TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA Juzuu 1

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA0%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA Mwandishi:
Kundi: tafsiri ya Qurani

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA

Mwandishi: Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya
Kundi:

Matembeleo: 35403
Pakua: 2975


Maelezo zaidi:

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
Juzuu 9 Juzuu 10 Juzuu 11
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 20 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 35403 / Pakua: 2975
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA Juzuu 1

Mwandishi:
Swahili

17

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KWANZA

AL - BAQARAH (NG’OMBE)

﴿ وَقَالَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ لَوْلَا يُكَلِّمُنَا اللَّـهُ أَوْ تَأْتِينَا آيَةٌ كَذَٰلِكَ قَالَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّثْلَ قَوْلِهِمْ تَشَابَهَتْ قُلُوبُهُمْ قَدْ بَيَّنَّا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ﴾

118. Na walisema wale wasiojua: Mbona Mwenyezi Mungu hasemi nasi au kutufikia ishara (tunazozitaka) Hivyo hivyo walisema wale waliokuwa kabla yao mfano wa kauli yao (hii).Nyoyo zao zimefanana. Hakika sisi tumezibainisha ishara kwa watu wenye kuyakinisha.

﴿إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ بِالْحَقِّ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَا تُسْأَلُ عَنْ أَصْحَابِ الْجَحِيمِ﴾

119.Hakika sisi tumekutuma kwa haki, uwe mbashiri na mwonyaji, wala hutaulizwa kuhusu watu wa motoni.

﴿وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّـهِ هُوَ الْهُدَىٰ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴾

120.Hawatakuwa radhi nawe Mayahudi wala Manaswara mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uongofu (hasa), na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi uliokufikia, basi hutapata mlinzi yoyote wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.

MBONA MWENYEZI MUNGU HUSEMI NASI

Aya ya 118-120

MAANA

Na walisema wale wasiojua; mbona Mwenyezi Mungu hasemi nasi au kutufikia ishara (tunazozitaka), Wale wenye inadi walimwambia Mtume(s.a.w.w) : Hatutakuamini mpaka Mungu atwambie ana kwa ana kwamba wewe ni Mtume; au atuletee malaika atakayetufahamisha hilo au atakayeleta hoja tunazozitaka sisi; kama vile alivyowazungumzia Mwenyezi Mungu aliposema:

﴿وَقَالُوا لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ تَفْجُرَ لَنَا مِنَ الْأَرْضِ يَنبُوعًا ﴿٩٠﴾ أَوْ تَرْقَىٰ فِي السَّمَاءِ وَلَن نُّؤْمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّىٰ تُنَزِّلَ عَلَيْنَا كِتَابًا نَّقْرَؤُهُ﴾

Na walisema: Hatuwezi kukuamini mpaka utububujishie chemchemi katika ardhi... au upande mbinguni na hatutaamini kupanda kwako mbinguni mpaka ututeremshie kitabu tukisome... (17:90,na 93)

Mwenyezi Mungu amewajibu hilo kwa kauli yake:Hivyo hivyo walisema wale waliokuwa kabla yao mfano wa kauli yao (hii). Nyoyo zao zimefanana. Hakika sisi tumezibainisha ishara kwa watu wenye kuyakinisha. Yaani kung’ang’ania huku kwa mawazo ya ubatilifu hakuhusiki na waliyoyatoa kwa Mtume(s.a.w.w) tu, kwani watu wa Nabii Musa walimwambia:...TuonyesheMwenyezi Mungu wazi wazi... (4:153)

Kwa hoja na dalili ambazo hazileti shaka katika nafsi isiyokuwa na shaka na wasiwasi, na kusafika kwa haki kwa njia ya haki. Mwenyezi Mungu amelifanya hilo na akabainisha dalili zenye kutosheleza juu ya Utume wa Muhammad. Ama kutaka zaidi ni kujitia mashaka na kutaka makubwa. Kimsingi ni kwamba mpinzani mwenye inadi, haipasi kumjibu bali hupuuzwa na kuachiliwa mbali. Na watu wenye yakini ndio ambao wanatafuta yakini kwa njia yake.

