TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TATU Juzuu 3

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TATU 30%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TATU Mwandishi:
: HASANI MWALUPA
Kundi: tafsiri ya Qurani

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
  • Anza
  • Iliyopita
  • 12 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 17921 / Pakua: 3852
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TATU

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TATU Juzuu 3

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

4

5

7

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA TATU

﴿قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴾

31.Sema: Ikiwa mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni Mwenyezi Mungu atawapenda na atawaghufiria madhambi yenu: na Mwenyezi Mungu ni mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

﴿قُلْ أَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ ﴾

32.Sema: Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume, kama wakikataa, basi hakika Mwenyezi Mungu hawapendi makafiri.

KUMPENDA MWENYEZI MUNGU

Aya 31 - 32

MAANA

Sema: Ikiwa mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni.

Yeyote anayempenda Mwenyezi Mungu, analazimika kumpenda Mtume wa Mweneyezi Mungu na Ahlu Bait wake, kwa sababu Mtume anawapenda. Na yeyote anayempenda Mtume,analazimika kumpenda Mwenyezi Mungu, Mapenzi hayo mawili hayaachani.

Mwenyezi Mungu anasema:

﴿مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ﴾

Mwenye kumtii Mtume basi ndio amemtii Mwenyezi Mungu (4:80)

Kwa sababu Mtume ndiye anayemsemea Mwenyezi Mungu na ndio ubainifu wake; vinginevyo mtu atakuwa ni adui. Yaani mwenye kufanya uadui na Mtume na Aali zake, basi ndio amejiwekea uadui na Mwenyezi Mungu, atake asitake. Kwa hivyo watu wa dini nyingine ambao wanalingania imani ya Mungu kisha wanamfanyia uadui Muhammad(s.a.w.w) basi wao ndio maadui zaidi katika maadui wa Mwenyezi Mungu. Kama mtu atasema kuwa kutojua kwao utume wa Muhammad ni udhuru; basi jibu ni kuwa hakuna udhuru kabisa kwa yule anayefuata mapenzi yake na akawa anawafuta tu mababu zake, isipokuwa baada ya kuthibitisha na kuangalia dalili zote juu ya utume wa Muhammad. Na, yeyote atakayeangalia dalili hizi kwa mtazamo wa uadilifu na kuchunga haki, ataamini na kunyeyekea.

Hakuna maana ya pendo la mdogo kwa mkubwa na mtumishi kwa bwana wake, isipokuwa ni utii na kufuata. Na, kila anayependa yale anayoyachukia Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na akachukia yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, basi yeye ni adui wa Mungu na Mtume wake; hata kama atafikiriwa kuwa ni katika wapenzi. Kwa sababu yale yanayodhaniwa kwake kuwa yeye ni mpenzi bila ya kuwako na athari yoyote, haya yatakuwa njozi tu.

Sema: Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume, na wakikataa, basi hakika Mwenyezi Mungu hawapendi makafiri.

Dhahiri ya Aya hii inaonyesha kuwa hakika ya dini ni kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume, na kwamba kuuacha utiifu huo kunalazimisha ukafiri, bali ni ukafiri hasa kwa dhati yake, kutokana na kauli yake hiyo:

"Na wakikataa, basi hakika Mwenyezi Mungu hawapendi Makafiri" Na wala hakusema hakika Mwenyezi Mungu hawapendi waasi au atawaadhibu, kwa maana kuwa Mungu ameuzingatia uasi kuwa ni ukafiri, sio sababu ya ghadhabu na adhabu tu. Jambo hili lina hatari na kuhofisha sana, kiasi ambacho hawatabakia kwenye dini na kwenye uislamu isipokuwa wachache kabisa, ila ikiwa makusudio ya ukafiri hapa ni uasi; kama ilivyo katika Aya hii:

﴿وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ﴾

Na ni haki ya Mwenyezi Mungu juu ya watu kuhiji Nyumba hiyo kwa mwenye kuweza njia ya kuendea na anayekufuru basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu (3:97)

Kwa hali yoyote iwayo, sisi tunaamrishwa kidini na kisharia kumtendea kiislamu kila mwenye kutamka shahada mbili, kama vile urithi, ndoa, utwahara, na kulinda mali na damu yake.

Yasiyokuwa hayo ataachiwa mwenyewe Mwenyezi Mungu (s.w.t) sisi hatuna majukumu nayo

﴿إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ آدَمَ وَنُوحًا وَآلَ إِبْرَاهِيمَ وَآلَ عِمْرَانَ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴾

33.Hakika Mwenyezi Mungu alimchagua Adam na Nuh na watoto wa Ibrahim na watoto wa Imran juu ya walimwengu wote.

﴿ذُرِّيَّةً بَعْضُهَا مِن بَعْضٍ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴾

34.Kizazi cha wao kwa wao na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.

﴿إِذْ قَالَتِ امْرَأَتُ عِمْرَانَ رَبِّ إِنِّي نَذَرْتُ لَكَ مَا فِي بَطْنِي مُحَرَّرًا فَتَقَبَّلْ مِنِّي إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴾

35.Aliposema mke wa Imran: Mola wangu! Nimeweka nadhiri kwako aliyemo tumboni mwangu kuwa wakfu. basi nikubalie hakika wewe ndiwe usikiaye uliye mjuzi.

﴿فَلَمَّا وَضَعَتْهَا قَالَتْ رَبِّ إِنِّي وَضَعْتُهَا أُنثَىٰ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا وَضَعَتْ وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالْأُنثَىٰ وَإِنِّي سَمَّيْتُهَا مَرْيَمَ وَإِنِّي أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ﴾

36.Alipomzaa alisema: Mola wangu! Nimemzaa mwanamke - Na Mwenyezi Mungu anajua sana aliyemzaa - Na Mwanamume si kama mwanamke na nimemwita Maryam. Na mimi namkinga kwako, yeye na kizazi chake (uwalinde) na shetani aliyefukuzwa.

﴿ فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٍ وَأَنبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنًا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّا كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيْهَا زَكَرِيَّا الْمِحْرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزْقًا قَالَ يَا مَرْيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَـٰذَا قَالَتْ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ إِنَّ اللَّـهَ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴾

37.Basi Mola wake akamkubalia kwa kabuli njema na akamkuza makuzi mema, Na akamlea Zakariya, Kila mara Zakariya alipoingia Mihrab hukuta vyakula. Akasema: Ewe Maryam unatoa wapi hivi. Akasema: Vinatoka kwa Mwenyezi Mungu, Hakika Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila hesabu.

MAMA WA MARYAM

Aya 33 - 37

Neno: Maryam katika lugha ya Kiibrania lina maana ya mtumishi wa Bwana (Mola). Na Mihrabu kwa Waislamu ni pale anaposimama Imam, na kwa Wakristo ni pale wanapopaita madhabahu

MAANA

Hakika Mwenyezi Mungu alimteua Adam na Nuh na watoto wa Imran na watoto wa Ibrahim juu ya walimwengu wote.

Muhammad bin Yusuf aliye mashuhuri kwa jina la Abu Hayan Al-Andalusi, katika Tafsir yake kubwa inayoitwa Al-bahrul Muhit anasema: Amesoma Abdullah; "Na kizazi cha Muhammad juu ya viumbe wote." (Qiraa) hiki kikiwa sawa au si sawa lakini Aya ya Tat-hir inasema:

﴿ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا ﴾

Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu watu wa nyumba (ya Mtume) na kuwatakasa kabisa kabisa" (33:33),

Inatosha kuwa Aya hii ni dalili ya kuwa Mwenyezi Mungu amekiteua kizazi cha Muhammad(s.a.w.w) na cheo chao na utukufu wao,yeye ni bora wa mitume wote basi kizazi chake pia ni bora ya vizazi vyote: bali ni kwamba wanachuoni wa umati wake ni kama mitume wa Bani Israil au ni bora kuliko mitume wa Bani Israil - sikumbuki tamko la Hadith yenyewe - hasa wakiwa wanavyuoni wenyewe ni kutokana na kizazi chake kitakatifu. Vyovyote itakavyokuwa, Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameanza kwa kutaja Adam kwa sababu yeye ndiye baba wa kwanza wa watu kisha akamtaja Nuh ambaye ni baba wa pili wa watu kwa sababu wakazi wote wa duniani wanatokana na kizazi chake cha watoto wake watatu; Sam, Ham na Yafith, baada ya tufani iliyomaliza watu wote. Mwenyezi Mungu aliwateua Adam na Nuh wao wenyewe tu, ndio maana hakutaja kizazi. Ama Ibrahim na Imran aliwateua pamoja na vizazi. Ibrahim naye ni baba wa mitume wote baada ya Nuh, kwani tangu wakati wa Ibrahim hakukuwa na Mtume ila atakuwa ametokana na kizazi chake. Kwa dhahiri ni kwamba makusudio ya Imran ni baba wa Maryam babu wa Isa, sio baba yake Musa. Kwa sababu jina hili limekuja tena mara ya pili, aliposema; "Aliposema mke wa Imran" Mfano huu uko katika mfano wa jina linalokuja katika jumla mbili kwa muundo mmoja; kama vile kusema; Mtukuze Zedi, hakika Zedi ni mtu mwema. Kwa hiyo basi makusudio ya kizazi cha Imran ni Bwana Masih na mama yake Maryam. Inasemekana kwamba Imran (baba yake Musa) alikuwa na bint aitwaye Maryam aliyekuwa mkubwa wa Musa; na kwamba baina ya Imran huyu na Imran babu wa Isa kuna miaka 1800. Makusudio ya viumbe wote ni kwamba kila mmoja wa waliotajwa alichaguliwa katika watu wa wakati wake tu sio kila wakati.

Kizazi cha wao kwa wao

Hakuna mwenye shaka kwamba Nuh anatokana na Adam na kwamba Ibrahim na kizazi chake wanatokana na Nuh; na Imran anatokana na Ibrahim. Kwa hiyo kulielezea hilo ni sawa na kufafanua kilichofafanuliwa, na maneno ya Mwenyezi Mungu, ni wajibu kuyachukulia kwa mfumo mzuri, Sasa nini makusudio ya habari hii?

Jibu : Makusudio sio kutoa habari kwamba wa mbele anatokana na wa nyuma, la! Isipokuwa makusudio - kama ilivyo dhahiri ya mfumo wa maneno - ni kuwasifu; na kwamba wao wanafanana katika utakatifu na ubora.

Baada ya utangulizi huu, twende kwenye kisa cha mke wa Imran, mama yake Maryam na nyanya yake Isa(a.s) . Kwa ufupi ni kwamba Qufadh bin Qubail Mwisrail, alikuwa na binti wawili mmoja akiitwa Hana aliyeolewa na Imran- ambaye ni Mwisrail vilevile - aliyemzaa Maryam. Na wa pili ni Isha aliyeolewa na Zakariya na kumzaa Yahya. Kwa hiyo Yahya bin Zakaria na Mariam mamie Isa, mama zao ni ndugu na wala sio Isa na Yahya; kama watu walivyozoea, Hivi ndivyo ilivyo katika Majmal-Bayan. Imran akafa huku Hanna akiwa na mimba, akaweka nadhiri kuwa aliyemo tumboni awe mtumishi wa Baitul-Maqdis. Akajidhalilisha kwa kumfanyia ikhlas Mwenyezi Mungu ili aikubali nadhiri yake. Hii ilikuwa inajuzu katika dini yao wala haijuzu katika dini ya kiislamu. Yeye alikuwa akitazamia kuzaa mtoto wa kiume, kwa sababu nadhiri ya mahekalu ilikuwa maarufu kwa watoto wa kiume tu. Alipomzaa mtoto wa kike alimwelekea Mwenyezi Mungu na kusema:"Nimezaa mwanamke "Na mwanamume si sawa na mwanamke na nimemwita Maryam"

Mwenyezi Mungu akaikubali nadhiri ingawaje alikuwa mtoto mke, Waisrail wakabishana, kila mmoja akitaka kumlea Maryam, Ubishi ulipozidi waliafikiana wapige kura. Mshindi akawa Zakariya mume wa mamake mdogo. Wakati huo Zakariya alikuwa ndiye mkuu wa hekalu la kiyahudi. Akamshughulikia sana. Ikawa kila Zakariya anapokwenda kumtazama Maryam anakuta chakula, na walikubaliana kuwa asiendewe na yeyote, akamuuliza kwa mshangao:

Unatoa wapi hivi? Akasema: Vinatoka kwa Mwenyezi Mungu.

Yaani moja kwa moja kutoka kwa Mungu bila ya kupitia kwa yeyote.

