TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA SITA Juzuu 6

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA SITA0%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA SITA Mwandishi:
: HASANI MWALUPA
Kundi: tafsiri ya Qurani

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA SITA

Mwandishi: Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya
: HASANI MWALUPA
Kundi:

Matembeleo: 16191
Pakua: 2342


Maelezo zaidi:

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 11 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 16191 / Pakua: 2342
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA SITA

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA SITA Juzuu 6

Mwandishi:
Swahili

8

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA SITA

﴿إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ﴾

55. Hakika walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.

﴿وَمَن يَتَوَلَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا فَإِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْغَالِبُونَ﴾

56.Na atakayemtawalisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini, basi kundi la Mwenyezi Mungu ndio watakaoshinda.

HUTOA ZAKAWAKIWAWAMERUKUI

Aya 55-56

MAANA

Hakuna hata mmoja anayebishana kuwa makusudio ya neno walii kwa Mwenyezi Mungu na Mtume ni kuwa msimamizi na kutawalia mambo ya Waislamu na wala sio mapenzi na usaidizi tu. Mwenyezi Mungu anasema:"Nabii ana haki zaidi kwa waumin kuliko nafsi zao" (33: 6)

Aya hii ni ubainifu na tafsiri ya neno (walii) katika Aya tuliyo nayo. Na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutuoa Zaka wakiwa wamerukui: Yaani wilaya ambayo imethibiti kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, imethibiti vile vile kwa aliyetoa zaka huku amerukui.

Amenukuu Tabari kutoka kwa Mujahid Utaba bin Hakim na Abu Jafar kwamba Aya hii ilishuka kwa sababu ya Ali bin Abu Talib.

Katika Kitabu Gharaibul-Qur'an wa raghaibul-furq'an cha Nidhamuddin, Ali-Hassan bin Muhammad Annaisaburi, katika Maulama wa sunni, imeandikwa hivi (ninamnukuu): "Aya imeshuka kwa Ali, kwa maafikiano ya wafasiri wengi" Vile vile katika tafsiri Arrazi imeandikwa (ninamkuu): "Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr, (r.a) kwamba yeye amesema: "Niliswali na Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) siku moja, akaja mtu kuomba, lakini hakuna yeyote aliyempa kitu. Ali alikuwa amerukui, akamwashiria kidole chake cha pete cha upande wa kuume.

Yule mwombaji akachukua pete huku Mtume(s.a.w.w) akiwa anamuangalia. Akasema Mtume: 'Ewe Mola wangu ndugu yangu Musa alikuomba kwa kusema:' 'Ewe Mola Wangu! Nikunjulie kifua changu na unifanyie waziri katika jamaa zangu, ndugu yangu Harun, nitie nguvu kwaye' 'Basi Ewe Mola wangu! Na mimi ni Muhammad Mtume wako na mteule wako, basi nikunjue kifua changu na unisahili she jambo langu, unifanyie waziri katika jamaa zangu na unitie nguvu kwaye", Abu Dharr anasema: Hakumaliza maneno haya na Jibril akashuka, na akasema "Ewe Muhammad! Soma: Hakika walii wenu ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake Mpaka mwisho wa Aya."

Lakini Razi amefasiri neno (walii) hapa kwa maana ya msaidizi, sio mtawala. Shia nao wakasema: Tamko la Mwenyezi Mungu na Mtume na mwenye kutoa zaka akiwa amerukui limekuja katika Aya moja na wilaya ya Mwenyezi Mungu na Mtume, maana yake ni utawala. Kwa hiyo ni lazima vile vile maana ya wilaya ya mwenye kukusanya sifa mbili hizi ni utawala vile vile. Vinginevyo, basi neno wilaya litatumika kwa maana mbili tofauti wakati mmoja, jambo ambalo haliwezekani. Na mwenye kumtawalisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waumini, basi kundi la Mwenyezi Mungu ndio watakaoshinda.

Aya hii ni kauli wazi isiyokubali taawil kwa hali yoyote kwamba maana ya makusudio ya kumtawalisha Mwenyezi Mungu na Mtume na waumini ni moja isiyokuwa na tofauti na kwamba mwenye kuichunga wilaya hii na wala asitofautishe baina ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na mwenye kutoa zaka akiwa amerukui, basi yeye yuko katika kundi la Mwenyezi Mungu litakaloshinda; kutokana na mantiki ya haki na hoja yake.

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَكُمْ هُزُوًا وَلَعِبًا مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَالْكُفَّارَ أَوْلِيَاءَ وَاتَّقُوا اللَّـهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴾

57.Enyi mlioamini! Msiwafanye marafiki wale walioifanyia mzaha na mchezo dini yenu katika wale waliopewa Kitab kabla yenu na makafiri. Na mcheni Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni waumini .

﴿وَإِذَا نَادَيْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ اتَّخَذُوهَا هُزُوًا وَلَعِبًا ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ﴾

58.Na mnaponadi Swala, wanaifanyia mzaha na mchezo. Hayo ni kwa sababu wao ni watu wasiokuwa na akili.

﴿قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ هَلْ تَنقِمُونَ مِنَّا إِلَّا أَنْ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلُ وَأَنَّ أَكْثَرَكُمْ فَاسِقُونَ ﴾

59.Sema: Enyi watu wa Kitab! Hivyo mnatuchukia kwa kuwa tumemwamini Mwenyezi Mungu na yale yaliyoteremshwa zamani na ya kwamba wengi wenu ni mafasiki.

DINI YENU WAMEIFANYIA MZAHA NA MCHEZO

Aya 57 - 59

MAANA

Enyi mlioamini! Msiwafanye marafiki wale walioifanyia mzaha na mchezo dini yenu katika wale waliopewa Kitab kabla yenu na makafiri.

Kwa mara ya pili Mwenyezi Mungu (s.w.t) anakataza kuwafanya maadui wa Mwenyezi Mungu kuwa marafiki, lakini hapa amebainisha sababu ya kukataza. Sababu yenyewe ni kuwa wao wameifanya dini ya kiislamu na Swala ya waislam ni vitu vya kuchezewa.

Ndivyo alivyo safihi anayeshindwa kujibu hoja, Wala haielekei kwa mwenye akili kumfanya walii safihi hasa yule anayechezea dini na utakatifu wake. Vilevile Mwenyezi Mungu (s.w.t) amezidisha, katika Aya hii, kuunganisha makafiri na watu wa Kitab, katika hali ya kuungisha mahsusi kwenye ujumla. Qur'an huunganisha mahsusi kwenye ujumla, kama Aya hii; na ujumla kwenye mahsusi kama Aya isemayo:

"Angalieni sana Swala na ile Swala ya katikati" (2:238)

Na pia huunganisha kitu kwenye mfano wake; kama pale aliposema."Basi hao atawaingiza katika rehema itokayo kwake na fadhila" (4:175)

Na mcheni Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni waumini.

Ndani yake mna utambulisho kuwa mwenye kumfanya mwenye kuchezea dini kuwa ndiye mwenzake na walii wake, basi huyo yuko mbali na watu. Kwa sababu mwenye kushahibiana na kitu kuvutiwa nacho.

Na mnaponadi Swala, wanaifanyia mzaha na mchezo.

Makanisa ya wakristo yanawaita wafuasi wake kwenda kuswali kwa kupiga kengele, na masinagogi ya Mayahudi huwaita wafuasi wake kwa kupiga tarumbeta. Ama Waislamu, huwaita wafuasi wake kwenye Swala kwa sauti ya mwadhini anayelingania kwa Mwenyezi Mungu peke yake asiye na mshirika, na kwenye amali njema ya kufaulu: Mwenyezi Mungu ni mkubwa Hapana mola i sipokuwa Mwenyezi Mungu Njooni kwenye kufaulu Njooni kwenye amali njema Baadhi ya watu wa Kitab walikuwa na bado wanaendelea kuidharau adhan hii na mwito huu. Ingefaa basi wazidharau kengele zao na tarumbeta zao.

Wakati huo huo Wakristo wasiokuwa na kasumba wanaifadhilisha adhan kuliko kengele. Mwenye Al-manar anasema: "Tuliwasikia baadhi ya wakristo wasiokuwa na kasumba nchini mwetu, yaani Lebanon, wakisifu maneno ya adhan na kuifadhilisha kuliko kengele. Katika mtaa wa Kalamon mjini Tripoli, baadhi ya jamaa wa kikiristo walikuwa wakisimama. Wanawake na wanaume wakawa wanasimama madirishani kusikiliza sauti ya mwadhini, ambaye alikuwa na sauti nyororo.

Ilikuwa mtoto wao anaweza kuhifadhi adhan na kumwigiza vizuri mwadhini, hapo mama hukasirika na kumkataza, lakini baba hucheka na kufurahia adhana ya mtoto wake, kwa sababu alikuwa yuko huru na wasaa." Hayo ni kwa sababu wao ni watu wasio na akili.

