MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE 0%

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE Mwandishi:
: SALMANI SHOU
Kundi: Misingi mikuu ya Dini

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

Mwandishi: KIMEANDIKWA NA SAYYID MUJTABAA MUUSAWIY LARI
: SALMANI SHOU
Kundi:

Matembeleo: 27508
Pakua: 2660

Maelezo zaidi:

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 28 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 27508 / Pakua: 2660
Kiwango Kiwango Kiwango
MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

Mwandishi:
Swahili

9

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

SOMO LA TISA

QUR'ANII INAMUWASILISHAJE MWENYEZI MUNGU

Tunapotaka kutathmini tabia na ujuzi wa kisayansi wa msomi, tunapima kazi zake na kuzichunguza kwa karibu zaidi. Vivyo hivyo, ili tuweze kupima kipaji, ubunifu na uwezo wa msanii wa kuvumbua michoro bunifu, tunafanya uchunguzi wa bidhaa zake za kisanii.

Kwa njia hiyo hiyo, tunaweza pia kutambua sifa na tabia za nafsi halisi ya Muumba kutokana na sifa na mpangilio ulioenea katika maumbile yote, pamoja na ustadi na utaratibu wake. Hapo, ndani ya mipaka iliyowekwa na uwezo wetu wa kujua na kutambua, tunaweza kufahamu ujuzi wa Mwenyezi Mungu, hekima, uhai na uwezo.

Endapo likiwa ni suala la ujuzi kamili na mpana juu ya Mwenyezi Mungu basi, kwa kweli, lazima tukubali kwamba uwezo wa mwanadamu wa kujua haufikii kiwango hicho. Sifa za Mwenyezi Mungu haziwezi kuwekwa ndani ya mipaka yoyote inayofahamika, na ulinganisho wowote au mfanano tunaoutoa juu ya sifa hizo hauna budi uwe wa uwongo, kwani chochote kinachoweza kuchunguzwa na sayansi na fikira katika nyanja ya maumbile ni kazi ya Mwenyezi Mungu na matokeo ya utashi na amri yake, ambapo dhati yake sio sehemu ya maumbile na haitokani na aina ya vitu vilivyoumbwa. Hivyo, dhati ya Mwenyezi Mungu haiwezi kueleweka kwa mwanadamu kwa njia ya ulinganisho na analojia - mfanano na kilichotangulia kuwepo.

Kwa ufupi, Yeye ni nafsi Ambaye kwa elimu ya dhati Yake hakuna kipimo au kigezo chochote kilichopo na kwa ukadiriaji wa uwezo Wake, mamlaka na ujuzi Wake, hatunazo tarakimu wala takwimu zake. Hivi, mwanadamu ni duni sana na asiye na uwezo wa kutambua kitu chochote cha dhati na sifa za ukweli wenye kutokeza kiasi hiki? Kukubali udhaifu wa uwezo wetu na kutoweza kwetu kupata elimu kamili, ya kina na pana ya Mwenyezi Mungu haimaanishi kwamba tumenyimwa kila aina ya ujuzi, uwe mdogo kiasi gani.

Mpangilio wa utaratibu wa ulimwengu unatangaza kwa sauti kubwa sifa Zake kwetu, na tunaweza kuuelewa uwezo na ubunifu usio na mipaka wa Mola Mlezi kutoka kwenye uzuri na manufaa ya maumbile. Maajabu yanayoonekana, kwetu sisi ni dalili ya Dhati Yake ya kipekee.

Mazingatio ya utashi, utambuzi ujuzi na upatanifu wa asili katika mpangilio wa maumbile na mambo yote mbalimbali ya maisha, hufanya iwezekane kwetu kutambua kwamba sifa zote hizi - pamoja na vipengele vingine vyote vinavyozungumzia lengo, mwelekeo na madhumuni ni muhimu vitoke kwenye utashi wa Muumbaji Ambaye Yeye Mwenyewe anazo sifa hizi kabla hazijaakisiwa katika kioo cha maumbile.

Kile kinachokuja kumjua Mwenyezi Mungu na kugusa nafsi Yake ni uwezo usio kifani wa fikra - mwanga wa ghafla ambao kutokea kwenye kile chanzo cha kabla ya umilele ukamulika juu ya mata na kuipatia uwezo wa kupata ujuzi na kusonga mbele kuelekea kwenye ukweli. Ni kutoka ndani ya zawadi hii kuu ya ki-Mungu ambamo elimu ya Mwenyezi Mungu inadhihirishwa.

Uislamu hushughulika na elimu ya Mwenyezi Mungu kwa njia ya wazi na ya simulizi. Qur'ani, chanzo cha msingi wa kujifunzia falsafa ya maisha ya Kiislamu, inatumia mbinu ya kukana na kuthibitisha kwenye swali hili. Kwanza ilikana, kwa njia ya ushahidi wa kusadikika na dalili, kuwepo kwa miungu ya uwongo, kwa sababu katika kuyaendea mafundisho ya juu sana ya upweke, kwanza ni lazima kukana aina zote za miungu ya uwongo na ibada ya mwingine mbali na Allah. Hii ndio hatua ya kwanza muhimu katika njia ya kuuelekea upweke.

Qur'ani inasema:

أَمِ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ آلِهَةً قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ هَـٰذَا ذِكْرُ مَن مَّعِيَ وَذِكْرُ مَن قَبْلِي بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ الْحَقَّ فَهُم مُّعْرِضُونَ ﴿٢٤﴾

"Au wanawaabudu miungu mingine badala yake? Sema: Leteni ushahidi wenu! Huu ni ukumbusho wa hawa walio nami, na ukumbusho wa walio kabla yangu. Lakini wengi wao hawaijui kweli, na kwa hiyo wanapuuza." (Anbiya:21:24).

قُلْ أَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا وَاللَّـهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٧٦﴾

"Sema: Je! Mnawaabudu, badala ya Mwenyezi Mungu, wale ambao hawawezi kukudhuruni wala kukufaeni? Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua." (Maida:5:76).

