TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA Juzuu 1

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA26%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA Mwandishi:
Kundi: tafsiri ya Qurani

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
Juzuu 9 Juzuu 10 Juzuu 11
  • Anza
  • Iliyopita
  • 20 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 39077 / Pakua: 4816
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA Juzuu 1

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

4

5

6

15

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KWANZA

AL - BAQARAH (NG’OMBE)

﴿ قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ﴾

97.Sema: Anayemfanyia uadui Jibril Hakika yeye ameiteremsha Quran moyoni mwako, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inayosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake, na ni uongozi na bishara kwa waumini.

﴿ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ﴾

98.Anayemfanyia uadui Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Mitume wake na Jibril na Mikail, basi Mwenyezi Mungu ni adui kwa makafiri.

﴿ وَلَقَدْ أَنزَلْنَا إِلَيْكَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ وَمَا يَكْفُرُ بِهَا إِلَّا الْفَاسِقُونَ ﴾

99.Na hakika tumekuteremshia hoja zilizo wazi; na hawazikatai ila mafasiki.

﴿ أَوَكُلَّمَا عَاهَدُوا عَهْدًا نَّبَذَهُ فَرِيقٌ مِّنْهُم بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴾

100.Je, kila mara wanapofunga ahadi, kikundi katika wao huitupa? Bali wengi katika wao hawaamini.

ANAYEMFANYIA UADUI JIBRIL

Aya 97 - 100

LUGHA

Imesemekana kuwa maana ya neno Jibril ni mja wa Mungu (Abdullah) na Mikail ni mja mdogo wa Mwenyezi Mungu (Ubaidullah)

MAANA

Sema: Anayemfanyia uadui Jibril basi yeye ni kafiri, laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake.

Wamekubaliana wafasiri kwamba sababu ya kushuka Aya hii ni Mayahudi walimuuliza Mtume(s.a.w.w) kuhusu Malaika anayemteremshia wahyi. Akawajibu: Ni Jibril. Wakasema Ah! Huyo ni adui yetu, kwa sababu yeye huleta shida na vita na Mikail huleta amani na raha: lau angelikuwa Mikail ndiye anayekuletea wahyi tungelimwamini.

Wameufanya ushindani kwa dhahiri, kwanza kwenye ukabila wa Muhammad(s.a.w.w) kwamba wahyi ushuke kwa mmoja wa Waisrail. Mwenyezi Mungu na Mtume wake alipowashinda kwa hoja, wakabadilisha ushindani kwa Jibril sio Muhammad tena. Hakika ilivyo hasa - kama tulivyoelezea mwanzo - sio sababu ya Uarabu na Uyahudi au Jibril na Muhammad bali ni maslahi yao tu; ni uasherati, ulevi, riba na utapeli. Na wao wanafanya unafiki na kuficha uwongo wao. Kwa hivyo kwa upande wa malumbano na kuwapa hoja, Mwenyezi Mungu alisema:Hakika yeye ameiteremsha Quran moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu inayosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake :

Yaani uadui wenu kwa Jibril hauna msingi, kwa sababu yeye ni mpelekaji wahyi tu, kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenda kwa Muhammad. Na wahyi huo unasadikisha yaliyo katika Tawrat yenu, miongoni mwa sifa za Muhammad na bishara kwa wanaoamini. Kwa hivyo uadui wenu kwa Jibril ni uadui kwa Mwenyezi Mungu, wahyi, Tawrat, uongozi wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe vyake na bishara kwa waumini.

Hakika tumekuteremshia hoja zilizo wazi na hawazikatai ila mafasiki: Yaani yaliyomjia Muhammad(s.a.w.w) hayana shaka baada ya kuwa na hoja na dalili, na wala hayakanushi isipokuwa mwenye kukufuru Mwenyezi Mungu; mwenye kuipinga haki. Makusudio ya ufasiki hapa ni ufasiki wa itikadi yaani ukafiri sio ufasiki wa vitendo ambao unatendwa na mtu anapokuwa na imani.

Je, Kila mara wanapofunga ahadi, kikundi katika wao huitupa? Ahadi walizozitupa Mayahudi na kuzivunja ni nyingi; Kama ya kumwamini Muhammad, ya kuacha kuwasaidia makafiri, ya kuwaamini Mitume na kutowaua na kutomwabudu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, n.k. kwa hiyo wakamkadhibisha Muhammad na wakawasaidia washirikina, walio maadui wao na wa Muhammad. Vile vile huko nyuma waliwakadhibisha Mitume wakawa tayari kumsulubu Masih, na waliabudu ndama na mengine mengi.

Bali wengi katika wao hawaamini. Yaani kuna kundi lililoabudu ndama na lililowaua Mitume, n.k; na wengi wao ingawaje hawakufanya hivyo, lakini bado ni makafiri, waovu. Kwa ufupi ni kwamba: asiyekuwa na haki anaweza kudai haki, na mwenye makosa anaweza kudai kuwa hana makosa. Wanayaweza hayo kwa mbinu za kusema. Lakini mara moja wanafedheheka zinapowashinda hoja na dalili ambazo hawawezi kuzikimbia; kama walivyofedheheka Mayahudi katika uwongo wao na madai yao kuwa wanafanya kama vile alivyoteremsha wahyi Mwenyezi Mungu.

Kuishi kwa amani na kumwamini mwenyezi mungu Wenye kulingania amani wanakusudia kuwa watamaliza tofauti za wanaozozana kwa mikutano. Lakini tumejifunza kuwa mazungumzo ya amani na haja ya kuwa na amani, hayawezi kufaa kitu kwa watu wenye kuangalia manufaa yao. Wenye tamaa hawawezi kuacha tamaa zao isipo-kuwa kwa njia ya vikwazo na vitisho. Maisha ya amani yanahitaji akili iliyofunguka na tabia njema. Ni tabia gani tukufu itakayokuwa mbele za mtu asiyeamini isipokuwa maada, ulanguzi na kutaka utajiri wa haraka haraka? Na ni hoja gani zitakazomkinaisha mwenye tamaa?

Inasemekana kwamba mataifa mawili makubwa ya Mashariki na Magharibi yanadai amani kati yao, lakini wakati huo huo kila mmoja anajitengeneza silaha za hali ya juu na kujikinga kwa kumhofia mwenzake. Kwa hivyo amani wanayodai ni ya maneno na wala si ya vitendo. Maumbile ya kiakili yanathibitisha kwamba kila taifa lina haki kamili katika kujiamulia mambo yake haliwezi kuingiliwa. Sasa je ni nani anayefuata misingi hii? Amani na haki haiwezi kupatikana kwa ukamilifu mpaka pande zote zinazohusika ziamini haki kwa njia ya haki. Ni muhali kuongoka kwenye heri na kutarajia heri yule asiyamini chochote isip-okuwa dhati yake na yule asiyejishug- hulisha na lolote zaidi ya manufaa.

﴿ وَلَمَّا جَاءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ نَبَذَ فَرِيقٌ مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ كِتَابَ اللَّـهِ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ كَأَنَّهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴾

101.Na walipojiwa na Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu mwenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nao, kikundi kimoja miongoni mwa wale waliopewa Kitabu cha Mwenyezi Mungu kilikitupa kitabu cha Mwenyezi Mungu nyuma ya migongo yao kama kwamba hawajui.

WALIPOJIWA NA MTUME

Aya 101

MAELEZO

Na walipojiwa na Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ambaye ni Muhammad(s.a.w.w) ; aliyepelekwa na Mwenyezi Mungu kwa watu wote wakiwemo Mayahudi waliokuwa zama zake.Mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nao . Yaani kusadikisha yaliyo katika Tawrat miongoni mwa misingi ya Tawhid na bishara ya Muhammad.Kikundi kimoja miongoni mwa wale waliopewa Kitabu. Nao ni wanavyuoni wa Kiyahudi.Kilitupa kitabu cha Mwenyezi Mungu nyuma ya migongo yao. Makusudio ya Kitabu, cha Mwenyezi Mungu, ni Quran. Imesemekana pia kuwa ni Tawrat, kwa sababu kumkana kwao Muhammad ni kuikana Tawrat ambayo imetoa bishara ya kuja Muhammad(s.a.w.w) . Hapa wanaingia wote Mayahudi na Manaswara. Kwani wote wamekipotosha Kitabu, hasa sehemu zile zinazofungamana na bishara ya kuja Muhammad(s.a.w.w) ; Bali hakuna tofauti kati ya Mayahudi na wale wanaoondoa maneno ya Mwenyezi Mungu kwa kufuata mapenzi yao.

﴿ وَاتَّبَعُوا مَا تَتْلُو الشَّيَاطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَانَ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ وَمَا هُم بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴾

102.Wakafuata yale yaliyofuatwa na mashetani, katika ufalme wa Suleiman; na Suleiman hakukufuru, bali mashetani ndio waliokufuru, wakiwafundisha watu uchawi na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili, Haruta na Maruta, katika (mji wa) Babilon Wala hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni fitna (mtihani), basi usikufuru. Wakajifunza kwao mambo ambayo kwayo waliweza kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawakuwa wenye kumdhuru yoyote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.Na wanajifunza yatakayowadhuru wala hayawanufaishi. Na kwa hakika wanajua kwamba aliyeyanunua haya hatakuwa na sehemu yoyote katika akhera. Na hakika ni kibaya kabisa walichouzia nafsi zao laiti wangelijua.

WAKAFUATA YALE YALIYOFUATWA NA MASHETANI

Aya 102

MAELEZO

Wafasiri hapa wamerefusha maneno.Wengi wao hawana tegemeo lolote isipokuwa ngano ambazo hazikubaliki kiakili: Razi amechafua karibu kurasa ishirini katika kufasiri Aya hii, akazidisha mikanganyo.Mwenye Majmaul-Bayan naye akafanya hivyo hivyo. Ama Sayyid Qutb yeye ameingilia kuelezea mambo ya kuzugwa watu, ndoto, athari, n.k. Na huku hasa ndiko kukimbia. Kwa hivyo nikabaki muda mrefu nikitafuta na kupekuwa vitabu na tafsir. Hakikutulia kiu changu hata kwenye tafsir ya Sheikh Muhammad Abduh na wanafunzi wake wawili - Al-Maraghi na mwenye Tafsir ya Al Manar, Bora zaidi ya niliyoyasoma katika mlango huu ni yale yaliyotajwa katika kitabu cha Annuwatu fi Haqli I-hayat cha Sayyid Ubaydiy, Mufti wa Musul (Iraq). Na haya ndiyo aliyoyasema ninamnukuu: Niliendelea kutofahamu maana ya Aya tukufu kiasi ambacho hakikunitosheleza kwa mfasiri yoyote, mpaka nilipotua kwenye historia ya Free Mason, ndipo nikajua maana yake.

