TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA SITA Juzuu 6

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA SITA0%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA SITA Mwandishi:
: HASANI MWALUPA
Kundi: tafsiri ya Qurani

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA SITA

Mwandishi: Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya
: HASANI MWALUPA
Kundi:

Matembeleo: 16172
Pakua: 2327


Maelezo zaidi:

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 11 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 16172 / Pakua: 2327
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA SITA

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA SITA Juzuu 6

Mwandishi:
Swahili

2

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA SITA

﴿إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ قَدْ ضَلُّوا ضَلَالًا بَعِيدًا ﴾

167.Hakika wale waliokufuru na kuzuilia (watu) na njia ya Mwenyezi Mungu, wamekwishapotea upotevu ulio mbali.

﴿إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَظَلَمُوا لَمْ يَكُنِ اللَّـهُ لِيَغْفِرَ لَهُمْ وَلَا لِيَهْدِيَهُمْ طَرِيقًا﴾

168.Hakika wale waliokufuru na kudhulumu, haitakuwa kwa Mwenyezi Mungu kuwasamehe wala kuwaongoza njia.

﴿إِلَّا طَرِيقَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴾

169.Isipokuwa njia ya Jahannam, humo watadumu milele. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.

﴿يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُمُ الرَّسُولُ بِالْحَقِّ مِن رَّبِّكُمْ فَآمِنُوا خَيْرًا لَّكُمْ وَإِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴾

170.Enyi watu! Amekwishawafikia Mtume kwa haki kutoka kwa Mola wenu, basi aminini (itakuwa) kheri kwenu. Na kama mtakataa, basi hakika ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo mbinguni na ardhini, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi mwenye hekima.

WALIKUFURU NA KUZUILIA

Aya 167 – 170

MAANA

Hakika wale waliokufuru na kuzuilia (watu) na njia ya Mwenyezi Mungu wamekwishapotea upotofu ulio mbali.

Anasema Razi na wengineo katika wafasiri, kuwa sifa hizi ni za Mayahudi, kwa sababu wao waliukufuru Uislamu na kuwazuia wengine kwa kuingiza shaka kwenye nyoyo za wenye akili.

Hakika wale waliokufuru na wakadhulumu haitakuwa kwa Mwenyezi Mungu kuwasamehe wala kuwaongoza njia, isipokuwa njia ya Jahannam, humo watadumu milele.

Baadhi ya wafasiri wanaona kuwa Aya ya kwanza inahusika na Mayahudi, na hii inahusika na washirikina; na kwamba Mayahudi walizuilia watu na uislamu kwa kuingizia shaka, na washirikina wakazuia kwa dhulma, ambapo walimtangazia vita Muhammad(s.a.w.w) na wakapigana naye mara nyingi.

Mwenyezi Mungu hatawasamehe wao wala wengine maadamu wako kwenye upotevu, wala hatawaongoza huko akhera isipokuwa kwenye njia ya Jahannam. Kwa sababu hapa duniani walifuata njia ya upotevu, wakaiacha njia ya uongofu ingawaje walionywa.

Kauli yake Mwenyezi Mungu'milele' ni dalili ya kubakia kwao motoni na kutokatikiwa na adhabu. Lau si tamko hilo (Milele) basi ingekuwa kuna uwezekano ama wa kudumu milele au kukaa sana katika Jahannaam.

Enyi watu! Amekwishawafikia Mtume kwa haki kutoka kwa Mola wenu. Basi aminini (itakuwa) kheri kwenu.

Makusudio ya Mtume ni Muhammad(s.a.w.w) . Na mwito unawaenea watu wote, wakati wote na mahali popote. Kwa sababu kumwamini Muhammad(s.a.w.w) na mwito wake ni haki; na wajibu wa imani ya haki hauhusiki na mtu fulani wala wakati fulani.

Kauli yake Mwenyezi Mungu:kwa haki kutoka kwa Mola wenu, inajulisha kuwa; Uislamu haukubali utawala wowote isipokuwa utawala wa haki. Mwenye kutii, atakuwa mwenye kukurubishwa kwa Mwenyezi Mungu na mwenye kuasibasi hakika ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo mbinguni na ardhini; na Mwenyezi Mungu ni mjuzi mwenye hekima.