CHENYE KUTOLEWA DALILI NA AINA YA DALILI

Tumetangulia kueleza katika kufasiri Aya ya 111:(...Sema: Leteni dalili zenu,kama nyinyi ni wasema kweli) Kwamba kila dai linahitaji dalili na dalili inahitaji dalili mpaka iishie kwenye asili iliyo wazi ambayo haipingani.Katika kifungu hiki, tutazungumza aina hiyo ya dalili. Dalili inatofautiana kwa kutofautiana tabia ya kitu. Kwa mfano tukitaka kujua vitu ambavyo vinatengeneza kitu katika vitu vya maumbile tutategemea majaribio na mtaalamu mtafiti. Tukitaka kuthibitisha kuwapo kwa mwenye kupanga mambo mwenye hekima, tutarudia akili. Tukitaka kujua hukumu yoyote katika hukumu za sharia tutarudia Quran na Hadith. Kama tukitaka kujua lugha ya Kiarabu na matamko yake ni lazima kuwarudia wajuzi na istihali za Waarabu wa mwanzo: Ikiwa kuna masuala ya kikanuni tutarudia kanuni au masuala ya kihistoria tuatawarudia wanaakiolojia na wapokezi wenye kutegemewa. Hivyo ndivyo zinavyotofautiana dalili kutokana na yanayotakiwa kuthibitisha. Kwa hivyo haifai kwa yeyote, vyovyote alivyo kutoa maoni yake kwa namna ya dalili anayoitaka au kutaka uthibitisho zaidi baada ya kukamilika dalili zote zinazowajibisha yakini na kukinaisha. Kwa hivyo dalili ya kutosha ikipatikana kisha mwingine akatoa maoni ya dalili nyingine au zaidi, basi huyo ni mwenye inadi na mwenye kutaka makubwa.

Mtume Muhammad(s.a.w.w) amewashinda wenye shaka na wapinzani kwa Quran; kukathibiti kushindwa kwao na hoja ikatimu. Basi wanapotaka zaidi baada ya kushindwa huko kwenye kufedhehesha, itakuwa matakwa yao hayo ni inadi. Kwani lau kama kusudio lao ni haki, kama ilivyo, basi wangelikinai na wengeliikiri baada ya kuwadhihirikia kwa sura ya ukamilifu iliyo wazi. Hakika sisi tumekutuma kwa haki, uwe mbashiri na mwonyaji, wala hutaulizwa juu ya watu wa motoni. Hiki ni kiwango cha kazi ya Mtume na jukumu lake na kwamba yeye ni mwalimu sio mtenza nguvu, na ni mwenye kubainisha haki sio mlazimishaji. Aya hii ni kama Aya inayosema:

﴿وَقُلِ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ فَمَن شَاءَ فَلْيُؤْمِن وَمَن شَاءَ فَلْيَكْفُرْ ﴾

Na sema:Ni ukweli uliotoka kwa Mola wako, basi anayetaka na aamini na anayetaka na akufuru... (18:29)

Aya hiyo ni kumuondolea uzito Mtume(s.a.w.w) asipatwe na jaka moyo kwa sababu ya kufuru ya mwenye inadi na ya mwenye kufanya upinzani. Hawatakuwa radhi nawe Mayahudi wala Manaswara mpaka ufuate mila yao. Mwenye Majmaul-Bayan anasema: Mayahudi na Wakristo walimwomba Muhammad(s.a.w.w) kupatana nao kwa muda kisha watamfuata wamwamini.Ndipo Mwenyezi Mungu akamkatisha tamaa. Hii inafahamisha kuwa haifai kuwaridhisha Mayahudi na Wakristo kwa hali yoyote iwayo. Kwa sababu Mwenyezi Mungu ameambatanisha kuwaridhisha na kuwa Myahudi au Mkristo. Ikiwa haliwezekani hilo, basi haiwezekani kuwaridhisha. Kwa hakika ni kwamba dini zote na vikundi vyote ni hivyo wala sio Mayahudi na Wakristo tu; bali baadhi ya watu hawawi radhi nawe mpaka uwe mtumwa kwao. Quran inapinga hali hii ya kuchukiza na ikatoa mwito kuishi kidini pamoja na dini zote, kuwatukuza Mitume wote na kuwataja kwa heri, na ikawajibisha kuamini Utume wao. Haya ndiyo yenye nguvu zaidi katika kuleta udugu kati ya watu wa dini na kusaidiana.