Wamesema wafasiri, akiwemo Razi na mwenye Al-Manar, kuwa makusudio ya Wasio na akili ni kwamba wao hawajui hakika ya Uislam. Lau wangeijua hakika yake wasingeufanyia mchezo, Ama sisi tunasema kuwa wanaujua Uislamu, na wanajua lengo lake. na kwamba wale walioupiga vita, walifanya hivyo kwa sababu waliona hatari yake kwa manufaa yao. Walijua kuwa Uislam ni mapinduzi ya kujikomboa na dhulma, unyonyaji, ufukara, ujinga na ubaguzi, na kwamba hakuna ubora wa kiumbe yeyote kumzidi kiumbe mwengine ila kwa kuwahudumia watu na kufanya kazi kwa ajili ya masilahi ya wote, Hili ndilo kosa la Uislam kwao. Ndio maana wakaupiga vita kwa silaha zote walizonazo, hata kebehi na dharau.

Mwito wa kiislamu unadhihiri kwa maana yake kamili katika wito wa mwadhini. Mwenyezi Mungu ni mkubwa, hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu. Kwani maana ya Mwenyezi Mungu ni Mkubwa ni kwamba hakuna mkubwa wala adhimu ila yeye peke yake hana mshirika. Na maana ya Hapana mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, ni kwamba mali na cheo na nasabu sio mungu wa kuabudiwa wala nguvu ya kunyenyekewa, ni haki peke yake, na watu wote katika haki ni sawa, hakuna yeyote mwenye ruhusa ya kuugusa uhuru wa mwengine vyovyote atakavyokuwa. Hili linatosha kuwa ni kosa kwa maadui wa binadamu. Na kwa ajili ya uadui wao huu, si kwa ajili ya kutojua uhakika wa Uislamu, ndipo Mjuzi mwenye hekima akawasifu kwamba wao ni watu wasiokuwa na akili.

Sema: Enyi watu wa Kitab! Hivyo mnatuchukia kwa kuwa tumemwamini Mwenyezi Mungu na yale yaliyoteremshwa zamani, na ya kwamba wengi wenu ni mafasiki?

Ndio! Wao hawamridhii ila yule wanayemwamini wao na unyonyaji wao. Huyo ndiye mtakatifu wa watakatifu, katika vipimo vyao, hata ikiwa anamkufuru Mwenyezi Mungu na Mitume wote. Ama mwenye kukana dhulma yao na utaghuti wao, basi huyo kwao ni mshari wa mwanzo na wa mwisho, hata kama ni walii wa mawalii.

Dalili kubwa ya hilo ni kuwa wao wanawatuhumu wazalendo na kuwazulia kuwa wametoka katika dini, si kwa lolote ila ni kwa kuwa wanapinga siasa za kikoloni na za ubaguzi. Pamoja na tuhuma zao hizi, wao wanadai kuwa ni wahami na walinzi wa dini na walahidi.

Unaweza kuuliza : Kauli yako hii ndivyo mambo yalivyo, tunavyoyaona na tunavyoyashuhudia, lakini hayafai kuwa ni tafsiri ya Aya hii. Kwa sababu wao wanahasimiana na Waislam kwa sababu ni Waislamu wanaomwamini Mwenyezi Mungu Qur'an, Tawrat na Injil?

Jibu : Dhahiri ya Aya inafahamisha waziwazi kuwa, Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimwamrisha Mtume wake Mtukufu kuwaambia Je sisi tunakosa linalotusababisha kuwa na uadui na nyinyi kwa vile tu ni kuwa sisi tuko kwenye haki na nyinyi mko kwenye batili; sawa na mzalendo halisi anavyomwambia kibaraka mhaini: 'Je, unanichukia kwa vile mimi ni mzalendo na wewe ni kibaraka'

Hakuna shaka kwamba maana haya yanafikiana na tafsir yetu ya Aya, bali hiyo ndiyo iko dhahiri zaidi. Ameyaelezea hayo mwenye Majmaul-bayan alipoeleza kwenye Tafsir yake: "Maana ya Aya hii ni: Je, mnatuchukia kwa imani yetu na ufasiki wenu;" yaani mmeichukia imani yetu na nyinyi mnajua tuko kwenye haki na kwamba nyinyi mko kwenye dini yenu kwa kupenda kwenu ukubwa na kuchuma mali? Kisha akaendelea kusema: "Na maana ya ufasiki ni kuwa wao wametoka katika amri ya Mwenyezi Mungu kwa kutaka ukubwa."

﴿قُلْ هَلْ أُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ مِّن ذَٰلِكَ مَثُوبَةً عِندَ اللَّـهِ مَن لَّعَنَهُ اللَّـهُ وَغَضِبَ عَلَيْهِ وَجَعَلَ مِنْهُمُ الْقِرَدَةَ وَالْخَنَازِيرَ وَعَبَدَ الطَّاغُوتَ أُولَـٰئِكَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضَلُّ عَن سَوَاءِ السَّبِيلِ﴾

60.Sema: Je, niwaambie yule mwenye malipo mabaya kuliko haya mbele ya Mwenyezi Mungu? Ni ambaye Mwenyezi Mungu amemlaani na kumkasirikia na akawafanya miongoni mwao manyani na nguruwe na akamwabudu Taghuti. Hao ndio wenye mahali pabaya na wapotofu sana na njia iliyo sawa.

﴿وَإِذَا جَاءُوكُمْ قَالُوا آمَنَّا وَقَد دَّخَلُوا بِالْكُفْرِ وَهُمْ قَدْ خَرَجُوا بِهِ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا كَانُوا يَكْتُمُونَ ﴾

61.Na wanapowajia husema: Tumeamini hali wao wameingia na ukafiri wao na wametoka nao. Na Mwenyezi Mungu anayajua sana wanayoyaficha.

﴿وَتَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يُسَارِعُونَ فِي الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴾

62.Na utawaona wengi katika wao wanakimbilia kwenye dhambi na uadui na kula kwao haramu. Hakika ni mabaya waliyokuwa wakiyatenda.

﴿لَوْلَا يَنْهَاهُمُ الرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ عَن قَوْلِهِمُ الْإِثْمَ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَصْنَعُونَ﴾

63.Mbona watawa wao na maulama wao hawawakatazi maneno yao ya dhambi na uadui na ulaji wao wa haramu? Hakika ni mabaya waliyokuwa wakiyafanya.

AKAWAFANYA WENGINE MANYANI NA NGURUWE

Aya 60 - 63

MAANA

Sema: Je, niwaambie yule mwenye malipo mabaya zaidi kuliko hayo mbele ya Mwenyezi Mungu?

Yaani sema Ewe Muhammad kuwaambia maadui wa haki na wa dini ambao wanaucheza shere Uislamu na adhan kuwa, ikiwa kumwamini Mwenyezi Mungu na vitabu vyake ni shari inayowajibisha chuki, basi mimi ninawapa habari ya shari kuliko hii, nayo ni ambao Mwenyezi Mungu amewaalani na kuwakasirikia na kuwafanya manyani na nguruwe na wakamwabudu Taghut. Sifa zote hizi ni za mayahudi, ambazo Mwenyezi Mungu amewaorodheshea katika ziada ya Aya hii na akawasifu kwa kuabudu Taghut.

Aya zilizo mfano wa Aya hii ni kama zifuatavyo:-

1."...kama tulivyowalaani watu wa Sabato (Jumamosi). (4:47)

2."Kwa hiyo wakastahili ghadhabu juu ya ghadhabu" (2:90)

3."Basi tukawaambia kuweni manyani wadhalilifu." (2:65)

Na analosema Mwenyezi Mungu kuwa, huwa

4. "Wanaamini sanamu na taghut" (4:51).

Imesemekana, makusudio ya taghuti ni shetani na ikasemekana ni ndama, na sahihi ni kuwa kila anayemtii mja katika kumwasi Mwenyezi Mungu, basi huyo amemwabudu yeye.

Arrazi amesema: " wametoa hoja masihabu zetu- yaani Ash-ari- kwa Aya hii, kwamba ukafikiri ni maajaliwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu makadirio hapa ni, Na akawajalia Mwenyezi Mungu kuabudu Taghut." Lakini usahihi ni kuwa hayo yanaungana na laana ya Mwenyezi Mungu, yaani: Je, niwaambie yule mwenye malipo mabaya kuliko haya ni ambaye Mwenyezi Mungu amewalani na akamwabudu Taghut; kwa hivyo haifai kutoa dalili na Aya hii kwamba ukafiri unatokana na Mwenyezi Mungu na sio mja.

Hao ndio wenye mahali pabaya na wapotofu sana na njia iliyo sawa.

Hao ni ishara ya Mayahudi, kwa dhahiri. Na ilivyo hasa inawachanganya wote wanaoipiginga haki.Wala haitoshelezi kauli ya kusema: Hapana mola ila Allah na Muhammad ni mtume wa Mwenyezi Mungu.Kwani hakuna imani bila ya Takua.

Na wanapowajia husema: Tumeamini hali wao wameingia na ukafiri wao na wametoka nao.

Wanafiki wa kiyahudi walikuwa wakiingia kwa Mtume na kumwambia: sisi tumekuamini; na hali wao ni waongo.Mwenyezi Mungu anauelezea unafiki wao huu kwamba wao wameingia kwa Mtume na ukafiri na wakatoka kwake na ukafiri. Ibara hii inafahamisha kuwa lau kama wao walikuwa wanaitafuta haki kweli wangelitoka mbele za Mtume wakiwa waumini baada ya kusikia na kuona dalili na ubainifu.

Na Mwenyezi Mungu anayajua sana wanayoyaficha katika ukafiri na unafiki na kuwalipa wanayostahiki.

