyo si mwumini mwenye imani halisi juu ya imam".

Dondoo hilo limechukuliwa kutoka wasia hiyo. kwa hakika, ikiwa mtu ana imani juu ya imam(a.s) basi lazima atamkumbuka imam wake. wakati wowote waumini wanapokutana jambo la kwanza la kuzungumzia liwe ughaibu wa imam(a.s) , upinzani dhidi ya uislam na masikitiko ya waumini. hivyo ndivyo inatakiwa iwe hali halisi. kwa hali ilivyo kwa wakati huu, ijapokuwa waumini wanamwamini humkumbuka imam(a.s) lakini mwaka mara moja tu, tarehe 15 shaaban au wanaposoma dua-ul-iftitah (dua inayosomwa usiku wa ramadhani) lailatulqadr, au katika maamkizi baada ya swala za kila siku. ni jambo la kuhuzunisha kwamba baada ya nyakati hizo hatuzungumzii chochote juu ya imam(a.s) wala hatumkumbuki. katika mikutano yetu hupitisha maazimio kuwatakia kheri watawala wa dunia, lakini hatufanyi hivyo kwa ajili ya mfalme wa dunia na akhera, baba yetu wa kiroho, na wala hatuombi msaada kutoka kwake kufanikisha mikutano yetu au kupatiwa faraja kutoka kwake (imam a.s.).

Kwa hiyo, ni wajibu wa viongozi wetu wa jamii, masheikh, wahubiri, pamoja na ulama kuendelea kueleza na kuhubiri habari za imam(a.s) , kughibu kwake na alama zitazotokeza siku za mwisho za dunia. Kwa kufanya hivyo, watachomeza hisia na kuzidisha matumaini ya waumini na kuepusha jamii kutokana na maasi, faraja na burudani, eti ndiyo maendeleo hayo! Lazima tutambue kuwa kughibu kwa imam(a.s) ni jaribio gumu kwa waumini. Mwenyezi Mungu aliwajaribu wafuasi wa mitume waliopita kama ilivyoelezwa bayana katika kitabu kitukufu na hadithi tulizonakili.

Ni ole wetu kuwa hata katika nyakati za taklifu na dhiki hatumkumbuki mhifadhi na imam(a.s) wetu na kuomba msaada wake. tunaamini kwamba mwenyezi mungu hakubali ibada zetu bila wasila ya imam(a.s) lakini bado tunaghafilika na imam wetu.

10. Katika zama za imam Ali(a.s) Sahaba wake mmoja ramila alisimulia: "safari moja nilipata homa kali. baada ya siku chache nikapata ahueni. ilikuwa siku ya ijumaa. kwa hivyo, niliamua kuoga tohara na kwenda msikitini ili niswali nyuma ya imam wangu na kufanya ziara yake. nikaoga na kubadilisha nguo zangu na kwenda msikitim. katikati ya hotuba nilikuwa ninahisi baridi na mwili wangu ukitetemeka lakini nikasubiri. Baada ya swala imam ali(a.s) alikwenda nyumbani na mimi nilimfuata nyumbani kwake.

Alinikaribisha na kuniambia kwamba nilikuwa natetemeka wakati hotuba ilipokuwa inatolewa. mimi nikamweleza hali yangu na imam(a.s) akssema: "oh Ramila, wakati wowote dhiki inapowakabili wapenzi wetu au wanapokuwa wagonjwa sisi vile viie huathirika kwa yale yanayowakabili wapenzi wetu". Mimi nikamwuliza: "Eh bwana wangu, hii athari hutokea kwa wakazi wa kufa tu wanapokabiliwa na dhiki?" imam(a.s) akajibu, "mfuasi wetu anapokabiliwa na tatizo au kuwa mgonjwa popote duniani sisi hupata taarifa papo hapo na kuathirika".

11. ikiwa kuna madhara au hofu kutokana na adui lazima tuombe msaada kutoka imam wa wakati huu kwa kuswali rakaateeni, kusoma ziara (maamkizi) kwa imam(a.s) na kusoma dua ifuatayo mara 70. ya mawlay, ya sahibazzamani; ana mustageethum bika, ya mawlay ikfini sharra many;udhini.

12. Namna nyingine ya kumkaribia na kuomba msaada kutoka kwa imam(a.s) ilivyonakiliwa katika vitabu vingi ni kumtumia aridhah na hayo hutupwa baharini, mtoni au ziwani. jambo hilo sana hufanywa siku ya 15 shaaban baada ya swala ya alfajiri kabla ya jua kuchomoza. aridhi hiyo huandikwa juu ya karatasi nadhifu na tohara na hufukizwa kwa udi na uturi na kufungwa katika udongo tohara na kutupwa majini kwa taadhima.

ili kufupisha maelezo hatuelezi kwa urefu dua inayosomwa wakati wa kutupa aridha hiyo majini, lakini mwumini yeyote anayetaka kupata msaada kwa kutumia njia hii anaweza kupatiwa aridha na dua inayohusika. bila shaka malalamiko haya humfikia imam(a.s) . mwumini yeyote mwenye imani madhubuti juu ya imam(a.s) na kuishi maisha ya kidini kwa kuswali, kufunga mwezi wa ramadhani na kujiepusha na maasi, anaweza kuomba msaada kutumia njia hii siku yoyote (siyo lazima iwe 15 shaaban). utaratibu huu humpa mtu nafasi kueleza bayana mapenzi na imani yake juu ya imam(a.s) na heshima ya kumtumia salaam kwa njia ya maandishi. hapa tunaeleza visa viwili kuhusu namna aridhi zilivyomfikia imam(a.s) na wahusika walivyo saidiwa.