Yule ambaye amevunja uhusiano wake na upweke wa Mwenyezi Mungu husahau pia, nafasi yake halisi kuhusiana na dunia na uhai na nafasi hiyo inakuwa imetenganishwa na yeye mwenyewe. Kwani namna mbaya kabisa ya mfaraka binafsi ni kukata viunganisho vyake vyote na hali yake ya asili kama mwanadamu. Kinyume chake, pindi mtu anapotenganishwa na asili yake mwenyewe, kwa athari ya mambo ya ndani na ya nje, pia atatengwa na Mungu wake na kufanywa mtumwa na asiyekuwa Mwenyezi Mungu.

Kujiweka chini ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ndipo basi huchukua nafasi ya fikira yote ya kimantiki. Hii inawakilisha kugeuka na kuanza kuabudu maada, kwani kuabudu sanamu na kuweka ubora kwenye maada, zote ni aina za muanguko ambao unamnyang'anya mwanadamu uwezo wake wa asili wa ukuaji.

Tauhiid (Upweke wa Mungu mmoja) tu, ndio nguvu inayomwezesha mwanadamu kukamata tena uumbwaji wa maadili ya binadamu. Kwa kuirudisha tena hadhi yake halisi, mtu huingia katika hali ya uelewano na asili yake mwenyewe ya kibinadamu na asili ya msingi ya viumbe wote, hivyo kufikia muundo kamilifu zaidi wa uhai ukiwa wazi kwa ajili yake. Katika historia yote, miito yote na vuguvugu za kidini zilianza kwa kutangaza upweke wa ki-ungu na utukufu pekee wa Mwenyezi Mungu.

Hakuna fikra ambayo imepata kutokea kwa mwanadamu ambayo ni yenye kuleta matunda zaidi ya utambuzi wa ubunifu na wenye kuhusika zaidi kwenye maeneo mbalimbali ya maisha ya binadamu, kizuizi chenye nguvu zaidi katika upotovu wa mwanadamu, kuliko dhana ya upweke wa Mwenyezi Mungu. Kwa kutumia ushahidi wa wazi kabisa, Qur'ani inamwonyesha mtu njia ya kupata elimu juu ya Mwenyezi Mungu kama ifuatavyo:

أَمْ خُلِقُوا مِنْ غَيْرِ شَيْءٍ أَمْ هُمُ الْخَالِقُونَ ﴿٣٥﴾ أَمْ خَلَقُوا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بَل لَّا يُوقِنُونَ ﴿٣٦﴾

"Ama wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana yakini." (52:35-36).

Qur'ani inamwachia mwanadamu atumie fikira na akili yake ya kawaida ili atambue uwongo wa nadharia mbili hizi - kama mwanadamu ametokea kuwepo mwenyewe tu vivi hivyi, au kama alikuwa amejiumba yeye mwenyewe - kwa kuzifanyia majaribio na kuzichanganua kwenye maabara ya akili yake. Kwa kutafakari juu ya dalili na ishara za Mwenyezi Mungu, atatambua kwa uhakika uliowazi na dhahiri kabisa kile chanzo cha maumbile yote na kuelewa kwamba hakuna tathmini yoyote inayoweza kutolewa juu ya mtindo wowote wa ulimwengu isipokuwa pawepo na akili inayopanga na yenye uwezo inayofanya kazi nyuma yake.

Kwenye Aya zingine, mazingatio ya mwanadamu yameelekezwa kwenye jinsi alivyoumbwa na kutokeza kwake pole pole kutokea kwenye hali ya kutokuwepo kabla. Hivyo, anakuja kutambua kwamba uumbwaji wake wa kipekee, pamoja na maajabu yote uliyonayo, ni dalili na ishara za utashi wa ki-ungu usiyo na ukomo, miale inayopenyeza na kugusa viumbe vingine vyote. Qur'ani inasema:

وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن سُلَالَةٍ مِّن طِينٍ ﴿١٢﴾ ثُمَّ جَعَلْنَاهُ نُطْفَةً فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ ﴿١٣﴾ ثُمَّ خَلَقْنَا النُّطْفَةَ عَلَقَةً فَخَلَقْنَا الْعَلَقَةَ مُضْغَةً فَخَلَقْنَا الْمُضْغَةَ عِظَامًا فَكَسَوْنَا الْعِظَامَ لَحْمًا ثُمَّ أَنشَأْنَاهُ خَلْقًا آخَرَ فَتَبَارَكَ اللَّـهُ أَحْسَنُ الْخَالِقِينَ ﴿١٤﴾

"Na kwa yakini tumemuumba mwanadamu kutokana na asili ya udongo. Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti. Kisha tukaliumba tone kuwa damu iliyoganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa na mifupa tukaifunika na nyama. Kisha tukamfanya kiumbe kamili. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu, Mbora wa waumbaji." (23:12-14).

Wakati ambapo kijusi (mimba) kinapokuwa tayari kuanza kupata mwili na umbo, chembehai zote za macho, masikio, ubongo na viungo vingine, huanza kufanya kazi na huanza utendaji wao usiyo na ukomo. Huu ndio ukweli ambao Qur'ani inaelekeza mazingatii ya mwanadamu. Halafu, Qur'ani inamuuliza mwanadamu swali la kwamba kama maajabu yote haya yanaendana na ile nadharia ya kwamba hakuna Mungu.

Wala sio suala la kwamba mambo kama haya yanathibitisha na kuonesha, kwa msisitizo mkubwa, kuwepo na haja ya mpango, usanifu, mkono unaoongoza ukisukumwa na utashi makini? Hivi inawezekana kwamba chembe hai za mwili ziweze kujifunza kazi zao, zifuatilie malengo yao kwa mtindo sahihi na mpangilio, na kujidhihirisha kimuujiza kiasi hicho katika ulimwengu wa viumbe, bila ya kuwepo nafsi yenye utambuzi na uwezo mkubwa na ambayo inatoa maelekezo?

Qur'ani inajibu swali hili ifuatavyo:

هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٤﴾

"Yeye ndiye Muumbaji, Mtengenezaji, Mtiaji sura, Mwenye majina mazuri kabisa. Kila kilichoko katika mbingu na ardhi kinamtakasa, naye ni Mwenye kushinda, Mwenye hikima." (Hashir:59:24).