Na utawaona wengi wao wanakimbilia katika dhambi na uadui na kula kwao haramu. Hakika ni mabaya waliyokuwa wakiyatenda.

Kukimbilia ni kuashiria kushindana katika dhambi na kula haramu.

Sifa hii hawaepukani nayo Mayahudi, na ndio maana watu wa zamani na wa sasa wamewachukia isipokuwa yule atakayewatumia kufanyia shari, sawa na sumu kwa muuaji. Hata huko Marekani, ambako ni kiota cha Uyahudi, pia wako wengi wanaowachukia Mayahudi.

Mbona watawa wao na maulama wao hawawakatazi maneno yao ya dhambi na uadui na ulaji wao wa haramu? Hakika ni mabaya waliyokuwa wakiyafanya.

Kutahayarizwa huku, kunakofahamishwa na neno, mbona na ubaya, kwa dhahiri kunaelekezwa kwa viongozi wa dini katika watu wa Kitab, na kwa hali halisi, kunaelezwa kwa kila aliyejua haki na akainyamazia. Kwa hakika mwenye kumjua Mwenyezi Mungu kikweli na kumfanyia Ikhlasi yeye tu peke yake, hupinga udhalimu kwa nyenzo zote.

Akiwa na yakini kuwa kifo chake katika njia hii kitawazindua waliolala na kuwapinga madhalimu anakuwa tayari na kuueleza upinzani wake kwa kufa shahidi. Historia ya mashahidi wote ni historia ya kupinga makosa ya dhulma na uadui.

﴿وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّـهِ مَغْلُولَةٌ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم مَّا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَانًا وَكُفْرًا وَأَلْقَيْنَا بَيْنَهُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ كُلَّمَا أَوْقَدُوا نَارًا لِّلْحَرْبِ أَطْفَأَهَا اللَّـهُ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ﴾

64.Walisema Mayahudi: Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba. Mikono yao ndiyo iliofumba, na wamelaaniwa kwa waliyoyasema, Bali mikono yake iko wazi hutoa apendavyo. Kwa hakika yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako yatawazidisha wengi katika wao uasi na kufru. Na tumewatilia uadui baina yao na chuki mpaka siku ya Kiyama. Kila mara wanapowasha moto wa vita Mwenyezi Mungu anauzima, Na wanajitahidi kuleta ufisadi katika ardhi, Na Mwenyezi Mungu hawapendi wafisadi.

﴿وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْكِتَابِ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَكَفَّرْنَا عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَأَدْخَلْنَاهُمْ جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴾

65.Na lau kwamba watu wa Kitab wangeliamini na wakamcha Mungu, tungeliwafutia makosa yao na kuwaingiza katika bustani (pepo) zenye neema.

﴿وَلَوْ أَنَّهُمْ أَقَامُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِم مِّن رَّبِّهِمْ لَأَكَلُوا مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِم مِّنْهُمْ أُمَّةٌ مُّقْتَصِدَةٌ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ سَاءَ مَا يَعْمَلُونَ﴾

66.Na lau wangelisimamisha Tawrat na Injil na yale yaliyoteremshwa kwao kutoka kwa Mola wao kwa hakika wangelikula vya juu yao na vya chini ya miguu yao. Miongoni mwao wako watu walio sawa na wengi wao wanayoyafanya ni mabaya.

MAYAHUDI WALISEMAMKONO WAMWENYEZI MUNGU UME FUMBA

LUGHA

Neno 'mkono' lina maana nyingi ikiwemo hizi zifuatazo:-

i. Kiungo, yaani huu mkono wa kawaida ninaoandikia maneno haya.

ii. Neema, kama kusema fulani ameniunga mkono, ninamshukuru.

iii. Uwezo.

iv. Milki, hutumiwa kutoa na kuzuia kulingana na hali ilivyo.

Unaweza kusema : Amenyoosha mkono wake; kama ukikusudia kutoa. Na kusema: Ameufumba mkono wake; kama ukikusudia kuzuia.

MAANA

Walisema Mayahudi: Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba.

Hii ni picha miongoni mwa picha kadhaa zinatolewa na Qur'an kwa Mayahudi, kama vile kusema kwao: "Hakika Mwenyezi Mungu ni fukara na sisi matajiri."

Kulingana na makisio yao ni kuwa wao wawe waungu. Mwenyezi Mungu umetukuka ukuu wake. Utovu wao huu wa haya na ufidhuli, ulidhihiri ubaya wa maana yake katika kukiuka kwao makubaliano ya kimataifa kwa kuivamia Quds mnamo mwaka 1967.

Baadhi ya mapokezi yanasema kuwa aliyetamka neno hili la kufuru, ni Myahudi mmoja anayeitwa Finhas. Inawezekana kuwa riwaya hii ni sahihi, na ni kweli kuwa kauli ya mtu mmoja haiwakilishi kundi la watu wote; na pia ni kweli kwamba baadhi ya Waislamu dhaifu husema hivi wanapozongwa na masaibu wakiwa hawana la kufanya.

Yote haya yanaweza kuwa kweli, lakini mwenye kuichunguza sera ya Mayahudi atajua kuwa wao wanalisema neno hili kwa lugha ya vitendo ingawaje hawatamki kwa mdomo. Wao wanataka Mwenyezi Mungu awape dunia yote na vilivyomo, vinginevyo basi Mwenyezi Mungu ni bakhili aliyefumba mkono.

Mikono yao ndiyo ilifumba na wamelaaniwa kwa yale waliyoyasema

Na waliyoyafanya ya kushindana katika dhambi, uadui na vile vile kula kwao mali ya haramu.

NJAMA ZA MAYAHUDI NA WANAZI [18]

Mwenye Tafsir Al-Manar anasema: "Mikono yao ndiyo iliyofumba, ni maapizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ubakhili wao. Na bado wao ndio mabakhili zaidi, Yeyote katika wao hawezi kutoa kitu mpaka awe na faida sana."

Ilikuwa faida yao pekee ni mali. Na kwa ajili ya mali wanahalalisha kila la haramu. Ama leo, hawana faida bora kuliko kumwua Mwarabu hata kama ni mtoto. Nembo takatifu ya kidini ya jumuia zao za kujitolea ni 'Toa Dola moja itamwua Mwarabu,' awe Mwislamu au Mkiristo. Bali wao, wake kwa waume na hata watoto wanatoa roho zao ili wawatoe wapalestina nchini mwao na wachukue mahali pao. La kushangaza katika niliyoyasoma ni kwamba viongozi wa Kizayuni akiwemo. Wiseman, Moses Sarit, David ben Gorin na viongozi wa Custavo, walikula njama pamoja na wanazi kuwachinja Mayahudi na kuwatesa kwa malengo mawili:

Kwanza : Wayahudi wawe na sababu ya kuhamia Palestina,

Pili : kupatikane sababu ya kuunda serikali ya Kiisraeli. Hayo yamo katika kitabu kilichofasiriwa kwa kiarabu na Asal kwa jina la Itlaqul-hamama 5 Julai, kilichotungwa na Belyalev, Costanchenko na Primakov.

Ikiwa Mayahudi wanaweza kupanga njama pamoja na maadui zao wakubwa na kuwatoa mhanga maelfu katika wao ili tu isimame dola ya Israil, je watashindwa kusema kuwa Mwenyezi Mungu ni fukara na wao ni matajiri na kwamba mkono wake umefumba hautoi. Kuna ajabu kusema: Sisi tunaihami amani na waarabu wanachochea vita na uharibifu, baada ya kuwa washasema Mwenyezi Mungu ni fukara na sisi ni matajiri?

Ikiwa mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba kwa vile hakuwapa dunia na vilivyomo, basi waarabu kwao watakua ni mataghuti na wachokozi kwa vile hawakuwachia Mayahudi. Mimi sisemi maneno haya kama ngonjera au kwa sababu ya hamaki. Kwani si ni hao mayahudi waliowang'ang'ania waarabu waitambue Israil?

Je,kuna maana nyingine ya kutaka kutambuliwa huku zaidi ya kutaka waachiwe wao tu?

Bali mikono yake iko wazi.

Makusudio ya mikono ni yale makusudio ya mkono wake wa kuume katika Aya isemayo:

"Na mbingu zitakunjwa kwa mkono wake wa kuume" (39:67)

Yaani kwa uwezo wake. Amesema Mikono na wala sio mkono kwa sababu ndiyo picha iliyo fasaha zaidi na inayokusanya zaidi maana.

Hutoa apendavyo.

Kwa kuleta sababu yenye kuwajibisha hilo:

﴿هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولًا فَامْشُوا فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا مِن رِّزْقِهِ وَإِلَيْهِ النُّشُورُ ﴾

"Yeye ndiye aliyeidhalilisha ardhi kwa ajili yenu, Basi nendeni katika pande zake zote na kuleni katika riziki yake Na kwake yeye ndio kufufuliwa" (67:15)

Kwa hakika yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako yatawazidisha wengi katika wao uasi na kufuru.

Makusudio ya wengi ni viongozi na wapenda anasa ambao hawatoi mwito wa haki kwa kuhofia vyeo vyao. Na mwito huu umewazidishia chuki kwa Muhammad(s.a.w.w) , kwa sababu umefichua aibu zao na maovu yao, yakiwemo kubadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu na mahali mwake, kula kwao mali ya haramu na kuacha kukataza maovu.

