TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA Juzuu 1

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA13%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA Mwandishi:
Kundi: tafsiri ya Qurani

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
Juzuu 9 Juzuu 10 Juzuu 11
  • Anza
  • Iliyopita
  • 20 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 39812 / Pakua: 5109
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA Juzuu 1

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

4

5

6

7

16

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KWANZA

AL - BAQARAH (NG’OMBE)

﴿أَمْ تُرِيدُونَ أَن تَسْأَلُوا رَسُولَكُمْ كَمَا سُئِلَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ وَمَن يَتَبَدَّلِ الْكُفْرَ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ ﴾

108.Je mnataka kumuuliza Mtume wenu kama alivyoulizwa Musa zamani? Na anayebadilisha imani kwa ukafiri, hakika amepotea njia iliyo sawa.

﴿وَدَّ كَثِيرٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يَرُدُّونَكُم مِّن بَعْدِ إِيمَانِكُمْ كُفَّارًا حَسَدًا مِّنْ عِندِ أَنفُسِهِم مِّن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْحَقُّ فَاعْفُوا وَاصْفَحُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴾

109.Wengi miongoni mwa watu wa kitabu wanatamani lau wangewarudisha nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa sababu ya husuda iliyomo nafsini mwao, baada ya kuwapambanukia haki. Basi sameheni na muwache mbali mpaka Mwenyezi Mungu alete amri Yake. Hakika Mwenyezi Mungu Ni muweza wa kila kitu.

JE MNATAKA KUMUULIZA MTUME WENU

AYA YA 108-109

MAANA

Je, mnataka kumuuliza Mtume wenu kama alivyoulizwa Musa zamani? Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwaambia waumini: msijali kwa kupingwa ufutaji wa hukumu za dini yenu, kwa sababu mambo yote yako chini ya uweza wake Mwenyezi Mungu, na Ndiye anayewachagulia lililo na maslahi kwa ajili yenu na wengineo; baada ya kuwambia haya, aliwaambia mwataka nini kutoka kwa Mtume wenu Muhammad(s.a.w.w) na hali amewajia na dalili za kutosha? Mwataka kumdodosa kama walivyofanya Mayahudi kwa Musa kwa kumuuliza yasiyofaa kuulizwa? Mtu anaweza kuwa na shaka na akataka dalili ya kukinaisha kuondoa shaka yake. Ama kutaka jabali liwe dhahabu, hiyo itakuwa ni ukaidi na kiburi.Basi enyi waumini msiwe wakaidi wenye kutakabari.

Na anayebadilisha imani kwa ukafiri, hakika amepotea njia iliyo sawa. Kila mwenye kuwa na msimamo safi wa kutafuta dalili za kiakili kwa kutaka kuthibitisha haki, huyo ni muumini wa haki. Na kila mwenye kuwa na msimamo wa kiburi kudadisi na kutaka mambo yasiyoingia akilini basi huyo ni mpinzani wa haki. Na asiyetegemea aliyokuja nayo Muhammad(s.a.w.w) na kutaka zaidi, atakuwa amechagua inadi na kufuru juu ya imani.

Wengi miongoni mwa watu wa kitabu wanatamani lau wangewarudisha nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa sababu ya husuda iliyomo nafsini mwao.

Kila mtu anapendelea watu wawe kwenye dini yake.Mwanafalsafa mmoja anasema: Siku nzuri kwangu ni ile ninayomuona anayeniafiki yuko kwenye rai yangu. lakini Mayahudi walikuwa wakifanya juhudi kubwa ya kuwafitinisha Waislamu, kuwatoa kwenye dini yao ya Kiislamu na kuwarudisha kwenye dini yao ya kijahili ya kwanza, si kwa lolote bali ni kwa uhasidi. Ingawaje wao wanaweza kuwa Waislamu, kama walivyofanya wengine, lakini wao walihofia biashara zao na faida zao za pombe, kamari na uasherati. Mayahudi walitaka kuwavunja Waislamu siku ya vita vya Uhud kwa kumlia njama Mtume. Imeelezwa kuwa baada ya tukio la Uhud walikuwa wakiwaita vijana wa Kiislamu majumbani mwao na kuwapatia pombe pamoja na kuwahadaa na mabinti zao, kama wanavyofanya leo na kila siku; kisha wanawatia shaka Waislamu kuhusu Quran na Utume wa Mtume mtukufu(s.a.w.w) .

Mtume alihisi mipango hii ya hatari akawakataza wasihudhurie kwenye vikao vya mambo ya upuuzi, akitilia mkazo kukataza zina, pombe, kamari na nyama ya nguruwe. Wakajizuilia Waislamu kwenda kwenye majumba ya Wayahudi waliyoyafungua kwa lengo lao hilo, ambayo hivi sasa yanajulikana kama Baa na Casino.Baada ya kuwapambanukia haki.

Yaani Mayahudi walijaribu kuwarudisha Waislamu kwenye kufuru na upotevu pamoja na kujua Uislamu kuwa ndio dini ya haki na kwamba ushirikina na kuukana Utume wa Muhammad ni batili. Haya si kwa Mayahudi tu, kwani wako watu wengi hukanusha haki na kuipinga sio kwa lolote isipokuwa ni kwa vile haiafikiani na tamaa zao. Kwa sababu ya kupelekwa na mapenzi na manufaa yake na wala sio kwa dini na akili. Amirul Mumini anasema:Vita vya akili mara nyingi viko kwenye tamaa.

Basi sameheni na muwache mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake. Yaani achaneni nao hivi sasa wala msiwaingilie kuwatia adabu mpaka Mwenyezi Mungu awaamrishe hilo; kwani mambo yana wakati wake. Tafsiri nyingi zinasema kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliwaamrisha Waislamu kuachana nao mpaka iliposhuka kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

﴿قَاتِلُوا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ ﴾

Piganeni na wale wasiomwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho.... (9:29)

Na Aya nyenginezo za vita.

Razi amesema: Imam Muhammad Baqir(a.s) anasema:Hakika Mwenyezi Mungu hakumwamrisha Mtume wake vita mpaka aliposhuka Jibril na kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

﴿أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا وَإِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ ﴾

Wameruhusiwa (kupigana) wale wanaopigwa, kwa sababu wamedhulumiwa na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni muweza wa kuwasaidia. (22:39)

KUIKHALIFU HAKI

Mambo yote ya maisha miongoni mwa kufuru, ulahidi, uovu, kuvunjwa heshima na ufisadi. Vile vile dhuluma, utaghuti, vita na ufukara, yote hayo yanasababishwa na kitu kimoja: kuihalifu haki. Lau watu wote, si kadhi peke yake, wangelichunga haki, wangeliishi wote kwa amani na raha. Kauli yake Mwenyezi Mungu:

﴿فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ﴾

Na nini kilicho baada ya haki isipokuwa upotevu?. (10:32)

Ni kuonyesha hakika hii.Ni kweli kuwa haki haikosi watetezi wakati wowote ule, lakini ni wachache.

Lau haki ingelipata watetezi kama ilivyo batili, basi ulimwengu wote ungelikuwa katika uzuri na amani. Bali lau kila mtu angeliitaka haki yake na akatekeleza wajibu wake,tusingeliona dhulma wala batili hata athari yake. Mwenyezi Mungu ameisimamishia haki dalili za kuongoza kwenye hiyo haki. Hayo yanatolewa dalili na maumbile, kitabu chake Mwenyezi Mungu na kutokana na Mtume Mtukufu.Vile vile watu watakatifu wa nyumba ya Mtume aliowaweka sawa na Quran; kama ilivyoelezwa katika Hadith thaqalayn ambayo ameipokea Muslim katika Sahih yake. Mwenye kuipinga dalili hii hali anajua atakuwa amempinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake; sawa na walivyofanya Mayahudi na washirikina.

﴿وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّـهِ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴾

110.Na simamisheni swala na toeni zaka, na heri yoyote mtakayoitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta mbele ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mnayoyafanya.

NA SIMAMISHENI SWALA

Aya 110

MAANA

Aya hii imekusanya mambo matatu:

1. Kuamrisha kusimamisha swala

2. Kuamrisha kutoa zaka

3. Kuhimiza heri kwa ujumla

Katika Tafsir ya Al-Manar imeelezwa kwamba Aya hii ina madhumuni ya hukumu mahsusi ambayo ni kuamrisha swala na zaka. Kisha imetaja hukumu kwa ujumla ambayo iko peke yake, lakini ujumla wake unakusanya pia hukumu mahsusi iliyotangulia. Na huu ni katika mfumo wa Quran ambao ni wa aina yake.

Mtaikuta mbele ya Mwenyezi Mungu Makusudio yake ni kukuta malipo yake na thawabu zake sio kukuta amali yenyewe,kama ilivyosemwa ,kwa sababu amali hazibaki. Unaweza kuuliza: Tumeona Quran mara kwa mara inakutanisha amri ya swala na ya zaka; Je, kuna siri gani? Limejibiwa swali hili kwamba swala ni ibada ya kiroho na zaka ni ibada ya kimali, mwenye kuitekeleza kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu inamuwia wepesi kujitolea katika njia ya Mwenyezi Mungu.

SWALA NA VIJANAWA KISASA

Vijana wengi wa kisasa wanapuuza dini na wanaoshikamana nayo; wengine wanasema wazi kuwa hakuna chochote zaidi ya hivi vitu vilivyoko. Wengine wanasema kuwa yuko mwenye kupanga mambo vizuri na mwenye hekima, lakini hakuwajibisha saumu wala swala. Aina zote hizo mbili za watu mbele ya Mwenyezi Mungu ziko sawa katika ukafiri. Kwa sababu mwenye kuacha swala kwa kuamini kuwa sio wajibu, huyo ni sawa na anayemkanusha Mwenyezi Mungu. Na sisi wanavyuoni tunawaangalia vijana wa kisasa wakiendelea kupuuza dini na kuikataa haki, bila ya kufanya kazi yoyote au kuwakinaisha kwa namna yoyote ile. Nikisema kazi, nakusudia kazi za ushirikano zenye kuleta matunda ambazo zinataka maadili na vikao vya kujadili namna ya utekelezaji kisha kufunguliwe shule na vyuo vya elimu ya Quran, Hadith, Falsafa ya Itikadi ya Kiislamu, Historia ya Kiislamu na elimu ya nafsi (Saikolojia).

