MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE 0%

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE Mwandishi:
: SALMANI SHOU
Kundi: Misingi mikuu ya Dini

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

Mwandishi: KIMEANDIKWA NA SAYYID MUJTABAA MUUSAWIY LARI
: SALMANI SHOU
Kundi:

Matembeleo: 27580
Pakua: 2669

Maelezo zaidi:

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 28 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 27580 / Pakua: 2669
Kiwango Kiwango Kiwango
MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

Mwandishi:
Swahili

13

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

SOMO LA KUMI NA TATU

ELIMU YA MWENYEZI MUNGU ISIYO NA MIPAKA

Muumbaji ambaye hawezi kuzingirwa na mahali, Ambaye Dhati yake haiwezi kuwekewa ukomo, Ambaye uhai wake umeenea kila sehemu ya mbingu na dunia - Muumbaji kama huyu kwa kawaida anatambua vitu vyote, hapana kitu kilichomo katika mpangilio wote wa maumbile ambamo miale yenye nuru kali ya elimu yake haikiangazii.

Matukio yanayotokea sehemu za mbali sana za ulimwengu, matukio yaliyotokea mabilioni ya miaka iliyopita au ambayo yatatokea mabilioni ya miaka ya wakati ujao baadaye - yote yamo ndani katika ujuzi wake, na majaribio makubwa, mapana sana katika kuitafsiri elimu yake, hayana budi kwa hiyo kutofanikiwa.

Ili kuweza kuuelewa upeo mkubwa wa elimu Yake, tunapanua wigo wa fikra zetu, tunatumia akili zetu kutafakari na kutafiti, na kujaribu kusonga mbele kuelekea lengo letu tukiwa na akili nzuri. Mambo mengine yote yakishindikana, hata hivyo, chombo chetu cha kiakili hupungukiwa ustadi unaohitajika kufikia lengo hilo. Kama tungekuwa tuwepo kila mahali kwa namna ile ile ambayo tunaishi mahali maalum kwa muda uliopangwa, ili kwamba hakungekuwa na mahali ambapo panakoseshwa kuwepo kwetu sisi, hakuna kitu kingefichikana kwetu na tungetambua kila kitu.

Kwetu sisi, dunia ya maumbile imegawanywa katika sehemu mbili: sehemu tunayoiona dhahiri na ile tusiyoiona. Vitu "vimefichikana" kwa maana kwamba, ukweli fulani, ambao hauna ukomo na usio na umbile, hauwezi kutambuliwa na milango ya fahamu za nje. Ni muhimu kukumbuka kwamba mfumo wote wa uhai hauwi na mambo yaliyomo kwenye upeo wa sayansi za kutegemea majaribio. Ili kuzielewa siri na miujiza ya maumbile, tunahijati, kama ilivyo kuwa, jukwaa la kujiinulia (kielimu). Muinuko tunaoweza kufika unategemea nguvu ya akili yetu tuliyonayo na kiwango cha uelewa wetu unaosukuma mbele mwinuko wetu. Pindi tunapokuwa na jukwaa linalofaa, ukweli mwingi utakuwa ni wenye kujulikana kwetu.

Kwa kupitia matumizi ya neno ghaibu (fichwa) Qur'ani Tukufu inamfunulia mwanadamu mwonekano mpana wa ukweli halisi. Mitumbe wa Mwenyezi Mungu pia wamejitahidi kuunyanyua utambuzi wa mwanadamu juu ya ulimwengu ulioumbwa hadi kwenye kiwango kinachojumuisha visivyo na ukomo na vyenye ukomo na mipaka ya visivyoonekana na vipimo vya vinavyoonekana. Kwa upande wa Mwenyezi Mungu, hayo "yaliyofichika" hayapatikani kamwe; kwake Yeye, ulimwengu wote 'unaonekana.'.Qur'ani inasema:

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿٢٢﴾

" ..Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayoonekana. Yeye ni Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu." (59:22).

Chochote kilichotengenezwa na binadamu kinatokana na ustadi, akili na ujuzi wa mtu aliyekitengeneza. Jinsi kitu hicho kitakavyokuwa kigumu kiufundi na kisafi zaidi, ndivyo kitakavyoonyesha wazi wazi ukubwa na upana wa elimu ya mtengenezaji wake, na ndivyo kwa ukamilifu zaidi kitakavyozidi kuthibitisha uwezo wake wa kubuni na kuunda. Kazi za mikono za mwanadamu haziwezi kulinganishwa kwa hali yoyote na ule mwujiza na utukufu ya maumbile. Hata hivyo, kwa upande wetu inatuashiria kwamba ule utaratibu wa ulinganifu na mpangilio wa ulimwengu, na kuonekana kwa akili nyingi kwenye mtindo huu ulio mpana, mzuri na wa kustaajabisha mno wa maumbile, lazima uwe unaonyesha kwa umuhimu kwamba mtayarishaji mwenye kuupanga lazima awe na elimu kubwa isiyo na mipaka. Mpangilio wa ulimwengu ndio uthibitisho wenye nguvu zaidi juu ya kuwepo kwa dhati ambayo inafurika kwa elimu, utashi, utambuzi na hekima na imebuni maajabu ya maumbile kwa mujibu wa mpango uliokadiriwa kwa ufasaha na usahihi. Dalili za ujuzi Wake usio na ukomo unaonekana wazi kwenye kila sehemu ya kila kiumbe.

Majaribio na nadharia za wanasayansi yanatoa uthibitisho kwa yeyote anayeutaka kuhusu ujuzi wa Mwenyezi Mungu usio na mipaka na kujidhihirisha kwake kwenye wadudu, wanyama na katika nyanja ya mimea. Mwenyezi Mungu ana utambuzi wa njia zipitamo nyota angani, dunia ya nyota nyingi za mbali sana iliyojaa ghasia na mzunguko wa makundi makubwa ya nyota; wa vitu vyote vya kabla ya umilele na baada ya umilele; wa jumla ya idadi yote ya chembechembe ndani ya maumbile yote ya mbinguni; wa miondoko ya mabilioni ya viumbe, vikubwa na vidogo, vile vinavyotembea kwenye mgongo wa dunia na ndani ya vina vya bahari; wa desturi na kanuni zinazodhibiti maumbile bila ya kukosea; wa vipengele vya mambo yote, vilivyofichika na vya dhahiri. Yeye anaijua pia ile mikanganyiko yenye kufadhaisha, vizuri zaidi kuliko wanavyoijua wao wenyewe.