Ni kawaida ya mwenye kujigamba kuzidisha ujeuri akifichuliwa aibu yake na madhambi yake.

Na tumewatilia uadui na chuki baina yao mpaka siku ya Kiyama.

Mwenye Tafsir Al-Manar amesema: "Hajui katika Tafsiri zilizopokelewa kutoka kwa waliotangulia ila ni kuwa dhamiri katika 'Baina yao' inawarudia mayahudi na wakristo walioelezwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu: "Enyi mlioamini msiwafanye mayahudi na manaswara marafiki."

Na katika Tafsir za kisasa wanasema kuna uwezekano wa kuwa dhamiri ni ya mayahudi peke yao. Sisi tuko kwenye rai ya waliotangulia kwa sababu mbili:

Kwanza : kwa sababu wao ndio wajuao zaidi misamiati ya Qur'an na Hadith kuliko waliokuja baadaye. Kwani wao wako karibu zaidi na zama za mtume na kushuka Qur'an.

Pili : kwa sababu uadui baina ya mayahudi na manaswara upo. Mayahudi wanaitakidi kuwa Masih ni mdanganyifu, mwenye hila na mtoto wa zina - Mungu apishe mbali - Na manaswara (Wakristo) wanaitakidi kuwa yeye ni mwana wa mungu, ambapo Waislamu wanaitakidi kuwa yeye ni Mtume aliyetakaswa na ujinga na maasi. Kwa hiyo ni muhali kuondoka uadui baina ya mayahudi na wakristo maadam kila upande una itikadi yake.

Alijaribu Papa wa Roma mnamo mwaka 1965 kuyasogeza pamoja makundi mawili, lakini Mayahudi bado wanang'angania rai yao kwa Bwana Masih(a.s) . Hata hivyo kuna aina ya ushirikiano wa kitamaa, bali wakuu wa mashirika wameungana pande zote mbili lakini kwa misingi ya kibiashara tu, sio misingi ya dini.

MAYAHUDI NA MOTO WA VITA

Kila mara wanapowasha moto wa vita Mwenyezi Mungu anauzima. Neno 'vita' tangu mwanzo lilipowekwa liliwekwa kwa maana ya kupigana na kuuana. Limetumika kwa maana haya karne kwa karne. Siku zilipoendelea kupita nalo likakua mpaka hivi sasa limekuwa na maana ya kutokuwepo amani na raha.

Nchi yoyote inayohofia kuvamiwa na nchi yenye nguvu zaidi au maisha yake yakapanda kwa sababu ya vita vilivyoko nchi nyingine, basi nayo iko katika hali ya vita, hata kama halimwagiki tone la damu katika ardhi yake. Kwa sababu imeathirika na vita na vikaikosesha amani na raha.

Baada ya ishara hii, hebu tujiulize Je, Makusudio ya vita katika Aya ni kuhusu kuaana tu, au ni pamoja na kukosekana amani na raha? Kisha ikiwa makusudio ni mayahudi, kama walivyosema wafasiri, kutakuwa na majibu gani kuhusu vita vya 5 Juni 1967 vilivyowashwa na Mayahudi na ambavyo moto wake hauzimiki mpaka sasa?

Jibu : Neno Vita katika Aya makusudio yake ni kuuana. Kwa sababu neno hili wakati huo halikuwa na maana zaidi ya haya. Ama kuhusu vita vya 5th Juni, tunajibu kama ifuatavyo:

1. Wameafikiana wafasiri kuwa makusudio ya mayahudi ni kuwahusu mayahudi waliokuwa wakimfanyia vitimbi Mtume wa Mwenyezi Mungu na waislam. Katika vitabu vya sera imeelezwa kuwa mayahudi wa Madina waliungana na washirikina dhidi ya Mtume na Sahaba zake na kwamba wengine walikuwa wakiwasaidia maadui zao.

2. Lau tukichukulia kuwa makusudio ni mayahudi katika kila zama kwa kuchukua dhahiri ya ujumla, basi tukio la tarehe 5 Juni, halikuwa ni vita kwa maana yaliyo maarufu ya neno hili isipokuwa yalikuwa mauaji ya siri na usaliti wa woga. Kwani hata usiku huo huo Israil na Washington zilikuwa zikisisitiza kwamba hazikuanza mashambulizi, bali hata baada yake Israil ilitangaza kuwa Waarabu ndio walioanza vita.

Kisha baadaye uhakika ukadhihiri kwamba vita hivyo vya mwaka 1967 havikuwa baina ya waarabu na mayahudi isipokuwa vilikuwa hasa ni baina ya waarabu na waamerika. Amerika ndiyo iliyokuwa mhandisi, mwamrishaji na mtoaji silaha na mali. Vile vile ilikuwa ndio mpangaji wa udanganyifu na mlinzi, Israil ilitekeleza kazi ya askari mtiifu.

Mtungaji wa kitabu tulichokielezea punde hivi, anasema: "Magazeti ya Ufaransa na Ujerumani yalieleza kuwa majasusi wa kiamerika, kabla ya uchokozi kuanza, waliipa Israil habari zote muhimu, kuongezea faili maalum la Mashariki ya kati walilokuwa nalo viongozi wa Umoja wa NATO. Na kwamba aliyetoa amri kwa Israil kushambulia Waarabu kwa niaba ya Rais Johnson, ni mshauri wake myahudi. Na kamanda wa Kiamerika mfukoni mwake alikuwa na amri ya kutekeleza maandalizi ya vita katika sehemu zote zilizo chini yake. Ama meli ya ujasusi USS liberty, ilikuwa ikifanya kazi kwa ushirikiano wa Amerika na Israil.

3. Moto wa vita uliowashwa na Washington au kibaraka wake, Israil, ameuzima Mwenyezi Mungu bila ya shaka yoyote. Waliouwasha moto huo walikiri mara nyingi na kutangaza magazetini na kwenye idhaa kwamba haukutimiza lengo lililotakiwa - kumaliza uongozi wa kuwakomboa waarabu na kuwafanya wasalimu amri bila ya masharti yoyote, na hatimae kutatua matatizo ya Israil ya kisiasa.

Wakati huo huo tukio la mwaka 1967 lilikuwa ni mtihani mgumu kwa waarabu na kusisitiza dharura ya kutatua matatizo ya kimsingi. Vile vile kufahamu ni nani maadui zao na ni nani marafiki zao. Hata kama tukio hilo limeleta faida ya kufichuka vibaraka tu, inatosha.

Na wanajitahidi kuleta ufisadi katika ardhi.

Kwa sababu lengo lao la dhambi haliwezi kuthibitika ila kwa kuleta uharibifu na fitina. Wakuu katika Israil wamesema wazi kuwa kubakia kwa dola yao na uhai wake kumewekwa rahani na mizozo ya viongozi wa nchi za Kiarabu, 'Je yuko mwenye kukumbuka?'

Na Mwenyezi Mungu hawapendi wafisadi.

Hapo ndio mwisho wao - Maangamivu - hata kama muda utarefuka.

Na lau kwamba watu wa Kitab wangeliamini na wakamcha Mungu, tungeliwafutia makosa yao na kuwaingiza katika Bustani (pepo) zenye neema.

Huu ni mwito kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa Mayahudi na Wakristo kuwa watubie na waingie katika Uislam. Na kama wataitikia mwito wako atawafutia madhambi yao yote, hata yakiwa makubwa; Kwa sababu Uislamu unafuta yaliyokuwa kabla yake; kama ilivyoelewa katika Hadith: "Na wakimcha Mwenyezi Mungu baada ya kusilimu kwao, basi Mwenyezi Mungu atawaingiza katika bustani ambazo hupita chini yake mito."

RIZIKI NA UFISADI

Lau wangalisimamisha Tawrat na Injil na yale yaliyoteremshwa kwao kutoka kwa Mola wao, kwa hakika wangelikula vya juu yao na vya chini ya miguu yao.

Kuisimamisha Tawrat na Injil ni kufanya vitendo kulingana na vitabu hivyo. Makusudio ya yaliyoteremshwa kwao, ni mafunzo waliyokuwa wakiyasikia kutoka kwa Mitume, yanayojulikana kama Hadith za Mtume. Vilivyo juu yao, ni fumbo la riziki kubwa, sawa na unavyosema: Fulani amejawa na neema kuanzia utosini hadi unyayoni. Kuna Aya nyingi zilizo katika maana ya Aya hizi, kama hivi ifuatavyo:-

﴿وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَىٰ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم بَرَكَاتٍ مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ﴾

"Na lau watu wa miji wangaliamini na wakawa na takua, hakika tungaliwafungulia baraka kutoka mbinguni na ardhini" (7:96)

﴿إِنَّ اللَّـهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ﴾

"Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa kaumu mpaka wabadili wao yaliyomo katika nafsi zao" (13:11)

﴿ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ﴾

"Umedhihiri ufisadi barani na baharini kwa iliyoyachuma mikono ya watu" ( 30:41)

﴿ وَمَا أَصَابَكُم مِّن مُّصِيبَةٍ فَبِمَا كَسَبَتْ أَيْدِيكُمْ﴾

"Na misiba inayowasibu ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu" (42:30)

Aya zote hizi zinatuongoza kwenye mambo mawili:

Kwanza : kudhihiri ufisadi, ukiwemo umasikini maradhi na ujinga ni hukumu kutoka duniani na wala si hukumu ya mbinguni. Na ni kutokana na mikono ya watu walioiua haki na kuihuisha batili, na wala sio kutokana na kadha na kadari ya Mwenyezi Mungu. Na kwamba kundi lolote litakalojua haki na kuitumia litaishi kwa raha na wema.

