TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA Juzuu 1

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA13%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA Mwandishi:
Kundi: tafsiri ya Qurani

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
Juzuu 9 Juzuu 10 Juzuu 11
  • Anza
  • Iliyopita
  • 20 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 39802 / Pakua: 5104
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA Juzuu 1

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

4

5

14

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KWANZA

AL - BAQARAH (NG’OMBE)

﴿وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ لَا تَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّـهَ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَقُولُوا لِلنَّاسِ حُسْنًا وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ ثُمَّ تَوَلَّيْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنكُمْ وَأَنتُم مُّعْرِضُونَ﴾

83.Na tulipochukua ahadi na wana wa Israil: Hamtamwabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu; na muwafanyie wema wazazi na jamaa na mayatima na maskini; na semeni na watu kwa uzuri na simamisheni swala na toeni zaka. Kisha mkageuka isipokuwa wachache tu katika nyinyi na nyinyi mnakengeuka.

AHADI NAWANAWA ISRAIL

Aya 83

AYA HII IMEKUSANYA MAMBO YAFUATAYO

I. Kuwatendea wema wazazi wawili Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameikutanisha shukrani ya wazazi wawili na yake na akawajibisha kuwatendea wema na ku-wafanyia hisani; sawa na alivyowajibisha kuabudiwa kwake. Kuanzia hapa ndio mafakihi wamesema kwa kauli moja kwamba kuwaasi wazazi wawili ni katika madhambi makubwa, na kwamba mwenye kuwaasi ni fasiki hauwezi kukubaliwa ushahidi wake. Hadith tukufu inasema: Hakika mwenye kuwaudhi wazazi wawili hatapata harufu ya pepo. Makusudio ya kuwatendea wema wazazi wawili ni kuwatii na kuwachukulia upole.

Kuna kisa cha mwanamke mmoja aliyembeba baba yake mgongoni kutoka Yemen mpaka Makka. Akatufu naye katika Al-Kaaba. Mtu mmoja akamwambia Mwenyezi Mungu akulipe heri, umetekeleza haki yake. Akasema: Hapana sijatekeleza; yeye alikuwa akinibeba huku akinitakia uhai (niishi) na mimi hivi sasa ninambeba huku nikimtakia mauti (afe).

II. Jamaa, Mayatima na Maskini Aya imewajibisha muungano wa udugu kwa kuungana kwake na wazazi wawili. Pia imewajibisha kumchunga yatima na mali yake kwa yule ambaye atakuwa ni walii (msimamizi) au wasii wa yatima huyo. Vile vile Aya imemwajibishia fakiri fungu katika mali za matajiri.

III. Kuchukulia usahihi Kama mtu akifanya amali yoyote au akisema kauli yoyote inawezekana iwe sahihi au isiwe sahihi. Sasa je, uchukuliwe usahihi juu ya kitu chochote au la; au ni lazima iweko dalili mkataa? Mfano kumwona mtu pamoja na mwanamke, hujui kama ni mkewe au ni mtu kando. Au usikie maneno nawe hujui kuwa msemaji alikusudia wewe au la. Mafakihi wameafikiana kuchukulia usahihi katika hilo (afanyalo si kosa) na mfano wake. Wametolea dalili hilo kwa kauli yake Mwenyezi Mungu: Na semeni na watu kwa uzuri.

Amirul Muminin Ali(a.s) naye amesema:Liweke jambo la ndugu yako juu ya uzuri wake.

Vile vile kwa kauli ya Imam Jafar Sadiq(a.s) :Yakadhibishe masikio yako na macho yako kwa ndugu yako. Wakitoa ushahidi kwako watu hamsini kwamba yeye amesema kadhaa, na yeye akuambie sikusema, basi mwamini yeye na uwachukulie kuwa ni waongo wale watu hamsini.

Huu ndio msingi wa kiutu hasa. Kwa sababu unajenga heshima ya mtu na unatilia mkazo mfungamano wa kusaidiana na kuchukuliana upole kati ya watu, na unawaepusha na yale yanayoleta chuki. Kwa hivyo basi, inabainika kuwa Uislamu haujishughulishi na itikadi na ibada pekee, bali unajishughulisha na utu na heri zake na unaonyeshea njia itakayopelekea uhai wenye matunda ya kufaulu. Lakini wale ambao wameiuza dini yao kwa shetani wameupoteza msingi huu wa kiutu, wakaenda kombo na malengo yake; na wakaboresha kazi ya uharamia na kuchukua riba. Ilivyo hasa kama tulivyoonyesha ni kwamba msingi wa kuchukulia usahihi haufungamani na kazi ya unyanganyi, ujambazi, kupoteza na mengineyo yanayofanana na hayo, ambayo tunayajua kwa yakini kuwa ni katika mambo ya haramu na yenye kuangamiza. Isipokuwa msingi huo tuliotaja unakuwa katika mambo ambayo yana uwezekano wa kuwa kweli au uwongo, usawa au upotevu.

﴿وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ لَا تَسْفِكُونَ دِمَاءَكُمْ وَلَا تُخْرِجُونَ أَنفُسَكُم مِّن دِيَارِكُمْ ثُمَّ أَقْرَرْتُمْ وَأَنتُمْ تَشْهَدُونَ﴾

84.Na tulipochukuwa ahadi yenu kuwa Hamtamwaga damu zenu, wala hamtatoana majumbani mwenu; nanyi mkakubali na hali mnashuhudia.

﴿ثُمَّ أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ تَقْتُلُونَ أَنفُسَكُمْ وَتُخْرِجُونَ فَرِيقًا مِّنكُم مِّن دِيَارِهِمْ تَظَاهَرُونَ عَلَيْهِم بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَإِن يَأْتُوكُمْ أُسَارَىٰ تُفَادُوهُمْ وَهُوَ مُحَرَّمٌ عَلَيْكُمْ إِخْرَاجُهُمْ أَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍ فَمَا جَزَاءُ مَن يَفْعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمْ إِلَّا خِزْيٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰ أَشَدِّ الْعَذَابِ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴾

85.Kisha nyinyi hao hao, mnajiua watu na mnawatoa baadhi yenu majumbani mwao, mkisaidiana dhidi yao kwa (njia ya) dhambi na uadui. Na wakiwajia mateka mnawakomboa na hali kumeharamishwa kwenu kuwatoa. Je mnaamini baadhi ya kitabu na kukataa baadhi? Basi hakuna malipo kwa mwenye kufanya haya katika nyinyi ila fedheha katika maisha ya dunia, na siku ya Kiyama watarudishwa kwenye adhabu kali; na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda.

﴿أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا بِالْآخِرَةِ فَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴾

86.Hao ndio walionunua maisha ya dunia kwa akhera, kwa hivyo hawatapunguziwa adhabu wala hawatanusuriwa.

HAMTAMWAGA DAMU ZENU

Aya 84 - 86

MAELEZO

Mazungumzo ya Mayahudi na matatizo yao hayajakwisha; na yanayokuja ni mengi. Kwa muhtasari wa Aya za Mayahudi, ni kwamba: wao kila wanapopewa mwito wa uongofu na msimamo mzuri wanakakamia katika kueneza ufisadi duniani na wanaendelea katika upotevu, kama kwamba wao wameumbwa kumuasi Mwenyezi Mungu na kuikhalifu haki. Tawrat yao inawaamrisha kumwabudu Mwenyezi Mungu, wao wanaabudu ndama; Musa anawaambia: Hii Tawrat kutoka kwa Mwenyezi Mungu, wao wanasema; Tuonyeshe huyo Mwenyezi Mungu wazi wazi. Tena Musa anawaambia: Zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu kwenu na mumwombe msamaha, wao wanafanya mzaha na stihizai.

Ikiwa Nabii Musa(a.s) tu walimfanyia hivyo naye ni Mwisrail mwenzao, je mwingine watamfanyiaje? Mfalme Edward I aliwafukuza Uingereza na wakateswa na Hitler huko Ujerumani baada ya kuwajua walivyo.Wao wanastahili zaidi ya hayo. Tumekwishaeleza vile walivyofanyiwa na Firaun, Nebukadnezzar na Warumi. Kwa vyovyote ilivyo ni kwamba miongoni mwa ahadi alizozichukua Mwenyezi Mungu kwa Mayahudi katika Tawrat ni kutouana wenyewe kwa wenyewe wala wasimtoe yeyote katika nyumba yake. Na Mayahudi hawakanushi ahadi hizi, bali hawana nafasi ya kuzikanusha kwa sababu zinapatikana katika Tawrat ambayo wanaiamini kwa ukweli na kwamba hiyo ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Lakini pamoja na hayo yote waliikhalifu kwa makusudi, kwa hivyo ikawasimamia hoja.

