MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE 0%

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE Mwandishi:
: SALMANI SHOU
Kundi: Misingi mikuu ya Dini

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

Mwandishi: KIMEANDIKWA NA SAYYID MUJTABAA MUUSAWIY LARI
: SALMANI SHOU
Kundi:

Matembeleo: 27561
Pakua: 2664

Maelezo zaidi:

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 28 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 27561 / Pakua: 2664
Kiwango Kiwango Kiwango
MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

Mwandishi:
Swahili

8

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

SOMO LA NANE

FITINA BANDIA ZA KISAYANSI

Watu wa maada wanasema kwamba kuasisiwa kwa kitivo chao cha fikra mnamo karne ya 18 na 19 kulihusiana moja kwa moja na maendeleo ya sayansi na kwamba ile mbinu pembuzi ilikuwa ni tunda ambalo lilichumwa kutoka kwenye mti uliostawi vizuri wa sayansi.

Wanaonyesha kila falsafa mbali na uyakinifu kama aina ya udhanifu, unaopingana na mbinu ya fikra ya kisayansi, na wanasisitiza kwamba msimamo wao ni wa kisayansi na endelevu. Kwa mujibu wa msimamo wao, uhalisia unategemea katika kukengeuka kutoka kwenye ukweli wa metafizikia; kila mtu anapaswa ategemeze falsafa yake ya maisha juu mantiki ya fahamu na majaribio na kuchagua uyakinifu. Lakini madai haya si lolote zaidi ya ndoto za kishabiki ambazo zimetegemezwa kwenye nadharia zisizothibitishwa. Mawazo kama haya yanakuja moja kwa moja kutoka kwenye mfumo wa fikra uliolenga kwenye uyakinifu; ambamo ndani yake, kila kitu kimeainishwa na kuwekewa mipaka kwa mujibu wa uyakinifu.

Imani kuhusu kitu cha kuabudu bila shaka ni mojawapo ya vyanzo vikuu vya utamaduni na elimu ya mwanadamu. Kupendekeza imani juu ya Mwenyezi Mungu kama msingi wa falsafa ya maisha kumesababisha mabadiliko makubwa katika misingi ya jamii na fikra katika historia yote ya binadamu. Sasa, pia, katika zama za sayansi na teknolojia, ambapo mwanadamu amekwishagundua kwenda angani, idadi kubwa ya wanasayansi wanao mtazamo wa kidini kama sehemu ya mfumo wa kisomi; wamekuja kuamini juu ya kuwepo kwa muumbaji, chanzo cha viumbe vyote, sio tu kwa njia ya moyo na dhamira, bali pia kupitia maamuzi na mantiki.

Kama uthibitisho wa wayakinifu juu ya falsafa yao ya maisha ungekuwa wa kweli, badala ya kutegemea kwenye ujuzi pungufu wa historia ya fikra za uyakinifu, panapaswa pawepo na uhusiano maalumu baina ya sayansi na mwelekeo kwenye uyakinifu; ni mawazo ya kiyakinifu tu yangewakilishwa kwenye nyanja ya kisayansi. Hivi kila mwana falsafa na msomi, katika kila kipindi, alishikilia falsafa ya maisha ya ukana-Mungu na akawa mtu wa kambi ya wayakinifu. Uchunguzi wa kisomi wa maisha na kazi za wanafikra wakubwa zitatosha kuonesha kwamba fulan kwamba kambi ya kidini kwa hali yoyote haina wanasayansi wa kweli, lakini pia kwamba wanafikra wa kisayansi wakubwa na watu wengine maarufu, wakiwa ni pamoja na waasisi wa nyingi ya sayansi ya wakati huu, wamekuwa na imani juu ya mungu mmoja.

Kwa nyongeza, itikadi za kiyakinifu na ukana-mungu kwa namna yoyote zimewekewa mipaka kwenye kipindi cha mageuzi na mendeleo ya sayansi, tangu nyakati za kale na kwa kweli wakati wote wa historia, wayakinifu wamebaki katika upinzani dhidi ya muungano wa umoja wa waumini. Leo hii hasa zaidi ni katika muundo wa Umarx uliorahisishwa kwamba bidhaa za sayansi zimegeuzwa kuwa chombo cha udanganyifu. Wale ambao mathalan wangekuwa wapange njia yao kwenye mwanga angavu wa elimu na kutathmini mambo yote kwa utambuzi na uchunguzi wa kina na wa kimantiki, katika hali ya kutokutawaliwa kabisa na ushabiki na ubaguzi wa haraka haraka - watu hawa hasa wamenaswa katika mtego wa kuvia na kuiga kijinga. Wamekataa kwa kuonyesha kiburi tu, maadili yote yaliyo bora zaidi kuliko akili na fikra, na hata wanajivunia ukanushaji wao wa kijinga.

Madai yao kwamba kuja kwa sayansi kumeondoa ile dhana ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu ni ufasaha wa usemaji tu na hauhusiani chochote na utaratibu wa kimantiki, kwa sababu hata maelfu ya majaribio ya kisayansi yasingeweza kwa hali yoyote ile kutosheleza kuonyesha kwam- ba hakipatikani kuwepo kiumbe au kitu chochote kisichokuwa cha kimaada. Uyakinifu ni itikadi ya ki-metafizikia, na kwa hiyo, lazima ithibitishwe au ikanushwe kwa mujibu wa utaratibu wa kifalsafa. Kwa sababu hii haswa, ukubalikaji wa uyakinifu hauwezi kufanywa kuwa ndio msingi kwa ajili ya ukanushwaji wa metafizikia. Kutafsiri uyakinifu kwa maana kama hiyo, ni katika uchambuzi wa mwisho utakuwa hauna maana kabisa; itakuwa ni dhana ya kishirikina ikihusisha upotoshaji ukweli, na kuifikiria kama ni ya kisayansi, kwa kweli itakuwa ni uhaini kwa sayansi.

