MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE 0%

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE Mwandishi:
: SALMANI SHOU
Kundi: Misingi mikuu ya Dini

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

Mwandishi: KIMEANDIKWA NA SAYYID MUJTABAA MUUSAWIY LARI
: SALMANI SHOU
Kundi:

Matembeleo: 27498
Pakua: 2657

Maelezo zaidi:

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 28 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 27498 / Pakua: 2657
Kiwango Kiwango Kiwango
MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

Mwandishi:
Swahili

4

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

SOMO LA NNE

KUAMINI UKWELI WA KISICHOONEKANA KUNAHUSISHA MENGI ZAIDI YA MWENYEZI MUNGU

Sifa moja wapo ya Mwenyezi Mungu wa pekee kwa elimu na ibada ya Ambaye Mitume na viongozi wa kidini wanatuitia ni kwamba Yeye hafikiwi kabisa na hisia za utambuzi. Kwa nyongeza, Anazo sifa za kutokuwa na mwanzo au mwisho. Wa kuwepo kila mahali, Ha. Katika dunia yote ya maumbile na uhai wa kihisia ishara Zake zina madhubuni ya kuwepo kwake na matakwa Yake yanaonekana kila mahali katika dunia hii iliyo uhai, mambo yote ya maumbile vikitangaza uwezo wa ile Dhati yenye hekima.

Kwa kweli, dhati kama hiyo ambayo binadamu hawezi kuitambua kwa milango yake ya fahamu, ambayo kwa vyovyote vile haikupambwa kwa rangi za kimaada, na ambayo hailingani na uzoefu na mawazo yetu ya kawaida, ni vigumu sana sisi kuidhania. Pindi inapokuwa vigumu kudhania kuwepo kwa kitu, inakuwa rahisi kukataa (kuwepo kwake). Watu wanaotaka kutatua suala la kuwepo kwa Mwenyezi Mungu kwa kutumia muundo wa mipaka yao wenyewe ya ki-akili na ufinyu wa mawazo huwa wanahoji inawezekana vipi kuamini kitu kisichoonekana.

Wanashindwa kuzingatia ukweli kwamba utambuzi wa fahamu, ambayo imewekewa mipaka, inaweza kumsaidia mwanadamu kujua na kutambua muundo mmoja tu wa asili; haiwezi kugundua miundo mingine ya asili na kupenya ukubwa wote wa maumbile. Viungo vya fahamu havituruhusu kuendelea hatua moja mbele kuvuka ng'ambo ya vipengele vya nje ya tukio, kwa namna ile ile tu ambayo sayansi za majaribio haziwezi kubeba fikra ya mwanadamu kuvuka mipaka ya hisia za kiwango cha juu zaidi.

Endapo mwanadamu, kwa kupitia nyenzo na vigezo vya kisayansi, hawezi kutambua kuwepo kwa kitu, hawezi kukanusha kuwepo kwa kitu hicho kwa sababu tu hakiendani na vigezo vya kilimwengu, isipokuwa labda atupe baadhi ya ushahidi kwamba hicho kitu husika hakiwezekani. Tunagundua kuwepo kwa kanuni ya busara kutoka ndani ya utimilifu wa tukio kwamba ina uwezo wa kutafsiri. Endapo, basi, kusimama kwa hoja ya ukweli wa kisayansi kunawezekana tu kwa njia ya hisia za moja kwa moja, itakuwa hapana budi kuacha ukweli mwingi wa kisayansi, kwani mambo mengi ya kisayansi hayawezi kutambulika kwa njia ya uzoefu wa kihisia au kufanya vipimo.

Kwa kadiri ambavyo uhakika wa dunia ya kimaada uhusikanavyo, hakuna mtu mwenye busara ambaye atachukulia kikawaida kutokukiona au kutokigusa kwake kitu maalum katika maisha yake ya kila siku kuwa sababu ya kutosha kukikataa. Hataweza kuhukumu kwamba hakipo, kitu chochote kinachoshindwa kuingia kwenye upeo wa utambuzi wake wa hisia. Vivyo hivyo hili litasisitiza ukweli wenye nguvu zaidi wa vitu visivyo vya ki-maada.