MAANA

Na tulipochukuwa ahadi yenu kuwa hamtamwaga damu zenu wala hamtatoana majumbani mwenu. Anarudia Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwakumbusha Wana wa Israil ahadi walizoziweka kwa ulimi wa Musa na Mitume wengine waliokuwa baada yake. Miongoni mwa ahadi hizo ni kutomwaga damu na kutotoana majumbani mwao.Nanyi mkakubali na hali mnashuhudia . Yaani mlikubali ahadi na kushuhudiana nyinyi wenyewe. Unaweza kuuliza: Kukubali na kushuhudia ni kitu kimoja, sasa vipi ikafaa kuunganisha kitu kwa kitu chenyewe?

Jibu : Inawezekana kuwa ni katika upande wa kutilia mkazo. Vile vile inawezekana kuwa makusudio ya kukubali ni kukubali Mayahudi wa zamani na kushuhudia ni kwa watakaokuja. Kwa sababu wa zamani walikubali na wakakiri ahadi.

Kisha nyinyi hao hao mnajiua, na mnawatoa baadhi yenu majumbani mwao. Yaani nyinyi baada ya kukiri kwenu ahadi, mnaivunja wenyewe, mwenye nguvu anamuua mnyonge na kumtoa katika nyumba yake. Mkisaidiana dhidi yao kwa (njia ya) dhambi na uadui. Aya inaonyesha kugawanyika Mayahudi na kusaidiana kila kikundi na Waarabu dhidi ya kikundi kingine cha Mayahudi.

KISA

Kwa ufupi kisa kilikuwa hivi: Aus na Khazraj ni koo mbili za Kiarabu zenye asili moja, kwa sababu Aus na Khazraj walikuwa ndugu. Koo mbili hizi zilikuwa na uadui na vita kati yao kabla ya Uislamu na walikuwa wakimshirikisha Mwenyezi Mungu, hawajui pepo wala moto wala Kiyama au Kitabu.

Na Mayahudi nao walikuwa na koo tatu: Bani Qaynuqaa, Bani Quraidha na Bani Nadhir, nao walikuwa na uadui na vita kama ilivyokuwa kati ya Aus na Khazraj pamoja na kuwa hawa Mayahudi walikuwa katika asili moja na dini yao ni moja. Wote hao, Mayahudi na Waarabu walikuwa ni wakazi wa Madina. Bani Qaynuqaa walikuwa wakisaidiana na Aus dhidi ya Bani Nadhir na Quraidha; kama ambavyo Bani Nadhir na Bani Quraidha walikuwa wakisaidiana na Khazraj dhidi ya Qaynuqaa. Vita vinapochacha Myahudi alikuwa akimuua ndugu yake Myahudi na kumtoa nyumbani kwake akiweza. Lakini kama Yahudi akitekwa na Mwarabu, basi Mayahudi hukomboana hata kama ni adui yake mkubwa.

Kwa ufupi ni kwamba Mayahudi hawaoni kizuizi kuwaua Mayahudi wenzao kiasi cha kusaidiana na Waarabu, lakini Mwarabu akimteka nyara Yahudi, basi Yahudi mwenzake huingiwa na huruma na kutoa fidia kumkomboa mwenzake ingawaje ni adui yake. Kwa hivyo Yahudi anahalalisha kumuua ndugu yake na kumfukuza, lakini asiwe mateka. Walikuwa wakidai kwamba Tawrat yao ndiyo inayowaamrisha kukomboa mateka wa Kiyahudi. Ndipo Mwenyezi Mungu akawajibu kwamba Tawrat yao vile vile imewaamrisha kutouana na kutotoana majumbani; sasa vipi mmeiasi Tawrat katika kuua, na kuitii katika kukomboa mateka? Hii ndiyo tafsiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

Na wakiwajia mateka mnawakomboa na hali kumeharamishwa kwenu kuwatoa. Je mnaamini baadhi ya kitabu na kukataa baadhi?

Walilolikataa ni kule kukatazwa kuua, kusaidiana katika dhambi na uadui na kutoana majumbani. Waliloamini, ni lile la kutoleana fidia mateka. Na hii ndiyo istihzai hasa na kucheza na dini.

Unaweza kuuliza, lenye kuharamishwa kwao ni kuua na kusaidiana na kutoana majumbani; kwa nini Mwenyezi Mungu amehusisha kutoana majumbani katika Aya hii?

Jibu : Ndio yote ni haramu, lakini Mwenyezi Mungu amehusisha kutoana kwa kutaja mara ya pili kwa sababu ya kutilia mkazo tu. Kwa sababu kutoana majumbani huendelea, kinyume na kuua kama walivyosema wafasiri wengine.Basi hakuna malipo kwa mwenye kufanya haya katika nyinyi ila fedheha katika maisha ya duniani. Malipo yanaweza kuwa ya heri au ya shari; kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

﴿ وَجَزَاهُم بِمَا صَبَرُوا جَنَّةً وَحَرِيرًا ﴾

Na malipo yao kutokana na vile walivyosubiri ni pepo na nguo za hariri. (76:12)

﴿ وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا﴾

Na mwenye kumuua mumin kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannam, humo atadumu... (4:93)

Hao ndio walionunua maisha ya dunia kwa akhera; kwa hivyo hawatapunguziwa adhabu wala hawatanusuriwa. Mwenyezi Mungu hakuharamisha, katika Aya hii wala nyingine chakula kizuri na mavazi ya kifahari, isipokua anamkemea mwenye kuiuza dini yake kwa ajili ya dunia yake na akaishi maisha ya kidhulma na upotevu. Hakika Mwenyezi Mungu anakataza ufisadi duniani na sio vipambo na neema za dunia, bali hakika Yeye Mwenyezi Mungu amekanusha sana kuharamisha neema na ladha katika dunia hii; kama anavyosema:

﴿ قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّـهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا ﴾

Sema: Ni nani aliyeharimisha pambo la Mwenyezi Mungu ambalo amewatolea waja wake.Na, vitu vizuri katika riziki? Sema: hivyo ni kwa walioamini.... (7:32)

Yaani ni halali kwa aliyevichuma kwa njia ya halali na ni haramu kwa anayevitafuta kwa kunyanganya, kuhadaa na utapeli. Kwa ufupi ni kwamba misingi ya ki-Quran ni kuishi watu katika kusaidiana yale yaliyo na wema kwa wote. Ama misingi ya Kizayuni ya kikoloni, ni Maadamu mimi ninaishi basi na uangamie ulimwengu na kila mwenye kwenda na msingi huu, basi ni Mzayuni akijua au asijue; hana budi kukumbana na uadilifu wa mbingu na ardhi na kuteremkiwa na mateso na balaa.

MAYAHUDI NA UKOMUNISTI NA UBEPARI

Inadhihiri kutokana na Aya tukufu kwamba kugawanyika Mayahudi katika makundi mawili ni mambo waliyoyarithi kutoka kwa mababa na mababu zao ili wazidishe moto kuwaka kwa upande fulani na wapate masilahi yao kwa upande wa pili. Kama ilivyo kuwa kugeuka geuka kwao ndio asili yao na ada yao. Kabla ya nusu karne walikuwa wakilingania ukomunisti na ndio wao leo wanaoulemea ubepari. Hawana lengo lolote isipokuwa kuugawa ulimwengu na kuanzisha vita na fitina ili watekeleze siasa zao za ukandimizaji na ukupe wa kunyonya jasho la watu.

﴿ وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَقَفَّيْنَا مِن بَعْدِهِ بِالرُّسُلِ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ أَفَكُلَّمَا جَاءَكُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُكُمُ اسْتَكْبَرْتُمْ فَفَرِيقًا كَذَّبْتُمْ وَفَرِيقًا تَقْتُلُونَ﴾

87.Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukawafuatisha Mitume baada yake; na tukampa Isa, mwana wa Maryam, hoja zilizo wazi wazi, na tukamtia nguvu kwa roho takatifu. Kila alipowafikia Mtume kwa yale yasiyoyapenda nafsi zenu, mlijivuna, kundi moja mkalikadhibisha na kundi jingine mkaliua!

﴿ وَقَالُوا قُلُوبُنَا غُلْفٌ بَل لَّعَنَهُمُ اللَّـهُ بِكُفْرِهِمْ فَقَلِيلًا مَّا يُؤْمِنُونَ ﴾

88.Na walisema: Nyoyo zetu zimefunikwa, bali Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kufuru zao; kwa hivyo ni kidogo tu wanayoyaamini!

TULIMPA MUSA KITABU

Aya 87 - 88

LUGHA

Neno Maryam, lina maana ya mtumishi kwa lugha ya kiebrania. Kwa sababu mama yake Maryam aliweka nadhiri ya kumtoa awe mtumishi wa Baitul -Maqdis (Quds). Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukawafuatisha Mitume baada yake.Yaani tumempa Musa Tawrat; kisha tukawapeleka Mitume baada yake, mmoja baada ya mwengine. Inasemekana kuwa hazikupita zama kati ya Musa na Isa ambaye ndiye Mtume wa mwisho wa Kiisrail, isipokuwa kulikuwa na Mtume Mursal au Mitume tofauti wanaoamrisha mema na kukataza mabaya. Imesemwa katika Tafsirul Razi na ya Abu Hayan El-Andalusi kwamba Mitume hao ni Yoshua, Samuel, Shamun, Daud, Suleiman, na Shiau. Vile vile Armiya, Uzayr, Ezekiel, Eliyas, Yunus, Zakaria na Yahya.