Sikiliza tena Qur'ani inasema nini:

أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٤﴾

"Je! Hivi asijue Yeye aliyeumba? Naye ndiye mjuzi wa ya siri Mwenye habari? (67:14).

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَخْفَىٰ عَلَيْهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ ﴿٥﴾

"Hakika hakifichiki Kwake Mwenyezi Mungu kitu chochote kilichomo ardhini au mbinguni."(3:5).

Wataalam wa sayansi ya viumbe wanafahamu vema zaidi kuliko wengine kuhusu miujiza yenye kutatiza na ya sahihi ambayo imepandikizwa kwenye kila chembe ya maumbile; wanatambua kutokana na uchunguzi na utafiti wao wa mahesabu mbalimbali ambayo yamewekwa ndani ya viumbe vyote, vile vyenye uhai na visivyo na uhai, kwenye seli na matone; wa aina mbali mbali ya matendo na matokeo, ya nje na ya ndani, yale yanayofanyika ndani mwao, na athari za vitu na maudhui zao.

Hivyo, wanashuhudia ishara za hekima ya kushangaza ya Mwenyezi Mungu na ujuzi usio na ukomo katika maumbile au kama Qur'ani inavyoliweka, " ..katika upeo wa mbali." (41:53).

Zaidi ya wengine, wanasayansi hao wamepata fununu ya sifa za Mwenyezi Mungu na ukamilifu Wake, ikiwa ni pamoja na ujuzi Wake usio na mipaka, na endapo hawakatai wito wa dhamira zao, pia watatambua kuwepo kwa Muumbaji kwa uwazi zaidi. Mwanafikra fulani alisema; "Dunia yetu inafanana na dhana kubwa kuliko inavyofanana na mashine kubwa. Kama nadharia au ufasiri wa kisayansi, inaweza kusemekana kwamba dunia ni matokeo ya dhana kubwa, udhihiri wa fikira na dhana iliyo kubwa kuliko yetu. Fikra ya kisayansi inaelekea kusonga kuelekea upande wa nadharia hii."

Ujuzi wa Mwenyezi Mungu haukomeshei kwenye mambo yalivyopita au matukio na mambo ya sasa; ujuzi Wake wa wakati ujao ni sawa kabisa na ule ujuzi wa wakati huu. Ujuzi wa Mwenyezi Mungu, ni kusema kwamba ni wa "papo hapo" katika maana kamili ya neno lenyewe. Sio muhimu kwanza kabisa kwamba pawepo na kitu cha kielimu ambamo ujuzi Wake upasike kujiambatanisha nacho. Vitu vyote vinabakia wazi mbele Yake, kwani kwa wakati huo huo dhati Yake tukufu ingawa ni nyingine tofauti kabisa na viumbe na vitu vyote, pia haikutengana mbali navyo; vitu vyote, vilivyopita na vya wakati ujao; vyote viko kwenye hadhira Yake ya moja kwa moja bila kuingiliwa.

Ali(a.s) Amirul-Mu'minin, anasema:"Yeye Anajua vitu vyote, lakini si kwa kutumia njia au vifaa; ambavyo kutokuwepo kwao kungeweka ukomo wa elimu Yake. Hakuna kitu kilichoongezwa kiitwacho elimu kilichoingilia kati baina Yake na vitu vya ujuzi Wake; hakuna kitu chochote isipokuwa dhati Yake pekee." [39] Hapa, Ali(a.s) anazungumzia kanuni ya kiteolojia kwamba utambuzi wa mambo wa Mwenyezi Mungu ni wa moja kwa moja na wa papo hapo. Katika ujuzi wake wa vitu, Mwenyezi Mungu hana haja ya mifumo ya kiakili ambayo ndio msingi wa elimu inayopatikana. Angekuwa apate ujuzi Wake kwa kutumia mifumo hiyo, hali ya kuhitaji ingejitokeza ndani Yake, ambapo Yeye ameepukana na kuhitaji kabisa.

Yule ambaye kutoka Kwake dunia na vilivyomo humo vimepatikana, ambaye anaweza kutimiza kila mahitaji yanayofikirika, ambaye hutoa kila ukamilifu na neema - hivi inaweza kufikirika kwamba yeye mwenyewe awe wa kufungwa na kuhitaji? Mifumo ya kiakili inabakia akili mwetu tu almradi tunataka idumu humo; inatoweka pindi tu tunapoindolea nadhari zetu kwa sababu zinabuniwa na kutengenezwa na sisi wenyewe. Namna hii ya elimu sio ya moja kwa moja na isiyoingiliwa kati, na kwa hiyo inaitwa "ujuzi wa kupatikana," kwa kutofautisha na "ujuzi wa papo hapo", ambao hauna haja ya njia. Tofauti baina yetu, sisi ambao tunatengeneza mifumo yetu wenyewe ya akili na Muumba aliyeanzisha maumbile yote ipo hapa, kwamba sisi kuwepo kwetu kwenyewe hasa kunatokana na Yeye, na kwa hiyo sisi tunakuwa ni wenye kumhitaji Yeye, ambapo yeye ndiye Muumba wa kweli na mhuishaji wa vitu vyote, si muhitaji, na hana haja ya zoezi la kutazama ili apate ujuzi.

Ufafanuzi wa matukio yaliyopita na yajayo ambayo hutokea katika upeo nafsi na fikra zetu ni lazima una ukomo, kwani tunatumia muda na nafasi maalum ambao nje ya hapo sisi hatuna kuwepo tena. Sisi ni viumbe vya maada tu; na dutu, kwa mujibu wa kanuni za fizikia na nadharia ya uwiano, inahitaji muda na mahali katika maendeleo ya polepole endelevu ya kukua na kubadilika. Yaliyopita na yajayo hayana maana kwa nafsi ambayo imekuwepo kabla na baada ya umilele, kila mahali na wakati wote na iliyoepukana ufungiwaji wa maada na athari zake.

Kwa kuwa kila kiumbe kinategemea juu ya uwepo wa milele wa Muumba kwa ya asili yake na uhai wake, hakuna pazia au kizuizi ambacho kinaweza kuwepo kati ya Mwenyezi Mungu na kiumbe hicho; Mwenyezi Mungu anazienea sehemu zake za ndani na nje na anao uwezo mkubwa kabisa juu ya kiumbe hicho. Mtu mmoja alimuuliza Amirul-Mu'minin Ali(a.s) , "Hivi! Mwenyezi Mungu yupo wapi?" Ali alimjibu: "Sio sahihi kuuliza Mwenyezi Mungu yuko wapi kwa sababu ni Mwenyezi Mungu ndiye Aliyeumba nafasi. Wala si sahihi kuuliza Mwenyezi Mungu alivyo, na ni wa asili gani, kwani ni Mwenyezi Mungu ndiye aliyeumba kila asili. Zaidi ya hayo, si sahihi kuuliza Mwenyezi Mungu ni nini kwa sababu ni Mwenyezi Mungu ndiye aliyeumba vyanzo (vinavyofanya kitu kiwe kitu - quiddity) vya vitu vyote.