Qur'ani inaelezea kila jambo la hisia ambalo mtu analiona karibu yake kama ni kitu kinachohitaji kutafakari na kupata hitimisho lake:

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾ إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَالْفُلْكِ الَّتِي تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِمَا يَنفَعُ النَّاسَ وَمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ السَّمَاءِ مِن مَّاءٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَابَّةٍ وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ الْمُسَخَّرِ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿١٦٤﴾

"Na Mungu wenu ni Mungu mmoja tu, hapanaa Mungu ila Yeye. Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kuhitilafiana usiku na mchana, na marikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na maji anayoyateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza kila aina ya wanyama; na katika mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayoamrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, bila shaka humo zimo Ishara kwa watu wanaozingatia" (Baqarah :2:163-164.

قُلِ انظُرُوا مَاذَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا تُغْنِي الْآيَاتُ وَالنُّذُرُ عَن قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠١﴾

"Sema: Angalieni kwa makini yaliyomo mbinguni na kwenye ardhi! Na Ishara zote na maonyo hayawafai kitu watu wasioamini". (Yunus: 10:101).

Qur'anii pia inataja uchunguzi wa historia ya mwanadamu na watu wa kale pamoja na mabadiliko yote ambayo yamefanyika kama chanzo maalum cha elimu. Qur'ani inamlingania binadamu kuzingatia, ili aweze kugundua ukweli, kwenye ushindi na kushindwa, utukufu na udhalili, bahati na misiba ya watu mbali mbali wa zama za kale, hivyo kwamba kwa kujifunza mpangilio na sheria sahihi za historia, ataweza kunufaika yeye na jamii yake kwa kulinganisha historia ya wakati wake mwenyewe na sheria hizo.

Kwa hiyo Qur'ani inatangaza:

وَكَمْ قَصَمْنَا مِن قَرْيَةٍ كَانَتْ ظَالِمَةً وَأَنشَأْنَا بَعْدَهَا قَوْمًا آخَرِينَ ﴿١١﴾

"Na mingapi katika miji iliyokuwa ikidhulumu tumeiteketeza na tukawasimamisha baada yake watu wengine." (21:11).

قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُمْ سُنَنٌ فَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ ﴿١٣٧﴾

"Kabla yenu zimepita nyendo nyingi; basi tembeeni katika ulimwengu muangalie vipi ulikuwa mwisho wa wanaokanusha" (Imran: 3:137).

Qur'ani pia inatambua dunia ya ndani ya mwanadamu, ambayo inaielezea kwa neno anfus (nafsi) kama chanzo cha tafakari yenye kutoa matunda mazuri na ugunduzi wa ukweli. Inaonyesha umuhimu wake kama ifuatavyo:

سَنُرِيهِمْ آيَاتِنَا فِي الْآفَاقِ وَفِي أَنفُسِهِمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ الْحَقُّ أَوَلَمْ يَكْفِ بِرَبِّكَ أَنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿٥٣﴾

Tutawaonyesha ishara zetu kwa dhahiri kabisa katika dunia na ndani ya nafsi zao, mpaka iwabainikie kwamba Mwenyezi Mungu ni Haki." (Fussilat: 41:53)

وَفِي الْأَرْضِ آيَاتٌ لِّلْمُوقِنِينَ ﴿٢٠﴾ وَفِي أَنفُسِكُمْ أَفَلَا تُبْصِرُونَ ﴿٢١﴾

"Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini. Na pia katika nafsi zenu. Je! Hamwoni? ( Zariyat: 51:20-21).

Kwa maneno mengine ni kwamba kipo chanzo kikubwa cha elimu katika uzuri na mpachano wa mwili wa binadamu, pamoja na viungo vyake vyote na uwezo, matendo yake na athari zake, taratibu zake zilizo sahihi na stadi, nishati zake mbali mbali na silika zake, utambuzi wake, hisia na misisimko yake, yote, ya kinyama na kibinadamu, na hasa zaidi katika uwezo wa kushangaza wa akili na utambuzi ambao mtu amepewa - uwezo ambao bado unabakia kwa kiadi kikubwa haujajulikana, kwani mwanadamu amechukua hatua chache tu katika kuichunguza nguvu hii isiyoonekana na uhusiano wake na umbile la mwili wake.

Qur'ani inatangaza kwamba inatosha kutafakari na kuipima nafsi yako mwenyewe ili uweze kuongozwa kwenye chanzo cha milele na kisichokuwa na ukomo kisichohitajia kitu chochote, chenye ujuzi usio na mipaka, ustadi na uwezo, na ule mfano dhaifu ambao unaonekana katika utu wako. Hapo ndipo utakapojua kwamba ni huo ukweli usio na ukomo ambao umezikusanya mahali pamoja mchanganyiko wenye manufaa kiasi hicho wa vitu asili na kuutokeza kwenye uwanja wa uhai.

Kujulikan kwa dalili za wazi kama hizo na uthibitisho wenye maamuzi, ambao umewekwa wazi mikononi mwako na ndani ya mwili wako mwenyewe ili uweze kutafuta elimu ya Mwenyezi Mungu, hakuna kisingizio kitakachokubaliwa kutoka kwako kwa upotofu na ukanusho. Qur'ani pia inatumia mbinu ya ukanushaji na uthibitisho kwenye suala la sifa za Mwenyezi Mungu. Hivyo, inatoa maelezo ya sifa ambazo kwamba dhati ya Muumbaji inakuwa nazo kama 'sifa za kukubali.' Miongoni mwa hizo ni ujuzi, uwezo, utashi, ukweli kwamba kuwepo Kwake hakukutanguliwa na kutokuwepo na kwamba dhati Yake haina mwanzo, na ukweli kwamba misogeo yote ya dunia inapatikana kutokana na utashi Wake na uwezo Wake.

Qur'ani inasema:

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿٢٢﴾ هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٢٣﴾

"Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, ambaye hapana Mungu isipokuwa Yeye tu. Mwenye kuyajua yaliyofichikana na yanayoonekana. Yeye ndiye Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana aabudiwaye isipokuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye nguvu, Anayefanya analolitaka, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayomshirikisha nayo." (Hashir: 59:22-23).