Kutokana na kugongana wafasiri kiasi ambacho walionyesha kuwa Aya ina vitu viwili vyenye kutofautiana na kuingiza katika Aya hii ngano za watu wa kale ambazo sharia iliyowazi inazikataa, nimeona ni wajibu nikitumikie kitabu cha Mwenyezi Mungu kuthibitisha haya. Ulipotukuka Ufalme wa Suleiman, mfalme wa Babiloni alikuwa na chuki na tamaa katika Palestine na Syria, na akaingiwa na hofu badala ya tamaa yake. Wakafanya msafara watu wawili walio wajanja na werevu wakitafuta mafunzo yatakayowawezesha kuuharibu ufalme wa Suleliman. Wakaingia dini ya Kiyahudi na kuonyesha utawa, kama kawaida wakapata wafuasi, wakawa wanaharibu fikra za watu na kuacha chuki kwa Suleiman mpaka wakamzulia ukafiri. Watu hawa walikuwa kama Malaika kwa wanavy- oonyesha utawa. Lakini walikuwa ni mashetani na mafunzo yao yalikuwa kama uchawi kutokana na ufasaha, na mara kwa mara walikuwa wakitumia neno mfalme kwa mtu mwema, na neno shetani kwa mtu mwovu na neno uchawi kwa ibara ya fitina. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu kumzungumzia Yusuf, alivyozungumziwa:

﴿ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا مَلَكٌ كَرِيمٌ ﴾

...Hakuwa huyu ila ni Malaika mtukufu. (12:31)

Na kauli yake:

﴿ شَيَاطِينَ الْإِنسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا﴾

Mashetani katika watu na majini wakifundishana wao kwa wao maneno ya kupamba kwa udanganyifu. (6:112)

Vile vile kauli yake Mwenyezi Mungu akimzungumzia Walid:

﴿ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ ﴿٢٤﴾ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ ﴾

Hayakuwa haya ila ni uchawi ulionukuliwa, hayakuwa haya ila ni kauli ya binadamu. (74:24-25)

Na kuna Hadith inayosema:Katika ufasaha kuna uchawi.

Tumeelezewa historia ya Nebukadnezzar, mfalme wa Babelon katika vita vya Palestin baada ya Suleiman na alivyoiharibu Baitul Maqdis. Na tunaiona Quran inatilia nguvu matukio ya historia katika Aya isemayo:

﴿ وَقَضَيْنَا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ فِي الْكِتَابِ لَتُفْسِدُنَّ فِي الْأَرْضِ مَرَّتَيْنِ وَلَتَعْلُنَّ عُلُوًّا كَبِيرًا ﴿٤﴾ فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ أُولَاهُمَا بَعَثْنَا عَلَيْكُمْ عِبَادًا لَّنَا أُولِي بَأْسٍ شَدِيدٍ فَجَاسُوا خِلَالَ الدِّيَارِ وَكَانَ وَعْدًا مَّفْعُولًا ﴾

Na tukawafahamisha wana wa Israil katika kitabu: Hakika nyinyi mtafanya uharibifu katika nchi mara mbili na kwa yakini mtatakabari kutakabari kukubwa. Basi ilipofika ahadi ya kwanza yake tukawapelekea watumishi wetu wenye mapigano makali, mno wakaingia majumbani kwa nguvu, na hii ilikuwa ahadi iliyotimizwa. (17:4-5)

Ukiyajua haya, basi tunasema: Dhamiri katika kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.), na wakafuata, inawarudia Mayahudi wa Madina, ambao zimetangulia zaidi ya Aya sitini na mbili katika kuwaeleza wao tu. Utakapoyajua haya, kisha ukazingatia vizuri Aya zinazoambatana na Aya ya Suleiman, na ukafikiria kwa ndani kauli yake Mwenyezi Mungu juu ya ufalme wa Suleiman na madhumuni yake, utajua kwamba maana ya Aya tukufu ni kwamba Mayahudi wa Hijazi walikuwa wak-imfanyia Mtume wa Kiarabu vitimbi na propaganda kwa kufuata nyayo za mab-abu zao ambao waliwasaidia wajumbe wa Babilon katika kuvunja ufalme wa Suleiman.

UFAFANUZI

Tutafasiri Aya kwa misingi ya alivyofahamu Ubaydiy.Wakafuata. Yaani walifuata Mayahudi wa Madina waliokuwa zama za Mtume Muhammad(s.a.w.w) .Yale yaliyofuatwa na mashetani: Makusudio ya mashetani ni wadanganyifu; miongoni mwao ni wale watu wawili wa Babilon ambao walijionyesha kuwa ni watakatifu kumbe ni maibilisi.

Katika ufalme wa Suleiman. Yaani Mayahudi wa Madina walitumia dhidi ya Muhammad, sawa na vile walivyokuwa mababu zao Mayahudi dhidi ya ufalme wa Suleiman.Suleiman hakukufuru, bali mashetani ndio waliokufuru. Yaani kila walilomnasibishia Suleiman alikuwa yuko mbali nalo ulikuwa ni udanganyifu na uzushi wao.Wakiwafundisha watu uchawi: Yaani wanawafundisha watu mambo ya ubatilifu.Na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili . Yaani watu wawili wa Babilon waliodhihirisha utakatifu na ucha Mungu. Mak-usudio sio kuteremshiwa Wahyi wa Mitume, bali ni kiasi cha kupewa ilham na kufundishwa.Wala hawakumfundisha, yoyote mpaka wamwambie: Sisi ni fitna (mtihani) basi usikufuru Walikuwa wakisema hayo kwa unafiki ili wawapumbaze watu kwamba elimu zao ni za kutoka kwa Mungu na kwamba wao ni watakatifu, wasafi wa nia; sawa na anavyosema mlaghai kumwambia yule anayemfundisha kuandika chuki na mapenzi: Tahadhari kuandika hivi usije ukawafarikisha waliooana kisheria, au kumfanya mke wa mtu kumpenda asiyekuwa mumewe.Wakajifunza kwao mambo ambayo kwayo waliweza kumfarikisha mtu na mkewe.

Yaani yale wanayofikiria kuwa yanaweza kutenganisha mtu na mkewe kama wanav-yochukua watu kutoka kwa walaghai, maandishi ya mapenzi na chuki. Kwa ujumla ni kwamba Aya haifahamishi kuthibiti athari ya uchawi wala kukanusha. Kwa sababu kauli yake Mwenyezi Mungu:Wakijifunza kwao ambayo waliweza, sio hukumu ya uhakika ya kutenganisha mtu na mkewe: Sawa na kusema kunywa kiponyesho, yaani kilichowekwa kwa ajili ya uponyeshaji. Kwa ufupi ni kwamba: Aya haithibitishi wala haikanushi. Mara nyingi hekima ya kiungu hupitisha kubainisha kwa upande fulani na kwa ujumla kwa upande mwingine; hasa katika masuala yasiyo ya kiitikadi. Wala hawakuwa wenye kumdhuru yoyote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Yaani hawawezi kumdhuru yoyote vyovyote iwavyo kwa sababu ya kusoma na kuandika; kama akidhurika basi ni kutokana na sadfa tu, kwamba mtu amedhurika na sababu nyingine ya nje ikaonekana ni sababu hii. Makusudio ya idhini ya Mwenyezi Mungu ni sababu ya nje iliyodhuru.Na wanajifunza yatakayo wadhuru wala hayawanufaishi. Ni kiini macho tu, na kiini macho hudhuru wala hakinufaishi. Na kwa hakika wanajua kwamba aliyenunua haya hatakuwa na sehemu yoyote katika akhera.

Wanajua wao kwamba mwenye kupendelea ulaghai hana fungu mbele za Mwenyezi Mungu.Na bila shaka ni kibaya kabisa walichouzia nafsi zao. Yaani wamebadilisha kitu cha thamani kwa kitu duni.Imepita tafsiri yake katika Aya ya 61 ya sura hii.

﴿ وَلَوْ أَنَّهُمْ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَمَثُوبَةٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ خَيْرٌ لَّوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴾

103.Na lau wangeamini na kuogopa, basi thawabu zitokazo kwa Mwenyezi Mungu zingekuwa bora kwao, laiti wangelijua.

LAU WANGEAMINI

Aya 103

MAELEZO

Baada ya Mwenyezi Mungu kuyaorodhesha maasi ya Mayahudi na kampeni zao mbaya dhidi ya Muhammad(s.a.w.w) , amesema kuwa ukafiri wao huu na upinzani wao hautawafaa kitu. Lau wangelimwamini Muhammad, kama ilivyowaamrisha Tawrat yao, wangelistarehe na kupata daraja ya juu kwa Mwenyezi Mungu.

Amirul Mumini anasema:Hakika kumcha Mungu ni ngome yenye nguvu na uovu ni ngome dhalili, haiwakingi watu wake wala haimhifadhi mwenye kuikimbilia. Fahamuni kuwa kumcha Mungu (takuwa) kunavunja uti wa mgongo wa makosa na hupatikana malengo kwa yakini.