Hakika Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu

Hakuna mwenye kutia shaka kwamba karama hii ni ya Maryam(a.s) . Ama kukanusha karama hii kuwa ati chakula alichokuwa akikiona Zakariya kwa Maryam kilitoka kwa wafadhili wa kike waumini, ni kinyume na dhahiri ya Aya. Kwani karama hii ina ukubwa gani zaidi ya kumzaa Isa bila ya baba. Ikiwa karama hiyo ya chakula inatiliwa shaka, basi hii ya kuzaa itatiliwa shaka zaidi.

Maana ya "Akamkuza makuzi mema" ni kwamba yeye alikulia na tabia njema, kumtii Mwenyezi Mungu na kumwabudu. Imepokewa Hadith kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mariam alipofikia umri wa miaka tisa alikuwa akifunga mchana na kuswali usiku, mpaka akawashinda watawa. Inasemekana kwamba hakuwahi kufanya kosa lolote.

FATIMA NA MARYAM

Alitokewa na mfano wa karama hii bibi wa wanawake Fatima bint wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Katika Tafsir Ruhul-Bayan ya Sheikh Ismail Haqi wakati wa kufasiri kisa cha Maryam kuhusu chakula anasema: "Mtume alishikwa na njaa katika wakati wa kahati (ukame). Fatima akamletea mikate miwili na nyama, mara alipoona sahani imeshehenezwa mkate na nyama, alisema "umevipata wapi hivi? Akajibu: "Vinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila hisabu" Mtume akasema: "Sifa njema ni za ambaye amekushabihisha na bibi wa Bani Isriali.' Kisha Mtume akamwita Ali, Hassan, Hussein na watu wa nyumbani kwake; wakala, wakashiba na chakula kikabaki kama kilivyo, Fatima akakigawanya kwa majirani zake."

Katika kitabu Dhakhairul-Uqaba cha Muhibbudin Attabari imeandikwa kuwa, siku moja Ali alikopa Dinar ili akawanunulie chakula watu wake. Akakutana na Mikdad bin As-wad, akiwa katika hali ya mfazaiko alipomuuliza, alisema: "Nimeacha familia yangu wanalia kwa njaa" Basi Ali akampa ile dinar, akaenda zake kuswali nyuma ya Mtume. Baada ya Swala Mtume alimuuliza Ali, "Je una chochote kwako tukale?" Kama kwamba Mtume alipewa wahyi wa kwenda kula kwa Ali. Basi Ali akawa amechanganyikiwa hana la kujibu, Mtume akamshika mkono Ali wakaenda kwa Fatima, walipofika tu wakakuta chakula. Ali akasaili: "Umekipata wapi hiki?" Mtume akasema: "Hiyo ni thawabu za Dinar; inatoka kwa Mwenyezi Mungu naye humruzuku amtakaye bila ya hisabu. Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu aliyekufanya kama Zakariya na akamfanya Fatima mfano wa Maryam. Kila mara Zakariya alipoingia Mihrab hukuta riziki." Kisha Muhibuddin akaongeza kusema: "Ameitoa Hadith hii Al-Hafidh Dimeshqi katika Arbaina Twiwal.

Katika Sahih Muslim mlango wa fadhila za binti wa Mtume imeelezwa kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alimwambia binti yake Fatima. "Hivi huridhii kuwa wewe ni bibi mkubwa wa waumini au bibi mkubwa wa umma huu" Anasema Seyyid Muhsin Al-Amin katika kitabu A'yanushia Juz. 2 sera ya Zahra, akimnukuu Bukhari katika Sahih yake; kwamba Mtume alisema: "Fatima ni bibi mkubwa wa wanawake wa peponi." Vilevile Ibn Sibagh Al-Malik katika Fausulul-muhimma amemnukuu Ahmad katika Musnad akipokea kutoka kwa Mtume kwamba amesema: "Fatima ni bibi mkubwa wa wanawake wa ulimwengu." Katika kitabu Dhakhairul-uqaba cha Muhibbuddin Attabari amesema: Siku moja Mtume alikwenda kumwangalia Fatima alipokuwa mgonjwa, akamuuliza "Waonaje ewe mwanangu?" Akajibu: "Naumwa sana na njaa yanizidisha ugonjwa." Mtume akasema: "Ewe

﴿هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُ قَالَ رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ﴾

38.Pale pale Zakariya akamwomba Mola wake, akasema: Mola wangu nipe kutoka kwako mtoto mwema hakika wewe ndiwe usikiaye maombi.

﴿فَنَادَتْهُ الْمَلَائِكَةُ وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي فِي الْمِحْرَابِ أَنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحْيَىٰ مُصَدِّقًا بِكَلِمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَسَيِّدًا وَحَصُورًا وَنَبِيًّا مِّنَ الصَّالِحِينَ﴾

39.Mara Malaika wakamlingania hali amesimama akiswali kwenye Mihrab kwamba Mwenyezi Mungu anakubashiria (kupata mtoto) Yahya atakayekuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu na Bwana na mtawa na Nabii anayetokana na watu wema.

﴿قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَقَدْ بَلَغَنِيَ الْكِبَرُ وَامْرَأَتِي عَاقِرٌ قَالَ كَذَٰلِكَ اللَّـهُ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ﴾

40.Akasema: Mola wangu! Nitapataje mtoto na hali ukongwe umenifikia na mke wangu ni tasa! Akasema: Ndivyo hivyo Mwenyezi Mungu hufanya apendalo.

﴿قَالَ رَبِّ اجْعَل لِّي آيَةً قَالَ آيَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ النَّاسَ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ إِلَّا رَمْزًا وَاذْكُر رَّبَّكَ كَثِيرًا وَسَبِّحْ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ ﴾

41.Akasema: Mola wangu niwekee alama akasema alama yako ni kutozungumza na watu siku tatu isipokuwa kwa ishara tu. Na umtaje Mola wako sana na mtakase wakati wa jioni na asubuhi.

mwanangu huridhii kwamba wewe ni bibi mkubwa wa wanawake wa ulimwengu wote? Akasema: "Maryam bint Imran atakuwa nani basi?" Mtume akajibu: "Yule ni bibi mkubwa wa wanawake wa wakati wake, na wewe ni bibi mkubwa wa wanawake katika dunia na akhera." Kisha Tabari akasema kuwa Hadith hii imetolewa na Abu Umar na Al-Hafidh Abul-Kassim Dimeshqi. Ufafanuzi uliobakia utakuwa katika tafsir ya Aya 42

ZAKARIYA

Aya 38 - 41

MAANA

Pale pale Zakariya akamwomba Mola wake, akasema: Mola wangu nipe kutoka kwako mtoto mwema.

Tumekwishaeleza kuwa Zakariya alikuwa mume wa mama mdogo wa Maryam na kwamba yeye ndiye aliyemlea. Zakariya hakuwa na mtoto; na alipoona utengeneo wa Maryam na karama alizokuwa nazo, basi aliingiwa na mapenzi ya baba na kupenda kuzaa, Akamwomba Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu; na Mwenyezi Mungu akamwitikia maombi yake.

Mara Malaika wakamlingania,hali amesimama akiswali kwenye Mihrabu kwamba Mwenyezi Mungu anakubashiria (kupata mwana) Yahya.

Yahya ni jina alilopewa na Mwenyezi Mungu kabla ya kuzaliwa, na hakupewa jina hilo yoyote kabla yake kama ilivyoeleza Aya ya 7 katika Sura Maryam. Kwa hiyo basi hakuna haja ya kufanya utafiiti kwamba je, jina hili ni la Kiibrania au la kiarabu, kama ilivyo katika baadhi ya tafsir. Hata hivyo, linaingia katika lugha, kwa maana ya uhai na linanasibika jina lake pamoja na kuuhuisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) utasa wa mama yake.

Mwenye kusadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu

Inasemekana kuwa neno la Mwenyezi Mungu ni ishara ya Isa ambaye Mwenyezi Mungu amemuumba kwa neno 'Kuwa' bila ya baba. Lakini kwa ujumla neno linachukuliwa kuwa ni Aya zake zote na hukumu zake. Mwenye Majmaul-bayan anasema kuwa Yahya ni mkubwa kuliko Isa kwa miezi sita, yeye ndiye wa kwanza kumsadiki na kushuhudia kuwa kuzaliwa kwake ni muujiza kutoka kwa Mwenyezi Mungu; na hilo lilikuwa ni nguvu ya hoja kuhusu Isa. Kwa sababu watu walikuwa wakimwamini Yahya na kumkubalia anayoyasema,Na atakayekuwa bwana. kielimu, dini na tabia njema. Na mtawa, yaani anayejizuwia na kufanya madhambi. Inasemekana ni kujizuwia na wanawake.

Na Nabii atokanaye na watu wema.

Manabii wote ni wema, bali ni Maasum; na Maasum ni zaidi ya uadilifu na wema. Kwa hiyo makusudio ya watu wema ni kuwa Zakariya anatoka katika kizazi kitakatifu. Haya yanaaafikiana na kauli ya Shia kuwa wazazi wote wa mitume ni wajibu wawe wanamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. La kushangaza ni kauli ya badhi ya wafsiri - kama katika Tafsiri ya Razi - Kwamba makusudio ya neno Mina-swalihin ni kuwa hakuna nabii isipokuwa amefanya maasi au kudhamiria kuasi isipokuwa Yahya, hakuasi wala kudhamiria kuasi. Mbali ya kuwa kauli hii inatia dosari cheo cha Mtume Muhammad(s.a.w.w) , pia inapingana na akili. Kwa sababu Mtume ameletwa kuondoa maasi; kama akiasi watu watatoa hoja kuwa yeye pia anafanya. Ametakata Mwenyezi Mungu na wayasemayo wasiojua.

Akasema: Mola wangu nitapataje mtoto na hali ukongwe umenifikia na mke wangu ni tasa! Akasema: Ndivyo hivyo hivyo; Mwenyezi Mungu hufanya apendalo.

Wanasema kuwa Zakariya aliposema haya, alikuwa na miaka 120 na mkewe miaka 98. Hapa kuna swali linalojitokeza, kuwa Zakariya aliomba Mwenyezi Mungu apewe mtoto mwema ikimaanisha kuwa yeye aliomba kitu kinachowezekana katika itikadi yake, sasa vipi tena arudi kuona ajabu alipopewa habari na Malaika?

Jibu : Hiyo haikuwa ni kutia shaka au kushangazwa, isipokuwa ni kuutukuza uwezo wa Mwenyezi Mungu ambao umepetuka mipaka na kawaida; kama vile mtu anavyomwambia mtu aliyetoa sana vitu vya thamani, "Vipi umefanya jambo asilolifanya yeyote isipokuwa wewe?" Vilevile kuadhimisha huko na kustaajabu kunakusanya shukrani kwa Mwenyezi Mungu juu ya neema hii tukufu ambayo hata hakuifikiria. Vilevile tunapata faida kutokana na muujiza huu kwamba mtu asiyalinganishe matakwa ya Mwenyezi Mungu na lile ambalo yeye analiona linawezekana au la.

Akasema: Mola wangu! Niwekee alama:

Kwa kuwa kutunga mimba ni jambo lisilojulikana upesi, alipenda Zakariya kujua itakapotungwa mimba, ili aanze kushukuru tangu mwanzo. Kwa hiyo ndio akamwomba Mola wake amjaalie alama itakayomfahamisha kutungwa mimba. Ndipo Mwenyezi Mungu akasema:

Alama yako ni kutozungumza na watu siku tatu isipokuwa kwa ishara tu na umtaje Mola wako sana na mtakase wakati wa jioni na asubuhi.

Yaani alama ya kutungwa mimba ni kuwa ulimi wako utafungika na utashindwa kuzungumza na watu isipokuwa utaelewana nao kwa ishara utakuwa kama bubu, lakini ulimi wako utafunguka kiasi unachotaka wakati unapofanya ibada. Na huu ni muujiza wa pili baada ya mimba ya tasa.

Mwenye Tafsiri Al-Manar, akimnukuu Ustadh wake Sheikh Muhammad Abduh, anasema kuwa Mwenyezi Mungu alimwamrisha Zakariya ajishughulishe na dhikr na tasbih tu muda wa siku tatu bila ya kuzungumza na watu, basi atatoa ishara, baada ya siku tatu ndio atampa. Tafsir ya kwanza ndiyo iliyo wazi na mashuhuri zaidi.

﴿وَإِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَاكِ وَطَهَّرَكِ وَاصْطَفَاكِ عَلَىٰ نِسَاءِ الْعَالَمِينَ ﴾

42.Na Malaika waliposema: Ewe Maryam! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteua na akakutakasa na akakuteuwa juu ya wanawake wa ulimwenguni.