Mwenyezi Mungu amewahusisha kuwataja Mayahudi na Wakristo ili Mtume akate tamaa nao kuwa watamfuata kama alivyosema mwenye Majmaul-Bayan.Sema: Hakika uongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uongofu (hasa). Tumetangulia kueleza katika tafsir ya Aya 26, kwamba neno Huda (uongofu) lina maana nyingi; kama vile kubainisha haki, kuwafikisha kwenye uongofu, thawabu na mengineyo. Hapa lina maana ya Uislamu ambao Mwenyezi Mungu amempelekea Mtume wake Muhammad(s.a.w.w) ; usiokuwa huo ni upotevu sio uongofu. Maana yake ni, sema ewe Muhammad, niliyonayo mimi ndiyo haki na mliyo nayo nyinyi ni upotevu na batili, vipi niache, niifuate upotevu?

MAADUI WA DINI NA MSINGI WAKE

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemfahamisha Mtume wake mtukufu kwamba Wayahudi na Wakristo hawatamridhia mpaka afuate mila yao; pamoja na kujua kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) isma ya Mtume wake Muhammad(s.a.w.w) kwamba yeye hatafuata mapenzi yao kwa hali yoyote. Lakini amempa tahadhari hii:Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi uliokufikia, basi hutapata mlinzi yoyote wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu. Wafasiri wametaja kufaa hali mbili kutokana na tahadhari na katazo:

Kwanza : kwamba maasi yanawezekana kutokea kwa Mtume lakini anajizuia; yaani yeye anaacha maasi pamoja na kuwa anaweza kufanya; vinginevyo ingekuwa hakuna ubora wowote katika kuyaacha, na ndio yakaja makatazo na hadhari kwenye lile linalowezekana kufanyika bila ya kuangalia isma.

Pili : kwamba kwa dhahiri msemo unaelekezwa kwa Mtume, lakini ni kwa watu wote. Mimi nimefikiria hali ya tatu, kwamba: huenda Mtume ilimpitia kuwa Mayahudi watasogea na kuongoka au wamsaidie katika mambo ambayo yataleta heri au yatakayopunguza ugoigoi wao na kuzuia baadhi ya shari zao; ndipo akabainisha Mwenyezi Mungu kwamba maadui wa dini na msingi wake hawawezi kuridhia chochote kwao isipokuwa uache haki uliyo nayo na ufuate upotovu walio nao; kisha akamkataza kupatana nao na kukurubiana. Kwa sababu hilo litawasaidia na kuwapa nguvu; na kutia nguvu huko ni haramu kwako ewe Muhammad na mwingine kama ilivyo haramu kufuata dini yao.

Zaidi ya hayo ni kwamba Mayahudi wana maumbile ya shari na ufisadi, kupinga haki na watu wake na kumfanyia uovu mwenye kufanyia wema; wala halifai kwao jaribio lolote la amani. Jawabu bora ni kwamba Mwenyezi Mungu anaweza kumwamuru na kumkataza masum; kama anavyoweza kumwamuru asiyekuwa masum kwa kuangalia utukufu wake na ukubwa wake. Kisha makatazo haya na hadhari hii inawavunja wale wanaowabembeleza maadui wa dini wanaotoa udhuru kuwa wanafanya hivyo kwa masilahi ya Waislamu. Kwa sababu adui wa dini na wa nchi, hataki usalama wowote isipokuwa kwa biashara ambayo yeye daima atakuwa ndiye mwenye faida; na nembo yake pekee ni chukua wala usitoe, ukiweza chukua zaidi ya unavyotoa, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amebainisha hakika hii ya wafanyi biashara hawa kwa ufasaha na uwazi aliposema:

﴿وَلَتَجِدَنَّهُمْ أَحْرَصَ النَّاسِ عَلَىٰ حَيَاةٍ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا﴾

Na utawaona wana pupia zaidi maisha kuliko watu wengine na kuliko wale walioshirikisha (2:96)

﴿الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلَاوَتِهِ أُولَـٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ وَمَن يَكْفُرْ بِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴾

121.Wale tuliowapa Kitabu wakakisoma kama inavyostahiki kukisoma, hao ndio wanaokiamini. Na wanaokikanusha, basi hao ndio wenye hasara.

﴿يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴾

122.Enyi wana wa Israil! Kumbukeni neema yangu niliyowaneemesha na hakika nimewafadhilisha kuliko viumbe wengine.