Na tukampa Isa mwana wa Maryam, hoja zilizo wazi wazi na tukamtia nguvu kwa roho takatifu.

Isa(a.s) ndiye Mtume wa mwisho wa wana wa Israil, na kati yake na Musa kulikuwa na karne 14.Ni kidogo tu wanayoamini. Yaani hawakuamini katika Mayahudi isipokuwa wachache tu, kama Abdallah bin Salam na wafuasi wake. Mwenye Majmaul-Bayan amechagua kusema kuwa maana ya:ni kidogo tu wanayoamini, kwamba hakuamini yoyote katika wao, si wachache wala wengi; kama vile inavyosemwa ni nadra kufanya. Kwa maana ya kutofanya kabisa. Lakini maana tuliyoyaeleza mwanzo ndiyo yaliyo sahihi zaidi, kwa kuangalia kauli yake Mwenyezi Mungu: ﴿ وَقَوْلِهِمْ قُلُوبُنَا غُلْفٌ بَلْ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَيْهَا بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا﴾

...Na kwa kusema kwao nyoyo zetu zimefumbwa, bali Mwenyezi Mungu amezipiga mhuri kwa kufuru yao, basi hawataamini ila wachache tu. (4:155).

MKWELI NA TAPELI

Inatakikana tuangalie tena kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu:Kila walipowafikia Mitume mpaka mwisho.

Hakika Aya hii tukufu pamoja na kuwa na madhumuni ya kumsuta mwenye kuwaasi Mitume na kuikataa haki, kama haikuafikiana na matakwa yake, pia vile vile ina madhumuni ya kumsuta mwenye kuwapuuza watu na asiwakabili kwa tamko la haki kwa kutaka kujipendekeza kwao kwa tamaa ya cheo nk. Hakika mtengenezaji wa kweli anaizungumza haki wala haogopi lawama katika kazi ya Mwenyezi Mungu. Kwa sababu lengo lake la kwanza na la mwisho ni kumridhisha Mwenyezi Mungu peke yake. Kwa ajili hiyo ndio anajitoa muhanga na kufa shahidi kwa ajili ya kuwapelekea na kuwaonyesha haki umma. Ama mharibifu aliye mwongo anakuwa na lengo la kuwaridhisha watu ili wanunue bidhaa yake: Imam Ali(a.s) anasema:Usimchukize Mwenyezi Mungu kwa kumridhisha yeyote katika viumbe vyake.

﴿ وَلَمَّا جَاءَهُمْ كِتَابٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ وَكَانُوا مِن قَبْلُ يَسْتَفْتِحُونَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَمَّا جَاءَهُم مَّا عَرَفُوا كَفَرُوا بِهِ فَلَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴾

89.Na kilipowajia kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kisadikishacho yaliyo pamoja nao, na zamani walikuwa wakiomba ushindi juu ya makafiri. Lakini yalipowafikia yale waliyoyajua waliyakataa. Basi laana ya Mwenyezi Mungu iko juu ya makafiri.

﴿ بِئْسَمَا اشْتَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ أَن يَكْفُرُوا بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ بَغْيًا أَن يُنَزِّلَ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ فَبَاءُوا بِغَضَبٍ عَلَىٰ غَضَبٍ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴾

90.Kibaya kabisa walichokiuzia nafsi zao ni kule kukataa kile alichokiteremsha Mwenyezi Mungu kwa kuona maya kuwa Mwenyezi Mungu amemteremshia fadhila zake amtakaye katika waja wake. Kwa hiyo wakastahili ghadhabu juu ya ghadhabu, na watakuwa nayo makafiri adhabu idhalilishayo.

﴿ وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا نُؤْمِنُ بِمَا أُنزِلَ عَلَيْنَا وَيَكْفُرُونَ بِمَا وَرَاءَهُ وَهُوَ الْحَقُّ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَهُمْ قُلْ فَلِمَ تَقْتُلُونَ أَنبِيَاءَ اللَّـهِ مِن قَبْلُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴾

91.Na wakiambiwa: Yaaminini aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu husema: Tunaamini yaliyoteremshwa juu yetu; na hukataa yaliyo nyuma yake; na hali yakuwa hii ndiyo haki inayosadikisha yaliyo pamoja nao. Sema: Mbona mliwaua Mitume wa Mwenyezi Mungu hapo zamani kama mlikuwa mkiamini

KILIPOWAFIKIA KITABU

Aya 89 - 91

MAELEZO

Mayahudi wa Madina walikuwa wamejipa tumaini la kujiwa na Mtume na walikuwa wakimtaja Muhammad, wakiwaambia Aus na Khazraj: Kesho atakuja Mtume ambaye sifa zake tumezikuta katika Tawrat na atawashinda waarabu na washirikina wote. Mayahudi walikuwa wakifikiria kuwa huyo Mtume ni Mwisrail sio Mwarabu. Basi Mwenyezi Mungu alipomtuma Muhammad Mwarabu, waliona unyonge, wakaingiwa na ubaguzi na kuupinga Utume wake na kukanusha yale waliyokuwa wakiyasema kwa Muhammad. Ikawa baadhi ya Aus na Khazraj wanawambia: Enyi Mayahudi, jana mlikuwa mkitutisha kwa Muhammad(s.a.w.w) kuwa sisi ni watu wa shirk: mlikuwa mkimsifu na kumtaja kwamba yeye ni Mtume. Sasa mbona sisi ndio tunaomwamini na nyinyi mmegeuka na kurudi nyuma? Wakajibu Mayahudi: Hakutujia na kitu tunachokijua na wala yeye siye yule tuliyekuwa tukiwatajia. Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii:Na kilipowajia kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kisadikishacho yaliyo pamoja nao.

Yaani ilipowajia Quran walikanusha. Quran waliyoikanusha ndani yake mna usadikisho wa yale yaliyo katika Tawrat yao iliyobashiri kuja Muhammad(s.a.w.w) . Kwa hiyo wanamfanya mwongo yule anayewasadikisha wao, bali wanajikadhibisha wenyewe. Hili si geni wala si ajabu kwa yule anayefanya matakwa yake na mapenzi yake ndiyo kigezo cha kuhalalisha, kusadikisha na kukadhibisha. Kila mwenye kujihalalishia yale yaliyo haramu kwa wengine, basi anaingia katika mkumbo huu. Ewe Mwenyezi Mungu tukinge na shari ya kutojifahamu sisi wenyewe.

Na hapo mbele walikuwa wakiomba ushindi juu ya makafiri lakini yalipowafikia yale waliyokuwa wakiyajua waliyakataa. Mayahudi kabla ya kuja Mtume Muhammad(s.a.w.w) walikuwa wakiwaonya Aus na Khazraj kwa Muhammad. Lakini alipokuja mambo yaligeuka, Aus na Khazraj wakamwamini na wakamsaidia mpaka wakaitwa Ansar (wasaidizi) na Mayahudi wakamkanusha; wakaangamizwa na kufukuzwa na hao Ansar kupitia kwa Muhammad; kama vile walivyokuwa wao wakiwaonya Ansar. Namna hii wanapata wenye vitimbi vibaya, na balaa humshukia yule anayemtakia mwenzake hiyo balaa.

Unaweza kuuliza: Kwa nini Mayahudi waligeuza imani waliyokuwa nayo kwa Muhammad?

Jibu : Walikuwa wakiitakidi kwamba Mtume atakayekuja atakuwa Mwisrail kutoka katika kizazi cha Is-haq, kwa kufikiria wingi wa Mitume Waisrail. Walipomwona ni Mwarabu kutoka katika kizazi cha Ismail, walimkanusha kwa uhasidi na ubaguzi tu wa Kiyahudi. Na kila mwenye kuipinga haki kwa ubaguzi wa kikabila au vinginevyo, basi huyo ni sawa na Mayahudi hao ambao walikataa kumkiri Muhammad, si kwa lolote isipokuwa kwamba yeye ni Mwarabu tu. Kibaya kabisa walichokiuzia nafsi zao ni kule kukataa alichokiteremsha Mwenyezi Mungu.

