TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TANO Juzuu 5

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TANO0%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TANO Mwandishi:
: HASANI MWALUPA
Kundi: tafsiri ya Qurani

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TANO

Mwandishi: Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya
: HASANI MWALUPA
Kundi:

Matembeleo: 17059
Pakua: 2272


Maelezo zaidi:

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 14 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 17059 / Pakua: 2272
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TANO

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TANO Juzuu 5

Mwandishi:
Swahili

9

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA TANO

﴿لَّا خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَاهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلَاحٍ بَيْنَ النَّاسِ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴾

114.Hakuna kheri katika siri zao nyingi, ila mwenye kuamrisha sadaka au wema au kusuluhisha watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutampa ujira mkubwa.

﴿وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴾

115.Na mwenye kumpinga Mtume baada ya kumdhihirikia yeye uongofu, na akafuata njia isiyokuwa ya wenye kuamini, tutamwelekeza alikoelekea na tumtie katika Jahannam na ndio marejeo maovu.

SIRI YA KHERI NA YA USULUHISHI

Aya 114 - 115

MAANA

Hakuna kheri katika siri zao nyingi, ila mwenye kuamrisha sadaka au wema au kusuluhisha watu.

Baada ya Mwenyezi Mungu kutaja katika Aya zilizotangulia wale wanaokula njama usiku ya kauli asizoziridhia na kuwatetea wahaini, sasa katika Aya hii anasema siri zao nyingi hazina kheri. Kwa hiyo dhamiri ya 'siri' zao' inawarudia hao waliotajwa katika Aya zilizotangulia, kwa dalili ya dhahiri ya mfumo, lakini katika maana inaenea kwa watu wote. Kwa vile sababu inayowajibisha ni ya ujumla, haihusiki na watu maalum wala kundi maalum.

Sadaka ni kutoa mali kwa masikini wahitaji. Kuwasuluhisha watu kunawaokoa na taabu nyingi na kuwaondolea matatizo. Na wema ni kila linalokubaliwa na akili na sharia kwa kuliona kuwa ni zuri. Ikiwemo elimu na mambo yote mazuri kama vile sadaka na kuimarisha udugu. Mwenyezi Mungu amehusisha kuyataja hayo mawili kwa kufahamisha umuhimu wake.

Arrazi anaema: "Mkusanyiko wa kheri zote umetajwa katika Aya hii." Na mkusanyiko zaidi umetajwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu:

﴿إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ ﴿٢﴾ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ﴾

"Hakika mwanadamu yumo katika hasara, Ila wale ambao wameamini wakatenda matendo mema, wakausiana haki, wakausiana kusubiri." (103: 2-3)

Unaweza kuuliza : Watu huwa wakifanya siri za biashara, kazi, kilimo, na nyinginezo katika mambo ya maisha, sasa je siri hii ni katika mambo yasiyokuwa na kheri?

Jibu : Siri hiyo ni kheri maadam iko katika mipaka ya sharia, na katika yale ambayo ni wajibu kisharia, kikawaida na kiakili. Nayo ni yale ambayo maisha hayatimii bila hayo. Na Aya imeepuka aina hii ya siri na kuingilia wale wanofanya siri na kuwazungumzia watu; kama kawaida ya wasio na haki; hupoteza muda wao kwa porojo na kujishughulisha na yule ni zaidi na yule ni mchache. Tamko la nyingi katika Aya linafahamisha kuwa siri nyingi za watu hazina heri ila kama itawarudia faida na manufaa kwa namna fulani. Ama siri katika mambo ya maisha, Aya haikuelezea kwa uzuri au ubaya.

Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutampa ujira mkubwa.

Kuamrisha mema ni vizuri, hilo halina shaka. Lakini mwenye kulifanya kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu sio kwa kuchuma, na kutaka jaha ni bora kuliko ambaye anaamrisha mema na kuyaletea falsafa kubainisha mazuri yake na faida zake, lakini hayafanyi, bali itakuwa ni hoja yenye nguvu na ya fasaha zaidi kwake. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:"Hakika sisi hatupotezi ujira wa anayefanya vitendo vizuri." (18: 30)

Wala hakusema mwenye kauli nzuri. Kuamrisha mema kuyatolea mwito ni nyenzo na kuyafanya ndio lengo. Mwenye kuamrisha na yeye mwenyewe akafanya, atakuwa katika waliomsaidia Mwenyezi Mungu kwa kauli yake:

﴿ وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِّمَّن دَعَا إِلَى اللَّـهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ ﴾

"Ni nani asemaye kauli bora zaidi kuliko alinganiaye kwa Mwenyezi Mungu na akafanya vitendo vizuri" (41: 33)

Kwa hiyo kauli bora ni nzuri, na inazidi uzuri kama itaambatanishwa na vitendo.