Ni kweli kwamba mpaka hivi karibuni mwanadamu alikuwa kwa kiasi kikubwa hajui vyanzo vya asili na vipengele vinavyosababisha mambo na kwamba alikuwa na utambuzi mdogo sana wa matukio yaliyojitokeza karibu yake. Lakini imani yake haikutokana na ujinga, kwani endapo ingekuwa hivyo, ile misingi juu ya kumwamini Mwenyezi Mungu ingeporomoka pale mambo fulani yahusuyo dunia yalipovumbuliwa. Kinyume chake, tunaona katika zama hizi kwamba pamoja na uvumbuzi wa miujiza mingi kuhusu maumbile, imani juu ya Mwenyezi Mungu imepanuka zaidi. Sasa sayansi inanururisha eneo finyu sana; falsafa ya maisha ya kisayansi ni ujuzi wa sehemu moja, sio ujuzi wa kitu kizima.

Sayansi inashindwa kuonyesha hali na muundo wa maumbile yote. Lakini wakati huo huo, kwa vile mtindo wa utambuzi wa kisayansi ni sahihi na wa dhahiri, imani juu ya Mwenyezi Mungu inapata asili ya kisayansi zaidi na aina mpya ya mantiki kupitia maendeleo ya sayansi. Utambuzi wa mwanadamu hupatikana kupitia uelewa wake juu ya kisababisho na athari, na mtu anayeamini katika kisababisho kilichoko chini ya kitu haiwezekani kupuuza kirahisi wajibu wa jambo la msingi ambalo linafanya kazi juu, na kuzidi visababishi vingine vyote.

Hadi hivi karibuni, mwanadamu alidhani kuwepo kwake kulikuwa ni muundo tu wenye sehemu mbili na zinazowiana vizuri sana; alikuwa haitambui miujiza yenye utata iliyokuwemo kwenye maumbile yake. Leo hii amegundua ukweli wa kustajabisha sana na wenye athari nyingi kuhusu sehemu ya ndani ya mwili wake mdogo, akitambua kwamba kuna makumi ya mamilioni ya mabilioni ya chembe chembe hai mwilini mwake. Hali hii inawezesha kuwepo mazingatio maalum juu ya utukufu wa muumba anayehusika na matokeo-sanifu haya ambayo hayakuwezekana kufanyika zamani.

Je, kuna mantiki kusema kwamba imani ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu ni ya kipekee kwa wale wasiojua chochote kuhusu kubuniwa na kuumbwa kwa mwanadamu, na kwamba kinyume chake, mwana sayansi ambaye anatambua sheria za maumbile na mambo yanayohusiana na kukua na kuendelea kwa mwanadamu, ambaye anatambua kwamba sheria na mahesabu sahihi ndio yanaongoza hatua zote za uhai wa mwanadamu, analazimika kuamini kwamba mata, pamoja na kukosa utambuzi wote na fahamu, ndio chanzo cha sheria za kustaajabisha za maumbile? Hivi ugunduzi na ujuzi wa kisayansi unasababisha mwana sayansi kama huyo kuhitimisha kwamba mata ambayo haina utambuzi na ujuzi, ndiye muumbaji wa yeye na wa viumbe vingine vyote? Uyakinifu unaitazama dunia huku jicho moja likiwa limefumbwa na, matokeo yake ni kwamba, hauwezi kutoa majibu kwa mengi ya maswali.

Pia, sayansi haitoi jibu kwa lile swali la kama dunia inaweza kugawanyika katika sehemu mbili, ya kimaada na isiyo ya kimaada, au kwa swali la kama dunia ina lengo la kimaumbile. Maswali haya hayapo kwenye nyanja ya sayansi, elimu ya kisayansi inaweza kutufahamisha sisi - kwa kiwango fulani - kwamba ni nini, lakini haitaweza kutuonyesha mwelekeo katika uhai au kutuzindua na njia ya kufuatwa. Falsafa ya maisha, ya kisayansi, kwa hiyo, haiwezi kuwa msingi wa itika- di ya mwanadamu.

Tathmini ya ujuzi wa kisayansi zaidi ya yote ni ya kimatendo, kwa vile inamfanya mwanadamu aweze kutawala maumbile. Ni mifano na tathmini ya kinadharia ndio ambayo inahitajika kama msingi wa imani. Zaidi ya hayo, sayansi imeegemea kwenye majaribio na uchunguzi, na sheria zenye kuwa na majaribio juu ya msingi wao hulazimika kubadilika na kuyumba. Imani inahitaji msingi wenye umilele, ikiwa na kinga dhidi ya mabadiliko, na iwe na uwezo wa kujibu maswali kama vile asili na umbo la dunia kwa ujumla katika namna ya kuaminika na ya kudumu. Ni hapo tu ambapo mahitaji ya mwanadamu ya tafsiri na uchambuzi wa kina wa kuwa hai unaweza kutimia.

Kadiri anavyoelekea kwenye ukamilifu, mwanadamu anahitaji uwiano wa kiroho na kiakili; bila kuwa na lengo, atapotea na kwenye njia zisizo sahihi na kujihatarishia mabalaa. Mtu asiyeweza kupata lengo lake katika dini, atafuata lengo analolielewa yeye mwenyewe ambalo halitakuwa chochote isipokuwa maasi dhidi ya matakwa ya maumbile, halitahusiana na uendelevu au ukomavu wa akili.