Pili : Ibara ya kaumu na watu katika Aya hizo tukufu, inafahamisha kuwa uovu utakuwa katika hali yote kwa ujumla; na kwamba kuwa mwema mtu mmoja hakusaidii kitu maadamu wako watu wafisadi, bali wema wake utamwingiza kwenye balaa na Mashaka. Mwenyezi Mungu anasema:

﴿وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَّا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنكُمْ خَاصَّةً﴾

"Na iogopeni fitna ambayo haitawasibu waliodhulumu tu kati yenu (8:25)"

Yaani athari ya ufisadi na uovu katika jamii mbovu inaenea kwa wote wema na waovu. Hakuna mwenye shaka kwamba taifa vivu linalonyenyekea dhuluma, halina budi kuishi maisha ya udhalili na unyonge. Kwa hiyo basi makusudio ya imani inayoleta riziki ni kumwamini Mwenyezi Mungu pamoja na kutumia hukumu zake zote na misingi yake yote na wala sio kusimamisha Swala tu, bali na kutoa Zaka na kuwakomboa wanaokandamizwa na kusimamisha uadilifu katika kila kitu. Pia hakuna mwenye shaka kuwa uadilifu ukienea na ukawa juu, basi hali nayo itakuwa nzuri na umasikini na uovu utakwenda zake, Hili ndilo lengo la Qur'an.

Uislamu umegundua kuwa kuna mfungamano mkubwa baina ya ufisadi na maendeleo. Na Uislamu umemtangulia, katika kujua hakika hii, kila mtaalamu katika wataalamu wa elimu ya jamii ni kila kada katika makada wa ujamaa, wa kidemokrasia na wengineo.

Wote hawa wakiwa wana kitu cha kutaja, basi watakuwa wamechukua kutoka katika Uislamu, Lakini kuna hila gani kwa ambaye anakimbia kila linalolenga kwenye dini, kwa vile tu lina jina la dini?

Miongoni mwao wako watu walio sawa, na wengi wao wanayoyafanya ni mabaya.

Dhamiri ya katika wao inawarudia watu wa Kitab waliotajwa kwa uwazi katika Aya ambao ni mayahahudi na wakristo. Na ambao Mwenyezi Mungu ameiwasifu kuwa wako sawa ni wale waliokubali Uislamu katika mayahudi na wakristo, baada ya kuwadhihirikia wao dalili ya haki na ubainifu wa ukweli. Watu wa historia na sera wametaja majina mengi ya watu wa Kitab waliosilimu. Ama wale walioung'ang'ania ukafiri baada ya kuwabainikia wao haki, ndio waliokusudiwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na wengi wao wanayoyafanya ni mabaya"

9

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA SITA

﴿ يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴾

67.Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako; na kama hutafanya, basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu, Hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi watu makafiri.

FIKISHA ULIYOTEREMSHIWA

Aya 67

MAANA

Dhahiri ya Aya inafahamisha kuwa kulikuwa na jambo muhimu aliloteremshiwa Mtume(s.a.w.w) na kuamriwa kulifikisha kwa watu. Akawa anaona uzito kulifanya, kwa sababu ni zito katika nafsi zao. Akasitasita akingoja hali na minasaba maalum, kwa kuepuka migongano na wale wanaopindua mambo, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t) akamuhimiza kulifikisha wakati huo huo bila ya kufikiria lolote. Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) atamuhami na kumlinda na machukivu yote.

Unaweza kuuliza : kauli yake Mwenyezi Mungu "Na kama hutafanya basi hukufikisha ujumbe wake" haina faida yoyote, kwani jawabu lake ni hilo hilo swali. Ni kama kusema: Kama hukufanya basi hukufanya, Je, kuna wajihi gani?

Jibu : Kauli hii inafahamisha kuwa jambo hili ambalo Mtume anasitasita nalo, katika kulifikisha kwa kuhofia watu, limefikia umuhimu kuweza kulinganishwa na kufikisha ujumbe wote, kiasi ambacho, akiacha kulifikisha basi ni kama ameacha kufikisha ujumbe wote; sawa na unavyomwambia mtu aliyekufanyia hisani kama hutafanya hivi, basi hujanifanyia hisani kabisa.

Kwa hiyo maana yake ni kuwa kama hukufikisha jambo hili, basi ni kama hukutekeleza chochote katika risala yangu, na malipo yake ni malipo ya aliyeficha hukumu zake zote.

Swali la pili : Je, ni jambo gani hilo lililofikia kiwango hiki mpaka Mwenyezi Mungu akalipima na risala yote katika kulifikisha kwake, na likamfanya Mtume asitesite kulifikisha na hali yeye ni mwenye kupupia kudhihirisha aliloamrishwa kwa vyovyote iwavyo?

Jibu : Baada ya kuafikiana wafasiri wa Kishia na Kisunni kuhusu tafsir ya Aya hii kwa maana tuliyoyataja wamehitalifiana katika kulielezea jambo hilo lililomfanya Mtume(s.a.w.w) kusitasita kulifikisha na ambalo Mwenyezi Mungu hakulitaja kwa uwazi.

Shia wanasema kuwa Aya hii ilishuka kwa Ali bin Abu Talib na jambo lenyewe lilikuwa ni utawala wake kwa watu, na kwamba Mtume alisitasita katika kulifikisha si kwa kuhofia nafsi yake, hapana si hivyo! Yeye alivikabili vigogo vya Kiquraish na ukubwa wao akawatukana miungu yao na kuwaabisha wafu wao na hali wao wana nguvu na hadhi za kijahiliya.

Aliyafanya yote haya Mtume na hakuogopa lawama ya mwenye kulaumu hata siku moja.

Itakuwaje aogope kufikisha hukumu yoyote miongoni mwa hukumu baada ya kuwa Uislamu una ngome kubwa ya jeshi lenye nguvu? Isipokuwa Mtume(s.a.w.w) alihofia kumuelezea Ali kuwa Khalifa, kutuhumiwa kuwa na upendeleo kwa kuwa ni mkwewe na binamu yake, na kwamba makafiri na wanafiki wanaweza kulifanya hili ni jambo la kueneza propaganda dhidi ya Mtume(s.a.w.w) na kuingiza shaka katika Utume wake na isma yake. Na ilivyo hasa ni kuwa propaganda kama hii wanaikubali wenye akili hafifu na wajinga.

Kwa muhtasari, haya ndiyo waliyoyasema Shia na kuyatolea dalili kwa hadith zilizopokelewa kutoka hata kwa Sunni. Wamezinukuu baadhi, Razi na mwenye Tafsir Al-manar

Ama Sunni, wametofautiana; kuna wenye kusema kuwa Mtume alinyamazia baadhi ya hukumu zinazohusiana na Mayahudi, wengine wakasema kuwa hukumu aliyoinyamazia Mtume inaambatana na kisa cha Zaid na Zainab bint Jahsh.

Kundi kubwa katika Sunni wamesema kuwa Aya ilishuka katika ubora wa Ali bin Abu Talib na si katika ukhalifa wake. Na kauli hii alinukuu Razi na mwenye Tafsir Al- Manar.

Anasema Razi: " Ya kumi- yaani kauli ya kumi- ni kuwa Aya imeshuka kuhusu ubora wa Ali bin Abu Talib. Iliposhuka Aya hii Mtume aliushika mkono wa Ali na akasema: "Ambaye mimi ni bwana wake basi Ali ni bwana wake. Ewe Mwenyezi Mungu mpende mwenye kumpenda na muhasimu mwenye kumhasimu" Umar akamkabili na kusema: "Pongezi Ewe bin Abu Talib, umekuwa bwana wangu na bwana wa kila mumin mwanamume na mwanamke." Hiyo ni kauli ya Ibn Abbas, Barrau bin Azib na Muhammad bin Ali".

MWENYE AL-MANAR NAAHLUBAYT

Amesema mwenye Tafsir Al-Manar: "Ama Hadith isemayo: Ambaye mimi ni bwana wake basi Ali ni bwana wake, ameipokea Ahmad katika Musnadi yake. Vilevile Tirmidh, Nasai, Dhiyai katika Mukhtar na Ibn Maja na baadhi yao wameifanya ni Hasan; na Dhahabi akaifanya Sahih kwa tamko hili na akaitilia nguvu Isnad ya mwenye kuzidishia: "Ewe Mwenyezi Mungu mpende mwenye kumpenda na mhasimu mwenye kumhasimu."

Kuna Riwaya nyingine isemayo kuwa yeye Mtume aliwahutubia watu, akataja misingi ya dini, akawausia Ahlu bayt wake na akasema: "Mimi ninawachia vizito viwili: Kitab cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlubayt wangu, basi angalieni vile mtakavyonifuata nyuma yangu katika viwili hivi, kwani havitaachana mpaka vinijie katika birika (siku ya kiyama). Mwenyezi Mungu ni Bwana wangu na mimi ni Bwana wa kila mumin.