Zaidi ya haya ni kwamba kauli hata kama kwa dhahiri itaambatana na athari za kiislamu; kama vile ndoa na mirathi, haziwezi kufahamisha imani sahihi, ila vitendo vizuri. Amesema Imam Ali Amirulmuminin(a.s) :"Imani inafahamisha mambo mema na mambo mema yanafahamishwa na imani."

Na mwenye kumpinga Mtume baada ya kumdhihirikia yeye uongofu, na akafuata njia isiyokuwa ya wenye kuamini, tutamwelekeza alikoelekea na tumtie katika Jahannam na ndio marejeo maovu.

Upinzani ni uadui na kila mwenye kumwasi Mwenyezi Mungu ni adui wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Amirul-muminin(a.s) anasema: "Hakika mpenzi wa Muhammad ni mwenye kumtii Mwenyezi Mungu hata akiwa mbali naye (huyo Mtume) kwa nasabu, na hakika adui wa Muhammad ni yule mwenye kumwasi Mola hata kama akiwa karibu naye (mtume) kwa nasabu."

Adui wa Muhammad hapa ni kila ambaye imemdhihirikia haki, akaikana, akasimamishiwa hoja za kutosha, lakini pamoja na hayo akakanusha kwa inadi na kung’ang’ania mapenzi ya nafsi yake; kama anayejua kuwa uislamu ni haki au kuwa ni uongofu zaidi kuliko dini y a watu wake, lakini pamoja na hayo akang'a ng'ania dini ya mababu zake kwa kupupia masilahi yake ya kiutu au jaha.

Wafasiri wametaja kuwa Aya hii ilishuka kuhusu Bashir bin Ubairiq ambaye alisilimu kisha akartadi na kuungana na washirikina. Inajulikana kuwa ni desturi ya wafasiri kujipachikia sababu za kushuka Aya. Wanataja tukio lolote linaloambatana na zama za kushuka Aya ikiwa linanasibiana nayo. Na Aya hii inafungamana na kurtadi kwa Bashir na kila mwenye kupinga baada ya kumbainikia uongofu.

Maana ya Tutamwelekeza alikoelekea ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) humtegemezea kila mtu kwenye lile alilolitegemea. Mwenye kujitukuza kwa mali, cheo, siha au ukoo, basi Mwenyezi Mungu huachana naye na kumwachia lile alilojitukuzia. Katika Hadiith Qudsi Mwenyezi Mungu anasema:"Naapa kwa utukufu wangu na enzi nitakatilia mbali matumaini ya kila anayemtumainia mtu."

Aya hii inatujulisha yafuatayo:

i). Kauli yake Mwenyezi Mungu Tutamwelekeza alikoelekea ni wazi kuwa binadamu ana hiyari, si mwenye kuendeshwa.

ii).Kauli yake Mwenyezi Mungu Baada ya kumbainikia uongofu ni dalili kwamba mwenye kufanya utafiti wa ndani na usimbainikie uongofu basi huyo anasameheka; sawa na ambaye hakufikiliwa na mwito wowote, lakini kwa sharti ya kuwa awe ni mwenye kuelekea kuitafuta haki na kuitumia pale itakapomdhihirikia.

iii). Mtu ni mwenye kukalifiwa na yale anayoyafahamu kutokana na dalili, na wala hana jukumu la hali halisi ilivyo. Kinachotakiwa kwake ni kufanya utafiti tu, mpaka akate tamaa ya kupata dalili. Akipatia hali halisi baada ya utafiti huu, basi atakuwa na malipo mara mbili, na akikosea atakuwa na malipo mara moja; kama ilivyoelezwa katika Hadith.

iv).Yaliyoelezwa katika Tafsiri Razi kwamba Shafii aliulizwa kuhusu Aya ya Qur'an inayofahamisha kuwa Ijmai ni hoja? Akasoma Qur'an mara mia tatu mpaka akapata Aya isemayo: "Na akafuata njia isiyokuwa ya waumini." Ambapo imefahamisha kuwa kufuata njia isiyokuwa ya waumini ni haramu, kwa hiyo basi kufuata njia ya waumini ni wajibu; na njia yao ni Ijmai yao juu ya jambo.

