TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA Juzuu 1

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA0%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA Mwandishi:
Kundi: tafsiri ya Qurani

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA

Mwandishi: Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya
Kundi:

Matembeleo: 35714
Pakua: 3042


Maelezo zaidi:

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
Juzuu 9 Juzuu 10 Juzuu 11
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 20 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 35714 / Pakua: 3042
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA KWANZA Juzuu 1

Mwandishi:
Swahili

10

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KWANZA

AL - BAQARAH (NG’OMBE)

﴿ وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ﴾

34.Na tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipokuwa Iblis; alikataa na akajivuna; na akawa miongoni mwa makafiri.

MSUJUDIENI ADAM

Aya 34

Mwenyezi Mungu aliwaamrisha malaika kumsujudia Adam kwa kudhihirisha ubora wake kuliko wao na kuliko viumbe vyake vyote. Hapana tafsiri ya ubora huu isipokuwa ubora wa elimu au ubora wa aliye nayo. Kwa sababu elimu, kama ilivyothibiti, ndiyo kipimo cha kila hatua anayopiga mtu ya maendeleo na ukamilifu; kama vile ambavyo ujinga ni msingi wa kurudi nyuma. Hawezi kuwa juu isipokuwa kwa elimu. Mwenye elimu siku zote hufuatwa, na mjinga siku zote hufuata. Kwa ajili hii Uislamu umewajibisha elimu kwa kila Mwislamu mwanamume na mwanamke.

Wafasiri wengi wamesema kwamba sijda ilikuwa ni ya ki-maamkuzi tu; Kama kuinama na kuinua mkono. Kwa sababu kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni haramu. Lakini haya sio kweli kwa mujibu wa mwenye tafsiri ya Majmaul-Bayan, kwani kama ingelikuwahivyo,basi, Iblis asingelikataa kumsujudia. Kimsingi sijda ilikuwa ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu sio kwa ajili ya Adam.

Amri ya kumsujudia Adam iliwahusu Malaika wote bila ya kumvua yoyote, hata Jibril na Mikail pia, kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

﴿ وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ الْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِ﴾

Na tulipowaambia Malaika, msujudieni Adam.Basi wakamsujudia isipokuwa Iblis; yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake. (18:50)

Hakuna njia ya kumjua Iblis, shetani na jini, isipokuwa kwa njia ya wahyi tu; kama ilivyo katika kuwajua Malaika.Maelezo yamekwishaelezwa katika Aya iliyotangulia.

Wafasiri wameonyesha utafiti usiokuwa na manufaa. Kwa hivyo tumeuacha kwa kufupiliza yale yanayofahamishwa na dhahiri ya maneno. Tumekwishaonyesha katika kurasa zilizotangulia baadhi ya yale yanayona- sibishwa kwa Iblis katika vigano. Ni picha iliyo wazi ya watu wengi wa siku hizi katika kuchezea kwao matamko, ambako hakutimizi elimu au fani yoyote zaidi ya kubobokwa tu.

﴿ وَقُلْنَا يَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ وَكُلَا مِنْهَا رَغَدًا حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ ﴾

35.Na tukasema: Ewe Adam! kaa wewe na mkeo katika Pepo (bustani); na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, wala msiukurubie mti huu; msije mkawa miongoni mwa waliodhulumu (nafsi zao).

﴿ فَأَزَلَّهُمَا الشَّيْطَانُ عَنْهَا فَأَخْرَجَهُمَا مِمَّا كَانَا فِيهِ وَقُلْنَا اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ﴾

36.(Lakini) Shetani akawatelezesha wote wawili na akawatoa katika ile hali waliyokuwa nayo. Tukasema: nendeni hali yakuwa maadui nyinyi kwa nyinyi, na mtapata katika ardhi makazi na starehe kwa muda (maalum).

﴿ فَتَلَقَّىٰ آدَمُ مِن رَّبِّهِ كَلِمَاتٍ فَتَابَ عَلَيْهِ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴾

37.Akapokea Adam maneno kutoka kwa Mola wake na Mola wake akapokea toba yake; hakika Yeye ni Mwingi wa kukubali toba, Mwenye kurehemu.