UCHAWI NA HUKUMU YAKE

Mafaqihi wa Kishia wamezungumzia sana kuhusu uchawi, na wamerefusha maneno katika kuelezea maana yake, mafungu yake, yanayowezekana na yasiyowezekana. Pia wamezungumzia kuhusu kufundisha, kujifundisha na kuutumia. Uchawi uliozungumziwa na Quran ni namna fulani ya udanganyifu na hadaa, kwa kuufanya uwongo uwe haki. Mwenyezi Mungu anasema:

﴿ فَإِذَا حِبَالُهُمْ وَعِصِيُّهُمْ يُخَيَّلُ إِلَيْهِ مِن سِحْرِهِمْ أَنَّهَا تَسْعَىٰ ﴾

...Tahamaki kamba zao na fimbo zao zikaonekana mbele yake (Musa) zinakwenda mbio kwa uchawi wao. (20:66)

﴿ وَمَا هُم بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ﴾

...Hawakuwa wenye kumdhuru yeyote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (2:102)

Imam Sadiq(a.s) amesema kwamba:uchawi uko namna nyingi; kama vile wepesi na haraka na kufanya hila, kwa sababu wenye hila wamegeuza uzima kuwa ugonjwa na maana kuwa hila.

Ama mambo ya kuandika, kuzungua na kutumia azima au kutabana na mengineyo ambayo yamesemekana kuwa yana athari, kama kufungwa mume wakati wa ndoa kiasi cha kushindwa kumwingilia mke. Vile vile mambo ya kuzidisha mapenzi, kutia chuki kati ya watu wawili na kuwatumia malaika na mashetani katika kupiga ramli na kutopoa, yote hayo, Shahidi wa pili ameyazungumzia katika Masalik mlango wa biashara akisema kuwa: Wanavyuoni wengi wa Kishia wanaitakidi kwamba ni mambo ya kuwazia na dhana zisizokuwa na msingi wowote; na baadhi yao wanaona kuwa ni matukio ya kweli. Na yeye ni miongoni mwa wasemao kuwa ni hakika. Bukhari amepokea katika Sahih yake J-4, mlango wa kisa cha Iblis na Askari wake, kwamba Mtume alirogwa mpaka akawa anaonekana kama anafanya kitu na wala hakifanyi. Lakini hayo ameyakanusha mmoja wa Maimamu wa Kihanafi katika kitabu Ahkamul-Quran J-1; Uk.55 chapa ya mwaka 1347 A.H.

Vile vile Sheikh Muhammad Abduh amekanusha katika kufasiri Sura ya Falaq.Sisi tuko pamoja na wale wanaouona uchawi kuwa hauna msingi wowote. Imam Sadiq anasema: Uchawi ni wenye kushindwa kabisa kugeuza aliyoumba Mwenyezi Mungu... Lau mchawi angelikuwa na uwezo angelijizuwia asizeeke na pia angelijikiinga na maafa na magonjwa pia angelizuwia uzee, na ufukara. Na kwamba uchawi ni fitina inayotenganisha watu wanaopendana na kuleta uadui kwa wanaosikilizana.Vyovyote iwavyo, wameafikiana mafaqihi wa Kishia kwamba adhabu ya mchawi ni kuuliwa akiwa ni Mwislamu. Akiwa si Mwislamu ni kutiwa adabu ya viboko na jela, kama atakavyoona hakimu.

*27 Mwenye kutaka ufafanuzi kuhusu uchawi na hukum yake asome kitabu Al-Jawahir mlango wa Biashara na mlango wa kisasi. Vile vile kwenye kitabu Makasib cha Sheikh Ansari. Mwenye Jawahir anasema : sio kila Jambo geni ni uchawi, kwani elimu nyingi zina athari za ajabu; kama vile wanavyofanya wazungu wakati huu. Hivi sasa ni mwaka 1967; miaka 121 imepita tangu alipokufa mwandishi huyu mkuu. Lau angelikuwako wakati huu asingeliona ajabu. Kwa sababu kila la ajabu hivi sasa litakuwa ni la kawaida wakati ujao.

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقُولُوا رَاعِنَا وَقُولُوا انظُرْنَا وَاسْمَعُوا وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴾

104.Enyi mlioamini msiseme Raaina bali semeni Undhurnaa na sikilizeni; na makafiri wana adhabu iumizayo.

﴿مَّا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلَا الْمُشْرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْكُم مِّنْ خَيْرٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَاللَّـهُ يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ﴾

105.Hawapendi waliokufuru miongoni mwa watu wa kitabu wala washirikina mteremshiwe heri kutoka kwa Mola wenu. Na Mwenyezi Mungu humhusisha kwa rehema zake amtakaye; na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.

ENYI MLIOAMINI

Aya 104 - 105

MAELEZO

Enyi mlioamini msiseme Raaina bali semeni Undhurna Mwenye Majmaul-Bayan anasema: Waislamu walikuwa wakisema Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Raina; Yaani tusikilize. Mayahudi nao wakalitumia neno hili kwa maana ya mpumbavu (katika lugha yao). Walipolaumiwa, wakasema tunasema kama wasemavyo Waislamu. Ndipo Mwenyezi Mungu akawaka-taza hilo kwa kauli yake: Msiseme Raina na semeni: Undhurna. Makusudio ya Undhurna katika Aya ni kuangalia Mtume hali yao wakati anapozungumza; angoje ili wafahamu na waelewe maneno yote.

Uzindushi Mwito wa kwanza katika Sura ya Baqara umekuja kwa watu wote na mwito wenyewe ni Uislamu na kumwabudu Mwenyezi Mungu; pale aliposema Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika Aya ya 21:Enyi watu mwabuduni Mola wenu ambaye amewaumba... Mwito wa pili ulikuwa kwa wana Israil, taifa kubwa ambalo lilileta taifa la Kikristo. Mwito huu wa pili ulikuja kukumbusha kuondolewa mateso kwa waana wa Israil na kupatiwa neema; ni pale aliposema Mwenyezi Mungu katika Aya 40:Enyi wana wa Israil kumbukeni neema yangu niliyowaneemesha.... Mwito wa tatu umekuja kwa umma wa Muhammad(s.a.w.w) katika Aya hii:Enyi mlioamini msiseme Raaina , ambayo ni kuwafundisha Waislamu adabu za sheria baada ya kusilimu na kumwamini Mwenyezi Mungu. Utaratibu huu wa miito hii mitatu ndio utaratibu wa kikawaida; yaani kuanza kuwalingania watu kwenye imani ya Mwenyezi Mungu, kisha kumtajia fadhila za Mwenyezi Mungu yule mwenye kumwamini Mungu kabla ya Utume tena kumfunza kuamini adabu za Mwenyezi Mungu yule mwenye kuamini Utume. Hii ni namna mojawapo ya ufasaha wa Quran.Hawapendi waliokufuru miongoni mwa watu wa kitabu wala washirikina mteremshiwe heri kutoka kwa Mola wenu.

Si ajabu kwa washirikina, Wayahudi na wakristo pamoja na makafiri, kuchukia yote aliyoteremshiwa Muhammad na vile alivyohusishwa na Mwenyezi Mungu kwa fadhila na hidaya na utengeneo; isipokuwa ajabu ni kutolichukia hilo.Na Mwenyezi Mungu humhusisha kwa rehema Zake amtakaye . Amirul Muminin anasema:Makusudio ya rehema hapa ni Utume .

HUSUDA NA HASIDI

Husuda ni tabia za watu wengi, isipokuwa wale waliohifadhiwa na Mwenyezi Mungu, na wala haiko kwa washirikina, Mayahudi au Manaswara peke yao, bali iko pia kwa Waislamu wengi; hata kwa wanavyuoni wakubwa na baadhi ya wale wenye vyeo vya kuwa Marja (Mufti mkubwa) wa kidini ingawaje cheo hicho ndicho pekee kinachokurubiana na cheo cha maasum. Mwenyezi Mungu, Mitume Maimamu na wenye hekima, wamezungumzia sana kuhusu hasadi. Miongoni mwa hayo ni kauli ya Imam Jafar Sadiq: Hasadi asili yake ni upofu wa moyo na kukana fadhila za Mwenyezi Mungu, na hayo yote mawili ni mbawa za kufuru. Lugha fasaha zaidi niliyoiona katika kuisifu hasadi ni kauli ya bwana wa mafasaha na kiongozi wa wenye hekima, Amirul Muminin(a.s) alipowaeleza kuwa ni mahasidi wa raha na wenye kutilia mkazo balaa. Akasema tena: Inatosha kuwa ni shari kwa mahasidi kuhuzunika wakati unapofurahi. Huenda itakuwa ni vizuri kunakili mfano huu kutoka kwa mwanahekima mmoja aliyesema: Mfano wa hasidi ni kama mtu anayetupa jiwe kwa adui yake, kisha jiwe limrudie mwenyewe upande wa kuume na apandwe na hasira. Mara ya pili tena analitupa kwa nguvu kuliko kwanza, na limrudie upande wa kushoto na hapo ataingiwa na chuki na kisha alitupe jiwe kwa nguvu zote na hamasa halafu limrudie kichwani na limjeruhi na huku adui yake yuko salama.

Ni muhali kwa hasidi kuweza kutubu husuda yake, kwa sababu hasidi ni sawa na mwoga na bakhili. Atawezaje bakhili na mwoga kutubu? Ndio maana Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume kuwaambia mahasidi

﴿قُلْ مُوتُوا بِغَيْظِكُمْ﴾

....Sema; kufeni na ghadhabu zenu. (3:119).

﴿مَا نَنسَخْ مِنْ آيَةٍ أَوْ نُنسِهَا نَأْتِ بِخَيْرٍ مِّنْهَا أَوْ مِثْلِهَا أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴾

106.Aya yoyote tunayoifuta au kuisahaulisha tunaleta iliyo bora kuliko hiyo au iliyo mfano wake. Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu?

﴿أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴾

107. Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni mfalme wa mbingu na ardhi? Nanyi hamna mlinzi wala msaidizi asiyekuwa Mwenyezi Mungu.

AYA YOYOTE TUNAYOIFUTA

Aya 106 - 107

KUFUTA

Kwanza tutaeleza maana ya kufuta kwa ujumla katika hukumu za sheria, kisha maana ya kufuta katika Quran.