Vile vile kuwe na mazoea ya kutoa mawaidha na ya kulingania kwenye dini kwa njia nzuri na ya kisasa. Ndio,wengine wamefanya juhudi zao zilizoleta natija ambazo zinafaa kutolewa shukurani. Lakini linalotakikana hasa ni kuzishirikisha pamoja juhudi hizo na kuwa na Ikhlasi katika nia na kujitolea mhanga katika yote. Lakini vipi zitashirikishwa pamoja juhudi na hali wenye kutaka kuchuma kwa jina la dini ni wengi ambao hawaoni umuhimu na haliwashughulishi lolote zaidi ya lile litakalowapatia jina na mali tu? Kwa hiyo jukumu la kuwalea vijana ni letu sisi wanavyuoni wa dini, na tutaulizwa hilo mbele ya Mwenyezi Mungu; sawa na vile ambavyo wao nao wataulizwa kutokana na kupuuza na kuacha kutafuta kujua dini ya haki na kutumia hukumu zake.

﴿وَقَالُوا لَن يَدْخُلَ الْجَنَّةَ إِلَّا مَن كَانَ هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ تِلْكَ أَمَانِيُّهُمْ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴾

111.Na walisema: Hataingia peponi ila aliye Myahudi au Mnaswara (Mkristo). Hayo ni matamanio yao tu. Sema: Leteni dalili zenu kama nyinyi ni wasema kweli.

﴿ بَلَىٰ مَنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَلَهُ أَجْرُهُ عِندَ رَبِّهِ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴾

112.Si hivyo! Yeyote anayeuelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu kwa nafsi yake hali anatenda mema, basi ana malipo yake kwa Mola wake, wala haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.

NAWALISEMA HATAINGIA PEPONI

Aya ya 111-113

LUGHA

Neno: Hud linatokana na Haid lenye maana ya kutubia na kurudi kwenye haki. Na neon: Naswara tumelifafanua katika kufasiri Aya ya 62.

MAANA

Na walisema: Hataingia peponi ila aliye Myahudi au Mnaswara (Mkristo). Mwenye Majmau anasema: Hii ni kufupisha maneno: Kukadiria kwake ni kama kusema hivi: Husema Myahudi: Hataingia peponi ila aliye Myahudi, na husema Mkristo: Hataingia peponi ila aliye Mkristo. Imekadiriwa hivi kwa sababu inajulikana kwamba Mayahudi hawakubali kuwa Wakristo wataingia peponi. Kwa hivyo tukafahamu kuwa yameunganishwa maneno kwa kufupiliza maneno bila ya kuharibu maana, kwani umashuhuri wa hali unatosha kuwa ni ubainifu.

﴿وَقَالَتِ الْيَهُودُ لَيْسَتِ النَّصَارَىٰ عَلَىٰ شَيْءٍ وَقَالَتِ النَّصَارَىٰ لَيْسَتِ الْيَهُودُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُمْ يَتْلُونَ الْكِتَابَ كَذَٰلِكَ قَالَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ مِثْلَ قَوْلِهِمْ فَاللَّـهُ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴾

113. Na Mayahudi walisema: Manaswara hawana chochote na Manaswara walisema: Mayahudi hawana chochote na hali (wote) wanasoma Kitabu. Na hivi ndivyo wale wasiojua wasemavyo mfano wa kauli yao. Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihitilafiana.

ULANGUZI WA PEPO

Inadhihiri kutokana na Aya hii tukufu kwamba Mayahudi na Wakristo wanaamini nadharia ya ulanguzi tangu zamani na kwamba nadharia hiyo kwao inaingia pia kwenye neema za dunia na akhera. Vile vile imedhihiri kwamba ulanguzi wa pepo unahusika na watu wa dini. Kwa misingi hiyo ndio likawa kanisa linauza cheki za msamaha kwa waasi na wenye dhambi kwa pesa. kanisa likachuma mali nyingi sana, lakini lilizidisha makosa na kueneza ufisadi. Miongoni mwa mambo yanayoandikwa kwenye cheki hiyo ya msamaha ni: Unafungwa mlango ambao wataingia wenye makosa kwenye adhabu na mateso na unafunguliwa mlango wa kwenda kwenye pepo ya furaha; na hata ukiendelea kuishi muda mrefu neema hii itabaki bila ya kubadilika mpaka ifikie saa yako ya mwisho, kwa jina la Baba na Mwana na la Roho Mtakatifu. Hayo ni matamanio yao tu.

Ni matamanio yao ambayo ni mengi sana. Miongoni mwayo ni kwamba Waislamu warudi kuwa makafiri na maadui zao waadhibiwe na kwamba pepo ni yao peke yao. Sema: Leteni dalili zenu,kama nyinyi ni wasema kweli. Madai yote huhitaji dalili na vile vile kila dalili ya kinadharia inahitaji dalili mpaka iishie kwenye asili yenye kuthibitika kimsingi. Maana ya kuthibiti kwake ni kuafikiana wote wenye akili kuhusu usahihi wake wala visipingane vitu viwili; kama ilivyo asili hii Kila madai yanahitaji dalili isipokuwa ikiwa madai yenyewe ni ya kimsingi, kwani mwenye kudai madai ya kimsingi yaliyo wazi hayawezi kuitwa madai; kwa sababu madai huhitaji dalili; na madai ya kimsingi yanakuwa pamoja na dalili yake haiepukani nayo. Kwa hivyo huwezi kumuuliza dalili mwenye kusema: Kumi ni zaidi ya moja.

Katika Tafsir Al-Manar anasema katika kutaja Aya hii kwamba wahenga wa Kiislamu walio wema walikuwa na asili hii ya kuonyesha dalili juu ya wanayosema na wakitaka dalili kwa watu kwa wanayoyadai. Lakini waliokuja baadaye walio waovu - kama asemavyo mwenye Al-Manar - wameifanya kinyume Aya; wamewajibisha kufuata tu na kuharamisha dalili ila kufanya kwa kufuata tu. Wamezuia kufanya amali kwa kauli ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakawajibisha kufanya amali kwa kauli ya fulani. Si hivyo! Yeyote anayeuelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu kwa nafsi yake hali anatenda mema basi ana malipo yake kwa Mola wake.

Hii ni kuyakomesha madai kwamba pepo ni yao peke yao. Maana ni kuwa kila anayemwamini Mwenyezi Mungu kwa kumsafia nia katika amali zake bila ya kuichanganya na shirk; wala ria, basi yeye ni katika wenye kutukuzwa kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu yeye hapotezi malipo ya mwenye kutenda wema. Ama kauli yake na hali anatenda mema, ni ishara kwamba. Kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kunatokana na amali njema sio mbaya, kwa sababu Mwenyezi Mungu hatiiwi pale anapoasiwa. Na Mayahudi walisema: Manaswara hawana chochote na Manaswara walisema: Mayahudi hawana chochote. Mwenye Majmaul-Bayan amesema akimnukuu Ibn Abbas kwamba Wakristo wa Kinajran walibishana na Mayahudi mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) Myahudi mmoja akasema: Hamna chochote nyinyi. Akajibiwa na Mkristo: Mayahudi hawana chochote, ndipo ikashuka Aya hii ikisajili kauli ya vikundi vyote viwili.

DINI YA MASLAHI KWA MAYAHUDI NAWAKRISTO

Ni maarufu kwamba Wakristo wanaeleza kwa uwazi kwamba Mayahudi na kizazi chao ndio waliohusishwa na kumsulubu Yesu. Pamoja na hayo yote Baba mtakatifu wa Roma alifanya juhudi za kufa na kupona mnamo mwaka 1965 za kuwatakasa Mayahudi wa sasa na wa kizazi kijacho. Ikabidi kugongana na kanisa la Mashariki.Na gharama za mkutano zilifikia dola milioni ishirini.

Lengo la kwanza na la mwisho la mkutano huo ni siasa tu ya kuipa nguvu dola ya Israil na kuyapa nguvu makao yake katika Palestina na siasa yake ulimwenguni. Kwa usahihi zaidi ni kuupa nguvu ukoloni na kuweka nguvu zake katika mashariki kwa ujumla na hasa katika miji ya kiarabu. Hii inafahamisha kwamba dini kwa baadhi yao ni manufaa ya kimaada. 28 Na hali wote wanasoma Kitabu Yaani Mayahudi wana Tawrat ambayo inaelezea habari njema za kuja Isa na kukubali Utume wake. Vile vile Wakristo wana Injil inayomtambua Musa na Tawrat yake. Kwa hivyo Mayahudi na Wakristo wako katika hukumu ya taifa moja, kwa sababu dini yao ni moja na kati ya Tawrat na Injil, ni fungu la kuitimiza nyingine. Lakini pamoja na hayo wamekufurishana.

WAISLAMU VILEVILE WANAKUFURISHANA

Ikiwa Mayahudi na Wakristo wako katika hukumu ya taifa moja, kwa sababu tu Tawrat inamtambua Isa na Injil inatambua Musa, basi bora zaidi ni Sunni na Shia wawe taifa moja kwa uhakika kabisa. Kwa sababu kitabu chao ni kimoja ambacho ni Quran moja wala sio viwili, na Mtume wao ni mmoja ambaye ni Muhammad sio Muhammad wawili.Sasa imekuwaje wengine wawakufurishe ndugu zao katika dini? Na Mayahudi walisema: Manaswara ha-wana chochote na Manaswara walisema: Mayahudi hawana chochote na hali wote wanasoma kitabu. Lau tukiangalia maana tuliyoyabainisha ya Aya hii na wafasiri wote wakaafikiana; kisha tukaikisia na Mwislamu anayemkufurisha ndugu yake Mwislamu, basi hali ingelikuwa mbaya zaidi ya mara elfu kuliko Mayahudi na Wakristo.