﴿يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ وَلَا تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ إِنَّمَا الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ رَسُولُ اللَّـهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَىٰ مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِّنْهُ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَلَا تَقُولُوا ثَلَاثَةٌ انتَهُوا خَيْرًا لَّكُمْ إِنَّمَا اللَّـهُ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ سُبْحَانَهُ أَن يَكُونَ لَهُ وَلَدٌ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴾

171.Enyi watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila yaliyo haki. Masih Isa bin Maryam ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na neno lake tu alilompelekea Maryam, na ni roho iliyotoka kwake. Basi mwaminini Mwenyezi Mungu na mitume wake; wala msiseme watatu. Komeni!, itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ameepukana kuwa na mtoto. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini; na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa mlinzi.

﴿لَّن يَسْتَنكِفَ الْمَسِيحُ أَن يَكُونَ عَبْدًا لِّلَّـهِ وَلَا الْمَلَائِكَةُ الْمُقَرَّبُونَ وَمَن يَسْتَنكِفْ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيَسْتَكْبِرْ فَسَيَحْشُرُهُمْ إِلَيْهِ جَمِيعًا﴾

172.Masih hataona unyonge kuwa mtumwa wa Mwenyezi Mungu wala Malaika wenye kukurubishwa. Na watakaoona unyonge utumwa wa Mwenyezi Mungu na kutakabari, basi atawakusanya wote kwake.

﴿فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُوَفِّيهِمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدُهُم مِّن فَضْلِهِ وَأَمَّا الَّذِينَ اسْتَنكَفُوا وَاسْتَكْبَرُوا فَيُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَلَا يَجِدُونَ لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا﴾

173.Ama wale ambao wameamini na wakatenda mema, atawalipa ujira wao sawa, na atawazidishia kwa fadhila yake. Na ama wale walioona utumwa na wakafanya kiburi, basi atawaadhibu adhabu iliyo chungu. Wala hawatopata mlinzi wala wa kuwasaidia.

MSIPETUKE MIPAKA KATIKA DINI YENU

Aya 171-173

MAANA

Enyi watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila yaliyo haki. Masih Isa bin Maryam ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na neno lake tu alilompelekea Maryam, na ni roho iliyotoka kwake. Basi mwaminini Mwenyezi Mungu na mitume wake; wala msiseme watatu. Komeni!, itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ameepukana kuwa na mtoto. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini; na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa mlinzi.

Haufichiki kwake utiifu wa mwenye kutii wala uasi wa mwenye kuasi, Na hekima yake imepitisha kumlipa kila mmoja anavyostahiki katika thawabu au adhabu.

Hatujui dini iliyosisitiza na kutilia mkazo katika itikadi ya Tawhid (Umoja wa Mungu), kama Uislamuu. Mwenyezi Mungu hana mfano wala kinyume chake, hana maingiliano wala mfungamano."Hakuna chochote kama mfano wake" (42:11) Huu ndio msingi unaosimamia itikadi ya kiislamu.

Ajabu ni ya yule asemaye. "Ikiwa Mwenyezi Mungu ana uwezo wa kuumba kila kitu, basi inatakikana kuweza kuumba Mwenyezi Mungu mfano wake." La ajabu katika kauli hii ni kuchanganya sifa za Muumbaji na aliyeumbwa, na mwenye kuabudu na mwenye kuabudiwa, katika dhati moja. Ni wazi kuwa mwenye kuumba hawezi kuwa mwenye kuumbwa isipokuwa kwa yule asemaye kuwa Masih ana hali mbili: Ya kimungu na ya kibinadamu.

Tumezungumzia yaliyosemwa kuhusu Bwana Masih katika kufasiri Sura (3:58), na kuhusu Tawhid na kukanusha ushirikina na utatu katika kufasiri (4:50), Vile vile tumezungumzia kupetuka mipaka katika kufasiri Sura (3:128). Na sasa tunarudia tena maudhui haya kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Enyi watu wa Kitabu, 'Msipite kiasi katika dini yenu, wala msiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila yaliyo haki.