Sababu za ukanushaji na kutoamini Vitabu juu ya historia ya dini hujaribu kufafanua kinaga ubaga mambo ambayo yamewavuta watu kwenye dini. Lakini majaribio kama hayo wanayoyafanya hayana maana yeyote na hayawezi kufichua ukweli wenyewe wa mambo. Ni muhimu kushabahia kwenye muelekeo wa asili wa mwanadamu kwenye imani ya mungu mmoja, ile sifa ya kiuhai ya jamii za wanadamu ambayo humpa mwanadamu - pamoja na tofauti zake zote ndani yake, fikira na matamanio yake - sehemu maalumu katika maumbile. Hapo ndipo inapowezekana kugundua mambo ambayo humwongoza mwanadamu kuikanyaga asili yake mwenyewe kwa kukataa dini, kwa viapo kabisa.

Mahusiano ya kidini ya mwanadamu ni matokeo ya asili yake, na uyakinifu ni kitu kinachopingana na maumbile yake. Kwa kulingana na tabia yake ya dhahiri, binadamu atajiumbia mungu wake mwenyewe kama hatamgundua Mungu wa kweli, na mungu anayemgundua yeye anaweza kuwa ni maumbile au mambo ya kihistoria yasiyoepukika. Na mungu huyu wa uwongo anachukua nafasi ya Mwenyezi Mungu wa kweli kwa kuzingatia ufahamu na mamlaka, kufaa kwa maagizo, na uwezo wa kumwongoza mtu kwenye njia fulani na kumsogeza mbele, bila kuzuiwa na matakwa ya mtu yeyote.

Huu ndio mwanzo wa kubadilishana miungu wa uwongo, ufuasi kwenye uabudu masanamu upya, ambao ungemtoa kafara Mwenyezi Mungu kikatili kwenye historia na kubadilisha lulu kwa shanga. Inasikitisha kwamba, watu wengi waliojiangamiza kwa unyonge waliojiingiza wenyewe wakawa wameinama chini mbele ya sanamu ambalo wameliunda wenyewe na kulifanya kuwa mungu! Wamempa kisogo muumba asiye na kifani na kwa hiari yao wakakubali fedheha inayochafua ya ibada iliyoongozwa vibaya kama hiyo.

Kama tukilichunguza jambo hili kwa ukaribu zaidi, tunaona kwamba kujitokeza kwa uyakinifu huko Ulaya kama kitivo cha fikra, ukatwaji wa uhusiano wa binadamu na kanuni ilioyo tukufu, kufungwa kwao kwenye nyororo za maada, kuchagua kuendekeza sayansi mahali pa dini - yote haya yalisababishwa na mlolongo wa mambo ya kijamii na kihistoria yaliyojitokeza katika nchi za magharibi.

Mojawapo ya mambo yaliyoamsha upingaji wa mabadiliko ulioenea katika Ulaya yote na kusababisha kutokeza kwa fikra zisizofuata dini na propaganda dhidi ya dini, ilikuwa shinikizo baya mno lililowekwa na mamlaka za kikanisa mwanzoni mwa kipindi cha mwamko-sanaa juu ya wasomi waliokuwa wanaleta mawazo mapya ya kisayansi. Kwa kuongezea kwenye mafundisho maalum ya kidini, kanisa pia liliwiwa shukrani kwa ajili ya kanuni fulani za kisayansi kuhusu mwanadamu na dunia ambazo lilizirithi kutoka kwa wanafalsafa wa kale - hasa wa Kigiriki - na ambazo ziliwekwa katika ulinganifu sawa na imani za dini. Nadharia yoyote iliyojitokeza kupingana na Biblia na hizi kanuni zilizorithiwa zilifikiriwa kama za uasi, na yeyote aliyezitetea angeadhibiwa vikali.

Upinganaji wa dhahiri baina ya dini na sayansi ulianzisha uadui wa pamoja katika pande hizi mbili. Wasomi na wanasayansi waliona kwamba Kanisa la Kikristo lilikuwa linazifunga akili na fikra, na kuzuia maendeleo huru ya mawazo; kupitia kwenye ufuasi wake wa mfumo unaoogofya wa fikra na desturi ya kwenda kinyume na akili, lilikuwa linatengeneza mazingira yenye kusonga kwa ajili ya mwanadamu wa zama hizo mpya. Hivyo, mabingwa walikimbilia kwenye kujitenga kunakohuzunisha kutoka kwenye dini.

Mashinikizo haya yaliyokuwa yakilimbikizana kwa siku nyingi, hatimaye yalisababisha majibu ya vurugu zilizoikumba Ulaya yote. Hapo ndipo nguvu na utawala wa Kanisa ulididimia na uonevu wake ulikoma, uhuru wa fikira za kimagharibi ulipatikana tena na ulionyesha hisia kali dhidi ya mipaka iliyokuwa imewekwa hapo mwanzoni. Wasomi waliondoa nyororo zote za taratibu za kizamani toka kwenye shingo zao na wakatoka kwenye dini. Maumivu na hasira zote walizokuwa wamezipata zilidhihiri kwenye wimbi kubwa la uadui dhidi ya dini. Hali ya wasi wasi mkubwa wa kiroho ilianza ambayo ilifikia kilele katika kutenganishwa sayansi na dini. Tamaa ya kisasi kisicho na mantiki dhidi ya dini kilisababisha kukanushwa kwa ukweli mwingi wa ki-Mungu na wa imani ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu.