Hakuna linalofahamishwa na maelezo haya zaidi ya kuwa hakuna chimbuko la Ijmai katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kwa vile makusudio ya njia isiyokuwa ya waumini ni njia ya washirikina na wanafiki ambao wanampinga Mwenyezi Mungu na Mtume baada ya kuwabainikia wao uongofu. Kuongezea aliyoyasema Sheikh Muhammad Abduh: "Ijma wanayokusudia ni kuafikiana mujtahiid wa umma huu baada ya kufa Mtume wake na Aya imeshuka zama za Mtume sio baada ya zama zake."

NZI KUFIA KIDONDANI

Ametaja mwenye Tafsir Al-manar kisa cha anyeathiriwa na hawaa ya nafsi kuliko uongofu. Tutakinukuu kwa faida ya msomaji, anasema: "Mtu mwenye hawa ya nafsi anashawishika na manufaa ya kidunia kwa udhaifu wa nafsi yake.

Kuna kisa kuwa Hajjaj aliandaa karamu ile ya 'nyote mwaalikwa' Wakawa wanakula huku akiwaangalia, akamwona bedui mmoja anakula kwa umero sana. Lakini mara ilipokuja haluwa aliacha chakula na akairukia. Hajjaj akaamrisha muuaji wake atangaze kuwa atakayekula haluwa atakatwa shingo yake. Ikawa bedui mara anamwangalia muuaji akipima uchungu wa mauti na ladha ya haluwa. Mara akamwelekea Hajjaj na kumwambia: "Nakuusia uwafanyie vizuri watoto wangu." (akiwa na maana kuwa atauliwa kwa kula haluwa) Akaishambulia haluwa kwa pupa sana kama mtu anayekula mlo wa mwisho maishani! Hajjaj akamwachilia mbali"

﴿إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴾

116.Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kufanyiwa mshirika, lakini humsamehi yasiyokuwa hayo kwa amtakaye.Na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, basi hakika amepotea upotofu ulio mbali.

﴿إِن يَدْعُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا إِنَاثًا وَإِن يَدْعُونَ إِلَّا شَيْطَانًا مَّرِيدًا﴾

117.Hamwabudu asiyekuwa yeye ila (Masanamu) ya kike na hawamwabudu ila Shetani Muasi.

﴿لَّعَنَهُ اللَّـهُ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنْ عِبَادِكَ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا﴾

118.Mwenyezi Mungu amlaani shetani, Naye alisema kwa hakika nitajifanyia katika waja wako fungu maalum.

﴿وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الْأَنْعَامِ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّـهِ وَمَن يَتَّخِذِ الشَّيْطَانَ وَلِيًّا مِّن دُونِ اللَّـهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا ﴾

119.Kwa hakita nitawapoteza na nitawatia tamaa. Na nitawaamrisha, watayakata masikio ya wanyama na nitawaamrisha wabadili umbile la Mwenyezi Mungu, Na mwenye kumfanya shetani kuwa mlinzi badala ya Mwenyezi Mungu basi amehasirika hasara ya waziwazi.

﴿يَعِدُهُمْ وَيُمَنِّيهِمْ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلَّا غُرُورًا ﴾

120.Anawaahidi na kuwatia tamaa; na shetani hawaahidi ila udanganyifu.

﴿أُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَلَا يَجِدُونَ عَنْهَا مَحِيصًا ﴾

121.Hao makazi yao ni moto wa Jahannam wala hawatapata pa kuukimbia.

﴿وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا وَعْدَ اللَّـهِ حَقًّا وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ قِيلًا ﴾

122.Na wale ambao wameamini na wakafanya matendo mema, tutawatia katika pepo zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele, ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu, na ni nani msema kweli zaidi ya Mwenyezi Mungu?

MWENYEZI MUNGU HASAMEHE KUFANYIWA MSHIRIKA

Aya 116 - 122

MAANA

Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kufanyiwa mshirika, lakini humsamehe yasiyokuwa hayo amtakaye,

Imetangulia Aya hii na maelezo yake katika kufasiri Aya 48 katika Sura hii. Hakuna tofauti yoyote kati ya nukuu mbili ila katika kumalizia ambapo huko imesemwa: "Na mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu hakika amezusha dhambi kubwa," na hapa ikasemwa: "Na mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu hakika amepotea upotevu wa mbali," maana ni moja tu.