* 28 Angalia kifungu cha Masilahi ndio sababu katika tafsir ya Aya 96 ya Sura hii. Mayahudi waliwakufurisha Wakristo na Wakristo wakawakufurisha Mayahudi.Na hali wote wanasoma kitabu. Yaani Tawrat na Injil. Sasa itakuaje Mwislamu amkufurishe ndugu yake Mwislamu na hali naye anasoma Quran? Basi na wamwogope Mwenyezi Mungu wale wanaopinda ndimi zao kwa kusoma kitabu na nyoyo zao hazijui maana yake na makusudio yake. Na hivi ndivyo wale wasiojua wasemavyo mfano wa kauli yao. Makusudio ya wasiojua katika Aya hii ni makafiri wa kiarabu kutokana na vile wali-vyosema, sawa na Mayahudi na Wakristo kwamba wao peke yao ndio watakaoingia peponi. Quran imewajibu, kwanza, kwamba haki haifungamani na watu fulani tu wala na majina, isipokuwa kuingia peponi kunatokana na imani njema. Pili, kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamjua mwenye haki na mwenye batil na yeye atamlipa kila mmoja kwa amali yake. Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao siku ya Kiyama katika yale waliyohitalifiana.

KILA MMOJA AVUTIA KWAKE

Unaweza kuuliza kila watu wa dini na vikundi wanadai kuwa wao wako kwenye haki na wenzao wako kwenye batili; kama walivyodai Mayahudi, Wakristo na washirikina wa kiarabu. Sasa je, vipi tutamjua mwongo na mkweli? Kabla ya kujibu, kwanza tunaanza kuelezea hakika hii: Kila mwenye kudai haki hana budi kuwa na moja ya mambo mawili: Ama kukubaliana kabisa na rai yake tangu mwanzo na kuendelea nayo na wala asione uwezekano wa makosa wala asifuate vingine vyovyote itakavyokuwa. Au awe anaitafuta haki kwa juhudi zake mpaka aone dalili ya kuitegemea kwa kuazimia kwamba akibainikiwa na haki kwa upande mwingine aifuate na kugeuza rai yake. Kwa sababu yeye anaitafuta haki popote na wakati wowote ilipo na itakavyokuwa. Hapana budi kuwatofautisha wawili hawa.Wa kwanza hakuna njia ya kumkinaisha kwa hoja na mantiki ya kiakili, bali hana dawa isipokuwa kuachana naye. Wa pili inakua wepesi kufahamiana naye.Kila mmoja wetu anajua kuwa kuna mambo ambayo yako wazi. Mfano, maisha mazuri ni raha, na ufukara ni balaa na mashaka, mapenzi ni bora kuliko kugombana, usalama ni wenye manufaa kuliko vita, elimu ni nuru na ujinga ni giza, uadilifu ndio haki na dhulma ni batili na kwamba kitu kimoja hakiwezi kuwa pamoja na kinyume chake, n.k.

Tukianza kuangalia hayo na kuyajua, kisha mtu akadai kwamba yeye ni mwenye haki kinyume cha mwingine tutampima na kumhukumu kwa hakika hizo, zikiafikiana naye atakuwa ni mkweli, vinginevyo atakuwa mwongo. Kwa hivyo basi inatubainikia kwamba kauli ya mwenye kusema: Kila mmoja anavutia dini yake nitatambua vipi iliyo sahihi?, ni ya hatari na duni yenye shabaha ya kueneza vurugu na ujinga. Lau ingekuwa ni kweli ingelipasa sehemu za kuabudu na vituo vifungwe, jambo ambalo halina msimamo wa kiakili wala kikanuni au kitabia. La upuuzi zaidi ni kwamba kauli hiyo (nitajuaje ukweli) ni maneno ya kishairi yaliyokuja kutokana na mawazo yasiyo-kuwa na mantiki yoyote. Mwenyezi Mungu amesema kweli aliposema:

﴿وَالشُّعَرَاءُ يَتَّبِعُهُمُ الْغَاوُونَ ﴿٢٢٤﴾ أَلَمْ تَرَ أَنَّهُمْ فِي كُلِّ وَادٍ يَهِيمُونَ ﴿٢٢٥﴾ وَأَنَّهُمْ يَقُولُونَ مَا لَا يَفْعَلُونَ﴾

Na washairi wanafuatwa na wapotofu. Je huoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde? Na kwamba wao wanasema wasiyoyatenda? (26:224-226)

﴿وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَاجِدَ اللَّـهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ وَسَعَىٰ فِي خَرَابِهَا أُولَـٰئِكَ مَا كَانَ لَهُمْ أَن يَدْخُلُوهَا إِلَّا خَائِفِينَ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴾

114.Ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayezuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa humo jina lake na akajitahidi kuiharibu? Hao haitawafalia kuingia humo ila nao wanaogopa; wana fedheha katika dunia na katika akhera wana adhabu kubwa.

KUZUIA MISIKITI YA MWENYEZI MUNGU

Aya ya 114:

MAELEZO

Aya hii ni katika Aya ambazo kauli za kuifasiri zimekuwa nyingi. Dhahiri yake inafahamisha makemeo na kiaga kwa asiyeiheshimu misikiti au sehemu yoyote ya kufanyia ibada na kuzuia kujengwa au kufanyiwa ibada ndani yake.Vile vile kuivunja au kuipuuza. Na kwamba wajibu wa kimungu na wa kibinadamu unafaradhishia kila mtu kuzitakasa sehemu za kufanyia ibada na kuziingia kwa heshima na unyenyekevu, na hali ya kuogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu na kutaraji thawabu zake, sio kuzivunjia heshima na kuzidharau. Kwa sababu ziliwekwa kwa lengo la ibada. Kisha Mwenyezi Mungu amebainisha kwamba mwenye kuziingilia sehemu za ibada kwa nia mbaya atamdhalilisha katika maisha ya dunia na kesho atamwadhibu adhabu kubwa.Kwa ufupi Aya inabainisha kwamba mwenye kufanya jambo kadha atafanyiwa kadha. Na hilo ni suala la kijumla sio lililopita wala la wakati wa kushuka Aya au kungoja kutokea. Lakini wafasiri wamesema kuwa ni suala maalum; kisha wakahitalifiana kwamba je suala lenyewe lilitokea kabla ya Utume wa Muhammad(s.a.w.w) au baada yake?

Wale waliosema kuwa lilitokea kabla nao pia wamehitalifiana katika kulielezea tukio lenyewe.Kuna baadhi yao waliosema kwamba Aya inaelezea tukio la Titus wa Roma alipoingia Baytul-Maqdis baada ya kufa Masih kwa kiasi cha miaka sabini; akaiharibu kiasi ambacho halikubaki jiwe juu ya jiwe jengine; akavunja hekalu la Suleiman na akachoma baadhi ya nakala za Tawrat. Na Masih alikuwa amewehadharisha Mayahudi kuhusu hilo. Inasemekana kwamba Titus aliiharibu Baytul Maqdis, kwa kuhimizwa na Mayahudi ili awatese Wakristo. Miongoni mwa wale wanaosema kuwa Aya inaelezea matukio yaliyopita kuna wanaosema kwamba inaelezea yale aliyofanya Nebukadnezzar katika kuiharibu Baitul Maqdis.

Katika Tafsir Al-Manar anasema ninamnukuu: Jambo la kushangaza ni kwamba Ibn Jarir amesema katika Tafsir yake kwamba: Aya inaonyesha kuungana Wakristo pamoja na Nebukadnezzar wa Babilon kuiharibu Baitul Maqdis, ambapo tukio la Nebukadnezzar lilikuwa kabla ya kuja Masih na Ukristo kwa miaka mia sita na thalathini na tatu (633).

Vile vile kuna wengine wanaosema kuwa Aya inatoa habari ya jambo lililokwisha tokea, kwamba imeshuka kwa ajili ya washirikina wa Kiquraish waliomzuia Mtume na sahaba zake kuingia Makka katika kisa cha Hudaybiya.

* 29 ilitokea sadfa siku niliyosoma kosa hili la Tabariy, nikasoma makala ndefu katika gazeti la Aljumhuriya la Misr la tarehe 5 May 1967, inayosema ...Tabariy bila shaka ni nguzo ya wanahistoria wa Kiislamu na kitabu chake ndio kiongozi cha tafsir....Tabari alikufa mwaka 310 AH yaani karibu miaka 1050 iliyopita. Ikiwa hali ya wanahistoria waliotangulia na wanaotegemewa ni hii, je, ategemewe nani?Ama wale wanaosema kuwa Aya inatolea habari jambo linalongojewa kutokea, pia nao wamehitilafiana. Kuna wale waliosema kwamba Aya inaonyesha uvamizi wa Wakristo juu ya Baitul-Maqdis na miji mingine katika miji ya Waislamu. Wengine wanasema kuwa inatolea habari tukio la Wakaramet (Karmathians) la kuivunja Al-Kaaba na kuwazuia watu kuhiji. Kisha kundi linalosema hivi likasema: Hii ni katika miujiza ya Quran, kwa sababu ilitolea habari mambo yatakayotokea.

Hayo ndiyo kwa ufupi waliyoyasema wafasiri.Na sisi hatutegemei chochote katika kauli hiyo; kwani hakuna dalili ya kiakili au kauli itakayoweza kuituliza akili. Sisi tunategemea dhahiri ya Aya ambayo haipingani na akili wala hakuna kauli ya Hadith inayoeleza jengine. Dhahiri hiyo ni: Wajibu wa kuheshimu sehemu za kuabudu na kuharamisha kuziingilia na kwamba mwenye kukusudia uovu, atapata malipo yake.