Ni kweli kwamba baadhi ya mafundisho yaliyounganishwa na dini hayakuwa na mantiki au hata msingi, yakiwa hayana uhusiano na ujuzi wa kidini uliothabiti. Lakini kulipiza kisasi juu ya Kanisa ni jambo moja na kuangukia kwenye chuki haraka na kwa makosa dhidi ya dini, kama hivyo, ni kitu kingine tofauti. Ni dhahiri kwamba kulipa kisasi, kukiwa ni jambo ambalo linatokana na hisia, halina uhusiano wowote na ufasaha wa kisomi.

Umasikini wa kiroho wa mwanadamu uliongezeka kwa kiwango kinacholingana na utajiri wake wa kisayansi na kiteknolojia. Jinsi alivyoendelea katika viwanda vingi, ndivyo maadili na nguvu yake ya kiroho vinazidi kupungua, hadi kufikia kiwango ambapo alikosa uwezo wa kimaadili wa kuweza kutumia inavyostahili ujuzi wake mpya alioupata. Ujuzi wa kisayansi haujishughulishi na maadili, mtu hawezi kuamua kazi za mwanadamu mwenye kuwajibika kwa kutumia kigezo cha sayansi. Sayansi hata ifike mbali vipi, bado haina uwezo wa kuona hata hatua moja mbele yake. Ujuzi wa kibinadamu hauwezi kufika kwenye chimbuko la dunia na kutambua kwa ufasaha yaliyomo, wala hauwezi kutabiri mustakabali wa baadaye wa mwanadamu.

Ni falsafa ya maisha ya Mungu Mmoja tu ambayo haijaribu kumfungia mwanadamu kwenye vipengele vya kimaada vya maisha yake. Kinyume chake kupitia kwenye ishara na dalili ambazo mwanadamu amepewa ili zimwongoze katika njia yake, imani ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, inaonyesha utukufu wa asili na mustakabali kwa ajili ya mwanadamu.

Mara tu mwanadamu anapoingia kwenye njia ya kumwamini Mwenyezi Mungu, hupata falsafa ya maisha pana ndani ya mfumo ambamo huweza kupata majibu kuhusu swali lake la msingi la ki-uchunguzi. Mara akishafikia hatua hii ya imani pana na yenye vipimo vingi, maisha yake mwanadamu huchukua juhudi mpya na maadili ambayo ndio matunda mazuri ya hiyo falsafa ya maisha huja kuwa kweli. Mapambano na kanisa yalikuwa kwa hiyo, kipengele kimoja katika kutenganisha sayansi na dini. Kundi lingine liliitekeleza dini na kukimbilia kwenye uyakinifu kwa sababu mawazo yaliyoshauriwa na Kanisa hayakuwa sahihi na hayaku- tosheleza, yaliyokosa na maadili yaliyo nje ya uwezo wa mwanadamu.

Mawazo haya kwa kawaida yalionekana kutokubalika na yasiyovutia kwa watu wenye akili. Kanisa lingemwonyesha Mwenyezi Mungu katika hali ya maada na kibinadamu kwa maana ambayo ilipingana na haja ya mwanadamu juu ya maadili kamili na kule kujitahidi kupenya na kuvuka mifumo yote yenye kuweka mipaka. Hapawezi kuwa na shaka kwamba endapo ukweli usiopingika unaingizwa kwenye ubongo wa mtu katika muundo wa hekaya wenye dosari, mtu huyo atakwenda kinyume nao mara tu atakapofika ukomavu wa kiakili.

Wakikabiliwa na taswira ya Mungu mwenye kupachikwa umbo la kibinadamu, iliyotengenezwa katika theolojia ya Ukristo, kutukuza imani zaidi kuliko matumizi ya akili na msisitizo kwamba imani lazima itangulie akili, watu walioelimika walitambua kwamba jitihada hizi zitokanazo na akili finyu, kwa lengo la kuzuia matumizi ya busara na sayansi katika ukiritimba wa theolojia ya Kikristo hazikuendana na kigezo cha mantiki na mbinu ya kisayansi. Kwa vile hazikuwa na chanzo thabiti ambacho kutokana nacho wangejifunza mafundisho ya kweli kuhusu Mwenyezi Mungu, yote yakiwa huru kabisa kutokana na taasisi za Kanisa na vitabu vyake vipotovu, na kwa kuwa hawakuwa na njia ya kuwafikisha kwenye mfumo ulio bora zaidi ambao ungeweza kutosheleza mahitaji yao ya kiroho na kimwili na kuwapa muundo unaofaa kwa ajili ya kuunganisha vipengele vyote muhimu vya maisha, vya kimwili na kiroho, hisia na kiakili, falsafa ya maisha ya uyakinifu iliota mizizi ndani yao, na kuwaelekeza kukana maadili yote yaliyo nje ya uwezo wa kibinadamu na yaliyo zaidi kinyume cha ubinadamu.

Walikuwa hawatambui kwamba ingawa kosa hupotosha dini wakati linapofuata njia ya ujinga, dini ya ukweli, isiyokuwa na uwongo wowote, ushirikina na upotovu inaweza kumkomboa mwanadamu kutoka kwenye utumwa wa visasili na ushirikina, na kumshikilia kwa umadhubuti kwenye mhimili wa imani ya kweli na kumpatia uelewa sahihi wa mafundisho yahusuyo Mwenyezi Mungu, ambayo hutosheleza akili yenye udadisi. Badala yake, wasomi wa nchi za Magharibi walitambua upande moja tu wa ushirikiana wa dini ya uwongo na jinsi mfumo ulioundwa wa imani wa dini, usio na kuswali, ulivyokosa kuwa na msingi wa kimantiki, kwa hiyo hawakusita kushutumu dini kwamba haina msingi wowote. Uamuzi wao uliegemezwa kwenye ile hali halisi ya kukatisha tamaa iliyomo kwenye dini yao wenyewe, na uamuzi huo haukuweza kushindwa kuwa wa haraka, usio wa kweli, usio na busara na mantiki.