Tunapokuwa kuhakikisha sababu ya jambo katika majaribio ya kisayansi, hali hii haituelekezi kukanusha kanuni ya usababishaji. Sisi tutasema tu kwamba sababu hatuijui kwa sababu kanuni hiyo inajitegemea juu ya jaribio maalum tu; hakuna jaribio linaloweza kukanusha kuwepo kwa asili. Je, sio kweli kwamba vitu vyote tunavyokubali na kuamini kwamba vipo, vina uwepo wake wenye uhusiano wa jinsi ile ile kama ya kwetu au kama ya vitu vile tunavyoviona kwa macho? Je, tunaweza kuona au kuhisi kila kitu katika dunia hii maumbile? Hivi ni Mwenyezi Mungu tu ndiye ambaye hatuwezi kumwona kwa fahamu zetu? Wayakinifu (wa ki-maada) wote wanatambua kwamba vitu vingi tunavyovijua vinakuwa na maada na uhalisia ambao hatuwezi kuhisi na kidesturi hatuvijui. Vipo viumbe visivyoonekana vingi tu hapa ulimwenguni.

Maendeleo ya sayansi na ujuzi katika zama hizi vimegundua ukweli mwingi sana wa aina hii, na mojawapo ya milango yenye mafanikio sana katika utafiti wa kisayansi ni ubadilishaji vitu vya kimaada kuwa nguvu ya nishati. Wakati viumbe na maumbile yayoonekana katika ulimwengu huu vinapotaka kuzalisha nishati, hulazimika kubadili sura zao za asili na kugeuka kuwa nishati. Sasa, je, nishati hii - mhimili ambamo huzunguka misogeo mingi na mabadiliko ya ulimwengu - inaonekana na kugusika? Tunajua kwamba nishati ni chanzo cha nguvu lakini asili ya nishati bado inabakia ni kitendawili.

Tuchukue umeme ambamo nyingi ya sayansi yetu, ustaarabu wetu na maisha vimetegemea. Hakuna mtaalamu wa fizikia kwenye maabara yake - au mtu awaye yeyote, juu ya jambo hilo, ambaye anashughulika na vifaa na zana za umeme - anayeweza kuuona umeme wenyewe au kuhisi na kugusa uzito au ulaini wake. Hakuna mtu anayeweza kutambua moja kwa moja njia ya umeme kwenye waya; anaweza tu kutambua kuwepo kwa mkondo wa umeme kwa kutumia vifaa muhimu.

Fizikia ya kisasa inatuambia kwamba vitu ambavyo tuna hisia ya utambuzi ni thabiti, vigumu na imara, na hakuna nguvu inayoonekana kwa macho katika kusogea kwao. Lakini licha ya muonekano na wa nje, kwa kweli kile tunachokiona na kutambua ni mlundikano wa chembe ndogo ndogo (atomu) ambazo wala sio thabiti, ngumu, wala imara; vyote hivi si chochote isipokuwa migeuko, mabadiliko na misogeo. Kile ambacho viungo vyetu vya hisia vinadhania kuwa ni imara na hakisogei kinakosa uimara na utendaji na kutosogea; kinavikusanya vyote; misogeo, mabadiliko na maendeleo kwa pamoja, bila ya hili kutambulika kwetu sisi kwa njia ya uchunguzi wa hisia wa moja kwa moja.

Hewa inayotuzunguka ina uzito mkubwa na hutoa shinikizo wakati wote kwenye mwili, kila mtu hubeba shinikizo la kilo 16,000 la hewa. Lakini hatuhisi usumbufu kwa sababu shinikizo la hewa limewekwa sawa na shinikizo la ndani ya mwili lenyewe. Ukweli huu wa kisayansi uliothibitishwa ulikuwa haujulikani hadi wakati wa Galileo na Pascal, na hata sasa hivvi hisia zetu haziwezi kutambua[11] . Sifa zilizotolewa kwenye vipengele vya kimaumbile na wanasayansi katika misingi ya majaribio ya hisia na maamuzi ya kimantiki haziwezi kutambuliwa moja kwa moja. Mathalani mawimbi ya radio yapo kila mahali na bado hayaonekani popote. Hakuna mahali maalum ambapo hakuna nguvu ya mvutano ya kitu fulani chenye umbo, lakini kwa hali yoyote hii haikiondoi kwenye kuwepo kwake au kupunguza umbo lake.