TENA KUKARIRIKA KATIKA QUR'AN

Tumezungumzia kukaririka Qur'an katika kufasiri Aya 2; 48; sasa tunaunganisha na aliyoyasema mwenye Tafsiri Al-manar katika kufasiri Aya hii; "Qur'an sio kanuni wala si kitabu cha fani kinachotaja suala mara moja, bali ni Kitabu cha mwongozo.

Inakusudiwa uongozi kwa kuyaleta maana yanayotakiwa katika nafsi katika kila mfumo wa maneno unaoukubali maana ya makusudio.

Na hilo litatimia kwa kukaririka makusudio ya kimsingi; wala mwito wa kiujumla hauwi ila kwa kukaririka. Kwa hiyo ndio tunaona watu wa madhehebu za dini na wa siasa ambao wanajua desturi ya kijamii, tabia za watu na hulka zao, wanarudia khutba zao, malengo yao na makala zao wanazozisambaza katika magazeti yao na vitabu vyao."

Hawamwabudu asiyekuwa yeye ila( masanamu ) ya kike.

Waarabu kabla ya Muhammad(s.a.w.w) walikuwa wakidai kwamba Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu anasema:

﴿ أَفَأَصْفَاكُمْ رَبُّكُم بِالْبَنِينَ وَاتَّخَذَ مِنَ الْمَلَائِكَةِ إِنَاثًا ﴾

"Je, Mola wenu amewachagulia watoto wa kiume, na mwenyewe akajifanyia watoto wa kike katika Malaika?." (17:40)

Itikadi yao hii iliwapelekea kufanya masanamu waliyowapa majina ya wanawake; kama vile Lata, Uzza na Manata. Wakiwatia alama za Malaika waliodai kuwa ni mabinti wa Mwenyezi Mungu. Mwanzo walikuwa wakijikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa hayo masanamu.

Baada ya kupita vizazi masanamu hayo yakageuka kuwa Mungu anayeumba na kuruzuku. Na hivi ndivyo kulivyogeuka kuzuru makaburu - kwa waarabu na watu wote - kutoka kuwa ni kutukuza alama za Mwenyezi Mungu na kutukuza misingi ambayo amekufia aliyemo kaburuni, na kuwa ni itikadi ya kuwa ni nguvu ya juu inayoleta manufaa na kukinga madhara.

Na hawamwabudu ila muasi.

Yaani ibada ya washirikina kwa masanamu ilivyo hasa ni ibada ya shetani, kwa sababu yeye ndiye aliyewaamrisha hivyo, wakamtii. Yeyote mwenye kumtii mwingine na kufuata njia yake basi yeye ni mtumwa wake mwenye kuamrishwa naye.

Mwenyezi Mungu amlaani, Naye alisema kwa hakika nitajifanyia katika waja wako fungu maalum.

Maana ni kuwa shetani alimwambia Mwenyezi Mungu Mtukufu; Mimi nina fungu katika waja wako uliowaumba, na ukawaambia katika uliyowaambia:

"Na sikuumba majini na watu ila waniabudu" (51: 56)

Na kwamba fungu hili ni faradhi ya wajibu kwangu wanitii na kukuasi.

Unaweza kuuliza : Dhahiri ya Aya yaonyesha kwamba shetani ni kiumbe hasa na kwamba yeye anamwambia Mwenyezi Mungu kwa nguvu na kujiamini, Je maneno yako kwenye dhahiri yake au kuna taawili?