Haya yamefafanuliwa ifuatavyo na msomi wa fiziolojia na biokemia: "Ukweli kwamba wasomi fulani hawakuongozwa, katika njia ya utafiti wao, kwenye utambuzi wa kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, una sababu nyingi sana. Hapa tunataja mbili miongoni mwa hizo. Kwanza; hali ya kisiasa iliyotengenezwa na udikteta, pamoja na hali zinazoambatana na mambo ya kijamii na kiutawala, zilielekea kumsababisha mwanadamu kukana kuwepo kwa Muumbaji. Pili, mawazo ya mwanadamu wakati wote yamekuwa yakivutiwa na njozi fulani na uwongo, na ingawa mwanadamu anaweza kuwa hana woga wa maumivu makali ya kiroho na kimwili, bado hana uhuru kamili wa kuchagua njia iliyonyooka.

"Katika familia za Kikristo, watoto wengi huamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu afananaye na mwanadamu, kana kwamba mwanadamu aliumbwa katika umbo la Mwenyezi Mungu. Wanapoanza kuingia kwenye nyanja ya sayansi na kujifunza na kutekeleza fikira za kisayansi, hawawezi tena kupatanisha dhana yao dhaifu ya kumpa Mwenyezi Mungu viungo vya mwanadamu na ushahidi wa kimantiki na mbinu za sayansi. Kwa hiyo baada ya muda fulani, wakati ambapo matumaini yote ya kupatanisha imani na sayansi yanatoweka, wanaitelekeza kabisa fikira yote ya Mwenyezi Mungu na kuifuta kabisa kwenye akili zao. "Sababu yake kubwa ni kwamba ushahidi wa mantiki na aina za sayansi hazirekebishi hisia na imani zao za mwanzoni, lakini badala yake, huwafanya wahisi kwamba walikosea katika imani yao ya mwanzo kuhusu Mwenyezi Mungu. Kwa mvuto wa hisia hizi, ikiunganishwa na mambo mengine ya kisaikolojia, wanashangazwa na upungufu wa fikra zao na huachana kabisa na majaribio ya namna yoyote ya kumjua Mwenyezi Mungu.[25] .

Kwa hiyo, wanasayansi, walijaribu, kwa kufafanua aina zote za sheria na fomyula na kutoacha nafasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na dini katika kutafuta ufumbuzi wa maswali yanayogusa kuwepo uhai na maumbile. Walijaribu kukatisha matumaini ya wanadamu kutoka kwenye dini na kumweka kando Mwenyezi Mungu katika kuwa na wajibu wowote katika utendaji wa ulimwengu na mpango wa maumbile.

Kila walipofikia kukwama walijaribu kutafuta ufumbuzi wa tatizo kwa kutumia nadharia tete mbali mbali au kuahirisha ufumbuzi bayana wa tatizo hadi hapo utafiti mkubwa zaidi utakapokuwa umefanywa. Walidhani kwamba kwa njia hii walikuwa wanaepuka kujisalimisha kwenye fomyula isiyo ya kisayansi na ushirikina. Hivyo, ingawa waliepuka hatari ya kukubali ushirikina, kwa masikitiko walianza kupiga vita upagani na ukana-Mungu.

Ingawa imani juu ya Mwenyezi Mungu na kuamini katika kanuni ya uasilishaji ni jambo la kawaida na msingi kwa mwanadamu, haliwezi kulinganishwa na mahitaji ya kimaada ambayo mwanadamu wakati wote anajitahidi kuyapata. Liko tofauti kabisa na maisha ya kimaada, na kwa kuwa ni hitajio la ndani ya mwanadamu, linahusiana na namna tofauti kabisa. Zaidi ya haya, ni rahisi kukanusha kitu kisichoonekana kwa macho kuliko ilivyo kwa kukithibitisha, tukichukulia kutoweza kwetu kukielezea vya kutosha. Watu wanaokosa uwezo wa kiakili, kwa hiyo, huchagua njia rahisi na isiyo na usumbufu ya kukataa badala ya kujitahidi kutumia akili. Njia ya kukanusha aidha, haihusishi madhara yoyote yaliyodhahiri. Kwa kugeukia mbali na Mwenyezi Mungu, watu pole pole hujenga msimamo wa ukaidi na uadui kwenye dini, ulioathiriwa na ushabiki. Athari kubwa za msimamo kama huo zinaweza kuonekana kwa urahisi kwenye hoja zenye uovu za wale ambao wameipa mgongo dini.

Pia ni rahisi zaidi kukana kitu kisichoonekana kwa sababu kukithibitisha kuwepo kwake kutamaanisha wajibu mbali mbali kwa mwanadamu, wale wanaotaka kuzitupilia mbali wajibati hizo, kwa urahisi hukataa kuwepo kwa kanuni ya uanzishaji. Qur'anii inasema:

بَلْ يُرِيدُ الْإِنسَانُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُ ﴿٥﴾ يَسْأَلُ أَيَّانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ ﴿٦﴾ فَإِذَا بَرِقَ الْبَصَرُ ﴿٧﴾

"Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilizioko mbele yake. Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama? Basi jicho litapoduwaa." ( Qiyama:75: 5-7).