Quran tukufu mara nyingi hutumia tamko la kuuza na kununua na biashara, kuhusu amali njema na mbaya. Kwa vile mtu akiamini na akafanya amali njema, ni kama kwamba amefanya biashara ya nafsi yake na kuiokoa; na kama akikufuru na kuacha kunufaika, ni kama kwamba ameiuza nafsi yake kwa shetani kwa thamani duni kabisa. Kuziuzia nafsi zao hapa ni kwa maana ya kuwa Mayahudi wameziuzia shetani nafsi zao na wame-

* 26 Haya ndiyo waliyoyataja wafasiri kwa kuangalia dhahiri ya Aya. Utakuja ubainifu wa sababu za hakika za kumkanusha kwao Muhammad(s.a.w.w) katika Aya ya 91 ambazo ni manufaa na chumo lililotokana na uasherati, udanganyifu, riba, na mengineyo yaliyoharamishwa na Uislamu. jiangamiza; wala hapana thamani ya nafsi zao isipokuwa hasadi na ubaguzi wa Kiyahudi tu. Kwa hivyo ndiyo Mwenyezi Mungu akasema:Kwa kuona maya kuwa Mwenyezi Mungu humteremshia fadhila zake amtakaye katika waja wake. Yaani walimkanusha Muhammad(s.a.w.w) si kwa jingine isipokuwa wao walitaka kuhodhi wahyi na fadhila kwao tu peke yao. Hawakubali kutoka kwa Mwenyezi Mungu wala kwa mwengine isipokuwa yale yanayoafiki mapenzi na manufaa yao. Kwa hiyo wao wanastahili adhabu mara mbili, kwa kukanusha na kwa ubinafsi wao.

Na wanapoambiwa: Yaaminini aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu. Yaani aminini wahyi kama ulivyo bila ya kuangalia utu wa mwenye kuufikisha wahyi huo. Kwa sababu Mtume ni wasila tu wa kufikisha. Ama sharti lenu la kuamini wahyi kuwa uteremshwe kwa taifa la Kiisrail tu, na kama ukiteremshiwa mwengine basi hamwamini, sharti hili linafichua kukosa kuamini wahyi kimsingi. Isitoshe, itakuwa nyinyi mnatoa hukumu kwa Mwenyezi Mungu kwa mapenzi yenu. Maana yake nyinyi mnataka Mwenyezi Mungu awanyenyekee na mnakataa kumnyenyekea.

Husema: Tunaamini yaliyoteremshwa juu yetu. Huku ni kukiri wazi kwamba wao hawaamini wala hawataamini isipokuwa kwa sharti la kuteremshwa wahyi kwao, na hawataamini wahyi utakaoteremshwa kwa mwingine, hata kama kutakuwa na dalili elfu.Sema: Mbona mliwaua Mitume wa Mwenyezi Mungu hapo zamani kama mlikuwa mkiamini.

Hakuna hoja yenye nguvu zaidi ya hii; yaani sema ewe Muhammad kuwaaambia Mayahudi: Nyinyi ni waongo katika madai yenu ya kuamini wahyi kwa kuuhusisha na taifa la Kiisrail, bali nyinyi hamwamini wahyi kabisa, hata ule uliowahusu nyinyi! Dalili ya hayo ni kwamba Mwenyezi Mungu amepeleka Mitume kutoka kwenu na kwa ajili yenu na akawajibisha muwasadiki na kuwatii, lakini pamoja na hayo wengine mliwafanya waongo; kama vile Isa(a.s) na wengine mkawaua kama vile Zakaria na Yahya. Hii inafahamisha uongo wenu na kugongana vitendo vyenu na maneno yenu na kujidaganya wenyewe.

Imekuwa sawa kuuelekeza msemo wa kuua kwa Mayahudi wa Madina pamoja na kuwa walioua ni mababu zao. Hiyo ni kwa sababu umma wao ni mmoja kwa kushiriki kuridhia kuua.

WALIOFANANA NA MAYAHUDI

Mayahudi walimkataa Muhammad(s.a.w.w) , kwa sababu alikuwa si Mwisrail; Naye Abu Sufian alimkanusha na kuongoza jeshi kumpinga kwa sababu Mtume ni katika ukoo wa Hashim. Alikataa kwa sababu ukoo wa Hashim utapata utukufu wa Utume kuliko ukoo wake yeye Abu Sufiani wa Umayya. Vile vile Maquraish waliukana ukhalifa wa Ali(a.s) , kwa sababu walichukia kukusanyika Utume na Ukhalifa katika nyumba ya Hashim. Baadhi ya wasiokuwa Waarabu wanaona uzito kuwa Marjaa (Mufti) wa kwanza awe Mwarabu; kama ambavyo baadhi ya waarabu nao wanaona uzito kuwa Marjaa (Mufti) ambaye si Mwarabu. Mimi nawajua watu ambao wako tayari kubaki kwenye upotevu lau wanahiyarishwa kuifuata haki kwa wasiokuwa wao. Vile vile lau wanahiyarishwa kati ya kusikiliza sifa za mwingine, basi wangeona bora kusikiliza za Yazid.

Kwa ajili hiyo ndipo ukaona mtu anafanya juhudi ya kutafuta aibu ya mwenzake akipata chembe tu, huikuza na kuifanya jabali, na akiikosa huizusha. Mwenye kuona fadhila kuwa ndio msingi, huikuza vyovyote iwavyo na njia yoyote itakavyokuwa na humwonyesha mwingine kama anavyoona yeye; bali hufanya kazi ya kuieneza. Ama mwenye kuikanusha, hutumia muundo huo ambao wameutumia Mayahudi kwa inadi.

﴿ وَلَقَدْ جَاءَكُم مُّوسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِن بَعْدِهِ وَأَنتُمْ ظَالِمُونَ ﴾

92.Na aliwajia Musa na hoja zilizo wazi wazi, kisha mkafanya ndama baada yake na hali nyinyi ni madhalimu.

﴿ وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاسْمَعُوا قَالُوا سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَأُشْرِبُوا فِي قُلُوبِهِمُ الْعِجْلَ بِكُفْرِهِمْ قُلْ بِئْسَمَا يَأْمُرُكُم بِهِ إِيمَانُكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴾

93.Na tulipochukua ahadi yenu na tukauinua mlima juu yenu: Kamateni kwa nguvu haya tuliyowapa na sikilizeni. Wakasema: Tumesikia na tumekataa na wakanyweshwa nyoyoni mwao (imani ya) ndama kwa kufuru yao. Sema: Ni kibaya kabisa kilichowaamrishia imani yenu; mkiwa ni wenye kuamini.

﴿ قُلْ إِن كَانَتْ لَكُمُ الدَّارُ الْآخِرَةُ عِندَ اللَّـهِ خَالِصَةً مِّن دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴾

94.Sema: Ikiwa nyumba ya akhera iliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni yenu nyinyi tu bila ya watu wengine, basi tamanini mauti kama nyinyi ni wa kweli.

﴿ وَلَن يَتَمَنَّوْهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ﴾

95. Wala hawatayatamani kabisa kwa sababu ya yale yaliyotangulizwa na mikono yao, na Mwenyezi Mungu anawajua madhalimu.

﴿ وَلَتَجِدَنَّهُمْ أَحْرَصَ النَّاسِ عَلَىٰ حَيَاةٍ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا يَوَدُّ أَحَدُهُمْ لَوْ يُعَمَّرُ أَلْفَ سَنَةٍ وَمَا هُوَ بِمُزَحْزِحِهِ مِنَ الْعَذَابِ أَن يُعَمَّرَ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴾

96.Na Utawaona wanapupia zaidi maisha kuliko watu wengine na kuliko wale wamshirikishao Mwenyezi Mungu. Kila mmoja katika wao anapenda lau angelipewa umri wa miaka elfu. Na huko kupewa kwake umri mwingi hakuwezi kumwondoshea adhabu; na Mwenyezi Mungu anayaona wanayoyatenda .

MUSAALIWAJIA NA HOJA

Aya 92 - 96

MAELEZO

Aya hizi ziko wazi na zinayakariri yaliyotangulia. Kwa hiyo tutaeleza maana kwa ujumla. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimwamrisha Mtume wake kujadiliana kwa uzuri na wapinzani. Maana ya kujadiliana kwa uzuri ni kuzungumza na moyo na akili. Hoja zote za Quran ziko namna hiyo; imewataka wakanushaji wajifikiriie wao wenyewe na kuumbwa mbingu na ardhi; akamwambia mwenye kumnasibisha Bwana Masih uungu, kuwa yeye Masih na mama yake walikuwa wakila chakula. Na inazungumza na nyoyo za Mayahudi kwa Aya hizi kwa kuwakumbusha neema ya Mwenyezi Mungu ya kuwapelekea Tawrat ambayo ndani yake mna uongofu na nuru; kama zilivyowakumbusha Aya zilizotangulia kukombolewa kwao kutoka kwenye minyororo ya Firaun, n.k.

Kisha Mwenyezi Mungu akawakemea kwa kuabudu kwao ndama wakaikufuru na kuipinga neema Yake, amekariri kutaja kuinuliwa jabali juu yao kutokana na uasi wao na mantiki ya kiakili ikayakadhibisha madai yao ya kuwa wao ni watoto na wapenzi wa Mwenyezi Mungu, na kwamba pepo inawahusu wao tu hataingia mwengine zaidi yao. Vilevile amewaamrisha kutamani mauti ikiwa wao ni wakweli. Kwa sababu mwenye kuitakidi kwamba pepo ni yake, basi atachagua mauti yenye raha kuliko kuwa na maisha ya balaa na mashaka. Kisha Quran ikatoa habari kwamba wanapupia sana dunia na wana pupa zaidi kuliko wale wasioamini pepo wala moto. Bali hata mtu katika wao anaweza kutamani lau angeliishi miaka elfu. Lakini kurefusha kwake umri hakutamfaa kitu wala hakutamwokoa na adhabu.