﴿يَا مَرْيَمُ اقْنُتِي لِرَبِّكِ وَاسْجُدِي وَارْكَعِي مَعَ الرَّاكِعِينَ﴾

43.Ewe Maryam! Mnyenyekee Mola wako na usujudu na urukuu pamoja na wanaorukuu.

﴿ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيْكَ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يُلْقُونَ أَقْلَامَهُمْ أَيُّهُمْ يَكْفُلُ مَرْيَمَ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يَخْتَصِمُونَ﴾

44.Hizi ni habari za ghaibu tunazokupa wahyi; nawe hukuwa nao walipotupa kalamu zao nani katika wao atamlea Maryam na hukuwa nao walipokuwa wakishindana.

EWE MARYAM MWENYEZI MUNGU AMEKUTEUA

Aya 42 - 44

MAANA

Na Malaika waliposema: Ewe Maryam! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteua na akakutakasa na akakuteua juu ya wanawake wa ulimwenguni.

Kwanza Mwenyezi Mungu amemtaja mama yake Maryam, mimba na nadhiri yake; kisha akamtaja Zakariya mlezi wa Maryam; akamtaja tena Maryam na kuruzukiwa kwake na Mwenyezi Mungu bila ya hisabu. Kisha akamtaja Zakariya, maombi yake na kukubaliwa kwake maombi. Hivi sasa anarudia tena kwa Maryam kama ilivyo kawaida ya Qur'an, kuingilia suala jengine ambalo linafungamana na suala la kwanza, kisha tena kulirudia suala la pili. Makusudio ya kuteuliwa kwa kwanza, ni kukubaliwa kuwa waqfu wa kuitumikia nyumba ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu hilo lilikuwa likihusika na wanaume, na kwa pili, ni kuzaa Mtume bila ya kuguswa na mtu yeyote. Inasemekana kuwa kuteuliwa kwa pili ni kutilia mkazo kuteuliwa kwa kwanza. Kuhusu kutakaswa, mwenye Tafsir Al-manar anasema: "Kumefasiriwa kutakasika kwa maana ya kukosekana hedhi. Na imepokewa kuwa bibi Fatima Zahra hakutoka hedhi, na ndio maana akaitwa Zahra"

Tunaloliona kuwa lina nguvu ni kwamba kutakasika ni usafi wa Maryam, wa kutakasika na kila shubha kuhusu kuzaa kwake. Kongamano la wanavyuoni limeafikiana kuwa Maryam hakuwa Mtume; na wala hakuna Mtume mwanamke. Mwenyezi Mungu anasema:

﴿وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِي إِلَيْهِم﴾

Na hatukutuma kabla yako isipokuwa wanaume tuliowapa wahyi" (12:109)

Na utume umekoma kwa Muhammad(s.a.w.w)

Ama kule kuzungumza na Malaika, hakumaanishi kuwa yeye ni Mtume; hata mama yake Musa pia alizungumza na Malaika; kama Aya hii isemavyo:

﴿وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ أُمِّ مُوسَىٰ أَنْ أَرْضِعِيهِ﴾

"Na tukampa wahyi mama yake Musa ya kwamba mnyonyeshe (28:7)

Tutafafanua zaidi kuhusu kuteuliwa Maryam Inshaallah

UBORA WA QUR'AN KWA WAKRISTO

Yametangulia maelezo kwamba ujumbe wa Kinasara kutoka Najran ulikwenda Madina kumhoji Mtume wa Mwenyezi Mungu kuhusu utume wake, huku ukilingania uungu wa Isa, Mtume akawasomea: Ewe Maryam hakika Mwenyezi Mungu amekuteua na kukutakasa." Kusoma kwa Mtume Aya hii kwa ujumbe wa kikristo wa Najran, ambao umekuja kuhojiana naye, ni dalili ya mkato juu ya utukufu wa uislam na ukweli wa Mtume Mtukufu. mayahudi hawakuichunga haki kwa kusema uongo na kumzulia Maryam pamoja na kuleta tuhuma kuhusu kuzaliwa kwake, lakini Mwenyezi Mungu amewakadhibisha na akaandika katika kitabu chake (Qur'an) usafi wake, na akakata njia zote za uzushi. Lau kama Muhammad hakuwa mkweli katika ujumbe wake na kutojiamini, basi angelificha hilo (la Maryam) kwa wakristo kwa namna ambayo mayahudi walimtukana Maryam na kumfanya mwongo. Uislam kwa Aya hii umewatendea wema wakristo, wema mkubwa mno; lau si hivyo yangelisikika mengi kutoka kwa baadhi ya waislam wakati wa kugombana, kama yale yaliyosikika kwa mayahudi kuhusu Maryam mtakatifu. Lakini mwislamu anajua kuwa utakatifu wa bibi Maryam ni sehemu ya uti wa mgongo wa itikadi yake; na kwamba kumtusi ni kufru na ni kutoka katika uislam, Yatakuja maelezo zaidi katika kufasiri Aya (5:82) Inshaallah.

Ewe Maryam! Mnyenyekee Mola wako na usujudu na urukuu pamoja na wanaorukuu.

Alimwamrisha ibada kwa kujiandaa na jambo kubwa ambalo ni kumzaa Isa(a.s) . Jambo lolote kuu ni lazima liwe na maandalizi. Pia Mwenyezi Mungu alimwamrisha kuswali na kutoa Zaka madamu yuko hai.

Hizi ni habari za ghaibu tunazokupa wahyi.

Msemo unaelekezwa kwa Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu; maana yake ni kuwa unayowaambia watu kwa ujumla na yale unayowahusisha wakristo na ujumbe wa Najran, kama vile kisa cha Maryam na mama yake, mke wa Imran na kisa cha Zakariya na Yahya, yote hayo na mengineyo hukuyasoma katika kitabu wala hukuyasikia kutoka kwa wasimulizi, kwa sababu wewe husomi na huandiki. Yote hayo ni ujuzi wa ghaibu na ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na, hii ni hoja kwa wahasimu wako, na ni dalili ya ukweli wako. Wasimulizi kamwe hawakunukuliwa kusema kuwa ujumbe wa Najran uliweza kujibu au kupinga hoja hii.

Nawe hukuwa nao walipotupa kalamu zao nani kati yao atamlea Maryam na hukuwa nao walipokuwa wakishindana.

Kalamu ni kitu maarufu, ni ile ambayo inaandikiwa; na makusudio yake hapa ni mishale waliyokuwa wakipigia kura. Maana kwa ujumla ni kuwa kuwafahamisha kwako habari hii na undani huu kuhusu Maryam na Zakaria, kwamba hukusoma wala kusikia, basi imebakia kuwa umeona tu, lakini inajulikana kuwa kuna mamia ya miaka kati yako na kisa hicho (hivyo hukuona). Kwa hivyo basi kujua kwako habari hizo ni kwa wahyi tu. Kwa ufupi kisa hicho cha kutupa 'kalamu' kwa kupiga kura, ni kwamba, Hanna, mke wa Imran alipomzaa Maryam alikuwa ameweka nadhiri kuwa atumikie Baitul-Maqdis. Na alimzaa baada ya kufa baba yake (Imran) Basi makuhani na makasisi wa Israil wakashindana kuhusu atakayemlea. Hatimaye wakapiga kura ambayo ilimwangukia Zakariya, mume wa mamake mdogo. Akawa ndiye mlezi na msimamizi wake.

NANI BIBI MKUU WA WANAWAKE WA ULIMWENGUNI?

Imekwishaelezwa kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimwambia Maryam: "Na akakuteua juu ya wanawake wa ulimwengu" Aya hii imeleta kutofautiana kati ya wanavyuoni wa Kiislamu; kwamba je, Maryam binti Imran ndiye bora zaidi au Fatima binti Muhammad? Kundi katika wanavyuoni wamesema kuwa wanawake bora ni wane Maryam binti Imran, Asiya binti Muzahim (mke wa Firaun), Khadija bint Khuwaylid na Fatima bint Muhammad. Hadith hii imetajwa katika Sahih sita; pia nimeiona katika Tafsir tabari, Razi, Bahrul-muhit, Ruheil-bayan, Maraghi na Al-Manar. Wengine wamesema Maryam ndiye bora kutokana na Aya hii. Mashia na baadhi ya Masheikh wa Kisunni wamesema kwamba Fatima ni bora zaidi. Mwenye Tafsir Bahrulmuhit, wakati alipofasiri Aya hii: Alisema: "Baadhi ya Masheikh wetu wamesema: Yale ambayo wameyasema wanavyuoni wakiwanukuu masheikh wao ni kwamba Fatima ni bora wa wanawake waliotangulia na watakaofuatia; kwa sababu yeye ni sehemu ya Mtume."

Wale wanaosema Fatima ni bora, wametolea dalili hilo kutokana na Hadith Mutawatir zilizopokewa kutoka kwa baba yake akisema: "Fatima ni sehemu yangu, atakayemkasirisha ndio amenikasirisha mimi." Ama kauli yake Mwenyezi Mungu kuhusu Maryam: "Na akakuteua juu ya wanawake wa ulimwenguni," makusudio yake ni wanawake wa ulimwenguni wa wakati wake si wakati wote. Ibara hii ni maarufu na imezoeleka; kama kusema: "Fulani ndiye mshairi hodari zaidi ya watu wote." Hapo anakusudiwa kuwa ni mshairi zaidi kwa wakati alioko au kwa watu wake tu. Mifano ya hilo katika Qur'an ni mingi, kama vile kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema kuhusu wana wa Israil:

"Na tukawafadhilisha juu ya walimwengu" (45:16)

Hakuna hata mmoja aliyehitalifiana na wenzake kuwa makusudio ya Aya hii ni walimwengu wa wakati wao. Au kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

﴿وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا وَكُلًّا فَضَّلْنَا عَلَى الْعَالَمِينَ﴾

"Na Ismail na Al-Yasan na Yunus na Lut na wote tumewafadhilisha juu ya walimwengu." (6:86)

Hakuna yeyote anayesema kuwa Lut ni bora kuliko Isa au kwamba ni sawa, au kuwa Ismail ni bora kuliko babake. Aya nyingine ni ile isemayo:

﴿إِنِّي وَجَدتُّ امْرَأَةً تَمْلِكُهُمْ وَأُوتِيَتْ مِن كُلِّ شَيْءٍ﴾

"Hakika mimi nimekuta mwanamke anawatawala; naye amepewa kila kitu" (27:23)

Yaani kila kitu kwa wakati wake. Turudie kwenye wanawake wane ambao imepokewa Hadith kwamba wao ni wanawake bora. Tukiwaangalia bila ya kutilia maanani Hadith na Aya tutaona kwamba kila mmoja katika wao ana ubora wake kwa upande wake kuliko wengine. Asiya mke wa Firauni alimwamini Mungu kwa Ikhlas akimtegemea Yeye peke Yake kuwa ndiye muhifadhi wake, wakati huo akiwa katika nyumba ya mtu mwovu zaidi kuliko yeyote, aliye kiongozi wa ukafiri na ulahidi. Akadhihirisha imani yake, hali ya kuupinga ukafiri na ufisadi wa Firaun na kupinga dhulma na utaghuti wake.

Firaun akamlaza ardhini kwa kumpigilia vigingi mpaka akafa akiwa shahidi wa haki na imani, Karama hii hawakuwa nayo wanawake wengine watatu. Bibi Maryam karama yake ni kumzaa Bwana Masih bila ya baba. Karama hii hakuwa nayo mwanamke yeyote duniani, Bibi Khadija yeye ni wa kwanza kumwamini na kumsadiki Mtume wa Mwenyezi Mungu; akaswali yeye na Ali pamoja na Mtume(s.a.w.w) - Swala ya kwanza katika uislam. Ndiye yeye aliyejitolea mali yake kwa ajili ya kuinusuru dini hii. Hivyo kwa mali yake na himaya ya Abu Twalib uislamu ulisimama na kuimarika, Karama hii nayo hakuwa nayo mwanamke yeyote ulimwenguni. Ama Fatima yeye ni sehemu ya Mtume, vilevile ni nafsi yake kwa umbo, tabia na taqwa; linamridhisha Mtume lile analoliridhia yeye na linamuudhi lile linalomuudhi yeye. Yeye ni mama wa Hassan na Hussein mabwana wa vijana wa peponi. Na, ni mke wa bwana wa mbingu na ardhi baada ya Mtume, Karama hii nayo hakuwa nayo Khadija (mamake) wala Asiya au Maryam.