Fikra kama vile uadilifu, uzuri, mapenzi, chuki, uadui, hekima ambazo hutengeneza ulimwengu wetu wa kiakili, hazina uwepo unaoonekana na wa wazi kabisa au mwelekeo mdogo kabisa wa kimwili; hata hivyo, tunazifikiria kuwa ni ukweli. Mwanadamu hajui kiini cha umeme, mawimbi ya radio au nishati, ya elektroni na nutroni, hutambua kuwepo kwao kwa njia ya matokeo na athari zao tu.

Uhai ni dhahiri kwamba upo; hatuwezi kukanusha kwa vyovyote. Lakini tutaweza kuupima vipi na kwa kutumia njia gani tunaweza kupima kasi ya fikra na dhana? Kutokana na yote haya ni wazi kabisa kwamba kukanusha chochote kilichopo nje ya upeo wa uoni wetu wa kiakili na kusikia ni kinyume na mantiki na kanuni za kawaida za akili. Kwa nini wakana Mwenyezi Mungu wanashindwa kutumia kanuni za kawaida za sayansi kuhusu suala mahsusi la kuwepo kwa uwezo unaotawala maumbile yote? Myakinifu fulani wa Misri alikwenda Makka ili aanzishe mjadala na huko 8

alikutana na Imamu Sadiq(a.s) . Imamu akamwambia, "Anza kuuliza maswali yako." Myakinifu kutoka Misri hakusema kitu. Imamu: "Unakubali kwamba dunia ina juu na chini?" Mmisri: "Ndio." Imamu: "Kwa hiyo unajuaje kile kilichomo chini ya ardhi?" Mmisri: "Sijui, lakini nadhani hakuna chochote chini ya ardhi." Imamu: "Kudhania ni dalili ya kutokuwa na uwezo unapokabiliwa na jambo ambalo huna uhakika nalo. Sasa niambie, umewahi kamwe kwenda juu angani?" Mmisri: "Hapana."

Imamu: "Hii ni ajabu ya kiasi gani kwamba hujawahi kwenda Magharibi au Mashariki, kwamba hujateremka chini ya ardhi au kuruka juu angani hadi mbinguni, au kupita juu yake ili ujue yaliyoko huko, lakini hata hivyo unavikanusha vile vilivyopo huko. Mtu yeyote mwenye busara angeweza kukataa ukweli wa kile asichokijua? Na unakanusha kuwepo kwa Muumba kwa sababu huwezi kumwona kwa macho yako!" Mmisri: "Hakuna mtu aliyewahi kuzungumza nami kwa namna hii kabla yako." Imamu: "Kwa hiyo, kwa kweli unayo mashaka kuhusu kuwepo kwa Mwenyezi Mungu; unadhani Anaweza kuwepo na Anaweza asiwepo?"

Mmisri:"Labda ndivyo" Imamu: "Ewe mtu, mikono ya mtu asiyejua haina uthibitisho wowote; asiyejua kamwe hawezi kuwa na ushahidi wa aina yoyote. Ufahamu vema kwamba kamwe hatuna wasi wasi wa aina yoytote au kusitasita kuhusu kuwepo kwa Mwenyezi Mungu. Je, hulioni jua na mwezi, mchana na usiku, vinapishana wakati wote na vikifuata njia maalum iliyowekwa? Kama vina uwezo wao vyenyewe, hebu viondoke kwenye njia zao na visirudi tena. Kwa nini wakati wote vinarudi? Endapo viko huru katika kubadilishana na kubiringika kwao, kwa nini usiku haugeuki kuwa mchana na mchana kuwa usiku? Ninaapa kwa Jina la Allah kwamba vitu hivi havinav uhuru wa kuchagua katika misogeo yao; ni Yeye Ndiye husababisha vitu hivi kufuata njia iliyowekwa; ni Yeye Ndiye anayeviamuru vitu hivi: na ukuu na ufahari ni vya kwake pekee." Mmisri: "Unasema kweli!"

Imamu: "Kama unadhani kwamba maumbile na muda vinawapeleka watu kimbele mbele, sasa kwa nini wao haviwarudishi kinyume nyume? Na kama vinaweza kuwarudisha nyuma, kwa nini haviwapeleki kimbele mbele? Tambua kwamba mbingu na ardhi vinatii matakwa Yake. Kwa nini mbingu haziporomoki na kuanguka ardhini? Kwa nini matabaka ya ardhi hayapinduki chini juu na kwa nini hayapandi na kufika juu mbinguni? Kwa nini hao waishio juu ya ardhi hawagandamani?" Mmisri: "Mwenyezi Mungu Ambaye ni Mola na Mlezi wa mbingu na ardhi ndiye anayevilinda vitu hivi visiporomoke na kuangamia." Yale maneno ya Imamu sasa yalianzisha mwanga wa imani kuangaza kwenye moyo wa Mmisri; aliukubali ukweli na akaingia kwenye Uislamu[12] .