Lengo la majadiliano haya ya kimantiki ya akili yaliyo salama ni kuwathibitishia Mayahudi hoja kwamba wao ni waongo wanavyodai kuwa wanaamini Tawrat, na kudai kwao kuwa wao ni taifa teule la Mwenyezi Mungu. Sheikh Maraghi katika tafsir yake anasema: Imekuja Hadith kwamba Abdalla bin Rawaha alipokuwa akipigana na Warumi alikuwa akiimba: Kwa hamu naitamani, Pepo ilokaribia Yenye vinywaji laini, Vilo baridi jamia Na Ammar bin Yasir katika vita vya Siffin alisema: Hapo kesho twaazimu, Kukutana na wapenzi Muhammad muadhamu, Na swahabaze wa enzi

Ikiwa Mayahudi hawatatamani mauti basi wao si wakweli wa imani. Hoja hii inawahusu watu wote. Kwa hivyo ni wajibu kwa Waislamu kuifanya hoja hiyo ni mizani watakayopimia madai yao ya imani na kusimamia haki za Mwenyezi Mungu. Wakiwa wanaona raha kujitolea roho zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, watakuwa ni waumini wa kweli, vinginevyo watakuwa kinyume na madai yao.

MASLAHI NDIO SABABU

Hatuna shaka kabisa kwamba suala la kumkadhibisha Muhammad (s.a.w.) sio suala la kuhusiana na ubaguzi tu. Isipokuwa sababu hasa ni maslahi yao ya kiutu na manufaa yao ya kimaada. Kwani wao wanaishi kwa utapeli, riba, na uasherati; na Muhammad(s.a.w.w) anayaharamisha hayo. Vipi wataamwamini? Ushahidi wa hayo ni kwamba wao hawana sababu nyingine isipokuwa pupa ya manufaa ya kibinafsi. Na kila mwenye kupupia manufaa yake, haumfai mjadala mzuri. Na kaui yake Mwenyezi Mungu: Na utawaona wanapupia zaidi maisha, inafahamisha hilo.

11

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KWANZA

AL - BAQARAH (NG’OMBE)

﴿ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴾

47.Enyi wana wa Israil, ikumbukeni neema Yangu niliyowaneemesha, na nikawatukuza kuliko viumbe wengine.

﴿ وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا شَفَاعَةٌ وَلَا يُؤْخَذُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ﴾

48.Na iogopeni siku ambayo nafsi haitafaa nafsi kwa lolote.Wala hayatakubaliwa kwake maombezi (shufaa), wala hakitapokelewa kikomboleo; wala hawatanusuriwa.

WANAWA ISRAIL TENA!

Aya 47 - 48

MAELEZO

Enyi wana wa Israil ikumbukeni neema Yangu.

Aya hii inatilia mkazo Aya iliyotangulia, na ni maandalizi kwa yatakayokuja baada yake. Tutaonyesha katika sehemu itakayofuatia hekima ya kukaririka. Makusudio ya kukumbuka hapa ni kushukuru; yaani zishukuruni neema zangu kwa usikizi na twaa. Na nikawatukuza kuliko viumbe wengine.

Mwenyezi Mungu aliwafadhilisha kuliko mataifa mengine ya wakati huo. Herufi lam katika neno Alamin ni ya kuenea kwa kawaida, sio kuenea kwa kiuhakika. Inatosha kuwa ubora ni katika upande mmoja na sio pande zote. Upande ambao Waisrail wamepambanuka na watu wengine ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwapelekea idadi ya Mitume; kwa mfano Musa, Harun, Yoshua, Zakaria na Yahya na wengineo. Wote hao ni Waisrail. Vyovyote ilivyo, kuwa bora kwao kwa watu wa zama zao kwa upande fulani, hakufahamishi kuwa bora katika kila upande kwa watu wa wakati huo; wala sio kwamba mtu wao ni bora kuliko mtu mwingine. Bali kule kuwa Mitume wengi wamekuja kutokana na kabila lao ni hoja juu yao na wala sio hoja yao, kwa sababu hilo linafahamisha kwamba wao walikuwa katika upotevu sana, ikawa kuna haja sana wapate waonyaji na wahadharishaji. Na ogopeni siku mbayo nafsi haitaifaa nafsi nyingine kwa lolote. Yaani kila mtu na lake hakuna dhahiri wala batini, hakuna kusaidiana wala kuoneana huruma.

﴿ يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ ﴾

Siku ambayo mtu atamkimbia ndugu yake. (80:34).

Wala hayatakubaliwa kwake (hiyo nafsi) maombezi (shufaa), wala hakitapokelewa kikomboleo; wala hawatanusuriwa. Yaani Kiyama ni sawa na mauti, haufai usaidizi wowote, haitafaa fidiya yoyote, hata ikiwa ghali, wala haitazuia nguvu yoyote hata iwe kubwa kiasi gani. Hakuna chochote isipokuwa Rehema ya Mwenyezi Mungu:

﴿ لَئِن لَّمْ يَرْحَمْنَا رَبُّنَا وَيَغْفِرْ لَنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴾

Kama hataturehemu Mola wetu na kutusamehe, bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliopata hasara. (7:149)

KUKARIRIKA KATIKA QURAN

Mara ya pili Mwenyezi Mungu anawaku-mbusha wana Israil neema Zake na amerudia baada ya Aya tano. Hiyo siyo Aya peke yake iliyorudiwa katika Quran, zimeka-ririka Aya nyingi hasa zile zinazofungamana na wana wa Israil pamoja na Musa(a.s.) . Wengi hujiuliza sababu ya kukaririka Aya.Wameafikiana wafasiri kwamba hekima ya kukaririka ni kutilia mkazo. Baada ya kupita siku, wakuu wa vyama, wanasiasa, wafanyibiashara na wenye mashirika wamegundua kwamba, kukar-irika jambo ndio njia nzuri ya kulipendekeza, kulikinaisha na kulifanyia propaganda. Kwa ajili hiyo ndio wakaweka mitindo mbali mbali ya matangazo, kukawa na watu maalum wa kuhusika nayo na yakawa ghali sana.

Gustave Lebon anasema katika kitabu chake kiitwacho The man and his work: Mwenye kulikariri tamko mara kwa mara hulibadilisha kuwa itikadi. Dr Gibson katika kitabu kilichotarjumiwa kwa kiarabu kayfa tufakkir (Vipi utafikiri) anasema Ibara zina sumaku zinapokaririka mara kwa mara mbele ya macho yetu na masikio yetu, zinapumbaza akili zetu kabisa. Kwa hivyo basi Quran inakariri kwa mfumo mwingine pamoja na kuzidisha makemeo na mengineyo kwa kiasi cha hekima inavyotaka.

SHUFAA (UOMBEZI)

Hapana budi shufaa iwe na pande tatu: Mwenye kuombwa, mwenye kuombewa na muombezi ambaye anakuwa kati ya hao wawili, anaomba kwa yule wa kwanza ili amsaidie wa pili ni sawa apate idhini ya yule mwenye kuombwa au la. Hiyo ndiyo Shufaa kwa viumbe. Ama shufaa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) maana yake ni msamaha na maghufira kwa mwenye dhambi; haitakuwa shufaa mbele ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa idhini yake.

Amesema mwenye Majmaul-Bayan Shufaa kwetu ni yenye kuhusika na kuondoa madhara na kuondoa mateso kwa mumin mwenye dhambi. Muutazila na Khawarij wamekanusha Shufaa ya Muhammad(s.a.w.w) kwa wenye madhambi makubwa katika umati wake, kwa maana hii tuliyoinakili kutoka kwa mwenye Majmaul-Bayan, lakini Imamiya na Ashaira wameithibitisha kwamba iko.Akili haihukumu kutokea Shufaa au kutotokea, lakini haioni pingamizi yoyote ya kupatikana. Kwa hiyo, kusihi kwake na kuthibiti kwake kutategemea kunakili kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Ambaye kumemthibitikia kunakili huko, basi ni wajibu kwake kuamini Shufaa, na kama hakuthibitikiwa basi atasamehewa. Kwa hali hiyo inatubainika kuwa shufaa si msingi wa dini na kwamba mwenye kuikanusha na huku anamwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi huyo ni Mwislamu bila shaka.