Ama kutofautisha ubora katika karama hizi, ni kama kujaribu kutofautisha ubora kati ya waridi na asmini au kati ya mahurulain wawili. Lakini inatosha kwa Fatima awe na jambo moja tu kutokana na baba yake, ambaye ni bora ya Mitume. Katika Sahih Bukhari Juz.5 mlango wa sifa za ukoo wa Mtume, kuna Hadith ya Mtume isemayo: "Fatima ni bibi (mkuu) wa watu wa peponi." Ikiwa Fatima ni sehemu ya Mtume, basi mumewe Ali ni nafsi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Nafsi zetu" (3:61).

MAELEZO

Utafiti huu unaungana na utafiti uliotangulia katika Tafsir ya Aya 36 ya Sura hii kifungu "Fatima na Maryam."

﴿إِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِّنْهُ اسْمُهُ الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ وَجِيهًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ﴾

45.Waliposema Malaika: Ewe Maryam! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria neno litokalo kwake; jina lake ni Masih mwana wa Maryam; mwenye heshima duniani na akhera na ni miongoni mwa waliokurubishwa.

﴿وَيُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا وَمِنَ الصَّالِحِينَ﴾

46.Na atasema na watu katika uchanga na katika utu uzima na atakuwa miongoni mwa watu wema.

﴿قَالَتْ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي وَلَدٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ قَالَ كَذَٰلِكِ اللَّـهُ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ إِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴾

47.Akasema: "Mola wangu! Nitakuwaje na mtoto na hali hajanigusa mtu,yeyote?" Akasema: Ndivyo hivyo, Mwenyezi Mungu huumba anavyotaka anapohukumu jambo, huliambia'kuwa'likawa.

﴿وَيُعَلِّمُهُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ﴾

48.Na atamfundisha kuandika na hekima na Tawrat na Injili.

﴿وَرَسُولًا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنِّي قَدْ جِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ أَنِّي أَخْلُقُ لَكُم مِّنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ فَأَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِ اللَّـهِ وَأُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ وَأُحْيِي الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِ اللَّـهِ وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأْكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمْ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴾

49.Na Mtume kwa wana wa Israil. Mimi nimewajia na Ishara kutoka kwa Mola wenu, hakika mimi nitawafanyia kama namna ya ndege katika udongo; kisha nimpulizie awe ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na niwaponye vipofu na wenye mbalanga. Niwafufue wafu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na niwaambie mnavyovila na mtakavyoweka akiba. Hakika katika haya ipo ishara kwenu mkiwa ni wenye kuamini.

﴿وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَلِأُحِلَّ لَكُم بَعْضَ الَّذِي حُرِّمَ عَلَيْكُمْ وَجِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ﴾

50.Na msadikishaji wa yale yaliyokuwa kabla yangu katika Tawrat, na ili niwahalalishie baadhi ya mliyoharamishiwana nimewajia na ishara kutoka kwa Mola wenu, kwa hiyo mcheni Mwenyezi Mungu na mtiini.

﴿إِنَّ اللَّـهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴾

51.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na ni Mola wenu basi mwabuduni. Hii ndiyo njia iliyonyooka

MARYAM MUNGU AKUBASHIRIA

Aya 45 - 51

LUGHA

Mwenye Tafsir Bahrul-muhit amenukuu kauli saba kuhusu sababu za kuitwa Masih (mpakaji au mpangusaji): Kupaka baraka, kupaka dini wakati wa kuzaliwa, kutwaharika na dhambi na kupanguswa na mbawa za Jibril. Vile vile kupakwa uzuri, kupangusa uchafu kwa sababu mama yake alikuwa hatoki hedhi wala hakuchafuka na damu ya nifasi.

LISILOWEZEKANA KIAKILI NA KIDESTURI

Jambo lisilowezekana ni lile ambalo halikufanyika wala haiwezekani kufanyika siku za baadae. Nalo liko namna mbili: Kwanza ni kutowezekana kufanyika hilo lenyewe kidhati na kiakili, kwamba akili haikubali kuwezekana kutokea kwa namna yoyote; kama kuwa pamoja mambo mawili yaliyo kinyume: Mfano kuwa mtu ni mumin na wakati huo huo ni kafiri; au kipofu awe anaona na wakati huo huo awe kipofu, au bubu na msemaji wakati huo huo. Kwa hiyo jambo hilo litakuwa haliwezekani kiakili na kikawaida. Namna ya pili: Ni kutozuilika kuwepo kwake kidhati na akili, bali inawezekana kwa namna fulani, lakini kwa kawaida halitokei. Mifano yake ni mingi sana, Qur'an tukufu imetaja matukio mengi sana; kama vile kukaa Ibrahim katika moto bila ya madhara yoyote kugeuka nyoka fimbo ya Musa, kusimama maji ya bahari kama milima, kuyeyuka chuma kama mshumaa kwa ajili ya Daud, nabii Suleiman kujua matamshi ya ndege na kufufuliwa Uzair baada ya miaka mia.

Mfano mwengine ni wa Isa kuzaliwa bila ya baba, kuzungumza wakati wa kuzaliwa, kufufua wafu, kuwaponya vipofu na wenye mbalanga bila ya tiba yoyote na kuwaambia watu vile walivyokula na walivyoviweka akiba katika majumba yao bila ya kuviona; au kumwambia mtu matukio yote haya. Na yote haya na mengineyo ambayo yanawezekana kutokea, laki ni sio kikawaida. Lau kama ingekuwa muhali kutokea, basi yasingewezekana kutokea kwa Mitume na wasiokuwa Mitume. Kwa hiyo ikiwa matukio haya yanawezekana kutokea na tena wahyi ukayatolea habari kutokea kwake waziwazi, basi ni wajibu kwa kila mumin kuyakubali bila ya kusita. Kundi la wanafalsafa na wafasiri wametaja njia nyengine za kuumbwa Isa bila ya tone la manii ya baba, lakini waliyoyasema hayana msingi wowote. Ilivyo hasa ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni muweza wa kila kitu, anafanya kitu kiweko kwa neno 'Kun' (kuwa) kutokana na kitu ambacho hakikuwepo. Na hekima yake ilipitisha ililotaka, basi limekuwa alilolitaka.

Sisi hatuna ulazima wa kujua kiini cha matukio aliyoyaleta Mwenyezi Mungu yasiyo ya kawaida; wala kujua vipi yametokea. Huenda akili zetu zikawa zinashindwa kujua kama zilivyoshindwa kujua hakika ya roho ambayo ni katika amri ya Mola. Ndio! Tunaloweza kufahamu ni athari zake na natija zake, lakini sio kiini chake na hakika yake. Kwa hiyo Aya zinazomhusu Masih(a.s) na zinazofanana nazo zinazohusu mambo mengine, tutazifasiri kwa misingi hii.

MAANA

Waliposema Malaika: Ewe Maryam! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria neno litokalo kwake; jina lake ni Masih Isa mwana wa Maryam.

Makusudio ya Malaika hapa ni Jibril kutokana na kauli Yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

﴿فَأَرْسَلْنَا إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا ﴾

Na tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu (19:17)

Ambapo makusudio ya Roho hapo ni Jibril. Amemtaja kwa tamko la wengi kwa sababu yeye ndiye kiongozi wa Malaika. Neno litokalo Kwake ni kusema Kwake "Kun fayakun" (kuwa ikawa)

Mwenye heshima duniani na akhera na ni miongoni mwa waliokurubishwa.

Heshima yake duniani, ni kufanywa mtakatifu na kuadhimishwa na watu mpaka siku ya ufufuo. Ama heshima yake huko akhera, ni utukufu wa daraja yake kesho kwa Mungu.

Na atasema na watu katika uchanga na katika utu uzima na atakuwa miongoni mwa watu wema.

Kusema katika uchanga ni kwa ajili ya kumtakasa mama yake na walivyomsingizia mayahudi kuwa alitembea na Yusuf Seremala; Mungu awalaani! manaswara wamedai kuwa hakusema uchangani. Ibn Abbas anasema: "Maneno ya Isa yalikuwa muda mchache na sio zaidi ya yaliyoelezwa katika Qur'an; kisha hakusema mpaka alipofikia makamo ya kusema, kama walivyo watoto wengine. Kauli hii inasaidiwa na mazingatio Kwa sababu lengo la kuzungumza kwake ni kumwepusha mama yake na tuhuma na wasiwasi wa watu; na lengo likapatikana kwa aliyoyasema.

Na katika utu-uzima

Yaani atawazungumzia watu Wahyi akiwa ni mtu mzima Huu ni muujiza mwengine wa kufahamisha Utume wake. Kwa sababu, hilo ni kulitolea habari jambo la ghaibu kwamba yeye ataishi mpaka marika ya utu-uzima.

Inasemekana kuwa aliishi duniani miaka thelathini, Na inasemekana kwamba aliletewa wahyi akiwa na umri wa miaka thelathini, Na akaishi miaka mitatu baadaye.

Akasena: "Mola wangu! Nitakuwaje na mtoto na hali hajanigusa mtu yeyote?.

Swali hili ni la kutukuza uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa sababu ni jambo lisilo la kawaida, hakuna wajihi wowote wa waliyoyaeleza baadhi ya wafasiri kwamba yeye aliuliza kuwa je, atazaa kwa ndoa? Hakuna wajihi wa swali hili kwa sababu jibu lake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Akasema: "Ndivyo hivyo; Mwenyezi Mungu huumba anavyotaka, anapohukumu jambo, huliambia 'kuwa' likawa"

Linafahamisha kuwa yeye Maryam alikuwa akijua kwamba yeye atazaa bila ya kuingiliwa

Na atamfundisha kuandika na hekima na Tawrat na Injili

Maana ya neno 'kitab' (katika lugha ya kiarabu) ni masdar ya kuandika, lakini mara nyingi linatumiwa kwa maana ya kitabu. Makusudio yake hapa, ni maana yake halisi (kuandika), kwa sababu kutajwa Tawrat na injil baada yake, kunatilia nguvu kuchukulia maana ya kuandika: Wengine wamesema maana yake ni kitabu na kwamba kutajwa Tawrat na Injil baada yake ni kutilia umuhimu tu; kama ilivyo katika kauli Yake Mwenyezi Mungu:

﴿حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ﴾

Angalieni sana Swala na ile Swala ya katikati (2:238)

Hekima, ni kuliweka jambo mahali pake. Na Tawrat na Injil, Aya hii ni dalili mkataa kuwa Tawrat ndio nguzo ya kwanza ya dini ya kinaswara na kwamba Injil ni endelezo la Tawrat na baadhi ya marekebisho; kama vile kuhalalisha baadhi ya yaliyoelezwa kuwa ni haram, kunakoelezwa na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na ili niwahalalishie baadhi ya yale mliyoharamishiwa."

Na Mtume kwa wana wa Israil

Mwenyezi Mungu alimtuma Muhammad (s.a.w.w) kwa watu wote kama inavyosema Aya:

﴿وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴾

"Na hatukukutuma ila kwa watu wote mtoaji bishara na muonyaji, Lakini watu wengi hawajui" (34:28)

Ama Isa akiwa Mwisrail, yeye alitumwa kwa watu wake, kutokana na muktadha wa dhahiri ya Aya hii, kuufanya ujumbe wake kuwa ni kwa watu wote, kunahitaji dalili. Hakika mimi nimewajia na ishara kutoka kwa Mola wenu.

Msemo huu unatoka kwa Isa kuwaambia watu wake Waisrail akiwatolea hoja ya ukweli wa utume wake, kwamba yeye anayo miujiza inayofahamisha kuwa ametumwa na Mwenyezi Mungu; kama anavyotaja miujiza yenyewe kwa kusema:

Hakika mimi nitawafanyia kama namna ya ndege katika udongo, kisha nimpulizie, awe ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na niwaponyeshe vipofu na wenye mbalanga na niwafufue wafu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na niwaambie mnavyovila na mtakavyoweka akiba majumbani mwenu. Hakika katika haya ipo ishara kwenu mkiwa ni wenye kuamini"

Hii ni miujiza minne:

Wa kwanza : Ni kuleta uhai katika udongo na kufanya ndege.

Pili : Kuponya aliyezaliwa kipofu na mwenye mbalanga.

Inasemekana elimu ya tiba likuwa imeendelea sana katika wakati wa Isa(a.s) , lakini pamoja na kuendelea kwao, Madaktari mabingwa walishindwa na magonjwa haya mawili (upofu na mbalanga) ndipo Mwenyezi Mungu akayapoza kupitia mkono wa Isa bila ya tiba yoyote, ukiwa ni muujiza unaofahamisha utume wake.

Tatu : kumrudishia uhai maiti.