﴿ قُلْنَا اهْبِطُوا مِنْهَا جَمِيعًا فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴾

38.Tukasema: Tokeni humo nyote: Na kama ukiwafikia uongozi wangu basi watakaoufuata mwongozo wangu haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.

﴿ وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴾

39.Na ambao wamekufuru na kukadhibisha ishara zetu, hao ndio watakaokuwa watu wa motoni, humo watadumu.

ADAMU PEPONI

Aya 35

Mwenyezi Mungu aliamwamrisha Adam na Hawa kukaa peponi; akawahalalishia kula yaliyomo ndani yake isipokuwa mti mmoja tu, waliokatazwa kuula. Lakini shetani aliwahadaa kwa kuwataka waule. Walipokubaliana naye ilipita hekima yake Mwenyezi Mungu ya kuwatoa pepo ni kuwapeleka ardhini na akawatia mtihani kwa taklifa na kazi, uzima na ugonjwa, shida na raha, kisha mauti muda wake unapofika.

Adam alihisi msiba na akajuta. Akamwomba Mola wake kwa ikhlasi amtakabalie toba yake, akamkubalia na akamsamehe, kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba Mwenye rehema. Nadhani kwamba Hawa pia alitubia pamoja na Adam, lakini Mwenyezi Mungu hakuitaja toba yake. Hakuna tofauti kati ya Mwanamume na mwanamke. Mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na akafanya amali njema, Mwenyezi Mungu atamuweka peponi, na mwenye amali mbaya atamwingiza motoni awe mume au mke.

Wamejiingiza wafasiri wengi kuelezea pepo aliyotoka Adam,ilikuwa wapi?Mti ulikuwa mtini au ngano? Kuhusu nyoka ambaye aliingia Iblis ndani yake, na mahali aliposhukia Adam, je palikuwa India au Hijaz? Na mengineyo yaliyokuja katika hadithi za Kiisrail.Quran haikudokeza lolote katika hayo; wala haikuthibiti katika hadithi kwa njia sahihi. Pia akili haiwezi kujua chochote katika hayo, na hayo hayaambatani na maisha kwa karibu au mbali. Hata hivyo hakuna budi kutanabahisha mambo yafuatayo:-

HAWA NA UBAVU WA ADAM

Imeenea habari kwamba Hawa aliumbwa kutokana na ubavu wa Adam, lakini hakuna maelezo sahihi ya kutegemewa. Na habari zilizoelezea hilo si za kutegemewa. Ikiwa tutazichukulia kuwa ni sahihi basi ni kwamba makusudio yake ni kuonyesha usawa na kukosa kutofautisha kati ya mume na mke, yaani mke ametokana na mume na mume naye ametokana na mke. Katika kitabu Malla yahdhur hul-faqih, imesemwa, Imam Sadiq(a.s) wakati alipoulizwa usahihi wa uvumi huu, aliukanusha na akasema:Mwenyezi Mungu Ametukuka na hayo kabisa.

Je Mwenyezi Mungu alishindwa kumuumbia Adam mke isipokuwa kutokana na ubavu wake mpaka ikabidi Adam aoe sehemu yake ya mwili?

MTAKA YOTE HUKOSA YOTE

Hekima ya Mwenyezi Mungu ilipitisha kuwa Adam akae na mkewe peponi wakati fulani, kisha atoke kwa sababu maalum ambayo wao wawili ndio walioifanya kwa matakwa yao na hiyari yao; lau si hivyo wangelibaki peponi milele wakistarehe bila ya taabu yoyote.

Vile vile hekima yake Mwenyezi Mungu ilipitisha kuwa Adam na Hawa wabaki katika ardhi hii mpaka watakapozaana na kupatikana koo na vizazi, wakati ambapo wataulizwa wote, kauli na vitendo walivyovifanya. Kama ilivyohukumilia hekima yake kurudi Adam na mkewe peponi baada ya kufa na wadumu humo milele.

Unaweza kuuliza: Kuna hekima gani ya kuingia Adam peponi na kutoka kuja ardhini, kisha kuitoka hiyo ardhi na kurudi tena peponi mara ya pili baada ya kufa?