Mafundisho ya wale wataalamu wa kujihini, wajinga na wasio na mantiki pia hayawezi kutoonekana kama kipengele kinachosukuma vikundi fulani vya watu kuelekea kwenye uyakinifu. Zile silika zinazokuja kuwepo pamoja na maisha ya kawaida ya mtu ambazo zimefungamanishwa na uhai wake, si tu kwamba hazikosi maana na lengo; zenyewe pia ni nguvu ya kuumua na kuandaa takdiri, kipengele cha maendeleo na msogeo, ambacho ndio humsukuma mtu na kusonga mbele kuelekea kwenye lengo lililozingatiwa katika kuumbwa kwake. Ni kweli kwamba, mtu hatakiwi kuwa mtumwa aliyefunikwa macho kwenye silika zake kama mfungwa ambaye uhai wake wote na nyendo vinadhibitiwa na mwangalizi wa jela. Lakini, pia hapaswi kupigana vita na ukweli wa uhai wake mwenyewe na kutafuta kuzuia shughuli zote na nyendo kwa upande wa silika zake. Uhai wa mwanadamu wenye matunda mazuri, kwa kweli hutegemea juu ya kuwepo hai katika maisha yake kwa silika zake, zilizoenea kwa uwiano unaofaa; kuzuia silika kunasababisha utata na uharibifu wa haiba ya mtu.

Falsafa ya maisha iliyokuwepo kwenye Ukristo katika kipindi cha kati ilikuwa kwenye msingi wa maelekezo ya mazingira pekee ya Akhera ambayo yaliingiza na ushushaji thamani wa dunia ya kimaada. Sasa, matokeo yatakuwaje endapo mtu anakanusha uhalali wote wa nguvu za silika, kwa jina la Mwenyezi Mungu na dini, akajaribu hata kuziharibu kabisa; kama mtu anatukuza useja na maisha ya utawa na akakanusha hadharani ndoa na kuzaana kama ni uchafu, shughuli yenyewe hasa ambayo ndiyo inayolinda uhai wa spishi mbali mbali; na kama mtu anaona umasikini na kutojiweza kama ndio uhakikisho wa furaha ya hali ya juu? Je, kwa hiyo, itawezekana kutegemea dini kuchukua jukumu mashughuli na endelevu?

Jukumu halisi na kazi ya dini ni kusafisha, kuongoza na kudhibiti silika, kuwekea mpaka wa eneo la ushughulikaji wao, na kuzitakasa na upotofu na uovu wote. Sio kuziharibu na kuziondoa kabisa. Kwa kuzidhibiti silika na kujitahidi wakati wote kujinasua mwenyewe kutoka kwenye mtego unaoweza kuwepo, mwanadamu hujitengenezea hatima yake yenye lengo. Endapo mwanadamu anashindwa kufanya hivi, mgongano mkubwa wa silika ndani mwake ni mkubwa mno hivyo kwamba hawezi kuwa mdhibiti wa nafsi yake mwenyewe kwa urahisi. Kwa hiyo, anahitaji mfumo wenye maarifa mengi juu ya elimu ya maadili. Kwa upande moja binadamu anapatwa na mvuto wa shauku ya kidini, hali hii, humtiisha kwa siri na huzikusanya pamoja zile nguvu zake zilizotawanyika, kwenye mshiko wa uwezo wake, na kuzielekeza kwenye kupata maadili na manufaa. Kwa upande mwingine binadamu pia anapatwa na mvuto wa silika zake.

Katika jamii yoyote ambamo watu wakati wote wanaambiwa, kwa jina la Mwenyezi Mungu na dini, kwamba njia ya kwenye furaha ipo katika kuzikataa zawadi za dunia hii, mwanya unajitengeneza wenyewe kwa ajili ya maendeleo ya uyakinifu na umakinifu zaidi juu ya thamani ya vitu vya kimaada, ili kwamba zile fikra tukufu za dini, pamoja na athari zake zenye kufika mbali, zitoweke kwenye mazingira.

Lakini, hii haiwakilishi mantiki halisi ya dini. Dini za kweli huelekeza mazingatio ya mwanadamu kwenye maadili thabiti ya kiroho, yakijiegemeza katika imani juu ya muumbaji na kumpatia mtu mafundisho mapana na kanuni kwa ajili ya maisha yake. Maadili haya hupanua uwanja wa uoni wake hadi kwenye mipaka ya eneo la ki-mbingu, na kumtoa kutoka kwenye utumwa wa kuabudu matamanio yake mwenyewe na anasa za kidunia (uyakinifu), na wakati huo huo, yanamruhusu afurahie starehe za kidunia kwa kiasi cha kutosheleza tu.

Baadhi ya watu wanadhani kwamba starehe holela juu ya vitu fulani ambavyo vimepigwa marufuku na dini itawahakikishia kudumu furaha yao. Wanafikiri kwamba dini inapigana kwa ukaidi dhidi ya starehe zote na haiko tayari kukubaliana raha za dunia hii, kana kwamba Mwenyezi Mungu anamlazimisha mwanadamu kuchagua kati ya furaha ya hapa duniani na furaha ya Akhera. Mwelekeo huu kwenye dini ni wa unapotoshaji kabisa usiowezekana kuwa kweli. Ikiwa dini kuwajibika katika jitihada za binadamu na uchaguzi wake wa mwelekeo, ni kwa sababu kujiendekeza kusikozuilika kwenye matamanio, kujisalimisha bila masharti kwenye silika na hamu, na utiifu kwenye amri za umimi, hutia giza maisha ya mtu na humpeleka kwenye hali ya utumwa wa kutojitambua. Licha ya asili yake safi kimsingi, anaanguka kutoka kwenye daraja lake halisi na kukengeuka kutoka kwenye njia yake ya kweli. Kama kule kujiendekeza kiholela kwenye silika za matamanio kungekuwa sio sababu ya mateso ya milele na kujivunjia hadhi kuchungu, kusingeweza kukatazwa.