Nne : kuelezea mambo ya ghaibu kutokana na wanavyokula na wanavyoweka akiba. Si kazi yetu kufanya utafiti wa kujua siri ya miujiza hii, au vipi ameleta uhai na kuponya maradhi yasiyotibika bila ya dawa; na kama tuking'ang'ania kufanya utafiti wa hayo, basi tutaishia kwenye shub'ha na giza. Linalobaki kwetu ni kusalimu amri na kuitambua hekima ya Mwenyezi Mungu na amri Yake ambayo Bwana Masih(a.s) ameieleza wazi wazi na kwa kuikariri, kuwa yeye ameifanya kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, ili aufunge mlango wa wanaofikiri umungu wa Isa.

Tumetangulia kueleza katika Tafsir ya 2:225 kwamba Mwenyezi Mungu anaupitisha utaratibu wa maumbile kwenye desturi ya kawaida ya kimaumbile; isipokuwa kama hekima Yake ikitaka kufanya vingine kwa matakwa Yake ya kuumba ambayo ni ibara ya 'kuwa'. Hapo tena hakuna nafasi ya desturi wala kawaida, Ama Isa kuelezea mambo ya ghaibu, kulikuwa ni kwa kupitia wahyi, na wala hakuhusika nako yeye pekee, bali mitume wote walielezea mambo ya ghaibu. Nuh alitengeneza safina kabla ya tufani, Shuaib alitolea habari mwisho wa maisha ya watu wake, Muhammad(s.a.w.w) alitoa habari ya kuwa warumi wata washinda wafursi na ushindi wa watu wake dhidi ya dola zote hizo mbili na Imam Ali naye alitolea habari mapinduzi ya Zenj na mengineyo, mpaka akaambiwa: "Amirul-mumin! Hakika umepewa elimu ya ghaibu

"Akasema: "Siyo ilimu ya ghaibu,bali ni mafundisho kutoka kwa mwenye elimu." Akimaanisha Mtume(s.a.w.w) ambaye naye ameichukua kutokana na Wahyi.

3

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TISA

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُهُمْ وَلَا يَضُرُّهُمْ وَكَانَ الْكَافِرُ عَلَىٰ رَبِّهِ ظَهِيرًا ﴿٥٥﴾

55. Na wanaabudu wasiowadhuru wala kuwanufaisha badala ya Mwenyezi Mungu. Na kafiri daima ni msaidizi wa mpinzani wa Mola wake.

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا مُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿٥٦﴾

56. Na hatukukutuma ila uwe mbashiri na muonyaji.

قُلْ مَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِلَّا مَن شَاءَ أَن يَتَّخِذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا ﴿٥٧﴾

57. Sema: Siwaombi ujira juu yake, isipokuwa mwenye kutaka ashike njia iendayo kwa Mola wake.

وَتَوَكَّلْ عَلَى الْحَيِّ الَّذِي لَا يَمُوتُ وَسَبِّحْ بِحَمْدِهِ وَكَفَىٰ بِهِ بِذُنُوبِ عِبَادِهِ خَبِيرًا ﴿٥٨﴾

58. Na mtegemee aliye hai ambaye hafi na umtukuze kwa sifa zake. Na yatosha kuwa yeye ni mwenye habari za dhambi za waja wake.

الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ الرَّحْمَـٰنُ فَاسْأَلْ بِهِ خَبِيرًا ﴿٥٩﴾

59. Ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha akastawi juu ya Arshi. Mwingi wa rehema! Uliza habari zake kwa ajuaye.

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اسْجُدُوا لِلرَّحْمَـٰنِ قَالُوا وَمَا الرَّحْمَـٰنُ أَنَسْجُدُ لِمَا تَأْمُرُنَا وَزَادَهُمْ نُفُورًا ﴿٦٠﴾

60. Na wanapoambiwa msujudieni Mwingi wa rehema, wanasema: Ni nani huyo mwingi wa rehema? Je, tumsujudie unayetuamrisha wewe? Na huwazidishia chuki.

تَبَارَكَ الَّذِي جَعَلَ فِي السَّمَاءِ بُرُوجًا وَجَعَلَ فِيهَا سِرَاجًا وَقَمَرًا مُّنِيرًا ﴿٦١﴾

61. Amekuwa na baraka yule aliyejaalia katika mbingu buruji na akajaalia humo taa na mwezi wenye nuru.

وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ خِلْفَةً لِّمَنْ أَرَادَ أَن يَذَّكَّرَ أَوْ أَرَادَ شُكُورًا ﴿٦٢﴾

62. Naye ndiye ambaye ameujaalia usiku na mchana kufuatana, kwa yule anayetaka kukumbuka au anayetaka kushukuru.

KAFIRI NI MSADIZI WA MPINZANI WA MOLA WAKE

Aya 55 – 62

MAANA

Na wanaabudu wasiowadhuru wala kuwanufaisha badala ya Mwenyezi Mungu.

Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 11 (10 18).

Na kafiri daima ni msaidizi wa mpinzani wa Mola wake.

Yaani anawasaidia watu wa batili dhidi ya haki. Kila mwenye kusaidia batili atakuwa amesaidia dhidi ya Mwenyezi Mungu na kuwa adui yake; hata kama atamsabihi na kumtukuza kwa ulimi wake. Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :“Mwenye kumsaidia dhalimu na huku anajua kuwa ni dhalimu basi amejitenga na Uislamu.”

Kadiri nitakavyotia shaka, lakini siwezi kutia shaka kuwa mwenye kumtegemea dhalimu ni kafiri; bali kafiri aliye mwadilifu ni bora kuliko yeye. Aya za Qur’an kuhusu hilo ni nyingi na ziko wazi. Ama Hadith za Mtume zimepituka kiwango cha mutawatir.

Ndio! Ni wajibu wetu kuamiliana naye muamala wa kiislamu kwa vile tu ametamka: Lailaha illallah Muhammadurrasulullah (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.)

Na hatukukutuma ila uwe mbashiri na muonyaji.

Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 15 (17:105).

Sema: Siwaombi ujira juu yake, isipokuwa mwenye kutaka ashike njia iendayo kwa Mola wake.

Mimi sina tamaa ya mali yenu wala siwauzii pepo. Ninalotaka ni kutengeneza tu. Anayetaka kufanya njia ya kumwendea Mola miongoni mwenu, basi malipo yake yako kwa Mungu. Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:90) na Juz.12 (11:88).

Na mtegemee aliye hai ambaye hafi na umtukuze kwa sifa zake. Na yatosha kuwa yeye ni mwenye habari za dhambi za waja wake.

Ewe Muhammad! Toa bishara na onyo ukimtegemea Mwenyezi Mungu kwa kuwa na ikhlasi naye katika kauli yako na vitendo vyako na ujitakashe na kumfanyia mfano na kila lile ambalo halifanani na utukufu na ukuu wake. Yeye anamjua zaidi aliyepotea njia, na atamhisabu na kumlipa.

Ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha akastawi juu ya Arshi.

Makusudio ya kustawi ni kutawala. Lililo na nguvu ni kuwa makusudio ya siku ni mikupuo, kwa sababu hakuna siku kabla ya kupatikana ulimwengu na jua. Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:54), Juz. 11 (103), na Juz. 12 (11:7).

Mwingi wa rehema! Uliza habari zake kwa ajuaye.

Habari yake, ni habari ya huko kuumbwa mbingu na ardhi, ambako kunafahamika kutokana na mfumo wa Aya. Hapa kuna maneno yaliyotan- gulizwa na ya kukadiriwa. Maana ni: Yeye ni Mwingi wa rehema, ulizia habari za kuumbwa mbingu na ardhi kwa yule ajuaye ambaye ni Mwenyezi Mungu.

Na wanapoambiwa msujudieni Mwingi wa rehema, wanasema: ‘Ni nani huyo mwingi wa rehema? Je, tumsujudie unayetuamrisha wewe?’ Na huwazidishia chuki.

Nabii(s.a.w.w) akiwaambia washirikina: ‘Mwabuduni Mwingi wa rehema, wala msiabudu masanamu,’ wao husema kwa kujitia hamnazo, kwa madharau, ni nani huyo unayetuambia tumwabudu unayemuita Mwingi wa rehema? Unataka tukutii wewe na tuwaasi baba zetu katika yale waliyokuwa wakiyaabudu?’

Ujinga na upumbavu huu unatukumbusha ujinga wa vijana wetu wanapoambiwa swalini na mfunge, husema: “Bado kuna Swala katika karne hii ya ishirini? Jambo la kushangaza ni kuwa vijana hawa wanaimba uhuru wa bianadamu; kama kwamba uhuru ni uzandiki na utu ni kujitoa kwenye misimamo.

Hawajui kuwa aliye huru ni yule anayemwabudu Mwenyezi Mungu wala hamnyenyekei asiyekuwa yeye na kwamba utu ni dini ya Mwenyezi Mungu ambayo inakataza maovu na munkar.

Amekuwa na baraka yule aliyejaalia katika mbingu buruji na akajaalia humo taa na mwezi wenye nuru.

Makusudio ya buruji ni mashukio ya jua na mwezi. Tazama Juz.14 (15: 16). Makusudio ya taa hapa ni jua, kutokana na kuunganisha na mwezi. Mahali pengine Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

هُوَ الَّذِي جَعَلَ الشَّمْسَ ضِيَاءً وَالْقَمَرَ نُورًا ﴿٥﴾

“Yeye ndiye aliyefanya jua kuwa mwanga na mwezi kuwa nuru.” Juz.11 (10:5).

Wengine wametofautisha baina ya nuru na mwanga. Kwamba mwanga unategemea sayari moja kwa moja; kama vile mwanga wa jua, unatoka kwenye jua moja kwa moja.

Nuru inategemea sayari kupitia sayari nyingine; kama vile nuru ya mwezi inavyotegmea jua. Wametoa dalili wanaotofautisha, kwa Aya hiyo ya Juz. 11 (10:5) tuliyoitaja punde.

Naye ndiye ambaye ameujaalia usiku na mchana kufuatana, kwa yule anayetaka kukumbuka au anayetaka kushukuru.

Usiku unaondoka kisha unakuja mchana, nao unaondoka kisha unarudi usiku na kuendelea; wala hakuna unaobakia muda mrefu kuzidi kiasi cha haja ya viumbe.

Kufuatana kwa namna hii kunafahamisha kuweko mpangiliaji mwenye hekima. Kufuatana huku kunategemea harakati za ardhi, nazo zinategemea msababishaji wake wa kwanza.

Ama hekima ya mfuatano huu, ni kwamba lau lingelibakia giza tu, au mwangaza tu, maisha yangelikuwa magumu hapa ardhini.

Kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t) ‘Kwa anayetaka kukumbuka,’ maana yake ni kuwa mwenye kutaka dalili ya kuweko Mwenyezi Mungu ataipata katika vitu vyote, vikiwemo kufuatana usiku na mchana.

Na kauli yake ‘Au anayetaka kushukuru,’ ni kuwa anayetaka kumshukuru Mweneyzi Mungu kwa neema yake naashukuru vile vile kwa kufuatana usiku na mchana, kwa sababu hilo ni katika neema kubwa.

وَعِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا ﴿٦٣﴾

63. Na waja wa Mwingi wa rehema ni wale wanaotembea ardhini kwa unyenyekevu. Na wajinga wakiwasemesha, husema: ‘Salama.’

وَالَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا ﴿٦٤﴾

64. Na wale wanaokesha kwa ajili ya Mola wao kusujudu na kusimama.

وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا ﴿٦٥﴾

65. Na wale wanaosema: ‘Mola wetu! Tuondolee adhabu ya Jahannam,’ hakika adhabu yake ni yenye kuendelea.

إِنَّهَا سَاءَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا ﴿٦٦﴾

66. Hakika hiyo ni mbaya kuwa kituo na mahali pa kukaa.

وَالَّذِينَ إِذَا أَنفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَٰلِكَ قَوَامًا ﴿٦٧﴾

67. Na wale ambao wanapotumia hawafanyi israfu wala hawafanyi uchoyo wanakuwa katikati baina ya hayo.

وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا ﴿٦٨﴾

68. Na wale ambao hawamwombi mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaiui nafsi aliyoiharamisha ila kwa haki, wala hawazini. Na mwenye kuyafanya hayo atapata madhambi.

يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا ﴿٦٩﴾

69. Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama na atadumu humo kwa kufedheheka.

إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٠﴾

70. Isipokuwa atakayetubia na akatenda matendo mema, basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللَّـهِ مَتَابًا ﴿٧١﴾

71. Na aliyetubu na akafanya mema, basi hakika huyo ametubu kwa Mwenyezi Mungu toba ya kweli.

وَالَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ الزُّورَ وَإِذَا مَرُّوا بِاللَّغْوِ مَرُّوا كِرَامًا ﴿٧٢﴾

72. Na wale ambao hawawi kwenye uzushi, na wanapopita kwenye upuzi hupita kwa heshima zao.

وَالَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ لَمْ يَخِرُّوا عَلَيْهَا صُمًّا وَعُمْيَانًا ﴿٧٣﴾

73. Na wale ambao wanapokumbushwa ishara za Mola wao hawajifanyi ni viziwi nazo na vipofu.

وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا ﴿٧٤﴾

74. Na wale ambao wanasema: Mola wetu! Tupe katika wake zetu na wanetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wenye takua.

أُولَـٰئِكَ يُجْزَوْنَ الْغُرْفَةَ بِمَا صَبَرُوا وَيُلَقَّوْنَ فِيهَا تَحِيَّةً وَسَلَامًا ﴿٧٥﴾

75. Hao ndio watakolipwa ghorofa kwa walivyosubiri na watakuta humo maamkuzi na salaam.

خَالِدِينَ فِيهَا حَسُنَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا ﴿٧٦﴾

76. Watadumu humo kituo na makao mazuri.

قُلْ مَا يَعْبَأُ بِكُمْ رَبِّي لَوْلَا دُعَاؤُكُمْ فَقَدْ كَذَّبْتُمْ فَسَوْفَ يَكُونُ لِزَامًا ﴿٧٧﴾

77. Sema, Mola wangu asingewajali lau si kupewa kwenu mwito, lakini nyinyi mmewakadhibisha, basi (adhabu) ni lazima.

WAJA WA MWINGI WA REHEMA

Aya 63 – 77

MAANA

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutaja sifa za makafiri na kiaga chao, kama kawaida yake, anataja sifa za waumini na malipo aliyowaandalia. Zifuatazo ndizo sifa zao:

1.Na waja wa Mwingi wa rehema ni wale wanaotembea ardhini kwa unyenyekevu.

Imam Jafar Sadiq(a.s) anasema katika tafsiri ya hilo:“Ni yule mtu anayetembea kwenye asili yake aliyoumbiwa, hajikalifishi wala hajifanyi.” Ndio, anayetembea kwenye umbile lake aliloumbiwa, tena akiwa peke yake bila ya kuwa na wapambe na wafuasi wanaomfuta nyuma na wengine mbele wakiwa wamepanda farasi au pikipiki na kupiga ving’ora vinavyohanikiza watu kwa sauti zake vikitangaza kuja kwake ili aachiwe njia, kwa ajili ya kumheshimu na kumtukuza.

2.Na wajinga wakiwasemesha, husema: ‘Salama.’

Makusudio ya kusemeshwa na wajinga ni kama vile kejeli zao, shutuma zao au mijadala ya hawa na masilahi. Amani ni kinaya cha kuachana nao, kwa kuwadharau na kuchunga mtu heshima yake. Maana ni kuwa, muumini akisikia neno ovu, aachane nalo; kama kwamba hakulisikia au kama anayekusudiwa ni mwingine sio yeye. Huu ndio mwepuko mwema aliousema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَاهْجُرْهُمْ هَجْرًا جَمِيلًا ﴿١٠﴾

“Na uwaepuke mwepuko mwema.” (73:10).

Hakuna mwenye shaka kwamba kuachana na jambo ni pale ikiwa hakuna uwezo au nguvu za kulikabili. Vinginevyo itakuwa ni wajibu kulikabili. Hapana budi kuihusisha Aya na hilo.

3.Na wale wanaokesha kwa ajili ya Mola wao kusujudu na kusimama.

Waumini wanasimama usiku kwenye giza wakifanya ibada ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu hilo liko mbali na ria, wala hawaupitishi usiku mikahawani na kwenye mambo ya mchezo mchezo tu, huku wakifuja mali na kupanga njama dhidi ya waumini na wenye ikhlasi. Mfano wa Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:

كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ ﴿١٧﴾

“Walikuwa wakilala kidogo usiku.” (51:17).

4.Na wale wanaosema: ‘Mola wetu! Tuondolee adhabu ya Jahannam, hakika adhabu yake ni yenye kuendelea. haikwepeki na ni yakudumu. Hakika hiyo ni mbaya kuwa kituo na mahali pa kukaa,

Waliamini Pepo na Moto, kutokana na waliyoyashuhudia na kuyaona; ndio wakauhofia moto wakaitumai pepo. Imam Ali(a.s ) anasema: “Wao na Pepo ni kama walioiona wakiwa ndani yake wananeemeshwa. Na wao na moto ni kama waliouona wakiwa ndani yake wanaadhibiwa.”

5.Na wale ambao wanapotumia hawafanyi israfu wala hawafanyi uchoyo wanakuwa katikati baina ya hayo, hakuna kupitisha kiasi, Si ubakhili wala ubadhirifu.

Huu ndio mwenendo wa Uislamu, wastani katika kila kitu; hakuna ulahidi wala waungu wengi, udikteta wala ukiritimba na hakuna kutaifisha mali ya mtu wala ubepari. Tazama Juz. 15 (17:29) kifungu cha ‘Uislamu na nadharia ya maadili.’

6.Na wale ambao hawamwombi mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu.

Mwenye kufanya riya au akamtii kiumbe katika kumuasi Muumba, basi huyo ni kama aliyemwomba mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu.

Wala hawaiui nafsi aliyoiharamisha ila kwa haki.

Nafsi inayouliwa kwa haki na kwa uadilifu ni ile iliyoua nafsi nyingine bila ya haki, aliyezini akiwa kwenye ndoa, kurtadi dini au kuleta ufisadi katika ardhi.

Ufafanuzi wa hayo uko katika vitabu vya Fiqh.

Wala hawazini

Kwa sababu zinaa ni katika madhambi makubwa. Ndio maana Mwenyezi Mungu (s.w.t). Akaiweka sawa na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kuua nafsi na akajaalia hukumu ya haya matatu ni kuuliwa kwa masharti yaliyotajwa kwenye vitabu vya fiqh.

Na mwenye kuyafanya hayo atapata madhambi.

Hayo ni hayo ya shirk, kuua na kuzini. Na madhambi ni adhabu.

Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama na atadumu humo kwa kufedheheka.

Kuna adhabu gani kubwa na kufedheheka zaidi kuliko adhabu ya Jahannam? Si kwambii tena ikiwa itazidishwa pamoja na kudumu kusiko na mwisho.

Isipokuwa atakayetubia na akatenda matendo mema, basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mwenye kurehemu.

Mwenye kutubia dhambi ni kama asiyekuwa na dhambi, zaidi ya hayo, Mwenyezi Mungu atampa thawabu kwa kule kutubia kwake na atampa mema kulingana na maovu ya dhambi zake; kiasi ambacho toba itafuta maovu ya dhambi.

إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ﴿١١٤﴾

“Hakika mema huondoa maovu.” Juz. 12 (11:114).

Haya ndiyo maana ya ‘Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema’ kwa sababu uovu, kwa ulivyo, haustahiki kuwa wema, wala wema, kwa ulivyo, haustahiki kuwa uovu’

Na aliyetubu na akafanya mema, basi hakika huyo ametubu kwa Mwenyezi Mungu toba ya kweli.

Baada ya kubainisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika Aya iliyotangulia kwamba mwenye kutubia atampa thawabu za mwenye kufanya mema, hapa anamsifu kuwa amerejea kwa Muumba wake kurejea kuzuri.

7.Na wale ambao hawawi kwenye uzushi, na wanapopita kwenye upuzi hupita kwa heshima zao.

Neno ‘hawawi’ limefasiriwa kutokana na neno la kiarabu ‘laa yash-hadu- una’ kama ilivyotumika tafsiri hiyo katika Juz. 2 (2:185). Makusudio ya uzushi ni mambo ya batili na upuzi ni kila lisilo na kheri. Maana ni kuwa waumini hawahudhurii vikao vya ubatilifu wala hawavisaidii, sikwambii kuvifanya. Pia hawashiriki mazungumzo yasiyokuwa na kheri na wanapoyapitia hayo masiko yao huyaepuka; kama wanavyoziepusha ndimi zao kuayatamka; sawa na nyuki anavyopita haraka kwenye mzoga na harufu mbaya.

8.Na wale ambao wanapokumbushwa ishara za Mola wao hawaji- fanyi ni viziwi nazo na vipofu.

Mshairi huwa anasikiliza mashairi kwa umakini kabisa. Vile vile kila mwenye kuhusika na jambo akizungumziwa huwa anakuwa makini nalo sana anapolisikilza. Mtu unapomzungumzia jambo lililo mbali naye atakuepuka na hayo mazungumzo yako, hata kama ni ya uongofu na mwangaza.

Hapa ndipo inabainika siri ya muumini kuikubali Qur’an, na kafiri kuachana nayo. Mumin anakikubali Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa vile anakiamini na kutambua maana yake na makusudio yake. Anakikuta kwenye nafsi yake, itikadi yake, matendo yake mema na malipo aliyomuandalia Mola wake.

Kafiri anakipa mgongo Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa sababu anakipinga na hajui malengo yake na siri yake; wala hapati humo isipokuwa kushutumiwa na kukosolewa itikadi yake na sifa zake na pia makaripio ya ukafiri wake.

9.Na wale ambao wanasema: Mola wetu! Tupe katika wake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wenye takua.

Muovu huwa anatamaani watu wamfuate katika uovu wake, sio kwa kuwa amekinai kuwa yuko kwenye uongofu kutoka kwa Mola wake, hapana! Isipokuwa anataka kupunguza lawama na shutuma na kufunika kosa lake kwa kuwa wengi wakosefu. Lakini hataki mkewe na watoto wake wawe hivyo; kama vile mgonjwa asivyopenda watu wake wapatwe na ugonjwa alio nao.

Ama yule aliye mwema na mwenye takua ana yakini na dini yake na ana busara katika mambo yake. Kwa hivyo huwa anatamaani kwa dhati ya moyo kimsingi na kiitikadi kuwa watu wote wafuate njia yake na kwamba watoto wake wakimuiga yeye huwa anafurahi.

Kwa hiyo wenye ikhlasi humuomba Muumba wao wapate wa kuwaiga, sio kwa kuziba vitendo vyao kwa watu wala kutaka jaha duniani na kuchukua mali kwa kutumia haki za Mwenyezi Mungu; bali ni kwa kujipendekeza mbele ya Mwenyezi Mungu aliye peke yake.

Hao ndio watakaolipwa ghorofa kwa walivyosubiri na watakuta humo maamkuzi na salaam. Watadumu humo kituo na makao mazuri.

Ghorofa ni kinaya cha makao ya juu. Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kubainisha wasifu wa wenye takua na watiifu, sasa anataja malipo yao watakayoyapata kwake, ambayo ni kudumu katika raha, amani na neema pamoja na heshima.

Mwenyezi Mungu amehusisha kutaja subira hapa kuashiria kuwa kila mwenye haki hana budi kupata taabu na udhia kutoka kwa wasio na haki na kwamba thawabu za Mwenyezi Mungu hatazipata ispokuwa mwenye kuwa na uvumilivu na subira na akaendelea kuwa na msimamo kadiri hali itakavyokuwa ngumu.

Sema, Mola wangu asingewajali lau si kupewa kwenu mwito, lakini nyinyi mmewakadhibisha, basi (adhabu) ni lazima.

Makusudio ya neno ‘duakum’ hapa ni kupewa mwito kutokana na maneno yanayovutia, lakini mlikadhibisha. Ni mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu:

فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا لَهُمْ ﴿٥٢﴾

“Basi watawaita nao hawatawaitikia.” Juz. 15 (18:52)

Kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwapa mwito kwenye imani na utiifu kupitia kwa Mtume wake.

Maana ni kuwa nyinyi washirikina hamstahiki hata kutajwa pia lau si kuwa mliitwa kwenye imani na utiifu, ili kuweko na hoja siku ya hisabu na malipo, ikiwa hamtasikia na kuitikia mwito. Nanyi mmeupinga mwito na mkadhibishaji aliyetoa mwito huo, basi adhabu inawastahiki na ni lazima.

Sura Ya Ishirini Na Sita: Surat Shua’rau.

Twabrasiy amesema imeshuka Makka isipokuwa Aya 224 hadi mwisho, zimeshuka Madina. Ina Aya 227

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu.