Jibu : Huenda hekima iliyopo ni kuwa Adam apitie majaribio atakayonufaika nayo na kufaidika nayo, yeye na watoto wake, na kurudi kwenye pepo hii akiwa amejaa majaribio yenye kunufaisha. Yaani ni kwamba mtu hawezi kuishi milele bure bure tu vile anavyotaka na kwamba mwenye kuyachunga hayo majaribio kwa kuyamiliki matakwa yake bila ya kukubali kusukumwa na matamanio yake, basi ataishi maisha mazuri ya wema usiokuwa na mwisho. Na mwenye kuwa na msimamo hafifu na akawa mdhaifu mbele ya matamanio yake, atakuwa amepata aliyoyapata Adam majuto, kujaribiwa, taabu na mashaka.

ISMA (KUHIFADHIWA MITUME)

Wameafikiana Waislamu wote kwamba Adam ni katika Mitume, na Mitume kama inavyofahamika ni wenye kuhifadhiwa na madhambi na makosa.Sasa nini maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu; Akawahadaa shetani katika hali waliyokuwa nayo? Kwa ajili hiyo ndio wameonelea wanachuoni kuwa iko haja kubwa ya kufanya utafiti juu ya Isma ya Mitume; kisha kuifasiri Aya hii katika hali ambayo italeta natija. Nasi tunakusanya kauli juu ya hilo kama ifuatavyo ili iwe ni asili katika kila linaloambatana na maudhui haya. Maana ya Isma ya Mtume ni kutakata na makosa katika kila jambo

*15 Kuna maelezo yanayosema kuwa Adam ana jina la kubandikwa peponi la Abu Muhammad kwa heshima na kutukuzwa, na hakuna mtu mwenye jina la kubandikwa peponi ispokuwa yeye tu. linaloambatana na dini na hukumu zake, kiasi ambacho atafikilia Mtume utakatifu na elimu na kumjua Mwenyezi Mungu na yale anayoyataka kwa waja wake; kwa hali ambayo inakuwa muhali kuikhalifu, iwe kwa makusudi au kwa kusahau. Mwenye kuthibitisha Isma kwa Mitume kwa maana hayo na kwa mafungu yake yote yatakayokuja, ataifanyia taawil Aya inayopingana na dhahiri ya msingi huu, kwa kwenda na kanuni ya kiujumla ambayo ni wajibu wa kufanya taawil kwa kuafikiana na dhahiri ya akili. Na, mwenye kukanusha Isma kwa mitume, atabakisha dhahiri kwa dhahiri yake.

Wanavyuoni wa madhehebu mbali mbali wana kauli nyingi katika Isma, zenye kukhitalifiana kwa tofauti za mafungu yafuatayo:

1. Isma katika itikadi na misingi ya dini; yaani kutakasika kwa Mtume kutokana na ukafiri na ulahidi. Hilo ni lenye kuthibiti kwa kila Mtume kimisingi na kwa maafikiano.Kwani haiingii akilini kuwa Mtume amkanushe yule aliyempa Utume.

2. Isma katika kufikisha amri za Mwe-nyezi Mungu. Akisema, Mwenyezi Mungu anaamrisha hili na anakataza lile, basi amri itakuwa ile ile aliyoisema. Wameafikiana Shia Imamiya kuthibiti Isma hii kwa kila Mtume. Kwa sababu lengo la kufikisha ni kuwachukua wale wanaokalifiwa na sharia kwenye haki.Akikosea mwenye kufikisha itakuwa lengo la kufikisha limebatilika. Hayo yanatiliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu:

﴿ وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴾

Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake) (53:3)

Na kauli yake:

﴿ وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا﴾

Na anachowapa Mtume kipokeeni na anachowakataza jiepusheni nacho. (59:7)

Kwa maneno mengine Isma ya Mitume haiwezi kuepukana kabisa na kusema kuwa kauli yao, kitendo na uthibittisho wao ni hoja na dalili. Baada ya Razi kusema katika tafsiri yake: Wameafikiana Waislamu kwamba kukosea katika kufikisha hakujuzu kwa kusudi au kusahau, aliendelea kusema: Wako watu wanaojuzisha hilo kwa kusahau. Sijui aliwakusudia watu gani.