"Atukuzwe Mwenyezi Mungu Mweza wa yote ambaye kwenye mawimbi ya utukufu Wake wenye hekima hushindwa kuogelea, ukumbukaji wa umilele Wake husimamisha fikra zote katika mkondo wake, na Ambaye katika mbingu yake pana ya utakatifu akili hupotea njia!"[40] .

Qur'ani inasema:

وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٥٩﴾

"Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilichoko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinachobainisha." (6:59)

Hebu tufikirie kwamba tumo katika chumba kinachoelekea mtaani na tunatazama kupitia dirisha dogo msururu mkubwa wa magari ambayo yanapita kwa kasi mtaani hapo. Ni wazi kwamba hatuwezi kuyaona magari yote kwa wakati mmoja; bali tunayaona moja moja yanapopita mbele ya dirisha hilo, halafu yanatoweka machoni. Kama tungekuwa hatujui lolote kuhusu magari, tungeweza kudhani kwamba yanakuja kuwepo pole pole upande moja wa dirisha halafu yanakoma kuwepo ule upande mwingine wa dirisha.

Sasa dirisha hili dogo linashabihiana kabisa na nyanja yetu ya kuona, linathibitisha wakati uliopita na unaokuja wa magari hayo. Wale walioko nje ya chumba hicho wakiwa wamesimama kando kwenye nia ya migu wanayaona magari yote yakipita kwa pamoja. Hali yetu kuhusiana na muda uliuopita na ujao wa dunia hii ni kama ile ya mtu yule anayetazama magari kupitia kwenye dirisha dogo. Pindi tutakapotambua kwamba Mwenyezi Mungu yuko juu ya muda na nafasi, tunaelewa kwamba matukio yote yaliyopita na yajayo wakati wote huwa yanakuwepo na yanaendelea kuwepo mbele Yake, kama mchoro.

Kwa hiyo, tunatakiwa kuwa na hisia ya wajibu kwa Mumba Ambaye anatambua hata chembe ndogo sana ya shughuli na kitendo cha maumbile - kama isemavyo Qur'ani:"..Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yale mnayoyatenda." (2:283) - na tuepuke dhambi au kosa lolote ambalo linaweza kusababisha sisi k uwa mbali na Yeye. Tunapaswa kumuabudu Mwenyezi Mungu, Mmiliki wa elimu yote Ambaye ametufanya sisi kupita kwenye hatua zote hizi mbali mbali na kupata uwezo tulio nao sasa. Hatupaswi kutozitii amri Zake ambazo hutufungulia njia yetu kuelekea kwenye furaha ya kweli na shabaha ya mwisho ya mwanadamu na tusikubali lengo jingine mbali na Yeye.

Ili tuweze kumfikia Mwenyezi Mungu lazima tujipambe sifa takatifu na tujiandae, katika muda wetu mfupi hapa duniani, kwa ajili ya kukutana Naye. Halafu tuweze kurejea Kwake, ambaye ni chanzo, chimbuko na mwanzo wa kuwepo kwetu. Jambo hili linahitaji bidii ya utendaji yenye kulenga katika utakasaji wa nafsi, kwani wajibu wa kutekeleza busara hii umewekwa juu ya mwanadamu kama dhamana tukufu.

14

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

SOMO LA KUMI NA NNE

MAONI KUHUSU UADILIFU WA MWENYEZI MUNGU

Tatizo la uadilifu kama mojawapo ya sifa za Mwenyezi Mungu limekuwa na historia yake iliyo dhahiri. Madhehebu mbali mbali za Kiislamu zimeshikilia maoni tofauti kuhusu suala hili, wakilitafsiri kwa mujibu wa kanuni zao bainishi. Baadhi ya Sunni ambao hufuata maoni ya mwanateolojia Abul-Hasan Ash'ari hawaamini katika uadilifu wa Mwenyezi Mungu kuwa ni suala la imani na wanakanusha kwamba uadilifu unatimizwa na matendo ya ki-Mungu.

Hata hivyo, kwa maoni yao, Mwenyezi Mungu humtendea mtu fulani, na adhabu yoyote au thawabu Anazompa, bila kuzingatia ni nini angeonekana kustahili kupewa, itawakilisha uadilifu na wema kamili, hata kama itaweza kuonekana si haki ikipimwa katika viwango vya kibinadamu. Hawa Ash'ari, kwa hiyo hutofautisha sifa ya Mwenyezi Mungu ya uadilifu mbali na matendo Yake na kwa hiyo, wanafikiri chochote kinachohusishwa na Mwenyezi Mungu kuwa ni haki. Kama anampa thawabu muadilifu na kumwadhibu mkosaji, huu ni uadilifu, na ndivyo itakavyo kuwa kwa kinyume chake; bado ingekuwa kwenye nyanja yake pana ya uadilifu Wake.

Madai yao kwamba maneno yenyewe hasa 'uadilifu' na 'udhalimu' hayana maana yanapotumiwa kwa Mwenyezi Mungu, bila shaka yanakusudiwa kunyanyua dhati ya Mwenyezi Mungu takatifu hasa kufikia upeo wakuvuka mipaka. Lakini hakuna mtu mwenye mawazo kamili atakayeziona dhana hizi za juu juu na pungufu kuwa na uhusiano wowote na uvuka mipaka wa Mwenyezi Mungu. Kwa kweli, wanahusisha ukanusho wa mpango hapa duniani, wa kanuni ya uababishaji katika mpango wa jumla wa dunia na katika tabia na matendo ya watu binafsi.