طسم ﴿١﴾

1. Twaa Siin Miim.

تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿٢﴾

2. Hizo ni Aya za Kitabu kinachobainisha.

لَعَلَّكَ بَاخِعٌ نَّفْسَكَ أَلَّا يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ ﴿٣﴾

3. Huenda ukaiangamiza nafsi yako kwa kuwa hawawi waumini.

إِن نَّشَأْ نُنَزِّلْ عَلَيْهِم مِّنَ السَّمَاءِ آيَةً فَظَلَّتْ أَعْنَاقُهُمْ لَهَا خَاضِعِينَ ﴿٤﴾

4. Tungelipenda tungeliwateremshia kutoka mbinguni ishara zikainyenyekea shingo zao.

وَمَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ مُحْدَثٍ إِلَّا كَانُوا عَنْهُ مُعْرِضِينَ ﴿٥﴾

5. Na hauwajii ukumbusho mpya kutoka kwa Mwingi wa rehema ila hujitenga nao.

فَقَدْ كَذَّبُوا فَسَيَأْتِيهِمْ أَنبَاءُ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٦﴾

6. Kwa hakika wamekadhibisha, kwa hivyo zitakujawafikia habari za yale waliyokuwa wakiyafanyia stihizai.

أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَى الْأَرْضِ كَمْ أَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ ﴿٧﴾

7. Je hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri.

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٨﴾

8. Hakika katika hayo kuna ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٩﴾

9. Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.

HUENDA UKAANGAMIZA NAFSI YAKO

Aya 1-9

MAANA

Twaa Siin Miim.

Umetangulia mfano wake mwanzo wa Sura Baqara, Juz. 1

Hizo ni Aya za Kitabu kinachobainisha.

Hizo ni ishara ya Aya za Sura hii, kitabu ni Qur’an na chenye kubainisha ni kubainisha haki na kudhihirisha.

Huenda ukaiangamiza nafsi yako kwa kuwa hawawi waumini.

Maneno yanaelekezwa kwa Muhammad(s.a.w.w) kwamba asiikere na kuiumiza nafsi yake kwa sababu ya watu wake kuukataa uongofu na haki. Umetangulia mfano wake katika Juz.7 (6:35) na Juz. 15 (18:6).

Tungelipenda tungeliwateremshia kutoka mbinguni ishara zikainyenyekea shingo zao.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamwambia Mtume wake mtukufu: Poa moyo wako! Lau tungelitaka waamini kwa nguvu tungeliteremsha adhabu kutoka mbinguni waione kwa macho na kuwaambia chagueni imani au adhabu; bila shaka wao wangelisalimu amri kwa unyenyekevu.

Lakini je, hii itahisabiwa kuwa ni imani? Hapana! Imani ya kweli inakuwa kwa utashi na hiyari, sio kwa kulazimishwa kwa nguvu. Ndio maana tukawakadiria kheri na shari, tukawaamrisha hili na kuwakataza lile; kisha tukawaachia hiyari, waweze kustahiki thawabu kwa utiifu na adhabu kwa uasi.

Unaweza kuuliza : Mwenyezi Mungu (s.w.t) alifanya hivyo katika zama za Musa(a.s) kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na tulipoinua mlima juu yao kama kwamba ni kiwingu kilichowafunika na wakadhani kuwa utawaangukia. Tukawaambia: shikeni kwa nguvu tuliyowapa.” Juz. 9 (7: 171).

Jibu : kwa hakika Qur’an Tukufu inafahamisha waziwazi kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ana muamala maalum na Mayahudi usiofanana na waja wengine. Kwa sababu wao wana tabia za pekee zisizokuwa na mfano. Tumelizungumzia hilo kwa ufafanuzi zaidi kwa anuani ya ‘Mayahudi hawana mfano’ katika Juz. 1: (2:63-66).

Na hauwajii ukumbusho mpya kutoka kwa Mwingi wa rehema ila hujitenga nao. Kwa hakika wamekadhibisha, kwa hivyo zitakujawafikia habari za yale waliyokuwa wakiyafanyia stihizai.

Tumewaongoza washirikina, kupitia kwako ewe Muhammad, kwenye yale yaliyo na kheri yao na masilahi yao, wakaachana nayo, wakayadharau na kuyafanyia masikhara. Basi nawe achana nao na watakumbana na adhabu waliyoahidiwa tu. Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:68).

Je hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri. Hakika katika hayo kuna ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.

Alikufuru Mungu aliyekufuru huku akiona dalili na ubainifu wa kupatikana kwake na ukuu wake. Miongoni mwa dalili hizi ni kutoa mimea ya aina na rangi mbali mbali. Kwa maelezo zaidi angalia Juz.7 (6:99) na Juz. 13 (13:3).

Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.

Kwa nguvu zake anawashinda mataghuti na rehema zake anawapa muda bila ya kuwaharakishia adhabu mpaka awajie mbashiri na muonyaji na kuwapa fursa ya kufikiria vizuri na kutubia.

Imam Ali(a.s) anasema:“Hasira zake hazimfanyi kuacha huruma yake, wala huruma haimfanyi kupuuza adhabu yake.”

وَإِذْ نَادَىٰ رَبُّكَ مُوسَىٰ أَنِ ائْتِ الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠﴾

10. Na Mola wako alipomwita Musa kwamba nenda kwa watu madhalimu.

قَوْمَ فِرْعَوْنَ أَلَا يَتَّقُونَ ﴿١١﴾

11. Watu wa Firauni. Hawaogopi?

قَالَ رَبِّ إِنِّي أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ ﴿١٢﴾

12. Akasema: Mola wangu! Hakika mimi naogopa watanikadhibisha.

وَيَضِيقُ صَدْرِي وَلَا يَنطَلِقُ لِسَانِي فَأَرْسِلْ إِلَىٰ هَارُونَ ﴿١٣﴾

13. Na kifua changu kinadhikika, na ulimi wangu haukunjuki vyema, basi mtumie ujumbe Harun.

وَلَهُمْ عَلَيَّ ذَنبٌ فَأَخَافُ أَن يَقْتُلُونِ ﴿١٤﴾

14. Nao wanalo kosa juu yangu basi naogopa wasije wakaniua.

قَالَ كَلَّا فَاذْهَبَا بِآيَاتِنَا إِنَّا مَعَكُم مُّسْتَمِعُونَ ﴿١٥﴾

15. Akasema, sivyo kabisa! Nendeni na ishara yetu. Hakika sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza.

فَأْتِيَا فِرْعَوْنَ فَقُولَا إِنَّا رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦﴾

16. Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni wajumbe wa Mola wa walimwengu wote.

أَنْ أَرْسِلْ مَعَنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿١٧﴾

17. Ya kwamba uwaachilie wana wa Israil waende nasi.

قَالَ أَلَمْ نُرَبِّكَ فِينَا وَلِيدًا وَلَبِثْتَ فِينَا مِنْ عُمُرِكَ سِنِينَ ﴿١٨﴾

18. Akasema: Je, hatukukulea utotoni, na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi?

وَفَعَلْتَ فَعْلَتَكَ الَّتِي فَعَلْتَ وَأَنتَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿١٩﴾

19. Na ukatenda kitendo chako ulichokitenda, nawe ukawa miongoni mwa wasio na shukrani?

قَالَ فَعَلْتُهَا إِذًا وَأَنَا مِنَ الضَّالِّينَ ﴿٢٠﴾

20. Akasema: Nililifanya hilo nikiwa miongoni mwa wasioelewa.

فَفَرَرْتُ مِنكُمْ لَمَّا خِفْتُكُمْ فَوَهَبَ لِي رَبِّي حُكْمًا وَجَعَلَنِي مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٢١﴾

21. Basi niliwakimbia nilipowahofia. Na Mola wangu akanitunukia hukumu na akanijaalia niwe miongoni mwa mitume.

وَتِلْكَ نِعْمَةٌ تَمُنُّهَا عَلَيَّ أَنْ عَبَّدتَّ بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿٢٢﴾

22. Na hiyo ndiyo neema ya kunisimbulia na wewe umewatia utumwani wana wa Israil?

MUSA

Aya 10 – 22

MAANA

Aya hizi hadi kufikia Aya ya 28 ni za kisa cha Musa ambacho kimetangulia mara kadhaa. Katika Juz. 16 (20: 9) tumeleza sababu za kukaririka kisa hicho.

Na Mola wako alipomwita, Musa kwamba nenda kwa watu madhal- imu watu wa Firauni.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (20:24).

Hawaogopi?

Hii ni jumla nyingine, maana yake ni kuwa, umefika wakati sasa Firauni na watu wake waogope mwisho wa uovu na utaghuti.

Akasema: Mola wangu! Hakika mimi naogopa watanikadhibisha.

Katika Juz. 16 (20 45) ni: “Ewe Mola wetu! Hakika sisi tunaogopa asije akapindukia mipaka juu yetu au kufanya jeuri.”

Yaani asije akatuwahi kutuadhibu kabla kufikishia ujumbe.

Na kifua changu kinadhikika, na ulimi wangu haukunjuki vyema, basi mtumie ujumbe Harun.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimtuma Musa kupeleka ujumbe wake kwa Firauni. Na hili, kwa upande mmoja, ni jambo zito na lenye mashaka sana, kutokana na utaghuti wa Firauni na nguvu za utawala wake. Na kwa upande mwingine, ujumbe wenyewe ni mzito.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimwambia Mtume wake Muhammad(s.a.w.w) :

إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا ﴿٥﴾

“Hakika sisi tutakuteremshia kauli nzito.” (73:5).

Musa alikuwa ni mwepesi wa kughadhibika kwa ajili ya haki, na ulimi wake ulikuwa na kigugumizi kinachomzuia kutamka. Kwa hiyo akahofia kutotekeleza vizuri ujumbe mkuu. Hakuna yeyote anayehofia kutekeleza haki ya Mwenyezi Mungu kuliko mitume; hasa wale Ulul-a’zm. Hii inatokana na isma. Ndipo Musa akamtaka Mwenyezi Mungu kumtuma Jibril kwa nduguye, Harun, ili awe msaidizi wake katika jambo hili muhimu.

Nao wanalo kosa juu yangu basi naogopa wasije wakaniua.

Anaishiria lile tukio la kumuua mtu wa upande wa Firauni pale alipom- saidia mtu wa upande wake; kama ilivyoelezwa katika Aya hii:

فَوَجَدَ فِيهَا رَجُلَيْنِ يَقْتَتِلَانِ هَـٰذَا مِن شِيعَتِهِ وَهَـٰذَا مِنْ عَدُوِّهِ فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ فَوَكَزَهُ مُوسَىٰ فَقَضَىٰ عَلَيْهِ ﴿١٥﴾

“Na akakuta humo watu wawili wanapigana – mmoja ni katika wenzake na mwingine ni katika maadui zake. Yule aliye katika wenzake akamtaka msaada juu ya adui yake. Musa akampiga ngumi akammaliza.” (28:15).

Musa alihofia kuchukua risala ya Mwenyezi Mungu kwa Firauni asije akamuua kabla kukamilisha lengo, lakini akiwa na nduguye na ikatokewa kuuawa, basi atachukua nafasi yake kuendeleza malengo.

Akasema – Mwenyezi Mungu –sivyo kabisa! Nendeni na ishara yetu, Hakika sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza. Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni wajumbe wa Mola wa walimwengu wote. Ya kwamba uwaachilie wana wa Israil waende nasi.

Musa alihofia dhiki ya kifua, kufungika ulimi na kuuliwa, lakini Mwenyezi Mungu akamhakikishia usalama na akamwambia kuwa hakuna kitu kitaka- chokuwa katika hayo, kwa sababu mimi nitawasaidia na kuwanusuru. Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (20: 46 – 47).

Akasema: Je, hatukukulea utotoni, na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi? Na ukatenda kitendo chako ulichokitenda, nawe ukawa miongoni mwa wasio na shukrani?

Musa na Harun walielekea kwa Firauni, wakaingia kwake wakiwa wamevaa deraya ya sufu, mikononi mwao wakiwa na fimbo. Wakampa mwito wa kumwamini Mungu na kumpa sharti la kusilimu na kutii ili utawala wake ubakie na kudumu enzi yake.

Firauni aliwabeza wawili hawa, waliompa masharti ya kudumu utawala na enzi yake, wakiwa hawana cheo chochote wala mali. Hakutaka kuwaua kwa kuhofia asiambiwe kuwa ameshindwa na hoja akakimbilia upanga.

Lakini Firauni anaweza kuwa na hoja gani? Ni kwa mantiki gani atakayoweza kujadili? Hana kitu isipokuwa kuvungavunga na kumtajia Musa yaliyopita.

Je, hatukukulea na ukakaa nyumbani kwetu miaka, kisha ukatuulia mtu wetu na ukakimbia? Hii ndio shukrani yako? Zaidi ya hayo unadai kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwetu? Unataka tukusikize na kukutii na sisi ndio mabwana zako na wafadhili wa neema zako?