Tusije tukasahau kwamba sisi tumefungwa ndani ya mfumo wa maada na mapana yake; hatuwezi kubunia kitu kisichokuwa na mipaka kwa kutumia tabia zetu za kawaida za kifikra. Endapo tutamuambia mwanakijiji kwamba kuna jiji kubwa na lenye watu wengi liitwalo London, akilini mwake atafikiria juu ya kijiji kikubwa, labda mara kumi zaidi ya ukubwa wa kijiji chake, na itakuwa hivyo hivyo kuhusu majengo yake, jinsi watu wanavyovaa, namna wanavyo endesha maisha yao na wanavyoingiliana katika shughuli zao. ataona kwamba tabia za watu kila mahali ni hizo hizo kama zilivyo kijijini kwake.

Jambo pekee tunaloweza tu kumwambia ili kusahihisha namna yake isiyo sahihi ya kufikiria ni kwamba London kwa kweli ni sehemu ya makazi ya watu, lakini sio ya namna unayodhania wewe, na hali zake sio za namna moja na zile unazoona pale kijijini kwako mwenyewe. Tunachoweza kusema kuhusiana na Mwenyezi Mungu ni kwamba Mwenyezi Mungu yupo, na kwamba Yu ana uhai, uwezo na ujuzi, lakini kuwepo Kwake na ujuzi na uwezo wake sio vya namna ile tuliyo na mazoea nayo. Kwa njia hii tunaweza, kwa kiwango fulani, kuepuka mipaka iliyowekwa katika uelewa wetu. Kwa myakinifu vile vile, ni vigumu yeye kutambua kiini cha msingi wa vitu asili (maada).

Ingawa inaonyesha kuwa vitu vyenye kuhisia ni vitu tunavyojua kwa uwazi na ufasaha zaidi, hatuwezi kutegemea moja kwa moja juu ya vitu hivyo pekee katika mambo ya kisayansi na kifalsafa. Tukiweka pembeni misimamo yote yenye shabiki, lazima tutathmini asili halisi ya vitu vya hisia na kiwango ambacho vinaweza kumsaidia mwanadamu katika kugundua ukweli. Vinginevyo, vitatupotosha, kwa sababu utambuzi wa hisia unahusiana tu na sifa fulani za mielekeo ya nje ya vitu vyenye kuhisia. Hauwezi kutambua ukamilifu wa sifa hizo au asili na kiini tu cha vitu vyenye kuhisi, tukiviacha vitu visivyokuwa na hisia.

Jicho ambalo ndio njia ya uhakika zaidi ya utambuzi wa ukweli, mara nyingi, hushindwa kutuonyesha sisi ukweli. Jicho linaweza kutazama mwanga pale tu ambapo urefu wa mawimbi yake haupungui 4% ya mikroni (kipimo cha urefu wa mamilioni ya mita) na sio zaidi ya 8% ya microni na, kwa hiyo, haliwezi kuona mwanga wa juu zaidi ya rangi ya urujuani au chini zaidi ya rangi nyekundu. Zaidi ya hayo, makosa yanayofanywa na utambuzi wa hisia hutengeneza sehemu muhimu kwenye vitabu vya saikolijia: jicho linajulikana kwa kufanya makosa mengi sana.

Rangi tunazozitambua katika ulimwengu wa nje, kwa kweli, si rangi. Hiyo ni mitetemo iliyoko kwenye marefu tofauti ya mawimbi. Uzoefu wa hisia zetu za macho, una marefu mbalimbali ya mawimbi ya mwanga, kwa mujibu wa utaratibu wake mahsusi kama rangi. Kwa maneno mengine, kile tunachokitambua kwa njia ya hisia zetu kimewekewa mipaka na muundo na uwezo wa hisia hizo. Mathalan, muundo wa hisia za macho katika wanyama fulani kama vile ng'ombe na paka husababisha waone uhalisi wa nje wa kitu usiobadilika, kama kimepakwa rangi. Kutokana na maoni ya uchunguzi wa kisayansi, utaratibu ndani ya hisia za macho ya mwanadamu ambao humruhusu kuona rangi haupo wazi kabisa na nadharia ambazo zimetangulizwa hadi sasa zote ni za kubuni. Suala la uwezo wa mtu kuona rangi halieleweki vizuri na lenye utata.