Tukirudi kwenye Aya za Quran tunakuta nyingine zinakanusha; kama ile inayosema:

﴿ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خُلَّةٌ وَلَا شَفَاعَةٌ ﴾

...Siku ambayo hapatakuwa na bishara wala urafiki wala Shufaa (uombezi).... (2:254)

Hapo inaonyesha kukanusha Shufaa kabisa.Na Aya nyingine zinathibitisha kwa sharti; kama ile inayosema:

﴿لَا تُغْنِي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا إِلَّا مِن بَعْدِ أَن يَأْذَنَ اللَّـهُ لِمَن يَشَاءُ وَيَرْضَىٰ ﴾

....Hautafaa chochote uombezi (shufaa) wao isipokuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia. (53:26)

Tukiziunganisha Aya mbili hizi na tukazikusanya pamoja, natija itakuwa, Mwenyezi Mungu atakubali Shufaa kutoka kwa mwombezi baada ya kumpa idhini. Sio lazima kupatikana idhini ya Mwenyezi Mungu kwa jina la mmoja mmoja, bali inatosha tu kwa Mtume kujua kwamba Shufaa ni halali ikiwa yule mwenye kuombewa si katika wenye kuwakandamiza watu na kunyanganya riziki zao; bali ni katika watu wa kawaida tu, ambao wanafanya madhambi ya kawaida.

Kwa maneno mengine ni kwamba makusudio ya idhini ya Mwenyezi Mungu kwa Shufaa ni kumpa wahyi Mtume wake kwamba Mimi nimekuruhusu kuwaombea uwatakao katika Umma wako ambao wamefanya mad- hambi maalum. Hapo basi mambo ya hao wenye madhambi yatakuwa mikononi mwa Mtume(s.a.w.w) ; naye atamwombea yule mwenye kustahiki kuombewa. Imethibiti kwamba yeye amesema: Nimeuweka akiba uombezi wangu kuwaombea wenye madhambi makubwa katika Umma wangu.

Sisi tuna yakini kuthibiti Shufaa katika Uislamu.Lakini hatujui kwa ufafanuzi; wakati huo huo tunaamini kwa imani ya mkato, kwamba mwombezi bora wa mtu ni matendo yake, na kwamba kitakachowaombea wenye dhambi ni toba. Hakika Mwenyezi Mungu haweki kizuizi kwa mwenye kutaka kuokoka akiwa na ikhlasi na akakimbilia kwenye ukarimu wa Mwenyezi Mungu hali ya kunyenyekea.

﴿وَإِذْ نَجَّيْنَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ ﴾

49.Na tulipowaokoa kwa watu wa Firaun waliowapa adhabu mbaya; wakiwachinja watoto wenu wakiume na kuwaacha hai wakike; na katika hayo ulipatikana mtihani mkubwa uliotoka kwa Mola wenu.

﴿وَإِذْ فَرَقْنَا بِكُمُ الْبَحْرَ فَأَنجَيْنَاكُمْ وَأَغْرَقْنَا آلَ فِرْعَوْنَ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ﴾

50.Na tulipoitenga bahari kwa ajili yenu na tukawaokoa, na tukawazamisha watu wa Firaun na hali mwatizama.

NA TULIPOWAOKOA

Aya 49 - 50

LUGHA

Neno: Aal, lina maana ya kurudi; kwa hiyo kila mwenye kurudiwa kwa nasaba, rai au itikadi basi yeye ni Aal wa wale wanaomrudia, kisha likawa linatumiwa zaidi kwa maana ya watu wa nyumba ya huyo mtu atakayetajwa, lakini hawezi kuitwa mtu Al mpaka awe na utukufu fulani. Makusudio ya Al-Firaun hapa ni wafuasi wake ambao walikuwa wakiwatesa wana wa Israil kwa amri yake. Abu-Hayan Al-Andalusi (Mhispania) amesema: Katika tafsir yake kubwa Al-Bahrul Muhit; Firaun ni lakabu (msimbo) ya wafalme wa Misri wakati huo; kama vile Kisra wa Fursi, Kaizari wa Roma, Najashi wa Uhabeshi, Tubba wa Yemen na Khaqani wa Uturuki.

Lakini alhamdulillah misimbo hii yote imebakia kuwa ni vigano tu!

MAELEZO

Baada ya Mwenyezi Mungu kuwakumbusha neema zake kwao kwa ujumla, sasa anawakumbusha kwa ufafanuzi. Bora zaidi ya neema aliyoidokeza ni kuwaokoa na Firaun na wafuasi wake ambao waliwapa Mayahudi adhabu kali. Mwenyezi Mungu ameifasiri adhabu hiyo kwa kusema: wakiwachinja watoto wenu wakiume na kuwaacha hai wakike. Yaani wanawaua watoto wanaume na kuwaacha wanawake waje kuwafanya watumishi.

* 18 Mwenye Majmaul Bayan anasema: Firaun aliota mambo yaliyomtisha. Wakamfasiria makuhani kuwa atazaliwa kijana wa kiume kutoka kwa wana wa Israil ambaye atakuja muua, ndipo Firaun akawafanyia hivyo wana wa Israil. Zaidi ya hayo Wamisri walikuwa wakiwadhalilisha Wayahudi kwa kuwatuma kazi za kuvunja mawe, kuchimba mifereji na kazi nyinginezo za sulubu. Msemo umewaelekea Mayahudi waliokuwepo zama za Mtume Muhammad(s.a.w.w) , kwa sababu wao walikuwa kwenye dini ya mababu zao na waliridhia amali zao. Na,mwenye kupenda amali ya watu wengine anakuwa ameshirikiana nao.

Na katika hayo ulipatikana mtihani mkubwa uliotoka kwa Mola wenu: Yaani, Enyi wana wa Israil, Mwenyezi Mungu amewatahini katika shida na raha, ili ijulikane kuwa je mtapigana jihadi na kuwa wavumilivi katika shida? Na je,mtashukuru raha? Au mtasalimu amri katika shida na mkufuru katika neema? Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamtahini mtu ili ajue, la! Yeye anajua lenye kuwa kabla ya kuwa; isipokuwa yeye anamtahini mtu kwa ajili ya kusimamisha hoja juu yake. Kwani hakuna madai kwa asiyekuwa na hoja, hata kama yenye kudaiwa yanathibiti katika elimu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Mwenyezi Mungu amewaonyesha Waisrail neema ya pili aliposema: Na tulipoitenga bahari kwa ajili yenu na tukawaokoa, na tukawazamisha watu wa Firaun

Yaani tulitenga bahari na tukafanya njia kumi na mbili kwa hisabu ya wajukuu. Wajukuu katika wana wa Israil ni koo katika kizazi cha Yaqub(a.s) Kwa ufupi Wayahudi walikuwa katika unyonge na udhalili wa hali ya juu; na adui yao alikuwa na nguvu za hali ya juu. Lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akabadilisha hali hiyo kupitia mikononi mwa Mtume wake Musa(a.s) , wao wakawa ndio wenye nguvu; na adui yao akawa dhalili, hilo wakaliona kwa macho yao; kama inavyosema Aya: Na hali nyinyi mnaangalia. Mwenyezi Mungu alimdhalilishia yule aliyewadhalilisha na akamwangamiza yule aliyetaka kuwaangamiza. Kwa hivyo basi wamelazimiana na hoja na imewalazimu kuwaidhika na kuzingatia, wala wasiwafanyie wengine yale waliyofanyiwa na wengine.

Lakini hivi leo mfano ule ule waliokuwa wakifanyiwa na Firaun ndio wanawafanyia Wapelestina. Na waendelee hivyo, lakini wajue hali itakuja wabadilikia tu, na yatawafika yale yaliyompata Firaun. Na waangalie ilivyokuwa kwa Nebukadnezzar na Warumi; na kwamba shujaa huvuma kisha akaisha. Jambo la kustaajabisha sana kwa mtu ni kwamba anapokuwa kwenye shida, kisha akaokolewa na Mwenyezi Mungu, basi hupetuka mipaka akafanya uovu na kusahau kila kitu. Wafasiri wengi wamesema, kwamba bahari iliyotajwa ni Bahari nyekundu (Red Sea).

﴿وَإِذْ وَاعَدْنَا مُوسَىٰ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِن بَعْدِهِ وَأَنتُمْ ظَالِمُونَ﴾

51. Na tulipomwahidi Musa masiku arobaini mkafanya ndama (kuwa Mungu) badala ya Mwenyezi Mungu mkawa madhalimu (wa nafsi zenu).

﴿ثُمَّ عَفَوْنَا عَنكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴾

52.Kisha tukawasamehe baada ya hayo ili mpate kushukuru.

﴿وَإِذْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَالْفُرْقَانَ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ﴾

53.Na tulipompa Musa kitabu na upambanuzi ili mpate kuongoka.

NA TULIPOMWAHIDI

Aya 51 - 53

LUGHA

Neno: Musa kwa lugha ya Kiarabu lina maana ya: kifaa cha kunyolea nywele kilichotengezwa kutokana na chuma; lakini maana yanayokusuduwa kwa Musa bin Imran siyo ya Kiarabu, bali ni ya Kikibti ambayo ni matamko mawili: Mu lenye maana ya maji na Sa lenye maana ya mti. Kwa hiyo maana ya Musa ni maji ya mti, Ama maana ya kuitwa Maji ya mti, kama ilivyoelezwa katika Majmaul-Bayan, ni kwamba wajakazi wa Asiya(mke wa Firaun), walitoka kwenda kuoga wakakuta sanduku lililokuwa na Musa ndani yake baina ya maji na mti; wakawa naye.