Wafuasi wa al-Ash'aria wanaamini hata hivyo, kwamba taa ya akili yenye mwanga mkali, huzimika wakati wowote inapokabiliwa na utambuzi na matatizo ya dini, kwamba haiwezi kumnufaisha mwanadamu au kuangaza njia yake. Madai haya wala hayaendani na mafundisho ya Qur'ani wala maudhui ya Sunna. Qur'ani inaona kupuuza akili ni namna ya upotovu na inarudia kuwataka watu watafakari na kuzingatia ili waweze kujifunza elimu bora zaidi na imani za kidini. Wale wanaoshindwa kunufaika kutokana na taa hii angavu iliyomo ndani mwao wanalinganishwa na hayawani. Qur'ani inasema:

إِنَّ شَرَّ الدَّوَابِّ عِندَ اللَّـهِ الصُّمُّ الْبُكْمُ الَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ ﴿٢٢﴾

"Hakika ya viumbe wabaya zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni wale viziwi na mabubu ambao hawatafakari." (8:22)

Mtume wa Uislamu anasema:"Mwenyezi Mungu amemwekea kila mtu walinzi wawili: mmoja ni wa nje yake, wajumbe wa Mwenyezi Mungu, na mwingine wa ndani, uwezo wake mwenyewe wa akili".

Wafuasi wa Mutazilite na Shia wanapingana na al-Ashari na madhehebu yake. Kati ya sifa zote za Mwenyezi Mungu, wao wamechagua uadilifu kuwa kama kanuni ya imani yao. Kwa kutegemea uthibitisho wa mapokezi au wa kihekima, pia wamepinga na kukataa kama isiyoendana na kanuni ya uadilifu, mafundisho ya athari za hatima ya ki-Mungu na kudra ya matendo ya mtu (kabla hajayafanya). Wanaamini kwamba uadilifu ndio msingi wa matendo ya Mwenyezi Mungu, katika mpangilio wa ulimwengu na katika kuanzisha sheria. Kama vile ambavyo matendo ya mtu yanavyoweza kupimwa kwa mujibu wa kigezo cha wema na uovu, matendo ya Muumbaji pia yanatakiwa kupitishwa kwenye kigezo cha namna hiyo hiyo. Kwa kuwa mantiki ya akili huamua kwamba uadilifu ni wa kutukuzwa kiasili na udhalimu kiasili ni wa kulaumiwa, basi lengo la kuabudiwa ambalo sifa zake ni pamoja na akili isiyo na ukomo na mawazo hakiwezi kamwe kufanya kitendo ambacho mantiki inakiona hakiruhusiwi.

Tunaposema kwamba Mwenyezi Mungu ni mwadilifu, ina maana kwamba dhati Yake yenye kujua kila kitu na bunifu haifanyi kitu ambacho ni kinyume cha busara na manufaa. Dhana ya hekima, inapotumiwa kwa Muumbaji haimaanishi kwamba Yeye huchagua njia bora ya kufikia malengo Yake au kurekebisha mapungufu Yake, kwani ni mwanadamu tu ambaye anayetakiwa kutoka kwenye upungufu kuelekea kwenye ukamilifu. Anachotaka Mwenyezi Mungu kuwafanya viumbe waondoke kutoka kwenye mapungufu na kuwasukuma kwenda kwenye ukamilifu na malengo ya asili ya dhati zao. Hekima ya Mwenyezi Mungu ni pamoja na hili; kwamba kwanza hupandikiza aina ya upendeleo wake kwenye kila kiumbe, na halafu baada ya kukipa uhai juu yake, hukisukuma kuelekea kwenye ukamilifu wa uwezo wake kupitia utekelezaji zaidi wa ukarimu Wake.

Halafu, uadilifu una maana pana, ambayo kwa kawaida inajumuisha kuepuka ukandamizaji na matendo yote ya kipumbavu. Imamu Jafar as- Sadiq(a.s) anasema katika kuelezea uadilifu wa Mwenyezi Mungu:"Uadilifu katika suala la Mwenyezi Mungu maana yake ni kwamba usihusishe jambo lolote kwa Mwenyezi Mungu ambalo kwamba kama ungelifanya wewe lingekusababishia kulawamiwa na kukosolewa." [41] Kwa mwanadamu, ukandamizaji na aina zote za shughuli za kidhalimu ambazo huzifanya, bila shaka, hutokana na ujinga na upungufu katika umtambuzi na kuhitaji kulikoungana na uduni wa hulka, pia wakati mwingine ni kuakisi kwa chuki na uadui, kunakochomoza kutoka kwenye nafsi ya ndani kabisa ya mwanadamu kama cheche.

Ni watu wengi sana ambao huchukizwa na ukandamizaji na uovu wao wenyewe. Hata hivyo, kwa sababu ya kutokujua kuhusu matokeo ya mwisho ya matendo yao, wanaendelea mara kwa mara, kufanya udhalimu na kujichafua wenywe kwa aina zote za matendo ya fedheha na uovu. Wakati mwingine mwanadamu anahisi kwamba anataka kupata kitu ambacho yeye mwenyewe hana njia au uwezo wa kukipata. Hii ndio sababu ya msingi ya maovu mengi. Hisia za kuhitaji, njaa na ulafi, mtu kuwa na tamaa ya kuumiza au kutawala - yote haya ni mambo ambayo huongozea kwenye tabia ya ugomvi.

Chini ya ushawishi wao, wanadamu hukosa udhibiti wa kujizuia. Huweka juhudi zake zote katika kutimiza matakwa yake na kukiuka masharti yote ya kimaadili, huanza kukaba makoo ya wanaogandamizwa. Dhati ya kipekee ya Mwenyezi Mungu, ile nafsi isiyo na ukomo, imeepukana na tabia na mipaka ya aina hiyo, kwani hakuna kinachofichikana kwenye elimu Yake bila ya mipaka, na haiingii akilini kwamba apatwe na udhaifu wa kutokuwa na uwezo kuhusiana na kitu chochote -Yeye, wa Tangu na Tangu, ambaye nuru Yake ya milele inagawa uhai na riziki kwa vitu vyote na Ambaye anawahakikishia mwenendo wao, namna zao mbalimbali na maendeleo.

Dhati stadi ambayo inakusanya viwango vyote vya ukamilifu haina haja ya kitu chochote ambacho kwamba kama hakipo kitatia hali ya wasiwasi ndani Yake Anapopatwa na kukihitajia. Nguvu na uwezo wake bila shaka hazina mipaka na hazipungukiwi na chochote hivyo kwamba anaweza kusababishiwa kupotoka kutoka kwenye njia ya uadilifu na kumfanyia uovu mtu au kulipiza kisasi ili kutuliza moyo wake au kufanya kitendo kisichostahili na kiovu. Hakuna hamasa yoyote ya tabia ya udhalimu inayoweza kupatikana kwa Mwenyezi Mungu, na kwa kweli dhana za ukandamizaji na udhalimu hasa hazitumiki kwa dhati, Ambayo ukarimu na huruma yake vinavienea vitu vyote na Ambaye utakatifu wa dhati yake unaonekana dhahiri katika maumbile yote.