Wote Mayahudi na Wakristo walisema kauli ya kupita kiasi. Mayahudi walimteremsha chini kabisa; na Wakristo wakampandisha juu mpaka kufikia uungu. Ama Waislamu wamesema yaliyosemwa na Qur'an; na hiyo ni kauli ya katikati baina ya kauli zote mbili.

Katika Aya iliyotangulia msemo ulielekezwa kwa Mayahudi na katika Aya hii unaelekezwa kwa Wakristo kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala msiseme watatu." Huku ndiko kupita kiasi katika dini na kauli ya batili. Kwa sababu Mwenyezi Mungu ametakata na ushirika na maingiliano yoyote au mafungumano na kuwa na mwenzi.

QUR'AN NA WANAOHUBIRI UTATU

Masih Isa bin Maryam ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na neno lake tu alilompelekea Maryam.

Hii ndiyo hakika ya Isa, na ndiyo waliyoizungumzia Waislamu. Ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi imetosha, kama Ibrahim, Musa na Mitume wengineo.

Tulikuwa pamoja na wahubiri wa kikristo katika sehemu zilizotangulia za tafsiri hii na sasa tuko nao katika tafsiri ya Aya hii; Kwa sababu wana kisa chao utakachokijua baadaye.

Kwanza tunaanza na swali, kama desturi yetu, katika kutaka kufafanua, ili msomaji aendelee mpaka mwisho bila ya kuhisi kuchoka au kukimwa.

Swali ni: Vipi Isa awe kama mitume wengine na yeye amezaliwa bila baba, jambo ambalo si la kawaida, na wengine wote wamezaliwa na baba zao?

Mwenyezi Mungu Mwenyewe amelijibu swali hili na akalifupisha kwa mfupisho huu wa ajabu: "Na neno lake alilompelekea Maryam, na ni roho iliyotoka kwake."

Kwa ufafanuzi zaidi, ni kuwa kauli ya Wakristo, kuzaliwa bila baba ni sahihi. Vilevile ni sahihi kuwa hili si jambo la kawaida, lakini kosa linakuwa pale wanaposema kuwa huku kutokuwa kawaida ndio dalili ya uungu wa Isa. Njia ya makosa ni kuwa kukosekana baba hakulazimiani na kupatikana uungu. Vinginevyo, basi inalazimika Adam awe Mungu, bali yeye ndiye anayestahiki zaidi kuwa Mungu kuliko Isa, kutokana na mantiki yao, kwa sababu ameumbwa bila ya baba na bila ya mama; na Isa amezaliwa na mama.

Zaidi ya hayo, ni kwamba kutokuwepo kawaida si hoja, kwani moto ulikuwa baridi na salama kwa Ibrahim; basi inatakikana awe Mungu, kwa vile hilo ni jambo lisilo la kawaida. Kisha je, kuna la zaidi gani kwa aliyeumba ulimwengu wa ajabu bila ya kitu chochote ila kwa neno moja tu, 'kuwa na ikawa' (36:82),na kuumba mtu bila ya baba? Je, kuumbwa Isa(a.s) ni jambo kubwa kuliko kuumbwa mbingu na ardhi?

﴿لَخَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَكْبَرُ مِنْ خَلْقِ النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴾

"Kwa hakika umbo la mbingu na ardhi ni kubwa kuliko umbo la wanadamu, lakini watu wengi hawajui" .(40:57)

Kwa hiyo neno 'kuwa na ikawa,' ndilo lile lile alilolitumia kwa mja wake Isa, katika kauli yake 'na neno lake alilompelekea Maryam.' Maana ya kumpelekea Maryam, ni kuwa Mwenyezi Mungu alimfahamisha Maryam kuzaliwa mtoto huyu kupitia Malaika. Kwa hiyo 'neno' hapa ndiyo 'neno' kama ilivyo hapo nyuma.