Kisha akashika mkono wa Ali na akasema maneno hayo: yaani; ambaye mimi ni bwana wake basi Ali ni bwana wake". Kisha mwenye Al-Manar akaendelea kurefusha maneno akasema katika aliyeyasema: " Makusudio ya Wilaya katika Hadith ni kumsaidia na kumpenda". Lakini tafsir yake hii alifuatishia na kauli hii. "Mfano wa mjadala huu umetofautisha baina ya waislam na kuwaingizia uadui na chuki, maadamu ubaguzi na madhehebu una nguvu kwa watu basi hakuna matumaini ya kuitofanyia utafiti haki katika masuala ya ukhalifa."

Haya ni sahihi anayakubali kila mwenye akili, Lau si kung'ang'ania batili isingelitokea tofauti baina ya Waislamu, wala yasingeliandikwa marundo ya vitabu katika suala moja. Mwenye Tafsir Al-Manar anaendelea kusema: "Ama Hadith ya ambaye mimi ni bwana wake basi Ali ni bwana wake, sisi tunaifuata na tunampemda Ali Al-Murtadha, tunampenda amependaye na tunamchukia amchukiaye. Hilo tunalihisabu kama kumpenda Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) na tunaamini kuwa kizazi chake Mtume(s.a.w.w) hakitafarikiana na Kitab ambacho Mwenyezi Mungu amemteremeshia Mtume wake(s.a.w.w) , na kwamba Kitab na kizazi cha Mtume ni Makhalifa wawili wa Mtume. Hadith imekua sahihi kwa hilo katika matukio mengine yasiyokuwa kisa cha Ghadir. Kwa hiyo wakikubaliana katika jambo fulani tunalikubali na kulifuata na wakitofautiana katika jambo basi tutalirudisha kwa Mwenyezi Mungu na Mtume."

﴿قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَسْتُمْ عَلَىٰ شَيْءٍ حَتَّىٰ تُقِيمُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم مَّا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَانًا وَكُفْرًا فَلَا تَأْسَ عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴾

68.Sema: "Enyi watu wa Kitab! Hamna chochote, mpaka muisimamishe Tawrat na Injil na yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu. Kwa hakika yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako yatawazidisha wengi katika wao uasi na ukafiri, Basi usiwasikitikie watu makafiri.

﴿إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالصَّابِئُونَ وَالنَّصَارَىٰ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴾

69.Hakika wale walioamini na wale walio mayahudi na wasabai na wanaswara, watakao mwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na wakafanya amali njema, basi wao hawatakuwa na hofu wala hawatahuzunika.

KUSIMAMISHA TAURAT NA INJIL

Aya 68 - 69

MAANA

Sema: Enyi Watu wa Kitab! Hamna chochote.

Wala hayatawafaa mambo ya dhahiri haya ya kidini mpaka muisimamishe Tawrat na InjilImekwisha tangulia tafsiri ya Aya hii katika Sura hii Aya 64.

Hakika wale walioamini na wale walio mayahudi na wanaswara na wasabai.

Pia imetangulia tafsir yake katika (2:62)

﴿ لَقَدْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَأَرْسَلْنَا إِلَيْهِمْ رُسُلًا كُلَّمَا جَاءَهُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُهُمْ فَرِيقًا كَذَّبُوا وَفَرِيقًا يَقْتُلُونَ﴾

70.Hakika tulifanya agano na Wana wa Israil na tukawapelekea Mitume. Kila alipowafikia Mtume kwa yale zisiyoyapenda nafsi zao kundi moja wakalikadhibisha na kundi jengine wakaliua.

﴿وَحَسِبُوا أَلَّا تَكُونَ فِتْنَةٌ فَعَمُوا وَصَمُّوا ثُمَّ تَابَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ثُمَّ عَمُوا وَصَمُّوا كَثِيرٌ مِّنْهُمْ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ﴾

71.Na walidhani kwamba haitatokea fitna, basi wakawa vipofu na viziwi. Kisha Mwenyezi Mungu akawatakabalia toba, kisha tena wengi katika wao wakawa vipofu na viziwi; na Mwenyezi Mungu anayaona wanayoyatenda.

AGANO LAWANAWA ISRAIL

MAANA

Hakika tulifanya agano na Wana wa Israil.

Imekwishatangulia tafsir yake katika Sura hii hii Aya 12 na 13. Wafasiri wamesema kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amekariri kufanya agano na Mayahudi na kuvunja kwao ahadi na maagano kwa kuwaua Mitume, kwa kusititiza ujeuri na uasi wao. Nasi tunaongeza kwa kusema kuwa vilevile Mwenyezi Mungu Mtukufu amekusudia kwa kukaririka huku - Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi - kuvihadharisha vizazi vya kiislam, kutokana na vizazi vya kiyahudi. Ambapo alikwishajua kuwa Waislamu watatawanyika kwenye makundi na vijidola, na kwamba Mayahudi watautumia mgawanyiko huu kwa kuanzisha dola ndani ya miji ya kiislam, na kuwa kama ilivyokuwa.

Na tukawapelekea Mitume wawabainishie haki na uongozi, lakini kila walipowajia Mitume kwa yale zisiyoyapenda nafsi zao, kundi moja wakaliadhibisha na kundi jengine wakaliua.

Mapenzi ya nafsi tu, ndiyo mwamrishaji na mkatazaji kwa mayahudi. Wala hakuna malipo kwa atakayewahalifu, hata akiwa ni Mtume, ila kumuua wakiweza au kumkadhibisha wakishindwa kuua. Sifa hizi hawahusiki nazo mayahudi tu, ingawaje maneno ni yao. Kila mwenye kuhadaika na mapenzi yake anafanya kama walivyofanya; awe myahudi, Mwislamu au Mkiristo.

Na walidhani kwamba haitatokea fitna.

Makusudio ya fitna hapa ni shida, kama vile kukandamizwa na waliokuwa na nguvu zaidi kwa kuuliwa na kufukuzwa. Yaani walidhani Mayahudi kuwa wao hawatashindwa kabisa, kwa vile wao ni taifa la Mwenyezi Mungu lililoteuliwa kama wanavyodai. Zamani walitegemea madai yao haya, lakini hivi sasa wanategemea nguvu za wakoloni, hali ya ujinga wa watu, mashirika ya ulanguzi na kueneza fitina, ufisadi na kuwatofautisha watu.

Basi wakawa vipofu na viziwi.

Kila mwenye kuchukia jambo anakuwa kipofu wa mazuri yake. Mayahudi walichukia kila jambo isipokuwa linalopendeza nafsi zao, Kwa hiyo wamekuwa vipofu wa njia ya haki na kuwa viziwi wa sauti ya uadilifu. Ndipo Mwenyezi Mungu akawasalitia babilon, wakawaua wanaume wao na kunyang'anya mali zao na kuwateka wanawake wao na watoto wao.

Kisha Mwenyezi Mungu akawatakabalia toba.

Baada ya kutubia kutokana na shida waliyoipata kutoka kwa Nebukadnezza ya kudhalilishwa na kudharauliwa.

Kisha tena wengi katika wao wakawa vipofu na viziwi.

Yaani baada ya Mwenyezi Mungu kuwaokoa na adhabu ya kutekwa, wengi wao walirudia ufisadi na dhulma. Wakamuwa Zakariya na Yahya; wakamkadhibisha Masih na kujaribu kumuua na wakasema kuhusu yeye na mama yake mambo makubwa. Ndipo Mwenyezi Mungu akawasalitia

Wafursi na Waroma, wakawafanya kama walivyofanywa na Nebukadnezza.

Na Mwenyezi Mungu anayaona wanayoyatenda.

Ya kumwaga damu, kuipotosha, haki, kupanga njama na kutekekeleza kila njia na inayopangwa na taghuti na dhalimu, Mwenyezi Mungu (s.w.t) anayajua yote naye atawalipa udhalili hapa duniani kabla ya akhera. Sifa zote hizi alizozielezea Mwenyezi Mungu kuhusu mayahudi zinalingana sawa kabisa na mwenye kudhihirisha Uislamu kisha anazunguka kwa wale wanaoiunga mkono Israil na kuwasaidia.

﴿لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴾

72.Kwa hakika wamekufuru wale waliosema Mwenyezi Mungu ni Masih mwana wa Maryam. Na Masih alisema: Enyi wana wa Israil! Mwabuduni Mwenyezi Mungu Mola Wangu na Mola wenu: kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu amemharamishia pepo na makazi yake ni motoni. Na madhalimu hawatakuwa na wakuwanusuru.

﴿لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴾

73.Kwa hakika wamekufuru wale waliosema, Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa utatu. Hakuna Mungu ila Mungu Mmoja. Na kama hawataacha hayo wayasemayo, kwa hakika itawapata, wale waliokufuru miongoni mwao, adhabu iumizayo.

﴿أَفَلَا يَتُوبُونَ إِلَى اللَّـهِ وَيَسْتَغْفِرُونَهُ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴾

74. Je, hawatubu kwa Mwenyezi Mungu na kumwomba maghufira? Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghufira mwenye kurehemu.