Qur'ani inakanusha mara nyingi mawazo yote ya udhalimu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kumchukulia Yeye katika utukufu Wake kwamba ameondokana kabisa na matendo yote mabaya. Qur'ani inasema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ النَّاسَ شَيْئًا وَلَـٰكِنَّ النَّاسَ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٤٤﴾

"Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu kitu chochote; lakini watu wenyewe wanajidhulumu nafsi zao." (10:44).

Katika Aya hii, Mwenyezi Mungu Anajitenga Mwenyewe na fikra yoyote ya udhalimu, jambo linachukiza kwa wanadamu, na badala yake analirudisha kwao wenyewe.

Kwa nyongeza, inawezekanaje kwamba Mwenyezi Mungu awaite wanadamu kwenye uadilifu na usawa ambapo wakati huo huo achafue mikono Yake kwa matendo ya kidhalimu? Qur'ani inasea:

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿٩٠﴾

"Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu na hisani, na kuwapa jamaa, na anakataza uchafu na uovu na dhulma. Anakuwaihidhini ili mpate kukumbuka." (16:90).

Uislamu unathamini sana uadilifu hivyo kwamba endapo kundi moja la Waislamu linataka kupotoka kwenye njia ya uadilifu na kuanza kujihusisha na ukandamizaji, lazima wazuiwe, hata kama hili litahusisha vita. Haya ndio maagizo ya Qur'ani:

وَإِن طَائِفَتَانِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ اقْتَتَلُوا فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا فَإِن بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَىٰ فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّىٰ تَفِيءَ إِلَىٰ أَمْرِ اللَّـهِ فَإِن فَاءَتْ فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا بِالْعَدْلِ وَأَقْسِطُوا إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ ﴿٩﴾

"Na ikiwa makundi mawili katika waumini yanapingana, basi yapatanisheni. Na ikiwa moja kati yao linamdhulumu mwenzie, basi lipigeni linalodhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu. Na likirudi basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaohukumu kwa haki." (49:9).

Jambo la kuvutia linalojitokeza kutoka kwenye Aya hii ni kwamba mpatanishi amepewa maagizo kumuelekeza kuhakikisha, pale anapofanya usuluhishi, ugomvi uishe kwa mujibu wa uadilifu, bila kuonyesha huruma kwa yule mchokozi. Inaweza kutokea, katika hali ambapo vita vimeanzishwa kwa malengo ya uchokozi, kwamba mpatanishi anajaribu kumaliza ugomvi kwa kusisitiza juu ya huruma na kutoyaangalia makosa, na hatimaye, anashawishi upande mmojawapo wa wagomvi kuacha madai yake kwa manufaa ya upande wa pili. Utaratibu huu wa huruma, ingawa una uhalali ndani yake, unaweza kuzidisha moyo wa uchokozi ulikuwepo tayari kwa wale walionufaika kwa kuanzisha vita. Kwa kweli ni jambo la kawaida kumridhisha mchokozi katika hali kama hizi kwa kumpatia tahafifu.

Ingawa kusamehe madai kwa hiari, lenyewe ni jambo la kupendeza, katika hali kama hiyo, linaweza kuwa na athari mbaya katika fikra za mchokozi. Lengo la Uislamu ni kung'oa matumizi ya nguvu na udhalimu kutoka kwenye jamii ya Ki-Islamu na kuwahakikishia Watu wake kwamba hakuna mtu anayeweza kupata kitu chochote kwa uchokozi na mabavu.

Kama tukitazama utaratibu wa maumbile, tunaweza kuona kwamba upo uwiano mkubwa na mpana mno miongoni kwa viumbe vyote vya kimaada. Hali hii, inadhihiri kwenye ukawaida wa Atomu, haraka ya elektroniki, mzunguko wa sayari, na kusogea kwa viumbe vyote. Inaonekana kwenye madini na kwenye nyanja ya mimea na chanikiwiti, kwenye uhusiano sahihi uliopo baina ya viungo vya kiumbe hai, katika ulingano miongoni mwa vijenzi vya ndani ya atomu, katika uwiano miongoni mwa maumbo makubwa ya angani na nguvu zao za mvutano zilizokokotolewa vizuri.

Aina zote hizi za ulingano na uwiano, pamoja na kanuni zingine sahihi ambazo sayansi bado inatafuta, kuzigundua, zinatoa ushahidi wa kuwepo kwa mpangilio usiokanika katika ulimwengu, ambao unathibitishwa kwa mlinganyo wa kimahesabu. Mtume wetu mkweli ameuelezea kuhusu uadilifu huu wa jumla na uwiano mpana - ukweli kwamba hakuna kisicho sawa au kilichoko nje ya sehemu yake - kwenye tamko hili fupi na fasaha: "Ni uwiano halisi na mpachano ambao unaendesha dunia na mbingu."

Qur'ani inayahusisha maneno yafuatayo na Musa(a.s) na Mtume wetu:"Akasema: Mola wetu Mtukufuni yule aliyekipa kila kitu umbo lake, kisha akakiongoa." (20:50).

Katika sentensi hii fupi, Musa anamfafanulia Firauni jinsi dunia ilivyoumbwa pamoja na mpangilio na uzuri wake, ambavyo ni miongoni mwa ishara za Mwenyezi Mungu. Lengo lake Musa lilikuwa ni kumkomboa Firauni kutoka kwenye fikra zake potofu na kumsaidia kutambua kuwepo kwa mpango wa adilifu na mtukufu uliowekwa ulimwenguni.

Mojawapo ya kanuni zinazotawala maumbile bila kuzuilika, kwa hiyo ni mpangilio na uadilifu, na vitu vyote, kwa sababu ya kuwa chini ya kanuni na taratibu za maumbile, vipo katika mlolongo wa mageuzi kuelekea kwenye ukamilifu ambao ni mahsusi kwa kila kimoja chao. Ukengeukaji wowote kutoka kwenye mkondo huu wa jumla wa mpangilio na uhusiano ulioandaliwa juu yake utasababisha utatanishi na ghasia. Wakati wowote panapotokeza hali isiyo ya kawaida kwenye maumbile, vitu vyenyewe huonyesha athari, na vitu vya ndani au nje hujitokeza kuondoa vikwazo vya maendeleo na kuanzisha upya ule utaratibu unaohitajika kuendelea kwenye njia ya kwenye ukamilifu.