3. Isma katika Fatwa; yaani Mtume kufutu kitu cha wote; kama kuharamisha riba na kuhalalisha biashara. Razi ametaja kifungu hiki katika tafsiri yake kwa kusema: Wameafikiana kwamba kukosea Mtume katika hilo hakujuzu kwa kukusudia ama kwa kusahau, wengine wamejuzisha na wengine hawakujuzisha. Kifungu hiki kinarudi katika kifungu cha pili cha kufikisha. Inatakikana kifanywe kifungu cha tatu ni Isma katika hukumu sio fatwa.16 Wameafikiana Imamiya kwamba Mtume ni mwenye kuhifadhiwa na makosa katika hukumu kama ilivyo katika kufikisha; pamoja na kwamba kwao wamenakili kutoka kwa Mtume mtukufu(s.a.w.w) kwamba yeye amesema:

*16 Tofauti ya hukumu na Fatwa ni kwamba maudhui ya hukumu yanakuwa ni mahsusi kama kadhi kuhukumu mapatano yaliyopita kati ya Zaid na Bakari ni batili. Ama maudhui ya Fatwa yanakuwa ni kwa wote kama kuhalalisha biashara na kuharamisha riba. Hakika mimi ninahukumu kati yenu kwa hoja (ushahidi) na yamini. Mimi ni mtu. Nyinyi mkiwa na ugomvi, huenda mmoja akawa mjanja kuliko adui yake - kwa hiyo nitahukumu kutokana na nilivyosikia kutoka kwake, basi kama mtu nikimpa haki ya ndugu yake asichukue; kwani ninamkatia kipande cha moto. Kama ni kosa hapo katika hukumu yake, imetokana na hoja au kiapo n.k. yaani katika kutegemea hukumu sio katika hakimu mwenyewe.

4. Isma katika vitendo vya Mitume na mwenendo wao hasa. Amesema Iji katika Mawaqif Juz.5; Hakika Hashawiya wanajuzisha kwa Mitume kufanya madhambi makubwa; kama uwongo, kwa makusudi au kusahau; na wamekataa Ashaira - yaani Sunni - kwa kusudi sio kusahau. Ama madhambi madogo inajuzu kwao hata kwa kusudi wachilia mbali kusahau.

Wamesema Imamiya: Hakika Mitume ni wenye kuhifadhiwa katika kila wanayoyasema na wanayoyatenda; kama vile ambavyo wamehifadhiwa katika itikadi na kufikisha. Ni muhali kwao kufanya madhambi madogo, wachilia mbali makubwa, na wala hayawezi kuwatokea kabisa, si kwa kukusudia wala kusahau, si kabla ya Utume wala baada yake. Aya yoyote ambayo haiafikiani dhahiri yake na msingi huu, basi wameiletea taawil.Wakasema katika Adam kula tunda, kwamba kukatazwa kule hakukua ni kwa uharamu au kwa ibada, kama vile kukatazwa kuzini na kuiba, bali kulikuwa ni kimwongozo na nasaha tu; kama kumwambia mtu unayemtakia heri, usinunue nguo hii kwa sababu sio nzuri, ikiwa hakukusikia, basi atakuwa hakufanya haramu wala hakumdhulumu mtu; atakuwa amejidhulumu yeye mwenyewe na amefanya jambo ambalo ilikuwa ni vizuri asilifanye.

Kimsingi kula tunda hakuambatani na kumdhulumu mtu yeyote isipokuwa kula tu. Kwa hivyo maana ya toba ya Adam inakuwa ni toba ya kuacha kutenda jambo lenye kupendekezwa na lililo bora. Na, jambo la toba ni jepesi sana, kwani mara nyingi Mitume na watu wema hulikariri neno Namtaka msamaha Mwenyezi Mungu na ninatubia. Inatosha kuwa ni dalili juu ya hilo dua ya Imam Zainul-Abidin katika Sahifa Sajjadiyya yenye kujulikana kwa dua ya toba akisema: Ninaomba msamaha kutokana na ujinga wangu.