MAELEZO

Baada ya Firaun kuangamizwa na Mwenyezi Mungu na waliokuwa pamoja naye, Waisrail Walipumua, wakarudi Misri wakiwa salama; kama livyoelezwa katika Majmau.Wakati huo, Tawrat ilikuwa bado haijateremshwa, wakamtaka Musa awaletee kitabu kutoka kwa mola wao. Basi Mwenyezi Mungu akamwahidi kumteremshia Tawrat na akamwekea wakati. Musa akawaambia: Hakika Mola wangu ameniahidi kitabu ambacho ndani yake mna ubainifu wa ambayo ni wajibu kwenu kuyafanya na kuyaacha. Akawambia wakati wake ambao ni masiku arobaini, na masiku hayo - kama ilivyosemwa - ni mwezi wa Dhul-Qaada, na siku kumi za mwezi wa Dhul- Hijja.

Musa akenda kwa Mola wake ili awachukulie watu wake kitabu; ndugu yake Harun akawa naibu wake. Kabla ya kwisha muda wa kuja Musa, walianza kuabudu ndama badala ya Mwenyezi Mungu, wakajidhulimu wao wenyewe.

Hiyo ndiyo maana ya dhahiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

Na tulipomwahidi Musa masiku arobaini mkafanya ndama (kuwa Mungu) badala ya Mwenyezi Mungu mkawa madhalimu ( wa nafsi zenu).

Baada ya Musa kurejea kwa watu wake, walitubia na wakarudi kwa Mola wao; Mwenyezi Mungu akawakubali toba yao, na hii ni neema ya tatu ambayo imeelezewa katika Aya:Kisha tukawasamehe baada ya hayo .

Ama neema ya nne ni; kitabu cha Mwenyezi Mungu:Na tulipompa Musa kitabu na upambanuzi ili mpate kuongoka. Kitabu chenyewe ni Tawrat; yenye kukusanya kila kitu kwa ajili ya kubainisha haki na batili, na halali na haramu.

Kunganisha kati ya neno, kitabu na kupambanua, ni kuunganisha sifa kwenye kile kinashosifiwa. Kwa muhtasari ni kwamba: Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewakumbusha Waisrail katika Aya zilizotangulia, neema nne, Kuwaokoa kuchinjiwa watoto wao wa kiume na kuachwa wa kike wawe watumwa, kuangamia kwa Firaun, kusamehewa na kuletewa Tawrat.

Maelezo mazuri zaidi niliyoyasoma kuhusu maudhui haya, ni kauli ya Abu Hayan Al-Andulusi katika Tafsir Al -Bahrul Muhit; namnukuu: Tazama uzuri wa safu hizi ambazo zimepangika kwa mpango wa mtungo wa lulu na wa sayari katika falaki zake, kila safu katika hizo, yaani neema, imeishia kwa mnasaba wake na ikafikia daraja ya juu ya ufasaha ukitoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia mdomoni mwa Muhammad mwaminifu wake, bila ya kusoma kitabu chochote kabla yake, wala kuandika kwa mkono wake.

Abu Hayan anaonyesha kuwa mpangilio huo wenye kupangika vizuri ni katika miujiza ya Muhammad; kwamba yeye anauelezea bila ya kujifundisha. Mwenyezi Mungu awarehemu wahenga, awasamehe na awape neema nyingi. Kwani hakika wao hawakuona chochote chenye harufu ya kuitilia mkazo dini hii na Mtume wake mtukufu isipokuwa walikinyooshea shingo kwa pupa na shauku; wakafanya haraka kukisherehesha, kukifafanua na kukitolea dalili. Lakini tuko wapi sisi wanavyuoni wa sasa ambao twapupia zaidi dunia; hatuoni umuhimu wowote isipokuwa umuhimu wetu tu; wala matatizo isipokuwa matatizo ya watoto wetu tu! Tuko wapi sisi na hao watukufu waliojitolea kila kitu kwa ajili ya kuutukuza Uislamu na Mtume wa Uislamu? Mwenyezi Mungu awasamehe na awainue, na kila mwenye kuitumikia dini, kwenye daraja ya juu.

﴿وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِنَّكُمْ ظَلَمْتُمْ أَنفُسَكُم بِاتِّخَاذِكُمُ الْعِجْلَ فَتُوبُوا إِلَىٰ بَارِئِكُمْ فَاقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ عِندَ بَارِئِكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴾

54.Na Musa alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmejidhulumu kwa kufanya kwenu ndama (kuwa ni Mungu). Basi tubuni kwa Muumba wenu na jiueni; hilo ni bora kwenu mbele ya Muumba wenu.Basi akapokea toba yenu.Hakika Yeye ndiye apokeaye toba Mwenye kurehemu.

﴿وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ نَرَى اللَّـهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْكُمُ الصَّاعِقَةُ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴾

55.Na mliposema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpaka tumwone Mungu waziwazi.Ukawanyakua ukelele na hali mwatizama.

﴿ثُمَّ بَعَثْنَاكُم مِّن بَعْدِ مَوْتِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴾

56.Kisha tukawafufua baada ya kufa kwenu ili mpate kushukuru.

﴿وَظَلَّلْنَا عَلَيْكُمُ الْغَمَامَ وَأَنزَلْنَا عَلَيْكُمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴾

57.Tukawatilia kivuli kwa mawingu na tukawateremshia Manna na Salwa: Kuleni katika vitu vizuri tulivyowaruzuku.Na hatukuwadhulumu, lakini wamejidhulumu wenyewe.

MUSA ALIPOWAAMBIAWATU WAKE

Aya 54 - 57

LUGHA

Manna ni kitu fulani kinachonata mithili ya asali, na Salwa ni tombo (aina ya ndege wa jamii ya kware, kama kuku).

MAELEZO

Na Musa alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mumejidhulumu kwa kumfanya kwenu Ndama (kuwa ni Mungu). Basi tubuni kwa Muumba wenu. Maana yoyote inayofahamika kwa kusikia tu haihitaji tafsiri, bali kuifasiri na kuisherehesha ni ufedhuli tu! Na Aya hii iko katika hali hiyo.

Na jiueni Makusudio ya kujiua yako wazi, ni kujitoa roho: wala hapana haja ya kufasiri vingine, kwa maana ya kuhalifu mapenzi na kuidhalilisha nafsi kwa kukiri dhambi na makosa au kumwabudu sana Mwenyezi Mungu; kama ilivyosemwa. Makusudio ya kujiua hapa, ni baadhi wawaue wengine. Kwa hivyo yule ambaye hakurtadi dini yake kwa kuabudu ndama ndio atamuua yule aliyertadi dini yake. Sawa na kusema kwake Mwenyezi Mungu:

﴿فَإِذَا دَخَلْتُم بُيُوتًا فَسَلِّمُوا عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ ﴾

...Mnapoingia katika majumba jitoleeni salamu.... (24:61).

Na vile vile kusema kwake

﴿وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ ﴾

...Wala msijikejeli: yaani msikejeliane (49:11)

Amesema Tabrasi katika Majmaul-Bayan kwa upande wa Shia, na Razi katika Tafsir Al-Kabir, kwa upande wa Sunni, kuwa Mwenyezi Mungu aliijaalia toba yao ni huko kujiua, sio kwamba wajiue baada ya kutubia. Hukumu hii ina mfano wake katika sharia ya Kiislamu, pale ulipozingatia kuua kuwa ni hadi na adhabu ya kosa la kurtadi.Hilo tutalieleza katika kifungu cha kurtadi kinachofuatia. Zinaendelea Aya kueleza maovu ya Waisrail: Na mliposema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpake tumwone Mungu waziwazi Wakati Musa alipowaendea na Tawrat, baadhi yao walisema: Hatuamini kuwa kitabu hiki kinatoka kwa Mungu mpaka tumwone kwa macho; bila ya kizuwizi chochote kati yetu sisi na Yeye; na atueleze ana kwa ana kuwa Yeye amekutuma na kitabu hiki.

Sijui kama wale wanaokanusha kuwepo Mwenyezi Mungu wakati huu, kwa kuwa tu hawajamuona kwa wazi, wanategemea Waisrail na inadi yao? Au vipi? Mayahudi walimwambia Musa: Hatutakuamini mpaka tumwone Mungu. Hawa wa sasa nao wanasema: Hakuna chochote chenye kupatiana isipokuwa kile tunachoweza kukiona kwa jicho, kukigusa kwa mkono, kukinusa kwa pua au kukionja kwa mdomo. Hivyo ndivyo inavyokaririka historia ya picha ya upinzani wa haki katika kila kizazi.