Ama roho aliyomsifu nayo Mwenyezi Mungu (swt) Isa katika Aya hii na nyinginezo makusudio yake ni uhai ambao hauna chimbuko isipokuwa kwake Yeye Mtukufu, na kwamba Mwenyezi Mungu (swt) alimpa uhai huo Isa na akaupa uhai udongo wa Adam:

﴿إِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِّن طِينٍ ﴿٧١﴾ فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِي﴾

"Mola Wako alipowaambia Malaika: Hakika mimi nitaumba mtu kwa udongo. Na nitakapomkamilisha na kumpulizia roho yangu" (38:71-72) Kwa hiyo roho katika udongo wa Adam ndiyo roho katika tumbo la Maryam. Yasemwayo huko ndiyo yasemwayo hapa. Kutofautisha ni kuonea tu!

Wahubiri wa kanisa wamejaribu kuwababaisha wasiokuwa na ujuzi wa Kitabu na siri za lugha, kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu 'na neno lake na roho iliyotoka kwake' ni hoja yao sio jibu la kuwarudishia wao baada ya kufasiri neno na roho, kwa maana ya mfano wa Mwenyezi Mungu na sifa zake, sio kwa maana ya athari miongoni mwa athari za uwezo wake na ukuu wake, kama ilivyo sawa.

Lau lingekuja neno la Mwenyezi Mungu na roho yake katika mfumo mwingine, basi tungeichukulia tafsiri ya makosa kuwa si hadaa wala vitimbi. Lakini wahubri wameyageuza maana ya kukataza yaliyo katika matamko haya mawili, kwa niya mbaya. La kwanza linakataza kupita kiasi katika Bwana Masih(a.s) . La pili linakataza kauli ya utatu na kumnasibishia mtoto. Kisha wakayafasiri matamko hayo kulingana na vile inavyoafikiana na matakwa yao na makusudio yao, sio vile ilivyo katika makamusi ya lugha. Maana ya haya yote ni kuhadaa na kutatiza.

Hebu turudie Aya yote ili msomaji asipotee.

Enyi watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila yaliyo haki. Masih Isa bin Maryam ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na neno lake tu alilompelekea Maryam, na ni roho iliyotoka kwake. Basi mwaminini Mwenyezi Mungu na mitume yake; wala msiseme watatu. Komeni!, itakuwa kheri kwenu. Hakika Mungu ni mmoja tu. Ameepukana kuwa na mtoto. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini; na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa mlinzi.

Je, baada ya maandishi haya yaliyo wazi kuna sababu za kufasiri Neno la Mungu na roho ya Mwenyezi Mungu kuwa ni dhati yake na sifa zake? Hakuna sababu yoyote, hata kama matamko haya yangekuja mbalimbali, haiwezi kufaa tafsiri hii kwa namna yoyote kwa Qur'an ambayo imesema kwa lugha iliyo wazi:

﴿لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ﴾

"Hakika wamekufuru wale waliosema kuwa Mwenyezi Mungu ni watatu wa utatu" (5:73)

Ni umbali ulioje wa kukufurisha huku kuliko wazi, kuwa Qur'an inawaunga mkono Wakristo katika kusema kwao kuwa Masih ni Mungu au ni mwana wa Mungu au kuwa ana sifa za uungu! Ikiwa Qur'an ni hoja katika Aya zake au matamko yake, basi ni wajibu vilevile kauli yake iwe ni hoja:

﴿يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَلْبِسُونَ الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ﴾

"Enyi watu wa Kitabu! Mbona mnachanganya haki na batil na mnaficha haki, hali mnajua" [4] (3:71)

Ikiwa Qur'an si hoja katika kauli yake hii, basi ni wajibu kutokuwa hoja pia mahali pengine. Ama kuamini yote au kukanusha yote, kutofautisha ni hadaa tu.

Wengi katika wahubiri wamemfanyia uovu Bwana Masih na wakajifanyia uovu wao wenyewe, kwa kubadilisha na kugeuza ambako tumekutolea mfano katika yale matamko mawili. Hebu tukisie kwamba mtu wa kawaida amehadaika kwa sababu yao, je, hii itakuwa ni faida kwa Masih au Wakristo? Itakuwaje ukweli wa mambo ukifichuka?