Ili kuweza kuona jinsi hisia ya mguso inavyoweza kudanganywa, unaweza kujaza maji kwenye mabakuli matatu: la kwanza yajazwe maji ya moto sana, la pili maji ya baridi sana, na la tatu maji ya vuguvugu. Halafu weka mkono mmoja kwenye maji ya moto na mwingine kwenye maji ya baridi, na uiache humo kwa muda kiasi. Kisha iweke mikono yote kwenye maji ya vuguvugu, na utaona kwa mshangao wako mkubwa kwamba utapata hisia zinazohitilafiana. Mkono moja utakuambia kwamba yale maji ya vuguvugu ni ya baridi sana, na mwingine utadai kwamba ni ya moto sana. Kwa kweli, maji ni yale yale, na joto lake linafahamika.

Sasa, akili na mantiki zinasema kwamba haiwezekani maji kuwa moto na baridi kwa wakati mmoja, kuwa na sifa mbili zinazo tofautiana. Ni hisia ya mguso ndio yenye dosari, baada ya kupoteza hali yake ya kujidhibiti kama matokeo ya yale mabakuli mawili ya maji ambamo mikono ilitumbukizwa. Inachokihisi kinatofautiana na ukweli, na mantiki na akili hulionesha kosa hilo. Ikiwa hali ni hii, tutawezaje kutegemea utambuzi wa hisia bila ya mwongozo wa kigezo cha akili na fikira? Je, kuna njia yoyote ya kujilinda dhidi ya dosari za utambuzi wa hisia zaidi ya uamuzi wa busara? Wakati fulani mtu alimuuliza Amirul-Mu'minin(a.s) , "Je, umewahi kumuona Mola Wako?"

Yeye akajibu:"Sitamwabudu kamwe Mola ambaye siwezi kumwona!" Huyo mtu halafu akauliza: "Wewe ulimwona vipi? Hebu tuelezee." Yeye(a.s.) akajibu:"Ole wako wewe! Hakuna mtu ambaye amewahi kumuona Yeye kwa jicho halisi, lakini nyoyo zilizojaa ukweli wa imani zimemzingatia Yeye." [13] Kwa hiyo ni uamuzi wa akili ndio unaopewa dhamana ya kusahihisha makosa ya utambuzi wa hisia, na chanzo cha uamuzi huo kiko nje ya upeo wa himaya ya hisia. Kwa hiyo, utambuzi wa hisia hauwezi kuzalisha uoni wa kiakili wenye uhalisi, manufaa yake ni ya mazoezi ya vitendo tu. Wale wanaotegemea utambuzi wa hisia pekee katika uchunguzi wao hawataweza kuyatatua kamwe matatizo ya uhai na kitendawili cha maumbile.

Kutokana na tathmini ya ufanisi wa utambuzi wa hisia, tunafikia hitimisho kwamba hata kwenye nyanja ya hisia za kimajaribio, yenyewe peke yake haiwezi kutoa ujuzi wa uhakika kwa mtu na kumwongoza kwenye ukweli. Kwa ukweli wenye nguvu zaidi, hali itakuwa ni vivyo hivyo katika mambo ambayo yapo nje ya upeo wa utambuzi wa hisia. Wafuasi wa metafizikia (falsafa ya uchunguzi wa chanzo cha uhai na maarifa) wanasadiki kwamba kama ilivyo katika njia ile ile ambamo majaribio na upimaji ndio mbinu za uchunguzi na utambuzi zinatakiwa kufuatwa kwenye sayansi ya hisia, ni uwezo wa kufikiria ndio njia ya kugundua ukweli kwenye mambo yahusuyo falsafa ya kuchunguza chanzo cha uhai na maarifa - metafizikia.

UMUHIMU WA KANUNI ZA UHAI

Sayansi inasema kwamba ni uhai ndio unaoumba uhai. Maisha ya viumbe hai yanawezekana tu kwa njia ya kizazi, kuzaana na kutengenezeka upya kwa aina husika. Hakuna chembe ya uhai hata moja ambayo imegundulika kuzaliwa na kiini asili kisicho na uhai. Hata aina ndogo za viumbe vyenye uhai, kama vile kuvu na vimelea, haviwezi kuwepo na kukua isipokuwa pawepo na kisababisho ambacho chenyewe ni kishiriki katika uhai kiwe ni chenye kuonekana kwenye mazingira yake.