HUKUMU ZA MISIKITI

Ni Sunna kujenga misikiti, kuiamirisha kwa sababu ya kutajwa Mwenyezi Mungu, kui-safisha na kuingarisha, Ni haramu kuivunja, kuingia mwenye janaba na mwenye hedhi. Ni Suna kuswali raka mbili za kuuamkia (kuusalimia) wakati wa kuingia. Ni makuruhu kujenga mahali palipo juu; kwa sababu Ali(a.s) aliuona msikiti katika mahali palipo juu akasema: Kama Sinagogi yaani Hekalu la Kiyahudi. Kuna hadith inayosema: Nyumba hujengwa mahali palipo juu na msikiti hujengwa mahali tambarare. Vile vile ni makruhu kutengeneza mihrabu ndani yake; kwa sababu Amiril-Muminin alipokuwa akiiona husema: Kama kwamba ni madhabahu ya Mayahudi. Makusudio ya ya Mihrabu hii iliyo makuruhu, ni ile inayotokeza ndani ambayo huwadhikisha wenye kuswali, bali jamaa wamesema kuwa ni haramu,Ama mihrabu inayojitokeza nje haina ubaya wowote.

* 30 Amenakili mwenye Miftahul-Karama kutokana na wanachuoni umakaruhu wa kuiinua misikiti na wamesema, bali hujengwa kwa wastani; kama ambavyo imenukuliwa kutoka vitabu saba vya kifiqhi umakaruhu wa mihrabu yenye kutokeza. Mimi ninadhani kwamba Waislamu wanavyojihimu kujenga misikiti mikubwa ni kwa ajili ya kushindana na makanisa tu na kauli ya Amirul Miminin (kama sinagogi) inaashiria hilo.

﴿وَلِلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّـهِ إِنَّ اللَّـهَ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴾

115.Na Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu, basi mahala popote mnakoelekea ndiko kwenye uelekeo wa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua.

﴿وَقَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا سُبْحَانَهُ بَل لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ﴾

116. Na wanasema: Mwenyezi Mungu amejifanyia mtoto. Ameepukana na hilo. Bali ni vyake vilivyomo mbinguni na ardhini,Vyote vinamtii Yeye.

﴿بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ﴾

117.Mbunifu wa mbingu na ardhi; na anapotaka jambo basi huliambia tu kuwa, likawa.

NA MASHARIKI NA MAGHARIBI NI ZA MWENYEZI MUNGU

Aya ya 115-117

LUGHA

Mashariki ni mawiyo ya jua na mwezi, na Magharibi ni machweo. Mwenyezi Mungu amehusisha kutaja Mashariki na Magharibi tu bila ya Kusini na Kaskazini kwa sababu zinaingia sehemu zote, maana hakuna mahali kusiko chimbukiwa na jua na mwezi au kuchwea na jua. Kwa hiyo mgawanyo wa ardhi ni Mashariki na Magharibi tu.

MAANA

Na Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu, basi mahali popote mnakoelekea ndiko kwenye uelekeo wa Mwenyezi Mungu. Yaani ardhi na pande zote na vitu vyote ni vya Mwenyezi Mungu. Popote mtakapoabudu na popote mtakapoelekea kwa kukusudia ibada na radhi ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atawatakabalia. Basi mwenye kuzuiliwa kufanya ibada ndani ya msikiti, na aabudu popote anapopata na popote atakapoelekea, kwani ardhi yote ni msikiti na pande zote ni Qibla.

Mfasiri mmoja amesema kwamba Aya inahusika na upande tu, na sio mahali, yaani ni upande wowote tu, na wala sio mahali popote.Kwa sababu Mwenyezi Mungu amesema:Na Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu. Lakini mfasiri huyu amesahau kauli yake Mwenyezi Mungu: Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa (na) Mwenye kujua kwamba maadamu pande zote na sehemu zote ni za Mwenyezi Mungu, basi inasihi kumwabudu katika mahali popote na kuelekea pande zote kwa kuangalia kuwa kuenea kwa sababu ya kuhukumu ndio kuenea hukumu kwa kufuata sababu na kilichosababisha. Kwa maneno mengine ni kuwa: maadamu pande zote na mahali pote ni pa Mwenyezi Mungu, basi inasihi kuabudu popote na kuelekea upande wowote. Unaweza kuuliza: hakika dhahiri ya Aya inafahamisha kwamba Mukallaf ana hiyari katika swala yake kuelekea upande wowote, wala hana lazima ya kuelekea Al-Kaaba, jambo hilo ni kinyume na Waislamu wote?

Jibu : Ni kweli kuwa dhahiri Aya inafahamisha hivyo na inakusanya swala ya faradhi na sunna katika hali zote, lakini imethibiti kutoka kwa Mtume, Maimamu na kwa Ijmai kwamba swala ya faradhi haiswihi kama mtu akielekea pengine ikiwa anaweza kuelekea Al-Kaaba, na swala ya sunna inasihi kwa kuelekea popote katika hali ya kupanda kwenye chombo cha kusafiria na katika hali ya kutembea kwa miguu. Vile vile inaswihi kuswali swala ya faradhi kwa kuelekea upande wowote kwa yule aliyeshindwa kujua Qibla.

Kwa hadith hizi na Ijmai tunaihusisha kauli yake Mwenyezi Mungu:Popote mnapoelekea huko kuna radhi ya Mungu, na swala ya sunna katika hali ya kwenda na kupanda na swala ya faradhi kwa mwenye kuchanganyikiwa. Vile vile kutokana na hadith na Ijmai tunaihusisha Aya 149 ya Sura hii inayosema:Na popote wendako geuza uso wako kwenye msikiti mtakatifu (Masjidul-Haram), na swala ya faradhi katika hali ya hiyari; na tunaihusisha na swala ya sunna katika hali ya kutopanda chombo cha kusafiria.

* 31 Kwa hali hii linabainika kosa na kuchanganyikiwa katika kauli ya mwenye kusema kwamba kauli yake Mwenyezi Mungu:Geuza uso wako kwenye msikiti mtakatifu, imefuta hukumu ya kauli yake Mwenyezi Mungu:Popote mnapoelekea huko kuna radhi ya Mwenyezi Mungu . Kwa sababu sharti za kufuta ni kukanusha na kupingana kati ya yenye kufuta na yenye kufutwa; ambapo hali ya kuthibitisha na kukanusha inakuja katika maudhui moja. Umeshajua kwamba maudhui: elekeza uso wako kwenye msikiti mtakatifu, yanahusika na swala ya faradhi na sunna katika hali ya kutulia. Na maudhui ya: popote mnapoelekea huko kuna radhi ya Mwenyezi Mungu, yanahusika na isivyokuwa hivyo.

Na wanasema:Mwenyezi Mungu amejifanyia motto. Tumetangulia kueleza katika tafsiri ya Aya ya 113 kwamba: Mayahudi, Wakristo na washirikina, kila kundi lilisema kwamba liko kwenye haki na wengine si chochote. Kwa hivyo dhamiri katika kauli yake Mwenyezi Mungu:Na wanasema, inarudia kwenye makundi haya matatu. Imeelezwa katika Quran kwamba Mayahudi wanasema: Uzayr ni mtoto wa Mungu, Na Wakristo wanasema: Masih ni mtoto wa Mungu na Washirikina wa kiarabu walisema; Malaika ni watoto wa Mungu. Kwa hiyo sio kosa kuwa wanazungumziwa wote.

*31 Tazama tafsiri ya Aya inayofuatia 142 inayotimiza tafsiri hii katika kifungu cha; kwa nini swala iswaliwe kwenye upande maalum.Ameepukana na hilo . Ni tamko la kutakasa, Katika Aya nyengine ni:...Ameepukana kuwa na mtoto... (4:171).

Kwa sababu kupatikana mtoto kwa Mwenyezi (s.w.t.) Kutalazimisha mambo mengi ya kujihadhari kama ifuatavyo:-

Kwamba ambaye huzaliwa hana budi kuwa katika jinsi ya huyo aliyemzaa ili aweze kuzaa; na Mwenyezi Mungu hana jinsi.

Kuzaa kunalazimisha udugu, na udugu unahitaji kuwa na mwili; na Mungu sio mwili.

Sababu inayowajibisha kuzaa ni kumuhitajia mtoto; na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujitosha na viumbe vyote.

Ambaye anazaa hana budi kuwa amezaliwa; na Mwenyezi Mungu hakuzaliwa.

Amirul Muminin(a.s) amesema:Hakuzaliwa akawa na mshirika katika utukufu, Yaani kushirikiana na baba yake katika utukufu.Wala hakuzaa akawa mwenye kurithiwa kwa kufa. Yaani kuwa na mtoto atakayemrithi baada ya kufa.Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo kabisa. Jambo jengine ni kuwa kila kilicho katika mbingu na katika ardhi ni chenye kuumbwa na kumilikiwa na Mwenyezi Mungu; na chenye kumilikiwa hakiwezi kuwa mtoto wa Muumbaji. Wala Muumbaji hawezi kuwa ni baba wa mwenye kuumbwa mwenye kumilikiwa. Kwa hali hiyo inatudhihirikia njia ya kutoa dalili juu ya kukanusha Mungu kuwa na mtoto katika kauli yake.

Bali ni vyake vilivyomo mbinguni na ardhini. Vyote vinamtii Yeye. Yaani vinamfuata Yeye na kumtii. Unaweza kuuliza kwamba: herufi Ma, hutumiwa kwa kisicho na akili na neno qaanituuna hutumiwa kwa aliye na akili. Sasa imekuaje kitu kimoja mara nyingine kuwa katika ibara ya kisicho na akili na mara nyingine kuwa katika ibara ya kilicho na akili?