AHLUL- BAIT

Amesema Muhyiddini anayejulikana kwa jina Ibnul Arabi katika kitabu chake Futuhatul Makkiya Juz. 1;Uk. 196 chapa ya zamani. Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemtoharisha Mtume wake na kizazi chake kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

﴿ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا ﴾

...Mwenyezi Mungu anawatakia kuwaondolea uchafu enyi watu wa nyumba (ya Mtume) na kuwatakasa kabisa. (33:33)

Hakuna kitu kichafu zaidi ya dhambi kwa hivyo hakutegemewi kwa watu wa nyumba (ya Mtume) isipokuwa usafi na utohara, bali wao ni dhati ya utohara. Kisha akasema Ibnul Arabi kwamba Salmanul Farisi ni mwenye kuhifadhiwa na dhambi kwa ushahidi wa Mwenyezi Mungu, na imethibiti kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwamba yeye amesema: Salman ni katika sisi Ahlul Bait. Kwa hiyo Salman ni mwenye kuhifadhiwa na dhambi kwa ushahidi wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Katika juzuu ya pili ya kitabu hicho hicho Uk. 127, amesema: Hatabaki katika moto mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika waliotumwa na Mwenyezi Mungu, kwa sababu moto kwao unakuwa ni baridi na salama kwa baraka ya Ahlul Bait katika akhera. Ni utukufu ulioje wa baraka za Ahlul Bait!

﴿ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَوْفُوا بِعَهْدِي أُوفِ بِعَهْدِكُمْ وَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ﴾

40.Enyi wana wa Israil! Kumbukeni neema yangu niliyowaneemesha; na tekelezeni ahadi yangu nitatekeleza ahadi yenu; na niogopeni Mimi tu.

﴿ وَآمِنُوا بِمَا أَنزَلْتُ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُمْ وَلَا تَكُونُوا أَوَّلَ كَافِرٍ بِهِ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا وَإِيَّايَ فَاتَّقُونِ﴾

41.Na aminini niliyoyateremsha ambayo yanasadikisha mliyonayo wala msiwe wa kwanza kuyakataa, wala msiuze ishara zangu kwa thamani ndogo; na niogopeni Mimi tu.

﴿ وَلَا تَلْبِسُوا الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُوا الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴾

42. Wala msichanganye haki na batili, na mkaficha haki na hali mnajua.

﴿ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ ﴾

43.Na simamisheni swala na toeni zaka na inameni pamoja na wanaoinama.

﴿ أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴾

44.Je, mnawaamrisha watu kutenda mema na mnajisahau, hali mnasoma Kitabu? Basi je,hamfahamu?

﴿ أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ أَفَلَا تَعْقِلُونَ﴾

45.Na takeni msaada kwa kusubiri na kwa kuswali na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu.

﴿ الَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَاقُو رَبِّهِمْ وَأَنَّهُمْ إِلَيْهِ رَاجِعُونَ ﴾

46.Ambao wana yakini kwamba wao watakutana na Mola wao na kwamba watarejea Kwake.

ZIKUMBUKENI NEEMA ZANGU

Aya 40 - 46

Mwenyezi Mungu amewataja Mayahudi katika Aya nyingi za Quran tukufu.Zimebainisha Aya hizo neema za Mwenyezi Mungu na kuua kwao Mitume bila ya haki. Vile vile zimebainisha uadui wao kwa Musa na Harun(a.s.) , kuabudu kwao ndama na kufanywa watumwa na Mafirauni, kisha kukombolewa. Vile vile Aya zimeeleza walivyookoka wasife maji na kuteremshiwa Manna na Salwa. Pia zimeelezea chuki yao hao Mayahudi kwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) , au njama zao dhidi yake na uadui wao mkubwa kwa Waislamu, kuchukia kwao haki na mengineyo ambayo yatakuja maelezo yake kwa ufafanuzi. Surah ya Ngombe, waliyemchinja, hii inaelezea kwa upana sifa na matendo yao.