Ni fikira kama hizi ambazo zinafanya iwezekane kuelewa ni kwa nini dini imekataza mambo fulani na ni jinsi gani starehe ya dunia ilivyo na ulinganifu na furaha ya Akhera. Fikira kama hizi hutumika katika kumlazimisha wajibu fulani juu ya mwanadamu. Jaribio ya kutekeleza matendo ya faradhi ya ibada, kwa uaminifu na bila unafiki, huleta mabadiliko ya ndani kabisa mwa mtu, lengo la matendo haya kwa namna yoyote sio kupunguza furaha ya mtu ya kidunia.

Kuabudu ni sawa na tufani kali kwenye dimbwi (wangwa) tulivu la moyo, inayobadilisha tabia ya ndani ya mwanadamu na kigezo chake cha maamuzi. Ndiyo jiwe la pembeni ambapo msingi wa dini huimarishwa, mazoezi ya kuelimisha yenye manufaa yanayopenya kwenye vina virefu vya nafsi. Upanga wake mkali hukata fundo la upotofu na udhalili ndani ya binadamu na kumwezesha yeye kukimbilia eneo pana na safi, lisilo na mipaka. Kwa ufupi humwezesha mwanadamu kukua na kufikia ukomavu halisi.

Si tu kwamba hakuna mikinzano kati ya mambo ya maisha na yale ya kiroho; mambo ya kiroho yanafaa sana kwenye maisha ya furaha kubwa zaidi hapa duniani. Inaweza kuwa labda kwamba mafundisho yasiyoaminika na yasiyo na mantiki ya Ukristo yameathiri mielekeo ya kinyume na dini ya watu kama Betrand Russell. Kwa dhahiri aliamini kwamba kumwamini Mwenyezi Mungu ni kujitakia huzuni, kama inavyodhihirika katik a maneno yafuatayo: "Mafundisho ya Kanisa yamefanya binadamu achague baina ya aina mbili ya mateso na umasikini. Ama mateso ya hapa duniani na kukosa starehe zake au mateso ya maisha ya akhera na kukosa furaha ya peponi.

Kuhusu Kanisa, mojawapo ya aina hizi mbili za mateso lazima na muhimu ivumiliwe. Ama mtu lazima ajisalimishe kwenye mateso ya hapa duniani na kuteseka kwa umasikini na upweke ili aweze kufurahia starehe za akhera, au, ikiwa mtu anataka kufurahia starehe za dunia hii lazima akubali kwamba atanyimwa starehe za akhera." Ueneaji wa maoni kama haya, ambayo yanadhihirisha ujinga mkubwa sana na wa kina falsafa ya maisha kidini, kunaweza kuamua hatima ya dini iliopo katika jamii fulani. Athari za maoni haya kwa itikadi na matendo ya binadamu ni nzito sana kuweza kupimwa vizuri, kwa mtazamo wa mpito wa juu juu. Muundo huu wa fikira umesababisha mazingatio ya mwanadamu kuelekezwa kipekee kwenye nyanja ya kimaada - awe anatambua au hatambui. Umakinifu unaojitokeza juu ya starehe na anasa umesababisha kudhoofika kwa mambo ya kiroho na maadili.

Dini haimshutumu mtu kuvumilia mojawapo ya aina mbili hizi za mateso. Inawezekana kabisa kuunganisha furaha ya dunia hii na ya Akhera. Kwa nini, Mwenyezi Mungu Ambaye hazina yake ya huruma na neema haipungui, asitake waja Wake wapate furaha kamili ambayo inakusanya dunia hii na Akhera? Hivi ndivyo kwa usahihi hasa anavyopenda Yeye.

Jambo lingine katika kuenea kwa fikira za kiyakinifu limekuwa ni uendekezaji wa tamaa na kuzama kwenye shimo la ashiki. Kila utambuzi wa kiakili na mawazo hufanya msingi wa baadhi ya matendo ya nje; njia ya matendo ya mwanadamu huchukua umbo la njia ya mvuto wa itikadi zake. Kinyume chake matendo na maadili ya mwanadamu pia huleta mabadiliko yenye ubora katika tabia yake ya kiakili na muundo wa fikira. Mtu anayeabudu matamanio yake polepole atapoteza mawazo yote matukufu kuhusu Mwenyezi Mungu. Mara tu anapochagua mhimili wa uhai wake kinyume na Mwenyezi Mungu na kudhania kwamba chochote kilichopo katika dunia hii, kimetupwa hivi hivi tu juu yake, bila madhumuni yoyote, hivyo kwamba wazo la kuwa na lengo katika maisha linakuwa halina maana kabisa, huanza kutoa uwezo wake wote wa kiakili katika kufanya starehe kwa wingi zaidi. Kutumbukia huku kunakofedhehesha, kwenye kiwango cha chini cha maisha, kunanyausha mizizi ya matumaini yote kwa ajili ya makuzi na maendeleo.

Mawazo ya kumwamini Mwenyezi Mungu; kwa kulinganisha, ni kama mbegu ambayo inahitaji udongo unaofaa ambamo inaweza kumea. Mbegu hiyo inaweza tu kustawi kwenye mazingira safi, mazingira ambamo mwanadamu anaweza kupata kwa haraka na urahisi kiwango cha ubora ambao ni wa kipekee kwake, kwa sababu ya muundo ambamo kanuni za maisha yake zimewekwa. Imani ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, haiwezi kustawi kwenye mazingira yaliyo jaa uovu.