﴿وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا تَنفَعُهَا شَفَاعَةٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ﴾

123.Na ogopeni siku ambayo nafsi haitafaa kitu nafsi nyingine, wala hakitakubaliwa kwake kikomboleo; wala maombezi (shufaa) hayatafaa, wala hawatanusuriwa.

WAKAKISOMA KAMA INAVYOSTAHIKI

Aya ya 121-123

MAELEZO

Wale tuliowapa Kitabu wakakisoma kama inavyostahiki kukisoma, hao ndio wanaokiamini. Baada ya Mwenyezi Mungu kumbainishia Mtume wake, Muhammad(s.a.w.w) kwamba Wakristo na Mayahudi hawamwamini, bali hawatamridhia mpaka afuate mila yao, sasa anawavua wale wema wanaoichunga haki katika wao; wale ambao wamesilimu na wakamwamini Muhammad(s.a.w.w) na akawaeleza kuwa ni wale ambao wanakisoma kitabu inavyostahiki. Makusudio ya Kitabu ni kila kitabu alichokiteremsha Mwenyezi Mungu, kiwe ni Quran, Tawrat au Injil, kama vilivyoteremshwa na Mwenyezi Mungu. Kuacha kukihusisha kitabu maalum katika maelezo yake Mwenyezi Mungu ni dalili ya kuwa ni vitabu vyote alivyoviteremsha. Maana ya kukisoma inavyostahiki, ni kuzingatia vizuri maana yake na kufuata amri na makatazo yake; sio kusoma vizuri, kudhibiti matamko, na kuzitoa herufi sawa sawa (tajwidi tu). Kwani hilo si chochote ikiwa hakuna kuzingatia vizuri na kuongoka. Kuna Hadith tukufu inayosema: Hakuiamini Quran mwenye kuhalalisha yaliyoharamishwa.

Jumla ya maneno ni kwamba Tawrat na Injil vyote vimebashiri Utume wa Muhammad(s.a.w.w) ; kama ambavyo Quran imefahamisha ukweli wake. Ndio maana wengi walisilimu miongoni mwa Mayahudi, Wanaswara na Washrikina ambao walizingatia vizuri Aya na wakaifuata haki kama ilivyo. Na wanaokikanusha,basi hao ndio wenye hasara. Yaani mwenye kukanusha aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ambayo yanalazimisha kumkanusha Muhammad(s.a.w.w) , huyo ni katika wenye kuhasirika, kwa sababu ni sawa na mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu. Ni wazi kwamba hapana hasara kubwa zaidi kuliko hasara ya akhera na neema yake yenye kubaki.

Enyi wana wa Israili! Kumbukeni neema Yangu niliyowaneemesha na hakika nimewafadhilisha kuliko viumbe wengine. Tafsir ya Aya hii imeshatangulia katika Aya 40. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amekariri kuwakumbusha Mayahudi neema yake katika Aya nyingi kwa lengo la kuwatahayariza kwa namna ya ufasaha zaidi na hekima; kama alivyotumia katika kauli yake:Na iogopeni siku ambayo nafsi haitafaa kitu nafsi nyingine, ambayo pia tafsir yake imepita katika Aya 48.

MUJTAHIDI NA MUQALLID

Sheikh Muhammad Abduh alitoa mwito wa ijtihad (kujitahidi) na kuwakemea watu wa Taqlid wenye kufuata tu, na alikuwa na darasa ya kufasiri Quran alipofika kwenye kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):Wakakisoma kama inavyostahiki. Alisema: Yule ambaye anasoma Quran kwa kusoma tu, mfano wake ni kama punda aliyebeba vitabu vikubwa, hana imani kwa sababu hafahamu siri yake wala hajui uongofu wa Mwenyezi Mungu ulio ndani yake. Kusoma matamko tu, hakuna faida yoyote, hata kama msomaji atajua maana ya hayo matamko. Kwa sababu itakuwa kama picha; na picha ni mawazo, yanakuja kisha yanapotea. Hakika fahamu sahihi ni kufahamu kwa imani na kusadikisha, kwa yule anayezingatia vizuri kitabu na kutaka kuongoka akijua kuwa anasoma Aya zake ili aongoke na kupata uongofu kutokana na maana yake. Basi baadhi ya masheikh wa Taqlid wakamwingilia kati kwa kusema Wanavyuoni wanasema: Quran ni ibada kwa kuisoma. Sheikh Abduh akajibu: Lakini Mwenyezi Mungu amesema:

﴿كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴾

Kitabu tumekiteremsha kwako,kilicho barikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wenye akili wawaidhike. (38:29)

Na katika rai za Sheikh Abduh, kama ilivyo katika Tafsir Al-Manar ni kwamba, ni juu ya kila Mwislamu asome Quran au kuisikiliza yote ijapokuwa mara moja tu katika umri wake.