Masih hataona unyonge kuwa mtumwa wa Mwenyezi Mungu wala Malaika wenye kukurubishwa.

Kwa sababu hana njia ya kupata thawabu na kuokoka na adhabu yake isipokuwa kwa kumwabudu yeye peke yake.

Na watakaoona unyonge utumwa wa Mwenyezi Mungu na kutakabari, basi atawakusanya wote kwake.

Huko watangojwa na adhabu kali. Hatuna la zaidi la kutafsiri kauli yake Mwenyezi Mungu:

Ama wale ambao wameamini na wakatenda mema.

Mpaka mwisho wa Aya. Kwa sababu ni wazi zaidi kuliko kufasiriwa. Hata pale niliposema "Huko watangojewa na adhabu kali" Ni kiasi cha kujaza nafasi tu kama ambavyo msomaji ataona, Namna hii wamefanya wengineo katika wafasiri. Sheikh wao mkubwa Tabari amesema:

"Hataona unyonge yaani hajitukuzi,Na watakaoona unyonge yaani watakaojitukuza: Na mwanafalsafa wao Arrazi akasema:" Hataona unyonge, Amesema Azzujaji yaani hajitukuzi, Na watakaoona unyonge yaani walio na unyonge"

Mifano ya hayo ni mingi. Ndio mshairi akajisemea: Wameyafasiri maji baada ya juhudi kuwa ni maji. Hilo walilifanya kwa kujua na kwa makusudi, si kwa lolote ila ni kwamba mfasiri wa Qur'an ni wajibu, kama wanavyodai, afasiri kila linalomjia, hata kama Aya iko wazi. Wameghafilika na yale waliyoyasema walipofasiri kauli yake Mwenyezi Mungu: "Ndani yake zimo Aya zilizo waziwazi, ambazo ndizo msingi wa Kitabu, na nyingine zenye kufichikana." Na kwamba kuzifafanua zilizo wazi, ni mushkeli zaidi ya mushkeli.

﴿يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُم بُرْهَانٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ نُورًا مُّبِينًا ﴾

174.Enyi watu! Imewafikia hoja kutoka kwa Mola wenu na tumewateremshia nuru iliyo wazi.

﴿فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَاعْتَصَمُوا بِهِ فَسَيُدْخِلُهُمْ فِي رَحْمَةٍ مِّنْهُ وَفَضْلٍ وَيَهْدِيهِمْ إِلَيْهِ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا﴾

175.Ama wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na wakashikamana naye, basi atawaingiza katika rehema itokayo kwake na fadhila na atawaongoza kwake kwa njia iliyonyooka.

IMEWAFIKIA HOJA KUTOKAKWA MOLA WENU

Aya ya 174 - 175

MAANA

Enyi watu! Imewafikia hoja kutoka kwa Mola wenu, na tumewateremshia nuru iliyo wazi.

Aya zilizotangulia zimeelezea hoja ya Mayahudi na Wakristo. Baada ya Mwenyezi Mungu kusimamisha hoja kwa wote, amewatolea mwito wote kumwamini Muhammad(s.a.w.w) na Qur'an Tukufu.

Wameafikiana wafasiri kuwa makusudio ya hoja ni Muhammad, na nuru iliyo wazi ni Qur'an na kila anayemfuata Muhammad. Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni dalili ya mkato ya kuhakikisha haki na kubatilisha batili, na ni nuru iliyoenea inayoongoza kwenye usawa. Kwa sababu vyote viwili vinazungumza kwa Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu tu. Mwenyezi Mungu anasema:

﴿قُلْ مَا كُنتُ بِدْعًا مِّنَ الرُّسُلِ وَمَا أَدْرِي مَا يُفْعَلُ بِي وَلَا بِكُمْ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ وَمَا أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ﴾

"Sema: mimi si kioja katika mitume; wala sijui nitakavyofanywa mimi wala nyinyi, sifuati ila niliyopewa wahyi na mimi si lolote ila ni muonyaji mwenye kubainisha." (46:9)

Ama dalili ya kuwa Muhammad na Qur'an ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kwamba ni hoja, haiwezi kufupilizwa na yanayosemwa katika tafsiri ya Aya.