Maana ya kufuta katika hukumu ya sheria ni kuja dalili inayofahamisha kuthibiti hukumu ya sheria kwa kudumu na kuendelea muda wote; baada ya kutumika hukumu hiyo kwa muda fulani, inakuja dalili nyingine ya kuthibitisha kwamba hukumu ile ilihusika na kipindi fulani tu; na kwamba masilahi yanahukumilia kutumika katika wakati fulani tu, sio kila wakati. Lakini hekima ya Mwenyezi Mungu ilidhihirisha kudumu na kuendelea. Sawa na Daktari ambaye anaona masilahi ya mgonjwa ni kutokula nyama kwa muda wa wiki moja tu, lakini akaona ni vizuri amfiche ule muda wa kumka-taza.Baada ya kupita wiki moja akamruhusu kula nyama. Kwa hivyo kufuta kunakuwa kwa maana ya kufuta yale yaliyoonekana kuwa ni ya kudumu na wala sio kuwa ni kwa sababu ya kutojua au kubadili mawazo.

Hakuna mwenye kutia shaka kwamba kufuta kwa maana haya kumethibiti katika sheria ya Kiislamu; kwani sheria imefuta baadhi ya hukumu zake zilizotangulia; kama vile sharia za Musa na Isa. Bali hukumu za Quran zenyewe zinafutana; kama vile kugeuza Qibla kuwa Al-Kaaba (huko Makka) baada ya kuwa Baytul-Maqdis (huko Jerusalem).

Ama kufuta katika Quran kunawezekana kukugawanywa katika njia tatu: 1. Kufuta Aya kisomo na hukumu, yaani kuondolewa tamko lake na hukumu yake.

2. Kufutwa kisomo tu; kufutwa tamko na kubaki hukumu.

3. Kufutwa hukumu tu, si kusomwa, yaani inasomwa lakini haichukuliwi dhahiri yake baada ya kutumiwa wakati fulani. Lakini fungu la kwanza na la pili hayapo, kwa sababu yataleta upungufu na mageuzi katika Quran ambayo haifikiwi na batili mbele yake wala nyuma yake.

Ama fungu la tatu linawezekana na limethibiti; ndilo walilolikubali Waislamu wote na wafasiri wote, na limetungiwa vitabu mahsusi. Hivi sasa kimetolewa kitabu kikubwa kwa jina Annasikh wal-mansukh (Inavyofuta na inayofutwa) cha Dkt. Mustafa Zaydi wa Misri. Kwa ujumla inaonyesha kuwa hukumu ya sharia ikithibiti kwa njia sahihi haiwezekani kufutwa isipokuwa kwa Aya ya Quran au kwa Hadith mutawatir. Kwa sababu kufuta ni jambo kubwa na la muhimu. Kwa hivyo kufuta hakuwezi kuthibiti kwa habari moja. Kwa sababu kila umuhimu hauna budi kuenea na kutangaa midomoni. Mtu mmoja tu akinakili tukio kubwa au watu wengi, lakini bila ya kuenea, itakuwa ni uwongo. Kwani huoni kifo cha mtu mashuhuri kinanukuliwa na watu wengi! Vile vile mapinduzi! Lakini kifo cha mtu wa kawaida hunukuliwa na baadhi ya majirani na ndugu tu! Ufafanuzi zaidi uko katika Usulul-fiqh (elimu ya misingi ya Fiqh)

MAANA

Aya yoyote tunayoifuta au kuisahauliza, tunaleta iliyo bora kuliko hiyo au iliyo mfano wake.Wafasiri wengi wanasema kwamba Mayahudi walikuwa wakisema kuwa: Muhammad anawaamrisha masahaba zake jambo kisha anawakataza, leo anasema hili kesho anasema lile, lau anayoyasema kama yangelikuwa ni wahyi, kusingelitokea mgongano huu. Ndipo ikashuka Aya hii, kuwajibu.Makusudio ya Aya, ni Aya za Quran tukufu, kwani maana haya ndiyo yanayokuja haraka kwenye fahamu. Amenakili Sheikh Maraghi katika tafsir yake kutoka kwa mwalimu wake, Sheikh Muhammad Abduh, kwam- ba makusudio ya Aya ni muujiza unaofahamisha utume wa Mtume; kwamba Mwenyezi Mungu anampa Mtume muujiza wa Mtume mwingine, kisha anauacha na kuumpa Mtume mwingine muujiza mwingine. Maana haya yenyewe yako sawa, lakini mpangilio wa Aya unayakataa. Maana yanayoelezwa na wanavyuoni na kundi kubwa la wafasiri ni Aya za Quran.

Maana ya kufuta Aya ya Quran ni kubakia tamko na kisomo pamoja na kuacha hukumu iliyofahamishwa na Aya hiyo ambayo iliwahi kutumika wakati fulani. Ama maana ya neno Nunsiha likisomwa bila ya harufi Hamza litakuwa lina maana ya kusahau; yaaani kuacha sio kwa kughafilika nayo yani twaiacha kama ilivyo bila ya mabadiliko. Kwani yafaa kusema kitu hiki nimekisahau kwa maana ya kukiacha kama kilivyo. Na likisomwa kwa Hamza, litakuwa na maana ya kuchelewesha na kuahirisha yaani tunaacha kuiteremsha mpaka wakati mwingine.

Vyovyote iwavyo kupatikana herufi Ma ya sharti haifahamishi kutokea kufutwa hasa,bali inafahamisha kuwa lau inatokea, basi Mwenyezi Mungu angelileta bora kuliko ile iliyofutwa. Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu, hujui kwamba Mungu ni wake ufalme wa mbingu na ardhi? Inasemekana kwamba msemo hujui unaelekezwa kwa Mtume na makusudio yake ni Waislamu ambao walidhikika kutokana na upinzani wa Mayahudi na wengineo kuhusu kufutwa. Ilivyo hasa ni kwamba msemo unaelekezwa kwa kila anayeona ajabu kufutwa au yule anayeumizwa na upinzani. Maana yake ni kuwa kufutwa sio jambo geni.

Kimsingi ni kwamba Mwenyezi Mungu anamiliki kila kitu na anapanga na kupitisha anavyotaka, iwe ni kufuta au kubakisha bila ya kufutwa. Ama kuhusisha kutaja mbingu na ardhi kunafahamisha kukusanya vitu vyote. Kwa sababu mbingu na ardhi zinakusanya viumbe vyote vya juu na vya chini.Nanyi hamna mlinzi wala msaidizi asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Yaani msijali enyi waumini kwa anayepinga suala la kufutwa au kitu chochote katika dini yenu; kiumbe hawezi kuwadhuru maadamu Mwenyezi Mungu ndiye anayetia nguvu na ndiye msaidizi.

Kwa ufupi ni kwamba kufuta ni haki, hakuna kizuwizi cha kutoka akilini au kwenye sharia, kinyume na wanavyofikiri wakanushaji na wapinzani! Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza Sura Al-Baqara 187

6

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA PILI

﴿الشَّهْرُ الْحَرَامُ بِالشَّهْرِ الْحَرَامِ وَالْحُرُمَاتُ قِصَاصٌ فَمَنِ اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ فَاعْتَدُوا عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ ﴾

194.Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu; na vitu vitakatifu vina kisasi. Basi wanaowachokoza, pia nanyi wachokozeni kwa kadiri walivyowachokoza. Na mcheni Mwenyezi Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaomcha.

﴿وَأَنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ وَأَحْسِنُوا إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ﴾

195.Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamivu, na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.

MIEZI MITAKATIFU

Aya 194 - 195

MAANA

Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu.

Miezi mitakatifu ni minne; mitatu inafuatana, nayo ni Dhul-Qaada, Dhul Hijja na Muharram (mfunguo pili, mfunguo tatu na mfunguo nne). Na mwezi mmoja uko pekee na ni (Rajab). Miezi hii imeitwa mitakatifu kwa sababu ya kuharamishwa kuuana ndani ya miezi hiyo. Katika wakati wa ujahiliya na wa Uislamu, ilikuwa mtu anaweza kukutana na mtu aliyemuua baba yake katika miezi hiyo na asimfanye chochote. Yameshatangulia maelezo kwamba Mtume na sahaba zake walitaka kufanya umra katika mwezi wa dhul-Qaada (mfunguo pili) mwaka wa sita (6 Hijriya), wakazuiwa na washirikina na wakatupiwa mishale na mawe; kisha waka-fanyiana suluhu kuwa Waislamu warudi mwaka utakaofutia. Lakini Waislamu wakaogopa washirikina wasije wakaanza kupigana katika mwezi mtakatifu; ndipo Mwenyezi Mungu akawapa idhini ya kupigana na washirikina na akabainisha kuwa lenye kukatazwa ni kuanza uadui wa kupigana na sio kujikinga. Kwa hivyo maana ya mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu ni kwamba mwenye kuihalalisha damu yenu enyi Waislamu katika mwezi huu, basi nanyi ihalalisheni damu yake katika mwezi huo huo.

Na vitu vitakatifu vina kisasi. Yaani mwenye kuvunja heshima ya Mwenyezi Mungu atalipizwa kisasi na atafanywa kama alivyofanya. Hiyo ndiyo asili kwa ujumla inayoondoa kila udhuru wa mwenye kuvunja heshima. Mwenye kuhalalilisha damu za watu, mali zao na heshima zao, naye atahalalishwa kwa kiasi kile alichowafanyia. Heshima kwa mtu mwingine inatokana na heshima ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kama akivunja heshima ya mwingine. Hapo itakuja haki ambayo daima inakuwa juu na wala haikaliwi. Hapa ndipo tunapata tafsiri ya:

Anayechokoza pia nanyi mchokozeni kwa kadiri alivyo wachokoza. Sharti la kulipiza ni kuwa sawa na kosa la aliyeanza bila ya kuzidisha au kupunguza. Hicho ndio kisasi hasa kilivyo. Unaweza kuuliza: Mwenye kuchokoza , yeye ni mchokozi bila ya wasiwasi wowote, lakini mwenye kulipiza kisasi bila shaka siye mchokozi. Kwa hiyo kuna wajihi gani kwa Mwenyezi Mungu kusema:Mchokozeni

Jibu : Makusudio ya kuwafanyia uchokozi, sio uchokozi hasa kwa maana yake, isipokuwa makusudio ni malipo ya uchokozi uliofanywa kwa kipimo chake bila ya kudhulumu. Hayo ni mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu(s.w.t.):

"Na malipo ya ubaya ni ubaya ulio sawa na (ubaya) huo..." (42:40)

KUTOA KATIKA NJIA YA MWENYEZI MUNGU

Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kutoa katika njia yake Mwenyezi Mungu kunakuwa ni kwa masilahi ya umma; kama vile shule, hospitali na nyumba za kulea mayatima. Vile vile jihadi, sadaka kwa mafukara na masikini na kuwalisha watu wa nyumbani. Bora zaidi ya kutoa ni kule kunakohusika na kutia nguvu na kuieneza dini, kuthibitisha haki na kuibatilisha batili.