'Sifa za ukanushaji' ni zile ambazo Mwenyezi Mungu yupo huru nazo. Ni pamoja na ukweli kwamba Mwenyezi Mungu hana mwili na hana mahali; dhati yake takatifu haina mshirika wala wakufanana nayo; Yeye si mfung- wa kwenye mipaka iliyowekwa na ukomo wa hisia; Hakuzaa wala hakuzaliwa; wala hakuna mabadiliko wala msogeo katika dhati Yake, kwani Yeye ni mkamilifu kabisa, na Yeye haikabidhi kazi ya uumbaji kwa yeyote.

Qur'ani inasema:

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾ اللَّـهُ الصَّمَدُ ﴿٢﴾ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ ﴿٣﴾ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ ﴿٤﴾

"Sema; Yeye Mwenyezi Mungu ni Mmoja. Mwenyezi Mungu ndiye anayekusudiwa kwa haja. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anayefanana naye hata mmoja." (Iklas: 112:1-4).

سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٨٠﴾

"Ameepukana Mola Wako, Mola Mwenye enzi na yale wanayomsifu nayo." (37: 180).

Mantiki ya kibinadamu, ambayo bila kupingwa hufikiria kwa namna yenye ukomo, hana uwezo wa kuketi katika kuhukumu utakatifu, kwa sababu lazima tukubali kwamba si rahisi kutambua msingi halisi wa nafsi hiyo ambayo juu yake hakuna kifanani au kilingano cha kuonekana au kufahamika kinachopatikana katika ulimwengu wa maumbile. Madhehebu kubwa sana na mbinu kubwa sana za tafakuri hapa zinaangukia kuwa mawindo ya utatanishi.

Kama vile ambavyo viumbe vyote hai lazima virudi nyuma kwenye asili ambayo kwayo uhai unafanana, kwa nafsi huru ambayo juu yake viumbe vyote vingine vinategemea, hivyo pia, lazima vitokane na chanzo cha uhai, uwezo na ujuzi, kutoka kwenye ile nafsi ambamo humo ndimo sifa hizi na ubora zinamochipukia.

10

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

SOMO LA KUMI

MASHARTI YA LENGO BORA LA IBADA

Mola wa ulimwengu, kama anavyowasilishwa ndani ya Qur'ani, anayo masharti yote muhimu ya lengo bora la ibada. Yeye ndiye muumba wa upendo na aina zote za uzuri, mwanzilishi wa aina zote za uwezo na nguvu. Yeye ni bahari pana ambamo kwenye uso wa wimbi lake dogo sana muogeleaji wa kutafuta elimu na akili yake anasukwasukwa huku na huko kama kitu cha kuchezea. Ni yeye ambaye anayezilinda mbingu zisianguke na dunia isiporomoke. Endapo kwa sekunde moja tu, Atafumba jicho lake la huruma au kuligeuzia mbali na dunia, ulimwengu wote utatoweka na kuvurumishwa kuelekea kwenye kutokuwepo katika hali ya mavumbi. Kule kuwepo na ule uhai wa kila chembehai katika ulimwengu, kwa hiyo kunamtegemea Yeye.

Ni yeye ndiye Anayegawa neema na furaha zote; anayetumiliki sisi na anaweza kutuondoa sote kwa hiari atakavyo. Wakati anapoamuru, agizo hutoka na kuendelea, mara anaposema, "Kuwa!" kiumbe kinatokea kuwepo. Ukweli na uhakika hupata nguvu kutoka kwenye dhati Yake, na uhuru haki na sifa na sifa nyinginezo za ukamilifu zinapatikana kutoka kwenye miale ya sifa Zake. Kukimbia kuelekea Kwake, kutafuta uwezekano wa kuwa karibu na lango lake tukufu, ni kupata mahitaji yenye kufikirika kwa kiwango cha juu sana. Yeyote anayeusalimisha moyo wake kwa Mwenyezi Mungu, hupata mwenzi mwenye upendo na rafiki ampendaye; mtu anayemtegemea Yeye ameyaweka matumaini yake kwenye msingi imara, ambapo yule anayeambatanisha moyo wake kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni windo la njozi za uwongo na anajenga msingi kwenye upepo.

Yeye ambaye anautambua ule msogeo ulio mdogo zaidi unatokea katika maumbile pia anaweza kutuamulia njia inayoelekea kwenye furaha na kuweka njia ya maisha na mfumo wa uhusiano wa kibinadamu unaotenda kufuatana na kanuni ambazo Ameziweka katika mpango wa uumbaji. Yeye, hata hivyo anayatambua manufaa yetu halisi, na vile vile ni haki Yake kuweka njia kwa ajili yetu kama matokeo ya kimantiki na ni matokeo ya asili la utakatifu Wake. Kutenda kwa mujibu wa mpango ambao Ameuweka ndio uhakika maalum tu kwa ajili yetu sisi kupanda kuelekea Kwake. Inawezekanaje kwamba mtu awe na mapenzi juu ya ukweli na uadilifu na kwamba yuko tayari hata kujitolea mhanga uhai wake kwa sababu hiyo, alimradi tu awe anajua chanzo asili yake?

Kama kitu kinastahili kuabudiwa haiwezekani kiwe kingine isipokuwa Muumba ambaye ndiye mhimili wa viumbe vyote. Hakuna kitu au mtu yeyote mwenye daraja kama hilo na akastahili kusifiwa na kutumikiwa na mwanadamu. Malengo mengine yote isipokuwa Mwenyezi Mungu hayana uhakika na ubora na hayajitoshelezi ndani yake, na yenyewe tu; ni viwakilishi na hutumika tu kama njia ya kupata viwango vya juu zaidi kuliko yenyewe.