Mojawapo ya vipingamizi vinavyo mzuia mtu asipate kumjua Mwenyezi Mungu na sababu za mwanadamu kukanusha kuweko huku, pamoja na kuwepo dalili zilizowazi na ushahidi wenye maamuzi ambao upo, kwa hiyo, ni kujisalimisha kwenye dhambi na kuendekeza matamanio. Imam Jafar as-Sadiq(a.s) alisema alipomjibu Mufadh'dhal ndani ya Risalah-yi Ahlija: "Ninaapa kwa nafsi yangu mwenyewe kwamba Mwenyezi Mungu hajashindwa kujijulisha Yeye kwa wasiomjua, kwani wanaona ushahidi dhahiri na ishara zisizo na shaka za Muumba katika mumbile Yake na wanatazama mambo ya ajabu katika Ufalme wa angani na duniani ambayo yanaelekeza kwa Muumba wao.

"Watu wajinga ni wale ambao wamefungua milango ya dhambi mbele yao na wakafuata njia ya kujiendekeza kwenye tamaa na ashiki. Matamanio ya nafsi zao yametawala nyoyo zao, na kwa sababu ya dhulma zao juu ya nafsi zao wenyewe shetani amechukua mamlaka juu yao. Mwenyezi Mungu amezipiga muhuri nyoyo za waovu."[26]

Tamaa ya starehe, ushindani, ubadhirifu, mantiki dhaifu ya waumini fulani wasio na elimu - hawa pia ni miongoni mwa vipengele vinayomlazimisha mwanadamu kukimbilia uyakinifu. Ghasia na mchafuko wa maisha, wingi wa bidhaa zinazozalishwa, utajiri na mamlaka, mielekeo ya maisha ya kisasa inayozuzua na kushughulisha, kuenea haraka kwa vitu vya anasa na starehe - yote haya yanawafunikiza kabisa watu walafi. Watu hawa wanajaribu kabisa kujitoa kwenye mazingira ya masuala ya kidini na hukataa kukubali mamlaka ya madaraka yoyote makubwa zaidi, kwani si tu kwamba hii isingewaletea manufaa yoyote ya kidunia, bali pia ingeshika hatamu kwenye mawimbi ya matamanio yao yaliyokomaa.

Kwenye mazingira ambayo watu wamezama kwenye dhambi, ufujaji, na uovu, na wakakataa kukubali mipaka yoyote inayotawala matendo yao, dini itabakia jina tu. Watu wanaojiendekeza na wayakinifu hawawezi kuwa wenye kumtafuta na kumwabudu Mwenyezi Mungu. Wakati ambapo mojawapo ya kanuni mbili zinazopingana; kanuni ya kusaka anasa na ile ya kumwamini Mwenyezi Mungu, inapokuwa imetawala nafasi ya akili ya mhusika, kanuni nyingine lazima iondoke humo. Mara tu moyo wa kuabudu unapokuwa katika maisha ya mwanadamu, huiondoa mielekeo yote ya kiyakinifu kwa kuzikata pingu imara za matamanio duni na wakati wote hutia msukumo juhudi ya mtu kupanda kuelekea kwenye lengo lake. Hivyo, muundo kamili wa uhuru wa binadamu wa kutoka kwenye utumwa na kuingia kwenye hali ya asilihujitokeza.

Jinsi lengo analojiwekea mtu mwenyewe linavyokuwa la juu na la mbali zaidi, ndivyo mwelekeo wa kuliendea utakavyo kuwa mkali zaidi na ndivyo jitihada inayohitajika ili kulifikia itakavyozidi kuwa kubwa zaidi na ya muda mrefu zaidi. Kwa hiyo, kama tunamchagua Mwenyezi Mungu kama lengo letu, tutakuwa tumechagua lengo la hali ya juu lisilo na ukomo, na njia inayoelekea kwenye mafanikio ya lengo hilo vivyo hivyo itakuwa haina ukomo, ingawa njia hiyo ni wazi na iliyonyooka wakti huo huo.

Ni lengo ambalo litajibu matatizo na maswali mengi, na kwa kuwa litatulazimisha kukataa udhalimu wa nafsi, utatupatia uhuru kamili juu yetu. Kama tukimkubali Mwenyezi Mungu kama ndio lengo letu, uhuru utapatanishwa na makuzi na maendeleo yetu. Juhudi zetu za kujiendeleza na kupiga hatua zitakuwa na maudhui na maana, kwa msaada wa silika za kiungu na tamaa ya uzima wa milele. Kwa ufupi, tamaa ya kupiga hatua na maendeleo, mara tu inaporekebishwa na ibada ya Mwenyezi Mungu, ama kwa hakika haipingani na uhuru wa binadamu wala haiishii kwenye yeye kuwa mtumwa.

Tunaweza kudai kuwa tumepata uhuru hapo tu tunapokuwa tunakwenda sambamba na kusonga mbele kwa ujumla kwa dunia yote kuelekea kwenye ukamilifu, kwa akili, na utambuzi kamili wa manufaa yatakayoletwa na hatua hii. Kufanya matendo kwa kutii hali ya asili au kwa kutoepukika kwa historia sio uhuru, kwani wakati mwanadamu anapoacha kujali ustawi wake mwenyewe kwa kufuata maamuru ya maumbile, hili si jingine mbali na utumwa au utii wa kijinga.