Wala msijitie, kwa mikono yenu, katika maangamivu

Mwenyezi Mungu ametumia neno mikono kwa maana ya mtu kujiingiza mwenyewe. Kama tukiangalia jumla hii peke yake tu bila ya kuangalia mfumo mzima wa maneno, ingelikuwa maana yake ni kuwa haijuzu kwa mtu kufanya lolote ambalo lina madhara na bila ya kuwako manufaa kwa ujumla. Lakini tukichunga mfumo wa maneno na kuja kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):"wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamivu" baada ya kusema:"Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu", basi maana yanakuwa, toeni katika mali zenu sio kwa ubahili wala ubadhirifu, kwa sababu yote hayo mawili yanaleta uangamivu. Kwa hivyo Aya kwa maana haya inakuwa kama ile Aya isemayo:

﴿ وَالَّذِينَ إِذَا أَنفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَٰلِكَ قَوَامًا ﴾

"Na wale ambao wanapotoa hawafanyi ubadhirifu wala ubahili, bali wanakuwa katikati ya hayo."( 25:67)

Inasemekana pia kwamba maana yake ni: Msijitie kwa mikono yenu kwenye maangamivu kwa kuacha kupigana jihadi na maadui wa dini na kutoa mali kwa ajili ya kuwaandaa wapigania jihadi, kwa sababu hilo litawaogopesha na atawaweza adui; muangamie na mdhalilike. Haya ndiyo yaliyothibitishwa na majaribio waliyoyapitia Waislamu. Wamekosa uhuru wao na heshima yao tangu walipoacha jihadi na kutoa mali kwa ajili ya kuinusuru haki na uadilifu. Hivyo akapata tamaa kila mnyang'anyaji na mnyakuzi; hata Wazayuni, vibaraka wa ukoloni, nao waliivamia Palestina mnamo 1948. Baada ya Waarabu kunyamaza na wasifanye jihadi. Baada ya miaka ishirini wakateka Sinai na ukanda wa Gaza Magharibi mwa mto Jordan; wakazikalia sehemu hizo kwa msaada wa Amerika, Uingereza na Ujerumani Magharibi. Wakawaua wanaume na kuwafukuza wanawake na watoto. Lau Waislamu wangefanya jihadi kabla yake, wangeliokoka na maangamizo haya na udhalili huu, na wala dola ya Israel isingekuwepo kabisa.Na fanyeni wema Kwa jihadi na kujitolea mali katika njia ya Mwenyezi Mungu na katika kila njia inayomridhisha Mungu na yenye sifa nzuri.

﴿ وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّـهِ فَإِنْ أُحْصِرْتُمْ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ وَلَا تَحْلِقُوا رُءُوسَكُمْ حَتَّىٰ يَبْلُغَ الْهَدْيُ مَحِلَّهُ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ بِهِ أَذًى مِّن رَّأْسِهِ فَفِدْيَةٌ مِّن صِيَامٍ أَوْ صَدَقَةٍ أَوْ نُسُكٍ فَإِذَا أَمِنتُمْ فَمَن تَمَتَّعَ بِالْعُمْرَةِ إِلَى الْحَجِّ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ فِي الْحَجِّ وَسَبْعَةٍ إِذَا رَجَعْتُمْ تِلْكَ عَشَرَةٌ كَامِلَةٌ ذَٰلِكَ لِمَن لَّمْ يَكُنْ أَهْلُهُ حَاضِرِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴾

196.Na timizeni Hijja na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na kama mkizuiliwa, basi (chinjeni) wanyama walio wepesi kupatikana. Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjioni mwao. Na ataka-yekuwa mgonjwa katika nyinyi au ana adha kichwani mwake, basi atoe fidia kwa kufunga au sadaka au kuchinja mnyama. Na mtakapokuwa salama, basi mwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra, kisha akahiji, achinje mnyama aliye mwepesi kumpata. Na asiyepata, ni kufunga siku tatu katika Hijja na siku saba mtakaporudi; hizo ni siku kumi kamili. Hayo ni kwa yule ambaye watu wake hawako karibu na Msikiti Mtakatifu. Na mcheni Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.

﴿ الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ وَاتَّقُونِ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ﴾

197.Hijja ni miezi maalumu. Na anayejilazimisha kufanya Hijja katika miezi hiyo, basi hakuna kuchafua wala ufuska wala mabishano katika Hijja. Na heri yoyote mnayoifanya Mwenyezi Mungu anaijua. Na chukueni masurufu, na hakika masurufu bora ni takua; na nicheni Mimi, enyi wenye akili.

﴿ لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَبْتَغُوا فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ فَإِذَا أَفَضْتُم مِّنْ عَرَفَاتٍ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ عِندَ الْمَشْعَرِ الْحَرَامِ وَاذْكُرُوهُ كَمَا هَدَاكُمْ وَإِن كُنتُم مِّن قَبْلِهِ لَمِنَ الضَّالِّينَ ﴾

198.Si vibaya kwenu kutafuta riziki ya Mola wenu. Na mtakapomiminika kutoka Arafa, mtajeni Mwenyezi Mungu katika Mash'aril- Haram: Na mkumbukeni kama alivyowaongoza, ijapokuwa zamani mlikuwa miongoni mwa waliopotea.

﴿ ثُمَّ أَفِيضُوا مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴾

199.Kisha miminikeni kutoka mahali wanapomiminika watu (wote), na mumwombe Mwenyezi Mungu maghufira; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kughufiria Mwenye kurehemu.

﴿ فَإِذَا قَضَيْتُم مَّنَاسِكَكُمْ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَذِكْرِكُمْ آبَاءَكُمْ أَوْ أَشَدَّ ذِكْرًا فَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ﴾

200.Na mmalizapo kuzitimiza ibada zenu, basi mtajeni Mwenyezi Mungu kama mlivyokuwa mkiwataja baba zenu; bali mtajeni zaidi. Na kuna baadhi ya watu wasemao: Mola wetu! Tupe duniani; nao katika Akhera, hawana lolote.

﴿ وَمِنْهُم مَّن يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴾

201.Na miongoni mwao kuna asemaye; Mola wetu! Tupe mema duniani na (tupe) mema Akhera, na utulinde na adhabu ya Moto.

﴿ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ نَصِيبٌ مِّمَّا كَسَبُوا وَاللَّـهُ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴾

202.Hao ndio wenye fungu katika waliyoyachuma, na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.

﴿ وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ فَمَن تَعَجَّلَ فِي يَوْمَيْنِ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ لِمَنِ اتَّقَىٰ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ﴾

203.Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika siku zinazohisabiwa. Na mwenye kufanya haraka katika siku mbili, basi si dhambi juu yake; na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake, kwa mwenye takua. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba nyinyi mtakusanywa Kwake.

TIMIZENI HIJJA NA UMRA

Aya 196 - 203

MAANA

Aya hizi zimeonyesha baadhi ya hukumu za Hijja, Mafaqihi wameweka vitabu maalumu vinavyohusu Hijja, nami nimetunga kitabu kwa jina Al- Hajj ala Madhahabil-Khamsa; kisha nikakiunganisha katika kitabu Al- Fiqh ala Madhahabil Khamsa wakati kiliporudiwa kuchapishwa kwa mara ya tatu. Vile vile nimeizungumza kwa urefu katika Juzuu ya pili ya kitabu Fiqh ul-Imam Jaffar Sadiq(a.s) Hijja imekuwa maarufu tangu zama za Nabii Ibrahim na Ismail(a.s) na iliendelea katika zama za ujahiliya; na Uislamu ukaithibitisha baada ya kuisafisha na mambo machafu, na kuongeza baadhi ya ibada.

Na timizeni Hijja na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Maana ya Hijja kilugha, ni kukusudia, na kisharia ni ibada maalum katika mahali na wakati maalum. Umra kilugha ni ziara yoyote; na kisheria ni ziara katika Al-Kaaba kwa namna maalum, Hijja ni wajibu katika Quran, Hadith na Ijami. Bali wajibu wake umethubutu kwa dhahiri ya dini. Na mwenye kuikanusha sio Mwislamu, sawa sawa na aliyekanusha wajibu wa Saumu na Swala. Shia Imamiyya na Shafii wamesema Umra ni wajibu, Hanafi na Malik wamesema ni Sunna. Kusema kwake Mwenyezi Mungu Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Yaani Hijini na fanyeni Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake na sio kwa makusudio ya kidunia. Kwani Waarabu walikuwa wakikusudia kuhiji kwa ajili ya kukutana, kujifaharisha, kutafuta mahitaji na kuhudhuria soko. Ndipo Mwenyezi Mungu akaamrisha Hijja iwe ni kwa makusudio yake Yeye kwa ibada safi yenye kutakasika na makusudio yoyote mengine.

Na kama mkizuiliwa, basi (chinjeni) wanyama walio wepesi kupatikana.

Yaani ikiwa mmeherimia Hijja, kisha mkazuilika kukamilisha ibada kwa njia yake ya kisheria kutokana na maradhi au adui na mengineyo, basi ni juu yenu kuchinja mnyama atakayepatikana kwa urahisi; kwa uchache awe ni mbuzi, wastani ni ng’ombe na wa juu zaidi ni ngamia.

Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjioni mwao.