﴿تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُم مَّا كَسَبْتُمْ وَلَا تُسْأَلُونَ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴾

124.Na Mola wake alipomjaribu Ibrahim kwa matamko, naye akayatimiza. Alimwambia: Hakika mimi nimekufanya Imam wa watu. Akasema: Na katika Kizazi changu (pia) Akasema: Ahadi yangu haiwafikii madhalimu.

AHADI YANGU HAIWAFIKII WAOVU

Aya ya 124

LUGHA

Makusudio ya kujaribiwa hapa ni kukalifishwa. Makusudio ya maneno ni amri na makatazo ikiwa ni pamoja na kukalifishwa kumchinja mwanawe. Makusudio ya kuyatimiza ni kutii.

MAANA

Na Mola wake alipomjaribu Ibrahim kwa matamko naye akayatimiza. Ibrahim Al-khalil(a.s) ni baba wa Mitume. Dini tatu (Uislamu, Ukristo na Uyahudi) zinakubali na kuthibitisha Utume wake. Washirikina wa Kiarabu wakijitukuza kwa kunasibika kwao na mwanawe Ismail(a.s) na kwa kutumikia kwao Al-Kaaba, na kuihami, ambayo imejengwa na Ibrahim na mwanawe Ismail(a.s) . 32 Mwenyezi Mungu anabainisha kwamba Yeye alimwamrisha Ibrahim baadhi ya taklifa, kama vile kumchinja mwanawe, akawa mwaminifu mwenye kutekeleza amri na kuitii. Mwenyezi Mungu amemsifu Ibrahim kuwa mtekelezaji aliposema:Na Ibrahim aliyetekeleza (ahadi). (53:37)

* 32 Mwenye Bahrul Muhit amesema: Ibrahim ni babu wa thalathini na moja wa Muhammad; naye ni Ibrahim bin Tarih, bin Najur bin Sarugh, bin Arghu, bin Faligh bin Abir ambaye ni Mtume Hud. Naye alizaliwa katika ardhi ya Ahwaz,Akasema: hakika mimi nimekufanya Imam wa watu Hii ni bishara kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Ibrahim, ya kumfadhilisha na Uimamu tangu mwanzo na bila ya yeye kuomba, ikiwa ni malipo ya Ikhlasi yake na utekelezaji wake, na pia kujitolea kwake mhanga. Akasema na katika kizazi changu pia. Haya ni matakwa na dua kutoka kwa Ibrahim(a.s) kwamba Mwenyezi Mungu aneemeshe baadhi ya kizazi chake, kama alivyomnemeesha yeye. Kwa sababu neno katika hapa ni kufahamisha baadhi. Hapa yanadhihiri mapenzi ya mzazi kwa mwanawe, kwa vile alivyotaka Ibrahim wema kwa baadhi ya kizazi chake na wala asijitakie yeye mwenyewe peke yake. Akasema: Ahadi yangu haiwafikii madhalimu.

Kauli hii ni kumwitika Ibrahim maombi yake ya kufanywa Maimam baadhi ya kizazi chake kwa masharti ya kuwa wawe kama yeye; watekelezaji ahadi na wacha Mungu. Kwa sababu kazi ya Imamu ni kuzuia maasi, vipi awe yeye ndiye mwasi. Sioni kauli inayofahamisha zaidi uadilifu wa Imamu na huruma yake kwa raia kuliko kauli ya Imam Ali(a.s) alipokuwa ni khalifa wa Waislamu: Umma hivi sasa unaogopa dhulma ya viongozi wake na mimi nahofia kuwadhulumu raia zangu. Kiongozi anaogopa kuwadhulumu raia; mwenye nguvu anaogopa kuwadhulumu wanyonge; tena mtu mwenye nguvu ambaye hajali mauti. Yaani imekuwa yule mwenye utawala anahofia juu ya raia zake ambapo ingekuwa kinyume; kama ilivyozoeleka! Ni jambo ambalo si la kawaida.