Sifa kuu ambazo zinashawishi ibada ya mwanadamu zinakuwa ndio watoaji wa neema zote na kuwa watambuzi wa kila uwezekano, mahitaji, uwezo na nguvu zilizomo kwenye mwili na roho wa binadamu. Sifa hizi ni zake Mwenyezi Mungu pekee; viumbe vyote vinakuwa vyenye kuhitajia na hutegemea juu ya nafsi hiyo ambayo Ipo kwa uwezo wa dhati Yake Yenyewe. Msafara wa uhai wakati wote unaosonga mbele kuelekea Kwake kwa njia ya msaada Wake, amri zake huteremka bila ukomo za kila kitu (japo chembe ndogo) hapa ulimwenguni. Kujisalimisha halisi na ibada ni vyake, tena pekee chini ya Dhati Yake Tukufu Kabisa. Kuwepo Kwake kutukufu, kusikoingiliwa kati na hata sekunde moja ya kutokuwepo, kunahisiwa kwenye moyo wa kila kiini cha chembe ya uhai. Vitu vyote isipokuwa Mwenyezi Mungu hufanana na sisi kwa kuwa udhaifu na upungufu vinakuwepo juu yao. Kwa hiyo, havistahili sisi kujisalimisha kwavyo na havistahili kutwaa mamlaka juu ya sehemu yoyote ya milki ya Mwenyezi Mungu ambayo ni uwanda wote mpanawa uhai. Mwanadamu pia ni kiumbe bora na chenye thamani mno kuweza kutawaliwa na kudhalilishwa na kitu kingine chochote mbali na Mwenyezi Mungu.

Katika uwanda wote mzima wa uhai, ni Mwenyezi Mungu pekee Anayestahiki kusifiwa na mwanadamu. Mwanadamu lazima atoe kwenye mapenzi yake kwa Mwenyezi Mungu, kwenye jitihada zake za kujisogeza karibu Naye na kupata radhi Zake, kipaumbele juu ya viumbe na malengo mengine ya upendo. Hali hii itasababisha kumboresha mwanadamu na kuzidisha thamani yake, kwani mwanadamu ni tone dogo sana na kama hakuungana na bahari (maumbile yote) ataangamizwa na wimbi la uovu, na kukaushwa na joto la machafuko. Mwanadamu hupata utu wake halisi na kuwa wa milele pale anapojiambatanisha na kile chanzo chenye kutia nuru, ambapo Mwenyezi Mungu hutoa maana ya dunia yake naye anakuwa mfasiri wa matukio yote yahusuyo maisha yake. Ni kwa maana hii kuwa dunia za wanadamu zinaweza kuwa ama ni pana na kubwa sana au finyu na zinazobana.

Amirul-Mu'minin Ali(a.s) anasema anapozungumzia udhaifu wa mwanadamu na uwezo wake pungufu:

"Mambo ya mwanadamu ni mageni na ya ajabu ilioje! Kama anakuwa na matumaini kuhusu tamaa fulani, ulafi utamfanya adharauliwe; tamaa itamletea choyo, na choyo kitamuangamiza. Kama atashikwa na kukosa matumaini, huzuni na masikitiko vitamuua. Kama akipata furaha na bahati njema, atashindwa kuvihifadhi. Endapo atashikwa na hofu na woga vitamfanya achanganyikiwe. Endapo atapewa usalama wa kutosha, atakuwa mzembe. Kama atarudishiwa neema zake, anakuwa kiburi na muasi. Kama anapatwa na balaa, atafedheheka kwa masikitiko na huzuni. Endapo mwanadamu anapata utajiri, anakithirisha majivuno. Endapo anakumbwa na ufukara, atatumbukizwa kwenye mateso. Endapo anadhoofishwa na njaa, atashindwa kunyanyuka kutoka ardhini. Endapo anakula kupita kiasi, ghasia tumboni mwake itamkosesha raha. Kwa hiyo upungufu wote katika maisha ya mwanadamu una madhara kwake, na ziada zote ile zinasababisha uovu na maangamizo." [27]

Kuzungumzia kwa ujumla, uadilifu, ubora, wema na sifa zingine zinazobeba heshima na utukufu ama lazima ziwe za uwongo na za kudhania au lazima tuyaone maadili haya kuwa ni ya kweli na muhimu, yenye kutokana na msingi wa utambuzi wa dhamira na silika. Katika suala hili la pili, lazima tukubali kwa unyeyekevu kwenye maumbile ya kilimwengu na ukamilifu wa dhahiri unaoenea pamoja na faida (manufaa), uhai na uwezo, na ambamo maadili yote yanatokana namo.

Tunapoliangalia jambo lenyewe kwa uangalifu, tunaona kwamba viumbe vyote visivyo na idadi ambavyo vinaishi ulimwenguni, pamoja na upendo na tamaa ambayo imeota mizizi ndani ya nafsi zetu, vyote hukusanyika mahali pamoja, vyote vinarudi kwenye chanzo kimoja - Mwenyezi Mungu. Asili yenyewe hasa na uhalisi wa dunia inafanana na uwiano wake, uhusiano na mwambatano kwa Mwenyezi Mungu. Kiumbe hupanda tena kwa kufuata njia tofauti hadi kwenye sehemu kilipoanzia na ambayo kiliteremkia, na sehemu hiyo pekee ndio inastahili mapenzi na kujitoa kwa mwanadamu. Pindi binadamu anapogundua sehemu hii, huvutiwa sana na uzuri wake halisi na ukamilifu kiasi kwamba anasahau vingine vyote.

Tunanona kwamba vitu vyote vimejitokeza kwenye kutokuwepo na kuja katika hali ya kuwepo na kwamba katika kipindi chote wakati cha kuwepo kwao, imma kipindi kifupi au kirefu, vinategemea kwenye chanzo cha nje yao vyenyewe juu ya misaada na riziki; vitu hivi vimewekwa alama ya utegemezi usiofutika na kukosa kujitawala.

Ikiwa lengo bora la ibada tunalotafuta na ambalo tunajaribu kuliendea lingekuwa halitambui matatizo tunayoyapata na hali ya dunia; kama lingekuwa haliwezi kutosheleza matakwa na tamaa zetu, likawa lenye udhaifu na mapungufu tele kama vile sisi tu na likawa katika kundi moja kama lile tulimo sisi - lisiingeweza kuwa kusudio letu la mwisho na lengo letu la mwisho kabisa au kuwa na thamani kamili.

Tunapotafuta utimilizaji wa matakwa yetu kwa njia ya ibada, ni Mwenyezi Mungu peke yake Anayeweza kutujibu. Qur'ani inasema:

إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ عِبَادٌ أَمْثَالُكُمْ فَادْعُوهُمْ فَلْيَسْتَجِيبُوا لَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٩٤﴾

"Hakika wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu ni waja mfano wenu nyingi. Basi hebu waombeni, nao wakuitikieni; kama mnasema kweli." (7:194).