DHAHIRI YA MAISHA

Aina nyingi za hali ya maisha wanayoishi watu ni natija ya Historia ndefu. Aina ya mavazi tunayovaa, mapishi ya chakula tunachokila na ujenzi wa nyumba tunazokaa, vyote hivi ni kutokana na usanifu wa waliotangulia. Hata meli zinazotumia mashine zimeundwa baada ya majahazi yanayotumia matanga,baada ya kupita vipindi vya maendeleo. Hakika maigizo ya kihistoria yanafanya kazi kama desturi za kitabia; sawa na mawimbi yanayotulia kutokana na msukosuko wa kupwa maji na kujaa. Kwa hivyo matukio yanayotumika katika maisha yetu ya kila siku na mfungamano tunaokuwa nao na watu wengine, mbaya au mzuri, ni natija ya yaliyopita zamani sana au hivi karibuni.

Hapa ndipo wanafalsafa wakasema: Historia ni miongoni mwa njia za maarifa. Na Aya hizi ambazo Mwenyezi Mungu anawazungumzia Mayahudi, zina mfungamano mkubwa na Historia yao, kama tutakavyoona.

ISRAIL

Israil: ni jina jingine la Yaqub bin Is-haq bin Ibrahim(a.s.) , Khalilullah. Ishaq ni ndugu wa Ismail, babuye Mtume Muhammad(s.a.w.w) . Waarabu na Wayahudi wote wamekutana kwa Ibrahim. Mwenyezi Mungu amesema:

﴿ مِّلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ﴾

Mila ya baba yenu Ibrahim (22:78).

Katika Majmaul-Bayan imesemwa kwamba: Waarabu wote ni uzao wa Ismail; na wengi wasiokuwa Waarabu ni uzao wa Is-haq. Maana ya Israil katika lugha ya Kiebrania ni Abdullah (mja wa Mungu), Isra: ni mja, il: ni Mwenyezi Mungu. Alitumia upole Mwenyezi Mungu katika kuwazungumzia Wayahudi kwa kuwategemeza na Mtume mtukufu Israil ili kuwakumbusha nasaba hii tukufu. Huenda wakahisi utukufu ikiwa umo ndani ya nafsi zao; sawa na kusema: Ewe mtoto wa watu wema! Kuwa kama baba zako na babu zako. Ama sababu ya kuitwa kwao Yahudi ni kwamba ukoo mmoja kati yao unatokana na Yahudha ambaye ni mtoto wa nne wa Nabii Yaqub. Sehemu ifuatayo tutaeleza kwa muhtasari historia ya Mayahudi kutokana na Aya tuliyonayo.

HISTORIA YA MAYAHUDI

Yatakuja maelezo katika Sura ya Yusuf kwamba Mtume Yaqub(a.s) alihama na watoto wake kutoka Palestina kwenda Misri alipo mtoto wake Yusuf(a.s) akiwa waziri wa Firaun wakati huo. Firaun akawakatia kipande cha ardhi yenye rutuba kwa heshima ya Yusuf. Kikaendelea kizazi cha Yakub kwa muda kiasi. Lakini Mafiraun waliokuja baadaye waliwakandamiza na kuwapa adhabu na mateso; waliwachinja watoto wao wa kiume wakawaacha wa kike; na wakawafanya watumwa. Kisha Mwenyezi Mungu akawapelekea Mtume aliyekuwa mmoja wao ambaye ni Musa bin Imran, kuwak-omboa na dhulma na utumwa; akawataka warudi Palestina kupigana na akawaahidi ushindi. Wakakataa kwa woga. Mwenyezi Mungu akawapangia kutangatanga katika jangwa la Sinai miaka arobaini. Utakuja ufafanuzi Inshallah.

Katika kipindi hiki Harun alikufa kisha Musa pia akafa. Akachukua uongozi mpwawe Yashua bin Nun. Ilipofika karne ya 13 kabla ya kuzaliwa Nabii Isa(a.s) walivamia ardhi ya Palestina wakiongozwa na Yoshua wakawafukuza wenyeji; kama kilivyofanya kizazi chao (Wazayuni) katika Palestina mwaka 1948.17 Baada ya Yoshua Mwenyezi Mungu alituma mitume wengi waliotokana na wao.