Jibu : Mbingu na ardhi inakusanya kuwa na akili na kutokuwa na akili; na, Aya imekusanya jumla mbili; ya kwanza imethibitisha ufalme wa vilivyokusanywa na mbingu na ardhi, na jumla ya pili imethibitisha kumtii Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo wakati Mwenyezi Mungu alipotaka kuelezea kumiliki, alielezea kwa kisichokuwa na akili, na alipotaka kuelezea twaa ameelezea kwa aliye na akili, kwa sababu twaa huwa ni kwa mwenye akili na mwenye hiyari.

MBUNIFU WA MBINGU NAARDHI

Neno: Badiu (Mbunifu) lina maana ya mtengenezaji ambaye ametengeneza yeye mwenyewe bila ya kuchukuwa kwa mwengine ni kama kauli yake Mwenyezi Mungu:Na utawa wameubuni. (57:27).

Kwa hivyo maana yanakuwa: Ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye mwanzilishi wa mbingu na ardhi, basi vipi anaweza kunasibishwa aliyemo ndani yake kuwa ni mwanawe?Na anapotaka jambo, basi, huliambia tu: Kuwa, likawa. Hili ni fumbo la ukubwa wa Mwenyezi Mungu na uweza wake; kwamba Yeye kwa kutaka tu, basi jambo huwa, ni sawa kuwe hakuna kitu chochote halafu kipatikane kwa kutaka kwake; au kuwe na kitu, lakini akataka kukigeuza.

Tumeeleza katika kufasiri Aya ya 26-27 kwamba: Mwenyezi Mungu ana matakwa aina mbili: Matakwa ya utengenezaji na matakwa ya kutoa sharia. Miongoni mwa matakwa ya utengenezaji ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

﴿إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ اللَّـهِ كَمَثَلِ آدَمَ خَلَقَهُ مِن تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُن فَيَكُونُ﴾

Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam, aliyemuumba kwa udongo kisha akamwambia kuwa, akawa. (3:59)

13

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KWANZA

AL - BAQARAH (NG’OMBE)

﴿وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تَذْبَحُوا بَقَرَةً قَالُوا أَتَتَّخِذُنَا هُزُوًا قَالَ أَعُوذُ بِاللَّـهِ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ ﴾

67.Na Musa alipowaambia watu wake: Hakika Mwenyezi Mungu anawaamrisha mchinje ng’ombe. Wakasema: Je! Unatufanyia mzaha? Akasema: Najikinga kwa Mwenyezi Mungu kuwa miongoni mwa wajinga.

﴿قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا فَارِضٌ وَلَا بِكْرٌ عَوَانٌ بَيْنَ ذَٰلِكَ فَافْعَلُوا مَا تُؤْمَرُونَ ﴾

68.Wakasema: Tuombee kwa Mola wako atupambanulie ni ng’ombe gani? Akasema: Hakika yeye anasema kwamba ng’ombe huyo si mpevu wala si mchanga, ni wa katikati baina ya hao. Basi fanyeni mnavyoamrishwa.

﴿قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا لَوْنُهَا قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ صَفْرَاءُ فَاقِعٌ لَّوْنُهَا تَسُرُّ النَّاظِرِينَ ﴾

69.Wakasema: Tuombee kwa Mola wako atupambanulie rangi yake ni ipi? Akasema: Yeye anasema ng’ombe huyo ni wa manjano, na rangi yake imeiva sana, huwapendeza wanaomtazama.

﴿قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ إِنَّ الْبَقَرَ تَشَابَهَ عَلَيْنَا وَإِنَّا إِن شَاءَ اللَّـهُ لَمُهْتَدُونَ ﴾

70.Wakasema: Tuombee kwa Mola wako atupambanulie ni vipi hali yake; hakika ng’ombe wamefanana na hakika sisi kama Mwenyezi Mungu akipenda (tutakuwa) ni wenye kuongoka.

﴿قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا ذَلُولٌ تُثِيرُ الْأَرْضَ وَلَا تَسْقِي الْحَرْثَ مُسَلَّمَةٌ لَّا شِيَةَ فِيهَا قَالُوا الْآنَ جِئْتَ بِالْحَقِّ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُوا يَفْعَلُونَ ﴾

71.Akasema: Yeye anasema: Kuwa huyo si ng’ombe anayefanyishwa kazi ya kulima ardhi wala kutilia maji mimea, mzima, hana kipaku. Wakasema: Sasa umeleta haki. Basi wakamchinja, na walikaribia wasifanye.

﴿وَإِذْ قَتَلْتُمْ نَفْسًا فَادَّارَأْتُمْ فِيهَا وَاللَّـهُ مُخْرِجٌ مَّا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴾

72.Na mlipoiua nafsi, kisha mkahitilafiana kwa hayo, na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuyatoa hayo mliyokuwa mkiyaficha.

﴿فَقُلْنَا اضْرِبُوهُ بِبَعْضِهَا كَذَٰلِكَ يُحْيِي اللَّـهُ الْمَوْتَىٰ وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴾

73.Tukasema: Mpigeni kwa kipande chake (huyo ng’ombe). Ndivyo hivi Mwenyezi Mungu huwahuisha wafu; na anawaonyesha ishara zake ili mpate kufahamu.

MWENYEZI MUNGU ANAWAAMRISHA MCHINJE NG’OMBE

Aya 67 - 73

MUHTASARI WA KISA

Aya hizi tukufu haziwezi kufahamika maana yake bila ya kufahamu tukio lililoteremshiwa. Kwa ufupi tukio lenyewe ni hili: Mzee mmoja tajiri katika Waisrail aliuliwa na binamu yake kwa tamaa ya kurithi mali yake; kisha akadai kuwa ameuliwa na watu wengine, na wakatakiwa walipe fidia. Ukazuka ubishi mkubwa na wakamwendea Musa(a.s) . Kwa vile hakukuwa na ushahidi wowote wa kugundua mambo walimtaka Musakama kawaida yao - kumwomba Mwenyezi Mungu awabainishie muuaji. Ndipo Mwenyezi Mungu akampa wahyi kuwa wachinje ngombe na sehemu ya huyo ngombe wampige yule aliyeuliwa atafufuka na ataeleza yule aliyemuua. Baada ya udadisi mwingi walifanya vile walivyotakiwa kufanya na yule aliyeuliwa akafufuka na akamtaja aliyemuua.

MAANA

Wakasema: Je unatufanyia mzaha? Yaani tunakuuliza kuhusu kuuliwa mtu nawe unatuamrisha kuchinja ngombe hakika huu ni mzaha. Akasema: Najikinga kwa Mwenyezi Mungu kuwa miongoni mwa wajinga. Yaani mimi sifanyi mzaha, hata katika mambo yasiyokuwa ya kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu, sembuse hayo ya kufikisha neno la Mungu ambaye umetukuka msemo Wake? Ilikuwa inatosha tu wamchinje ngombe yoyote, kwa sababu waliamrishwa wachinje ngombe tu; lakini kwa udadisi wao.

Wakasema:Tuombee Mola wako atupambanulie ni ng’ombe gani? Wakajibiwa kuwa ni ambaye yuko katikati si mkubwa wala si mdogo, basi fuateni amri wala msingoje, lakini wakarudia tena kuuliza Wakasema:Tuombee Mola wako atupambanulie rangi yake ni ipi? Akasema: ni wa manjano, lakini tena wakazidi kudadisi na kuuliza swali mara ya tatu, kwa sababu ngombe walio katika rangi hii na umri huu ni wengi. Akawaambia kuwani yule asiyefanyishwa kazi na asiyekuwa na kasoro yoyote. Wakamtafuta mpaka wakampata, wakamchinja; kisha wakampiga maiti kwa kipande cha nyama akafufuka na siri ikafichuka baada ya kumtaja aliyemuua. Ndivyo hivi Mwenyezi Mungu huwahuyisha wafu na anawaonyesha ishara zake ili mpate kufahamu.

Yaani huku kumfufua huyu aliyeuliwa ni ushaidi wazi na dalili wazi ya kufufuliwa watu baada ya kufa, kwa sababu mwenye kuweza kufufua nafsi moja hawezi kushindwa na nyingine. Je, baada ya ushahidi huu wa kuona kwa macho mnaweza mkakanusha na kutia shaka na kuasi? Lakini pamoja na hayo na yasiyokuwa hayo nyoyo zenu zimesusuwaa, bali zimesusuwaa zaidi na zimekuwa ngumu zaidi kuliko jiwe, kama itakavyoeleza Aya inayofuatia. Baada ya maelezo tuliyoyaeleza kuhusu Mayahudi haiwezekani tena kuuliza swali lolote kuwa,kwa nini Mwenyezi Mungu hakumfufua yule aliyeuliwa tangu mwanzo, na hali Mwenyezi Mungu alikuwa anaweza kufanya hivyo? Vipi anaweza kufufuka mtu kwa kupigwa na nyama ya ngombe? Kwa nini ilikuwa lazima ngombe huyo? Kisha kuna faida gani ya kumpiga na ngombe huyo aliyeuliwa?

Maswali yote haya hayana nafasi baada ya kuthibitisha kuwa Mwenyezi Mungu aliwafanyia Mayahudi mambo maalum wao tu; na kwamba Yeye kwa upande huu ndio amewafadhilisha juu ya watu wote.

﴿ ثُمَّ قَسَتْ قُلُوبُكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ فَهِيَ كَالْحِجَارَةِ أَوْ أَشَدُّ قَسْوَةً وَإِنَّ مِنَ الْحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنْهُ الْأَنْهَارُ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخْرُجُ مِنْهُ الْمَاءُ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَهْبِطُ مِنْ خَشْيَةِ اللَّـهِ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴾

74. Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, zikawa kama mawe au ngumu zaidi; kwani kuna mawe mengine yanayobubujika mito ndani yake, na kuna mengine yanayopasuka yakatoka maji ndani yake; na kuna mengine huanguka kwa sababu ya kumwogopa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu si Mwenye kughafilika na mnayoyafanya.