Msemo unaelekezwa kwa wale waliozuilika ambao hawakuweza kutimiza Hijja au Umra. Wao hawatakuwa wametoka katika ihram yao (miko ya Hijja) mpaka wajue kwamba mnyama amefika mahali pake pa kuchinjwa. Na mahali pa kuchinja ni Mina ikiwa ni Hijja; na kama ni Umra basi ni Makka. Hayo ni itakapokuwa kizuizi ni maradhi. Ama ikiwa kizuizi ni adui, basi mahali pa kuchinja ni pale mahali palipotokea kizuizi. Kwa sababu Mtume(s.a.w.w) alichinja mnyama katika Hudaybiya, alipozuiliwa na washirikina kuzuru nyumba ya Mwenyezi Mungu tukufu (Al Kaaba).

Na atakayekuwa mgonjwa katika nyinyi au ana adha kichwani mwake, basi atoe fidia kwa kufunga au sadaka au kuchinja mnyama.

Yaani ikiwa mwenye kuhirimia atanyoa kichwa chake kwa dharura, basi ni juu yake kutoa kafara, atakuwa na hiyari baina ya kufunga siku tatu, kuwalisha masikini sitini au kuchinja mnyama; kwa uchache awe ni mbuzi.

Na mtakapokuwa salama, basi mwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha akahiji, achinje mnyama aliyemwepesi kupatikana.

Yaani mtu asiyekuwa na kizuizi, akafanya Umra kisha akahiji baadae katika mwaka huo huo, basi ni juu yake kuchinja mnyama. Hii ndiyo aina ya Hijja inayojulikana kwa jina la Haj Tamattui (Hijja ya starehe) ambayo ni wajibu kwa wasiokuwa watu wa Makka.

Imeitwa Hijja ya starehe, kwa sababu mwenye kuhiji baada ya kumaliza amali za Umra anatoka kwenye miko ya Umra mpaka aje ahirimie Hijja.

Na asiyepata, ni kufunga siku tatu katika Hijja na siku saba mtakaporudi; hizo ni siku kumi kamili.

Imam Jaffar Sadiq(a.s) amesema;Mwenye kufanya Hajj Tamattu, asipopata mnyama atafunga siku tatu katika Hijja; siku ya saba, ya nane na ya tisa katika Dhul-Hijja (mfungu tatu) wala hakuna sharti la Iqama na siku saba atafunga atakaporudi kwa watu wake. Hizo ni siku kumi kamili za kutosheleza mnyama.

Hayo ni kwa yule ambaye watu wake hawako karibu na msikiti mtakatifu.

Mwenye Majmaul Bayan amesema kuwa hayo yaliyotangulia kutajwa katika Tamattui ya Umra kisha Hijja, sio kwa watu wa Makka na walio karibu yake. Isipokuwa ni kwa ambaye hayuko Makka, yule ambaye yuko mbali na Makka kwa zaidi ya maili kumi na mbili (12) kwa kila upande. Mafaqihi wa Kishia Imamiya wamesema Hajj Tamattui ni wajibu kwa walio mbali na Makka, wala haijuzu kwa aliyembali na Makka kuhiji Hijja Qiran na Ifrad, kwani hizo ni wajibu kwa watu wa Makka na wa kando kando yake; na wao haijuzu kwao kuhiji Hajj Tamattui. Kwa ufafanuzi zaidi angalia vitabu vya Fiqh.

Hijja ni miezi maalumu.

Nayo ni kuanzia Shawwal, Dhul-qaad na kumi la mwanzo la Dhul-Hijja. (mfunguo mosi, mfunguo pili na mfunguo tatu) Mwenye kuhirimia kabla yake Hijja yake haitaswihi na mwenye kuhirimia ndani ya miezi hiyo itaswihi na ataleta amali zilizobakia.

Na anayejilazimisha Hija katika miezi hiyo, basi hakuna kuchafua wala ufuska wala mabishano katika Hijja.

Makusudio ya uchafuzi hapa ni kujamii. Mtu akimjamii mkewe na huku amehirimia Hijja, basi Hijja yake imeharibika, sawa sawa na aliyejamii au kula huku akiwa amefunga. Kwa hiyo atakamilisha Hijja yake, kisha aje alipe mwaka ujao; kama ilivyo kwa mwenye kuiharibu Saumu. Makusudio ya ufuska, ni uongo na kutukana. Ama kuhusu kubishana riwaya za Ahlul Bait zinasema, hilo ni kusema mtu; Hapana wallahi au Kwa nini, wallahi n.k.

Si vibaya kwenu kutafuta riziki ya Mola wenu.

Kwa vile wakati wa ujahilia watu walikuwa wakifanya biashara na kuchuma siku za Hijja, kukadhaniwa kuwa ni haramu, ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t.), akaondoa tuhuma hii na akabainisha kwamba kuchuma hakupingani na ikhlasi katika amali za Hijja.

Na mtakapomiminika kutoka Arafa, mtajeni Mwenyezi Mungu katika Masharil Haram.

Arafa ni mahali maalum. Kumiminika kutoka Arafa ni kuondoka, Masharil-Haram ndipo pale panajulikana kama Muzdalifa na kutua hapo ni wajibu; kama ilivyo kwa Arafa.

Kisha miminikeni kutoka mahali wamiminikapo watu (wote). Inasemekana kuwa Maquraish walikuwa hawatui Arafa pamoja na watu wengine kwa kiburi tu, ndipo Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake kutua hapo na kutoka pamoja na watu ili abatilishe waliyokuwa wakiyafanya Maquraish.

Na mmalizapo kuzitimiza ibada zenu, basi mtajeni Mwenyezi Mungu zaidi.

Imepokuwa kutoka kwa Imam Baqir baba wa Imam Sadiq(a.s) kwamba watu walikuwa wanapomaliza Hijja wanakusanyika huko na kuwataja wazazi wao kwa fahari, ndipo Mwenyezi Mungu akawaamrisha kuliacha hilo na badala yake wamtaje Mwenyezi Mungu na jinsi alivyowaneemesha. Kwa sababu Yeye ndiye mwenye kuwaneemesha wao na mababa zao.

Na baadhi ya watu kuna asemaye: Mola wetu! Tupe duniani; nao katika akhera hawana lolote. Na miongoni mwao kuna asemaye: Mola wetu! Tupe mema duniani na (tupe) mema akhera, na utulinde na adhabu ya moto. Hao ndio wenye fungu katika waliyoyachuma, na Mwenyezi Mungu ni mwepesi wa kuhisabu.

Watu katika Hijja zao wako aina mbili. Aina ya kwanza ni yule asiyetaka lolote isipokuwa starehe ya dunia na hana makusudio yoyote isipokuwa dunia tu, na anapomwabudu Mwenyezi Mungu humwabudu kwa ajili ya dunia. Hawa ndio wenye kunyimwa neema ya Akhera. Ama aina ya pili ni yule anayetaka heri ya dunia na akhera na anafanya amali kwa ajili ya dunia yake na akhera yake. Huyu ndiye mwenye radhi mbele ya Mwenyezi Mungu kesho kwa kulipwa amali yake njema. Mwenye Tafsiri Rawhul Bayan amenukuu kutoka kwa Imam Ali bin Abi Twalib(a.s) kwamba wema katika dunia ni mwanamke mwema na katika akhera ni Hurulain. Ama adhabu ya moto makusudio yake ni mwanamke muovu.

Iwe ni sahih Hadith hiyo au la, lakini mimi najua kuna watu wanaohisi kwamba lau wao wangekuwa katika Jahanam kisha wakahiyarishwa kutoka katika Jahanam na warudi kwa wake zao waliokuwa nao duniani au wabaki Jahannam, basi wangelichagua kubaki katika Jahannam kuliko kuishi tena na wake zao hao.

Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika siku zinazohisabiwa.

Makusudio yake ni siku tatu za Tashriq nazo ni; Tarehe kumi na moja, kumi na mbili na kumi na tatu katika mwezi wa Dhul-Hijja (mfungo tatu). Si wajibu kwa mwenye kuhiji kulala Mina usiku wa kumi na tatu, lakini kwa sharti ya kuwa atoke Mina siku ya kumi na mbili baada ya kupinduka jua na kabla ya Maghrib na awe hakuvunja mwiko wa kuwinda au kujamii. Kwa hali hiyo ndipo tunapopata tafsiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

Na mwenye kufanya haraka katika siku mbili, basi si dhambi juu yake; na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake kwa mwenye takua.

Yaani mwenye kuacha kuwinda na wanawake katika ihram yake. Ikiwa amevunja mwiko wa kulala na mke au kuwinda au alichelewa na jua siku ya kumi na mbili akiwa yuko Mina, basi itakuwa wajibu kwake kulala usiku wa kumi na tatu na kutupia mawe vikuta vitatu (shetani).

7

﴿ وَمِنَ النَّاسِ مَن يُعْجِبُكَ قَوْلُهُ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيُشْهِدُ اللَّـهَ عَلَىٰ مَا فِي قَلْبِهِ وَهُوَ أَلَدُّ الْخِصَامِ ﴾

204.Na katika watu kuna ambaye kauli yake inakupendeza katika maisha ya duniani, naye humshuhudiza Mwenyezi Mungu kwa yaliyo moyoni mwake na hali ni hasimu mkubwa kabisa.

﴿ وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِي الْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ﴾

205.Na anapotawala hufanya bidii katika ardhi kufanya ufisadi, na huangamiza mimea na viumbe, na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.

﴿ وَإِذَا قِيلَ لَهُ اتَّقِ اللَّـهَ أَخَذَتْهُ الْعِزَّةُ بِالْإِثْمِ فَحَسْبُهُ جَهَنَّمُ وَلَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴾

206.Na anapoambiwa. Mche Mwenyezi Mungu, hupandwa na mori wa kufanya dhambi. Basi Jahannam inamtosha, napo ni makao mabaya mno

﴿ وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْرِي نَفْسَهُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ وَاللَّـهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ ﴾

207.Na katika watu yuko auzaye nafsi yake kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni mpole kwa waja.