Wahakiki wametunga mamia ya vitabu kuhusu hizo dalili, Tumevitaja vingi kila inapohitajika katika Tafsir yetu hii, Ni juu ya mwenye kuitafuta haki kufanya utafiti na kufuatilia. Kuna kitu kimoja tunachomwomba huyo mtafutaji, asighafilike nacho - alinganishe baina ya mafunzo ya Qur'an na mafunzo ya vitabu vya dini nyingine.

Vilevile afanye utafiti wa idadi ya Injil, zilikuwa ngapi katika karne ya kwanza au ya pili baada ya kuzaliwa Isa (a.s)? Afanye utafiti, kwa nini walifanya mkutano wa Maaskofu huko Nicaea[5] mwaka 325 AD ambao uliwajumuisha Maaskofu elfu mbili na arobaini (2040) waliwakilisha makanisa yote ulimwenguni? Je, waliafikiana nini katika kongamano hili? Je, waliafikiana Maaskofu wote kuwa Isa ni Mungu, au kuna wengine waliosema ni kiumbe na wengine wakasema ni Mungu? Je, waliingilia suala la asili ya tatu - roho mtakatifu na kutaja uungu wake, au uliokubali uungu wa asili hii ni mkutano uliofanywa Constantine mwaka 381 AD na kwamba asili hii haikujulikana[6] kabla ya tarehe hii?

Tunamtaka yule anayetafuta haki kufanya utafiti kwa upande huu na sisi tuko pamoja naye katika natija yoyote atakayoishilia nayo.

Ama wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na wakashikamana naye, basi atawaingiza katika rehema itokayo kwake na fadhila na atawaongoza kwake kwa njia iliyonyooka.

Baadhi ya wafasiri wametofautisha baina ya rehema na fadhila, kwamba rehema inakuwa duniani na fadhila itakuwa akhera. Mwingine akasema akimnukuu Ibn Abbas, kwamba rehema ni pepo na fadhila ni ile ambayo hakuna jicho lilioiona wala sikio lililoisikia, Lakini huyu inaonekana alitaka kutofautisha, akachanganya. Kwa sababu sifa hizi ni za pepo hasa.

Ama sisi hatuoni tofauti yoyote baina ya rehema na fadhila. Inafaa kuunganishwa kimatamko tu, jambo ambalo linaptikana sana katika lugha ya kiarabu na linapendeza, Nalo huitwa kuunganisha tafsiri.

Maana kwa ujumla ni kuwa mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu na akamtegemea yeye tu, basi atakuwa katika rehema ya Mwenyezi Mungu na fadhila yake duniani na akhera. Duniani atapewa tawfiki na uongofu wa njia ya kuielekea haki, hataiacha kabisa. Ama huko akhera basi ni raha, manukato na mabustani yenye neema.

Ufupisho wa tafsiri ya Aya hii ni kauli ya Amirul-Muminin(a.s) :"Mola mwenye kurehemu na dini iliyo sawa." Kila mtu na alichokichagua.

﴿يَسْتَفْتُونَكَ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِي الْكَلَالَةِ إِنِ امْرُؤٌ هَلَكَ لَيْسَ لَهُ وَلَدٌ وَلَهُ أُخْتٌ فَلَهَا نِصْفُ مَا تَرَكَ وَهُوَ يَرِثُهَا إِن لَّمْ يَكُن لَّهَا وَلَدٌ فَإِن كَانَتَا اثْنَتَيْنِ فَلَهُمَا الثُّلُثَانِ مِمَّا تَرَكَ وَإِن كَانُوا إِخْوَةً رِّجَالًا وَنِسَاءً فَلِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ أَن تَضِلُّوا وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴾

176.Wanakuuliza fatwa; sema: Mwenyezi Mungu anawapa fatwa juu ya mkiwa. Iwapo mtu amekufa hali hana mtoto na anaye ndugu wa kike, basi (huyo dada) atapata nusu ya alichokiacha. Naye atamrithi nduguye wa kike akiwa hana mtoto. Wakiwa ni ndugu wa kike wawili basi watapata theluthi mbili za alichokiacha. Na wakiwa ni ndugu wa kiume na wa kike, basi fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili. Mwenyezi Mungu anawabainishia ili msipotee; na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

MWENYEZI MUNGU ANAWAPA FATWA JUU YA MKIWA

Aya 176

MAANA

Wanakuuliza fatwa; sema Mwenyezi Mungu anawapa fatwa juu ya mkiwa.

Mkiwa katika mrithi ni asiyekuwa mzazi au mtoto. Pia yule anayerithiwa na huyo anaitwa mkiwa, kwa vile hakurithiwa na mzazi au mtoto. Natija ni moja katika sifa zote mbili.

Neno hili limekuja katika Aya mbili katika Qur'an, katika Sura Annisa. Moja ni mwanzo wa Sura hii, ambapo makusudio yake huko ni ndugu wa marehemu wa upande wa mama tu, na Aya ya pili ni hii tuliyo nayo, ambapo makusudio yake hapa ni ndugu wa marehemu na dada zake wa upande wa baba na mama, au wa baba tu.

Iwapo mtu amekufa hali hana mtoto wa kiume au kike, kwa sababu neno Walad linatumiwa kwa aliyezaliwa (mtoto). Mwenyezi Mungu anasema katika kutumia neno walad:"Mwenyezi Mungu hakujifanyia mtoto" (23:91)

Na pia akiwa hana mmoja wa wazazi wawili, kama linavyofahamisha neno "ukiwa" kuongezea Hadith.

Na anaye ndugu wa kike, basi (dada huyo) atapata nusu ya alichokiacha. Makusudio ya ndugu wa kike ni ndugu baba mmoja mama mmoja, ikiwa hayuko basi ni wa baba mmoja tu. Ama ndugu wa kike wa upande wa mama tu, hukumu yake imekwishaelezwa katika Aya 11 ya Sura hii.

Yaani, ikiwa yuko dada wa tumbo moja au wa upande baba tu hakuna mtoto wala mmoja wa wazazi wawili, basi dada atachukua nusu kama fungu lake na atachukua nusu ya pili kwa kurudishwa; yaani atachukua mali yote.

Hiyo ni kwa upande wa Shia. Ni sawa awe marehemu ana asaba (ami wa marehemu n.k) au la. Ama Sunni wanaitoa nusu iliyobaki kwa asaba akiwepo, kama hayupo basi atachukua mali yote. Tofauti baina ya Sunni na Shia ni kuwepo asaba tu. Maelezo zaidi yako kwenye vitabu vya Fiqh.

Naye atamrithi nduguye wa kike akiwa hana mtoto wa kike au wa kiume, wala mmoja wa wazazi wawili na atachukua mali yote kwa kurithi, kwa maafikiano ya madhehebu zote.

Wakiwa ni ndugu wa kike wawili basi watapata theluthi mbili za alichokiacha.

Yaani ndugu wa kike wa upande wa baba na mama au upande wa babu tu. Yameafikiana madhehebu yote ya kiislamu kuwa hukumu ya dada wawili ndiyo ya wengi; Kwa hiyo maana hapa itakuwa wakiwa ni wawili na zaidi basi watapata theluthi mbili ya alichokiacha marehemu awe kaka au dada.

Na wakiwa ni ndugu wa kiume na wa kike, basi fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili.

Baada ya kubainisha fungu la ndugu wa kike peke yao, na fungu la dada wawili na zaidi wasiokuwa na kaka zao, amebainisha wakiwa pamoja ndugu wa kike na kiume kwamba wanaume watapa mara mbili zaidi ya wanawake.

Yamekwishatangulia maelezo kwa urefu na ufafanuzi kuhusu mirathi ya binti na dada katika kufasiri Aya ya 11 ya Sura hii pamoja na kauli za Shia na Sunni na dalili zao.