Jibu : Mwenye tafsir Al-manar kutokana na ustadh wake Sheikh Muhammad Abduh anasema kwamba kila mtu ana maandalizi ya kufanya kheri na shari na kufuata haki na batili. Maandalizi hayo Mwenyezi Mungu ameyaashiria katika kauli yake:"Na tukamwongoza njia mbili." (90:10)

Na kwamba fungu la wajibu la shetani kutoka kwa bindamu ni kujiandaa kwake na shari ambayo ni moja ya njia mbili. Kwa hiyo tamko la shetani ni fumbo la uandalizi huu. Tumezungumza kuhusu makusudio ya neno shetani katika juzuu ya kwanza maelezo ya Audhubillahi sio mbali kuwa kauli hii iliyokuja kwa lugha ya shetani, Nitashika fungu la lazima, kuwa ni picha ya matuk io ya waasi ambao maandalizi ya shari kwao yameshinda ya heri, na wala sio mazungumzo ya uhakika pamoja na Mwenyezi Mungu (s.w.t)

SIASA YA SHETANI NA SAYANSI

Mmoja aliwahi kusema kuwa fikra ya shetani ilitawala akili za watu pale elimu ilipokuwa ni mazungumzo tu yanayozungumzwa kwenye vikao vya kufundishana na misitari tu inayojaza kurasa za vitabu; wala haifikilii kwenye vitendo.

Ama leo fikra ya shetani imekuwa ni uzushi na ngano kwa tafsiri zake zote, baada ya kuwa elimu ni kipimo cha kila hakika, msingi wa kila hatua anayopiga binadamu, nguvu katika nyanja zote na uwezo unaokifanya chuma kipige marefu ya masafa ya mita katika ardhi, kuchimbua miamba ya dhahabu na kuruka angani mpaka mwezini na kwenye Merikh (mars) huku kikizungumza na watu wa ardhini wanoshuhudia safari yake.

Jibu : Hatudhani kuwa kuna yeyote anayeipuza elimu na faida zake na kwamba hiyo ni nguvu na ni utajiri vilevile na kuwa jinsi watu wanavyoihitajia ni sawa na vile mtu anavyohitajia maji na chakula. Lakini hakuna yeyote asiyejua kwamba elimu ni sawa na binadamu; ina maandalizi ya heri na shari na mara nyingine inaelekeza kwenye heri, ikazalisha chakula kwa walio na njaa, kuwavisha walio uchi na kuwatibu walio wagonjwa. Na mara nyingine inaelekeza kwenye shari; ikaua na kuvunja.

Shari ndiyo nguzo ya kwanza ya siasa ya shetani tunayemkusudia na leo elimu katika siasa, imekuwa inaelekeza kubomoa na kutawala na kunyonya. Fungu la shari au shetani - vyovyote utakavyoita - limezidi kwa maendeleo ya elimu (Sayansi).

Zamani wasaidizi wa shari walikuwa na silaha ya nguvu na viungo, ama hivi leo baada ya elimu kuwafikia wakorofi, basi wanachama wa shetani wanatumia silaha za tonoradi, na mabomu na mengineyo yanayotetemesha ardhi kutokea chini.

Kuna mahali nimesoma kwamba Amerika imeweka mpango wa kuwanunua machipukizi wa elimu popote ulimwenguni na kwamba dalali wake anayetembea aliwahi kufika Uingereza katika baadhi ya ziara zake na kukubaliana na wataalamu mia saba wahamie Amerika. Mbinu hizi wanazitumia wanasiasa wa Amerika kutengeneza vifaa vya kupiga ulimwengu wote na kutawala nguvu zake. Hawa ndio shetani adui wa Mwenyezi Mungu na wa binadamu.

Ama mashule ya kisasa yaliyoenea kila mahali, mengi ni katika fungu la shetani hamna chochote chenye mwelekeo wa dini na maadili mema. Hivi ndivyo zilivyoitikia akili kubwa na ndogo mwito wa shetani alioutangaza kwa kusema: Kwa hakika nitashika fungu la lazima katika waja waiko. Kwa hakika nitawapoteza na nitawatia tamaa.

Shetani kumpoteza mtu ni kumpambia haki aione batili na kheri aione shari, au ampe dhana za kuwa hakuna haki wala heri katika kuwapo kwake wala hakuna pepo na moto na kwamba dunia ni ya mwenye kuimiliki, kama alivyosema Nietezshe [14] . Kuna hadith isemayo: Ibilis ameumbwa na umbo la kupendeza.

Ama kutia tamaa kwa shetani ni kumpa mawazo ya kupata anayoyatamani kutokana na muda mrefu na kuokoka siku ya hisabu na malipo na mengineyo katika matamanio ya uongo na ndoto za uokofu.

Na nitawaamrisha, watayakata masikio ya wanyama na nitawaamrisha wabadili umbile la Mwenyezi Mungu.