KUWA NGUMU NYOYO

Aya 74

Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo. Yaani ilikuwa ni wajibu kwa wazee wenu - enyi Mayahudi wa Madina - wazingatie na zilainike nyoyo zao baada ya kushuhudia waliyoyashuhudia katika miujiza na maajabu; ambayo miongoni mwake ni kufufua aliyeuliwa, lakini, kwa ukhabithi wao, wakafanya kinyume na vile inavyotakiwa; wakafanya ufisadi na nyoyo zao zikasusuwaa kama kwamba zimetokana na mawe, bali baadhi yake ni ngumu zaidi kuliko mawe, kwani kuna mawe, mengine yanayobubujika mito ndani yake, na kuna mengine yanayopasuka yakatoa maji. Unaweza kuuliza: Mito ni maji, sasa mbona yametajwa maji na mito? Inawezekana kutofautisha jengo na nyumba? Jibu: Hakika Aya tukufu imegawanya maji kwenye mafungu mawili mengi ambayo ni mto, na machache ambayo ni chemchem. Ibara ya mgawanyiko imekuja kwa tamko la maji, kwa hivyo kumetajwa kububujika maji kwa maana ya wingi na kupasuka kwa maana ya uchache.

Vyovyote iwavyo, lengo la Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwa amefadhilisha aina za majabali na mawe kuliko nyoyo za Mayahudi, ni kwa sababu jiwe linaweza kupasuka likatoa maji, na kwamba jiwe mara nyingine huwa linatikisika likaondoka pale lilipokuwa. Lakini nyoyo za Mayahudi hazina hata chembe ya kheri wala hazitikiswi na uzuri wowote na hazielekei kwenye uongofu. Unaweza kuuliza kuwa mawe hayana uhai wala utambuzi, kwa hiyo hayawezi kumwogopa Mwenyezi Mungu, sasa kuna wajihi gani katika kauli yake Mwenyezi Mungu: Na kuna mengine huanguka kwa sababu ya kumwogopa Mwenyezi Mungu.

Swali hilo limejibiwa kwa majibu mengi, yaliyo karibu zaidi ni mawili: Kwanza, hayo ni makisio kwamba lau kama mawe yangelikuwa na fahamu na akili kama Mayahudi, yangelianguka kwa kumwogopa Mwenyezi Mungu. Mifano hii ni mingi sana katika maneno ya waarabu. Jibu jingine, ni kwamba ni kawaida ya mawe kumnyenyekea Mwenyezi Mungu ambaye ndiye aliyeumba maumbile yote. Mwenyezi Mungu anasema:

﴿تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ وَلَـٰكِن لَّا تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا﴾

Zinamsabihi (zinamtakasa) mbingu zote saba na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake, na hakuna chochote ila kinamsabihi kwa sifa Zake njema. (17:44)

Utakuja ufafuanuzi tutakapofika Aya hiyo inshallah.

TOFAUTI YA HULKA

Anaweza kuuliza muulizaji: Je ndani ya binadamu kuna nguvu inayompa msukumo wa harakati; au yanayompa harakati ni matukio ya nje, kiasi ambacho ndani ni tawi lakini nje ndio shina? Au kila moja ni shina hiyo yenyewe peke yake, kwamba mtu mara nyingine hupata msukumo kutoka ndani na mara nyingine nje au mara nyingine ndani na nje? Kama tutafaradhia kuwa ndani ya binadamu kuna msukumo wa aina ya peke yake usioshirikiana na kitu kingine, Je msukumo huo ni wa aina moja kwa watu wote au kila mtu ana wa aina yake? Jibu: Hakika mtu anakuwa mtu kwa silika yake na nguvu yake ya kiroho. Lau tunavitoa vitu hivyo au tanavizuia utendaji kazi wake, basi binadamu atakuwa ni kama ganda tupu au unyoya katika mavumo ya upepo. Ndio! Ni kweli kwamba nguvu za kindani zinafanya kazi pamoja na matukio ya nje na kuathirika nazo, lakini kufanya kazi ni kitu kingine na kuathirika ni kitu kingine. Kwa mfano, silika ya kuchunguza inakuwa pamoja na mtu na ndio maana mtoto anakuwa mdadisi kwa umbile lake; bali sili- ka hiyo ni katika mambo yanayomuhusu mtu. Kisha silika hii inakua na kukoma kwa kuona matukio ya nje vilevile kwa utafiti na uvumbuzi; na kwa kukua kwake binadamu anaweza kuathirika vitu vya nje kulingana na haja yake na matakwa yake. Kwa hivyo harakati za binadamu zinachimbuka kutoka ndani na nje, yaani kutoka katika nafsi yake na kutoka katika matukio.

Hapa kuna kifungu cha tatu ambacho nimekigundua kutokana na majaribio yangu maalum; Kifungu hicho nimekipa jina Tawfik katika heri na kufaulu. Kifungu hiki hakitokani na nafsi wala matukio, bali kinatokana na nguvu iliyojificha ambayo iko katika ulimwengu uliojificha (usiojulikana), inawaandalia baadhi ya watu njia ya heri na inaingia katika kuwaelekeza watu kwenye lile linalomridhshia Mwenyezi Mungu bila ya mtu kutambua. Ni kawaida kwamba hatanikubalia juu ya hili isipokuwa yule anayemwamini Mwenyezi Mungu na hekima yake na kumpa cheo kinachomstahiki. Ninakiri kwamba mimi sina ufahamu wa ujumla wa kifungu hiki, isipokuwa nimekifahamu kutokana na majaribio yangu; kama nilivyotangulia kueleza.23 Ama jawabu la kuwa je, watu wanakuwa na namna moja katika silika na sifa za kinafsi, linataka ufafanuzi. Katika sifa za kinafsi kuna zile ambazo watu wanashir-ikiana; kama vile utambuzi wa kupambanua kati ya haki na batili, heri na shari, na kati ya baya na zuri.

* 23 Jambo la kushangaza lilotokea kwa sadfa.Baada ya kuandika maneno haya nikasoma nakala fulani, kuwa kiongozi mmoja wa kijeshi wa Kiingereza maarufu sana anayeitwa Montgomery alijieleza kwa kusema: Hakika yeye ni askari mdogo chini ya uongozi wa nguvu kuu; na kwamba yeye hakushinda katika vita isipokuwa kwa matakwa ya kudra hiyo; na kwamba bila ya kuamini nguvu hii kubwa yenye akili, haiwezekani kushinda katika vita vya dunia vya pili. Yeye anaamini kwamba kuna nguvu iliyofichika ambayo iliwaandalia njia ya kumshinda Romel, ambaye alikuwa akiitwa mbweha wa jangwani, naye alikuwa amirijeshi mkubwa wakati huo. Lau si ushirikiano huu isingeliwezekana kwa vyovyote vile kuthibitisha uovu na wema na isingelifaa kwetu kumlaumu au kumsifu mtu kwa kufanya jambo fulani. Vile vile kuna ushirikiano katika kujipenda na upendo wa mzazi na mwana, na mengineyo ambayo wanayo watu wote, ijapokuwa kuna tofauti ya wingi na uchache.

Kuna sifa nyingine za kinafsi, ambazo watu wanatofuatiana kama vile; ushujaa, woga, ukarimu, ubahili, ugumu wa moyo, ulaini wa moyo, udhaifu wa matakwa na nguvu yake na kupondokea kwenye heri au shari. Watu katika sifa hizi wanatofuatiana, kila mtu sio karimu au bahili,wala mwoga au mshari. Unaweza kuuliza: Hakika kauli yako si inakhalifu kawaida maarufu iliyozoeleka, kuwa hakuna mtu yoyote isipokuwa ana pande mbili, mzuri na usiokuwa mzuri; na wewe umetilia mkazo upande mmoja tu, na ukaufinyia jicho upande mwingine?. Jibu: Hakika uvivio wa heri ambao mara nyengine tunauona kwa baadhi ya watu wa shari, unakuwa umeingia kighafla tu, bila ya kukusudiwa; na kwamba suala la kuwa kila mtu ana pande mbili linawezekana kwa wasiokuwa Mayahudi.Kwa sababu, Mayahudi hawana lolote wao isipokuwa uovu tu; hawana wema kabisa. Ushahidi wa hayo ni Tawrat yao, Quran tukufu na historia sahihi. Vile vile vitendo vyao katika Palestina na kwingineko, mambo ambayo ni dalili wazi kwamba dini, maadili na mfungamano wote wa kiutu, kwao ni biashara na manufaa tu.Maudhui haya tutayarudia kila itakapolazimika.

﴿أَفَتَطْمَعُونَ أَن يُؤْمِنُوا لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِن بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ﴾

75.Je mna matumaini ya kwamba wataamini na hali baadhi yao walikuwa wanasikia maneno ya Mwenyezi Mungu kisha wanayabadili baada ya kuwa wameyafahamu na hali wanajua?

HAKUNA MATUMAINI

Aya 75

MAELEZO

Kila mwenye ujumbe fulani huwa anapupia watu wauamini ujumbe huo. Kwa hivyo anaueneza kwa matumaini ya kupata wafuasi wengi, na anahimili taabu na mashaka katika hilo, kama alivyofanya Mtume(s.a.w.w) na sahaba zake, waliueneza mwito wa Uislamu katika pembe zote kwa kutaraji kupata wafuasi. Kulikuwa na mfungamano wa kijirani, kibiashara na hata kunyonyeshana watoto kati ya Ansar na Mayahudi. Hivyo wakawalingania kwenye Uislamu kwa amri ya Mtume. Wakawatolea dalili kwa hoja zinazoingia akilini na kwa mantiki mazuri, wakatumai kwamba nyoyo zao zitashtuka, hasa kwa kuzingatia kwamba wao ni watu wa Kitabu na kwamba sifa za Muhammad(s.a.w.w) zimetajwa kwa uwazi katika Tawrat yao. Walipoendelea Wayahudi kukaidi mwito wa Uislamu na kuendelea kukufuru na kuipinga haki, ndipo Mwenyezi Mungu alipomwambia Mtume wake kwa kusema: Je mnatumaini nyinyi Waislamu ya kwamba watawaamini hao Mayahudi, na hali wazee wao hawa Mayahudi walikuwa wakisikia maneno ya Mwenyezi Mungu kutoka kwa Nabii Musa(a.s) pamoja na miujiza, lakini wakiyabadilisha na kuyageuza vile matamanio yao yanavyotaka pamoja na kujua kuwa hayo maneno ni ya haki?