Amirul-Mu'minin(a.s) alipokuwa anaomba dua kwa Mola Wake kwenye msikiti wa Kufah alisema: "Ewe Mola Wangu, Ewe Mola Wangu! Wewe ni Mwenyezi Mungu na Mkuu na mimi ni mtumwa wako duni nisiye na thamani. Nani awezaye kuonyesha huruma kwa mtumwa wake asiye na thamani isipokuwa Mwenyezi Mungu Mkuu? Ewe Mola Wangu, Ewe Mola Wangu! Wewe unazo nguvu na uwezo mimi ni mnyonge na dhaifu; nisiyekuwa na nguvu na uwezo, ni nani ambaye anaweza kuonyesha huruma kwa wanyonge?

Ewe Mola Wangu, Ewe Mola Wangu! Ni Wewe Ambye humkirimu mwombaji, na mimi ni mwombaji kwenye lango lako. Nani atakayeonyesha huruma kwa mwombaji isipokuwa yule aliye mpaji na mkarimu mno? Ewe Mola Wangu, Ewe Mola Wangu! Wewe ni uzima wa milele na mimi ni kiumbe niliyekadiriwa kutoweka. Nani atakayemhurumia yule mtu aliyekadiriwa kuangamia isipokuwa ile dhati ya milele, na ya kudumu? Ewe Mola Wangu, Ewe Mola Wangu! Wewe ndiye mwongozaji unayeelekeza njia, na mimi nimepotea na kukanganyikiwa. Nani atakuwa na huruma na yule aliyepotea na kukanganyikiwa kama siye yule mwongozaji anayeelekeza njia?

Ewe Mola Wangu, Ewe Mola Wangu! Nihurumie kwa huruma zako zisizo na ukomo, nikubali na utosheleke na mimi katika ukarimu Wako, upendeleo, na wema wako, Ewe Mwenyezi Mungu, mmiliki wa ukarimu, upendeleo na wema, na katika huruma zako zote, Ewe mwenye huruma zaidi ya wenye huruma!" [28]

Kwa hiyo kuonyesha heshima kuu kwa yeyote asiye Mwenyezi Mungu, kujielekeza mwenyewe kwa mwingine mbali na dhati Yake halisi, si njia iliyo halali; mbali na Mwenyezi Mungu, hapana chochote kinachoweza kuwa na athari hata kwa kiwango kidogo tu juu ya mustakabali wetu halisi. Kama lengo la kuabudiwa kinastahili utii na upendo wa mwanadamu na lina uwezo wa kumnyanyua yeye kwenye vilele vya furaha kuu, lengo hilo la ibada lazima lisiwe na dosari na upungufu wowote ule. Miale yake ya umilele lazima iguse viumbe vyote kwa kuruzuku na maisha, na uzuri wake lazima usababishe kila mtu mwenye umaizi kupiga magoti chini mbele yake. Kwa kule kuwa na uwezo usio na ukomo, hukata kiu kali ya nafsi zetu, na kuipata elimu yake, si vinginevyo mbali na kupata chanzo cha msingi cha asili yetu halisi.

Kama tunachagua lengo la upendo na ibada mbali ya Mwenyezi Mungu, linaweza kuwa na uwezo fulani na kuweza kukamilisha matamanio yetu hadi kiwango fulani, lakini pindi tufikapo kwenye kiwango hicho, halitakuwa lengo la upendo na ibada tena kwetu sisi. Halitaweza tena kutushawishi na kutuvutia, kinyume chake, litasababisha sisi tukwame hapo hapo. Kwani sio tu kwamba kitashindwa kutosheleza silika zetu za tamaa ya ibada, litatuzuia kutafakari kuhusu manufaa mengine yoyote ya juu zaidi na kutufungia kwenye mduara mfinyu, kwa jinsi ambavyo tunawa

hatuna dhamira yoyote tena ya kusonga mbele au kunyanyuka. Ikiwa lengo tunalochagua kuabudu na kulipenda ni duni kwetu, kamwe halitaweza kutufanya sisi tunyanyuke na kutakasa nafsi zetu. Mwelekeo wetu kwenye lengo hilo, kinyume chake, utatuburuza na kuturudisha nyuma, na tutakuwa kama mshale wa dira ambao umeelekezwa pembeni mwa nguzo kwa nguvu ya athari ya eneo geni kabisa la sumaku. Matokeo yake yatakuwa ni kupoteza kabisa mwelekeo; mateso ya milele yatakuwa ndio mustakabali wa mwanadamu usiokwepeka.

IBADA, NJIA BORA YA BINADAMU YA KUONYESHA SHUKRANI

Lengo la kuabudiwa linaweza kutoa maelekezo kwa mwenendo wa mwanadamu na kumuondolea giza lake kwa mng'aro wake wakati linapoweza kumpatia mifano bora, linapokuwa limejaaliwa uhai wa hakika na ulionyanyuliwa kwa daraja, na kuwa ni chanzo cha athari, na kuwa asili hasa ya uimara na hali ya kudumu. Halafu, lengo hilo la kuabudiwa hutoa athari za ndani zaidi kwa mwanadamu na kumwongoza katika fikra na matendo yake. Linarahisishia asili ya mwanadamu, ile sehemu yake inayolelewa na hekima ya ki-Mungu katika utafutaji wa ukamilifu wake.

Jitihada yoyote au msogeo kwa upande wa binadamu kujichagulia mwelekeo mbaya, kufuata njia isiyo sahihi katika maisha, matokeo yake yatakuwa kutenganishwa na nafsi yake, kupoteza kuridhika kwake, na kubadilisha utu wake. Mwanadamu hataweza kujitambua kwa usahihi kama atakuwa amejitenga na Muumba wake. Kumsahau Mwenyezi Mungu maana yake ni kujisahau mwenyewe, kutokuyaelewa malengo ya jumla ya maisha ya binadamu na dunia inayomzunguka, na kushindwa kutafakari kuhusu aina yoyote ya maadili ya juu zaidi.