Mwili unaposhambuliwa na viini na mambo mengine ya maradhi, chembechembe za damu nyeupe huanza kuvidhoofisha, kwa mujibu wa kawaida isiyozuilika. Dawa yoyote itakayoagizwa na daktari ni kipengele cha nje ambacho kinazisaidia chembe chembe nyeupe katika kazi ya kudhoofisha viini vya maradhi na kuanzisha upya uwiano mwilini. Mwisho kabisa, haiwezekani kwamba Mwenyezi Mungu, Ambaye upendo Wake niwa milele na Ambaye kwa ukarimu hutoa fadhila Zake kwa waja wake, afanye kosa lolote dogo sana la kidhalimu au tendo lisilofaa. Jambo hili ndilo ambalo hakika Qur'ani inaelezea ifuatavyo:

اللَّـهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ قَرَارًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ فَتَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٦٤﴾

"Ni Mwenyezi Mungu aliyekufanyieni ardhi kuwa ni mahala pa kukaa, na mbingu kuwa dari. Na akakutieni sura, na akazifanya nzuri sura zenu, na akakuruzukuni vitu vizuri. Huyo ndio Mwenyezi Mungu, Mola Wenu. Na ametukuka Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote." (40:64).

15

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

SOMO LA KUMI NA TANO

UCHAMBUZI KUHUSU BALAA NA DHIKI

Suala la uadilifu wa Mwenyezi Mungu linahusisha matatizo fulani, kama vile kuwepo kwa maafa, hasara na uovu katika mpangilio wa asili, na kutokuwepo usawa katika mpango wa kijamii. Suala hili, kwa kweli, linazua wimbi kubwa la maswali na ugumu kwenye akili za watu wengi. Matatizo wanayokabiliana nayo ni ya msingi mno hivyo kwamba kinachoanza kama mashaka na kusita, hatimaye huwa tatizo sugu.

Watu kama hao, wanahoji kwamba inawezekanaje katika dunia iliyoumbwa kwa misingi ya akili na hekima, iwe inakumbwa na mateso mengi sana, maumivu na uovu, mara nyingi ipatwe na misukosuko ya dhiki na mabalaa yasiyokwisha; pamoja na hasara na upungufu kuongezeka kila mara. Kwa nini kwamba katika sehemu mbali mbali za dunia, matukio ya kuogofya na kugharikisha yanashambulia wanadamu, na kusababisha hasara na maangamizi yasiyosemekana? Kwa nini mtu huyu ana sura mbaya na mwingine ana sura nzuri, huyu ana afya nzuri na yule mgonjwa? Kwa nini watu wote hawakuumbwa sawa na je, kutokuwa sawa kwao hakuonyeshi kukosekana kwa uadilifu duniani?

Uadilifu katika utaratibu wa mambo unategemea juu ya kuwa kwake huru kutokana na dhulma, ubaguzi na maafa, au kutokuwepo ndani yake dosari, maradhi na umasikini, hii peke yake, wao wanasema, ingesababisha matokeo ya ukamilifu na uadilifu.

Lazima tuanze kwa kukubali kwamba tathmini yetu juu ya mambo ya ulimwengu haiturusu sisi kupenya vile vina hasa vya mambo; haitoshelezi kwa ajili ya uchambuzi wa matokeo na malengo ya vitu. Uelewa wetu wa mwanzo wa matukio yasiyopendeza na maafa una uhakika wa kuwa wajuu juu; hatupo tayari kutambua ukweli wowote ulioko nje ya maoni yetu ya mwanzo. Hatuwezi pale mwanzoni kabisa, kufafanua yale malengo ya juu kabisa ya matukio hayo, na kwa hiyo, sisi tunayachukulia kama dalili za udhalimu. Hisia zetu huamshwa na hutuongoza kwenye uchunguzi usio wa kimantiki kabisa.

Lakini endapo tutatafakari kwa kina zaidi, tutaona kwamba tathmini hii ya matukio ya upande moja ambayo tunaiita udhalimu inatokana na kuzifanya nadhari zetu, au zile za watu ambao tuna uhusiano nao wa moja kwa moja au wa mzunguko, kuwa ndio mfano au kigezo chetu. Chochote kitakachosalimisha maslahi yetu ni kizuri na kile kinachotuumiza tutakiona kibaya. Kwa maneno mengine, uamuzi wetu wa uzuri na ubaya umeegemea kwenye utambuzi dhaifu, upeo mfinyu wa fikra, na kutokuwa na ujuzi sahihi kuhusu kanuni za maumbile.

Kuwepo kwetu tu ndio jambo linalohusika katika kila tukio? Je, tunaweza kupata faida na hasara zetu kuwa mfano wa wema na ubaya? Dunia yetu hii ya kimaada siku zote inashughulika katika kuzalisha mabadiliko. Matukio ambayo hayakuwepo leo yatatokea kesho; baadhi ya vitu vitatoweka na vingine vitaziba nafasi yao. Ni dhahiri kwamba kile chenye faida na manufaa leo kwa baadhi ya watu, kesho kitakoma kuwepo. Lakini kwetu sisi ambao ni binadamu na tulioambatana na uhai wetu wenyewe vitu vya dunia, upatikanaji wa vitu ni mzuri na kukosekana kwao ni kubaya. Lakini licha ya binadamu na viambatanishi vyake, asili inayobadilika ya dunia inatoa vitu vinavyobadilika siku zote. Kama dunia haikutambua uwezekano wa mabadiliko, viumbe vyenyewe visingekuwepo, na kwa hiyo, pia kusingekuwepo na suala la wema na uovu.

Katika dunia ya kinadharia na isiyobadilika kama hiyo wala kisingekuwepo na hasarana upungufu ama kustawi na kuendelea, hakuna kinyume wala utofautishaji, aina mbali mbali au wingi, uachanishaji au mwendo. Kwenye dunia isiyokuwa na dosari au hasara, pia kusingekuwepo na binadamu, kigezo cha maadili au kijamii, mipaka au sheria. Maendeleo na mabadiliko ni matokeo ya mwendo na mzunguko wa sayari; kama zingekoma kuwepo, kusingekuwepo na ardhi, mwezi, jua, siku, hakuna mwezi na hakuna mwaka.