Kwa hivyo, hali ya Wayahudi wa Madina ni kama hali ya wazee wao waliopita, ambao walibadilisha halali ikawa haramu na haramu kuwa halali kwa kufuata matamanio yao na wakabadilisha sifa za Muhammad(s.a.w.w) zilizopokewa katika Tawrat, ili isiweko hoja juu yao. Mwenye Majmaul-Bayan anasema: Katika Aya hii kuna dalili juu ya ukubwa wa dhambi ya kuibadilisha sheria. Na dhambi hiyo inapatikana katika kuleta Bida katika fatwa au hukumu na mambo yote ya kidini. Kuongezea juu ya maneno hayo ya mwenye Majmau ni kuwa Aya hii ni dalili juu ya kuwa mwenye kufuata upotevu kwamba sio kuwa anajifanyia uovu yeye mwenyewe tu, bali athari yake inaenea kwa vizazi, kama ilivyoelezwa katika Hadith.

﴿وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَا بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ قَالُوا أَتُحَدِّثُونَهُم بِمَا فَتَحَ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ لِيُحَاجُّوكُم بِهِ عِندَ رَبِّكُمْ أَفَلَا تَعْقِلُونَ﴾

76. Na wanapokutana na wale walioamini husema: Tumeamini. Na wanapokuwa peke yao, wao kwa wao husema: Mnawaambia yale aliyowahukumia Mwenyezi Mungu ili wapate kuhojiana nanyi mbele ya Mola wenu? Je,hamna akili?

﴿أَوَلَا يَعْلَمُونَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ﴾

77.Hawajui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua wanayoyayafanya siri na wanayoyadhihirisha?

WANAPOKUTANA NAWALE WALIOAMINI

Aya 76 - 77

MAELEZO

Baadhi ya Mayahudi walikuwa wakifanya unafiki na uwongo kwa Waislamu na wakisema: Sisi tunaamini yale mnayoyaamini nyinyi na tunashuhudia kuwa Muhammad ni mkweli katika maneno yake, kwani tumekuta katika Tawrat sifa zake. Lakini wanafiki hao wanapochanganyikana na viongozi wao, basi viongozi wanawalaumu kwa kusema: Vipi mnawahadithia wafuasi wa Muhammad yale aliyowahukumia Mwenyezi Mungu? Hivi hamfahamu kwamba huko ni kukubali nyinyi wenyewe kwamba mko katika batili na wao wako katika haki? Hawajui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua wanayoyafanya siri na wanayoyadhihirisha? Yaani kwa vyovyote watakavyojaribu wanafiki, kuficha unafiki wao na viongozi wapotevu wanavyowaelekeza wafuasi wao, lakini kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakifichiki chochote. Basi nyinyi Mayahudi mnaficha njama zenu, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamfahamisha Mtume wake Muhammad(s.a.w.w) na anavifagia vitimbi vyenu.

﴿وَمِنْهُمْ أُمِّيُّونَ لَا يَعْلَمُونَ الْكِتَابَ إِلَّا أَمَانِيَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ ﴾

78.Na wako miongoni mwao wasiojua kusoma; hawajui kitabu isipokuwa matamanio tu nao hawana isipokuwa kudhani tu!

﴿فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَـٰذَا مِنْ عِندِ اللَّـهِ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا يَكْسِبُونَ﴾

79.Basi ole wao wanaoandika kitabu kwa mikono yao. Kisha wakasema hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu ili wachukue kwacho thamani ndogo. Basi ole wao kwa yale iliyoyaandika mikono yao. Na ole wao kwa yale wanayoyachuma.

WAKO MIONGONI MWAO WASIOJUA KUSOMA

Aya 78 79

MAELEZO

Na wako miongoni mwao wasiojua kusoma. Yaani katika Mayahudi kuna wale waliokuwa hawakusoma; hawajui chochote katika dini ya Mwenyezi Mungu na kwamba mambo yao zaidi ni ya kudhania dhania tu, bila ya kutegemea elimu. Kimsingi ni kwamba ingawa maelezo haya yamekuja kwa sababu ya Wayahudi, lakini shutumu inamwendea kila mjinga.

TAFSIRI INA MISINGI NA KANUNI

Katika Aya hii kuna dalili wazi kwamba haifai kufasiri Quran na Hadith kwa kudhania na kukisia, bali hapana budi lazima mfasiri awe na elimu ya kanuni za tafsiri na misingi yake, na kuchunga kanuni hizi katika kubainisha makusudio ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kujihadhari na kuwazulia. Sharti la kwanza la kufaa kufasiri ni kujua kusoma na kuandika; kisha hujua elimu za Kiarabu kwa aina zake zote, ambazo ni kujua msamiati, Sarfa, Nahw, Bayan, Fiqh na misingi yake. Vile vile kujua elimu ya Tawhid na kuongezea elimu nyingine ambazo zitamsaidia katika kufasiri baadhi ya Aya. Yote haya mfasiri anaweza kuyajua kwa kuwaendea wenye kuhusika nayo. Basi ole wao wanaoandika kitabu kwa mikono yao. Hapa Mwenyezi Mungu anamkemea kila anayemnasibishia yale asiyokuwa nayo kwa ajili ya kuchukua thamani kwa shetani. Si lazima thamani iwe ni mali (pesa) tu; inaweza kuwa ni kupata jaha au chochote katika anasa za kidunia.

Mwenyezi Mungu amekariri makemeo mara tatu katika Aya moja kwa kutilia mkazo kwamba kumzulia yeye Mwenyezi Mungu na Mtume ni katika maasi makubwa na yenye adhabu kali; kama alivyosema mahali pengine:

﴿قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ وَيْلَكُمْ لَا تَفْتَرُوا عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا فَيُسْحِتَكُم بِعَذَابٍ وَقَدْ خَابَ مَنِ افْتَرَىٰ﴾

Ole wenu msimzulie uwongo Mwenyezi Mungu asije akawafutilia mbali kwa adhabu, Na ameruka utupu anayezua uwongo. (20:61)

MWANACHUONI HAWEZI KUHUKUMU KWAMATUKIO

Tunadokeza kwa mnasaba huu kwamba mwanachuoni, kwa namna yoyote atakavyokuwa na elimu, ni juu yake kutomnasibishia chochote Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kwamba kitu hicho kinatoka katika Lawh Mahfudh. Akitoa fatwa kwa uhalali au uharamu; au kuhukumia kitu kuwa ni haki; au kufasiri Aya au Hadith, basi ni juu yake kuifanya hukumu yake hiyo, fatwa yake au tafsiri yake kuwa ni rai yake tu. Inaweza kuwa ni makosa au sawa. Hapo ndio atakuwa anakubaliwa msamaha mbele ya Mwenyezi Mungu kama akijitahidi kadiri ya uwezo wake. Lakini kama hakujitahidi sana au amejitahidi sana, lakini akasema kuwa kauli yake hiyo ni kauli ya

* 24 W amethibitisha wenye kuhusika na historia ya lugha na ada zake kwamba Tawrat ya sasa, ambayo Wayahudi wanaitakidi kuwa iliteremshwa na Mwenyezi Mungu kwa Musa, imetungwa. W atafiti wametoa hakika hii kutokana na muundo wa lugha ulivyo na ustawi wa kijamii na wa kisiasa ambao uko kinyume na Tawrat. Tutarudia kueleza maudhui haya kwa upana zaidi Inshallah. Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi atakuwa ni sawa na wale wanaomzulia Mwenyezi Mungu uwongo, ajapokuwa ni mwanachuoni wa wanachuoni. Kwa sababu mwanachuoni hatoi fatwa ya kweli wala hukumu ya kweli,bali anaitikadi tu kuwa ni haki. Huu ndio msingi wa kwamba yeye sio maasum.

﴿وَقَالُوا لَن تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَّعْدُودَةً قُلْ أَتَّخَذْتُمْ عِندَ اللَّـهِ عَهْدًا فَلَن يُخْلِفَ اللَّـهُ عَهْدَهُ أَمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ﴾

80.Na walisema: Hautatugusa moto isipokuwa kwa siku chache tu. Sema: Je, mmepata ahadi kwa Mwenyezi Mungu Kwa hivyo hatakhalifu ahadi yake.Au mnamsingizia Mwenyezi Mungu mambo msiyoyajua?

﴿بَلَىٰ مَن كَسَبَ سَيِّئَةً وَأَحَاطَتْ بِهِ خَطِيئَتُهُ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴾

81. Ndiyo, wanaochuma ubaya na makosa yao yakawazunguka, hao ndio watu wa motoni; humo watadumu.

﴿وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴾

82.Na wale walioamini na kutenda mema, hao ndio watu wa peponi, watadumu humo.

WALISEMA HAUTATUGUSA MOTO WA JAHANNAM

Aya 80 - 82

Na walisema: Hautatugusa moto isipokuwa kwa siku chache tu Mayahudi wanadai kwamba wao ni watoto wa Mungu na taifa lake teule na kwamba watu wote ni watoto wa shetani, isipokuwa wao tu, na ni mataifa yaliyotupiliwa mbali. Kwa hivyo ati Mwenyezi Mungu hatawaweka milele motoni, isipokuwa atawaadhibu kwa adhabu hafifu tena kwa muda mfupi, kisha atawaridhia. Yaani kwamba Mwenyezi Mungu anawaendekeza na kuuendekeza ukoloni wa kizayuni ambao unaikalia ardhi ya Palestina. Sema: Je, mmepata ahadi kwa Mwenyezi Mungu. Yaani waambie ewe Muhammad, kwamba madai yao haya ni porojo tu, na kama si hivyo, basi ni ahadi gani mliyowekeana na Mwenyezi Mungu? Madai yao haya, hayafahamishi chochote zaidi ya kudharau kwao madhambi na kufanya uovu.