Makusudio ya wanyama ni ngamia, ng'ombe na kondoo. waarabu wakati wa Ujahiliya walikuwa wakiyakata masikio ya baadhi ya wanyama wao na kuyasimamisha kwenye masanamu halafu wanajiharamisha nao. Utakuja ufafanuzi wakati wa kufasiri (5: 103) Inshallah.

Baada ya kuwa shari au shetani akiwaamrisha wanachama wake wakati wa ujahiliya kukata masikio ya wanyama na kubadilisha umbile la Mwenyezi Mungu, hivi sasa amekuwa akiwaamrisha kutupa mabomu ya sumu (Napalm) kwa wanawake na watoto na kutupa mabomu ya Atomic huko Hiroshima na Nagasaki kwa ajili ya kumaliza viumbe vya Mwenyezi Mungu. Haya ni matokeo ya wanasiasa kutawala akili na elimu.

Na mwenye kumfanya shetani kuwa mlinzi badala ya Mwenyezi Mungu - yaani akimtii -basi amehasirika hasara ya waziwazi , Ambapo anakuwa ni mateka wa matamanio na hawaa za nafsi na vilevile mateka wa njozi na uzushi.

Anawaahidi na kuwatia tamaa; na shetani hawaahidi ila udanganyifu. Ambapo amewawekea kwenye njia ya maangamivu baada ya kuwadanganya kuwa ni uokofu. Kwa mfano, mzinifu au mnywaji pombe anaweza kuwa yeye anastarehe kwa ladha na kumbe ilivyo hasa anajitwisha madhara makubwa ya kidunia na akhera.

Hao makazi yao ni moto wa Jahannam wala hawatapata pa kuukimbia. Yaani wanachama wa shetani katika washirikina na wafisadi hawataokoka na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Baada ya Mwenyezi Mungu kutaja kiaga kikali, alifuatisha na ahadi kama ilivyo desturi yake ilivyozoelekea - kukutanisha himizo na kitisho. Anasema Mwenyezi Mungu:

Na wale ambao wameamini na wakafanya matendo mema, tutawatia katika pepo zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele. Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu; na ni nani msema kweli zaidi ya Mwenyezi Mungu?

Katika Aya hii kuna masisitizo matatu: Umiliki, ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kweli na ni nani mkweli zaidi. Lengo la kukaririka huku ni kufahamisha kuwa ahadi ya shetani ni ya uongo, tamaa inayokwisha na amri zake ni batili; na kwamba kauli ya Mwenyezi Mungu ndiyo ya haki na ukweli na twaa yake ni heri na wema.

Unaweza kuuliza kuwa : ahadi ya pepo mara nyingi katika Aya hukutanishwa na kudumu milele (Abadan) ambapo Aya nyingi za kiaga cha moto hukutanishwa na kudumu tu, je, kuna siri gani?

Jibu : Kudumu ni kukaa muda mrefu, inawezekana kuwa milele na inawezekana isiwe, mwenye kuingia peponi hatoki kwa hiyo inanasibu kusema milele.

Ama mwenye kuingia motoni anaweza kukatikiwa na adhabu na kuto- ka humo kwa hiyo ndio haikukutanishwa adhabu na umilele ila katika hali maalum; kama vile ushirikina na kuua makusudi.

﴿ لَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَا أَمَانِيِّ أَهْلِ الْكِتَابِ مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ وَلَا يَجِدْ لَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴾

123.Si matamanio yenu wala matamanio ya watu wa Kitabu. Mwenye kutenda uovu atalipwa kwa ovu huo, Wala hatajipatia mlinzi wala msaidizi zaidi ya Mwenyezi Mungu.

﴿ لَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَا أَمَانِيِّ أَهْلِ الْكِتَابِ مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ وَلَا يَجِدْ لَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴾

124. Mwenye kufanya mema - mwanamume au mwanamke - hali ya kuwa ni mwenye kuamini, basi hao wataingia peponi wala hawatadhulumiwa hata kitobwe cha kokwa ya tende.

Unaweza kuuliza kuwa : ahadi ya pepo mara nyingi katika Aya hukutanishwa na kudumu milele (Abadan) ambapo Aya nyingi za kiaga cha moto hukutanishwa na kudumu tu, je, kuna siri gani?