Mtazamo mpana kiasi wa dunia utaturuhusu kutambua kwamba jambo tunaloliona kuwa baya kwetu leo, au linaweza kuwa hivyo siku za usoni, ni lenye manufaa kwa wengine. Dunia kwa ujumla husogea kuelekea kwenye upande ambao ulioamriwa na kusudio la jumla la kuwepo kwake na manufaa ya kuwepo kwake; mtu mmoja mmoja wanaweza kupata madhara katika utaratibu huu; na inaweza hata ikawa kwamba binadamu wote kwa ujumla hawafaidiki.

Endapo tungeweza kutumbukia kwenye kina kirefu zaidi cha bahari ya elimu na tupekuwe kurasa za kitabu chake kilichojaa miujiza kwa kidole chetu cha uelewa, lengo la mwisho na matokeo ya matukio yote na mambo yote yatajionyesha kwetu. Hata hivyo, uwezo wetu wa maamuzi si mpana vya kutosha kuweza kushughulika na mtandao tata unaotukabili: wala hatujui mlolongo wa sababu zilizotangulia ambazo zimezaa haya matukio ya leo, wala mlolongo wa athari za siku za usoni ambazo baadae matukio haya yatazaisha.

Kama ingekuwa inawezekana sisi kutazama chini kutoka juu ya uwanda mpana wa dunia, namna ambayo tungeweza kuona vipengele vyote vya dhahiri na hasi ya kila kitu, miujiza yote ya kila kitu inayotokea hapa duniani; kama ingewezekana sisi kutathmini athari na matokeo ya kila tukio katika historia, iliyopita, ya sasa na ijayo na kila kitu kinachotokea baina ya kabla ya mwanzo na baada ya umilele, na kama, jambo hili lingewezekana kwetu sisi, tungeweza kusema kwamba madhara ya tukio lililotajwa yamezidi uzito manufaa yake na kuyaita uovu.

Lakini je, binadamu anao utambuzi mpana kiasi hicho wa minyororo iliyonyyka na iliyosimama ya visababishi? Binadamu anaweza kujiweka kwenye muhimili unaosogea wa dunia? Kwa kuwa hatuthibiti uwezo wa aina hiyo, kwa kuwa hatutaweza kamwe kusafiri mwendo mrefu hivyo, hata kama hatua zetu zingekuwa ndefu kiasi gani, kwa kuwa hatutaweza kufunua pazia kutoka kwenye changamano zote hizi na kuchukua vipimo vya vinavyostahili, ni vema tujizuie kufanya uamuzi ulioegemezwa upande moja na wa haraka ambao msingi wake ni uoni wa upeo mfupi. Lazima tutambue kwamba tusifanye manufaa yetu wenyewe kuwa ndio tu kigezo pekee cha kuitambua dunia hii pana. Uchunguzi kiasi tunaofanya katika mfumo wa takwimu chache tulizonazo na mazingira maalum ambayo yanatutawala hayawezi kamwe kutoa na kigezo cha kutuwezesha kutoa uamuzi wa uhakika.

Mara nyingi asili inaweza kuwa inafanya kazi kuelekea kwenye ukamilishaji wa lengo maalum ambalo mwanadamu hawezi kulifikiria, kama ilivyoelezewa hali yake ya kawaida. Kwa nini isidhaniwe kwamba matukio mabaya ni matokeo ya jitihada zinazolenga kutayarisha uwanja wa vitu vingi na vipya ambavyo vitakuwa zana ya utashi wa Mwenyezi Mungu juu ya duniani? Inawezekana kwamba hali na mazingira ya zama hizi yanalazimisha utaratibu kama huo.

Kama mabadiliko na mageuzi yote yanayotuogofya hayakutokea katika mpango na ubunifu unaotakiwa na kwa sababu ya lengo maalum, kama yangeongezwa wakati wote bila kutoa matokeo yoyote mazuri au ya yenye kusaidia, kusingekuwepo na dalili yoyote ya kiumbe hai hapa duniani, pamoja na mwanadamu. Kwa nini tuilaumu dunia kwa kutotenda haki, kwa yenye vurugu na kuyumba, kwa sababu tu ya matukio machache ya ajabu na mambo ya asili? Je, tuanze kukataa kwa sababu ya kiasi cha ubaya; kikubwa na kidogo, na kusahau udhihiri wa usahihi wote na busara, maajabu yote tunayoyaona kwenye dunia na viumbe vyake, ambavyo vinashahidilia utashi na akili ya dhati tukufu?

Kwa kuwa mwanadamu huwa anaona ushahidi mwingi sana wa upangaji makini katika ulimwengu wote, lazima akiri kwamba dunia kwa ujumla ni kitu kizima chenye lengo, utaratibu unaosogea kuelekea kwenye ukamilifu. Kila jambo ndani humo linatawaliwa na kigezo chake maalum, na kama jambo linaonekana halielezeki au lisiloweza kutetewa, hii ni kwa sababu ya kutoona mbali kwa binadamu. Mwanadamu lazima aelewe kwamba katika ukomo wake, anakosa uwezo wa kuelewa malengo ya mambo yote na maudhui zao; si kwamba maumbile yana dosari yoyote.

Msimamo wetu kwenye matukio yenye uchungu yasiyopendeza ya dunia hii hufanana na uamuzi uliofanywa na mwenyeji wa jangwani anapokwenda mjini na kuona mabuldoza yenye nguvu yanavyovunja nyumba za zamani. Yeye anauona uvunjaji huu kama ni kitendo cha kipumbavu cha maangamizi, lakini ni busara kwake kufikiri kwamba uvunjaji huo haukupangwa na hauna malengo? Kama mambo yalivyo, hivyo sivyo, kwa sababu yeye anaona ule utaratibu wa uvunjaji tu, sio mahesabu na mipango ya wasanifu ujenzi na mengineyo yanayohusika. Kama alivyosema mwanasayansi mmoja: "Hali yetu ni kama ile ya watoto wanao tazama vifaa vya sarakasi vinafungashwa na kujiandaa kuondoka. Hili ni muhimu kwa kundi la wanasarakasi kuondoka na kwenda mahali pengine na kuendelea na maisha yake ya msisimko, lakini wale watoto wasioona mbali wanaona mahema yanavyokunjwa na kule kuja na kuondoka kwa watu na wanyama, hakuna kingine chochote isipokuwa kuvunjwa na kuhamishwa kwa sarakasi hizo."