UIMAMU NA FIKRA YA ISMA

Neno Imam (kiongozi) hutumika katika maana nyingi kama vile: njia, kwa sababu inamwongoza mwendaji kwenye makusudio yake. Pia lina maana ya anayoyafuata mtu kumwongoza au kumpotosha, Mwe-nyezi Mungu anasema:

﴿وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا﴾

Na tukawafanya ni maimamu wanaoongoza kwa amri yetu... (21:73) Katika Aya nyingine amesema:

﴿وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ﴾

Na tukawafanya ni maimamu waitao katika moto... (28:41)

Mtu anakuwa Imam, ikiwa anafuatwa katika jambo fulani, na anakuwa Maamum ikawa yeye ndiye anayefuata. Hayo ni kwa mujibu wa lugha. Ama kwa mujibu wa dini na sharia, ni kwamba neno Imam linatumiwa kwa anayeongoza swala, lakini katika maana hayo hutumiwa kwa kuunganishwa na neno jingine; kama vile Imam wa Ijumaa na jamaa. Ikiwa ametajwa Imam tu, bila ya neno lolote jingine, basi litatumika kwa maana mbili:Kwanza : kwa maana ya Utume. Hiyo ni daraja ya juu zaidi ya Uimamu.Pili : kwa maana ya Wasii wa Mtume.

Imam kwa maana ya Utume na Imam kwa maana ya wasii, anakuwa ni mwenye kufuatwa katika kila kitu, naye hamfuati yeyote wakati wa Uimamu wake. Uimamu kwa maana ya Utume unahitajia nukuu (nassi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwa Roho mwaminifu. Na Uimamu kwa maana ya wasii hauna budi kuwa ni kwa nukuu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwa ulimi wa Mtume wake mtukufu. Sharti ya nassi hiyo ni kuwa kwa jina na kwa mtu maalum, sio kwa sifa na kwa tamko la ujumla; kama ilivyo kwa Mujtahid na hakimu wa sharia (kadhi). Bali ni lazima iwe ni kwa nukuu mahsus isiyokubali taawil au uwezekano wa kinyume. Kuanzia hapa ndio inabainika kwamba kutumia neno Imam peke yake kwa asiyekuwa Mtume au Wasii ni jambo la kuangaliwa vizuri na sio mbali kuwa ni haramu, sawa na kutumia neno Wasii wa Mtume kwa asiyekuwa Imam Massum.

Vyovyote iwavyo, kauli ya Imam huyu - awe Mtume au Wasii - ni kauli ya Mwenyezi Mungu; uongozi wake ni wa Mwenyezi Mungu; hukumu yake ni hukumu ya Mwenyezi Mungu ambayo haina kinyume. Yeyote mwenye kudai kitu bila ya kuthibitisha kwa nukuu inayomuhusu basi huyo ni mzushi mwongo. Bora ya niliyoyasoma katika sifa ya Imam ni kauli ya Imam mtukufu Zainul-abidiin(a.s) katika Sahifa Sajjadiyya:

Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika wewe umeitia nguvu dini yako kila wakati kwa Imam uliyemweka kuwaelimisha waja wako; na ni mnara katika miji yako baada ya kuiunganisha kamba yake na yako. Na ukawajaalia ni nyenzo ya radhi zako. Na umefaradhisha kutiiwa na ukahadharisha kuasiwa; umeamrisha kufuatwa maamrisho yake na kuachwa makatazo yake na kutotanguliwa na mtangulizi yeyote au kubaki nyuma naye yeyote. Yeye ni ngome ya wanaotafuta hifadhi na ni pango la Waislamu: Ni tegemeo la waumini na ni fahari ya Mola wa viumbe vyote.