Jibu : Kudumu ni kukaa muda mrefu, inawezekana kuwa milele na inawezekana isiwe, mwenye kuingia peponi hatoki kwa hiyo inanasibu kusema milele. Ama mwenye kuingia motoni anaweza kukatikiwa na adhabu na kutoka humo kwa hiyo ndio haikukutanishwa adhabu na umilele ila katika hali maalum; kama vile ushirikina na kuua makusudi.

ANAYEFANYA UOVU ATALIPWA

Aya 123 - 124

MAANA

Aya mbili hizi zinaelezea msingi wa dhahiri ambao hakuna anayeweza kuutolea mjadala na kuuondoa au kuubadilisha mfumo wake kutokana na mabadiliko ya wakati au hali; wala pia hauhusiki na mwanamume peke yake au mwanamke tu. Msingi wenyewe ni "Mtu atalipwa amali zake ikiwa ni heri basi ni heri na ikiwa ni shari basi ni shari". Maana haya yamekaririka katika kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa mifumo mbali mbali; kama vile katika Aya mbili hizi tulizo nazo.

Nyingine ni:"Ili Mwenyezi Mungu ailipe kila nafsi yale iliyoyachuma" (14: 51)

"Ili awalipe wale waliofanya ubaya kwa yale waliyo yafanya" (53:31)

Si matamanio yenu wala matamanio ya watu wa Kitabu.

Wakanushaji waliwaambia wale wanaowalingania kwenye imani kuwa ni sawa tu muwe mmetupa mawaidha au la, haya ni mambo ya zamani tu sisi hatutaadhibiwa. Mayahudi walisema hataingia ila aliye yahudi au naswara. mmoja katika waislamu alisema kuwa moto umeumbiwa wasiokuwa waislamu. Hivi ndivyo walivyo watu wote kufarahia dini waliyo nayo. Ndipo Mwenyezi Mungu akawajibu kwa kusema kwake:

Mwenye kutenda uovu atalipwa kwa uovu huo.

Vyovyote itakavyokuwa Mwenyezi Mungu hana nasaba wala sababu na yeyote, isipokuwa ikhlas na amali njema. Dalili tosha ya hilo ni kauli yake Mwenyezi Mungu:"Hakika mtukufu wenu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchae Mungu zaidi katika nyinyi" (49:13)

Imam Jafar as-Sadiq(a.s) amesema:"Hatukuwa sisi ila ni watumwa wa ambaye ametuumba na kutuchagua, Wallahi sisi hatuna hoja yoyote kwa Mwenyezi Mungu wala hatuwezi kumwepuka. Sisi tutakufa na tutasimama (mbele ya Mwenyezi Mungu) na tutaulizwa. Mwenye kuwapenda Ghulat ametuchukiza na mwenye kuwachukia ametupenda. Ghulat ni makafiri na mufawadhaa ni washirikina "[15]

MWANAMUME NA MWANAMKE

Mwenye kufanya mema - mwanamume au mwanamke - hali ya kuwa ni mwenye kuamini, basi hao wataingia peponi wala hawatadhulumiwa hata kitobwe cha kokwa ya tende.

Maadamu mke na mume wako sawa katika taklifa na kuchukua majukumu, basi inalazimika kuwa sawa katika malipo. Kama kuna tofauti kwa namna fulani, basi tofauti hiyo haisihi kwa hali yoyote katika malipo mema na mabaya.

Yametangulia maelezo katika kufasiri (2: 228) kifungu 'Mwanamume na Mwanamke katika sharia ya kiislamu Kauli yake Mwenyezi Mungu: "Hali ya kuwa ni mwenye kuamini." Ni sharti la kuingia peponi; kama ilivyofafanuliwa katika Aya:"Basi hao wataingia peponi," Lakini sio sharti la malipo mengine ya amali njema.

Kafiri akifanya amali njema kwa njia ya kheri kwa fahari au biashara, Mwenyezi Mungu atamlipa kwa sababu Mwenyezi Mungu ni mwadilifu hapotezi malipo ya mwenye kufanya amali njema. Kwa nini isiwe hivyo, na yeye ndiye aliyesema:"Hakuna malipo ya hisani ila hisan." (55: 60)

Si lazima malipo ya hisani kuwa ni pepo, inaweza kuwa malipo duniani au Akhera kwa kupunguziwa adhabu au kwa kutokuwa motoni wala peponi. Tumeyafafanua hayo katika kufasiri 3: 176 kifungu 'Kafiri na amali njema,' Pia katika kufasiri 4: 34.rejea