KAULI ZAO ZINAKUPENDEZA

Aya 204 – 207

MAANA

Baadhi ya wafasiri wapya wamejaza kurasa kwa maneno matamu katika kufasiri Aya hizi, lakini hawakuzidisha chochote zaidi ya kuwagawanya watu kwenye wema na uovu. Kwa dhahiri haya yanajulikana na wote, hayahitaji ubainifu wowote, sikwambii tafsiri ndefu tena. Unaweza kuuliza; Ikiwa kugawanyika watu kunajulikana na wote, basi kubainisha kunakuwa ni maelezo ambayo tayari yameshaelezwa na kufafanua lililofafanuliwa na yapasa kuyachukulia maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) vizuri? Jibu: Inawezekana kuwa makusudio ni kuongoza na kuelekeza kwamba mwenye akili anatakikana kutohadaliwa kwa mambo ya nje wala asimwamini mwenye kutegeneza maneno matamu. Kwa sababu wafisadi ni mabingwa wa kazi hiyo na kazi ya ria. Kwa hivyo ni juu yetu kutomtegemea yeyote isipokuwa baada ya kufanya majaribio na kupatikana dalili ya ukweli wake na usafi wake.

Hiyo ndiyo asili ya ujumla inayoenea katika hukumu nyingi za dini na za kidunia; kama kuchagua Hakimu, Kadhi, Naibu, Kadhi, Mufti na kila anayesimamia masilahi ya Umma. Ajabu ya maajabu ni kutakiwa shahada ya kielimu tu kwa mwenye kujitokeza kwa kazi muhimu ya mji au nchi na inayogusa maisha ya watu. Lakini haulizwi uaminifu wake na tabia yake, pamoja na kuwa hayo ndio msingi. Wengi wenye shahada wanazitumia kuwa ni zana za kuibia.

Na katika watu kuna ambaye kauli yake inakupendeza hapa duniani, naye humshuhudia Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali ni hasimu mkubwa kabisa.

Yaani wanadhihihirisha mapenzi na heri na hali wao ndio maadui zaidi wa heri na watu wa heri.

Na anapotawala hufanya bidii katika ardhi kufanya ufisadi.

Wamehitaliafiana wafasiri kuhusu neno Tawalla. Je makusudio ni kuondoka na maana yake kuwa ni, anapoondoka kwa yule aliyemdanganya, huhangaika katika ardhi kwa ufisadi. Au kwamba makusudio ni kutawala na usultani, na maana yawe, na atakapokuwa mtawala atafanya wanayoyafanya watawala waovu ya kuangamiza mimea na viumbe? Mwenye Tafsir Al manar amenakili kutoka kwa Ustadha wake Sheikh Muhammad Abduh kwamba ameyapa nguvu maana ya utawala kwa kuunganisha na kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

"Na anapoambiwa mche Mwenyezi Mungu, hupandwa na mori wa kufanya dhambi."

Kwa maana ya kuwa mtawala mkaidi anakuwa na kiburi kuongozwa kwenye maslahi au kupewa tahadhari ya mambo ya ufisadi, yeye hujiona yuko juu ya haki; kama vile alivyo juu ya watu wake anaowatawala, basi itawezekanaje kwa mtu kumwambia amwogope Mwenyezi Mungu.

Na huangamiza mimea na viumbe.

Mimea ni kilimo na viumbe ni wanyama. Makusudio ni maslahi yote ya kiuchumi katika kilimo, viwanda na ufugaji, mali ghafi, na mengineyo yanayohusika na uhai wa watu na maisha yao. Mwenyezi Mungu amehusisha kutaja kilimo na ufugaji kwa vile viwanda wakati huo havikuwa na umuhimu wowote kama ilivyo sasa. Uharamu wa mambo hayo kwa mtazamo wa Uislamu ni sawa na uharamu wa kumwaga damu; na mwenye kukusudia ubaya katika vitu hivyo, ndio amekusudia ubaya wa utu hasa; hata kama vitu hivyo ni milki ya adui anayepiga vita Waislamu. Mtume(s.a.w.w) amekataza kukata miti, kuharibu mimea na majengo na kutia sumu miji ya washirikina siku za vita, n.k. Lau tunailinganisha sharia ya Kiislamu na mambo yanayofanywa leo na dola za kikoloni na vita vyao vya silaha za kemikali kwenye mimea, watu na wanyama, na kuitia sumu anga kwa mabomu ya Atomic na kuyatupa kwa wanawake na watoto, lau hayo yote tunayaunganisha na Uislamu, basi tutajua huruma, uadilifu na utu wa Uislamu na unyama wa dola za Magharibi na jinsi zilivyopetuka mipaka katika dhulma na unyang'anyi.

Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hapendi ufisadi.

Hakuna uharibifu mkubwa zaidi kuliko kuzusha vita na kutumia silaha zenye kubomoa ili kuwatawala watu na kuwanyang'anya chakula na matunda ya jasho lao.

Na anapoambiwa mche Mwenyezi Mungu hupandwa na mori wa kufanya dhambi.

Mtu mwema wenye ikhlasi anakubali masahihisho na nasaha, bali huzitafuta na kuzikaribisha, kwa sababu yeye hana lengo jengine zaidi ya haki, wala hatafuti sifa; kwa sababu amali yake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) sio umashuhuri.

Imam Amirul Muminin(a.s) anasema katika maneno anayowasifu wanaomcha Mwenyezi Mungu:"Hawaridhii na amali zao chache wala hawakioni kingi kilicho kingi; wao wanajituhumu na wao ni wenye kunyenyekea katika amali zao."

Katika hotuba yake siku za ukhalifa wake alisema: "Mtu hata kama ana cheo kikubwa katika haki na fadhila kubwa katika dini hawezi kuwa hahitajii kusaidiwa katika aliyobebeshwa na Mungu katika haki zake; wala si mwenye kutaka kujitukuza; wala mtu hata kama nafsi zinamfanya mdogo na kudharauliwa na macho sio kuwa hawezi kusaidia au kusaidiwa... Wala msinidhanie kuwa mimi ni mzito katika haki nitakayoambiwa, kwani mwenye kuifanya nzito haki atakayoambiwa au uadilifu atakaoonyeshwa, basi kwake kuitumia haki na uadilifu ni kuzito zaidi."

Hivyo ndivyo anavyotakikana mwanachuoni mwenye ikhlasi ya kweli. Ama mnafiki mwenye hiana, haki inakuwa nzito juu yake kwa sababu itamfedhehesha; na hununua sifa kwa thamani kubwa ili azibe upungufu wake na uovu wake.

Na katika watu yuko auzaye nafsi yake kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu.

Yaani baadhi ya waumini wanaikabili Jihadi na wanapenda mauti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. sawa na wale wengine wanaopenda uhai. Hawana lengo jengine isipokuwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu na thawabu Zake. Razi katika kutafsiri Aya hii anasema kuhusu sababu za kushuka kwake kuwa kuna riwaya tatu; Mojawapo ni kwamba Aya hii imeshuka kwa sababu ya Ali bin Abi Twalib(a.s) alipolala kwenye kitanda cha Mtume wakati wa Hijra, alisimama Jibril kichwani mwake, Mikail miguuni mwake na Jibril: Pongezi! Pongezi! ewe Ali akisema: Mwenyezi Mungu anajionea fahari kwako, mbele ya Malalika( [7] ).

﴿ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ﴾

208.Enyi mlioamini! Ingieni katika usalama nyote, wala msifuate nyayo za Shetani. Kwa hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.

﴿ فَإِن زَلَلْتُم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْكُمُ الْبَيِّنَاتُ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴾

209.Na kama mkiteleza baada ya kuwafikia ubainifu, basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

﴿ هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴾

210.Hawangoji ila kuwafikia (adhabu ya) Mwenyezi Mungu katika vivuli vya mawingu na Malaika, na liishe jambo; na mambo yote hurudishwa kwa Mwenyezi Mungu.

INGIENI KATIKA USALAMA NYOTE

Aya 208 - 210

MAANA

Enyi Mlioamini! Ingieni katika usalama nyote.

Imesemekana kuwa makusudio ya neno Silmi hapa ni Uislamu, na kwamba msemo unawaelekea wanafiki ambao wameificha kufuru na kudhihirisha Uislamu. Na imesemekana kuwa msemo unawaelekea wenye kumwamini Mwenyezi Mungu katika Ahlul Kitab ambao hawakusilimu. Na ikasemekana kuwa unawaelekea Waislamu wote kwa hivyo maana yake yanakuwa ni kumtii Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea katika hukumu Zake zote sio baadhi. Na pia imesemekana maana yake ni suluhu kwa maana kuwa ingieni katika suluhu nyote. Tuonavyo sisi ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemwamrisha mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu, kwa imani sahihi kuingia katika lile ambalo lina salama yake ya dunia na akhera. Na njia ya usalama inajulikana na wote, nayo ni kusaidiana, kuungana, na kuacha vita na uhasama. Vile vile kuyashinda matamanio na kuwa na ikhlasi katika kauli na vitendo.

Makusudio ya maneno hayo yanatiliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu:Wala msifuate nyayo za shetani. Kwa hakika yeye kwenu ni adui wa wazi, Aliyoileta mara tu, baada ya kusema.Ingieni katika usalama nyote. Hapo Mwenyezi Mungu amezingatia kuwa nyayo za shetani kinyume chake ni usalama; na amemweka mtu mbele ya mambo mawili tu, hakuna la tatu; Ama kuingia katika usalama au kufuata nyayo za shetani ambazo ndio dhati ya uovu, ugomvi, shari na ufisadi.

Na kama mkiteleza baada ya kuwafikia ubainifu, basi jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye hekima.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuamrisha kuingia katika usalama na kukataza kufuatwa nyayo za shetani, amemhadharisha yule atakayehalifu amri yake na makatazo yake na akatishia kwa kusema: "Basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye hekima." Mwenye nguvu, hashindwi katika amri Yake wala hakimzuwii chochote kwa alilokusudia kulifanya. Mwenye hekima, humlipa mema mtiifu na humwadhibu mwasi. Razi anasema: "Huo ndio ukomo wa kiaga kwa sababu ni kuhofisha bila ya kutaja adhabu. Huenda mzazi akamwambia mtoto wake: "Ukiniasi basi wewe wanijua na wajua uwezo wangu kwako", basi maneno hayo yanakuwa ni makemeo ya ufasaha zaidi kuliko kutaja kipigo na mengineyo.