Kwa mujibu wa ushahidi wa sayansi, dunia ilipita kwenye vipindi virefu ambapo hapakuwepo na uwezekano wa uhai kwa sababu ya joto kali sana lililokuwepo. Hapakuwa na uoto wowote ulioweza kuonekana kwenye uso wa sayari hii na hapakuwepo na mito au chemchem. Angahewa ilijaa metali zilizoyeyuka na milipuko ya volkano. Baadaye, wakati ambapo gamba la dunia lilipoanza kupoa, ni vitu visivyo na uhai tu ndivyo vilivyoweza kuonekana kwa mamilioni ya miaka. Kwa ufupi wakati wote wa kukurukakara zote za mabadiliko zilizofanyika kwenye uso wa ardhi, hapakuwepo na dalili za uhai juu yake. Ni vipi basi uhai ulivyojitokeza ghafla?

Hapana shaka uhai ulitokeza muda fulani baada ya kutokeza kwa ardhi; ni kwa muda mrefu kiasi gani utengenezaji huo ulifanyika na jinsi ulivyotokea, hilo halijukani. Kwa karne nyingi watafiti wamekuwa wakijitahidi kwenye maabara zao kugundua muujiza wa uhai, hili jambo la ajabu kwelikweli, lakini hadi sasa hawajakaribia hata kidogo kukifumbua kitendawili hiki. Mtafiti mmoja ameandika kwenye kitabu kiitwacho 'Distant World' "ni neno kichawi lililoje hili, la uhai! Je, hivi kuishi kulikuja kuwepo kutokana na kutokuwepo kitu chochote? Hivi dutu ya viumbehai inaweza kutokana na dutu viumbe visivyo hai? Au upo mkono fulani wenye uwezo na ubunifu unaofanya kazi hii? Wakati mwingine inapendekezwa kwamba inawezekana uhai umekuja kwenye sayari yetu kutoka kwenye maumbile mengine ya kimbingu, kwa sababu wakati ambapo aina ya chini sana ya uhai - viini vya mbegu za mboga - vinavyoogelea kwenye angahewa ya umbile la kimbinguni hupanda kufikia kilele cha juu sana, miale ya jua inaweza kuvibeba kwa njia ya shinikizo hadi kwenye anga, hivyo kwamba hatimaye vinafika kwenye uso wa umbile jingine la kimbinguni ambamo hustawi na kujiendeleza.

"Nadharia tete hii haiashirii maendeleo japo kidogo tu katika kupata ufumbuzi wa kitendawili hiki kikubwa, kwa sababu endapo nadharia hii ingekuwa ya kweli, bado hatujajua ni jinsi gani uhai ulivyojitokeza, ama ulitoka kwenye mojawapo ya sayari zilizopo kwenye mfumo wa jua na sayari zake au mojawapo ya 'Nyota ya Shiraa.' Kama vile ambavyo saa haikutengenezwa kwa kulundika pamoja springi, vikorokoro, bolti na nyenzo, vivyo hivyo, pia uumbaji wa uhai hauwezekani bila kuwepo moyo - yaani kile kinachouweka uhai kwenye msongo - na wito ambao hutamka 'kuwa hai!'" Tunatambua kwamba maada ndani mwake na yenyewe inakosa uhai na kwamba hakuna elementi ya kimaada yenye kumiliki uhai bila ya kusaidi wa.

Hivyo basi, uhai hauwezi kufikiriwa kutokea kutokana na uchanganyaji wenye mpangilio mzuri wa chembehai zinazounda kitu. Swali linajitokeza kwamba kwa nini kitu chenye uhai hakiwezi kujinakili kama kilivyo isipokuwa kwa kuzaliana na kuota upya kwa spishi husika. Utendaji wa kikemikali na athari zake wakati wote zinaendelea katika viumbe visivyo na uhai bila ya dalili yoyote ya uhai kuonekana ndani yao. Kusema kwamba kitu cha kimaada kina mwelekeo wa mkusanyiko na kwamba uhai ghafla hujitokeza wakati wa maendeleo na mabadiliko yake ni kufafanua jambo la uhai na lenye umuhimu ambalo tunalitambua kihisia; sio kuelezea chimbuko la uhai na sababu yake.