Yakawanyakua mauti ya ghafla na hali mwalizania Yaani adhabu kutoka mbinguni iliwapata wale waliomwambia Musa hatukuamini mpaka tumwone Mungu wazi wazi, wakaangamizwa mbele ya macho ya wale wasiopinga. Kisha tukawafufua baada ya kufa kwenu ili mpate kushukuru. Baadhi ya wafasiri kama vile Muhamad Abduh, katika tafsiri Al-Manar, amesema: Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakuwarudishia uhai mara ya pili baada ya kuchukuliwa na ukelele; na kwamba makusudio ya kufufuliwa kwao ni kizazi chao kuwa kingi. Wengine wakasema kuwa sio hivyo, hayo hayafahamiki kutokana na dhahiri yake ilivyo, na kwamba waliorudishwa ni wale wale waliouliwa na ukelele.Na hii ndiyo sawa, kwani hapana sababu inayolazimisha taawil, madamu kurudishwa kuwa hai kunawezekana kiakili. Na hilo lilimtokea Uzair, kama inavyofahamisha Aya:

﴿قَالَ أَنَّىٰ يُحْيِي هَـٰذِهِ اللَّـهُ بَعْدَ مَوْتِهَا فَأَمَاتَهُ اللَّـهُ مِائَةَ عَامٍ ثُمَّ بَعَثَهُ﴾

Akasema: Mwenyezi Mungu atauhuisha vipi (mji) huu baada ya kufa kwake? Mwenyezi Mungu Akamfisha kwa miaka mia, kisha akamfufua.... (2:259)

Kimsingi,lililotokea haliwezi kuwa muhali. Kwa hakika inaonyesha kwamba makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu: Yakawanyakua mauti ya ghafla, na kauli yake tukawafufua ni wale waliokuwa wakati wa Musa waliosema: Mpaka tumwone Mungu waziwazi Kwa hiyo, kauli haiwahusu Mayahudi waliokuwa na mtume, msemo umeele-kezwa kwao kwa kuangalia kuwa wanatokana na kizazi kilichosema hivyo.

Tukawatilia kivuli cha mawingu na tukawateremshia Manna na Salwa. Hayo yaliyotokea wakati Waisrail walipotoka Misri wakahangaika katika jangwa la Sinai, kusikokuwa na majengo; wakamlalamikia Musa kwa joto la jua; Mwenyezi Mungu akawaneemesha kwa wingu lililowafunika na kuwakinga na joto la jua kali. Vile vile Mwenyezi Mungu akawaneemesha kwa Manna na Salwa ili wale. Yatakuja maelezo katika tafsiri ya Aya ya 60 kuwa maji yaliwabubujikia kutoka katika jiwe alilolipiga Musa kwa fimbo yake. Inashangaza kuona baadhi ya wafasiri, wakifasiri yale aliyoyanyamazia Mwenyezi Mungu kuyabainisha; kama vile idadi ya waliojiua kwa toba ya kuabudu ndama, kuwa ni watu elfu moja; vile vile walionyakuliwa kuwa ni watu sabini. Ama kuhusu Manna, wanadai kila mtu alikuwa akipata pishi moja na kwamba Salwa ilikuwa ikishuka kutoka mbinguni ikiwa moto moto huku ikifuka moshi, na mengineyo ambayo hayana kauli yoyote iliyopokewa au kudhaniwa.

Imethibiti Hadith kutoka kwa Mtume mtukufu(s.a.w.w) :Hakika Mwenyezi Mungu amenyamazia mambo si kwa kusahau, ni kwa kuwaonea huruma, kwa hiyo msijikalifishe nayo.

Katika Nahjul-Balagha amesema Imam Ali(a.s) :Hakika Mwenyezi Mungu amewafaradhisha faradhi msizipoteze, na amewawekea mipaka msipetuke; na ameyakataza mambo basi msifanye; na ameyanyamazia mambo si kwa kusahau, basi msijikalifishe (nayo).

Na hawakutudhulumu sisi, lakini wamejidhulumu wenyewe .Kukanusha dhulma kwa Mwenyezi Mungu ni sawa na kukanusha kuwa na watoto na mshirika; yaani kumwepusha kabisa na hilo; sawa na kumwambia mseja kuwa hana mtoto. Ama kujidhulumu kwa Mayahudi ni kwa sababu ya usafihi wao na kuzikanusha neema za Mwenyezi Mungu ambaye hanufaiki na twaa ya mwenye kumtii wala hayamdhuru maasi ya mwenye kuasi na madhara ya uasi yanamrudia mwasi. Anasema Ali bin Abu Twalib (a.s.):Ewe mwanadamu ukiona Mola wako anaendelea kukuneemesha nawe unamwasi, basi mhadhari.

Kwa ufupi Aya hizi zinaonyesha ibada ya Waisrail kwa ndama, kutubia kwao kwa kujiua na kutaka kwao kumwona Mwenyezi Mungu. Vile vile kuangamia kwao na kufufuliwa kwao, kufunikwa na kiwingu na kulishwa Manna na Salwa.. Tutaelezea kisa cha Nabii Musa na Waisrail katika surah ya Maida (5) Inshallah. Waliposema kumwambia Musa:

﴿فَاذْهَبْ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَاتِلَا إِنَّا هَاهُنَا قَاعِدُونَ﴾

...Basi nenda wewe na Mola wako mkapigane sisi tutakaa hapa (5:24).

Hilo ni tamko linaloonyesha ukhabithi na uduni wa Mayahudi. Wa kwanza waliogundua uhabithi na uduni wao ni watu wa Firaun ambao waliwachinja watoto wao wa kiume na kuwaacha wa kike. Kumwona Mungu Kutokana na Aya tukufu:Mpaka tumwone Mungu waziwazi.

Tutaonyesha mzozo uliopo katika madhehebu ya Kiislamu na tofauti zao kuwa akili inajuzisha kuonekana Mwenyezi Mungu kwa macho au la?!

Wamesema Ashari (Sunni): Hakika kuonekana Mungu kwa macho kunawezekana kiakili, kwa sababu Yeye yupo na kila kilichopo kinawezekana kuonekana.

Imamiya na Mu’utazila wamesema; Haijuzu kuonekana Mwenyezi Mungu kwa macho katika hali yoyote ile, si duniani wala akhera, kwa sababu Yeye si umbo hata akaonekana, wala haingii katika umbo wala upande fulani.

Baada ya akili kuthibitisha kutoonekana, wamechukulia kwamba ataonekana kiakili sio kwa macho na kwa hakika ya imani sio ya viungo vya mwili, kwa mujibu wa alivyosema mwanafalsafa mkubwa na mashuhuri, Muhammad bin Ibrahim Shirazi, maarufu kwa jina la Mulla Sadra. Katika aliyoyatolea dalili Mulla Sadra kuhusu kutoonekana, ni kauli yake: Kuhisi kitu ni hali inayozuka kwa kile kinachohisi kikikutanishwa na kinachohisiwa kilichozuka. Hivyo basi, kulazimisha kitu ambacho hakikuzuka kuwa kinahisiwa ni kama kulazimisha kitu kisicho na upande kuwa kina upande.

Kauli yake hii - kama ninavyoona - ni kwamba jicho haliwezi kuona kitu isipokuwa kwa sharti mbili:

Liwe linaweza kuona na kiwe kile kinachoangaliwa kinaweza kuonekana kwa jicho. Hilo ni jambo la msingi; likikosa jicho uwezo wa kuona, au kikiwa kitu hakina uwezo wa kuonekana; itakuwa kuona hakuko. Jicho ni dogo na duni zaidi kuweza kuona dhati tukufu; kama vile ambavyo, Mwenyezi Mungu ni mkubwa wa kuonekana na jicho. Nilipokuwa nasoma ibara hii, tukufu akili yangu ilienda kwa mwanafalsafa wa Kiingereza John Luk, anayesema kuwa: kitu kina sifa yake ya kwanza yenye kukithibitikia, ambayo haipambanuki nayo, ni sawa mtu aitambue au asiitambue; kama vile vitu vinavyosimamisha kitu hicho.

Vile vile kuna sifa ya pili ambayo haiwezi kuepukana na kuhisiwa au kujulikana; kama rangi, sauti na ladha. Rangi siyo sifa ya kitu, kama inavyoonekana, isipokuwa ni mawimbi ya kimwangaza yanayohusika kati ya kitu na jicho; kama wasemavyo wataalamu. Vile vile sauti ni mawimbi ya kihewa; na ladha isingekuweko kama si mdomo. Kwa hiyo ladha inahitilafiana kwa uzima wa mdomo na ugonjwa.Kwa ufupi anataka kueleza kuwa hakuna rangi bila ya jicho; wala sauti bila ya sikio; au ladha bila ya mdomo. Hakuna mwenye kutia shaka kwamba nuru ya Mwenyezi Mungu imezidi mawimbi ya kimwanga na mengineyo.Kwa hivyo yakikosekana mawimbi haya, ndio kumekosekana kuona.


8

9

10

11

12

13

14

15