Mtume mtukufu(s.a.w.w) anasema:Hakika mumini anaona dhambi yake ni kama jiwe anaogopa lisimwangukie na kwamba kafiri anaona dhambi yake ni kama nzi tu aliyepitia kwenye pua yake....

Anasema Amirul Muminin(a.s) :Dhambi kubwa zaidi ni ile iliyodharauliwa na mwenye kuifanya.

Kauli yake Mtume mtukufu(s.a.w.w) : Kama kwamba dhambi ni nzi anayepita juu ya pua ya mwenye dhambi. Inafanana kabisa na ya Mayahudi ambao wanadai kwamba wao ni watoto wa Mwenyezi Mungu wenye kutendekezwa. Huenda haya yakamnufaisha na kumzindua yeyote ambaye anapuuza dhambi kwa kutegemea utukufu wa nasabu. Mwenye kujitegemea yeye mwenyewe tu wala asihisi makosa ya nafsi yake, na asikubali nasaha za mwingine, basi ni muhali kuweza kuongoka kwenye heri. Hakika mwenye akili hajiangalii mwenyewe tu kwa kujihadaa na ndoto zake, bali daima anakuwa na msimamo wa kujilaumu makosa yake na kupambanua yale aliyonayo na yale anayotakiwa awe nayo. Vile vile huitoa nafsi yake na fikra za kitoto na mawazo ya kishetani. Kwa hali hii pekee ndio atakuwa anafaa kuitwa mtu kwa maana sahihi. Kuna hadith tukufu inayosema: Mwenye kujiona kwamba yeye ni mwovu, basi ni mwema.

Ndiyo, wanaochuma ubaya na makosa yao yakawazunguka, hao ndio watu wa motoni na humo watadumu. Ubaya ni shirk na madhambi mengineyo, lakini makusudio yake hapa yanahukumu shirk tu! Kwa kulinganisha na kauli yake Mwenyezi Mungu hao ndio watu wa motoni humo watadumu. Mwenye Majmaul-Bayan anasema: Makusudio ya ubaya kuwa ni shirk ndiyo yanayoafiki, kwa sababu dhambi nyingine yoyote haiwajibishi kudumu motoni. Na wale walioamini na kutenda mema hao ndio watu wa peponi watadumu humo. Aya hii tukufu inafahamisha kuwa kuokoka na adhabu ya Mwenyezi Mungu kesho kutatokana na imani sahihi ikiambatana na matendo mema. Hadith tukufu inasema: Abu Sufyani Athaqafiy, alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Niambie neno katika Uislamu ambalo sitamuuliza yeyote baada yako.Akasema Mtume:Sema: Nimemwamini Mwenyezi Mungu, kisha ufuate unyoofu (msimamo).

Katika hadith yake hii Mtume(s.a.w.w) anaelezea Aya inayosema:

﴿إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ﴾

Wale waliosema: Mola wetu ni Mwenyezi Mungu kisha wakawa na unyoofu hao huwateremkia malaika (wakawambia): Msiogope wala msihuzunike, na furahini kwa pepo mliyokuwa mkiahidiwa. (41:30).

Makusudio ya kuwa na unyoofu katika Aya na Hadith, ni kuwa katika msimamo wa kufanya amali kwa mujibu wa Quran na hadith za Mtume(s.a.w.w) .

MWISLAMU NA MUUMINI

Mwislamu kwa kuangalia muamala wake na kuthibiti Uislamu wake, anagawanyika kwenye mafungu mawili:

Kwanza : kumkubali Mwenyezi Mungu kuwa ni mmoja na kukubali Utume wa Muhammad bila ya kuangalia itikadi yake na amali (matendo) yake. Lakini ni sharti asikanushe zile dharura za dini, kama ulazima wa swala na uharamu wa zinaa na pombe. Huyu ndiye anayejulikana kwa Waislamu kuwa yeye ni Mwislamu atafanya na kufanyiwa mambo ya Kiislamu; kama kurithi, kuoa, na kuzikwa kiislamu, ikiwa ni pamoja na kumwosha, kumtia sandani, kumswalia na kumzika katika makaburi ya Waislalmu, anafanyiwa hayo kwa vile amepiga shahada.

Pili : ni kuamini na kushikamana na Uislamu kwa misingi na matawi; hakanushi hukumu yoyote katika hukumu za Kiislamu, wala hafanyi uasi wa hukumu katika hukumu za sheria. Huyu ndiye Mwislamu wa kweli (muumin) mbele ya Mwenyezi Mungu na watu, bali ni Mwislamu mwadilifu ambaye zimethibiti kwake athari zote za uadilifu wa Kiislamu duniani na akhera. Athari za dunia ni kukubaliwa ushahidi wake, kufaa kuswalisha, kuchukua hukumu zake na fatwa zake akiwa ni mujtahidi. Ama athari za kiakhera ni kule kuwa juu hadhi yake na thawabu. Mumin ni yule mwenye kukiri kwa ulimi na kusadikisha kwa moyo wake shahada mbili, wala haitoshi kukiri kwa ulimi tu au kusaidikisha kwa moyo tu, bali hapana budi yote mawili yaende sambamba. Kwa hivyo kila mumin ni Mwislamu, lakini si kila Mwislamu ni mumin.

Hapa inatubainikia kwamba amali njema haiitwi imani, kwa dalili kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Ameleta kiunganishi baina ya imani na amali njema kwa maana ya kuwa ni vitu viwili tofauti. Hata hivyo amali njema inaingia katika ufahamu wa uadilifu kama tulivyoonyesha. Utakuja ufafanuzi wake mahali pake. Mafaqihi wa kishia wanahusisha tamko la mumin kwa yule anayeamini Maimamu kumi na wawili, wakisema zaka inapewa mumin, na mwenye kuswalisha awe mumin, basi wanakusudia yule mwenye kuamini maimamu kumi na wawili tu. Istilahi hii wanahusika nayo mafaqih tu. Lakini hata huyo fakihi wa Kishia kama akizugumzia mumin katika mswala yasiyokuwa ya kifikihi, basi huwa anakusudia kila mwenye kukiri shahada mbili na kuzisadikisha kwa moyo; hata kama siye mwenye kuamini Maimamu kumi na wawili.

Kwa vyovyote ilivyo Uislamu na imani kwa maana tuliyoyaelezea, hautamuokoa mtu na adhabu ya Mwenyezi Mungu kesho, isipokuwa uwe pamoja na unyoofu ambao ni kufanya amali kulingana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume Wake(s.a.w.w) .

MWENYE MADHAMBI MAKUBWA

Mafakihi wameyagawanya madhambi katika mafungu mawili Makubwa; kama kunywa pombe. Na madogo kama kukaa kwenye meza ya pombe bila kunywa. Utakuja ufafanuzi wa madhambi makubwa na madogo Inshallah, katika Aya isemayo:Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu; isipokuwa makosa hafifu...

Wamehitalifiana Waislamu katika yule mwenye kukiri shahada mbili na akafanya madhambi makubwa, Je, yeye ni kafiri atakayebakia milele motoni au yeye ni mwislamu fasiki ambaye ataadhibiwa kiasi anachostahili, kisha atiwe peponi? Khawarij wamesema kuwa atabakia milele motoni.Shia, Ashari, Masahaba wengi na Tabiin, wamesema atatolewa motoni. Mutazila wamezusha fikra ya tatu ya kuthibitisha mawili, yaani hatakuwa kafiri wala Mumin. Allama Hilli ametoa dalili katika sherehe ya Tajrid juu ya ushahidi wa kauli ya kuwa mwenye madhambi makubwa ni fasiki hatokaa milele motoni, kuwa: Lau atabakishwa milele motoni, ingelazimika mwenye kumwabudu Mwenyezi Mungu muda wa umri wake wote; kisha akamuasi mwisho wa umri wake mara moja tu, pamoja na kubakia na imani yake, aingie motoni milele, awe sawa na yule aliyemshirikisha Mwenyezi Mungu katika umri wake wote. Na hilo ni muhali na haliingii akilini.

Hapana mwenye shaka kwamba ovu moja haliwezi kuondoa mema yote, bali ni kinyume; kama alivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t). Kwa ajili hiyo basi, inapasa kulichukulia neno ubaya katika Aya (Na wanaochuma ubaya na makosa yao yakawazunguka, hao ndio watu wa motoni, watadumu humo), kuwa na maana ya shirk. Kama ambavyo Aya inayofuatia hiyo (Na wale walioamini na kutenda mema hao ndio watu wa peponi, watakaa humo milele) inafahamisha kwamba mwenye kufanya madhambi makubwa ataingia peponi,

* 25 Aya hii tukufu inakuwa ni jibu la yule anayesema: Katika madhambi hakuna kubwa wala dogo, bali yote ni makubwa. Jibu lenyewe ni tamko,Lamam, lenye maana ya uhafifu. wala hatakaa milele motoni. Kwa sababu Aya ile inamhusu pia mwenye kuamini na akafanya amali njema kisha akafanya madhambi makubwa na wala asitubie.

MAYAHUDI TENA

Madai ya Mayahudi kwamba wao ni watoto wa Mungu na taifa teule, ni kwamba dini na maadili yake, katika itikadi yao, ni kazi ya kibiashara na manufaa ya kiutu. Vinginevyo itakuwa ni bure tu. Unaweza kusema, hayo hayahusiani na Mayahudi tu, bali wako watu wa namna hiyo. Jibu, ndio, lakini tofauti iliyopo ni kwamba Mayahudi wana hasadi kwa watu wote isipokuwa wao.


10

11

12

13

14

15