Zaidi ya hayo, chembechembe za maada kiasili hazikuwa hazikuwa zenye kutofautiana zenyewe kwa zenyewe; kwa hiyo ni lazima kuna sababu iliyofanya kazi kuleta mkusanyiko wa baadhi yao na kuzuia mkusanyiko wa zingine. Na ni sababu gani ya baadhi ya chembe chembe kupewa uhai na zingine kunyimwa uhai? Jambo pekee la kutokea kutokana na mchanganyiko wa elementi mbili au zaidi ni kwamba kila elementi inaipatia elementi nyingine baadhi ya sifa ilizokuwa nazo; inawezekanaje itoe zawadi ya kitu ambacho hainacho? Elementi zinapata sifa ya pamoja kama matokeo ya kuchanganyika, sifa ambayo haiwezi kutoka nje ya sifa ambazo kila elementi inazo, lakini uhai pamoja na tabia yake ya kipekee haina kufanana kokote na sifa za maada.

Uhai unajionyesha wenyewe katika njia ambazo kwamba maada haiziwezi, na katika namna nyingi, kwa kweli, uhai hutawala maada. Ingawaje uhai huonekana kutegemea maada, yenyewe maada ikiwa ndio umbile linaloupokea uhai, msogeo, dhamira na hatimaye utambuzi na ujuzi huonekana kwenye maada pale tu uhai unapotupa miale yake juu yake. Kwa hiyo, sio haki kujaribu kutafsiri uhai kilingana na athari za kikemikali.

Ni kipengele kipi kinachotengeneza chembechembe kwa aina nyingi tofauti na kwa mipango tofauti na halafu kikaziweka kwenye muundo uliofikiriMwenyezi wa? Kinachotayarisha chembechembe zinazozaliana ambazo huhamisha tabia na upekee wa akina baba kwa watoto wao, bila ya kosa hata kidogo kutokea katika utekelezaji wa shughuli hiyo. Tunaona kwamba chembehai zinazo tabia fulani mahsusi katika sehemu zao mbalimbali, miongoni mwao ikiwa ni ukarabati, ujenzi upya, uhifadhi wa spishi, na uwezo wa mabadiliko.

Kila chembehai ndani ya mwanadamu hufanya kazi katika wakati unaotakiwa na kwa namna inayotakiwa. Mgawanyo wa kazi na utendaji wake miongoni mwa chembehai ni wa kipekee. Zimegawanywa katika idadi inayihitajika kuhakikisha ukuaji wa mwili, na kila chembehai huenda pale mahali ilipopangiwa kwenye ubongo, mapafu, ini, moyo na figo. Mara chembehai zinapokuwa zimechukua nafasi zao zilizopangiwa, hazishindwi hata kwa nukta moja katika kutekeleza kazi zao muhimu; zinatawanya na kuondoa vitu visivyohitajika na visivyo na maana na kutunza hasa tu ule ujazo wao unaolingana.

Kuhusisha upambanuzi huu wa kipekee ambao unalengo la kuunda, kwa uwiano unaostahili, viungo na sehemu, vinavyohitajiwa na viumbe hai, kwenye mambo yatendayo bila kufikiri na yasiyo na fahamu ni tafsiri isiyotosheleza kabisa. Ni mtu gani mwenye mawazo huru ambaye angekubali ukosefu wa mantiki kama huu? Uhai, kwa hiyo, ni nuru inayoangaza kutoka kwenye upeo wa juu sana juu ya vitu vya kimaada ambavyo vina uwezo wa kuipokea; inaviweka vitu hivyo kwenye msogeo na kuweka kila kimoja kitaalamu kabisa mahali pake maalumu.

Ni utashi wenye mwongozo wa Muumba, uwezo Wake wa kuamua kwa njia ambayo inahakikisha mwendo na ukuaji kuelekea kwenye ukamilifu, na hekima Yake yenye maarifa mengi na yenye athari nyingi, ambayo ndio inayouweka muujiza mkuu wa uhai, na sifa zake zote, kwenye vitu visivyo na uhai.

Mtu ambaye anautambu a ukweli huona uelekeo wa kudumu wa uhai ukipita kwenye kiini cha kitu kinachobadilika na kutembea. Humtafakari Mwenyezi Mungu katika hali Yake ya kuendelea uumbaji na uanzilishaji, msukumo Wake usio na kikomo wa vitu vyote kuelekea kwenye ukamilifu.