Hawangoji ila kuwafikia (adhabu ya) Mwenyezi Mungu katika vivuli vya mawingu na Malaika. Maana kwa ujumla ni kwamba wale wenye kukadhibisha na wakaasi watajiwa na adhabu kwa ghafla wala hawataokoka. Aya iko katika mwelekeo wa Aya inayosema:

﴿ فَهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً ﴾

"Na hawangoji ila saa ya Kiyama kiwajie kwa ghafla...?" (47:18).

Na lishe jambo; na mambo yote hurudishwa kwa Mwenyezi Mungu. Mauti ambayo hapana budi nayo, yakija na Kiyama kikija, kila kitu kitakuwa kimekwisha na hapatabakia mbele ya wenye makosa isipokuwa hisabu na mateso.

SIRI NA MATUKIO YA GHAFLA

Hakuna yeyote ajuaye yatakayomtokea mbele na siri ya wakati, heri au shari. Hawezi kuyajua hayo vyovyote atakavyokuwa na elimu au imani:

"Na nafsi yoyote haijui itachuma nini kesho." (31:34)

Mara nyingi mtu hujiwa na heri kwa ghafla wakati yeye anatazamia kupata shari; na hujiwa ghafla na shari wakati anapotazamia heri. Hakuna kitu kinachotia uchungu kama hicho cha kupata shari wakati wa kutazamia heri; kama vile ambavyo hakuna kitu kitamu kama kupata heri wakati wa kutazamia shari. Mwenye akili hawezi kughurika na alivyo navyo, bali hufikiria mzunguko wa zama; kama vile ambavyo hakati tamaa na lolote linalompata; kwani dunia inageuka milele; ndio maana ikasemwa; "Kudumu hali ni muhali na faraja inakuja kutokana na dhiki." Imam Ali(a.s) anasema:"Baada ya dhiki ni faraja. Anaendelea kusema Imam:"Hakika Musa bin Imran alitoka kuwatafutia watu wake moto akasemeshwa na Mwenyezi Mungu na akarudi akiwa Mtume." Mwenyezi Mungu anasema:

﴿ إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِن رَّوْحِ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ ﴾

"...Hawakati tamaa ya rehema ya Mwenyezi Mungu isipokuwa watu makafiri." (12:87).

Na amesema tena:

﴿ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ ﴾

... Hawajiaminishi na mipango ya Mwenyezi Mungu ila watu wenye hasara." (7:99).

Imeelezwa katika vitabu vya Historia na Sera kwamba Ibn Ziyat alikuwa waziri na mtu wa kutegemewa na Mu'utasim, naye alikuwa ni katika mataghuti wa hali ya juu na dhalimu mkubwa. Alitengeneza tanuri la chuma alilolijaza misumari yenye ncha pambizoni mwake. Anapomkasirikia mtu humtupa ndani, kila anavyojitingisha ndivyo misumari inavyomwingia mwilini mwake. Mutawakkil alipotawala alimshika Ibn Ziyat na akamfunga kwa chuma mikononi mwake na miguuni mwake kisha akamtupa katika tanuri hilo, na baadaye akafa. Kabla ya kufa alisikika akiimba shairi hili: Sifazake tulia, hebu nenda pole pole, Kigeugeu dunia, huenda nyuma na mbele.

﴿ سَلْ بَنِي إِسْرَائِيلَ كَمْ آتَيْنَاهُم مِّنْ آيَةٍ بَيِّنَةٍ وَمَن يُبَدِّلْ نِعْمَةَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُ فَإِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴾

211.Waulize wana wa Israil, ishara ngapi zilizo wazi tulizowapa? Na anayezibadilisha neema za Mwenyezi Mungu baada ya kumfikia, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

﴿ زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَيَسْخَرُونَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ اتَّقَوْا فَوْقَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَاللَّـهُ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴾

212.Wamepambiwa makafiri maisha ya duniani, na wanawafanyia maskhara wale walioamini. Na wale wenye takua watakuwa juu yao Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila hisabu

WAULIZE WANAWA ISRAIL

Aya 211 – 212

MAANA

Waulize wana wa Israil, ishara ngapi zilizo wazi tulizowapa?

Makusudio ya waulize hapa sio swali hasa la kihakika, kwa sababu Mtume(s.a.w.w) anajua hali zao, wala makusudio sio kuelezea hali waliyokuwa nayo; kama ilivyo katika Aya ya 49 na inayofuatia. Isipokuwa makusudio hasa ni kuwa Waislamu wazingatie na wapate funzo na hali ya Waisrail. Njia ya kupata funzo ni kuwa Waisrail walijiwa na Mtume Musa(a.s) kwa miujiza na hoja ambayo ni mkono kuwa mweupe, fimbo kugeuka nyoka na kupasuka bahari. Vile vile kufunikwa na wingu, kuteremshiwa Manna na Salwa na jabali kutoka maji. Pamoja na hayo yote waliasi na kukhalifu, ndipo Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa madhila na utwevu katika dunia na adhabu iumizayo katika Akhera. Na Waislamu nao wamejiwa na Muhammad(s.a.w.w) kwa miujiza na hoja zinazofahamisha ukweli wa Utume wake na kuswihi sharia yake; naye akawafikilizia habari kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa waaingie katika Uislamu wote, kwani humo watapata heri na utengeneo wao; kama wakiasi kama walivyofanya Waisrail, basi yatawapata yaliyowapata Waisrail.

Na anayezibadilisha neema za Mwenyezi Mungu baada ya kumfikia, basi hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.

Makusudio ya neema hapa ni dalili za haki, kwani hizo ni katika neema kubwa. Kwa sababu ndani yake mna uongofu na kuokoka na kuhiliki na upotevu. Makusudio ya kuzibadilisha ni kuziasi na kuziharibu. Kwa hiyo kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.)Na anayezibadilisha neema za Mwenyezi Mungu baada ya kumfikia ni sawa na kauli yake:

﴿ فَإِن زَلَلْتُم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْكُمُ الْبَيِّنَاتُ﴾

"Na kama mkiteleza baada ya kuwafikia ubainifu..." (2:209).

Vile vile kusema kwake:

﴿فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴾

"Basi hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu" (2:209) ni sawa na kusema Kwamba:Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye hekima."

Maana ni moja na lengo ni moja.

HAPANA IMANI BILA TAKUA (UCHA MUNGU)

Wamepambiwa makafiri maisha ya duniani.

Hapana tofauti kati ya mwenye kukanusha kuwapo Mwenyezi Mungu na yule mwenye kuamini kinadharia tu, lakini matendo yakawa ni tofauti. Hapana tofauti kati ya wawili hao. Kwa sababu kila mmoja ameathiriwa na dunia na vipambo vyake, ameathirika na kitu cha sasa hivi kuliko cha muda ujao; heri na manufaa ameyapima kwa kiwango cha manufaa yake, wala hakupima na mambo aliyoharamisha Mwenyezi Mungu wala na msimamo wa kibinadamu. Mimi kila ninavyozidi kuzama katika tafsiri ya Qur'an na kuangalia kwa undani Aya zake, basi huwa na yakini zaidi kwamba imani bila ya ucha Mungu haina maana yoyote; na kwamba kila anayeiangalia dunia kuwa ndio makusudio yake yote, basi atakuwa ameiweka mbali sharia ya haki na dini, atake asitake.

Imekuja Hadith Mutawatir kutoka kwa Mtume Mtukufu akisema: "Dunia na akhera zina madhara" yaani zinadhuriana kuhujumu moja yao nikuiacha nyingine( [8] ).

Imam Ali(a.s) anasema: "Hakika dunia na Akhera ni maadui wawili wanaotofautiana, na ni njia mbili tofauti. Mwenye kuipenda dunia ataichukia akhera na kuwa adui yake; zote mbili ni kama Mashariki na Magharibi, mwenye kutembea kati yao huwa mbali na nyingine kila anapokaribia moja wapo.

" Na wanawafanyia maskhara wale walioamini.

Ni kawaida wale wanaozichezea Hoja za Mwenyezi Mungu na hukumu zake wakihalalisha damu na mali ya haramu kuwadharau na kuwachezea wale wanaojilinda na maharamisho na kuvumilia tabu na mashaka kwa ajili ya kumridhisha Mungu.

Na wale wenye takua watakuwa juu yao siku ya Kiyama.

Amesema wenye takua wala hakusema wale walioamini, kwa sababu imani bila takua si lolote; kama tulivyobainisha. Maana yako wazi ni kuwa makafiri wakiwadharau waumini hivi sasa, basi mambo yatabadilika kesho. Mwenyezi Mungu anasema:

﴿قَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ إِنَّ الْخِزْيَ الْيَوْمَ وَالسُّوءَ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴾

"...Watasema walio pewa ilimu: Hakika hizaya na ubaya leo itawafika makafiri." (16:27).

﴿فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ ﴾

"Basi leo wale ambao wameamini wanawacheka makafiri." (83:34)

Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila hisabu.

Riziki ni mbili ya dunia na riziki ya Akhera. Riziki ya dunia inajulikana na riziki ya Akhera, ni neema isiyokatika na isiyokuwa na chembe ya huzuni au hofu. hataipata yeyote isipokuwa kwa imani na amali njema: Anasema Mwenyezi Mungu:

﴿وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴾

"Na wale walioamini na kutenda mema, hao ndio watu wa Peponi, humo watakaa milele." (2:82).

Kila mtu anaweza kupata riziki duniani, awe ni kafiri au Mumin, mwema au mwovu, na anayehangaika au asiyehan-gaika; kama vile urithi, zawadi, wasiya, n.k. Vile vile inaweza kupatikana kwa njia ya halali, au haramu, kama vile kunyang'anya, kughushi na utapeli. Mwenye Tafsir Al-Manar amenakili kutoka kwa mwalimu wake Sheikh Muhammad Abduh kwamba, amesema wakati wa kutafsiri Aya hii, kwamba riziki bila ya kuhangaika inaweza ikapatikana kwa baadhi ya watu. Ama kwa Umma ni muhali kujitosheleza isipoku-wa kwa kuhangaika na kufanya kazi. Huo ni ukweli ulio wazi kabisa.

11

12

13

14

15