* 17 Tutaje mifano miwili: kwanza, Wazayuni waliwakusanya wanawake 25 wenye mimba katika kijiji cha Dair Yasin, wakawapasua matumbo yao kwa mabisu na mikuki. Pili, waliwakusanya watu wa kijii cha Zaituni msikitini, kisha wakawalipua kwa baruti. Mnamo mwaka 596 kabla kuzaliwa Nabii Isa(a.s) , Mfalme wa Babil Nebukadnezzar aliwashambulia akaondoa utawala wao katika Palestina, akawachinja wengi na kuwachukua mateka wengi. Wakaendelea kuwa chini ya utawala wa Nebukadnezzar mpaka mwaka 538 kabla ya kuzaliwa Isa(a.s) aliposhindwa na mfalme wa Fursi (Iran ya sasa), ndipo Mayahudi wakapumua. Wakaendelea kuwa chini ya utawala wa Fursi kiasi cha miaka mia mbili, baadaye wakatawaliwa na makhalifa wa Alexandria mkuu. Kisha wakawa chini ya utawala wa Roma.

Ilipofika mwaka 135 kabla ya kuzaliwa Isa(a.s) , Mayahudi walifanya mapinduzi kwa Warumi, lakini hayakufanikiwa. Walifukuzwa Palestina, wakakimbilia sehemu mbali mbali za mashariki na magharibi; wengine Misri na wengine Lebanon na Syria, wengine wakaenda Iraq na wengine Hijaz. Ama Yemen walikujua Mayahudi na kuhamia huko kwa ajili ya biashara tangu zama za Nabii Suleiman ambaye alimwoa Malkia wa Yemen, Bilqis (Malkia wa Sheba).

Neema za Mwenyezi Mungu kwao ambazo Mwenyezi Mungu amezitaja kwa kauli yake; Zikumbukeni neema Zangu nilizowaneemesha, ni nyingi; zikiwa ni pamoja na kuwachagua Mitume kutoka katika kabila lao; kama Musa, Harun, Yoshua, Daud, Suleiman, Ayub, Uzair, Zakaria, Yahya n.k. Ama Maryam, mama yake Isa pia ni Mwisrail, nasaba yake inaishia kwa Nabii Daud(a.s) , lakini Mayahudi hawamkubali Masih mwana wa Maryam na wanadai kwamba Masih aliyetajwa katika Tawrat hajakuja bado.

MUHAMMAD NA MAYAHUDI WA MADINA

Mtume(s.a.w.w) alipohamia Madina kutoka Makka, Mayahudi walikuwa na koo tatu: Bani Qaynuqa, Bani Quraydha na Bani Nadhir. Walikuwa wana vilabu vya pombe, madanguro na sehemu za kufugia nguruwe. Na walikuwa wakihodhi dhahabu na fedha, kutengeneza silaha na kufanya biashara ya riba. Kwa ujumla wao ndio waliokuwa wakuu katika mambo ya uchumi mjini Madina, kama walivyo sasa (duniani).

Alipofika Mtume(s.a.w.w) , Mayahudi walihisi hatari kwa faida zao na mapa to yao ya kibiashara, kwa sababu vijana wa Madina wasingekwenda kwenye maduka na mabucha yao na watu wa Madina wasingekula nyama za nguruwe. Maana yake ni kwamba mayahudi wangepoteza vitega uchumi vyote. Kwa ajili hiyo wakawa wanamchimbia vitimbi Mtume mtukufu(s.a.w.w) na kupanga njama pamoja na makafiri dhidi ya Waislamu, kama zinavyofanya leo nguvu za dola kubwa zinavyolinda maslahi yake.

Mtume naye ni kama aliyejua hilo pale alipoingia Madina, akataka kuwatafutia hoja na kuwaadhibu kwa kauli zao. Kwa hiyo akawachukulia upole, akawekeana nao mkataba: kwamba wao wana uhuru katika dini yao na Mahekalu yao kwa masharti ya kuwa wasimsaidie adui na kama wakiamua kupigana pamoja na Waislamu, basi watapata fungu katika ngawira. Ni juu yao kushirikiana na Waislamu, kuulinda mji wa Madina, kwa sababu mji ni wa wote sio wa kundi maalum.Lakini walivunja ahadi upesi sana.Tangu lini ahadi ikasimama mbele ya maslahi? Je inaingia akilini usalama na hadaa kuwa pamoja? Vipi anaweza kuishi mbwa mwitu pamoja na punda kwa amani? Kutafaa nini kukumbushwa neema, hadhari na nasaha kama zikigongana na maslahi ya kiutu na mapatano ya kibiashara?