Endapo tutaangalia kwa undani zaidi na kwa ubunifu zaidi matatizo na mabalaa yanayomkera binadamu na kuzitafsiri kwa usahihi, tutatambua kwamba kwa kweli, matukio hayo ni neema, sio balaa. Neema kuwa neema, na balaa kuwa balaa inategemea na jinsi binadamu atakavyolichukulia tukio hilo; tukio moja linaweza kuhisiwa tofauti na watu wawili tofauti. Matatizo na usumbufu ni sawa na kengele ya inayomtahadharisha mwanadamu ili arekebishe dosari zake na makosa yake; yamekuwa kama mfumo wa kinga ya asili au utaratibu wa urekebishaji wa kiasili kwa binadamu.

Kama utajiri huelekeza kwenye kupenda anasa na starehe, hayo ni matatizo na balaa, na kama umaskini na ufakara huelekeza kwenye utakaso na maendeleo ya nafsi ya mwanadamu hizo ni neema. Hivyo, utajiri hauwezi kuhesabiwa kama ni wema moja kwa moja wala umaskini kuwa balaa hasa. Kanuni kama hiyo inajumuisha neema yoyote ya asili anayoweza kuwa nayo binadamu.

Mataifa ambayo yanakabiliwa na makundi mbali mbali yenye uhasama na kulazimishwa kupigania kudumu kwao huimarishwa hapo. Pindi tunapochukulia juhudi na mpambano kuwa ni jitihada za uhakika na zinazosaidia, hatuwezi kuacha kutilia maanani majukumu yanayofanywa na shida, katika kukuza uwezo wa utambuzi wa ndani zaidi na kumsukuma kwenye maendeleo. Watu ambao hawalazimiki kupambana na ambao huishi kwenye mazingira yasiyo na mikanganyiko yoyote kwa urahisi sana watatumbukia kwenye ustawi wa mali katika starehe na anasa zao.

Ni mara ngapi hutokea ambapo mtu hustahamili dhiki na matatizo kwa hiari yake mwenyewe, kwa sababu ya lengo kubwa! Isingekuwa dhiki na matatizo hayo, lengo hilo lisingeonekana la kutamanika kwake! Njia nyepesi ambayo hupita mtu bila kuangalia na bila kufikiria haifai kwa maendeleo na ustawi, na jitihada ya binadamu ambamo dalili ya utashi wa nafsi imeondolewa, haiwezi kuleta mabadiliko ya msingi kwa mwanadamu.

Mapambano na kuhitilafiana ni kama mateso yanayomsukuma mwanadamu mbele. Vitu vigumu huvunjika kwa shinikizo la kipigo cha kurudia tena na tena, lakini binadamu huundwa na kuimarishwa na matatizo wanayoyastahimilia. Hujitupa baharini na kuanza kujifunza jinsi ya kuogelea, ni kwenye hali ngumu ya matatizo ambapo kipaji hujitokeza. Mambo yaliyokithiri bila vikwazo, mapenzi juu ya dunia, kutafuta starehe bila vipingamizi, kutokujali malengo ya juu zaidi - yote haya ni dalili za upotofu na kutokutambua. Kwa kweli, watu mafedhuli kabisa ni wale waliokulia kwenye raha na starehe, ambao kamwe hawajawahi kupitia kwenye matatizo mengi ya maisha au kuonja siku zake chungu sambamba na zile za furaha; jua la maisha yao huchomoza na kuchwa ndani yao bila kuonekana na mtu yeyote.

Kufuata mwelekeo wa mtu na kuambatana na matakwa yake haviendani na uimara na kunyanyuliwa roho kwa juhudi zenye malengo na kujitahidi. Utafutaji wa starehe na uovu, kwa upande mmoja, na nguvu na dhamira na kuwa na lengo kwa upande mwingine, zinadhihirisha mielekeo ya pande mbili tofauti inayopingana kwa binadamu. Kwa vile hakuna unaoweza ama kukanushwa au kukubaliwa ukiacha nyingine, mtu lazima ajitahidi kupunguza tamaa ya starehe na kuimarisha ile nguvu pinzani ndani ya muelekeo mmoja.

Wale ambao wamepewa malezi ya starehe, ambao hawajaonja siku za uchungu na utamu wa hapa duniani, ambao wakati wote wamekuwa wakifurahia neema na kamwe hawajadumu na njaa - kamwe hawawezi kuelewa ladha ya chakula kitamu wala furaha ya maisha kwa ujumla na hawana uwezo wa kuuelewa uzuri hasa. Starehe za maisha zinaweza kufurahikiwa tu hasa na wale ambao wamepitia maisha ya dhiki na kushindwa katika maisha yao, ambao wana uwezo wa kuhimili matatizo na kuzivumilia dhiki hizo zinazomngojea katika kila hatua ya njia ya mwanadamu. Raha ya kidunia na kiroho huwa na thamani kwa binadamu hapo baada tu ya kuyaona mema na mabaya ya maisha na mashinikizo ya matukio yake yachukizayo.

Pale mwanadamu anaposhughulishwa zaidi maisha yakinifu, vipimo vyote vya maisha yake hufungwa minyororo na hupoteza tamaa na hoja. Bila kukwepa, pia atatelekeza maisha yake ya milele na utakaso wa ndani. Almuradi matamanio yanazingira maisha yake na roho yake inakamatwa na giza, atakuwa kama doa dogo linalotupwa huku na kule kwenye mawimbi ya mata. Atatafuta kimbilio kila mahali isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, anahitaji kitu cha kumwamsha na kudukiza ukomavu katika fikra zake, kumkumbusha yeye kuhusu mpito wa dunia hii ya muda mfupi na kumsaidia kupata madhumuni ya mafundisho yote ya ki-mbinguni - uhuru wa Mnafsi yake kutoka kwenye vikwazo vyote na njia zinazomzuia mtu kupata ukamilifu wa kiwango cha juu.

Mazoezi na utakasaji wa nafsi sio vya kupatikana kirahisi; inahitaji ukanushajiwa raha na starehe mbali mbali, na utaratibu wa kujitoa humo ni mchungu na mgumu.

Ni kweli kwamba jitihada kama hizo zitakuwa kwa ajili ya kutakasa nafsi ya ndani ya mwanadamu na kuruhusu uwezo wake uliojificha kutokeza. Hata hivyo uvumilivu wa kujizuia kutenda dhambi na kutafuta starehe siku zote ni mchungu kwa utashi wa binadamu na ni kwa upinzani wa kikaidi wa kushusha msukumo kwamba anaweza kutimiza kazi yake ya kuvunja vizuizi ambavyo vinamkabili na hivyo kupanda juu kwenye uwanda wa maadili ya juu.