Kama vile kujiambatanisha na mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu kunavyomtenga binadamu na nafsi yake mwenyewe na kumgeuza kuwa kama mashine fulani ya kibaiolojia inayotembea, hivyo, pia ndivyo ilivyo kwa mtu anayemtegemea Mwenyezi Mungu na kuomba dua mbele ya lango lake kunavyomchukua mtu asiyekuwa na uelekeo wowote, ambaye hana kabisa maisha ya kiroho, kutoka kwenye kina kirefu cha bahari ya kutojali, kumhuisha na kumrudisha kwenye utu wake tena. Kwa kumwabudu Mwenyezi Mungu, uwezo wa kiroho na nguvu za kimbinguni ndani ya mwanadamu zinastawishwa. Mwanadamu huelewa hali ya uduni wa umbile lake lisilo na thamani, matumaini na tamaa na kuyaona mapungufu na udhaifu bila ya utu wake mwenyewe. Kwa ufupi, hujigundua mwenyewe kama alivyo hasa.

Kumtambua Mwenyezi Mungu na kukimbilia kwenye kile chanzo kisichoonekana cha viumbe vyote huwa kunatia nuru na kuuamsha moyo. Inafurahisha sana, furaha ambayo haiwezi kulinganishwa na furaha ya ile dunia ya kimaada ya pande tatu. Ni kupitia kwa mtu kujielekeza mwenyewe kwenye nadharia hiyo, yaani, ukweli wa kitu kisicho cha kimaada, kwamba fikira huchukua nafasi ya juu sana na maadili hugeuzwa. Amirul-Mu'minin, Ali(a.s) anazungumzia kuhusu athari ya ajabu ya utambuzi wa Mwenyezi Mungu katika nyoyo za watu kama ifuatavyo:

"Muumba Mwenye Nguvu zote ameufanya umtambuzi juu Yake kuwa ni njia ya kutakasa moyo. Ni kupitia kumtambua Mwenyezi Mungu ambapo nyoyo zilizokufa masikio huanza kusikia, nyoyo zilizopofuka huanza kuona, nyoyo zenye uasi hulainika na kuwa tiifu." [29] .

Pia anasema:"Ee Mola Wangu! Wewe ni mwenza mzuri zaidi kwa wale wanaokupenda Wewe na ni chanzo kizuri zaidi cha kuponya kwa wote wanaoweka mategemeo yao juu Yako. Unawaona wao katika hali zao za ndani na matendo yao ya nje na unatambua undani wa nyoyo zao. Unajua kiwango cha utambuzi na ujuzi wao, na siri zao zipo wazi Kwako. Nyoyo zao hutetemeka zinapotenganishwa na Wewe, na kama upweke wao unawasababishia woga na wasi wasi, utambuzi wao juu Yako huwapa faraja, na kama wanakumbwa na shida na matatizo, ni Kwako pekee ndiko yaliko makimbilio yao." [30]

Imam Sajjad(a.s) , yule aliye mfano bora wa usafi na uadilifu ambaye alikuwa na dhamana isiyovunjika na Mola Wake, anatuonyesha katika dua zake za maombi, udhihirisho wa hali ya juu sana wa upendo. Huu ulikuwa upendo uliotakasika ambao uliuwasha moto utu wake wote, na ingawa nafsi yake ilikandamizwa sana na huzuni ya kibinadamu ya kutenganishwa, ubawa wa upendo wenye nguvu kubwa ulimwezesha kupaa juu kwenye mbingu zisizo na ukomo, kwa hiyo, kwa utiifu na unyenyekevu usioelezeka, yeye aliomba kwenye lango la Mwenyezi Mungu, wa milele:

"Ee Mola Wangu! Nimehamia kwenye msamaha wako na nimetoka kuiendea huruma Yako. Kwa shauku kubwa ninahitaji msamaha wako na ninategemea juu ya ukarimu wako, kwani hakuna chochote katika tabia yangu cha kuweza kunifanya mimi nistahiki kusamehewa, na upole Wako tu ndio matumaini yangu pekee. "Ewe Mwenyezi Mungu, niongoze kwenye njia iliyo nzuri zaidi na ujaalie kwamba nifariki nikiwa muumini katika dini Yako na nifufuliwe kama muumini katika dini Yako.

"Ewe Mola Wangu Ninayekuabudu! Oh, Ewe ambaye msaada wako, walio watenda dhambi wanauomba kupitia huruma Yako! Oh, Ewe ambaye katika kukumbuka ukarimu wako, wanyonge hutafuta kimbilio! Oh, Ewe Ambaye kwa kukuogopa Wewe, wenye dhambi hulia kwa uchungu!

"Ewe chanzo cha utulivu juu ya nyoyo za wale ambao wamehamishwa makwao kwa hofu! Ewe mliwazaji wa wale ambao wanahuzunika kwa nyoyo zilizovunjika! Ewe unayewasaidia wenye upweke, msaidizi wa waliotupwa na wenye kuhitaji! Mimi ni yule mja ambaye nimeitika kwa utiifu pale ulipowaamuru watu waje Kwako. "Ewe Mola Wangu! Mimi hapa nimesujudu juu ya udongo kwenye lango Lako. Ewe Mwenyezi Mungu, ikiwa unaonyesha huruma kwa yeyote anayekuja Kwako kwa maombi na dua basi naomba nifanye niwe na bidii ya dhati katika dua zangu, au ikiwa unamsamehe kila mwenye kulia mbele Yako, basi naomba unifanye niharakishe kulia.

"Ewe Mwenyezi Mungu, usimkatishe tamaa yule ambaye haoni mpaji isipokuwa Wewe; usinisukumie mbali kwa mkono wa kukataa, kwa sasa ambapo nimesimama hapa kwenye lango Lako."[31] Yeyote anayetaka kuelewa maana ya kina ya dua lazima atambue kwamba maelezo ya busara na maamuzi ya kimantiki hayawezi kutoa uelewa wa kina juu ya maswali yanayogusa nuru ya kiroho.