Hizo ndizo sifa za ambaye amechaguliwa na Mwenyezi Mungu kuwa Imam kwa waja wake. Kimsingi ni kwamba Uimamu wa Utume na ule wa Uwasii unahitajia Isma (kuhifadhiwa na dhambi) haiwezekani bila ya hivyo, kwa sababu kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzake. Mwenye uchafu na ambaye ana haddi (adhabu) hawezi kumfanyia haddi mwingine. Wamelitolea daili hilo Shia Imamiya kwa kauli yake Mwenyezi Mungu: Hakika mimi nimekufanya Imam wa watu. Kwamba Uimam hauwi ila kwa kufanywa na Mwenyezi Mungu. Hilo linatiliwa nguvu na ombi la Nabii Ibrahim kwa Mwenyezi Mungu kufanywa Maimamu katika kizazi chake. Ikiwa Uimamu ni kwa kufanywa na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) utakuwa unatokana na nukuu kutoka kwake. Vile vile wametolea dalili Shia, kauli Yake Mwenyezi Mungu:Ahadi yangu haiwafikii madhalimu. Kwamba ni wajibu kupatikana Isma kwa Mtume na Wasii. Njia ya kutolea dalili ni kuwa Mwenyezi Mungu amewabainishia wazi wazi kuwa Yeye hautoi Uimamu kwa dhalimu; na dhalimu ni yule aliyefanya madhambi katika maisha yake kwa namna yoyote ile, hata kama atatubia baada yake, lakini jina hili litakuwa limempitia. Kwa hivyo mwenye kuwa na hilo hawezi kuwa Imam.

Inatokea sadfa mtu mwengine asiyekuwa Ali kukua katika malezi ya ushirikina na uchafu, kuabudu masanamu, kuzama katika uchafu wa kijahilia na wala asitamke shahada mbili ila baada ya kuyashiba masanamu na kuyasujudia. Kwa upande mwingine Mwenyezi Mungu akataka Ali bin Abi Twalib akulie katika malezi ya Mtume yaliyo na usafi; na Mtume amtengeneze kulingana na matakwa ya Mwenyezi Mungu na kuyaangusha masanamu kutoka kwenye hadhi yake na kuyatupa chini ya miguu ya Muhammad(s.a.w.w) Hapa kuna swali tunalolitoa kwa kila mwenye akili mwenye kuchunga haki, ili ajijibu yeye mwenyewe kwa akili yake; nalo ni hili: Mtu asiyejua kutumia vizuri, amerithi mali kutoka kwa baba yake, ikabidi awe na msimamizi atakayemlinda na kumuhifadhia mali yake. Sasa kukawa na utatanishi wa kumpa usimamizi mtu ambaye hakuwahi kumwasi Mwenyezi Mungu katika uhai wake, si kwa dhambi dogo au kubwa, au apewe usimamizi mtu aliyewahi kumwasi Mwenyezi Mungu kwa muda mrefu akiwa amekwisha baleghe, kisha akatubia; je tumchague yupi? Inatosha kuwa ni dalili ya kuhifadhiwa na madhambi (Isma) kwa Ahlul Bait(a.s) kutokana na alivyowatolea ushahidi Mwenyezi Mungu aliposema:

﴿إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا ﴾

Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu enyi watu wa nyumba ya Mtume na kuwatakasa kabisa kabisa. (33:33)

Tumezungumzia Isma kwa ufafanuzi katika kufasiri Aya ya 39 kifungu cha Isma ya Mitume na kifungu cha Ahlul Bait: Tafadhali rejea, kwani kifungu hiki ni ukamilisho wa vifungu hivyo vilivyopita.

Fikra ya Isma (kuhifadhika na makosa) haihusiki na Shia tu. Masunni pia wameizungumzia, lakini wao wanaijaalia kwa umma, wakitegemea Hadith ambayo haikuthibiti kwa Shia, nayo ni:Umma wangu hauwezi kukusanyika juu ya jambo la upotovu. Wakristo nao wanasema Baba mtakatifu ana Isma. Wakomunisti wamesema Marx na Lenin pia wana Isma. Makabaila wa Syria nao wamesema iko Isma kwa Antony Saada, na wanachama wa Ikhwanul-Muslimin (ndugu wa Kiislamu) wamesema Hassan Al-Banna anayo Isma. Huko China, hivi leo ninapoandika tafsir hii ni mwaka 1967, mamilioni ya watu wanaamini kuwa Mao Tse Tung ana Isma na wanajizatiti kwa mafunzo yake.

Wakomunisti; tuliowataja wakitofautiana huwa wanatofautiana katika kauli za viongozi na makusudio, sio katika wajibu wa kuwafuata na kuwafanya viongozi; sawa na vile wanavyohitlafiana Waislamu katika tafsir ya Quran au Wakristo katika tafsir ya Injil. Yeyote atakayeihuisha Isma kwa Mashia peke yao, basi atakuwa ni mmoja kati ya hawa wawili. Ama atakuwa ni mjinga mwenye kughafilika au mzushi mwenye njama.