1. Agha Mirza ibrahim shirazi anasimulia: "nilipokuwa shirazi nilikuwa na haja zangu chache ambazo zilikuwa zikinisumbua sana. kuiiko zote shauku ya kwenda karbala kuzuru kaburi la imam hussein(a.s) ilikuwa kubwa mno. ili kupata msaada wa imam-al-zaman(a.s) nilituma aridha kwa imam(a.s) . siku moja saa za jioni bila mtu yqyote kuniona nikatupa aridha yangu katika ziwa lililojaa maji. bila mwenyezi mungu hakuna aliyeshuhudia kitendo hicho.

Siku ya pili kama desturi nilikwenda darasani. walikuwa wanafunzi wengi huko darasani. mwalimu wangu kwa kunitaja jina alinijulisha kwamba ardhilihali yangu ilikwishamfikia imam(a.s) . Nilifurahi mno. Hata hivyo, nilimwuliza mwalimu wangu alipata vipi habari hiyo na akanijulisha: "jana usiku nilimwona hadhrat salman farsi katika ndoto. alikuwa na watu wengi pamoja na rundo kubwa la barua iliyokuwa mbele yake na ambazo akizikagua. aligeuka upande wangu na kunitajia jina lako pamoja na wachache wengine ili niwajulishe kwamba aridhi zenu zimekwishamfika imam(a.s) . baadaye niliona kwamba karatasi zilizokuwa mikononi nwa hadhrat salman zilikuwa na mhuri wa imam(a.s) .

Kwa hivyo, mimi nilielezwa kwamba aridha zote zilizoshughuiikiwa zilipatiwa muhuri wa imam(a.s) na zile zisizofanikiwa zilikosa muhuri. wanafunzi waliobaki waliniuliza kuhusu aridha hiyo na ndoto ya mwalimu wetu. niliwasimulia kuhusu aridha yangu ambayo iliwayakinisha kuhusu ndoto ya mwalimu wetu. kwa ufupi, nilipatiwa mahitaji yangu yote na vilevile nilifanikiwa kwenda karbalaa." Seyyid Muhammad Seyyid Abbas mkaazi wa Jabalul Amil, anahadithia: "mimi nilikuwa ninaishi najaf katika nyumba mojawapo iliyojengwa katika eneo la kaburi la hadhrat Ali(a.s) . nilikabiliwa na ufukara sana. mara nyingi ilibidi nipitishe siku zangu kwa kula tende kidogo na kunywa maji tu. Nilimwomba Mwenyezi Mungu kila siku nifarijike lakini sikumweleza mtu dhiki iliyonikabili. mwishowe nikaamua kutuma aridha kwa imam(a.s) .

Kila asubuhi wakati mlango wa najaf (mji mmoja huko iraq na pahala alipozikwa Imam Ali(a.s) ulipokuwa unafunguliwa nikienda kutupa aridhia yangu mtoni, siku 39 zilipita. Siku hiyo nilipokuwa ninarudi baada ya kutupa hiyo aridha nilihisi kama kuna mtu ananifuata. Nilipogeuka kuangalia nyuma nilimwona mwarabu kama mkaazi wa jabalu amil, akanisalimu na akaanza kufuatana nami. mimi nilijibu hiyo salam. yeye aliniuliza: "Sayyid Muhammad kwa muda wa siku 39 zilizopita kila asubuhi unapofunguliwa mlango wewe unatoka nje na kutupa aridha yako mtoni. una haja gani? unafikiri kama imam wako haelewi mahitaji yako?" mimi nilishangazwa vipi huyu mtu amejua shughuli zangu za kila siku maana sikumweleza mtu yeyote."

Papo hapo nikafahamu kwamba huyu anaweza kuwa imam(a.s) . nilisoma katika vitabu kwamba kitanga cha mkono uliobarikiwa wa imam(a.s) huwa chororo mno, hivyo kujitopsheleza nikakunjua mkono ili tupeane mikono. huyo imam(a.s) akanipa mkono wake na kitanga kilikuwa chororo mno. nilithibitisha kwamba huyo mtu alikuwa imam(a.s) na papo hapo niliinama ili nimbusu mikono lakini ghafla nikajikuta niko peke yangu. lakini nilifarijika kujua kwamba aridha yangu ilimfikia imam(a.s) na nilikuwa na bahati nzuri ya kuonana naye. Baada ya muda mfupi tu hali yangu ikatengemaa.