Qur'ani tukufu inaeleza tabia na njia ya maisha ya wasioamini na wayakinifu kama ifuatavyo:

وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَعْمَالُهُمْ كَسَرَابٍ بِقِيعَةٍ يَحْسَبُهُ الظَّمْآنُ مَاءً حَتَّىٰ إِذَا جَاءَهُ لَمْ يَجِدْهُ ﴿٣٩﴾

"Na waliokufuru vitendo vyao ni kama sarabi (mazigazi) uwandani. Mwenye kiu huyadhania ni maji. Hata ayafikiapo hapati chochote."( 24:39),

لَهُ دَعْوَةُ الْحَقِّ وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَسْتَجِيبُونَ لَهُم بِشَيْءٍ إِلَّا كَبَاسِطِ كَفَّيْهِ إِلَى الْمَاءِ لِيَبْلُغَ فَاهُ وَمَا هُوَ بِبَالِغِهِ وَمَا دُعَاءُ الْكَافِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَالٍ ﴿١٤﴾

"Maombi ya haki ni Kwake Yeye tu. Na hao wanaowaomba badala yake hawawajibu chochote; bali ni kama mwenye kunyoosha viganja vyake kwenye maji ili yafike kinywani mwake lakini hayafiki. Na maombi ya makafiri hayako ila katika upotovu." (13:14).

مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتًا وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنكَبُوتِ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٤١﴾

"Mfano wa wale waliochukua miungu badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui ajitandiaye nyumba. Na hakika nyumba mbovu mno kuliko zote ni nyumba ya buibui, laiti wangelijua" (29:41).

مَّثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ أَعْمَالُهُمْ كَرَمَادٍ اشْتَدَّتْ بِهِ الرِّيحُ فِي يَوْمٍ عَاصِفٍ لَّا يَقْدِرُونَ مِمَّا كَسَبُوا عَلَىٰ شَيْءٍ ذَٰلِكَ هُوَ الضَّلَالُ الْبَعِيدُ ﴿١٨﴾

"Mfano wa waliomkufuru Mola wao vitendo vyao ni kama majivu yanayopeperushwa kwa nguvu za upepo katika siku ya kimbunga. Hawawezi kupata chochote katika waliyoyafanya. Huo ndio upotovu wa mbali" (14:18).

Udhihirisho wa kiwango cha juu sana wa hali ya shukurani ambao mwanadamu anaweza kufanya kwenye lango la lengo lake la ibada ni dua, kule kutangaza imani ya mapenzi juu ya ukamilifu Wake halisi na bidii juu yake. Anafanya hivi kwa ulingano na maumbile yote, kwa sababu viumbe vyote humsifu na kumtukuza Mwenyezi Mungu. Qur'ani inasema:

تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ وَلَـٰكِن لَّا تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا ﴿٤٤﴾

Zinamtukuza mbingu saba na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake. Na hapana chochote ila kinamtukuza kwa sifa zake njema. Lakini ninyi hamfahamu kutukuza kwao. Hakika Yeye ni Mpole, na Mwingi wa maghfira." (17:44).

Kwa kawaida ibada hii na utukuzaji ni vitendo ambavyo havimletei Mwenyezi Mungu manufaa japo madogo, kwani Yeye anao ukamilifu wote kwa kiwango kisicho na ukomo na wala sio dunia ama binadamu anayeweza kuongeza kitu chochote Kwake au kuchukua chochote kutoka Kwake. Hivi inaingia akilini kwa hali yoyote ile kwamba, Angemuumba mwanadamu kwa sababu ya kunufaika kutokana na ibada na kumtukuza kwake. Kinyume chake, ni mwanadamu ndiye ambaye, kwa kupata elimu juu ya Dhati ya hali ya juu sana na kumwabudu Yeye katika utukufu Wake, hufikia lengo lake la mwisho na ukamilifu halisi.

Profesa Ravaillet, mwanafalsafa maarufu na bingwa wa fizikia, anayo haya machache yafuatayo ya kusema kuhusu utambuzi wa ulimwengu: "Kosmolojia mpya inasema kwamba atomu na molekuli zinatambua zinafanya nini; katika maana ya kawaida ya usemi huo; vitu hivi vina utambuzi wa kazi zinazofanya na mwenendo wa maisha yao. Utambuzi wao huu ni bora zaidi ya ujuzi wa bingwa wa fizikia, kwa sababu chote anachofahamu bingwa wa fizikia juu ya atomu ni kwamba kama isingekuwa inagusika na kutambulika, hakuna mtu ambaye angejua chochote kuihusu hiyo.

"Miili, msogeo, kasi, mawazo ya hapa na pale, mnururisho, ulingano, nafasi, anga, umbali pamoja na vitu vingine vingi - vyote vilikuja kuwepo kwa sababu ya atomu. Endapo atomu haingekuwepo, chanzo cha viumbe vyote vya kustaajabisha kingekuwa nini? Upo uhusiano huo huo baina ya utambuzi na mwili kama ilivyo baina ya msogeo na mtuamo, au vipengele chanya na hasi vya mwendo.

"Sasa, angahewa, ikichukuliwa kama ilivyo kwa ujumla wake, sio pofu. Kama unakumbuka tulionyesha, tulipokuwa tunachunguza eneo la uoni, kwamba jicho sio kile kipengele cha msingi na uamuzi. Kwa kuwa limepangiwa mahali maalum katika dunia, kwa mujibu wa mazingira yenye mipaka, ya jamii ya binadamu na viumbe vingine vya dunia, lina eneo maalum finyu la kimwili ambamo hufanya kazi ndani yake. Lakini kuhusu angahewa baina ya dunia na jua, baina ya jua na kundi la nyota, na baina ya kundi la nyota na sayari kubwa sana za mbali, ambamo nguvu kubwa zenye masafa marefu mno zinashughulika katika kubadilishana nishati - huko, kiungo kama jicho cha viumbe vya duniani halina fursa kujionyesha lenyewe au kudhihirisha jinsi linavyo fanya kazi.

"Lakini hasa kwa sababu hii hutuwezi kuamini kwamba kunakuweko na ukosefu wa utambuzi na ufahamu kwenye nyanja hiyo kwa ajili ya kubadilishana nishati kubwa sana na nguvu inayotawaliwa na kununi ya mvutano, ulingano, msogeo, mwanga na nguvu ya mzunguko wa kati. Upofu unakuwa haupo kwenye vitu hivi vya ajabu, na hata chembechembe za mwanga haziwezi kufikiriwa kama kitu kinachofanana na msambaza barua asiye na elimu, ambaye kazi ni ile tu ya kuwasilisha barua ambazo hawezi kuzisoma."[32] .