Imeelezwa katika kitabu Muhammad Rasullul-huriyya (Muhammad Mtume wa Uhuru) hivi: Mtume aliwaambia wafanyabiashara wa Kiislamu waanzishe soko jipya mjini Madina, wakaanzisha; likawa na nguvu soko hilo; wafanyi biashara wageni wakawa wanaelekea huko, na soko la Mayahudi likaathirika. Kwa sababu biashara katika soko la waislamu ilikuwa ya uadilifu sana kwa muuzaji na mteja. Hiyo peke yake ilitosha kujaza nyoyo za Mayahudi hasadi na chuki kwa Muhammad(s.a.w.w) na kuwafanya wavunje ahadi.

MAELEZO

Mwenyezi Mungu ameanza kuwaambia Mayahudi kukumbuka neema zake kwao.Miongoni mwa hizo neema ni kuwaletea Mitume wengi na kuwatukuza kwa Tawrat na Zabur. Vile vile kuwakomboa katika utumwa wa Firaun, kuokoka kwao kutokana na kufa maji, kuwateremshia Manna na Salwa, kuwapa milki na ufalme katika zama za Mtume Suleiman na mengineyo ambayo yanawajibisha kuamini na kushukuru na wala sio kukanusha na kukufuru. Unaweza kuuliza: Kwa nini msemo unawaelekea Mayahudi wa Madina pamoja na kujua kuwa neema zinazoelezwa zilikuwa kwa baba zao na sio kwao? Jibu: Neema kwa baba ni neema kwa watoto vile vile; ambapo mtoto anapata utukufu kutokana na baba yake. Zaidi ya hayo ni kwamba umma wote ni mmoja.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuwakumbusha neema zake aliwaambia: Tekelezeni ahadi yangu nitatekeleza ahadi yenu. Ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kuchukua yale yanayofahamiwa na maumbile na yale ambayo vimeteremshwa vitabu kwayo, ikiwa ni pamoja na kumwamini Mwenyezi Mungu na Mitume yake na kufanya amali kwa hukmu zake. Mwenye Majmaul-Bayan anasema: Hakika Mwenyezi Mungu aliwaahidi katika Tawrat kwamba Yeye atawapelekea Mtume anayeitwa Muhammad. Fikra hii ndiyo wanayoielezea wafasiri wengi nayo ndiyo inayotolewa ushahidi na Quran. Ama ahadi ya Mayahudi ni ile ahadi ya Mwenyezi Mungu kwao. Na,kila mwenye kuamini akafanya amali njema basi Mwenyezi Mungu atamlipa thawabu siku ya Kiyama.

Imesemekana maana yake ni kwamba kama wakimcha Mwenyezi Mungu, basi atawainua katika maisha haya ya duniani.Tutaeleza fikra ya malipo katika dunia mahali pake Inshaallah. Kisha Mwenyezi Mungu amewaamrisha kuamini Quran na wasifanye haraka kuikanusha, kumkanusha Muhammad na kutaka maslahi tu. Na kwamba ni juu yao kuisimamisha swala na kutoa zaka ili wazitakase nafsi na mali zao.

Ama kauli yake Mwenyezi Mungu: Je, mnawaamrisha watu kutenda mema na mnajisahau, hali mnasoma kitabu, inawaelekea viongozi na wakubwa, sio kwa watu wote, kwa sababu watu wengine ni wafuasi, na viongozi ndio wenye kufuatwa. Wao ndio wanaoficha haki na hali wanaijua na wanatoa mawaidha lakini hawayafuati. Tunakariri tena kwamba mawaidha na nasaha haziendi pamoja na kutaka maslahi; na hayawezi kuacha athari yoyote isipokuwa katika nafsi isiyotaka maslahi na isiyokuwa na lengo lolote zaidi ya haki.

Ama kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Na takeni msaada kwa kusubiri na kwa kuswali Imeelezwa tena katika Aya ya 153 ya Sura hii, kwa hivyo utakuja ufafanuzi wake huko Inshallah. Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza 2 Sura Al-Baqara