﴿مَّا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ كَانَا يَأْكُلَانِ الطَّعَامَ انظُرْ كَيْفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ الْآيَاتِ ثُمَّ انظُرْ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴾

75.Masih mwana wa Maryam hakuwa ila ni Mtume, Wamepita kabla yake Mitume. Na mama yake ni mkweli, Wote wawili walikuwa wakila chakula, Angalia jinsi tunavyowabainishia ishara, kisha angalia jinsi wanavyogeuzwa.

MWITO WA MASIH KWAWANAWA ISRAIL

Aya 72 - 75

MAANA

Kwa hakika wamekufuru wale waliosema: Mwenyezi Mungu ni Masih mwana wa Maryam.

Mayahudi walipita kiasi kumdharau Masih na mama yake na wakristo nao wakapita kiasi katika kumsifu, mpaka wakampandisha kwenye cheo cha uungu. Kupita kiasi, katika mtazamo wa Uislam, ni ukafiri kwa aina zake zote. Imam Ali(a.s) anasema:"Watu wawili wataaangamia kwa ajili yangu: Mwenye kunipenda kupita kiasi, pendo likampelekea kusiko na haki, na mwenye kunichukia kupita kiasi, chuki ikampelekea kusiko haki. Mbora wa watu kuhusu mimi ni yule mwenye hali ya katikati, basi shikamaneni naye".

Na Masih alisema: Enyi wana wa Israil, mwabuduni Mwenyezi Mungu Mola Wangu na Mola Wenu; kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu amemharamishia pepo na makazi yake ni motoni. Na madhalimu hawatakuwa na wa kuwanusuru.

Masih ni katika Wana wa Israil na aliowaonya kwanza ni jamaa zake. Akawaaamrisha kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, akikiri kuwa yeye ni Mola wake na Mola wao, na kuwaonya wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu kuwa watapata adhabu kali, lakini Wakristo wamekataa hayo, isipokuwa Isa ni Mwenyezi Mungu tu, na mwenye kupinga hayo, basi amempinga muumbaji wa ulimwengu, katika itikadi yao.

Kwa hakika wamekufuru wale waliosema Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa utatu.

Kwanza Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewakanushia Manasara uungu wa Bwana Masih, kisha katika Aya hii amewakanushia kumfanya kwao Mwenyezi Mungu ni mmoja kati ya watatu.

Kwa kusema kwao kuwa Mwenyezi Mungu ni baba na Masih ni Mwana, kisha baba na Mwana wakachanganyika na kuungana akawa roho mtakatifu. Kila mmoja kati ya hawa watatu ni mwingine na huyo mwengine ni yeye. Yametangulia maelezo ya hilo katika tafisir ya (4:170) na tafsir ya Aya 17 ya Sura hii tuliyo nayo.

Hakuna mungu ila Mungu Mmoja.

Imam Ali aliulizwa kuhusu Tawhid na Uadilifu wa Mungu, akasema: "Tawhid ni kutomuwazia, na uadilifu ni kutomtuhumu." Yaani kumpwekesha Mwenyezi Mungu ni kutomfanyia picha yoyote katika mawazo yako kwa sababu kila linalowaziwa lina mpaka na Mwenyezi Mungu hawezi kuwekewa mpaka na mawazo. Na uadilifu ni kutomtuhumu Mwenyezi Mungu kwa hekima yake kwamba yeye amefanya lisilotakiwa kufanywa.

Na kama hawataacha hayo wayasemayo, kwa hakika itawapata, wale walio kufuru miongoni mwao, adhabu iumizayo.

Unaweza kuuliza kuwa : katika Aya neno 'miongoni mwao' kwa dhahiri linafahamisha kwa miongoni mwao wako makafiri na waumini; na inajulikana kuwa wote wanasema uungu wa Isa, na Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: "Hakika wamekufuru wale waliosema: Mwenyezi Mungu ni Masih mwana wa Maryam?"

Wafasiri wamejibu kuwa : neno 'miongoni mwao' linawatoa waliotubia na kusilimu na kuwabakisha wanaoendelea na ukafiri. Lakini ilivyo ni kuwa mwenye kusilimu hawezi kuhisabiwa kuwa ni miongoni mwao. Ilivyo ni kuwa Wakristo walikuwa na itikadi ya Tawhid (Umoja wa Mungu) kwa muda mrefu, kisha wakagawanyika makundi mawili: Lile linaloamini Tawhid na jingine linaloamini idadi ya waungu. Wakaendelea hivyo, kisha wakaafikiana wote na neno la utatu. Kwa hiyo, basi neno miongoni mwao linatoa kundi lile lililoamini Utume wa Isa na sio Ungu wake. Yametangulia maelezo kwa ufafanuzi katika kufasiri Aya 17 ya Sura hii.

Je, hawatubu kwa Mwenyezi Mungu na kumwomba maghufira? Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghufira mwenye kurehemu?

Maneno yako wazi kabisa, lakini pamoja na uwazi wote huo baadhi ya wafasiri wamekataa ila kufafanua tu, na kusema kuwa hapa kuna maneno yaliyokadiriwa, kuwa hawasikii tunayowaambia wakatubia, Hivi ndivyo kinavyokuwa kitu baridi kilichoganda kikiwa mahali pasipokuwa kwake.

Masih mwana wa Maryam hakuwa ila ni Mtume, Wamepita kabla yake Mitume.

Kama vile Nuh, Ibrahim, Musa na wengineo. Mwenyezi Mungu alidhihirisha miujiza mikononi mwao, kama alivyoidhihirisha mikononi mwa Isa. Kwa hiyo kauli ya Uungu wake haina nguvu yoyote. Na mama yake ni mkweli. Mwenyezi Mungu ameibaini maana ya kuwa mkweli aliposema:

﴿وَصَدَّقَتْ بِكَلِمَاتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِ وَكَانَتْ مِنَ الْقَانِتِينَ﴾

"Na akayasadikisha maneno ya Mola wake, na vitabu vyake, na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu" (66:12)

Wote wawili walikuwa wakila chakula.

Kila mwenye kuhitajia kitu chochote, ijapokuwa ni mahali, au wakati, basi huyo ni kiumbe aliyeumbwa. Kwa sababu anahitajia kwa hali yoyote, vinginevyo itakuwa ni muumbaji asiyeumbwa; kama ambavyo kujitosheleza ni sifa inayolazimiwa na Muumbaji na wala haepukani nayo, vinginevyo atakuwa ameumbwa.

Ilivyo ni kuwa anayekula chakula huwa ni muhitaji sana, kwa hiyo huyo ni kiumbe na wala siye muumba. Ni jambo la kushangaza kufichika uwazi huu kwa mwenye akili. Na kwa mantiki haya na ufasaha wake, anaufuatishia msimamo wao huo kwa kauli yake:Angalia jinsi tunayvowabainishia ishara.

Na miongoni mwa ishara hizo ni kwamba Masih na mama yake walikuwa wakila chakula, basi vipi watakuwa waungu? Kisha Angalia jinsi wavavyogeuzwa, yaani kuicha haki na kuikadhibisha kwao.

﴿قُلْ أَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا وَاللَّـهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴾

76.Sema: Je, mnamwabudu badala ya Mwenyezi Mungu, ambaye hawezi kuwadhuru wala kuwanufaisha? Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia, mwenye kujua.

﴿قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ غَيْرَ الْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعُوا أَهْوَاءَ قَوْمٍ قَدْ ضَلُّوا مِن قَبْلُ وَأَضَلُّوا كَثِيرًا وَضَلُّوا عَن سَوَاءِ السَّبِيلِ﴾

77.Sema: "Enyi watu wa Kitab! Msipite kiasi katika dini yenu bila haki, wala msifuate matamanio ya watu waliokwishapotea tangu zamani; na wakawapoteza wengi, na wenyewe wakapotea njia iliyo sawa.

﴿لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ﴾

78.Walilaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israil kwa ulimi wa Daud na wa Isa mwana wa Maryam. Hayo ni kwa sababu waliasi, nao walikuwa wakiruka mipaka.

﴿كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ﴾

79.Walikuwa hawakatazani mambo mabaya waliyokuwa wakiyafanya. Hakika ni maovu waliyokuwa wakiyafanya.

﴿تَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يَتَوَلَّوْنَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَبِئْسَ مَا قَدَّمَتْ لَهُمْ أَنفُسُهُمْ أَن سَخِطَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ وَفِي الْعَذَابِ هُمْ خَالِدُونَ﴾

80.Utawaona wengi katika wao wanawafanya marafiki wale waliokufuru. Kwa hakika ni mabaya waliyotanguliziwa na nafsi zao; ya kwamba Mwenyezi Mungu amewakasirikia na watadumu katika adhabu.

﴿وَلَوْ كَانُوا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالنَّبِيِّ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مَا اتَّخَذُوهُمْ أَوْلِيَاءَ وَلَـٰكِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ﴾

81.Na lau wangelikuwa wanamwamini Mwenyezi Mungu na Nabii na yale yaliyoteremshwa kwake wasingeliwafanya hao kuwa marafiki. Lakini wengi katika wao ni mafasiki.

HAWAWEZI KUWADHURU WALA KUWANUFAISHA

Aya 76 - 81

NAHW

Qur'an hutumia herufi Ma katika kisichokuwa na akili na kilicho na akili na katika vyote viwili. Hata hivyo matumizi ya herufi Ma katika visivyo na akili ni zaidi.