Kisha Firauni akawegeukia watu wa baraza lake na akasema: “Basi mbona hakuvikwa vikukuku vya dhahabu?” (43:53). Kwenye dhahabu tu ndio kuna kuwa na siri ya mantiki ya mataghuti. Hakuna utume wala ubwana au ubora isipokuwa kwa ajili ya dhahabu na dhahabu yenyewe.

Musa (a.s) akamjibu kuhusu kuua akasema: “Nililifanya hilo nikiwa miongoni mwa wasioelewa.”

Yaani sikuelewa kuwa ngumi yangu itamuua. Nami nilikusudia kukinga na kutia adabu, nikakosea makusudio. Basi mimi nina dhambi gani katika hilo? Kukusudia ni nguzo ya msingi ya kosa la jinai kwa watu wa sharia.

Basi niliwakimbia nilipowahofia.

Sikukimbia hukumu ya uadilifu, bali nilikimbia dhulma kwa kuhofia kunichukulia kuwa ni muuaji wa makusudi. Kuna mmoja alimwambia Musa:

إِنَّ الْمَلَأَ يَأْتَمِرُونَ بِكَ لِيَقْتُلُوكَ فَاخْرُجْ إِنِّي لَكَ مِنَ النَّاصِحِينَ ﴿٢٠﴾

“Hakika wakubwa wanashauriana kukuua. Basi toka! Hakika mimi ni katika wanaokupa nasaha.” (28:20).

Na Mola wangu akanitunukia hukumu na akanijaalia niwe miongoni mwa mitume.

Firauni alimtajia Musa ufukara na utoro; Musa naye akamwambia kuwa utukufu haupimwi kwa mali wala kwa ufalme; isipokuwa uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu, humpatia amtakaye katika waja wake. Na mimi Mwenyezi Mungu amenitunukia elimu ya dini yake na sharia yake kwa njia ya kheri na usawa na akanitukuza kwa kunituma kwako na kwa watu wako.

Musa aliendelea kumjibu Firauni, kuhusu malezi na akasema:

Na hiyo ndiyo neema ya kunisimbulia na wewe umewatia utumwani wana wa Israil?

Yaani unanisimbulia kwa malezi yako kwangu na unajitia kutojua kuwa sababu ni uadui wako wa kuwachinja watoto wa kiume wa watu wangu na kuwatia utumwani watoto wao wa kike? Mama yangu alipohofia wewe kunichinja akanitupa baharini na matokeo yake yakawa ni kuishi mimi mbali ugenini bila ya huruma ya mama na mapenzi ya baba? Hii ndiyo fadhila yako kwangu? Firauni alizibwa mdomo, akaanza kuwatafuta wabatilifu wake; kama utakavyoona katika kifungu kifuatacho.

قَالَ فِرْعَوْنُ وَمَا رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٢٣﴾

23. Akasema Firauni: Na ni nani huyo Mola wa walimwengu wote?

قَالَ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ ﴿٢٤﴾

24. Akasema: Ni Mola wa mbingu na ardhi ikiwa nyinyi mna yakini.

قَالَ لِمَنْ حَوْلَهُ أَلَا تَسْتَمِعُونَ ﴿٢٥﴾

25. Akawaambia waliomzunguuka: Je, hamsikii?

قَالَ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ ﴿٢٦﴾

26. Akasema: Ni Mola wenu na Mola wa baba zenu wa kwanza.

قَالَ إِنَّ رَسُولَكُمُ الَّذِي أُرْسِلَ إِلَيْكُمْ لَمَجْنُونٌ ﴿٢٧﴾

27. Akasema: Hakika mtume wenu mliyetumiwa ni mwenda wazimu.

قَالَ رَبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَمَا بَيْنَهُمَا إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٢٨﴾

28. Akasema: Ni Mola wa mashariki na magharibi na viliomo baina yake, ikiwa nyinyi mna akili.

قَالَ لَئِنِ اتَّخَذْتَ إِلَـٰهًا غَيْرِي لَأَجْعَلَنَّكَ مِنَ الْمَسْجُونِينَ ﴿٢٩﴾

29. Akasema: Kama ukimfanya mungu mwingine asiyekuwa mimi basi bila shaka nitakufanya miongoni mwa wafungwa.

قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكَ بِشَيْءٍ مُّبِينٍ ﴿٣٠﴾

30. Akasema: Ijapokuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi?

قَالَ فَأْتِ بِهِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٣١﴾

31. Akasema: Kilete basi kama wewe ni katika wakweli.

فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ ﴿٣٢﴾

32. Akaitupa fimbo, mara ikawa nyoka dhahiri.

وَنَزَعَ يَدَهُ فَإِذَا هِيَ بَيْضَاءُ لِلنَّاظِرِينَ ﴿٣٣﴾

33. Na akautoa mkono wake. Mara ukawa mweupe kwa watazamao.

قَالَ لِلْمَلَإِ حَوْلَهُ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ عَلِيمٌ ﴿٣٤﴾

34. Akasema kuwaambia wakuu waliomzunguka: Hakika huyu ni mchawi, mjuzi.

يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُم بِسِحْرِهِ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ ﴿٣٥﴾

35. Anataka kuwatoa katika ardhi yenu. Basi mnatoa shauri gani?

قَالُوا أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَابْعَثْ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ ﴿٣٦﴾

35. Wakasema: Mwache kidogo yeye na ndugu yake, na uwatume wakusanyao watu mijini.

يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَحَّارٍ عَلِيمٍ ﴿٣٧﴾

37. Wakuletee kila mchawi mkubwa, mjuzi.

MAJIBIZANO BAINA YA MUSA NA FIRAUNI

Aya 23 – 37

MAANA

Akasema Firauni: Na ninani huyo Mola wa walimwengu wote?

Ewe Musa! Wewe unadai kuwa ni Mtume wa Mola wa walimwengu wote; hebu tubainishie jinsi yake na hakika yake huyo Mola?

Akasema: “Ni Mola wa mbingu na ardhi ikiwa nyinyi mna yakini.”

Musa alisema: Mwenyezi Mungu hajulikani isipokuwa kwa sifa zake na athari zake; zikiwa ni pamoja na huku kuumbwa ulimwengu huu wa ajabu katika mpangilio wake na nidhamu yake. Basi fikirini na mzingatie ikiwa mna akili zinazoweza kutambua kuwa nidhamu hii haiwezekani ila kwa uweza wa ujuzi na hekima.

Firauniakawaambia waliomzunguuka: Je, hamsikii?

Yaani mnasikia maajabu hayo. Hatujawahi kusikia haya kwa mababa zetu wa kwanza.

Akasema: Ni Mola wenu na Mola wa baba zenu wa kwanza.

Musa alisema kwa kusisitiza kwamba Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa ulimwengu, muumba wenu na muumba wa baba zenu wa mwanzo na pia ndiye muumba wa huyu Firauni mnayemfanya mungu na kumwabudu.

Akasema: Hakika mtume wenu huyu mliyetumiwa ni mwenda wazimu.

Musa ni mwendawazimu katika mantiki ya Firauni, kwa nini? Kwa sababu amesema Firauni si mungu bali ni kiumbe. Mantiki haya ya kifirauni anayo kila anayedai asichokuwa nacho. Yeyote anayedai kuwa na elimu naye ni mjinga, ikhlasi naye ni mhaini au ukweli naye ni mrongo, basi yeye yuko katika mila ya Firauni na desturi yake. Lau atapata wanaomwamini atasema: Mimi ndiye mola wenu au simjui mungu mwingine kwenu zaidi ya mimi; kama alivyosema Firauni.

Akasema: Ni Mola wa mashariki na magharibi na viliomo baina yake, ikiwa nyinyi mna akili.

Musa aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa kila kitu. Akaashiria kuchomoza jua na kuchwa kwake, ambapo Firauni hawezi kujasiri kusema kuwa yeye ndiye anayelichomoza jua mashariki na kulipeleka magharibi.

Kwa hiyo alipigwa na butwaa aliposikia maneno haya kutoka kwa Musa; sawa na alivyopigwa na butwaa Namrud kabla yake, pale Ibrahim(a.s) alipomnyamazisha kwa kusema:

فَإِنَّ اللَّـهَ يَأْتِي بِالشَّمْسِ مِنَ الْمَشْرِقِ فَأْتِ بِهَا مِنَ الْمَغْرِبِ ﴿٢٥٨﴾

“Hakika Mwenyezi Mungu hulichomoza jua mashariki, basi wewe lichomoze magharibi.”

Juz. 3 (2:258).

Firauni alipoishiwa, alikereka, akawa anatoa vitisho naakasema: Kama ukimfanya mungu mwingine asiyekuwa mimi basi bila shaka nitakufanya miongoni mwa wafungwa.

Jela na kutesa ndio silaha pekee ya utawala muovu wa mabavu dhidi ya haki uadilifu na uhuru, tangu zamani. Lakini jihadi ya wakombozi na ukakamavu wao, unaifanya silaha ya mataghuti ishindwe kwenye shingo zao na vifua vyao; kama ilivyoshindwa silaha ya Firauni.

Walisema wa kale: Mwenye kuchomoa upanga wa dhulma atauliwa nao.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

فَكُلًّا أَخَذْنَا بِذَنبِهِ فَمِنْهُم مَّنْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِ حَاصِبًا وَمِنْهُم مَّنْ أَخَذَتْهُ الصَّيْحَةُ وَمِنْهُم مَّنْ خَسَفْنَا بِهِ الْأَرْضَ ﴿٤٠﴾

“Kila mmoja tulimtesa kwa makosa yake. Kati yao wapo tuliowapelekea kimbunga cha changarawe, na kati yao wapo walionyakuliwa na ukelele na kati yao wapo ambao tuliwadidimiza katika ardhi.” (29:40).

Akasema: Ijapokuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi?” Akasema: Kilete basi kama wewe ni katika wakweli.

Musa hakuogopa vitisho vya Firauni na akamwambia kwa kujiamini kuwa utanifanya mfungwa hata kama ni mwenye haki, kwa kukuletea dalili isiyo na shaka kwako na kwa mwingine?

Atajibu nini Firauni? Je, amwambie ndio nitakufunga hata kama ni mwenye haki? Hawezi kumwambia hivi, kwa sababu itakuwa ni kukubali ukweli kuwa Musa ni Mtume wa Mola wa viumbe wote na kwamba yeye ni mzushi katika madai yake ya uungu. Kwa hiyo ndio akalazimika kusema lete hiyo dalili kama wewe ni mkweli.

Akaitupa fimbo mara ikawa nyoka dhahiri. Na akautoa mkono wake. Mara ukawa mweupe kwa watazamao. Akasema kuwaambia wakuu waliomzunguka: Hakika huyu ni mchawi mjuzi. Anataka kuwatoa katika ardhi yenu. Basi mnatoa shauri gani? Wakasema: Mwache kidogo yeye na ndugu yake, na uwatume wakusanyao watu mijini. Wakuletee kila mchawi mkubwa, mjuzi.

Aya hizi sita zimetangulia katika Juz. 9 (7:107 - 112) zikifanana kiutaratibu, kimpangilio na hata herufi; isipokuwa katika mambo mawili:

Hapa imesemwa: ‘mchawi mkubwa’ na kule ikasemwa ‘mchawi’ hakuna tofauti katika maneno haya isipokuwa kutilia mkazo.

Hapa imesemwa: ‘Akasema kuwaambia wakuu waliomzunguka: Hakika huyu ni mchawi mjuzi,’ na kule imesemwa: ‘Wakasema wakuu wa watu wa Firauni: Hakika huyu ni mchawi mjuzi.’ Tofauti hapa ni kubwa kama inavyojionyesha.

Kwa sababu hapa aliyesema ni Firauni kuwaambia wakuu na kule wakuu ndio waliosema kumwambia Firauni. Sasa je, kuna wajihi gani wa kuunganisha baina ya Aya mbili hizi?

Jibu : Sikupata ishara yoyote ya hilo katika tafsiri nilizonazo, wala sijui sababu yake. Kwa vyovyote iwavyo, jibu ninaloliona ni kuwa Firauni ndiye aliyeanza kuwaambia jamaa zake kuwa huyu ni mchawi; kisha jamaa zake nao wakaanza kuambiana kuwa ni kweli Musa ni mchawi; kama ilivyo kwa wanaoongozwa, wanaigiza kiongozi wao na kutolea ushahidi kauli zake.

Hapo basi hakuna kupingana baina ya Aya mbili. Firauni aliwaambia jamaa zake nao wakamwambia yeye kwa kumwigiza.

9

10