MAANA

Sema Je, mnamwabudu badala ya Mwenyezi Mungu, ambaye hawezi kuwadhuru wala kuwanufaisha? Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia mwenye kujua?

Hoja juu ya Wakristo katika Aya hii ni kwamba Mwenyezi Mungu mwenye kuabudiwa ni yule anayeweza kuwadhuru waja wake au kuwanufaisha.

Ama anayeshindwa na hayo, basi ni muhali kuwa Mungu. Injili zimetaja kuwa Isa, wanayedai kuwa ni Mungu, alidharauliwa, akasulubiwa na kuzikwa baada ya kuvishwa kilemba cha miba kichwani mwake, Ambaye hawezi kujikinga yeye mwenyewe basi ataweza wapi kumkinga mwingine? Basi ambaye yuko hivyo, hawezi kuabudiwa na mwenye akili. Ibrahim alimwambia baba yake:

﴿يَا أَبَتِ لِمَ تَعْبُدُ مَا لَا يَسْمَعُ وَلَا يُبْصِرُ وَلَا يُغْنِي عَنكَ شَيْئًا﴾

"Ewe baba yangu! Kwa nini unaabudu kisichosikia na kisichoona na kisichokufaa chochote" (19:42)

Bedui mmoja alikuwa na sanamu lake analoliabudu na kulitukuza. Siku moja alikwenda kulisujudia kama kawaida yake, Akaona kicheche karibu naye, Akadhani kuwa kicheche kimekuja kutabaruku.

Alipotaka kusujudia akaona kinyesi cha kicheche kwenye kichwa cha sanamu, akapata akili akalivunja sanamu huku akisema: "Kicheche kinamkojolea Mungu kichwani, akojolewaye na vicheche amekua duni."

Sema Enyi watu wa Kitab! Msipite kiasi katika dini yenu bila haki.

Msemo huu kwa dhahiri unaelekezwa kwa watu wa Kitab na kwa undani hasa unawakusanya watu wa dini zote. Upambanuzi asili wa Uislamu ni kwamba unayaweka madhara na manufaa mikononi mwa Mwenyezi Mungu peke yake, na unamweka binadamu mbele ya muumba wake bila ya kuweko mwingiliaji kati wa kiroho au wa kimaada. Mwenyezi Mungu anasema:

﴿مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ وَلَا يَجِدْ لَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا﴾

"Mwenye kutenda uovu atalipwa kwa uovu huo, Wala hatajipatia mlinzi wala msaidizi zaidi ya Mwenyezi Mungu" (4:123)

Wala msifuate matamanio ya watu waliokwishapotea tangu zamani; na wakawapoteza wengi, na wenyewe wakapotea njia iliyo sawa. Makusudio ya watu ni viongozi wa dini ambao wanaifanyia biashara na kuipotoa vile wanavyo taka.

Kwanza : Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasifu kuwa wao wenyewe ni wapotevu.

Pili : ni wapotezaji. Kisha akabainisha aina ya kupotea na upotevu kwamba ni kupotea kufuata njia iliyo sawa. Njia iliyo sawa ni kuwa katikati na kuacha kupita kiasi katika dini. Huu ndio Uislamu hasa, dini ya sawa sawa na njia iliyonyooka. Ili Waislam wasiseme kuhusu Muhammad(s.a.w.w) , kama walivyosema wakristo kuhusu Masih(a.s) , Mwenyezi Mungu alimwaamrisha Mtume wake awaambie waumini:

﴿قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا ﴾

"Sema hakika mimi ni mtu kama nyinyi tu. Ninaletewa Wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu mmoja. Basi anayetarajia kukutana na Mola wake na afanye matendo mema, wala asimshirikishe yoyote katika ibada ya Mola wake." (18:110)

Mtu mmoja aliingia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, akawa anatetemeka kutokana na haiba ya Mtume. Mtume akampigapiga mabegani kwa upole na kumwambia: "Poa, Mimi ni mtoto wa mwanamke ambaye alikuwa akila mtanda huko Makka."

Walilaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana Waisrail kwa ulimi wa Daud na wa Isa mwana wa Maryam.

Wafasiri wanasema kuwa Daud aliwakataza Wana wa Israil kuvua samaki siku ya Jumamosi (Sabato), kwa wahyi wa Mwenyezi Mungu. Walipoasi amri yake aliwaalani na kuwaapiza wakawa manyani. Ama Isa alitakiwa na watu elfu tano (5000) awateremshie meza ya chakula kutoka mbinguni, wale, ndipo wamwamini. Walipoteremshiwa wakala na wasimwamini. Isa akasema:"Ewe Mwenyezi Mungu walaani kama ulivyowalaani watu wa Sabato (Jumamosi)," Lakini katika Aya hakuna kitu kinachoashiria ufafanuzi huu.

Maana yaliyo dhahiri ni kuwa Daud na Isa waliwalaani waliokufuru katika Wana wa Israil Hayo ni kwa sababu waliasi na wakapituka mipaka. Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) alinyamaza kueleza aina ya uasi na upitukaji mipaka, sio kwa ujinga au kusahau.

Nasi tunayanyamazia yale aliyoyanyamazia Mwenyezi Mungu. Wakati huo huo tukiamini kuwa laana ya Mwenyezi Mungu na nakama yake inamshukia kila mwenye kupetuka mpaka na kila anayemwasi, awe Mwisrail au kutoka uko wa Hashim.

Walikuwa hawakatazani mambo mabaya waliyokuwa wakiyafanya, Hakika ni maovu waliyokuwa wakiyafanya.

Aya hii inafahamisha kwamba mambo mabaya hayakuwa kwa watu fulani katika jamii ya Mayahudi, isipokuwa ilikuwa ni kazi ya watu wote na kwamba mambo maovu yalienea kwao mpaka yakawa ni mambo ya kawaida yaliyozoeleka kwa wakubwa na wadogo. Kwa hiyo hakupatikana miongoni mwao anayekataza mabaya na kuyapinga.

Katika Sahih Muslim na Bukhari kuna Hadith inayosema kuwa Mtume alisema:"Mtawafuata waliokuwa kabla yenu vile vile wafanyavyo, hata wakiingia tundu ya kenge nanyi mtaingia" . Wakasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni mayahudi na wakristo?" Akasema: "Kumbe, ni nani tena."

Utawaona wengi katika wao wanawafanya marafiki na wale waliokufuru.

Dhamir ya katika wao inawarudia mayahudi, na ya wale waliokufuru hapa, ni washirikina wa kiarabu. Wengi katika mayahudi walikuwa marafiki pamoja na washirikina dhidi ya Mtume(s.a.w.w) na kuwachochea. Bali walikuwa ni maadui wakubwa wa Mtume, ingawaje Mtume alikuwa aki- aamini Mwenyezi Mungu na Utume wa Musa(a.s) na yale aliyoteremshiwa; na washirikina ni waabudu masanamu wasioamini Musa wala Kitabu chochote miongoni mwa Vitab vya Mwenyezi Mungu. Usawa kwa Mayahudi ni kuwa pamoja na waumini dhidi ya waabudu masanamu sio pamoja na waabudu masanamu dhidi ya waumini.

Lakini Mayahudi walikuwa na bado wako kwenye msingi ya faida na biashara, sio kwenye misingi ya dini. Mayahudi wa Madina walikuwa wanatawala biashara ya ndani na washirikina wa kiarabu walikuwa wakitawala biashara ya nje.

Mtume akafanya kazi ya ukombozi ya tawala hizo mbili, Hapo mayahudi na washirikina wakaungana na kuwa na mshikamano mmoja dhidi ya Waislamu; sawa na ilivyo leo walivyoungana mayahudi na wenye mashirika ya unyonyaji miongoni mwa wakiristo dhidi ya wazalendo na wanyonge, Yametangulia maelezo katika Sura hii Aya 51.

Kwa hakika ni mabaya waliyotanguliziwa na nafsi zao; ya kwamba Mwenyezi Mungu amewakasirikia, na watadumu katika adhabu.

Hii ni natija ya ufisadi wao na uadui wao. Na kila mtu atalipwa kutokana na aliyoyafanya awe Mwislamu au mshirikina.

Na lau wangelikuwa wanamwamini Mwenyezi Mungu na Nabii na yaliyoteremshwa kwake wasingeliwafanya hao kuwa marafiki.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja katika Aya iliyotangulia kwamba mayahudi au wengi wao walikuwa wakifanya urafiki na washirikina, kisha akabainisha Mwenyezi Mungu (s.w.t), katika Aya hii kwamba hao mayahudi hawakumwamini Mwenyezi Mungu wala Musa wala yaliyoteremshwa katika Tawrat kama wanavyodai. Lau wangelikuwa wakweli katika madai yao, wasingeliwafanya washirikina kuwa marafiki badala ya Waislamu. Kwa sababu hilo ni haramu katika sharia ya Tawrat.

Lakini wengi katika wao ni mafasiki.

Kwamba maswala kwao sio maswala ya dini na itikadi, isipokuwa ni maswala ya masilahi na manufaa; kama tulivyotangulia kueleza.

MWISHO WA JUZUU YA TANO

12

SHARTI YA KUCHAPA

au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

1